Search This Blog

Wednesday, 1 June 2022

MAJAALIWA - 5

 







    Simulizi : Majaaliwa

    Sehemu Ya Tano (5)



    "Endelea bwana ...hakuna njia nyingine. Dokta lmu ni muhalifu, anaweza akaja kumtia matatani hata huyo ndugu yenu Zainabu. Ni bora yametokea haya kabla hajamuoa!”

    Dallas alijihisi kuchanganyikiwa.

    Alikumbuka ni jinsi gani alivyoona upendo uliopo katika familia ya Mzee Mirambo. Kwa hiyo alikumbuka jambo na kuuliza kwa upole.

    "Ngoja nikuulize swali moja Gevas!"

    "Haya... uliza!"

    "Hivi ni nani hasa aliyetuajiri kazi hii ya ushahidi?"

    Gevas alimuangalia tena Dallas na kumuuliza, badala ya kumjibu, "Unasema kweli Dallas humjui aliyetupa kibarua hiki ambacho wewe ndiye mtekelezaji mkuu?"

    “Haki ya Mungu vile, simjui!"

    "Bosi wetu bwana ni yule yule jamaa tuliyekwenda naye akatuonesha nyumba Upanga!"

    "Ahaa, sasa tutaweza tukampata wapi, sababu nina maswali kidogo ninataka kumuuliza!"

    "Maswali gani? Au ndio hivyo ulivyosema unataka kumsaidia Dokta lmu, baada ya kugundua kumbe ni shemeji yako?"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dallas alicheka kidogo kisha akasema, "Hakuna ubaya mtu kumsaidia shemeji yake, lakini basi, suala hili si limekwishafika mahakamani? Si ndivyo ulivyokuwa unasema hapa sasa hivi? Basi ni sheria ndiyo itakayo amua. Mimi ninahitaji kumuona, sababu nina vitu niliulizwa mahakamani, nikashindwa kuvijibu. Naamini ufafanuzi wake utanielekeza kumshinda Dokta lmu, ambalo ndio kusudio lake."

    Gevas alikunja mabega na kusema kumwambia Dallas, "Kama ndivyo hivyo, basi na tupange ni lini nikupeleke nyumbani kwake!"

    "Ni vizuri tukaenda kumuona siku yoyote ile ambayo unafikiri yeye pamoja na wewe mnayo

    nafasi ya kutosha kimazungumzo, ili mradi siku hiyo iwe ni kabla ya kesi kuendelea kusikilizwa tena.

    "Sawa, tutapanga siku ya kwenda nitakujulisha"



    ******

    Baada ya kumuacha Mzee Majaliwa msikitini, na kumrudisha Dallas nyumbani kwake, Amani alikwenda zake moja kwa moja mpaka Kijitonyama kwa mchumba wake Fatima. Alipofika, baada ya kusalimiana na watu wote hapo kwa wakwe zake watarajiwa aliomba atoke na Fatima, kwani a!ikuwa na mazungumzo nae. Fatima alijitayarisha haraka haraka, wakatoka na kuelekea mgahawa mmoja mkubwa na tulivu. Waliagiza watayarishiwe chakula cha jioni wakati huo. Waliletewa vinywaji baridi wakati wanasubiri chakula walichoagizia.

    Wakati wanakunywa taratibu, ghafla Amani alimwambia Fatima.

    "Unajua Fatima ...mimi si mtoto halisi wa wazazi wangu?"

    Fatima alishituka kidogo na kuuliza kwa mshangao mkubwa.

    “Eh! Unasemaje Amani?''

    “Nina sema hivi aliyokuwa anayasema Dallas mahakamani ni kweli... mimi ni mdogo wake hallsi na si mtoto wa kuzaliwa na Mzee Mirambo na mama yangu!”

    Amani alinyanyua bilauri ya juisi akaipeleka mdomoni wakati Fatima ameshikwa na butwaa na kubaki kumkodolea macho.



    *****

    Amani alipotua bilauri na kuiweka pale ilipokuwa juu ya meza, alirudia tena usemi wake kumuhakikishia Fatima.

    "Ndio ... mimi si mtoto halisi wa kuzaliwa na baba na mama Mirambo ... baba yangu hasa wa kunizaa ni Mzee Majaliwa . . . ! Na mama wa kunizaa, inasadikika kuwa alifariki zamani kwa kuchomwa moto ndani ya nyumba yao huko kijijini ambae a!ikuwa ndie sababu, kwa kusingiziwa uchawi!"

    Akaendelea kumueleza mchumba wake Fatima kila kitu kilichoelezwa nyumbani kwao, pasipo kumficha chochote, mwishowe alimwambia, "Pamoja na yote hayo mama na baba hawapo tayari kuwachana na mimi kwa hali yoyote iwayo, pamoja na kusema ukweli kwa mimi si mtoto wao wa kumzaa. Halikadhalika na mimi nitabaki kuwa Mirambo. Sitawaacha baba na mama yangu kabisa, ingawa mzee Majaliwa nitakuwa naye vile vile."

    Fatima alirudisha pumzi kwa nguvu baada ya kusikia haya.

    “Sasa itakuwaje kuhusu kesi unayomtetea Dokta lmu?" Alimuuliza.

    "Niambie wewe kwanza, kutokana na niliyokueleza unanifikiriaje mimi? Niambie hilo kabla hatujajadili kuhusu kesi ya Dokta Imu!"

    "Nikufikirie nini Amani? Wewe u mchumba wangu ambaye ninakupenda. Kutambulika kwa uzawa wako halisi hakuwezi kubadili pendo langu. Kwa hali yeyote ile mama na baba Mirambo watabaki kuwa ni wako kama vile pendo langu. Na kuongezeka kwa kutambulika kwa Mzee Majaliwa na Dallas kwamba wao ni baba na kaka yako, nako pia kutaongeza pendo langu juu yako,ondoa shaka Amani kuhusu uhusiano wetu, zuri na baya litakuwa ni letu sote."

    Amani alifarijika mno kwa jibu lile, kwani ingawa alikwisha kubali na alikwisha kubaliana na wazee wake kuwa hapana mabadiliko zaidi ya kutambua kuwa yeye si mtoto mzaliwa wa mzee Mirambo bali ni wa Mzee Majaliwa, lakini alikuwa bado anao mshituko wa moyo na mfadhaiko wa akili. Lakini baada ya mazungumzo haya na mpenzi wake Fatima, alijihisi uzito fulani uliokuwa umemuingia ghafla moyoni na kichwani mwake, ukimtoweka. Chakula walichoagiza kililetwa, wakaanza kula huku wakiendelea na mazungumzo yao. Amani alirudisha suala la kesi na kusema, "Pamoja na yote hayo, bado nitaendelea kumtetea Dokta lmu mpaka dakika ya mwisho, kama si kwa sababu yeyote ile nyingine, basi ni kwa sababu ya mdogo wangu Zainabu."

    Baada ya hapo alizungumza mengi yanayohusu kesi ya lmu na kisha akamuuliza Fatima.

    "Kweli...vipi zile picha ambazo nilitarajia kuzipata, . . . za marehemu Mwanamtama, alizopiga na Dokta lmu wakati akiwa hai, . . kutoka kwa Zaituni . . . zi.mepatikana?”

    Fatima alionekana kugwaya kidogo kujibu swali hilo.

    "Sina uhakika…” Hatimaye alijibu, na kuendelea, “… kwa sababu kusema kweli tangu siku ile tulipoliongelea suala hilo, sijawahi kumuuliza tena Zaituni. Lakini huenda akawa amezipata, tukitoka hapa, tutakapofika nyumbani wakati wa kunipeleka nitamuuliza kabla hujaondoka."

    Alikuwa Zaituni mdogo wake Fatima anajitayarisha kwenda kulala, wakati Amani na Fatima wanaingia hapo nyumbani kwa kina Fatima. Zaituni aliitwa sebleni, na alipofika Amani alimuuliza.

    "Vipi kazi yangu uliyoahidi kunifanyia Zaituni, umeitekeleza?"

    Zaituni kwanza alipigwa na mshangao na kuuliza.

    "Kazi ipi shemeji Amani?"

    Amani alijibu kwa kuongeza maskhara kidogo kwa kusema, "Ah, bibi wewe siku hizi mawazo yako yapo kwa mwenzangu nini? Tuliahidiana nini mimi na wewe mara ya mwisho tulipozungumza? Si ulisema utafanya bidii ya kufuatilia na kuzipata picha alizopiga marehemu Mwanamtama enzi za uhai wake akiwa na Dokta lmu?"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zaituni alicheka na kusema kumwambia shemeji yake Amani, "Samahani shemeji, unajua tena hizo picha nilizipata siku nyingi! Na wewe nawe shemeji Amani unakaa muda mrefu mno kabla hujatutembelea, ndo maana nikasahau.. Ngoja nikakuletee."

    Baada ya kutoweka kwa muda wa dakika tano hivi, Zaituni alikuja na picha zipatazo tano. Alianza kumpa Amani picha moja baada ya nyingine huku akimuelekezea kuhusu picha hizo.

    "Picha hizi tatu, zilipigwa kwenye 'party’ na mbili, moja ni ya marehemu Mwanamtama peke yake, na nyingine ni ya Dokta lmu peke yake…"

    Akaendelea kutoa maelezo ya picha moja moja.

    "Hii ya kwanza ni ya Mwanamtama peke yake, hii ya pili ni ya Dokta lmu peke yake, hii ya tatu ni ya Mwanamtama na Dokta lmu wakiwa pamoja kwenye 'party'… hii ya nne ni ya hao watu wawili yaani Mwanamtama na Dokta lmu na marafiki zao. Na hii ya mwisho ni ya baadhi ya watu wengi waliokuwepo kwenye 'party' hiyo akiwemo na Dokta lmu na Mwanamtama, ... ziangalie vizuri."

    Amani alItoa macho na kuziangalia picha hizo, tena na tena. Aliiangalia zaidi ile picha ya Dokta lmu peke yake. Alikunja uso wake na kuonekana amepotea ndani ya mawazo. Halafu alinyanyua uso na kumuangalia Zaituni.

    "Una uhakika Zaituni, kuwa Dokta lmu huyu ndiye aliyekuwa 'boyfriend' wa marehemu Mwanamtama?"

    "Mimi ndivyo ninavyoelewa shemeji Amani. Kwa uhakika zaidi, labda ukawaulize hao waliopiga nao picha hasa huyo..." Alimnyang'anya moja ya picha, ile ya nne kumpa ambayo ni ya marafiki wa Dokta lmu na kumueleza Amani kwa kugusa picha kwa kidole na kuendelea kusema, "... Huyu ni rafiki yake Dokta lmu, kwa nilivyoambiwa na y eye ni Daktari vile vile, wanafanya kazi pamoja Muhimbili."

    "Wamekuambia jina lake ni nani?!" Amani alimuuliza.

    "Hapana, jina lake sikutajiwa!"

    "Basi, nashukuru sana Zaituni, na samahani kwa usumbufu."

    "Hata shemeji bila samahani na wala ha•kuna usumbufu wowote!"

    Amani aliagana na Fatima pamoja na Zaituni kwa kuwaambia, "Mimi ninaona sasa niwaage, na hizi picha ninaomba kuondoka nazo!"



    *****

    Siku iliyofuata wakati wa saa za asubuhi, Amani alitua hospital ya Muhimbili kwa ajili ya kumsaka rafiki yake Dokta lmu aliyekuwa nae kwenye 'party' ambaye wamepiga picha ya pamoja na marehemu Mwanamtama alipokuwa hai. Kwa kuwa hakumjua kwa jina, alijaribu kufanya upelelezi kwanza kwa kutumia ile picha, ili apate jina lake. Aliwaendea wafanyakazi wa chini, wa huduma ndogo ndogo zisizokuwa na taaluma ya udaktari. Hivyo, hakupata tabu, mtu wa kwanza tu kumuuliza na kumuonesha ile picha ambaye alikuwa mfanyakazi wa idara ya maakuli wa jikoni, mama wa makamu, baada ya kuiona picha alisema, "Huyu ni Dokta Kaiza, nenda ukamuulize kwenye ofisi zile pale!" Akamuelekeza kwenye jingo lililo na ofisi.

    Amani alipoona kuwa huyo mama anatoa ushirikiano mzuri katika kuelekeza na kujibu analoulizwa, alitaka kumjaribu kwa jingine, kwahiyo alitoa ile picha ya Dokta lmu na kumuuliza huku akicheka cheka, "Samahani shangazi, inaonekana nitakupa tabu sana leo kwa kukuuliza habari za watu ambao nina picha zao tu, nami pia nimeagiziwa!"

    “Bila samahani baba, lakini kwema? Hakuna matatizo yoyote?”

    "Hapana shangazi. Hakuna matatizo ndio maana nina picha tu sina majina ya watu hawa, je huyu jina lake ni nani?”

    Mama yule alishika ile picha mkononi mwake na kuiangalia, kisha akasema, "Huyu, si Dokta lmu huyu!"

    "Ahsante sana mama"

    "Ahsante baba!"

    Amani alikwenda moja kwa moja kwenye ofisi alizoelekezwa. Alipofika hapo, hakutaka kuonesha picha, bali aliuliza moja kwa moja kwa kujiamini. Alimuuliza mtu aliyemkuta, ambaye alioneka naye ni daktari vile vile. Baada ya kusalimiana alimuuliza.

    "Samahani ndugu, mimi jina langu ni Mirambo, ninamuulizia Dokta Kaiza!"

    Yule bwana alijibu kwa uchangamfu na kusema, "Nimefurahi kukufahamu ndugu Mirambo, mimi ni Dokta Simon, tafadhali subiri nikakuitie Dokta Kaiza, kwani alikuwa hapa hapa dakika chache tu zilizopita…alisema anakwenda wodini. Subiri tafadhali, unaweza kukaa

    hapo juu ya kiti."

    Wakati Amani anakaa kwenye kiti alichokaribishwa Dokta Simon alitoka ofisini kuelekea wodini. Kwa muda usiopungua robo saa, Dokta Kaiza alitokezea akiwa ameongozana na Dokta Simon.

    Amani aliweza kumtambua baada ya kumuona, kuwa yeye ndiye aliyekuwemo kwenye picha ile ya 'party.' Walisalimiana na kutambuana. Amani alimpa asante Dokta Simon, kisha akamuambia Dokta Kaiza.

    "Samahani Dokta nilikuwa nina mazungumzo ya faragha ambayo ninahitaji kuongea na wewe!"

    Dokta Kaiza alikuwa kijana bado wa miaka 30 hivi, mweusi, mwenye sura na umbile zuri sana. Tabasamu yake ilimfanya aonekane mtanashati zaidi kwa meno yake yaliyopangi ka vizuri kinywani mwake yanayoonekana meupe zaidi kutokana na ngozi ya uso wake iliyo nyeusi. Pia alionekana mpole na mwenye sauti ya taratibu alimkaribisha Amani wakae katika kimoja cha vyumba vya ofisi kilichokuwa hakina mtu. Aliuliza Kaiza baada ya kukaa.

    "Ndio, tukusaidie nini ndugu Mirambo?"

    Amani alitoa ile picha ya kwenye 'party' aliyopiga Kaiza, Dokta lmu, Mwanamtama na wengine, akaiweka mbele ya macho ya Dokta Kaiza na kumwambia, "Dokta, mimi ni ndugu wa karibu wa marehemu Mwanamtama. Msaada ninaouomba kwako, tafadhali kwa jina la Mungu niambie kiasi ulichowahi kukitambua kinachohusu uhusiano wa Dokta lmu na Mwanamtama. Sababu tunaelewa wewe ni rafiki wa Dokta lmu wa karibu sana.”

    Kaiza aliinama kidogo kama anayefiklria kitu kisha akasema, "Ni kweli kabisa mimi nilikuwa rafiki wa karibu wa Dokta lmu, lakini ni hapo zamani sio siku hizi za karibuni. Ni marafiki sababu sote tunafanya kazi pamoja na sote bado tungali vijana, lakini tuliachana kuwa marafiki wa karibu kwa vile tunatofautiana sana tabia zetu. Yeye mwenzangu alikuwa ni mtu wa kupenda sana wasichana. Tena basi, ni afadhali angekuwa mmoja lakini kila siku au wiki ni msichana mwingine. Kama yupo msichana aliyewahi kuishi naye kwa muda mrefu basi ni huyu Mwanamtama. Ninavyojua mimi, msichana huyo alimpenda sana Dokta lmu kuliko vile yeye alivyokuwa akimpenda.

    Walikuwa wanakwenda 'outing,' kwenye starehe na sherehe kama hiyo ya 'party' ambayo tuliwahi kwenda pamoja. Ndio hivyo ninavyojua kuhusu Dokta lmu na marehemu Mwanamtama. Pole sana hata habari sina kama Mwanamtama amefariki. Kusema kweli urafiki wangu na lmu naweza kusema umekufa siku nyingi!"

    Amani alimuangalia Kaiza na kumuuliza kwa makini na taratibu.

    "Lakini Dokta Kaiza, wewe na Dokta lmu si bado mnafanya kazi pamoja? Ndio tuseme hufahamu kweli kuwa mwanamtama amefariki?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ni kweli tunafanya kazi pamoja, ya udaktari, lakini katika vitengo na idara tofauti. Yeye yupo idara ya magonjwa ya kifua na kifua kikuu, mimi nipo idara ya magonjwa ya mifupa. Na kwa vile sio marafiki tena, ni vigumu kujua habari zake, kwa mara ya mwisho habari nilizozisikia ni kuwa anagombea msichana aitwae Zainabu."

    Amani alimshukuru, lakini kabla hajaondoka, alitoa picha ya Dokta Imu aliyopiga peke yake na kumuonesha kaiza huku akimuuliza.

    "Si ndie huyu Dokta lmu mwenyewe?"

    Kaiza aliichukua na kuitazama na kusema kwa kuthibitisha, "Hasa ndiye huyu-huyu, wala habadiliki"



    ******

    Siku mbili kabla ya kesi ya Dokta lmu kuendelea kusikilizwa, Dallas na Gevas walikutana na muajiri wao wa kibarua cha ushahidi ambaye alimuuliza maswali mengi Dallas baada ya Dallas kumuuliza yeye. Aliuliza, "Dallas, unadai kuwa umeulizwa aliekuajiri ni nani, kwani umekubali mbele ya mahakama kuwa wewe umeajiriwa?"

    "Ndio, baada ya maswali mengi kunibana, hata hivyo, nimeiambia mahakama kuwa kuajiriwa kwangu kulikuwa ni kumnasa muhalifu na sio ushahidi. Jambo la ushahidi limekuja baadae, baada ya kumtia mbaroni muhalifu na kuonekana kuwa nitakuwa shahidi kwa kuisaidia Jamuhuri dhidi ya Dokta lmu!"

    Muajiri alimuuliza swali jingine Dallas kwa sauti ya hofu ya kupoteza kesi.

    "Hebu bwana Dallas niambie, wewe nimeambiwa kuwa una uzoefu wa mahakama na kesi, je kesi hii inaendeleaje mpaka sasa? Unafikiri Dokta lmu ataingia hatiani?"

    Dallas alimuangalia yule kijana muajiri wao na kumwambia kwa kumuuliza.

    "Hivi wewe wasi wasi wako ni nini? Dokta lmu ndie mtuhumiwa, na yupo ndani hivi sasa au kuna mtuhumiwa mwengine?"

    “Hapana. . .hapana, ninauliza tu, si unajua kesi inayosimamiwa na wakili? Mambo yanaweza kubadilika na Dokta lmu akaachiwa huru bila kuadhibiwa."

    Naye Dallas alimuuliza muajiri wao kwa sauti ndogo yenye wasi wasi.

    "Samahani boss, uliniambia kuwa Mwanamtama alitolewa mimba wakati wa mchana, ambao mimi sikuwepo, ama sivyo?"

    "Ndio hivyo! Kuna nini kwani?"

    "Sasa kuna utata hapo, huko mahakamani inasemekana kwa•wakati huo, Dokta lmu alikuwepo sehemu nyingine, na mashahidi wapo!"

    Muajiri alionesha kuchanganyikiwa kidogo, alibabaika na baadae kusema, "Dokta Imu ni mjanja kuliko anavyoonekana, inawezekana ikawa alikwisha lifahamu hilo jambo la kuwa sehemu mbalimbali kwa wakati mmoja na akalifanyia kazi. Linapotolewa ushahidi uwe macho. Njia ya muongo ni fupi, atapatikana tu!"

    Dallas alimwambia bosi wake huyo ambaye yeye na Gevas walizowea kumwita kwa jina la “Bosi.”

    “Niinawaomba nyote wawili muwe munahudhuria mahakamani wakati kesi inaendelea kusikilizwa. Kwa kufanya hivyo, mtanipa moyo wa kujiona siko peke yangu. Ingawa Mwanasheria Ndugu Mkuki yupo lakini ninahitaji zaidi kuwepo kwenu ninyi."

    Bosi alijibu haraka haraka na kusema, "Lakini Gevas si unaye? Si yeye anahudhuria mahakamani?"

    "Bosi, Gevas pekee hatoshi, afadhali mngekuwa mnakuja nyote wawili. Tafadhali bosi, naomba kesho kutwa na wewe ufike mahakamani mtanisaidia sana katika kujenga hoja ya maana pale ambapo labda ningekwama ... iwapo mtapata nafasi ya kusikiliza kesi hii inavyoendelea."

    Gevas aliyekuwa amekaa kimya kwa muda wote huu, naye alitamka neno la kumuunga mkono Dallas kwa kusema, "Nadhani ombi la Dallas ni la maana Bosi, kwa sababu waswahili wanasema 'Vichwa viwili ni bora kuliko kichwa kimoja', kwa hiyo tutakapokuwa sisi sote tupo mahakamani, na sote tunasikia kipengele ambacho labda kinambabaisha Dallas katika kusikilizwa kwa kesi, tutakapo kutana tena nje ya mahakama kama hivi sasa, tutaweza kujadili na kupata ufumbuzi."

    Boss alionekana kuridhika na maneno ya Gevas, kwa hiyo alikubali na akasema, "Basi vizuri Dallas, mimi na Gevas tutahudhuria mahakamani kusikiliza kesi, na kukupa msaada angalau wa kimorali, sasa hebu nikumbushe Dallas…umeniambia kesi yenyewe itasikilizwa tena lini?"

    Dallas bila kusita alimjibu boss wake kwa kumkumbusha.

    "Ni kesho kutwa Bosi, tuna leo na kesho tu."

    "Basi vizuri, tutakuwa pamoja mahakamani hapo keshokutwa."



    Siku hiyo ya kesi ilipofika, kama kawaida jamaa zake Dokta Imu wote walikuwepo, isipokuwa mama yake. Dokta Imu alipoingia kizimbani, alionekana amedhoofu kuliko kawaida. Alionekana kupoteza matumaini, hakuwa na furaha kabisa na sura zake nzuri zilionekana kuwa zimezeeka kuliko umri wake. Kufikia siku ile alielewa kila kitu kilichotokea baina ya Amani, Mzee Majaliwa na Dallas. Amani alikwenda mahabusu na kumuelezea, kabla ya siku hiyo ya kesi. Hivyo Dokta Imu alitambua kuwa wale aliokuwa amewategemea mno katika kesi ile ambao ni Amani na Mzee Majaliwa, sasa wamekuwa jamaa zake wa damu Dallas ambaye ni mkandamizaji katika kesi ile. Jambo hilo lilipoteza matumaini ya Dokta lmu na kwa hali alivyoonekana ki-wajihi, kila aliyekuwa jamaa yake alisikitika. Kwa muda mfupi huo wa kuahirishwa kesi, Dokta lmu alidhoofu sana. Alijiinamia hapo hapo alipokuwa kizimbani, hakutaka kuangaliana na mtu yeyote. Mtu aliyepata taabu zaidi kutokana na hali hiyo alikuwa ni Zainabu, kwani kila alipomtupia jicho Dokta lmu na kumuona hali aliyokuwa nayo, machozi yalimtoka. Jambo ambalo lilimzidisha Zainabu kulia zaidi siku hiyo ni kuwepo kwa Dokta Faimu hapo hapo mahakamani.

    Dokta Faimu wakati anaingia chumba cha mahakama alikutana uso kwa uso na Zainabu, na salam zake Dokta huyo kwa binti huyo zilikuwa ni kumwambia, "Nadhani kwa sasa umekwisha fahamu kuwa boyfriend wako ni mtu wa aina gani. Leo hii nimefika hapa, ili utakapothibitishwa uhalifu wa rafiki yako Dokta Imu, utakubaliana na mimi, na ni matumaini yangu kwamba utalitumia bega langu kwa kulia na kudondosha machozi."

    Zainabu hakutaka kumjibu kwa maneno bali alimpiga msonyo wa nguvu na kutema mate.

    Amani alionekana kuwa mtu mwenye kujiamini na furaha mno siku hiyo pamoja na kuonesha utulivu. Mzee Majaliwa hakuwa na raha kabisa. Mzee Musa na Jabir walionekana kuwa watulivu na wapole mno. Mama yake Zainabu na Fatima, wao walikuwa wakionekana kumbembeleza na kumfuta machozi Zainabu. Dallas naye alikuwa mpole mno siku hiyo kuliko kawaida yake. Kama alivyokuwa Dokta lmu, naye pia alikwepa sana macho ya watu. Yeye ndiye aliyeulizwa kwanza baada ya kesi kuanza. Hakimu alimuuliza, "Ndugu Dallas, kutokana na yote uliyosema yanayohusu ushahidi wako dhidi ya mtuhumiwa Dokta lmu, je unalo lolote la kuongeza?"

    Dallas alijibu swali hilo pasipo kumuangalia mtu yeyote.

    "Hapana muheshimiwa, sina la kuongeza!"

    Hakimu aliandika na kisha akaiacha kalamu yake juu ya karatasi na kumuangalia ndugu Zablon Mkuki na kumuuliza, "Una lolote la kuongeza au kusema?"

    Zablon Mkuki alisimama, akajipinda kidogo mbele ya Hakimu, kisha akamuelekea Dallas

    na kumuuliza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ndugu Dallas, kwa hiyo unaihakikishia mahakama kuwa Dokta Imu ndiye aliyemtoa mimba marehemu Mwanamtama na kusababisha kifo chake?"

    Dallas alinyamaza kimya kama vile anayefikiria kitu. Ndungu Mkuki alirudia tena.

    "Ndugu Dallas, unathibitisha kuwa Dokta lmu ndiye aliye na hatia ya tuhuma za kusababisha kifo cha mwanamtama?"

    Dallas alinyanyua uso wake, akatupa jicho Zainabu pale alipokuwa amekaa

    Dallas alinyanyua uso wakeakatupa jicho la kumuangalia Zainabu pale alipokuwa amekaa katikati ya wasikilizaji, kisha akageuza uso wake na kumuangalia Dokta Imu pale kizimbani. Waliangaliana na Dokta lmu kwa sekunde kadhaa kisha Dallas alirudisha macho yake na kuangalia chini.

    Alitikisa kichwa kukataa.

    Miguno ikasambaa mahakamani.

    Ndugu Mkuki alihamaki kidogo kwa tendo hilo la Dallas kukataa kwa kichwa. Alimuuliza

    kwa kufoka, "Una maana gani kukataa kwa kichwa? Una maana umeiambia mahakama uongo?"

    Dallas alimuangalia hakimu na kusema, "Hapana muheshimiwa, sijaiambia mahakama uongo. Nitakaposema kuwa ninathibitisha kwamba Dokta Imu ana hatia, nitakuwa ninatoa hukumu,jambo ambalo sijui, wala sio kazi yangu. Nitakaposema kuwa Dokta Imu amemtoa mimba Mwanamtama nitakuwa ninasema jambo ambalo sikulishuhudia.

    “Lakini nimekwisha iambia mahakama kuwa mimi nimekodishwa kwa ajili ya kumtia mbaroni Dokta lmu, na nimefanya hivyo na nikasema jinsi nilivyomkamata Dokta lmu, huo ulikuwa ndio ushuhuda wangu"

    Ndugu Mkuki alimgeukia Dallas na kumwambia kwa kufoka, "Wewe Dallas unataka kubadilisha ushahidi wako hapa mahakamani kwa sababu umegundua kuwa wakili wa mtuhumiwa ndugu Amani ni mdogo wako? Unataka kucheza na mahakama?"

    Dallas alibisha "Hapana mheshimiwa, sithubutu kuichezea mahakama, lakini ninalosema ni kweli kuwa sikushuhudia Dokta lmu alipokuwa anamtoa mimba Mwanamtama, na kama jambo hilo ndilo lililomtia hatiani, siwezi kuthibitisha hatia hiyo!"

    Gevas aliyekuwa pembeni mwa chumba hicho amekaa yeye na bosi, alikunja uso kidogo, lakini bosi mwenyewe alikasirika kabisa na kupiga mguno mkubwa uliowafanya waliokuwa karibu na yeye wageuke na kumuangalia. Ndugu Mkuki kwa hasira alimgeukia hakimu akainama kidogo kasha akaenda palipo kuwa na kiti chake akakaa.

    Amani alisimama akaomba kusema na akaruhusiwa na hkimu.

    Alianza kwa kusema, "Muheshimiwa hakimu, nilikwisha kuiambia mahakama hii kuwa Dallas ni muongo, wakili muendesha mashtaka Ndugu Mkuki akanipinga. Lakini sasa atakubaliana na mimi kuwa Dallas ni muongo!" Alipofika hapo alitulia kidogo. Dokta lmu aliyekuwa amejiinamia alinyanyua uso wake taratibu na kumuangalia Amani kwa macho ya kutoamini kama ni yeye kweli anayemsema Dallas kwa ajili yake. Wakili Amani aliendelea kusema, “Lakini muheshimiwa, kitu kimoja kizuri kuhusu Dallas ni kuwa, hasemi uongo mtupu, analosema lina kweli ndani yake. Anakiri kuwa yeye hakushuhudia kitendo cha utoaji wa mimba. Kwa hiyo upo uwezekano kuwa Dokta lmu siye aliemtoa mimba Mwanamtama. Pia Dallas anakiri kuwa yeye amekodishwa kumtia mbaroni mtuhumiwa, na ameifanya kazi yake hiyo, pamoja na uongo aliousema kuwa yeye ni binamu wa marehemu…Sasa labda tumuulize kitu kimoja au viwili ndugu Dallas..." Amani aligeuka na kumwendea Dallas pale kizimbani aliposimama na kumuuliza.

    "Ndugu Dallas uliambiwa au ulishuhudia kuwa Dokta Imu amemtoa mimba Mwanamtama?"

    Dallas alijibu kwa sauti ya huzuni kidogo, "Mimi niliambiwa, sikushuhudia!"

    "Uliambiwa ilikuwa ni saa ngapi tendo hilo lilipotokea?... hilo la kutoa mimba?"

    "Nimeambiwa ilikuwa ni majira ya mchana ... adhuhuri!"

    Kabla Amani hajaendelea ndugu Mkuki alinyoosha mkono, akasimama na akaruhusiwa kusema, ndipo alipoiambia mahakama.

    "Muheshimiwa hakimu, uongo au ukweli wa Dallas bado haujamfanya Dokta Imu kuwa hana hatia ya kumtoa mimba Mwanamtama. Yeye hakushuhudia lakini ameambiwa, na ametumiliwa kumnasa Dokta lmu na bahati nzuri amempata, basi sasa nini tena?"

    Amani alipomsikia Mkuki anasema hivyo, alitabasamu, kisha naye akamgeukia hakimu na kumwambia, "Muheshimiwa hakimu, la ajabu ni kuwa kwa siku hiyo, inayosemekana Mwanamtama ametolewa mimba, tarehe hiyo na wakati huo, Dokta lmu hakuwepo ndani ya nyumba ya Upanga pahali ambapo tukio hilo limetokea, yeye Dokta lmu alikuwa maeneo mengine ya jiji hili, tena alikuwa pamoja na mtu mwengine!"

    Hakimu aliandika kisha akamuuliza Amani, "Huyo mtu aliekuwa pamoja na Dokta Imu kwa siku tarehe na wakati wa tukio la utoaji wa mimba wa Mwanamtama anaweza kupatikana?"

    Amani aliitikia kwa kutabasamu.

    "Ndio muheshimiwa!”

    “Basi na aitwe aje hapa mbele ya mahakama kama shahidi"

    Askari alie!ekezwa na Amani akaenda kumchukua Mzee Majaliwa na kumLeta kizimbani.

    Mzee Majaliwa aLiapishwa kwanza, kIsha akaulizwa na kuombwa aeleze ukweli wa siku na wakati wa tukio, Dokta Imu alikuwa yuko wapi? Mzee Majaliwa alieleza kwa ufasaha kabisa kuwa siku hiyo baada ya swala ya mchana ambayo ni adhuhuri, alikutana na Dokta lmu mpaka majira yanayokaribia alasiri walikuwa pamoja.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzee aliruhusiwa kuondoka pasipo kuulizwa maswali na pande zote mbili. Baada ya hapo, Amani aliomba kuendelea na kumuuliza Dallas. Aliporuhusiwa, alikwenda na kumuuliza, "Samahani Ndugu Dallas, nilikwisha kukuuliza swali hili, lakini kwa vile, sikupata jawabu, naomba nikuulize tena…" Dallas yeye aliitikia kwa kichwa tu. Amani aliendelea, "Naomba uiambie mahakama muajiri wako ni nani? Nina maana huyo aliyekupa kibarua cha kumnasa Dokta lmu!"

    Dallas aliangalia upande ule aliokaa Gevas na Bosi, akamuona bosi amejawa na wasi wasi, na

    anaelekea kumkataza kwa ishara kwamba asimtaje, lakini Dallas alisema pole pole huku akinyoosha kidole upande waliokaa Gevas na bosi "Ni boss...yule pale!"

    Amani aligeuka akaangalia na yeye upande aliokuwa amekaa Gevas na bosi, miguno ikirindima mle mahakamanai, na Amani alitabasamu kidogo huku akitingisha kichwa kukubaliana na Dallas, na akiendelea kumuuliza.

    "Bosi nani, hana jina? Taja jina lake!"

    "Ni Faimu!"

    ******



    Watu wote waliokuwepo chumba cha mahakama waligeuza shingo zao na kuangalia upande aliokuwa amekaa Gevas na bosi, ambapo ni nyuma kwenye kipembe cha chumba cha mahakama. Faimu alionekana dhahiri kuwa anatetemeka, alishikwa na butwaa akawa hawezi kusema wala kutikisika kwa muda wa dakika zaidi ya tano. Bumbuwazi lilimjaa akabaki hapo alipo kama sanamu la jiwe. Aligutuka alipokuja shikwa mkono na askari na kutakiwa apande kizimbani kwa mahojiano.

    Hapo tena sina hata haja ya kukwambia ni jinsi gani Zainabu na Imu walivyokuwa wamebutwaika kwa ushuhuda ule wa Dallas.

    Kule kizimbani Faimu aliulizwa dini yake, kisha akaapishwa. Hata katika kuapa Faimu alianza kubabaik a. Aliombwa ajieleze kuhusu kumuajiri kwake Dallas na nini anajua kuhusu Dokta Imu na marehemu Mwanamtama. Faimu aliieleza mahakama kuwa anavyofahamu yeye ni kuwa Dokta Imu ni 'boyfriend' wa Mwanamtama,na yeye anao uhusiano wa udugu na marehemu, kwa hiyo alijua kuwa Dokta Imu amempa mimba Mwanamtama. Alishindwa

    hata jinsi ya kujieleza. Ilipofika wakati wa maswali, Amani alipewa nafasi ya kumuuliza Faimu, ndipo alipoanza kumuhoji.

    "Faimu unafanya kazi gani?!"

    "Mimi ni Daktari!"

    "Unafanya kazi wapi?"

    "Muhimbili Hospitali…"

    "UnamfahamuDokta lmu?"

    "Ndio, ninamfahamu, ...tunafanyakazi pamoja."

    "Wewe ni Dokta Faimu, yeye ni Dokta Abdulrahim, kwa ufupi, nyote wawili mnajulikana kama Dokta lmu au sio?"

    Faimu alinyamaza kimya, na kutulia kama vile hayupo. Amani aliendelea kumuuliza

    "Dokta Faimu wewe ndie Dokta lmu, boyfriend wa marehemu Mwanamtama!"

    "Hapana!"

    "Wewe ndie uliyejaribu kumtongoza mchumba wa Dokta lmu…Abdulrahim, anayeitwa

    Zainabu!"

    "Hata, Hapana…”

    "Wewe umewahi kupatilizana kimameno na Dokta Abdulrahim vile vile kwa ajili ya Zainabu na ukamtishia Dokta mwenzako huyo kuwa utamfanyia na atakutambua!"

    "Hapana hatujawahi kugombana, simfahamu Zainabu!"

    "Wewe Dokta Faimu, marehemu Mwanamtama alikuwa ni msichana wako kwa muda mrefu!"

    "Si kweli, hakuwa msichana wangu!"

    "Baada ya wewe kukataliwa na Zainabu na kugombana na Dokta Abdulrahim, na ulipogundua kuwa tayari umekwisha mtia mimba Mwanamtama, uliona hapo hapo ndipo pa kuchukua kisasi cha kukataliwa na Zainabu kwa mchumba wake Dokta Abdulrahim."

    "Hapana sio kweli!"

    Faimu alijibu huku akihema hema kama vile anayekimbizwa. Amani naye aliendelea kumueleza pasipo kujali kukataa kwake.

    "Dokta Faimu, kwa kuwa ulitambua kuwa wewe ni daktari na Abdulrahim naye vile vile ni daktari, uliona kuwa kisasi chako kilikuwa ni rahisi na hasa kwa vile pia majina yenu yana tajika kwa kufanana Imu na Imu…na ndipo ulipopanga mipango na kumshawishi Mwanamtama aitoe mimba uliyokuwa tayari umempa."

    "Siyo hivyo, bwana Amani!"

    "Kama sio hivyo ni vipi basi?”

    Faimu alinyamaza kimya asijue la kusema.

    Amani aliendelea.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ulimshawishi na kumkazania atoe mimba. Tena utamtoa wewe mwenyewe!"

    Faimu alipofikishwa hapa,alionekana kuishiwa na nguvu kabisa. Ubaramaki wake wote ulikwisha. Wakati huo mahakama yote ilikuwa kimya. Yule aliyekuwa akionekana dhaifu na mnyonge kuliko wote wakati kesi hii inaanza kusikilizwa, Dokta lmu, sasa alionekana mwenye uso mng'avu na uliojaa nuru ya matumaini. Halikadhalika na Zainabu naye, kwa mara ya kwanza tangu afike kwa siku hiyo, uso wake ulionekana kuwa mkavu, hauchirizikwi na machozi.

    Amani aliendelea kumuandama Faimu kwa maelezo ya mambo yake yalivyokuwa.

    "Wewe ndiye ulimshawishi na kumkazania Mwanamtama aitoe mamba yake!"

    "Hapana mimi siye niliemshawishi"

    "Wewe ndiye uliyemkazania uitoe wewe mwenyewe mimba hiyo!"

    "Siye mimi!"

    "Ni wewe!"

    "Nasema si mimi!"

    "Nasema ni wewe!"

    "Si mimi!"

    "Ni wewe!"

    "Ni yeye mwenyewe ndiye aliyeniambia nimtoe mimba!”

    Chumba kizima cha mahakama kilijaa sauti za miguno na mastaajabu kutoka kwa wasikilizaji.

    Amani alimgeukia Hakimu.

    "Muheshimiwa, Dokta Faimu ambaye naye anajulikana kwa jina la Dokta lmu, ndiye aliyekuwa 'boyfiend' halisi wa marehemu Mwanamtama. Pamoja na kuwa ni Daktari, Faimu ni kijana anayependa sana wasichana kwa mahusiano ya ngono. Anao uhusiano wa kimapenzi ya ngono na wasichana wengi. Lakini wasichana wote hao, huwa hana uhusiano nao wa kudumu. Msichana pekee alieweza kudumu nae kwa muda mrefu alikuwa ni Mwanamtama. Msichana huyu ambae kwa sasa ni marehemu, alimpenda sana Faimu, kiasi cha kuwa hakuzijali dosari zake, lakini kwa upande wa Dokta Faimu, yeye alimtumilia tu Mwanamtama kwa jinsi na namna alivyotaka bila ya kujali hisia zake.

    “Dokta Faimu siku alipomuona Zainabu ambaye ndiye 'girlfriend' wa Dokta Imu ambae ni Abdulrahim, aliYekwenda hospitali ya Muhimbili kwa kumpeleka mama yake, Faimu aLimtongoza, Zainabu akakataa. Habari hizi zilitambulika kwa Dokta

    Imu Abdulrahim, ndipo walipo patilizana ki maneno…na ndipo Faimu alipodhamiria kumuonesha Abdulrahim na Zainabu vile vile. Wakati Dokta Faimu anadhamira hiyo ya kuwahujumu Zainabu na boyfriend wake, ikatokea kuwa 'girlfriend' wake yeye ambaye ni Mwanamtama ana mimba. Ndipo alipopanga mikakati thabiti ya kumuhusisha Abdulrahim na mimba ya Mwanamtama.

    “Muheshimiwa hakimu Dokta Faimu anaishi Mikocheni, lakini anayo nyumba ya shirika la nyumba la Taifa iliyopo Upanga, nyumba hiyo yeye ameachiwa tu na dada yake na shemeji yake ambao ndio wapangaji hasa wa nyumba hiyo. Wao wamekwenda Canada. Faimu, ndiyo anaifanya nyumba hiyo kuwa ni makutano yake makubwa na wasichana. Kwa hiyo alimchukuwa Mwanamtama kwenye nyumba hiyo ambayo si mgeni nayo, na kumshawishi amtoe mimba. Mwanamtama alipokubali alimpangia siku na tarehe hiyo ya tukio. Baada ya kufanya shughuli na kuona amefeli alitafuta watu wa kumnasa Dokta Abdulrahim, ndipo alipowaajiri Dallas na wenzake.

    “Dallas akachaguliwa kufanya kazi hiyo kwa vile aliwaeleza kuwa kutakuwepo na masuala ya kuhojiwa baada ya kumpata Abdulrahim. Lakini Faimu aliwapa maelezo wakina Dallas ya kuamini kuwa yupo mtu aitwaye Dokta Imu ndiye aliyeifanya kazi hiyo ya kumtoa mimba Mwanamtama. Dallas bila kutambua anachofanya, alipokea maagizo yote toka kwa Faimu pamoja na nambari za simu ya Dokta Imu, Abdulrahim. Pamoja na yote niliyosema muheshimiwa zipo picha alizopiga Faimu na Mwanamtama wakati wa uhai wake, wakiwa katika starehe."

    Amani alizipeleka picha zikapokelewa na kupewa hakimu, kisha akaendelea, "Muheshimiwa hakimu, kitu gani kilifanyika baada ya hapo, mahakama yako tukufu imekwisha pata maelezo toka kwa Dallas, mashahidi wengine pamoja na mtuhumiwa Dokta lmu pia anayejulikana kama Abdulrahim. Kwa hiyo muheshimiwa, mtuhumiwa halisi wa kesi hii ni Dokta Faimu ambaye pia anajulikana kama Dokta lmu. Naiomba mahakama yako imtie hatiani kij:ana huyu Faimu, na kumuachia huru Abdulrahim ambaye ametiwa katika tuhuma zisizomuhusu kwa makosa."

    Baada ya hapo Amani aliinama kidogo mbele ya hakimu akarudi kitini pake na kukaa kitako. Mahakama nzima ilipiga kimya. Hakukusikika sauti ya kiumbe chochote Zaidi ya mihemo ya watu na vikohozi vya hapa na pale.

    Hakimu alikuwa ameshughulika na kuandika. Faimu nae hapo alipokuwa amesimama kwenye kizimba alijiinamia kwa uso wake kuuelekeza chini, jasho jembamba lilikuwa linamtoka kila sehemu ya mwili wake, alijaribu kuyakwepa macho ya watu wotewaliokuwepo mahakamani hapo, ambayo yote yalikuwa yakimuangalia yeye.

    Aliyakwepa kwa kuanza kufikiria ni adhabu gani itakayotolewa?

    Akiwa amezama katika mawazo hayo, hakusikia alipoulizwa na hakimu, aligutuka aliporudiwa kuulizwa tena kwa mara ya pili.

    "Ndugu Faimu, ninakuuliza wewe…unalo lolote la kusema kuhusu tuhuma ulizotupiwa na wakili mtetezi Amani?!"

    Faimu alionekana kugwaya kiasi cha kutia huruma, ghafla alionekana kumbe siye baramaki, siye mchangamfu, siye jasiri wala mwenye ujanja wa kupanga mambo. Hakuwa na la kujibu isipokuwa machozi mengi kumtiririka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipoonekana kuwa hana la kunena, hakimu alimuuliza ndugu Zablon Mkuki kama ana chochote cha kuongeza. Yeye alisimama na kumwambia hakimu kuwa hana chochote cha kuongeza.

    Hakimu aliuliza upande wa mashtaka na upande wa utetezi kwa ujumla iwapo kuna lolote la kusema, au kama yuko shahidi yeyote anayehitaji kufika mahakamani.

    Kutoka pande zote mbili jibu alilopata ni kuwa hakuna la kuongezwa.

    Kwa hiyo aliamuru Faimu atiwe ndani kama mtuhumiwa wa pili na kuahirisha mahakama na kutaja siku ambayo ndio itakayotolewa hukumu.

    Faimu wakati anachukuliwa alikuwa analia kama mtoto mdogo.

    Hakimu alikataa kuwa kuna dhamana yoyote inayokubaliwa kwa ajili yake. Hakukubali dhamana kwa ajili ya Dokta lmu vile vile. Lakini Dokta lmu mwenyewe hakuonekana kujali. Siku hiyo alisalimiana na jamaa zake kwa furaha mno, alipeana mikono na Mzee Musa, Jabiri, Mzee Majaliwa, Zainabu, mama yake Zainabu na Fatima, lakini alipofika kwa Amani, hakujizuia. Alimkumbatia na kusema, "OH, kaka Amani asante, asante sana, sitajali kubaki kwangu ndani kwa siku zilizobaki, naamini Mungu atanisaidia, kwani amekwisha nionesha dalili."

    Wakati huo Dallas alikuwa amesimama kando na kubaki kuwaangalia jamaa zake Dokta lmu wanavyomsali mu. Alishikwa na hamu ya kwenda karibu na lmu kumuomba radhi lakini alishindwa.



    *****



    Wiki moja kusubiri hukumu ya kesi ya Dokta lmu itolewe, ilikuwa ni gumzo katika nyumba za familia ya wahusika wa kesi hiyo. Zaidi lilizuka zogo kubwa nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mwanamtama ambao kwa muda wote wa kesi ya Dokta Imu ilipokuwa inasikilizwa, hawakuonesha kupendezewa. Lakini waliposikia Faimu naye amekamatwa na

    kuhusishwa na kifo cha Mwanamtama, walifurahi na mmoja wao ambaye ni mdogo wake marehemu Mwanamtama alisema kwa mastaajabu.

    "Nashangaa hiyo serikali kuchukuwa muda wote huo kumtambua muhalifu hasa ni nani! Wangekuja kutuuliza sisi kuhusu huyo 'playboy' Faimu na jinsi alivyokuwa akimtesa marehemu dada yetu!''

    Nyumbani kwa marehemu Mwanamtama, Faimu hakuzungumzwa vizuri kabisa.

    Nyumbani kwa mama yake Dokta lmu, wao walizidi kumuomba Mungu kwa njia ya dua na kutoa makafara ili Dokta Imu aachiliwe. Mzee Majaliwa naye hakuchoka kumuombea kila baada ya sala zake.

    Mama yake Amani alikuwa anawataka kila mara Mzee Majaliwa na Dallas wafike nyumbani kwao kwa mzee Mirambo. Kwa hiyo baada ya siku hiyo ya kesi ya kutolewa hukumu kufika, aliwaomba tena Mzee Majaliwa na Dallas waende kwake. Walipanga siku na muda wa kukutana, siku hiyo ilikuwa Jumapili saa za mchana baada ya swala ya adhuhuri, ili kumpa nafasi mzeeMajaliwa ya kuswali kwanza.

    Siku hiyo ilipofika, Amani ambaye bado alikuwa anaishi na baba na mama yake Mirambo

    pamoja na mdogo wake Zainabu kama kawaida, alilolifanya kwanza wakati wa asubuhi ni kwenda kumchukua mama yake Dokta lmu na kumpeleka akaonane na mwanaye kule Mahabusu kama ilivyokuwa kawaida yake.

    Mama yake Dokta lmu alikuwa yupo tayari Amani alipofika huko kwake kumchukua. Alikutwa katika hali ya furaha na matumaini makubwa siku hiyo. Alionekana ni mzima wa

    afya zaidi kuliko ilivyokuwa kawaida yake, kwani pamoja na kuwa yeye hahudhurii mahakamani, lakini baada ya kesi kusikilizwa mara ya mwisho, alikuja kupewa habari zote za yaliyotokea mahakamani, zinazohusu Faimu na jinsi Amani alivyomtetea Dokta Imu.

    Mama lmu alimpokea Amani kwa kumkumbatia mikononi mwake baada ya kusalimiana huku akisema, "Asante mwanangu, asante baba Mungu akubariki, kwa kumsaidia lmu na kumtoa katika janga hili…"

    Amani hakutaka mama huyo apate furaha kikamilifu kwa wakati huo, kwahiyo, alimkatisha mazungumzo ya shukrani zake kwa kumjibu, "Mama wakati bado kwanza wa kutoa shukrani, na tusubiri mpaka lmu atakapoachiwa huru"

    Mama lmu alitabasamu na kutoa mguno wa furaha kisha akamwambia,"Baba mwanangu Amani, mtu asiposhukuru kwa kidogo Mungu alichompa, basi hata kikubwa pia hatashukuru. Kwa vyovyote hukumu itakavyokuwa, wewe umekwisha fanya kazi yako ya kumtetea lmu inavyostahili. Kwahiyo huna budi kushukuriwa, mengine tumwachie mwenyewe Mwenye- ezi Mungu"

    Amani alijiwa na hisia za upendo kwa mama huyu baada ya kusikia maneno haya, nae kwa ghafla akamkumbatia tena na kumwambia, "Asante sana mama kwa kunishukuru, na lolote litakalo tokea kwa lmu, kama nilivyo ahidi tangu awali tulipokutana mimi na wewe kuwa utabaki kuwa mama yangu nami naomba niwe kama alivyo lmu kwako."

    Mama yake lmu tayari alikuwa anatoa chozi la furaha na akamuambia, "Ninatoa ahadi kwako Amani, kuanzia sasa wewe utakuwa kama mwanangu wa pili, kwani lmu, atakuwa hakupata shemeji tu kwa wewe, bali pia amepata kaka na rafiki wa kweli"



    "Kaka Amani, kwa hali halisi niiyonayo hivi sasa, kati ya mimi, mama na wewe Aman, hata kama hukumu ya kesi yangu itakuwa ni mimi kunyongwa, basi nitakufa nikiwa niko radhi, kwani naamini mama yangu nitamuacha katika mikono ya mtoto wake mwingine ambaye ni wewe. Najihisi nimepata kaka kwako wewe, kwa hiyo wacha nianze kukushukuru bila kujali hukumu itakuwaje!" Alimwambia huku akimuangalia machoni.



    Amani alijihisi yuko katika hali ya upendo na ukaribu mno na watu wawili hawa, mtu na mama yake. Pasipo kujijua alimvuta lmu kutoka mikononi kwa mama yake na kumkumbatia na kusema huku macho yake yametota machozi ambayo anajikaza yasidondoke "lmu usiseme hivyo, ya kuwa wewe utanyongwa, hapana, tafadhali lmu mdogo wangu usiseme hivyo. Utaachiwa huru na mimi na wewe tutamtunza, kumpenda na kumlea mama yetu"

    Wote wawili waliachiana na kwenda kumkumbatia mama yake lmu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *****

    Saa saba na nusu mchana Amani alikuwa yuko pamoja na Dallas ndani ya gari la Dokta lmu ambalo ndilo analolitumia Amani kwa sasa, hasa siku za kwenda kumpeleka mama yake lmu mahabusu. Walikuwa wanaelekea msikitini kumchukua baba yao Mzee Majaliwa. Kimya kilitawala safari yao hiyo, lakini hatimaye Dallas alivunja kimya hicho kwa kumuuliza Amani kwa sauti ya chini.

    "Mani?!"

    "Naam!"

    "Unafikiri ni nini itakuwa hatima ya kesi hii?”

    "Sheria ndiyo itakayo hukumu…"

    Walikuwa wamefika msikitini, na bila kupata taabu ya kuulizia waliweza kumuona Mzee Majaliwa tayari anawasubiri. Amani aliegesha gari karibu naye, Dallas haraka aliteremka akamsalimu baba yake kasha akamuongoza kuingia garini kiti cha mbele kushoto kwa dereva. Alipoingia, wakati anasalimiana na Amani, Dallas alifungua mlango wa nyuma, akaingia na kukaa kiti cha nyuma.

    Amani aliondoa gari na kuanza kuendesha kuelekea Masaki kwa Mzee Mirambo. Dallas alianza kuendeleza mazungumzo yao kwa kuuliza, "Enhe Mani, unasema sheria ndiyo itakayohukumu, lakini wewe ni mwanasheria, unafikiri itakuwaje?”

    Amani aliendelea kuendesha taratibu, kisha akamjibu kwa sauti ya kawaida.

    "Kesi hii mpaka sasa kutokana na uzoefu na ujuzi wangu, naona hukumu itakuwa sio mbaya

    kwa Imu, na ni mbaya kwa Faimu na ni. . . ni. ..haieleweki itakuwaje kwako wewe!"

    Dallas alicheka kisha akasema, “Kwa hali yoyote ile itakavyokuwa, hata kama nitanyongwa, na nife, nitakufa nikiwa niko radhi, kwani naamini baba yangu nitamuacha katika mikono ya mwanaye ambaye ni wewe, akiwa katika hali ya usalama. Nina muomba Mungu yule kijana wa watu Dokta lmu aachiwe huru tu."

    Baada ya hapo Amani aliendesha, hali ikawa ndani ya gari hiyo ni kila mtu yumo ndani ya mawazo. Hatimaye Amani alimuuliza Dallas.

    "Dallas, inaonekana unahisi mimi sikupendi kabisa... unahisi ninakuonea au vipi?”

    Dallas alipiga kimya kwanza, kisha akarudisha pumzi kwa nguvu, kama vile amekata tamaa na kusema kwa sauti hiyo hiyo ya kukata tamaa.

    "Sikulaumu hata kidogo mdogo wangu Mani. Hata usiponipenda, unayo haki ya kufanya hivyo. Ninalotaka mimi uliamini ni kuwa mimi ninakupenda sana kama mdogo wangu. Nilipodhani kuwa nimepoteza jamaa wote wa familia yangu, nilikuwa nikiwakumbuka sana, lakini nilimkumbuka zaidi Mani ambaye ni wewe. Leo hii Mungu amenioneshea kuwa baba yangu yu hai na mdogo wangu Mani pia yu hai, ambao wanaweza kuendesha maisha. Mani akim.saidia baba, basi mimi hata nikifa potelea mbali!"

    Amani alikuwa amefika karibu na nyumbani kwao.

    Alisimamisha gari aliyokuwa anaiendesha na kuiegesha kando ya barabara. Kisha akageuza kichwa na kumuangalia Dallas, akacheka kidogo kisha akasema, "Fikiri unavyofikiri kaka, lakini usifikiri kuwa sikupendi. Kuna tabia ya upendo wa ndugu kuonekana kuwa wale wakubwa ndio wanao wapenda wadogo zao, au wazazi wanawapenda watoto wao zaidi kuliko watoto wanavyowapenda wazazi wao, lakini hata wadogo wanawapenda wakubwa zao vile vile…isipokuwa sio aghalabu kuwaonesha pendo lao, sababu wadogo mara nyingi huwa wanadeka. Nataka uamini kuwa ninakupenda kaka Abdallah ambae ni wewe.

    “Na ni leo tu huko ninakotoka nimegundua kuwa wapo watu wawili wanaonipenda kama ndugu yao wa damu, nao ni Dokta lmu na mama yake… sasa mimi chuki nitazitoa wapi? Ninaoujua ni upendo tu na sio chuki. Kwa hiyo siwezi kumchukia mtu. Ninakupenda kaka

    Abdallah, hata nikikuita Dallas, Dulla, Abdul au Abdi, lakini ndani ya moyo wangu utabaki kuwa ni kaka yangu Abdallah Bin Bilal Majaliwa."

    Baada ya maelezo hayo marefu yaliyotoka kwa Amani, Dallas alijihisi vizuri mno nafsini mwake.



    *****

    Katika mkutano huo waliokutana nyumbani kwa Mzee Mirambo, watu wote walionekana kuwa na furaha na zaidi alikuwa Zainabu. Walikula, kunywa na kuzungumza. Sehemu kubwa ya mazungumzo yao ilikuwa na habari za lmu na mama yake. Mzee Majaliwa aliuliza, "Hivi ni kwa nini mama yake Dokta Imu hapendelei kufika mahakamani?"

    Amani alimjibu baba yake huku akicheka.

    "Lakini wewe baba si ulikuwa hutaki kufika mahakamani kabla ya suala hili la ushahidi?"

    "Ni kweli baba Amani, lakini mimi ninazo sababu za kutopenda mahakama . . . samahani sana wewe na baba yako mzee Mirambo, lakini mimi ninaona sharia hazichukuliwi ipasavyo, hasa inapofika kwenye ushahidi, hauthibitishwi kuwa ushahidi ni wa kweli au uongo, wanasheria wanatoa hukumu tu wanavyopenda wao na wanaowapendelea, ndio maana sipendi kuona sheria zikififilishwa!"

    Amani alicheka sana kisha akasema kumwambia mzee Majaliwa.

    "Ni kweli kabisa unayosema baba, lakini palipo na kweli siku zote uongo hujitenga." Aliendelea kusema na kujibu swali linalohusu mama yake Dokta Imu, "Mama yake Dokta lmu ni mgonjwa wa presha , na lmu ni mtoto wake wa pekee, ambaye baba yake alifariki zamani. lmu amekuwa mtoto wa karibu sana na mama yake, kwa hiyo mama yake huwa hawezi kuvumilia kuona mtoto wake akivurugwa kwa maswali ya mahakamani… ameamua abaki nyumbani kusikilizia tu!"

    Mzee Majaliwa alikubaliana na wazo hilo na akazidi kusema, "Na hata mimi nakubaliana nae huyo mama…asirnde, kwa sababu mambo yanaweza yakabadilika tofauti na watu wanavyotegemea, mwanamke wa watu akaja kuzimia au kufa mahakamani bure... Mungu ayapishie mbali!"

    Amani alicheka kidogo na kumuuliza tena Mzee Majaliwa.

    "Kwahiyo baba wewe pia hutakuja siku hiyo ikifika?"

    "Siji, sitakuja kabisaa. Nitabaki msikitini nikiwasubiri nyinyi mje mniambie matokeo ya kesi

    ambayo ni hukumu!”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ****

    Siku ya hukumu ya kesi ya Dokta Imu mahakama ilijaa watu tele waliokuwa wakihudhuria kila siku na wengine wengi kuongezeka, wakiwepo jamaa zake marehemu Mwanamtama na jamaa zake Faimu. Ni watu wawili wa karibu na Dokta lmu ammbao hawakuhudhuria,

    Mzee Majaliwa na mama yake mzazi Dokta Imu.

    Hakimu alipoingia watu wote ndani ya mahakama walisimama kisha baadae walikaa baada ya hakimu kuketi kwenye kiti chake kikubwa nyuma ya meza kubwa juu ya membari. Madaktari Abdulrahim (Dokta Imu) na Faimu (Dokta Imu) walisimama pamoja ndani ya kizimba wakiwa kama watuhumiwa.

    Hakimu alifunuliwa faili lililokuwa lipo tayari juu ya meza yake, aliperuziperuzi kidogo, akawaangalia watu waliohudhuria, halafu akarudisha uso wake kwenye faili na kuanza kusoma. Alisoma kesi yote na jinsi ilivyoendeshwa na kueleza ushahidi wa kila shahidi aliyetoa ushahidi katika kesi hiyo. Hatimate alitoa hukumu baada ya kulinganisha kesi ile na kesi nyingine zilizofanana na ile zilizowahi kutokea ulimwnguni miaka iliyopita, na halafu akatoa hukumu wa kesi iliyokuwa mbele yake.

    "Kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapa, kutokana na maelezo aliyojieleza mthumiwa mwenyewe…mahakama imeona kuwa Dokta lmu ambaye ni Dokta Abdulrahim Kasongo hana kosa la kujibu, hivyo inamuachia huru kuanzia sasa hivi. Anao uhuru wa kufanyakazi yake kama ipasavyo na kwenda popote anapotaka."

    Mihemko ya mchanganyiko wa hisia ilisikika kutokea sehemu mbali mbali mle mahakamani. Dokta lmu - Abdulrahim hapo kizimbani aliposimama, alitulia tuli bila kutikisika, ni mapigo ya moyo tu yaliyokuwa yakimpiga, ndiyo aliyoyahisi, pamoja na machozi ya furaha yaliyokuwa na joto kali yaliyotiririka juu ya mashavu yake.

    Kabla ya mtu yeyote kufanya lolote, hakimu aliendelea kusema.

    "Zaidi ya yote hayo, mahakama inamtia hatiani Dallas kwa kosa la kuiambia uongo mahakama, yaani kwa kutoa ushahidi wa uongo pale aliposema kwa yeye ni binamu yake marehemu Mwanamtama. Pamoja na kuwa baadae alikiri kuwa baadhi ya ushahidi wake haukuwa wa kweli, lakini kwa kutoa fundisho kwa wengine kuwa mahakamani si pahali pa kuchezea, au sheria kuifanya ni bahati nasibu kama alivyofanya yeye kwa ushahidi wa kukodiwa, mahakama inampa adhabu ya kifungo cha nje cha miezi mitatu, awe anaripoti mahakamani kila siku za kazi kasoro siku za sikukuu zilizoruhusiwa na serikali. Adhabu hiyo itaanza tokea leo , akitoka hapa aende akaripoti kwenye ofisi za mahakama"

    Dallas aliinamia chini kisha akanyanyua uso wake wenye tabasamu kubwa likiandamana na machozi.

    Hakimu aliendelea kusema kwa kusoma makaratasi yake.

    “Sasa tunakuja kwenye swala la Dokta Imu mwingine, naye ni Dokta Faimu…”

    Alipofika hapo hakimu alitulia na kumtazama moja kwa moja Faimu, ambaye alionekana wazi kuwa alikuwa akitetemeka na miguu ilikuwa inamshinda kuuhimili uzito wa mwili wake, akawa amejiegemeza kwenye kingo za kizimba, mashavu yakimcheza. Hakimu akazungusha macho kwa watu wote mle mahakamani, kisha akayatuliza tena kwa Faimu.





    "Kutokana na yote hayo yaliyoendeshwa kwa kusikiliza ushahidi wa kila upande, na utetezi wa kila upande, mahakama inamuona kuwa Dokta lmu – Faimu…anayo kesi ya kujibu, kwa hiyo anatuhumiwa kwa kosa la kumtoa mimba Mwanamtama na kusababisha kifo chake. Kesi yake itaendelea kusikilizwa tarehe itakayopangwa. Naye atabaki kuwa ndani mpaka tarehe hiyo. lwapo atakuwa na shahidi au mtetezi yeyote, basi na ajitokeze siku hiyo. Kwa leo mahakama imeahirishwa!”

    Dokta Faimu alilia kama mtoto mdogo hapo kizimbani alipokuwa.

    Umati wa watu ulianza kutimka, Dokta lmu alizungukwa na watu nje ya mahakama, wengi wakimpa pole na wengine wakimkumbatia. Zainabu alimng'ang'ania mkono, hakutaka kuuachia, alitoa machozi ya furaha pasipo kuyazuia.

    Baada ya dakika kadhaa, Dallas alitokea akiwa anatoka ofisi za mahakama. Alisimama kando kama mkiwa. Dokta Imu alimuona hivyo, aliwatenga jamaa zake, akawaacha na akamwendea Dallas pale aliposimama, alipofika alifunua mikono yake naye Dallas hakusita, ilikuwa ni kama vile ni jambo alilokuwa na hamu nalo kubwa, hivyo alinyanyua mikono na yeye wakakumbatiana huku akisema:

    "Nisamehe Dokta, nisamehe sana!"

    “Usitaje, wala usiombe msamaha kwangu, huna ulilomikosea! Kesi yangu mimi ndio iliyokuponza ukapewa adhabu, kwa hiyo nisamehe mimi!”

    Dallas aliruk a akamshika mabega Dokta Imu kwa mikono yake yote miwili na kumuangalia usoni, kisha akamwambia, "Hapana hapana Dokta zaidi ya yote kifungo cha nje si adhabu ya kutisha kwangu mimi. Ninachokuomba, ni hiki…tafadhali nipe nafasi ya kuwa kama kaka yako, nakuomba uwe mdogo wangu!"

    "Hilo sio la kuomba kaka Dallas, kwa sababu mimi tayari ni rafiki motto wa mzee Majaliwa, kwa hiyo wewe, kwa kuwa mzee ni baba yako tayari u kaka yangu!"

    Baadae Amani alishauri kila mtu arudi nyumbani, alimuomba mzee Musa na Jabir waende wakamfahamishe matokeo ya kesi mama yake Dokta lmu. Na akashauri kuwa yeye, Dallas na Dokta lmu watakwenda kumchukuwa mzee Majaliwa, kisha kwa pamoja watakwenda naye nyumbani kwa mama yake lmu.

    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzee Majaliwa alikuwa tayari yupo nje ya Msikiti wakati Amani, Dallas na Dokta lrnu, wanawasili ndani ya gari ndogo ya Amani. Gari ilipoegeshwa tu, Dokta Imu alitoka kwanza na kumkimbilia Mzee Majaliwa, alionekana kuwa na furaha kubwa mno. Mzee Majaliwa alikumbatiana kw anguvu na Imu, kasha akawageukia Amani na Dallas, akawaambia, "Wanangu, ninyi bado hamjawahi kutiwa ndani kwa jambo la kusingiziwa, mimi ninaijuwa taabu aliyokuwa nayo huyu kijana, kwa hiyo leo nina furaha kubwa mno kwa ajili yake Alhamdulilah! Haya sasa niambieni tunaelekea wapi kwa siku hii ya leo ya furaha?"

    Amani alimjibu mzee wake huku na yeye akiwa ameridhika na furaha ya baba huyo.

    “Baba tutakwenda kwa mama yake Dokta lmu, sote pamoja na wewe halafu leo jioni sote pamoja na mzee Musa na familia yake tunakutana kwa mzee Mirambo…unasemaje?”

    “Mimi sina la kusema kwa leo kila kitu ninakiona ni cha furaha kwangu, kwa hiyo lolote utakalolipanga wewe baba Amani ni sheria, kwa hiyo mimi nitafuata tu mwanasheria wangu . ..Haya twendeni!"

    Waliingia ndani ya gari na kuelekea Kinondoni Hananasifu kwa mama yake Dokta lmu.

    Mama yake Dokta lmu alikwisha pashwa habari za matokeo ya hukumu ya kesi ya mwanawe na ujio wa Dokta lmu akiwa na hao jamaa zake watatu. Kwa hiyo mlango ulipogongwa, yeye aliamua kubaki sebleni na mzee Musa na mkewe, pamoja na mke wa Jabir. Mzee Musa alimwambia Jabir aende akafungue mlango huo.

    Aliwakaribisha wageni kwa furaha na uchangamfu. Dokta lmu ndiye alikuwa ametangulia, kwa hiyo moja kwa moja alikwenda akamkumbatia mama yake, sababu wote wengine walikuwepo mahakamani. Baada ya kulizana na mama yake kwa furaha. Mama alimuacha lmu na kugeuka kutaka kuwakaribisha wageni…ndipo aliposhikwa na butwaa baada ya kumuona mzee Majaliwa.

    Walibaki kutazamana bila kusema kitu kwa dakika zisizo pungua mbili, mwishowe mzee Majaliwa kwa sauti ya chini ya kujikaza alitamka kwa kusema kwa kuuliza:

    "Mama Abdallah?!"

    Naye mama yake lmu akajibu,"Baba Abdallah!!"

    "Mke wangu!"

    "Mume wangu!"

    Dallas naye aliyekuwa amekodoa macho karibu yadondoke kwa kumuangalia mama yake Dokta lmu, aliropoka kwa sauti kubwa.

    "MAMAA?"

    Mama yake lmu alipotazama upande alipokuwepo Dallas naye alimuangalia Dallas na kutamka kwa sauti ndogo.

    "Abdallah? Mwanangu Abdallah, uko hai baba?"

    Dallas alikwenda akamkumbatia mama yake kisha wakaachiana, mama akamkaribia mzee

    Majaliwa nao wakakumbatiana, kisha kwa sauti ya kilio cha furaha mama yake Imu alimshika mkono Dokta lmu na kumwambia mzee Majaliwa, "Baba Abdallah, huyu ni Abdulrahim…mtoto wetu afiyekuwa mchanga!"

    Marna lmu kama vile aliekuwa amepangawa kwa furaha, alimgusa Dallas na kumwambia, "Abdallah huyu ni Abdulrahim mdogo wako aliyekuwa bado mchanga unamkumbuka?"

    Dallas alishikwa na bumbuwazi hali kadhalika Dokta lmu, na Amani pia. Dallas na Imu walibaki wakiangaliana kwa kutoamini. Mama lmu ndiye aliekuwa akisema sana jambo lililoshangaza wote kwani siku zote mwanamke huyo alionekana kuwa na mawazo na ni mkimya mno. Aliendelea kufanya utambulisho kwa mzee Musa na mkewe na watoto wao.

    “Kaka…wifi, huyu ni mume wangu niliyedhani amefariki. Na huyu ni mwanangu wa kwanza anaitwa Abdallah. Tulipochomewa nyumba mimi na mtoto wangu mchanga ambaye ni lmu, nilikuwa nimekwenda shamba na nyumbani nilikuwa nimemwacha Mani na mkwe wangu na mwanangu mwIngine Abdlraahmani. Abdallah na baba yake wao walikuwa wamekwenda Magu siku hiyo, lakini niliambiwa jinsi mume wangu aliporudi, alivyopigwa na kuchomwa moto. Niliamini na Abdallah naye alifariki. Mimi nilikimbia na kupanda gari moshi na kuja hapa Dar es salaam. Kaka Mzee Musa, maisha yangu yote unayafahamu. Niliamini kuwa mume wangu na wanangu wote wamekwisha kufa, kumbe bado mume wangu na mwanangu mkubwa Abdallah bado wapo hai nashukuru Mungu. Mkwe wangu na mwanangu Abdulrahmani kumbe ndiyo waliokufa kifo kibaya cha uonevu cha kuchomwa moto!"

    Alipofika hapo mama yake lmu akaangua kilio kikubwa. Akakaa juu ya kochi na kuendelea kulia huku kila mmoja amenyamaza kimya na mawazo yake kichwani. Amani akiwa macho yamemuiva kwa machozi ya joto alimwendea mama yake Dokta lmu akapiga magoti mbele yake na kutamka kwa sauti ndogo lakini iliyosikika na kila mtu.

    "Mama mimi pia sikufariki . . . Mimi ni Abdulrahmani!"

    Mama alinyamaza ghafla, akamuangalia vizuri. Amani alirudia tena kusema.

    ”Mimi ni Adulrahmani Bilal Majaliwa, mdogo wake Abdallah na kaka wa Abdulrahim. Ndie mimi mama na ndio maana siku zote nilikuambia kuwa tulikwisha kutana mahali kabla ya hapa, kumbe ni akili za udogoni zilikuwa bado zina kumbukumbu, mimi ni mwanao mama!"

    Mama yake lmu hakujua afanye nini baada ya hapo.. acheke au alie. Alikishika kichwa cha Amani ndani ya viganja vyake, akamuangalia, akambusu kwenye paji la uso kisha akamuegemeza klfuani kwake. Akamuita Dallas na Imu nao akawakumbatia wote kwa pamoja. Mzee Majaliwa aliwasogelea taratibu, alipofika karibu yao alinyanyua mikono juu na kusema, "Alhamdulilah haya yote ni majaaliwa yake bwana Mola!!"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    * * *

    Baada ya miezi sita Dokta lmu alimuoa Zainabu. Amani alimuoa Fatima, na Dallas naye alihamia Tanga na kufunga ndoa na Huba. Amani aliendelea kuishi na mama Mirambo, na Dokta lmu naye aliendelea kuishi na mama yake na baba yake Mzee Majaliwa, pamoja na mkewe Zainabu.



    MWISHO.

0 comments:

Post a Comment

Blog