Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

PUMBAZO - 3

 





    Simulizi : Pumbazo

    Sehemu Ya Tatu (3)



    RAMA alisubiri kwa siku mbili zaidi ili aweze kusikia kuwa anatafutwa.

    Lakini haikuwa hivyo, siku zilikatika bila kuona dalili yoyote ya matumaini.

    Rama alijutia kila alichokifanya hadi kumfikisha hapo gerezani lakini hakujutia kulibadili jina lake kutoka lile la Ramadhani na kujiita Alexander ili kukwepa rungu la kuadhibiwa kwa kosa la kunywa pombe ilihali yeye ni muumini wa dini ya kiislamu nchini Oman jiji la Muscat.

    Laiti kama Rama angejitambulisha kwa jina lake halisi angekuwa matatani zaidi na si ajabu angeweza kupoteza uhai wake.

    “Zay B atanitafuta kwa jina la Rama!” alijifikiria akiwa ndani ya gereza na kutambua wazi kuwa hiyo italeta utata mkubwa sana, kichwa kilimuuma na hakuwa na yeyote wa kumpa msaada katika mazingira yale.

    Kuhusu kumtegemea Zay B hilo ama yeyote yule anayemtambua kwa jina la Ramadhani alifuta kabisa kichwani kwake ili asizidi kujiumiza kifikra.

    Na hapo rasmi akajiandaa kisaikolojia kutumikia kifungo cha miezi sita gerezani.

    Tabasamu la karaha likamponyoka, kisha akajiita kwa sauti ya chini jina lake jipya.

    Alexander!

    _____

    GEREZA lilimpokea Rama katika namna ya kipekee, alikuta makundi makuu matatu ya wafungwa katika gereza lile huku kundi lililokuwa na nguvu sana likiwa lile la waarabu, kundi dhaifu likiwa la wafungwa wenye asili ya kihindi hawa walikuwa kama watumwa wa waarabu. Na walinyenyekea haswa kila kilichosemwa na wafungwa wa kiarabu…

    Kundi la watu weusi lilikuwepo kama halipo, wafungwa weusi walikuwa wachache sana hivyo Rama hakuweza kutambua upesi ni maisha gani wanapitia katika gereza hilo.

    Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba!

    Hata weusi nao hujuana kwa rangi zao!

    Rama alipoingia gerezani, wafungwa weusi wawili pekee katika gereza lile walimpokea, mmoja alikuwa mfungwa kutoka nchini Brazil anayengoja nchi yake ifanye utaratibu wa kumrudisha nyumbani akatumikie kifungo, na mfungwa mwingine alikuwa anatokea Jamaica.

    Mbrazil akiwa pale kwa kosa la kukamatwa na madawa ya kulevya huku yule wa Jamaica akitumikia kifungo kwa kukamatwa na misokoto ya bangi pamoja na vitambulisho feki.

    Kesi zao zilikuwa tofauti kabisa.

    Lakini walau waliweza kuzungumza kiingereza na kuelewana, japokuwa kwa shida.

    Kitu kimoja cha msingi alichokigundua Rama ni kwamba gereza lile lilikuwa linatoa huduma nzuri sana na wafungwa walikuwa wanajaliwa sana. Kuanzia suala la kulala hadi chakula.

    Gereza lilitoa usawa lakini wafungwa kwa wafungwa ndo walionekana kunyimana usawa.

    Hali nzuri ya utulivu na ya amani aliyoitazama pale hakutaka kuamini kuwa miezi sita yote patakuwa hivyohivyo, aliamini kuwa wale wafungwa wanaojifanya gereza lilijengwa kwa ajili yao ipo siku wataanza ‘kumzingua’

    Kweli baada ya juma moja kupita ndipo vitimbi vikaanza kutoka kwa wafungwa wenye asili ya kiarabu.

    Wakati vitimbi hivi vikianza gerezani nchini Oman, huko nchini Tanzania, kwa kauli moja wote waliofahamu juu ya oparesheni iliyompeleka Rama nchini Oman walitamka wazi kuwa Rama anasadikika kupoteza maisha nchini Oman.

    Waliyatamka haya katika kikao cha dharula kilichomuhusisha pia mke wa Rama.

    Bi Aneth akiwa na mwanaye Jose.

    Tofauti na wengi walivyodhani kuwa mama Jose atatoa kilio kikubwa sana hivyo wakawa wameandaa namna ya kumfariji, lakini baada ya taarifa ile mama Jose alitulia tuli akiwa na mwanaye mgongoni.

    Kisha baada ya sekunde kadhaa akaangukia mezani akitanguliza uso.

    Na kisha akatulia zaidi.

    Mama Jose alikuwa amepoteza fahamu!!

    Sajenti Pilipili aliingiwa na mchecheto mkubwa haswa, akachukua simu yake upesi na kuwasiliana na Zay B ambaye alikuwa Oman.

    Akamueleza kilichotukia nchini Tanzania baada ya taarifa ile, kisha akamuonya juu ya habari ya Rama kuingizwa katika oparesheni ile iishie kwao na isiende mbali zaidi.

    Hofu yao ilikuwa juu ya umoja wa mataifa, ukifahamu juu ya jambo hili ambalo Rama amelifanya pasi na hiari yake mwenyewe na kisha kumgharimu maisha yake.

    Hali ilikuwa tete!!

    Baada ya kuzungumza na Zay B, akampigia simu inspekta jenerali wa polisi na kumweleza hali halisi.

    “Pilipili nilikuonya lakini….” Alizungumza kimalalamiko kisha akakata simu bila kusikiliza lolote kutoka kwa Pilipili.

    Hili nalo likamvuruga zaidi Inspekta Pilipili, akaanza kuona dalili ya kuachiwa jumba hili bovu kumuangukia yeye peke yake.

    Inspekta jenerali alikuwa anajitoa kimyakimya!

    Pilipili akabaki kuduwaa, akifikiria walivyoshirikiana vyema katika maamuzi haya baada yay eye kupeleka wazo…. Sasa anageukwa.

    Pumbazo!

    ____

    ILIKUWA ni siku tulivu kabisa baada ya wafungwa kufanya shughuli za hapa na pale kisha kupata chakula cha mchana, Rama akiwa na mfungwa kutoka Jamaica wakipiga soga, mara mfungwa wa kiarabu aliwaendea na kuwasemesha kiarabu.

    Hakuna aliyeelewa!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa mara nyingine tena Rama akamkumbuka ustadhi Karimu ambaye alikuwa mwalimu wake wa madrasa, kitendo cha kuzikimbia zile mboko za madrasa sasa kikawa kinamgharimu asiweze hata kulinasa neno moja la kiarabu. Ustadhi Karim licha tu ya kufundisha maandiko tukufu,lakini pia alikuwa akiwafundisha maneno mawili matatu ya kiaerabu nje ya maandiko.

    “Unazungumza nini we jamaa?” Rama naye akamuuliza Kiswahili, kisha akataka kuendelea kuzungumza zaidi Kiswahili akagundua kuwa hata yule mjamaika hakuna anachoambulia.

    Kitendo cha kuzungumza kiswahuli kikamfanya yule mwarabu amtolee macho, kisha akapaza sauti akiendelea kuzungumza kiarabu.

    Punde yakaingia mapande ya watu wawili, ni wafungwa Rama alikuwa akiwafahamu.

    “Wamesema waarabu tunanuka!!” sasa alizungumza kiingereza yule bwana.

    Rama na yule mjamaika wakagutuka, mjamaika akaingiwa hofu zaidi. Bila shaka alikuwa anafahamu fika usumbufu wa wale watu waliofanya gereza kama la kwao.

    Bila kuuliza swali lolote wakawaamrisha Rama na mjamaika wapige magoti.

    Mjamaika akaenda chini Rama akahoji kulikoni!

    Hiki ni kitu ambacho waarabu wale hawakutaka kusikia, wakachukizwa na ukaidi wa Rama.

    Mwarabu mmoja akamtandika konde la usoni, lakini halikumuingia vizuri Rama aliyewahi kurudi nyuma.

    Hapo sasa wafungwa wengine walianza kusogea kutazama kinachojiri!

    Jela jela tu! Huwa inafikia kipindi hata maaskari jela wanaacha gomvi kama hizi zitokee wajionee sinema za bure!!

    Kuona Rama amemkwepa akamfuata akirusha makonde mfululizo kizembe.

    “Sitaki kupigana na wewe bila sababu jamaa…” Rama akazungumza Kiswahili maksudi!

    Hawakumuelewa zaidi aliwapandisha hasira!

    Rama alikuwa hajanyanyua mkono wake hata mara moja kurusha ngumi, alitambua kuwa wao walikuwa wachache sana wenye rangi nyeusi na tayari aliuona ubaguzi wa waziwazi hivyo kujitia kurusha ngumi ni kujitafutia balaa.

    Rama akawa upande wa kufyata! Hakurusha ngumi….

    Lakini hili halikumfanya mwarabu amuache, sasa walikuwa wawili….. wote wakitaka kumkaribisha Rama kwa kipigo gerezani ili awaheshimu.

    “Nitawaumiza jamani achene…” akazungumza kiingereza, sasa hakurudi nyuma bali alisimama imara.

    Maneno haya ya kishujaa yakawashangaza wale waarabu.

    Wakajaribu kuyapima kwa vitendo.

    Askari mkakamavu kutoka Tanzania aliyeacha kazi hiyo kwa sababu ya kuogopa ushirikina akasimama imara akakunja ngumi.

    Kikazuka kivumbi cha hali ya juu.

    Ebwana wee! Waarabu wana ushirikiano jama….

    Alipoweza kuwapasua wale wawili kwa ngumi motomoto, wale wafungwa wengine wakamfuata ili na wao waweze kumkabili.

    Alipambana katika maana halisi ya ule usemi wa ‘kupambana kiume’

    Mwishowe umoja wa waarabu ukamwangusha chini, askari wakaingilia kati Rama akiwa hoi akivuja damu.

    Ushujaa wake siku ile ukazua gumzo gerezani, na hata alipopata nafuu na kurejea tena gerezani wengi walikuwa wanamuogopa na hakuna aliyemtikisa.

    Alikumbuka kuwapa onyo huku akiwa bendeji, akawaeleza kuwa nchini Tanzania aliua samba wawili kwa mikono yake mwenyewe hivyo wakimgusa tena ataua wawiliwawili.

    Licha ya umoja, waarabu ni waoga pia.

    Japokuwa ulikuwa ni mkwara, wakafyata!!

    Mkwara ule ukapenya hadi nje ya selo kupitia wale wafungwa waliomaliza muda na maaskari jela walioamua kuzishirikisha familia zao na marafiki pia.

    Hatimaye zikafika mbalizaidi sifa zile.

    Baada ya mwezi mmoja wa kutumikia kifungo, kwa mara ya kwanza Rama ama Alexander kwa pale gerezani akapata mgeni.

    Mgeni aliyemtambua kwa jina la Alexander.

    Maajabu, jina feki kisha unapata mgeni anakutambua kwa jina hilo??

    Rama akamsikiliza kwa makini, yule bwana alikuwa na nia ya kumsaidia Rama ili aweze kuwa huru.

    Akaelezea kuwa yeye ni muislamu na ni mtanzania, ameguswa na kitendo cha Rama kufungwa jela kwa kuvunja sharia asizozijua!

    Alikuwa ni ngozi nyeusi na aliongea lugha ya Rama!

    Rama akafarijika na kukubaliana na yule bwana aliyeahidi pia kumrejesha nchini Tanzania.

    Lakini kigezo cha Rama kuukubali msaada huu ni kwamba alihitaji hatua zifanyike za yeye kukutana kwanza na mwenyeji wake wa nchini Oman!

    Akawatajia Zay B!

    Yule mgeni akamweleza kuwa hilo halina tatizo.

    Baada ya siku tatu Rama akatembelewa tena….

    Mbele yake alikuwa ni yule mgeni akiwa ameambatana na Zay B, yule mwanadada askari wa kizanzibar Nchini Oman!!

    Zay B hakuzungumza kabisa bali alimpungia tu mkono Rama kwa muda mrefu huku akionyesha majonzi ya waziwazi.

    Rama akatambua kuwa Zay B anamuonea huruma kwa uwepo wake gerezani.

    Kwa siku hii hapakuwa na mazungumzo mengi, Rama akakubali kiroho safi kabisa ule msaada.

    Msaada kutoka kwa mgeni anayezungumza Kiswahili!

    Alikuwa amedumu gerezani kwa mwezi mmoja na siku kadhaa.

    Akaachiwa huru kabisa…. Asijue wale waliomsaidia walikuwa na nia gani.

    Alipoivuta hewa nje ya gereza kitu cha kwanza kilichokuja katika akili yake ni Vonso!

    Akaapa kwa kila majina aliyojua kuwa anajitoa katika msako huo asioujua, akafikia maamuzi magumu ya kwenda ubalozi wa Tanzania na kuelezea kwa kina tukio lake ili aweze kusaidiwa!

    Hiyo ilikuwa ni azma yake ya kwanza kabisa katika uhuru ule.

    Alibaki na hatihati iwapo amshirikishe Zay B ama ajichukulie maamuzi ya kibinafsi!

    Akaweka kituo katika wazo lile na kujipa muda zaidi wa kufikiri!

    Waliingia katika jumba la kifahari, hakujiuliza sana juu ya jumba lile kwa sababu Muscat kuna majumba mengi zaidi ya kifahari zaidi ya lile, geti likafunguliwa wakapita, likafunguliwa na geti la pili, hatimaye geti la tatu likafunguliwa, na hapo palikuwa kama ukumbi.

    Rama akashtuka ghafla anasukumwa kwa nguvu sana, kwa sababu hyakutarajia kitendo kile akajikuta anapiga mweleka chini, kabla hajafukurukuta alifungwa kamba kwa nyuma. Kisha kamba ile ikaanza kuvutwa na kitu kisichojulikana ili kumnyanyua Rama, kamba ile haikuishia kumnyanyua ikazidi kumvuta juu katika namna ya kumnin’iniza.

    Hapo sasa Rama alianza kupiga mayowe. Lakini wale watu waliomfunga kamba hawakujali.

    Sasa alikuwa hewani na kamba ikizidi kumvuta kwenda juu.

    Alivutwa hadi akatokea upande mwingine wa juu kabisa.

    Mara alipofika juu akasikia watu wakipiga makofi kwa juhudi sana.

    Rama akageuka kutazama makofi yanapotokea.

    Hakuamini macho yake asilani, akafumbua na kufumba kisha akafumbua tena…. Hali ilikuwa kama akili yake ilivyokuwa imetafsiri!

    BALAA!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    MACHO yake hayakukutana moja kwa moja na watu waliokuwa wanapiga makofi, badala yake yalitua katika miili iliyokuwa mahututi kama sio kutokwa na uhai kabisa.

    Damu ilikuwa imetapaa huku na kule. Rama akataka kusema neno, lakini koo lilikuwa limekauka sabna kutokana na kilio kikuu alichotoa wakati akipandishwa na zile kamba ngumu kuelekea juu.

    Laiti kama usingekuwa ukakamavu wake alioupata akiwa katika mafunzo ya jeshi la kujenta taifa (J.K.T) basi hali yake ingekuwa mbaya sana.

    Bila kufunguliwa zile kamba alishtukizwa na pigo moja kali katika kisogo chake!

    Fahamu zikamtoka!!

    _____

    RAMA ANASIMULIA.

    NILIKUJA kushtuka baada ya kumwagiwa maji ya baridi, niliposimama miguu yangu ilikuwa inatetemeka sana, na tumbo lilikuwa wazi kabisa.

    Njaa ilikuwa imenishika kwa kiwango cha juu!

    Mbele yangu alikuwa amesimama kijana wa kiafrika mwenye ngozi kama yangu.

    “Ako unatokea wapi wewe?” alinisemesha kwa Kiswahili nilichobaini kuwa ni cha nchi jirani kabisa na taifa langu.

    Kenya!

    Na kama si Kenya basi alikuwa ni mjaruo!!

    Nikataka kumjibu kuwa natoka Tanzania lakini badala yake nikajikuta namweleza kuwa nina njaa kali sana.

    Akanitazama kwa jicho ola dharau na akionyesha wazi kuwa hajafurahishwa na uwepo wangu pale.

    Akatoka nje, baada ya muda akarejea na birika la uji wa moto akanipatia. Nikauvamia kwa pupa, tumbo likaupokea kwa shangwe.

    Wakati naendelea kunywa uji, yeye akatoka nje na kurejea nasahani lililokuwa na chakula aina ya tambi.

    Nikaimaliza sahani ile, na hapa nikajisikia kuwa na nguvu na imara.

    Akaniuliza iwapo nimetosha, nikamkubalia.

    Akasimama na kuanza kutembea kuelekea huku na kule kisha akaanza kuzungumza.

    “Naitwa Abdulkarim bin Swaleh…nimesema nani??” akaniuliza.

    “Abdulkarim bin Swalehe!” nikarejea kulitaja jina lake kwa umakini. Akacheka kidogo nikaona kuwa hakuwa na meno mawili ya mbele.

    “Mimi ni bosi yako, kuanzia dakika hii hautaniita Abdulkarim ila utaita mimi Masta…. Na uite jia hii wakati Masta kubwa haiku around, akiwa around utaniita Abdulkarim… akiwa mbali utaita mimi Masta. Baadaye ntapeana na wewe kazi za kufanya….” Alizungumza kwa msisitizo huku akinitazama machoni, na kila mara akiipandisha nguo yake juu kimajigambo.

    Nilibaki nimeduwaa nisijue anachomaanisha,nikamuuliza kulikoni.

    Naye akashangaa kusikia namuuliza swali.

    “Kwani haukupewa instructions wakati unakuja hapa? Hili ni eneo la kazi… na mimi ni masta wako…” majibu ya yule bwana yalianza kunichanganya.

    Nikamuuliza pale ni wapi.

    “Oman…. Muscat Oman….” Alijibu kwa msisitizo. Kisha akatoa maelekezo yaliyonifanya niingiwe na ubaridi mkali sana.

    Akanieleza kuwa nimetia saini mkataba wa kufanya kazi katika kasri lile kwa kipindi cha miaka mitano. Wakati anazungumza haya akanipatia karatasi ambayo niliona kweli kabisa nilikuwa nimetia sahihi yangu katika mkataba ambao umeandikwa kiarabu nisijue hata ni kitui gani kilikuwa kimeandikwa.

    Nilijikaza nisionekane kuwa nimeingiwa na hofu lakini kiukweli nilikuwa nimepagawa tayari.

    Niliwaza kuhusu mtoto wangu Jose ambaye bado alikuwa mdogo sana, nikamfikiria pia mke wangu.

    Chozi la uchungu likanitoka!!

    Na haikuwa ndoto bali kweli tupu.

    Yule bwana anayetaka nimuite masta alinichukua hadi katika chumba kingine akafungua mfuniko uliokuwa sakafuni. Tukaingia chini……

    Macho yangu yakaanza kukutana na sura nyonge kabisa zikiwa katika kazi, hakuna hata mmoja aliyeonyesha kuwa na furaha.

    Joto lilikuwa kali na kila nilivyozidi kwenda mbele lilikuwa linaongezeka.

    Hofu ikazidi kuchukua nafasi yake. Masta akanikabidhi kwa bwana mwingine ambaye alionekana kuwa kiongozi kule chini ya ardhi kwenye mitambo ambayo sikujua inahusu nini.

    “Una ujuzi gani?” aliniuliza kiingereza.

    Swali lile lilikuwa la kushtukiza sana, nikabaki kujiumauma.

    “Unajua kuongoza mashine? Unajua kuchanganya kemikali? Unaweza kuendesha gari kubwa? Unaweza kupanga pampu za mafuta?” aliuliza maswali mengine mfululizo….. nikakosa jibu.

    “Send him to Utaah! (Mpeleke kwa Utah)” akampa maelekezo masta.

    Masta akanichukua na hapohapo akawa ananinong’oneza.

    “We ako mpumbavu kiasi gani,. Ungesema profesheni yoyote ile kwa huyu bwana, sasa Utah atakuua na venye ulivyo legelege… atakuua mjinga yule.”

    Kusikia juu ya kifo nikaingiwa ganzi, nikatamani kukimbia lakini hadi wakati huo Masta Abdulkarim alikuwa amenionya nisije kujaribu kufanya ujinga kama ule kwa sababu nitakuwa nimejiingiza matatani, akanieleza kuwa yeye alioingizwa pale akiwa na miaka kumi na nane tu na sasa ana miaka thelathini na mbili. Hajawahi kuipata walau njia ya kuthubutu kutoroka.

    Nilipokumbuka mawaidha ya masta nikawa mtulivu.

    Hadi tukamfikia Utah!

    Mwarabu mwenye ngozi nyeusi, mwili mpana na uso wa kikatili.

    Nilipofikishwa mbele yake akanikamata na kunitikisa kwa takribani sekunde thelathini.

    Yule mwarabu alikuwa na nguvu ya ajabu!!

    Alinitikisa hadi nikakumbwa na kizunguzungu!

    “Peleka geti namba nne huyu!” alimweleza masta kwa Kiswahili.

    Masta akanichukua tena tukapita milango kadhaa, huko nikawa nawaona watoto wa kike dhaifu kabisa wakiwa wanashughulika, miili yao ilikuwa imelegea haswa.

    Tukalifikia geti namba nne, nikapokelewa pale masta akazungumza na wale watu kisha akaniita kando akaninong’oneza.

    “Tajia mimi namba za simu za ndugu zako, ikiwa utakufia huku niwape taarifa…wajue tu ati ulifia huku.” Alizungumza kwa kusihi, hakuwa katika utani bwana yule.

    Nikamtazama kwa mshangao.

    “Usinitazame machoni watauliza chenye ninaongea na wewe… sema nambari ya simu.”

    Ni kweli nilikuwa nimekariri namba za watu kadhaa katika kichwa changu, lakini kwa kauli ile tatanishi nikajikuta hata namba ya mke wangu naisahau palepale.

    Kifo! Nani asiyeogopa kifo, sasa masta anakitamka kana kwamba ni kitu cha kawaida.

    “Kumbuka jina langu vizuri linaweza kukusaidia…. ABDULKARIM BIN SWALEHE” alisema haya kisha akanikumbatia na kuondoka, nilimuona waziwazi kuwa alikuwa na wasiwasi mkubwa sana.

    Nilibaki nimesimama pale kwa sekunde kadhaa kabla sijasukumwa ndani, nikaingia katika chumba kilichosheheni maji yaliyofanana na kutu ama matope ya moramu!

    Niligeuza macho huku na kule mara nikamuona binti mmoja akiwa amelalakatika maji yale akiwa ametulia tuli.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikashtuka na jicho langu likaganda pale nikijiuliza nini kimemsibu binti yule.

    “Do you want to help her? (Unataka kumsaidia?)” mwarabu mmoja liyekuwa msimamizi wa chumba kile aliniuliza, kabla sijamjibu kauli ile ikageuka kuwa amri, akaniamrisha niende kumchukua yule binti pale.

    Nikaanza kujishauri mara akanifyatua kibao kikali usoni. Kikaniingia sawasawa!!

    Nikataka kumkabili lakini nikaona kifuko cha kuhifadhia mtutu katika kiuno chake na hakikuwa kitupu.

    “Mchukue umlete hapa!” aliniamrisha. Nikapig hatua moja moja hadi nikaufikia ule mwili ambao sikujua kama una uhai ama la.

    Nikamnyanyua yule dada!!

    Mungu wangu! Shingo yake ikaangukia upande, nikashtuka sana kwa jinsi alivyokuwa wa baridi.

    Bila shaka hakuwa hai!

    Jambo hili kwa wengine lilionekana la kawaida sana, waliendelea na shughuli zao.

    Niliunyanyua ule mwili na kuupakata katika mikono yangu na kisha nikamwendea yule mwarabu.

    “Nenda ukamzike!!” aliniambia huku akitupa mikono yake juu, kama mtu ambaye anakueleza neno ambalo anajua huliwezi lakini anakukomesha kwa sababu ulijifanya kulijua sana.

    Nilibaki kumtazama yule bwana huku nikitamani yatokee mauzauza yoyote yale ili tujikute tupo wawili mahali niweze kumfunza adabu.

    “Nifuate! Mjinga wewe..” alibwatuka huku akiondoka, nami nikimfuata nyuma…mkononi nikita na maiti.

    Mwili ule ulikuwa mwepesi ajabu, uliokonda kwa kiasi kikubwa sana.

    Moyo uliniuma!

    Niliendelea kluwa nyuma yake, baadaye alisimama na kunielekeza mahali pa kuupeleka mwili ule.

    Nilifuata maelekezo yake!

    La! Haula… niliingia mahli ambapo nilikuta miili mingine si chini ya kumi ikiwa imetupwa hovyo, wengi wakiwa wanawake wasiokuwa na nguo katika miili yao.

    Niliutua ule mwili na sikutaka kugeuka nyuma, niliondoka nikiwa natetemeka sana.

    “Nguo zake wapi?” nilikutana na amri nyingine. Na hakurudia yule bwana.

    Nikalazimika kurejea kuziondoa nguo katika mwili wa yule binti asiyekuwa na uhai tena.

    Niliitoa nguo yake na hapo nilisahau kuhusu harufu kali ya pale ndani, badala yake nilishuhudia alama za mijeledi ilivyouchana mwili wa yule dada.

    Pasi na shaka alisulubiwa kabla ya kupoteza uhai.

    Kwanini? Na ni mpango wa nani huu?

    Nilijiuliza huku nikitoka nje, nikaelekezwa pa kuitupa ile nguo.

    Kisha nikaingia kazini rasmi, kazi ya kusafisha vyuma chakavu vyenye kutu kali ambavyo sikujua hata vinatumika kufanya nini.

    Ama! Pale gerezani palikuwa ni sawa na paradiso kabisa, lakini hapa nilipokuwa palikuwa ni jehanamu penye maisha ya mashaka na hofu ya kila dakika.

    Hofu ya kutokwa na uhai kisha mwili wako kutupwa kama mzoga wa mbwa koko.

    Hapa sasa nikaanza kuhisi kuwa huenda ni zile laana ambazo baba aliwahi kunambia pindi ninamgomea katukatu juu ya kumuoa Mama Jose.

    Lakini sikutaka kuziruhusu hata kidogo fikra za kumdhania vibaya mama Jose.



    Ama! Pale gerezani palikuwa ni sawa na paradiso kabisa, hapa nilipokuwa palikuwa ni jehanamu penye maisha ya mashaka na hofu ya kila dakika.

    Hapa sasa nikaanza kuhisi kuwa huenda ni zile laana ambazo baba aliwahi kunambia pindi ninamgomea katukatu juu ya kumuoa Mama Jose.

    Lakini sikutaka kuziruhusu hata kidogo fikra za kumdhania vibaya mama Jose.

    Ila kwa kiasi fulani nilijiona kama niliyekosea sana kutomsikiliza mzee wangu.

    ____ ______

    Wakati Rama nchini Oman akiwa katika mkanganyiko wa kumuwaza Aneth na kuhisi anaweza kuwa chanzo cha yote haya yanayomtokea.

    Nchini Tanzania Aneth alikuwa hana amani hata chembe na alikuwa ni mjane rasmi!!

    _____ _____

    NCHINI TANZANIA

    ANETH akiwa hana nywele kichwani alikuwa amerejea nyumbani kwa baba yake, mzee Fidelis.

    Alikuwa yu mjane rasmi, lakini hakuna mwanafamilia aliyeguswa sana na jambo hili.

    Wote walihesabia kuwa ni laana kutoka kwa wazazi wake baada ya kulazimisha kufunga ndoa na mwanaume asiyekuwa wa dini yake.

    Aneth alijua karaha ambayo angekutana nayo akirejea nyumbani baada ya kifo cha maajabu cha mumewe, lakini hakuwa na namna baada ya ile nyumba ambayo alikuwa akiishi na Ramadhani kuvamiwa na nduguze Rama wakamsimanga kuwa amemroga kijana wao na sasa amemuua.

    Jopo hili la wasimangaji liliongozwa na mzee Saidi Matelu, baba mzazi wa Ramadhani.

    Huyu alifikia hatua ya kumwapia Aneth kuwa atamsomea albadiri ili ageuke kuwa kichaa.

    Mzee huyu hakusikia lolote jambo zaidi ya kumtambua Aneth kama chanzo cha mabaya yote yaliyomkumba kijana wake.

    Sasa Aneth akageuka kuwa mpira wa kona, huku unapigwa na huku unapigwa… kila mtu akiusaka ili aupige.

    Nyumbani kwao kila akigusa hiki anatukanwa, akisema hili anaonekana asiyekuwa na maana.

    Afya yake ikazorota, maziwa yakagoma kutoka katika himaya yake, Jose naye akaanza kudhoofika kwa kukosa lishe hiyo muhimu kabisa.

    Jose akajikuta akiachishwa kunyonya angali anayahitaji sana maziwa ya mama.

    Licha ya kupitia magumu haya hata siku moja mama Jose hakuwahi kujilaumu kwa uamuzi wake wa kuolewa na Rama ndoa ya bomani.

    Kila pambazuko kilizuka kisa na kabla ya jua halijaondoka zake kilikuwa ni kisa kingine. Vyote hivi kwa Aneth na mwanaye ambaye alikuwa amemfanana haswa baba yake mzazi.

    Jambo hili lilimkera sana baba yake Aneth ambaye alikuwa akiona waziwazi ile damu asiyoitaka ikiwa bado inazunguka pale ndani.

    Kuna siku Aneth alikuwa anaosha vyombo alivyokuwa amevitumia kupika chakula…. Jose alikuwa anatambaa akaenda hadi sebuleni, huko akamkuta babu yake, mzee Fidelis.

    Aneth akiwa hana hili wala lile mara anashtuliwa na sauti ya Jose akitokwa na kilio kikubwa haswa, akaviacha vile vyombo na kukimbilia sauti ilipokuwa inatokea.

    Sebuleni! Masikio yake yakamuelekeza…

    Akaivamia sebule na kumkuta Jose akiwa ameketi chini akilia kwa uchungu mkubwa sana, baba yake Aneth akiwa ameshika gazeti akiendelea kusoma.

    Aneth akamnyanyua Jose, na jicho lake likaenda moja kwa moja mahali ambapo Jose alikuwa anajikuna.

    Ebwana eeh!! Alama za vidole vya mtu mzima katika shavu la mtoto mdogo kiasi kile.

    Kilio kile kilipenyeza pia katika ngoma za masikio ya mama yake Aneth! Naye akafika pale sebuleni na kuuliza kulikoni.

    Alimkuta Jose akiwa bado analia, huku mama yake naye akiwa anabubujikwa machozi. Akalazimika kuhoji.

    Jamani kulikoni hapa!

    “Nimemchapa makofi huyu mjinga alikuwa anataka kuvunja chupa ya chai”….. alijibu bila kumtazama yeyote.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Analeta akili mbovu kama za baba yake!!” aliendelea kuzungumza.

    Wakati huo mama Jose analia kwa kwikwi tu, macho yake yakaitazama ile chupa ya chai yenye thamani ya kawaida akamtazama tena Jose. Kisha akamtazama mama yake bila kusema neno lolote, alimwona mama yake jinsi alivyoguswa na tukio lile.

    Akapiga hatua kuelekea chumbani kwake bila kusema neno lolote.

    “TEna ufanye umpeleke huko kwao, mi sitaki kufuga makaidi hapa kwangu!” mzee Fidelis akapaza sauti juu.

    Aneth hakujibu! Akaenda hadi chumbani, akambembeleza Jose hadi aksasinzia.

    Baada ya hapo akamnon’oneza vitu kadhaa Jose aliye katika usingizi.

    Kisha akatoka.

    Safari hii alitembea upesiupesi hadi akafika sebuleni.

    “Mzee Fidelis, kwanini umenipigia mwanangu kiasi kile hadi misuli imemtutumka?” alihoji Aneth, mzee Fidelis akashtuka. Kwa mara ya kwanza katika maisha yake mtoto wake wa kumzaa anamuita kwa ubini wake.

    “Mtoto mdogo kama yule baba umemjaza kofi lenye uzito mkubwa kiasi kile, amekuwa mwekunduu… Jose hajawahi kulia kwa kiasi kikubwa hivyo… baba kwanini….” Aneth akazidi kuhoji.

    “Umeniitaje we mwanahizaya uliyefungia adabu zako stoo kisha ukapoteza funguo .” Sasa alisimama mzee Fidelis.

    Kisha kama alivyokuwa akifanya utotoni, kufungua mkanda na kuwacharaza wanawe wakifanya makosa, akafanya tena asijue kuwa yule si Aneth tena bali ni mama Jose.

    Hata hakumaliza kuutoa ule mkanda Aneth akamvaa mzee Fidelis mzimamzima akatua nay echini.

    Akaliona shavu dodo la baba yake akauvuta mkono kwa nguvu zote na kuutuliza katika shavu la baba yake.

    “Sijawahi kukudharau baba, sijawahi hata siku moja… ila umenipigia mwanangu kiasi kile cha kunitangazia kuwa hunitaki mimi wala mwanangu katika macho yako…. “ alizungumza huku akiendelea kumshambulia baba yake, sasa alikuwa anamkwaruza na makucha yake, mzee Fidelis akaanza kupiga mayowe.

    “Wankuruuuuu…” mama mtu alishafika na kumuita Aneth jina lake la ukoo huku akipiga mayowe. Akamvaa Aneth ana kumchomoa pale.

    “Mama… mama… nilipokuwa mdogo siwezi kusimama, siwezi kusema mtu akinikosea sina akili… ukamkuta baba yako mzazi amenifanya kitendo ambacho mzee Fidelis amekifanya kwa Jose ungechukua hatua gani. Usikwepeshe macho mama uliyenilea kwa miaka yote.” Akavuta kwikwi kadhaa zilizoambatana na kilio kikuu kisha akaendelea, “Mama mzee Fidelis na huu mkono wake mzito amenipigia mtoto wangu mama… amempiga Jose hadi misuli imemtutumka mama… eeh mama” akasita akameza mate.

    “Kama laana ipo naomba mnipe maana mlinilaani zamani tu nilipochukua maamuzi yangu sahihi, sasa naomba mnilaani… ila na yeyoye asije kuthubutu kunitesea mtoto wangu ambaye hadi sasa hajui dini ya mama wala baba yake….. yaani kweli mzee Fidelis ametaka kuniulia mtoto mama….” Hakuweza kuongea akamkumbatia mama yake kwa nguvu sana.

    Hapa sasa hata mama yake hakuweza kujizuia alianza kulia. Wakakokotana kuelekea chumbani kwa Aneth wakimuacha mzee Fidelis akibwatuka maneno ya kishujaa hasahasa akijitapa kuwa ile nyumba ni yake na atamtimua Aneth.

    Shavu lake lilikuwa limeumuka haswa.

    Alitoweka bila kumuaga mtu, akiongozwa na hasira huku akiwa amepanga lolote lile baya aweze kulifanya kwa Aneth ikiwa ni namna moja ya kulipa kisasi.

    Majira ya saa mbili usiku akiwa anaambatana na watu wawili alirejea nyumbani.

    Huku akamkuta mkewe akiwa mkiwa sana, akamsalimia na hapohapo akamuulizia Aneth.

    Mama akamtazama mumewe kwa muda na kisha akatoa jibu lililozua tafrani katika kichwa cha mzee Fidelis.



    Majira ya saa mbili usiku akiwa anaambatana na watu wawili wababe alirejea nyumbani.

    Huku akamkuta mkewe akiwa mkiwa sana, akamsalimia na hapohapo akamuulizia Aneth.

    Mama akamtazama mumewe kwa muda na kisha akatoa jibu lililozua tafrani katika kichwa cha mzee Fidelis.

    Aneth alikuwa ametoweka na hajamuaga mtu yeyote lakini ameacha ujumbe mfupi kabisa.

    “SITAKANYAGA HAPA NA MAITI YANGU ITUPWE JALALANI ISILETWE HAPA….Na kuanzia dakika hii naitwa ANETH RAMADHANI JOSEPH.”

    Mzee Fidelis alipigwa na bumbuwazi, wale watu alioambatana nao walipojaribu kumuuliza aliwagombeza na kisha kuwafukuzia mbali.

    Wakaondoka huku wakijiuliza iwapo huyu mzee amechanganyikiwa ama la!

    ______

    MJI ulikuwa tulivu tofauti na siku nyingine, familia ilishazoea ile tabia ya baba yao kufoka kila mara, iwe anakuita ama likitokea kosa umefanya yeye anafoka tu!

    Uzuri alikuwa anafoka tu lakini alikuwa na mkono mzito sana hakudiriki kuadhibu watoto wake hovyo, alikuwa ni mtu wa mikwara tu. Mkiwa mezani mnakula lazima atafute sababu ya kumgombeza walau mtoto mmoja!

    Ukila taratibu atakwambia unakula kama upo harusini, ukila upesiupesi atakuuliza unakula harakaharaka unawahi wapi.

    Ukinawa mikono wa kwanza anakukaripia kuwa hauna adabu unanawa kabla ya wakubwa, ukisubiri wakubwa wanawe ndo wewe unawe anakukebehi kuwa utaratibu huo ni wa kizamani yeyote anaweza akaanza kunawa.

    Mkewe alikuwa anaingilia kati mara moja moja huku akimtupia kijembe mumewe kuwa vita ya Kagera ilimwathiri akili anajiona yupo sawa kwa kila anachofanya.

    Akishaambiwa hivi na mkewe anasusia chakula anaenda chumbani, wakikutana huko wanayamaliza.

    Japokuwa hali hii ukiisoma unaweza kudhani ilisababisha familia hii isiwe na furaha,. Lakini tabia hii ilifanya furaha itawale nyumbani na upendo kuimarika zaidi miongoni mwa wanafamilia.

    Lakini siku hazifanani!

    Siku hii ukimya ulitawala sana, vilisikika vijiko vikigombana na mabakuli na sahani, na midundiko ya matonge kuanzia yanavyoshambuliwa na meno mdomoni kisha kupita katika koromeo na kudondoka tumboni.

    Ukimya huu ukasababisha mama azungumze ili kumchokonoa baba mwenye nyumba..

    “Naona leo Pilipili imetiwa ndimu nyingi! Imeishiwa makali?” usemi huu wa mama ukasababisha familia nzima wavunje mbavu kidogo, kasoro mlengwa wa kijembe hiki yeye alikuwa mtulivu.

    Tofauti na matarajio ya wengi kuwa ataanza kugomba kama kawaida yake au kurudisha kijembe kikubwa zaidi haikuwa hivyo!

    Kimya kikatanda tena!

    “Afande Pilipili, unaumwa?” mkewe akamuuliza kimasihara. Badala ya kujibu, baba mwenye nyumba ambaye nyumba yake pia ilimwita kwa jina la utani la Sajenti Pilipili akasimama badala ya kuelekea chumbani akaelekea dirishani na kusimama akawa anatazama nje.

    Hapa sasa hayakuwa masihara tena mkewe akamwendea na kumkokota wakaenda chumbani. Tayari alishagundua kuwa ubavu wake haukuwa sawa kabisa.

    Utani kando, mapenzi yakachukua nafasi.

    Ni huko chumbani ambapo Pilipili alimweleza mkewe juu ya jinamizi la Rama linavyomsumbua na kumkosesha raha. Akaelezea ni kiasi gani yule kijana asiyekuwa na hatia alivyoingia katika domo la kifo kimasihara na hapo akailaani kauli ya mkuu wake wa kazi ya kuamua Rama aende Oman kwa oparesheni ya kumsaka Vonso.

    “Sidhani hata kama Rama alitakiwa tu kulijua hilo jina, ni jina zito sana kuliko umri wake! Sijui tu nini kilitokea kati yetu…” akasita akamgeukia mkewe. “Hivi unajua ameacha mke na mtoto mdogo… katoto kadogo kabisa.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mkewe akataka kusema neno sajenti akaendelea, “Halafu mkewe naye tumemsotesha rumande kizembe tu!”

    Mkewe akaguna kisha akamuuliza swali moja. “Lakini mume wangu mbona Oman inasdifika kwa sheria kali inawezekana vipi mtu kuuwawa kizembe hivyo!”

    “Ni kweli sheria zao ni kali haswa lakini ukali wa sheria hauzuii mtu mmoja kumtoa roho mwenzake kwa sababu zisizojulikana.

    Mkewe alimfariji na kumpa maneno ya kumtia nguvu upya kabisa. Walau faraja hii ilimpa nguvu za kutabasamu kidogo, Sajini Pilipili.

    Kisha mkewe akabadili mada ili kumpunguzia mumewe mzigo wa mawazo.

    Wakati wanaanza kubadili mada, mlango wa chumbani uligongwa mama Yohana akaenda kufungua. Akamsikiliza mgongaji ambaye alikuwa ni mtoto wake.

    “Baba Yohana, kuna ugeni….” Mkewe akamueleza kwa utulivu huku akionekana kuchukia ugeni huo wa usiku!

    Sajini akasimama na kutoka nje ya chumba chake. Alipotoka tu akakutana na mwanamke akiwa amesimama akibembeleza mtoto wake aliyekuwa analia.

    Sajini akashtuka vibaya mno!!

    “Mama Jose!” akaita.

    “Samahani kwa kukutembelea usiku huu imenibidi tu, nahitaji kuzungumza nawe.” Alijibu mama Jose.

    Sajini akajivuta na kutoka nje, mama Jose akamfuata nyuma. Huku mkewe akiwasindikiza kwa macho yenye viulizo vingi.

    Walizungumza mengi sana huko nje, mama Jose akajieleza.

    “Sina pa kwenda Sajini, sina yeyote wa kunisikiliza, si upande wa nyumbani kwetu wala upande wa mume wangu… tafadhali naomba ufanye kitu.” Akasita akamgeuza Jose ambaye alikuwa bado hajasinzia.

    “Sajini, baba yangu… baba aliyenizaa mimi… amempiga Jose kibao kwa nguvu zake zote… mwone mwanangu asiyekuwa na baba anavyoanza kuteseka…” akataka kuendelea koo likagoma kutoa sauti, akajaribu tena kuzungumza akajikuta anaangua kilio cha uchungu!

    Kumwona mamaye analia, Jose naye akaanza kulia!!

    Sajenti alijiskia vibaya sana na kuzidi kuwa upande wa hatia! Alijiona amepambwa na damu mikononi mwake.

    Ili kukabiliana na hatia hii, akaona ni heri amsaidie kadri awezavyo mama Jose.

    Akaamini kuwa msaada wake wa dhati pamoja na ukaribu wake kwa Mama Jose utafuta kidogo kumbukumbu ya Rama kupoteza maisha nchini Oman.

    Sajenti Pilipili akachukua maamuzi ambayo yalimwaga maji ya ubaridi katika moyo wake wa nyama uliokuwa umeganda kwa sababu ya fikra juu ya Rama.

    Baba wa mtoto mchanga!!

    Kwa siku ile Mama Jose alilala pale nyumbani, siku iliyofuata sajini aliwaagiza vijana wake wakatafuta chumba na kuweka vitu vya msingi, baada ya siku tatu mama Jose akaanza kuishi katika nyumba ya kupanga. Mara kwa mara Sajini Pilipili alikuwa akienda kumjulia hali.

    Baadaye akamfungulia duka la vipodozi jirani na nyumba aliyokuwa amempangishia!

    Sajini Pilipili akabaki kuwa ndugu pekee wa Mama Jose.

    Jose akaanza kumtambua sajini kama baba yake.

    Rama akasahaulika!!

    Wakati Rama anasahaulika Sajini kwa amri ya mkuu wake wa kazi akatakiwa kufanya mawasiliano na Zay B ili mara moja rejee nchini Tanzania akatulie nyumbani kwao Zanzibar!

    Na akatakiwa rasmi kulifunga jalada la kumsaka Vonso na kampuni yake lililokaa wazi kwa miaka zaidi ya kumi bila muafaka.

    Ni simu hii ya kutoka Tanzania kwenda Oman iliyozuka balaa jipya.

    Majibu yakaelezea kuwa kuna wawakilishi rasmi kutoka Tanzania walifika Oman katika makazi aliyokuwa akiishi Zay B na kuelezea kuwa anatakiwa mara moja nyumbani Tanzania, watu hao walikuja na nyaraka zote za kiofisi kuthibitisha kuwa wapo pale kihalali.

    Watu wale wakatokomea pamoja na Zay B na mizigo yake michache.

    Walikuwa na tiketi ya ndege kabisa maalumu kwa ajili ya Zay B.

    Sajini Pilipili alichoka, lakini Inspekta generali wa polisi alichoka zaidi.

    Ilikuwa ni vita mpya!!

    Vita dhidi ya watu wanaojulikana lakini wasiojulikana kwao!!

    IGP akaingia katika Pumbazo na kwa ghadhabu kubwa sana ya kuona kuwa adui yao anawafanya kama watoto wadogo. Akachukua simu yake akatafuta namba aliyokuwa anaihitaji.

    Akapiga na kusikiliza kwa muda, ikapokelewa na mtu aliyekuwa kilabuni analewa, alizungumza kilevilevi.

    IGP akakata simu huku akitokwa na tusi zito haswa kwa lugha ya kifaransa.

    Akaitazama simu ile kisha akalisoma lile jina katika simu.

    GEZA ULOLE!!

    Akamalizia kwa kulitafsiri.

    IGA UFE!

    Na mwisho akaponyokwa na kicheko kisichokuwa kichekesho!

    _____

    RAMA aliendelea kufanya kazi ngumu huku akipata chakula kidogo tofauti na kazi ile iliyojaa suluba, siku mkurugenzi akiwepo wanapewa chakula kizuri sana na hawafanyishwi kazi nyingi sana.

    Rama akaanza kujifunza kitu, kuna jambo lilikuwa haliendi sawa hata kidogo katika chimbo lile. Akahisi kuna manyanyaso ambayo wanafanyiwa lakini ni nyuma kabisa ya upeo wea mkurugenzi.

    Akafikiria kushtaki lakini mkurugenzi yule alikuwa hazungumzi kiingereza wala Kiswahili.

    Hapa sasa Rama akalazimika kubadili mfumo wake wa kuishi maisha ya kimyakimya, akaamua kubadilika na kuunda urafiki na wenzake katika geti nambari nne ambao wote kwa pamoja walifahamu fika kuwa hatma yao ni kufanya kazi kila siku na ili utoke mle ndani lazima uwe umekufa!

    OMANI haikujua kuhusu hili, Tanzania haikujua kuhusu hili, Afrika ilikuwa gizani na dunia haikuwa na huu ufahamu.

    Walifahamu wachache walionufaika na mradi huu.

    Katika kuunda urafiki na kuanza kuzungumza na wenzake hasahasa wakati wa chakula… hatimaye walianza kutambuana kwa majina na nchi wanazotoka.

    Rama akakutana na Latipha!

    Binti kutoka Kenya ambaye mara yake ya mwisho kuishi Afrika alitokea nchini Tanzania. Ni huyu ndiye aliyemsimulia Rama na kuanza kumfungua akili yake walau kidogo.

    Alikuwa anamsimulia Rama huku wakiendelea kufanya kazi, haikuwa rahisi binti yule kuanza kumsimulia Rama kwa sababu hakuamini kuna msaada wowote anaweza kuupata, aliiona hatma ya wote katika ficho lile ni kifo cha kifedhuli.

    Lakini ule ukarimu wa Rama kumsaidia yule binti kazi walizokuwa wanapewa hatimaye Latipha aliamua kumsimulia rama. Na alimsimulia haya huku akimpa angalizo kubwa.

    LATIPHA

    Naitwa Latipha… Latipha Kasim Sadiki, nina miaka ishirini na moja sasa. Nitakufa kabla sijafikisha miaka ishirini na mbili, nitakufa kwa mateso makali sana, nitakufa na kutupwa kama mzoga.

    Mama yangu hatajua, wala ndugu yangu yeyote. Mchwa na wadudu watakaonitafuna pekee ndio watatambua kuwa mimi ni mfu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilifanya kazi mbalimbali jijini Mwanza nchini Tanzania, kwa asili mimi ni mkikuyu kutoka Kenya.

    Nilienda Tanzania kutafuta maisha nikipitia njia ya Mombasa kisha Tanga.

    Nimefanya kazi katika mgahawa mdogo Mwanza, kipato kilikuwa chini na dharau kubwa kutoka kwa wateja nilizizoea.

    Maisha yangu yalipata Nuru tena baada ya kukutana na kijana mstaarabu sana anayeitwa Eric Mlewa…. Awali nilidhani kuwa ananitaka kimapenzi lakini siku moja aliniita kando na kupeleleza juu ya mshahara wangu, nikamjibu akastaajabu sana na kisha akanieleza iwapo nipo tayari kufanya kazi hiyohiyo ya mgahawa lakini nje ya Tanzania, nikamjibu nipo tayari lakini sio nchini Kenya.

    Akanieleza ni Oman, akasema mshahara ni mara kumi ya ule niliokuwa napokea. Nilipokea taarifa ile kwa furaha lakini sikuamini kama itatekelezeka, ajabu kijana yule alikeleza.

    Mara nikapigwa picha za paspoti, mara pasipoti ikakamilika.

    Hatimaye ikawa safari, nakumbuka jina moja lilikuwa linasemwa mara kwa mara lakini sikutilia maanani kwa sababu ya ushamba wqa kupanda ndege lakini nilisikia juu ya kampuni inaitwa VONSO kama sikosei… na hata tulipofika Dubai nilisikia tenma kuhusu hiyo kampuni, na Oman vilevile nilisikia.

    Lakini baada ya kufika Oman tukapokonywa pasi zetu za kusafiria, tulikuwa wane… tukapokonywa simu zetu. Mimi na mwenzangu, wenzetu wawili hawakuwa na simu.

    Tulipofika Oman haikuwa kazi ya mgahawa wala hoteli, ilikuwa ni kazi ya ndani ya ntyumba za watu. Makabidhiano yao yalifanyika katika lugha ya kiarabu na hakuna nilichoambulia asilani.

    Kaka yangu, kazi ni kazi aidha iwe ya mgahawa ama la! Lakini kilichosababisha mimi kuwa hapa sio ugumu wa kazi bali ni changamoto katika ile kazi… ni changamoto hizo zitakazopelekea mimi kupoteza maisha… na nitakufa kabla sijatimiza miaka ishirini na mbili……”

    Latipha alisita kusimulia, akatazama mlangoni, alikuwa anaitwa na yule msimamizi.

    “Anaenda kunibaka…” alisema Latipha kwa sauti ya chini. Rama akasikia kauli ile…….

    Lakini angefanya nini angali yule bwana alikuwa na bunduki katika kiuno chake??

    Akasubiri sana Latipha aweze kurejea na kuendelea kumsimulia ilikuwaje hadi akaingia katika chimbo hilo la mauti…..

    Lakini kamwe Latipha hakuwahi kurejea katika macho ya Rama!

    Alikufa binti yule!

    Hakika alikufa akiwa hajatimiza miaka ishirini na mbili



    Wakati Rama anasahaulika Sajini kwa amri ya mkuu wake wa kazi akatakiwa kufanya mawasiliano na Zay B ili mara moja arejee nchini Tanzania akatulie nyumbani kwao Zanzibar!

    Na hapohapo akatakiwa rasmi kulifunga jalada la kumsaka Vonso na kampuni yake lililokaa wazi kwa miaka zaidi ya kumi bila muafaka.

    Ni simu hii ya kutoka Tanzania kwenda Oman iliyozuka balaa jipya.

    Majibu yakaelezea kuwa kuna wawakilishi rasmi kutoka Tanzania walifika Oman katika makazi aliyokuwa akiishi Zay B na kuelezea kuwa anatakiwa mara moja nyumbani Tanzania, watu hao walikuja na nyaraka zote za kiofisi kuthibitisha kuwa wapo pale kihalali.

    Watu wale wakatokomea pamoja na Zay B na mizigo yake michache.

    Walikuwa na tiketi ya ndege kabisa maalumu kwa ajili ya Zay B.

    Sajini Pilipili alichoka, lakini Inspekta generali wa polisi alichoka zaidi.

    Ilikuwa ni vita mpya!!

    Vita dhidi ya watu wanaojulikana lakini wasiojulikana kwao!!

    IGP akaingia katika Pumbazo na kwa ghadhabu kubwa sana ya kuona kuwa adui yao anawafanya kama watoto wadogo, huku akilidhalilisha jeshi kakamavu kabisa la polisi la Tanzania

    IGP hakuwa tayari dharau hizi ziendelee huku raia wakiumia akaamua kuingia vitani tena, hakukubali kurudi nyuma.

    Akachukua simu yake akatafuta namba aliyokuwa anaihitaji.

    Akapiga na kusikiliza kwa muda, ikapokelewa na mtu aliyekuwa kilabuni analewa, alizungumza kilevilevi.

    IGP akakata simu huku akitokwa na tusi zito haswa kwa lugha ya kifaransa.

    Akaitazama simu ile kisha akalisoma lile jina katika simu.

    GEZA ULOLE!!

    Akamalizia kwa kulitafsiri.

    IGA UFE!

    Na mwisho akaponyokwa na kicheko kisichokuwa kichekesho!

    ____

    SIMU ya sajenti Pilipili iliita, ndo kwanza likuwa amefika nyumbani kwake majira ya saa mbili usiku akiwa anatoka katika uwajibikaji.

    Ilikuwa simu ya mkuu wakewa kazi, ambaye muda si mrefu walikuwa wamezungumza juu ya ukimya na utata mpya juu ya afande Zay B. afande aliyesifika kwa kuwa na shabaha kali atumiapo silaha na askari pekee wa kike aliyekuwa amewiva haswa katika mapambano ya ana kwa ana!

    Sasa alikuwa matatani!

    Mikononi mwa wale waliouondoa uhai wa Rama.

    Sajenti alipokea upesi huku akiliita jina la mkuu wake kwa kutangulisha heshima ya ‘mkuu’.

    “Pilipili… nakutumia namba ya mtu, sijui alipo kwa sasa lakini nadhani ni kumbi za starehe namuhitaji sana tafadhali naomba umlete usiku huu huu. Sitoki ofisini nakusubiri wewe nay eye. Narudia tena nakusubiri wewe nay eye, usije mwenyewe Pilipili.” Akamaliza kuzungumza akakata simu IGP.

    Afande pilipili akabaki kulalamika mwenyewe akijiona ameonewa sana kwa maelezo yale yasiyohitaji yeye kujibu lolote.

    Akiwa bado anaduwaa akatumiwa namba ya simu, ujumbe ule licha ya kuwa na namba ya simu ulikuwa na maneno ya ziada.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ANAJIITA GEZA….”

    Sajenti pilipili alikuwa na uchovu lakini angefanya nini na sheria zinamlazimu kuwajibika masaa ishirini na nne. Tena hapa ameagizwa na mkuu wake wa kazi anayemzidi vyeo.

    Sajenti akaishia kujilaumu mwenyewe huku akigeuza na kutoka nje ya nyumba yake.

    Akapiga simu katika kitengo cha siri, akajieleza shida yake na kuitaja ile namba ya simu akapewa maelekezo ni wapi inapatikana.

    Sajenti akatabasamu baada ya kusikia kuwa mwenye ile namba yupo Magomeni Mikumi!

    Alifurahi kwa sababu muhusika hakuwa mbali sana kutoka eneo alilokuwepo yeye la Mwembechai!

    Akaondoka hadi lile eneo akapiga tena simu akaelekezwa zaidi, kisha wale waliokuwa wanamuelekeza wakapiga simu ile inayotakiwa huku Pilipili akiwa makini kabisa kutazama ni nani atakayepokea.

    Mtego wake wa kwanza kabisa aliuweka katika ukumbi maarufu wea lango la jiji.

    Kweli!? Akawa sahihi , akamuona mwanaume mmoja asiyekuwa wa kisasa sana akinyanyua simu yake kilevilevi na kuanza kuzungumza na upande wa pili.

    “Nimemuona tayari!” sajenti Pilipili akautaarifu upandewa pili kisha akamfikia yule mtu na kuketi jirani naye kana kwamba hana habari naye.

    Swali likaja, ataanzaje kumkamata? Je amtie pingu ama azungumze naye… kistaarabu na kuondoka naye.

    Utata huu ukamfanya awasiline na mkuu wake wa kazi.

    “Hebu nipatie niongee naye…” IGP alisema na mara Pilipili akakurupuka kama mwendawazimu akamfuata yule mwanaume. Akampatia simu!

    Yule bwana badala ya kupokea akambwatukia pilipili! Pilipili akajirekebisha akamweleza kuwa kuna mtu anataka kuzungumza naye.

    Hapo ndipo akaipokea.

    “Geza ni mimi…ni mimi Sungura Sungura! Nakuhitaji sana tafadhali…” alizungumza IGP.

    Wkati IGP akitarajia Geza atajiuma uma ama kushtuka haikuwa hivyo Geza akajibu kama anayejiuliza.

    “Sasa leo vipi kuhusu mademu wangu sasa, halafu wako wawili.” Aliuliza Geza kwa sauti thabiti kabisa bila wasiwasi.

    “Mademu… ndo kina nani?” alihoji IGP.

    “Nina mademu wawili…. Wasichana nawapa pombe nan do kwanza tumeanza! Au nije nao!?” alihoji Geza kiumakini kabisa.

    Mazungumzo ya Geza Ulole yakamuacha hoi Pilipili, hakuwahi kumjua kiumbe huyu hata siku moja sasa anashanga aanavyoongea na IGP kama mtu na rafiki yake ambaye wanataniana kupita kiasi.

    Simu ikakatwa Geza akamgeukia Pilipili huku akimkabidhi simu.

    “Amekubali niongozane na mademu zangu.” Akamweleza huku akisimama, akamshika mkono Pilipili wakaondoka huku Pilipili akistaajabu mbona Geza amesema anaongozana na wanawake lakini hajafanya hivyo!

    Loh! Ni vile tu alikuwa hamjui Geza vizuri!

    Laiti kama angekuwa amewahi kukutana naye wala asingehangaika na vituko vyake.

    _____

    MAONGEZI yao yalichukua muda mrefu, vibweka vya Geza alivifahamu IGP lakini hivi havikusababisha ausahau utendaji kazi wa raia mwema huyu ambaye hapendi makuu lakini ukitaka ugombane naye basi mnyime haki yake, amewahi kuwafikisha pabaya watu mbalimbali waliokuwa wanaihujumu serikali na wala hakuwahi kudai malipo.

    Pia aliwahi kuwa MCHUMA JANGA pale aliponunua kesi isiyomuhusu kabisa akitokea kijijini nmkoani Mwanza. Kesi aliyoisikia redioni yeye akaamua kufunga safari hadi Dar es salaam ili kuutafuta ukweli.

    Huyu ndiye Geza, mwanaume asiyekuwa na ndugu. Anadai kwa mdomo wake kuwa ndugu yake ni maisha ya kumsaka adui na kumwadabisha.

    Sasa amesikia juu ya kampuni iitwayo VONSO ama si kampuni bali mtu, ambaye anasadikika kujihusisha na vitendo vya unyanyasaji lakini hajawahi kupatikana shuhuda kusema juu ya hili.

    Geza akatabasamu aliposhirikishwa juu ya hilo, akaambiwa kuwa atashirikiana kiukaribu kabisa na Pilipili.

    “Kwa hiyo na mimi nitapanda pipa kabisa kwenda Oman doh! Nitafurahi siku hiyo… nikaone sasa watoto wa kiarabu ikiwezekana sasa naoa hukohuko.” Geza alizungumza huku akitabasamu.

    Pilipili akashtuka akidhani yule bwana amerukwa na akili.

    IGP akamwambia ye akitaka kuoa aoe tu ila cha msingi jibu kwanza lipatikane.

    “We unajisemea tu kuoa unadhani wale mahari ni mbuzi kumi na ng’ombe kama kwenu usukumani!” IGP akarusha kijembe.

    Akidhani kuwa amemuweza Geza, mara likamtoka jibu Geza Ulole.

    “Unadhani hii kazi nitaifanya bure, pesa mtakayonilipa ndo hiyo nitatoa mahari! Lazima nioe mwarabu nasema!”

    IGP akakubali yaishe akawaaga wawili wale na kuwasihi wafanye kazi kwa ushirikiano ili watoe matunda mema.

    Sajenti Pilipili alibaki ndani kwa muda kama wa dakika moja wakati Geza akiwa ametoka nje tayari akiimba nyimbo kwa kabila la kisukuma, hakuwa anaimba vizuri lakini alionekana kufurahia sana.

    Tutajuaje? Labda nd’o zilikuwa zinampandisha mori?

    Acha aimbe bwana!

    Huko ndani Sajenti Pilipili alimshangaawaziwazi mkuu wake wa kazi kwa aina ya msaidizi aliyompatia, alimchambua Geza haswa kwa kauli zake alizoziona nzito lakini IGP akaziona ni nyepesi sana akawa anatikisa kichwa tu.

    “Tazama mkuu, nikitazama watu zaidi ya kumi majasiri kabisa na machachari waliopambana katika hili jambo kwa hiyo miaka kumi, tazama Shakir, Nunda, Kazimoto, Vandame, Suzani gaidi la kike, Inspekta Macha…. Wote hawa mkuu kweli kuna hata mmoja ambaye anaweza kulinganishwa na huyu jamaa yako sijui Giza……” hapo sasa IGP akampungia mkono kumzuia asizungumze kwa sababu alimwona anayevuka mipaka.

    “Anaitwa Geza, zingatia jina lake” akasita akamtazama kisha akamrushia swali.

    “Hao wote uliowataja zaidi ya kuwasoma katika mafaili umewahi kufanyanao kazi?” lilikuwa swali la ghafla ambalo jibu lake ni HAPANA……

    Pilipili hakujibu!

    “Simama uende.. tazama unayefanyanaye kazi na sio uliowasoma kwnye makaratasi waliojazwa sifa kedekede angali walikuwa waoga wa kutupwa waliojivika ubabe wa kuminya wafungwa kumbe wao wakifinywa kidogo tu wanataja hadi rangi za nguo zao za ndani…..” alizungumza kwa utulivu IGP.

    Utulivu ule ulimaanisha kuwa anakaribia kukasirika….. na lile jibu alilotoa lilikuwa tusi kwa Sajenti Pilipili, anayesifika kwa kuminya wafungwa!!

    Sajenti akasimama, akapiga saluti na kutoka nje!!

    Huko nje Sajenti alimkuta Geza sasa hakuwa akiimba tu, bali alikuwa anacheza ngoma anayoijua yeye huku akijipigia makofi mwenyewe.

    Sajenti alivyofika Geza naye akaimalizia ngoma yake kwa vigelegele.

    “Mwanamashimba namkumbukia hapa!” Geza akazungumza akiwa anamwambia Sajenti. Sajenti hakujibu akampuuza na kuzidi kuamini kuwa amepewa mgonjwa wa akili afanye naye kazi nzito.

    Kwa mara ya kwanza lile wazo lililopita kichwani mwa Rama kuwa amegeuzwa chambo, sajenti naye akawaza hivyo!!

    “Mi nakwenda nyumbani kulala, tutakutana kesho tuone tunapoanzia..” alizungumza kivivu huku akitaka kuondoka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Geza akaduwaa na hakumwacha hivihivi aende bila kumtolea uvivu. Sasa hakuwa na masihara hata kidogo. Akamdaka mkono, Sajenti akauhisi ule ukakamavu katika mikono ya bwana huyu ambaye alikuwa haelewekieleweki.

    “Tumezungumzia hapo ndani kuwa dada zetu wanakufa tena vifo vya kifedhuli, tumezungumzia kifo cha afande Rama kijana mtiifu aliyekufa kwa sababu zisizokuwa sababu, bado mmesema sijui afande Zainabu naye yupomatatani… halafu wewe unaenda kulala. Hivi mnatania mliyokuwa mnasema ama mnamaanisha!?” Geza alihoji akiwa anamkazia macho Pilipili.

    Kijasho chembamba kikamtoka Pilipili.

    Akataka kutoa hoja yoyote ya kujibu lakini akakosa la kusema. Hakutarajia shambulizi lile la ghafla kutoka kwa mshirika wake.

    Geza akawa mshindi!

    Pilipili hakurudi nyumbani kwake, wakaenda hadi nyumbani kwa Geza Ulole.

    Kalamu na karatasi mezani, Geza na Pilipili kazini!

    Usiku ule ulizaa matunda ya awali kabisa.

    Pilipili alirejea nyumbani kwake asubuhi huku akikiri kuwa Geza Ulole ni kichwa kingine cha aina yake kati ya vichwa alivyowahi kukutana navyo.

    _____

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog