Simulizi : A Sex Video Scandle
Sehemu Ya Nne
(4)
Hayo ndio maisha ambayo walikuwa wakiishi
kila siku, walikuwa ni watu wa kufanya ngono kila siku tena huku wakijirekodi na
kisha kuzihifadhi video zile kwenye email zao. Wakaonekana kuzoea sana mpaka
kuwajengea tabia ambapo waliona bila kujirekodi wakati wanafanya mapenzi tendo
hilo halikuwa likikamilika.
Filbert bado alikuwa akiendelea kwenda
shuleni kama kawaida. Ndoto yake nyingine kubwa ambayo alikuwa amejiwekea
ilikuwa ni kusoma sana na hatimae baada kuja kugombea urais katika chama
chochote kile nchini Tanzania. Hilo ndio lilikuwa lengo kubwa ambalo alijiwekea
katika maisha yake na kuhakikisha kwamba siku moja linakuja
kutimia.
Saado alikuwa ameuteka moyo wake, hakumfikiria tena Amanda
ambaye alimuahidi mambo mengi likiwa la kutokumsaliti katika maisha yake.
Filbert alionekana kusahau kila kitu, mapenzi ya Saado yalikuwa yakimlevya kila
siku. Hakukumbuka kumpigia simu Saado, hakukumbuka kuwasiliana nae kwa kutumia
mtandao wa Skype, mtu ambaye alikuwa muhimu kwake wakati huo alikuwa mtoto wa
kisomali, Saado.
Siku ziliendelea kukatika kama kawaida, jina lake
liliendelea kuwa kubwa kila siku. Baada ya ligi hiyo kumalizika hapo ndipo
Filbert alipotakiwa kuachana na timu ya Westerlo ambayo alikuwa akichezea kwa
mkopo na hatimae kujiunga na timu ya Gent, timu ambayo ilikuwa imemsajili.
Kutokana na jina ambalo alianza kujijengea, mashabiki wengi wa timu ya Genk
wakaonekana kuturahia kwa kuona kwamba mchezaji huyo angeweza kuifanyia makubwa
timu hiyo.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kitendo cha kupata
jina kubwa nchini Ubelgiji, jina lake nalo lilikuwa likikua kwa kasi sana nchini
Tanzania. Watanzania wakajivunia sana kuwa na mchezaji kama Filbert ambaye kila
siku kazi yake ilikuwa ni kuitangaza nchi ya Tanzania. Kupitia jina lake, jezi
nyingi za timu ya Genk zikaletwa nchini Tanzania, watu wakaanza kuzinunua kama
njugu, jina la Filbert likaonekana kuwa kivutio kwa kila
mtanzania.
Huo ndio ulikuwa wakati ambao ligi hiyo ilipoanza dhahiri.
Kila siku Filbert alikuwa akiamka asubuhi kama kawaida yake na kisha kwenda
mazoezini hata kabla wachezaji wenzake hawajafika uwanjani hapo. Hiyo ilikuwa ni
njia mojawapo ya kukamilisha ndoto yake ya kuwa mchezaji mkubwa zaidi ya pale
alipokuwa. Mazoezini alikuwa akijituma sana kitu ambacho kilimfurahisha kila
kiongozi wa timu ile.
“WE LOVE U FILBERT, MARRY ME TONIGHT FILBERT,
FILBERT AM FREE TONIGHT” Hayo yalikuwa ni baadhi ya mabango ambayo yalikuwa
yameshikiliwa na wanawake ambao walikuwa wakiingia katika uwanja wa timu ya
Genk. Mabango yale na sauti nyingi za mashabiki zikamfanya Filbert kupata nguvu
ya kuzidi kucheza mpira.
Katika kila mechi ambayo Filbert alikuwa
akiingia uwanjani bado alikuwa akionekana kuwa mwiba mkali kwa timu pinzani.
Katika kipindi hicho alikuwa ndio kwanza ameingia miaka kumi na nane, alionekana
kuwa mshambuliaji machachari ambaye kila alipokuwa akisimama mbele ya goli wazo
lake lilikuwa moja tu, kufunga.
Hiyo ndio siafa ambayo ilimfanya
kujulikana, watoto wa kike hawakuwa nyuma, kila siku walikuwa wakimsumbua huku
wakimuonea wivu Saado kutokana na kuwa na mwanaume ambaye alionekana kuwa mvuto
kwa kila mwanamichezo ambaye alikuwa akimwangalia. Filbert hakutaka kuwa na
wanawake wengi, alichokuwa akikitaka ni kuwa na Saado tu.
“Yaani
sikusomi kabisa siku hizi” Dennis alimwambia
Filbert.
“Kivipi?”
“Kuhusu huyu Saado. Hivi inakuwajekuwaje
hapa?” Dennis aliuliza.
“Kuwaje kivipi?”
“Ni mpenzi wako
au?”
“Wewe unaonaje?”
“Hapo ndipo unaponichanganya. Kila
nikiangalia naona dalili zote za kuonyesha kwamba ni mpenzi wako, ila nilipokuwa
nikikuuliza uliniambia kwamba ni rafiki yako. Hebu nieleze leo” Dennis
alimwambia Filbert.
“Saado ni rafiki
yangu”
“Hapana”
“Sasa kwa nini hutaki
kuamini?”
“Rafiki! Hivi rafiki yako unaweza kulala nae chumba kimoja
tena usiku?” Dennis alimuuliza Filbert.
“Kwa nini
nisiweze?”
“Sisi ni waafrika na ngozi zetu zina joto, mambo hayo
wanayaweza wazungu. Nadhani kuna kitu unanificha” Dennis alimwambia
Filbert.
“Huo ndio ukweli bro”
“Hapna. Hebu niambie
ukweli”
“Sawa. Saado ni mpenzi wangu”
“Sasa ulikuwa
ukinificha nini?”
“Mambo mengine siri sana”
“Hapo hakuna
siri. Na vipi kuhusu Amanda?” Dennis alimuuliza Filbert.
“Hilo ndio
linaniumiza kichwa”
“Moyo wako umeamua nini?”
“Kiukweli moyo
wangu umeamua kuwa na Saado” Filbert alijibu.
“Basi kuwa na
Saado”
“Kwa sasa hivi poa ila kwa baadae nadhani Amanda atanihusu
sana” Filbert alimwambia Dennis.
“Kwa hiyo Saado sio wa
kuoa?”
“Hiyo ndio maana yangu. Huyu ni wa kupita na
kuacha?”
“Hilo ni jibu”
Hivyo ndivyo ambavyo Filbert
alivyokuwa amejipangia, alijua fika kwamba alikuwa akimpenda sana Saado lakini
hakuona kama kulikuwa na uwezekano wa kumuoa msichana huyo maisha yake ya
baadae. Alionekana kuwa msichana mrembo lakini bado hakuwa na sifa za kuweza
kuwa mke wake.
Filbert alijua fika kwamba Saado alikuwa Msomali na
hakuwa Mtanzania hivyo kama angemuoa basi asingeweza kujisikia uhuru kama
ambavyo angekuwa na msichana wa kitanzania. Hiyo pamoja na sababu nyingine za
msingi zikamfanya Filbert kuona kwamba Saado hakutakiwa kuwa mke
wake.
Shuleni alipokuwa akisoma mambo yalikuwa ni balaa. Watu wengi
walikuwa wakimzunguka kila siku huku wengine wakitaka kusainiwa vitabu vyao.
Sura ya Filbert ikaonekana kuwa dili kwa wakati huo, wanawake wengi walikuwa
wakimfuata na kamera zao na kisha kupiga nae picha kwa ajili ya kuwaonyeshea
marafiki zao.
Ucheshi wake pamoja na kuwa na roho ya unyenyekevu kwa
watu wengine ndivyo vilikuwa vitu pekee ambavyo vilimfanya kufagiliwa na watu
wengi ambao walikuwa wakikutana nae. Kila alipokuwa akiingia katika supermarket
mbalimbali hali haikuonekana kuwa ya amani kabisa, watu walikuwa wakimfuata na
kisha kumzunguka kitu ambacho alikuwa akipigwa marufuku kuingia supermarket na
kama alikuwa akitaka kuingia, watu walikuwa wakitolewa katika kila duka ambalo
alitaka kuingia.
Jina lake likazidi kuwa kubwa, Filbert akaonekana
kuwa na nyota ya kupendwa sana na watu wa hapo Brussels. Ni kweli katika ligi
kuu kulikuwa na wachezaji wengi lakini kwa Filbert alionekana kupendwa zaidi na
kila mtu mahali hapo. Kila alipokuwa akipita alikuwa akisimamishwa na watu kwa
lengo la kupiga picha hali ambayo ilimfanya kuanza kutembea na gari na kuanza
maisha ya kujificha.
“Kumbe kuwa supastaa raha sana” Filbert
alimwambia Dennis.
“Kwa nini?”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Heshima. Kila
ninapopita ninapewa heshima kitu ambacho kinanifariji sana” Filbert alimjibu
Dennis.
“Ila kuwa makini na pia endelea kukumbuka kwamba ndoto zako
hazitakiwi kuishia hapo, ikibidi tufanye mchakato uende Uingereza” Dennis
alimwambia Filbert.
Maisha yaliendelea zaidi, hakuacha kucheza mpira
na wala hakuacha kusoma. Mwaka wa kwanza ukakatika, bado aliendelea kusakata
kabumbu. Katika kila msimu wa ulipokuwa ukimalizika wachezaji walikuwa wakipewa
likizo ya mwezi mmoja, kwa Filbert hakutaka kuja nchini Tanzania, alikuwa
akiondoka zake na kuelekea nchini Marekani na kuponda raha huku akiwa pamoja na
msichana wake, Saado.
Katika kipindi hicho Filbert alikuwa na fedha
nyingi na za kutosha huku akiwa kijana mdogo sana, hakuwa amezoea fedha hivyo
alikuwa akizitumia kadri alivyotaka na wala hazikuisha kabisa. Kama starehe,
katika kila mwisho wa msimu alikuwa akifanya starehe ya kila aina, alikuwa
akitembelea katika kumbi zilizokuwa na gharama ambazo zilikuwa zikitembelewa na
masupataa na watu wenye fedha tu.
Filbert hakuchungulia mfuko wake,
alikuwa akiendelea kuzitumia kila siku huku kila wiki kiasi kikubwa cha fedha
kikiingizwa kwenye akaunti yake. Mtu mwenye ngozi nyeusi ambaye alikuwa katika
maisha ya kimasikini akawa na fedha. Alifanya kila kitu alichokuwa akitaka
kukifanya. Alifika mpaka nchini Marekani, nchi ambayo alikuwa akiisikia katika
vyombo vya habari tu.
Leo alikuwa akilala New York na kesho kuhamia
Washington, leo alikuwa akienda kula chakula cha mchana Ohio na kesho alikuwa
akienda kula chakula cha usiku Calfornia. Hayo ndio maisha ambayo alikuwa
kiyapenda, katika kila sehemu ambayo alikuwa akienda, mpenzi wake, Saado alikuwa
pembeni yake.
Hayo yakawa maisha ya kisupastaa ambayo alikuwa akiishi.
Baada ya kukatika siku kadhaa, msimu mwingine ukaanza, huo ulikuwa mwaka wake wa
tatu kukaa nchini Ubelgiji bila kurudi nchini Tanzania. Kama kawaida yake,
uwanjani hakuwa akitaka kuleta mbwembwe nyingi, kitu ambacho alikuwa akikitaka
ni kuudhihirishia ulimwengu kwamba alikuwa mchezaji wa kipekee ambaye alistahili
hata kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia.
Makali yake yakaongezeka
zaidi, starehe ambazo alikuwa amezifanya zikaonekana kama kumpa nguvu ya kucheza
zaidi mpira. Mashabiki walivutiwa nae na hata kumuona kama mungu mtu kwenye timu
yao. Kila alichokuwa akikitaka alikuwa akipatiwa bila kuulizwa swali lolote
lile. Katika kipindi chote ambacho Filbert alikuwa ameichezea Genk, tayari
walikuwa wamechukua kombe la ligi mara tatu.
Jina lake likakuzwa
zaidi, timu za Uingereza zikamuona, hapo ndipo purukushani zilipoanza rasmi.
Manchester United, Arsenal, Chelsea na Liverpool zilikuwa miongoni mwa timu
ambazo zilikuwa zikimhitaji sana Filbert ambaye alionekana kuwa kama lulu katika
maisha ya soka. Fedha zikawekwa mezani kwa ajili ya kumsajiri mchezaji huyo
ambaye aliitwa kwa jina la utani “Mtambo wa mabao”.
“Ofa zimekuja
nyingi tu, tena za fedha ndefu. Unataka nifanye mchakato na timu gani?” Dennis
alimwambia Filbert na kisha kumuuliza.
“Kuna timu zipi
zimekuja?”
“Zote kubwa unazozijua nchini Uingereza” Dennis alimwambia
Filbert.
“Hakuna timu ndogo iliyokuja?”
“Labda na
Newcastle”
“Hiyo ndio nzuri.Nataka kwenda kucheza Newcastle” Filbert
alimwambia Dennis ambaye akaonekana
kushtuka.
“Unasemaje?”
“Nataka kwenda kucheza
Newcastle”
“Hapana. Nadhani utakuwa unanitania. Hebu kuwa serious
kidogo Filbert” Dennis alimwambia Filbert.
“Huo ndio
ukweli”
“Kwa hiyo umeichagua Newcastle mbele ya Arsenal? Umeichagua
Newcastle mbele ya Manchester, Chelsea na Liverpool?” Dennis aliuliza huku
akionekana kutokumuelewa Filbert.
“Ndio”
“Kuna nini
Newcastle?”
“Kuna fedha nyingi”
“Fedha nyingi? Yaani
Newcastle kuna fedha nyingi?”
“Ndio”
“Acha
masihala”
“Ndio hivyo. Kwani Manchester wameweka mezani bei
gani?”
“Wameweka paund milioni kumi na tano, Arsenal wameweka paund
milioni kumi na nne, Liverpool paundi milioni kumi na saba Chelsea paund milioni
ishirini” Dennis alimwambia Filbert.
“Na vipi kuhusu
Newcastle?”
“Wameweka paundi milioni kumi”
“Hapo ndipo
ninapotaka kwenda”
“Mungu wangu! Filbert, una akili?”
“Kwa
sasa utaona sina akili, ila baada ya miaka minne utaona kwamba nina akili”
Filbert alimwambia Dennis.
Huo ndio uamuzi ambao alikuwa ameuweka
mahali hapo, aliichagua klabu ya Newcastle kwa moyo mmoja na wala hakutaka
kwenda katika klabu kubwa ambazo zilikuwa zikimuhitaji kwa wakati huo. Baada ya
tetesi za kutaka kuihama klabu hiyo zilipoanza kusikika, Genk wakaamua kuweka
kikao pamoja nae huku wakimtaka kusaini mkataba mpya ambao ule wa zamani ulikuwa
umebakisha miaka miwili.
Hilo likaonekana kuwa gumu kwa Filbert,
hakutaka kuongeza mkataba zaidi ya kutaka kuhama katika timu hiyo ambayo
ilionekana kumthamini sana. Hilo likaonekana kuwa kama pigo kwa Genk jambo
ambalo liliwafanya waandishi wa habari kuanza kumtafuta kwa ajili ya kufanya
mahojiano nae, walikuwa wakitaka kujua sababu ya kutosaini mkataba na kama
kulikuwa na timu anayotaka kuhamia ilikuwa timu ipi.
“Nataka kwenda
Uingereza” Filbert alimjibu mwandishi wa habari.
“Kipi kimekupelekea
kwenda nchini Uingereza?”
“Nataka kucheza soka katika timu kubwa
zaidi. Najua kwa hapa Ubelgiji hii Genk ni timu kubwa ila nadhani huu ni wakati
wa kwenda kucheza klabu kubwa zaidi ya hii” Filbert aliwaambia waandishi wa
habari.
“Na si kwamba unafuata fedha Uingereza?”
“Hapana.
Nataka kujitangaza zaidi”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Utakwenda timu
gani kwa sababu naona timu zote kubwa nchini Uingereza zimeweka ofa mezani?”
Mwandishi mwingine wa habari aliuliza.
“Nitakwenda
Newcastle”
“Unakwenda Newcastle?”
“Ndio”
“Kwa nini
isiwe Manchester, Arsenal au Chelsea”
“Ni kwa sababu nataka
kuwaonyeshea mashabiki wa Genk kwamba sikuondoka mahali hapa kwa sababu ninataka
fedha zaidi, hapana, ninaondoka mahali hapa kwa sababu ninataka kuwa na
changamoto mpya” Filbert aliwaambia waandishi wa habari.
Kitendo cha
kusema kwamba alikuwa akitaka kwenda kuchezea klabu ya Newcastle, mazungumzo ya
malipo ya mshahara binafsi yakawekwa mezani na kuahidiwa kulipwa paund elfu
sitini kwa wiki ambazo zilikuwa ni sawa na milioni mia ishirini na nne kwa fedha
za kitanzania tena malipo hayo yakifanyika kila wiki.
Katika kipindi
hicho cha mapumziko Filbert hakurudi nchini Tanzania, alikuwa bize
akishughulikia mambo yake ya uhamisho. Mpaka msimu mwingine unafunguliwa,
Filbert alikuwa ndani ya jezi ya klabu ya Newcastle United ya nchini Uingereza.
Kwake, hiyo ikaonekana kuwa ndoto kubwa ambayo alikuwa akiisubiria katika maisha
yake.
Picha nyingi zikapigwa, magazeti mengi yakatangaza ujio wake
ndani ya klabu hiyo kwa paund milioni kumi. Mashabiki wengi wa mpira wakaonekana
kumshangaa kwa kuzikataa klabu kubwa na kuamua kucheza katika klabu hiyo, kati
ya watu ambao walikuwa hawamuelewi kabisa Filbert alikuwa
Dennis.
“Manchester walisema wangekulipa paundi elfu tisini, Arsenal
paundi elfu themanini na Chelsea paund laki moja. Yaani umekataa huko na kuja
hapa kwa paundi elfu sitini!” Dennis alimwambia Filbert.
“Najua
nilifanyalo. Nimekuja hapa ili tupate fedha zaidi, au wewe hautaki?” Filbert
alimuuliza Dennis.
“Tupate fedha nyingi, kivipi?”
“Kihivyo
hivyo”
“Utakuwa umechanganyikiwa”
“Najua, ila baada ya miaka
mitano utaniona nina akili timamu” Filbert alimwambia Dennis.
Jijini
Newcastle, mashabiki wa timu hiyo hawakutaka kutulia, kila wakati walikuwa
wakishangilia, kitendo cha kumpata Filbert kilionekana kuwafurahisha sana na
kuwaona wapinzani wao, Sunderland kuwa si lolote lile. Filbert alionekana kuwa
mwiba mkali uwanjani na kwa upande wa timu pinzani. Uwezo wake wa juu ndio ambao
ulimfanya kila mtu kumwamini na kuona kwamba angekwenda kufanya mambo makubwa
katika maisha yake ya soka ndani ya klabu hiyo.
“Amanda....!” Filbert
alijisemea katika kipindi ambacho alikaa kimya kwa muda chumbani kwake, picha ya
Amanda ilikuwa imemjia kichwani mwake, akaanza kumkumbuka msichana huyo ambaye
hakuwa amewasiliana nae kwa kipindi kirefu sana, miaka
mitatu.
KWA WASOMAJI
WAPYA.
Filebrt alikuwa kijana wa kitanzania,
kijana ambaye alikuwa na ndoto za kuwa mwanasheria mkuu nchini Tanzania. Ndoto
yake hiyo ya kuwa mwanasheria ilikuja kukatika mara baada ya kugundua kwamba
alikuwa na uwezo wa kucheza mpira wa miguu. Alicheza sana mpira wa miguu kiasi
ambacho baba yake, mzee Martin akaamua kumpeleka katika shule ya vipaji vya
michezo, Makongo.
Huko aliendelea kusakata kabumbu mpaka pale
alipochaguliwa kujiunga na timu ya mkoa wa Dar es Salaam na kisha kushiriki
katika mashindano ya Copa Coca Cola. Timu hiyo ikachukua kombe na Filbert kuwa
mfungaji bora na mchezaji bora pia. Timu ikachaguliwa kwenda nchini Ubelgiji.
Siku kadhaa kabla ya kwenda Ubelgiji, Filbert akakutana na msichana ambaye
alimpa namba ya simu, huyu alikuwa Amanda. Walipokutana wakaongea mengi na
kujikuta wakiwa wapenzi waliopendana kwa dhati.
Siku ya safari
inapofika, Filbert anaondoka na kuelekea nchini Ubelgiji. Nchini humo,
anafanikiwa kununuliwa na timu ya mpira wa miguu ya Genk ambayo inamtoa kwa
mkopo na kuchezea timu ya Westerlo. Filbert anaonyesha uwezo wake, anafunga sana
magoli, anapata umaarufu mkubwa uliompeleka kukutana na msichana wa kisomali,
Saado.
Wawili hawa wanaanza uhusiano wa kimapenzi huku wakijirekodi
video katika kila kipindi walichokuwa wakifanya mapenzi. Japokuwa Filbert
alikuwa akiwasiliana sana na Amanda lakini baada ya kumpata Saado, mawasiliano
yanapungua na kufa kabisa. Yeye na Saado, Saado na yeye. Filbert akaamua kurudi
darasani, lengo la kurudi darasani ni kwamba anataka kuwa rais wa Tanzania hapo
baadae, anasoma na kucheza mpira.
Timu zote kubwa za Uingereza
zikamtaka lakini yeye akaamua kwenda Newcastle huku akisema kwamba baadae
angepata fedha nyingi mno kitu kinachomchanganya wakala wake ambaye ni kaka
yake, Denis. Maisha ya soka nchini Uingereza yanaanza na huku mahusiano yake na
Saado yakiendelea kama kawaida. Filbert hamkumbuki Amanda, anayemkumbuka ni yule
ambaye yupo nae katika kipindi hicho, Saado tu. Inatokea siku, siku ambayo
alikaa na kulitamka jina ambalo hakulitamka katika kipindi kirefu cha nyuma,
AMANDA.
*******************
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Amanda hakuonekana
kuwa na furaha nchini Tanzania, kila siku mawazo yake yalikuwa kwa mvulana
ambaye alikuwa akimpenda kuliko mtu yeyote yule, Filbert Martin. Katika kipindi
hicho Filbert hakuwepo nchini Tanzania, alikuwa amesafiri na kuelekea nchini
Ubelgiji kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mpira wa miguu pamoja na timu ya taifa
ya vijana ya Tanzania.
Usiku, mawazo yake yalikuwa yakimfikiria sana
Filbert, kila wakati alikuwa akikosa raha, hakuwa akijisikia vizuri kwani
alitamani kipindi chote cha maisha yake awe pamoja na Filbert kwani ndiye
alionekana mfariji wa maisha yake. Filbert hakuwa pamoja nae, alikuwa
akimfikiria kila siku lakini hali hiyo haikuonekana kubadilisha kitu chochote
kile kwani Filbert aliendelea kuwa mbali na uwepo wa macho
yake.
Wakati mwingine Amanda alionekana kuchukia na kujuta kwa
kuuruhusu moyo wake kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na Filbert, alijiona
kama mtu ambaye alikuwa amefanya kosa kubwa la kumruhusu mwanaume huyo kuushika
moyo wake kama kupita kawaida. Wiki ya kwanza ikakatika tangu Filbert aondoke na
kuelekea nchini Ubelgiji, Amanda aliendelea kuvumilia kwa kuona kwamba ilikuwa
imebakia wiki moja tu na hatimae mpenzi wake arudi nchini Tanzania na kuendelea
kuonana kama kawaida.
Wiki ya pili ikaingia na kumalizika lakini
Filbert hakuwa amerudi nchini Tanzania. Maswali mengi yakaanza kumiminika
kichwani mwake kwamba kulikuwa na kitu gani ambacho kilitokea nchini Ubelgiji
mpaka mpenzi wake kutokuja ndani ya wiki hiyo, maswali hayo yalijibiwa na gazeti
la michezo la Champion ambalo liliandika kwamba wachezaji kadhaa wa timu ya
vijana wa Tanzania ambao walikwenda nchini Ubelgiji walikuwa wamesajiliwa na
timu za huko.
Taarifa hizo zikaonekana kuwa sifa kwa taifa zima la
Tanzania lakini kwa Amanda ilionekana kuwa kama taarifa ya msiba kwani aliposoma
majina ya vijana hao katika gazeti lile, Filbert alikuwa mmoja wapo. Amanda
akashindwa kuvumilia, akaanza kutokwa na machozi, kitu ambacho alikifahamu ni
kwamba Filbert asingeweza kuwa nae tena, alikuwa akimpoteza huku
akimuona.
Mawazo ya Amanda yakaonekana kuwa tofauti hasa pale ambapo
Filbert alipoanza kumpigia simu mara kwa mara na kuanza kuongea nae. Hiyo
ikaonekana kuwa kama faraja kwa Amanda, hakuamini kama angeweza kupokea simu
kutoka kwa Filbert na kumwambia kwamba bado alikuwa akimpenda kupita kawaida na
alikuwa akimhitaji zaidi ya msichana yeyote yule.
Maneno yale
yakamfariji na kumtia nguvu sana, akajiona kuwa msichana aliyekuwa na bahati
kuliko msichana yeyote katika dunia hii. Mawasiliano baina ya watu hao wawili
yalikuwa yakiendelea kama kawaida, mara kwa mara walikuwa wakiongea huku Filbert
akimwambia Amanda juu ya kila kilichokuwa kikiendelea nchini
Ubelgiji.
“Utarudi lini?” Hilo lilikuwa swali kutoka kwa Amanda,
alikuwa akimuuliza kila siku.
“Nitarudi hivi karibuni, lakini kwanza
subiri nikaekae kidogo huku mpenzi” Filbert alimwambia Amanda.
“Sawa.
Ila usinisahau tu kipenzi”
“Hilo usijali, siwezi kukusahau, wewe
ndiye mwanamke ambaye ninampenda kwa moyo wote maishani mwangu, naahidi kukuoa”
Filbert alimwambia Amanda.
“Nashukuru”
“Kuna kitu
nimekifikiria mpenzi”
“Kitu gani?”
“Nataka kuwa rais wa
Tanzania hapo baadae” Filbert alimwambia Amanda.
“Kwa nini umefikiria
hivyo?”
“Basi tu, nataka kuwa rais, ili kukamilisha ndoto yangu naomba
uniunge mkono” Filbert alimwambia Amanda.
“Hakuna tatizo mpenzi,
nitafanya hivyo” Amanda alimwambia
Filbert.
“Nitashukuru”
Hayo ndio yalikuwa maongezi ambayo
walikuwa wakiongea kila siku, walikuwa wakipeana ahadi za kuishi pamoja baadae
pamoja na kuwa na familia moja yenye amani na upendo. Walipendana na
kusikilizana japokuwa walikuwa katika nchi mbili tofauti. Kila mmoja alionekana
kumjali mwenzake, walikuwa wakipendana sana.
Baada ya mwaka mmoja,
mabadiliko yakaanza kutokea katika mahusiano yao, mawasiliano yakaanza kupungua
na hayakuwa kama zamani. Hilo likawa swali gumu kujibika kichwani mwa msichana
Amanda. Hakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikifanya hivyo lakini
alipofikiria kwamba Filbert alimwambia kwamba angeanza kuingia darasani
akaonekana kupunguza wasiwasi juu ya mahusiano yao kwa kuona kwamba Filbert
alikuwa bize na masomo.
Walizoea kuongea simuni, Filbert hakuwa
akipiga simu, walizoea kuongea kupitia mtandao wa Skype lakini Filbert hakufanya
hivyo. Hilo likaonekana kuwa kama pigo kwa Amanda, alikuwa amemkumbuka sana
mpenzi wake lakini hakujua ni kipi kilikuwa kimesababisha jambo hilo kutokea.
Huku akiwa analifikiria sana hilo, hapo ndipo akaanza kupata jibu, jibu la swali
ambalo lilikuwa likimsumbua kichwani.
Filbert alikuwa ameanza kupata
umaarufu, mara kwa mara picha zake zilikuwa zikionyeshwa katika magazeti mengi
Ulaya pamoja na magazeti ya kitanzania, hususani gazeti la Champion. Filbert
alionekana kuwa mwanasoka ambaye alipenda sana starehe, leo alikuwa hapa na
kesho alikuwa pale, alikuwa akitumia pesa bila kuwa na habari yoyote
ile.
Japokuwa alionekana kuwa hivyo lakini bado Filbert alikuwa
kipenzi cha wapenda soka duniani, alikuwa akijituma sana mazoezini na hata
kwenye mechi kitu ambacho kilimfanya kufunga magoli mengi. Amanda alikuwa
akifuatilia kila kitu, kila siku ambayo gazeti la Champion lilipokuwa likitoka,
Amanda alikuwa akilinunua, alihitaji kusoma taarifa nyingi kuhusiana na
Filbert.
Umaarufu, fedha vikaonekana kumsahaulisha Filbert ila pamoja
na hayo yote, kulikuwa na kitu kimoja kikubwa ambacho kilimfanya Filbert
kumsahau Amanda, kitu hiki kilikuwa ni mapenzi. Kwa mara ya kwanza Amanda
alipoona taarifa kwamba Filbert alikuwa amempata msichana wa kisomali, Saado,
mwili wake aliuhisi ukisisimka kupita kawaida, moyo wake ukawa na maumivu ya
ghafla, maumivu ambayo yalifanana na kuchomwa msumali wa moto kwenye kidonda
kibichi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hilo likaonekana
kuwa pigo kwa Amanda, akakosa raha, kila siku akawa mtu wa kulia tu. Katika
kipindi hicho Amanda alikuwa kidato cha tatu, hakuweza kusoma vizuri, hakuweza
kusoma kwa furaha kutokana na kile ambacho kilikuwa kikiendelea nchini Ubelgiji.
Alimpenda sana Filbert na alikuwa tayari kufanya kitu chochote kwa ajili yake
lakini Filbert alionekana kubadilika, akamsaliti na kuanza kutembea na msichana
mwingine, msichana aliyeonekana kuwa mrembo sana, Saado.
Mwaka huo
ukakatika na kuingia kidato cha nne, bado hakuwa akipata simu kutoka kwa
Filbert, hakumsahau mwanaume huyo, kila siku alikuwa akiendelea kununua magazeti
ya Champion huku lengo lake likiwa ni kuzisoma taarifa mbalimbali za Filbert,
alijua kwamba zilimuumiza sana lakini hakuwa na jinsi, alijisikia kuwa na
mapenzi ya dhati moyoni mwake.
“Ninashindwa kusoma mama” Amanda
alimwambia mama yake, Bi Vanessa.
“Kwa nini?” Bi Vanessa aliuliza kwa
mshtuko.
“Mapenzi mama” Amanda alimwambia mama
yake.
“Mapenzi! Yamefanya nini?”
“Ninampenda mwanaume
ambaye anaonekana kutokuwa tayari kunipenda kama ninavyompenda. Mwanaume huyu
amekuwa mwanaume wangu toka kidato cha pili ila kwa sasa hayupo pamoja nami”
Amanda alimwambia mama yake maneno ambayo yalionekana
kumshtua.
“Mwanaume gani?”
“Filbert. Yule mchezaji wa mpira
Ulaya” Amanda alimwambia mama yake.
Bi Vanessa akashindwa kuvumilia
kabisa, alionekana kukasirika sana lakini hakuwa na jinsi, alichoamua kukifanya
ni kumwambia mume wake, mzee Frank juu ya kila kilichokuwa kikiendelea kwa binti
yao. Kwanza mzee Frank akawa na hasira kali, hakutegemea kusikia kwamba binti
yake alikuwa kwenye mahusiano na mvulana yeyote yule, alitaka binti yake asome
kwa juhudi kubwa na hatimae kutimiza ndoto zake ambazo alikuwa amejiwekea toka
kitambo.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment