Search This Blog

Wednesday, 1 June 2022

MAJAALIWA - 3

 







    Simulizi : Majaaliwa

    Sehemu Ya Tatu (3)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa mshangao Zainab alimuona Dallas akinyanyuka kutoka pale alipokuwa amekaa, akasogea kwenye ukuta uliokuwa na picha zile alizoziulizia, na akazidi kuzikodolea macho badala ya kujibu swali aliloulizwa.

    Zainabu alirudia swali lake kwa msisitizo: "Bwana Dallas, ninakuuliza una shida gani hapa nyumbani kwetu?"

    Dallas aligeuka na kumuangalia, "Shida yangu ni Amani. Nilimuahidi kuwa nitamtembelea naye akaniruhusu kuwa ninaweza kuja wakati wowote hapa nyumbani, sijui nimemkuta?"

    Zainabu alimjibu kwa haraka haraka: "Nasikitika kaka Amani hayupo nyumbani…ametoka. Kwani ulimfahamisha kuwa utakuja saa hizi?”

    “Hapana…kusema kweli sikumpa ahadi ya siku wala saa.Nilisema kuwa nitakuja siku yoyote tu.”

    “Basi ndio hivyo…kaka Amani hayupo!”

    Dallas alirudia tena kuziangalia zile picha, kisha akamgeukia Zainab na kumuuliza: "Samahani dada, hivi wewe na Amani ni ndugu baba mmoja, mama mmoja?"

    Zainab hakupendezwa na maswali ya aina yoyote kutoka kwa Dallas, hivyo alijibu kwa kebehi kwa kumuuliza: "Kwani vipi bwana Dallas? Mbona maswali yamekuwa mengi? Uhusiano wangu mimi na kaka Amani, unautakia nini? Au na yeye unataka umtege kama ulivyomtega dokta lmu?”

    Dallas aliinamisha kichwa na kukitikisa kwa kukataa huku akisema:

    "Hapana,hapana dada…nakuomba unijibu swali moja tu dada, tafadhali!"

    Zainabu alimtulizia macho na kumuangalia, naye Dallas aliendelea kuuliza: "Hii picha hii…!" Alinyooshea kidole chake cha shahada ile ya mtoto aliyekaa juu ya kimeza: "Picha hii kweli ni ya Amani?"

    Zainabu alishangazwa na mabadiliko ya tabia yake iliyokuwa ikibadilika na kuonekana ni mwenye uchungu na huzuni nyingi. Alimjibu Dallas kwa kumwambia: "Nimekwisha kukuambia kuwa hiyo ni picha ya kaka Amani alipokuwa mdogo, sasa nini tena?"

    Dallas aligeuka akaitazama tena ile picha kwa muda, kisha akageuka na kuelekea mlangoni kwa haraka huku akisema: "Kwaheri dada, nisalimie sana Amani!"

    Alitoka na kwenda zake.



    *****

    Wakati Amani anafika mskitini waumini walikuwa wanatoka baada ya kumaliza swala ya alasiri. Aliegesha gari lake sehemu ya kuegeshea magari, kisha akaenda kukaa kwenye baraza ya nyuma iliyokuwa mkabala na msikiti. Alipoona kuwa msikiti karibuni mtupu isipokuwa kwa watu wachache tu waliobaki kwa kuendelea na ibada zao au waliochelewa swala ya jamaa, alimuuliza mmoja wa watu waliotoka msikitini ambaye alikuja na kukaa juu ya baraza ile ile aliyokalia yeye baada ya kusalimiana naye, "Samahani bwana!"

    "Bila samahani kijana!"

    "Naomba nikuulize ustadh!"

    "Sawa niulize tu muungwana."

    "Nina haja na bwana Majaliwa, sijui atakuwa bado anaswali?"

    "Ahaa, Mzee Majaliwa! Subiri nikakuitie!"

    Yule bwana akaondoka na akaenda kuingia msikitini tena, baada ya dakika tano, alitokeza tena akiwa ameongozana na mzee Majaliwa. Kuona vile, Amani alisimama na wazee wale walipofika karibu yake, alinyoosha mkono na kumpa kiganja mzee Majaliwa huku akisema: "Assalaam Alaykum?"

    "Waalaykum salaam! Karibu kijana."

    "Ahsante mzee…"

    Amani alijitambulisha kwa mzee Majaliwa: "Samahani mzee kwa kuchukua wakati wako, mimi ninaitwa Amani Mirambo, ni kaka yake Zainabu, mchumba wa dokta lmu. Vile vile mimi ndiye wakili ninayemtetea Dokta lmu katika kesi yake inayomkabili.Niliwahi kukuona siku moja wakati sisi tunatoka kumuangalia Dokta lmu mahabusu na wewe unaingia, lakini hatukuwahi kutambuana."

    Mzee Majaliwa alikubali kwa kichwa, kisha akaashiria wakae pale barazani, wakaketi.

    "Naam, bwana Amani. Mimi nadhani unanifahamu."

    "Ndio nimeelezwa kila kitu kuhusu wewe na Dokta Imu."

    Mzee Majaliwa alitikisa kichwa cha masikitiko na kusema: "Masikini, kijana mwema kama yule, ni masikitiko makubwa kufikwa na mitihani kama iliyomfika! Lakini baba haya yote ni majaaliwa yake Mungu, Mwenyezi-Mungu atamuokoa lnshaallah!"

    "Aamina!” Amani aliitikia kwa sautiyachini.

    "Haya bwana mdogo, lete habari. Bila shaka kuna jambo na ndio maana ukanijia mpaka huku niliko…"

    "Ni kweli baba, lipo jambo ambalo linahitaji msaada wako!"

    "Lipi hilo?" CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Linahusu kesi ya Dokta Imu!"

    Mzee Majaliwa alitulia baada ya kusikia hivi na kuonekana mwenye kufikiri. Kisha akarudisha pumzi na kumuuliza Amani kwa mkato: "Kwema?"

    "Ni kwema tu mzee usiwe na wasiwasi!"

    "Haya sema ni msaada gani unaohitajika kutoka kwangu?"

    Amani alitabasamu kidogo halafu akajiweka sawa na kuanza kusema: "Mzee Majaliwa kama utakumbuka vizuri siku aliyofikwa na maafa ya kukamatwa Dokta Imu na kutiwa kwenye tuhuma, ilikuwa usiku wa siku ya Jumamosi!"

    “Ndio nakumbuka vizuri, sababu siku iliyofuata ambayo ni Jumapili, ilikuwa ndio siku ya mimi na wenzangu tuje nyumbani kwenu kwa ajili ya habari ya ndoa ya Dokta lmu na mdogo wako Zainab!"

    Amani alichangamka na kukubali kwa kichwa kuona mzee ana kumbukumbu nzuri, na akasema: "Hasa,mzee unakumbuka vizur. Je unakumbuka ni majira gani aliyokuja Dokta Imu kukuona wewe na mkazungumzia habari za mambo ya ndoa yake?"

    Bila kubabaika mzee Majaliwa alijibu: "Ni siku hiyo hiyo ya Jumamosi, baada ya swala ya adhuhuri, kwa hiyo itakuwa ni majira ya mchana!"

    Amani aliongezea kwa kusema: "Kati ya saba na nusu hivi na saa nane?"

    "Ndio, ulikuwa ni wakati huo huo wa saa saba na nusu mpaka saa nane na nusu hivi, ndipo tulipoagana mimi na yeye!"

    Amani alitulia kidogo baada ya kusikia haya kutoka kwa mzee Majaliwa, kisha

    akamuangalia mzee huyo na kumwambia kwa sauti ya taratibu na ya chini: "Basi mzee wakati huo huo, kwa ushahidi unaoaminika, ndio wakati marehemu Mwanamtama ambaye amefariki kwa sababu ya kutolewa mimba, alipokuwa anafanyiwa shughuli hizo za kutolewa mimba. Sasa mzee hebu angalia, itakuwaje Dokta lmu awe anazungumza na wewe hapo mlipo na wakati huo huo awe anamfanyia mtu operesheni ya kumtoa mimba?"

    Mzee Majaliwa alikataa kwa kichwa na kusema: "Haiwezekani!"

    "Basi hiyo ndiyo inavyosemekana kuwa wakati mmoja huo huo dokta lmu ameweza kufanya shughuli mbili, tena mahali mbali mbali!"

    Baada ya kusema haya Amani alitulia na kumpa nafasi mzee Majaliwa kuyatafakari aliyoyasema. Mzee naye alisema baada ya kuwaza kwa dakika kadhaa: "Kwa hiyo hivyo ndivyo wanavyosema kumsingizia Dokta lmu?"

    "Eeeh, ndiyo hivyo mzee!"

    "Sasa wewe kama wakili wa dokta lmu unasema nini?"

    "Mimi ninalosema mzee wangu ni kukuuliza."

    "Kuniuliza vipi? Yaani swali gani?"

    “Je unaweza kumsaidia au kumtetea Dokta lmu?"

    "Ndio ninaweza, iwapo nitahitajika kufanya hivyo na pakiwa pana ukweli ni lazima usemwe!"

    Amani alimfikisha mzee Majaliwa pale alipotaka afike, kwa hiyo alimueleza, "lli umsaidie Dokta Imu kinachotakiwa ni wewe kuthibitisha kuwa siku ile ya Jumamosi wakati wa saa saba na nusu mpaka saa nane na nusu wewe na dokta lmu mlikuwa pamoja hapa

    eneo la msikitini. Ina maana mzee Majaliwa, wewe uwe shahidi wa dokta Imu katika kesi yake!"

    Mzee Majaliwa aliinama na kutazama chini pasipo kutoa jibu kwa haraka. Amani kuona vile aliendelea kusema: "Nimeambiwa kuwa hupendi kuonekana wala kufika mahakamani…vile vile umemuomba Dokta lmu akusamehe kwa hilo na kusema kuwa hutafika mahakamani kabisa. Mzee wangu, mimi pamoja na Dokta lmu tunauheshimu uamuzi wako, lakini tunakuomba kwa jambo hili la ushahidi, uhudhurie mahakamani

    japo mara moja tu. Maisha ya dokta Imu yanategemea na kuhitaji ushahidi wako, ambao naamini ni wakweli!”

    Mzee Majaliwa hakujibu kitu.

    “Unasemaje mzee Majaliwa?" Amani aliulizia tena.

    Kimya kilitawala eneo zima walilokuwa wamekaa. Kila mmoja wao akiwa amenyamaza kimya.





    Baadaye, mzee Majaliwa alimwambia Amani kwa sauti ya chini: "Bwana mdogo, lisilo na budi hutendwa. Ingawa ni azimio langu kutofika au kutohudhuria mahakamani kwa kusikiliza kesi, lakini papo hapo ni wajibu wangu kumsaidia dokta lmu ambaye ni rafiki yangu, katika kusema ukweli. Kwa hiyo basi ninaahidi mbele ya Mungu na mbele yako, kuwa nitafika mahakamani Mungu akinijaalia kwa kuja kumtolea lmu ushahidi!"

    Amani alitoa tabasamu kubwa la ushindi wa kumfanya mzee Majaliwa akubali, huku akisema: "lnshaallah!"

    "Sasa niambie ni lini nitahitajika huko mahakamani?"

    Amani alimtajia siku na tarehe ya kusikilizwa tena kesi ya dokta Imu na akamuahidi kuwa atakwenda kumchukua itakapofika siku hiyo.

    Wakaagana.



    *****

    Amani anaporudi nyumbani kwao, anapewa taarifa na Zainab kuwa Dallas alifika pale kwao. Alihamaki kidogo na kisha akauliza: "Amekuja kufuata nini hapa?”

    "Anavyodai yeye ni kwamba amekuja kukuona wewe, na kuwa mlikwisha agana!"

    "Alisema nini baada ya kunikosa?

    "Hakusema chochote, aliiangalia sana ile picha yako ya ulipokuwa mdogo, kisha akaenda zake."

    Amani alipotajiwa habari za picha, mara alikumbuka kitu na akamwambia Zainab, "Kweli Nimekumbuka, wacha niende kwa akina Fatima nikaonane na Zaituni kuhusu picha nilizomuagizia."

    Alitoka akaenda Kijitonyama kwa kina Fatima. Alipofika huko aliwakuta wote Fatima na Zaituni wapo nyumbani lakini taarifa aliyoipata si ya kupendeza. Alijulishwa na Zaituni kwamba mpaka wakati huo alikuwa bado hajafanikiwa kuzipata zile picha za marehemu Mwanamtama alizopiga na Dokta lmu kutokana na hali halisi iliyojitokeza ambayo kwamba hakuna picha hata moja ya marehemu Mwanamtama nyumbani kwao, licha ya hizo alizopiga na Dokta lmu, hata zile alizowahi kupiga na jamaa zake wengine au za peke yake pia hazikuonekana. Hata hivyo Zaituni alimwambia shemeji yake mtarajiwa, "Shemeji Amani usitie wasiwasi, bado yapo matumaini. Kuna msichana mmoja amenihakikishia kuwa yeye anazo picha za Mwanamtama na Dokta lmu, ameniahidi atanipatia picha hizo."

    Amani alitulia kidogo kabla hajaendelea kusema, kisha akakubaliana na Zaituni kwa kumwambia, "Sawa Zaituni, wewe endelea kuzisaka hizo picha... ingawa ingekuwa bora sana kama zingekuwa zimepatikana kwa sasa, kwa sababu tarehe ya kusikilizwa kesi tena ni kesho kutwa."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ******

    Siku ya kesi kusikilizwa tena ilifika. Jambo la kwanza alilofanya Amani siku hiyo ni kwenda kumfuata mzee Majaliwa na kumfikisha mahakamani. Alipofika hapo kwenye ukumbi wa mahakama, alimtafutia pahali pazuri akamuweka.

    "Kaa hapa mzee, sikiliza kesi yetu vizuri wakati itakapokuwa inazungumzwa. Nawe utaitwa wakati utakapohitajika kutoa ushahidi wako. Kazi itakuwa ni kusema kweli tu mzee, siku, tarehe na mahali ulipokuwa wewe na Dokta lmu... basi!" Alimwambia na kumuacha hapo alipomuweka.

    Wakati ulifika wa kesi ya Dokta lmu kusikilizwa, kila mtu aliyekuja kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo alikaa sawa kwa kutoa macho na kutega masikio. Hakimu aliamuru shahidi namba moja aitwe aingie kizimbani. Dallas alipanda kizimbani. Alifahamishwa kuwa ushahidi wake bado unaendelea kisha akasomewa namna alivyotoa ushahidi wake na jinsi wakili wa serikali upande wa mashtaka Zablon Mkuki alivyo ukubali na kuunga mkono ushahidi huo. Vile vile akasomewa ni jinsi gani wakili mtetezi ndugu Amani alivyoupinga ushahidi huo na hatimae kumtuhumu yeye Dallas kuwa ndiye muhusika aliyesababisha kifo cha Mwanamtama na anastahili kutiwa ndani.

    Baada ya hapo Dallas alitakiwa atoe maelezo kama anayo, ya kukubali au kukataa shutuma za wakili Amani. Lakini kabla Dallas hajasema neno lolote, Amani alimuomba hakimu amuachie yeye Amani aendelee na kumuhoji Dallas kwanza kabla yeye Dallas hajasema neno. Ombi la Amanl lilikubaliwa naye alianza kumuuliza Dallas kuhusu ile 'business card’ kwa kusema, “Ndugu Dallas…ni matumaini yangu kuwa umekuja na ile 'business card’, au sio?"

    Dallas alitulia tuli pale alipokuwa amesimama akiwa anamuangalia Amani tu, huku akitabasamu kama vile hasikii yale aliyokuwa anaulizwa, hakujibu kitu. Amani aliendelea kumuuliza tena swali lile lile, na Dallas naye aliendelea kumuangalia tu kwa jicho la kumuhusudu. Hakimu aliingilia kati kwa kusema "Ndugu Dallas, jibu swali unaloulizwa na wakili!"

    Dallas bila kuondoa macho yake kutoka kwa Amani alijibu kwa sauti ya chini na ya upole "Hapana sikuja na 'business card'!"

    Amani alimgeukia Hakimu na kumwambia, "Mheshimiwa Hakimu, huyu mtu ni muongo na naiomba mahakama yako tukufu isikubali ushahidi wake, kwani huyu Dallas ni tapeli wa taifa kwa ushahidi kuwa kila mji anaokwenda katika nchi, hujiita kwa jina jingine. Hapa Dar es salaam, anajiita Dallas, lakini Arusha anajulikana kwa jina la Abdi, wakati huo huo mtu huyu huyu mmoja anapokuwa Mwanza anajiita Abdul, lakini anajulikana kwa jina la Dulla anapokuwa mjini Tanga!"

    Mwanasheria Zablon Mkuki alisimama na kumtetea Dallas kwa kuiambia mahakama: "Mheshimiwa hakimu, naona upaande wa utetezi umeishiwa na hoja. Swali la ‘business

    card' lilikwisha. Na hili la majina sidhani kama linahusika katika kesi hii!"

    Amani aliomba aruhusiwe kutetea hoja yake, na aliporuhusiwa alisema kuiambia mahakama, "Mheshimiwa hakimu, maana ya kusema na kutaja majina mbalimbali ya ndugu Dallas, ambayo anayatumia kila mji na jina lake, ni kutaka kuonesha ni jinsi gani Dallas alivyo muongo, ni jinsi gani alivyo tapeli. Kwa hiyo mtu yeyote ambaye hana kauli ya msimamo, hawezi kuwa shahidi na akaaminiwa. Dallas hakuiambia kweli mahakama, Dallas ni yeye mwenyewe ndiye muhusika mkuu wa kifo cha Mwanamtama. Dallas hamjui kabisa Dokta lmu, na wala hana udugu wa damu na marehemu Mwanamtama! Uhusiano wao ni wa mvulana na msichana waliokuwa wakijihusisha na ngono. Ningeomba mahakama yako tukufu, imuite ndugu yeyote au wazazi wa marehemu waje wamtambue huyu Dallas. Huyu anaiambia mahakama uongo. Kwa hiyo Mheshimiwa, hayo majina yake mengi yanadhihirisha uongo wake! "



    *****

    Dallas wakati wote huu alikuwa akitabasamu tu, mwishowe alipomuona Amani amemaliza hoja zake kwa wakati huo, alinyoosha mkono juu kuashiria aruhusiwe kusema. Naye hakimu alimruhusu kwa ishara ya kichwa na mikono, ndipo Dallas alipoanza kutoa maelezo ya majina yake kwa kusema: "Mheshimiwa Hakimu, kwa ufafanuzi zaidi, naiomba mahakama yako tukufu inipe ruhusa ya kueleza historia ya maisha yangu kwani kwa kufanya hivyo ndipo jina au majina yangu yatakapoeleweka vizuri!"

    Hakimu alitikisa kichwa kumuashiria aendelee kueleza, na ndipo Dallas aliposema: "Kwanza kabisa ninataka ieleweke kuwa mara nyingi, jina la mtu huwa anapewa, anaitwa na hajipi wala kujiita. Ni kwa wachache wanaojipa majina wenyewe, wengi huwa wanapewa. Hilo ni la kwanza. Jingine ni kuwa majina mengine ni marefu, kwa hiyo yanakatishwa na wanaoyatumia sio wanaoyamili ki. Katika kukatishwa inategemea pahali na watumiaji. Mheshimiwa hakimu, jina langu mimi ninaitwa Abdallah." Dallas alipofika hapo alinyamaza kimya na kuangalia chini kama vile anayefikiria aseme nini. Kisha akanyanyua uso wake na kumuangalia Amani, huku macho yake yakiwa yamejaa machozi, aliendelea kusema, "Jina alilonipa baba yangu nilipozaliwa ni Abdallah, baba, mama na watu wote katika familia yangu waliniita kwa jina hilo, ABDALLAH. Hawakulikata wala kulipunguza. Lakini wazee wangu walipofariki, na wakati huo nina miaka kumi na saba. Ndipo watu wakaanza kuniita Abdul, hapa ni kwenye karakana nilipokuwa ninajifunza kazi ya makanika. Sikuwa na haja ya kuwabishia. Hapo ilikuwa ni Mwanza. Nilifanya shughuli hizo kwa muda wa miaka mitatu. Wakati huo wote nilikuwa nikiishi na vijana wa rika langu, tulikuwa tumepanga chumba kimoja watu watatu. Mimi Abdul na rafiki zangu Gevas na Mabula.

    “Mwaka wa nne nikiwa tayari nina umri wa miaka ishirini na moja, nilitoka karakana, nikiwa ninajua udereva na ufundi mdogo mdogo. Kwa hiyo nikapata kazi ya saidia dereva wa teksi. Mara nyingi niliachiwa kufanya shughuli kikamilifu wakati wa usiku. Siku moja wakati wa jioni nilikuwa nimeachiwa gari na dereva wangu, nilikuwa ninatoka kumpeleka abiria sehemu za mtaa wa Rufuji uliopo eneo la mjini, ninarudi kituo kikuu cha mabasi, mara nikasikia makelele yaliyonifanya nipunguze mwendo wa gari, ndipo nilipoweza kuona msichana anashikwa kwa nguvu kila sehemu ya maungo yake. Alikuwa anajaribu kukimbia kundi la vijana bila mafanikio. Alipoona gari langu linakuja taratibu mbele yake, alizidi kukimbia kulifuatia gari langu, alipofikia karibu, alirukia mlango wa nyuma akaufungua na kuingia ndani ya gari. Nami nilipoona vile, kwa usalama wa gari la watu nilizidisha mwendo na kundi lile la vijana lilionekana wazi kuwa wengi wao walikuwa wahuni lilichanguka na kupisha gari lipite. Nilikwenda mwendo wa kasi na badala ya kwenda kituo cha mabasi nilikwenda moja kwa moja mpaka sehemu iitwayo Mabatini. Nilitafuta sehemu nikaegesha, kisha ndipo nikamuuliza yule msichana. ‘Haya binti nieleleze, jina lako nani na unatokea wapi, na umepata masaibu gani hata ukaandamwa na genge la wavulana huku wakikuchezea na kukutania?’"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kabla sijamaliza Tabia alidakia maneno na kuuliza: "Vipi una mke...umekwishaoa?"

    “Nilimjibu kuwa sina mke wala sijaoa, halafu nikaendelea kumueleza ukweli wa ninapoishi, ‘Mimi ninaishi ndani y a chumba kimoja na wenzangu wawili wavulana, hii ni kutokana na hali zetu za kiuchumi na upatikanaji wa nyumba za kupanga vilevile; kwa hapa Mwanza, hali ni ngumu, sio rahisi kupata chumba cha kupanga kwa bei nafuu. Kutokana na hali hiyo, sasa sijui itakuaje?’"

    “Msichana yule hakuonekana kukatishwa tamaa na maelezo yangu, alinyanyua uso akaniangalia kwa muda, kisha akatamka kwa sauti ya chini na yenye

    kusikitisha, ‘lwapo tangu mwanzo kaka nilikwambia unisaidie hata kama unaye mke, sasa sembuse hao rafiki zako? Nikubalie kaka, mimi hata chini nitalala, angalau kwa wiki moja tu! Nisaidie na kuwaeleza hao rafiki zako, kama kweli ni rafiki zako basi naamini nao watakuelewa na kukusaidia. Naelewa ninakuweka katika hali ngumu, lakini nina amini Mungu amekuleta wewe kwangu wakati nimo ndani ya shida kubwa ili uje unisaidie. Tafadhali kaka usiniache!’”

    “Kwa hiyo niliamua nimchukue msichana huyo nyumbani nilipokuwa nikiishi. Bahati moja nzuri ni kuwa nyumba yenyewe tuliokuwa tunaishi, vyumba vyote vilikuwa vinaelekea uwani, na sote tulikuwa wapangaji. Mwenye nyumba alikuwa haishi humo. Kitu kingine kizuri kuhusu nyumba hiyo kilikuwa ni kila mpangaji wa nyumba hiyo anaangalia lake, hakukuwa na bughudha ya maneno. Vyumba vilikuwa sita, vyoo viwili na jiko kubwa. Kwa kuwa wengi au karibia wote tuliokuwa tukiishi humo ni wajane, basi tuliamua kazi ya kusafisha choo tumpe mpangaji mwenzetu mmoja mwanamke kwa kumlipa ujira. Sote tulikubaliana na hapakuwa na mgogoro, hasa kwa vile anayeshinda hapo nyumbani ni huyo mpangaji mwanamke tu, wengine wote tulikuwa ni watafutaji, makutano yetu ni usiku tena wa manane.

    “Ndani ya chumba chetu ambacho ni kikubwa tu, mlikuwa na vitanda viwili, kimoja kikubwa cha futi 6 kwa 5 na kingine cha futi 3 na kwa 6, kwa hiyo wenyewe tulikuwa tunalala vyovyote vile ili mradi mmoja kitanda kidogo na wawili kitanda kikubwa. Tulikuwa na kochi letu moja refu la mbao na mito ya pamba, na kabati moja dogo la vyombo na ndoo zetu tatu za plastiki, zaidi ni vibegi vyetu vya nguo…”

    Dallas alipofika hapo alitulia na kupiga kimya kwa muda mrefu kama vile aliishiwa na la kusema. Baadae alirudisha pumzi kwa nguvu, kisha akamuangalia Amani, akatoa tabasamu kubwa, kisha akageuza uso wake na kumuangalia hakimu na kusema, "Samahani muheshimiwa hakimu, naomba mahakama yako isinichoke kwa maelezo yangu marefu, kwani katika kufanya hivi, ndipo mifano mizuri ya uongo na ukweli wangu itakapojulikana. Vile vile ndipo mahakama na ndugu Amani atakapofahamu ni kwa nini nikaitwa Dallas, Dulla, Abdi au Abul. Maisha yana maajabu, mambo mengine huwa yanakujia tu pasipo wewe kuyatafuta au kuyafuata. Na haya majina...majina... penginepo hata huyu ndugu yangu wakili mtetezi Amani analo jina jingine analoitwa!"

    Hakimu alimsitisha asiendelee na maelezo mengine bali aendelee na hadithi ya maisha yake ambayo mahakama imempa ruhusa kuihadithia. Dallas aliendelea kusema, "Basi, niliondoka na yule msichana, lakini kabla ya kufanya lolote, kwa hali aliyokuwa nayo yule Tabia, akiwa amevaa kigauni kimoja tu kifupi sana, tena kilikwisha anza kuchanwa na wale vijana waliokuwa wanamzogoma, nilimuuliza, ‘Samahani bi Tabia, hivi huna nguo zozote zaidi ya hiyo uliyovaa ambazo tunaweza kwenda kuzichukua?’"

    “Alijibu kwa msisitizo na kwa haraka, kuwa anazo...lakini hatuwezi kwenda kuzichukua hapo zilipo...!. Jibu hili alipolitoa ilionyesha dhahiri kuwa hataki tena kuulizwa swali kuhusu nguo. Nami nilishangaa kimoyomoyo na kuwaza, sasa hali ile aliyokuwa nayo, nina maana kuhusu nguo aliyokuwa amevaa kwa wakati ule, itakuwaje? Basi kilichofuata mimi nilikaa sawa sawa nyuma ya usukani, nikaondoa gari kwa kuiendesha mpaka kwenye duka moja la muhindi ambalo ninalifahamu, nikasimama mbele yake. Nilimnunulia kwa njia ya mkopo kanga doti moja na pande mbili za kitenge. Niliondoka nae mpaka nyumbani tunakoishi, nilifungua mlango na kumkaribisha Tabia chumbani mwetu mimi na rafiki zangu Gevas na Mabula. Nilimuacha chumbani nikaenda mpaka walipo wenzangu kila mmoja sehemu yake anapofanyia kibarua kuwapa habari za Tabia na kuwafahamisha kuwa atakuwa mgeni wetu wa kuishi naye kwa muda. Gevas na Mabula kila mmoja kwa maoni yake walipinga kuhusu suala hilo mwanzoni, lakini baadae walikubali.

    “Tuliishi na msichana huyu kwa muda wa wiki mbili kama vile ni dada yetu. Chumbani mwetu tulifunga pazia, yeye akawa analala kitanda kile kidogo, na sisi sote watatu tukawa tunalala kitanda kimoja kikubwa. Alitupa msaada wa kutupikia, kutusafishia nyumba na hata kutufulia nguo zetu. Kwa wakati huo, alikwishakutueleza mkasa uliomfika kwamba Tabia alikuwa ni msichana mfanyakazi wa nyumbani. Alikuwa anafanya kazi kwa mama mmoja ambae ana mume na watoto na ndugu zake wa kiume wakubwa aliokuwa akiishi nao. Watoto wake wawili na ndugu yake mmoja ambaye ni mjomba wa watoto hao, walikuwa kila mara wanamtongoza Tabia, lakini Tabia alikuwa anakataa. Kwa hiyo siku ile

    niliyokutana naye, wavulana hao watatu, wakati wa alasiri, mama mwenye nyumba akiwa hayupo, walimvamia msichana huyo na kumbaka, mmoja baada ya mwingine. Mama mwenye nyumba alitokea wakati wavulana hao, watoto wake na ndugu yake wamekwisha maliza shughuli. Tabia alipolalamika na kushitaki kwa mama huyo, ndipo mama huyo akamuamrisha Tabia afungashe apate kumsindikiza kituo cha mabasi aende kwao siku hiyohiyo. Wakati Tabia anafungasha, mama yule alikuwa anazungumza na watoto wake pamoja na ndugu yake kwa kufoka, kuonyesha kuwa amekasirishwa na kitendo cha wavulana hao walichomfanyia Tabia. Kisha alimwendea Tabia na kumpa nguo na kumwambia aivae. Tabia alipoivaa alimwendea mama yule kumuambia kuwa nguo hiyo ilikuwa ni fupi mno. Lakini kwa mastaajabu ya Tabia mama yule aligeuka na kumfokea, akimuamrisha aingie ndani ya gari, na kuwa atamletea nguo zake na khanga ya kujifunga.





    Tabia alikwenda na kuingia ndani ya gari lililokuwa limeegeshwa hapo nje ambalo ni mali ya mama huyo. Japo aliingiwa na woga, wasiwasi na maumivu aliyokuwa nayo hakujua la kusema bali kutekeleza amri. Alibaki ndani ya gari hiyo kwa muda usiopungua nusu saa huku mama yule akiwa na mvulana ndani ya nyumba wanazungumza huku sauti ya mama ikisikika kwa mbali mara moja moja, akiwa anafoka.

    Mara kwa ghafla na kwa mshangao mkubwa wa Tabia, aliwaona wale wavulana wakija, wote watatu waliombaka, wawili wakaingia nyuma ya gari ambako ndipo alipokuwepo yeye, kila mmoja akaingia kwa mlango wa upande wake, wakamsukuma na kumuweka kati kati, na yule mmoja wa tatu, yeye aliingia mbele ya gari lile na kukaa nyuma ya usukani. Tabia alishtuka akataka kupiga kelele, lakini alinyamazishwa na akaambiwa iwapo atajaribu kufanya fujo ya aina yeyote ile, watamuuwa na kwenda kumtupa ziwani, hapo ilikuwa ni eneo la kirumba yalipotokea hayo. Tabia hakuwa na la kufanya bali kunyamaza kimya akiwa amechanganyikiwa. Mvulana aliekuwa mbele alianza kuendesha gari mpaka maeneo ya mjini, sehemu ambayo wanakaa vijana wa vijiweni wengi wao wakiwa wavuta bagi. Walipofika hapo, walimlazimisha Tabia kushuka toka kwenye lile gari. Ndipo Tabia alipoanza kuchapuka bila kujijua anaenda wapi. Hatua chache tu wavulana wa kihuni walimuona, na kwa jinsi alivyokuwa amevaa, walianza kumpigia mbinja, vigelegele na maneno ya kaa. Tabia alichanganyikiwa na kuanza kukimbia, lakini walimfikia na kuanza kumvuta huku na kule, na ndipo nilipotokea. Tabia alituambia kuwa kwao ni Magu…”

    Alipofika hapa Dallas, alitulia tena na kumuangalia Amani kwa kumtulizia jicho kwa muda mrefu. Mahakama ilibaki kimya. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Je umemaliza, Dallas?” Hakimu alimuuliza.

    Dallas kama vile aliyekuwa kwenye mawazo mazito aligeuza uso wake kutoka kwa Amani ambaye ndiye aliyekuwa akimuangalia mara zote kwa siku hiyo, na kumtazama hakimu huku akisema, "Hapana Muheshimiwa Hakimu… bado sijamaliza . . .bado sijamaliza kisa cha Abdul ... ” Alitulia kidogo, kisha akaendelea kusema, “…ninataka mahakama yako ione ni jinsi gani nilivyokuwa sina hatia kuhusu suala zima la Tabia.” Alishusha pumzi ndefu kisha akaendelea bila kujali sura za kutoelewa kutoka kwa Hakimu na baadhi ya wafuatiliaji wengine pale mahakamani akiwemo Amani.

    “Basi tulikaa na msichana huyo kama vile dada yetu, wiki ya pili ilipomalizika, siku moja wakati wa saa mbili usiku, ninaikumbuka siku hiyo tulikuwa tumekaa mimi, gevas na Mabula, tunakula ugali kwa sato aliotutayarishia Tabia, mara tulisikia kunabishiwa hodi mlango wa chumba chetu. Tabia ambaye kwa wakati huo alikuwa amesimama kwa ajili ya kutuwekea maji ya kunywa, alikwenda na kufungua mlango ule.

    “Naam, walikuwa maaskari watatu, mmoja wao akiwa ameshika bunduki, wakiongozana na balozi wa mtaa na watu wengine wawili. Tulishtuka, kwa sababu mpaka wakati huo, katika maisha yetu, yaani Mabula, Gevas na mimi Abdul, hatukuwa tumejiingiza katika tendo lolote ovu, liwe la wizi, kuvuta bangi, kubwia unga wala chochote chenye hatia ndani yake. Tuliamrishwa na kuambiwa sote watatu pamoja na yule msichanaTabia, tunahitajika kituo cha Polisi. Tuliacha chakula, tukanawa mikono, tukajitayarisha na tukachukuliwa na askari polisi mpaka kituo cha polisi. Tulipofika huko, tulielezwa malalamiko dhidi yetu kuwa ni kumtorosha msichana ambaye ni Tabia na sote watatu kwa pamoja kumfanya mke msichana huyo mmoja!

    “Siku hiyo sote wanne tulilala ndani. Siku iliyofuata tukapelekwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya kumtorosha na kumuingilia kimwili Tabia kwa kufanya naye mapenzi kwa zamu, Gevas, Mabula na Abdul. Hiyo ndio ilikuwa kesi ya kwanza ya Abdul. Tuliruhusiwa kwa dhamana na jamaa tuliokuwa tunafanya kazi za vibarua kwao. Na Tabia alipata dhamana kwa msaada wa yule mpangaji mwenzetu mwanamke ambaye alikuwa anaelewa kila kitu kuhusu uhusiano wetu na Tabia. Kesi iliendelea kwa muda wa miezi mitatu, mashahidi waliitwa, wazazi wa binti yule waliwasili, na hatimae wale wale waliokwenda kupeleka mashtaka ambao ni yule mama na vijana wake, kwa wasiwasi wao, walikutwa wanayo hatia na sisi tuliachiwa huru. Kwa hiyo muheshimiwa hakimu jambo ambalo linaweza kuonekana mbele ya macho ya watu kuwa ndilo, kama hii kesi ya Tabia, linawezekana likawa silo. Hiyo ilikuwa kesi yangu nikiwa kama Abdul wa Mwanza. Sikusema uongo!” Dallas/Abdul alimaliza na kuweka kituo.

    “Mheshimiwa Hakimu, hakika hakuna nililoliona kwenye maelezo yote haya ya bwana Dallas zaidi ya kupoteza muda tu…kutusimulia kisa kisichohusika na kesi hii bado hakutoshi kabisa kuifahamisha mahakama yako adhimu ni kwa nini basi, baada ya kuwa ameshatueleza kuwa wazazi wake walimpa jina la Abdallah, na baadhi ya raia wakamkatisha kwa kumwita Abdul, bado amekuja kwenye hii mahakama yako na kujinadi kwa jina la Dallas? Bado nasisitiza kuwa huyu bwana ni muongo na tapeli!” Amani aliinuka na kukazia hoja yake ya awali baada ya kuomba ridhaa kwa Hakimu kufanya hivyo, na kuruhusiwa.



    “Naomba wakili mtetezi amuachie shahidi aendelee kutoa ufafanuzi wa hayo majina mengi aliyomshutumu kuwa ndio kigezo cha yeye kuwa muongo na tapeli!” Wakili Mkuki naye alimpinga Amani baada ya kuomba ridhaa kwa hakimu na kuruhusiwa kufanya hivyo.

    “Tutaenda mapumziko ya dakika kumi na tano…na tukirudi hapa, bwana Dallas ataendelea na utetezi wake!” Hakimu alipitisha uamuzi.



    *******



    Baada ya mapunziko yale mafupi, Dallas alirudi kizimbani na kuendelea na utetezi wake.

    “Sasa ngoja nieleze kisa cha Abdi wa Arusha…” Alianza maelezo yake, huku akimtazama Amani moja kwa moja usoni.

    “Baada ya kesi ya Mwanza, rafiki zangu Gevas na Mabula waliuhama mji wa Mwanza na kwenda Arusha. Miaka mingi baada ya hapo, siku moja nilipata barua kutoka kwa Gevas akinishauri kama ningependa kubadili makazi basi ananikaribisha Arusha. Kwa hiyo miezi mitatu baada ya barua hiyo, niliwasili Arusha. Kazi yangu ya kwanza kufanya nikiwa Arusha ilikuwa ni kuendesha gari aina ya Toyota Pick Up ya msomali mmoja. Kazi ya gari hiyo ilikuwa ni kuchukua nyama kutoka machinjioni wakati wa asubuhi ya mapema na kuisambaza nyama hiyo kwenye mabucha ya sokoni na yale yaliyopo mitaani. Tajiri yangu huyo wa kisomali ndiye aliyeanza kuniita Abdi badala ya Abdul, na watu wote wengine wakawa wananiita kwa jina hilo la Abdi. Sikuona vibaya nami niliitikia. Pamoja na kufanya kazi ya kuendesha Pick Up ya nyama, kwa kuwa mchana kutwa nilikuwa huru, baada ya saa nne au tano hivi, basi nilijikuta ninafanya vibarua vya muda ambavyo ninaona vinaweza kunipatia kipato kidogo cha ziada, vik iwemo mtu wa kati katika biashara. Siku moja wakati nimerudi kazini kwangu nipo kijiweni au masikani ambapo ndipo tulipokuwa tukipata vibarua vya muda nikiwa pamoja na Gevas, wakati huo tayari nina miaka miwili ya kuwepo Arusha, mwenzetu Mabula kwa wakati huo naye alishaondoka Arusha na kuhamia Dar es Salaam. Alikuja mtoto wa miaka sita au saba hivi, alipofika alisalimu na kisha akauliza "Kaka Abdi ni nani hapa?"

    Kwa kuwa hapakuwa na Abdi mwengine zaidi yangu, na kwa vile aliyeuliza ni mtoto, basi sikuona sababu ya kuhofia, nilijitambulisha kwa kumjibu, "Ni mimi hapa…unasemaje kijana?"

    "Unaitwa pale nyumba ile!" Kijana alionesha kwa kidole nyumba iliyokuwa ya tano au sita kutoka pale tulipokuwa. Nilimuuliza yule mtoto,"Ninaitwa na nani?"

    "Sijui, nimeambiwa kamwite Abdi tu…”

    "Amekwambia nani?"

    "Watu wengi wapo pale barazani!"

    "Humjui hata mtu mmoja kati ya watu hao?"

    Mtoto yule alitikisa kichwa kwa kukataa. Tulitazamana na Gevas, kisha nikamuambia: "Wacha niende, iwapo ninakwenda kuuliwa basi kazi kwako Gevas, unajua wapi pa kuanzia!"

    Niliondoka nikaelekea nyumba niliyoelekezwa. Nilipofika nilikuta wanawake zaidi ya watano wamekaa barazani, nilipowasogelea, kabla hata sijauliza, mmoja wao aliyekuwa tipwa tipwa na mwenye sura nzuri sana, alisimama na kusema huku akianza kuondoka kuingia ndani, "Karibu Abdi, tafadhali pita ndani twende!''

    “Nilishikwa na butwaa na kubaki nimesimama na kukodoa macho, wakati huo yule mwanamke tayari yupo mlangoni anaingia ndani. Wale wengine waliobaki waliniangalia wakiwa wana tabasamu kubwa nyusoni mwao. Mmoja wao alitamka kwa kunikaribisha zaidi, "Pita ndani Abdi, usiwe na wasiwasi!"

    Nililazimisha tabasamu na mimi nikalitoa kubwa zaidi huku nikisema, "Aaah hamna wasiwasi…asante, asanteni sana!"

    Nilivuta hatua nikapanda barazani, kisha kwa kutanguliza bega langu la kulia niliingia katika nyumba ile nisiyo ijua. Nilipofika ukumbini, nilisikia sauti kutoka kule barazani nilikotoka ikinisindikiza kwa kusema, "lngia chumba cha pili mkono wa kulia!"

    Mara, kutoka chumba hicho nilichoambiwa niingie, uso wa yule mwanamke aliyetangulia ulijitokeza na kusema, "Njoo huku Abdi…"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niliingia taratibu ndani ya chumba hicho kilichokuwa safi sana. Nilipoingia tu mwanamke yule alifunga mlango kwa kutia tumbuu, kisha akafunga kitasa cha mlango kwa ufunguo. Sijatahamaki nilijikuta nimekumbatiwa na mama huyo huku akiniambia, "Nakupenda Abdi, nakupenda, nimeshindwa kujizuia, tafadhali usinikatalie!"

    Nilishangaa nisijue nifanye nini, akili kidogo ziliniruka lakini baadae ziliporudia, niliona lazima nitumie akili kwani nilikuwa mtegoni. Kwa hiyo nami nilimkumbatia kwa imani na kuonesha kuwa ninamjali kwa anayosema. Halafu nikamshika mabega na kumuweka juu ya kitanda kikubwa kilichokuwemo ndani ya chumba kile, kisha na mimi nikakaa karibu yake na kuanza kumtupia lawama ya kujali: "Sasa kwa nini usiniambie siku zote hizo?"

    "Sikuwa na njia wala jinsi Abdi, pia nilihofia kuwa huenda mwenyewe usinipende!"

    "Mrembo kama wewe? Hebu kwanza niambie jina lako nani?"

    "Mimi ninaitwa Mamii!"

    "Mamii?"

    "Ndio Mamii!"

    "Sasa unaonaje Mamii, kwa kuwa sasa hivi nilikuwa nina safari ya kwenda Usa River na wenzangu, ambao sasa hivi wananingoja, unaonaje mimi na wewe tukapanga muda mzuri wa kukutana baadae?" Mamii alikubali ushauri wangu, lakini baada ya kumbusu, kumkumbatia na kumpapasa. Yote hayo niliyafanya ili nijivue na kujinasua katika mtego huo nilokuwemo ndani yake. Tulikubaliana kuwa nitarudi tena hapo nyumbani kwake siku ile ile wakati wa jioni. Mamii aliniachia nikatoka nikaenda zangu. Kwa kweli sikurudi tena pale nyumbani kwake kwa siku ile, wiki ile, wala mwezi ule. Nikahama kabisa maskani ya mitaa ile ya karibu na kwa Mamii. Siku moja wakati wa saa 10 alasiri, nilirudi nyumbani ninapoishi ambako ni Majengo, nikaingia chumbani kwangu, ambamo kwa wakati huo nilikuwa ninaishi peke yangu, Gevas alikuwa ana chumba chake, lakini nyumba nyingine katika maeneo hayo hayo ya makazi mapya Majengo. Basi nilijitayarisha kwenda kuoga bafuni ambako ni uani, kwa hiyo nilivua nguo zote, nikachukua taulo langu kubwa na kujiviringisha nalo kiunoni. Nilikwenda bafuni, nikaushindika mlango wangu bila kuubana au kuufunga na ufunguo wala kufuli, sababu sikuwa na haja ya kufanya hivyo. Wakati nimetoka chooni, tayari nimekwisha oga, ninaingia chumbani kwangu nilimkuta Mamii amejilaza juu ya kitanda changu akiwa amevua nguo zote na kubaki na khanga moja tu. Aliponiona nimesimama na mshangao mkubwa usoni mwangu, mama yule alisimama, akaniangalia usoni na kutabasamu. Kusema kweli alikuwa ki - umri ni mkubwa kuliko mimi. Alitamka kwa sauti ya chini na ya kuringa, "Hivi ni kwa nini kijana mzuri kama wewe ukawa una roho mbaya hivyo? Kwa nini ulinidanganya? Sasa haya basi, nimekuja mimi kwako…na tupande juu ya kitanda tulale."

    Alipomaliza kusema hivyo, alirudi kitandani, akajilaza chali akajipekua ile khanga aliyokuwa amevaa na kubaki kama alivyozaliwa. Nilibaki nimesimama kama sanamu la kuchonga la jiwe, nilihisi kama vile nimo ndani y a ndoto ya ajabu. Aliponiona nimetulia tu pale nilipokuwa nimesimama sifanyi lolote, alisimama yeye kwa ghafla, akalivuta lile taulo langu nililovaa kiunoni na kuniwacha uchi kwa sekunde chache, lakini haraka haraka nilirukia taulo hilo na kurudia kujifunga tena kiunoni kwangu. Na yeye naye alisimama akaichukua ile khanga aliyokuwa ameivua akajifunga nayo kifuani, tukawa tumesimama tunaangaliana. Akiwa amekunja uso, aliniambia, "Unajidai wewe bora sana eeh? Unataka kuniadhiri sio? Sema wewe Abdi, sema!”

    Nilijaribu kujitetea nikiwa katika hali ya kutatizika, kwa kusema: "Sio hivyo Mamii. . .!''

    "Sio hivyo nini? Kama sio hivyo basi kubali tulale!"

    Sikuwa na shauku, haja, wala hamu ya kulala na Mamii, kwa hiyo nilitafuta sababu za haraka za kumkatalia, hivyo nikamuambia: "Unajua Mamii...mimi hivi sasa ninaumwa? Mbona huniulizi kwa nini sikutokea siku ile tuliyoagana?"

    Mamii aliruka kwa maneno na kuniambia: "Sikiliza Abdi, mimi ninakupenda sana, na ninafuatilia kila mwenendo wako, unadhani nimepajua vipi hapa nyumbani kwako? Huwezi kunidanganya tena, kama hunipendi, ni kwa nini siku ile hukuniambia? Sasa utafanya lile ninalotaka mimi ama sivyo nitakuadhiri. Ninasema toa hilo taulo lako na tupande kitandani tulale la sivyo ... !"

    Sikumwachia amalize maneno yake kwa vile wakati huo tayari nilikuwa nimepandwa na hasira kwa kuendeshwa na mama huyo ndani ya chumba changu, kwa hiyo nilimwambia, "Fanya unavyofanya lakini huwezi kunilazimisha nilale na wewe...mapenzi gani ya kulazimishana? Unalotaka wewe ni ngono na sio mapenzi! Tafadhali toka chumbani mwangu!"

    Kwa mastaajabu nilimuona Mamii akijivuruga vuruga nywele zake, akajisiriba-siriba rangi ya mdomo aliyokuwa amejipaka kwa kuifuta futa ovyo usoni mwake, akajikwaruza kwa makucha yake mabegani mwake, kisha akaifungua ile khanga aliyokuwa amejifunga kifuani kwake, akaishika kwa mikono yake miwili, akatoka kwa ghafla mle chumbani mwangu akipiga kelele za kutaka msaada, huku amejiziba sehemu zake nyeti tu kwa ile khanga, wakati sehemu nyingine zote za maungo yake ziko wazi. Aliguta makelele kwa kusema: 'SITAKI...SITAKI...JAMANI NISAIDIENII!!"

    Nilisimama kwenye mlango wa chumba changu, nikishangaa vituko na maneno aliyokuwa akisema Mamii, kwani vyote sikuvielewa maana yake.





    Muda si mrefu watu wachache walikusanyika wakiwemo wanawake wawili ambao niliwakuta siku ile barazani kwa Mamii. Mamii alizidi kulia kwa kusinasina, huku wale wenzake wakimfariji kwa kumfunga khanga vizuri kifuani na kumbembeleza.

    Haraka, kabla ya waliokusanyika kusikiliza mkasa uliotokea, balozi wa mtaa aliitwa. Baada ya balozi wa mtaa kufika, watu wote walimzunguka Mamii aliyekuwa akilia kama motto aliyechapwa fimbo.

    Watu walimnyamazisha na kumuuliza kulikoni. Shauku yao ya kutaka kujua ni kitu gani kinachomliza Mamii haikuwa kubwa kushinda yangu sababu sikufahamu ni kwa nini Mamii afanye alivyokuwa akifanya! Mamii alianza kueleza huku akifuta machozi kwa kusema, "Huyu kijana huyuu...Abdi!",Alininyooshea kidole.

    Balozi alimuuliza: "Ehe, ana nini?"

    "Anataka...anataka...!" Hakusema bali alianza kubwatua kilio kikubwa, kiasi watu waliokuwepo wakataharuki na kuanza kuniangalia kwa jicho la wasiwasi na shaka. Wale wanawake wawili niliamini kuwa walikuwa shoga zake, walizidi kumbembeleza kwa kumwambia, "Nyamaza Mamii...sema anataka kukufanyaje…?”

    Mamii alitulia na kuanza kuwaeleza waliokuwepo, ‘Huyu Abdi ni bwana wangu wa siku nyingi, lakini kila siku tukiwa pamoja wakati wa kufanya mapenzi, yeye huwa anataka anifanye kinyume na maumbile, mimi kila siku ninakataa. Sasa leo baada ya kuwa sote tumevua nguo akawa ananilazimisha kutaka kunii...kunilawiti kwa nguvu, ndipo nilipopata nafasi nikamsukuma na kuwahi kuchukua hii kanga tu, ndipo nilipotoka mbio kutoka chumbani kwake. Nguo zangu nyingine bado zipo humo chumbani...’

    Kufikia hapa miguno na misonyo kutoka kwa baadhi ya watu pale ilisikika kutoka kila kona, wote wakinitupia macho ya shutuma, nami sikuwa na nafasi ya kujitetea wakati Mamii akiendelea kunisingizia, ‘…ameniumiza kwa kunivuta nywele na kuniparura mabegani….!’

    Balozi pamoja na waliokuwepo waligeuza shingo zao na kuniangalia mimi hapo nilipokuwa nimesimama, nikiwasijui niseme nini. Nilibaki kinywa wazi na kushangaa tu.

    “Baadaye nilijiwa na fahamu na kuweza kutamka, ‘sio kweli ndugu zangu! Huyu mwanamke ni muongo! Mimi..."CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kabla sijamaliza nililokuwa ninataka kulisema, mmoja kati ya wale shoga zake Mamii alinidakia, ‘Sio kweli? Sio kweli nini? Huyu mwanamke si anatoka chumbani kwako? Tazama nguo uliyovaa, si taulo tu hilo? Na mwanamke huyu si ametoka chumbani kwako akiwa uchi wa mnyama huyu? Ni kitu gani kilichomtoa na kumkimbiza akiwa katika hali hiyo kama sio huo uafriti wako? Muongo ni wewe, sio huyu!’”

    “Alimaliza kusema maneno hayo huku akimkumbatia Mamii na kumpangusa machozi kama vile alikuwa ni motto mdogo wa miaka mitatu, kumbe alikuwa ni mkubwa kiumri kuliko hata mimi. Watu waliokuwepo pale wakaanza kudakia kwa jazba.

    "Huyu mtu apelekwe kituo cha polisi tu, mnamchelewesha nini? Watu kama hawa ndio wanaotutia aibu wanaume wenzao. Ashitakiwe, akiwekwa jela angalau kwa miezi michache, atakoma, mpelekeni polisi!"

    Mwingine naye akasema, "Naye kweli bwana. Wakati yuko jela, atawacha au atazidi, mambo hayo yanasemekana yapo huko…ajabu hii! Mtu umepata mwanamke unataka kumfanyia vioja! Balozi, apelekwe tu huyu mtu!”

    “Hakuna hata mmoja kati ya waliokuwepo ambae alitaka angalau kunisikiliza name nieleze au ambaye alinitetea, wote walikuwa na maoni dhidi yangu, kama vile wamepangwa katika mchezo wa kuigiza ambao muhusika na muigizaji mkuu ni Mamii. Nilifunguliwa kesi ya kutaka kubaka na kulawiti kwa nguvu. Kesi iliyounguruma na kuzungumzwa na kila maskani ya vijana mjini Arusha, kesi iliyonitia kwenye kashfa kubwa isiyonihusu. Hatima ya kesi hiyo baada ya miezi isiyopungua minne, nilishinda. Ushahidi uliotolewa baada ya Mamii kulalamika kuwa kwa siku ile tulikuwa sote kuanzia asubuhi, jambo ambalo halikuwa kweli, kuhakikishwa ni uongo na mengi yaliyombabaisha wakati akiwa mahakamani.” Dallas alipofika hapa alitulia tena na kumuangalia Amani ambaye alisimama na kuomba kusema. Baada ya kuruhusiwa na Hakimu, Amani aliiambia tena mahakama, "Mheshimiwa Hakimu, ndugu Dallas anatoa hadithi ndefu ambazo hazionekani kuwa na maana au uhusiano wowote na kesi hii inayomkabili mteja wangu Dokta Imu. Hii yote ni kupoteza muelekeo na hoja dhidi yake ambazo alikuwa azijibu. Samahani muheshimiwa, lakini nionavyo mimi katika kumruhusu aendelee kutoa historia yake ambayo haieleweki, ni kupoteza muda wa mahakama hii!” Baada ya kusema hivi, kabla hajakaa, Zablon Mkuki naye aliomba aruhusiwe tena kusema, alimtetea Dallas, "Muheshimiwa Hakimu, Dallas anayo haki ya kutoa ushahidi kwa kueleza chochote kile ambacho kinaweza kuifanya mahakama hii iamini kuwa anasema kweli. Narudia tena kusema kwamba sababu zilizomfanya Dallas aiombe mahakama kuelezea kwa ufupi historia ya maisha yake na uhusiano wa majina aliyowahi kuitwa kila mji ni kuwa tuhuma za kifo cha Mwanamtama zimeelekezwa kwake na wakili mtetezi Amani. Kwa hiyo naiomba mahakama yako iendelee kumsikiliza Dallas mpaka mwisho wa maelezo yake. Na nina amini hadithi zake zinaeleweka na pia upo uhusiano wa maelezo hayo na kesi hii ya Dokta lmu kutaka kupewa Dallas, ambaye yeye amekuja hapa akiwa ni shahidi!"

    Hakimu baada ya kusikiliza hoja za mawakili wote hao wawili, alimruhusu Dallas

    aendelee kueleza historia ya maisha yake.



    ***

    Dallas alimuangalia Amani kwa sura ya kumuhusudu kisha akatabasamu na kutikisa kichwa, halafu akaendelea kusema.

    “Nashukuru muheshimiwa kwa kuniruhusu niendelee na hadithi yangu. Huo ulikuwa ndio mwisho wa kesi ya Mamii na Abdi wa Arusha. Baada ya kesi hiyo iliyonisababisha kufukuzwa kazi niliyokuwa nayo wakati huo, nilikaa muda mrefu bila kazi maalumu. Nilifanya kazi za 'Mission Town' tu kuchukua kitu hapa kupeleka pale, kuingia mtu wa kati kwa muuzaji na mnunuzi, ndio hivyo nilivyoishi wakati huo wote nilikuwa naye rafiki yangu Gevas. Tulihama eneo la Majengo baada ya kesi ile ya Mamii na tukawa tunaishi Mianzini.”





    Basi Dallas aliendelea kuelezea kuwa aliendelea kuishi pale Arusha na kupata kazi nyingine kwa mzee mmoja mwenye asili ya kiarabu aliyeitwa Subeti Mali. Huyu alimuajiri kama dereva na aliendelea kumuita kwa jina hilo hilo la Abdi. Kisha akaeleza kuwa alifanya kazi ile kwa miezi ipatayo sita, na kwamba siku moja alisafiri na muajiri wake huyo kuelekea Tanga yeye akiwa dereva, na huko muajiri wake huyo akamkutanisha na mwanadada mrembo aliyeitwa Huba. Katika kukutanishwa kwake huko na Huba, Dallas alijikuta akivutiwa sana na urembo na umbile lake, na aliendelea kuelezea kuwa Mzee Subeti alimwambia kuwa yeye Dallas/Abdi atapata hifadhi pale nyumbani kwa Huba eneo la Makorora, wakati yeye Mzee Subeti mwenyewe angeenda kulala kwa jamaa zake eneo la Bombo. Dallas alikubali na akazidi kuieleza mahakama kuwa wakati anampeleka Mzee Subeti hukom Bombo, yule mzee alimwamuita:

    "Abdi?!"

    "Naam!"

    "Vipi, umemuonaje Huba?"

    "Nimemuonaje kwa vipi mzee? Mbona sielewi"

    Mzee Subeti alicheka kidogo na kasha akaniambia "Nina maana, kama msichana, je Huba anavutia?"

    Bila kujitambua nilijikuta nikaitikia haraka haraka, "Sana... tena sana ... anavutia sana tu . . . mwanamke kamili." Nilipogundua nimebabaika mno mbele ya mzee Subeti kuhusu bi Huba, haraka nilibadilisha maneno na kumuuliza mzee Subeti juu ya uhusiano wake na yule mwanadada.

    "Ni rafiki yangu wa karibu sana, wa shida na raha…" Nilipiga kimya kwanza, kwani jawabu hilo sikulielewa au halikunitosheleza. Nae mzee Subeti nafikiri alilifahamu hilo, kwa hiyo aliendelea kunieleza urafiki wake na Huba ulivyo.

    "Ni msichana mmoja anayeelewa sana matatizo ya binadamu wenzake, naye upo wakati alifikwa na matatizo, nami nilijitolea kumsaidia, kwa hiyo tumekuwa marafiki wa dhati na tusio na kificho mbele ya kila mmoja wetu, yaani mimi na y eye. Lakini hatuna uhusiano wa kimapenzi kati yetu kama wengi wanavyoelewa, isipokuwa uhusiano wetu ni wa upendo wa dahati usio na kificho.” Alipofika hapo alinyamaza, na mimi kwa mastajabu ya moyoni mwangu nikajiona nimefarijika kwa kusikia hivyo. Baadae kidogo mzee Subeti aliendelea kusema, "Sasa bwana mdogo Abdi, yule ndiye atakayekuwa mwenyeji wako wakati wote tutakapokuwa tupo hapo Tanga…"

    Nilirudisha pumzi za shauku na furaha na kuitikia "Sawa mzee, nimeafiki!"

    "Je hujihisi kulazimishwa?"

    "Aah, hapana mzee, hata ninakubali kwa dhati."

    Alinyamaza kidogo kama vile anaefikiria jambo fulani, kisha aliniangalia kwa kunitulizia macho, halafu akatamka kwa kusema, "Binadamu wameumbwa na udhaifu bwana mdogo, kwa hiyo usitie wasiwasi wowote kama litatokea jambo lolote ambalo halina madhara kwako wakati upo na Huba!”

    Maneno haya yalinitia shaka kidogo, lakini shaka yangu ilizibwa na hamu kubwa ya kuwa pamoja na Huba, nilijikuta ninamuwaza yeye tu. Bila kujua nilijikuta nikimwambia mzee Subeti, "Maadamu usalama wangu unahakikishwa na wewe mzee, basi sina hofu yoyote sasa hivi wala hapo nitakapokuwa na Bi Huba.”

    “Haya…”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tulifika kwa jamaa zake mzee Subeti, tulikaribishwa kwa furaha, tulipumzika, tukala

    chakula, halafu mzee alikwenda kuoga, na aliporudi baada ya kubadili nguo aliniambia, "Ninaona wewe ni bora ukaoge na kubadili nguo kule kwa mwenyeji wako au unaonaje?!"

    "Vema mzee, ni sawa kabisa."

    Tulitoka tukaelekea kwa Bi Huba. Tulipofika mbele ya nyumba ya Huba, Mzee aliniambia "Wewe Abdi, chukua begi lako na ingia kwa Huba, jingine ninalotaka kukuambia ni kuwa katika suala hili la mimi, wewe na Huba ni letu sote sisi watatu. Asilijue mtu mwingine, na kati yetu sisi watatu, pasiwe na kificho… unasikia hivyo?"

    "Ndio nimesikia mzee!"

    Nilitoka kwenye gari, naye akasogea nyuma ya sukani huku akisema, "Ninaondoka na

    gari, nitakuja baadae, usitie shaka bwana mdogo…kwa heri!"

    Huba alinipokea kwa mikono miwili, kwa hali halisi ya mikono miwili, kwani nilipoingia tu sebleni alinyanyuka, akanipokea begi, akaitua chini kwanza na akanikumbatia "Karibu bwana Dulla, karibu sana!"

    "Ahsante!"

    “Huba alikuwa amebadilika, wakati huo giza tayari limekwishaingia. Huba alikuwa amevaa khanga mbili tu. Mwili wake uliokwisha safishwa ulikuwa unanukia uturi, udi, mawaridi na asumini. Alinishika mkono na kunipitisha chumbani…”

    Hapo Dallas alitulia kwanza na kuacha kueleza. Mahakama nayo ilipiga kimya, kila mtu akawa makini, alitega sikio kumsikiliza yeye. Alizungusha shingo yake na kuwaangalia watu wote walliokuwepo hapo, na mwishowe akatuliza uso wake kwa Amani. Hakuna aliemwambia aache kuhadithia, wala hakuna aliyemuhimiza aendelee. Watu wote walimuangalia yeye tu, pamoja na hakimu. Dallas alirudisha pumzi na kisha akaangalia chini. Aliporudisha uso wake tena na kumuangalia Amani, aliendelea kuhadithia pasipo kumtazama hakimu, "Tulipofika chumbani, muheshimiwa hakimu, mimi na Huba tulisimama mkabala kila mmoja na mwenzie huku tukiangaliana. Aliliweka chini begi langu ampalo alilichukuwa kwa mkono mmoja wa kushoto wakati tunaingia ndani.

    Huba alianza kunivua nguo taratibu, bila ya kuongea neon lolote. Nami nilimuachia huru afanye atakavyo, kwani nilikuwa ninajihisi raha kufanyiwa hivyo. Alipohakikisha kuwa sina hata kipande cha nguo mwilini, alizikusanya nguo alizonivua na kuzitungika kwa utaratibu mzuri juu ya henga iliyokuwa kiwambazani. Kisha kwa haraka akafungua khanga aliyokuwa amevaa kwa kujifunga kiunoni na akanifunga nayo mimi kiunoni. Aliniongoza bafuni, chumba hicho kilikuwa kina choo cha bafu ndani kwa ndani.

    Tulipokuwa tayari tumeingia alinitambulisha kwa kila kitu kilichokuwemo humo chooni na bafuni, kuanzia dawa za meno mpaka sabuni za aina mbali mbali na shampuu, na akanitafadhalisha, “Tafadhali unisamehe Dulla, itakubidi uoge peke yako, kwani mimi nilikwishaoga kwa sababu ya kuondoa hina nilizokuwa nimepaka ...nadhani utanisamehe laazizi?"

    Kwa haraka na mfadhaiko niliokuwa nao tayari umejaa nilijibu "Nimekusamehe kabisa usitie wasi wasi!"

    "Ahsante swahibu wangu!"

    Alitoka na kuniacha hapo chooni, nilifanya na kumaliza haja zangu zote, kilsha nikaona kuwa kitu kimoja hakipo, nacho ni taulo. Kwa hiyo nilijifunga ile khanga kiunoni na kutoka, nikidhamiria kwenda kutoa taulo ndani ya begi langu. Nilipotoka chooni na kuingia chumbani, nilimkuta Bi Huba ameshika khanga nyingine mkononi. Mara baada ya kuniona alinishika mkono na kuniweka juu ya stuli iliyokuwepo mbele ya meza ya kujipambia. Kama vile mtoto, alianza kunipangusa maji mwilini kwa kutumia khanga hiyo. Alinipangusa kuanzia kichwa hadi nyayoni, kisha akatoa khanga nyingine na kuniviringisha nayo kiunoni, sababu ile ya awali ilikuwa tayari iko maji maji. Alinitana nywele, akanipaka mafuta ya mwili na kunipulizia pafyum. Baada ya hapo ndipo aliponiuliza.

    "Je, bwana Dulla.. nikutayarishie chakula?"

    "Hapana" Nilijibu, "Mimi tayari nimekwisha kula huko kwa Mzee Subeti!"

    "Basi wacha nikuletee angalau kikombe cha kahawa unywe...unapenda iwe ya maziwa? au bila maziwa?"

    "Nipatie bila ya maziwa ...tafadhali!"

    Bi Huba alitoweka chumbani kuelekea sebleni na baraza ya uani ambako ndiko kulikuwa na jiko la sehemu ya nyumba hiyo. Baada ya dakika chache alitokeza tena akiwa amenyanyua sinia ndogo iliyosheheni vikombe viwili vidogo vidogo na chupa ya chai moja ndogo. Aliviweka vitu hivyo juu ya stuli nyingine iliyokuwepo humo chumbani licha ya ile niliyokuwa nimekalia, kisha akachukua mswala uliokuwa kipembeni, akautandika sakafuni juu ya zulia la mpira.

    Akachukuwa ile sinia iliyokuwa na vikombe akaiweka katikati juu ya mswala, kisha akanikaribisha nami nikae juu ya mswala huo.

    Alipohakikisha nimekaa nae alikaa mkabala na mimi, kati yetu palikuwa na kile kisinia kidogo.

    Alifungua chupa na kumimina kahawa ndani ya vikombe vile vidogo viwili.

    "Karibu unywe kahawa bwana Dulla…"

    Bi. Huba ndiYe aliYependelea kuniita kwa jina la Dulla, tangu siku ya kwanza alipotambulishwa

    kwangu na akaambiwa kuwa ninaitwa Abdallah.” Dallas alisema na kuweka kituo, akibaki akiwa amemkazia macho Amani.





    Nami kwa upande wangu sikuwa na pingamizi kuitwa Dulla, kwa vile alikuwa hanitusi bali ananitukuza jina langu kwa upendo, bashasha na ashiki. Kwa hiyo tuli kunywa kahawa chungu tupu lakini iliyojaa tamu ya maneno, vicheko,mabusu na mazungumzo. Wakati wote huo, mimi nilikuwa khanga moja tu kiunoni na upande wa pili wa khanga hiyo alikuwa ameuvaa yeye kifuani. Basi mwisho wa mazunguzo na bashasha zetu na alivyokuwa Huba sikuweza kujikaza, nilikuta kichwa change kimepata mto juu ya mapaja yake, na hatimaye tulijikuta tuko juu ya kitanda kilichomwagiwa mauwa ya asumini na mawaridi. Kabla hatujapanda kitandani nilimwambia swala la kuzima taa ya muangaza mdogo wa bluu iliyokuwa ikiwaka chumbani humo pamoja na kufunga mlango, lakini Huba alikataa kwa kusema, "Usijali vitu hivyo mpenzi, viache viwake na kuwa wazi havitatuzuia tusiendelee na shughuli zetu...au una wasiwasi swahibu?”

    “Wakati huo nilikuwa tayari nimefikia hatua ya kutorudi nyuma, kwa hiyo nilisema, "Hapana sina wasi wasi swahiba...isipokuwa..."

    Sikumaliza nililokuwa ninataka kulisema, nilishtukia kinywa changu kikizibwa na kinywa cha Huba na kushonwa na shazia ya ulimi, nilibaki kupokea na kujibu mapigo kwa silaha hizo za mdomo na ndimi huku sauti za mihemo ya kupanda na kushuka

    zikisikika kati yetu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilikuwa katikati ya tendo la ndoa niliposikia mlango unafunguka, nilinyanyua kichwa na kuangalia kidogo ndipo nilipomuona Mzee Subeti, naye aliniashiria niendelee tu. Huba naye aliniambia huku akakizungusha kichwa change kisimuangalie mzee Subeti.

    "Usiwe na wasiwasi mpenzi endelea" Nilifumba macho nikaendelea, kumbe na Mzee Subeti alivuta kiti kilichokuwemo mule chumbani, akakaa juu yake na akatulia na kutuangalia tunafanya nini kwa makini na utulivu.

    Baada ya kumaliza, mzee Subeti kwa sura yenye furaha na kuridhika alisema, "Ahsante sana!"

    Alinigeukia mimi na kuniambia, "Abdi, usiwe na wasi wasi kijana. Nilikwisha kuambia kati yangu mimi, wewe na Huba, hakuna cha kificho, siri yetu hii isitoke kwa watu wengine. Kwa hiyo, wewe isikuumize kichwa!"

    Sikujua la kusema, nilibaki nimejiinamia. Nilishindwa kumtazama Mzee Subeti machoni. Baadae alinyanyuka, akanishika bega na kuniambia, "Kesho unaweza kupumzika tu hapa hapa nyumbani, mimi tutaonana hiyo hiyo kesho saa kama hizi… kwa heri!"

    Alitoka akaenda zake.

    Huku nyuma nilimgeukia Bi. Huba na kumuuliza, "Unafahamu Bi. Huba sielewi kinachoendelea? Ninajiona kama vile niko ndotoni, nimeingia mtengoni pasipo kujua...nini maana ya jambo hili lililotokea?"

    Bi. Huba alinyamaza kimya na kuniangalia tu kwa macho yake makubwa yaliyokuwa kwa wakati huo yanaanza kujaa machozi. Wakati huo tulikuwa tumekaa kitandani kila mmoja wetu amejiziba na khanga yake moja. Huba alianza kusema kwa kuniuliza kwa sauti ya huzuni, "Hivi bwana Dulla unafikiria nimekutia kwenye mtego, hivi huamini kuwa hisia zangu kwako ni za kweli? Hivi kumbe umelazimishwa kulala na mimi? Basi kama ndio hivyo naomba unisamehe bwana wangu, lakini mimi ninakula yamini kuwa tangu yalipotua macho yangu kwako wewe, yalituwa pamoja na moyo wangu. Nakupenda kweli Dulla,na wala sio mtego au dhihaka!"

    Ilibidi nianze kumbembeleza Bi. Huba aliyekuwa akilia kweli kwa wakati huo. Vile vile ilibidi nijieleze fikra zangu. Nikamwambia, "La hasha, BiHuba. Sizungumzii suala lako wewe na mimi. Hilo halina shaka,mimi pia nilitambua mara tu nilipokuona kuwa wewe ndiye wangu wa mayo hasa. Jambo ninalozungumzia mtego ni hili la mimi na wewe tukiwa tumo katika tendo la mapenzi huku Mzee Subeti akakaa kutuangalia kama vile sinema!"

    Huba aliinama huku akaniambia kwa sauti ya chini.

    “Mimi nilidhani jambo hilo unalifahamu. Wema wote, busara na ukarimu alio nao mzee Subeti, unafunikwa na udhaifu wake huu alionao wa kupenda kuangalia mume na mke wakati wakiwa katika tendo la ndoa. Hilo linafahamika na wachache walio naye karibu. Kwa upande wangu, wema na fadhila alizonitendea sikuweza kukataa aliponiomba hilo jambo likifanyika alione!"

    Niliutia uso wake viganjani mwangu na kuyaangalia macho yake moja kwa moja na kumuuliza, "Hebu niambie tafadhali bibie Huba…mimi ni wa ngapi kuletwa kwako na Mzee Subeti? Tafadhali sema usiogope, ninaamini unafanya hivi kwa kulipa fadhila kwa Mzee Subeti!"

    Huba aliutoa uso wake na kuanza kulia. Alilia kilio cha uchungu, kisha akafuta machozi na kuniambia, "Kilio ninacholia namlilia Mzee Subeti, mfadhili wangu, rafiki yangu, muhisani wangu, msiri wangu na msaidizi wangu mkubwa. Sikiliza nikuambie bwana Dulla, amini usiamini wewe ni mwanamme wa kwanza kuletwa na Mzee Subeti, na ni mwanamme wa pili kulala naye katika maisha yangu. Wa kwanza alikuwa ni marehemu mume wangu." Alipofika hapo alitulia kidogo, kisha akaendelea, "Niliolewa nikiwa mdogo wa miaka kumi na saba tu. Niliishi kwa mapenzi makubwa na mume wangu ambaye alinipita kiumri kwa miaka kumi. Nilimpenda sana, naye pia alinipenda sana. Alifanikiwa mapema katika maisha yake. Aliweza kumiliki nyumba mbili hapa mjini nzuri sana za kisasa, pia na shamba kubwa lililopo wilayani, pia alikuwa anazo gari mbili, pickup na saloon, ukiachilia mbali fenicha za nyumbani.Tulijaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume ambaye kwa sasa ana miaka mitano. Mume wangu alifariki kwa ajali ya gari wakati huo motto wetu alikuwa ana miaka mitatu na nusu hivi. Baada ya kifo cha mume wangu na miezi sita kupita, yaani miwili baada ya kutoka eda, mambo yalinigeukia.

    “Nilisingiziwa uchawi, kuwa mimi ndiye niliyemuuwa mume wangu.Nilifukuzwa ki-mbwa ki-nguruwe na ndugu wa mume wangu. Nilinyang'anywa kila kitu pamoja na mtoto wangu. Mimi binafsi nilikuwa yatima baba na mama yangu walifariki nikiwa bado ni mdogo na hawakuwa na mtoto mwingine zaidi yangu. Kwa hiyo sina ndungu wa karibu, ndugu nilionao ki-ukoo ni wa mbali na sio wengi. Janga hilo liliponipata nilichanganyikiwa. Mzee Subeti kwa mbali katika ukoo wake anahusiana na marehemu mume wangu. Nilikuwa ninamfahamu tangu enzi za uhai wa mume wangu.Tulikuwa tunamuita baby. Udhaifu wake huu niliusikia na kuufahamu toka wakati huo. Baada ya mimi kupata misukosuko hiyo mshauri pekee alyiejitokeza alikuwa yeye MzeeSubeti. Kwanza alinisaidia kwa kunipangishia hii nyumba upande mzima na akalipa kodi ya miaka miwili. Pili akanisaidia kupata kibarua cha kuuza duka la nguo la rafiki yake, amenisaidia kwa fedha, fenicha na ushauri, kwa kuniambia nitulie, maadam mtoto wamemchukua nihakikishe wanamsomesha, na kuwa mwisho wa yote motto huyo atajua haki zake na pia atamjua mama yake, kwa kweli amenifariji mno.

    “Tukija kwenye swala lako, ni kwamba ameniambia siku nyingi habari zako na jinsi ulivyo hodari, mpole na mzuri wa kila kitu.Pia akaniambia kama yupo mume ambaye angenifaa anioe basi ni wewe…na akaahidi kukuleta na kutukutanisha...”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***Mnh! Si nilisema hapa kuna kitu?? Huyu Mzee Subeti kumbe kozimeni? Na hiI stori ya Huba nayo...Inatupeleka wapi? Huyu Dallas hasa mwingi wa habari!



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog