Search This Blog

Thursday, 2 June 2022

11:00 PM - 4

 





    Simulizi : 11: 00 pm

    Sehemu Ya Nne (4)



    Eric alikuwa ametulia pale chini akiwaangalia tu wale mabwana ambao mda huo walikuwa wanaonekana kuchanganyikiwa sana



    dakika zikasonga huku eneo lote lile likionekana kujawa na mapolisi japo eric alionekana kimya ila alifikilia jinsi ya kutoka tena na begi moja wapo ambalo wale mabwana wapo nayo



    hapa hatuwezi kutoka kilahisi tunatakiwa kuondoka na mmoja wa wafanyakazi wa treni hii"aliongea kiongozi wa wale majambazi muda huo huo jambazi mmoja akapiga hatua za haraka haraka kisha akanyoosha mkono wake hadi kwa mtu aliyembele yake



    nyanyuka"alipaza sauti huku akimnyooshea mtutu bwana yule



    baada ya kuambiwa vile akanyanyuka na kumfata akapelekwa hadi kwenye mlango wa treni ile hapo hakuchukua mda mrefu akazawadiwa risasi ya kichwa



    vituo mbali mbali vya runinga vilikuwa vikilusha moja kwa moja tukio lile la kutekwa kwa treni hata kifo cha yule mfanyakazi wa treni kiliweza kurushwa moja kwa moja kupitia vituo vikubwa



    polisi wa kitengo maalumu cha kupambana na uhalifu cha BRITISH CRIME AGENT (bca) kilianza kujiweka tayari kuvamia kwenye treni ile kisha kuwakamata watu wale ,wakiwa katika harakati za kutaka kuvamiwa mala wanapata taarifa kuwa muuaji wa kimataifa ERIC RWOMA alikuwa kwenye treni hiyo

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    hapo umakini ukaongezeka kwakila polisi ambaye jukumu lake lilikuwa kuingia kwenye treni ile



    hatuwezi kutoka inabidi tufanye jambo"aliongea mmoja wa majambazi wale



    tuondoke na hili treni"alidakia mwingine hapo hapo wakapitisha hilo wazo wakamfata mzee ambaye kazi yake ilikuwa kuendesha ile treni wakamuamulu aiwashe kisha watimke mahala pale kwa spidi sana



    baada ya kuambiwa hivyo yule mzee akapiga hatua hadi kwenye chumba cha kuongozea ile treni huku jambazi mmoja akiwa pembeni yake amemnyooshea mdomo wa risasi



    eric alikuwa akiwapigia mahesabu tu mabwana wale



    baada ya kuingia kwenye chumba cha kuendeshea ile treni yule mzee aliiwasha na kisha akaanza kuondoka polisi baada ya kuona vile wakageuza gari zao na kuanza kuifatilia treni ile huku ndege za mapolisi na vituo vikubwa kama aljazeera na bbc nazo zikiwa angani zikifatilia jambo lile na kurilusha kwenye runinga



    baada ya treni ile kuanza kuondoka wale majambazi wakaanza kujigawa kwenye mabehewa ili kuweka ulinzi bahati mbaya ikawa kwao katika behewa ambalo alikuwapo eric walimuacha jambazi mmoja tena alionekana kuwa muoga sana



    treni lile lilianza kuvuta kasi zaidi hapo eric akaanza kumvia yule bwana ambaye mda mwingi alikuwa akichungulia dirishani kuangalia usalama



    eric alipoangaza upande mwingine aliona yale mabegi ya pesa yamekaa yakatulia hapo akanyanyuka kama mzimu kisha akamvamia yule bwana



    ngumi zake kali zilizotua kwenye mwili hafifu wa bwana yule ziliweza kumzimisha kabisa hapo akamfata yule aliyekuwa kwa dereva naye akampa mapigo hatari ya kuvunja viungo



    baada ya kuwamaliza wale wa kwenye lile behewa akamfata yule mzee ambaye alikuwa anaendesha lile treni akamwambia apunguze mwendo huku akijitambulisha kuwa yeye ni askali kutoka kitengo maalumu cha kupambana na uhalifu



    yule mzee baada ya kuambiwa vile akaanza kupunguza mwendo wa treni ile



    wale majambazi waliokuwa kwenye mabehewa ya nyuma wakapata wasiwasi baada ya kuona treni likipunguza mwendo wakaanza kuja huku mbele



    eric baada ya kuona amefanikiwa kuwatuliza wale majambazi wawili akachukua begi moja lenye fedha kisha akaliweka mgongoni mwake



    hapo akaangaza huku na kule macho yake yakatua kwenye dirisha lililokuwa mahala pale akachukua begi la abilia mmoja na kulilusha kwenye dirisha lile hapo hapo likavunjika



    kitendo cha yeyey kuvunja dirisha lile la treni wale mapolisi waliokuwa kwenye ndege wakasoge mahala pale wakajua na yeye mmoja wa majambazi wale hapo hapo wakaanza kupiga risasi mfululizo



    eric alipoona hivyo akaludi nyuma akaangaza na kuiona ndege ile ikiambaa angani akajua kuwa chochote atakachokifanya kizembe uhai utauacha mwili wake



    wale majambazi walizidi kusogea kwenye lile behewa ambalo eric alikuwapo huku ile ndege kizidi kumnyima eric mwanya wa kutoka kwenye ile treni



    treni nayo ilizidi kupungua kasi huku mapolisi nao wakizidi kukalibia treni ile ambayo ilishaanza kusimama kwa kipindi hicho



    eric alituliza akili zake akaangaza huku na kule

    yes"alinong'ona kisha akarudi nyuma hatua kadhaa



    treni iie ilishafikia kwenye daraja eric alipotupa jicho lake aliona gari la mizigo likipiyta chini ya draja lile ambalo kwa juu ile treni ilikuwa ikipita



    dakika chache baadaye kishindo cha kuvunjika kwa kioo kikasikika kisha mtu akarushwa kwa upande ule ile ndege ilijua ni yule jambazi wa kwanza ilisogea upande ule na kurusha siraha

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    eric baada ya kuona amefanikiwa kwa hilo akatokea upande wa pili na kuruka hadi kwenye lile gari huku mgongoni mwake akiwa na lile begi la pesa



    wakati analuka wale majambazi walikuwa wameshafika kwenye ile treni walipoangalia mabegi hayakuwapo mahala pale hapo wakachanganyikiwa wakimuangalia mwenzao mmoja alikuwa tayari ameshakufa walipoamuangalia yule mwenzao mwingine hakuwapo wakajua amewasaliti





    Macho yakawatoka pima majambazi wale hasira zikawapata mala dufu ..hawakujua hasira hasara hayo ndiyo yaliyowatokea kwani baada ya treni ile kusimama wale majambazi wakatoka wakiwa siraha zao mikononi nje walikutana na gari kama 18 za polisi zikija ukiachilia mbali ambulance



    baada ya kutoka wakaanza kurusha risasi ovyo kuelekea kule ambapo mapolisi walikuwa wanakuja hawa kuwa na mawazo na ndege iliyokuwa anagani



    baada ya kuwarushia risasi mapolisi hatimaye ikafikia zamu yao ndege ile ikaanza kuwamiminia risasi mfululizo ndani ya dakika mbili miili yao ilibaki mfu uhai ulikwisha toka



    polisi wa vitengo vya kupambana na uhalifu vikashuka kutoka kwenye magari yao maalumu kwa mwendo wa kunyata wakaifikia ile treni huku wakiwa makini na siraha zao mikononi



    wakaingia ndani ya treni ile ambapo waliwakuta tu raia wakiwa wamelala sehemu moja tena wamejikunyata kwa uoga



    baadaya kukagua usalama wa treni ile wakatambua hakukuwa na mhalifu aliyebakia hapo wakaludi nyuma kuangalia miili ya majambazi wale wanne waliokufa vibaya baada ya kujibizana na mapolisi



    shiit"alisikika akilalama askali mmoja hasira zake zikaelekea kwenye gari huko akapiga ngumi kadhaa kwenye bodi la gari lile alipojilidhisha akapeleka mkono wake mfukoni akatoa simu yake ya private kasha akabonyeza namba flani flani na baadaye akaiweka sikioni



    dakika chache baadaye simu ile ikasikika ikipokelewa na mtu mwenye sauti yenye mamlaka akasikika akiongea kwa pupa



    tumemkosa ametuzidi ujanja"alisikika yule askali akiongea kwa hasira huku akiwa makini kusikiliza upandea wa pili



    andaa team ingia african street hakikisha kabla sauti ya kwanza ya jogoo kuwika asubuhi., nataka kusikia sauti yako ikiwika kuwa umesha mkamata"ilisikika sauti ikiongea upande wa pili na dakika chache baadaye simu ile ikakatwa



    ...

    Baada ya eric kutua kwenye lile gari mguu wake wa kushoto uliteguka vibaya mno ila haikumpa shida sana alipokalibia kwenye daraja dogo akalusha begi lake pembeni kisha na yeye akaluka akaenda kutua juu ya maji baada ya hapo akatoka kwenye ule mto na kulifata begi lake



    mwili mzima alikuwa amelowa na maji ,maumivu ya mguu yalizidi kumuweka kwenye hali mbaya hasa pale alipoluka mtoni



    kwa mwendo wa kujikongoja akaanza kupiga hatua huku akichechemea njaa kali ilizidi kumtafuna na kummaliza nguvu zake za akiba



    kwa mwendo wa takribani dakika ishirini hatimaye akafikia nyumba iliyokuwa mbali kidogo na barabara akajikongoja taratibu hadi kwenye nyumba ile



    alipokalibia karibu ndipo akabaini kuwa ilikuwa sehemu wanayouza mafuta pia kulikuwa na supermarket na nyuma ya supermarket ile kulikuwa na guest ndogo yenye bar kwa pembeni



    hapo eric akatembea kwa kujivuta zaidi alipokalibia zaidi na mlango wa guest ile akajiweka sawa hapo akatembea kama hakuwa ameumia vile akajivuta hadi pale kaunta akaongea na muhudumu wa pale ambaye alimuonyesha mahala ambapo vyumba vinapatikana



    hapo akatembea kiukakamavu hadi kwenye dirisha dogo lililokuwa pembeni yake akaongea na muhudumu wa bar ile na dakika chache baadaye akapewa funguo kisha yule dada muhudumu ambaye alikuwa amevaa chupi tu na juu alivaa sindiria akaanza kupiga hatua kuelekea kwenye chumba ambacho eric atapanga

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    miguno ya kimahaba ilisikika kwa wingi kwenye vyumba vingi vya guest hiyo



    hatua kumi za mwanaume kamili ziliwafaikisha kwenye chumba ambacho eric alitakiwa kukaa yule dada kafungua kisha akamwambia eric aingie ndani



    chumba kilikuwa kimekaa sawa japo kwa mbali kulikuwa na harufu ya kama kuna watu walikuwapo ila eric hakujali ilo



    baada ya yule dada kumkabidhi eric funguo akaondoka ila alipokalibia mlango akainama kisha akashusha chupi yake kasha akakata viuno na kuondoka huku akijichekesha ovyo, eric alimuangalia tu kwa tuo hakuwa na mawazo na msichana yoyote kw mda huo



    baada ya kukaa mle chumbani kwa mda eric akaanza kujipa matibabu ya mguu wake akaunyoosha hadi ukakaa sawa ila tatizo lilikuwa kwenye chupa iliyochimba kwenye nyama za paja lake



    hapo akajinyanyua kisha akavaa suruali yake akajikongoja hadi kwenye ile counter hapo akaagiza pombe kali kisha akaludi chumbani kwake akajiweka kitandani kama awali



    huuu"alihema eric kisha akavuta pumzi ndefu kwa ndani akafungua kizibo cha pombe moja kali aina ya vodka akaimimina ile pombe kuzunguka kidonda chake kisha akaanza kuichomoa ile chupa damu zilichuruzika ila hakujali maumivu yale aliendelea kuichomoa chupa ile iliyoingia urefu wa kidole mwisho



    baada ya kufanikiwa kuchomoa chupa ile akachukua risasi iliyokuwa pembeni yake akautoa unga wake kisha akaumimina kwenye kidonda maumivu makali yalizidi kumuandama ila hakuishia hapo akachukua ile pombe na kumimina kisha akachukua kibiriti cha gesi akakiwasha kisha akaanza kukipitisha juu ya kidonda kile



    maumivu makali aliyokuwa anayapata hayakuwa na mfano kichwa kilimgonga maladufu huku mwili wake ukianza kupoteza nguvu...





    Polisi wa team tofauti za usalama wakamwagika ndani ya kitongoji cha storkhom pamoja na jiji la jirani yake la arsenal ,gari zote zilizokuwa zinapita kutokea storkhom kuelekea arsenal zilikuwa zinakaguliwa kabla ya kuingia arsenal



    eric alizidi kutafutwa katika kila kona ya british dau la dora laki 5 zikawekwa kama zawadi kwa yule atakayefanikiwa kumkamata eric au hata kutoa taarifa zozote zile ambazo zinaweza kumtia nguvuni eric



    taarifa hii ilimvutia sana katerina huyu alikuwa muhudumu wa ile guest ndogo alizitamani sana zile pesa ,kila alipokumbuka ugonjwa wa salatani unaomsumbua mama yake alijikuta akiingiwa na wazimu zaidi hapo akawa makini kwa kila mteja wake hakuwa akijua kuwa huyo mtu anayetafutwa ndiye yule alimpa chumba masaa kadhaa nyuma



    baada ya eric kutoa ile chupa na maumivu makali yaliyomkabili akajikuta akipitiwa na usingizi mkali sana usingizi huu ulichangiwa na ile pombe kali aina ya vodka aliyokuwa anaitumia kama ganzi ya kuchomolea chupa ile iliyozama mwilini mwake



    usiku huu wa saa moja eric aliamka kutoka kwenye ule usingizi mzito akajinyanyua kiuvivu kisha akaelekea bafuni maumivu yalishaanza kupungua kwenye mguu wake



    baada ya kuoga na kujiswafisha akarudi na kukaa kitako kwenye kitanda hapo ndipo akakumbuka zile fedha alizozibeba kule kwenye treni akafungua zipu ya begi lile kisha akashika chani ya begi na kulinyanyua pesa zote zikamwagika kitandani



    jesus"alijisemea eric huku mkono wake wa kulia ukibana mdomo wake macho yakimtoka pima



    haraka haraka akapeleka mkono wake kwenye plate moja ya kutengenezea dora za kimalekani hapo akachanganyikiwa zaidi hakuwai kufikilia kama ataipata plate ya kutengenezea dora ya kimalekani tena kilahisi namna hiyo



    baada ya kuiweka ile plate ya dora pembeni akaanza kuzihesabu zile pesa,zilikuwa pesa nyingi mno hapo akaona utajiri unamkalibia akatamani aludi bongo ila vifo vya wapendwa wake vikamfanya ajione mpumbavu kurudi Tz bila ya kummaliza mbaya wake



    akiwa katika harakati za kupanga zile pesa mala mlio wa simu ukaanza kusikika ukitokea kwenye like begi, akaacha kupanga zile pesa akapeleka mkono wake kwenye zip iliyokuwa pembeni yake hapo akaifungua na kukutana na simu ambayo ilikuwa inaendelea kuita

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    jina boss"ndilo lililokuwa linaonekana wakati simu ile inaita hapo eric aliipokea simu ile kisha akaiweka sikioni



    hallow"alisikika mtu akiita upande wa pili



    mmmh"aliguna eric kuonesha anamsikiliza



    akiwa ametulia akisikiliza simu ile mala mlango wa chumbani kwake ukagongwa hapo akazima ile simu na kutupia chini ya begi lile kisha akachukua shuka akaweka juu ya pesa zile



    hey"alisikika katerina akiongea baada ya kufunguliwa mlango



    nikusaidie nini"aliongea eric huku akimuangalia katerina



    nimekuja..."aliishia hapo katerina kwani jicho lake la kulia liliona damu pembeni ya kitanda pia kulikuwa na chupa juu ya stuli ambayo ilikuwa imetapakaa damu hapo akapata wazo kuwa yule mtu wanaye mtafuta ndiye huyu akapeleka jicho lake kwenye uso wa eric hapo akapata uhakika zile dola laki tano za kimarekani alihisi ameshazipata haraka haraka akapiga hatua na kwenda chumbani kwake hapo hakutaka kusubili akachukua simu yake kisha akachukua simu na kupiga kwenye kitengo cha polisi 911



    baada ya kupiga sekunde chache baadaye simu ile ikapokelewa sauti nzito ya kiume ikaanza kuongea upande wa pili



    minister thomson alikuwa ametulia nyumbani kwake usiku huu mawazo yalikuwa juu ya pesa ambazo mpango wake ulishakwenda sawa ila kibaya zaidi eric aliingilia mpango wake kisha akaondoka na pesa ukiachilia mbali plate ya kutengenezea dola ya kimalekani



    akiwa amekaa na mawazo tele mala simu yake ikaita hapo akaipokea na kuiweka sikioni akapewa taarifa na kijna wake kuwa kuna msichana amepiga simu kwenye kituo kidogo cha polisi cha stockhorm na ametoa maelezo kuwa eric ampenga kwenye guest yake taarifa hizo wamezipata kupitia mtandao wao wa siri uliokuwa hapo kituoni hivyo walipaswa kufika kwenye hiyo hotel kabla eric ajafikiwa na mapolisi



    dakika chache baadaye gari tatu zikaingia barabarani kuelekea kwenye hiyo guest huku mapolisi nao wakianza safari ya kuelekea huko stockhorm ambapo kwa taarifa walizopata kuwa eric alikuwa huko



    dakika kumi na tano ziliwatosha wale wanazi wa mr thomson sasa walishafika kwenye ile guest safari yao ikawafikisha hadi mapokezi hapo wakakutana na katerina ambaye alionekana ana uchu sana na ile zawadi



    wakajitambulisha kuwa wao ni kikundi maalumu cha kupambana na ugaidi na hapo wamekuja kwa kazi moja tu ya kumkamata eric awe hai au mfu bila kupoteza mda wakatoa na picha yake kisha wakamuonesha katerina



    niyeye"aliongea katerina huku akitoka pale kaunta safari yake ikaishia kwenye mlango wa chumba ambao eric alikuwa amepanga



    wale mapolisi vivuli wakajigawa wengine walikaa kwenye mlango wengine wakazunguka kwa nyuma upande wa dirisha walipochungulia kupitia kitasa wakabaini walimuona mtu akiwa kitandani kajifunika gubi gubi hapo wakajipanga kuachia shambulizi ambalo kamwe eric asingeweza pona



    baada ya kukizunguka chumba kile wakaweka siraha zao kamili mmoja wa wale majambazi akatoa amri ya kushambulia



    hapo wakaanza kupiga risasi mfululizo dakika chache baadaye baadaya kupiga risasi zao mlipuko mkubwa ukatokea kwenye chumba kile wale maasakali batili wakarushwa huku na kule..



    Baada ya eric kuona mabadiliko ya ghafla ya katerina akatambua kuna jambo linaendelea hapo hakutaka kuchelewa tena alishaona mahala pale si salama tena kwa maisha yake



    baada ya katerina kuondoka akamuacha kwa dakika kadhaa kisha na yeye akaja nyuma yake maongezi yote aliyokuwa anaongea katerina eric aliyasikia



    teh"alicheka kwa dharau eric kisha akatoka pale alipojibana safari yake ikamfikisha kwenye ile supermarket hapo akanunua mitungi miwili ya gesi kisha akaireta hadi kwenye dirisha la chumba alicho panga



    baada ya hapo akazunguka upande wa pili akaingia chumbani kwake moja kwa moja hadi pale dirishani akafungua dirisha haraka haraka kisha akaipitisha ile mitungi ya gesi na kuiweka kitandani kisha akaifungulia na kuacha ianze kusambaa baada ya hapo akachukua shuka na kupafunika huku akichukua baadhi ya vitu na kutengeneza muonekano wa mtu amelala baada ya hapo akakusanya vitu vyake muhimu na kuviweka kwenye begi lile lenye pesa akapenya pale dirishani na kuondoka zake

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akiwa njiani anaelekea arsenal akapishana na magari yakiwa mwendo kasi sana hapo akatambua kuwa kama angebaki bhasi ingekuwa bahati na sibu sana kuendelea kuiona dunia hii



    akiwa bado yupo kwenye safari yake dakika 45 baadaye akapishana na magari mengine ya polisi yakienda huko alipotoka hapo akatambua kuwa si polisi tupu wanaomtafuta bali kuna watu wengine wanamtafuta yeye



    safari yake ikamfikisha arsenal hakutaka kukaa sana kwenye jiji lile alipitiliza hadi totenham huko akafikia kwenye hotel kubwa ya yenye hadhi ya nyota sita



    baada ya kuingia kwenye ile hotel akawasha television hapo ndipo akapata tukio lililotokea kule alipotoka kuwa



    kuna mlipuko mkubwa umetokea na unasadikika ulitegwa na gaidi kutoka somalia katika nyumba ya wageni iliyokuwapo katakati ya kitongoji cha storkhom ..mtangazaji yule akaenda mbali kuwa mlipuko ule ulisababisha vifo vya watu nane na muhudumu wa guest ile ambaye mwili wake uliungua vibaya sana

    kutoka na mlipuko ule wa gesi



    sory"alijisemea eric huku akipanda kitandani



    akiwa amejipumzisha kitandani akakumbuka ile simu akajinyanyua kitandani na kwenda ile sehemu iliyokuwa na simu



    akaichukua simu ile kisha akaangalia ile namba iliyoseviwa boss,hapo akaweka tabasamu baada ya kutambua namba ile mpango wake sasa unakalibia kumalizika



    siku iliyofuata ilimkuta kwenye maduka makubwa ya simu hapo akaenda kununua simu ya magendo ambayo haiwezi kunaswa pindi mtumiaji akimpigia mtu simu



    baada ya kupata simu ile akarudi mule hotelini huku njiani akipishana na mapolisi kedewa kede



    baada ya kuingia chumbani kwake akaichukua ile namba kisha akaiweka kwenye ile simu aliyotoka kuinunua akaipiga namba ile ambayo iliita kwa dakika kadhaa kisha ikapokelewa sauti ya kiume yenye mashaka ikasikika upande wa pili wa simu ile hapo eric akatambua ni mr thomson



    yes mr thomson nadhani ni muda muafaka wa kusuka nywele za simba"aliongea eric kwa masihara



    hapo mr thomson akatambua kuwa anayeongea naye ni eric hofu ikampamba akashindwa kuamini kuwa eric amepona kwenye ule mlipuko



    nataka kufanya mpango na wewe nataka kuonana na wewe siku ya leo kwenye uwanja wa hill mount pia sihitaji uje na mtu nataka uje mwenyewe sababu nataka kukukabidhi mzigo wako wa plate ya kutengenezea dola na pesa zako "aliongea eric huku akionekana hana chembe ya utani



    nitafika "aliongea kwa unyonge bwana thomson



    deal done"aliongea eric huku akiweka tabasamu kwani mda ambao alikuwa anaongea na bwana thomson alikuwa akimlekodi



    usiku wa saa mbili eric alikuwa katika ile sehemu aliyoaidiwa mikononi mwake akiwa na begi alilolijaza vitabu



    baada ya kufika mahala pale akajitega mahala akiwa na siraha yake ya kupiga masafa marefu



    baada ya kukaa pale kwa mda mala akaona gari tano zikija kisha vijana wa bwana thomson wakajigawa kuzunguka eneo lile eric alikuwa amejibana mahala ambapo hauwezi ukamuona kwa urahisi ila yeye alikuwa akiwaona hadi mahala walipokuwa wamejificha



    baada ya hapo alimshuhudia bwana thomsoni akitoka kwenye gari la katikati huku mwili wake ukiwa umevishwa vifaa maalumu vya kunasa sauti ukiachilia mbali nguo ya kuzuia risasi



    eric alikuwa makini akimfuatilia bwana thomsoni kupitia lenz ya bunduki yake



    dakika chache baadaye simy yake ikaita akaipokea kisha akaanza kuongea na bwana thomson kwa sauti ya chini kuwa yupo karibu na makabuli bwana thomson akaanza kusogea huko



    hatua chache baadaye akamuona mtu amesimama akiwa amevaa koti kubwa sana pembeni yake kukiwa na begi hapo akatambua mtu yule ni eric



    Bwana thomson alizidi kusogelea kule ambapo aliamini eric alikuwa amesimama akiwa anakalibia kupafikia kabisa akalala chini ghafla kisha wale walinzi wake wakaanza kupiga risasi mfululizo kuelekea kwa kile walichoamini ni eric

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    loo! Bahati ilikuwa mbaya kwao kwani walipoteza risasi zao nyingi kwenye sanamu moja mbele yao



    baada ta mr thomson kubaini yule hakuwa eric akaongea kupitia kinasa sauti chake kilichokuwa kwenye kola ya shati lake kuwa waache kupiga risasi



    utulivu ulikuwa mkubwa baada ya risasi kutulia eric alikuwa ametulia na bunduki yake ya masafa marefu aina ya MTk 63b2 muda huu lenzi yake ilikuwa imeshakaa sawi kwenye kichwa cha mr thomson



    R.i.p boss"alijisemea eric kisha akafyatua kiruhusu risasi kufumba na kufumbua risasi ikatua kwenye kichwa cha bwana thomson hapo kikafumua ubongo na damu kutapanya



    taharuki ikawapa maaskali aliokuja nao kurushwa kwa bwana thomson kukawafanya kutoka kule walipojificha na kuanza kumsogelea mkubwa wao ambao kwa namna moja ama nyingine atakuwa ameshapoteza uhai jinsi risasi ilivyompasua vibaya sana kichwani mwake



    eric hakutaka kuhangaika sana baada ya kumaliza kazi yake akakusanya kila kilichochake na kutimka mahala pale huku akiwaacha wale mapolisi wakimtafuta



    ilishatimu saa tano na nusu usiku alitumia nusu saa kufika kwenye uwanja wa queen georgia hapo akapanda ndege ambapo alikuja kushukia south africa



    ndiphilile unjani wena"alisalimu eric kwa rugha ya kinzosa inayotumiwa na kabila la nzosa huko south africa



    teh teh"aliishia kucheka tu yule akiyeonekana mwenyeji wake hapo wakaongozana hadi kwenye gari lililokuwa nje ya uwanja ule wa ndege wa Nelson Mandera uliopo jo'burg



    baada ya kuingia kwenye ile gari safari yao ikaanza hadi kwenye mitaa ya maarufu ya wauza unga uko jo'burg baada ya kufika huko wakaelekea kwenye jumba moja kubwa sana ambalo linaonyesha kama vile liliachwa kutumika miaka mingi nyuma



    baada ya kuingia wakakalibishwa na vijana sita waliokuwa ndani ya suti kali sana huku mikononi mwao wakiwa na siraha kubwa kubwa



    ooh naza"aliongea kijana mmoja mwenye nywele nyingi kichwani tena zikiwa chafu sana kisha akakulupuka na kumkumbatia yule jamaa aliyekuja na eric



    brother"aliongea yule kijana huku wakikumbatiana kwa nguvu



    japo huyu kijana alikuwa na pesa nyingi sana ambazo alizipata kupitia biashara yake ya kuuza madawa ya kulevya aina ya heroin na bhangi ila hakuwa mtu msafi aliwajali walinzi wake kupita yeye alitumia pesa nyingi kulinda familia za walinzi wake kuliko yake ndio maana walinzi wake walikuwa wakimlinda kufa na kupona



    baada ya kusalimiana yule bwana akamtambulisha eric kwa yule kijana hapo wakasogea pembeni na kuanza kujadiliana mambo kadhaa baada ya kumaliza wakapeana mkono na kuondoka



    ni mdogo wangu tumetoka kijiji kimoja ila yeye amechanganyikiwa na madawa sana hata akawa vile"aliongea naza akimjuza eric



    safari yao iliishia kwenye hotel aliyopanga eric hapo yule jamaa alimuacha eric kisha wakakubaliana kuonana siku inayofuata uwanja wa ndege



    asubuhi ya siku inayofuata eric alikuwa uwanjani muda wa saa mbili asubuhi hapo akakutana nayule jamaa aliyeonana siku iliyopita akakabidhiwa kile alichokuwa anakiitaji kisha akaondoka nacho



    masaa kadhaa baadaye ndege ile ya shirika la southair ilitua kwenye uwanja wa jomo kenyata nchini kenya hapo eric akashuka kisha akapanda mabasi ya kutoka nje ya nchi hiyo



    safari yake iliishia sirali hapo akapita sehemu ya kugonga pass port ..baada ya kugongewa pasport yake akaondoka safari yake ikamfikisha bunda huko akapanda gari hadi nansio ukelewe jioni ile ile akapanda mari ya mwisho mv Nyehunge ambayo ilimfikisha mwanza



    huuuu"alishusha pumzi ndefu eric baada ya kufika mwanza jiji alilokuwa anapenda kuishi maisha yake yote



    mda huu wa saa tatu usiku ulimkutia eric akiwa nje ya hotel ya sparrow hapo alipanga chumba



    alijibwaga kitandani kiuvivu kisha akatoa kile cheti chake feki cha uaskali wa TSA alichotengeneza huko south africa



    baada ya kukiangalia na kuhakikisha kipo kama alivyotaka akatoa kidaftari chake kidogo hapo akaangalia majina ya watu ambao walitakiwa kupotea kwenye uso wa dunia

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    major samweli nduru"ndilo jina lililomjia haraka kichwani mwake hapo akaweka tabasamu lake la kazi akachukua dumu la maji akaligida kwa haja kisha akaingiza jina la bwana yule kwenye akili yake



    asubuhi ya siku inayofuata ilimkuta akiwa kwenye stand ya nyegezi huko akakta tiket ya kuelekea dar esalaam



    masaa kumi na moja ya barabarani yalimtosha kabisa kumaliza umbali sasa akawa ndani ya jiji lile ambalo linasifa ya kuitwa nchi ndani ya nchi





    Kelele zilikuwa chungu nzima katika stand ya ubungo jijini dar es salaam.honi za magari ukiachilia mbali makelel ya wapiga debe yalizidi kuleta kelo hasa kwa abilia waliokuwa wanawasili na kusafiri katika jiji hilo



    baada ya eric kushuka kwenye bus la prince shabaha akasimama hatua chache kutoka kwenye mlango wa bus lile akaangaza huku na kule kisha akaweka begi lake dogo sawasawa akaendea taks iliyokuwa upande wa kushoto wake akaaongea na dereva yule kwa mda kidogo akipata bei kwa mahala alipokuwa anaelekea na walipopatana akapanda gari ile na kutokomea



    .........

    Gari nyeusi aina ya verrosa iliingia kwenye jengo la ofisi nyeti za kijeshi lililopo posta, baada ya gari lile kukagulia pale getini na kugundulika lilikuwa salama hatimaye likaruhusiwa kuingia



    sekunde chache baadaye likaenda kupark sehemu ya parking



    hakuonekana mtu yeyote kushuka baada ya gari lile kupark ..nusu saa baadaye gari nyingine lenye langi ya ugoro likaingia likiwa na bendera ya nchi kwa mbele



    baada ya gari lile kuegeshwa mahala pake mlango ukafunguliwa kisha mzee mnene kiasi mwenye kitambi kikubwa akashuka mabegani mwake alichafuka kwa vyeo vingi sana



    baada ya kushuka kwenye gari safari yake ikaanza kuelekea ndani ya ofisi ile huku nyuma yake kukiwa na walinzi wawili wakiwa katika sale maalumu za kazi yao



    mzee yule alitembea hadi kwenye lift ya jingo lile na baada ya kuingia hapo mlango wa gari ile aina ya verrosa ukafunguliwa kijana aliyevaa suit nyeusi iliyomkaa vizuri hadi kuchonga kifua chake kilichojaa kwa mazoezi magumu akashuka kutoka kwenye gari ile mkono ni mwake akiwa na makaratasi yaliyopangwa vizuri kwenye file lake



    kitambulisho chake kilichoonesha askali kutoka katika ofisi nyeti za upelelezi TSA zilimpa heshima kwa kila aliyepishana naye..mwendo wake wa kujiamini ulimpoteza kila mtu hata kushindwa kumtilia shaka



    safari yake iliishia kwenye ngazi akapanda hadi ghorofa ya pili baada ya kufika akaanza kutembea kwa haraka haraka hadi kwenye ofisi ya major samweli hapo akakutana na katibu mukhitasi wake ambaye alikuwa bize na kuongea na simu



    akamsubili kwa dakika chache hadi alipomaliza kuongeza na simu ile hapo eric akajitambulisha huku akiachia tabasamu mwanana usoni mwake



    kutokana na mavazi yake na hata alivyoonekana ameulambia yule dada akashindwa kuhoji zaidi hapo akapiga simu kwa boss wake akatoa yale maelezo ya uwongo kama aliyopewa yeye na eric



    ingia "aliongea yule dada huku akimwangalia eric kwa macho ya matamanio makubwa



    karibu TSA jonh namalombe" alikalili jina ambalo alitajiwa na katibu mukhtasi wake



    ahsante"alijibu eric huku akikaa kwenye kiti akanyanyua makablasha yake na kuyaweka juu ya meza kisha aka jikohoza



    major samweli alikuwa kimya akimuangalia eric ambaye kwake alijitambulisha kwa jina la john namalaombe



    natamani kuwa mwema ila nikishamaliza kazi ya kuwauwa watu wawili nitaenda kutubu zambi zangu kisha nitaokoka kabisa na kama nitapewa nafasi ya kuwa mtumishi wa mungu hasa hasa u-padre bhasi sitasita"aliongea eric baada ya kuweka sawa makablasha yake



    major samweli hakuwa akijua yule bwana anamaanisha nini pia hakuwa akijua kama ndani kwake ameingia mtoa roho na yeye ndiye atakaye tolewa siku ya leo



    teh teh teh kijana kabla hata hujaanza kazi tayari unaanza kufikilia kuua"aliongea major sam kiutani



    hii kazi nina uzoefu nayo tena sana ila hapa tanzania nina mkataba na watu wawili wewe na alex ndaro kwani huko pengine nimesha pamaliza kama sudan kule nilipamaliza mwezi uliopita kisha british kule nimetoka ijumaa ile iliyopita tayari nilishamaliza kazi yangu"aliongea eric kimasihara huku akianza kuchukua bomba la sindano lililokuwa kwenye soks ya kiatu chake kisha akatoa na kichupa kidogo alikokiweka kwenye soks nyingine baada ya hapo akavuta dawa iliyokuwa kwenye kichupa kile

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    macho yalimtoka pima major samweli hakuwa akijua nini kitatokea juu yake hofu ya kifo ilishaanza kutambaa mwilini mwake



    katika hofu ile ndipo akaanza kukumbuka kilichotokea sudani na kumaliza british akipita ugerman hapo akatambua ofisini mwake alikuwa ameingia eric na sio TSA John namalombe



    kijasho kikaanza kumtoka kile kiyoyozi cha samsung kikashindwa kuzuia jasho lisimtoke maradufu



    baada ya eric kumaliza kuvuta dawa ile akajaribu kwa kuitoa nayo ikatii kwa kuruka



    mtoto subilia nikuchome sindano nina imani dakika tano baadaye utakuwa umepona ugonjwa wa tumbo lako kubwa"aliongea eric huku akinyanyuka pale kitini akamsogelea yule major ambaye sasa alikwisha nyanyuka pale kitini



    baada ya eric kunyanyuka major aliitoa bastora yake haraka haraka lakini kabla hajaitumia ngumi nzito ikatua mdomoni mwake hapo maji ya rangi nykundu yakaanza kumtoka bwana yule....



    Saa tatu na nusu ilitimu muda katibu mukhitasi akanyanyuka pale kitini mwake mkononi akiwa na chupa ya kahawa tayari kuipeleka ndani ya ofisi ya boss wake





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog