Sehemu Ya Tano
(5)
“Umesema huwezi
kusoma?” Mzee Frank alimuuliza Amanda kwa hasira.
“Mapenzi
baba”
“Hebu nijibu swali langu kwanza. Umesema huwezi kusoma?” Mzee
Frank aliuliza huku akiwa na hasira kali, kila alipokuwa akimwangalia Amanda
alijiona kuzidi kuwa na hasira.
“Ndio. Siwezi kusoma baba, nadhani
nitafeli, kila ninapojaribu kusoma ninashindwa” Amanda alimwambia baba
yake.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mzee Frank hakusema
kitu, akabaki kimya kwa muda, mwili wake ulikuwa ukitetemeka kwa hasira,
hakutegemea kusikia maneno kama yale yakitoka kinywani mwa binti yake ambaye
alimpa kila kitu katika maisha yake ili afanikiwe na kuwa mtu fulani hapo
baadae. Hakuipenda kauli ya Amanda, alipenda sana kumuona binti yake akiendelea
kusoma.
“Mapenzi! Yaani mapenzi ndio ambayo yanakufanya kukataa
elimu?” Mzee Frank alimuuliza Amanda.
“Nitafeli baba, siwezi kusoma,
saikolojia yangu imeharibiwa vibaya baba” Amanda alimwambia baba
yake.
“Haiwezekani, lazima uendelee kusoma, achana na mapenzi” Mzee
Frank alimwambia Amanda.
Maneno yake mengi hayakuweza kubadilisha kitu
chochote kile, bado Amanda alizidi kung’ang’ania kwamba asingeweza kusoma
kabisa. Ni kweli, akili yake haikuwa sawa, alikuwa katika mapenzi ya dhati na
Filbert, alimpenda sana na ndio maana hata kile kitendo cha kumsaliti kilimfanya
kuiharibu sana akili yake na kumuweka katika hali ya mawazo.
Hakuona
sababu ya kusoma, mapenzi yalikuwa yameuharibu sana moyo wake, hakujua kama
angeweza kusoma na kufaulu, hakuwa akijisikia sawa kwa wakati huo. Huo ndio
ukawa mwisho wa Amanda kusoma, hakwenda tena shule kitu ambacho kiliwakasirisha
sana wazazi wake lakini hawakuwa na jinsi. Walikuwa wakimpenda sana binti yao na
hawakuwa tayari kumuona akiwa katika hali ya majonzi kama ile ambayo alikuwa
nayo katika kipindi hicho.
Mwaka huo ukakatika na ndipo ambapo aliona
taarifa gazetini kwamba mtu aliyekuwa mpenzi wake, Filbert alikuwa akihama
kutoka katika klabu yake ya Genk ya nchini Ubelgiji na kuelekea nchini Uingereza
na kuanza kucheza katika timu ya Newcastle United. Hiyo ikaonekana kuwa furaha
kwa Amanda kwani aliamini kwamba kila wikiendi angeweza kumuona mpenzi wake wa
zamani akicheza mpira.
“Nakupenda Filbert” Amanda alijisemea kila
alipokuwa akimuona Filbert luningani akicheza mpira.
“Rudi kwangu
mpenzi wangu, nimeacha shule kwa ajili yako, umeuumiza sana moyo wangu,
ninakupenda sana, naomba usahau kila kilichopita, rudi kwangu, mimi nidye mtu
pekee niliye kwenye mapenzi ya dhati, naomba urudi kwangu mpenzi, ninakupenda,
nakupenda sana” Amanda alisema katika kipindi ambacho alikuwa akiziangalia picha
mbalimbali za Filbert.
Majonzi yake hayakuweza kubadilisha kitu
chochote kile, bado Filbert aliendelea kuwa na msichana Saado nchini Uingereza
na wala hakuonekana kuwa na dalili za kumrudia Amanda nchini Tanzania. Maumivu
yake yaliendelea zaidi na zaidi moyoni mwake. Huo ulikuwa ni mwaka wa pili toka
Filbert aache kuwasiliana nae lakini hakuweza kumsahau mwanaume huyo, alikuwa
akizidi kumpenda kila siku na alikuwa tayari kwa chochote kile wakati
huo.
“FORGIVE ME, I MISS YOU AMANDA (NISAMEHE, NIMEKUKUMBUKA AMANDA)”
Yalikuwa ni maneno ambayo yalisomeka vizuri sana katika fulana ambayo aliivaa
Filbert katika kipindi ambacho alifunga goli safi wakati Newcastle ilipocheza na
Manchester United. Filbert alionekana kama kuchanganyikiwa, alikuwa amekimbia
mpaka katika sehemu kilipokuwa kibendera cha kona na kisha kuteleza kwa kutumia
magoti yake na kuifunua jezi yake, fulana yake ya ndani iliyokuwa na maneno yale
ikaonekana na kusomeka vizuri.
Amanda akashtuka, akaikodolea macho
televisheni ile na kuyasoma maneno yale, hakuamini, alikuwa akiyasoma mara kwa
mara, alijiona kama alikuwa akiota na muda wowote ule angeamka kutoka katika
usingizi wa kifo, Filbert alionekana kuanza
kujirudi.
*****
Jina la Amanda ndilo ambalo lilikuwa
likijirudia sana kichwani mwake, kila wakati alikuwa akimfikiria msichana huyo
ambaye alitokea kumpenda kupita kawaida. Kila alipokuwa akikaa, jina la Amanda
lilikuwa likimjia kichwani na hata alipokuwa akiendesha gari bado alikuwa
akimfikiria Amanda.
Msichana huyo alionekana kuwa wa muhimu katika
maisha yake zaidi ya Saado ambaye alikuwa akipendana nae kwa sababu kulikuwa na
kitu cha zaidi, umaarufu na pesa. Filbert alijua fika kwamba Amanda alikuwa
akimpenda, hakumpenda kwa sababu alikuwa tajiri au maarufu bali alimpenda toka
katika siku ya kwanza ambayo alikutana nae nchini Tanzania, ndani ya jiji la Dar
es Salaam katika shule ya Kenton.
Amanda alikuwa tofauti sana na
Saado, msichana huyu wa Kisomali alionekana kuvutiwa na Filbert kwa sababu
alikuwa maarufu na alikuwa na fedha nyingi, ila endapo asingekuwa na vitu hivyo,
Filbert alijua fika kwamba Saado asingeweza kumpenda kama alivyokuwa akimpenda.
Kwake, Amanda akaonekana kuwa kila kitu, alianza kuyarudisha mapenzi yake kwa
Amanda ambaye alikuwa nchini Tanzania.
Filbert hakuwa na nguvu ya
kumpigia simu Amanda, alitamani kufanya hivyo lakini hakuiona kama ilikuwa njia
sahihi. Kutokana na kuandikwa sana magazetini kuhusiana na mahusiano yake na
Saado, alijua fika kwamba Amanda alikuwa akifahamu kila kitu kilichokuwa
kikiendelea, hivyo alihitaji kumuomba msamaha na kisha kumtaka warudiane
tena.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mahusiano yake na
Saado hayakuwa imara kama yalivyokuwa katika kipindi cha nyuma nchini Ubelgiji.
Mara baada ya kuingia nchini Uingereza Saado akaonekana kubadilika tofauti na
alivyokuwa nchini Ubelgiji. Kutokana na uzuri wake ambao alikuwa nao alijiona
kutamani kuwa na mtu ambaye alikuwa na fedha nyingi zaidi ya alizokuwa nazo
Filbert.
Kutokana na kutangazwa sana katika vyombo mbalimbali vya
habari kwamba alikuwa msichana mzuri ambaye alikuwa akimilikiwa na mchezaji soka
akaonekana kujisahau hasa pale ambapo alianzisha uhusiano na mmiliki wa timu ya
Middlesbrough, Bwana Williams Adrian.
Bwana Adrian alikuwa mzee
maarufu ambaye alikuwa akimiliki kiasi kikubwa cha fedha. Yeye ndiye ambaye
alikuwa ameinunua klabu hiyo ambayo ilikuwa na wachezaji wengi mashughuli ambao
alikuwa akiwalipa mishahara mikubwa tofauti na klabu nyingine hapo
Uingereza.
Bwana Adrian alikuwa akimiliki majumba mengi ya kifahari,
klabu za usiku, cassino na hata boti moja kubwa pamoja na ndege yake binafsi.
Uchimbaji wa mafuta katika nchi za Uarabuni ndio ambao ulikuwa ukimuingizia
fedha sana kiasi ambacho kila siku katika maisha yake alikuwa akitumia kiasi
kikubwa cha fedha.
Maisha mwake alikuwa akipenda fedha na alikuwa
amezungukwa na fedha kila alipokuwa. Bwana Adrian alikuwa na kawaida ya kutembea
na wanawake wazuri, wanawake ambao walionekana kuwa warembo sana. Mwaka huu
alikuwa akitembea na mwanamitindo kutoka nchini Brazil na mwaka kesho alikuwa
akitembea na mrembo wa Venezuela.
Hayo ndio yalikuwa maisha yake,
wanawake wengi wazuri alikuwa amekwishatembea nao na kila siku alitamani
kuendelea kutembea na wanawake wazuri maishani mwake. Kitendo cha magazeti mengi
nchini Uingereza kumsifia Saado tayari likaonekana kuwa kosa. Ni kweli Saado
alikuwa na urembo mkubwa sana lakini sifa ambazo alikuwa akimwagiwa na magazeti
mebgi ya Uingereza zikamfanya kuonekana mrembo zaidi na zaidi.
Kama
kawaida yake Bwana Adrian akaanza mishemishe zake, kila alipokuwa akijiangalia
jinsi alivyokuwa na alipokuwa akimwangalia Saado, hakutegemea kumuona msichana
huyo akimkatalia kuwa nae. Alichokifanya ni kuanza kuangaikia namba ya Saado,
alipoipata, akaanza kuwasiliana nae.
Waliongea mengi simuni na huku
wakiahidiana kuonana katika siku ambayo ingekuwa maalumu kwa ajili yao tu. Ndani
ya wiki moja tu, wakaonana katika boti ya Bwana Adrian na kisha kuanza kuongea
mambo mengi. Utajiri wa Bwana Adrian ukaonekana kumlevya Saado, kila alipokuwa
akiiangalia boti ile ilionekana kumshangaza kupita kawaida. Boti ilionekana kama
nyumba ya kifahari, kulikuwa na bwawa la kuogelea pamoja na vitu vingine
vingi.
“Ninakuhitaji Saado” Bwana Adrian alimwambia Saado ambaye
alikuwa akiumauma vidole tu.
“Ila si unajua kwamba nina
mpenzi”
“Najua sana. Na nilifahamu hilo hata kabla sijakufuata” Bwana
Adrian alimwambia Saado ambaye alionekana kutokuwa na ujanja siku
hiyo.
“Kwa sasa hivi siwezi kuwa na wanaume wawili”
“Lakini
hii itakuwa siri kati yangu na wewe”
“Siri! Unadhani kuna siri hapa
duniani? Kuna siku watu watafahamu tu” Saado alimwambia Bwana Adrian ambaye
akaanza kumsogelea mahali pale alipokuwa amekaa.
Tayari Bwana Adrian
aliona kwamba asingeweza kumuua nyoka na wakati alikuwa amekaa mbali,
alichokifanya ni kumsogelea Saado na kisha kuanza kumshika mkono. Saado
alionyesha utulivu wa hali ya juu huku Bwana Adrian akiendelea kuongea maneno
mengi ya kuchombezachombeza ambayo kwa kiasi fulani yalianza kumfanya Saado
kuanza kumsahau Filbert.
Hali ile iliendelea zaidi na zaidi, kila
alipokuwa akiulizwa swali hili, alikuwa akiulizwa swali jingine kitu ambacho
wakati mwingine ukampelekea kutokuwa na majibu yoyote yale. Kutoka mkononi,
akashikwa mapaja na mikono kuzidi kusogea juu mpaka kifuani. Mguso wa mtu mwenye
pesa ukaonekana kuwa tofauti na mtu mwingine, mguso ule ukamfanya Saado kuanza
kutetemeka kwa hisia kali, akayafumba macho yake huku akihisi kama wadudu fulani
walikuwa wakimtembelea, alipoyafungua, alikuwa mtupu.
Hakukuwa na
kilichoendelea mahali hapo, Bwana Adrian akafanya kile alichokuwa akikitaka, kwa
mara ya kwanza Saado akamsaliti Filbert ambaye nae pia alionekana kuanza
kubadilika. Huo ukawa mwanzo wa usaliti, Saado akawa akionana kisiri na Bwana
Adrian huku Filbert akijua kwamba alikuwa peke yake.
Katika kipindi
ambacho Filbert alikuwa akikutana na Saado, kila mmoja alionekana kuwa na
mabadiliko makubwa, mahusiano hayakuwa kama jinsi yalivyokuwa katika kipindi cha
nyuma. Saado aliyaamishia mapenzi yake kwa mwanaume mwenye pesa, Bwana Adrian
huku Filbert akiyaamishia mapenzi yake kwa msichana wake,
Amanda.
“Nitafanya kitu kwa ajili ya Amanda” Filebrt
alijisemea.
Siku hiyo akaamua kuondoka na kuelekea katika duka la nguo
ambapo huko akanunua fulana nzuri nyeupe na kisha kurudi nayo nyumbani. Akaiweka
juu ya kitanda na kisha kuanza kuiangalia. Kitu ambacho alikuwa akikitaka
kilikuwa ni kuandika ujumbe mzito, ujumbe ambao aliuona kama ungemfurahisha
Amanda na kujua kwamba ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea moyoni mwake
kwa sasa.
“Mbona umekuwa mwenye mawazo halafu unaiangalia sana fulana
hiyo?” Denis alimuuliza Filbert.
“Kuna kitu nataka kufanya” Filbert
alimjibu Denis.
“Kitu gani?”
“Nataka nimuombe msamaha
Amanda” Filbert alimwambia Denis.
“Msamaha wa nini?”
“Si
unajua kwamba nilimsaliti”
“Kwani haukuwa umemwambia kama
basi?”
“Hapana. Ilikuwa ghafla, sikutaka kuwasiliana nae” Filbert
alimwambia Denis.
“Kwa hiyo kuomba msamaha na hiyo fulana kuna
uhusiano gani?” Denis alimuuliza Filbert.
“Nitaiandika maneno ya
kuomba msamaha na kisha kuivaa” Filbert alimwambia Denis.
“Bado
unanishangaza. Kwa hiyo utaivaa mitaani?”
“Hapana” CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kumbe utaivaa
wapi?”
“Kwenye mechi ya jumamosi”
“Mechi na Manchester
United?”
“Yeah!”
“Sasa usipofunga
goli?”
“Nitafunga tu, nauamini uwezo wangu” Filbert alimwambia
Denis.
“Sasa Amanda ataionaje?”
“Nadhani nae ataangalia
mpira”
“Sidhani”
“Hata asipoangalia nadhani atasikia tu au
kuona picha kwenye magazeti” Filbert alimwambia Denis.
“Sawa. Kwa hiyo
wewe na Saado mmeachana?”
“Bado”
“Sasa inakuwaje
hapa?”
“Wewe niachie mimi” Filbert alimwambia Denis.
Hivyo
ndivyo alivyokuwa ameamua, alitaka kumuomba msamaha Amanda kupitia fulana ambayo
alikuwa akitarajia kuivaa kwa ndani siku ya jumamosi ambapo kungekuwa na mechi
kali kati ya Newcastle na Manchester United iliyotarajiwa kuchezwa katika uwanja
wa St’ James Park. Alichokifanya Filbert ni kuchukua maker pen yake yenye rangi
nyekundu na kisha kuiandika jezi ile maneno yaliyosomeka “FORGIVE ME, I MISS YOU
AMANDA (NISAMEHE, NIMEKUKUMBUKA AMANDA). Alipomaliza, akaanza kuiangalia na
kisha kushusha pumzi ndefu.
“Imependeza sana” Denis alimwambia
Filbert.
“Nashukuru kaka”
Hiyo ilikuwa ni siku ya Alhamisi,
Filbert alionekana kuwa na hamu ya kutaka kuuonyeshea ulimwengu kwamba alikuwa
na msichana ambaye ni zaidi ya alivyokuwa Saado, hakujua watu wangeongea nini
juu ya ujumbe ule lakini kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kuuonyeshea ulimwengu
kwamba kwa wakati huo alikuwa akimuomba msamaha Amanda.
Siku ya mechi
ikafikia na kisha Filbert kuichukua fulana ile na kuondoka nayo mpaka katika
uwanja wa mazoezi na kisha kuingia katika basi la timu na kuelekea uwanjani.
Kila mchezaji siku hiyo alionekana kuwa na mawazo mengi juu ya mechi ambayo
ilikuwa mbele yao. Mechi hiyo ilionekana kuwa ngumu lakini kila mmoja alikuwa na
kiu ya kutaka kushinda na hatimae kuwa miongoni mwa timu ambazo zimeifunga
Manchester United msimu huo.
Japokuwa wengi walikuwa wakiona kama
wakielekea kufungwa lakini uwepo wa Filbert ukaonekana kuwaondoa wasiwasi.
Walikuwa wakimuamini sana Filbert toka katika kipindi ambacho alikuwa akichezea
Genk ya nchini Ubelgiji.Walipofika katika vyumba vya kubadilishia nguo,
wakazikuta jezi zao ambazo zilikuwa zimewekwa tayari, akaichukua fulani yake
kutoka ndani ya begi lake na kisha kuivaa, akaanza kumuonyeshea kila
mchezaji.
“Who is Amanda? (Amanda ni nani)” Mchezaji mmoja, Baines
alimuuliza Filbert.
“My Only Love (Mpenzi wangu wa pekee)” Filbert
alijibu.
“What about Saado? (Na vipi kuhusu Saado?)” Baines alimuuliza
Filbert.
“Just forget about her (Msahau tu)” Filbert
alijibu.
Mashabiki walikuwa wakisikika wakishangilia uwanjani, hiyo
ilikuwa mechi ya pili kukutana na Manchester United na ndio mechi ambayo alitaka
kuudhihirishia ulimwengu kwamba ukiachana na Saado, pia kulikuwa na msichana
mwingine ambaye alionekana kuwa wa maana sana katika maisha yake na alikuwa hapo
siku hiyo kwa ajili ya kumuomba msamaha.
Katika kipindi ambacho
wachezaji walikuwa wakiingia, Filbert alionekana kuchangamka sana, alikuwa
akipiga makofi kila wakati huku akiwapungua mikono mashabiki wa timu yake ambao
asilimia kubwa walikuwa wakilitaja jina lake kwa sauti kubwa.
Mechi
ilipoanza, wala haikuchukua muda mrefu, Filbert akafunga goli zuri, akakimbia
mpaka sehemu ya kona ambayo ilikuwa na kamera nyingi, akateleza kwa magoti yake
na kisha kuionyesha fulana yake mbele ya kamera ile na mbele ya mashabiki. Watu
wakaripuka kwa furaha, kitendo kile kilionyesha kuwafurahisha sana watu. Goli
hilo lilidumu mpaka mpira ulipokwisha.
“Umeandika maneno ambayo
yanaweza kuwa maswali sana kwa mashabiki wa soka duniani ambao wanaufahamu
uhusiano wako na Saado. Hii ni ishara ya kuonyesha kwamba hampo pamoja kwa
sasa?” Mwandishi wa habari wa Sky Sport alimuuliza Filbert mara baada ya mechi
kumalizika.
“Nadhani huu ndio mwisho wa kila kitu” Filbert alijibu kwa
kujiamini.
“Ulimwambia kabla?”
“Nadhani mambo mengine ni ya
kibinafsi zaidi, ila naomba ujue kwamba nilichokiandika ndicho nilichomaanisha
kutoka moyoni” Filbert alimwambia mwandishi yule.
“Sawa. Ila huyo
Amanda ni nani?”
“Ni msichana wangu”
“Yupo
wapi?”
“Tanzania”
Siku hiyo ndio ikaonekana kuwa mwisho wa
kila kitu, Filbert na Saado wakaachana na kila mtu kuendelea na maisha yake.
Wala haikuchukua muda mrefu, siri ikawekwa wazi na uhusiano kati ya Saado na
Bwana Adrian kuwekwa wazi. Watu walishtuka, hapo ndipo walipoonekana kuhisi
kwamba inawezekana hiyo ilikuwa moja ya sababu ya Filbert kuachana na Saado kwa
sababu msichana huyo alionyesha kuwa na mahusiano na Bwana Adrian, mwanaume
ambaye alikuwa na fedha nyingi.
“Safi sana. Ujumbe umeonekana japo
sina uhakika kama Amanda ameuona” Denis alimwambia Filbert.
“Kama
atakuwa ameuona, nadhani itakuwa poa sana. Kama hajauona basi itanipasa kuelekea
Tanzania mwisho wa msimu” Filbert alimwambia Denis.
“Hakuna
tatizo”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku zikaendelea
kukatika, jina la Filbert lilikuwa kubwa kutokana na upachika mabao ambao
alikuwa nao. Alifunga katika kila mechi ambayo alikuwa akiingia uwanjani. Timu
kubwa zote Ulaya zikaanza kumendea, timu ya Real Madrid, Barcelona na timu
nyingine zikafikisha dau mezani lakini timu ya Newcastle haikuweza kukubali
kumuuza mchezaji huyo ambaye alionekana kuwa lulu.
Uwezo wake
haukumtangaza yeye tu bali uliitangaza mpaka nchi ya Tanzania. Kwa wale ambao
hawakuwa wakiifahamu nchi hiyo wakaifahamu kupitia Filbert. Watu wakafahamu
kwamba nchi iliyokuwa ikipatikana mlima wa Kilimanjaro ilikuwa ikiitwa Tanzania
tofauti na wao walivyokuwa wakifikiria kwamba nchi hiyo ilikuwa ikiitwa
Kilimanjaro.
Mapenzi ya mashabiki wa Newcastle yalikuwa juu kwa
Filbert. Walikuwa wakimpenda kuliko mchezaji yeyote yule. Kila siku walikuwa
wakiwatambia wachezaji wa timu ya upinzani, Sunderland kwamba walikuwa wamepata
mchezaji mzuri ambaye alikuwa na uwezo wa kubadilisha matokeo muda wowote ule.
Pamoja na umaarufu huo, fedha nyingi alizokuwa nazo, bado Filbert alikuwa
akimfikiria Amanda, hakutaka kuwa na msichana yeyote zaidi ya
Amanda.
Amanda hakuwa na cha kufanya zaidi ya
kutokwa na machozi, kile alichokuwa amekiona katika televisheni yake hakuweza
kukiamini. Ilikuwa imepita miaka mitatu bila kuwasiliana na mtu ambaye alimpa
nafasi kubwa moyoni mwake, leo hii mtu huyo alikuwa ameandika ujumbe mzito
katika fulana yake na kisha kuionyeshea dunia kwamba alikuwa amemkumbuka yeye na
pia alikuwa akimuomba msamaha, bila shaka kwa kila kitu
kilichotokea.
Amanda akachukua mto na kisha kuufunika uso wake,
machozi yalikuwa yakimtoka, hakufurahia kama alivyotakiwa kufurahia zaidi ya
kushikwa na uchungu mkubwa, kitendo cha kuyasoma maneno yale kilionekana kumgusa
kupita kawaida.
Amanda hakutoka chumbani kwake, alibaki akilia tu kana
kwamba alikuwa amefiwa. Mpaka katika kipindi ambacho wazazi wake walikuwa
wamerudi kutoka kazini bado alikuwa amejifungia tu. Mama yake, Bi Vanessa
akaonekana kushangaa, hiyo haikuwa kawaida kwa Amanda kuwa chumbani muda mrefu
bila kuja sebuleni na kuanza kuongea nae kama kuwajulia hali.
Kitu
cha kwanza alichokifanya ni kuwauliza wafanyakazi kama Amanda alikuwepo chumbani
kwake au alikuwa ametoka, alipoambiwa kwamba alikuwepo, akaanza kuondoka
kuelekea chumbani humo. Akapiga hodi, hata kabla hajakaribishwa, akaufungua
mlango na kuingia chumbani kwa Amanda.
“Kuna nini Amanda?” Bi Vanessa
alimuuliza Amanda ambaye alionekana kuwa kwenye hali isiyo ya kawaida, macho
yake yalikuwa mekundu, hiyo ilionyesha kwamba katika kipindi kichache
kilichopita alikuwa akilia.
“Filbert mama” Amanda alimwambia mama
yake.
“Filbert! Amefanya nini tena binti yangu?” Bi Vanessa alimuuliza
Amanda.
“Ameniomba msamaha”
“Amekuomba
msamah?”
“Ndio”
“Alikupigia
simu?”
“Hapana”
“Sasa amekuomba vipi msamaha?” BI Vanessa
alimuuliza Amanda.
Hapo ndipo Amanda alipoanza kuelezea kila kitu
kilichokuwa kimetokea. Hakumficha kitu, alimwambia ukweli mpaka katika kipindi
ambacho alikuwa akitazama mechi ambayo Filbert alifunga goli na kisha kuivuta
kwa juu jezi yake na fulana ile iliyokuwa na maneno ya kumuomba msamaha na
kumkumbuka yaliposomeka katika fulana ile.
“Umeamua nini mpaka sasa?”
Bi Vanessa alimuuliza binti yake, Amanda.
“Sijajua niamue nini
mama”
“Wewe ndiye ambaye uliumizwa Amanda, ni lazima uwe na maamuzi
yako mwenyewe, usimame kama mwanamke” Bi Vanessa alimwambia
Amanda.
“Nimsamehe kwa kila kitu”
“Hakuna tatizo. Umeacha
shule kwa ajili yake, litakuwa jambo lisilo na maana endapo utakuwa haumsamehi
kwa kile alichokifanya. Kama amejirudi, hakuna tatizo” Bi Vanessa alimwambia
Amanda.
Huo ndio uamuzi ambao Amanda alikuwa ameuweka moyoni mwake,
alijua fika kwamba Filbert alikuwa amemuumiza sana, aliishi kwa muda wa miaka
mitatu pasipo kuwasiliana nae tena mbaya zaidi akiwa na msichana mwingine kabisa
jambo ambalo lilimkasirisha na kuumiza sana moyoni, katika kipindi hicho
hakutakiwa kukumbuka kitu chochote kile, alijiona kuwa na kila sababu za
kumsamehe Filbert.
Kitu ambcho alikuwa anakisubiria katika siku za
karibuni ni kupokea simu kutoka kwa Filbert, aliombwa msamaha kupitia maandishi
lakini aliona kulikuwa na umuhimu wa kuombwa msamaha kupitia sauti pia. Aliamini
kwamba Filbert angekwenda kupiga simu kwa sababu alikuwa radhi kuionyeshea dunia
kwamba alikuwa amekosea na hivyo alitakiwa kuomba radhi.
Matarajio ya
Amanda ndio yakaenda vile vile, siku iliyofuatia Filbert akampigia simu Amanda.
Namba ilionekana kuwa ngeni tena ikiwa code za nchini Uingereza, Amanda hakutaka
kujiuliza kwamba mpigaji alikuwa nani, alijua fika kwamba mpigaji huyo alikuwa
ni Filbert. Moyoni mwake akajawa na furaha, hapo ndipo alipoamini kwamba Filbert
alikuwa amemaanisha kile alichokuwa amekisema kwamba alikuwa akiomba msamaha kwa
kila kilichokuwa kimetokea.
“Halllow” Amanda aliita mara baada ya
kuipokea simu ile.
“Amanda...!” Filbert aliita.
“Nakusikia
Filbert”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nilidhani labda
sauti yangu utakuwa umeisahau” Filbert alimwambia Amanda.
“Siwezi
kuisahau. Nitaweza kusahau sauti za watu wote pamoja na za wazazi wangu lakini
kamwe siwezi kuisahau sauti yako” Amanda alimwambia Filbert kwa sauti ya
chini.
“Naomba nikuulize swali” Filbert alimwambia
Amanda.
“Hakuna tatizo”
“Uliitazama mechi ya jana?” Filbert
alimuuliza Amanda.
“Mechi gani?”
“Manchester United na
Newcastle”
“Hapana” Alidanganya.
“Daah! Ungeiangalia ungeona
kitu fulani” Filbert alimwambia Amanda.
“Kitu
gani?”
“Nadhani ungeangalia ningeanzia hapo. Ila usijali. Ninapenda
sana kama tukianza upya mahusiano yetu ya kimapenzi, naomba unisamehe kwa kila
nilichokifanya” Filbert alimwambia Amanda.
“Nikusamehe?” Amanda
alimuuliza Filbert.
“Ndio Amanda”
“Kwani umefanya nini mpaka
kuomba msamaha?” Amanda alimuuliza Filbert.
Kwanza Filbert akabaki
kimya, sauti yake haikusikika japokuwa simu ilikuwa hewani. Alionekana kama mtu
ambaye alikuwa akifikiria kitu fulani cha kuongea kwa Amanda ili aweze kueleweka
zaidi. Swali alilouliza Amanda lilikuwa ni dogo lakini lilimaanisha kwamba
Filbert kama Filbert ilimpasa aseme kwamba alikosea wapi na alihitaji msamaha
kwa lipi.
“Niliivunja ahadi niliyokuwekea” Filbert alimwambia
Amanda.
“Ahadi gani?”
“Niliahidi kutokukuacha. Unakumbuka?”
Filbert alimwambia Amanda na kisha kumuuliza swali.
“Nakumbuka. Sasa
kikatokea nini?” Amanda alijibu na kuuliza.
“Nikakuacha kwa sababu ya
tamaa ya macho yangu” Filbert alimwambia Amanda.
“Hebu kuwa muwazi
Filbert” Amanda alimwambia Filbert.
Amanda alijifanya kama
kutokufahamu kitu chochote ambacho kilikuwa kikiendelea katika maisha ya
Filbert, hapo ndipo ambapo Filbert akaanza kuelezea kila kitu kilichokuwa
kimetokea toka alipokuwa amekwenda nchini Ubelgiji. Kwa sababu katika kipindi
hicho alikuwa akihitaji sana msamaha kutoka kwa Amanda, hakutaka kuficha kitu
chochote kile, kile alichokuwa amekificha kilikuwa ni filamu ambazo alikuwa
amejirekodi akiwa na Saado katika kipindi ambacho walikuwa wakifanya
mapenzi.
“Unajua kwamba uliuumiza moyo wangu Filbert?” amanda
alimuuliza Filbert.
“Najua Amanda na ndio maana nimeamua kukuomba
msamaha” Filbert alimwambia Amanda.
“Ok! Baada ya kukusamehe unadhani
kipi kitafuata?”
“Kunipa nafasi nyingine moyoni mwako, naahidi
kutokuichezea” Filbert alimwambia Amanda.
“Nitaamini vipi kama
hautoweza kuichezea kama ulivyoichezea ya mara ya kwanza?” Amanda alimuuliza
Filbert, kila swali ambalo lilikuwa likitoka mdomoni mwake lilikuwa
gumu.
“Sina cha kusema ila naomba uniamini Amanda”
“Na vipi
nikisema kwamba baada ya kuniacha kwa kipindi cha miaka mitatu nimempata mtu
mwingine aliyeonyesha kunijali zaidi yako, mtu ambaye nimekuwa nae katika
mahusiano kwa kipindi kirefu cha miaka mitatu zaidi yako?” Amanda alimuuliza
Filbert ambaye akabaki kimya.
“Umechelewa Filbert. Nadhani utaniumiza
zaidi ya ulivyoniumiza” Amanda alimwambia Filbet.
“Hapana. Siwezi
Amanda. Nakuahidi” Filbert alimwambia Amanda.
“Uliniahidi hivyo hivyo
kipindi cha nyuma” Amanda alimwambia Filbert.
“Nakuahidi. Sasa hivi
ninakuahidi kiukweli Amanda” Filbert alimwambia Amanda.
“Kwa hiyo
zamani ulikuwa ukinitania na haukuniadisi kukweli?” Amanda alimuuliza
Filbert.
“Amanda pleaseeee, nakuhitaji moyoni mwangu” Filbert
alimwambia Amanda kwani tayari alikwishaona kwamba kila swali alilokuwa
akiulizwa lilikuwa gumu.
“Nitaamini vipi kama hautoniumiza
Filbert?”
“Sijui nifanye nini ili uniamini. Labda niwe karibu na wewe
zaidi” Filbert alimwambia Amanda.
“Kumbuka zamani tulikuwa karibu.
Ulikuwa ukinipigia simu kila siku na tulikuwa tukichati kila siku” Amanda
alimwambia Filbert.
“Nataka uje kuishi na mimi huku” Filbert
alimwambia Amanda.
“Unadhani hiyo itakufanya kutokuuvunja moyo wangu
kwa mara nyingine tena?” Amanda alimuuliza Filbert.
“Itasaidia kwa
asilimia mia moja” Filbert alimwambia Amanda.
****
Filbert
akaonekana kuwa na furaha, kitu ambacho alikuwa akikitaka tayari alikuwa
amekwishafanikiwa kukipata. Alikuwa amemuomba msamaha Amanda na kutaka kurudiana
nae mara baada ya kutengana nae kwa muda wa miaka mitatu. Hapo, hakujali kama
watu wangemfikiria vipi kutokana na kumwacha mwanamke ambaye alikuwa akisifika
sana kwa uzuri, Saado.
Kwake alikuwa akimfikiria zaidi Amanda ambaye
alionekana kuwa kama mwanamke wa ndoto katika maisha yake. Alimpenda Amanda na
alikuwa akimhitaji kupita kawaida. Kila alipokuwa akikaa alikuwa akimfikiria
msichana huyo kiasi ambacho akaona ilikuwa ni bora kama angemsafirisha na
kumleta nchini Uingereza na kuishi pamoja nae.
Hapo ndipo ambapo
Filbert akaanza kufanya michakato yote kuhusiana na kumleta Amanda nchini
Uingereza. Kwa sababu alikuwa na fedha wala halikuonekana kusumbua sana, ndani
ya mwezi mmoja tu alikuwa amefanikisha kila kitu na hatimae Amanda kuelekea
nchini Uingereza.
Walipoonana kwa mara ya kwanza ndani ya uwanja wa
ndege uliokuwa jijini London, uwanja wa kimataifa wa Heathrow, Filbert
hakuonekana kuamini, alimwangalia Amanda mara mbili mbili huku akionekana
kumshangaa sana. Amanda alionekana kuwa mrembo hasa, alikuwa mara mbili zaidi ya
vile alivyokuwa amemuona kwa mara ya mwisho nchini Uingereza.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa mwendo wa
haraka haraka akamfuata na kisha wote wawili kukumbatiana kwa furaha. Amanda
akashindwa kujizuia, akaanza kutokwa na machozi mfululizo, hakuamini kwamba mara
baada ya miaka mitatu ya kutengana, leo hii walikuwa wameonana kwa mara nyingine
tena.
“Vua kofia nikuone vizuri mpenzi” Amanda alimwambia
Filbert.
“Hapana. Utaniona tukifika. Nikivua kofia nitajulikana na
watu kuanza kunizunguka zunguka” Filbert alimwambia Amanda.
Akamchukua
na kisha kuondoka nae kuelekea katika sehemu za kukata tiketi ya ndege.
Hawakutaka kubaki hapo, kitu ambacho walitaka kukifanya ni kuondoka na kuelekea
ndani ya jiji la Newcastle kwa ajili ya kuendelea na maisha kama kawaida. Ndani
ya nusu saa, tayari walikuwa ndani ya ndege ya Fly Emirates ambayo ilikuwa
ikitoka London kuelekea Manchester kwa kupitia Newcastle.
Ndani ya
ndege kila mmoja alionekana kuwa na furaha, walikuwa wamekumbukana sana kitu
ambacho mara baada ya kufika nyumbani tu, wakaelekea bafuni kuoga na walipotoka
kuanza kufanya kile ambacho mara nyingi wapenzi hufanya wanapokuwa peke yao
chumbani. Ile ikawa mara ya kwanza kwa Amanda kufanya mapenzi, akaitoa bikira
yake kwa mwanaume ambaye aliamini kwamba angekuja kuwa mume wake wa
ndao.
“Nitakuoa haraka iwezekanavyo” Filbert alimwambia Amanda huku
akiwa kifuani kwake.
“Mbona haraka sana?”
“Ninataka
kuendelea kuishi nawe kwa karibu zaidi” Filbert alimwambia
Amanda.
“Sawa. Na vipi kuhusu masomo yako?”
“Nimebakisha
miezi miwili. Baada ya hapo nitakuwa nimemaliza na kuanza kuchukua digrii ya
kwanza” Filbert alimwambia Amanda.
“Nakupenda
Filbert”
“Nakupenda Amanda” Filbert alimwambia Amanda na kisha
kuendelea na mchezo wao.
Hicho ndicho kitu ambacho wote wawili
walikuwa wakikitaka. Walitaka kuonana na kuwa karibu kama zamani, walijua fika
kwamba ukaribu wao ndio ambao ungewafanya kupendana zaidi na zaidi. Filbert
hakutaka kumfikiria Saado, aliamua kusahau kila kitu kuhusiana na Saado. Zile
picha za ngono ambazo zilikuwa kwenye email yake akawa amekwishazifuta, hakujua
kama katika email ya Saado zile video ziliendelea kubaki. Filbert alikuwa kama
kipofu, alisahau kwamba yeye ndiye ambaye alimuingiza Saado kwenye mahusiano ya
kimapenzi, akasahau kama yeye ndiye alikuwa mwanaume wa kwanza kuzitoa damu za
Saado kitandani, endapo angekumbuka mambo hayo, nadhani ilikuwa ni bora Amanda
kubaki nchini Tanzania kuliko kutaka kuwa karibu nae kwa kuelekea nchini
Uingereza.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Je nini
kitaendelea?
Je ni majanga gani yatakayotokea hapo mbele?
Je
ni kweli Filbert ataweza kuoana na
Amanda?
MWISHO
0 comments:
Post a Comment