Search This Blog

Sunday 19 June 2022

USINIBANIE - 1

 





     IMEANDIKWA NA : IGNAS MKINDI



    *********************************************************************************





    Simulizi : Usinibanie

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    NINAKUMBUKA kabisa siku ile ilivyokuwa, siiwezi kuisahau kwa jinsi nilivyouweka rehani utu wangu. Nakumbuka nilipokuwa chini ya dirisha nikinung’unika, nikimlalamikia mpenzi wangu Tausi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pamoja na ushupavu wangu wote wa kiaskari, nilijikuta

    nikilia kama mtoto mdogo. Sikupanga kulia bali niliuhisi

    moyo wangu ukivuja damu kwa majeraha yalioachwa na Tausi

    baada ya kuling’oa penzi lake kinguvu.



    Nilipokuwa pale chini ya dirisha, mawazoni nilipata twasira

    hasa ya Tausi, niliuhisi urembo wake akilini akiwa amejilaza

    chali kitandani katika mwanga hafifu japo kwa wakati huo

    sikuwa nachungulia.



    Naikumbuka kwa ukamilifu picha niliyokuwa nayo akilini,

    ngozi yake nyororo nyeupe, ilimfanya ang’ae katika mwanga

    hafifu, niliyaona matiti yake yakiwa yametulia kifuani pasi

    kufunikwa na chochote, niliviona vyote vilivyonifanya niwe

    punguani juu yake.



    Ilikuwa ni katika maeneo ya Kihesa, Iringa mji ulioko nyanda

    za juu, kusini mwa Tanzania. Giza nene lilikuwa limetanda na

    wakati huo ilikuwa yakaribia saa saba za usiku. Baridi

    lilikuwa ni kali mno kama ilivyo kawaida ya mji ule.



    Japo nilivaa koti kubwa na refu na sweta ndani yake lakini

    mavazi hayo hayakuweza kunifanya niache kujikunyata kwa

    baridi.



    Kwa kweli nilikuwa nafanya kitendo cha hatari sana, na laiti

    kama yeyote angebaini uwepo wangu pale angeweza kuniitia

    mwizi na nisipate la kujitetea, lakini sikuwahi kuiwazia

    hatari hiyo iliyokuwa ikinikabili.



    Kwa maneno niliyokuwa nikimwambia mrembo Tausi siku ile,

    hiki nikionacho leo hakinistaajabishi. Nakumbuka fika kuwa

    kabla ya kumtupia maneno yale matamu nilimuita Tausi kwa

    majina yake kamili, Tausi binti Nurdin.



    Ingawa hakuitikia, nina uhakiwa kuwa alisikia kwa kuwa

    nilichungulia dirishani mara tu nilipowasili mahali pale.

    Wakati nachungulia, nilimuona akiingia chumbani, nadhani

    alikuwa anatokea sebuleni.



    Nilitulia nikimwangalia kwa muda mrefu, nilikuwa

    nikishuhudia akitoa nguo zake moja baada ya nyingine.

    Alipomaliza zote nilijihisi kuishiwa nguvu, nikakaa chini.



    Niliamua kumrushia maneno nikiwa pale pale chini, nilijua

    fika kuwa aliutambua uwepo wangu mahali pale lakini kubwa

    alitambua hali yangu.



    Alijua ya kuwa niko taabani juu yake, sijiwezi.Nilimwambia, "Tausi binti Nurdin, kulikosa penzi lako nimebaki masikini,

    nimekuwa kama ndege mkiwa aliyenyeshewa mtini, umeniachia

    mwili lakini nafsi yangu yote unayo wewe. Nimeacha yote kwa

    ajili yako, na sitafanya lolote bila penzi lako, Tausi,

    nafsi zetu zimeumbwa kuishi pamoja, najua wajua ila

    unailazimisha miili yetu itengane, nihurumie mpenzi,

    niridhie nirudi penzini kwako."



    Pamoja na maneno yote hayo, Tausi aliendelea kuwa kimya na

    mimi nikajiapiza kuwa nisingeondoka pale hadi niisikie sauti

    yake. Niliendelea kunung’unika kila baada ya muda hadi

    ilipotimu saa tisa kasoro usiku.



    Jina langu ni Musa Njiwa, wakati huo nilikuwa nina miezi

    miwili toka niandike barua ya kuacha, kazi ya upelelezi

    ambayo ndiyo iliyokuwa ikinipa mahitaji yangu ya muhimu.

    Sikuwa nimejibiwa barua yangu hadi wakati huo.



    Pamoja na kutojibiwa lakini nafsini kwangu tayari nilikuwa

    nishaiondoa kazi hiyo na hata ningelazimishwa kuendelea

    nisingeweza japo hakuna aliyeamini kama ningeacha kazi hiyo

    niliyokuwa nikiipenda na kuifanya kwa ufanisi.



    Nilihojiwa sana na viongozi wangu kuhusu sababu ya kuchukua

    uamuzi huo mzito, lakini siri yangu ilikuwa iko moyoni.

    Sikuwahi kumwambia mtu yeyote japo kuna ambao waliihisi

    sababu ya kweli.



    Usiku ule nilitamani kumtazama Tausi usoni wakati

    nikimtamkia maneno yale, tena miili yetu ikiwa imegusana,

    lakini sikupata kibali machoni pake, alikuwa kajifungia

    chumbani kwake. Nilitamani kulihisi joto lake lakini

    nilibaki pale nikiumia kwa baridi.



    Nilimwomba anipe adhabu yeyote lakini asilitupe penzi letu,

    lakini maneno yote hayakusaidia kwa usiku ule. Tausi

    aliniacha pale nje nikiendelea kupata baridi kali

    lililoambatana na upepo.



    Saa tisa kasoro usiku, Tausi alisimama dirishani akaniita

    kwa sauti yake ya upole. Nikajiinua taratibu, tukawa

    tunatazamana japo tulikuwa tukitenganishwa na ukuta, nyuso

    zetu zilitazama kupitia dirishani.



    "Usifanye mambo yazidi kuwa magumu. Mimi na wewe basi" Japo hayakuwa maneno ya kutia moyo lakini nilifarijika kuisikia

    sauti yake.



    "Umenisikia nilichokueleza, fuata moyo wako utakavyokuambia"

    nilimwambia nikigeuka taratibu kuondoka kama mkware

    aliyefumaniwa na mkwewe.



    *********



    Miaka kadhaa iliyopita yalitokea mauaji ya kutatanisha ya

    mmojawapo wa watumishi wa Mzee Nurdin katika shamba lake la mifugo lililopo maeneo ya Chalinze, mkoani Pwani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzee Nurdin ni mfanyabiashara maarufu sana hapa nchini na ni

    mmojawapo wa watu wanaojitolea kwa hali na mali kukifadhili

    chama tawala, jambo linalomfanya awe karibu sana na viongozi

    wakubwa wa chama na serikali.



    Maiti ya mtumishi huyo aliyejulikana kwa jina la Kabuti

    ilikutwa ikiwa imeharibika vibaya kutokana na kukaa muda

    mrefu. Kabla ya maiti hiyo kugundulika, Kabuti alitoweka

    katika mazingira ya kutatanisha nyumbani kwa Mzee Nurdin.



    Hakukuwa na yeyote aliyehusishwa moja kwa moja na mauaji

    hayo ila ilisadikiwa kuwa Kabuti aliamua kujiua kwa

    kujinyonga. Lakini sababu za Kabuti kujinyonga hakuna

    aliyezifahamu.



    Kwenye msiba huo wa Kabuti, Mzee Nurdin aligharamia kila

    kitu na kuahidi kuendelea kuisaidia familia ya Kabuti hasa

    wazazi wake, kwa kuwa alikuwa hajaoa na hakuwa na mtoto.



    Watu wengi walimpongeza kwa moyo wake wa huruma lakini

    kutokana na fununu zilizoenea kuhusiana na kifo cha Kabuti

    kwamba Mzee Nurdin anahusika, nilipewa kazi ya kupeleleza

    mienendo ya Mzee Nurdin kwa namna yeyote.



    Kwa mujibu wa mkuu, kazi hiyo nilipewa mimi kwa kuwa ni muda mrefu sikuwa hapa nchini, kazi zangu nyingi nilizifanyia nje ya nchi kwa hiyo haikuwa rahisi kugundulika. Hakuna ofisa

    yeyote aliyejulishwa kuhusu kazi niliyopewa lakini wote

    waliambiwa kuwa naenda nje ya nchi kwa miezi sita ambayo

    ndiyo nilipangiwa kikamilisha kazi hiyo.



    Siku nne baada ya kupewa taarifa hiyo na Mkuu, nilipigiwa

    simu kuwa nikamuone dada mmoja niliyetambulishwa kwa jina

    moja la Marina ndani ya dakika arobaini na tano na

    niliambiwa kuwa nitamkuta kwenye jengo la Benjamini William

    Mkapa, ghorofa ya saba.



    Ilipofikia dakika ya arobaini na mbili, nilifika na kumkuta

    kasimama kama anayesubiri lifti. Tutakambuana kwa ishara

    ndipo a nikapewa maelezo yote ikiwemo utambulisho mpya

    nitakaoutumia katika kazi niliyopewa.



    "Utaitwa Hoza, kwenu ni Mashewa, Tanga. Maelezo mengine yako kwenye hii bahasha," aliniambia Marina akigeuka na kuingia kwenye lifti namba moya iliyokuwa inayopandisha juu.



    Nilibaki pale kwa sekunde kadhaa nikiangaza angaza huku na

    kule kisha nami nikaingia kwenye lifti namba tano iliyokuwa

    ikishuka chini.



    Baada ya maandalizi ya awali kukamilika nilifuatwa na mzee

    mmoja ambaye hakuwa na maneno mengi, akanipeleka kwa Mzee Nurdin.



    "Huyu ndio yule kijana uliyeniagiza, naomba umchukulie kama

    mwanangu kwa maana nimekabidhiwa na wazazi wake,"aliongea huyo mzee akimtazama usoni Mzee Nurdin.



    "Mara nyingi huwa sishughuliki na masuala ya wafanyakazi,

    ngoja nitamtuma dereva ampeleke nyumbani huko atapangiwa

    kazi za kufanya. Hata hivyo nashukuru," alisema Mzee Nurdin.





    SIKU ya kwanza wakanibwekea, walinzi wakaja fasta,

    nikawazuga kuwa nilikuwa nasafisha nje ya banda. Baada ya

    muda wale mbwa wakawa wamenizoea kiasi kwamba nilikuwa

    naweza kwenda wakati wowote hata nikaingiza mikono

    kuwachezea. Nikawa nimefaulu tena.



    Usiku wa kwanza ulikuwa wa kufanya ziara isiyo rasmi ya

    kukitafuta chumba cha Tausi kupitia madirishani,

    nikakigundua.



    Usiku uliofuatia, mapema tu baada ya giza kuingia nikawatoroka wenzangu kwa kujifanya naingia kulala, nikapitiliza hadi dirishani kwa Tausi. Ilipofika saa tatu, taa ya chumbani kwa Tausi ikawashwa.



    Tausi aliingia na kujifungia, akaanza kutoa kibanio alichofungia nywele zake ndefu, nywele zikafumuka na kummwagikia usoni. Akatikisa kichwa kuzirudisha nyuma. Akaanza kufungua vifungo vichache vya blauzi yake ya rangi

    ya bluu bahari.



    Baada ya maandalizi ya awali kukamilika nilifuatwa na mzee

    mmoja ambaye hakuwa na maneno mengi, akanipeleka kwa Mzee

    Nurdin.



    "Huyu ndio yule kijana uliyeniagiza, naomba umchukulie kama

    mwanangu kwa maana nimekabidhiwa na wazazi wake"aliongea

    huyo mzee akimtazama usoni Mzee Nurdin.



    "Mara nyingi huwa sishughuliki na masuala ya wafanyakazi,

    ngoja nitamtuma dereva ampeleke nyumbani huko atapangiwa

    kazi za kufanya. Hata hivyo nashukuru" alisema Mzee Nurdin.





    *****

    Nyumbani kwa Mzee Nurdin nilipangiwa kazi za utunzaji wa

    bustani na usafi wa mazingira ambayo niliifanya kwa ufanisi

    kiasi cha kuifanya jamii iliyo kwa Mzee Nurdin ianze

    kunipenda.



    Muda wote huo nilikuwa nikiishi katika mojawapo ya vibanda

    vitatu vya wafanyakazi vilivyo ndani ya eneo la jumba la

    kifahari la Mzee Nurdin.



    Kwa muda mfupi niliokaa pale niliwaona viongozi mbalimbali

    wakiingia na kutoka, pia niliwaona maafisa kadhaa wa polisi

    wakipishana kumtembelea Mzee Nurdin.



    Katika upelelezi wangu, cha kwanza kuhisi ni kuwa kuna njia

    nyingine ambayo Mzee Nurdin huitumia kutokea ndani ya eneo

    lake mbali na milango ya kawaida. Nikajaribu kulipata hilo

    toka kwa wafanyakazi wa ndani wa Mzee Nurdin lakini nikashindwa.



    Jitihada zangu zote za kuzoeana na watumishi wa ndani ya jumba la Mzee Nurdin zilishindikana kwa kuwa hawakuruhusiwa kuongea na mtu yeyote, hata wafanyakazi wenzao ambao wanafanya kazi za nje.



    Siku moja nikakata shauri kumvaa mmojawapo wa wafanyakazi wa ndani ya jumba hilo, alinijibu kifupi tu bila hata kusimama,



    "Ulizia kuhusu Kabuti". Mlio wa hatari ukaita kichawani. Ikanibidi nitulie kwanza nijipange upya. Niliona wazi kuwa kazi ni ngumu kuliko nilivyofikiria awali ila hali hiyo ilinipa uhakika kwamba kuna tatizo katika mwenendo wa Mzee

    Nurdin.





    ******

    Ilikuwa jioni moja, ukikaribia mwezi toka nianze kazi pale

    aliwasili binti mmoja mrembo sana. Baadae nilikuja kugundua

    kuwa anaitwa Tausi, binti kitindamimba wa Mzee Nurdin.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikuwa mrefu wa wastani, mweupe, mwenye mwili wa wastani,

    sio mwembamba sana wala mnene. Ila kikubwa alikuwa mpole na

    mkarimu tofauti na mabinti wanaotokea katika familia za

    kitajiri.



    Ni kama binti huyu alikuwa na sumaku, toka alipowasili mawazo yangu yakawa hayabanduki juu yake, lakini niliogopa kuchukua uamuzi wowote kwa kuogopa kuharibu kazi niipendayo. Ila tatizo kubwa ambalo hunikabili ni kuwa nikiwa na nimekolea kwa msichana, akili haiwezi kufanya chochote hadi nimnase.



    Katika vitu ambavyo vinaweza kunifanya niwe mtumwa ni

    mapenzi. Mi ni mgonjwa mno wa sekta hiyo. Kutokana na

    ugonjwa wangu huo nilijipa moyo kuwa miezi mitano iliyobakia

    ni mingi, ningeweza kumaliza kiu yangu ya kumpata Tausi

    ambaye sikuwa na uhakika na muda ambao angeendelea kuwepo

    pale.



    Nikajiwekea mkakati, kazi yangu ya kwanza ikiwa ni kumpata

    Tausi! Suala likawa nitampataje? Kwanza huwa hatoki mara kwa

    mara, pili uwezekano wa kumfanya anisikilize ulikuwa mdogo

    kwa hali niliyoivaa pale. Kichwa kikaanza kuniuma, akili

    yangu yote ilihama kutoka kwenye kazi iliyonileta pale.



    Nikaanza kuzisoma ratiba na tabia zake kama ambavyo makocha

    wa soka huzisoma timu pinzani. Ulinichukua takribani wiki

    mbili kumsoma Tausi na hatimaye nilihitimisha utafiti wangu.

    "Huyu anatakiwa kuchezewa kama soka la ki-Brazil maarufu

    kama Samba", nilifikia uamuzi.



    Soka la ki-Brazil halihitaji mapepe, unagonga pasi moja moja

    ukicheza taratibu kama vile hutaki kufunga. Na pindi

    mpinzani wako akizubaa unacheka na nyavu, na kuondoka na

    ushindi.



    Kwa kawaida napenda kulifananisha zoezi la kumtaka msichana

    kimapenzi na mifumo ya kucheza mpira wa miguu. Huwa kuna

    mitindo mitatu ambayo mara nyingi huwa napenda kuitumia,

    Kibrazili, Kihispania na Kiitalia. Kihispania ni mchezo wa

    kasi wa kushambulia kwa pasi fupi fupi, huu unawafaa masista

    duu kwa kuwa wanapenda mapenzi ya kujionyesha mbele za watu.



    Mtindo wa Kiitaliano huwa unatumika kutafunia kuku wa

    kienyeji, mademu wa uswahilini. Hawa ukijifanya kuremba tu

    umewakosa, ni fulu miguvu na kushambulia kibabe.



    Kikwazo kikawa namna ya kumuanza, ikabidi nianzishe mazoea

    na paka wa Mzee Nurdin. Tausi anampenda sana paka wa pale

    kwao kiasi kwamba mara nyingi alikuwa akimpa chakula

    mwenyewe. Nikaanza mchezo wa kudamka asubuhi sana na kwenda kuanzia usafi karibu na mlango mkubwa wa kuingilia kwa Mzee Nurdin.



    Karibu mara zote nilizokuwa nikifika pale nilikuwa nikimkuta

    yule paka akitoka au akikaribia kutoka. Nikawa naingia

    gharama za kumnunulia misosi yule paka. Akitoka tu nampa

    misosi, nacheza naye hadi akanizoea.



    Zoezi la kwanza likafanikiwa, nikaanza mpango wa pili.

    Asubuhi sana nikawa nampa chakula paka, lakini sikuwa

    nafanya usafi pale mbele ya lango kuu. Nikawa nafanya usafi

    muda mchache kabla ya saa tatu ambapo mara nyingi Tausi huwa

    anakuwa anazunguka zunguka maeneo yale akicheza na paka.



    Kutokana na mazoea na Paka yule, kila nilipofika alikuwa

    akinikimbilia, na mimi nilikuwa nikimbeba na kucheza nae

    hadi Tausi atoke. Mara zote Tausi akawa anasubiria nimruhusu

    paka aende kwake ndipo naye aanze kucheza nae. Lakini hakuwa

    akinisemesha chochote, na mimi sikuwa namuangalia hata mara

    moja. Nilikuwa nikimfanya kama hayupo.



    Mbinu hii huwa inanisaidia sana kupata wasichana warembo

    wanaoshindikana. Msichana anayeangaliwa sana na kufuatwa

    fuatwa na wanamme kutokana na urembo wake humshangaa sana

    mwanamme anayeonyesha kutomjali na hali hiyo humfanya

    amuangalie kwa jicho tofauti. Hapo inakuwa rahisi sana

    kumfanya akusikilize.



    Mara kadhaa Tausi akawa anataka kuniongelesha lakini sikuwa

    nampa nafasi. Akaanza kuwa anaulizia tabia zangu kwa

    wafanyakazi wenzangu, kitendo ambacho kilikuwa

    kikiwashangaza sana. Nikawa nimefaulu kumfanya autambue

    uwepo wangu.



    Lakini kwa upande mwingine nikawa nimejipalia makaa ya moto

    kwani kiongozi wetu wa wafanyakazi akaanza kunikasirikia

    akidhani nataka kuichukua nafasi yake. Nikamuona vipi sijui,

    mi nina mipango mingine ye’ ananiletea habari za kugombea

    madaraka!



    Basi jamaa likanibadilishia utaratibu, akamweka mtu mwingine

    kufanya usafi eneo la mbele karibu na mlango mkubwa wa

    kuingilia. Zikapita siku tatu bila kuonana na Tausi. Moyo ulikuwa ukiniuma sana, nikaamua kuwa namzuia paka asirudi

    maeneo ya mbele ya lango kuu ili Tausi ashawishike kuja

    nilipo lakini wapi! Haikusaidia.



    Kumbe Tausi naye akawa hana raha kwa kutoniona nikicheza na

    paka! Baadae tulipozoeana aliniambia eti alikuwa akivutiwa

    kuniangalia jinsi nilivyokuwa nikicheza na paka. Si dharau

    hizi jamani?



    Tausi ndiye aliyekuja kapata ufumbuzi wa tatizo letu la

    kutoonana, akawa anaingia chumba kimojawapo ambacho dirisha

    lake linatazama maeneo niliyopangiwa kufanyia usafi. Madai

    yake ananichungulia kumbe mi nilikuwa nimemuona muda mrefu

    tu. Nikawa najifanya naelekea lilipo dirisha, naye eti akawa

    anajificha nisimuone!



    Niliupenda sana mchezo huo tuliokuwa tukiucheza. Kwa tafsiri

    za haraka haraka nikaona kuwa mchezo wa Ki-Brazil, samba

    umeanza kuzaa matunda. Ikawa ndio maskani yangu, naye chumba kile kikawa ndiyo maskani yake.



    Kazi iliyokuwa ikinikabili ni namna ya kumvunjia ukimya,

    hapo nikamkumbuka mwalimu wangu wa saikolojia ambaye

    alinifundisha kuwa ukitaka kukipata kitu kwanza pata picha

    yake kichwani. Nikaanza kutafuta namna ya kuanza kumpigia

    chabo usiku ili nimjue vyema.



    Likaibuka tatizo jingine ambalo ni kubwa zaidi. Kilichokuwa

    kinanikwamisha ni kuwa usiku kunakuwa na mbwa wawili

    wanaachiwa. Mbwa hao wakibweka tu, walinzi wanafika mara

    moja kuangalia kinachojiri.



    Mbwa hao wamewazoea walinzi, na Mzee Nurdin tu! Yaani

    kikitokea chochote nje ya kufanywa na Mzee Nurdin wenyewe

    basi walinzi watakuwa wanahusika. Nikaanza kudili na banda

    la mbwa kwa kificho, baada ya kugundua namna wale walinzi

    wanavyowasiliana nao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Siku ya kwanza wakanibwekea, walinzi wakaja fasta,

    nikawazuga kuwa nilikuwa nasafisha nje ya banda. Baada ya

    muda wale mbwa wakawa wamenizoea kiasi kwamba nilikuwa

    naweza kwenda wakati wowote hata nikaingiza mikono

    kuwachezea. Nikawa nimefaulu tena.



    Usiku wa kwanza ulikuwa wa kufanya ziara isiyo rasmi ya

    kukitafuta chumba cha Tausi kupitia madirishani,

    nikakigundua.



    Usiku uliofuatia, mapema tu baada ya giza kuingia

    nikawatoroka wenzangu kwa kujifanya naingia kulala,

    nikapitiliza hadi dirishani kwa Tausi. Ilipofika saa tatu,

    taa ya chumbani kwa Tausi ikawashwa.



    Tausi aliingia na kujifungia, akaanza kutoa kibanio

    alichofungia nywele zake ndefu, nywele zikafumuka na

    kummwagikia usoni. Akatikisa kichwa kuzirudisha nyuma.

    Akaanza kufungua vifungo vichache vya blauzi yake ya rangi

    ya bluu bahari.



    Kadiri alivyokuwa akifungua kimoja baada ya kingine, mapigo

    yangu ya moyo yalizidi kasi. Alipokitoa kiblauzi kile

    nilijikuta miguu ikinitetemeka na mawasiliano kuanza

    kukatika kichwani kwa jinsi alivyojaaliwa matiti mazuri

    yenye chuchu zinazoelekea kwenye wekundu.



    "Ndio ugonjwa wangu huu!" Nilijikuta nikijisemea peke yangu

    kwa kunong’ona. Hakuwa amevaa sidiria binti huyu ambaye

    laiti angejua kuwa kuna mtu anamtazama sijui ingekuwaje.



    Taratibu akaanza kuangaza huku na kule akaichukua kanga na

    kujifunga kuyasitiri maziwa, nikajikuta nanung’unika kama

    shabiki wa ligi ya Uingereza aliyezimiwa televisheni

    katikati ya mechi kali ya Manchester United na Arsenal.



    Akajifungua zipu ya sketi na kuiacha idondoke kabla

    hajaiinua kwa mguu kama anayebetua mpira na kuirushia kwenye kasha la nguo chafu. Akamalizia kwa kuingiza vidole ndani ya khanga yake kuitoa nguo ya ndani, akainama kumalizia kuitoa miguuni.



    Sikukumbuka ni nini kilitokea lakini nilijikuta tu

    nimedondoka chini na miguu haiwezi tena kuhimili uzito wa

    mwili wangu. Mtoto kaumbika! Nilitulia pale pale chini kwa

    muda ili nikusanye nguvu kwanza.



    Akilini picha za Tausi zilikuwa zikinipitia kwa mtindo

    onyesho la mtelezo, ’slide show’. Baada ya mapigo ya moyo

    kuirudia kasi yake, nilijiinua taratibu na kuchungulia tena.



    Safari hii Tausi alikuwa ametoka kuoga, anajifuta na kataulo

    kake. Mashallah mtoto huyu, sijui nimfananisheje kwa jinsi

    alivyoumbika.



    Niliuhisi mwili wangu ukivutwa kutaka kuukumbatia wake,

    hakika sumaku ya mwili nayo ina nguvu. Niliendelea

    kumwangalia huku nikijiapiza kuwa ni lazima nimpate.



    Tausi akalivaa gauni lake la kulalia la rangi ya udhurungi,

    linaloonyesha kila kilichomo ndani. Akapanda kitandani na

    kujifunika shuka. Nikashusha pumzi ndefu.



    Nilirudi chumbani kwangu akili ikiwa haifanyi kazi katika

    mfumo wa kawaida, ilikuwa inavaibreti mithili ya simu ya

    ’Philips Savy’ nikiwaza na kuwazua mikakati ya kumnasa Tausi

    binti Nurdin.



    Kuna kitu kimoja ambacho nilikiona kutokana na macho yangu

    ya kipelelezi lakini kwa muda ule sikukitilia maanani. Ila

    baada ya kufikiria sana kitu hicho kikawa kinanirudia rudia.

    "Inaelekea ndio aina ya wanaume anaowapenda" nilijisemea

    nilipomaliza kuwaza.



    Katika chumba cha Tausi, ukutani kuna picha tatu za wanaume

    tofauti mastaa. Lakini wanachofanania ni kuwa wote wana

    miili iliyojengeka na wako vifua wazi.



    Nikakurupuka hadi kwenye kioo cha kakabati tulichoweka

    katika kila chumba huku nikivua shati. Nikaanza kujigeuza

    geuza nikiwa kifua wazi kama ninayeshiriki mashindano ya

    kutunisha misuli.



    "Bodi inalipa kimtindo", nilijisemea na kuzidi kujitia

    mzuka. Nikaweka miguu juu ya kitanda, mikono sakafuni

    nikaanza kupiga ’push up’ ili vimsuli vyangu vitunetune.

    Uzuri ni kwamba mwili wangu umejengeka kimazoezi kutokana na kazi yangu ya upelelezi.



    Asubuhi ilipofika nikapasha misuli moto nayo ikatutumka

    nikatafuta kashati kepesi fulani na jeans langu mpauko.

    Nilipojitazama kwenye kioo nilicheka. Nilikumbuka kipande

    cha shairi la wimbo wa msanii wa bongo fleva, Kali P,

    ’umevaa jeans lako la kupayuka, manguo yako na manywele

    yananuka halafu unadai huuzi nyago, huuzi nyago wewe?’



    Nikaenda moja kwa moja kwenye kituo changu cha kurushana

    roho na Tausi. Kama kawaida Tausi akawa katika sehemu yake

    ya uchungulifu. Nikajifanya simuoni nikawa naendelea kucheza

    cheza na paka wake kisha kabla ya kumuachia paka aondoke,

    nikafungua vifungo vya kale kashati kimtindo.



    Nikamtupia jicho Tausi wakati nikimruhusu paka aondoke,

    nikamwona ametulia kama amemwagiwa maji ya baridi. Nikajua nishamroga.



    Kwa kawaida nikimwachia tu paka aondoke na Tausi hutoka pale dirishani kwenda kumchukua paka wake, lakini siku ile

    alibaki pale pale dirishani kwa muda mrefu, ’mtoto kazimia

    bodi’. Basi babaako nikazidisha manjonjo ili niroge zaidi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tausi alibaki pale kwa muda mrefu sana, nikataka kulivua

    shati kabisa lakini nikasita kwa kuwa ngozi ya mwili wangu

    haionyeshi kama nastahili kuwa mfagizi.



    Baada ya siku hiyo ya ulozi, nikaendelea kuvaa nguo zangu

    kubwa kubwa kama kawaida na nikabadilisha ratiba kabisa.

    Nikamtia hamu Tausi, hamu ya kuniona.



    Mpango wangu ulikuwa ni kufanya shambulizi la kushtukiza,

    nikawa namtafutia nafasi. Kipindi chote ambacho alikuwa

    hanioni nilikuwa nikipokea umbeya kuwa ananiulizia mara kwa

    mara. Ila mimi nilikuwa namuona, unajua nilikuwa namuonaje?

    Nilikuwa sikosi dirishani kumpiga chabo!



    Siku ile ya kwanza niliyomfanyia manjonjo nilimuinjoi sana

    alivyokuwa akiwaza huku anaangalia na kuzigusa gusa picha za

    wale wanaume ukutani. Nikajua kisu kimegonga mfupa. Siku

    moja Mzee Nurdin alisafiri nje ya nchi kwa uwazi.



    Kama unakumbuka nilikwambia kuwa nilikuwa nimehisi kuwa ana mlango mwingine wa kutokea eneo lile hivyo siyo rahisi

    kuzijua safari zake. Kitu pekee kilichokuwa kikinijulisha

    kuwa yupo au hayupo ni uimara wa ulinzi katika eneo lile.



    Kuna wakati ulinzi unapwaya na wakati mwingine unakuwa wa

    hali ya juu.



    Basi akasafiri nje ya nchi na wapambe wake kadhaa katika

    safari zake za kibiashara. Pale nyumbani kukawa shwari, watu

    wakawa wamejiachia kwa kuwa wote walijua kuwa mzee hayupo.



    Siku iliyofuata tu, nikajifanya naumwa sana, na pale mkuu

    aliyebaki kama kiongozi alikuwa Tausi. Mke wa Mzee Nurdin ambaye ni mama yake Tausi alikuwa akitegemea sana kuongozwa na Tausi kwa kuwa elimu ya mama

    huyo haikuwa ya kutosha. Tausi akawaagiza wasaidizi wake

    wanipeleke nyumba kubwa.



    Mwanamume nikachukuliwa hadi mbele ya uso wa Tausi, malaika wangu. Nikafikishwa nikiwa nimeshikwa huku na huku

    nikijitetemesha kwa baridi na kwa kuwa nilishatafuna

    pilipili, mwili nao ulishakolea joto.



    Kama kuna kitu ambacho ndio mara ya kwanza kukiona kwa

    ufasaha katika mwili wa Tausi ni macho. Tausi ana macho

    mazuri balaa! Akaweka kiganja chake mwilini mwangu, sehemu

    ya shingo.



    Kwa kweli nilisisimka mwili mzima, Tausi akashtuka.

    Nikadhani amenishtukia kama nimesisikwa na mwili. Kumbe

    alishtuka kwa jinsi mwili wangu ulivyokuwa na joto kali.



    Haraka haraka akaagiza nipelekwe hospitali naye akiwa

    kiongozi wa msafara. Mungu anipe nini! Tukafika hospitali na

    kupokewa ki-VIP.



    Vipimo vilifanyika kwa umakini mkubwa. Wakati nasubiri

    majibu nikawa nimelazwa kitandani, Tausi amesimama pembeni

    yangu. Nikamuona jinsi anavyonionea huruma, nikaichukua

    fursa hiyo fasta.



    Nikamuonyesha ishara kuwa kuna kitu ninataka kumwambia,

    akaniinamia akilisogeza sikio lake karibu na mdomo wangu.

    "Naomba nishike mkono" nilimnong’oneza Tausi.



    Aliniangalia kwa huruma huku akiniloga na kwa macho yake mazuri, tukagongana macho akaangalia chini. Akanipa mkono,

    nikaushika nikaung’ang’ania na kuusogeza kifuani pangu.



    Akaketi pembeni yangu kitandani.



    Vipimo vilifanyika kwa umakini mkubwa. Wakati nasubiri

    majibu nikawa nimelazwa kitandani, Tausi amesimama pembeni

    yangu. Nikamuona jinsi anavyonionea huruma, nikaichukua

    fursa hiyo fasta.



    Nikamuonyesha ishara kuwa kuna kitu ninataka kumwambia,

    akaniinamia akilisogeza sikio lake karibu na mdomo wangu.

    Nikamnong’oneza.



    "Naomba nishike mkono" nilimnong’oneza Tausi. Aliniangalia

    kwa huruma huku akiniloga na kwa macho yake mazuri,

    tukagongana macho akaangalia chini. Akanipa mkono,

    nikaushika nikaung’ang’ania na kuusogeza kifuani pangu.

    Akaketi pembeni yangu kitandani.



    Mpambe mmoja aliyeng’ang’ania kubaki ndani akaona aibu

    mwenyewe, akatoka na kutuacha wawili. Tausi alikuwa katulia

    sana, nilihisi kuwa naye anajisikia raha mkono wake kuwa

    kifuani pangu. Madaktari nao kwa kutafuta sifa, wakaleta

    majibu haraka haraka! Yaani dah, wala sikuwa nimefaidi sana.



    Nahisi hata Tausi mwenyewe walim’boa kwa kuwahisha majibu ya

    vipimo. Kimsingi, hawakuona ugonjwa wowote, wakanipa dawa za

    kushusha homa. Ila wakataka nibaki kwa muda kwa uangalizi wa

    karibu, nadhani walikuwa katika mkakati wa kibiashara kwa

    kuwa kama ningelazwa kitanda kingelipiwa.



    Sikuuachia mkono wa Tausi naye akawa anasita kuniambia kuwa

    anataka kuondoka. Sijui kama aliogopa kumkatili mgonjwa au

    naye alisikia raha! Tausi akageuka kunitazama nikafumba

    macho kujifanya nimelala usingizi.



    Sijui kama aliendelea kuniangalia ama lah! Ila niliuhisi

    mkono wake ukitetemeka. Ghafla nikamsikia akiniita kwa mbali

    sana, inaelekea sauti yake iligoma kutoka. Akarudia tena,



    "Hoza.." Nikanyamaza kimya, akarudia mara tatu.



    Alipojiridhisha kuwa nimelala, akaanza kuutoa mkono wake

    taratibu nami nikalegeza wangu. Akafanikiwa kuutoa. Lakini

    cha ajabu hakuondoka. Nilimhisi bado kakaa pembeni yangu,

    nikawa nasubiri kujua anataka kufanya nini.



    Nikasubiri kama dakika tatu hivi, nikamsikia akishusha pumzi

    ndefu. Nilitamani kufungua macho nishuhudie kuwa yuko katika

    hali gani. Ghafla nikahisi giza likiukaribia uso wangu,

    kisha nikalihisi joto likinikaribia na hatimaye mdomo wa

    Tausi ukawa juu ya paji langu la uso. Alinibusu!



    Mwili wangu wote uliishiwa nguvu, niliuhisi umekufa ganzi.

    Laiti kama angeni-ofa penzi ghafla kwa muda ule sidhani kama

    ningeweza kufanya chochote. Nilichanganyikiwa!



    Baada ya muda mchache nikamsikia Tausi akitoa maagizo kwa

    dereva, kuwa amrudishe nyumbani kisha arudi kunifuata.

    Ukimya ulipotawala nikafumbua macho.



    Daktari mmoja mtu mzima hivi, anayeonekana kukaribia ama

    kuzidi kidogo miaka hamsini akaingia kuangalia naendeleaje.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Vipi Hoza?"



    "Niko safi dokta" nilimjibu. Ikabidi nimweleze dokta kuwa mi

    siumwi ila nilijifanya naumwa ili nipumzike kazi,

    nikamdanganya kuwa sijapata ofu siku nyingi. Badala ya

    kukasirika ikabidi daktari acheke sana.



    "We kijana ni mtundu sana. Haya nitakuandikia upumzike kwa

    siku tatu!"



    "Ahsante sana dokta."



    Baada ya kurudishwa, nilikaa bila kutoka mchana kwa siku

    zote tatu, ila usiku ilikuwa kama kawa, kunako chabo. Katika

    siku hizi tatu Tausi alikuwa akionekena mwenye mawazo mengi

    sana. Nilitamani kujua alichokuwa anakiwaza japo nilihisi

    kuwa ameanza kuzama penzini lakini akili yake haitaki

    kukubali.



    Unazijua dalili za mtu aliyezama penzini halafu akili yake

    haitaki kukubali? Nikianza kukuelezea tutapoteza muda,

    hadithi bado ndefu sana.



    Nilipomaliza siku tatu za mapumziko niliwahi asubuhi sana

    nikafanya usafi sehemu zote kisha nikakaa pale kwenye kijiwe

    changu.



    Baada ya muda kidogo nikamuona Tausi akichungulia. Nikatoa

    kalamu yangu kwenye nfuko wa suruari na karatasi la barua,

    nikaanza kuandika. Nikaandika kwa muda mrefu kiasi huku

    nikiwa na vipindi vya kufikiria mara kwa mara.



    Sio kwamba nilikuwa nafikiria cha kuandika bali nilikuwa

    namvuta Tausi ili apate shauku ya kujua ninachoandika, hizo

    ni baadhi ya mbinu za kimchezo.



    Nilipomaliza kuandika nikajifanya naisoma kwa umakini mkubwa

    kisha nikajifanya nawaza halafu ghafla nikaikunja kunja na

    kuitupia pembeni yangu nikainuka na kuondoka eneo lile.

    Nikaenda kujificha ndani ya kibanda ninachoishi nikiangalia

    pale nilipoliacha karatasi lile.



    Ghafla nikamuona Tausi akizuga zuga eneo lile kisha

    akaliokota lile karatasi na kuondoka nalo. Ilikuwa bado

    kidogo nishangilie kwa nguvu.



    "Hesabu zimekubali" Nikajisemea kabla sijakurupushwa na bosi

    wangu nitoke nje.



    Mijamaa mingine bwana ikipewaga vyeo sijui inakuwaje, eti mi

    nimemaliza kazi zote ye linataka nizagae zagae tu nje bila

    mpango wowote. Hili jamaa linanikumbusha afande wangu mmoja

    wakati natoka depo, Moshi. Ile kuripoti tu jamaa

    likanichukia ghafla likaanza kuniletea nongwa.



    Kwanza sikujua ni sababu gani, ila baadae nikaja kujua kuwa

    tatizo nimemzidi elimu kwa mbali sana hivyo akahisi

    nitapanda vyeo fasta na kumzidi. Utafikiri mi ndio baba yake

    niliyeshindwa kumlipia ada ya shule.



    Siku hiyo nilikuwa na furaha sana lakini hakuna aliyejua

    kuwa nafurahia nini. Nilitamani usiku ufike nikampige chabo

    Tausi. Sijui kama atavumilia kuniuliza.



    Kwa kile nilichoandika kwenye karatasi ulikuwa ni mtihani mzuri sana kujua maendeleo ya harakati zangu, ningejua kama kazama

    kwenye penzi au kama nimemtafsiri vibaya pia ningejua.



    Niliojiona nimedharaulika sana mwanamume mimi, lakini Tausi

    hakuonyesha kujali kabisa. "Unaweza kuniambia

    uliyemuandikia?" aliniuliza akiniangalia usoni.

    Mapigo ya moyo yalibadilika ghafla.



    Niliandika mistari mfano wa hadithi. Tausi alikuwa

    kajifungia ndani lakini nilikuwa kama namuona akiisoma

    karatasi ile, mistari yangu ikisomeka...



    ’Sikutegemea maishani ingekuja nitokea, Picha hii mawazoni

    haitakuja nipotea, Ndege mrembo pembeni yangu katulia,

    Nahisi joto la mwili wake huyu malkia, Kiganja chake

    kiganjani mwangu, Vimeweka makazi kifuani pangu, Macho yake

    yamelegea kama aliyekula kungu, Kitandani ametulia najikuta

    naishiwa nguvu, Sijui kama itakuja jirudia, Ninayojihisi

    natamani kumwambia, Lakini naogopa hatanisikia, Ila kwa busu

    la uso alonipa nimeridhia.’



    Niliandika bila kuyafikiria kabla maneno yale lakini kwa

    hakika yamewakilisha kilichomo katika mawazo yangu.



    Ulipofika usiku, nilinyata hadi kwenye chaka langu la

    kupigia chabo. Nikajiweka sawa kabla ya kujiinua ili nianze

    kupiga chabo. Kuinua uso nikakikuta chumba cheupe, hamna

    mtu.



    Nikasubiri kwa muda mrefu lakini Tausi hajatokea.

    Nikashtushwa ghafla na mlio wa mbwa waliokuwa wakibweka.

    Nikarudi mbio kwenye kibanda changu. Sikujua ni nini

    kilikuwa kinaendelea, ghafla nikasikia walinzi wakizunguka

    huku na kule.



    Nikatulia kimya kitandani japo hata viatu nilikuwa

    sijavivua, nafsi yangu haikuridhika kulala bila kupiga chabo

    huku nikijisema kuwa n’shazoea tabia mbaya. Hali ilipotulia

    nilikwenda tena dirishani kwa Tausi.



    Safari hii nikamkuta Tausi ameketi kitandani akiwa mwingi wa

    mawazo, sikujua nini kinamtatiza. Mara akainuka, akawa

    anajongea dirishani upande niliokuwepo.



    "Dah kaniona nini?" Nikajiuliza huku nikichuchumaa chini

    kujificha. Tausi akawa kasimama pale dirishani anaangalia

    nje. Nikahisi kuwa ni yeye aliyekuwa anabwekewa na mbwa.

    Kama ni kweli alikuwa, anataka kwenda wapi?



    Wivu ukaanza kunijaa moyoni, nikahisi nataka kuzidiwa kete.



    "Itanibidi nifanye fasta, chelewa chelewa utakuta mwana si

    wako. Sasa nitafanyaje mie? Huyu mtoto atanitia uchizi

    mimi!" nilijisemea.



    Alisimama pale dirishani kwa muda mrefu kisha akaondoka.

    Nilijiinua taratibu nikaanza kunyata kurudi kibandani

    kwangu. Usiku ule nilipata shida sana kupata usingizi,

    nilikuwa nikimuwaza Tausi na mbinu za kumpata. Nimeyaanzia

    nini mimi haya maswahibu?



    Nilipopitiwa na usingizi wala sikujua ilikuwa ni saa ngapi

    ila nakumbuka nilijikuta nimesimamiwa na kiongozi wangu

    akiwa kanishikia kiuno. Ilikuwa ni saa mbili asubuhi,

    nilipofungua macho nikatulia kwanza kwa muda. Jamaa likawa

    linaniangalia tu utadhani linanidai.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikamyeyusha kuwa sikuwahi kuamka kutokana na kujisikia

    vibaya, akaniambia nifanye fasta kutoka nikafanye usafi.

    Wakati najiandaa ukaja ujumbe kuwa naitwa katika nyumba

    kubwa. Nikajua kuwa tayari kishawaka, nikaanza kupanga

    maneno ya kujitetea.



    Nilipofika sebule ya nyumba kubwa nikajikuta niko uso kwa

    uso na Tausi anayeonekana amekasirika kweli kweli, kakunja

    uso. Nikaanza kujihami kuwa nilikuwa najisikia vibaya ndiyo

    maana nimechelewa kufanya usafi. Bila kutarajia Tausi

    akatabasamu.



    "Sikukuitia hilo" alisema. Kidogo akaja

    mtumishi mmoja wa mule ndani, Tausi akamgeukia.



    "Na ukirudia tena sitakusamehe" Tausi akamwambia binti yule,

    mtumishi wa ndani. Nikashusha pumzi nikajua kuwa lile soo

    sio langu,



    "sasa anataka nini we mtoto?" nikamuuliza kimoyo

    moyo. Tausi akanigeukia wakati yule mtumishi akiondoka,

    akaniangalia kwa muda akinikazia macho.



    Nikaona kuwa hapa nikikwepesha macho tu atanitawala, na mimi

    nikamkazia. "Nataka nikupe kazi, na nitakulipa vizuri

    ukinifanyia kazi hiyo" alianza kunieleza kwa kujiamini kabla

    ya kuendelea.



    "Nimeona maneno yako kwenye karatasi"

    aliniambia akiniangalia machoni.



    Nikajifanya kushtuka kisha nikajikakamua kumtazama lakini

    mwili wote ulikuwa ukinitetemeka. Sikujua nimjibu nini.



    "Nataka uniandikie maneno kama yale, kuna mtu nataka kumpa"

    alisema kwa upole akijiamini.



    Hasira zilinipanda kichwani nikajiona nadhalilika mwanamume

    mimi, niliona wazi kuwa nakosewa adabu. "Nimchape vibao

    nini?" Nilijikuta nikiwaza kwa haraka haraka.



    Bahati nzuri akaingia mmojawapo wa watumishi wa mule ndani,

    cha kushangaza Tausi hakuufurahia ujio ule. Akamdakia,



    "sihitaji usumbufu, nina shauri muhimu na Hoza. Waambie na

    wenzio!" Yule mtumishi akatoka haraka haraka na kuishia zake

    nje.



    Nikashusha pumzi ndefu kisha nikatulia kwa muda ili kuipa

    nafasi hekima ichukue mkondo wake. Akili ilipotulia

    nikamjibu. "Mimi sio mtunzi wa mashairi, huwa naandika

    kilichopo moyoni wangu. Samahani kama nimekukwaza" nilimjibu

    kwa upole lakini kwa chuki kubwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog