Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

SALHAT - 1

 







    IMEANDIKWA NA : SALMA R. RAMADHANI



    *********************************************************************************



    Simulizi : Salhat

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Ulikuwa usiku wa manane ulioambatana na radi za kutosha huku mvua nyingi na Kubwa ikiendelea kunyesha katika maeneo ya Arusha mtaana wa Moshono karibu kabisa na uelekeo wa chekereni alionekana msichana mmoja akiwa na Mtoto mdogo mbele ya kifua chake huku akikimbia kwa hofu Kubwa sana na kutizama nyuma ambako ndiko kulikomfanya hofu yake itande zaidi.

    Alijikwaa na kusimama tena kisha akambeba Mtoto yule na kuendelea kukimbia naye alikimbia naye hadi mahali alipohisi sasa ni salama kama atajificha hapo. Alijibanza katika kibanda kimoja na kuhisi kuwa hapo anaweza akawa salama wakati huo wote Mtoto yule mwenye miezi kama Minne alianza kulia na hivyo mama yule alichukua jukumu la kumnyamazisha kwa kumnyonyesha Mtoto yule ambaye alilipokea ziwa lake na kuanza kulinyonya akiwa hapo hapo liliingia kundi la watu wanne huku wakiwa wamevalia mavazi meusi na kushikilia bastola mikononi mwao huku wakiendelea kumtafuta hapo hapo liliingia gari jeuc na mlango ulifunguliwa na mmoja kati ya watu wale wanne waliowahi kutangulia. Vilishuka viatu vya kike vyenye rangi ya kijani na suruali nyeuc iliyoweza kumbana barabarah huku ikipokelewa na kibody cheupe kilicho chomekezwa ndani ya suruali ile na kikoti cha jeans cha kitop kilichoweza kuishia kwenye kifua chake.

    Alitoa miwani yake na kivua kofia iliyokuwa imefunika uso wake alikuwa ni binti ambaye makamo yake hayakuweza kupishana na mama yule mwenye mtoto........Jina lake aliitwa Badra.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mmeshampata huyo Malaya???!! Aliuliza. "Hapana bossi bado hatujampata ila nahisi hawezi kukimbia umbali mrefu Kwani tayari tulishamjeruhi kwa risasi katika mbavu zake changa. Alijibu msichana mmoja ambaye aliongozana naye huyu waliimwita Mainda.



    "Sawa nazihitaji mahiti zao hapa ziletwe sasa hivi hasa hasa huyo Mtoto" alizungumza Badra ambaye hakuonekana kuwa na hata roho ya huruma kwa Mtoto yule ambaye hata kujitambua bado.



    Watu wale wanne walianza kumtafuta mama yule mwenye Mtoto wakiongozwa na Mainda.



    Badra akiwa pale alifanikiwa kuyaona matone ya damu yakiwa yanaelekea katika njia ambayo ndimo alikojificha mama yule.



    Alitabasamu na kucheka kinafki kisha akaanza kuzifuata alama zile za damu huku akiita.



    "Samia!!! Samia!!!! Samia!!!!! Njoo rafiki yangu kipenzi kwanini unanipa wakati mgumu mimi wa kukutafuta wewe jaman ilihali unajua mimi sina shida sana na wewe zaidi ya huyo Mtoto wa Naseeb. Kwani huyo Mtoto anakipi kikubwa mpaka mnamficha hivyo jaman , Naseeb kafa leo kwaajili yake eti utaamini hilo. Samia!! Nilee tu huyo Mtoto hapa. Aliendelea kuongea huku akisogea karibu zaidi, wakati huo Samia alikuwa akitetemeka na asijue kipi cha kufanya ghafla mwanaye alianza kulia na kuwashtua hata wale waliokuwa hawajui ni upi upande alioko alimziba mwanaye mdomo na ghafla nayeye alizibwa mdomo na Mtu aliyetokea nyuma yake alijitahidi kumng.ata lakini Mtu yule alimgeuza na kumpa ishara ya kuwa anataka kumsaidia aliwasha simu yake iliyokuwa na mwanga hafifu kisha akaiplay sauti ya Mtoto iliyokuwa ikilia ndani ya simu na kumpa ishara ya Samia aondoke eneo lile pindi watu wale watakapoanza kumfuata yeye. Kijana yule alianza kupiga hatua na kuelekea chini kabisa ambako kulikuwa na kama bonde dogo tu lililobinuka kwa chini kidogo. Watu wale walianza kumfuata wakiamini ya kuwa ni Samia akiwa na mwanaye.

    Wote walianza kumfuata na kumuachia nafasi Samia ambaye aliinuka eneo lile na kuanza kutembea taratibu huku akihisi maumivu makali sana upande wa kushoto katika mbavu zake na hii ni kutokana na risasi aliyokwisha tayri kupigwa na Badra.







    Badra alipofika mbele kidogo baada ya kumfukuza Samia na kutokomea kusiko julikana alianza kuchezwa na machale na kuhisi tu huko siko baada ya kuanza kuisikia tena sauti ile ya Mtoto iliyokuwa ikilia kwa style ile ile tena kwa kujirudia wakati huo zilibaki mingurumo kadhaaa iliyokuwa ikisikika juu ya mbingu na radi chache zilizoweza kufanya waweze kuona hata kama siyo kwa mbali sana.



    Badra alishtukia mchezo ule na kugeuka nyuma ambako alifanikiwa kumuona Samia akianza kutokomea maeneo yenye vibanda.



    Samia alijitahidi kutembea lakini alishindwa kutokana na kidonda alichonacho wakati anaendelea kujisogeza zaidi aliviona viatu vya kike vikianza kumsogolea.



    "Tafadhali Badra, Tafadhali usiniulie mwanangu!!! Alizungumza Samia akijitahidi kumtizama ni nani aliyekuwa akisimama mbele yake alipofika usoni hakuweza kumtambua vzuri na Kwani tayari alishaanza kuona kizungu zungu hakuchukua muda mrefu alipokonywa na Mtoto na hapo hapo alidondoka chini na kuzimia.



    ***** ****** ******



    Ilikuwa acubuh yapata saa mbili kamili alionekana Badra akiwa amevalia gauni la kulalia na kutoka chumba kimoja ndani ya jumba Kubwa la kifahari alilokuwa akiishi tajiri mmoja aliyeweza kufahamika kutokana ma wingi wa Mali anazomiliki Jina lake walimwita Mr Matata huyo alikuwa tajiri aliyebahatika kuwa na Mtoto mmoja tu wa kiume ambaye alimpenda sana baada ya mkewe kufariki lakini mambo yalibadilika baada tu alipomuowa Badra Kwani hakumpenda tena mwanaye na mwisho wa siku kutokana na visa vya Badra baba huyo alimfukuza mwanaye ndani ya nyumba yake na kuishi na Badra.



    Badra alijinyoosha na kuelekea moja kwa moja kwa friji ambapo aliiifunua na kuanza kukagua kipi cha kutumia kwa asubuhi yake hiyo. Aliichukua juice mango na kuelekea kwenye glass kisha akaimimina na kuanza kuitumia taratibu kabisa huku akitizama TV.



    "Unaelekea wapi??! Aliuliza Badra baada ya kumuoma Mr Matata amevaa asubuhi asubuhi.



    "Nataka kwenda kumchukua mjukuu wangu sitaki akae na baba mpuuzi na mama kama yule Kwani mazingira wanayoishi hayatamfaa yeye" aliongea Mr matata na kuondoka zake.



    Badra alishikwa na hasira na kuitupa glass anayoitumia ukutani.



    "Mpumbavu wewe Salhat...... Unawezaje kuwa kikwazo kwangu ukiwa na miezi michache tu!! Aliongea kwa hasira na kuuma meno yake kisha kuyatoa macho yake yaliyokuwa makubwa naya mviringo.



    ******* *******



    Samia kutokana na jua alilokuwa akipigwa nao usoni na mawimbi ya habari kuwa makali kwa siku hiyo hakuweza kulala kwa muda mrefu. Alishtuka na kuita

    "Salhat"!!! Pembeni yake alimuona mwanamke mmoja aliyekuwa amembeba Salhat na kumpatia uji.

    Alimchukua mwanaye Salhat na kumuuliza.



    "Wewe ni nani???!! Na hapa ni wapi??! Tafadhali okoa maisha ya mwanangu yeye ni mdogo sana hajui wala hatambui chochote Tafadhali!! Aliongea Samia akihisi ya kuwa Mtu yule ni mbaya wake, hapo hapo aliingia kijana aliyeweza kumsaidia Jana ucku ili asikamatwe.



    "Huyu ni mke wangu anaitwa Lidia, mimi na yeye Jana tulisaidiana kwa pamoja kwaajili ya kuokoa maisha ya mwanao, na sasa usijali Kwani haupo tena Arusha alizungumza na kufungua upande aliotokea huku akimfanya Samia kuona bahari njee.



    "Huku wapi??!!! Aliuliza kwa mshangao.



    "Dar es salaam ila usijali pia kwasabab kesho kutwa tutaenda mwanza na huko itakuwa vigumu kwa Mtu yule kukufuatilia tena....... Lakini Dada!!!

    Aliongea na kunyamaza huku akihisi azungumze au.



    "Endelea" kauli ya ruksa ilitolewa na Samia.



    "Kwanini wnamuandama Mtoto mdogo namna hiyo??!!



    Samia alitizama chini na kumtizama mwanaye mdogo Salhat. Kisha akawaambia.



    "Kweli kwenye maisha kuna kupanda na kushuka, na siku zote unaambiwa fadhila mfadhili mbuzi binadamu anamauzi, na nimeamini mbuzi akikuuzi utamnywa mchzi ila mkataapo pema pabaya panamuita" alizungumza maneno hayo ya mafumbo na kuwa kama ameendelea kuwachanganya zaidi Joseph na mkewe Lidia ambao wlitizamana tu na kurudisha macho kwa Samia aliyekuwa akiendelea kulia tu baada ya kuyazungumz maneno Yale Kwani aliyaelewa mwenyewe.





    Huku nako Mr matata akiwa nyumbani kwake huku kundi Kubwa la watu wakiwa wamekaa mafungu mafungu na wengi wakiwa wamevalia nguo nyeusi.



    Alionekana kama Mtu anayejaribu kuvuta kumbukumbu kama vile anataka kukumbuka kitu lakini hakiingii akilini mwake. Alimwita mkewe Badra.



    "Badra......watu wanasema nilimfukuza Naseeb nyumbani, lakini mbona mimi sikumbuki hivyo nitawezaje kumfukuza Mtoto wangu wa pekee ndani ya nyumba niliyojenga na mama yake ambayo ni halali yake hapo ndiko ambako nashangaa" aliongea kwa kujishangaa ni kweli wala haikuwa akili yake Bali akili hiyo ni kutokana na madawa anayopewa na Badra.



    "Tumia kwanza haya maji kisha nitakuelezea kwann ulimfukuza nyumbani Naseeb"



    Mr matata aliichukua glass ile aliyopewa na Badra lakini aliitizama tu na kumtizama sana Badra usoni kisha akaipasua ile glass chini.



    "Nakuuliza kipi kimetokea mpaka Naseeb akaondoka nyumbni ww unanipa maji mimi, ilihali mwanangu tayri ameshakufa nitamwambia nini mm mke wangu aliyeweza kuyatoa maisha yake kwaajli ya Naseeb eti Leo na yeye kafa nitaiweka wapi sura yangu baada ya mwanangu kwenda kukutana na mama yake akimwambia kuwa mimi ndye niliyemfukuza nyumbani" aliongea akiwa mwingi wa hasira.



    Hapo hapo walikuja vijana kama ishirini waliokuwa wakiongozwa na kiongozi wao aliyeitwa Rajab.



    "Nauliza Yuko wapi mtoto wa mwanangu??!!



    "Tumefuatilia kwa makini ila hatujagundua lolote lile Kwani hata nyumba waliyokuwa wakiishi hakukuwa na Mtu yoyote tena zaidi ya damu ya Naseeb" alijib Raja.



    "Nimesema sitamzika Naseeb kama Mtoto wake hatakuwepo hapo kushuhudia maiti ya baba yake, mtafuteni huyo mwanamke popote alipo na mniletee mjukuu wangu hapa kwa garama yoyote namtaka mjukuu wangu"!! Aliongea na kuwaambia waendele kumtafuta.



    Hapo hapo waliingia kikosi cha jeshi la polisi kilichokuwa kinaongozwa na IGP Saidi.



    "Tumegundua ya kuwa Naseeb aliuwawa kwa kupigwa bastola tatu katika upande wa kushoto wa kifua chake ila bado hatujajua ni nani muuwaji kama tunavyohisi ni mkewe Samia na pia kuhusu habari za Mtoto bado hatujazipata"



    "Yeyote aliyehusika na mauji ya mwanangu sitamuacha mzima hata kama ni nzii akamatwe na aletwe hapa" aliamuru na kupiga simu mahali huku polisi wale wakiondoka.



    "Haloo hao wapelelezi wa kujitegemea umewapata wangapi, 30 sawa, kazi ianze Mara moja mission yao ni kumpata mjukuu wangu ndani ya masaa 24. Alikata simu na kupiga tena.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " halooo Raisi, Tafadhali naomba msaada wako!!!!!



    Nchi nzima ilichafuka kutokana na msako uliokuwa ukipita nyumba kila nyumba kwaajili ya kumtafuta Samia pamoja na Salhat huku ndege zote zilizokuwa zikitakiwa kusafiri kwaajili ya kwenda nchi za njee zikizuiliwa haikuwa kwa ndege tu Bali hata magari ya kusafiri ya kwenda mikoani meli na hadi pikipiki zote hazikufanya safar yoyote watu wote walitakiwa kuwa nyumbani kwao hivyo hata waliokuwa wakiuza masokoni siku hiyo walifunga.



    "Jamani leo kuna nini mbona hivyo?!??! Waliulizana wanawake wawili waliokuwa wamefunga vibanda vyao na kuanza kurejea nyumbni kwao ambako barabara nzima ilikuwa imepoa hakukuwa na hata kelele ya cm kuita kwa siku hiyo.



    "Siku zote uaambiwa pesa inaongea ni tajiri Matata anamtafuta mjukuu wake baada ya Mtoto wake kuuwawa na mke wake'



    "Heeee wewe usiniambie kwahiyo mwanamke akamuuwa Mme wake kisha akaondoka na Mtoto sindiyo…......…… sasa Kwani alikosa nini kwenye familia ya Mr Matata mbona ipo na kila kitu jaman???!! Aliuliza kwa kutia huruma.



    "Navyosikia ni kuwa mwanaye hakuwa anaishi kwenye nyumba yake alikuwa akiishi kwingne kabisa na mke wake... Na Mr Matata ndye aliyemfukuza mwanaye!!!!"" Aliongea mmama yule.



    "Sasa.......... Kama alimfukuza anamtafuta ya nn tena labda........ Wakiwa wanaendelea kuzungumza hapo hapo mbele yao walikutana uso kwa uso na Mr Matata ambaye sasa aliona kama gari linamchelewesha kumpata mjukuu wake.



    "Mnapenda sana kuzungumza siyo??? Aliwauliza na kuwapita bila kuwasemesha neno. Alikuwa maeneo ya Chekereni na huko ndiko Samia alikopita wakati anakimbizwa na na Badra damu haikuweza kuonekana kutokana na mvua iliyoweza kuendelea kunyesha hata Alama za viatu pia ziliweza kupotea kutokana na kuwa kulikuwa na watu waliokuwa wakiingia sokoni na kutoka, haisi zilizokuwa zikileta abiria na kuwachukua hivyo ilikuwa vigumu kupata ushahidi au kutambua ya kuwa Samia na mwanaye walipita eneo lile.



    Akiwa anatembea mbele zaidi Mr matata alikanyaga kitu kilichomfanya mguu wake ushtuke na kuutoa mguu wake kisha kutizama ni nini amekikanyaga hiyo ilikuwa ni cheni ambayo alimnunulia mkewe Saumu kama zawad baada ya kugundua kuwa ana mimba na alipofariki baada ya kumzaa Naseeb cheni hiyo alimpa mkewe na kumwambia amvalishe mwanaye.



    " hii cheni mwanagu Naseeb ndyo alikuwa nayo!! Imefikaje hapa???! Aliuliza kwa mshangao na kuiokota cheni ile.



    "Tafadhali iweke hapa alizungumza IGP Saidi aliyetoa kitambaa chake na kumuomba Mr matata aweke hapo.



    Mr Matata aliitazama na kuiweka kama alivyoambiwa.

    IGP alipiga simu na kuomba askri baadhi waongezwe kwaajili ya kuja kufanya upelelezi zaidi.





    Hapo hapo aliingia kijana mmoja na kuzuiliwa na mabodyghard wa mr matata.



    "Nina kitu chamaana nataka kuzungumza naye,, mr matata alitoa ruhusa ya kijana yule aachiliwe na aje mahali alipo.



    "Unashida gani???!



    Kijana aliingiza mkono wake mfukoni na kutoka na simu.



    "Yanini??! Aliulizs Mr matata.



    Aligusa simu ile na kumuonyesha picha ya Naseeb akiwa na mwanaye Salhat.



    "Nipe hiyo simu!! Aliongea mr matata baada ya kumuona mjukuu wake.



    "Hapana nataka million 20 ili nikupe kama hutaki naifuta hii picha" alizungumza kijana yule akiwa tayr ameshaanza kugusa kitufe cha kudelete.



    "Hapana nakupa"



    Aliingia mfukoni na kutoa check aliyotaka kuaza kuandika.



    "Hapana mimi siyo mjinga waweza kuninyang.anya pindi nitakapokupa simu hii"



    "Hapana niamini mimi!sitafanya chochote kile na utakuwa salama nipatie picha ya mwanangu na mjukuu wangu.



    Kijana yule alitoa simu ile na alipewa pesa yake kama alivyoahidiwa hpo hapo alikamatwa.



    "Itabidi ukalisaidie jeshi la polisi umeipata wapi hii simu. Alimkamata IGP na kuondoka naye eneo lile.



    *** **** ***



    Baada ya muda kupita Badra akiwa ndani ya nyumba yake alishngaa baada ya kuona picha zake zote alizozigaramikia na kuziwekea nakshi za kutosha zikitolewa na kubandikwa picha nyingne.



    " nyie mnafanya nini aliuliza baada ya kuona watu waliokuwa wageni katika upeo wa macho yake.



    Alishuka ngazi haraka haraka na kwenda kutizama hizo zilikuwa picha za Salhat zilizokuwa tayri zimesharembwa na kuwekwa kwenye fremu Kubwa kabisa na nyingne akiwa na baba yake.



    "Nilisema tu nilijua tu haka katoto cha huyu jini haka!!! Aliongea kwa hasira na kuyatoa macho yake kwa hasira na ghadhabu.



    ***** ****** ****



    Huku nako Samia akiwa na Lidia wakiwa wamerejea baada ya kukuta hakuna magari yoyote yanayosafiri kuelekea mikoani kwa siku ya Leo.



    "Samia nakuamini naamini hujafanya vile wanavyosema ila kasheshe ni kwamba utatokaje hapa, ungemrudisha huyu Mtoto kwa babu na wewe uangalie jinsi ya kujisaidia kwa maisha yako Kwani sasa yako hatarini.



    "Lidia, siyo kwamba napenda haya maisha ya mihangaiko hapana lakini sina cha kufanya wala siwezi kumpeleka mwanangu kule,Kwani nitakuwa nimemuuwa mwanangu mwenyewe" alizungumza na kumtizama Lidia ambaye alibaki akitizama.



    "Inabidi nirejee tu nyumbani na nikapokee adhabu yoyote nitakayopewa na hiyo ni kwaajili ya usalama wa Salhat wangu" alizungumza na kumtizama Salhat aliyekuwa amelala.





    " itabidi tumzike Kwani hatutaweza kusubiri siku nyingne zaidi!! Aliongea shehe ambaye aliamuru maiti ya Naseeb ichukuliwe na kuanza kufanyiwa utaratibu wa mazishi.



    Mr Matata ndye ambaye alishindwa kuelewa mtoto wa mwanaye Yuko wapi sasa!! Kwani tayri alishamtafuta bila mafanikio yoyote, alishindwa kuizuia maiti ya mwanaye isizikwe Kwani hakuwa na lakufanya tena.



    "Abdul nakuahidi mwanangu nitamtafuta Mtoto wako na nitamlelea mimi" aliongea huku akitizama nguo za Salhat na baadhi ya vitu vilivyoletwa baada ya kupatikana katika nyumba waliyokuwa wakiishi.



    Badra alitizama kwa hasira sana Kwani kila kitu sasa katika jumba lile kubwa la kifahara lilitawaliwa na Salhat pasina uwepo wake.

    Aliingia ndani ya chumba chake na kutizama chumba kuzima hakukuwa na Mtu alitoa kijiti ndani ya kabati lake na kukupiga mlangoni kisha akapotea katika hali ya kutatanisha sana.



    Alitokea katikati ya msitu ambao miti yake majani yake yalikuwa vichwa vya watu huku ardhi yake ikitawaliwa na mifupa ya binadamu, mito yake ikiwa inatiririsha damu kwa wingi pasina kukoma alipofika mtoni hapo pembeni yake kulikuwa na kiganja cha mkono wa Mtu ambapo alikichukua na kukitekea damu ile kisha kuinywa na baada ya hapo alipotea tena na kutokea sehemu nyingne.

    Huko alikotokea sasa kulitawaliwa na nyoka kila mahali waliokuwa wazima wakipisha katikati ya miguu yake na wengine wakimpanda.

    Kitendo hicho hakikuweza kumtishia Kwani tayri alishawazoea na huwa anakuja kila Mara anapohitaji msaada zaidi. Alitembea hadi kufikia Mti mmoja ulioko pekee yake na uliochongoka kisha kutoa shepu ya mlango alipofika hapo aliinama na kuingia ndani hatimaye Mti ule ulijifunga na hakukuwa tena na alama yoyote ya mlango wala Mti wowote pale.



    Alitokea sehemu nyingne akiwa tayri ameshavalia mavazi meusi yani akiwa amejifunga kaniki ambayo ilianzia kifuani na kuishia juu ya magoti yake cheni zilizoweza kubebana ndani ya shingo yake pamoja na bangili zenye rangi nyeusi huku akisindikizwa na ngozi yenye rangi nyeusi miguuni mwake na kuonekana kama vikuku ndan ya miguu yake yote miwili.



    Alitembea kwa hatua kadhaa baada ya hapo alifika mahali na kupiga magoti.



    "Nimewasili eeee malikia wa kuzimu wa ukoo wetu wa Abandandi Alizungumza kwa heshima Kubwa sana huku akiwa amekiinamisha kichwa chake.



    "Nimepokea heshima yako Mtoto wa malikia wa kuzimu wa ukoo wa Abandandi" alijibu mwanamk Yule ambaye aligeuka na kuweza kuonekana sura yake ikiwa ya kutisha na kustaajabisha Kwani ilikuwa imejaa mabaka ya nyoka na macho makali sana yenye kuwaka mithili ya pakaa.



    "Razzio kwanini mpka sasa umeshindw kumuuwa yule adui yetu kwann mpaka sasa Yuko hai!!!?? Aliuliza malikia wa kuzimu.



    "Nisamehe malikia wangu, ila nilijitahidi kwa kila mbinu ikashindikana Kwani kwa mbinu za kishetani hatumuwezi hata za kibinadamu pia ziligonga mwamba" aliongea Badra ambaye jina lake la kuzimu ni Razzio.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Tulikupeleka duniani mapema kwaajili ya kuidhibiti nyota ya Naseeb ambayo ingeweza kumleta mshindani mkubwa katika ukoo huu wa Abandandi, tulitumia nguvu zetu nyingi kukupeleka duniani na kukupa sura ya kibinadamu kwaajili ya kumuulia mbali Naseeb lakini ulishindwa kutokana na upumbavu wako wa kumpenda binadamu, tukakupa sharti la kulala naye ili umchafulie nyota yake hilo nalo ulishindwa na ukaishia kulala na baba yake ambaye hana faida kwetu. Pia ukashindwa zuia asikutane na msichana ambaye anatoka koo pinzani na sisi na hatimaye wakampata Mtoto atakayekuwa tishio kwa ukoo wetu sasa hata huyo mtt kummaliza umeshindwaaa!!!!, alizungumza kwa kueleza na kwa hasira zaidi malikia huyo wa kuzimu.



    "Kama kazi imekushindana sasa nitaenda mimi mwenyewe duniani kwaajili ya kupambana naye" alizungumza na kusimama juu yake chake na hapo ndipo tulipogundua ya kuwa hakuwa na miguu ya kawaida Bali miguu ya mikono ya wanadamu.



    ***** ****** *****



    Tukirudi duniani Mwili wa Badra ulikuwa uko kitandani tu pasina kujigusa wala kufanya chochote kwasababu nafsi yake tayri iisharudi kuzimu na alipatiwa adhabu baada ya kushindw kufanya kazi aliyopewa na mama yake.



    ***** ***** *****



    Samia aliwaaga na kuamua kuondoka.



    "Sasa lakini utawezaje kutoka hapa watu wamejaa kila mahali wakikutafuta wewe na nihatari sana" aliongea Joseph.



    "Sasa tutamsaidiaje mume wangu?? Aliuliza mkewe Lidia.



    Samia alitabasamu na kuwatizama kisha akayazungumza haya yafuatayo.



    "Hakuna Mtu atakayekuwa na uwezo wa kuniona kama mimi sijataka yeye anione labda mpaka awe na imani Kali sana"



    "Unamanisha nini?? Aliuliza Lidia.



    "Mimi siyo binadamu!! Alizungumza na hapo hapo alijibadilisha katika umbile lake la kijini.



    Alivaliaa gauni jeupe ndefu mpaka chini taji lililoweza kurembwa na mauwa ya kila rangi likiwa limezunguka nywele zake ndefu zilizokuwa kichwani mwake na kujiachia mpka kufika makalioni mwake uso wake ulioweza kurembeka kwa nakshi nakshi za Mtoto wa kike na harufu Kali ya marashi iliyoweza kupenya katikati ya tundu zao mbili za pua baina ya Lidia na Joseph.



    Walibaki wakimtizama na kushindwa kuelewa ni kipi kinatokea mbele ya macho yako.

    Ni kweli Samia hakuwa binadamu Bali ni Jini aliyeweza kutoka katika ukoo wa Sultan Shariphu baada ya kumpenda Naseeb na kuamua kuishi naye maisha ya kawaida kama waishivyo binadamu wengine.



    **** ***** ***** ****



    Katika kitu ambacho kilimshangaza Mr matata ni picha za Samia Kwani ziliweza kuonekana kwenye simu tu lakini alipotaka zitolewe katika majarida kwaajili ya kuandika matangazo ya kuwa anatafutwa hazikuweza kutoka kabisa.



    "Kwanini iwe hivi alijiuliza wakati huo akiwa hospitalini na akiwa amekaa pembeni kabisa ya Badra ambaye hakuwa yeye Bali mwili tu alioutumia pindi anapokuwa duniani.



    Hapo hapo dactar aliingia jina lake aliitwa Hassan huyu alikuwa dactari bingwa sana na alijulikana Africa nzima kutokana na kazi zake za kuweza kufanya operation pasina Mtu yoyote aliyemfanyia operation kupoteza maisha.



    "Ammmnhhh Mr matata najaribu kulitizama ni lipi tatizo la mkeo lakini nimeshindwa kugundua Kwani tumepima vipimo vyote na hatujaona sehemu yoyote yenye tatizo Kwani blood pressure yake iko normal, mapigo yake ya moyo yako kawaida tu presha pia iko kiasi, labda nahisi kafaint kutokana na mawazo yake kuwa mengi ila atarejea katika hali yake ya kawaida baada ya kurelax hivyo ungeweza kumpeleka tu nyumbni kwaajili ya kuendelea kupumzika zaidi aliyatoa maelezo hayo na kumpatia Mr matata.



    "Sawa docta Hassan nakushukuru lakini kuna jmbo lingne linaniumiza kichwa sana ni kuhusu hii picha aliitoa simu na kumuonyeshea picha ya Samia.



    "Nashangaa kwanini haitaki kutoka ndani ya hii simu ikiwa na hali hii hii Mara ukiweka katika laptop utaona picha zote hizi zake hutoziona nikitaka itoke katika majarida picha zake hazionekani vizuri hili nalo litakuwa tatizo gani ???!! Aliuliza baada ya kuhisi hilo nalo laweza kujibiwa na docta Hasan.



    Dr alizitazama zile picha kisha akamtizama Mr matata ambaye alionyesha anahamu kubwa kulisikia jibu lake.



    "Kwa kweli sijui" alijibu tu kwa ufupi kisha akamwambia.

    "Mr matata nafikiri hata wewe hali yako siyo nzuri basi naomba nikufanyie vipimo kidogo" alizungumza Dr Hasan baada ya kuona ya kuwa Mr matata anachokizungumza hakiwezi kuwa ni cha kweli. Ila alizungumza ukweli mtupu na picha hizo za Samia alibahatika kuziona yeye mwenyewe tu ila watu wengne waliona ni peusi tu hivyo walifikiri ya kuwa mzee huyo anaanza kuwa kichaa.



    **** ***** ***



    Samia akiwa na mwanaye na kuelekea ngomeni kama alivyosema alianza kuona miti mingi ikicheza huku upepo mkali ukivuma.



    "Jitokezee, sipendi kupigana Vita vya mafichonimekwambia jitokeze"



    Ghafla ulisikika mlio wa Mtu kutua nyuma ya mgongo wake na hapo Samia taratibu kabisa alianza kugeuza shingo yake na kutaka kujua ni nani huyo"



    Ni baada ya Samia kuhisi kuna Mtu na hatimaye alikisikia kishindo nyuma yake.



    Aligeuka akiwa makini na hapo hapo alisikia jina lake likitajwaa.



    "Samia!!!!! Aliitwa.



    Alishtuka baada ya kuhisi ya kuwa sauti ile anaitambua vyema kabisa.



    "Samir!! Aliita na kugeuka hapo alikutana uso kwa uso na mdogo wake.



    Samia na Samir walikumbatiana Kwani ni miaka mitatu sasa tangu Samia aondoke ujinini katika ukoo wa Sultan Shariphu.



    "Unaelekea wapi huku???! Aliuliza Samir baada ya kumaliza kusaidiana.



    "Naelekea ngomeni sasa, nahitaji kuyaokoa maisha ya mwanangu Salhat Kwani wanataka kumuangamiza!!



    "Wakina nani hao??! Aliuliza Samir.



    "Ukoo wa Abandandi wamemtuma Mtoto wa malikia kwaajili ya kumuangamiza mwanangu ila nimepambana nao mpaka sasa Salhat wangu Yuko hai!!



    "Ukoo wa Abandandi???! Kwanini unataka kumuangamiza Mjomba wangu?! Aliuliza huku akimchukua Salhat katika mikono ya mama yake na kuanza kumtizama.



    "Lakini Dada huwezi kurudi ngomeni Kwani Sultan anahasira sana na wewe baada ya kukataa kuolewa na mwanaye Sadick kisha kwenda kuolewa na binadamu!! Alizungumza Samir.



    "Samir huyu ni Mjomba wako lazima uhakikishe anakuwa katika hali ya usalama hata kama lolote litanikuta mimi, ila usiache baya lolote limtokee Salhat wangu. Kwani huyo ndiyo urithi pekee niliyoachiwa na mume wangu Naseeb.



    Alizungumza huku akianza kuyafuta machozi yake yaliyokuwa yakimtoka alianza kupiga hatua mbele ila alihisi upepo ambao siyo wa kawaida na hapo hapo alipigwa kibao cha kichawi na kujikuta ameenda akajigongeza kwenye Mti mgongoni mwake kisha mwikaruzo ya damu ikianza kumiminika mgongoni mwake.



    Alirusha kibao kingne ila tayari Samir Alishamuona hivyo alikwepa yeye na kuanza kumkwepesha Salhat kisha akajiweka sawa na kumuweka Salhat katika hali ya usalama baada kumkwepesha kibao kile cha kijini.



    Alikuwa mama yake Badra akiwa katika sura yake halisi uso wenye magamba ya nyoka pamoja na miguu yenye mikono ya Mtu ndyo iliyowastajabisha Samia na Samir.



    "Ni nini hiki??! Aliuliza Samir na kutizamana na ndugu yake.



    "Samir mpeleke Mtoto ngomeni mimi napambana naye!! Alitoa amri hiyo Samia huku akimtizama Malikia ambaye alikuwa mgeni kwake na ilikuwa ngumu yeye kutambua ya kuwa ni mama yake Badra.



    Samir alianza kukimbia na Salhat huku nyuma nako Malikia aliwachilia miale ya radi na moto iliyokuwa ikimfuata nyuma Samir na kumkosa kosa.



    Malikia wa Abandandi alimshika Samia na kuanza kumnyonga Kwani Samia hakuwa na nguvu za kutosha mbele yake na upungufuu huu ulitokea pale ambako aligundua anamimba ya binadamu. Samir aliondoka na kufika mbali sana lakini alimkumbuka Dada yake na kugundua ya kuwa hawezi kuwa na nguvu za kutosha kwaajili ya kupambana na Jini yule wa kuzimu aliyoweza kuwatokea. Alimuweka Salhat maeneo ya karibu kabisa na ngomeni kisha akaanza safari ya kurudi baada ya kuhisi hapo alipomuweka Salhat atakuwa katika hali ya usalama.

    Ila wakati anarudi na kumfuata Dada yake Sadick Mtoto wa sultan Shariphu alimuona na kumfuata Salhat mahali alipoweka kisha akamtizama na kutabasamu huku akisema huyu nahisi tu ni Mtoto wa Samia aliongea na kuanza kutabasamu huku akimchukua Mtoto na kumuingiza ndani ya ngome zaidi kwaajil ya usalama wake pasina yeye mwenyewe kujua akiwa anaelekea ngomeni kwao ghafla alipatwa na muale wa moto katiba ubavu wake wa kushoto aligeuka nyuma na kutizama.



    "Lilikuw jeshi la ukoo wa Abandandi waliokuja kwajili ya kuuteketezea mbali ukoo ule pamoja na Salhat Kwani ndye atakayekuwa kikwazo kwao pindi atapokuwa mkubwa.



    "Hawa maadui wametoka wapi alizungumza huku akianza kurudisha mashambulizi na kutoa taarifa ya kwamba kuna hatari hivyo kuwafanya waliokuwa ngomeni nao waanze kujipanga katika kuwakabili wapinzani wao.



    Sadick kwa nguvu na uwezo alionao aliweza kutengeneza kitu kama mfano wa yai kisha akamuweka Salhat ndani humo na kuweka sehemu ambayo alihisi hakuna Mtu atakayeweza kumgusa.



    Walipigana wakapigana na kupigana hatimaye baada ya mud maiti nyingi za ukoo wa Abandandi pamoja na maiti kadhaa za ukoo wa Sultan Shariph zilikuwa chini huku Samia akiwa ameletwa kwaajili ya kutibiwa na akiwa anavuja damu mwili mzima.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nilisema sitaki kumuona huyu Samia huku ngomeni mnaona ujio wake tu tayri unatusababishia sisi matatizo alizungumza malikia wa ngome ile jina lake Kuruthumu.



    Sultan Shariph alimtizama mkewe na kumtizama Salhat aliyekuwa Yuko chini huku viumbeu wenzake wakijitahidi kumkamulia dawa na kumpatia dawa zaidi.



    Sultan aliwaambia waondoke kwa kukaa mbali na hapo kisha akanza kumtoa sumu iliyoingia ndani kwa kutumia nguvu zake nyingi.



    "Sultan !!!! Watu wote walishangaa na kuanza kumtizama Sultan. Sultan alijitahidi hadi alipohakikisha ameitoa sumu yote iliyokuwa ndani ya mwili wa Samia.



    Alitapika damu na kudondoka chini Kwani alitumia nguvu zake nyingi sana katika kutekeleza jambo hilo.



    ******* ******** ****



    Bado Mr matata alikuwa akimtizama mkewe Badra aliyekuwa bado katikati ya usingizi mzito huku akitafakari mambo yake mengine akiwa pale hospitalini alirudishiw majibu na vijana wake wote pamoja na maaskari kwamba wameshindwa kumpata Salhat.



    Mr Matata alibaki tu akiwa tizama huku akijitahidi machozi yake yasitoke mbele ya wafanyakazi wake.



    Hapo hapo aliingia Frederick huyu alikuwa rafiki mkubwa sana wa mwanaye Naseeb baada ya kupata taarifa za kifo cha Naseeb alikuwa karibu sana na baba yake Naseeb.

    Aliwa ishara watu wote waondoke ndani na walifanya hivyo wakati huo wote mr matata alikuwa akitizama chini huku akiihurumia nafsi yake na kujiona kama mwenye mkosi, nuksi na balaa.



    Alisema Salhat. Jina hillo alilitamka Frederick na kumfanya Mr matata amtizame.



    "Jina la mjukuu wako ni Salhat hillo ndilo jina alilopewa na baba yake" alimalizia kwa kuongea hivyo.



    "Salhat!!! Alilirudia jina hilo na kutabasamu huku machozi yakiwa tayri yamesha lowanisha mashavu yake.



    "Salhat ni jina la mama yangu, Naseeb kaniletea mama yangu tena duniani............. Sasa Yuko wapi jamani mbona nimeshatumia nguvu zangu zote kumtafuta lakini sijampata mpaka sasa hakuna jambo ambalo sijalifanya kwaajili yake labda kwenda kwa waganga tu ndo ambako sijafika lakini tyr nimeshatumia majeshi wanapolisi na raia katika kumpats mjukuu wangu ila bado ni ngumu na nimeshindwa kumpata *alijielezea* Mr matata.



    "Hapo nimekuelewa twende nitakuonyesha njia ya kumpata Mtoto wa Naseeb" alizungumza huku akianza msafara na kumfanya Mr Matata aanze kumfuata nyuma pasina kipingamizi.



    Walitembea kwa gari na hatimaye walishuka na kuanza kutembea kwa miguu huku wakikatizana katikati ya majani mengi pamoja na vimiti vidogo vidogo vilivyovyembamba Mr Matata wala hakutaka kuuliza kwamba anapelekwa wapi yeye uwepo wake wa akili wote ulikuwa unawaza afanikiwe huko anakopelekwa.



    Hatimaye alianza kusikia kelele zisizoeleweka masikioni mwake kama vile yalikuwa majadiliano ya watu waliokuwa wakigombana vikali huku akisikia jina la "huyu Mtoto wa huyu binadamu hastahili kuishi hapa" hakuwezs kutembea zaidi kutokana na kelele nyingi alizoendelea kuzisikia masikioni mwake hatimaye alidondoka chini kwa kupiga magoti huku huku akiziba masikio yake.



    Frederick alirudi nyuma na kutaka kwenda kumgusa lakini alikatazwa na mganga aliyetokea huku akiwa amevaa nguo zake kuhukuhu na akiwa haoni kabisa Kwani macho yake yakiwa kama vile yalishatolewa miaka mingi iliyopita.



    Mr matata alijikuta Yuko sehemu ambayo ilikuwa na watu kama yeye lakini hakuna aliyekuwa akimsemesha Kwani walikuwa wakijadili juu ya jambo Fulani huku wakiwa wamemzunguka kama Mtu alijitahidi kupenya na mbele alimuona Mtoto ambaye alikuwa akizungumziwa alipotizama alimuona ni Salhat.



    Mjukuu wangu aliongea huku akitaka kwenda kumshikaa ila aliisikia sauti ya Mtu ikimkataza pasina kumuona.



    Hapo hapo alimuona mwanamk alikuja na kumbeba Salhat alikuwa Samia.



    "Kama hamtahitaji mwanangu aishi hapa sitaweza kuishi hapa pia kila alipo Salhat wang nami nitakuwa naye Kwani ni mwanangu mmi hata kama ni binadamu" maneno hayo aliyazungumza Salhat na hapo hapo alianza kuhisi ya kuwa kuna harufu ya binadamu mwingne tofauti na Salhat wake.



    "Lakini..............



    Shshshhshsshshshsh Samia alimnyamazisha mdogo wake aliyekuwa anataka kuongea kisha kuanza kunusa upande ambao Mr matata alikuwepo.



    Mganga yule alimrudisha mr matata sehemu aliyoko.



    "Huyu jina anahisia Kali sana endapo ungekamatwa basi ungekwisha!!! Alizungumza mganga yule akimwagia dawa kwaajili ya kumpotezea harufu Samia.



    .."namtaka mjukuu wangu Tafadhali mrudishe kwangu, nitakupa kila kitu utakachokihitaji ila namuomba mjukuu wangu Tafadhali.aliomba sana Mr matata.



    " unauhakika utanpa kile nikiombacho!!??



    "Ndyo chochote!!! Alizungumza kwa haraka



    "Npe mjukuu wako alizungumza huku akimtizama Mr matata ambaye aliacha kuzungumza na kumtizama kwa macho ya hasira.



    Ni baada ya mganga yule kumuhitaji Salhat kama ujira wake.



    "Unaweza????! Aliuliza.



    "Sasa nitawezaje kukupa tena mjukuu wangu ilihali yeye ndiye aliyefanya mimi nikawa hapa, Tafadhali niombe kingine. Aliongea Mr matata.



    Mganga yule alitabasamu na kumwambia



    "Kumchukua sio shida, shida ni kumtoa sehemu aliyopo na kumfikisha hapa ulipo kisha kumuwekea usalama hiyo ndiyo shughuli Kwani anakuwa salama zaidi pindi anapokuwa mikononi mwa mama yake.



    "Wewe kama unaweza kumtoa na kumleta hapa nilipo Fanya hivyo hayo mengine nitashughulika mimi mwenyewe!!!! Alizungumza Mr matata



    "Usifikirie ni kirahisi hivyo Mr matata na usije ukanilalamikia mimi kwamba sijakuonya" alizungumza babu yule aliyezeeka kisha akapiga mguu wake chini na kukatokea zulia lekundu na mkia wenye rangi nyekundu alikaa chini na kupapasa kisha akachukua mkia ule na kuupiga chini hapo palitokea vitu vingine zaidi vya kiganga na akaanza kunena mambo yake mengine.



    Hapo hapo alimuita Mr matata na kumwambia akae kwenye zulia lile. Baada ya kukaa alimpa taarifa ambazo alizisikia mzee matata mwenyewe kisha akampiga na mkia ule wa kichwani hapo hapo mwili wake ulipotea na kutokea ngomeni kwa Sultan.

    Wakati huo mzozo ulikuwa mzito baina ya Samia na majini wenzake waliotaka Salhat aondolewe lakini yeye aendelee kuishi pale.



    "Nimesema nitarudi duniani na mwanangu!! Aliendelea kuzungumza.



    "Hakuna ruhusa ya wewe kuondoka tena ndani ya hii ngome Kwani tayari umeshafika na unaelewa mila na taratibu za koo wetu" alizungumza Malikia aliyeonekana kumchukia sana Samia.



    "Kama ni hayo matatizo acheni yanipate mimi lakini mimi siwezi kumuacha mwanangu duniani kisha mimi nibaki huku"



    Hapo hapo aliingia Samir.



    "Dada!!!!! Aliita



    Wote waligeuka na kumtizama.



    "Salhat hayupo pale ulipomlaza" alizungumza na kufanya watu wote washtuke kisha kuanza kuelekea kule kwaajili ya udhibitisho zaidi.



    Ni kweli hakukuwa na Mtu yoyote pale.



    Samia aligeuka na kumtizama Kuruthumu kwa hasira.



    "Usiniingize mimi katika hillo Kwani tulikuwa wote tukijadili kuhusu swala la uwepo wake ngomeni" alizungumza Kuruthumu.



    Wakati huo upande wa pili tayari Mr matata alikuwa na mjukuu wake mkononi mwake.



    "Kafanana sana na mwanagu Naseeb alivyokuwa mdogo kafanana naye sana jamani! Alizungumza huku machozi yakimtoka na kuendelea kumtizama usoni mwake.



    Mganga alitoa kitu kisha akakinenea maneno kadhaa na kumpatia Mr matata.



    "Kwaajili ya usalama wake mvalishe mkononi mwake na uhakikishe ya kuwa hakitakaa kimtokee kabisa mkononi mwake endapo utamtoa basi utayahatarisha maisha yake kwa kiasi kikubwa Kwani huyu anakazi kubwa sana miaka ya mbeleni na faida katika dunia nzima"



    Mr matata alikipokea na kumvisha wakati akiyafanya hayo katika ngome ya Sultani waliweza kumuona kwa ukaribu zaidi Mr matata akiwa na Salhat.



    "Amewezaje kuja kumchukua mwanangu bila ruhusa yangu na kuondaka naye chochote kitakachompata mwanangu sitamuacha hai iwe yeye au huyo aliyemsaidia kumtoa mwanangu katika ngome hii" alizungumza na kuanza kuondoka.



    "Samia hutaruhusiwa tena kutoka ndani ya ngome hii Kwani tayri ulishaingia na unastahili adhabu kwa Yale uliyoyafanya takribani miaka mitatu sasa alizungumza Sultan Shariphu na kuwaamuru walinzi wake wamkamate Samia na kumpeleka sehemu ambayo angeweza kuzipata adhabu zke.



    "Sultan nitafanya vyovyote vile upendavyo lakini Tafadhali kwanza naomba nikamchukue mwanangu" aliomba Samia lakini Sultan aliwatizama na kuwambia wamshike na kumpeleka kwenye adhabu Kuruthumu alimtizama na kucheka chini kwa chini.



    Samia alikamatwa na kupelekwa huko wakati huo Sadick pamoja na Samir hawakuridhika kwa tendo lile lililokuwa likiendelea mahala pale.



    ***** **** ****

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Pumbavu kabisa ukoo wa Sultan umewezaje Kutushinda nguvu., nyie wote ni bure kabisa bure yani......na huyu mwanamke huyu ciwezi kumuacha kabisa nitapambana naye tu na hako katoto kake alizungumza na kumalizia.



    "Nitakaulia mbali kabisa!!!!!! Yuko wwapi huyo mpuuzi Razzio aliongea malikia akimwita mwanaye Badra.



    Badra alifika na kumtizama mama yake aliyekuwa ameumia vibaya sana katika mwili wake na akiwa na makovu mengi.



    "Unaona mwili wangu ulivyokuwa unajua ni kipi cha kufanya kwaajili ya kunirudishia nguvu zangu"



    "Ndyi malikia wangu alizungumza na kutoka hapo kisha kuwachagua wenzake sita na kuchukua mitungi yao ambayo tayari haikuwa na kitu ndani walitizamana kisha wakapotea na baadaye walirudi mitungi hiyo ikiwa imejaa damu kabisa walimiminia sehemu ambayo malikia huwa anaogea na baada ya hapo Malikia alivua nguo zake na kuingia ndani ya zile damu kisha kupotea kabisa humo ndani kwaajili ya kurudisha nguvu zake zilizopotea na kuufa ya mwili wake uwe katika hali ya kawaida.



    ***** ***** *****



    Huku nako duniani Mr matata akiwa na mjukuu wake alimremba pasina kifani na kumfanyia part bila kujua ya kuwa alikuwa akihatarisha maisha ya Salhat.



    Kwani tayari Badra alishapata taarifa ya kuwa Salhat hayuko tena ngomeni Bali Yuko kwa Mr matata hali hiyo ilimfanya yeye arudi duniani kwaajili ya kumuulia mbali sasa Salhat.

    Wakati huo bado Samia alikuwa ndani ya kifungo kizito akiendelea kutumikia adhabu Zake.



    Sultan alionekana akiteta Jambo na Sadick pamoja na Samir kisha akawaamuru waondoke.



    Wakiwa njiani Sadick alimkumbusha Samir



    "Sultan amesema tuhakikishe ya kuwa Salhat anakuwa katika hali ya usalama Kwani yeye ndy mkombozi wetu, na tumpeleka katika ukoo wa Sultan Kareem akalelewe huko alizungima Sadick na Samir alitingishwa kichwa kumaanisha ya kuwa amemuelewa.



    Huko nako safari ya majini wengine waliotoka katika ukoo wa Abandandi walikuwa wakizungumza.



    "Malikia amesema anahitaji kichwa cha Salhat haijalishi itatugarimu kiasi gani na tukikosa tusirudi tukiwa hai hivyo lazima tuitimize haja yake..





    Hatimaye msafara wa kwanza kufika ulikuwa wa Sadick na Samir wakati huo Salhat alikuwa mikononi mwa babu yake ambaye hakuhitaji hata kumshusha wala kumuweka chini.



    "Tutafanyaje sasa tunahitajika kumchukua Salhat kwaajili ya usalama wake!!! Alizungumza Samir.



    "Cha kufanya ni tuvae miili ya binadamu kisha tujiunge nao kwenye party hii hadi pale tutakapopata muda muhafaka wa kumchukua"alizungumza Sadick ambaye hapo hapo alijivisha umbo la binadamu kisha akafuatiwa na Samir na kuelekea kwenye party muda ule ule baada ya wao kutoka eneo lile waliingia kikosi cha Abandandi na wote walikuwa watoto wa kike.



    "Tufanyaje sasa mbona Yuko mikononi mwa babu yake???!



    "Tuvae maumbo ya kibinadamu kisha tuingie kwenye party hadi pale babu yake atakapomuweka chini kisha tutamuulia mbali.... Alijibu mmoja kati yao.



    "Lakini Razzio Yuko wapi yeye alitakiwa ashirikiane nasi ili haraka haraka tummalize huyo Mtoto"



    ***** ****** *****



    Ndani ya ngome Salhat aliendelea kumuomba mfalme aende kumchukua mwanaye Dunia Kwani ni hatari akiwa huko"

    Sultan hakusema neno zaidi ya kumtizama tu.



    Huku Kuruthumu akiendelea kutabasamia tendo lile la Sultan kutokumjali Salhat.





    **** ***** ******



    "Nahisi kuna majini ndani ya hii karamu!! Alizungumza Sadick na kuanza kunusa.



    Huku nako Samir akijitahidi kutizama huku na huko aliwaona wasichana wanne ambao alihisi ni majini.



    Alimficha Sadick kisha akaanza kusema "nahisi wametoka katika ukoo wa Abandandi na nimewaona wanne cha kufanya hapa ni tumchukue Salhat hata kama ni kwa kumpora ili tu awe salama!! Walishauriana huku wakianza kuwakwepa na kujimwagia vinywaji ili wapoteze harufu ya kijini waliyokuwa nayo.



    "Unashida gani mbona unashangaa shangaa sana??? Aliuliza mmoja kati ya watumishi waliotoka katika ukoo wa Abandandi



    "Nahisia ya kuwa kuko na majini zaidi ya sisi humu ndani!!!



    "Ni kweli na Jini alioko tofauti na sisi siyo huko ulikopeleka macho alimgeuza na kumuelekezea upande mwingine alioko Badra.



    "Yule pale kwahiyo acha upuuzi na tumchukue Salhat kabla watu wa ukoo wa sultan hawajafika hapa alizungumza na kuanza safari ya kueleka mahali aliko Salhat na wakati huo nao Samir alikuwa akielekea upande aliosimama Mr matata kwaajili ya kumpokonya Salhat na kuondoka naye kabla hajafika bahati mbaya alimwagikiwa na kinywaji na huyo aliyefanya hivyo ni Badra alifanya makusudi kummwangia ili kumzubaisha na kumfanya mtumishi wake afike kwa haraka.



    "Pole kaka angu alizungumza huku akiwa anamfuta futa na kumzuia asiende mbele"



    "Sawa Dada angu naomba uniache niendee sasa"



    "Lakini nimekumwagia nimekuchafua labda njoo ndani nikakufulie'



    Samir aliushika mkono wa Badra na kumwambia



    "Dada angu nimeshakwambia Niko sala.........." Kabla hajamalizia sentensi yake kwa kumtizama tu vidole alitambua ni Jini na wakati huo nao Badra aliyatoa macho yake makubwa na makali sana kumtizama Samir huku akimzuia ili asiende mahali wakati huo msichana yule alishamfikia Mr matata na kupeleka mkono kwajili ya kumchukua Salhat ghafla alipiga kelele na kudondoka chini damu zilianza mtokaa mdomoni na masikioni hapo hapo alipoteza maisha.



    Hapo watu wote walistaajabu na kuanza kushangaa huku wengne wakitimua mbio Kwani hawakuelewa ni kipi kimetokea hapo hata Mr matata alishangaa kilichomfanya huyo binti akafa kama anavyofikiri yeye ni nini??! Lakini kilichomsaidia Salhat ni kutokana na ushanga ambao Mr matata alipewa kwaajili ya ulinzi wa Salhat bila wao wenyewe kujua kitendo kile kiliwashangaza sana majini waliobakia kisha wote wakayatupa macho yao kwa Salhat aliyekuwa akilia huku akifikicha mikono yake usoni mwake.



    Baada ya majini walioko pale kuuona ushange ule wote walishtuka na kurudi nyuma kwa uwoga wa dawa ile Kwani wanatambua ya kuwa wakicheza watafariki kabisa.



    Sadick aliingia katikati ya hisia Kali kwaajili ya kufanya mawasiliano ya hisia baina yake na baba yake ili amuelezee hali iliyoko huku aliko. Baada ya kukaa kimya ndani yadakika tatu alishtuka na kurudi tena katika uwepo wa binadamu.



    "Imekuwaje!! Aliuliz Samir.



    "Nimeshampa taarifa Sultan......atatuma majini wengine zaidi" alijibu na kuendelea kuwatizama Wakina Badra ambao na wao waliweka kikao chao pembeni kidogo.



    "Taarifa hizi inabidi tumpe malikia" alizungumza mmoja kati yao.



    "Hapana mimi nitajua njia ya kufanya sitaki malikia aingilie hili haka katoto ntakauwa mimi mwenyewe.......pasina usaidizi kama na ninyi hamtaki kusaidian na mimi pia mwaweza ondoka tu. Aliongea Badra na kuwatizama.



    "Mimi nitabaki"



    "Na mimi"



    "Na mimi"



    "Hata mimi"



    "Sasa alijibu Badra na kuchukua simu yake kisha akasema "Game ianze sasa" aliongea hivyo na kukata simu.



    Hapo hapo aliingia msichana au mwanamke ambaye hata na yeye alishiriki katika tendo la kumuuwa Naseeb alikuaa amevaaa nguo kuhukuhuuu na alipofika karibu na Mzee Matata alipiga magoti na kuanza kuomba kazi wakati huo watu walikuwa katika hali ya sintofahamu juu ya kifo cha yule Jini aliyeonekana Mtu kwa upande wao.



    "Wew......mwanamk embu toka hapa nenda katafute kazi huko usiku huu umenitokea wapi unaniomba kazi mimi??! Alizungumza huku akimkwepa na kutoka na mjukuu wake hapo hapo Badra aliingia na kumsimamisha kisha kumkumbatia.



    "Regina hivi ni wewe mbona umebadilika hivyo jamani........nimekumiss sana ulikuwa wapi baba na mama yak wamekutafuta sana......alimgeukia Mr matata ambaye alikuwa akiwatizama tu.



    "Mme wangu hyu ni rafiki wangu wa damu kabisa kutoka kijijin kwetu tafadhali mpatie kazi ya kumlelea Salhat Kwani anaweza kufanya hivyo" aliomba Badra na Mr matata alimtizama tu kisha akatingisha kichwa ishara ya ndyo.



    "Nashukuru sana nashukuru sana jamani, basi naomba Mtoto nimtizame kama ata kuwa anahitaji huduma yoyote ya kubadilishwa nguo Kwani tayari umeshambeba ndani ya kipindi kirefu sana.. Alizungumza Regina.



    Mr matata alimtizama Badra na Badra alimpa ishara ya ampe kwani huyo hanashida kabisa.

    Basi Mr matata alimuweka vyema mjukuu wake na kuanza Kumtoa kwenye mikono yake huku akiwa anamkabithi Regina ambaye sura yake ilianza kuonyesha furahisho ya tendo lile.



    "Wanafanyaje hapo.......huyo atawezaje kuwa ndugu yake wkati yule naye ni Jini aliuliza Samir.



    "Kwa kuwa wao wameshindwa kumshika kutokana na dawa aliyowekewa wameamua kutumia akili ya kumuita binadamu ili wamuulie mbali sasa ngoja nikuonyeshe. Alizungumza Sadick na hpo hapo aligeuka na kuwa umbo la yule mganga.



    Wakati Mr matata ndyo anautoa mkono wake wa kwanza kwaajili ya kumpatia Mtoto hapo hapo alimuona mganga na mganga alimnyooshea mkono na kupotea huyo alikuwa Samir wala siyo mganga na kupotea.



    Mr matata alimtizama Regina na kutabasamu kisha akamchukua tena Mjukuu wake mikononi mwake.



    "Nitaenda mbadilisha mwenyewe"!! Alizungumza na kumfanya Badra na Regina wataharuki.



    "Lakini mme wangu huyo ni Mtoto wakike utawezaje kufanya hivyo ww n

    Mpe tu Regina" aliongea Badra.



    "Nani mjuukuu wangu nitaenda mbadilisha mwenyewe" alizungumza na kuondoka na Salhat pale alienda kuanza kumtoa nguo moja moja huku akianza kumbadilisha japo kuwa hakuwa na ujuzi katika hillo lakini alijitahidi awezavyo.



    "Ana kialama cha kiunoni kama cha bibi yake alizungumza hivyo na hapo hapo alisikia vitu vikidondoka chumba Cha jirani na kile alichokuwepo ndani.



    "Nani wewe!!! Aliita na kuanza kutembea hatua za mbele kisha kuelekea kule ambako vitu vilikuwa vikipasuka. Alitembea hadi alikofika alikuta ni TV imewashwa kwa sauti kubwa alichukua rimoti kwaajili ya kupunga Sauti na hapo hapo alikumbuka kidole alichonyooshewa na mganga yule.



    Alitupa remoti na kurudi ndani mbio mbio na kama alivyohisi ni kweli walikuwa wakimchezea mchezo wala Salhat hakuwa tena pale alipomuweka wakati huo nao Polisi walishafika eneo lile kwaajili ya kuja kuuchukua mwili wa binti yule.



    "Kuna mtu kamchukua mjukuu wangu na ninauhakika bado hajatoka tafadhali wekeni ulinzi..



    "Lakini tumekuja polisi wachache tu hatutaweza alijibi IGP Saidi.



    Mr matata alikimbilia hadi kwenye maiki kwa yeyote atakayeweza kunipatia mjukuu wangu nitampa million 30 kama ujira wake tafadhali nitafutieni mjukuu wangu bado yuko hapa ndani naamini hilo....



    Watu baada ya kusikua hivyo kila Mtu aliingia ndani ya ile nyumba na kila sehemu ambayo walihisi watamuona kimbembe kilikuwa kwa Regina Kwani watu walianza kumtafuta sasa.



    Hapo hapo walisikia kilio cha Mtoto juu kabisa gorofani hivyo watu wote walianza kukimbilia huko hadi Mr matata.



    "Twende" alizungumza Samir.



    "Hapana tusimame hapa Kwani hili ndyo langi pekee la kutokea sisi siyo wajinga kama binadamu" aliongea Sadick na kujificha nyuma ya pazia lililoko pembeni mwake hapo hapo vilisikika viatu vya kike vikikanyaga huku vikiongea na simu na kusema ndyo ninatoka sasa.



    Huku nako watu waliendelea kushindania kupanda juu hali iliyowafanya wengine wadondoke hapo hapo Mr matata alimuona mganga tena mbele ya macho yake na kumpa ishara ya arudi chini wala asipande juu.



    Mr matata alianza safari ya kurudi chini lakini haikuwa rahisi Kwani watu walikuwa wakipanda kuelekea juu hivyo aliutizama umbali wa kutoka hpo mpka chini kisha akajirusha mpka chini aliweza kuumia lakini hakujali Kwani alihitaji mjukuu wake.



    Sadick alicheka tu na kumtizama Kwani yeye ndye aliyekuja kwa sura tena ya mganga na wakati huo Sadick alikuwa na Regina chini aliyekuwa amembeba Salhat huku akimzubaisha kwa maneno...



    "Unipatie huyo Mtoto au unataka niite watu wote wajae pamoja na polis wakukamate na kufanya maisha yako yapotelee mbali gerezani Kwani hata unayemfanyia naye kazi hana uwezo wa kukusaidia wewe katika hilo.



    Hapo hapo aliingia Badra na kumwambia akimbie na Mtoto wala asijali kuhusu Samir Kwani hawezi mzuia kwa kufanya lolote lile.



    Regina alifanya kama alivyoambiwa Samir baada ya kuona Sslhat anatolewa njee alimpa taarifa Sadick naye alifika eneo lile.



    Wewe Mtoto wa kike usitake kutupima nguvu zetu alizungumza na kuaanza kuunganisha nguvu zao kwaajili ya kumzuia ila kabla hawajamtumia tayri walishapigwa na majini wngine waliokuwa wako eneo lile.



    Regina alitoka na Salhat njee bahati mbaya alijikwaa na kudondoka tendo lililofanya Salhat achomekee mkononi mwake na kwenda kuangukia kisiki kilichokuwa karibu na njee ya nyumba ile na kumchoma Salhat cha mgongo hadi kutokea tumboni wakati huo nao polis walioongezwa tayari walishaweza kufika pale na kumkamata Regina huku nako Mr matata ndo akiwa wa kwanza kufika pale.



    Alianza kupunguza mwendo baada ya kuhisi kama vile anaota wakati huo askri mmoja alienda kutizama kama Salhat mzima au lahh!!!!



    Alitingisha kichwa ishara ya kwamba Salhat ameshafariki.



    Hapo sasa Sadick na Samir walitizama huku wakiwa na majonzi mazito moyoni na wakati wote walimfikiria Samia.



    Hali hiyo ilikuwa furaha kwa wafuasi wa Badra kwani sasa kila kitu waliamini kimeenda sawa na hakutakuwa na mtu tena wa kutetea ukoo wa Sultan wala kuuharibu ukoo wao.



    Mr matata ndiye aliyeanza kuchanganyikiwa kwani sasa alikumbuka maneno ya mganga na ndipo alipotambua maana yake...kwamba hana huwezo wa kumlinda Salhat bora amuache kwa mama yake., akifikiria kuhusu mwanaye Naseeb alihisi amezid kumkosea zaidi kwani amesababisha kifo cha binti yake mdogo. Alitembea taratibu kabisa hadi alipomfikia Salhat ambaye tayari alikuwa marehemu kwa saa hiyo.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alimchomoa katika kile kisiki kilichokuwepo njee ya nyumba yake na kumuweka katika mapaja yake.



    "Mzee matata"......



    "Shshshshshshshshshsh mjukuu wangu amelala nyamazeni Salhat amelala" alizungumza huku akianza kumuimbia nyimbo za kumfanya alale kabisa hata baada ya usiku ule kupita bado Mr matata hakurejea katika hali ya kawaida kabisa aliubeba mdoli mkubwa ambao alimnunulia Salhat kwaajili ya kuuchezea na kuanza kuongea kwa kusema.



    "Salhat amelala bado akiamka ataanza kucheza na wewe"



    Mwili wa Salhat uliletwa na ilikuwa saa ya kuuzika na hapo ndipo kilipoamka kimbembe kwani Mr matata alihitaji kulala naye.



    "Nataka kulala naye tuende wote kwanini apande mwenyewe huko ndani???



    Mr matata tayari Alishanganyikiwa kabisa kiakili hivyo alibembelezwa na hatimaye mwili wa Salhat ulienda kuzikwa baada ya hapo lilikuja gari la vichaa na kumpeleka Mr matata katika hospitali ya vichaa huku utajiri wake mkubwa ukiwa mikononi mwa Badra ambaye sasa tamaa yake Kubwa ilikuwa ni kuishi duniani na siyo tena ujijnini kwao.



    Picha zote za Salhat,Naseeb mama yake pamoja na Mr matata zilitupiwa store na nyumb nzima sasa zilijaa picha za Badra na wasanii anaowapeda yeye.



    Alikuja mfanyakazi mmoja wa kike jina lake Ashura.



    "Mama, yalikuwa mawazo yangu tu kwamba umrudishe tu baba nyumbni mimi naweza kumlea na kumuwekea umakini mkubwa zaidi akiwa hapa pia anaweza kupata nafuu zaidi kuliko akiwa......................"



    "Shut up.......,,..... Ndicho kilichokuleta hapa sindiyo........nyumba yangu siyo ya kulelea ma vichaa akae huko huko na usinifundishe kipi cha kufanya juu ya Mme wangu umenipata wewe. Umenielewa alizungumza huku akimsogoa kichwa na hatimaye kumwagia juice aliyokuwa akiinywa. Kisha baada ya hapo ilisikika Sauti ya kiume ikikohoa kwa chini



    Badra alitizama chini na kutabasamu kisha akaanza kushuka huku akichekelea.



    "Swty wangu umekuja nilikuwa nakusubiri kweli alizungumza na alipofika pale alimbusu mdomoni kisha akamshika tai na kuanza kumvuta kwa nyuma huku akimuongoza wapi pa kwenda.



    Ashura: eeeeeehhh Mungu wangu ni balaa gani hili limeingia ndani ya hii nyumba tafadhli tuokoe Tafadhali tuondolee hili balaa alizungumza huku akitizama juu.



    **** ****** *****



    Afande Victor.



    "Ndyo mkuu"



    "Hiyo kesi ya kuibiwa kwa Salhat pamoja na kifo chake ifunge sasa kwani hakuna mtu wa kuifuatilia tena" alizungumza IGP Saidi na kuondoka naye.



    Afande Victor alifanya kama alivyoelekezwa ila kwa bahti mbaya picha moja ilidondoka chini.......picha hiyo ilikuwa ni ya siku ambayo Salhat alikufa kwani alipigwa picha akiwa pale pale chini ila katika mkono wake uliofungwa shanga wala haukuwa na shangaa yoyote tena na hiyo ilikuwa vigumu polisi kupata kujua kwani wangeliweza kutambua ya kuwa aliyelikufa hakuwa Salhat Bali mtoto mwingne kabisa na mchezo huo ulichezwa na Sultan Shariphu baada ya kupata taarifa alizotumiwa na Sadick kihisia ya kuwa Salhat yuko hatarini basi aliweza kumfungua Samia pasina jini yoyote kutambua kisha wakaja mpka duniani kwaajili ya kumuokowa Salhat hivyo waliona njia pekee ya kumuokowa Salhat na kufanya asifuatwe na kumtengenezea kifo na ndipo walipofika walifanikiwa kumuona Binti yule aliyekuwa na Salhat akipambana na Samir mlangoni na wakati anatoka Samia alimpiga kibao cha mguu hali iliyofanya ajione amejikwaa na kumuachia Salhat ambaye alidakwa na Sultan na hatimaye wakaweka mwili uliokuwa ukifanania na Salhat na kuondoka zao.



    Miili ya Sultan na Samia haikuwa ikifaa hiyo ni kutokana na kumbeba Salhat ambye alikuwa na kinga ya majini hivyo waliweza kuungua vibaya sana hadi kumfikisha hapo walipomfikisha.



    "Sultan Shariphu na shukuru sana kwa kunisaidia katika kumuokowa mwanagu Salhat"



    "Usijali yote nafanya hivyo kutokana na kwamba mama yako ndye mwanamk wa kwanza mm niliyempenda lakini nilishindwa baada ya mimi kulazimishwa kumuowa mwanamke mwingne hivyo mama yako na yeye hakuwa na chaguo zaidi ya kuolewa na mwanaume mwingne ila pindi alipokuzaa wewe tu aliaga dunia ila aliniomba nikuwekee umakini mkubwa sana" aliongea kwa taabu Sultan kwani tayri alitumia nguvu nyingi katika kumbeba Salhat kwa muda mrefu.



    Wakiwa pale pale alitokea Samer na Sadick.



    "Samir muwaisheni ngomeni kwaajili ya matibabu zaidi kwani hali yake siyo nzuri.



    "Kwani kimewakuta nini??? Aliuliza Sadick na hapo hapo alipokelewa na kilio cha mtoto walitizamana na Samir kisha kugeuza macho yao nyuma walishtuka kwa pamoja na kusema.



    "Salhatt!!!!!!!!............



    Baaada ya miaka 7 kupita



    Alionekana binti mdogo akiwa anashuka ngazi taratibu kabisa huku akiwa amevalia kigauni kifupi chekundu kilichoweza kuvutia kwa muonekane wake.



    Huyu aliitwa Grace alikuwa mtoto wa Badra aliyoweza kusema kuwa mimba niya Mr Matata japo kuwa ilikuwa ya utatanishi na hakuna mtu ambaye angelikuw na uwezo wa kufuatilia hilo.

    Alishuka taratibu kabisa na baada ya kukaribia kushuka tayri wafanyakazi walishajipanga chini ya ngazi na hivyo ndivyo alivyokuwa akitaka.



    Wakati anapita wote hao utizama chini kama ishara ya kumpa heshima alielekea hadi sehemu ya kunawia mikono hapo alimiminiwa maji na kunawishwa mikono yake baada ya hapo aliletewa taulo safi kwaajili ya kufutwa futwa mikono yake alielekea moja kwa moja hadi kwenye meza ya chakula hapo alivutiwa kiti na kukalishwa kisha mfanyakzi mmoja anapiga magoti chini na kukaa mkao wa mbuzi kwani Grace miguu yake haikuweza kufika chini hivyo hakutaka ining.inie alikuwa akiknyaga mtu mgongoni ale hadi amalize ndo mtu yule asimame pale.



    Aliwekewa chai pamoja na kusogezewa vitafunio ambavyo tayri vilishakatwa katwa kuandaliwa na kupoozwa pia.



    "Nani kapika chai???!! Aliuliza baada ya kuweka mdomoni.



    "Mimi hapa alijitokeza mfanyakzi mmoja wa kike jin lake Bahati.



    "Nilisemaje kuhusu chai kuwekea viungo vingi, si nilishasema sipendi viungo vingi kwenye chai" aliongea na kumwagia chai ile ya moto mkononi mwake.



    Na hiyo ndyo ilikuwa tabia yake ya kuzarau watu pasina kujali umri wao kwani aliona yeye ndye tajiri kwani ndiye anayemiliki Mali zote alizoacha Mr matata ambaye bado alikuwa kichaaa hospitalini.



    .

    Huku nako katika kijiji kimoja cha mbali ndipo alipokuwepo Samia na mwanaye Salhat.



    "Mama aliita Salhat"



    "Abeeee"



    "Hivi kweli we ni mama yangu..........mbona hatufanani kabisa we ni mbaya umeunguwa unguwa mwili mzima na watoto wenzangu shuleni wanasema kuwa wewe ulikuwa muizi ndyo maana ukachomwa hivyo ila walikuachia baada ya kugundua ya kuwa una mimba yangu"



    "Hapana mwanagu mama yako siyo mtu mbya hata kidogo ila niliungua hivi kwaajili ya kuokoa maisha yako kwani wewe ni mtu wa dhamni sana katika dunia hii" alimwambia mwanaye Samia.



    "Huwa nawaambai hivyo lakini wanakataa"



    "Usijali wewe mwamini mama yako na umsikilize yeye tu pekee yake na kama wanakusumbua ntakuja shuleni kwajili ya kuzungumza na mwalimu wenu!!!



    "Hapna mama yangu usijichoshe mimi nitavumilia yote hayo kwani mimi ni mtu wa muhimu sana hapa duniani baada ya kusema hayo mama yake alimtizama mwanaye Salhat na kumkumbatia.



    Katika kijiji hicho hicho lilikuja gari la kifahari na kupaki pembeni tu ya nyumba ya Samia kisha vikashuka viatu vya kike na kuanza kumfuata Samia ambaye alimpa mgongo na mwanaye Salhat.



    Msichana yule alitembea hadi kufika sehemu ambayo alikuwepo Samia.



    Alipofika karibu naye alimshika begani na kumfanya ageuke nyuma.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa sura ngeni kabisa machoni pa Samia.

    "Samahani naitwa Anna nilikuwa naomba kama nitapata sehemu ya kujisaidia kidogo,nimezidiwa alizungumza na kumfanya mama yake Salhat aamke na kumuonyesha sehemu ya chooni.



    "Kazuri jamani katoto kako kanaitwa nani?? Aliuliza Anna huku akimpapass Salhat.



    "Naitwa Salhat alizungumza huku akitabasamu.



    Anna alimshika kisha akamfuata Salhat kwajili ya kuelekea msalani baada ya muda alirejea na kumshukuru Salhat.



    "Mtoto wangu pia hajatofautiana sana umri na mtoto wako"



    "John!!! John!!!! Aliita na kufanya mlango wa gari ufunguliwe tararibu kabisa na kushuka viatu vya mtoto wa kiume makamo yake yaliweza kumzidi Salhat kwa miaka minne tu.





    Njoo msalimie mama alizungumza na kumfanya John aje na kumsalimia mama yake Salhat huku akimtizama Salhat.



    "Salhat msalimie kaka! Aliongea Samia na kufanya Salhat amsalimie John au Jay.



    "Mambo alizungumza John baada ya Salhat kumsalimia.



    Mama yake alicheka tu na kutabasamu



    "Ndivyo alivyo huyu ni muhuni sana" alizungumza huku akimshika shika kichwa John.



    "Sawa mama si ni wageni wa Mzee Mtapila ni baba yangu mkwe hivyo nimekuja kumsalimia lakini nikazidiwa ikabidi nipitie hapa" alizungumza kwa kujielezea zaidi



    "Aaaahaaa mzee Huyo namjua sana ni mzee mstaarabu hapa kijijini kwetu ila wanawe siwatambui sana kwasababu mimi siyo mzaliwa wa hapa" alijielezea Samia na hapo hapo alihisi upepo ambao ulimshtua kidogo na kusema Salhat kimbia ndani, na ninyi pia ingiieni ndani"



    "Kuna nini kwani??? Aliuliza Anna



    "Ingiza watoto ndani Fanya haraka alizungumza na kumfana Anna awakimbize watoto ndani katika nyumba aliyoweza kumuelekeza.



    Walipofika walifunga mlango na kushindwa kuona njee.



    Njee alipo Salhat alisema

    "Jitokeze popote ulipo.........Fanya haraka.....!!! Alizungumza baada ya kuhisi ya kuwa kitu kipo hapo.



    Hapo hapo alitizama nyuma na hakuona mtu yoyote yule aliyekuwa akimtizama hapo hapo alibadilika na kuwa katka umbile lake la kijini hapo alifanikiwa kuwaona majini wenzake alikuw ni Samir pamoja na Sadick walikuja kumuona.



    "Kwann mmekuja katika hali hii mnatakiwa mje katika hali ya kawaida sitaki mwanangu atambue ya kuwa mimi siyo binadamu alizungumza na hapo hapo akajibadilisha katika umbo la kawaida na kuwafanya nao warudi katika umbo lao la kawaida.



    Anna alifungua mlango na hapo hapo alisikia sauti ikisema "* tokeni njee ni salama.*"



    ****** ****** *****



    Grace alipelekwa shuleni kwa gari ya bei ghali sana na kila alikokuwa akipite yeye tayri kulishasafishwa na wafanyakazi wake pamoja na kumwagiwa mauwa ya Waridi hiyo ndyo ilikuwa mila na deaturi yake kiti chake kilikuwa tofauti sana na yeye pekee katika darasa zima alijitenga na wenzake na kukaa mwishoni kabisa tena pekee yake. Katika upande wa akili hakuwa mchovu kbisa kwani Mara nyingi yeye aliongoza darasani na hakukuwa na mtu yoyote ambaye angeweza kulandana naye.......



    Hivyo kila yalipotokea mashindano ya kushindana kishule lazima Grace angekuwepo kwenye orodha hiyo na hakuwahi hata siku moja kukosea kabisa hivyo kila Mara alirudi na kikombe cha ushindi shuleni. Mwaka huu pia mwalimu alikuja kutangaza wale watakao weza kwenda shule jirani kwaajili ya kushindana na jina la Grace Matata lilikuwa la kwanza kutajwa.



    Huku nako kijijini ikiwa ndyo Mara ya kwanza mashindano hayo yamefika Salhat alichaguliwa kwenda kukiwakilisha kijiji chao pamoja na shule yao huko mjini. Na hapo ndipo mzozo ulipozuka baina ya Samia na mwanaye Salhat.



    "Kwani mama kuna shida gani mimi nikienda kwajili ya masomo sijawahi kusafirigi hata kwenda kijiji cha pili nmekulia hapahpa na kulelewa hapahapa nikiwa siwafahamu ndgu zangu wengine zaidi ya wewe tu......kwani we mama huna ndugu........kijiji kizima hichi ni mimi tu pekee nisiyeifahamu hata ladha ya baiskeli wala raha ya kucheza kama watoto wengine muda mwingi unanibana sana.....hata nikienda kucheza haipiti dakika mbili tayari umeniita mama Tafadhali japo kwa Mara moja naomba na mimi nijisikia kama watoto wenzangu" alizungumza na kuondoka zake huku akikimbilia pasipo julikana.



    ******* ******* *****



    Mr matata akiwa katika hospitali ya vichaa sasa hali yake kidogo ilionekana kuanza kutangamaa kwani kuna muda anaweza akakaa na kuulizia wakili wake kisha akishaletwa anazungumza naye maswala ya biashara na mmbo yanavyoenda na kuna saa ukichaa wake unamrudia.



    ******* ********



    Salhat alikimbilia mtoni na huko alienda kukaa pekee yake huku akirusha rusha majabali ndani ya maji ghafla alisikia jabali lingine likirushwa na mtu kutoka nyuma yake aligeuka na kumtizama alikuwa ni John.



    Alisogea na kukaa karibu na yeye.



    "Nilisikia mama yako akiwa anakuulizia kwanini umetoka nyumbni bila ruhusa ya mama yako?? Aliuliza John.



    "Nitaenda kumuomba msamaha pindi nitakaporejea nyumbani sijisikii vizuri" alizungumza Salhat akikaa chini sasa.



    John naye alisogea sogea maeneo aliyo na yeye akaakaa pembeni yake huku akimtizama.



    "Unaonekana mzuri alizungumza huku akimtizama kwa makini Salhat ambaye aliweza kutizama chini kwa mshangao.



    Umri wa John ulikuwa ni miaka 11 huku umri wa Salhat ukiwa ni miaka 7..



    John alimtizama na kutabasamu tu huku akiendelea kutusha vijabali mtoni alimtizama Salhat kisha akamsukumia mtoni basi wote wakaanza kucheza huku wakirushiana maji na hiyo ndyo ililuwa Mara ya kwanza kwa Salhat kucheza muda mrefu namna hiyo tena akiwa na furaha Kubwa sana.



    Salhat alianza kuyapiga piga maji ambayo yaliweza kumrukia usoni mwake na kumfanya afurahie zaidi. John alimtizama kwa makini sana na kujikuta amevutiwa naye na kuendelea kumtizama zaidi na zaidi.



    **** ***** ****



    Hatimaye siku ya mashindano ilifika na walianza kutajwa wanafunzi waliokuwa wakiweza kuzirepresent shule zao ila dawati moja lenye kiti chake lilikuwa tupu kabisa na hilo ndilo alilostahili kukaa Salhat lakini hakuwapo.



    "Tumeshasubiria kwa dakika 10 lakini bado mashiriki wetu hajawasili hivyo hatuna haja ya kusubiri tena Bali tutaanza kugawa mtihani wa Hesabu, kiswahili na kumalizia na Kingereza" alitoa muongozo Mc Huyo naye alitoa ishara ya waliokuwepo mezani wapewe mitihani kwaajili ya kuanza kufany hata meza pia ya Salhat iliwekewa mtihani na mtihani ulianza sasa na hatimaye zikapita dakika tano lakini watu wakiwa kimyaa kwaajili ya kufanya mtihani na wazazi wao waliokiwa kwenye ukumbi ule ule wakitizama kwa makini ni nani anayeweza kuibuka mshindi. Hpo hpo vilisikia viatu vikiingia ndani hakuwa mwingne Bali Salhat aliyeweza kuongozana na mama yake pamoja na msaidizi wa mwalimu mkuuwa shule yao.



    Alitoa ishara ya samahani na kukaa kwenye paper alifanya paper zote tatu kwa umakini wa hali ya juu sana na ndvyo Grace naye alivyofanya.



    Mtihani uliisha na sasa ulikuw wakati wa kusahishwa na computer na hatimaye kutaja mshindi ni nani ililetwa bahasha yenye majina ya watu watatu walioweza kufuzu katkka mtihani Huo nao walikuwa ni.

    Agnes, Grace pamoja na Salhat.



    Hapo hapo ililetwa barua ys mshindi namba tatu naye alikuwa Agnes's alipewa zawadi yake kisha akaondoka zake na kuwaacha manguli wawili ambao ni Salhat na Grace.



    Aliamini ya kuwa hakuna atakayeweza kumpita yeye na medali ni zake kweli pamoja na kikombe ni cha shule yao.



    Na mshindi wa kwanza ni..................Mc alifungua bahasha aliyopewa na kusema tena ni ...... Grace alianza kupiga hatua za mbele kwa kueleke stejini.



    "Ni Salhat Naseeb" alizungumza Na ukumbi mzima ulibaki kwa mshangao kwani Mara nyingi walishafanya kama mazoea ya kuwa Grace ndye pekee.

    Ukumbi ulizizima kwa sekunde kadhaaa na hapo hapo Msaidizi wa mwal mkuu alianza kupiga makofi na kufanya wengne wakipokea.



    Salhat alitabasamu na kumtizama Grace ambaye alimtizama kwa macho makali sana na yenye jaziba.



    Wote walipewa medani za silver kwa kuvalishwa shingoni mwao na kisha kombe akapatiwa Salhat pekee. Grace alimtizama na kusema.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hicho ulichonacho ni chakwangu wala hakiwezi kwenda mbali na mimi". Alizungumza na kuanza kushuka ngazi zake taratibu kabisa huku macho ya hasira yakiwa juu ya mwili wa Salhat.



    Baada ya Salhat kupigwa piga nyingi na waandishi wa habari sasa walianza mtafuta mama yake kwaajili ya kumuhoji lakini hawakumuona kwasababu Samia alijificha na kusema.



    "Sura yangu yaweza leta balaaa kwa upande wako mwanangu ndiyo maana sitaki kabisa kuonekana mbele ya dunia aliazungumza Samia aliyekuwa amejificha mbali kidogo na pale huku akitizam jinsi mwanaye anavyohangaika kumtafuta.



    Samia akiwa palepale ukumbini zawadi zikianza kutolewa kwa wanafunzi wengne kwani siyo ktika kusoma tu hata wenye vipaji vingne pia kma kuchora kuimba nao walihudhuria.



    Ulifik muda wa kumtaja mshindi ambaye aliweza kutunga stori nzuri katika kwa kutumia picha na kabla hajapanda jukwaani zilianza kuonyeshwa picha zake ambazo ziliviutia sana machoni pa watu wengi na maneno chini ya picha ambzo zilielezea jinsi binti mmoja wa kijijini aliyeweza kupata ofa ya kuja katika mashindano hayo lakini mama yake alikataa kumruhusu kuja katika mashindano hayo baada ya hapo binti Huyo aliondoka hadi kwenda mtoni kwaajili ya kutuliza hasira zake huko alikutana na kijana mmoja mzuri ambaye naye hakumktisha tamaa na kuomba amuombe mama yake tena na tena hata yeye atamsaidia sehemu ambayo atakwama kwa kupitia babu yake.



    "Mbon kama picha zangu......alizungumza Salhat huku atikizama stori ile kwa makini.



    "Baada ya kijana yule kuachana na binti yule alienda hadi kwa babu yake na kumuomba akamuombee binti yule apewe ruksa ya kwenda katika mashindano kutokana na kuw mama yake na yule binti alikuwa akimuheshimu mzee yule kama baba yake basi alimruhusu binti yake na binti yake aliweza kufika katika chumba cha mtihani kwa kuchelewa lakini alifanya vizur zaidi ya wale aliowakuta na hatimaye alipewa kikombe km ushindi baada ya kufaulu vizuri sana.



    Na hapo ndiyo ukawa mwisho wa hadithi yake watu walipiga makofi sana kwani stori ile iliwavutia na hapo hapo alipanda kijna ambaye ndiye aliyehusila na hayo yote.



    Alipanda John ambaye aliwashukuru watu wote na kumtizama Salhat ambaye aliachia tabasamu zito Sana huku akimsindikiza kwa makofi muda wote ule Grace wala mama yake hawakuwa eneo lile hivyo hawakubahatika kuiona sura ya Samia ambayo ilionyeshwa na John katika uchoraji wake na huo ndiyo ukawa usalama wa Salhat.



    Ila mfanyakazi wao mmoja wa ndani aliweza kuitambua ile picha alikuwa Ashura.



    "Samia?!!!! Aliita kwa mshangao sana na kwa furaha



    "Inamaana Huyo ndye Salhat wa Naseeb, ama ni nini mbona Salhat alishakufa labda atakuwa amezaa na mwanaumw mwingine alijiaminisha hilo.



    "Kwanza hapana Samia hawezi kumfanyia hivyo Naseeb hata hivyo Huyo mwanamke ameharibika sura sana na Samia hana hata upele, kweli duniani wawiliwawili" alijiamisha kidasaign hiyo kisha akaamua kuondoka zake.



    ****** *******



    Baada ya pilikapilika kuisha John alionana na Salhat aliyekuwa akitabasamu tu baada ya kumuona Johnny.



    "Nashukuru kwani kwasababu yako kumenifanya na mimi nipatiwe kikombe kizuri cha uchoraji bora pamoja na hadithi nzuri"



    "Nashukuru pia kwani na wewe umeniwezesha kupata kikombe hichi bila ya we kuja kuzungumza na mma yangu ukiwa na babu yako sidhani kama ningalifika hapa leo" alizungumza kwa kutabasamu na kumtizama Johnny usoni na hap macho yao yakigongana na kuwafanya wapaki wakitizamana tu na kupigwa picha nyingi sana na waandishi baada ya kuwaona pamoja.



    Mama yake Johnny pamoja na mama yake Salhat walikuwa sehemu moja wakiwatizama.



    "Ni wadogo sana lakini upendo wa kweli unadhihirika machoni mwao" alizungumza mama yake Samia.



    "Natumaini kwaajili yake hata matatizo aliyonayo Johnny yataanza kupungua na hatimaye kuisha kabisa" alizungumza huku akimtizama Johnny na Samia.



    Walitizama kisha wakacheka kwa pamoja huku wakikumbatiana na kupeana hongera kwaajili ya ufaulu wa wanawe.



    ******* ******** *****



    Baada ya Grace kufika Nyumbani alipokelewa na shada la mauwa na watumishi wake pamoja na ka keki kadogo kalichoandaliwa juu yake na hii ni kawaida yake kuandaliwa kila atokap kwenye mashindano kwani mara zote huibuka mshindi.



    Watu walishangaa baada ya kuichukua ile keki na kuitupa chini kisha akaikanyaga kanyaga kwa hasira na kuvuruga maandalizi yote yaliyofanywa kwaajili yake huku akipiga kelele.



    "Unashida gani we??? Aliuliza mama yke ambay ndiye aliyeweza kuandaa karamu hiyo ndogo kwaajili ya mwanawe.



    Baada wa muda watumishi walikuwa jikoni wakicheka sana.



    "Pumbavu zke huyu mpumbavu sana bora hata leo kapata mtu wa kumzidi akili maana anajionaga ya kuwa yeye ni bora kuliko watu wote hapa duniani lakini leo kakomeshwa kabisaaaa" alizungumza bahati huku akionyesha vitendo Grace alivyokuwa akifanya baada ya kuingia ndani wafanyakazi waliokuwa mule ndani jikoni walijikuta wakiangua kicheko cha nguvu sana hapo hapo walijiziba midomo yao na kuanza kucheka kwa sauti ya chini..



    "Msichana mpuuuuuziiiiiiii wewe unawezaje kunifanyia mmbo ya Aibu namna hii hadi wafanyakazi ninaowalipa mm wewe umefanya leo wanicheke naapa utalipa kwa hilo sitoweza kabisa kukuwacha hai wewe sitoweza kukuachia uondokee tu kama ulivyokuja hapna nitafanya tu kitu kwaajili yako. Grace alikula kiapo juu ya hilo huku akiyang.ata meno yake kwahasira wakati huo mama yake alikuwa juu akimtizama na kuongea maneno Haya moyoni.



    "Sasa nataka kuyaona makucha yako, kwamaana nimekulelea mimi kwaajili ya kuweza kunifanikishia malengo yangu katika hii nyumba na uniondolee takataka yoyote itakayohitaji hzii Mali baada ya hapo nitakusambaritishia mbali sana wewe kwani sipatanagi kabisa na binadamu wanaoniamrisha mimi kipi cha kufanya juu yao.



    ********* **********



    Huku nako siku hiyo Samia, Salhat pamoja na mwalm msaidiz waliweza kwenda katika nyumba ya mama yake Johnny kwaajili ya kupata chakula cha usiku kama walivyoombwa na waondoke asubuhi yake kwaajili ya kwenda kijijini kwao.



    Basi Siku hiyo Johnny alikuwa kwenye swimming pool pamoja na Salhat akimfundisha kuogelea kisirisiri pasina mama yake kujua.



    Wakiwa pale hapo hapo mama yake aliingia na kuwakuta.



    "Johnny unafanyaje huko na matatizo uliyonayo unatambua yanasababishwa na maji ya baridi embu toka huko Fanya haraka Salhat tokeni huko" walitoka wote kwa pamoja na mama yake Johnny alianza kumfuta Johnny huku akilalamika na machozi kumtoka..



    "Mama niko salama bhna sina tatizo lolote mimi mbona nimekaa zaidi ya lisaa limoja na bado niko hai!! Alzungumza akmtizama mama yake aliyekuwa akidondosha machozi.

    " Nimeshampoteza baba yako kwaajili yako sitaki tena kukupoteza wewe kizembe",



    Hapo hapo aliingia mama yake Salhat na kuanza kumgombeza Salhat kwa kitendo cha kutaka kufundishwa kuogelea usiku ilihali maji ni ya baridi.



    "Mama nisamehe mimi ni kosa langu kumuomba anifundishe kuogelea usiku" aliongea Salhat huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini.



    Mama yake Johnny alimgeukia na taulo na kuanza kumfuta maji na yeye.



    "Johnny anamatatizo haruhusiwi kukaa ndani ya maji kwa muda mrefu hata kama ni ya moto kiasi gani -hivyo naomba unielewe tu binti yangu mzuri........Haya twendeni kwenye chumba cha joto.



    Waliingizwa katika chumba kimoja na Johnny hakuwa tena na furaha.



    "Kwann umenuna usinune mwaya kwasababu hata mimi ninaugonjwa na sijawahi kumwambia mama yangu"



    "Ugonjwa gani huo????? Aliuliza Johnny.



    Salhat aliiona Glass kwa mbali kisha akaitizama kwa macho na glass hiyo ikaanza kuja na hatimaye ikafika karibu yake.



    "Heeeeeew umewezaje kufanya hivyo!!!???



    "Hata sijui mm mwenyewe naogopaga kumwambia mama yangu" alizungumza Salhat.



    "Basi usijali sitamwambia mtu kwamba unaugonjwa wa kijini embu irudishe hiyo glass kule"





    Johnny pamoja na Salhat waliendelea kuufanya mchezo ule bila wao wenyewe kutambua ya kuwa ni hatari endapo mtu atapita na kumuona Salhat katika hali ile.



    "Salhat nivute na mimi nije hapo" aliongea Johnny na kukaa mbali kidogo na Salhat.



    "Hiyo sijui kama nitaweza!!!! Alizungumza Salhat.



    "Jaribu tu utaweza kuwa na imani" aliongea Johnny.



    Salhat alimtizama lakini alishindwa. "Siwezi"



    "Shida yako we unasema huwezi ndyo maana huwezi kama ni hivyo sitaki tena uwe rafiki yangu alizungumza Jonny na kugeuka upande mwingne.



    "Jay.....!!!!!



    "Usiniite we si umekataa kunibeba" aliongea Johnny.



    "Sawa.......ntaweza aliongea Salhat na kumtizama Johnny ghafla alimbeba kwa nguvu na kumfanya adondokee sehemu aliyopo hali iliyowafanya wote wadondoke chini na kufanya Johnny kuwa juu ya Salhat huku lipsi zao zikigongana walibaki wakiwa katika hali ile ile na kukutwa na Mama zao waliokuwa wakiingia ndani.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Johnny!!!!!



    "Salhat.....!!!!



    Kila mmoja alimwita mwanae kwa mshangao mkubwa sana.



    Baada ya muda wote walikuwa mezani huku Salhat akipiga kwikwi na alipewa maji ya kunywa na mama yake wakati Huo nao Johnny naye alikuwa akipiga kwikwi huku macho yake yakiw yametulia sehemu moja.



    "Johnny kunywa maji kwa utaratibu alizungumza mama yake baada ya kuona Johnny anafakamia maji sana kwa kiac kikubwa na kujimwagia.



    Alitizamana na mama yake Salhat na kubaki wakikaukia kucheka kwa ishara bila kuwaonyesha watoto wao.



    ******* ********



    "Mmeshafuatilia na kumtambua Huyo mtoto aliyeweza kukichukua hicho kikombe ni nani???! Aliuliza Badra aliyekuwa akiongea na mtu ambaye hakufahamika ndani ya simu.



    "Bado yuko hapa hapa mjini........basi hakikisha ili hicho kikombe mnakichukua na hata Huyo mtoto akiwasumbua muulieni mbali kisha akakata simu.



    Grace aliyekuwa amekaa pembeni ya Badra akiamini amekaa na mama yake alitabasamu kwa kiasi kikubwa sana baada ya kusikia mama yake akitoa kauli hiyo.



    Ashura aliyekuwa analeta juice mbili mahali walipo alishusha pumzi ndefu na kuitizama picha ya Naseeb iliyokuwa ndani ya nyumba ile hata yeye akashindwa kujua kwann kaitizama kisha akasema "muokowe mtoto huyo" .....upepo wa ajabu uliingia ndani ya nyumba ile na kufanya picha ya Naseeb ianze kucheza cheza ikiwa kwenye frame yake.



    Asubuhi hiyo Salhat akiwa ameamka na kuanza kutembea ndani ya nyumba kwaajili ya kuelekea sebleni ghafla aligongana na mtu kifuani na kufanya adondoke chini.



    Alikuwa ni Johnny ambaye na yeye alitoka kuamka muda si muda.



    "Salhat pole alizungumza huku akiinama mpaka chini na kumtizama kwenye paji la uso huku akimpuuliza tartibu kabisa.



    Wakati hayo yote yakitendeka mama yake Salhat na Jonny waliyaona na kubaki wakitizamana tu na kuishiwa pozi kabiss pindi wanapowaona watoto wao.



    ******** ********



    Grace akiwa shopping na mama yake huku akichagua vitu vyake vidogo vidogo bila kujua ya kuwa mmbaya wake kama yeye anavyofikiri yuko pale pale.



    Hata Samia hakuweza kuutambua uwepo wa Badra ndani pale.



    Wakati Grace anaenda kuichukua saa ambayo ilimvutia sana alinikuta mkono wake ukiwa umekamata mkono wa mtu ambaye tayri alikuwa ameshaishikilia ile saa.

    Alikuwa ni Johnny. Jay aligeuka na kumtizama Grace.



    Nafikiri miye ndye wa kwanza kuchukua kwahiyo toa mkono wako juu ya mkono wangu kwasababu cpendi kushikwa mm" alizungumza na kuutoa mkono wa Grace ambye alikuwa akitxasamu baada ya kumuona Johnny na kushindwa kuelewa kwanini anacheka.



    Johnny alimtizama kwa mshangao kisha akauinua mkono wake mmoja na kuutoa mkono wa Grace kwenye mkono wake kisha akaondoka na kuelekea caunta kulipia huku akinug.unika juu ya Grace.



    Akiwa anarudi na kiboksi chake mkononi alishtuka baada ya kumuona Grace mbele yake.



    "Kaka hiyo saa umemnunulia nani????



    "We inakuhusu nini??? Aliulizs Johnny na kumuona Grace kama kero kwa upande wake.



    "Umemnunulia girlfriend wako?????



    "We ni kichaaa nini nani kasema ni girlfriend wangu ni mdogo wangu yule ni mdogo wangu aliongea kwa hasira kiasi huku akisunya na kuondoka akiwa analalamika huku akilirudia neno lile la Girlfriend.



    Muda ulifika wa kuondoka kwa Salhat na mama yake hiyo ilikuwa huzuni Kubwa kwa Johnny na Salhat ambao walikuwa tayri wameshanza kuzoeana.



    "Johnny umsindikizi Salhat ndani ya gari?? Aliuliza mama yake akimtizama Johnny ambaye hakuwa tena na sura ya tabasamu usoni mwake. Alienda na kumshika mkono Salhat kisha kuanza kumpeleka kwenye gari kwaajili ya kuelekea stand.



    Wakati amemshika mkono Salhat akuweza kutizama nyuma ila Salhat alikuwa akiutizama mkono ulioshikwa na kutabasamu baada ya kufika karibu na gari alimuachia mkono wake na kumgeukia Salhat.



    "Salhat..... Nataka uwe mpenzi wangu pindi tutakapokuwa wakubwa sitaki uniambia kuwa unamwanaume mwingne hata kama unaye umuache kwasababu mimi ndye mpenzi wako kwanzia sasa" alizungumza na kutoa saa aliyoinunua kisha akamvalisha na kusema.



    "Unatakiwa ukae na hiyo saa mpaka Siku nitakayokuowa na kukuvisha pete" aliongezea Johnny na wakati huo Salhat alitaka kuongea kitu lakini Johnny alimzuia na kumwambia



    "Wewe tayari ni mpenzi wangu utake usitake"



    Salhat alitabasamu kisha akautoa mkufu uliokuwa shingoni mwake na hiyo ndyo iliyokuwa cheni pekee iliyoweza kumtambulisha yeye kuwa ni mtoto wa Naseeb kwani iliokotwa na babu yake na babu yake aliirudisha tena shingoni mwake.



    "Inamaa" aliongea Salhat na kumfanya Johnny aliname akiwa na tabasamu baada ya kumvisha naye alisema...



    "Hiyo ni alama ya kuwa wewe ni boyfriend wangu usije ukaitoa kwani ni ulinzi tosha kwako" aliongea na kutabasamu.



    Johnny alimshika mikono na kutizamana huku wakianza kuchekeana wenyewe kwa wenyewe.



    Wakati hayo yote yakiendelea kulikuwa na mtu aliyetumwa afuatilie ya kuwa Johnny anakaa wapi na anakutanaga na nani aliwapiga picha bila wao wenyewe kujua na alielekea nyumbni kwa wakiwa Grace na kumuonyesha

    .



    "Mungu wangu yani huyu ndiye mdogo wake.............alizungumza na kukumbuka order ya mama yake aliyesema auwawe hata kama ila alikihitaji kikombe.



    Grace alianza kukimbia ndani kwaajili ya kumwambia mama yake aache kufanya hicho anachotaka kukifanya ila wakati Huo sasa Gari waliyopanda Salhat nyuma yake walifuata na gari ndogo mbili huku fuso moja ikiwa inakuja kwa kasi mbele ya gari leo.







    Wakiwa katikati ya safari Samia na mwanaye Salhat lilitokea gari Kubwa mbele yao na Salhat pamoja na mama yake walikuwa mbele kabisa kwa dereva.



    Dereva alinyooshea scania kwa mbele na kutaka kuligonga lakini alishangaa baada ya kuona hakuna chochote kinachofanya kazi ndani ya gari lile.



    Akiwa katkati ya barabara na watu wakiwa wametamahaki na wengine wakiwa wamepiga kelele ndani ya gari wakiamini ya kuwa tayri ajali imeshafika mbele yao.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walishangaa baada ya kuona gari la aliyetaka kuwagonga haliji tena maeneo Yale watu walishuka ndani mbiombio na kuteremka chini wengine walienda na kumtoa dereva yule ndani ya ile Scania kisha kuanza kumpiga huku wengine wakisema "amelewa Huyo jamani tumuacheni".

    Samia alishangaa na kushuka hata Salhat naye hakujua ya kuwa baada ya kulitazama lile gari kwa hofu Kubwa basi kila kilichopo ndani ya lile gari kiliharibika.



    Magari madogo mawili baada ya kuona ya kuwa dereva wa gari lile ameshindwa basi walichomoa bastola zao na kuanza kumuelekezea Salhat ambaye alikuwa yuko mbele ya mama yake ghafla macho yake yalibadilika rangi bila hata yeye mwenyewe kujua na kugeuka sehemu ambayo risasi ilikuwa imepimwa kupitia upande wa kulia wa kichwa chake na kutokea upande mwingne wa kushoto.



    Baada tu ya kumtizama yule kijana hapo hapo aligeuka na kuwa kipofu mwingne alijitahidi kupiga bastola lakini haikutoka kabisa.

    Baada ya kumuona Salhat na macho Yale alianza kutimua mbio kwaajili ya kuyaokoa maisha yake.



    "Mama yule kule anabastola alizungumza Salhat na kunyooshea mkono sehemu ambayo mtu yule alionekana akikimbia.

    Abiria wachache wa kiume walianza kutimua mbio kwaajili ya kwenda na kumkamata.



    Yule aliyepigwa upofu basi na yeye alianza kulalamika macho yake hayao I macho yake hayaoni.



    Baada ya muda abiria wote walikuwa kituo cha polisi wakitoa maelezo jinsi ajali ilivyokuwa.

    Na sasa ilifika zamu ya Samia na mwanaye Salhat aliyekuwa akisimamia kituo cha polisi alikuwa ni IGP Saidi na alipishana na Samia pasina yeye kujua kwani alikuwa yuko busy na watu wengine huku akiwapa maelekezo ya kazi.



    IGP Saidi alitoka mpka njee kabisa kisha akapanda gari lake lakini alipokuwa yuko ndani ya gari lake alihisi kama amemuona mwanamke anayemtafuta au kumfananisha lakini hakujali sana ila alipofika mbele aliishika kwa ukali kabisa breki ya gari zake na kutizama njia aliyokuja nayo hapo hapo aliinua simu yake na kupiga kituo cha polisi ila hakuna aliyekuwa akipokea simu kutokana na kelele za abiria wa lile gari lililotaka kugongwa.



    Wakati Huo nao Salhat na Samia walipita hapo kisha wakaaga na kuondoka saa hiyo tena simu iliita na ilipokelewa na koplo aliyekuwa eneo lile.



    "Ndyo........ndyo........hapana wameshaondoka ila hawana muda mrefu.....ndyo mkuu" aliongea mtu yule na kukata simu kisha akasema Huyo mwanamke aliyetoka hapa akamatwe pamoja na mtoto wake.



    Polisi walitoka njee lakini hawakumuona mtu yoyote yule wakati Huo nao Samia alishasikia maneno Yale na kujificha kwenye chemba moja na mwanaye. Iliyokuwa karibu na eneo lile la polisi.



    "Mama kwani kuna shida gani?? Aliuliza Salhat.



    "Hamna chakufanya kaa kimya na Fanya vile mama yako anavyotaka wewe ufanye."



    Salhat alitingisa kichwa kwa ishara ya ndio.

    Akiwa pale aliingia IGP Saidi

    ...



    "Yuko wapi????



    "Mkuu tumejitahidi kumtafuta lakini tumeshindwa....kuna tumesearch kila mahali na kufunga geti kisha tukaweka ulinzi mkali ila bado hatujampata.



    "Basi bado hajatoka njee endeleeni kumtafuta Huyo mwanamke na mwanaye ni watu muhimu sana kwa upande wetu na Mr matata cha kufanya ni kuwatafuta. Aliongea kisha askari wengine wakaanzs tena rasmi kumtafuta.



    Hapo hapo Samia alimwambia mwanaaye afunge macho na asifungue mpka aambiwe.



    "Samahani mama ninaomba ugeuke" aliongea Askari mmoja na kumfanha Salhat ageuke sura yake ilikuwa tofauti kabisa ilikuwa sura ya mwanamke mwingne.



    Basi watu wakawa wanapita kwa Mstaari katika geti kuu njee la polisi.

    Wakati wote Huo Salhat alifunga macho alivyoambiwa na mama yake..



    Wakati Samia anataka kutoka alishtuka baada ya roho yake kwends mbio na alipogeuka na kutizama vizuri katika ule mlango kulikuwemo na mfupa wa nguruwe na ndiyo kitu ambacho hapatani nacho kwani kinaweza kumbadilisha na kumfanya awe na sura yake ya halisi.



    .."alianza kurudi nyuma taratibu kabisa pasina mtu yoyote kujua.



    "Mama kuna nini aliuliza tena Salhat.



    Salhat alimwambia usije ukafungua macho hata ukisikia nini sawa!!!....



    "Ndyo mama"



    Kutokana na watu kuwa wengi basi aliinama chini na hapo hapo alipotelea pasina mtu yoyote kuwatambua ila kulikuwa na mfanyakazi wa Polish aliyekuwa akiwatizama wakiwa wanarudi nyuma lakini ghafla hata yeye hakuwaona tena aliingi mpaka pale walipokuwepo na kuanza kuwatafuta lakini hakuwaona tena.



    "Mbona kama niliona mtu hapa alianza kujiuliza mwenyewe lakini hakupata jibu akahisi labda ni yeye tu jinsi alivyoona .



    Tarifa zilimfikia Badra aliyekuwa akitumia juice.



    .."sasa mnawezaje kushindwa mnafikiria nn kwamba mm nitamwambiaje Huyo Grace.!!! Aliuliza na ghafla alisikia sauti nyuma ikisema



    "Hapanaa mama muacheni tu wala msimguse tena" alizungumza Grace na kutabasamu kitendo ambach kilimfanya Badra amatizame kwa makini sana..



    ********* *************



    Taarifa za kuonekana kwa Samia zilimfikia Mt matata aliyekuaa hospitali ya vichaaa.



    "Nmechoka nataka kurudi nyumbani na kila kilichokuaa kikienda kinyume na mimi kukionyeshea kuwa mimi ni Mr Matata.



    ******** ***********



    Wakati huo nako kijijini ilikuwa nifuraha sana hadi akaandaliwa karama ndogo ya kumpongeza lakini wakati hayo yote yakiendelea mama yake alikuwa amekaa pembeni akimtizama kwa furaha Kubwa sana.



    "M/Mungu nakuomba ulichoniptia mimi kikakuwe mbali na uhusiano wangu. Sihitaji mwanangu awe jini Bali binadamu wa kawaida tu kama walivyo watu wengine kikombe hicho akamuepushie mwanangu kwani mimi ndye ninayetambua Adha ya kutokuwa binadamu



    Akiwa pale alishtuka baada ya kuhisi ya kuwa Salhat hakuwa na cheni shingoni alienda akamchukua kisha akamuuliza.



    "Cheni yako iko wapi????



    "Nilimpatia Johnny kama zawadi kwani sikuwa na kitu kingne cha kumpa na kwa kuwa ulishesemaga ya kuwa cheni ile ni ulinzi tosha pia nilimpa ili awe salama"



    "Vipi kuhusu maisha yako vipi kuhusu hali ya maisha yako nilikwambia ya kuwa ile ndo kinga yako hupaswi kumpa mtu mwingne" alizungumza huku mchozi yakimtoka.



    "Mama mimi nikiwa na wewe ni usalama tosha kabisa hakuna haja ya kuvaa chochoe kile kwani wewe ni kinga yangu. Samia alimkumbatia mwanaye na mtoto naye alimkumbatia mama yake hapo hapo Salhat askari waliokuwa wakija na magari yao eneo lile.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Samia alisimama na kumwambia mwanaye aingie ndani baada ya kuhisi ving.ora. vya polisi. Salhata alifanya kama alivyoagizwa na mma yake na akiwa ndani ya nyumba alishangaa kuona kitu ambacho hakuwahi kukionaga tangu afikie umri Huo. Alianza kutembea taratibu sana kukielekea kitu hicho na baada ya kukishika alipiga kelele hiyo ni kutokana na short aliyopigwa hapo hapo mama yake naye alikimbilia ndani na kuwaacha maaskari kadhaa njee ya nyumba yake alipofika ndani alimkuta Salhat chini huku akiwa anatizama mezani.

    Mama yake naye alitizama mezani na hapo alikutana na kinga ambayo alipewaga Salhat akiwa mdogo kwaajili ya kujikinga dhidi ya majini.



    "Hpana haiwezekani alizungumza Samia huku akiamini ni kama ndoto imekuwaje tena mwanaye anaanza kuogopa kinga ile ya majini ikiwa sasa ndiyo ulinzi uliobaki kwaajili yake.



    Akiwa anawaza hayo hapo hapo mlango uligongwa na kuvungu na alishtuka Samia alimfuata mwanaye kisha akamkumbatia kisha kupotea naye kijini na kitendo hicho Salhat aliweza kukiona na alishangaa sana. Askari alifungua na hakukuwa na mtu tena hapo alishangaa na kuwaita wenzake wakiwa eneo lile lile hapo hapo iliingia gari Kubwa na alishuka Mr matata akiwa na wakili wake wa kampuni zake.

    .

    Alikitizama chumba kile kwa umakini zaidi lakini hakuona kitu ambacho kingeweza nidhihirishia uwepo wa Mjukuu wake eneo lile.



    Alianza kupiga hatua za kivivu sana huku akianza kutoka katika kijumba kile lakini alipofika njee ya malngo alihisi kama alikiona kitu ndani alirudi mbiombio na ni kweli aliiona ile kinga ambayo alimpatia Salhat pindi alipokuwa mdogo kabsa na kinga hiyo alipewa na mganga.

    .

    Alianza kulia na kucheka kwa pamoja huku akiwa kama mtu asiyeweza kuamini ya kuwa mpaka leo mjukuu wake Salhat bado anaishi.



    Alipiga magoti na kumshukuru Mungu kwa kiasi kikubwa sana



    ****** ********



    "Mama!!!, aliita Salhat na kumtizama mama yake ambaye alimuona akifanya tukio ambalo lilimshangaza kwa kiasi kikubwa sana.



    Samia aliinama mpaka chini kisha akamshika Salhat na kuanza kutoa Machozi kwani alihisi kama ni ndoto hakupenda kabisa mwanawe awe jini kama alivyo yeye kwani vipo vitu vingi anashindwa kuvifanya kutokana na kwamba yeye Si binadamu.Alifuta machozi yake kisha akaanza kutazama kulia na kushoto akaaona tunda moja likiwa juu ha mti akamwambia mwanaye.



    "Nilitee lile tunda kule"



    "Mama mimi siwezi kupanda juu ya Huo mti!! Alizungumza Salhat.



    "Sijakwambia upande kwani najua ya kuwa unaweza kulileta pasina kupand Huo mti aya lilete lile tunda.



    Salhat alimtizama mama yake na kutizama chini.



    "Mimi siwezi mama aliongea Salhat huku akitizama chini.



    "Haya mtizame mama yako alizungumza na kumfanya Salhat amuangalie aliiurefusha mkono wake hadi juu ya ule mti kisha akakwanyua mti ule.



    Samia alimtizama mwanaye aliyeonekana kama anashngaa kwa alichokiona ndani ya mwili wa mama yake.

    ..

    "Hivi ndivyo nilivyo na wewe Je!??!!!alimuuliza akitaka mwanaye na yeye amuonyeshe ni uwezi gani alionso.



    Hapo hapo macho yake yaligeuka rangi na kuwa ya rangi ya kijani. Aliutizama mti ule na pale pale Matunda yote yalikuwa kwenye mti ule yalidondoka chini.



    Samia alimtizama binti yake na hapo hapo miguu yake ilimuishia nguvu na kujikuta amekaa chini.



    "Kwanini???? Kwanini????! Nauliza kwann???! Mwanangu na yeye amefuata nilivyo mimi kwann asingemfuata baba yake watoto wote duniani hufuata nyayo za baba yao kwann huyu afuate nyayo zangu Mungu nilikuomba mtoto huyu awe wa kawaida kabisa tangu nilipogundua ya kuwa niko na mimba sasa kwann hukunisikia Si nilikwambia ctaki awe jini kama mimi.....!!, alizungumza na kupiga kelele.



    "Mama unamaanisha nini unaposema Jini mimi siyo jini hata kidogo mimi ni Salhat mama......,......mimi ni mwanao Salhat huu nilionao ni ugonjwa na utakwisha tu kwani Johnny alinmbia ya kuwa ugonjwa wangu utakwisha.



    "Unamanisha nini ukisema Johnny alikwambia utakwisha!??? Aliuliza kwa mshangao.



    "Nilikuwa nikicheza naye kule ndani ndiyo maana hata tulidondoka naye" alimuelekeza mama yake .



    Samia alijua maisha ya mwanaye sasa yatakuwa katika hali ya hatari Kubwa sana na kama alivyowaza sasa alitaka kufanya jambo.



    "Hili siri hii iendelee kuwa siri basi sina budi kumuuwa Johnny" alizungumza kimoyo moyo bila Salhat kujua alichokizungumza.



    Alianda pa kulala na kwa Siku hiyo walilala ndani ya kibanda kilichokuwa hakina mtu msituni.



    Baada ya usingizi kumpitia Salhat.......Samia aliamka taratibu kabisa kisha kumsogelea mwanaye karibu zaidi akimpapasa kichwa. Hatimaye alipotea na kutokea nyumbani kwa wakina Jonny aliingia ndan ya chmba cha Johnny na kukuta picha za binti yake zikiwa zimetanda chumba kizima picha hizo alizichora Johnny mwenyewe ambapo kila alipoweza kukumbuka busara na upole wa Salhat aliendelea kuchora picha zaidi na zaidi.



    Samia alimsogelea kwa ukaribu zaidi kisha kuanza kutoa miale ya radi lakini alishindwa kabisa na kujikuta amedondoka chini kwa uchungu kishindo hicho Johnny alikisikia na kumfanya ageuke



    "Mama alimuita baada ya kumuona Mama yake Salhat aliificha picha ile ya Salhat aliyekuwa ameichora lakini aliona anafanya kitu cha ajabu atawezaje kuficha picha moja ilihali ziko karibia 50 ukutani.



    "Ma...... Alitaka kumuita mama yake lakini Samia alimzuia Asimuite.



    "Yuko wapi Salhat??!! Aliuliza Johnny



    "Salhat..........

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ""Niko hapa ilisikika sauti ya Salhat ikielekeza mahali alipo.



    Salhat hakuw amelala hivyo alimsikia mama yake pindi alipomuaga na kuja eneo lile kwahiyo alimfuata.



    Johnny baada ya kumuona alimfuata na kumkumbatia Salhat kwa nguvu sana.



    .



    ****** ********



    ITAENDELEA
    Pseudepigraphas

0 comments:

Post a Comment

Blog