Search This Blog

Thursday, 2 June 2022

11:00 PM - 5

 





    Simulizi : 11: 00 pm

    Sehemu Ya Tano (5)



    Eric alimkata sawia meja samweli ule mwili wake mkubwa haukuwa tatizo mbele yake ..baada ya kumkamata vilivyo akamchoma na ile sindano ya kusimamisha mapigo ya moyo



    sumu iliyokuwa ndani ya dawa ile ilitambaa kwa kasi sana dakika tatu baadaye mapigo ya moyo ya meja samweli yalikwisha simama hapo akajinyanyua na kuweka suti yake vizuri



    akiwa amesimama tayari kuondoka mala mlango wa ofisi ile ukagongwa hapo akajibana pembeni ya mlango kisha akaruhusu mtu aingie

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    dakika chache baadaye alishuhudia kikombe kikitangulia kuingia ndani hapo akatambua ni yule katibu mukhtasi kidogo akatuliza munkali hakutaka kutimiza adhima yake kwa msichana yule mrembo



    baada ya kuingia ndani macho yake yakatua kwa boss wake kwakile alichokiona alitambua boss wake tayari amekwisha uwawa kwani damu nzito zilikuwa zikimtoka puani na mdomoni pia na masikioni



    shiii"alisikika eric akiongea mda huu alikuwa nyuma ya msichana yule mrembo kidole chake kilichokuwa mbele ya mdomo kilionyesha dhahili hakutaka msichana yule aweuke zaidi na kupiga kelele



    mapigo ya moyo yalizidi kumuenda mbio msichana yule kwani alihisi kifo kipo hatua moja mbele yake, eric baada ya kumfikia akaanza kupeleka mkono wake na kuutambaza kutokea kwenye kiuno cha msichana yule hadi shingoni hapo akambinya sehemu flani ya msichana yule na dakika chache akawa ameshamzimisha



    baada ya eric kumaliza kazi yake akachukua makaratasi yake na kuyaweka kwenye file lake kisha akaweka miwani yake sawa na baadaye akatimka pale ofisini



    safari yake iliishia mlimani city hapo alienda sehemu ya kuegeshea magari akalitelekeza gari lile na kutimka



    saa mbili kamili usiku habari ile ya kuwawa kwa meja samweli ilitangazwa kupitia chanel ya taifa wananchi mbali mbali wakapata mashaka hasa pale waliposikia kuwa hali ya sekretari wake nayo ilikuwa mbaya ila kwa sasa imeshakuwa sawa na anaendelea vizuri



    asubuhi ya siku inayofuatia habari zikasambaa magazetini wale ambao hawakuwa na luninga habari hiyo ikawa mpya kwao jiji likazizima na taarifa ile ya mauaji ya major samweli



    eric alikuwa ametulia kwenye kitanda chake kikubwa kwenye hotel ya hill top



    mida hii ya saa mbili macho yake mawili yaliyomakini yalikuwa yametulia kwenye luninga ambayo mda huu ilikuwa ikilusha habari za kifo cha meja samweli



    akiwa anaendelea kufatilia habari ile akasikia kuwa uchunguzi unaendelea kufanyika na gari alilotumia muuaji huyo limepatikana katika maegesho ya mlima city



    09:18 asubuhi maasakli watatu kutoka katika kitengo maalumu cha upelelezi wakaingia katika hosptali ya muhimbili ,safari yao ikaishia katika wodi ambapo alilazwa rehema yule katibu mukhitasi wa meja samweli



    anaendelea vizuri nadhani mnaweza kuongea naye"aliwapa ruhusa doc aron jonas kama kitambulisho kilivyokuwa kikisomeka kwenye koti lake jeupe alilovaa



    dakika chache baadaye lily akiongozana na wapelelezi wenzie wawili walikuwa tayari wapo katika wodi aliyolazwa rehema allly au katibu mukhatsi wa meja samweli



    hali yake haikuwa mbaya sana hivyo aliweza kutoa ushirikiano kwa kila alichoulizwa hasa juu ya yule muuaji ambaye alifanikiwa kumuua major sam na yeye akapotezewa fahamu

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mahojiano yao yalichukua takribani dakika 30 hapo wakaaga na kuondoka huku wakidai watakuja tena kupata taarifa zaidi kama zitahitajika



    eric alikuwa pembeni mwa hospitari ile nywele zake zilizotiwa rangi nyeupe mfano wa mvi zilitosha kumlubuni kila amtupiaye shaka



    safari yake ilikuwa katika wodi ya msichana yule lakini kabla hajafikia aliona maaskali watatu wakitoka ndani ya wodi ile akanyanyua makaratasi aliyoyashika hadi kuiziba uso wake kabisa hapo akapishana nao



    safari yake iliishia kwenye wodi ya msichana yule akajifanya daktari kwa kumuuliza hali yake huku akichomoa vinasa sauti na kuviweka chini ya kitanda cha msichana yule



    baada ya kumaliza zoezi lake la kutega vinasa sauti akaaga na kuondoka bila ya kushitukiwa na mtu yeyote yule



    bwana alex ndaro alikuwa amejipumzisha pembeni ya kabuli la mke wake ambaye aliuliwa vibaya miezi mitatu nyuma



    kabuli la mke wake alilijenga mbele ya nyumba alifanya hivyo ili kila aliangaliapo kabuli lile bhasi asila iwe juu yake



    akiwa amekaa kwenye kabuli lile mala simu yake ikaita hapo akaipokea na kuiweka sikioni mwake sauti ya kike ikasikika nyuma ya simu ile



    maongezi yao yalichukua dakika tano na pale simu zilipokatwa bwana alex akabaki na hasira sana taarifa aliyopewa ya kuuwawa kwa major samweli ilimtikisa ubongo hapo akatambua yeye ndiye anayefata alikwisha tambua mbaya wake amerudi hivyo inabidi ajiandae kupambana naye japo yeye ndiye aliyemfunza kila kitu juu ya muaji kwa kumpeleka kwenye chuo cha kijasusi huko russia





    May/20/1996 07:18 pma BUKOBA



    upepo wa ziwa victoria ulizidi kuwapiga abiria waliokuwa wanasubili kusafiri katika meli ya mv bukoba usiku huu



    abiria wengi walikuwa wakizunguka huku na kule katika meli hii kubwa ambayo masaa kadhaa mbele ndipo ilitakiwa kutoa nanga



    pooo! Pooo ! Poooh !" ilisikika honi kubwa ya meli hiyo ikipigwa hapo abiria wakaanza kujiweka tayari kwa safari..dakika kadhaa mbele meli hiyo kubwa ya mv BUKOBA ikaanza safari



    baada ya meli ile kuanza safari kila abiria alikaa kwenye kiti siti yake



    meli ile ilipitia kwenye bandari ndogo ya kemondo hapo akapanda msichana mdogo sana aliyebeba kamfuko ka nailoni na mikononi mwake akiwa amekumbatia mtoto mdogo sana



    afya ya msichana huyu haikuwa sawa kabisa hii ilionyesha alikuwa ametoroka mahala kama sio hospitali baada ya kujifungua



    naenda mwanza na kama nitafanikiwa bhasi sitarudi tena bukoba najua wazazi wangu wataumia sana juu ya uamuzi wangu mgumu lakini nitafanya nini hii imenibidi sitaki kuitia aibu familia yangu hii ya kubeba mimba wakati ningali nasoma naona inatosha"alisikika akinong'ona msichana yule kimoyo moyo huku akiwa anaingia ndani ya meli ile



    safari ilianza kwa mala ya pili baada ya meli ile kuchukua baadhi ya abiria na mizigo pale kemondo



    usiku huu safari ilikuwa imetulia sana abilia wengi walikuwa kwenye utulivu mkubwa sana ,wapo walioanza kulala wengine wakicheza na watoto wao ,mda nao ulizidi kusonga msichana huyu mdogo asiyfahamika jina alikuwa amejibana kwenye siti moja huku mwanaye mchanga akiwa amemkumbati kile kitenge cha wax kilishindwa kabisa kupambana na baridi hili hata ikachangia hadi inafika mida bila kupata hata lepe la usingizi



    usiku ulizidi kuwa mkubwa sasa ilitimu saa nane usiku hapo meli ikaanza kuonyesha kama kuna tatizo mafundi wa meli ile walionekana wazi wazi baada ya sura zao kuwa na shaka kuu

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    abilia kadhaa waliokuwa macho nao wakaingiwa na hofu juu ya mwenendo wa meli ile ,baba koku alisikika mama mmoja akimumsha mme wake aliyekuwa ameshauchapa usingizi..



    Kuamka kwa mme wake kuka muamsha na mtu mwingine na mwingine zaidi sasa nusu ya abilia wakawa wamekwisha amka kwenye meli ile kila mmoja akionekana kuwa na hofu



    mpaka inafika saa tisa usiku meli ile ilianza kuonyesha zaidi kuzidiwa na mizigo iliyobebwa hii ilionyesha kuwa hali sasa imeshakuwa mbaya hapo mizigi mizito ikaanza kupunguzwa hali ikatulia kidogo lakini baadaye ikajirudia tena



    abilia waliokosa utulivu wakaanza kupayuka kuwa wanazama hii ilimtia hofu captain wa meli ile ya mv bukoba hapo akawasha vipasa sauti vya meli ile kisha akaanza kuongea na abilia wake lakini haikusaidia kila mmoja alikuwa na nia ya kutaka kujisaidia juu ya janga lile



    usiku huu ulikuwa usiku mbaya sana hasa kwa huyu mama mwenye mtoto ambaye alipandia pale kemondo hofu ilimkumba balabala akashindwa afanya nini hakuwa na nguvu za kujisaidia kwani masaa kadhaa nyuma alifanya tukio la kutoroka kwenye hospital ya bukoba akaiba pesa na kufanikiwa kupata tiketi ya hongo



    meli ile ilianza kuzama taratibu sasa hali ikawa mbaya kila abiria alianza kukimbilia kule ambapo aliona anaweza kuinusuru roho yake



    yule dada mwnye mtoto bila kujua akaanza kukimbia hovyo taamaki ilikuwa kubwa sana kwa upande wake meli ilishaanza kuzama ndani ya maji ya ziwa victoria



    abilia walisikika wakipiga makelel ya kusaidiwa mda huu ilishapita mda mrefu sana tangu ianze kuzama mama yule mwenye mtoto alifanikiwa kupata life jacket hapo akalivaa utaaramu kidogo alioupata shuleni juu ya kutumia life jacket aliutumia mahala pale



    akamchukua mwanaye na kumkumbatia kisha akamvilingisha na life jacket lingine hapo akambeba kasha akajitosa ndani ya maji



    asubuhi ya 21/05/1996 jiji la MWANZA liligubikwa na majonzi makubwa miili ya watu ilianza kutolewa nje ya ziwa lile abiria wanaosadikiwa 315 walifariki dunia na wengine 183 wakiwa hawajapatikana



    naam hata mama wa yule mtoto naye hakupatikana katika ile miili ila yule mtoto mchanga alikutwa akiwa salama hapo shirika la kulele a watoto yatima liitwalo chidren care lililopo mwanza likamchukua mtoto yule na kuanzia hapo akawa analelewa mahala pale



    kwakuwa hawakuwa na historia yoyote kuhusu mtoto yule wakambatiza jina la ERIC LWOMA na hata alipofikisha miaka ya kuanza shule alilitumia jina hilo



    miaka ikaenda hatimae Eric akaanza kukua salama uwezo wake wa darasani ulikuwa mfano wa kuigwa kwa wenzie



    miaka ikaenda hatimae eric akafadhiliwa na mtu mwingine aliyetambulika bwana ALEX NDARO huyu alikuwa tajiri na mfanyakazi wa serikali baaday kumchukua Eric akapanga mipango yake ya kutaka kumtumia kwenye kazi zake hapo baadaye



    kuna chuo cha kijasusi kipo russia nadhani tukimpeleka mapema huyu kijana atatusaidi sana"alisikika kopro samweli akiongea hapo ikapitishwa eric apelekwe kwenye hiko chuo lakini ilitakiwa itoke taarifa kuwa amefariki ili asifatiliwe zaidi





    10/01/2000 Gazeti la jioni leo linalotoka kila siku lilikuwa limebeba tukio ambalo wazazi wengi hawatarisahau maishani mwao



    vifo vya watoto 28 na wengine 17 kujeruhiwa vibaya sana ilikuwa tukio la kuhudhunisha kwa wazazi wengi wa jiji la mwanza



    japo ajali ile ya bus la wanafunzi kugongana na gari la mizigo maeneo ya pasiansi jijini mwanza mwanza ajali ile ilitafsiliwa kama ya kutengenezwa kama sio kifo cha dereva wa bus lile bhasi wazazi wale wangemshitaki



    eric alikuwa siti ya nyuma ya bus lao kabla ya ajali macho yake yalikuwa yakitambaa huku na kule kwenye bus sekunde kadhaa alisimama kisha kuelekea mbele alitamani kukaa siti yta mbele ambayo kuna mwanafunzi alishuka

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akiwa natembea kwenye kordo ya bus lile mala ajali mbaya ikatokea dereva wa bus ile alitaka ku over take gari kwa mbele lakini hakujua kama kulikuwa na gari upande ule akiwa ana jaribu kuingia hapo akavaana na gari la samaki vilio vikasikika eric alilusha vibaya na kwenda kujibamiza kwenye kioo cha gari lile chupa zikapenya kichawani mwake na kumchana vibaya sana



    habari ya ajali ile ikawa gumzo kubwa sana jiji mwanza na tanazania nzima

    bwana alex ndaro alikuwa amejipumzisha jioni hii katika jumba lake kubwa huko bwiru place akiwa anaperuzi kwenye gazeti moja la jioni leo akaipata ile taarifa hapo akaona mpango wake umekamilika tabasamu likapamba uso wake

    lakini akatamani kumalizia habari ile "Mtoto aliyepona kwenye ajali ya Mv bukoba apata ajaali na hali yake ni kuyasikitisha"sehemu hii ilimchanganya sana mwana alex ndaro hapo akainyanyua simu yake kisha akabonyeza kitufe frani frani sekunde kadhaa upande wa pili ukasikika



    alichouliza ndicho alichopata hasira zikampanda maladufu aliona kama amepoteza pesa zake kuandaa safari ya eric kuelekea kwenye hiko chuo cha kijasusi ukiachilia mbali malipo ya chuo hicho cha siri



    usiku wa saa mbili alex ndaro alimuita rafiki yake kipenzi kopro samweli mipango yao ni juu ya kumpata mrithi wa eric ambaye anatakiwa kusafiri punde kwani siku zilishaanza kuisha sasa zilibaki wiki mbili tu eric asafiri



    walipotafakali juu ya mipango ya kupona kwa eric wakatambua ingemchukua mda mrefu sana hapo wakaadhimia kumtafuta mtu mwingine ambaye angeenda badala ya eric kwani hivi sasa alikuwa yu mahututi kwenye hospital ya sekou-toure



    usiku wa saa mbili vijana wa alex ndaro wakaingia maeneo ya sahara huko wakakutana na vijana wengi wa kiuni maalufu kama watoto wa wakoma ..watoto hawa walikuwa hatari sana ndani ya jiji hili la mwanza



    baada ya vijana wale kufika katika mitaa ile ya sahara wakaelekea kwenye duka moja lililofungwa hapo wakakuta watoto wengi wakiwa wamelala wakapendezewa na kijana mmoja ambaye kwa muda huo alionekana kama ana miaka kumi na tatu



    baada ya kumpata kijana yule wakamchukua hadi kwenye lile jumba kubwa ajabu alikuwa anafanana sana na eric ...baada ya kumchukua wakaanza kumuandaa kwa ajili ya safari mda mwingi alikuwa akichomwa sindano ya usingizi hadi siku ikawadia hapo akachukuliwa na kupelekwa russia huko akajifunza vitu mbali mbali kuhusu mauaji tena ya kimafia ..katika kila mbinu ya kuua ambayo walifundishwa yeye alionekana anaweza kipindi hicho alishabadilishwa jina lake na kuitwa eric lwoma ili aendane na pasport za yule eric aliyepata ajali



    .....

    Mr Ndaro aliyafikilia yote hayo akiwa amejipumzisha kwenye kochi lake kubwa la sebleni anamtambua eric kuwa ashindwi kitu ,sasa yupo kwenye vita naye baaada ya kumtumia kwa miaka nane utajiri aliokuwa nao aliupata kupitia matukio ya unyang'anyi kutoka kwa eric



    ngriii ngriii"ilisikika simu ya mezani ikiita hapo akatoka kwenye mawazo yake akapeleka mkono wake kwenye simu ile



    shikamoo baba"alisikia sauti nzito ikiiongea hapo akapandwa na hofu mdomo ukawa mzito kuongea



    samahani baba nimemuua baba mdogo ila kwa bahati mbaya lakini nimepanga kuja kukuaa wewe kwa makusudi pia nitakuja na kile kisu ambacho ulikuwa unanikata nacho kila nilipokosea kazi yako leo nakuja nacho kukufanyia majaribio ya kuua kwani bado sijaimalika sana kwenye hiyo sekta"aliongea eric kwa mdhaa kisha akakata simu



    kijasho chembamba kikamchuruzika mr Ndaro mgongoni hapo akanyanyua simu yake na kumpigia vijana wake wa kazi dakika chache wakaja vijana wake sita akawaagiza waende kumteka yule katibu mukhitasi wa meja samweli



    asubuhi ya siku inayofuata vijana watano waliovalia nguo za kidaktar wakaingia katika hospital kubwa ya muhimbili safari yao iliishia kwenye chumba cha rehema wakiwa wanaendelea na kazi yao mala mmoja wapo simu yake ikaita akaitoa na kuanza kuongea na mwenzie ambaye mda huo alikuwa ameshaandaa ambulance kwa nje



    maongezi yao yote yalikuwa yananswa na vipaza sauti alivyoweka eric bila wao kuua



    baada ya kufanikiwa kumteka rehema wakaondoka naye

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    asubuhi ya siku inayofuata gari la wagonjwa lilikutwa limeterekezwa kando ya nyumba ya mr ndaro huku ndani yake kukiwa na vijana watano waliokatwa katwa vibaya na kisu damu ilitapakaa kwenye gari zima



    huku yule msichana akiwa hayupo





    Habari ya kuuwawa kwa vijana wake ilimpa hofu zaidi sasa alijiona tayari ameshakalibia kwenye mdomo wa kifo asubili kumezwa tu



    taarifa ya kuwawa kwa vijana wale watano kisha kutelekezwa kwenye gari lile la wagonjwa lilimuacha na maswali mengi sana pale ofisini kwake



    alifikili hiki na kile bila kupata majibu sahihi ya kile akiwazacho .rehema..ndilo jina liliomjia akilini mwake



    kwahiyo rehema ndiye aliyewauwa wale vijana watano "alijiuliza lily bila kupata majibu sahihi ya kile akitakacho



    saa saba ilitimu bila lily kupata majibu sahihi ya maswali yake muda huu ulipifika tumbo lake likaanza kuunguruma hapo akakumbuka kuwa hakutia chochote tangu alipoletewa taarifa ile,akajinyayua kiuvivu kisha akaenda nje sehemu ya parking akachukua gari yake na kuondoka



    akiwaanakalibia mitaa ya posta alimuona mtu ambaye hapo awali alitambua ameshakufa moyo ukampiga kwa kasi ile njaa ikakata hapo akashika breki za fasta sauti kubwa ya kuburuzika kwa tairi zikamtia hofu kila aliyekuwa mahala pale wapo walioshika upande wa moyo kwa hofu na wengine walishituka huku wakitoa matusi mazito kwa namna ya kulidhisha nafsi zao



    lily hakujali hayo yote baada ya kumuona mtu yule alishuka na kuanza kuelekea kule ambapo alihisi atakuwa ameelekea



    erii eric ..."alijisemea lily huku akiwa nauhakika kuwa aliyemuona ni eric kwani hapo awali walishakuwa kwenye mapenzi mazito kabla ya yeye kwenda kujiendeleza kipindi hicho eric alikuwa ameshapandikizwa katika team ya TSA tanzania



    baada ya lily kuangaza kwa muda mrefu kidogo sasa akapata kutulia huku akili yake ikimwambia kuwa yule ni eric na macho yakimuhakikishia hilo



    akaingia kwenye gari yake na kutimka mahala pale



    eric baada ya kuona ameshaonekana kwa lily hakuwa na jinsi akaamua kumfata kwa nyuma lily huku akiwa katika vazi la hijab na sura yake ikafichwa na nikabu na miwani miesi



    katika pikipiki ndogo aina ya one-ten aliyokuwa anaendesha eric hakuweza kufahamika hivyo alimfatilia lily hadi kwenye mgahawa wa leo leo uliopo maeneo ya Tabata



    hapo alimshuhudia lily akishuka kwenye gari yake alichokifanya eric ni kuwai ule mlango wa nyuma akaufungua kidogo kisha akauacha



    lily hakuwa akijua mawazo yake alitambua kuwa ame lock milango hakuwa akijua kama mlango mmoja ulikuwa wazi hivyo lock haikukamata vizuri



    baada ya eric kufungua ule mlango alitoa kidude kidogo kama arage akakiweka kwenye kiti cha nyuma kisha akaondoka mahala pale huku akimtupia busu la mbali lily ambaye muda huu alikuwa anakula chips



    ...

    Baada ya Mr ndaro kutoka kwenye kituo cha polisi ambacho aliitwa kwa ajili ya mahojiano maalumu safari yake ilimfikisha kwake akiwa na mawazo chungu nzima hasa alipofikilia kuhusu vijana wake ambao waliuliwa vibaya sana tena kwa kuchanwa chanwa na visu huku kichwa cha kijana mmoja kikiwa hakionekani katika gari ile



    huuu"alishusha pumzi ndefu Mr ndaro hapo akaona umuhimu wa maji koo lake lilimkauka vibaya sana akachukua kopo la maji na kuanza kuyanywa kwa fujo alipomaliza akajinyanyua pale kitini safari yake ikamfikisha kwenye kaburi la mke wake hapo akatulia na kuanza kufikilia juu ya nini afanya



    akiwa ametulia mahala pale mala mfanyakazi wake wa kike akaja kumpa taarifa kuwa kuna mzigo umeletwa na kijana kutoka kwenye kampuni ya DHL

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akanyanyuka pale alipokuwa amesimama kasha akaanza kurudi ndani huku akitoa ruhusa mzigo huo uchukuliwe na kuletwa ndani kwake ambapo muda huu aliamua kupumzika



    kijua kilishaanza kuzama magharibi utawala wa kiza ulianza kujiwekea mabavu yake



    muda huu wa saa moja jioni ulimkuta Mr ndaro akiwa chumbani kwake ..akiwa anafikilia hili na lile hapo akakumbuka lile box aliloletewa akanyanyuka hadi pembeni ya dirisha akakata kamba zilizofungwa kwenye box lile dakika chache baadaye likawa wazi kabisa



    shiit "alilopoka Mr ndaro hapo akaludi nyuma kwa haraka ule mlango anaofunguaga kwa sekunde leo ametumia dakika tatu hadi kuwa wazi , kitetemeshi kilimkumba sawasawa



    radi radi"aliita mr ndaro huku uso wake ukionekana kusawijika na kile alichokiona kwenye lile box



    .....

    Eric alikuwa nje ya geti kubwa la nyumba ya lily kile kidude alichokiweka kiliweza kumfikisha mahala ambapo lily alikuwa anakaa



    akaangaza huku na kule kama kuna mtu alikuwa anakuja baada ya kujihakikishia awezi kuonekana akaruka na kunasa juu ya ukuta ule zile seng'enge zilizowekwa juu ya ukuta ule hazikuweza kumzuia kuzama ndani ...baada ya kupanda sasa akashuka akaliona lile gari alilokuwa nalo lily mchana katikati ya magari mengine matano



    kwa mwendo wake wa kunyata akafanikiwa kuzama ndani kupitia kwenye dirisha moja lililokuwa wazi usiku huo



    safari yake ikamfikisha kwenye chumba cha lily hapo akazungulusha kitasa nacho kikatii akadhaman ndani hadi pale kitandani



    akiwa anakalibia kukifikia kitanda alihisi kitu kizito kikitua kichwani mwake kiza kikamtanda machoni japo alijitahidi kupambana nacho sekunde chache mwanga wa taa ukamulika chumba kile hapo akaona kitu kilichomfanya aweke tabasmu huku fahamu zikimpotea...





    Mwanga mkali wa balbu ndio uliomtoa katika hali ya kupoteza fahamu hapo akaanza kupepesa macho yake huku taswira ikianza kupenya kwenye macho yake kwa mbali sana akaanza kupata mwangaza



    kitu cha kwanza alichokanza kukitambua ni moshi mzito bila shaka mtu aliyekuwa mbele yake alikuwa anavuta sigara hapo akatuliza akili yake na punde fahamu zikaanza kumrudia akatembeza macho yake kwenye chumba chote kile hapo kwa hesabu zake akatambua kulikuwa na maaskali watano tena wote wana silaha kali



    alipojiangalia vizuri akatambua kuwa mikono yake ilikuwa imefungwa chain hivyo hakuwa anaweza kufanya chochote



    nilikusubilia mda mrefu sana"alisikika mzee mmoja mnene kiasi akiongea huku mdomo wake ukitoa moshi wa sigara



    unatumia "aliendelea kuongea mzee yule huku akitoa sigara na kutaka kumpatia eric



    eric alikataa kwa kutikisa kichwa hapo yule mzee aliludi kwenye kiti chake akafungua kabla ambalo ndani yake kulikuwa na picha za watu ambao alikuwa amewauwa katika yale mataifa pia kulikuwa na picha ya yule dada katibu mukhitasi ambaye anasadikika kuwa alimteka



    yule mzee alizidi kutoa vitu vingi ambavyo ni sehemu ya ushahidi kwa eric lakini eric hakuonekana kuleta ushirikiano zaidi alikuwa akitabasamu kila alipokuwa anaulizwa swali hali hii ilimpachukiza mzee yule hapo akatoa bastora yake na kuanza kumtishia eric kuwa kama hatoleta ushirikiano bhasi uhai wake utakuwa mali ya shetani kwakuwa alikuwa na dhambi nyingi



    eric hakuwa na zaidi yeye alitabasamu tu bila kuongea chochote wakiwa wanaendelea na mahojiano mala simu ya mzee yule ikaita hapo akanyanyuka na kwenda kwenye pembe ya chumba kile akaanza kuzungumza na mtu yule ambaye alimpa mamlaka kuwa kama hataongea bhasi atoke kwenye chumba kile akiwa hana uhai tena kishwa kiwe mbali na mwili wake



    wakati yule mzee anaongea na simu ile eric alihisi hatari zaidi hapo akatambua kuwa wale ni mapolisi ila wamesha vuliwa vyeo vyao kwa rushwa hivyo asipokuwa makini bhasi atauwawa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    baada ya yule mzee kupewa ruhusa ile akarudi kitini huku akiweka bastora yake sawia kwakuwa alishapewa ruhusa ya kuua na boss wake ambaye si serikali iliyomuajiri



    utatoa ushirikiano kwangu au hautatoa"aliongea mzee yule huku akimzunguka eric na alipofikia nyuma yake akachukua gobore kutoka kwa polisi alyekuwa nyuma yake kisha akaja nalo kitini akaliweka usawa wa uso wa eric ambapo sasa aliazimia kuutawanya uso ule



    teh teh teh"alicheka eric hapo alishapanga mbinu zake za kujitoa mahala pale..kicheko chake kikaleta hasira kwa bwana yule akapeleka mkono wake kwenye kifyatulio cha risasi lakini kabla hajafyatua eric aliichezesha meza kisha akanyanua mkono wake wenye chain kwa juu



    ile risasi ilivyotoka ilikosa uelekeo kwani ilepiga ile cheni na kukata kisha ikampiga askali aliyekuwa nyuma hapo eric hakutaka kukosea akapeleka mkono wake k kwa haraka kwenye ila bastora bila kupoteza mda akawashambulia wale mapolisi na kuwaangamiza kisha akammalizia yule mzee kwa kumpiga risasi ya kichwa



    akakata ile chain iliyobakia kisha akavua zile nguo alizokuwa amevaa hapo akabaki na suit nyeusi kwa ndani



    time to play"alijisemea eric huku akichukua siraha moja wapo ile bastora aliiweka kwenye ubavu wake



    milipuko ya risasi iliyokuwa kwenye chumba cha mahojiano iliwasitua maaskali waliokuwa zamu usiku huo hapo wakaanza kusogelea kile chumba



    eric baada ya kuona mda umefika akapanda juu ya meza kisha akafungua dali la chumba kile akapanda na kutokea chumba cha pili wale maasakali wahakuwa wakijua wao walikuwa wanasogea kwenye ule mlango wakidhani eric atakuwa ndani



    loo! Baada ya eric kutokea kwenye kile chumba kingine akawaona maasakali kama watano wakiwa wanasogelea kile chumba hapo akaweka sawa siraha yake kisha akaanza kuwashambulia kwa kuwapiga miguuni hadi akawamaliza wale watano mpambano ulizidi kuwa mkali kwani baada ya kuwatia ukilema wale mapolisi akawaendea wengine hadi akamaliza kituo



    aaah"alilalama eric baada ya kuona shati lake limechafuka kwa damu hapo akavua na kubaki na vest akadandia pikipiki moja ya polisi na kuondoka zake



    ...

    Wakati eric anavamia kwenye nyumba ya lily tayari lily alikuwa amevamiwa akapigwa na kitako cha bunduki kichwani kisha lily akapelekwa sehemu nyingine ya siri na eric akapelekwa kwenye kile chumba cha mahojiano lakini tayari ilishapitishwa kwamba akileta vurugu auwawe lakini kibao kimegeuka



    baada ya eric kutoka pale akaanza kukimbiza pikipiki ile kuelekea kwenye nyumba ya bwana ndaro akiwa nakalibia kufika anapisha na msafara wa magari matatu ambayo yakiongozana hapo akatambua ule ulikuwa msafara wa bwana ndaro tena anataka kutoroka hapo akashika breki kali sana hadi harufu za tairi zikasikika akageuza pikipiki na kuanza kuzifata gari zile







    Eric alizidi kufuatilia gari zile kwa muda zilikata kona na kuanza kuelekea maeneo ya bandarini



    hapo ndipo akafanya kile alichopanga alitoa bastora yake kisha akalenga gari ya nyuma sehemu ya kioo cha nyuma baada ya kioo kile kupasuka akavuta mafuta kwa nguvu na alipokalibia akashika breki ya mbele kwa ghafla hapo akarushwa na kwenda kupeneshwa nyuma ya gari lile ambapo kioo kilipasuriwa



    baada ya kutua nyuma ya gari lile na kwa ujuzi wake wa kutumia siraha alichukua dakika mbili kummaliza dereva na yule jambazi aliyekaa kushoto mwa gari ile



    kutokana na gari lile kukosa uelekea likaanza kwenda huku na kule hapo wale madereva wengine waliona gari lile likiyumba kupitia kwenye sitemirrol zao



    hapo wakatambua kuna tatizo majambazi wapatao wanne wakatoa vichwa vyao nje ya gari lile aina ya rangelover



    eric alikuwa ameshashikilia msikanio wa gari ile kwa huku mkono mwingine ukifanya kazi ya ziada ya kujibizana kwa risasi



    mapigano ya kurushiana risasi yalizidi kushika kasi mda huo eric alikwisha waangamiza majambazi kama wawili kutoka kwenye ile gari

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakiwa wanajibizana kwa risasi ile gari aliyokuwa anaitumia ndaro kutolokea ilikwisha fika bandarini huko wakapanda boti tayari kutoloka



    eric alikuwa bado yuko nyuma akipambana na wale majambazi kwa mbali aliona gari la bwana ndaro likisimama kisha akashuka na kuanza kupiga hatua za haraka kuelekea kwenye ile boti huku lily naye akipelekwa ndani ya hiyo boti



    hapo eric alizidisha nguvu kwenye mapambano muda huu kioo cha mbele kwenye gari yake kilikuwa kimepasuka na kuacha uwazi mkubwa sana



    wale majambazi walizidi kumrushia risasi eric ambazo kama sio uwezo wake wa kucheza na gari bhasi angeshakuwa marehemu



    wakati wale majambazi wanarusha risasi ovyo ovyo yeye eric alikuwa na target moja tu kupiga tairi za gari ile hapo akatuliza akili zake kisha akafyatua risasi ambayo bila kufanya makosa ilipiga tairi ile



    kutokana na mwendo mkali wa gari ile pia kukosa balance kwa dereva lile gari liliyumba na kwenda kugonga kontena moja hapo mlipuko ukawa mkubwa sana gari lile lilirushwa juu sana



    wakati gari lile linalipuka na kwenda juu eric alikuwa anapasua kwenye ule mlipuko na kupita chini .japo moto ulikuwa mkali ila gari yake ilipita bila shaka yoyote



    akavuta mafuta kwa mendo wa kasi sana kisha akaanza kuelekea kwenye ile boti ambayo sasa ilianza kushika kasi



    ving'ora vya magari ya polisi navyo vilikuwa nyuma ambulance nazo zilikuwa katika msafara huo



    ..

    Baada ya kufika ndani ya boti ile mr ndaro alitoa bastora yake kisha akaiweka sawa na dakika chache baadaye mlio mkubwa ukasikika ulikuwa mlipuko ea risasi



    sekunde kadhaa baadaye lily alitupwa baharini akiwa amlowa damu mwili mzima mr ndaro aliona bora amuue lily kuliko kutoloka naye



    eric alishuhudia kitendo kile hapo alikanyaga mafuta balabara na alipokalibia sehemu ya kusimama akvuta zaidi hapo gari iakaluka na kutua juu ya boti ile



    kutokana na kuruka kwa gari ile tenk ya mafuta ikawa imepasuka hapo mafuta yakaanza kuvuja kwenye ile gari kuelekea chini ya boti



    mwili wa lily ulianza kuzama chini ya maji fahamu hazikuwa tena mwilini mwake



    eric baada ya kutua kwenye ile boti akafungua mlango wa gari lakini kabla ajashuka akasikia mlio wa risasi kisha akaanza kuhisi upande mmoja wa mkono wake umekuwa wa baridi sana alipoangalia vizuri akatambua ulikuwa umepigwa risasi



    akaangaza huku na kule hapo akamuaona bwana ndaro akiwa amelaliwa na chuma kubwa damu zilikuwa zikimtoka mdomoni mkono wake ulioshika bastor aliulaza chini hapo eric alichukua ile bastora kisha akammaliza nayo na baada ya hapo akapiga risasi nyingine kwenye ile gari mlipuko mkubwa ukatokea yeye akarushwa mbali na kudondokea majini



    .....

    Asubuhi hii ya siku ya tatu ilimkuta lily akiwa kwenye hospitali ya muhimbili sasa hali yake ilikuwa nzuri kiasi



    taarifa za kifo cha ndaro zilimpa furaha ila hofu yake ilikuwa kwa eric hakujua kama mzima au amekufa kwani baada ya mlipuko maaskali walifika pale na mtu pekee alikuwa yeye ambaye alikutwa juu ya maji akiwa na hali mbaya sana



    ngoo ngoo"ulisikika mlango wa wodini kwake ukigongwa na baadaye mtu akaingia alikuwa kija mwenye umbile la kawaida uso wake ulifichwa kwa kapelo ya kampuni ya DHL ile ya kusambaza vitu mjini



    naomba usaini hapa"aliongea mtu yule kisha akampatia lily peni kusaini kama amepata ule mzigo



    baada ya kumaliza yule kijana akaondoka hapo lily akafungua ile box akaikuta simu ambayo dakika chache ikaita

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akaipokea simu ile furaha iliyopotea sasa ikarudi alikuwa ni eric akizungumza na lily



    baada ya eric kumaliza kuongea na lily akaichukua simu ile na kuitipa ziwani kisha akambusu yule mpenzi wake alibino aliyemuokoa hapo awali



    nakupenda sana"aliongea eric huku akimbusu mpenzi wake kwenye paji la uso



    nakupenda pia "aliitikia yule msichana huku akipeleka mdomo wake kwenye mdomo wa eric dakika chache mbele wakajikuta wakipata futasitahi ya asubuhi...



    MWISHO.



0 comments:

Post a Comment

Blog