Simulizi : 11: 00 pm
Sehemu Ya Pili (2)
Upepo mkali uliokuwa ziwani kwa siku hiyo ulizidi kuwapa shida wale maaskali wa Tsa mawimbi makubwa makubwa yalizidi kuyumbisha boti yao na kufanya hali ya uoga ianze kutawala kwenye mioyo ya maasakali wale
mtumbwi aliokuwamo eric ulizidi kuyumbishwa huku na kule hakuwa akijua chochote kilichokuwa kinaendelea duniani fahamu hazikuwa mwilini mwake
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wimbi kubwa lililoambatana na upepo lilibeba mtumbwi wa eric na kupeleka msobe msobe hadi kwenye mwamba uliokuwa humo ziwani kisha ukaubamiza pale na kuupasua
kitendo cha kubebwa kwa mtumbwi ule n wimbi kisha kupasuka kilishuhudiwa na maasakali wale wa TSA akiwamo na lily hapo wakabainisha kuwa eric atakuwa ameshafariki kwa kile walichokishuhudia
mawimbi yalizidi kupelekwa huku na kule katika ziwa hili hii ilimsaidia eric kupelekwa mbali sana na mwisho akaja kutupwa kwenye kisiwa kidogo cha ghana kilichokuwa karibu kabisa na mji wa bukoba
maumivu makali ya jeraha lake la mkononi ndio yaliyo mtoa eric katika guba lile la usingizi mzito
akaangaza huku na kule huku macho yake yakiwa kwenye usingizi mzito sana akajinyanyua na kujiweka vizuri kwenye kitanda kile cha kamba akaangaza huku na kule lakini bado hakuwa na kumbu kumbu sahihi ,maumivu makali yaliyokuwa yanamkabii kwenye mkono wake ndio yaliyomkumbusha kwa kiasi kidogo kuwa alikuwa anafukuzwa na maaskali wa TSa zaidi ya hapo hakuwa akijua nini kimemtokea hadi akawa sehemu ile ambayo ilionekana kuu kuu kwa jinsi nyumba ilivyoonekana
akiwa mahala pale alisikia kishindo cha mtu akija hapo akajiweka tayari kumvamia huyo mtu hakuwa akijua kama alimsaidia ama laa kikubwa alichokuwa anakitaka yeye ni kujiwekea ulinzi
akiwa amesimama pale mlangoni alishtushwa kumuona msichana akiingia huku akiwa amebeba mzigo wa kuni akataka kumvamia lakini akaikuta akimkumbatia tu na kumlalia hakuwa amelejewa na nguvu kama hapo awali
maji ya vuguvugu yaliyochanganywa na chumvi ndio yaliyomtoa kwenye hali ile ya kuzimia kajitahidi kunyanyuka lakini akarudi kitandani sumu ya risasi ile bado haikuwa imetoka mwilini mwake
akaangaza hapa na pale macho yake yakaja kutua kwa yule msichana ambaye aliamini ndiye alimsaidia alikuwa ila alishtushwa na hali ya yule msichana kuishi kwenye kile kisiwa peke yake
alitamani kumuuliza mambo mawili matatu ila alishindwa lakini moyoni mwake alitambua ulemavu wa ngozi aliokuwa nao yule msichana umechangia kumpeleka mahala pale kujificha
wiki ya pili ilipofikia ndipo hali ya eric ilikuwa imetengemaa hapa ndipo akapata fursa ya kumtambua vizuri huyu msichana ambaye ameonesha moyo wa kumsaidia
ahsante kwa msaada wako"alishukuru eric
usijari"aliongea yule msichana huku akijibaraguza ki kikekike
baada ya eric kufungua maongezi yake wakaanza kuongelea mambo mbalimbali hapo hapo eric akatumia mwanya huo kumuuliza yule dada kwanini ameamua kujificha kwenye kile kisiwa
swali la eric lilikwangua kovu lililopona kwa msichana yule sasa kidonda chake kilichopona kikawa kimetoneshwa na maumivu yake yakawa mala mbili ya mwanzo
baada ya kumuuliza vile yule dada akaanza kudondosha chozi kisha akaanza kusimulia kuwa
ilikuwa tarehe mosi ya mwezi tano miaka mitatu nyuma
siku hiyo nilikuwa natoka shuleni sekondari moja ya wasichana inaitwa kagunguri ipo ukelewe
nikiwa natoka shule nilikutana na wazee wawili ambao walikuwa walisema kuwa wamepotea hivyo waliitaji niwapeleke kwenye kivuko cha kuelekea ukala kwakuwa sehemu waliyokuwa wanaelekea ilikuwa karibu na nyumbani nikaamua niende nao
tulitembea umbali mrefu sana hapo mzee mmoja akmwambia mwenzie kuwa anaitaji kujisaidia hivyo yule mzee akabaki nyuma akijisaidia mimi na yule mzee mwingine tukaelekea mbele lakini kabla hatujafika mbali nilijikuta nikipigwa na kitu kizito kichwani hapo hapo nikapoteza fahamu
nilikuja kuamka baada ya kusikia watu wakigombana sana sikujua walikuwa wakigombania nini lakini baadaye nilimuona mjomba wangu akibishana na wale watu hapo nikatambua kuwa mjomba wangu alihusika katika bishana yao kukatokea ugomvi mzito wakapigana mapanga na kuchomana visu
wakati hayo yote yanaendelea nilikuwa kwnye chumba kidogo ambacho sikuwa najua nilikuwa sehemu gani
wale watu waligombana sana hapo na mimi nikaona ni nafasi yangu ya kujiokoa kwakuwa dirisha la chumba kile lilionekana kuisha nikajitahidi kulibomoa hadi nikafanikiwa kisha nikatimka pale
huku nyuma nilishuhudia kumuona mjomba akiuwawa kikatili na wale watu ambao niliamini walikuwa wanataka kumdhurumu mjomba pesa ambazo alitakiwa kupewa baada ya kuniuza mimi kwao ila wale watu walimuua na mimi wakataka kuniua
nilikimbia sana hadi nikafika mahala penye wavuvi walikuwa wametia nanga hapo nikawaambia kila kitu nashuru mungu walinielewa na kunipa hifadhi ambapo masaa kadhaa nikaondoka nao
nilifika kwenye kisiwa chetu usiku sana mmoja wa wale wavuvi akawaambia wenzake kuwa ni kheri anisindikize kwani mimi niliwaambia siwezi kulala nao pale ufukweni
baada ya kuondoka na yule jamaa njiani akaanza kuniletea vibweka
ambapo alitaka kunibaka ili akiingia ziwani apate samaki wengi
Yule kijana aliyenisindikiza usiku ule alizidi kunisumbua na tulivyokifikia karibu na kichaka akanikaba kisha akaanza kunipeleka kwenye hiko kichaka na kuanza kuzichana nguo zangu
japo nilijitahidi kujinasua ila ilishindikana yule bwana akafanikiwa kuniingilia
baada ya kumaliza akaondoka na kuniacha mahala pale nikiwa na maumivu makali makali sana kwakuwa ilikuwa mara yangu ya kwanza kufanya tendo lile tena kinguvu
nilijizoa zoa kwa kuyumba yumba hadi nyumbani ambapo nilimkuta baba akiwa na mama pale nje waliponiona wakanifata ambapo baba alinibeba na kunipeleka ndani
nilikuja kushituka baada ya kusikia makelele upande wa nje wa nyumba yetu,kwakuwa sikuwa na nguvu nikaenda dirishani kwangu na kuchungulia nje
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mungu wangu"nilijisemea baada ya kumuona mama akiwa chini akigaa gaa huku sehemu yake ya kichwani ikiwa inavuja damu nyingi sana nilipoangalia pembeni nilimuona baba yangu akitweta kwa shida sana kwani kisu kikali kilipenya tumboni mwake na kumchana vibaya sana
japo hali yangu ilikuwa mbaya ila nilijikuta nikipata nguvu nikajua hawa watu watakuwa ni wale ambao walimuua mjomba kule kisiwani hapo nikapata hofu kubwa sana familia yangu ambayo ilikuwa ikipambana kunipa usalama sasa imeangamizwa na mimi ndio nakalibiwa kuangamizwa kwa kukatwa katwa viungo vyangu
hata kuwa humu humu ndani"aliongea kijana mmoja ambaye mkononi mwake alikuwa ameshika panga lililokuwa likivuja damu ya familia yangu
tena ni bikra bhasi tutapata pesa nyingi sana"aliongea kijana mwingine na bila kupoteza mda akaanza kuja ndani na dakika chache baadaye nilishuhudia mlango wa chumba nilichokuwepo ukivunwa na wale jamaa wakiingia hapo sikuwa na ujanja nikakaa kusubili kifo ambacho sasa kinataka kujenga urafiki nami
wale vijana walinikamata kisha mmoja akanipiga na kitu kizito kichwani mwangu hadi nikapoteza fahamu
nilikuja kushituka baada ya upepo kunipuliza nikafungua macho yangu na kuangalia sehemu niliyokuwepo
hapo nikatambua kuwa tulikuwa tunaelekea kwenye kisiwa cha kakukulu, mapigo ya moyo yalinienda kwa kasi sana
dakika chache baadaye tukiwa ziwani hali ya hewa ikaanza kubadilika na ziwa likachafuka vibaya mno , mvua ilianza kunyesha huku mawimbi makubwa makubwa yakianza kuupiga mtumbwi ule tuliokuwepo
hii itakuwa ni laana inabidi tukitupe hiki kiumbe cha ajabu ziwani"aliongea kijana mmoja kati ya majambazi wale na bila kupoteza mda akaanza kunifata
ndio hii ni laana kwa mtu kama huyu kupita ziwani mizimu itakuwa imekasirika na inaweza ikatuangamiza tumtupe tu tutamtafuta mwingine
"alidakia mwengine na kuongeza
hapo likanzishwa zogo kali ambalo mada kubwa ni mimi kutupwa mle ziwani tena kibaya zaidi wale watu walinifunga kamba mikononi na miguuni
wale wenzie walibaki wakiniangalia tu tena sura zao zilioneshwa kuchukizwa sana kwani waliamini mimi ndio chanzo cha dhoruba ile ziwani
baada ya bwana yule kunifikia hakutaka kuongea nami akanibeba na kunitupa majini kisha akanitema mate kuashilia nilikuwa mkosi mkubwa kwao kisha wakawasha mtumbwi wao na kuondoka mahala pale wakiniacha nikizama ndani ya maji
japo nilipiga makelele ya kuomba msaada lakini wale bwana hawakunisaidia tena walizidi kuongeza mwendo wakiamini uwepo wao karibu yangu utakuwa laana kubwa kwao
nilizidi kuzama hadi chini na kwakuwa sikuwa naweza kuogelea kutokana na kufungwa kamba miguuni na mikononi nikawa nasubilia kifo changu tu
nilizidi kunywa maji ya mle ziwani huku pumzi ikizidi kukata mwilini mwangu nguvu nazo zikaanza kuniisha kwa kasi ya ajabu hapo nikaona nakaribia kufa kifo kibaya cha maji
nikiwa katika hali mbaya nikaanza kukumbuka vifo vya familia yangu hapo roho yangu ikawa na ujasiri wa kukikalibia kifo nikawa tayari kufa maji nikafumba macho kusubili kifo
pwaaa"nilisikia kitu kikizama ndani ya maji kisha nikahisi nikishikwa na kuvutwa juu kisha nikawekwa kwenye mtumbwi na baadaye yule aliyeniokoa akaanza kupiga kasia na kuja kwenye hiki kisiwa
nilikuja kupata fahamu siku ya tatu nikiwa kwenye hiki kitanda ulicholala wewe nilipoangaza kuangalia aliyenipa msaada alikuwa ni mzee ambaye alikuwa akikooa mala kwa mala
yule mzee alinieleza kuwa usiku ule wakati wale mabwana wananitosa ziwani aliniona ndio maana akanisaidi kisha akaniambia kuwa yeye ni mvuvi wa miaka mingi pale kisiwani na katika kisiwa kile alikuwa akiishi mwenyewe kama mvuvi baada ya kutengwa na familia yao na kuitwa mchawi hivyo akaamua kuja kuishi pale mwenyewe
nilimshukuru mzee yule ambaye alinipa hifadhi na kunionesha upendo mkubwa hata nikaanza kusahau yaliyoitokea familia yangu
siku zikaenda lakini miezi mitatu mbele yule mzee alizidiwa na ugonjwa wa kansa nilimuhudumia kwa nguvu zangu zote lakini mungu alionesha mapenzi makubwa akaamua kumchukua ila aliniachia usia kuwa nisiwachukie maadui zangu ndio maana mimi nilikusaidia wewe japo hiyo ngozi yako inanidharau na kutamani kuniua
baada ya kumaliza kuadithia akanyanyuka pale na kueleka nje huku eric akibaki na maswali kadhaa juu ya msichana yule..
Simulizi ya yule msichana albino ilileta hisia nyingine kwaeric hii ilikuwa ni hisia ya kisasi japo hakutaka kuishi kwa visasi ila sasa ameamua kulipiza kisasi
akajinyanyua kutoka kwenye kile kitanda na kwenda nje ambapo akaunganisha hadi jikoni huko akamkuta yule msichana albino akiwa anachemsha viazi na samaki akaketi pembeni yake
nataka kukwambia jambo"aliongea eric kwa sauti ya upole huku akimuangalia msichana yule
jambo gani"aliuliza yule msichana
natarajia kuondoka siku ya kesho hivyo nimekuja kukuaga"aliongea eric kwa sura ya kumaanisha
yule msichana albino alibaki kimya akimuangalia eric alitamani kumwambia abaki ila akajikuta akimuangalia tu bila kuongea chochote
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
usiku wa siku hiyo eric alikuwa kimya kabisa huku macho yake yakiwa yametulia tulia kwenye ukuta alikuwa na mawazo mengi juu ya mpango wake wa kulipiza kisasi baada ya kufikilia kwa mda akapata jawabu sehemu ya kuanzia hapo akacheka kwa dharau sana
nakuja kumalizia dakika zilizobakia za mchezo hivyo mjiandae"alijisemea eric kisha akauweka mto vizuri na kulala
makelele yalikuwa yakisikika kwa sana katika stand kuu ya mabasi ubungo kila mmoja alionekana yupo bize na kile alichokuwa anakifanya
basi la green safari linalotokea jijini mwanza lilikuwa likiwasiri mda huu wa saa mbili usiku abilia wakaanza kushuka na kutawanyika huku na kule abilia wa mwisho kushuka alikuwa eric sasa anaikanyaga ardhi ya dar kuja kukamilisha adhima yake ya kisasi kwa bwana alex ndaro na jopo lake ambalo lilimpa mkataba wa kuua lakini wakamgeuka na kutaka kumuua baada ya kukamilisha kazi yao
naomba unipeleke manzese"alitoa maelekezo eric baada ya kupanda tax na dereva akaiwasha kisha akaanza kuelekea huko
dakika chache baadaye tax ile ikasimama kwenye kituo cha manzese hapo akashuka na kutokomea alipokuwa anapajua yeye
safari yake iliishia kwenye nyumba ya wageni iliyokuwa mahala hapo akachukua chumba na kujipumzisha usiku huo
siku ya pili ilimkuta eric akiwa mbele ya super market kubwa ya mlimani alikuwa amesimama kalibu kabisa na sehemu za kuegesha magari alikaa pale kwa dakika kadhaa kisha ikaonekana gari ndogo ikija nayo ikapaki mahala hapo bila kupoteza mda eric akapanda gari ile kisha akatimka nayo
safari yake iliishia mwenge ambapo eric alishushwa lakini mda huu alikuwa tofauti na alivyopanda mda huu alishuka akiwa na begi jeusi la mgongoni
baada ya kushuka akachukua bodaboda hadi tabata balakuda hapo akashuka kisha akaendea mnazi na kusimama hapo dakika chache baadaye akaja kijana mmoja akiwa na kiboks kidogo mkononi mwake wakakabidhiana kwa kubadilishana kisha eric akaondoka huku akijisifu kwa kila hatua aliyokuwa anaipiga
baada ya kuhakikisha amepata kila alichokuwa anakitaka akaludi tena kule guest akachukua mizigo yake na kutimka
....
Muito wa simu uliendelea kusikika maladufu kwenye ofisi ya bwana alex ndaro ,ilikuwa mala ya tano simu hii ikiita bila kupkelewa
japo ilikuwa haipokelewi ila mpigaji wa simu hakutaka kukata tamaa alizidi kupiga simu ile lakini bado haikupokelewa
baada ya simu ile kukata dakika tano baadaye mlango wa ofisi ya alex ndaro ukagongwa na sauti ya kuruhusu mtu aingie ndani ikasikika
katibu mukhtasi akaingia ndani akiwa ameshika barua ndogo akamkabidhi bwana alex ndaro na kutoka nje
bila kupoteza mda alex ndaro akaifungua bahasha ile na kuanza kuisoma lakini kabla hajamalizia kuisoma akajikuta akiitupa chini hapo hapo akatoka nje kwa kasi sana hadi kwa secrtary wake
huyu aliyeleta barua hii umemuona? Aliuliza bwana eric huku akionekana hana utulivu kabisa
baada ya kuona hapati jibu la kile alichouliza akaamua kurudi ndani kiti alikiona cha moto akawa anazunguka huku na kule ndani ya ofisi yake
dakika chache baadaye simu yake ikaanza kuita ila hii namba ilikuwa tofauti na ile ya awali akaipokea haraka haraka na kuiweka sikioni
unajua umeniuzi sana yani kama ungepokea simu yangu hapo awali nadhani haya yasingetokea kabisa"alisikika mtu yule akiongea simuni
bwana alex akapagawa ofisi ikawa chungu kwa mda huo
akiwa katika lindi la mawazo simu yake ikaita kwa mala nyingine namba ilikuwa ile ile
akaipokea na kuiweka sikioni haraka haraka
hallow"aliongea alex ndaro kwa pupa
ndio bwana mkubwa sasa nimeshamaliza kazi hapa nyumbani kwako na mda huu namalizia kutenganisha viungo vya mke wako na baadaye watafata wanao ila kwa sasa simu yangu inaisha chaji hivyo nitakupigia baadaye kukwambia kuwa nimefanikiwa kuwachinja wanao wote baada ya kuichaji simu yangu"alisikika mtu yule na simu ikakatwa japo alijitahidi kupoiga namba ile haikuwa hewani sasa akabaki kama kichaa akanyanyua simu yake na kumpigia mke wake lakini haikupokelewa hofu ikamjaa bwana alex
akiwa katikati ya mawazo ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yake ilikuwa ni picha imetumwa kwenye upande wa whatsapp akaufungua na kupakua simu ile
mung wangu"alipiga kelele alex ndaro kile alichokiona kwenye picha ile kikamfanya ashindwe kuzuia machozi yake kutililika mashavuni mwake
Picha ile aliyotumiwa bwana alex ndaro ilimuweka mashakani hakuwa akijua afanye nini kwa mda huo hofu ilikuwa kubwa sana kila alipoifikilia familia yake alihisi kuchanganyikiwa maladufu
akiwa amesimama kwa kuegemea ukuta mala simu yake ikaanza kuita ilikuwa ni namba ya mlinzi kama ilivyosomeka kwenye kioo cha simu yake ,akaipokea simu ile na kuiweka sikioni ajabu hakusikika mtu akiongea chochote zaidi alisikia vilio tu vya watu wakiomba msaada kisha kimya kikali kikachuka hatua hapo bwana ndaro akachanganyikiwa akajikuta akitoka nduki ofisini mwake hadi nje akapanda gari lake kisha akaondoka hakujali kama kuna dereva wake ambaye analipwa kwa shughuli hiyo ya kumuendesha
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
jumapili hii hakukuwa na magari kabisa ndani ya jiji hili la dar hali hii ilimuwezesha bwana ndaro kuendesha gari kwa mwendo kasi sana dakika 45 zilimtosha kufika kwake
hakutaka kuingia na gari alichokifanya ni kushuka na kuendea mlango mdogo wa geti akaufungua na kutoma ndani
macho yake yakatua kwenye mwili uliokuwa unaelea juu ya dimbwi la damu ulikuwa mwili wa yule mlinzi miguu yake ikapata kitetemeshi kikuu akaanza kusonga mbele zaidi akafungua mlango na kuzama sebuleni hapo akakutana na jambo lingine akajikuta akiishiwa nguvu na kuzirai
alikuja kupata fahamu usiku wa siku hiyo akiwa kwenye chumba chake maalumu ambacho alikuwa akitibiwa ,akajitahidi kunyanyuka lakini ikashindikana kwakuwa hakuwa na nguvu sahihi mwilini mwake
akaanza kuangaza huku na kule macho yake yakatua kwa watu watatu waliokuwa mbele yake kwa haraka haraka alimtambua huyu mmoja alikuwa IGP Mdoe
familia yangu"alisikika bwana ndaro akiuliza ambapo IGP mdoe alimtoa hofu na kumwmbia kuna msako mkali huko mtaani juu ya kumtafuta muuaji
....
Wakati hali ya hewa ikiwa mbaya tanzania polisi wakiwa wametapakaa kila mahali Eric alikuwa ametulia kwenye kiti cha dirishani kwenye ndege yashirika kubwa la emirates
masaa kadhaa mbele magurudumu ya ndege ile yakatua kwenye nchi ya Sudan kusini kwenye uwanja mkubwa wa YIROL AIRPORT abilia wote wakashuka wa mwisho alikuwa Eric kama kawaida yake akauendea mlango wa wanaowasiri akapita sehemu ya ukaguzi na alipokuwa safi akatoka na kuelekea nje akanyoosha mkono wake ambapo sekunde kadhaa mbele tax ikasimama akapanda na kuanza safari ya kuelekea kwenye motel kubwa ya ALJUBAL GRAND MOTEL
nusu saa baadaye tairi za tax ile zikasimama mbele ya hotel ile kubwa ya kifahali na kwakuwa alishaweka booking kwa njia ya mtandao hivyo haikumuwia shida sana alichokifanya ni kuelekea mapokezi ambapo alijitambulisha kisha akapewa kidaftari kidogo asaini ,alipomaliza akapewa kadi maalumu kisha akafatwa na muhudumu mmoja ambaye alimsindikiza hadi kwenye chumba chake
uchovu wa safari ulimlevya sana kwa mdaa huu aliingia bafuni na kuoga kisha akarudi na kukaa kwenye kochi kubwa lililokuwa chumbani humo akatoa kompyuta yake mpakato na kuanza kuperuzi kwenye mitandao mbali mbali iliyokuwa humo
baada ya kumaliza kuperuzi akafungua sehemu moja iliyokuwa kwenye hiyo kompyuta mpakato akaandika jina la King sudi hapo hapo yakaja maelezo mengi sana na hata ziara zake za nje ya nchi
akiwa anaendelea kuperuzi zaidi akakutana na kile alichotarajia mpaka akapanga kwenye hotel ile kubwa kama sio kuja sudan kusini
siku ya pili ilimkuta eric akiwa kwenye maduka makubwa ya kuuzia nguo zakike akazama kwenye duka kubwa ambalo lilikuwa maarufu sana kwenye jiji hilo hapo akachagua nguo kali za kike baada ya kupata akaachia tabasamu kiasi kisha akaondoka mahala na kurudi hotelini
akakaa ndani nakuanza kupanga mipango juu ya tukio ambalo alitakiwa kulitekeleza usiku huo
saa mbili usiku gari tano za kifahali zikasimama nje ya hotel ile ya kifahali dakika chache baadaye mlango wa gari ya kati kati ukafunguliwa hapo akatoka bwana mmoja mwembamba sana mdomo mwake akiwa na kipisi cha cigar akakidondosha chini kwenye zulia jekundu kisha akakikanyaga
karibu king sudi"alisikika mmoja wa watu wakimkaribisha ambapo baada ya kuingia akaelekea kwenye chumba cha mikutano
nusu saa baadaye kikao kikawa kimeisha king sudi akasindikizwa hadi kwenye chumba alichopanga kilikuwa chumba cha hazi ya juu ambapo kwa usiku mmoja alilipia dola laki 2 za kimalekani ulinzi mkali ulikuwa nje ya mlango wake
eric akalijiandaa kwa kuvaa kikikekike akawa kama shoga
baada ya kujiangalia na kujiona amekaa kama alivyotaka akaanza safari ya kuelekea kwenye chumba cha bwana yule ambaye hakuwa na familia sababu kila mwanamke alimtaka kinyume hivyo akakimbiwa kutokana na tabia yake hiyo baada ya kuona hivyo akaamua kununua wanaume na kuwafanyia mchezo huo
eric alitembea kwa madaha hadi kwenye mlango wa king sudi walinzi wake wakamkagua na walipojilidhisha hakuwa na siraha yoyote wakamluhusu aingie ndani wakiamini alikuwa mwanaume shoga
baada ya eric kuingia ndani hakutaka kuchelewa sana akapeleka mkono wake kwenye wigi alilovaa hapo akatoa sindano ya kusimamisha mapigo ya moyo akamvaa bwana yule na kumchoma dakika chache mbele akawa marehemu
Baada ya eric kumaliza kazi yake akapandisha vioo vya dirishani kisha akapita kisha akaanza kuambaa ambaa kwenye kuta za ghorofa ile hadi kwenye dirisha liliofuata hapo akapenya na kuondoka ambapo baada ya kufika alipitiliza hadi chumbani mwake huko akapakia kila alichokitaka kisha akaliweka begi lake mgongoni baada ya hapo akatimka nje ya chumba kile
jarbar airport"aliongea kwa kifupi eric lakini dereva alimuelewa hivyo gari ikawashwa na safari ya kuelekea huko ikaanza mara moja
mda ulizidi kwenda bila walinzi wale kumona yule mwanaume shoga aliyeingia kutoka nje tangu alipoingia mda wa saa 11:00 pm hofu zikawashika wakajaribu kufungua mlango lakini ulikuwa mgumu sana hii ilionesha ulifungwa kwa ndani hapo hapo wakatoa taarifa kwa wenzao waliokuwa kwa nje bila kupoteza mda nao wakaja juu wakajaribu kuufungua mlango lakini hali ilikuwa ile ile mlango haukufunguka hapo wakatumia siraha zao kufungua mlango ule na dakika kadhaa baada ya kupiga kitasa risasi mlango ukafunguka wakaingia ndani kwa kujigawa wengine walielekea bafuni ambapo kulisikika maji yakimwagika wengine wakaenda chumbani
amemuua"alisikika kijana mmoja baada ya kumuona king sudi akiwa amejiraza kitandani haraka haraka simu ikapigwa kwenye hospital kuu ya jiji hilo na dakika kadhaa mbele motel ile ikawa chini ya ulinzi huku king sudi akipakizwa kwenye gari kwenda kufanyiwa upelelezi wa kile kilichomuua
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
taarifa za kifo cha king sudi zikaenea kwa kasi ya kimbunga taarifa za habari zikalipoti taarifa hii ya kifo chake
walinzi wake walijigawa huku na kule kumtafuta aliyemuua kwakuwa walikuwa wamemuona wakajua haitowawia vigumu kumkata
wapo waliofurahi na waliopatwa na huzuni walio furahi ni wale wasichana walio kuwa wanatumikishwa kwenye madanguro yake katika miji mbali mbali ya nchi hiyo na walio patwa na huzuni ni wale wanaume mashoga ambao kwao king sudi alikuwa kila kitu yeye ndiye aliishauli serikali kupitisha ndoa ya jinsia moja kwakuwa na yeye alikuwa muhanga wa tabia hiyo chafu
tax ile ilitembea kwa dakika kumi hadi kufika airport hapo eric akashuka kisha akampatia pesa yule dereva akaelekea sehemu ya wanaosafiri na nusu saa baadaye ndege ile ikapasua anga lile la sudani kusini
masaa kumi na moja baadaye eric alishitushwa na sauti ya kike iliyokuwa ikitangaza kuwa kila abiria afunge mkanda wake na wale wenye simu na lap top wazizime
baada ya mhudumu yule kutoa taarifa ile kila abiria alifunga mkanda dakika tano baadaye ndege ile kubwa ya shirika la ameican airbus ilitua kwenye ardhi ya malekani kwenye uwanja mkubwa wa john f kennedy
hapo abiria wakaanza kushuka lakini leo eric alikuwa wa mwisho huku sura yake ikiwa na mabadiliko kiasi ndevu na nywele nyingi kichwani zilimpa utofauti sana katika muonekano wake wa kawaida
akashuka na kwenda sehemu ya ukaguzi kama kawaida yake kisha akaenda sehemu ya ukaguzi wa pasport
welcome to america mr fredrick anthony"alisikika msichana mwembamba mwenye asiri ya china akimkaribisha eric marekani hakuwa akijua kama alikuwa anamkalibisha mtu hatari sana kwenye nchi hiyo kubwa
baada ya eric kumaliza kukaguliwa akatoka na kuondoka huku akiwa amebadilika jina hadi muonekano
tax aliyopanda ilimfikisha salama kwenye PAX VIEW MOTEL hapo akaelekea mapokezi na kuchukua chumba baada ya kumaliza akatia sign na kuondoka pale hadi chumbani mwake
baada ya kufika huko akajibwaga kitandani huku begi lake likiwa mbali naye dakika chache baadaye usingizi ukajenga urafiki naye
mwanga hafifu wa jua ulimuamsha kutoka kwenye usingizi ule akaangalia saa yake mkononi ilikuwa saa 7:13 am hapo akajinyanyua kiuvivu sana akaelekea sehemu ya wazi ya chumba kile na kuanza kupiga pushup kadhaa hadi mwili ukachangamka akajinyoosha viungo kwa dakika kadhaa hadi pale ujumbe mfupi ulipoingia kwenye simu yake ndogo
home cafe at 12:30 pm " ulisomeka ujumbe ule mfupi hapo akaacha kile alichokuwa anafanya akaingia bafuni na kuoga kisha akatoka na kuendea kompyuta yake mpakato hapo akaanza kuperuzi hadi ilipotimu saa sita kamili hapo akaizima ile kompyuta yake kisha akaiweka kwenye kile kibegi kisha akakibeba na kuondoka hadi kwenye ile cafe
alipofika hapo alishtushwa na mwanga wa kioo uliompiga usoni akageuka kumuangalia aliyekuwa anammulika hapo akamtambua ni yule bwana aliyekuwa anawasiriana kupitia email
akapiga hatua kadhaa hadi kwa bwana yule alikuwa ni mweusi sana tena mwenye tatoo nyingi usoni sura yake haikuonesha utu hata kidogo
mr mog"aliongea eric huku akimpa mkono bwana yule lakini mr mog hakumpa zaidi alitoa kibegi kidogo akampa eric kisha na yeye akachukua pesa na kutimka
eric akacheka kidogo kisha akachukua kibegi kile na kuondoka zake
safari yake iliishia kwenye vilima cya north hill hapo akasimama na kukagua mzigo wake akafungua na kuukagua hapo akacheka kidogo kwa kupata sumu ile ya ricin kiurahisi vile
Baada ya eric kuhakikisha sumu yake ipo kama kawaida akapanda gari na kurudi zake hotelin
uchovu mkubwa aliokuwa nao mwilini mwake ulimfanya ajilaze kwenye kile kitanda cha thamani sana huku akiweka alarm kwenye saa iliyokuwa jirani yake
saa nne kasoro za usiku alarm ile ikaanza kuita hapo akaamka kiuvivu akaelekea bafuni ambapo alioga kisha akarudi mle chumbani akavaa nguo zake za kazi ambazo kwa ndani tena alivaa suti nyeusi iliyomkaa vizuri sana ,
baada ya kujiona yuko safi akachukua kichupa kidogo chenye sumu ya ricin akafungua kizibo kisha akaimwaga kwenye kile kitambaa baada ya hapo akachukua pasi na kupiga kwenye kitambaa kile mda huo alikuwa amefunika pua zake ili asivute hewa ile
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
baada ya kumaliza akatoka nje ya hotel ile kwa mwendo wa dakika tano akafika kwenye barabara hapo akasimamisha tax kisha akapanda kuelekea kwenye casino kubwa la NIGHT STRIPERS
dakika kumi na tano zilitosha kumfikisha kwenye casino hilo kubwa nchini marekani akaelekea kwenye mlango wa kuingilia casino hapo akakutana na watu wawili waliojazia vyema huku sura zao zikiwa hazina hata chembe la tabasamu
akatoa tiket yake ya kuingilia humo casino mmoja wa wale mabaunsa wakaichukua na kuikagua na walipolidhika nayo wakamruhusu aingie casino
usiku wa siku hii casino ilikuwa imechangamka sana viongozi mbali mbali wa nchi ya marekani wanaopenda starehe walikuwa ndani ya casino hili kubwa
ukiachana na viongozi hao kulikuwa na warembo wakila mataifa wao walikuwa wakishindana kukata nyonga zao tena wakiwa watupu kama walivyozaliwa
wasichana wengine walikuwa wamesimama juu ya meza za watu ambao kwa kuwaangalia tu walionekana watu na fedha zao
mmh"aliguna eric baada ya kumuona msichana mmoja akiwa amelala juu ya meza akiwa mtupu kabisa huku wanaume wakishindana kuchomeka pesa sehemu zake za siri nayeye alikuwa akizichomoa na kuzisika mikononi mwake hakika casino hili lilikuwa limetawaliwa na ushetani wa hali ya juu
akiwa anaangaza huku na kule hatimae macho yake yakatua kwa yule aliyemfanya akapoteza dora laki moja za kimarekanai kuingia kwenye casino hili huy alikuwa waziri wa fedha nchini marekani bwana jonh lincoln muda huu ndio alikuwa akiingia ndani ya casino lile akamuangalia kwa tuo hadi sehemu ambayo bwana yule alikuwa akielekea na mwisho sehemu aliyokaa hapo akalidhika
dakika chache baadaye alimuona mhudumu akiwa amebeba kisinia cha vinywaji alitambua alikuwa anapelekewa bwana lincorn hapo akanyanyuka kisha akaanza kuelekea kwa yule muhudumu alipomfikia akatoa unga kidogo na kuushika kwenye vidole vyake na alipomkalibia akashika grass moja wapo
ina oda hiyo"aliongea yule muhudumu
ooh samahani"aliongea eric lakini mda huo alikuwa ameshaweka ile dawa kwenye ile grass ya kinywaji
baada ya kuweka akapitiliza hadi bafuni huko akakitoa kitambaa chake alichokiwekea sumu ya ricin baada ya hapo akakiweka kwenye mfuko wa juu wa koti lake
alipomaliza hivyo akatoka na kurudi casino akakaa pale counter
ilikuwa imeshatimu saa 10:52pm zilibaki dakika 8 amalize kazi yake hapo akamuona lincorn amenyanyuka akielekea chooni huku walinzi wake wakimfata kwa nyuma hapo akanyanyuka na kuelekea chooni kabla lincorn hajaingia
baada ya kuzama akapitiliza sehemu za kukojoa dakika moja baadaye mlango ukafunguliwa bwana lincorn akazama ndani na walinzi wake wakakaa mlangoni
bwana lincorn bila kujua kama anawindwa alielekea sehemu ya kukojoa taratibu akafungua zipu na kuanza kukoja ile dawa aliyowekewa ya kumfanya mtu akojoe ilifanya kazi yake
baada ya kumaliza kukojoa chafya kali akaanza kupiga hapo eric akatoa kile kitambaa na kumpa bila kujua bwana lincorn akakichukua na kujifuta nacho maji maji yaliyotoka mdomoni yalilainisha kitambaa kile hapo sumu ile ikajichanganya kwenye maji na alipovuta hewa ikaingia mwilini
eric baada ya kuona amefanikiwa akatoka ndani ya choo kile na kwenda counter dakika chache mbele alishuhudia wale walinzi wake wakiingia ndani ya choo kile kisha wakatoka wakiwa wamembeba bwana lincorn ambaye muda huo alikuwa akivuja damu sehemu mbali mbali za mwili wake
damu nyingi zilimtoka puani na mdomoni dakika zilivyosonga zikaanza kumtoka machoni na masikioni hapo akapakizwa kwenye gari lake lakini kabla hajafikishwa kwenye hospital kubwa ya carfonia tayari alishakata roho
hadi anafikishwa hospital mwili wake ulikuwa hauna uhai tena doctor mathew aliwathibitishia hilo baada ya uchunguzi
kifo cha ghafla cha waziri wa fedha nchini marekani kilikuwa gumzo kubwa sana hadi siku ya tano ilipotoka liport ya uchunguzi kuwa alikuwa amevuta hewa yenye sumu mbaya ya ricin
habari ya kifo chake ilikuwa gumzo ndani ya jiji la carfonia na marekani na hata kwa dunia nzima habari zikaanza kurushwa huku na kule huku wapelelezi wakiingia kazini kulafatilia swala hili
siku ya tano ambayo marekani ilikuwa na huzuni ndege la shirika la japan airwings ilikuwa ikitua ndani ya mji mkuu wa jiji hilo hapo akashuka eric huku alikuwa na kazi nyingine
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment