IMEANDIKWA NA :NYEMO
CHILONGANI
*********************************************************************************
Simulizi : Mcheza Filamu Za
Ngono
Sehemu Ya Kwanza (1)
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kampuni ya kutengeneza filamu za ngono ya Digital Playground ndio ambayo ilikuwa ikivuma sana katika kipindi hicho duniani kutokana na filamu zake za
ngono kuwa katika ubora mkubwa huku wakijitahidi kuwasainisha mikataba wasichana mbalimbali ambao walikuwa warembo kwa ajili ya kucheza filamu
mbalimbali za ngono.
Kampuni hii ambayo ilianza mwaka 1988 ilikuwa kampuni ya tatu ya filamu za ngono zilizowahi kutengenezwa ambayo mpaka muda huo ilikuwa ikiendelea
kuwepo. Makampuni mengi ya kutengeza filamu za ngono yalikuwa yamefilisika hadi hatua ambayo iliyafanya kutokuwepo kabisa na kusahaulika.
Wasichana wengi walikuwa wakitamani kujiunga na kampuni hiyo, hawakujali kama wangejiunga na kampuni hiyo viungo vyao vyote vya mwili vingeweza
kuonekana na kila atakayekwenda kuziangalia filamu zile au la, kitu ambacho walikuwa wakikiangalia katika kipindi kile ni fedha tu.
Kampuni hiyo ndio ilikuwa kampuni ambayo ilikuwa ikiwalipa waigizaji wake kiasi kikubwa cha fedha huku nayo ikiingiza kiasi kikubwa zaidi kwa kufanya CD
za video zao kununulika kupita kawaida na hata wakati mwingine kuendelea kuziuza katika mitandao mbalimbali duniani ukiwepo mtandao wa Brazzers.
Watu walikuwa wakiingiza fedha kupita kawaida, siku ya usaili wa kuchagua wasichana ambao wangeingia mikataba ifikapo, wasichana zaidi ya mia tano kutoka
sehemu mbalimbali walikuwa wakikusanyika kwa ajili ya kufanyiwa usaili.
Kila msichana alitaka kuwa na jina kubwa pamoja na fedha nyingi kama alizokuwa nazo msichana Katie Mike ambaye alikuwa miongoni mwa masupastaa
wakubwa ambao walikuwa wakicheza filamu hizo nchini Marekani ndani ya kampuni hiyo kubwa ya Digital Playground.
Katie alikuwa miongoni mwa matajiri wakubwa ambao walikuwa wakijishughulisha na kucheza filamu zile. Kazi yake ile ndio ambayo ilionekana kumpa fedha
kila siku, kuuacha mwili wake wazi na kufanya mapenzi na wanaume mbele ya kamera ndio yalikuwa maisha yake ya kila siku.
Katie hakuonekana kujisikia aibu mbele ya kamera, kila alipokuwa mbele ya kamera, alikuwa akionekana kuwa makini na kazi yake kuliko muigizaji yeyote wa
muvi zile. Katie akapata jina kubwa nchini Marekani hasa kwa kila mtu ambaye alikuwa akipenda kuangalia filamu zile.
Katie alianza kuigiza filamu zile tangu alipofikisha miaka kumi na nane. Maisha ya shida ambayo alikuwa akiishi kipindi cha nyuma ndio ambayo yalimsukuma
kujiingiza katika uigizaji wa filamu zile. Wazazi wake walikuwa wamekwishafariki, hakuwa na ndugu yeyote yule, maisha ya mitaani ndio yalikuwa maisha
yake.
Alipofikisha umri wa miaka kumi na saba huku akiwa bado mtaani ndipo hapo alipoona tangazo kwamba watu ambao walikuwa wakitaka kuigiza muvi za
ngono walikuwa wakihitajika kwa ajili ya kufanyiwa usaili katika kampuni ya filamu zile ya Digital Playground. Katie hakuonekana kuamini, kila siku alikuwa
akihitaji kupata fedha kwa ajili ya kujikimu na maisha yake ya tabu, tangazo lile kwake likaonekana kuwa kama bahati kubwa na nzuri, hivyo hakutaka kuiacha
ikipita.
Siku iliyofuata asubuhi na mapema akaelekea bafuni kuoga. Kitu cha kwanza ambacho alikifanya bafuni mule ni kuangalia sehemu zake za siri. Alichukua muda
mrefu kuziangalia na kisha kuanza kuoga. Ingawa alijua kwamba alikuwa na umri mdogo lakini wala hakuonekana kujali, hakuonekana kuhofia kitu chochote
kile, bado alikuwa akitaka kuwa miongoni mwa waigizaji wa muvi zile.
Alipomaliza kuoga, akajiandaa na kuanza kuelekea katika ofisi za kampuni ile. Wanawake zaidi ya mia saba walikuwa wamefika mahali pale. Walikuwa
wanawake wa kila rika na kila ngozi. Walikuwepo wanawake wa kizungu, kiarabu, waswahili na hata wahindi na waarabu.
Kila mtu alikuwa akitaka kufanyiwa usaili na hatimae aanze kuigiza filamu zile huku lengo likiwa ni kupata fedha tu. Kila mtu ambaye alimuona Katie
alionekana kumshangaa, hakukuwa na mtu ambaye aliamini kama Katie angekuwa miongozi mwa wanawake ambao walikuwa mahali pale.
Kwa muonekano tu, alionekana kuwa binti mdogo ambaye hakuwa amefikisha miaka kumi na nane. Huku akiwa amepanga foleni kwa ajili ya kuchukua namba
kwenye kidirisha, akajikuta akifuatwa na wanaume wawili na kisha kutolewa katika foleni ile.
“What are you doing here? (Unafanya nini hapa?)” Mwanaume mmoja alimuuliza kwa sauti iliyojaa ukali kidogo.
“I want to be a porn movie star (Nataka kuwa muigizaji wa filamu za ngono)” Katie alijibu huku akimwangalia mwanaume yule aliyemuuliza swali lile.
Katie hakuonekana kujisikia aibu hata kidogo, lengo lake kwa wakati huo lilikuwa ni kutaka kuigiza filamu za ngono tu kwa ajili ya kupata fedha na kumuondoa
katika umasikini ambao alikuwa nao. Wanaume wale wakabaki wakiangaliana tu, hawakuamini kama Katie angekuwa jasiri kuwajibu namna ile.
“Damnfool! You are fucking too young, get out of here! ( Pumbafu kabisa! U mdogo mno, toka mahali hapa)” Mwanaume yule alimwambia Katie huku
akionekana kukasirika.
Katie hakutaka kuondoka, bado alikuwa aking’ang’ania kubaki mahali hapo kwa ajili ya kuchukuliwa na kupelekwa katika usaili. Fujo ikaanza kutokea,
wanaume wale walikuwa wakimtaka Katie aondoke mahali pale lakini Katie hakutaka kuelewa kitu chochote kile, bado alikuwa aking’ang’ania kubaki na
kuingia kwenye usaili.
Maisha ya mitaani yakaonekana kumharibu Katie, fujo ambazo alikuwa akizileta mahali pale zilikuwa kubwa. Hakushikika kirahisi, alikuwa akileta sana fujo
mpaka kufikia hatua Meneja wa kampuni ile kutokea mahali hapo hasa baada ya kusikia kelele.
“What the hell is going on here? (Nini kinaendelea hapa?)”
“This kid (Huyu mtoto)”
“What the hell with her? (Amefanya nini)”
“She wants to be a porn movie star (Anataka kuwa muigizaji wa filamu za ngono)” Mwanaume yule alijibu hali iliyowasababisha wanawake ambao walikuwa
wamepanga foleni kuanza kucheka.
“You must be kiddin’ me (Ni lazima mtakuwa mnanitania)” Meneja yule, Bwana Donald alisema huku akionekana kushangaa.
“I want to be a porn movie star (Ninataka kuwa muigizaji wa filamu za ngono)” Katie alimwambia Bwana Donald ambaye akaonekana kutokuamini.
Alichokifanya Bwana Donald ni kumchukua Katie na kuanza kuelekea ofisini mwake kwani aliona kama binti yule angeendelea kubaki mahali pale basi fujo
zaidi zingeendelea kutokea mahali pale. Walipofika ofisini, akaambiwa akae kwenye kiti kimojawapo kati ya viti vilivyokuwa ndani ya ofisi ile na kisha
mazungumzo kuanza.
“Unasema unataka kuwa nani?” Bwana Donald alimuuliza.
“Muigizaji wa filamu za ngono” Katie alijibu huku akijaribu kuyafuta machozi yaliyokuwa yakimtoka.
“Unaitwa nani?”
“Naitwa Katie Mike”
“Una miaka mingapi?”
“Kumi na saba”
“U mdogo sana Katie. Hatuwezi kukuajiri katika kampuni hii, na kama tukifanya hivyo basi tunaweza kuchukuliwa hatua kali za kisheria na Serikali. Hatutaki
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
jambo hilo litokee” Bwana Donald alimwambia Katie.
“Nataka kuigiza”
“Haiwezekani. Nenda nyumbani, tutakapohitaji watu wengine mwaka kesho, utatakiwa uje na kujaribu bahati yako” Bwana Donald alimwambia Katie.
Katie hakuonekana kuelewa kitu chochote kile, bado alikuwa aking’ang’ania kuwa miongoni mwa waigizaji wa filamu zile za ngono. Bwana Donald
akaonekana kumsoma Katie, tayari aliona kuna kitu ambacho kilikuwa kinaendelea katika maisha ya msichana yule.
“Unaishi wapi?”
“Mtaani?”
“Mtaani? Mtaa upi?”
“Woodmere 45”
“Unaishi na nani?”
“Na wenzangu”
“Wenzako wakina nani?”
“Wenzangu. Watoto wenzangu”
“Mungu wangu! Kwa hiyo wewe ni mtoto wa mitaani?”
“Ndio”
“Ok! Nimeshaelewa.” Bwana Donald alisema.
Hapo hapo Bwana Donald akaingiza mkono wake mfukoni na kutoa pochi yake, akaifungua na kutoa kiasi cha dola mia tatu na kumkabidhi Katie. Kiasi kile
kikaonekana kuwa kikubwa kwa Katie, akakichukua na kukiweka katika mifuko ya suruali yake ya jinzi.
“Sisi kama kampuni tutakuwa tunakutunza mpaka mwaka ujao utakapofika. Tutakupa mkataba bila kukufanyia usaili wowote ule. Tutakusaidia kwa kila kitu
katika kipindi hiki. Kama itawezekana, kila mwisho wa wiki njoo uchukue kiasi fulani cha fedha kwa ajili ya kukusaidia katika maisha yako ya kila siku.
Utakapofika mwaka kesho, tutakupa mkataba na kuanza kuigiza filamu hizo katika kampuni yetu hii” Bwana Donald alimwambia Katie ambaye akaonekana
kuelewa na kuondoka mahali hapo.
Kuanzia hapo kidogo maisha ya Katie yakaanza kubadilika, kiasi cha fedha ambacho alikuwa akikipata kila wiki kilionekana kumsaidia. Kitu alichokifanya kwa
wakati huo ni kuanza mazoezi mapema. Akaanza kufanya mapenzi na vijana mbalimbali wa mitaani, kitu ambacho alikuwa akikihitaji sana katika kipindi hicho
ni kuizoesha njia yake sehemu za siri ili hata atakapoanza kazi hiyo asiweze kusikia maumivu yoyote yale.
Kati ya wavulana wote ambao alikuwa akifanya nao mapenzi, Daniel. akaonekana kuvutiwa nae. Daniel akaanza kumpenda Katie. Mara kwa mara Daniel
alikuwa akifanya mapenzi na Katie. Kwake akaanza kumchukulia kama mpenzi wake japokuwa kichwani mwa Katie kulikuwa na kitu kingine kabisa, alikuwa
kwenye mazoezi mazito.
Kila siku Daniel alijitahidi kumwambia Katie maneno mbalimbali ya mapenzi lakini Katie hakuonekana kuelewa kitu chochote kile, kwake hakuhitaji uhusiano.
Uhusiano wala haukuwa ukikubaliwa hata kidogo lakini kila wakati Daniel alipohitaji kufanya mapenzi na Katie, Katie hakuweza kuleta kipingamizi chochote
kile.
Siku ziliendelea kukatika, njia ya sehemu ya siri ya Katie ikajitosheleza. Mwaka ukaisha na mwaka mwingine ulipoingia, mwezi wa nne, akaanza kuelekea katika
ofisi ile huku akiwa amekwishafikisha miaka kumi na nane. Kwa sababu walimuona kuwa mtu wao, moja kwa moja Katie akasaini mkataba wa kulipwa kiasi
kikubwa cha fedha na kisha kuanza kazi ya kuigiza filamu za ngono katika kampuni hiyo ya Digital Playground iliyokuwa nchini Marekani katika jiji la New
York.
Kwa sasa, miaka saba ilikuwa imepita, kwa kipindi hiki Katie alikuwa na miaka ishirini na tano. Tayari kile ambacho alikuwa akikihitaji alikuwa
amekwishakipata. Alikuwa akimiliki kiasi kikubwa cha fedha. Kwa kuwa alikuwa amejiingiza katika uigizaji wa filamu zile, kamwe hakuacha, bado alikuwa
akiigiza zaidi na zaidi.
Daniel hakuwa akilini mwake katika kipindi hicho. Aliamua kutengana nae mara tu alipoanza kuigiza filamu zile. Jina lake lilikuwa kubwa sana, alikuwa
akiigiza filamu nyingi sana ambazo zilikuwa zikiingizia kampuni kiasi kikubwa cha fedha.
Uzuri wake ndio ambao uliwafanya watu kupenda kununua filamu ambazo alikuwa ameigiza. Filamu nyingi ambazo zilikuwa zikitengenezwa na kampuni ile
zilikuwa ni filamu ndefu zilizojaa visa lakini zilikuwa zimejaa ngono kila wakati. Picha zake zilikuwa zikitolewa kwenye majarida na magazeti mbalimbali,
utajiri wake ulikuwa mkubwa.
“Kuna filamu moja inatupasa kuigiza” Bwana Donald aliwaambia waigizaji na kuendelea.
“Filamu hii itaigizwa barani Afrika hasa katika nchi moja iitwayo Tanzania. Sehemu ambayo tutakwenda kuigiza baadhi ya vipande vya filamu hii ni Zanzibar
kwa sababu kuna hoteli nzuri na mandhari mazuri pia. Miswada imeshaandikwa, wasanii jiandaeni, kama kawaida, Katie utakuwa muigizaji mkuu. Miswada ni
rahisi kuishika. Tutasafiri wiki ijayo kuelekea huko. Jiandaeni vilivyo” Bwana Donald aliwaambia hali ambayo iliwafanya waigizaji kuwa na furaha.
Ndani ya ndege kila mtu alionekana kuwa na furaha, waigizaji walikuwa wakipiga stori huku safari ikiendelea. Hiyo ndio iikuwa safari ya kwanza kuja Afrika
kwa kazi ya kuigiza. Kwao, safari hii ilionekana kuwa na baraka nyingi na walitumaini kuuza kazi hiyo zaidi ya kazi zote ambazo zilikuwa zimepita.
Katie alikuwa bize na kusoma jarida maalumu ambalo lilikuwa likielezea nchi ya Tanzania kuanzia uoto wa asili na mambo mengine mengi. Maeneo mengi
yakaonekana kumvutia, tayari akilini mwake ikajengeka picha kwamba nchi ya Tanzania ilikuwa ni miongoni mwa nchi zilizokuwa na mazingira mazuri hasa
kimisitu.
Ndani ya ndege hiyo kulikuwa na waigizaji wote ambao walikuwa wamechaguliwa kwa ajili ya kuigiza filamu hiyo ya ngono ambayo waliipa jina la MY
NEIGHBOURHOOD CHICKS. Katika kipindi hicho walikuwa na kila kitu, kamera kubwa zilizokuwa na uwezo mkubwa, wapiga picha na waongozaji, wote
walikuwa ndani ya ndege hiyo.
Ndege hiyo wala haikupitia jijini Dar es Salaam. Kwa kuwa ilikuwa ni ndege yao wenyewe, ndege ya kampuni yao, ikapita moja kwa moja mpaka katika uwanja
wa ndege wa Abeid Amani Karume, Zanzibar.
Hali ya hewa kwao ikaonekana kuwa nafuu. Nchini Marekani, baridi lilikuwa likiwapiga kila siku, hawakuipenda hali ile ya hewa lakini walikubaliana nayo. Joto
ambalo walikutana nalo nchini Tanzania likaonekana kuwafurahisha.
Kila kitu kilikuwa kimekwishapangwa. Mara baada ya kushuka kutoka ndani ya ndege, wakapanda kwenye magari maalumu ya hoteli ya Green Horse na kisha
kuanza kwenda katika hoteli hiyo.
Njiani, kla mmoja alikuwa akiangalia nje, majengo ya kizamani ambayo yalikuwa yametumiwa enzi za ukoloni yakaonekana kuwa na mvuto machoni mwao.
Kila wakati walikuwa wakitabasamu, hawakuamini kama kulikuwa na majengo mazuri kama yake.
Gari lile likafika katika hoteli ya Grean House ambayo ilikuwa pembezoni mwa bahari ya Hindi na kisha kuingia ndani. Muonekano wa hoteli ile ulikuwa

sawasawa na hoteli ambazo zilikuwa zimejengwa nchini Marekani. Upepo mwanana wa bahari ambao ulikuwa ukiwapiga ukaonekana kuwafurahisha.
Wakachukua vyumba ndani ya hoteli hiyo, kwa kuwa walikuwa na fedha za kutosha, kila mmoja akakabidhiwa chumba chake ila kwa wale ambao walitaka
kulala wawili wawili walikuwa wakiruhusiwa.
Katie akatulia kitandani kwake, akachukua kitabu cha Atlas ambacho kilikuwa mezani na kisha kuanza kukifungua na kuangalia mambo mbalimbali kuhusiana
na nchi ya Tanzania. Hapo ndipo alipogundua kwamba pale walipokuwa walikuwa katika moja ya kisiwa cha Unguja.
Moyoni mwake, Katie akaanza kuvutiwa, akatamani kuziona zile mbuga za wanyama ambazo zilikuwa zikionekana katika ramani ya nchi ya Tanzania.
Alichokifanywa kwa wakati huo ni kuifuata kompyuta ya mezani na kisha kufungua Internet na website ya Google na kisha kuandika ‘Mikumi National Park’
Picha za mbuga hiyo zikatokea, Katie akabaki akitabasamu tu. Hamu ya kutamani kuelekea katika mbuga ile ikaonekana kumkamata kupita kawaida. Katie
hakuishia hapo, bado aliendelea kuangalia zaidi na zaidi, akaandika Kilimanjaro.
Mlima mkubwa wa Kilimajaro ukatokea katika kioo cha kompyuta ile. Akaanza kuuangalia mlima ule ambao juu ulikuwa na barafu jingi. Katie akaachia
tabasamu pana zaidi, alichokuwa akikitaka ni kuchukua picha za mlima ule.
Akaenda kitandani na kisha kufungua begi lake na kutoa kompyuta yake ya mapajani na kisha kuiunganisha na Internet isiyotumia waya iliyokuwa katika hoteli
ile. Akafungua website ya Google na kisha kuandika Kilimanjaro. Ulipotokea mlima Kilimanjaro, akaanza kuzichukua zile picha na kisha kuziweka katika
kompyuta yake.
Baada ya siku mbili kupita, filamu hiyo ambayo walipanga kuuigiza ikaanza. Kwao ikaonekana kuwa filamu nzuri, kila miuigizaji ambaye alikuwa amepangwa
kuigiza katika filamu hiyo alikuwa akiigiza kwa umakini mkubwa na kujitolea hasa.
Kwa sababu Katie ndiye alikuwa muigizaji mkuu, aliigiza kwa ustadi mkubwa kiasi ambacho hata muongozaji akashangaa. Filamu hiyo wala haikuwa ndefu
sana, walichukua kipindi cha mwezi mmoja ikawa imekamilika.
Ni matukio ya ngono ndio ambayo yalikuwa yametawala ndani ya filamu hiyo ambayo ingeonekana kuwavutia wale wote ambao walikuwa wakipenda kuangalia
filamu za aina hiyo duniani.
Baada ya kumaliza kuigiza filamu hiyo, Katie akatoa wazo ambalo lilionekana kumvutia kila mtu. Alichoona yeye ilikuwa ni vizuri kwa wao wote kuelekea
katika mbuga yoyote ile ya wanyama kwa lengo kubwa la kuona wanyama.
Kila mmoja akaonekana kuridhika na wazo lile, lilionekana kuwa wazo zuri ambalo liliungwa mkono na kila mtu. Siku iliyofuata, safari ya kuelekea Morogoro
ikaanza huku wakitaka kuingia katika mbuga ya wanyama ya Mikumi na kuangalia wanyama.
Kwa kuwa walikuwa wametumia ndege, walichukua dakika arobaini na tano wakawa wamekwishafika Morogoro ambapo wakakutana na magari ya mbuga hiyo
na moja kwa moja kuanza kupelekwa katika mbuga hiyo iliyokuwa na wanyama wengi na wa aina mbalimbali.
Walipofika mbugani, wakapelekwa katika hoteli ya MIKUMI NATIONAL PARK na kisha kuchukua vyumba katika hoteli hiyo. Siku iliyofuata, wakachukuliwa
na magari ya mbugani na kisha kuanza kupelekwa sehemu mbalimbali katika mbuga hiyo.
Muda mwingi Katie alikuwa kimya ndani ya gari lile, macho yake yalikuwa yakimwangalia dereva ambaye alikuwa akiliendesha gari lile, Gibson. Gibson kwake
alionekana kuwa kijana wa tofauti, umbo lake kubwa lilimvutia Katie.
Kwake, Gibson alionekana kuwa kijana mwenye mvuto, fulana yake aliyokuwa ameivaa ambayo ilimbana sana mwili ilimfanya mwili wake uliojazia kuonekana
vizuri kabisa. Muda mwingi Katie alikuwa akiendelea kuutumia muda wake kumwangalia Gibson ambaye alikuwa bize akiwatembeza huku vijana wengine
wawili wakitumia muda huo kuwaelekeza wazungu wale sehemu mbalimbali na kuwaonyeshea wanyama mbalimbali.
Akili ya katie haikuwa sawa katika wakati huo, mvuto ambao alikuwa nao Gibson ukaonekana kuusumbua moyo wake. Ni kweli kwamba alikuwa amewaona
wanaume wengi na kufanya mapenzi na wanaume wengi pia lakini kwa Gibson hali ikaonekana kuwa tofauti sana.
Kwake, mwanaume huyo alikuwa na mvuto mkubwa, kifua kipana kilionekana kumchanganya kupita kawaida. Ingawa waigizaji wengine walikuwa bize
kuwasikiliza vijana ambao walikuwa wakiwaelekeza mambo mengi lakini kwa Katie muda wote macho yake yalikuwa yakimwangalia Gibson.
Katie akashindwa kuvumilia, alichokifanya ni kuanza kupiga hatua kumfuata Gibson, alipomfikia, akaamua kumsogelea karibu zaidi. Gibson hakuonekana kuwa
na wasiwasi, kwake, wazungu walionekana kuwa watu wa kawaida sana kiasi ambacho ilimjia vigumu sana kumtambua msichana wa kizungu kama alikuwa
ameangukia katika mapenzi.
“Hi” Katie alimsalimia Gibson huku tabasamu pana likiutawala uso wake.
“Hi” Gibson aliitikia.
Katie akaanza kujiumauma. Wakati mwingine alikuwa akijishikashika kiuno, mara akiikutanisha mikono yake na kujishika huku akijipindapinda, kwa wakati
huo alikuwa akijitahidi kuleta mapozi mengi ya kizungu ili Gibson aweze kuelewa ni kitu gani kilikuwa kinaendelea kwa wakati huo.
“Can I ask you something? (Naweza kukuuliza kitu?)” Katie alimuuliza.
“Yeah” Gibson alimwambia Katie.
Huo ndio ukawa mwanzo wa maongezi yao. Katika kila hatua ambayo ilikuwa ikiendelea kati yao, Gibson alikuwa akichukulia kawaida tu japokuwa muda
mwingi Katie alikuwa akionyesha dalili zote kwamba alikuwa akimhitaji Gibson kwa kipindi hicho.
Dakika ziiendelea kwenda mbele, Gibson akaja kugundua kwamba Katie alikuwa kwenye hisia kali hasa mara baada ya kufanya tukio ambalo lilionekana
kumshtua, kushika maeneo ya zipu yake.
Gibson alibaki akitetemeka, hakuamini kile ambacho Katie alikuwa amekifanya. Kwa mara ya kwanza alifikiri labda ilikuwa ni bahati mbaya lakini baada ya
kuyapeleka macho yake usoni mwa Katie, msichana yule alikuwa akitabasamu tu.
“Mmh!” Gibson aliguna.
Kuanzia muda huo Katie hakutaka kuficha kitu chochote kile, akaanza kujionyesha dhahiri kwamba alikuwa ametekwa na mapenzi ya mwanaume huyo.
Japokuwa Gibson alijitahidi sana kuzuga ili wazungu wengine wasiweze kuelewa kilichokuwa kinaendelea lakini hali ikaonekana kushindikana kabisa, kila mtu
akafahamu.
Kwa sababu maisha yao yalikuwa ni ya kawaida, Katie hakutaka kujificha, akaamua kuwaambia wenzake kwamba kwa kipindi hicho moyo wake ulikuwa
umetekwa kwa asilimia mia moja na Gibson. Gibson hakuongea kitu, muda wote alikuwa akijisikia aibu.
Muda wa kurudi hotelini ulipofika, wakaanza kurudi huku Katie akiwa kiti cha mbele kabisa. Katika kipindi hicho alikuwa akihakikisha kwamba anafanya kila
liwezekanalo mpaka mwanaume huyo, Gibson anakuwa wake bila kujua kwamba Gibson alikuwa na mchumba aliyeitwa Prisca, ambaye alikuwa akimpenda
kuliko mwanamke yeyote huku tumboni mwake akiwa na kiumbe alichosaidiana kutengeneza na Gibson, ujauzito.
****CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kijana Gibson alikuwa akijulikana sana katika mtaa wa Mwembechai sehemu ambayo alikuwa akiishi ndani ya jiji la Dar es Salaam. Maisha yake yalikuwa ni
maisha ya kawaida sana, utafutaji wake ambao alikuwa akiufanya kila siku ndio ambao ulikuwa ukimuweka hapa mjini kila siku.
Gibson alimaliza Elimu ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mbezi High iliyokuwa maeneo ya Mbezi ile ya kuelekea Kibaha. Katika maisha yake ya
shuleni ndani ya shule hiyo, Gibson akafanikiwa kupata marafiki wengi ambao walikuwa wakivutiwa nae kutokana na ucheshi mkubwa ambao alikuwa nao.
Wasichana nao hawakuwa nyuma, walikuwa wakimpenda sana Gibson kiasi ambacho kila msichana akatamani kuwa nae. Gibson hakutaka kujirahisisha kabisa,
kwa kipindi hicho maisha yake yalikuwa yakifikiria elimu tu.
Hakujua ni wapi alipokosea mpaka msimamo wake wa kutokutaka kuwa na msichana kupotea, akajikuta akiangukia katika mapenzi ya msichana Prisca.
Uhusiano wao wa kimapenzi ukaanzia hapo. Mara kwa mara walionekana kuwa pamoja, wanafunzi wakaufahamu uhusiano huo japokuwa wao wenyewe
walijaribu kuuficha ukweli.
Miezi ikaendelea kukatika mpaka pale ambapo wakamaliza elimu ya kidato cha sita na kukaa nyumbani kwa ajili ya kusubiria matokeo. Kwao, kumaliza kule
kulionekana kuwa na unafuu, wakaanza kujiachia vya kutosha, walikuwa wakifanya mapenzi mara kwa mara hasa katika kila kipindi ambacho msichana Prisca
alipokuwa akienda kumtembelea Gibson.
Miezi ikakatika na matokeo kutoka, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa amefanya vizuri, wote walikuwa wamefeli mitihani yao. Wote wakaonekana kuumia,
hawakuamini kile ambacho kilikuwa kimetokea lakini ikawabidi kukubaliana na ukweli kwamba walikuwa wamefeli mitihani yao.
Maisha ya mitaani yakaanza. Kwa kuwa kila siku alikuwa akishinda sana nyumbani, akaanza kuonekana kuwa mzigo kwa wazazi wake. Mzee Lyimo ambaye
alikuwa baba yake, akaamua kumpa kiasi cha shilingi milioni moja na nusu kwa ajili ya kwenda kuanzisha biashara.
Gibson akazitumia fedha zile vilivyo, akaanzisha biashara ndogo ndogo ambazo zikaanza kukua kila siku na kuanza kumuingizia fedha japokuwa hazikuwa
nyingi sana. Bado uhusiano wake na Prisca ulikuwa ukiendelea kama kawaida.
Kila siku walikuwa wakitumia kinga. Mioyoni mwao hawakuwa na wasiwasi na magonjwa ya zinaa au UKIMWI bali walikuwa na wasiwasi na mimba tu. Ndani
ya chumba cha Gibson, mipira ya kufanyia mapenzi ilikuwa mingi na alikuwa akiitumia katika siku ambazo Prisca alikuwa akija nyumbani hapo.
“Mmmh! Hili baridi” Gibson alimwambia Prisca huku manyunyu yakimwagika nje.
“Limefanya nini tena?” Prisca aliuliza.
“Linanipa hali fulani ya kuhitaji joto” Gibson alimwambia Prisca.
“Ngoja nikupe sweta” Prisca alimwambia Gibson huku akiachia tabasamu.
“Hapana. Hebu njoo karibu yangu” Gibson alimwambia Prisca ambaye akamsogelea pale kitandani na kisha kumkumbatia.
Hali ile ndio ambayo ikaonekana kuwa na unafuu kwa Gibson, kwa mbali akaanza kuhisi joto kutoka katika mwili wa Prisca. Gibson hakuona hali ile kutosha,
akaamua kuipitisha mikono yake katika kiuno cha Prisca. Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo Gibson alivyozidi kuipeleka mikono yake
zaidi na zaidi katika mwili wa Prisca, baada ya dakika chache, Prisca alikuwa mtupu.
Hilo ndilo lilikuwa lengo la Gibson, kilichofuata mahali hapo ni kuanza kumchezea Prisca. Aliendelea na mchezo ule mpaka pale alipoona ameridhika.
Akaupeleka mkono wake katika boksi la mipira, hakukuwa na mpira hata mmoja.
“Da! Kumbe yote iliisha!” Gibson alijisemea moyoni.
Hakuwa na jinsi. Kwa hali ambayo alikuwa nayo mahali pale ilikuwa ni vigumu kuinuka na kuelekea duka la madawa kununua mipira, alichokifanya ni kufanya
mapenzi na Prisca bila kutumia mpira wowote.
Hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kufanya mapenzi na Prisca bila kutumia mpira, hiyo ndio ilikuwa siku ambayo ikamsababishia Prisca kuanza kutapika na
kujisikia kichefu chefu, siku hiyo ndio ambayo ilimfanya Gibson kujiandaa kuitwa baba.
Prisca akawa na ujauzito. Marafiki zake Gibson walikuwa wakimshauri mara kwa mara kwamba amwambie Prisca aende akautoe ujauzito ule lakini Gibson
hakuonekana kukubali. Moyo wake ulikuwa ukimpenda sana mtoto wake ambaye alikuwa tumboni mwa mpenzi wake, Prisca.
Kutokana na kuwa bize na ujauzito wa Prisca, biashara zake zikaanza kuyumba. Faida aliyokuwa kipata alikuwa akiitumia kumtunza Prisca ambaye alionekana
kuwa kwenye wakati mgumu. Kwa kuwa kipindi hicho alikuwa amepanga, hakutaka wazazi wake wafahamu kitu chochote kile.
Tayari Gibson alikwishaona kwamba mambo yalikuwa magumu. Kiasi cha fedha ambacho alikuwa amebaki nacho, akaamua kujifunza udereva. Alisoma kwa
muda wa mwezi mmoja, alipoona amekuwa tayari, akaamua kwenda kusoma NIT ili aweze kuendesha magari ya viongozi mbalimbali wa Serikalini.
Gibson akawa dereva mzuri, masomo yake akawa amemaliza kwa kufanya vizuri mpaka pale ambapo alipewa cheti tayari kwa kuanza kazi pale ambapo
angeipata. Kwa wakati huo, kiasi ambacho alikuwa amebaki nacho kilikuwa kidogo sana, akaamua kukibana hivyo hivyo mpaka pale kilipokwisha.
Kazi zikaonekana kuwa ngumu kupatikana. Aliangaika kwa muda wa miezi mitatu na ndipo alipoona kwenye gazeti kwamba kampuni ya Utalii ya Filbert Royal
Tourism iliyokuwa Morogoro katika mbuga ya Mikumi ilikuwa ikitafuta madereva.
Gibson hakutaka kupuzia, japokuwa alikuwa amejaribu kuomba kazi sehemu nyingi na kukosa, hapo napo akaamua kujaribu. Baada ya wiki moja, akaitwa kwa
ajili ya kufanyiwa usaili na alipoonekana kustahili, akaanza kazi.
Hiyo ikaonekana kuwa furaha kwake. Mshahara wake wa kwanza, akamsafirisha Prisca na kuishi nae mkoani Morogoro huku wazazi wa binti huyo wakiwa
wameridhia kwa kila kitu. Ukaribu ambao alikuwa nao kwa mpenzi wake ulikuwa mkubwa, kila alipokuwa akitoka ofisini, moja kwa moja alikuwa akielekea
nyumbani na kukaa na mpenzi wake, Prisca.
Maisha yaliendelea kila siku. Tumbo la Prisca kwa kipindi hiki lilikuwa kubwa. Alichokifanya Gibson ni kumuajiri mfanyakazi wa ndani kwa ajili ya
kumwangalia mpenzi wake na kumfanyia kazi nyingine.
Simu ndio kilikuwa chombo ambacho alikuwa akipenda sana kukitumia kuwasiliana na Prisca kila alipokuwa mbali nae. Hakujisikia raha kama yalipita masaa
mawili bila kuwasiliana na Prisca. Prisca, kwake alikuwa kila kitu, alimpenda kuliko msichana yeyote katika dunia hii.
Wasichana wa Morogoro wakaonekana kuvutiwa sana na Gibson ambapo mara kwa mara walikuwa wakimtaka kimapenzi. Gibson hakuonekana kukubaliana
nao, hakuwa tayari kumsaliti Prisca kwa msichana yeyote yule, mapenzi ambayo alikuwa nayo kwa Prisca yalikuwa ni makubwa sana.
“Ninakupenda sana mpenzi wangu” Gibson ailimwambia Prisca.
“Ninakupenda pia”
“Ulikumbuka kwenda hospitali leo?” Gibson alimuuliza.
“Ndio”
“Dokta amesemaje baada ya kukupima?”
“Otea”
“Wa kike” Gibson alimwambia Prisca.
“Hapana”
“Kwa hiyo ni wa kiume?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndio” Prisca alijibu na kutoa tabasamu kali.
“Asante Mungu. Nilikuwa na kiu ya kupata mtoto wa kwanza awe wa kiume. Mungu amejibu maombi yangu” Gibson alimwambia Prisca.
“Kwa nini haukuomba wa kike?”
“Ninataka kwanza niwe na mlinzi wa nyumba yangu. Wa pili akiwa wa kike, nitafurahi zaidi. Hata kama baadae watakua, huyu wa kike inabidi awe na heshima
kwa kaka yake” Gibson alimwambia Prisca.
“Kwani akiwa wa kwanza wa kike hatokuwa na heshima?”
“Hilo jibu niachie moyoni mwangu. Si unajua nyumbani kwetu wa kwanza ni wa kike! Niachie tu jibu langu kwani naamini mwenyewe umeshaona sana
ulipokuwa ukija nyumbani” Gibson alimwambia Prisca.
Kwa wakati huo walikuwa wakipiga stori ambazo kwa mtu mwingine zingeonekana kuwa za kijinga lakini kwao zilikuwa ni stori nzuri ambazo zilimvutia kila
mmoja. Waliendelea kuongea usiku kucha mpaka katika kipindi ambacho wote wakapitiwa na usingizi.
Siku ya leo haikuonekana kuwa nzuri kwa Gibson, alikuwa amefika nyumbani hapo huku akionekana kutokuwa na furaha kabisa, alikuwa katika hali ambayo
ilikuwa ikimuonyeshea kuwa na unyonge wa hali ya juu. Prisca akaonekana kuishangaa hali ile, hakuwahi kumuona Gibson akirudi katika hali ya unyonge kama
siku hiyo.
Prisca akawa na kiu ya kufahamu sababu iliyomfanya Gibson kuwa katika hali hiyo lakini wala Gibson hakuwa radhi kusema zaidi ya kusingizia kwamba
hakuwa akijisikia vizuri kiafya, hakutaka kumwambia Prisca kwamba msichana Katie ambaye alikutana nae ofisini ndiye ambaye alikuwa amemsababishia hali
ile.
Kichwa cha Gibson kikatawaliwa na jina la Katie, msichana yule, kwake alionekana kuwa msichana mrembo lakini hakuona kama alikuwa na urembo ambao
ungemfanya kumsaliti mpenzi wake, Prisca. Bado alikuwa akimpenda Prisca, bado alikuwa akiona kuwa na uhitaji wa kuendelea kuwa mwaminifu kwa Prisca.
“Kichwa kinauma. Na ninadhani hata mafua yameanza kuuma pia” Gibson alidanganya.
“Pole mpenzi wangu. Ila naona ungekunywa dawa”
“Nimekwishakunywa ofisini. Nilikuwa sijisikii vizuri kwa kipindi kirefu sana” Gibson alimwambia Prisca.
Tayari Katie akaonekana kuanza kuharibu kila kitu moyoni mwake, alijitahidi sana kutokumfikiria lakini jambo hilo likaonekana kuwa gumu moyoni mwake.
Kipindi cha nyuma hasa alipokuwa shuleni kabla hajampata Prisca alikuwa akitamani sana kuwa na msichana wa kizungu huku lengo lake kubwa likiwa kama
tiketi ya urahisi ya kumfanya kuingia katika nchi za Ulaya au Marekani.
Kile kitu ambacho alikuwa akikifikiria, leo kilikuwa kimefika ila kilikuwa kimefika katika wakati mbaya sana. Hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kufanya,
Katie kwake nae alionyesha kuwa na mapenzi ya kweli huku akiwa hajui kabisa kwamba msichana yule alikuwa muigizaji bora wa filamu za ngono duniani.
“Siwezi kumsaliti Prisca” Gibson alijisemea.
Kesho asubuhi ilipofika, asubuhi na mapema kama kawaida yake akaanza kwenda ofisini. Bado akili yake ilikuwa ikimfikiria Katie ambaye alimuona kuwa na
asilimia kubwa ya kuharibu mapenzi yake na Prisca. Gibson hakutaka kuficha, alichokifanya ni kumuita rafiki yake, Richard na kuanza kumpa taarifa.
“Da! Una zali ile kinoma” Richard alimwambia Gibson.
“Nina zali?”
“Sasa unataka niliite nini hilo? Demu wa kizungu mtu wangu, yaani hapo uhakika wa kupata viza nje nje bila usumbufu” Richard alimwambia Gibson.
“Kwa hiyo unataka nifanyeje?”
“Swali la kitoto hilo wewe. Mchukue tu. Lala nae. Yeye si ndio anavyotaka. Kula mshiko wewe” Richard alimwambia Gibson.
“Ushauri wako unaonekana kutokuniingia”
“Tatizo lako moja. Yaani unataka mpaka Mungu akutokee usiku akwambie kwamba hiyo ni nafasi yako ya kwenda Marekani na kuutoka umasikini. Acha hizo
Gibson. Wakati mwingine baraka za Mungu zinakuja kimafumbo. Kama ukiiacha hii, haiji mara mbili” Richard alimwambia Gibson.
“Lakini si unajua ninaishi na mpenzi wangu, Prisca ambaye ni mjauzito?”
“Ndio. Ila ukiwa na huyu mzungu, Prisca atajua? Sikiliza Gibson, ngoja nikueleze kitu kimoja. Wasichana wa Kibongo si wa kuwawekea dhamana. Unaweza
ukagoma kumchukua huyo mzungu kwa ajili yake, halafu huyo huyo Prisca baadae anakuja kutembea na mshikaji mwingine. Hii ndio nafasi. Wazungu
wanasema ‘Nafasi ya dhahabu haiji mara mbili’. Yaani hata misemo ya wahenga umeisahau. Kama hautaki, basi acha ila baadae usije ukajuta tu” Richard
alimwambia Gibson.
Maongezi yao yalikuwa yakiendelea zaidi na zaidi, muda wote Richard alikuwa akimwambia Gibson kuanza uhusiano na Katie. Ingawa maneno yale yalikuwa
hayamuingii kabisa akilini, lakini kadri Richard alivyokuwa akimwambia na ndivyo ambavyo yakaanza kumingia akilini.
“Mmmh! Lakini inawezekana bwana kwamba Mungu ameamua kunipa baraka kimafumbo. Ngoja nami niitumie nafasi hii” Gibson alisema katika kipindi
ambacho alikuwa akiitwa kwenda kuwachukua wazungu wale kuwaingiza ndani ya mbuga huku Katie akiachiwa nafasi ya mbele kabisa kukaa na dereva,
Gibson.
****
Muda mwingi Gibson alikuwa akiyaangalia mapaja ya Katie ambaye alikuwa amekaa pembeni yake ndani ya gari lile. Kwa wakati huo, akili yake haikuwa mahali
hapo tena, ilikuwa ikifikiria ngono tu. Tayari akajiona akianza kuvutwa katika himaya ya msichana yule ambaye alikuwa mcheza filamu za ngono mkubwa
ambaye alikuwa akijulikana sana na watazamaji wa filamu zile.
Katie alijifanya kutulia huku akimuangalia Gibson kwa macho ya wizi, tayari akajiona kufanikiwa juu ya lile lengo lake ambalo alikuwa amejiwekea la kumteka
kimapenzi Gibson. Katie akashindwa kujizuia, akaanza kumgusa gusa Gibson begani mwake, yaani wakati wote alikuwa akimgusagusa tu.
Walipofika mbugani, wote wakaanza kupitishwa huku na kule huku wakiangalia wanyama mbalimbali. Kwa wakati huo kichwa cha Gibson kilikuwa kikifikiria
fedha, tayari akaonekana kugundua kuwa kama angekubali kuwa na Katie, kwa kiasi fulani angekuwa akipata fedha kutoka kwa msichana huyo.
Japokuwa Katie alikuwa akipenda wanyama na wazo la kwenda mbugani lilikuwa lake lakini kwa wakati huo hakuwa na habari na wanyama, kitu ambacho
alikuwa akikifikiria kwa wakati huo ni kuwa pamoja na Gibson tu.
“Will you be ready? (Utakuwa tayari?)” Katie aliuliza.
“For what? (Kwa lipi?)”
“I need you tonight in my bedroom (Ninakuhitaji usiku wa leo chumbani kwangu)” Katie alimwambia Gibson.
Mawazo ya Gibson yakahama kwa wakati huo, akaanza kumkumbuka Prisca wake ambaye alikuwa amemuacha nyumbani akiwa mjauzito. Maneno yale ambayo
aliyaongea Katie yalikuwa na maana kwamba kama alikuwa tayari kumsaliti Prisca usiku wa siku ile. Kichwa chake hakikuweza kutulia, alimpenda sana Prisca
na alimpa ahadi nyingi huku miongoni mwa ahadi hiyo ikiwa ni ya kutokumsaliti katika maisha yake yote.
“Haiwezekani” Gibson alijisemea moyoni.
Huku akiwa amelifikiria jibu hilo, mara kumbukumbu ya rafiki yake Richard ikaanza kujirudia kichwani mwake. Maneno mengi ya Richard ambayo yalikuwa

yakimtaka kutokuacha kumkubali Katie yalikuwa yakijirudia kichwani mwake.
Maneno yale bado yalikuwa yakijirudia kwamba ile ilikuwa ni bahati ambayo Gibson alikuwa ameipata na kamwe asikubali kuipoteza kwani kama angeipoteza
kamwe isingeweza kurudi tena mikononi mwake.
Tayari hapo akatengeneza jibu la kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya na ambacho kilionekana kuwa uamuzi sahihi kutoka moyoni mwake. Hakukuwa na
kingine alichokifikiria zaidi ya kukubali kile ambacho kilikuwa kikitakiwa kufanyika na Katie.
“Kwani Prisca atajua? Hawezi jua bwana. Kwanza kufanya mapenzi na mwanamke wa kizungu bahati kwa sisi wenye ngozi nyeusi tuishio Afrika” Gibson
alijisemea.
Akayarudisha macho yake usoni mwa Katie na kisha kuachia tabasamu pana ambalo lilionyesha kukubaliana na kile kitu ambacho alikuwa amezungumza Katie.
Matembezi ndani ya mbuga ile yaliendelea zaidi na zaidi mpaka ilipofika saa kumi na mbili, muda ambao walitakiwa kurudi hotelini.
Kitu cha kwanza alichokifanya Gibson mara baada ya kufika hotelini ni kuanza kumtafuta Richard na kisha kumwambia uamuzi ambao alikuwa ameupanga na
ambao aliuona kufaa kwa kipindi hicho.
“Kama umekubali hapo sawa. Wanawake kama hao ambao wanakuja kuja wewe chukua tu” Richard alimwambia Gibson.
“Ila kitu hii nataka kibaki siri kati yangu na wewe”
“Usijali. Yule mjauzito hatojua” Richard alimwambia Gibson.
“Baadae ndio naenda chumbani kwake”
“Safi sana. Ila kuna kitu nataka ukifanye”
“Kitu gani?”
“Mkamue hasa ukifika nae kitandani. Yaani mkamue hadi aite mama” Richard alimwambia Gibson.
“Du!”
“Usishangae wala kushtuka. Kama ukimkamua haswa, hata akifika Ulaya atakukumbuka na atakuwa akitamani kukutana nawe kimapenzi zaidi. Ila ukipiga
rasharasha, hatorudi tena” Richard alimwambia Gibson ambaye akaonekana kuyakariri maneno yote.
Ilipofika saa tatu usiku, akashtuliwa simu na kwamba alikuwa akihitajika chumba namba ishirini na mbili. Kitendo cha kuitwa tu, tayari hamu ya kufanya
mapenzi ikamshika, akaanza kupiga hatua za haraka haraka kuelekea katika mlango wa kuingilia chumba kile, alipoufikia, akapiga hodi na kuingia ndani.
Katie alikuwa amejilaza kitandani huku akiwa na nguo ya ndani tu. Mapigo ya moyo ya Gibson yakaanza kudunda, alipokikodolea vizuri kifua, kilikuwa kile
ambacho alikuwa akikipenda sana na si kama cha Prisca ambacho kilikuwa kikiendelea kujaa tayari kwa kunyonyesha.
Akaanza kusogeza pale kitandani. Akapokelewa kwa mikono miwili na kuanza kuvuliwa nguo. Hiyo ndio ilikuwa siku ya kwanza kwa Gibson kumsaliti Prisca.
Kadri alivyokuwa akiucheza mchezo ule na ndivyo ambavyo kichwa chake kilivyozidi kumkumbuka Prisca.
Walichukua masaa matano, wakawa wamekwishamaliza, wakaenda bafuni kuoga na kisha Gibson kuondoka chumbani mule huku mfukoni mwake akiwa
amewekewa kiasi cha zaidi ya dola za Kimarekani elfu mbili mfukoni mwake bila kujijua.
Ilikuwa ni saa tisa usiku katika kipindi ambacho Gibson alikuwa akirudi nyumbani kwake kwa kutumia bajaji ambayo ilimpeleka salama. Alipofika nyumbani,
akagonga hodi, mfanyakazi wa ndani, Hilda akaja na kuufungua mlango.
Prisca bado hakuwa amelala, muda wote huo alikuwa macho akimsubiria mpenzi wake. Usingizi kwake wala haukupatikana kabisa, mawazo kibao yalikuwa
yamemsonga kichwani mwake. Moyo wake haukujisikia amani kabisa, alikuwa akimkumbuka mpenzi wake kupita kawaida.
Katika kipindi ambacho Gibson aliingia chumbani mule, akakaribishwa na kumbatio la nguvu na mabusu mengi mashavuni mwake. Kwa jinsi alivyoonekana
kuwa na furaha, Prisca akashindwa kuvumilia, akajikuta akitokwa na machozi.
“Nimerudi mpenzi. Usilie, niko salama” Gibson alimwambia Prisca huku moyo wake ukijihukumu kwa kile ambacho alikuwa amekifanya hotelini.
“Nakupenda mpenzi. Nilikuwa na wasiwasi mpenzi” Prisca alimwambia Gibson.
“Usijali. Niko salama. Nimekumisi pia” Gibson alimwambia Prisca huku nae akianza kumbusu.
“Mbona ulizima simu mpenzi?”
“Iliisha chaji. Niliiacha ofisini nikiichaji huku mimi nikiwa nimewapeleka wazungu mbugani. Ila wazungu wa leo walikuwa wanazingua sana. Yaani mpaka
wakatuchelewesha” Gibson alimwambia Prisca.
“Pole na kazi mpenzi. Vumilia, hayo ndio maisha”
“Usijali. Nitafanya kila liwezekanalo kwa ajili yako” Gibson alimwambia Prisca na kisha kumbusu.
Prisca akatoka nje ya chumba kile na kwenda kumuandalia mpenzi wake chakula. Muda wote ambao Gibson alikuwa akimwangalia Prisca, alikuwa akiendelea
kujuta moyoni mwake. Alijuta kufanya mapenzi na Katie, alikosa amani kwa sababu alikuwa amemsaliti mpenzi wake.
“Sifanyi nae tena. Sitokubali kumsaliti mpenzi wangu kwa mara ya pili” Gibson alijisemea huku akionekana kujuta.
Akavua suruali yake. Huku akitaka kuitundika katika mbao ya kutundikia nguo, akajikuta akigusa kitu kama karatasi mfukoni mwake jambo lililomfanya
kuuingiza mkono mfukoni mwake. Kiganja chake kikagusa karatasi kadhaa, alipozitoa zilikuwa dola.
Akazihesabu haraka haraka, zilikuwa ni dola elfu mbili ambazo zilikuwa zaidi ya milioni tatu. Uso wake ukaonyesha tabasamu, akaonekana kufurahi kupita
kawaida. Akatamani kuruka ruka kwa furaka, akajikuta akijilaza kitandani.
“Haya ndio maisha bwana. Kwa staili hii, wala siwezi kumuacha, kesho nampa dozi zaidi” Gibson alisema huku akitabasamu.

Je nini kitaendelea?
Je nini kitatokea Gibson atakapoendelea zaidi kutembea na Katie?
Je Prisca atajua?
Na je Katie atajua kama Gibson ana mchumba mjauzito?

ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment