Simulizi : 11: 00 pm
Sehemu Ya Tatu (3)
Baada ya ndege ile kubwa kutua kwenye uwanja mkubwa wa ndege wa Achinginijo wa japani eric akashuka huku alikuwa amebadilika kidogo kichwani mwake alikuwa ameweka nywele za kusokota rasta na ndevu nyingi huku kichwani mwake akiwa na kofia kubwa sana
kwenye hotel ya Chinagawa prince ndipo eric alifikia huku jina lake likiwa faree zigi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
huku eric alikuja kwa nia moja tu kuja kumuangamiza bwana shinji inamoto huyu naye alihusika kwa namna moja au nyingine kushiriki katika mchezo wa kutaka kumuangamiza
japo mzee huyu umri ulikuwa umeenda hata akastaafu kazi yake ya waziri humwambii kitu hasa linapokuja suala la mchezo wa sumo akiwa madarakani alishawekeza sana kwenye mchezo huu ambao umeanza kuwa maarufu dunian
leo katika uwanja wa shanching kulikuwa na mpambano mkali kati ya viana wawili mijitu ya miraba minne mchezo huu uliitwa mkali kutokana na wachezaji wake kuwa na upinzani mkubwa
bwana shinji inamoto alikuwa mbele kabisa ya ukumbi akishuhudia pambano hili kali ambalo hakutaka alikose
pambano likiwa linazidi kasi mala simu yake inaita hapo anaiweka sikioni taarifa mbaya aliyoipata inamnyanyua pale kitini haraka haraka anaanza kupiga hatua nje ya uwanja ule
akiw anatoka nje simu mfululizo zinaingia kila anayeongea naye anampa pole juu ya kiwanda chake kuwaka kichwa kinamuuma sana hapo hapo anapoteza fahamu
kitendo kile cha kupoteza fahamu kilimpa ushindi bwana eric alichokifanya usiku huu ni kwenda kwenye hospital ya royal ambapo bwana shinji alipelekwa baada ya kufanikiwa kuingia safari yake ikamfikisha ghorofa ya sita kwenye wodi za viongozi na watu matajiri wa nchi hiyo
ulinzi ulikuwa mkali sana katika wodi ya mzee shinji hii ilimpa hofu kidogo eric kwani alijua kazi yake haiwezi kukamilika kama walinzi wataendelea kuwepo kwenye chumba kile ambacho bwana shinji inamoto alilazwa
akiwa amejibana kwenye kordo moja alimshuhudia mzeee mmoja wa makamo akiingia huyu alikuwa ni daktari baada ya mzee yule kuingia hakukaa sana akatoka na kwa bahati nzuri au mbaya alikuwa akielekea kule ambapo eric alikuwapo
samahani doc kuna mgonjwa wangu yupo hapa sijui unataarifa naye"aliongea eric ila kwa kutumia kijapan fasaha yule mzee alisitaajabika sana kumuona mtu mweusi akimuongelesha kijapani
yupoje"aliuliza yule mzee
mweusi mwembamba mrefu"alieleza eric huku mikono yake ikionesha ishara sambamba naye
ok nifate"aliongea yule mzee kisha akaanza kupiga hatua kufuata kordo
usiku huu hospitar ilikuwa kimya sana hata watu hawakuwa wengi hospitalin
eric alikuwa nyuma akiongozana na yule mzee lakini walipokaribia na mlango wa stoo alitoa sindano yake yenye dawa kali ya usingizi na kumchoma nayo mzee yule shingoni dakika chache usingizi mzito ukawa naye
alichofanya eric ni kumbeba kisha akampeleka hadi kwenye kitanda kimoja kilichokuwa wodini mle akamlaza kisha akamfunika na shuka na alipomaliza akamvua nguo zake za kitabibu kisha akazivaa yeye
ahsante mzee nitakupa zawadi siku zijazo"alijiongeresha eric kimoyomoyo huku akiachia tabasamu usoni mwake hapo akapiga hatua za haraka haraka na kurudi kule kwenye wodi aliyolazwa bwana shinji inamoto huku mkononi mwake akiwa na sinia iliyosheheni dawa na sindano
baada ya kufika kwenye ile wodi akaingia huku sura ikiwa ndani ya tabasamu fake la kitabibu hakuwa na hofu yoyote sura yake ilivaa vazi la kupotosha ambalo ni tabasamu alilokuwa akilitumia kwa kila aliyekuwa anamuangalia mule wodini
baada ya kufika kwa mzee yule akatoa sindano yake ndogo kisha akakitoa na kichupa kidogo akaichomeka ile sindano na kuvuta dawa kisha akaijaribisha kwa kuitoa dawa
kilikuwa ni kichupa kidogo cha dawa yenye rangi ya blue bahari kwa nje unaweza kusema ni dawa au hata ukisoma maandishi ya kichupa kile rakini yeye eric alifanya ujanja wa kuitoa dawa ile kisha akaiweka dawa nyingine ya kutuliza mapigo ya moyo kwa mda wa dakika 45
walinzi wa shinji inamoto walikuwa wakimuangalia hawakuwa wakijua chochote juu ya daktari huyu aliyesimama mbele yao
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
eric aliifanya kazi yake kwa ustadi mkubwa sana kwani saa 10:15 ndipo alipo mdunga sindano ile ya kusimamisha mapigo ya moyo alitambua ikifika saa tano kamili bwana shinji inamoto hatokuwa katika ulimwengu huu kwa jina lake halisi bali kwa jina la marehemu shinji inamoto
baada ya kumaliza kumchoma sindano ile akakusanya vifaa vyake na kuondoka mahala pale huku sura yake ikigubikwa na furaha ya kumaliza kazi ile kiurahisi sana hapo akarudi kwenye ile hotel yake aliyofikia kwa mda huo kisha akajiradha
asubuhi ya saa moja jiji la tokyo likawa kimya kabisa hii ni baada ya taarifa ya waziri mstaafu shinji inamoto kufa ghafla usiku wa siku hiyo muda wa saa tano kamili
eric alikuwa anaangalia tv mda huo akiwa kwenye kile chumba alisikitishwa na taarifa za mtangazahi yule kusema eti bwana shinji alikuwa makalimu na mpole kwenye jamii yake
baada ya kutoka japani safari yake ilikuwa ni ugerman huko napo alikuwa na home work napo...
asubuhi ya saa tatu eric alikuwa ndani ya jiji kubwa la munich
gari ndogo aliyokodisha asubuhi ya siku hiyo ilimfikisha kwenye jingo kubwa la kibiashara jengo la MUNICH BUY&SALES
hapo akasimamisha na kuzama ndani ya jingo hilo mkononi mwake akiwa na kijitabu kidogo ambacho kilikuwa na ramani nzima ya jingo hilo safari yake iliishia kwenye mlango ambao kwa juu kulikuwa na kibao kilichoandikwa Mr schwein Aitkinson hapo akafunga kijitabu chake kisha akagonga mlango ule kwa sekunde kadhaa na baadaye mlango ule ukafunguka
karibu karibu ndani"alisikika mzee yule akimkalibisha eric naye eric akazama ndani
huko akakaa kwa dakika kadhaa kisha akatoka akiwa na mfuko mdogo lakini upande mmoja wa shati lake ulionekana kulowa damu kiasi ila si rahisi kwa mtu kumshuhudia damu ile
baada ya kutoka akaliendea gari lake huku akiwa na kazi moja tu ambayo ndiyo iliyomfanya kumuua yule mzee aliyekwenda kuonana naye muda huo
akawasha gari lake na kutimka mahala pale
tairi za gari ile aina ya voxy wagen zilisimama mbele ya hotel kubwa ya BRAUNSHWERY LOWER SAXOUY HOTEL (BLS HOTEL) hapo akashuka kisha mhudumu wa hotel ile akachukua funguo na kwenda kuipak
baada ya kutoka kwenye ile gari akaziendea ngazi akapanda hadi ghorofa ya pili hapo akakata kushoto kisha akaanza kufata kordo ambayo iliishia kwenye chumba namba 305 akatoa kadi aliyokuwa nayo kisha akazama ndani ya chumba kile
huuu"alishusha pumzi ndefu eric kisha akajibwaga kitandani hapo akaanza kuvuta kumbukumbu ya maisha yake kitu cha kwanza alichokikumbuka ni vifo vya watoto wake mapacha pili kifo cha mke wake na tatu kifo cha yule mwanamke aliyekuwa akiishi naye kule ukala hapo hasira zikampanda japo dakika zilikuwa zikikata kwa kasiila yeye aliona mda hauendi nadhani haraka yake ilimfanya aone hivyo
akiwa pale kitandani huku mawazo mazito yakiwa juu yake usingizi ukaanza kumnyemelea kwa kasi na dakika chache baadaye akawa ndani ya dimbwi la usingizi
alikuja kustuka saa tatu na dakika zake hapo akajinyanyua kiuvivu kisha akaelekea bafuni akaoga na kisha akatoka akaelekea kwenye ule mfuko wake akaufungua hapo akatoa sura bandia iliyokuwa imetengenezwa kwa mfano wa sura ya msichana tena mwafrika
akaivaa sura ile kisha akavaa na nguo za kike zilizoshonewa na maips kwa pembeni baada ya hapo akavaa sindilia iliyokuwa na maziwa feki nusu saa baadaye akawa katika umbile kamili la kisichana ambalo hamna mtu ambaye angeweza kulibaini kwa urahisi
kwa jinsi alivyokuwa wanaume wakwale ambao alipishana kwenye ngazi za hotel hiyo walikuwa wakimdondoshea mate hasa walipoona kijungu cha mwanamke yule
akaliendea gari lingine alilokodisha kisha akaondoka lilikuwa gari la kifahali sana
safari yake iliishia kwenye kambi kubwa ya jeshi iliyokuwa mashariki mwa jiji la munich akasimamisha gari yake sehemu ya ukaguzi na bahada ya kubainika hakuwa amebeba siraha yoyote akaruhusiwa kupita
kwa mwendo wake wa madaha huku akizungusha nyonga yake huku na kule wanajeshi waliokuwa lindo usiku huo walipata shida sana naweza sema kwa muda huo michele leka (eric)alionekana kuwavutia wanajeshi wale hadi wakapagawa
baada ya kufika kwenye nyumba ya kifahari iliyokuwa pembeni mwa kambi ya jeshi hilo michele leka akagonga mlango na dakika kadhaa mlango ukafunguliwa macho ya mfunguaji wa mlango ule yakatua kwenye nido zilizopigwa jerk hapo akameza funda tatu za mate ya tamaa huku moyoni akikili huyu ni mmoja wa wasichana wazuri ukiachana na mama yake
we..wel..welcome"alikaribisha mfunguaji yule wa mlango kwa namna ya kubabaika
thank you"alijibu michele kwa malingo na kwakuwa alishamtambua mlinzi yule akamsogelea kisha akampa busu la shavu na akamshikisha business kadi yake hapo yule mlinzi akapagawa akajihisi anaanza kupandwa na wazimu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
baada ya michele kutoka pale akaelekea kwenye mlango uliokuwa mbele yake akagonga na dakika chache ukafunguliwa hapo akazama ndani
welcome miss michele"mr dwell abraham akamkaribisha ndani
tabasamu pana likaupamba uso wa eric aliyekuwa kwenye umbile la kike
hakutaka kupoteza mda akatoa kibegi chake mgongoni kisha akakiweka sawia akapeleka mkono wake ndani ya kibegi hicho na kuutoa akiwa ameshikilia makaratasi fulani
akamkabidhi bwana yule ambaye naye akayapokea kisha akaanza kuyasoma alipomaliza akamwangalia eric vizuri mda huu sura yake ilikuwa kwenye umakini tofauti na mwanzo
kabala hajafanya chochote eric alipeleka mkono wake kwenye paja lake hapo akatoa bastora ndogo sana ambayo ni vigumu kuitambua akainyanyua na kutaka kufyatulia risasi bwana yule lakini alishangaa kuona akipigwa teke la ghafla lililompata vyema akajikuta akipoteza umakini na bastora ile kumluka mbali
teh teh teh "alicheka bwana yule kwa dharau kisha akamrushia eric picha kadhaa za sura yake halisi hapo eric akabutwaa hakutaka kuamini kama amegundulika na bwana yule kengere ya hatari ikagonga kichwani mwake
Mpambano mkali ulizidi kushika kasi ndani ya ofisi ya captain dwelll si michele wala cap dwell aliyeonekana kushindwa kila mmoja alionekana yupo makini juu ya mwenzie
dakika zilikatika hatimae zile dakika ambazo michele alikuwa anazisubilia zikafikia hapo akajiandaa kumaliza mpambano
japo mwili wa cap dwell ulikuwa umeenda sana ila alikuwa imara katika kupambana hasa mbele ya maadui ambao walitaka kuitoa roho yake
michele alisimama imara baada ya kudondoka chini hapo akajifuta vumbi kama tayari amemaliza mpambano hili lilimpa uoga kiasi capt dwell kwani hakuwa akijua adui yake anajiamini nini mpaka kuweka ishara ya kumaliza kazi
baada ya michele kujifuta vumbi alimshuhudia capt dwell akija bila umakini hapo akafanya jambo ambalo capt dwell hakulitegemea kwani teke alilolushwa lilikwepwa kiutaalamu sana hili likamfanya kushindwa kujiwekea ulinzi hivyo ngumi nzito ikatuo kwenye paji la uso akiwa katika hamaki alishitukia akichomwa na kitu chenye ncha kali kwenye koo lake hapo damu zikamtoka kama kuku aliyechinjwa akadondoka chini kama mzigo wa kuni huku jina lake likibadilika na kuwa marehemu captain dwell abraham
baada ya michele kumaliza kazi yake akarudisha kisu chake mahala ambapo anakificha kisha akatoa kibomu cha masaa na kukiweka chani ya mwili wa capt dwell kisha akaondoka mahala pale
akiwa anatoka nje akakutana na yule mlinzi hakutaka kuongea naye sana kwakuwa mahala pale hakukuwa na watu akamvuta mlinzi yule kwenye kordo iliyokuwa karbu na choo mlinzi yule alijua anapewa utamu ila alishtukiwa akipigwa pigo kali hadi kumpotezea fahamu
baada ya kumzimisha mlinzi yule safari yake iliishia kwenye gari yake akapanda na kuondoka
dakika tano baadaye lile bomu lililowekwa chini ya mwili wa capt dwell likalipuka,mlipuko wake haukuwa wakawaida hata kidogo
magari ya kuzima moto yaliyokuwa hapo jeshini yakaanza kazi ya kuzima moto huku baadhi ya sehemu zilizozimika zikianza kufanyiwa uokoaji wowote ule hadi masaa matatu yanapita hakuna kilichoonekana hii ilionesha bwana dwell aliungua vibaya na kubaki majivu
usiku wa saa nane taarifa ya kifo cha bwana dwell kikatangazwa huzuni ikaikumba nchi ya ujerumani hasa kwa jeshi la nchi hiyo
01:42 pm Moscow-russia
treni ya umeme ilisimama kwenye kituo chake kwenye jiji la moscow hapo wakashuka watu wengi akiwapo na eric ambaye alikuwa amevaa kofia nyeusi aina ya frankfurt
baada ya kushuka akaendea bus kubwa lililokuwa pembeniya kituo kile akapanda na safari yake ikaishia katikati ya jiji hili kubwa la moscow
baada ya kushuka kwenye lile bus akatembe kwa miguu hadi akafikia nyumba ndogo ya wageni hapo akachukua chumba na huku alijibadilisha jina kwa kujiita deric sakho anatokeo senegal na yupo kwenye jiji lile kufanya utafiti wa seruji kwani kipindi hicho kulikuwa na baridi sana ndani ya nchi hii ya russia
baada ya kuchukua chumba akakabidhiwa fungua kisha akaelekea kwenye hiko chumba alichopanga
usiku wa siku hiyo akatoka akiwa ndani ya koti kubwa safari yake ikamfikisha kwenye bar ndogo ya vocticy hapo akaingia na safari ikaishia counter ambapo alinunua chupa ndogo ya vodka kisha akatafuta sehemu iliyojificha akaketi na kuanza kukata ulaji wake taratibu huku macho yake yakiwa yanaangaza huku na kule ndani ya bar hiyo ya vocticy
akiwa amekaa mahala pale huku akikata kinywaji chake simu yake ikasikika ikiita aliutambua mlio ule alichokifanya ni kunyanyuka kisha akaanza kupiga hatua za taratibu safari yake iliishia nje kulikuwa na gari kubwa aina ya range rover imesimama pembeni mwa bar ile
akapiga hatua za taratibu hadi kwenye gari hilo na baada ya kuingia humo akakaa kwa dakika kadhaa kisha akatoka akiwa na begi kubwa kiasi akaliweka mgongoni mwake na kuondoka
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kwa mwendo wa dakika tano akafika kwenye ile guest aliyopanga akaingia ndani kisha akaliweka lile begi kitandani
hakutaka kulifungua kwa mda huo alichokifanya ni kuingia kwenye mtandao akalisachi jina la waziri wa biashara wa russia minister scot vladmill
baada ya kupata taarifa alizokuwa anaziitaji hapo akazima tehama mpakato yake akaiweka pembeni kisha akalifata lile begi lilikuwa na siraha ya kupiga masafa malefu akalifungua na kuanza kuikagua siraha yake baada ya kuhakikisha ipo vizuri akalifunga begi kisha akaliweka chini ya kitanda na yeye akalala
asubuhi ya siku inayofuata eric alikuwa yupo mbele ya jengo kubwa la makumbusho ya taifa ilo akaingia ndani kisha akaanza kuzunguka huku na kule alichokuwa anakitafuta yeye ni target ya kukaa ambayo atafanikiwa kumlenga mr vladimir siku ambayo atakuwa na mkutano akiongoza mamia ya wanachama wake waliokuwa wakisikiliza hotuba yake ya kutangaza nia ya kugombea uraisi
baada ya kuzunguka huku na kule akafanikiwa kupata mahala ambapo alifahamu anaweza kujificha na kutimiza malengo yake baada ya hapo akaanza kupeleleza juu ya ulinzi wa pale alipoona amepata kila kitu akaondoka huku akiwa na mpango wa kurudi kesho yake kufanikisha lengo lake
Baada ya eric kujua ulinzi wa kwenye ile maktaba ya vozdvizhenkta akaondoka huku akijipa kazi ya kurudi kisha kuingiza siraha katika maktaba ile pasipo kujulikana
safari yake iliishia kwenye supermaket ndogo iliyokuwa kwenye mtaa wa filyovisky hapo akachukua bomba la dogo la kupitisha kisha akanunu na dumu la maji kisha akaondoka
nusu saa baadaye akawa kwenye mtaa wa kitay-gorod akaegesha gari yake kwenye sheri ya mafuta kisha akaanza kupiga hatua hadi kwenye ile nyumba ya wageni aliyopanga hakukaa sana alichukua vifaa vyake kisha akaondoka
safari yake ilitia tamati kwenye hotel yenye hadhi kidogo hotel ya victory hapo akachukua chumba kwa jina la samweli okelo mzaliwa wa kenya yupo moscow kimasomo
baada ya kuchulia chumba akaingia akiwa na begi lake lenye zile bomba alizonunua na yale maji
akalitoa lile bomba na kuliweka kitandani kisha akachukua na yale maji akayafungua kisha akachukua maji mengine ya rangi ya blue akayachanganya kisha akachukua unga wa risasi akauweka kwenye yale maji hapo yakawa na rangi nyeusi,baada ya kumaliza akachukua lile bomba na kuliweka kwenye mdomo wa chupa ile ya maji kisha akaunganisha alipomaliza akavifungasha vitu vyake na kuviweka kwenye lile begi
saa kumi na dakika zake eric alisimama mbele ya maktaba ile ya Ul-vozdvizhenkta mgongoni akiwa na begi lake lenye vifaa vyake vya kazi
koti lake jeusi na kitambulisho chake cha electrical limit sambamba na kofia iliyoandikwa hivyo vilimfanya ahaminike kwa kila aliyepishana naye wakati anaingia ndani ya maktaba hiyo
safari yake ilimpeleka hadi kwenye lift akapanda wakati lift inapanda juu yeye alifungua sehemu moja juu ya lift ile akakwea kisha akawa juu ya lift ile ilipomfikisha sehemu aliyotaka akanasa huku akiiacha lift ile ikipanda pekeyake
baada ya kunasa juu ya jengo lile safari yake ilikuwa ni kuelekea kwenye mfumo mkubwa wa umeme kwenye ghorofa hiyo ya maktaba
akiwa na ramani mkononi mwake hatimae akafanikiwa kufika kwenye mfumo mkubwa wa umeme ambapo hapo ndipo panatumika kusambaza umeme katika jengo lote lile
hakutaka kupoteza mda akatoa begi lake mgongoni kisha akatoa yale maji akayatikisa hadi yalipoanza kutoa rangi ya uzurungi
baada ya kumaliza kutikisa yale maji akachukua bomba na kulichomeka kisha akachukua kamba ya plastiki akaifunga kwenye nondo zilizokuwa mahala pale alipomaliza akachukua lile dumu na kulifunga kwenye kamba ambayo aliiunganisha kwenye zile nondo
akachukua lile bomba akalikunja kunja huku akiacha nafasi ndogo ya kupitisha yale maji baada ya hapo akachomeka lile bomba ambalo alipojaribu vitone tu ndivyo vilivyokuwa vinatoka
baada ya kumaliza hapo akatoa chocolate akaipaka juu ya nyaya zile ambapo alitambua panya watakuja na kula nyaya zile kisha yale maji yanye unga wa risasi yatapenya kwenye zile nyaya na baadaye kutatokea mlipuko
baada ya kutega vile akaondoka ila akiwa hatua chache kutoka pale alishuhudia panya wakianza kusogea kwenye zile nyanya huku yale maji yakianza kudondosha vitonye kwenye zile nyaya
baada ya kutoka kwenye ile mitambo safari yake ikaishia kwenye lift akaidandia kwa juu kisha akaanza kushuka nayo ilipokaribia kufika akaruka na kutua kwenye nguzo zilizokuwa pembeni ya lift ile akapenya kwenye njia za emergency hadi akatokea kwenye vyoo vya maktaba akatega siraha yake kisha akaludi kwenye lift akaidandia kwa juu bahati ilikuwa kwake hakukuwa na mtu kwenye lift hivyo baada ya kushuka kwenye lift akabonyeza kitufe cha namba mbili hapo lift ile ikaanza kupanda juu kuelekea ghorofa namba mbili
lifti ile ikiwa inapanda akautumia muda huo kuvua zile nguo za kazi na kubaki na suti iliyomkaa sawa kisha akaziweka zile nguo kwenye begi
lift ile ilipofika kwenye ghorofa namba mbili akatoka akiwa na muonekano tofauti hakutaka kupoteza akaziendea ngazi zilizokuwa pembeni mwa lift ile akaanza kushuka
dakika tatu baadaye akawa nje ya maktaba ile akaliendea gari lake kisha akaondoka mahala pale ilishatimu saa moja usiku hivyo hakutaka kwenda hotelin baridi la russia lilimpa hisia tofauti ambazo hakutarajia kuwa nazo kwa mda huo
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
barabara zilikuwa kimya mda huu gari ya eric ilitembea taratibu hadi kwenye mitaa ya molodyozvity mitaa hii ilikuwa maalufu kwa dada poa hivyo eric aliendesha gari yake na kupaki mbele ya kikundi kidogo cha wasichana hapo akavutiwa na msichana mmoja mwenye asili ya china
akamuita msichana yule na kuondoka naye safari yake iliishia kwenye ile hotel ya victory aliyopanga
akaingia na yule msichana ambaye kwa kumuangalia tu alionekana mzoefu kwa kazi ile kwani baada ya kuzama kwenye chumba alimsukumiza eric kitandani kisha akamwangukia eric kwa juu
mkono wake laini ukaanza kutambaa hadi kwenye kasuku wa eric ambaye sasa alikuwa ameanza kukasilika
eric hakuwa nyuma alipeleka mikono yake na kumvua nguo kisha kufuri la msichana yule hapo jakutaka kupoteza mda akaanza kuzungusha kiuno kama feni mbovu
dakika chache baadaye wakawa hoi eric alikuwa ameshinda kwa magori mawili kwa mashuti ya mbali
Kijua hafifu cha asubuhi kilichompiga usoni eric ndicho kilichomtoa katika usingizi mzito akajinyanyua kiuvivu na kuangaza huku na kule
macho yake yakatua kwa msichana aliyekuwa pembeni yake ,akapiga mihayo miwili mfululizo kisha akaangalia saa iliyokuwa mikononi mwake ilishatimu saa mbili kasoro hapo akajiburuta hadi bafuni akafungua maji kisha akasimama bila kufanya chochote na kuyaruhusu maji yamwagike na kutambaa sehemu mbali mbali za mwili wake
baada ya kutosheka akachukua tauro na kujifuta maji kisha akatoka bafuni kama alivyotoka tumboni mwa mama yake safari yake iishia kwenye begi lake hapo akatoa suit kali za rangi ya zambalau kisha kachukua kiatu kirefi kilicho chongoka mbele baada ya kuvitayarisha hivyo vyote akaanza kuvivaa dakika chache baadaye akawa ndani ya suit zile nzuri
welcome mr gander"alijisemesha eric kisha akacheka hapo akakumbuka kitu kimoja ni yule msichana wa kichina aliyekuwa amelala naye usiku wa jana
alichokifanya alichukua sindano ndogo iliyokuwa na dawa ya usingizi akamchoma msichana yule kisha akamnyonya mate baada ya hapo akaondoka akiwa na briefcase lake lililokuwa na nguo
safari yake ilimfikisha kwenye mgahawa mdogo uliokuwa jirani na maktaba ile ya ul-Vozdvizhenka hapo akakaa na kuagiza kifungua kinywa asubuhi hiyo huku macho yake yakiwa katika maktaba ile
dakika chache baadaye gari aina ya benzi ilisimama kwenye jengo kubwa lililokuwa nusu km kutoka mahala pale alipokuwa amekaa
baada ya gari lile kusimama vijana wanne wenye miili iliyojengeka kimazoezi wakashuka kisha wakaelekea upande wa kushoto wa gari lile mmoja kati yao akafungua mlango na hapo akashuka bwana vladimill akiwa na sura ya tabasamu
baada ya kushuka aliongozwa na mpambe wake kuingia ndani ya jingo hilo kubwa hapo naye eric hakutaka kulaza damu akanyanyua ile kahawa lakini hakuipeleka mdomoni kabisa akaimimina hapo ikamchafua zile nguo zake anyanyuka na kutoka mahala pale kisha akaelekea kwenye vyoo vya mgahawa ule
akavua nguo zile kisha akavaa nyingine zilizokuwa kwenye briefcase lake kisha akatoka mle bafuni mda huu alikuwa amevaa pens nyeusi na body nyeupe huku kichwani akiwa na earphone kama zile za ma dj wa kumbi za starehe
baada ya kutoka chooni akaelekea kwenye ile maktaba kisha akaelekea kwenye upande mmoja wa vitabu hapo akaweka begi lake vizuri akatoa kijikaratasi kidogo na kujifanya kama anaandika jina la kitabu flani hiyo ilikuwa zuga yake kwa mapolisi waliokuwa wakilanda landa mle kwenye maktaba
baada ya mapolisi kuondoka upande ule akatoka kwa spidi hadi kwenye vyoo vya maktaba huko alivua zile nguo za unyangema kisha akavaa nyingine za kampuni moja ya umeme baada ya kuvaa nguo zile akajiweka sawa sawa
dakika chache baadaye umeme ukaanza kusuwa suwa ukawa unazima na kuwaka alitambua mpango wake umeenda kama alivyotaka alichofanya ni kutoka mle chooni
kutokana na lile tatizo la umeme hawakumtilia shaka eric hilo ndilo alilokuwa analitaka
alitembea haraka haraka hadi kwenye lift hapo akapanda lakini kabla haijafika sehemu ambayo alitakiwa afike yeye alilukia juu ya lift kisha akatoka alipofikia sehemu aliyopanga akaluka na kutua juu yake mda huu akiwa makini sana
kwa mwendo wake wa panya akafika pale alipotega siraha yake
panya walizidi kula magamba ya nyaya zile huku yale maji nayo yakizidi kulowanisha mfumo ule wa umeme ,eric alishatambua kuwa ndani ya masaa kumi na tatu mlipuko mkubwa utatokea kutokana na maji yale yenye unga wa risasi kuanza kuganda juu ya nyaya zile zenye umeme
saa tano kasoro dakika kumi na tano watu wengi wenye vipeperushi vyenye sura ya vladmil walisimama mbele ya jingo kubwa la kisiasa huku maaskali wenye siraha wakiwa wamesimama hatua kumi na tano kutoka mahala ambapo vladimil alikuwa amesimama kuhutubia
eric alikuwa amekaa imara kwenye sehemu yake ya ulengaji mda huu alikuwa ametulia sana huku mala kwa mala alikuwa akipima mwendo wa upepo mahala pale
saa tano kasoro dakika tano bwana vladimil alisimama mbele ya hadhara ile hapo akawasabahi wanachama wake kwa kuonyesha ishara ya ngumi juu hii ilikuwa ni alama yao
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
baada ya kuonesha alama ile akakooa kisha akajiweka sawa na dakika chache baadaye akaanza kuhutubia kuhusu nia yake ya kuingia madarakani
eric alikuwa makini na siraha yake mda huu macho yake yalikuwa yanahesabu sekunde na ilipotimu saa tano kamili akafyatua risasi mbili moja ilitua kichwani na kutawanya ubongo na nyingine ikapasua upande wa moyo
taharuki kubwa ikatokea mahala pale eric baada ya kumaliza kazi yake akanyanyuka na kutoka pale mafichoni
akaliendea begi lake kisha akalifungua na kutoa suti nyingine kali sana akazivaa na baada yahapo akapita njia za panya na kutokea juu ya lift akaifungua kwa juu kisha akapenya na kuingia ndani
dakika chache baadaye akawa upande wa chini hapo akakaa kwa dakika kadhaa akiangalia saa yake
..
Wananchi mbali mbali waliokuwa eneo lile wakaanza kukimbia huku na kule wengine wakaanza kulusha mawe amani ikapotea mahala pale
Vurugu zilikuwa kubwa sana katika jiji hilo amani ikatoweka
barabara zikaanza kufungwa huku vijana walioshika mabango yenye picha ya vladimill wakianza kuzurula huku na kule , wengine walikuwa wakichoma matairi barabarani wengine walianza kupasua vioo vya maduka kwa pamoja amani ilipotea katika jiji lile
polisi wakutuliza fujo nao wakawa mahala pale kuleta amani kwa kutawanya vikundi vile vya vijana
mda ambao polisi wa jiji la moscow wanashughulikia tatizo lile kwa kuleta amani,eric alikuwa airport akishughulikia usafili ambao utampeleka moja kwa moja hadi katika jiji la london
mr michael wayne "aliitwa eric baada ya kusubilia kwa muda visa yake ikamilike ,hapo akanyanyuka pale kwenye viti na kuendea dirisha dogo lililokuwa linaendesha shughuli ya ugongwaji visa
baada ya kuchukua pass yake akaongoza hadi sehemu ambayo kulikuwa na abilia wanaotarajia kusafili kwa mda huo na kujumuika nao
dakika 45 baadaye sauti ya kike ilisikika kuwa wanaosafiri na ndege ya british air wajiandae kwani ndege ipo kwenye hatua za mwisho za ukaguzi
dakika chache baadaye abilia wanaosafili na ndege hiyo wakaambiwa wanatakiwa kuingia kwenye ndege kuianza safari ya kuelekea london
baada ya kusikia hivyo eric akawa wa kwanza akanyanyua mzigo wake na kuanza safari ya kuelekea kwenye ndege hiyo
dakika 5 baadaye abilia wote wakawa kwenye ndege safari hii eric alikuwa amepanda kwenye daraja la vip
safari ile ilichukua kasi na masaa kadhaa magurudumu ya ndege ile yakatua kwenye uwanja wa queen georgia uliopo london
abilia wakaanza kushuka na eric akiwapo akafika sehemu ya ukaguzi na kukaguliwa ila kabla hajatoka ndani ya uwanja wa ndege alishuhudia kundi la maaskali wakija kule alipokuwepo hofu ikaanza kumjenga akatupa macho yake haraka haraka huku na kule kisha akawaangalia na wale mapolisi saba waliokuwa wanakuja
akawaangalia mikono yao kwa haraka haraka akatambua kitendo cha yeye kukimbia kitachukua sekunde mbili hadi kufikia mbele kwenye mlango wa private wa kutokea nje pia wale maaskali watatumia sekunda ishirini mpaka wapige risasi zao
hapo hakutaka kuchelewa akachomoka kwa kasi sana wale mapolisi walivyoona vile wakatoa bostora zao lakini walikuwa wameshachelewa eric alishapiga mahesabu kabla yao hivyo akaufikia mlango na kutokomea pasipo julikana
.....
Taarifa nyeti zilizotoka sudan,japan,german,russia zilimchanganya sana minister thomson eti watu wale waliuwawa na mtu mmoja ambaye alijibadilisha jina na kuwawuwa hao watu bila kujulikana hapo akachanganyikiwa alikwisha tambua mtu huyo atakuwa ERIC GODRICK LWOMA
kwa jinsi alivyokuwa anamfaham eric alitambua kazi aliyokuwa nayo
hivi ni yeye au sio yeye"alijipa maswali bwana thomson bila kupata majibu sahihi
akiwa ametulia kwenye ofisi yake akitafakali hili na lile mala ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yake akaitoa na kuangalia
taharuki ikamkumba hapo hapo akachukua simu yake ya ofisini na kubonyeza namba kadhaa dakika chache baadaye akaanza kuwasiliana na rafiki yake ambaye ni mkuu wa kituo cha polisi hapo london
atafika leo nahisi kama ataingia nchini hali yangu kiusalama haitakuwa sawa huyu mtu ni hatari zaidi ya neno lenyewe naomba mumkamate haraka iwezekanavyo"aliongea bwana thomson kisha akakata simu yake
dakika kumi baadaye simu yake ya private ikaita akaipokea na kuiweka sikioni
umeniuzi sana unajua nilitaka kuongea na wewe habari njema ila kwakuwa unataka shari bhasi ngoja nianze kile ambacho sikutaka kukifanya kwako"simu ikakatwa
kijasho chembamba kikaanza kumtoka bwana thomson alipojaribu kupiga simu ile haikuwa hewani tena wazimu ukampanda maladufu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
baada ya eric kukimbia mapolisi wale safari yake iliishia kwenye pub ndogo inayoitwa loyalty akaingia ndani ya pub hiyo kisha akaelekea sehemu yenye maficho kiasi huko akakaa kwa mda kisha akampigia simu mr thomson hakuwa akijua kama simu ile ilikuwa ikifuatiliwa hivyo
dakika chache baadaye baadaya kumaliza maongezi yake kundi la maaskali wakajiandaa kuelekea huko ambapo eric alikuwapo
dakika tano baadaye wakawa wamefika kwenye hiyo pub ya royalty wakaingia ndani ya pub hiyo huku wakianza msako wao wa kumtafuta eric
eric alikuwa makini akiwafuatilia wale maaskali hakuwa na chochote ambacho kingemfanya ajihami kupambana na wale maaskali
akiwa amekaa mahala pale kwenye kigiza kiasi eric akanyanyuka kisha akaelekea sehemu ya kubadilishia nguo wahudumu
alipofika huko akavaa nguo za kike kisha akatoka akiwa na mavazi yale ya kike akapishana na maaskali kadhaa waliokuwa bize wakifanya msako huo
baada ya eric kuwatoka maaskali wale hadi akafika nje hakutaka kupoteza mda alichokifanya ni kutafuta sehemu ambayo ingemfaa kwa mda huo
manchester"ndilio jina lililomjia haraka haraka alichokifanya ni kumwambia dereva yule ampeleke kwenye kituo cha treni ya umeme ambazo zinaelekea manchester kwa mda huo
dakika ishirini wakawa kwenye kituo hicho lakini mapolisi nao hawakuwa nyuma nao wakawa katika steshen ile wakifanya uchunguzi wao
Hali ilikuwa tete katika stesheni ile ya treni
mapolisi walizidi kuangaza huku na kule msako juu yake ulikuwa mkubwa sana
akiwa amekaa kwenye nguzo moja kwa mbele yake alishuhudia vijana wakipita kwenye njia za magendo na kuingia ndani ya treni moja ambayo hakuwa anajua ilikuwa inaelekea wapi
haraka haraka akajitoa katika ile nguzo akapiga hatua za haraka hadi nyuma ya treni moja ya umeme ambayo aliona wale vijana wakiingia
hapo akapenya kwa mlango wa nyuma wa behewa lile kisha akazama chooni moja kwa moja
samahani dada"alisikia mtu akiongea kwa nyuma yake hapo akakumbuka kuwa alikuwa amevaa nguo za kike
akaachia tabasamu kisha akageuka na kumuangalia bwana yule
shiit"aliongea yule bwana huku akipeleka macho yake kwenye kipepelushi alichobeba sura iliyokuwa kwenye kipepelushi kile iliendana kabisa na sura ya huyu bwana anayemuona mbele yake
hapo akatoa redio call yake iliyokuwa kwenye kiuno chake lakini kabla hajaongea chochote alisitukia akipigwa ngumi kadhaa kichwani dakika chache akapoteza fahamu
radio call yake ilikuwa on wakati eric anamvamia bwana yule hivyo sauti ya purukushani ikawafikia polisi waliokuwa nje wakiwasiliana naye ,bila kupoteza mda wakaanza kuelekea kwenye treni ile ambayo kwa mda huo ilishaanza kuondoka taratibu
sekunde kadhaa mbele ile treni ikawa imeanza kukoleza mwendo japo wale maaskali walijaribu kumpigia dereva asimishe treni ile ili wamkamate mtu wao lakini ilishindikana bwana yule alizidi kukoleza mwendo ila aliwaambia kama wanaitaji kumkamata mtu wao bhasi wafike kwenye kituo kinachofuata kituo cha stockhorm
treni ilizidi kushika kasi mda huu eric alimvua nguo askali yule wa kwenye treni kisha akazivaa akaichukua picha yake na kuiweka mfukoni mwake ,akaangaza huku na kule macho yake yakatua kwenye pama la marbolo akalivaa pama lile kisha akatulia kwenye mlango wa behewa la mwisho akiamini yule mzee alikuwa akilinda mahala pale
ving'ola vya magari ya kipolisi vilizidi kusikika kwenye barabara iendayo stockhom kila aliyepishana na msululu huo wa mapolisi alitambua siku hiyo kuna mtu hatari alikuwa akitafutwa au anaenda kukamatwa
ndege za kulinda usalama zilikuwa angani zikifuatilia treni ile kwa ukalibu zaidi
treni ile ilizidisha mwendo wake na ilipokaribia kwenye kituo cha stockhorm polisi wa mji huo wakaanza kukaa sawa ukiachilia mbali wale waliokuwa wakifatilia treni hiyo tangu london
eric alishatambua kuwa muda huu alitakiwa kuwa makini kupita maelezo kwani kama atakosea na akakamatwa bhasi mwisho wake utakuwa umefikia
akiwa anakalibia kwenye kituo kile treni ikaanza kupunguza mwendo kisha milango kadhaa ikafungwa na kuruhusu mlango mmoja tu kufunguliwa ili kila abilia akaguliwe ipasavyo akitoka
hapo akili ikamwenda mbio katika angaza yake mule kwenye treni akawaona wale vijana waliongia kimagendo wakiwa na hofu sana hapo akatambua kuwa wale vijana hawakuwa wahuni tu bali walikuwa wamefanya jambo baya alipowaangalia mikononi mwao aliwaona wakiwa na siraha huku migongoni mwao wakiwa na mabegi akatambua wale vijana nao walikuwa kwenye harakati za kujinasua huenda walikuwa wametoka kufanya ujambazi mahala flani tena hasa hasa kwenye bank
inabidi nifanye jambo"alijisemea eric huku akiwaangalia vizuri wale mabwana ambao tayari hofu ilikuwa mioyoni mwao
treni ilizidi kupunguza mwendo na ilipofika kituoni ikasimama hapo wale maaskali wakaanza kuisogelea wale mabwana hawakutaka hilo litokee eti wakamatwe na maaskali walichokifanya ni kutoa siraha zao kisha wakapiga risasi zao juu hapo abilia waliokuwa kwenye behewa lile wakalaza vichwa vyao ardhini huku kila mmoja akiwa na hofu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
baada ya kupiga risasi zao juu wakavunja kioo cha treni cha upande wa nyuma kwa risasi mda huo polisi walikuwa wameshajazana pale kituoni
eric alikuwa ametulia tuli ardhini akipiga mahesabu yake mwenyewe mda mwingi alikuwa akiangalia moja ya mabegi ya wale majambazi ambao muda huu walikuwa kwenye mpambano mkali na wale maaskali
walipomaliza kuvunja dirisha mmoja wa majambazi akapenya kutokea upande wa pili lakini kabla hajatua chini risasi kama tisa zilipenya mwilini mwake akadondoka chini kama mzigo huku damu zikiluka huku na kule
hasira zikawapanda wale majambazi wengine waliobaki wakamchukua mmoja wa abilia kisha wakaenda naye mlangoni bila kupoteza muda wakamfyatulia risasi ya kichwa na umauti ukawa naye
kama hamtatupatia gari la kuondokea mahala hapa tutaua kila abilia aliyekuwa humu ndani ya treni"alisikika mmoja wa majambazi wale akiongea kupitia kwenye kipaza sauti alichochukua kwa mfanyakazi mmoja wa treni ile
mapolisi walizidi kuongezeka kwenye eneo lile la stesheni wale majambazi wakaanza kuingiwa na hofu ila kila walipoona zile pesa mioyo yao ikaingiwa na ujasiri
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment