Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

JERAHA LA HISIA - 2

 





    Simulizi : Jeraha La Hisia

    Sehemu Ya Pili (2)



    Naomi alikuwa amechanganyikiwa, angeanza vipi kumweleza Walter kuwa anahusika katika kifo kile? Hakuwa tayari kumpoteza Walter ama kumliza tena.

    Hakuwa na maamuzi na siku zilizidi kwenda, damu ya Maureen ikazidi kukitekenya kichwa chake. Ilikuwa ni aidha akiri kuwa anahusika ampoteze Walter ama aendelee kuishi na siri hiyo iliyovuruga kichwa chake.



    Ni hapo mshikemshike ulipoanzia na Walter kujikuta katika utumwa wa aina yake.

    Alijaribu kufanya kila jambo ili Naomi akae sawa, haikuwezekana.



    Siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa Naomi alitegemea kumfanyia jambo la kipekee sana. Lakini ajabu na kweli Naomi akamtia aibu, hakutokea ukumbini. Aibu kubwa sana.

    Walter akaaminika kuwa alikuwa amelishwa vitu ambavyo vimeiteka akili yake.

    Ukweli aliujua yeye tu kuwa alikuwa anampenda sana Naomi na hakuhitaji kuona anapotea tena kama awali.

    Naomi alikuwa amechanganyikiwa, angeanza vipi kumweleza Walter kuwa anahusika katika kifo kile? Hakuwa tayari kumpoteza Walter ama kumliza tena.

    Hakuwa na maamuzi na siku zilizidi kwenda, damu ya Maureen ikazidi kukitekenya kichwa chake. Ilikuwa ni aidha akiri kuwa anahusika ampoteze Walter ama aendelee kuishi na siri hiyo iliyovuruga kichwa chake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maisha ya Walter yakabadilika na afya yake ikaporomoka.

    Si kwa kuwa hakupata lishe bora lakini la!!

    Ni mabadiliko ya Naomi mkewe. Walter hakuwa na mtu wa kumshirikisha, hakuwaamini marafiki wanaomzunguka kwani mara kwa mara waliwahi kumshauri afanye mpango wa kuachana na Naomi.

    Walter aliwasikiliza na almanusura aingie mkenge lakini akiwa katika hatua za mwisho za kutimiza hayo akauvaa moyo wa Naomi na kujiuliza atajisikiaje punde atakapoipokea taarifa ya kuachwa.

    Walter akakumbuka kuwa Naomi aliwahi kukataa katakata kuoana naye, lakini Walter akawa king’ang’anizi hatimaye ndoa ikafungwa kimya kimya.

    Naomi akawa kila kitu kwa Walter.

    Sasa amekuwa mzigo wa miiba.

    Walter hana wa kumlaumu.

    Jambo jingine ambalo lilimfanya Walter asifikirie kabisa kuachana na Naomi, lilikuwa suala la mtoto, hadi wakati huo Naomi hakuwa amebeba mimba.

    Walter aliamini kuwa tatizo lipo kwa Naomi, lakini aliogopa kumweleza moja kwa moja kwa kuhofia kumwathiri kisaikolojia. Sasa maamuli ya kuachana naye yangeweza kumweka Naomi katgika hali ya kuhisi alikuwa ameachwa kwa sababu hazai.

    Walter akauvaa uanaume halisi akasimamia msimamo.

    “Nitaishi naye kwa shida na raha.”

    Maisha yakaendelea.

    Naomi akitulia siku tano, basi siku ya sita lazima asumbue na kisa kipya ama la akirudia basi ni mikasa yake ya maudhi.

    Kunywa pombe na kulewa kisha kwenda kuwafanyia vurugu majirani na marafiki zake wa zamani.

    Walter hakumbuki ni mara ngapi alimwekea dhamana Naomi baada ya kufikishwa mahabusu lakini anakumbuka kuwa ni mara mbili aliwalipa mawakili waweze kumtetea mahakamani baada ya kukamatwa na makosa ya kuendesha gari akiwa amelewa.

    Huyu nd’o alikuwa mkewe wa ndoa ya kiserikali.



    Tofauti na mtu yeyote ambaye angeweza kudhani kuwa Naomi anayafurahia yale ambayo anayafanya, haikuwa hivyo. Akiwa faragha Naomi alikuwa analia sana na kuomboleza kwa mambo mabaya anayomfanyia Walter na jamii kwa ujumla.

    Walter alibahatika kukumbana na maajabu haya siku moja baada ya kuwa amemtoa mahabusu alikopelekwa kwa kosa la kumtukana matusi ya nguoni kiongozi wa kiroho aliyekuwa anahubiri barabarani kisha alipopita Naomi akiwa na kinguo kifupi akamsema kama mfano.

    Japokuwa alikuwa anamjibu mwanzoni alipoanza kutukana kuwa ‘shetani yu kichwani mwake’ matusi yakamzidia. Naomi hakupata shahada ya kawaida ya chuo kikuu lakini katika matusi hapakuwa na la kumshinda.

    Kozi ya kiingereza aliyosoma akiwa katika ndoa ilimwezesha kupanua msamiati wake sasa aliweza kutukana na kiingereza.

    Nani kama Naomi, mtumishi akazidiwa akamshtaki Naomi. Naomi akakamatwa.

    Walter akapewa taarifa.

    Siku hii Walter alijifanya kichwa ngumu, akajaribu kutikisa kiberiti ili aone je Naomi ni wa thamani kwake ama la.

    Akazuga kuwa hajali lolote.

    Ni siku hii ambapo aliamini kuwa hawezi kuishi bila mlevi huyu.

    Akiwa katika ofisi yake ya burudani, alishangaa haelewi chochote anachofanya.

    Kila alichogusa alikuwa anakosea.

    Akili iliganda na kumuaminisha kuwa hawezi kufanya kazi iwapo moyo anaoupenda u mahabusu.

    Walter akachukua pesa za kutosha. Akaiendea gari yake, alipoiwasha akagundua kuwa hawezi kuwa makini barabarani.

    Akakodi taksi.

    Moja kwa moja katika kituo cha polisi.

    Pesa ikakohoa, Naomi akatolewa.

    Kwa kutumia teksi ileile Walter akizuga kuwa amekasirika alimpakia Naomi kisha akamlipa dereva ampeleke nyumbani.

    Hakuandamana naye.



    Akaiacha teksi iondoke ili aweze kurejea kazini.

    Aliweza kurejea, lakini je? Kazi angeweza kuzifanya bila kumsikia Naomi.

    Hapana ikawa ngumu.

    Walter akafurahi kwa kuwa alikuwa amejiajiri, bila hivyo huenda angekuwa amefukuzwa kazi kwa sababu ya Naomi.

    Akafunga ofisi na kuondoka zake.

    Akafika nyumbani.

    Kimya kimya akaenda hadi katika mlango wa chumbani kwa kunyata.

    Kilio kilisikika, na kuna maneno yalikuwa yakitamkwa na Naomi.

    Naomi alikuwa anamlilia Mungu, alimlilia kwa maisha anayoyaishi, alikuwa anajuta kwa anayomfanyia Walter. Aliapa kuwa anampenda Walter kuliko wanaume wote duniani, lakini anajuta kumpenda.

    “Kwanini Mungu haunipi japo chembe ya furaha? Hukunipa nafasi ya kuelimika darasani, umeninyima na nafasi ya kufurahia maisha, basi ungeniacha nife tu, ungeniacha kabisa nisikutane na Walter, kwa nini umempa mzigo huu mtakatifu huyu?? Kwa nini umempa zawadi hii mbaya. Zawadi isiyobebeka. Nitafanyaje sasa mimi, ni wewe ujuaye uchungu ninaoubeba, unajua naumia kiasi gani, unajua kuwa sipendi nilivyo. Mimi si msafi mbele yako lakini iweke huruma yako kwangu walau niupate ufumbuzi wa tatizo hili. Siwezi kuishi nikiwa hivi!!” alilia sana Naomi, Walter akiwa msikilizaji.

    Kati ya siku ambazo upendo ulijifunga moja kwa moja na kuwa katika damu ya Walter ni siku hii. Hakuwahi kuamini kama Naomi alikuwa anampenda kwa dhati. Alidhani anajilazimisha, sasa leo hii anamsikia akisema na Mungu wake.

    Akamtaja na yeye kuwa ni mwanaume wa kipekee.

    Walter akawalaani marafiki waliowahi kumshauri kuwa Naomi hamfai na wala hampendi.

    Walter akarejea sebuleni na kuugonga mlango kana kwamba ndio alikuwa amefika.

    Naomi akachelewa kama dakika tano kisha akafika kuufungua mlango ambao ulikuwa umeegeshwa tu.

    Tayari alikuwa amenawa uso wake. Ilikuwa ngumu kutambua kuwa alikuwa ametoka kumwaga machozi.

    Walter akamkumbatia na kumbusu shavuni.

    Baada ya kuvua nguo za ofisini, aliingia jikoni, akaandaa pishi la mchemsho wa samaki, ambalo lilipendelewa sana na Naomi.

    Kisha akampelekea huko huko chumbani.

    Naomi akatabasamu huku akikwepesha kumtazama Walter machoni, kwani kwa kufanya hivyo lazima angepitiwa na kumwaga machozi jambo ambalo Naomi hakutaka litokee.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ****

    Usiku ulikuwa tulivu sana. Walter alikuwa akicheza karata na Naomi, walikuwa na furaha sana siku hiyo. Baada ya kushindia ufukweni sasa walikuwa nyumbani hakuna aliyekuwa na usingizi.

    Majira ya saa tatu usiku mlango ukagongwa ishara ya mtu mlangoni.

    Haikuwa kawaida kabisa kwa mji huu kupata wageni usiku.

    “Anayemfunga mwenzake nd’o anaenda kufungua mlango..” Walter alimtania Naomi baada ya kuona kuna kila dalili ya kufungwa katika awamu ile.

    “We chizi kweli, kwa hiyo anayegonga aendelee kusubiri..kwa taarifa yako sikufungi.” Naomi naye akajibu kiutani.

    Walter akasimama na kuliendea geti.

    Akauliza nani mgongaji, akajibiwa na sauti nzito ya kibabe.

    “Baba Farida.”

    Walter akafunua kitundu kidogo na kumchungulia.

    Hakika alikuwa yeye baba Farida. Upesi akalifungua geti lote.

    Akamrukia kwa furaha kubwa huku akipiga mayowe.

    Naomi akasikia akatoka mbiombio na kukuta wanaume wawili wakiwa wanashangaana.

    “Baba Farida aaaah…..vibaya ulivyonifanyia yaani eeeh dah si jambo zuri hata kidogo. Utaniua kwa presha mwenzako.” Alilalamika Walter. Yule mwanaume akawa hana jipya zaidi ya kucheka.

    Ndevu zake nyingi kidevuni zilianza kuwa nyeupe, uzee ulikuwa unajongea.

    Alizivuta vuta ndevu zake kwa mkono mmoja huku mwingine ukiambaa katika kitambi chake.

    “Ama kwa hakika duniani hakuna wembamba.” Walter alikiri.

    Akalichukua begi na kuliingiza ndani ya nyumba, nyuma yake akafuatia Naomi na baba Farida.

    “Hamis….umetisha, kwanza shkamoo.”

    “Marhabaa….” Aliitikia.

    Sasa walikuwa sebuleni.

    “Mamaa…huyu ni mlezi wangu, anaitwa Hamis..muite baba Farida anapenda zaidi……Mzee huyu nd’o mkweo..mama Walter.” Alitambulisha Walter wote wakashukuru kufahamiana.

    Yule mzee wa kiislamu akawatakia heri.



    Maongezi yaliendelea lakini Hamis alikuwa na mashaka, kuna jambo lilimtatiza na aliungoja upenyo aweze kulilipua na kubaki huru.

    Aliyekuwa mbele yake alikuwa kama aliwahi kujitokeza katika maisha yake na kisha kutoweka kama upepo ambao bado unahitajika sana.

    Lakini huyu alikuwa amenawiri sana.

    “Au ni dada yake?” alijiuliza. Hakupata jibu.

    “Walter hajui lolote inamaana?” swali jingine akajiuliza.



    Majira ya saa sita usiku, Naomi aliaga kuwa anakwenda kulala.

    Mzee huyu ambaye aliwahi kuishi Tanzania, kisha akatoweka na kwenda kufanya biashara za mafuta uarabuni kisha kupata mwenza na kuzaa naye hukohuko. Hatimaye akatakiwa kumuoa, akalazimika kubadili jina na dini na hatimaye akajiita Hamis, wakamwita mtoto wao wa kike Faridah.

    Akafumba macho yake na kujenga hoja upya kabla hajaifikisha kwa Walter. Akajirejesha miaka kadhaa nyuma ambapo hakuwa na ndevu nyingi na hakuwa akivaa kibalaghashia, akazikumbuka enzi za kwenda kanisa jumapili pekee, akazisahau enzi hizi za swala tano na kufunga ramadhani, Hamis akauvua usasa akauvaa uzamani ili aweze kupata jibu sahihi.

    Hamis akarejea kuwa Frank. Baba yake mdogo na pia baba mlezi wa Walter ambaye aliwazika wazazi na bibi wa Walter kisha akamzika na Maureen dada yake Walter huku akijilaumu kwa kumwamini msichana wa kazi na kumwachia nyumba.

    Machungu hayo yalimfanya aikimbie Tanzania kwa gia ya kutafuta maisha zaidi.

    Hatimaye amerejea kumsalimia na kumwona mke wa mwanae.

    Amerejea akiwa ‘mufti’ haswaa.

    Lakini anakutana na sura tatanishi ya mke wa Walter.

    Sasa anajiuliza je yule ni Naomi muuaji ama ni dada yake Naomi, ama nd’o mambo ya duniani wawiliwawili?

    Aliamua kufumbua macho yake, akakutana na Walter akitabasamu.

    Hamis akaamua kuutafuta ukweli.

    “Walter amemuoa muuaji??” swali hili lilimuumiza.







    Frank akakifanya kinywa chake kiwe chepesi na ubongo ufanye kazi kwa makini. Asiweze kumfadhaisha na kumwathiri Walter na pia ndoa ile kama ni kubaki salama iendelee kuwa salama.

    “Walter mwanangu…” aliita ka sauti nzito tulivu.

    “Ndio mzee wangu…..” alijibu Walter huku akiitua glasi ya maji aliyokuwa ameshikilia.

    “Tunaweza kutoka nje tutete kidogo…”

    “Aaah ni wewe tu mkuu…” alijibu Walter huku akisimama.

    Wakafika nje na kujiweka katika msingi wa nyumba.

    Walter akamsifia Walter kwa kumiliki nyumba nzuri, kisha akaingia katika mada husika.

    “Walter samahani kama ninaweza kuwa nakurejesha miaka ya nyuma sana, ama nitakukera kwa mambo ninayohitaji kuzungumza na wewe….”

    “Usijali baba.”

    “Walter umemtambulisha yule mwanamke kama mkeo lakini nasikitika kuwa hata jina hukunieleza anaitwa nani…”

    “Anaitwa Naomi baba, ah nimezoea kumuita vile.” Alijibu Walter huku akitabasamu.

    Frank akapatwa mshtuko lakini akajikaza kiutu uzima, akalikabili jambo hili.

    “Ahaa ok……Walter unakumbuka kifo cha dada yako…nimetanguliza samahani mapema.”

    “Nakikumbuka baba kwani kuna nini? Muuaji amepatikana?” alikurupuka na kukosa utulivu Walter.

    “Hapana hebu kuwa mtulivu basi.” Alitoa karipio dogo. Walter akatulia.

    Zikapita sekunde kadhaa, Frank akaanza kutiririka yote ya moyoni.

    “Kwa hiyo unamaanisha inawezekana Naomi wangu akawa anamtambua muuaji.”

    “Aidha anamtambua ama la ni yeye alikuwa msaidizi wangu wa ndani mwaka ule. Akili yangu haijanidanganya hata kidogo na sijamsahau binti yule hata kidogo.” Alijibu Frank.

    Walter akakosa utulivu. Akahamanika.

    “Kwani wewe ulikutana naye wapi?”

    “Kimboka….alikuwa changudoa baba….” Walter akausema ukweli.

    Frank aliposikia neno changudoa, akafanya swala fupi kwa kupitisha viganja katika uso wake.

    “Basi hamna shaka tena, ni huyu huyu Naomi ambaye alikuwa msaidizi wa Maureen, maana kwa taarifa za chini chini nilizozipata wakati ule ni kwamba Naomi alikuwa changudoa.” Frank akakazia, kisha akaendelea, “Lakini hala hala usimkaripie wala kumfukuza, jaribu kutafuta jibu sahihi, halafu ya kale hayanuki. Kama mnapendana samehe.” Frank akamwaga busara zake.

    “Nini? Nisamehe? Muuaji wa Maureen, niliapa kuwa sitamsamehe.” Aliwaka Walter.

    “Wanadamu hatuishi hivyo, acha visasi…” alisema Frank huku akimkazia macho Walter.

    “Hebu kwanza kaniletee kale kabegi kadogo.” Aliagiza Frank. Walter akasimama na kuingia ndani.

    Akarejea na begi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Frank akalifungua na kutoka na bahasha.

    Akaipekua na kutoka na picha mbili.

    “Hebu tazama au ndo tuseme duniani wawili wawili?”

    Walter akapokea zile picha na kuzikodolea macho.

    Naomi akiwa na marehemu Maureen wakitabasamu na kukumbatiana kwa upendo.

    “Mke wangu huyu baba, baba Naomi wangu huyu.” Alianza kukosa ustahimilivu.

    Frank alizidi kutoa nasaha.

    Walter alikuwa amevurugwa sana.

    “Nenda ukalale, kesho tutalitatua tatizo hili.” Alimaliza mjadala.

    Walter akakubali kinyonge kisha akaongozana na Frank, akamwonyesha chumba cha wageni na maelekezo ya hapa na pale.

    Wakaagana.

    Walter akaelekea chumbani kwake, taa ilikuwa imezimwa. Walter akaiwasha, Naomi alikuwa amesinzia, usoni alikuwa amepambwa na tabasamu hafifu.

    Walter akataharuki, alikuwa anatazamana ana kwa ana na muuaji wa dada yake mpenzi.

    Mara akafadhaika baada ya kukumbuka kuwa anatazama na mwanamke ambaye moyo wake ulikuwa umeamua kuishi naye milele na alikuwa amefanya kiapo hicho.

    Ni mengi ambayo Naomi alikuwa amemfanyia ya kukera lakini hili halikuwa kero bali maumivu makali.

    Mbaya zaidi alikuwa amejiwekea kiapo kuwa ni yeye na Naomi mpaka anapokufa.

    Jasho likamtiririka alipojiuliza swali.

    Naomi na Maureen yupi natakiwa kusimamia kiapo chake?

    Aidha nisimsamehe kamwe ambaye mkono wake umehusika na kifo cha dada yangu mpenzi ama niishi na Maureen katika namna yoyote ile.

    Mara akajihisi kutetemeka.

    Akaitazama saa yake.

    Ilikuwa ni saa sita na nusu usiku.

    Walter akakosa maamuzi. Baadaye akagundua kuwa Maureen na Naomi katika mzani wake wa moyo kuna mmoja ana kilo hamsini na aliyebaki pia ana kilo hizohizo.

    Umaarufu kando, utajiri wake kando, kila kitu kikawekwa kando, ikabaki akili ya kupima na kutatua matatizo.

    Walter hakutaka kabisa kushuhudia machozi ya Naomi baada ya kutamka kuwa kamwe hawezi kumsamehe. Na pia hakutaka kuishi na Naomi kinafiki bila kumshirikisha.

    Lile jeraha la kumpoteza dada yake katika mazingira tatanishi, na jeraha la kufanyiwa visa na Naomi ambaye ndiye aliyekuwa na jukumu la kuliponya jeraha la Walter, yakaungana na kuzaa kidonda.

    Maumivu mapya kabisa.



    Walter hakupiga hatua yoyote mbele, mapenzi yalikuwa mazito na ile damu iliyopotea miaka kadhaa nyuma nayo ilikuwa nzito.

    Kumbukumbu za kubadilika kwa Naomi zikamkumbusha jambo moja kuwa kamwe hakuwahi kumshirikisha Naomi juu ya kifo cha utata cha Maureen.

    Siku ya kwanza Naomi kutambua hilo ilikuwa siku ya ufunguzi wa nyumba yao mpya. Ni siku hiyo na kuendelea ambapo Naomi alianza kubadilika na kuzua visa na mikasa.

    “Kwa hiyo Naomi anajijua kuwa ni muuaji?” alijiuliza Walter.

    “Naomi ni mbinafsi sana, kwa nini sasa hakunishirikisha walau nimsikilize kabla sijagundua? Kama aliamua kujifia na siri yake hiyo na kunipa penzi la kinafiki tena linaloumiza basi na mimi ni heri nibaki na maamuzi yangu binafsi.” Akamaliza akapiga kite cha ghadhabu.

    Akavua shati lake kisha suruali.

    Akaingia maliwatoni.

    Akafungulia maji ya juu.

    Yakaanza kumlowanisha, kadri yalivyomwagikia ndivyo alivyozidi kulainika katika maamuzi.

    Tone la mwisho likarejea na maamuzi.

    “Siwezi kulala na muuaji wa dada yangu, na siwezi kumuumiza muuaji huyu.”

    Alipotoka bafuni, akavaa nguo zake zilezile alizozivua.

    Akamtazama Naomi kwa uchungu mkubwa, akamsogelea na kumpiga busu katika paji la uso.

    Naomi akazidi kutabasamu akiwa usingizini.

    Walter hakugeuka nyuma tena.

    Baada ya juma moja magazeti yakatawaliwa na habari za kushtua sana, yule Dj maarufu kabisa Dj Walter alikuwa ametoweka nyumbani kwake katika hali ya kushangaza hapakuwa na taarifa yoyote ya ni wapi alipo.

    Utata mtupu, kila mtu akawaza lake.



    Mara yule mgeni mtanzania mwenye ndevu nyingi kama mwarabu akashushiwa shutuma kuwa kuna jambo anafahamu.

    Frank akaingia matatani.

    Kila leo akawa anahitajika katika kituo cha polisi kwa mahojiano.

    Alikuwa amepanga kuishi Tanzania kwa siku tano tu, lakini haikuwezekana.

    Frank alikuwa amejivika moyo wa kiarabu katika shutuma hizi, hakuhitaji kusema iwapo kuna taarifa zozote alizomletea Walter kutoka Oman.

    Moyo huu ukamewepusha na mengi, maana polisi ukijaribu kuwaeleza unachojua wanataka uwaeleze na usiyoyajua kwa lazima.

    Mwisho wa siku unaitwa kama shahidi ili uidanganye mahakama.

    Frank alitamani sana kumweleza Naomi kuwa chanzo cha Walter kutoweka yawezekana ni mazungumzo baina yao juu yake.

    Lakini akakumbwa na hisia mbaya kuwa, je iwapo wawili hawa wakipatana tena.

    Je hataonekana mnafiki? Aliyejaribu kuwatenganisha?? Wakiwa chumbani watazungumza yapi juu yake? Je sio aibu hii na kujihanithi mbele ya mtoto wa kike?

    Frank akaufuta mpango wa kusema tetesi yoyote ile. Akabaki na kauli moja tu, kuwa hajui nini kinaendelea.

    Ya wapenzi waachie wapenzi usije ukaumbuka. Alijikanya Frank.



    ****

    NYUMBA ya wastani lakini iliyosheheni vitu mbalimbali vya thamani ilikuwa imetawaliwa na vumbi jingi sana ikimaanisha kuwa muhusika alichukua muda mrefu sana bila kuifanyia usafi.

    Lilian alibadili nguo zake, akajifunga kanga vyema kiunoni.

    Akachukua ndoo na kwenda nyumba ya jirani, akarejea na maji.

    Akaanza kusafisha sehemu kadha wa kadha huku akiendelea kumsimulia Walter mambo kadhaa juu ya mkoa huo mpya.

    Walter alikuwa anamshangaa bado Lilian, hakujua amuweke katika kundi gani la wanawake maana mambo aliyokuwa anayaongea yalikuwa yanaishi, hayakuwa ya kubuni.

    Lilian hakudumu na mada moja kwa muda mrefu sana, alipogundua inaanza kupooza aliingiza nyingine ya moto zaidi.

    Walter alichangamka haswaa na akausahau uchovu wote wa safari ndefu.

    Lily hakumpa Walter nafasi ya kukumbuka mambo kadhaa aliyoyapitia japo hakuwa akiyafahamu.

    Akadeki nyumba, akabadilisha mashuka kitandani, akatoa mapazia ya madirishani yaliyokuwa na vumbi, akaweka mapazia mengine.

    Hapa sasa Walter alijikuta akimsaidia aliachana na kitabu alichokuwa ameshikilia, wakashirikiana kama watu wanaofahamiana kwa siku nyingi sana.

    Walter akaifurahia hali ile. Alijikuta akifurahia kuwa na Lily.

    Yote hayo yalitokea huku Walter akiwa ameahidiwa kupelekwa katika nyumba ya kulala wageni baada ya usafi ule. Na pia baada ya kufanya makubaliano ya kuhusu kitabu.

    Usafi ukakamilika hatimaye.

    Kama Walter alidhani wanawake wa kinyakyusa hawajui kutunza mwanaume alikosea.

    Lilian akaingia jikoni upesi. Akatoka na mchele.

    Akiwa na kanga yake vilevile akaanza kuupembua.

    “He hadi upike tena si tutachelewa.” Walter aliweka mashaka yake wazi.

    “Unahitaji kukimalizia hicho kitabu?” badala ya kujibu Lily aliuliza swali.

    Walter akacheka, kisha akaendelea kusoma kile kitabu.

    Baada ya masaa mawili ikiwa saa mbili usiku walikuwa wanapata chakula.

    Lily kama kawaida yake. Akaendelea kumchamkia Walter bila kuweka neno lolote la kumkera.

    Baada ya mlo, Walter alidai kuwa ameanza kupata dalili za uchovu.

    “Nakupeleka kulala, kama utapenda kuendelea na hicho kitabu asubuhi njoo mimi nitakuwepo.” Alisema yule binti, kisha akasimama.

    Akampeleka walter katika hoteli ambayo ilikuwa maeneo ya Ilomba mkoani Mbeya.

    Walter akapata chumba.

    Akakilipia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakaagana na Lilian.

    Kabla ya kulala Walter akakiri kuwa kuna kitu alikuwa amenufaika kwa kuwa karibu kabisa na Lilian.

    Maajabu. Lilian alikuwa amemuwezesha kusahau kuhusu mtihani ambao alikuwanao. Lakini si Lilian pekee aliyemfanya atokwe na kumbukumbu hizo mbaya.

    Akakikumbuka pia kitabu cha riwaya. Riwaya ile ilimteka akili na kumsahaulisha kabisa kama kuna mtihani unamkabili.

    “Lazima nimfuate Lilian asubuhi.” Alijiahidi, kisha akalala akiwa na uamuzi huo ambao kwake aliuona ni sahihi sana.

    Walter akaanza maisha katika jiji la kijani. Jiji la Mbeya.

    Akayafumba macho yake na kurudisha kumbukumbu za kukutana na binti yule wa maajabu ambaye hakukumbuka hata kumuuliza alikuwa akijishughulisha na nini.

    *****

    KIUBARIDI kilitawala na kuwafanya abiria wengi wajikunyate huku baadhi wakisugua mikono yao ili kulipata joto.

    Hali ilikuwa tofauti sana kwa kijana aliyevalia fulana nyepesi akiwa na kibegi chake kidogo.

    Hakuonyesha dalili ya kusumbuliwa na kiubaridi kile.

    Alikuwa amekaa siti ya dirishani akiangalia mandhari ya jiji la dare s salaam ilivyotapakaa watu wengi, kila mmoja akiwa na shughuli yake ya kufanya.

    Basi lilianza kupiga honi kuashiria kuwa safari inakaribia kuanza hivyo abiria ambao hawajaingia katika basi wafanye kuingia.

    Honi hizo zilimkurupua kijana yule na kuyarejesha mawazo yake katika basi, akaangaza huku na huko akaona hakuna jipya akaendelea kushangaa nje.

    Mara gari lilianza kuunguruma.

    Akaingia abiria wa mwisho akiwa amechelewa kupita wote.

    Alikuwa akitweta na jkijasho kilikuwa kinamtoka.

    Abiria yule aliitoa tiketi yake na kuisoma, akaikariri namba ya siti yake kisha akaanza kuitafuta.

    “Mambo kaka.” Alisalimia abiria yule, alikuwa ni mwanadada.

    Hakupata jibu, akasalimia tena ndipo akashtuka yule kijana.

    “Salama dada hali…aah samahani sikukusikia.” Alizungumza huku akilazimisha uchangamfu.

    “Mwenzangu kidogo basi liniache dah…” aliendelea kuzungumza yule dada huku akilipanga begi lake katika nafasi ya kuweka mizigo. Kisha akakaa.

    Kimya kikaendelea kutanda.

    Safari ikaanza.

    Yule kijana aliendelea kutazama jinsi basi lilivyokuwa linaongeza mwendo na kuiacha ardhi ya Dar es salaam.

    Kadri alivyoiacha ardhi ile alijipa moyo kuwa anayakimbia matatizo.

    Aliona anakimbia swali gumu la kufanya maamuzi ambalo linamkabiri.

    Maamuzi ya aidha kusamehe na kusahau ama kutunza kiapo chake ambacho hakikuwa kiapo tena bali nadhiri.

    Walter alikuwa katika mtihani mgumu.

    Jeraha la hisia lilimvuruga.

    Sasa yu katika basi linaloelekea Mbeya, anaamua kujiweka mbali na matatizo. Huku akiamini kulikimbia tatizo nd’o kulisuluhisha.



    Baada ya kimya kirefu, Walter alimgeukia yule dada aliyekuwa amejikita sasa katika kusoma kitabu.

    “Mh. Huyo ni Beka Mfaume ama?” Walter alijikuta ameuliza.

    “Yeah. Riwaya yake mpya hii Marry Mariam.”

    “Mh. Hivi si mara ya mwisho alikuwa ametoa hii ya Wivu na Mama Jenifer” Walter alidadisi.

    “Wewe yaani hapo mbona ni zamani, alitoa Mzee Beka, akatoa na nyingine inaitwa Msalaba wa Shetani, halafu akatoa mzee Beka sehemu ya pili, kuna nyingine sasa inaitwa Mwiba…hiyo sasa ni balaa, halafu sasa nd’o hii mpya katoa juma lililopita.” Yule dada alimuelezea Walter kwa kirefu akionyesha ni jinsi gani anamtambua mtunzi bora wa riwaya nchini Tanzania, Beka Mfaume.

    “Aisee basi huku kukaa nje ya nchi kumenikosesha mengi sana.” Alilaumu Walter, kisha akaendelea. “Sasa hata sijui nitavipataje hivyo vingine.” Alizungumza kama anayejiuliza mwenyewe.

    Yule dada badala ya kujibu akazama katika mkoba, akaibuka na vitabu.

    “Kipi unataka nikuazime, lakini mwisho wa safari unanirudishia.”

    “Hebu nipe Msalaba wa shetani kama kipo.”

    “Hicho kipo lakini hebu jaribu kuusoma MWIBA” Binti alisema huku akipekua mkoba wake mdogo, akachomoka na kitabu.

    Kilikuwa kinaonekana kana kwamba ni kipya, hakika binti yule alikuwa mtunzaji.

    Vitabu vya riwaya vya mzee Beka Mfaume vikawasababisha watambuane wawili hawa.

    “Huyu Lilian nd’o wewe.” Walter aliuliza baada ya kukuta jina mwanzoni mwa kitabu.

    “Yeah ni mimi, na wewe unaitwa nani.”

    “Naitwa Walter….niite Dj ukipenda.”

    Yule dada akajibu kwa kichwa kisha wakaendelea kuburudika kila mmoja na kitabu chake. Hakuna aliyemsemesha mwenzake.

    Beka alikuwa amewateka katika maudhui tofauti, huku MWIBA huku Mary Mariam.

    Walikuja kuzungumza tena wakati gari liliposimama, abiria waweze kuchimba dawa.

    Na kwa mara nyingine tena walizungumza wakati wa kupata chakula, basi liliposimama.

    Kisha kikafuata kimya kikubwa hadi basi lilipogota.

    Kituo kikuu cha mabasi Mbeya.

    Walter kwa mara ya kwanza akajikuta akimueleza Lily kuiwa yeye alikuwa mgeni katika mji ule.

    Lily akajitolea kuwa mwenyeji wake katika kumsaidia kupata nyumba ya kulala.

    “Na kitabu chako pia kimenivutia sana, unaweza kuniachia mpaka nimalize.” Walter aliomba.

    “dah..ni hilo tu huwa nagombana na kila mtu, yaani sijui kwanini tu huwa siamini kuwa hakuna mwanadamu anayeweza kutunza kitu change kama ninavyoweza kukitunza mimi mwenyewe.” Alijibu kwa hoja yule binti.

    Walter akakunja sura yake. Ni kama alikuwa anakatishwa utamu wa namna yake.

    “Lakini usijali utakisoma tu…….sasa tunaenda kwangu upajue kwanza, kama ukihitaji kukisoma ukipata muda njoo nyumbani. Utakisoma utamaliza.” Alisema kwa sauti iliyochangamka.

    Wakaongozana na kuzifikia daladala.

    “Ilomba…” kondakta aliuliza.

    “Shushaa..” alijibu Lily.

    Safari yao ikaishia hapo.

    Wakajikokota kwa mwendo wa miguu.

    Hatimaye wakaifikia nyumba ya Lily.

    Yakendelea yaliyotokea.

    Sasa Walter anamkumbuka Lily na kitabu cha Beka kama mojawapo ya vitu vilivyompa furaha sana katika siku hiyo.

    Anajiahidi kumtafuta Lily siku inayofuata.

    Yawezekana Lily na vitabu vya riwaya vikawa suluhu ya matatizo yangu. Alijiwazia Walter.

    Usiku mnene ukapita, alilala fofofo.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Na kitabu chako pia kimenivutia sana, unaweza kuniachia mpaka nimalize.” Walter aliomba.

    “dah..ni hilo tu huwa nagombana na kila mtu, yaani sijui kwanini tu huwa siamini kuwa hakuna mwanadamu anayeweza kutunza kitu change kama ninavyoweza kukitunza mimi mwenyewe.” Alijibu kwa hoja yule binti.

    Walter akakunja sura yake. Ni kama alikuwa anakatishwa utamu wa namna yake.

    “Lakini usijali utakisoma tu…….sasa tunaenda kwangu upajue kwanza, kama ukihitaji kukisoma ukipata muda njoo nyumbani. Utakisoma utamaliza.” Alisema kwa sauti iliyochangamka.

    Wakaongozana na kuzifikia daladala.

    “Ilomba…” kondakta aliuliza.

    “Shushaa..” alijibu Lily.

    Safari yao ikaishia hapo.

    Wakajikokota kwa mwendo wa miguu.

    Hatimaye wakaifikia nyumba ya Lily.

    Yakendelea yaliyotokea.

    Sasa Walter anamkumbuka Lily na kitabu cha Beka kama mojawapo ya vitu vilivyompa furaha sana katika siku hiyo.

    Anajiahidi kumtafuta Lily siku inayofuata.

    Yawezekana Lily na vitabu vya riwaya vikawa suluhu ya matatizo yangu. Alijiwazia Walter.

    Usiku mnene ukapita, alilala fofofo.



    ****

    Naomi alihangahika huku na kule kujiuliza ni wapi Walter atakuwa ameelekea, jitihada zake akishirikiana na jeshi la polisi zikagonga mwamba.

    Frank akaonekana hana chochote cha kulisaidia jeshi la polisi. Akaruhusiwa kuendelea na ratiba zake.

    Upesi akaandaa safari ya kurejea Oman ambapo aliacha familia yake.

    Naomi akawa katika mitihani miwili.

    Kumuuguza dada yake ambaye alikuwa muathirika wa magonjwa yanayosababishwa na Ukimwi. Huku akiwa na mtihani mwingine wa kumtafuta Walter.

    Kipenzi cha moyo wake.

    Huu ukawa utata wa hali ya juu.



    Ile hali ya kulala kitandani peke yake ikamfanya ajikute katika hisia fulani za maajabu, hisia zilizomfanya aamini kuwa uwepo wa EWalter pembeni yake ulikuwa na maana kubwa, maana ya kuleta furaha katika maisha yake.

    Amani ilikuwa imetoweka.

    Naomi akajikuta kwa mara ya kwanza akijuta kumsababisha Walter ajiweke mbali naye. Kauli kali za kuchoma moyo kutoka kwa Walter ambazo hazikuonekana kuwa na maana yoyote katika wakati ule sasa zikaanza kumchoma moyo maradufu.

    Naomi akakurupuka kutoka kitandani akawasha taa, akasimama wima. Safari yake ikaishia katika kioo.

    Akajitazama, alikuwa yu uchi wa mnyama.

    Akajitazama kuanzia uso wake, uso ulikuwa na makunyanzi kwa mbali. Makunyanzi yaliyosababishwa na matumizi ya madawa mbalimbali makali katika vipodozi, pia matumizi ya pombe kali enzi za biashara yake ya uchangudoa.

    Macho yakashuka chini kidogo, akajitazama kifua chake, licha ya kwamba alikuwa bado hajapata mtoto lakini matiti yake yalikuwa yamekongoroka, hayakuwa ya kutamanisha. Yalitaka kufanana na ya mzee.

    Naomi akashuka chini zaidi katika mapaja yake, nayo pia hayakuwa na mng’aro wa kike. Yalikuwa yamechoka haswaa na pia yalikuwa na misuli ya kijani iliyosababishwa na matumizi ya mikorogo yenye madhara katika ngozi. Halafu alikuwa na matege.

    Naomi akastaajabu sana, ilikuwa ni kama mara yake ya kwanza kujitazama katika kioo. Hakika hakuwa na mvuto wa kuweza kumpagawisha mwanaume kama Walter.

    Kijana maarufu mwenye pesa.

    Pesa nyingi.

    Mara jicho la Naomi likaanza kutalii katika chumba cha kifahari alichokuwa analala na Walter. Hakuna kilichokosekana katika chumba kile.

    Walter aliweka kila kitu katika nyumba ile ambacho kilikuwa fahari kwa Naomi. Licha ya kwamba Walter hakuwa mtumiaji wa pombe aliweka utaratibu wa kuhifadhi chupa kadhaa za pombe katika jokofu, yote hii kumfurahisha Naomi.

    Naomi akaanza kutetemeka na kujiona kuwa yu mkosaji sana na wala hakustahili kumtendea Walter yote ambayo amewahi kumtendea. Naomi hakuwa na hadhi yoyote ya kuishi na mwanaume kama Walter.

    Hakika Naomi akakiri kuwa ni upendo wa dhati wa Walter uliomfanya amtendee yote yale.

    Ni wangapi wanaweza kumpenda mtu kama yeye? Changudoa…tena changudoa mzoefu.

    Kwa mwanaume yeyote mwenye akili hawezi kufikiria walau kuwa na urafiki na Naomi.

    Lakini Walter alimuoa, tena na ndoa wakafunga.

    Maajabu….

    Akiwa katika kuwaza hayo akakikumbuka chanzo cha haya yote ni kifo cha Maureen.

    Naomi akajishangaa ni kwanini alijitwisha mzigo wa kifo kile wakati hakuhusika nacho moja kwa moja.

    Ni kweli alitoroka na kumwacha Maureen peke yake, lakini hakutegemea iwapo mvua ingeweza kunyesha na kuzua balaa lile.

    Naomi akajiona kuwa alikuwa na mengi sana ya kujieleza katika jamii na kusamehewa na kisha kujitua mzigo ule.

    Naomi akatamani Walter ajitokeze mbele yake aweze kumweleza kisa chote cha kufikia hatua ya kutoroka usiku na hatimaye kukutana na kifo hiki asubuhi.

    Naomi alikuwa amechelewa, yule Walter aliyewaza kumweleza kila kitu kilivyokuwa alikuwa katika jiji la Mbeya tayari.

    Naomi akalala, akitegemea kuamka na kukutana na Walter asubuhi.

    Lakini hapakuwa na ndoto kama ile.

    Walter hakuwepo.



    ****

    Asubuhi iliyofuata Walter alidamka, akajiandaa kisha akaitazama saa yake, tayari ilikuwa imetimu saa mbili asubuhi.

    Akakifunga chumba chake, akawaomba wahudumu wasihangaike kufanya usafi wowote ndani ya chumba chake.

    Kisha akatoka nje.

    Akakumbana na baridi kali lakini linaloburudisha la jijini Mbeya. Jiji geni kabisa katika macho ya Walter.

    “Ilomba….pazuri kweli hapa.” Walter alijisemea kwa sauti ya chini huku akisugua mikono yake kulitafuta joto.

    Hali ya hewa ya Mbeya ilimpendeza.

    Walter akaichukua simu yake ambayo ilikuwa imehifadhi namba moja tu ya simu. Akabofya, ilaanza kuita.

    Mara ikapokelewa.

    Alikuwa Lilian.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hujaamka tu…” Walter aliuliza.

    “Mh. Niliamka kitambo tu, nimemalizia kufanya usafi. Nipo naandaa stafutahi.”

    “Stafutahi nd’o nini?” Walter aliuliza kiudadisi akidhani Lilian ameongea kwa kabila lake.

    Lilian akacheka kab la ya kujibu, “Stafutahi ni kifungua kinywa….”

    Walter akastaajabu kidogo kisha akarejea katika maongezi, “Kumbe nd’o hivyo? Mwenzangu, mimi na Kiswahili mbalimbali. Nilikimbia umande mwenzako.”

    “Pole, hii stafutahi inamngoja mtu lakini…” Lilian alisema kisha akasita.

    Walter akajikuta anajisikia vibaya, maana alihisi jibu linalofuata litakuwa la kumtambulisha mchumba ama mume wa Lilian, Walter hakutaka kusikia lolote juu ya mapenzi. Aliamini kwa kusikia mapenzi lazima atakumbuka chanzo cha yeye kuwa katika jiji la Mbeya.

    Walter hakutaka kumkumbuka Naomi na visa vyake. Pia hakutaka kumkumbuka marehemu dada yake.

    “Nani tena huyo?” aliuliza kwa unyonge mkubwa.

    “Kijana mmoja anaitwa Walter….” Alisema Lily kisha akashusha pumzi.

    Walter naye akashusha pumzi, hakutegemea jibu kama lile.

    Akataka kutia neno la nyongeza, simu ikapiga mlio wa kuishiwa pesa, akakata na mazungumzo yakakomea hapo.

    Alipoongeza pesa, alimjulisha Lilian kuwa alikuwa njiani kuelekea nyumbani kwake.



    Baada ya dakika kumi Walter alikuwa mezani katika nyumba ya Lilian. Chakula kilikuwa mbele yao.

    Lilian akaongoza sala, wakaanza kustafutahi.

    Chai nzito ya maziwa, chapati zilizowekewa shehena ya mayai ya kukaangwa, matunda kadhaa yalikuwa yakingoja kusalimiana na matumbo ya wawili hawa.

    Hakika kilikuwa kifungua kinywa cha uhakika.

    Baada ya kila mmoja kuridhika. Lilian akiwa anatoa vyombo alianza kupepeta mdomo kama ilivyo kawaida yake.

    Maneno yalitoka katika mpangilio mzuri hayakumchosha Walter.

    Hakika alipata burudiko la aina yake.



    Lilian alikumbuka kumpatia Walter kitabu cha riwaya cha mzee Beka.

    Walter akakikamata na kufungua ukurasa ambao aliishia siku iliyopita.

    Akajikita katika kuendelea kunyonya mafunzo baadhi na burudani kutoka katika riwaya.

    Lilian aliaga kuwa anaelekea sokoni. Walter akabaki mwenyewe nyumbani.

    Ilimstaajabisha Walter kwa imani iliyoonyeshwa na Lilian kwake, ni kweli hakuwa na kitu kikubwa sana cha kuweza kuibiwa lakini vipo baadhi kama kompyuta mpakato ‘laptop’ vingeweza kuibiwa. Lakini Lilian hakujali.



    *****





    Mwanadada aliyejivika mavazi nadhifu ambayo bila shaka yangeweza kumpa heshima popote ambapo angeweza kwenda. Alikuwa akiangaza huku na kule.

    Madereva wa taksi wakamshtukia kuwa alikuwa anahitaji huduma. Dereva mmoja akajongea na kumkabili.

    Akanadi usafiri wake, dada yule akavutika na lugha yake tamu akaingia katika gari lake.

    “Hospitali ya mkoa….” Aliamrisha.

    Dereva akatia moto gari ikaondoka.

    Baada ya muda mfupi waliipita shule ya sekondari ya Loleza., wakaingia mitaa ya Sokomatola, hatimaye wakaifikia hospitali.

    Mwanadada akafanya malipo kisha akatelemka.

    Macho kadhaa yaliyompokea yaliburudika kumtazama. Hata waliokuwa wagonjwa walifurahi kuiona sura ile.

    Nani hakuwa anamfahamu Suzi?

    Daktari mdogo kupita wote katika hospitali ya Mbeya, tena akiwa na vitu vingi vya ziada kwa kila rika.

    Alipendwa na watu, naye aliwapenda.

    Licha ya kufahamika na umuhimu wake kuthaminiwa kwa kiasi kikubwa sana, katu hakuwa na maringo.

    Akanyata hatua kadhaa, akiwa anawapungia mkono aliogonganisha nao macho. Nao wakampungia kwa furaha na jicho la matumaini.

    Aliwajibu kwa tabasamu hafifu.

    Hatimaye akaufikia mlango wa ofisi ya ushauri nasaha.

    “We Beatrice wewe….ndo nini kuja kimya kimya hivyo?” alipokea swali likiambatana na mshtuko kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi waliokuwa katika ofisi ile.

    “Mwenzangu kuna mama amenililia huyo…..mume wake analalamika kuwa unyumba hauna kiwango.” Suzi akanong’ona, kisha wakacheka kwa pamoja.

    “Basi akanitumia nauli. Ndo hivi nimefika kuwajulia hali.”

    “Kwa hiyo ukimaliza nd’o unaondoka tena….” Akauliza yule mfanyakazi. Suzi akatikisa kichwa huku na kule kisha akajibu, “Sina uhakika sana kama nitaondoka ama nitabaki…..si unajua tena.”

    Mazungumzo yao yakaishia pale.

    Msululu wa wahitaji huduma ulikuwa unaongezeka. Suzi akajishtukia, akamwacha mwenzake aendelee na kazi.

    Alipotoka kila mmoja alihitaji kuzungumza neno naye, alitamani sana kuzungumza nao lakini muda haukuwa unaruhusu.

    Akawaahidi kuwa siku itakayofuata atakuwa ofisini.

    Wakamsindikiza kwa macho ya aina tofauti tofauti, wapo waliomtazama kwa jicho la husda na wengine walimtazama kwa jicho la kumbariki.

    Hakujali, akatoweka.

    Akajikongoja kwa mwendo wa miguu.

    Akalifikia soko la vyakula.

    Soko matola.

    Akatembelea mabanda kadhaa, akanunua kuku mkubwa wa kienyeji, akanunua mapochopocho kadhaa, akapita buchani akanunua nyama ya ng’ombe kiasi kidogo.

    Akaridhika kuwa alikuwa amefanya manunuzi ya maana.

    “Hapa Walter lazima atambue kuwa wanyakyusa nasi tulipewa talanta ya kulea mwanaume…” Suzi alijisemea.

    Kisha akaitazama saa yake, yalikuwa yamepita masaa mawili tangu amuage Walter kuwa anaelekea sokoni.

    Muda muafaka kabisa wa kurejea nyumbani.

    Suzi akachukua taksi tena, ikamchukua mpaka nyumbani.

    Aliposhuka hakuwa Suzi tena alikuwa Lilian.

    Walter alikuwa amezama katika riwaya.

    Hakuweza kumsikia Lilian alipoufikia mlango

    Lilian akamtazama Walter alivyokuwa ametulia. Shati lake liliruhusu kifua chake kuchungulia nje, alikuwa na vinyweleo fulani ambavyo vilikuwa vinapendeza macho ya msichana kumtazama.

    Mwili wake ulikuwa umegawanyika kimazoezi.

    Damu ikasafiri kwa kasi mithili ya shoti ya umeme baada ya jicho lake kukiona kidole cha Walter.

    Walter alikuwa amevaa pete. Pete katika kidole maalum kwa wanandoa.

    Ilikuwa mara yake ya kwanza kukiona kidole kile na pete.

    “Walter amefunga ndoa??” alijiuliza.

    Mara maumivu makali yakapenya katika moyo wake. Akajikuta anatoneshwa jeraha la miaka sita iliyopita.

    Jeraha la hisia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Furaha ikatoweka.

    Akajikuta katika mfadhaiko wa namna yake.

    Mara yule jogoo akawika.

    Walter akashtuka na kubaini kuwa Lilian alikuwa mbele yake.

    Lilian akajilazimisha kutabasamu.

    Tabasamu likagoma.

    Maumivu ya jeraha lililotoneshwa yakamsokota huku na kule.

    “He..umefika hapa sijakusikia?” Walter akahoji.

    Lilian akakosa la kumjibu………..



    Damu ikasafiri kwa kasi mithili ya shoti ya umeme baada ya jicho lake kukiona kidole cha Walter.

    Walter alikuwa amevaa pete. Pete katika kidole maalum kwa wanandoa.

    Ilikuwa mara yake ya kwanza kukiona kidole kile na pete.

    “Walter amefunga ndoa??” alijiuliza.

    Mara maumivu makali yakapenya katika moyo wake. Akajikuta anatoneshwa jeraha la miaka sita iliyopita.

    Jeraha la hisia.

    Furaha ikatoweka.

    Akajikuta katika mfadhaiko wa namna yake.

    Mara yule jogoo akawika.

    Walter akashtuka na kubaini kuwa Lilian alikuwa mbele yake.

    Lilian akajilazimisha kutabasamu.

    Tabasamu likagoma.

    Maumivu ya jeraha lililotoneshwa yakamsokota huku na kule.

    “He..umefika hapa sijakusikia?” Walter akahoji.

    Lilian akakosa la kumjibu………..



    Lilian alikuwa amefadhaishwa na hisia zake. Akakitua kikapu chake kikubwa kisha akabadili mada.

    Akamhadaa Walter kwa maneno mawili matatu. Walter akahadaika, Lilian akaendelea na maandalizi ya chakula cha mchana.

    Hakuwa mchangamfu alifanya kujilazimisha tu.

    Furaha ingetoka wapi, Lilian alikuwa amemkumba marehemu Daktari Mbaule na mkewe Rose.

    Wakati akiendelea kukatakata viungo, alijaribu kupambana na hisia zile za kitambo zisiweze kumrudia tena, lakini ziligoma na kuendelea kumtawa.

    “Walter kichwa kinaniuma……”

    Walter akakiacha ghafla kitabu chake cha riwaya, akatilia maanani maneno ya Lilian. Akasimama, na kumsogelea, Lilian alikuwa amepooza sana.

    “Una dawa za kutuliza maumivu humu ndani….” Walter akamuuliza kwa utulivu huku akiwa amemshika bega.

    Lilian akanyoosha mkono kumwelekeza Walter, upesi kijana akajongea na kurejea na dawa za kutuliza maumivu, akachukua na maji ya kunywa akampatia Lilian.

    “Pumzika kidogo, dawa ifanye kazi.” Walter akatoa wazo, Lilian akajikongoja kitandani, akajilaza.

    Hapo sasa akairuhusu akili yake kupumzika kidogo.

    Usingizi ukampitia.



    *****



    Jitihada za kumbembeleza zilikuwa zimekwama, alikuwa akiomboleza kuliko wanawake wote waliohudhuria msiba huo.

    Hakuna aliyejua ni kipi kilitokea baina yake na bwana Mbaule hadi binti huyu aumizwe kiasi kile na msibu ule wa kushtukiza.

    Lilian alikuwa hakamatiki hata kidogo.

    Tabu zaidi ilikuja pale ambapo mwili daktari Mbaule ulivyokuwa ukifukiwa chini katika nyumba ya kudumu.

    Lilian aling’ang’ania kuingia kaburini, wanaume wenye nguvu wakamkamata ipasavyo, Lilian akawa mjanja akamng’ata mwanaume mmoja mkononi, akamuachia lakini yule wa pili alikuwa imara akamkwida vyema binti yule. Kisha akamnasa vibao viwili akatulia.

    Lilian akazimia baada ya mchanga wa mwisho kurushwa kaburini.

    Alikuja kuzinduka masaa kadhaa baadaye, alikuwa kitandani akiwa na sindano iliyotoka katika chupa ya maji yaliyokuwa yakimwingia mwilini.

    Lilian hakuweza kubadili jambo lililotokea, Mbaule alikuwa marehemu.

    Lilian alikuwa amekaribia kupona jeraha la kifo cha Rose ambaye alikuwa mke wa marehemu Mbaule. Huyu alikufa kwa shinikizo la damu baada ya kumfumania Lilian akiwa katika mapenzi mazito na Mbaule. Mama yule ambaye alikuwa na mtoto mmoja alianguka chini na alivyofikishwa hospitali alikuwa amekufa tayari.

    Siri hii ya kifo ikabaki katika mioyo miwili, moyo wa Lilian na ule wa Mbaule. Wakasimama kikamilifu bila kuivujisha siri ile.

    Lilian alizilaumu sana hisia zake za maajabu, akiwa binti wa mwisho katika familia yake, hakuwahi kupatwa na hisia zozote za kimapenzi.

    Wazazi wake walikuwa na wasiwasi huenda binti yao alikuwa na homoni za kiume huku jinsia pekee ikiwa ya kike, kutokana na kipato cha kawaida sana walichokuwanacho hawakuweza kuchukua hatua zozote za ziada.

    Alipomaliza kidato cha nne, akaunganisha kozi ya uuguzi. Ni huku binti huyu alipokutana na dokta Mbaule.

    Dokta ambaye tangu amguse kwa mara ya kwanza nesi huyu katika chumba cha akina mama cha kuzalia. Lilian alijikuta akipatwa na hisia za tofauti.

    Dokta alipoligundua hilo akamfanya kuwa mpenzi wake kwa siri kubwa huku wakisahau kuwa map[enzi ni kikohozi. Hayafichiki.

    Siku walipogundulika wakasababisha kifo.

    Ili kudumisha walichokian zisha wakaendelea na uhusiano wa kimya kimya.

    Dokta Mbaule akiamua kumsomesha Lilian, kwa kuwa vyeti havikuruhusu kwa elimu ambayo dokta alitaka binti yule aipate.

    Akafanya mpango wa kununua cheti.

    Cheti kikapatikana kwa jina la Suzan Nyangeta. Lilian akaingia chuo, huku daktari akitoa ahadi kuwa baada tu ya kumaliza chuo wataweza kuoana. Ahadi murua kabisa.

    Jina la Lilian awapo chuoni likasahaulika.

    Akabadilika kuwa Suzi.

    Masomo yakaendelea na mapenzi yakiendelea pia.

    Baada ya miaka kadhaa Suzi akamaliza hatua ya kwanza ya elimu yake.

    Ni hapa kilipokuja kutokea kimbwanga.

    Akiwa chuoni Lilian alikutana na kijana wa rika lake.

    Awali hakuwahi kutegemea kuwa anaweza kumsaliti bwana Mbaule.

    Lakini kwa kuwa hakuwa na uzoefu katika mapenzi anajikuta akiuingia mkenge. Anamwagiwa uongo mwingi, anaumeza kama ukweli.

    Anaamua kumtupilia mbali yule mzee, kimya kimya bila kumwambia.

    Anaanza kushiriki mapenzi na yule kijana.

    Cha kushangaza hapatwi na hisia wawapo sirini, anakuwa kama anajilazimisha, lakini hamwelezi yule kijana ambaye siku zote anahisi kuwa anamridhisha Lilian.

    Lilian anaanza kuyaona mahusiano haya kama mzigo, anatamani kuyatua lakini kijana yule haonyeshi dalili zozote za kuhitaji kuachana na Lilian.

    Hatimaye wanamaliza chuo.

    Wanapoingia mtaani linatokea fumanizi la aina yake.

    Daktari huyu mtaalamu wa saikolojia anaisoma akili ya Lilian na kugundua kuwa binti amebadilika, anaamua kumpeleleza kimatendo.

    Upelelezi huu unakomea katika nyumb a ya kulala wageni.

    Lilian akiwa na yule kijana wakifurahia raha za dunia.

    Hofu ikatanda, daktari yule akaamini kuwa kwa namna yoyote ile lazima Lilian atakuja kuropoka siri wanayohifadhi katika mioyo yao juu ya kusababisha kifo cha Rose.

    Mawazo yakatanuka zaidi na daktari akajikuta akipatwa na hisia kali za kushangaza. Hakika alikuwa anampenda binti yule.

    Binti aliyesababisha mkewe aage dunia leo hii amemsaliti.

    Inauma sana hakika.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kikasikika kilio cha mkewe, picha mbaya za kumbukumbu zikapita kwa kasi sana.

    Kama ilivyokuwa kwa marehemu mkewe, mara naye akaanza kujisikia hovyo.

    Hakusikia hata mlango ulivyokuwa unagongwa, baada ya dakika kadhaa akaingia yule binti msaliti.

    Mzee akaanza kulalamika, alilalamika huku jasho kali likimtoka.

    “Lilian..ni kipi ulitaka nikupe katika maisha yako, ulitaka kipi cha ziada ukiondolea mbali roho ya mke wangu ambayo sasa haipo tena? Lilian, licha ya yote ninayokugharamikia bado umeenda kunisaliti na vijana wasiokuwa na mwanga wowote kwako maishani? Kilio chako kwangu kilikuwa bure Lilian. Ulinilaghai, hukunipenda kumbe, niue basi niue….” Alilalamika Mbaule.

    Kiyoyozi kikafanya kazi ya ziada kumpooza lakini bado ilikuwa kazi bure.

    Lilian akakosa cha kujitetea. Akaanza kulia.

    Akalia huku akijuta na kuomba msamaha.

    Kilio hiki huenda hakikuwa kikimwendea mtu yeyote.

    Daktari mkongwe Mzee Mbaule alikuwa amelala kimya.

    Na hakuamka tena hata akafukiwa chini.

    Lilian alihudhuria msibani kama wahudhuriaji wengine, lakini alitofautishwa na kile kilio kikali ajabu hadi akapoteza fahamu.

    Alipozinduka bado hakuwa na nguvu mwilini na pia hakuwa na lolote la kusema. Maana angeweza kujiingiza matatani.

    “Daktari akautwa kitandani kwake akiwa amekufa…” machapisho ya magazeti yaliandika hivi. Lilian hakujulikana kama ndiye shuhuda.



    Kilichofuatia Lilian alivunja mahusiano na yule kijana, akaendelea na masomo kwa jina la Suzi.

    Akakutana na wanaume wengine lakini cha ajabu hakuwa na hisia za kimapenzi, mwili haukumsisimka kwa aina yoyote ile, haikujalisha aidha kuguswa na mwanaume ama kusikia sauti ya kiume.

    Lilian akarejea kuwa yule Lilian wa miaka kadhaa iliyopita.

    Elimu ikamfikisha hatua ya kuwa msaidizi wa daktari na baadaye daktari kamili.

    Akajitolea muda wake kutatua matatizo ya watu wengine kimawazo.

    Yeye akiwa na kila kitu isipokuwa hisia za mapenzi.



    Safari ya kurejea jijini Mbeya kutoa huduma inamkutanisha na kijana ambaye baada ya kugusana naye kidogo alkajisikia kusisimka sana.

    Sauti yake ilivyopenya masikioni mwake ikasafiri hadi katika kizibo cha hisia kilichofunikwa juu ya moyo, ikakifunua.

    Hisia zilizojidunduliza kwa miaka kadhaa zikatambaa mwilini kwa kasi.

    Lilian akajihisi yu karibu na marehemu Mbaule.

    Mwanaume pekee aliyeweza kuziamsha hisia zake za kimapenzi.

    Yalikuwa maajabu makubwa sana haya kwa binti huyu.

    Hisia zake zikiwa zimezagaa kila kona, anakutanisha jicho na pete ya ndoa.

    Yule ambaye anahisia anampenda, kumbe ana mke?

    Lilian anapagawa, hisia za kitambo zinamshambulia, na hatimaye kichwa kinaanza kumuuma.

    Sasa yu usingizini na kumbukumbu hizi za maajabu zinapita katika kichwa chake.

    “Lazima nimpate Walter, walau kwa usiku mmoja tu kama kweli ameoa? Na kama hajaoa namtaka awe wangu milele.” Lilian alijiapiza punde tu baada ya kuzinduka kutoka usingizini.

    Alikuwa amelala masaa kadhaa.

    Harufu nzuri ilimpokea, alipofumbua macho yake, hapakuwa na lile kapu la mapochopocho alilolinunua sokoni.

    Akaangaza huku na kuke hata Walter hakuwepo.

    Lilian akakurupuka kitandani na kutoka nje.

    Akasimama na kustaajabu kwa mshangao.

    Walter alikuwa amejikita katika kupika.

    Majiko mawili yalikuwa yamewashwa.

    Jiko moja pilau ilikuwa imebanikwa tayari.

    Jiko jingine, mapande ya yule kuku yalikuwa yakiruka huku na kule.

    Walter alikuwa amekaa katika kigoda akikatakata matunda kiudstadi.

    Mikono miwili ikaufunika mdomo wake, hakika alikuwa amestaajabu.

    Hakutegemea haya.

    Akapiga hatua kadhaa nyuma, akajirudisha kitandani akajifanya kulala tena. Alitaka kuuona mwisho wa Walter.

    Pia alihitaji kuutumia mwanya huu kufanya jambo.

    Akajilaza kwa dakika nyingine sabini.

    Akazisikia purukushani za vyombo hapa na pale.

    Akajua mambo tayari.

    Akaongeza dakika nyingine kumi na tano, akajifanya kushtuka kutoka usingizini.

    Walter akageuka wakatazamana. Lilian akajinyoosha.

    Walter akamkaribia, akamjulia hali.

    “Sasa hivi afadhali.”

    “Nimekuwekea maji bafuni ni vyema uoge kisha uje kula. Nakusubiri.” Walter alizungumza huku akimnyanyua Lilian kutoka kitandani.

    Lilian akalihisi joto la kiume kutoka katika mikono ya Walter.

    Akasulubika katika nafsi. Hakika alikuwa katika hisia kali.

    Hisia ambazo hutokea mara moja moja sana katika maisha yake. Na hii ilikuwa mara ya pili katika miaka yake ishirini na saba tangu azaliwe.

    Kwa mara ya kwanza hisia hizi ziliamshwa na marehemu dokta Mbaule. Sasa ni kijana mtanashati, kijana wa maajabu. Walter.

    Zilikuwa ni hisia zinazoleta raha zaidi kuliko kuumiza.

    Ni hisia ambazo zilitakiwa kufanyiwa kazi kwa namna yoyote ile.

    Lilian akajikongoja hadi bafuni.

    Walter akamuachia ukumbi, yeye akarejea ndani.

    Chakula kilikuwa mezani tayari.



    Walter alikuwa akiwaza machache kichwani mwake.

    Baada ya kula amalizie kurasa kadhaa za kitabu chake kisha ajiondokee.

    Kitu ambacho hakikuwa kichwani mwake ni kuzama katika mapenzi mapema kiasi kile.

    Kiapo chake kwa Naomi kilikuwa kimemfunga haswaa.



    Lilian alirejea na kuingia chumbani, akajivika nguo zake. Akaungana na Walter kwa ajili ya chakula.

    Sifa pekee alizotoa hazikutosha kulithaminisha pishi bora la Walter katika maandishi.

    Hakika lilikuwa pishi bora la kiume.



    *****

    Naomi alijiandalia stafutahi asubuhi ile.

    Alipoweka mezani akakumbuka kuwa, mida kama hiyo Walter alikuwa akimbeba katika mikono yake kutokea cvhumbani hadi anamfikisha katika eneo la kulia chakula. Mchezo huu walifanya zamu kwa zamu.

    Leo walter akimbeba, kesho inakuwa zamu yake kumbeba.

    Naomi akakumbuka jinsi alivyokuwa mbishi ikifika zamu yake.

    Alimuonea sana Walter. Kila mara alisingizia kuwa jana yake ni yeye alimbeba Walter.

    Maskini Walter akawa mpole na kumbeba Naomi.

    Wakimaliza kustafutahi Naomi anamtania Walter kuwa amemdanganya na akadanganyika, Walter anajifanya kushtuka na kukasirika anaanza kumkimbiza Naomi, huku na kule safari yao inaishia chumbani.

    Naomi anajiruisha kitandani, Walter naye anamrukia wanapigana kitoto toto, Naomi analia kwa kuigiza, Walter anambembeleza, mara wanakutanisha ndimi zao, Naomi anaweka ujuzi wake katika kunyonya ndimi, Walter naye anafanya jitihada.

    Mara wanasalia kama walivyozaliwa.

    Kiyoyozi kinashuhudia vita ya miili ya wanandoa hawa.

    Wakimaliza wanaoga pamoja.

    Kisha Walter anaingia ofisini.

    Naomi akipitiwa na mawazo haya, alihisi chumvi chumvi ikitambaa mdomoni.

    Yalikuwa machozi.

    Naomi alikuwa analia.

    Chai ilikuwa hainyweki tena.

    Yuko wapi Walter ampakate hadi sebuleni? Yuko wapi Walter akimbizane naye na mwisho wabembelezane chumbani?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walter hakuwepo tena.

    Mateso mateso mateso kwa Naomi.

    Ile chai akaiona haina maana tena.

    Akaachana nayo na hakutaka kuitazama mara mbili.

    Asingeweza kunywa chai ile akiwa mwenyewe bila Walter.

    Naomi alidhani kuisusia chai ile ambayo aliiandaa mwenyewe lilikuwa suluhisho.

    Akaenda nje.

    Huko ni kama vile aliambiwa tazama kushoto.

    Akakutanisha macho yake na ‘bembea’ akakazia macho eneo lile, ikaja kumbukumbu ya Walter akimsukuma na yeye akibembea kwa furaha.

    Walter mara amtekenye, mara agome kumsukuma mara amfinye. Ilimradi furaha tu.

    Anaikumbuka siku ambayo alianguka kutoka katika bembea ile.

    Walter akambembelezea pale pale chini.

    Mara wakajikuta penzini pale pale chini.

    Walipomaliza wakakimbia mbiombio uchi hadi bafuni.

    Hakika walipokuwa pamoja walikuwa kama watoto wadogo wenye furaha.

    Naomi na Walter walikuwa kama mapacha.

    Sasa pacha mmoja hayupo tena.

    Naomi akajikuta akilia kwa sauti ya juu. Sauti yenye majuto ndani yake.

    Jeraha la hisia lilikuwa linamsulubu, jeraha lilikuwa linatoneshwa na kila alichokiona mbele yake.

    Naomi alikuwa mkosefu lakini yu wapi wa kumwomba msamaha.

    “Rudi Walter mume wangu, rudi nyumbani baba, rudi nateseka mwenzio, bibi popote ulipo peponi, muite Walter. Tazama nitaishi vipi iwapo mzimu wake unanitesa hivi, nitaishi vipi na jeraha hili….bibi? nakuita bibi, sina mwingine wa kunirudishia mume wangu, polisi wameshindwa bibi, niletee mume wangu…bibi najua unanisikia, litazame chozi langu bibi, nitazame moyo wangu bibi, nitalia mpaka lini sasa bibi, bibi kama uliweza kunirudisha kwake na yeye mrudishe kwangu….bibi nakuomba nipo chini ya miguu yako…..” alishindwa kuendelea kuzungumza Naomi akaangua kilio kikubwa.

    Kilio kilichokatizwa na simu yake.

    Naomi akatimua mbio kwenda kutazama, alimini huenda mzimu wa bibi umefanya maajabu na Walter amejirudi.

    Kweli? Akakutana na namba mpya.

    Huenda ni yeye jamani. Aliwaza.

    Akajifuta machozi kisha akapokea.

    “Naongea na Naomi hapo?” sauti ya kiume ilihoji.

    “Ndio mimi ni Naomi, nani mwenzangu?” aliuliza kwa hamu kubwa.

    “Naitwa Kassim, nipo nyumbani kwa dada yako, hali yake ni mbaya, mbaya sana, anakuhitaji mara moja hapa…Naomi tafadhali nakuomba. Fanya upesi.” Sauti ilisihi kilaneno likasikika ipasavyo.

    Naomi akajikuta anakosa la kusema.

    Akiwa bado anamlilia mume wake, sasa anapokea taarifa mbaya zaidi.

    Dada muathirika wa vimelea vya Ukimwi alikuwa hoi.

    UTATA……..









    Naomi akajiona mpumbavu kulialia huku akiwa peke yake.

    Kilio kingesaidia nini wakati dada yake yu maututi??

    Mwanamama akasimama imara, akaifunga milango ya nyumba kisha akalifunga geti kuu.

    Akatoweka akijilazimisha ujasiri huku moyo wake ukiwa dhaifu na uliokufa ganzi.

    Mfululizo wa matukio ya mazishi ya mama yake mzazi ukaanza kujirudia katika kichwa chake, akaikumbuka siku ile nd’o siku ambayo alikuwa yatima rasmi.

    Ni kweli mama yake hakuwa akifanya lolote kuu kwa ajili yake lakini uwepo wake ulikuwa kitu kingine kabisa.

    Msiba wa mama yake ukabadili historia, akabaki kumtegemea dada yake ambaye naye sasa alikuwa katika hali tata. Naomi akafanya dua zote yasitokee ambayo yanapita katika kichwa chake.

    Hakuwa tayari kumzika Naomi.

    Akiwa katika kumfikiria dada yake, mara akalifikia gari.

    Macho yake yakatua katika mlango wa ile gari.

    “NAWA” akakutana na maneno yake yaliyonakshiwa kwa rangi ya dhahabu.

    Akasita akaikumbuka siku ambayo Walter alimnunulia lile gari.

    “NAWA? Nawa nd’o nini?” Naomi akamuuliza Walter huku akiwa anashangaa.

    “NA- Naomi, WA-Walter” Walter akamjibu kwa utulivu.

    Naomi akatokwa machozi ya furaha.

    Sasa Walter hayupo tena??

    Naomi akatokwa na machozi lakini safari hii yalikuwa machozi ya uchungu.

    Uchungu mkubwa.

    Nguvu zikamwishia, akaamini kuwa hatakuwa makini katika barabara. Akahairtisha kutumia lile gari.

    Akaondoka mpaka nje.

    Akachukua taksi, akamuelekeza dereva mahali anapokwenda.

    Wakaondoka zao.

    Safari ya kuelekea nyumbani kwa dada yake maeneo ya Mtoni Kijichi ambapo alikuwa amehamia katika nyumba kubwa.

    Nyumba hii aliitafuta Walter na kodi alilipia yeye.

    Ni upendo wa namna gani alikuwanao mwanaume huyu?

    Labda ni upendo uliopitiliza.



    Mwendo wa dakika ishirini, tayari walikuwa wameifikia njia ya kuelekea nyumbani kwa dada yake. Naomi alikuwa amefanya malipo mapema kabisa. Akaufungua mlango, akaifuata njia ya panya, akiwa amelikamata vyema gauni lake refu la kung’ara.

    Alikuwa anasikitisha hakika, hakueleweka iwapo alikuwa anakimbia ama anatembea. Lakini alikuwa na haraka sana.

    Pochi ndogo mkononi.

    Hatimaye akauona mlango wa kuingia nyumbani kwa dada yake.

    Mazingira yalikuwa tulivu sana, kuku na bata walirandaranda huku na kule. Papapara za Naomi zikaishia pale, nguvu zikamwishia. Miguu ikafa ganzi. Ni kama aliuona umauti mbele yake.

    Hisia za maumivu ambayo huwa yanabebwa na Walter, zikajijenga.

    Hakika Walter huwa anaumia sana..

    Naomi akausikia uchungu bila kupigwa, hisia zilikuwa zinatesa kuliko maumivu ya kupigwa mwilini.

    Hisia alizokuwa analalamika Walter kuwa zinamtesa sasa alizihisi katika mwili wake. Moyo ulikuwa unauma sana.

    Naomi akanyanyua mguu, akazidi kuikaribia nyumba.

    “We Naomi wewe wahiii.” Sauti ya kiume iliita.

    Sura mpya kabisa katika macho ya Naomi. Lakini hakuweza kuuliza.

    Akashtuka, akajikaza zaidi akaufikia mlango.

    Hakuweza kuona mbele vizuri, ukungu ulikuwa umetanda katika macho yake.

    Machozi yalikuwa yamemziba.

    Hatimaye akaweza kufika ndani.

    Jicho lake likapata mwaga baada ya kufutwa machozi.

    Akakutana na kiwiliwili kikiwa kimekakamaa kitandani.

    Alikuwa ni yule dada yake.

    Alikuwa ni Suzi.

    Naomi akajiziba midomo yake. Hakuweza kusema neno.

    Kijana mmoja akamvuta nje.

    Akazungumza naye kuhusu jambo lililotakiwa kufanyika.

    “Kuna daktari wake, sasa fanya kuzungumza naye maana sisi hatujaelewana.”

    “Nani? Ni Dokta wake yule mwanamke.”

    “Eheee huyo huyo, walau atushauri nini cha kufanya maana ni huyo alikuwa anamuhudumia na kumshauri.”

    “Ok.” Alisema Naomi, kisha akaendelea. “Dada bado anaishi mbona kama…….niambieni ukweli…” alilalamika. Machozi yakaanza kumtiririka tena, kamasi nazo zikachukua nafasi.

    Alitia huruma kiuhakika.

    Kijana akakosa la kusema, akamfuta machozi na kumpa uhakika kuwa dada yake alikuwa bado anapumua.

    “Nipe namba ya dokta…” akajitutumua na kuzungumza.

    Upesi yule kijana akachukua kadi na kumkabidhi Naomi.

    Akaingiza namba katika simu yake.

    Simu ikaanza kuita.

    Tayari ilikuwa saa sita mchana.

    *****

    Baridi ya siku hii ilikuwa kali kuliko ya siku nyingine, mwili wake uliota vipele vingi sana kumaanisha kwamba mwili upo katika kupambana na ile baridi.

    Shuka zito liliufunika mwili wake.

    Ilikuwa nadra sana kwa mwanadada huyu kusumbuliwa na baridi la kawaida na lisilokuwa la kawaida la mkoani Mbeya, lakini siku hii hali ilikuwa tofauti sana. Lilian alikuwa kama anaumwa ugonjwa mbaya kabisa wa Malaria.

    Alitamani sana kumweleza jambo Walter ili apate farijiko la nafsi lakini akasita na kujiuliza ataanza vipi.

    Lilian akiwa mtaalamu wa saikolojia na akiolojia aliweza kumsoma vyema kijana Walter. Hapakuwa na dalili yoyote kwa kijana huyu kuwa katika hisia za mapenzi.

    Jambo hili lilimnyanyasa ipasavyo.

    Alikuwa ana kila dalili ya kuzidiwa na hisia hizi. Hisia zilizokichimba kidonda kwa fujo bila huruma na sasa zilikuwa zinazidi kulitanua jeraha.

    Jeraha la hisia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Simu yake ya mkononi ilipounguruma alinyanyuka upesi, akaliacha shuka akasimama wima.

    Alikuwa yu uchi wa mnyama. Akaona alibu alipokutana na kioo mbele yake.

    Akawahi kujiziba matiti yake yanayotamanisha kuendelea kuyatazama.

    Kisha akaanza kucheka mwenyewe alipogundua kuwa katika chumba kile alikuwa peke yake. Akafanya mfano wa tabasamu hafifu.

    Akaitazama cheni nyembamba katika kiuno chake, kisha akaichukua mikono yake na kuyabeba matiti yake kidogo.

    Kabla ya kwenda kuipokea simu, akageuza mgongo, akajitazama. Kisha akaanza kutembea.

    Alikuwa anatikisika vizuri.

    Akafanya kicheko kwa sauti ya juu.

    Alikuwa mrembo haswaa.

    Lakini mrembo asiyekuwa na hisia zozote za mapenzi kwa mtu mwingine isipokuwa watu wawili tu, Marehemu Mbaule na sasa kijana Walter.

    Lilian akaifikia simu, ilikuwa inaita kwa mara ya pili.

    Akafanya msonyo mrefu alipogundua kuwa ni namba mpya.

    Almanusura asipokee.

    Lakini roho wa udanganyifu akamvamia, akamdanganya kuwa huenda ni Walter ametumia namba mpya……upesi akaipokea.

    Akaipokea. Akasikiliza ni nani anaongea.

    “Dokta ni mimi Naomi…..Suzi amezidiwa amekakamaa kitandani…”

    “Naomi yupi…taratibu tafadhali.” Alionya Lilian.

    “Dar..ni Suzi yule muathirika, dada yangu tulikutana Muhimbili…”

    “Suzi amezidiwa? Nini tatizo anaonekana vipi?” aliuliza kwa utulivu.

    Naomi akajieleza kila alichokiona, kisha simu ikakatwa.

    Lilian akiwa yu uchi alikuwa amepagawa, taarifa ile ilimshtua sana, hakutegemea hata kidogo taarifa ile.

    Aliyekuwa katika hali inayofanania na kifo alikuwa ni wajina wake.

    Suzi ambaye ni dada yake Naomi.

    Hali tete.

    Lilian akajisikia uchungu kwa ajili ya roho ile.

    Akafanya upesi kuwasiliana na daktari mwingine ambaye alikuwa anamuamini sana.

    “Tafadhali Joshua naomba unisaidie, mimi nakuja huko kesho tafadhali msaidie.” Alisihi Lilian.

    Akaeleweka.

    Simu ikakatwa, Lilian ama Suzi akiwa yu uchi wa mnyama, akaikwapua kanga akajifunga, akaacha matiti nje.

    Akajikuta katika mtihani mgumu, akawaweka watu wawili katika mzani.

    Kushoto akamuweka Suzi na kulia akamuweka Walter.

    Kuondoka kwake Mbeya kulimaanisha kuwa alikuwa tayari kujiweka mbali na na kijana Walter ambaye hakuelewa hadi wakati ule alikuwa na mipango gani Mbeya.

    Na kung’ang’ania kubaki Mbeya ni kuiruhusu roho ya Suzi ipotee bila jitihada zozote.

    Lilian akakumbuka kuwa alikuwa amechukua pesa nyingi sana kutoka kwa Naomi, hivyo alitakiwa kulipa fadhila.

    Katika mzazi, suzi akaonekana kuwa na uzito zaidi japo hisia juu ya Walter zilikuwa palepale.

    Lilian akaamua kurejea jijini Dar es salaam kujaribu kupigamia uhai wa Suzi.







    Lilian aliamini kuwa kitendo cha kujaribu kumpigia simu Walter kwa ajili ya kumuaga kingemwongezea jeraha jingine ama la yangezuka maumivu mengine. Japo alikuwa amechukua maamuzi ya kusafiri kurejea jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuitazama afya ya Suzi, lakini kiuhakika alikuwa katika mateso makubwa moyoni.

    Lilian akasimama wima akachukua begi lake dogo akapakia jozi tatu za nguo na viatu jozi mbili.

    Vilimtosha kabisa kwa safari ile. Isitoshe alikuwa na nguo zake nyingi tu jijini Dar es salaam.

    Akiwa katika kujiandaa na safari mara simu yake ikaita.

    Sasa alikuwa ni Walter.

    Tofauti na awali alipotamani sana kupata simu kutoka kwa Walter, sasa alikuwa anaogopa kuipokea. Hakujua Walter anataka kumwambia nini.

    Akaipokea huku hofu ikiishi jirani naye.

    “Lilian…..” sauti tulivu ya Walter iliita.

    “Yes Walter….” Alijibu huku akiizuia hofu yake kumchukua kwa kiasi kikubwa.

    “Yaani sijui nikwambieje….anyway….aah tutaongea…tutaongea…” alijiumauma Walter.

    Mara akakata simu.

    Lilian akashusha pumzi zake kwa nguvu sana. Ni kama alikuwa amezungumza na kitu cha kutisha sana.

    Kitu hiki kilikuwa ni Walter. Ilistaajabisha.



    Lilian akaanza kuhisi kuwa huenda Walter naye ameanza kuingia katika hisia ambazo kwake zilikuwa zinamnyanyasa sana.

    Hisia za mapenzi. Lakini ataanza vipi kumuuliza juu ya jambo hilo?

    Huu ukawa mtihani mkubwa sana.

    Akapuuzia mawazo yake, akaendelea kuiandaa safari yake.



    Kitanda kikamuita akajiegesha na kupitiwa na usingizi.

    Alikuja kushtuka majira ya saa moja. Bado kijua kilikuwa kinamulika.

    Laiti kama kwa muda huo ingekuwa katika jiji la Mwanza, ama Dar es salaam isiyokuwa na umeme basi giza lingekuwa limetanda.

    Uzembe wa usingizi ukamfanya akae kitandani akishangaa tu chumbani mwake.

    Hadi alipooga ndipo akili ilifanya kazi vizuri.

    Akaikumbuka safari ambayo inamkabili.

    Akamkumbuka na Walter ambaye atamuacha nyuma katika mji huu.

    Lilian akapata namna ya kujiweka karibu na kijana Walter.

    Akili yake ikafyatuka baada ya kukumbuka kuwa mtunzi chipukizi na mahiri katika fani ya uandishi wa hadithi, mtunzi ambaye alimsoma mara kadhaa magazetini, mtunzi mwenye kila ladha ya mkongwe Beka Mfaume ama Hussein Tuwa. Kijana aliyejulikana kwa jina la Christian Boniphace, alikuwa ameachia kitabu chake cha kwanza, kitabu kikienda kwa jina la ‘CHOKORAA’.

    Walter alikuwa mtumwa wa riwaya.

    Lilian akachukua simu yake akampigia muuza magazeti katika kituo cha mabasi makubwa.

    Akamjulisha kuwa amesaliwa na nakala mbili za kitabu cha CHOKORAA, Lilian akamsihi ampitishie nakala hizo.

    Muuza magazeti akafanya kama alivyoagizwa.

    Majira ya saa mbili usiku vitabu viwili vya kufanana vilikuwa katika himaya ya Lilian.

    Upesi Lilian akachukua simu yake akaunda ujumbe wa maandishi.

    Akautuma kwa Walter.

    “Kesho asubuhi njoo nyumbani, utakuta zawadi yako. Ukishaipata nitafute katika simu nikueleze jambo.” Ujumbe ulisomeka vile.



    Lilian akalala baada ya kuhakikisha ujumbe umesomwa.



    Asubuhi alikuwa katika basi la ABOOD, tayari kwa safari ya kuelekea jijini Dar es salaam.



    ****

    Walter alikosa kabisa usingizi, ni kama alijisikia yu katika dhambi kubwa. Dhambi ya kuhukumu.

    Walter alikuwa amehukumu hata wasiotakiwa kuhukumiwa.

    Katika chumba cha hoteli ambayo alikuwa amefikia palikuwa na luninga. Siku hiyo ambayo hakwenda kumtembelea Lilian kutokana na kutokuwa na jipya la kuzungumza naye alijikita katika kutazama filamu.

    Ilikuwa filamu iliyokuwa imeigizwa magharibi mwa bara la Afrika na maudhui yake makubwa yalikuwa juu ya janga zima la UKIMWI.

    Walter alijikuta akimkumbuka Suzi, yule shemeji yake wa pekee ambaye alikuwa muathirika wa gonjwa hilo.

    Walter alikumbuka jinsi binti huyo alivyokuwa anafarijika kwa kuwa karibu yake mara kwa mara, lakini cha kusikitisha, kesi ya Naomi na marehemu Maureen imemfanya amuhukumu hata yeye pasi na makosa.

    Sauti ya Suzi ilimlilia masikioni, ilimlaumu na kuna wakati ilisema maneno kama ya kulaani. Walter alizima luninga na kujikita katika kumwazia Suzi.

    Makosa ya Naomi, Suzi anahusika vipi? Alijiuliza.

    Mwisho akafikia uamuzi wa kumfikishia salamu za aina yoyote Suzi.

    Namba zake za simu alikuwa amezishika ipasavyo na pia zilikuwa katika kitabu chake cha kumbukumbu.

    Akafikiria kuongea naye moja kwa moja, lakini akaona si jambo la busara, kwani angejiweka katika mazingira ya kumtangazia Naomi mahali ambapo yupo.

    Akaamua kumtumia Lilian, rafiki yake pekee wa jijini Mbeya.

    Usiku huo akaamua kumpigia simu Lilian ili aweze kumweleza.

    Simu ikapokelewa na sauti tulivu ya Lilian.

    Mara ujasiri ukayeyuka baada ya kuisikia sauti yake, akakosa pa kuanzia akajiuma uma. Mara akajikuta anakata simu.

    “Ni heri kumweleza ana kwa ana….” Alijisemea Walter huku akisikilizia mapigo yake ya moyo yalivyo katika kiwango cha juu.

    Akaiweka simu yake kando na kujilaza akiulazimisha usingizi.

    Kabla hajalala, ujumbe ukaingia katika simu yake, mtumaji akiwa ni LIlian.

    Ujumbe huu ukamfanya atabasamu.

    “Afadhali nimepata cha kunipeleka kwake….” Walter alijisemea.

    Sasa aliweza kuupata usingizi.

    Usingizi uliombeba hadi majira ya saa mbili asubuhi.

    Akajiandaa, akaingia mgahawani akastafutahi. Kisha bila kumpigia simu Lilian akaanza safari ya kwenda nyumbani kwa Lilian.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati Walter akifurahia safari yake ya kwenda kuonana na Lilian, binti huyu wa kinyakyusa ambaye anamiliki shahada ya udaktari katika makablasha yake alikuwa ndani ya basi wakifanya jitihada za kuutafuta mji wa Makambako, kisha waupite na kuendelea kuitafuta, Mafinga, Iringa, Milima ya Kitonga, Mbuga za Mikumi kisha watalii Morogoro kabla ya kuingia katika jiji la Dar es salaam.

    Lilian alikuwa safarini.



    ****



    Walter alishtushwa na ukimya uliokuwa umetanda katika nyumba ya Lilian, haikuwa kawaida yake kutulia kiasi hicho.

    Ilikuwa aidha usikike mziki kutoka katika redio ama asikike akiimba yeye mwenyewe.

    Leo hii palikuwa kimya.

    Alipokifikia kitasa kilikuwa kimefungwa.

    Akapapasa mahali ambapo Lilian alimuelekeza huwa zinawekwa funguo. Akaupata.

    Akafungua mlango akitegemea kukutana na Lilian ndani ya kile chumba lakini zaidi ya picha zake mbili tatu hakuambulia kitu kingine.

    Kitanda kilichotandikwa vyema na shuka nyeupe kilikuwa na doa fulani ambalo halikuwa na mvuto sana, doa hili lilifanania na picha ya mtu ambaye alikuwa analia.

    Doa hili liliandikwa neno moja tu ‘CHOKORAA’.

    “Au nd’o zawadi hii…..” akajisemea kwa sauti ya chini.

    Alipochukua lile doa, lilikuwa ni kitabu cha riwaya.

    “Christian ametoa kitabu?” alijiuliza.

    Akaketi. Kabla ya kukisoma akampigia simu Lilian.

    Simu ikapokelewa.

    “Walter…..” Lilian akaita.

    “Lilia, nipo chumbani kwako upo wapi?” aliuliza Walter.

    “Walter nisamehe, nimesafiri kidogo kuna mdogo wangu anaumwa sana, nimekuja kumuona. Nilishindwa kukuaga kwa sababu shangazi alinishtukiza. Lakini nimekuachia riwaya hiyo….itakuburudisha hakika.” Alizungumza Lilian.

    Walter akampa pole, wakaendelea na mazungumzo mengine.

    “Nikifika nitakueleza ni lini nitarudi.” Lilian alimalizia.

    Simu ikakakatwa.



    Walter akajiweka sawa katika kochi dogo pembeni ya kitanda, akafanya kosa kubwa sana kuanza kuusoma utangulizi wa kitabu kile.

    Utangulizi ukamkamata, mara ukurasa wa kwanza.

    Kimya kikubwa hadi saa kumi na mbili jioni. Kitabu kikamalizika.

    Walter alijikuta katika ulimwengu mwingine baada ya kuimaliza riwaya ile. Kwanza alifanya tafakari mbili tatu, tafakari kuu ikawa juu ya ugonjwa wa Ukimwi ambao umeondoka na wahusika kadhaa katika riwaya.

    Walter akamkumbuka Suzi tena. Suzi alikuwa anamuhitaji sana kimawazo na msaada wa kipesa inapobidi.

    Lakini Suzi alikuwa jijini Dar es salaam.

    Hisia za uonevu zikamshambulia sana. Akajikuta analia.

    Alilia kwa sababu alikuwa amemuonea Suzi pasipo makosa yoyote.

    Lilian wa kumfikishia ujumbe naye hakuwepo.

    Kwa mara ya nyingine tangu afike katika jiji la Mbeya, Walter akajikuta akiutambua umuhimu wa Lilian kwa kiasi kikubwa. Kitabu cha riwaya alichokuwa anasoma hakikuwa na maana tena maana alikwisha kimaliza tayari, ukiwa ukaanza kumtawala.

    Akayakumbuka ambayo hakutaka kuyakumbuka.

    Walter akamkumbuka Naomi na maswahibu yake.

    Kichwa kikaanza kumuuma tena.

    Dawa yake pekee ilikuwa ni kuwa karibu na Lilian, aisikie sauti yake tulivu na midomo yake isiyoisha kutema maneno yanayofurahisha kusikiliza.

    Lilian hakuwa pale.

    Walter akajikuta katika msukumo wa ajabu, msukumo wa kumweleza jambo Lilian. Alihitaji binti huyu atambue kitu ambacho hakuwa akikifahamu hapo awali.

    Akaichukua simu yake, akaongozwa na hisia, sio hisia za mapenzi lakini zilikuwa hisia za namna ya pekee.

    Akauandika ujumbe mfupi sana kwa herufi kubwa.

    “LILIAN WEWE NI KILA KITU KWANGU, SIJUI NITAISHI VIPI BILA UWEPO WAKO.”

    Ujumbe ukatumwa kwa Lilian.





    Ujumbe huu ulimkuta Lilian ambaye katika jopo hili alitambulishwa kwa heshima yake ya udaktari. Walimuita Dokta Suzi.

    Alikuwa ndani ya gari ya Naomi, ileile yenye alama NAWA mlangoni.

    Akaufungua ujumbe ule.

    Tabasamu pana likajitokeza usoni mwake, kisha machozi yakaanza kumtoka.

    Naomi akapagawa, alidhani daktari alikuwa anamlilia mgonjwa, ama alikuwa amekata tamaa juu ya kupona kwake.

    “Dokta…dadangu atapona kweli, tafadhali dokta….eeh ..nambie.” Naomi alihamaki.

    Lilian akamtazama, kisha akajaribu tena kutabasamu.

    “Ananipenda pia…” Lilian alijikuta akimjibu Naomi jambo ambalo hakutarajia.

    “Nani?” Naomi akamuuliza huku akiwa ametaharuki bado.

    “Ahh…aah basi tu…” alijiumauma Lilian.

    Naomi, hakujua kuwa daktari huyu yu katika dimbwi la hisia, hisia kali sana juu ya mume wake, na aliyeutuma ujumbe ule wa kumtoa machozi na kumfanya daktari yule ajikute anaropoka alikuwa ni Walter, mume wake kipenzi.

    “Ni nini daktari…” Naomi alikuwa hajaridhika.

    “Ni mume wangu, ameniambia neno zuri, limenikumbusha mbali.” Hatimaye Lilian alidanganya.

    Kama Dokta Suzi alidhani uongo huo ni mzuri basi alikuwa amekosea kabisa.

    Neno ‘mume wangu’ lilikimbia mbiombio hadi katika moyo wa Naomi, likafukunyua huku na kule likakipata kidonda kibichi cha Naomi, likaanza kukikwangua. Maumivu mapya yakaanza.

    Naomi akamkumbuka mume wake, akaitazama pete yake ya ndoa.

    Maumivu ya kuishi bila Walter yakarejea.

    Naomi akajikaza sana asiweze kutokwa machozi, lakini jitihada hazikuweza kuyazidi machungu.

    Machozi yakaanza kumtoka.

    Daktari akatambua kuwa Naomi bado hajamwamini.

    Hakutaka kuendeleza mjadala. Akatulia kimya.

    Dereva akaendelea kuendesha hadi walipoifikia hospitali ya mtu binafsi maeneo ya Mtoni Mtongani.

    Liliani akatelemka. Hatua kwa hatua hadi katika chumba alichokuwa amelazwa Suzi.

    Daktari akaingia kazini baada ya utaratibu maalum kufuatwa ikiwemo utambulisho maalumu kwa daktari mkuu wa hospitali hiyo.

    Lilian alimkuta Suzi akiwa amerejewa na fahamu lakini hakuwa amesema neno lolote lile na mtu yeyote.

    Walipogonganisha macho yao, Suzi akatabasamu.

    Lilian naye akatabasamu. Hakika walikuwa wameivana wawili hawa.

    Lily akajisogeza na kuketi katika kitanda alichokuwa amelala Suzi. Akampigapiga shavuni kidogo. Suzi akachangamka, japo alikuwa amedhoofika lakini alionekana kuufurahia ujio ule.

    Daktari akafanya yote ayajuaayo kuiteka akili ya Suzi.

    Akamrejesha katika hali ya unafuu.

    Uwezo wa daktari Suzi kucheza na akili ya mwanadamu ulimpa chati za juu sana akiwa daktari mdogo, ni madaktari wachache wanaopewa uwezo huu wa aina yake kisaikolojia na kiakiolojia.

    Lilian (Dokta Suzi) alikuwanavyo.

    Siku iliyofuata, Suzi aliweza kukaa, akala chakula pamoja na daktari.

    Mwisho aliweza kusema maneno mawili matatu.

    Lilian alicheza naye na hakukasilishwa na jambo lolote lililofanywa na mgonjwa wake, aliwatambua vyema waathirika wa virusi vya Ukimwi walivyo.

    Hivyo Suzi hakumpa tabu, maneno pekee kutoka katika kinywa chake yaliweza kumtibu Suzi na kumpa unafuu sana.

    Licha ya haya yote aliyoweza kuyafanya, daktari huyu alikosa daktari wa kumtibu ugonjwa wake wa maajabu.

    Ugonjwa wa hisia za mapenzi.

    Wale madaktari bingwa walikuwa wameshindwa kabisa.

    Alikuwepo daktari mmoja tu aliyebakia.

    Alienda kwa jina la Walter.

    Lakini Daktari huyo hakujua kama ana hadhi kubwa kiasi hicho.



    Siku mbili baadaye, Suzi akiwa katika hali ya kawaida japo alikuwa katika kitanda bado, Lilian alimchukua Naomi kando kwa ajili ya mazungumzo.

    Mazungumzo kuhusiana na afya ya Suzi.

    “Naomi….Guda ni nani? Ama unalifahamu jina hili?” aliuliza Lilian.

    Naomi alishtuka kwanza kusikia jina lile, jina ambalo alipendelea kumuita mume wake Walter, jina lililotambuliwa na watu wachache sana. Alikodoa macho yake. Alikuwa kama zezeta.

    Lily akatambua kuwa binti ameshtuka na hakutegemea swali kama lile.

    Moyo wake ukatabasamu maana alichokiwaza aliamini asa kinaenda kupata majibu.

    “Guda?” Naomi aliuliza kibwegebwege kana kwamba hakusikia vizuri.

    “Ndio..Guda..”

    “Dokta….ninamfahamu, umemuona wapi kwani?”

    “Nimeuliza tu, unamfahamu vipi?”

    “Ni mume wangu wa ndoa…”

    Sasa ikawa zamu ya Lilian kushtuka, hakutegemea jibu lile. Naye akaduwaa.

    Lazima aduwae, hakutegemea kama mume wa Naomi anaweza kuwa amenata katika akili ya dada yake ambaye ni mgonjwa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Suzi alikuwa akishtuka usiku na kumtaja Guda, na hata katika mang’amu ng’amu ya usingizi alikuwa anamtaja Guda.

    Kutokana na maelezo ya Naomi, Guda ni shemeji yake Suzi.

    Kwa uzoefu wa daktari, alimini palikuwepo na kitu hapo katikati.

    Guda alikuwa na mahusiano ya karibu sana na Suzi nd’o maana akawa anajia katika ndoto na mauzauza ya usingizi.

    Ukaribu wa ushemeji unaweza kusababisha haya? Hapana. Alijipatia jibu.

    “Daktari, Guda amefanya nini?” Naomi alimuuliza Lilian aliyekuwa bado katika mshangao.

    “Umesema ni mume wako eeeh.” Alijaribu kujirejesha katika hali ya kawaida.

    “Ndio daktari ni mume wangu, anakaribia mwezi hayupo nyumbani sasa. Amepotea katika mazingira ya kutatanisha” Alikuwa ametaharuki Naomi wakati anazungumza haya..

    Hili nalo likawa jipya katika kichwa cha Lilian.

    Mume ana mwezi mzima haonekani nyumbani, hakuna taarifa.

    Shemeji mtu anapatwa na maluweluwe juu yake.

    Maajabu haya.

    Ina maana shemeji ana mawasiliano na mume aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha. Mwezi mzima.

    Kazi mpya kabisa.



    ***JERAHA LA HISIA………NANI ATAFANIKIWA KUPONA JERAHA KABLA YA MWENZAKE??

    **WALTER ana jeraha, NAOMI anaugulia jeraha, LILIAN naye yu katika jeraha......



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog