Simulizi : A Sex Video Scandle
Sehemu Ya Tatu
(3)
Alikuwa mrembo sana
ambaye alikuwa na kila sifa za kuitwa msichana mrembo. Alikuwa na wembamba wa
kawaida, hipsi zake zilikuwa zimetokeza kidogo huku tumbo lake likiwa limeingia
ndani. Ngozi yake ilikuwa nzuri, uso wake ulikuwa ni wa kitoto sana uliokuwa
ukipendeshwa na kidoti kimoja ambacho kilikuwa juu ya mdomo pembeni ya pua yake
nzuri ya kisomali.
Mwendo wake ulikuwa ni wa kawaida sana lakini
kutokana na mvuto ambao alikuwa nao kwa kila mwanaume ambaye alikuwa
akimwangalia, alionekana kutembea kwa mwendo wa madaha kana kwamba alikuwa
akitembea katika ardhi yake, ardhi ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa dhahabu na
madini mengine ya gharama.
Sauti yake ilikuwa ikikamilisha uzuri wake,
alipokuwa akiongea, alisikika vizuri masikioni mwa kila mtu ambaye alikuwa
karibu yake. Wakati mwingine alikuwa akiiweka sauti yake kimahaba kama
ilivyokuwa ya msanii wa maigizo kwa nchini Tanzania, Wema Sepetu. Kwa muonekano
wa kawaida tu, msichana huyu alionekana kuwa tofauti sana na wasichana wengine,
urembo ambao alikuwa nao ulikuwa mkubwa ambao uliwavutia wanaume wote ambao
walibahatika kumtia machoni. Msichana huyu alikuwa akiitwa
Saado.
Saado alikuwa na urembo wa kipekee, uzuri wake ulionyesha
kwamba kweli duniani kulikuwa na wasichana wazuri, wasichana ambao walihitaji
kumpata mwanaume mwenye uwezo wa kuthamini, mwanaume aliyekuwa radhi kufanya
jambo kwa ajili ya msichana mrembo kama huyo. Uzuri wa Saado wala haukujificha,
ulionekana kwa kila mtu ambaye alikuwa akimwangalia huku marafiki zake wengi
chuoni wakiwa wakimuita kwa jina la Cleopatra, mwanamke mwenye asili ya Misri
ambaye anasadikiwa kuwa mwanamke mwenye mvuto kuliko wote waliopata kutokea
katika dunia hii.
Saado alikuwa akiishi hapo Ubelgiji ndani ya jiji la
Brussels katika mtaa wa Hoogstaraat, mmoja wa mitaa ambayo ilikuwa ikikaliwa na
Wasomali kwa wingi nchini Ubelgiji. Saado alionekana kuwa gumzo mtaani kwao,
kila siku majirani zake walikuwa wakimsifia kutokana na urembo ambao alikuwa
nao. Hakuwa na urembo uliochuja kwamba leo utamuona kuwa mzuri na baada ya
kumzoea sana ungeona urembo kupotea machoni mwako.
Sifa za urembo wake
zilikuwa zikisikika katika kila kona, watu wengi walikuwa na hamu ya kumuona
Saado kwani kwa jinsi sifa alizokuwa akipewa zilikuwa nyingi kiasi ambacho kila
mtu alikuwa akitaka kumuona, alifanana vipi.
“Anafanana na Angeline
Jolie?” Mvulana mmoja alimuuliza mwenzake katika kipindi ambacho alikuwa
amesikia sifa kuhusu msichana Saado.
“Wewe twende, utamuona tu” Jamaa
mwingine alimwambia mwenzake, alikuwa amemsifia sana Saado na sasa alikuwa
akimpeleka Hoogstaraat.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Vijana wale
wakafika Hoogstaraat. Wasomali walikuwa wengi ndani ya mtaa huo huku wakiwa
wamejengewa makazi na serikali, majengo marefu ambayo walitakiwa kuishi katika
kipindi ambacho walikuwepo nchini Ubelgiji, kwa sababu wengi walikuwa wamezaliwa
ndani ya nchi hiyo, nao wakachukuliwa kama raia wa nchi hiyo ambao walikuwepo
toka katika kipindi cha nyuma.
Mara baada ya kijana yule kuonyeshewa
msichana Saado, kwanza alibaki kimya kwa muda, alikuwa akimwangalia Saado kwa
umakini mkubwa sana. Saado alionekana kuwa mrembo, ni kweli kwenye maisha yake
kijana huyo alikuwa ameona wanawake wengi warembo lakini kwa Saado alionekana
kuwa tofauti kabisa.
“Huyu ni binadamu au malaika?” Kijana yule
aliuliza huku akimwangalia vizuri Saado ambaye wala hakuwa na habari, ndio
kwanza alikuwa akichezea kompyuta yake ya mapajani.
“Nilipokwambia
kwamba Saado ni mzuri ulitakiwa kuniamini” Jamaa yule alimwambia
mwenzake.
Bado Saado aliendelea kuwa mrembo sana, baada ya siku hiyo,
kuna watu wengi walikwenda mpaka Hoogestraat kwa ajili ya kujionea msichana huyo
na kweli walipomuona, walikiri kwa midomo yao kwamba katika maisha yao
walibahatika kuona msichana mzuri kama Saado na ndio maana hata muigizaji wa
filamu za utupu, Skin Diamond alipoanza kuigiza filamu hizo na kuonekana, kila
mmoja alimuona kufanana sana na Saado.
Huyo ndiye alikuwa Saado.
Alizaliwa mwaka 1992 nchini Somalia ambapo mara baada ya mapigano yaliyodumu
muda mwingi nchini kwao wazazi wake, mzee Jaabir akaamua kuhama pamoja na
familia yake na kuelekea nchini Ubelgiji kwa ndugu zake. Nchini humo wala
hawakupata kipingamizi chochote kile, wasomali wengi walikuwa wameruhusiwa
kuishi ndani ya nchi hiyo kwa kuwa walikuwa wakiepuka vita vya wenyewe kwa
wenyewe ambavyo vilikuwa vikiendelea nchini kwao.
Kuzaliwa kwa Saado
kulionekana kumkasirisha sana mzee Jaabir, alikuwa na watoto watatu ambao wote
hao walikuwa wasichana, katika kipindi hicho alitarajia kupata mtoto wa kiume
lakini mara baada ya mtoto kuzaliwa, alikuwa msichana. Kila wakati mzee Jaabir
alionekana kuwa na hasira, kila alipowaona ndugu zake wakiwa na watoto wao wa
kike moyoni alikuwa akijisikia wivu sana kwani tamaa ya moyo wake katika kipindi
hicho ilikuwa ni kutamani kuwa na mtoto wa kiume.
Hakuwa na jinsi,
hasira zake hazikuweza kubadilisha kitu chochote kile, hazikuweza kumbadilisha
Saado na kuwa mvulana, aliendelea kubaki kama alivyokuwa, aliendelea kubaki
msichana tu.
Baada ya miaka mitano kuishi nchini Ubelgiji, mzee Jaabir
akaamua kurudi Afrika ndani ya nchi yake ya Somalia. Lengo kubwa la kurudi
nchini Somalia lilikuwa ni kuchukua kila kitu ambacho kilikuwa ni mali yake hasa
fedha. Baada ya kuingia nchini Somalia, hakukuwa na ndugu yeyote yule ambaye
alijua ni kitu gani kilitokea huko kwani mzee Jaabir hakuweza kurudi tena na
mwili wake haukuonekana kabisa.
Bi Duddo alijaribu kuulizia kuhusu
mume wake lakini wala hakupata jibu. Kila wakati alikuwa akiwasiliana na ndugu
zake ambao waliamua kubaki nchini humo lakini wote walisema kwamba hawakuweza
mzee Jaabir kwani hali ya nchini Somalia bado haikuwa imetulia, mapigano ya hapa
na pale yalikuwa yakiendelea.
Baada ya miaka kumi, Bi Duddo akaamua
kusahau kila kitu, alijua fika kwamba mumewe alikuwa amefariki na hivyo alikuwa
na jukumu lote la kuwalea watoto wake. Bi Duddo hakupata tabu sana katika malezi
ya watoto wake kutokana na serikali ya Ubelgiji kuwajali sana, alipewa kila kitu
ambacho alikuwa akikihitaji huku watoto wake wakisomeshwa shule, huo ndio
ulikuwa mpango wa nchi ya Ubelgiji, kwa sababu nchi ilikuwa kubwa na watu
wachache, walitaka watu waendelee kujazana ndani ya nchi
hiyo.
Alipofikisha miaka kumi, urembo wa Saado ukaanza kuonekana
machoni mwa watu, nyota njema tayari ilikwishaanza kuonekana maishani mwake.
Japokuwa watu wengine walikuwa wakimshangaa Saado kutokana na urembo ule mahali
alipoupata lakini bado siri kubwa iliendelea kubaki moyoni kwa Bi Duddo, yeye
ndiye ambaye alikuwa akifahamu kila kitu, Saado alikuwa na rangi mchanganyiko,
alikuwa na asili kutoka kwa baba na mama.
Katika miaka ya nyuma Bi
Duddo hakuwa ametulia ndani ya ndoa yake, alikuwa ni mmoja wa wanawake waliokuwa
kwenye ndoa ambao bado walikuwa na tamaa ya kutaka kutembea nje ya ndoa. Tamaa
yake hiyo ndio ambayo ilimkutanisha na Bwana Reese, mwanaume mzungu kutoka
nchini Marekani.
Wakaanzisha mahusiano ya siri. Kila siku Bi Duddo
alipokuwa akielekea katika mghahawa, mahali alipokuwa akifanyia kazi, alikuwa
akiendelea kukutana na Reese ambaye kwa moyo mmoja wakaingia kwenye mahusiano ya
kimapenzi ambayo yaliwapelekea kufanya mapenzi sana na mwisho wa siku kupewa
ujauzito ambao baadae akaja kutoka Saado.
Mzee Jaabiri hakuwa
akifahamu lolote lile, kwa sababu yeye alikuwa mtu wa kukaa nyumbani tu huku
akitumiwa fedha zamatumizi na ndugu zake waliokuwa Ubelgiji, hakuweza kugundua
kwamba mke wake, Bi Duddo alikuwa akitembea nje ya ndoa na hata Saado hakuwa
mtoto wake wa kumzaa.
Hiyo iliendelea kuwa siri ya Bi Duddo, hakutaka
mtu yeyote afahamu kuhusu Saado, mara kwa mara alikuwa akiwaambia kwamba mtoto
wake huyo ndiye ambaye alikuwa amechukua urembo wake katika kipindi ambacho
alikuwa binti wa miaka kumi na nne.
Saado aliendelea kukua zaidi na
zaidi, urembo wake uliendelea kuongezeka na watu kupeana taarifa. Alipofikisha
umri wa miaka kumi na nane hapo ndipo alipoanza masomo ya chuo. Urembo wake huo
uliendelea kuwa gumzo, vijana wengi chuoni hapo walikuwa wamevutiwa na Saado na
kwa nia moja walikuwa wamejaribu kurusha karata zao lakini Saado hakuonekana
kuwa mwepesi kuwakubalia.
“Nakupenda sana Saado” Kijana mmoja
alimwambia Saado ambaye alibaki akitabasamu tu.
“Umenipendea nini?”
Saado alimuuliza kijana yule.
“Kila kitu ulichokuwa
nacho”
“Kama kipi?”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kila
kitu”
“Sawa. Kwenye hicho kila kitu, nitajie vitatu
tu”
“Sura, tabia pamoja na umbo lako, umetokea kuuteka sana moyo
wangu” Kijana huyo wa hapo chuoni alimwambia
Saado.
“Nashukuru”
“Kwa hiyo umekubali kuwa mpenzi wangu?”
Kijana yule alimuuliza.
“Hapana”
“Kwa nini
tena?”
“Siwezi kupenda”
“Kwa nini hauwezi
Saado?”
“Sijafahamu kwa nini”
“Nakuomba unikubalie, nakuomba
uwe wangu Saado”
“Hapana Willem, sihitaji kuwa na mvulana katika
kipindi hiki” Saado alimwambia kijana huyo, Willem ambaye alionekana kutia
huruma japokuwa Saado aliendelea kumuua nyani bila kumwangalia
usoni.
“Au unataka mpaka ningekuwa msomali?” Kijana yule aliuliza,
tayari kwa mbali alionekana kuwa na hasira.
“Hapana. Sina ubaguzi,
kuna wasomali wengi wamekuja na nimewakatalia. Kwangu ninaweza kumkubali kila
mtu, haijalishi ni mzungu, mtu mweusi au msomali. Ninaposema sitaki kuingia
kwenye mahusiano wewe nielewe tu” Saado alimwambia Willem ambaye akakaa kimya
kwa muda.
Huyo ndiye alikuwa Saado, bado alikuwa msichana bikira,
aliithamini bikira yake na hakuwa radhi itolewe na mwanaume yeyote yule. Kila
alipokuwa akijiangalia chumbani kupitia katika kioo chake alikuwa akijiona kuwa
mrembo ambaye alistahili kuendelea kukaa na bikira yake vile vile huku
akijiahidi kwamba mwanaume wa kwanza kumruhusu kuitoa basi angekuwa yule
mwanaume ambaye angekuwa radhi kumuoa tu.
Huo ndio uamuzi ambao
alikuwa amejiamulia. Maisha yaliendelea kwenda mbele zaidi na zaidi na ndipo
alipokuja kuugundua udhaifu wake mkubwa. Saado akatokea kuvutiwa na wavulana
ambao walikuwa na ngozi nyeusi. Japokuwa wazungu wengi pamoja na wasomali
wenzake walikuwa wakimfuata lakini Saado hakuvutiwa nao ila kila alipokuwa
akiwaangalia watu weusi, aliwaona kumvutia kupita kawaida.
Saado akawa
akihitaji sana kuwa na mwanaume mweusi. Hakujua kama wanaume hao walikuwa
wameambiwa au la kwani baada ya mwezi mmoja kuugundua udhaifu wake, wanaume
wengi weusi wakaanza kumtongoza. Saado hakujua afanye nini, wanaume ambao
walikuwa ni ugonjwa wake wakawa wamekwishaanza kumfuata na kumwambia maneno
mengi ya kimapenzi, alitamani kukubali lakini kuna kitu alijiona kutokuwa nacho
kwa kia mwanaume ambaye alikuwa akimfuata, MAPENZI.
Hali ile
iliendelea zaidi na zaidi mpaka pale ambapo vijana kutoka nchini Tanzania
walipokuja nchini Tanzania na kisha kuanza kufanya mazoezi katika chuo hicho
alichokuwa akisoma Saado. Hakuwa akipenda kuangalia mpira lakini mara baada ya
kusikia sifa kemkem juu ya uwezo wa wanaume hao uwanjani tena wakiwa na ngozi
nyeusi, Saado akaamua nae kwenda huko.
Mara baada ya macho yake kutua
kwa Filbert, Saado akaanza kujisikia kitu cha tofauti moyoni mwake, mapenzi
ambayo wala hayakuwepo moyoni mwake yakaanza kumuingia na kujikuta akiwa katika
mapenzi ya dhati kwa Filbert.
Kila siku akawa akiumia sana moyoni
mwake, alijitahidi sana kutafuta kila nafasi ya kuongea na Filbert lakini nafasi
hiyo wala hakuipata kitu ambacho kilimuumiza sana. Siku ambayo alikuwa ameamua
kwamba ni lazima amwambie ukweli Filbert juu ya jinsi alivyokuwa akijisikia
moyoni mwake, siku hiyo wachezaji hawakuja mazoezini, siku zao za kufanya
mazoezi zilikuwa zimekwisha.
Hiyo ikaonekana kuwa habari mbaya kwa
Saado, alikuwa akipenda sana kupata japo dakika kadhaa kuongea na Filbert na
kisha kumwambia ukweli juu ya moyo wake, alijiona kuwa na mzigo mkubwa wa
mapenzi na ni mwanaume mmoja tu ndiye ambaye angeweza kuushusha, huyu alikuwa
Filbert ambaye kwa wakati huo hakuonekana tena machoni mwake.
Siku
zikaendelea kukatika huku moyo wake ukizidi kuumia zaidi. Kila siku alikuwa
akimuwaza Filbert, alimkumbuka sana lakini hakuwa akimuona machoni mwake. Siku
ambayo alikuja kuonana nae katika supermarket moja iliyokuwa katikati ya jiji la
Brussels, Saado hakuonekana kuamini, kwanza akaanza kumwangalia vizuri Filbert,
alipokuja kuhakikisha kwamba ni yeye, akaanza kumfuata, Filbert alikuwa pamoja
na kaka yake, Dennis.
“Excusez-moi (Samahani)” Saado alimwambia
Filbert
“Mmmh!” Dennis ambaye alikuwa pembeni mwa Filbert alitoa
mguno.
“Can you speak English? (Unaweza kuongea Kingereza)” Filbert
alimuuliza Saado ambaye alikuwa ameongea lugha ya Kifaransa.
“Yes. I
can speak English (Ndio. Naweza kuongea Kingereza)” Saado alimwambia Filbert
huku akionekana kuwa na furaha.
Wote kwanza
wakabaki kimya, wakaanza kuangaliana kana kwamba walikuwa wakifananishana. Kwa
Filbert, alikuwa ametulia na kuanza kuufikiria urembo ambao alikuwa nao Saado.
Alionekana kuwa msichana mrembo kupita kawaida na kwa urembo ambao alikuwa nao,
Amanda hakuwa akiingia hata nusu yake.
Tabasamu pana lililotawala uso
wa Saado ndilo ambalo lilimchanganya sana Filbert, akajiona kuhamishwa na
kupelekwa sehemu moja nzuri sana, sehemu ambayo aliiona kuwa kama pepo ndogo.
Kwa Dennis, alibaki akimwangalia Saado, alionekana kuwa msichana mrembo ambaye
kwa mwanaume wa kisasa, mwanaume rijali hakutakiwa kumuacha hata mara
moja.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nakufananisha,
sijui ndio wewe” Saado alimwambia Filbert huku akiachia
tabasamu.
“Inawezekana ndio mimi. Unanifananisha na nani?” Filbert
alimuuliza Saado.
“Na kijana mmoja
hivi”
“Yupi”
“Alikuwa akicheza mpira chuoni. Alitoka
Afrika”
“Mmmh! Si mimi”
“Hapana. Inawezekana kuwa
wewe”
“Sikuwahi kucheza mpira chuoni, yaani sijawahi kusoma chuo huku”
Filbert alimwambia Saado.
“Hapana. Haukuwa mwanachuo, ulikuja na timu
na kuanza kufanya mazoezi, mlitokea Afrika” Saado alimwambia
Filbert.
Hapo ndipo ambapo Filbert akaanza kuvuta kumbukumbu zake na
kugundua kwamba msichana ambaye alisimama mbele yake alikuwa miongoni mwa watu
ambao walikuwa wakiwatazama katika kipindi ambacho walikuwa wakichukua mazoezi,
hapo, furaha ikaongezeka moyoni mwake kwani kwa jinsi dalili zilivyokuwa
zikionyesha, kulikuwa na kila sababu ya kumchukua msichana
yule.
“Nadhani ni mimi”
“Unadhani au ni
wewe?”
“Nadhani. Tulikuwa wengi, inawezekana umenifananisha na mmoja
wa wachezaji wengine” Filbert alimwambia Saado.
“Hapana. Ni wewe”
Saado alimwambia Filbert.
Katika kipindi chote hicho Dennis alikuwa
amekaa kimya huku akiwasikiliza. Kila wakati alikuwa akimuona Filbert akipoteza
muda kwani kwake hasa huku Tanzania akitokea msichana wa hivyo huwa unakamilisha
mambo haraka haraka bila kuchelewa hata kidogo. Kwa Filbert hali ilionekana kuwa
tofauti, alikuwa akitoa maelezo marefu ambayo hakutakiwa kuyatoa mahali hapo
zaidi ya kuelewana na Saado na kisha kuamua kipi kifanyike baada ya
hapo.
Waliendelea kuongea pamoja na hata kutambulishana majina yao,
kila mmoja akaonekana kufurahia urafiki wao ambao ulianza mahali hapo. Huo ndio
ulikuwa mwanzo, waliendelea kuwasiliana mara kwa mara huku katika kila mechi
ambayo timu ya Westerlo ilipokuwa ikicheza Saado alikuwa akielekea uwanjani kwa
ajili ya kumwangalia Filbert.
Walikuwa ni marafiki wa kawaida japokuwa
kila mtu moyoni mwake alikuwa akijisikia mapenzi juu ya mwenzake ila hakukuwa na
mtu ambaye aliweza kulizungumzia suala hilo. Walikuwa wakipeana zawadi
mbalimbali na hata kutembeleana mahali walipokuwa wakiishi.
Kwa
Filbert tayari umaarufu ukaanza kumsogelea, akaanza kujiona mtu wa tofauti kila
alipokuwa akiyaangalia magazeti yakiwa yameandika habari zake kwamba alikuwa
staa ajae katika ulimwengu wa mpira duniani. Hilo lilikuwa likimhamasisha sana,
hakutaka kabisa kuvimba kichwa zaidi ya kuendelea kufanya mazoezi zaidi na
zaidi.
Timu ya Westerlo ikaonekana kupata bahati ya kumsajili kwa
mkopo mchezaji huyo ambaye alionekana kuwa moto wa kuotea mbali. Filbert
aliendeleza mwiba wake kama kawaida, alikuwa akifunga magoli mengi ambayo
yalionekana kuwa muhimu katika timu yake jambo ambalo lilimfanya kupendwa sana
na mashabiki wa timu hiyo, hasa wanachuo.
Hapo ndipo ambapo Filbert
alipoanza kuona matatizo ya kuwa mtu maarufu, kila alipokuwa akipita watu
walikuwa wakimzunguka na kutaka asaini vitabu vyao. Mambo ambayo alikuwa
akiyaona kwenye televisheni yakiwatokea masupastaa wengi kama David Beckham na
wengine wengi tayari yakaanza kutokea katika maisha yake pia.
Kila
kitu kikaonekana katika maisha yake kikaonekana kubadilika. Kitendo cha kufanya
vizuri uwanjani ndicho ambacho kilimfanya kuandikwa sana magazetini na hatimae
kuwa mtu maarufu. Kila kona ndani ya jiji la Brussel lilikuwa likisikika jina
lake kama mchezaji chipukizi ambaye alikuwa mwiba na ambaye angekuja kutisha
sana siku za usoni.
Kutokana na fedha ambazo alikuwa akizipokea kuwa
nyingi, hakuwasahau wazazi wake, kila wiki alipokuwa akipokea mshahara alikuwa
akiwatumia kiasi fulani kwa sababu aliamini kwamba bila wao asingeweza kuwa
mahali hapo katika kipindi hicho. Vilevile Filbert hakutaka kumsahau Amanda,
msichana huyo bado alikuwa msichana wake na hivyo alitakiwa kumuonyeshea mapenzi
japokuwa katika kipindi hicho kulikuwa na mtu mwingine ambaye alikuwa ameleta
mabadiliko moyoni mwake, Saado.
“Hapa inakuwaje Filbert?” Dennis
alimuuliza Filbert.
“Kuwaje kivipi?”
“Kuhusu huyu Amanda na
Saado” Dennis alimwambia Filbert.
“Mbona kawaida
tu”
“Kawaida?”
“Ndio. Amanda mpenzi wangu na Saado rafiki
yangu” Filbert alimwambia Dennis.
“Acha masihala. Unasema Saado ni
rafiki yako na wakati mnafanya mambo mengi kama wapenzi!” Dennis alimwambia
Filbert.
“Kama mambo gani?”
“Hivi unafikiri mimi ni kipofu
Filbert? Huu ni wakati wa kuchagua ni yupi uwe nae. Umekwishapata umaarufu, kuna
wengi watakufuata tena ni wazuri kuliko Saado na Amanda, uamuzi ni wako” Dennis
alimwambia Filbert.
“Ninampenda sana Amanda”
“Najua. Na vipi
kuhusu Saado?”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kama
nilivyokwambia, ni rafiki tu” Filbert alimwambia Dennis.
Huo ndio
ukweli ambao ulikuwepo kwa wawili hao, bado urafiki mkubwa ulikuwa ukiendelea
kama kawaida lakini kila mmoja alikuwa akijisikia mapenzi moyoni mwake. Kila
mmoja alikuwa akiogopa kumwambia mwenzake kwa kuona kwamba asingeonekana mtu wa
kawaida kwani wote wawili walikuwa wakitambua kwamba walikuwa marafiki wa
damu.
Kutokana na Filbert kutikisa sana jiji la Brussels, vyombo vingi
vya habari vikaanza kuutangaza ukaribu ambao alikuwa nao pamoja na msichana
Saado. Jambo hilo liliwafanya wengi kuona kwamba Filbert alikuwa amepata rafiki
mzuri ambaye alikuwa akipendwa na watu wengi ambao walikuwa wakimwangalia.
Katika kila mahojiano ambayo yalikuwa yakifanyika, Filbert alizungumza kweli
kwamba walikuwa ni marafiki na yeye alikuwa na msichana wake aliyeitwa Amanda
ambaye alikuwa nchini Tanzania.
Maneno yake yakaonekana kumuumiza sana
Saado lakini akavumilia kwa sababu hakuwa amemwambia Filbert ukweli kuhusiana na
moyo wake na ndio maana mwanaume huyo alikuwa tayari kumtambulisha msichana
Amanda kama msichana wake ambaye alikuwa akimpenda sana na alikuwa tayari kumuoa
endapo angempa nafasi ya kufanya hivyo.
Ukaribu ukaendelea na urafiki
kusonga mbele kila siku. Mabadiliko yakaanza kutokea. Wakaanza kubusiana na
kupeana kumbatio la tofauti kabisa. Mabusu ambayo walikuwa wakiyatumia kubusiana
ni yale ya pajini pamoja na shavuni na wakati mwingine mikononi. Mabusu
yaliendelea na kadri siku zilivyozidi kwenda kunogeshwa zaidi na kuanza
kubusiana midomoni na walipokuja kujishtukia, midomo ilikuwa wazi na kuanza
kubadilishana mate.
Hao walikuwa marafiki, marafiki ambao wakajikuta
wakianza kufanya vitu vingine kama wapenzi. Hali ile iliendelea zaidi na zaidi
na mwisho wa siku kujikuta wakiwa kitandani watupu kabisa, kilichofuatia ni
Filbert kuitoa bikira ya Saado ambayo ilishindwa kutolewa na wanaume wengi
nchini Ubelgiji.
Mahusiano ya kimapenzi yakaanza rasmi kati ya Filbert
na Saado. Wote wawili waliamua kwa pamoja kwamba uhusiano huo wa kimapenzi uwe
siri ya watu wawili na hakutakiwa mtu yeyote afahamu juu ya kilichokuwa
kikiendelea, wakawekeana makubaliana kwamba hivyo ndivyo ilivyotakiwa kufanyika
katika maisha yao ya mahusiano.
Kila siku wakawa watu wa kulala pamoja
huku wakifanya mapenzi ambayo yaliwafanya kujisikia vizuri na kujiona kwamba
walikuwa wakikosa kitu fulani muhimu katika maisha yao. Kitendo cha kupenda
kufanya mapenzi kila siku ndicho ambacho kikawafanya kuanza kutazama filamu za
ngono. Hapo ndipo ambapo walionekana kuchanganyikiwa zaidi kwani filamu zile
zilionekana kuwa kitu cha tofauti sana ambazho kiliiweka miili yao kuwa kwenye
hali ya tofauti kabisa.
“Mmmh!” Saado alimwambia Filbert katika
kipindi ambacho walikuwa kitandani usiku huku mkanda wa filamu za ngono
ukionekana kwenye televisheni yao.
“Nini tena?”
“Yaani
nimeangalia kwa dakika kumi tu, tayari nishaanza kupata msisimko” Saado
alimwambia Filbert.
Filbert hakutaka kujiuliza, tayari alikwishajua
Saado alikuwa akimaanisha nini, alichokifanya ni kumsogeza upande wake na kisha
kama kawaida yao kuanza kufanya mapenzi. Maisha ambayo walikuwa wakiyaishi
mahali hapo ndio ambayo yalimfanya Filbert kuanza kumsahau Amanda. Ni kweli
katika kipindi cha nyuma alikuwa akimpenda sana msichana huyo lakini muda huo
tayari Saado alikuwa amekwishachukua nafasi maishani mwake.
Ni maisha
ya ngono tu ndio ambayo yalikuwa yakiendelea. Filbert hakufikiria kuhusu kushuka
kiwango, kila alipokuwa akifanya mapenzi na ndivyo ambavyo alikuwa akifanya
mazoezi zaidi zaidi kitu ambacho kilimfanya kuwa katika nafasi nzuri
uwanjani.
“Kamera ya nini?” Filbert alimuuliza Saado katika kipindi
ambacho alikuja chumbani huku akiwa na kamera.
“Kila siku
tunawaangalia watu wakifanya mapenzi, kwa nini na sisi tusiwe tunajitazama
wakati mwingine?” Saado alimwambia Filbert.
“Kwa hiyo unataka
tujirekodi?”
“Ndio”
“Hapana. Huo ni upuuzi Saado” Filbert
alimwambia Saado.
“Upuuzi wa nini sasa? Mbona Ray J alijirekodi na
aliyekuwa mpenzi wake, Kim Kardashian, mbona yule mwanamuziki Eve nae
alijirekodi na mpenzi wake, au umesahau?” Saada alimwambia
Filbert.
“Sasa hauoni kama ile mikanda ilivuja na dunia kuiona na hata
huu wetu utaonekana” Filbert alimwambia Saado.
“Huu hauwezi kuvuja.
Mikanda yao ilivuja kwa sababu waliachana” Saado alimwambia
Filbert.
“Sasa si umeona kwamba hilo ni tatizo”
“Sasa kwani
sisi tutaachana?”
“Hapana”
“Sasa unahofia
nini?”
“Ila hatuwezi kujua kipi kitatokea baadae Saado”
“Kwa
maana hiyo utaniacha na kisha kumrudia huyo Amanda?”
“Simaanishi
hivyo”
“Kumbe unamaanisha nini?”
“Mkanda unaweza kuonekana
kwa staili yoyote ile na si lazima uvuje” Filbert alimwambia
Saado.
“Hapana. Hakuna atakayeweza kuuvujisha zaidi yetu sisi” Saado
alimwambia Filbert.
“Una uhakika?”
“Asilimia mia
moja”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sawa. Ila lengo ni
nini hasa kutengeneza mkanda huu?”
“Kila siku umekuwa ukiangalia utupu
wa wanawake wengine, najisikia wivu, nataka uwe unaangalia utupu wangu tu kwenye
televisheni” Saado alimwambia Filbert.
Kwa kila swali ambalo alikuwa
akiuliza Filbert mahali hapo lilikuwa likijibiwa kisomi zaidi kitu ambacho
kilimfanya Filbert kutokuwa na swali lolote lile zaidi ya kukubali kuutengenza
mkanda huo wa ngono kati yake na Saado. Kila kitu ambacho walikuwa wameanza
kukifanya kilikuwa kikirekodiwa jambo ambalo lilimfurahisha sana
Saado.
Huo haukuwa mwisho wala kuwa mkanda wao wa mwisho bali
waliendelea kurekodi mikanda mingine zaidi na zaidi huku mikanda yote ile
wakiifuta katika kamera na kuiingiza katika email zao. Mchezo huo ukaonekana
kuwa siri, siri ambayo wala haikuweza kuvuja. Mpaka msimu unaishi na Filbert
kuiongoza Westerlo kupanda daraja na kuingia ligi kuu, bado mchezo wao wa
kujirekodi ulikuwa ukiendelea kama kawaida.
Filbert na Saado wakaacha
kuwaangalia Micky Blue, Skin Diamond, Victoria Allure na wasanii wengine wa
filamu za utupu na kuanza kujitazama wao wenyewe. Hayo ndio yakawa maisha yao,
kila siku ukawa mchezo wao, hakukuwa na mtu aliyefikiria kwamba mazoea hujenga
tabia, na kama ni mazoea mabaya basi yangeweza kujenga tabia
mbaya.
Filbert hakuonekana kufahamu kitu chochote kwamba yale mazoea
yangeweza kujenga tabia, tabia ambayo angeifanya hata sehemu nyingine na
kumletea matatizo hasa katika maisha yake ya baadae, kwake, kila kitu ambacho
kilikuwa kikiendelea mahali hapo alikichukulia kuwa kawaida tu, wala hakutaka
kujali sana kwa kuwa filamu zote ambazo alikuwa akiigiza na Saado kitandani
alikuwa akizihifadhi katika email yake.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Je nini
kitaendelea?
Je nini hatma ya maisha yao?
Je Filbert ataweza
kumkumbuka Amanda?
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment