Simulizi : A Sex Video Scandle
Sehemu Ya Pili
(2)
Mawasiliano yakawa yameanza rasmi kati ya
Filbert na Amanda. Kila siku walikuwa ni watu wa kupigiana simu na kuzungumza
mengi kuhusiana na mapenzi. Kila mmoja alionekana kumjali na kumsikiliza
mwenzake, mapenzi yao machanga yakaonekana kuanza kuchipua kwa kasi sana, kasi
ambayo iliwashangaza hata wao wenyewe.
Kila siku wakawa watu wa
kupigiana simu usiku na kutumia muda mwingi wa kuzungumza pamoja. Katika kipindi
hicho ndicho ambacho kilimfanya Amanda kuchelewa sana kulala, kila siku alikuwa
akilala saa nane usiku kwani muda wote alikuwa akiongea na Filbert simuni.
Filbert ndiye alionekana kuwa kipenzi chake cha moyo wake, kila siku Amanda
alijiona kuwa malikia huku akimchukulia Filbert kuwa mfalme. Mapenzi yalikuwa
yamewalevya wote, wakajikuta kila siku wakizidi kuogelea katika dimbwi kubwa la
mahaba.
Filbert hakusahau, alikuwa akikumbuka sana kwamba siku chache
zijazo alikuwa akitarajia kusafiri na kuelekea Ubelgiji. Kwenda ulaya ndio
ilikuwa sehemu ya ndoto ambazo alikuwa amejiwekea moyoni mwake, kwa sababu
alikuwa mcheza soka, alikuwa akitamani kwenda kucheza soka katika nchi mojawapo
ulaya.
Filbert hakutaka kuikatisha ndoto yake kwa sababu ya mapenzi,
japokuwa alijua fika kwamba alikuwa akimpenda sana Amanda lakini hakutaka
kuikatisha ndoto yake hiyo kwa ajili ya msichana huyo. Bado mapenzi aliyaona
kuwa na sehemu yake lakini hata mpira nao ulikuwa na sehemu
yake.
“Nataka tufanye mapenzi” Amanda alimwambia
Filbert.
“Tufanye mapenzi?” Filbert aliuliza kwa
mshtuko.
“Ndio” Amanda alijibu kwa sauti ya
chini.
“Haiwezekani Amanda. Kwa sasa hivi ni ngumu sana mpenzi”
Filbert alimwambia Amanda.
“Nakuomba mpenzi. Mwili unanisisimka kila
ninapoisikia sauti yako” Amanda alimwambia Filbert.
“Najua mpenzi
lakini naomba unipe muda”
“Muda wa nini tena?”
“Wa kupata
nafasi ya kucheza soka Ulaya”
“Kwani si unakwenda huko keshokutwa
mpenzi, kwani nimekuzuia?”
“Najua haujanizuia. Ila tukifanya najua
magoti yangu yatalegea sana. Acha nipate nafasi kwanza, baada ya hapo tutafanya
mapenzi mpaka uchoke” Filbert alimwambia Amanda.
“Ninapata tabu sana
usiku mpenzi”
“Najua Amanda. Vumilia kipenzi changu, vumilia tu”
Filbert alimwambia Amanda.
Amanda alikuwa akipata tabu kila siku,
mwili wake ulikuwa ukimsisimka kupita kawaida, kila siku alikuwa akitamani
kufanya mapenzi na mwanaume, mwanaume pekee ambaye alikuwa akimpenda na
kumhitaji sana, Filbert. Amanda hakuwa akilala vizuri usiku, muda mwingi alikuwa
akiyachezea matiti yake kila alipokuwa akilala kitandani, tena alikuwa akipenda
kulala mtupu kabisa.
Ndoto za kufanya mapenzi ndizo ambazo zilikuwa
zimemtawala muda huo, hakutaka kuendelea kubaki katika hali hiyo na ndio maana
aliamua kumwambia Filbert ukweli juu ya alivyokuwa akijisikia japokuwa Filbert
hakutaka kuelewa kabisa.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Filbert alikuwa na
ndoto moyoni mwake, ndoto ambayo aliiona ikikaribia kukamilika kwa wakati huo,
alikuwa akitaka kuwa mmoja wa wachezaji soka wa kulipwa katika nchi mojawapo
ndani ya bara la Ulaya. Uwezo wake wa kucheza mpira ulikuwa mkubwa sana kiasi
ambacho hakujiona kama alistahili kucheza mpira hapa barani Afrika. Kila siku
alikuwa akiamini kwamba kuwa na mwanamke ndio kilikuwa chanzo cha wanasoka wengi
kushuka viwango.
Filbert hakuwa na lengo la kuwa na mwanamke lakini
mara baada ya Amanda kumuonyeshea uhitaji mkubwa, akajikuta akikubali kuwa nae.
Sasa hivi Amanda alikuwa amemwambia kitu kingine kabisa, kufanya mapenzi kama
wapenzi wengine walivyokuwa wakifanya. Huo ukaonekana kuwa mtihani mkubwa kwa
Filbert, ni kweli alikuwa amemkubalia Amanda kuwa mpenzi wake lakini hakujiona
kama alikuwa tayari kufanya mapenzi na msichana huyo.
Kitu ambacho
alikuwa akikiogopa ni kushuka kiwango katika uwanja wa mpira. Alijua fika kwamba
endapo angethubutu kufanya mapenzi na msichana Amanda basi kwa namna moja au
nyingine ni lazima magoti yake yangepungua kufanya kazi na mwisho wa siku
kulegea kabisa na hivyo kushusha uwezo wake wa kusakata kabumbu uwanjani. Hiyo
ndio ilikuwa sababu kubwa ambayo ilimfanya Filbert kukataa katakata kufanya
mapenzi na Amanda, kila siku alijiona kutaka kuwa katika uwezo wa juu mpaka pale
atakaposajiliwa na timu kubwa yoyote ile barani Ulaya.
“Kwa hiyo
tutafanya lini?” Amanda alimuuliza Filbert.
“Nikirudi kutoka Ubelgiji”
Filbert alimwambia Amanda.
“Sawa. Ila uliniambia kwamba usingerudi
sasa hivi” Amanda alimwambia Filbert.
“Nitarudi tu, wewe vumilia
kwanza mpenzi, tatizo lipo wapi? Nimekuwa wako kwa hiyo hutakiwi kuhofia kitu
chochote kile” Filbert alimwambia Amanda.
“Sawa...ila unanifanya
kujisikia vibaya sana mpenzi. Nina hamu sana” Amanda alimwambia
Filbert.
“Umekwishawahi kufanya
mapenzi?”
“Hapana”
“Sasa hiyo hamu inatoka
wapi?”
“Jamani mpenzi, si nina mwili na pia nina kila kitu ambacho
msichana anatakiwa kuwa nacho” Amanda alimwambia Filbert.
“Kwa maana
hiyo wewe ni bikira?”
“Ndio”
“Safi. Naomba uitunze mpaka
nitakaporudi. Utaweza kuitunza?” Filbert alimwambia Amanda na
kumuuliza.
“Kwa ajili yako nitaweza mpenzi. Ila usichelewe kurudi”
Amanda alimwambia Filbert.
“Kwani nikichelewa nitakuta
imetolewa?”
“Hapana bali nitakuwa nikipata tabu zaidi ya kutamani kuwa
pamoja nawe” Amanda alimwambia Filbert.
“Naomba uitunze kwa ajili
yangu”
“Usijali laazizi...ila naomba usiniumize huko
mbeleni”
“Usijali. Sitokuumiza, nitayakumbuka mapenzi yako kila
siku.
Maneno mengi ya faraja ambayo walikuwa wakiambiana yalionekana
kumfariji kila mmoja. Kila wakati walikuwa wakitamaniana sana kiasi ambacho
walikuwa wakichukia sana kwa sababu gani mpaka katika kipindi hicho bado
walikuwa wakiishi kwa wazazi. Kwa upande wa Amanda, darasani hakuwa akisoma kwa
raha, kila wakati mawazo yake yalikuwa kwa mvulana wake ambaye katika kipindi
hicho alionekana kuwa kila kitu, Filbert.
Kama ambavyo mapenzi
yalivyojulikana kwamba yalikuwa kikohozi, marafiki zake wakaanza kufahamu juu ya
mapenzi hayo. Amanda akashindwa kabisa kujizuia jambo ambalo likamfanya
kumwambia rafiki yake mpendwa, Happiness. Mara ya kwanza Happiness alionekana
kushtuka sana, alimfahamu vilivyo Amanda, alionekana binti mrembo na mkimya sana
ambaye wala hakuwa akijihusisha na mwanaume kabisa, katika kipindi hicho ambacho
alisikia kwamba Amanda alikuwa na mpenzi, Happiness alionekana kushtuka
sana.
“Una mpenzi?” Happiness aliuliza huku akionekana
kushtuka.
“Ndio”
“Yupo wapi?”
“Makongo Secondary
School”
“Umeonana nae vipi na wakati huwa hautoki nyumbani?” Happiness
alimuuliza Amanda.
“Siku ile walivyokuja kucheza mpira”
“Au
unamzungumzia yule aliyefunga magoli siku ile?”
“Yeah! Anaitwa
Filbert”
“Waoooo! Una bahati Amanda. Lucy na wenzake walikuwa
wakimzungumzia sana” Happiness alimwambia
Amanda.
“Walisemaje?”
“Eti ni mwanaume mzuri ambaye ana umbo
linalomvutia kila mwanamke. Hebu niambie vizuri kuhusu yeye” Happiness
alimwambia Amanda.
“Unataka kujua nini kuhusu
yeye?”
“Chochote kile”
“Ni mzuri sana, halafu anajua
kupenda”
“Kweli?”
“Ndio hivyo”
“Kweli una bahati
sana Amanda kwani wanaume wengine majanga” Happiness alimwambia
Amanda.
“Kwani wewe na John vipi?”
“Mmmh! Yaani ni balaa.
Sijawahi kuwa na mwanaume anayependa sketi kama yule. Kila sketi inayopita mbele
yake anaitamani. Yaani ni balaa” Happiness alimwambia Amanda.
“Pole
sana”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Asante
sana”
Hao walikuwa wanafunzi wa kidato cha pili, japokuwa walikuwa
wadogo lakini katika masuala ya mahusiano walikuwa wakiyapenda na kushika nguvu
katika maisha yao. Kila mmoja alikuwa na mpenzi wake ambaye alikuwa akimpenda
kwa moyo wa dhati. Walikuwa wakiendelea kusoma huku katika upande mwingine wa
maisha yao wakiwa wameyaacha mapenzi yachukue nafasi.
Siku hiyo
ikapita na kubaki siku moja kabla ya timu ya mpira ya vijana kuondoka kuelekea
nchini Ubelgiji. Kwa Filbert ilikuwa ni furaha tupu, kila wakati alikuwa
akiwaambia wazazi wake kwamba ile ndio ilikuwa nafasi yake ya kubadilisha maisha
yake na maisha ya familia yake. Alionekana kuwa mwingi wa furaha, kila wakati
alikuwa akiwataka wazazi wake wamtamkie maneno ya baraka hata kabla hajasafiri
kuelekea nchini Ubelgiji.
Wakati Filbert akiwa na furaha, kwa Amanda
moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali mno. Alikuwa ahamini kama mpenzi wake
ambaye alikuwa amedumu nae katika mahusiano kwa kipindi cha wiki mbili alikuwa
akitaka kuondoka kuelekea nchini Ubelgiji na hivyo kumuacha katika hali ya
mawazo na maumivu makali.
Kila siku sala yake ilikuwa ni kuona akikaa
na Filbert kwa zaidi na zaidi, hakutaka kumuacha na wala hakutaka kuona mtu huyo
akienda mbali nae. Sala yake ikaonekana kutokujibiwa, yalikuwa yamebaki masaa
ishirini na saba kabla ya Filbert kuondoka na timu nzima ya vijana kuelekea
nchini Ubelgiji kwa ajili ya kuchukua mazoezi kwa muda wa wiki
mbili.
“Sina cha kufanya. Siwezi kusema nisiende huko mpenzi, ni
lazima niende nikajaribu bahati yangu” Filbert alimwambia
Amanda.
“Nakupenda mpenzi”
“Nakupenda pia. Ila hautakiwi
kulia, yakupasa kufurahia kwani kama nitabadilisha maisha yangu na kuwa ya juu,
basi amini hata maisha yako nawe yatakuwa hivyo hivyo” Filbert alimwambia
Amanda.
Katika kipindi hicho walikuwa Kijitonyama, katika mtaa ambao
Filbert alikuwa akiishi lakini si ndani ya nyumba ya mzee Martin. Filbert
alikuwa amekaa na Amanda katika chumba cha rafiki yake, Enock ambaye hakuwa
akiishi mbali kutoka katika nyumba ya mzee Martin.
Siku hiyo Amanda
hakutaka kwenda shuleni japokuwa alikuwa ameaga kwamba angekwenda shuleni.
Safari yake ya kuelekea shuleni iliishia katika mtaa wa Kijitonyama, alijiona
kuwa na muda mwingi wa kukaa na mpenzi wake na kuongea mambo mengi kuhusiana na
maisha yao ya mahusiano.
Siku hiyo walikuwa kitandani, kipindi chote
Amanda alikuwa amelala kifuani mwa Filbert. Mwilini alikuwa na nguo za nyumbani,
nguo za shule ambazo alikuwa amezivaa siku alipotoka nyumbani kwao hakuwa nazo
mwilini bali alikuwa ameziweka katika begi lake. Hakuona sababu ya kwenda shule
na wakati mpenzi wake alikuwa akisafiri kuelekea Ubelgiji siku
inayofuatia.
“Hivi unajua kwamba hii ni kesi?” Filbert alimuuliza
Amanda.
“Kesi ipi?”
“Kutokwenda shule na kuja
kwangu”
“Najua”
“Sasa unataka niingie kwenye
matatizo?”
“Hapana”
“Ulifika shule
leo?”
“Niliishia getini. Baada ya kushushwa kutoka garini, nikaondoka
zangu” Amanda alimwambia Filbert.
“Mchezo mbaya sana huo. Usijaribu
kuufanya siku nyingine” Filbert alimwambia Amanda.
“Kwani umekasirika
kuniona mahali hapa?”
“Hapana”
“Sasa kwa nini uwe mchezo
mbaya?”
“Ungeweza kunifanya nisiende Ubelgiji, ungeweza kuzizima ndoto
zangu mpenzi” Filbert alimwambia Amanda.
Walibaki wakiongea mambo
mengi, walibuasiana na kushikana hapa na pale lakini hawakufanya mapenzi.
Japokuwa Amanda alikuwa aking’ang’ania mara kwa mara kwamba kama wapenzi
walitakiwa kufanya mapenzi lakini kwa Filbert jambo hilo lilikataliwa kwa nguvu
zote moyoni mwa Filbert. Bado mawazo yake yalikuwa juu ya mchezo wa mpira wa
miguu, hakutaka kufanya mapenzi kwa kuona kwamba nguvu zake za miguu zingeshuka
kwa kiwango kikubwa sana, alitaka kwanza kutafuta mafanikio.
“Kwa
hiyo, hiyo safari itakuwaje?”
“Tunakwenda kulala hotelini leo na kesho
asubuhi safari” Filbert alimwambia Amanda.
“Unakwenda saa ngapi
hotelini?”
“Saa mbili usiku”
“Kwa hiyo nikiondoka hapa ndio
basi tena hatutoonana mpaka utakaporudi?” Amanda alimuuliza
Filbert.
“Nafikiri” Filbert alimjibu Amanda.
Kama alivyosema
Filbert ndivyo ilivyokuwa. Saa mbili usiku siku hiyo akawaaga wazazi wake na
ndugu zake na kisha kuingia ndani ya gari la wachezaji na safari ya kuelekea
hotelini kuanza. Ndani ya basi hilo kulikuwa na baadhi ya wachezaji kwani
wengine bado hawakuwa wamepitiwa. Kila mmoja ndani ya basi alionekana kuwa na
furaha, walikuwa wakiongea huku wakionekana kutokuamini kama kweli siku hiyo
ndio ilikuwa siku ambayo walikuwa wakielekea Ulaya kwa ajili ya kufanya mazoezi
ya kujiweka fiti.
“Tukifika huko tutawaandalia mechi kadhaa, jitahidi
sana kucheza kwa uwezo wa juu, huwezi jua, hii inaweza kuwa nafasi yako ambayo
haitoweza kutokea tena katika maisha yako” Kocha wa timu hiyo, Abdulazak
aliwaambia wachezaji.
“Kama wewe ni mshambuliaji, funga magoli ya
kutosha, kama wewe ni kipa, daka vya kutoka, kama wewe ni kiungo, kaba na kugawa
mipra uwezavyo na hata kama wewe ni beki, zuia uwezavyo. Japokuwa tunakwenda
ishirini na tano huko, nata turudi sisi tu, wachezaji wote tuwaache huko wakiwa
wamenunuliwa na timu mbalimbali” Kocha mkuu aliongezea.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maneno hayo
yalionekana kuwa kama sumu mioyoni mwa wachezaji, kila mmoja akaonekana kuwa na
chachu ya kuonyesha uwezo mkubwa mara baada ya kuanza kucheza mechi za majaribio
nchini Ubelgiji. Kila wakati wachezaji walikuwa wakipena amaneno ya hamasa ya
kutiana nguvu.
“Nitahakikisha nabaki Ubelgiji, huku bongo hakunifai”
Filbert alimwambia rafiki yake ambaye nae alikuwa amechaguliwa,
Steven.
“Nakuamini sana, unaweza kufanya unachokisema, cha msingi
jitume zaidi, funga magoli uwezavyo” Steven alimwambia
Filbert.
Filbert bado alikuwa na furaha isiyo kifani moyoni mwake,
ndoto ambayo alikuwa ameipanga itokee katika maisha yake ilikuwa ikielekea
kutimia na ni juhudi binafsi tu ndizo ambazo zilikuwa zikihitajika katika
kipindi hicho. Moyo wake uliamini kwamba maisha yake yalikuwa ni mpira, aliamini
mambo mengi katika maisha yake yangeweza kutimia endapo angeweza kufanikiwa kuwa
mchezaji mkubwa wa kulipwa. Kwa sababu alikuwa amekataa kufanya mapenzi na
msichana Amanda, alitaka kuhakikisha kwamba anachaguliwa kujiunga na timu yoyote
ile ili aone kwamba kulikuwa na maana kubwa sana kukataa kufanya mapenzi na
Amanda, msichana aliyekuwa akimpenda sana.
Ulikuwa
ni mwezi wa kumi na mbili, kipindi ambacho kilikuwa na baridi kali katikanchi
nyingi barani Ulaya. Theluji zilikuwa zimemwagika ardhini, magari ambayo
yalikuwa maalumu kwa ajili ya kusafisha barabara kwa kuondoa theluji ambazo
zilikuwa zimefunika ardhi yalikuwa yakifanya kazi yake kama kawaida katika kutoa
theluji zote ili barabara zionekane na hivyo magari yaweze kupita kama
kawaida.
Katika kipindi hicho ndicho ambacho ndege ya shirika la Fly
Emirates ilikuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Brussels uliokuwa
ndani ya jiji la Brussel. Hali ya hewa bado ilikuwa ni ya ubaridi mkali katika
kipindi hicho, wafanyakazi wengi wa hapo uwanja wa ndege walikuwa wamevaa makoti
mazito huku wakiendelea kufanya kazi zao kama kawaida.
Ukungu mzito
ulikuwa umetawala katika sehemu kubwa ya jiji la Brussel, theluji ambazo
zilikuwa zimedondoka kwa wingi zilikuwa zikionekana kukusanywa sehemu moja. Lami
ndani ya uwanja huo wa ndege ilikuwa ikionekana vizuri japokuwa napo bado
theluiji ilikuwa ikiendelea kudondoka kutoka angani.
Wachezaji wa
mpira wa timu ya taifa ya vijana walikuwa ndani ya ndege. Kila mmoja alikuwa
amekabidhiwa koti zito kutokana na kujulikana kwamba mwezi wa kumi na mbili bara
zima la Ulaya huwa katika kipindi cha baridi kali. Kila mmoja akaonekana
kuhofia, hasa Filbert pamoja na baadhi ya wachezaji ambao walikuwa wametoka
katika jiji la Dar es Salaam.
“Mmmh!” Filbert alisikika akiguna huku
macho yake yakiangalia nje kupitia dirishani.
“Hii kweli balaa” Steven
alimwambia Filbert.
“Yaani bora ningekuwa nimeishi Arusha, Mbeya au
hata Iringa. Kweli mpira utachezeka kaka?” Filbert alimuuliza
Steven.
“Hali itakuwa ni ya hatari sana. Hewa itakuwa nzito sana”
Steven alimwambia Filbert.
Kila mchezaji kwa wakati huo alikuwa
akiangalia nje, hali ya hewa ikaonekana kuwaogopesha kupita kawaida. Walikuwa
wametoka katika moja ya nchi iliyokuwa na joto kali na sasa walikuwa wameingia
katika nchi nyingine kabisa, nchi ambayo ilikuwa na baridi kali. Hali ile ya
hewa ikaonekana kuwa kikwazo katika kuonyesha uwezo wao uwanjani kutokana na
hali hiyo kusababisha hewa kuwa nzito hasa pale unapokuwa
uwanjani.
Ndge iliposimama, ngazi zikateremshwa na kisha abiria kuanza
kuteremka. Kila mmoja alikuwa na koti zito ambalo lilikuwa juu ya maswata yao
ambayo walikuwa wameyavaa. Japokuwa walikuwa na nguo hizo mwilini lakini bado
walikuwa wakisikia baridi kali ambalo liliwafanya kutetemeka kila
wakati.
Mizigo ikachukuliwa na wao kuruhusiwa kuondoka kuelekea ndani
ya jengo la uwanja wa ndege. Walikuwa wakitembea kwa haraka haraka, theluji bado
ilikuwa ikiendelea kudondoka jambo ambalo wakati mwingine lilionekana kuwa kama
karaha miilini mwao huku wakiona kama walikuwa wakiongezewa baridi zaidi na
zaidi.
Kila hatua ambayo walitakiwa kupitia ndani ya uwanja huo
wakaipitia na kisha kuanza kuondoka kuelekea nje ya uwanja huo ambapo wakakuta
basi kubwa likiwa linawasubiria na kisha kuanza kuwapeleka katika hoteli moja
kubwa ya Sheraton ambayo ilikuwa katikati ya jiji hilo la
Brussel.
Kila chumba walitakiwa kulala watu wawili, kwa sababu Filbert
na Steven walikuwa marafiki wa karibu sana, wakakaa katika chumba kimoja. Kila
mmoja ndani ya chumba kile alikuwa akifurahia, maisha kwao yakaonekana kuanza
kubadilika, uwepo wao ndani ya hoteli ile uliwafanya kuanza kufikiria maisha
mengine kabisa.
Hiyo ndio ilikuwa ni mara ya kwanza kukaa ndani ya
chumba ambacho kilikuwa kizuri namna ile, walikuwa wakikishangaa kila kitu
ambacho walikuwa wakikitazama. Kitanda kilikuwa kikubwa tena cha duara ambacho
kilikuwa na swichi ambayo mara unapobonyeza tu basi kitanda kile kilianza
kuzunguka.
“Mmmh! Hiki kitanda noma Steven. Unaweza kulala huku ukiwa
umeelekea Magharibi, unaamka ukiwa umeelekea Mashariki” Filbert alimwambia
Steven.
“Kizuri sana. Unaweza kuamka asubuhi na ukaanza kujisikia
kizunguzungu” Steven alimwambia Filbert.
Hiyo kwao ikaonekana kuwa
kama nyota njema ambayo ilionekana mapema sana. Chumba kile kikaonekana
kuwatabiria maisha yao ya baadae kwamba walitakiwa kupanga chumba kama kile kwa
kutumia fedha zao na si fedha za mtu mwingine. Kila mmoja akaanza kuiona ndoto
yake ikianza kutimia, muonekano wa chumba kile na nchi ile kwa ujumla
viliwafanya kujisikia vizuri.
Siku hiyo wakabaki katika vyumba vyao.
Usiku hawakulala, kwa sababu chumba chao kilikuwa ghorofani, wakafungua dirisha
na kisha kuanza kuangalia mazingira ya jiji la Brussels. Ghorofa zilikuwa nyingi
zilizopendezeshwa na taa za kila aina, walikuwa wakifarijika sana kuangalia
mazingira hayo japokuwa kulikuwa na baridi kali sana wakati huo.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ndoto zao za kufika
Ulaya zikawa zimetimia na ilikuwa imebakia ndoto moja tu, kuishi ndani ya bara
hilo katika kipindi chote cha maisha yao. Hiyo ndio ndoto pekee ambayo ilikuwa
imebakiwa, walimshukuru Mungu kwa kuwawezesha kufika ndani ya bara hilo lakini
walijiona kuwa na shukrani zaidi endapo wangefanikiwa kukaa ndani ya bara hilo
zaidi na zaidi.
Asubuhi ya siku iliyofuata wakaanza kutembea sehemu
mbalimbali kama kulizoea jiji la Brussels. Barabarani kulikuwa na wazungu wengi
lakini nao watu weusi walikuwa katika idadi kubwa japokuwa haikuwa kama idadi ya
wazungu. Watu weusi waliokuwa wakionekana katika mitaa mingi ndani ya jiji hilo
walikuwa ni Wakongo ambao walitoroka kwao na kuzamia nchi hiyo au hata
kupokelewa kutokana na nchi ya Kongo kuwa na mapigano ya mara kwa
mara.
Ukiachana na wakongo, pia kulikuwa na watu wa Rwanda pamoja na
Burundi bia kuwasahau wasomali ambao kila siku walikuwa wakizidi kumiminika
ndani ya nchi hiyo. Kwa waafrika, nchi ya Ubelgiji ikaonekana kuwa kama nchi
yao, walikuwa wakijikusanya kwa wingi kila siku. Matembezi hayo yaliendelea
zaidi na zaidi mpaka pale walipoamua kurudi saa sita mchana, muda wote huo wala
jua halikuwa likionekana zaidi ya mawingu mazito ambayo yalikuwa yametanda
angani.
“Hii nchi nzuri sana. Nzuri sana, kumbe ukisikia Muafrika kaja
kuzamia wala hautakiwi kumlalamikia” Filbert alimwambia Steven huku wakiwa
wamekwisharudi ndani ya chumba chao.
“Hivi hatuwezi kubaki
huku?”
“Kubaki tunaweza, ila tufanye juhudi katika kucheza mpira”
Filbert alimwambia Steven.
“Simaanishi kubaki kihalali, nataka tubaki
kizurumishi” Steven alimwambia Filbert.
“Unamaanisha
tuzamie?”
“Ndio”
“Mchezo mbaya sana huo. Tunaweza
tusifanikiwe”
“Kivipi?”
“Kucheza mpira”
“Kwani si
tunakimbia kuelekea mitaani”
“Sawa. Una passport na
viza?”
“Hapana”
“Sasa unafikiri utaweza kupata kazi kihalali
huku?”
“Daah! Yaani hapa nafikiri kama tukirudi, yaani kweli tukanyage
Ulaya halafu turudi ndani ya jiji la Dar es Salaam, kweli haki hii Filbert?”
Steven alimwambia Filbert na kumuuliza.
“Haina jinsi. Hivi wamesema
mazoezi tunaanza kufanya lini?”
“Niliwasikia wakisema
kesho”
“Wapi?”
“Sijui. Ila kama napo niliwasikia kwenye
uwanja wa chuo”
“Chuo gani?”
“Mmmh! Wala sikijui” Steven
alimwambia Filbert.
Université Libre de Bruxelles,Hiki kilikuwa ni
moja ya vyuo vikubwa sana nchini Ubelgiji ambacho kilikuwa kikipatikana ndani ya
jiji la Brussels. Chuo hiki kilikuwa kaskazini mwa jiji la Brussels na kilikuwa
kikichukua wanachuo wengi kutoka katika nchi mbalimbali duniani. Chuo hiki
kilikuwa kikubwa na ni lugha mbili ndizo ambazo zilikuwa zikitumika ndani ya
chuo hicho, Kifaransa ambayo ilikuwa ni lugha ya taifa ya nchi hiyo pamoja na
Kiholanzi.
Watu wengi wa hapo Ubelgiji hawakuwa wakifahamu lugha ya
Kingereza, lugha yao kubwa ilikuwa ni kifaransa na hiyo ilikuwa moja ya sababu
ambazo ziliwapelekea wakongo wengi kuingia ndani ya nchi hiyo. Kutokana na
ukubwa huo, chuo hicho kilikuwa na wanachuo elfu thelathini na mbili na mia tano
ambao walikuwa wakisoma chuoni hapo kila mwaka.
Kilikuwa ni moja ya
vyuo ambavyo vilikuwa vikiwafanya wanachuo kuwa bize sana na masomo, kila wakati
wanachuo walikuwa wakikaa kimakundi kwa ajili ya kujisomea huku muda mwingi
wakionekana kuwa bize kupita kawaida. Pamoja na kutoa elimu bora ndani ya chuo
hicho, pia chuo hiki kilikuwa kikitoa wanamichezo bora ambao walikuwa wakicheza
michezo mbalimbali kama soka, kikapu, raga na michezo mingine
mingi.
Chuo hicho kilikuwa chuo pekee kati ya vyuo themanini na tano
ambavyo vilikuwa vikipatikana ndani ya nchi hiyo ambayo ilikuwa na timu ya soka
ambayo ilikuwa ikiendelea kushiriki ligi daraja la kwanza nchini humo. Timu hiyo
ilikuwa ikiundwa na wachezaji waliokuwa wamechanganyika, kulikuwa na wachezaji
kutoka chuoni hapo pamoja na wachezaji kutoka mitaani ambao walikuwa na malengo
ya muda mrefu kuchezea katika timu hiyo.
Uwanja wa chuoni hapo ndio
ambao ulikuwa ukitumika katika mazoezi ya timu yao ambayo walikuwa wameipa jina
la Westerlo.Timu hiyo ya chuo ilionekana kuwa na kocha mzuri lakini kila siku
ilikuwa na tatizo moja tu, wachezaji wake hawakuwa na uwezo mkubwa. Kocha pamoja
na viongozi wa chuo hicho walikuwa wakijitahidi sana kuisukuma timu hiyo iweze
kusonga mbele lakini bado haikuonekana kusogea hata kidogo, bado ilionekana kuwa
nyonge sana kwa timu nyingine.
Mishahara ambayo walikuwa wakilipa kwa
wachezaji ilikuwa midogo mno na hiyo ndio ilikuwa sababu ambayo iliwafanya
wachezaji kutokujituma sana jambo lililopelekea wachezaji wengi kutimuliwa na
timu kudorora zaidi.
Katika kipindi ambacho timu ya vijana wa Tanzani
walipokuwa wameingia ndani ya nchi hiyo, timu hiyo ilikuwa ikishika nafasi ya
kumi na sita kati ya na timu kumi na nane ambazo zilikuwa zikishiriki ligi
daraja la kwanza. Hiyo ilionekana kuwa nafasi mbaya kwao, ilionyesha dhahiri
kwamba kama kusingekuwa na wachezaji wenye uwezo kuongezeka basi timu hiyo
ingeshuka, ingeshuka na kushuka mpaka kusahaulika katika ramani ya soka nchini
Ubelgiji.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Saa sita na nusu
mchana basi la wachezaji wa kitanzania lilikuwa likisimama ndani ya eneo la
uwanja huo kutokea hotelini ambapo walikuwa wamefika mahali hapo kwa ajili ya
kuchukua mazoezi ambayo yangefanyika kwa muda wa wiki mbili hata kabla ya kurudi
nchini Tanzania. Katika kipindi ambacho wachezaji walikuwa wakiteremka kutoka
katika basi lile, wanachuo walikuwa wamesimama wakiwaangalia, vijana wale
walionekana kuhisi baridi kali miilini mwao japokuwa walikuwa wamevaa makoti
makubwa.
Uwanja mzuri wa mpira wa miguu ulikuwa ukionekana machoni
mwao. Kila mmoja akaanza kutabasamu, nyasi za uwanja ule zilikuwa zikivutia,
uwanja ulikuwa umenyooka tofauti na viwanja ambavyo walikuwa wakivitumia nchini
Tanzania. Kila mmoja akashikwa na kiu ya kutaka kucheza juu ya uwanja mzuri
namna ile, wakaambiwa wajiandae huku viongozi wakipelekwa ofisini kwa ajili ya
kwenda kutoa taarifa kwamba walikuwa wamekwishafika mahali
hapo.
Wanachuo wakaanza kukusanyika, kitendo cha kuwaona vijana wale
wakijiandaa kuvaa kwa ajili ya kuanza mazoezi kilikuwa kikiwavutia. Watu wengi
chuoni hapo walikuwa wakipenda sana kuangalia mpira na ndio maana walipowaona
wachezaji wale wakijiandaa, wakakaa katika sehemu za mashabiki kwa ajili ya
kuwaangalia vijana wale.
“Hii ndio nafasi yetu” Steven alimwambia
Filbert.
“Hapa ndipo pa kuonyesha uwezo. Nikifanikiwa, kurudi Tanzania
itakuwa kipindi cha likizo na mecho za taifa tu” Filbert alimwambia
Steven.
“Mimi nikichaguliwa kujiunga na timu mojawapo, Tanzania
sirudi, nitachukua uraia wa huku huku” Steven alimwambia Filbert.
Hiyo
ndio ilikuwa siku ya kwanza kwa timu hiyo kuanza kufanya mazoezi ndani ya uwanja
huo. Kila siku watu walikuwa wakijazana kuwaaangalia vijana hao ambao
walionekana kuwa na uwezo wa juu katika kucheza mpira wa miguu. Kadri siku
zilivyokuwa zikizidi kusonga mbele na ndivyo ambavyo watazamaji walivyokuwa
wakiendelea kumiminika ndani ya uwanja huo kwa ajili ya kuangalia mazoezi ya
timu hiyo.
Baada ya wiki moja na nusu kupita huku wakiwa wamefanya
mazoezi ya kutosha hapo ndipo ambapo timu mbalimbali zikaanza kuomba mechi
kucheza na timu hiyo ya vijana kutoka nchini Tanzania. Uwezo ulikuwepo, vijana
wenye uwezo walikuwepo nchini tanzania japokuwa vipaji vyao vilikuwa vimefichwa
porini.
Wachezaji wakajitoa, waliokuwa mabeki wakazuia vya kutosha,
kipa akadaka kupita kawaida huku Filbert akifunga magoli zaidi ya manne katika
kila mechi ambayo walikuwa wakicheza chuoni hapo.
“Ces cing personnes
deveraient se joindre à notre êquipe cette fenêtre transifer(Vijana wale watano
wanatakiwa kujiunga na timu yetu katika kipindi cha usajiri)” Proffesa wa chuo
alisikika akimwambia rais wa chuo huku akimnyooshea kidole Filbert, Steven,
Godwin, Idrissa na Khatibu.
Kwa jinsi wachezaji
walivyokuwa wakifanya mazoezi walionekana kuwa fiti kupita kawaida, uwezo wao
ulikuwa ukionekana dhahiri jambo ambalo liliwafanya maprofesa waliokuwa ndani ya
chuo kile ambao walikuwa wakiangalia mazoezi yale kuvutiwa na baadhi ya vijana.
Kila mwanachuo ambaye alipata bahati ya kuyaangalia mazoezi yale alionekana
kukubali kwamba hapa duniani kulikuwa na watu ambao walikuwa na uwezo mkubwa wa
kucheza mpira.
Uwezo wa wachezaji wale ukawa gumzo chuoni hapo, kila
mtu ambaye alikuwa akisikia kuhusu timu hiyo akatamani kwenda kuiangalia jinsi
ilivyokuwa ikifanya mazoezi. Kila siku watu walikuwa wakizidi kuongezeka katika
uwanja huo, mazoezi ya wachezaji hao yalionekana kumvutia kila aliyekuwa
akiyaangalia.
Sifa zao zikaanza kutapakaa katika sehemu mbalimbali
nchini Ubelgiji, wanachuo wengine walikuwa wakiwapiga picha na kisha kuziweka
katika mitandao mbalimbali ya kijamii na kuwamwagia sifa nyingi kitu ambacho
kilipelekea hata wale ambao hawakuwa wamepata taarifa kuhusiana na uwepo wa timu
hiyo kuelekea huko kuyaangalia mazoezi hayo.
Viongozi wa timu nyingine
hawakubaki nyuma, nao walikuja katika uwanja huo wa chuo kwa ajili ya kuangalia
jinsi vijana wale walivyokuwa wakifanya mazoezi. Kila aliyekuwa akiwaangalia
alikuwa akikubaliana na sifa hizo jambo ambalo kila mtu akataka vijana hao
wajiunge na timu zao.
Uwezo ule ambao walikuwa wakiuonyesha ndio ambao
uliwafanya maskauti wa timu kubwa nchini Ubelgiji kutaka kucheza mechi pamoja na
vijana wale. Maombi yao yalipokubaliwa, wakaziandaa timu zao za vijana ambazo
zote hizo zilifungwa katika michezo yote waliyokuwa wamecheza.
Hilo
ndilo ambalo liliwatangaza zaidi, uwepo wao ukazidi kutangazwa ndani ya nchi ya
Ubelgiji, watu wengi waliokuwa wakipenda mpira wa miguu walikuwa wakizidi
kumiminika katika uwanja huo wa chuo kwa ajili ya kuwaangalia vijana hao huku
kila mmoja akiwaona kuwa nyota wa miaka ya baadae endapo wangeendelea kufanya
mazoezi zaidi na zaidi.
Baada ya wiki ya kwanza kukatika, mtafaruku
ukaanza kutokea. Katika siku ya kwanza ambayo Professa wa chuo hicho alipowaona
vijana wale wakichukua mazoezi aliwasifia lakini hakuchukua hatua yoyote ile
japokuwa alikuwa amewachagua kwa kuwaonyeshea vidole wachezaji watano ambao
walionekana kuwa mwiba mkali. Ni kweli alikuwa amepanga kuwasajili katika timu
yake wa Westerlo lakini mambo yake alikuwa akiyaendesha kwa taratibu
sana.
Katika ambacho maskauti kutoka timu nyingine walipokuja mahali
hapo, hawakutaka kuchelewa, kwa sababu walikuwa na uhitaji mkubwa wa wachezaji
waliokuwa na uwezo, wakaanza kuongea na viongozi wa timu ya taifa. Hapo ndipo
ambapo professa alipoona kwamba alikuwa amekosea sana, aliona kwamba tayari
alifanya kosa kubwa kujifanya yupo bize na wakati alikuwa amekwishawaona vijana
ambao walikuwa na uwezo mkubwa uwanjani.
Viongozi wa timu tatu ambazo
zilikuwa zikishiriki ligi kuu ya Ubelgiji iliyojulikana kama Jupiler League,
Genk, Standard Liege na Anderlecht tayari walikuwa wamekwishafika mahali hapo na
kitu ambacho walikifanya ni kuanza mazungumzo ya kuongea na viongozi wa timu ya
taifa ya Tanzania ili kujua ni kipi kifanyike na baadhi ya wachezaji waweze
kubaki nchini hapo kwa kujiunga na timu zao.
Vijana hao hawakuwa na
mawakala, hilo likaonekana kuwa kama kipingamizi lakini kwa sababu kila kitu
kilikuwa kwenye mipango, viongozi wakaambiwa kwamba ilitakiwa wachukue nafasi
kama mawakala wa muda wa wachezaji hao kabla ya wao wenyewe kuamua ni nani na
nani kuwa mawakala wao wa muda mrefu katika maisha yao ya
soka.
“Hakuna tatizo” Kocha msaidizi aliwaambia.
Hapo ndipo
kazi ilipoanza. Kwa haraka bila kupoteza muda mikataba ikaandaliwa, hakukuwa na
suala la kupelekwa kufanyiwa majaribio, uwezo ambao wachezaji hao waliouonyesha
mahali hapo ilitosha kabisa kuwaambia kwamba ni kwa kiasi gani walikuwa wameiva
katika mchezo wa soka japokuwa walikuwa na umri mdogo.
Mara baada ya
wachezaji nane kuchaguliwa, wakapelekwa katika chumba maalumu ambapo huko
wakawekwa kikao na kuambiwa kila kilichokuwa kikiendelea mahali hapo. Kwanza
hakukuwa na mtu ambaye aliamini kile ambacho alikuwa amekisikia, kuchaguliwa na
kujiunga na timu za hapo Ubelgiji ilionekana kuwa kama ndoto ya kila mtu mahali
hapo.
Filbert akatamani kusimama na kuruka ruka, hakuamini kwamba
safari ambayo iliwatoa nchini Tanzania na kuwapeleka nchini Ubelgiji ndio ambayo
ingewafanya kukamilisha kila ndoto ambayo walikuwa wamejiwekea maishani mwao.
Baada ya kupewa darasa dogo na viongozi wao, moja kwa moja maskauti wa timu hizo
tatu zinazoshiriki ligi kuu ya hapo Ubelgiji wakaingia, wanaanza kuongea huku
kukiwa na mkalimani pembeni.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Skauti wa timu hizo
wakawachagua wachezaji wao na Filbert kujikuta akiangukia katika mikono ya timu
ambayo ilikuwa ikiongoza ligi katika kipindi hicho, timu ya Genk huku rafiki
yake, Steven akienda kujiunga na timu ya Anderlecht.
Kwa wakati huo
hakukuwa na muda wa kupoteza, kila kitu kilitakiwa kufanyika kwa haraka sana.
Mchezo wa kuibiana wachezaji ulikuwa mkubwa sana barani Ulaya na ndio maana
ilitakiwa kufanya mambo haraka haraka katika kuhakikisha kwamba wachezaji hao
wanasaini mikataba.
Kwa kuwa walikuwa chini ya miaka kumi na nane na
pia walikuwa kama wachezaji huru, sheria ya soka ya shirikisho la soka la Ulaya,
UEFA ikawaruhusu kujiunga na timu hizo huku wakiwa na mawakala wao wa muda
mfupi.
“Unataka nani awe wakala wako?” Kocha mkuu, Zakayo alimuuliza
Filbert.
“Kaka yangu, Dennis” Filbert alijibu na kocha yule
kuandika.
Kila mmoja akamtaja wakala wake ambaye alitakiwa kusimamia
mikataba yao yote kuhusiana na soka pamoja na matangazo ya biashara endapo
yangetokea katika maisha yao ya soka. Kwa sababu professa wa chuo hicho alikuwa
amechelewa kutokana na uzembe wake mwenyewe, akaziomba timu hizo kubaki na
wachezaji watatu kwa mkopo ili kuiwezesha timu yao kupanda daraja na kisha
kuwaruhusu kuondoka kuelekea katika timu zao hizo mara ligi
itakapomalizika.
Hilo halikuonekana kuwa tatizo kabisa, kwa sababu
bado wachezaji wale walikuwa wachanga, walionekana kuwa na uhitaji wa kukomaa
katika ligi ndogo hata kabla ya kuja katika ligi kuu. Siku hiyo hiyo mikataba
ikasainiwa na Filbert kuahidiwa kulipwa paundi elfu tano kwa wiki, kiasi ambacho
kilikuwa ni sawa na milioni kumi na mbili na laki tano kwa fedha za kitanzania,
hicho kilikuwa ni kiwango cha chini kabisa.
Hapo ndipo ambapo maisha
yao yalipotakiwa kuwepo. Kila mmoja alionekana kuwa na bahati na kwa wale ambao
hawakuwa wamechaguliwa wakaonekana kuumia sana mioyoni mwao. Baada ya wiki moja,
nauli pamoja na vibali vikaandaliwa na kisha mawakala wote ambao waliteuliwa
kuwasimamia ndugu zao wakawa wamekwishafika nchini Ubelgiji, Dennis, kaka yake
Filbert akiwa mmoja wapo.
“Daaah!” Dennis alisema mara baada ya
kumuona mdogo wake, Filbert, alionekana kutokuamini.
“Vipi tena?”
Filbert alimuuliza.
“Una bahati sana. Aiseee, yaani kuja huku tu ndio
imekuwa moja kwa moja” Dennis alimwambia Filbert.
“Nilimwambia baba
kwamba hii ndio ilikuwa ndoto yangu, uwezo wangu wa kucheza mpira haukutakiwa
kuishia Tanzania” Filbert alimwambia Dennis.
“Safi sana dogo. Siamini
kama na mimi nimekuja Ulaya” Dennis alimwambia Filbert.
“Ndio hivyo.
Nimeamua kukuchagua wewe kuwa wakala wangu kwa sababu ninataka familia nzima iwe
na fedha, yaani fedha zizunguke kwenye familia yetu” Filbert alimwambia kaka
yake, Dennis.
“Nimefurahi sana”
“Na baba alisemaje mara
baada ya kupata taarifa?”
“Hahaha! Mzee wa watu angekufa kwa presha
aiseee”
“Ilikuwaje?”
“Sijui niseme nini ila angekufa kwa
presha, alishtuka sana” Dennis alimwambia Filbert.
“Watanzania wamejua
kila kilichoendelea huku?”
“Hiyo ndio imekuwa gumzo ya jiji sasa hivi,
kila kona mnazungumziwa nyie, ila wadau wengi wameonya msije kukubali
kubadilisha uraia, nchi bado inawahitaji” Dennis alimwambia
Filbert.
“Siwezi kubadilisha uraia, ninaipenda sana nchi yangu”
Filbert alimwambia Dennis.
Siku hiyo walikaa hotelini huku wakiongea
mengi, Filbert bado alijiona kuwa kwenye ndoto moja yenye kutia faraja kuliko
ndoto zote maishani mwake ambapo baada ya muda angeshtuka kutoka katika usingizi
mzito na kujikuta yupo Kijitonyama. Safari yake ya mafanikio akaiona kuanzia
nchini Ubelgiji.
“Kwa hiyo utacheza hapa maisha yote?” Dennis
alimuuliza Filbert.
“Haiwezekani. Nitatamani siku moja niende kucheza
soka Uingereza” Filbert alimwambia Dennis.
“Hahaha! Kumbe una akili
sana”
“Najua. Kule ndio pa kujitangaza zaidi. Huku porini sana”
Filbert alimwambia Dennis.
Siku ya kwanza ikapita. Baada ya wiki moja
ya mapumziko Filbert akaanza kufanya mazoezi na timu ya soka ya Westerlo ambayo
alikuwa ametolewa kwa mkopo kutoka katika timu mpya iliyomnunua ya Genk. Muda
mwingi Filbert alionekana kuwa na furaha, kitendo cha kuanza kucheza soka la
Ulaya kilimpa faraja sana, yaani kila kilichokuwa kikiendelea hakikuwa
kikiaminika kabisa.
Maskauti wa Genk hawakuwaacha wachezaji wao peke
yao, walikuwa wakiwafuatilia kwa ukaribu sana. Katika kila mechi ambayo Westerlo
walipokuwa wakicheza, maskauti hao walihakikisha wapo uwanjani kwa ajili ya
kuwaangalia wachezaji wao wawili, Filbert na Idrissa ambao walikuwa wametolewa
kwa mkopo.
Uwezo wa Filbert ulionekana kuwa mkubwa sana ambao
ulimshangaza kila mtu. Filbert alikuwa akilijua sana goli, alikuwa akijua sana
kufunga kitu ambacho ndani ya mechi tano za kwanza akawa amefunga magoli sita
jambo ambalo liliwaonyeshea maskauti wa Genk kwamba chaguo lao halikuwa baya,
lilikuwa chaguo sahihi huku wakiona kwamba Filbert angekuwa mchezaji tishio
katika siku za usoni.
Japokuwa katika kipindi hicho alijiona kupata
nusu ya kitu alichokuwa akikihitaji hakuweza kumsahau msichana wake, Amanda.
Mara kwa mara alikuwa akiwasiliana nae kwa njia ya simu au hata kuwasiliana kwa
njia ya mitandao ya kijamii. Kila siku Filebrti alionekana kuwa na furaha, kila
kilichokuwa kikiendelea hakikuweza kuaminika katika macho
yake.
“Ninataka kuendelea na masomo Amanda” Filbert alimwambia
Amanda.
“Kwa hiyo unataka kurudi Tanzania?”
“Hapana.
Ninataka kusoma huku huku”
“Lengo la kusoma ni nini na wakati una
fedha na utakuwa tajiri mkubwa?” Amanda alimuuliza Filbert, katika kipindi hicho
walikuwa wakiongea katika mtandao wa Skype.
“Nina ndoto moja kubwa
maishani mwangu” Filbert alimwambia Amanda.
“Ndoto gani?”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kuwa rais wa
Tanzania. Hilo tu” Filbert alimwambia Amanda.
“Unataka kuwa
rais?”
“Ndio. Miaka ijayo. Ninataka kuwa rais” Filbert alimwambia
Amanda.
“Sawa. Kwa hiyo unataka kuanza shule lini?”
“Wiki
ijayo”
“Kwa hiyo utakuwa ukisoma na kucheza mpira?”
“Hiyo
ndio maana yangu” Filbert alijibu.
Hivyo ndivyo Filbert alivyokuwa
amepanga, kitu ambacho alikuwa akikitaka katika wakati huo ni kuingia darasani
na kuendelea kusoma. Ndoto yake ambayo aliona iimebakia ilikuwa ni kuwa rais wa
nchi ya Tanzania. Alipomfikishia wazo lake kaka yake, Dennis, wala hakupinga,
kwa moyo mmoja akakubaliana nae na hata uongozi wa timu ya Weserlo na Genk nao
wakakubaliana nae na hivyo moja kwa moja kuanza masomo yake katika shule ya St’
Phillip, shule iliyokuwa pembeni kidogo mwa jiji la Brussels.
Maisha
ya Ubelgiji yalikuwa mazuri, wachezaji walikuwa huru sana na baada ya miezi
miwili Filbert akapangiwa nyumba ndani ya jiji la Westerlo, nyumba ambayo
angekuwa akikatwa mshahara wake na mwisho wa siku nyumba hiyo kuwa yake. Kiasi
cha fedha ambacho alikuwa akilipwa kilikuwa kikubwa sana, japokuwa milioni mbili
kwa fedha za kitanzania zilikuwa zikitumika kulipia kodi lakini milioni kumi
bado zilionekana kuwa nyingi.
Akafanikiwa kununua gari huku akiendelea
kuishi na kaka yake ambaye alikuwa kila kitu nchini Ubelgiji. Mazoezi
hayakuonekana kuwa rahisi kwake, kila siku alikuwa akiacha usingizi, baridi kali
na kisha kuelekea mazoezini na mchana kuelekea shuleni kabla ya kwenda mazoezini
kwa mara nyingine jioni. Hali hiyo ilionekana kumuumiza sana lakini hakuwa na
jinsi, ili kufikia malengo yako na mafaniko makubwa basi haina budi kupigana
sana katika kipindi kigumu.
“Excusez-moi (Samahani)” Msichana mmoja
alimwambia Filbert katika kipindi ambacho alikuwa supermarket, alipogeuka na
kumwangalia msichana huyo, alikuwa msicha mrembo, msichana aliyekuwa na
mchanganyiko wa rangi, bila shaka baba yake alikuwa Mzungu na mama yake
Msomali.
“Mmmh!” Dennis ambaye alikuwa pembeni mwa Filbert alitoa
mguno, msichana aliyekuwa amemuongelesha Filbert alionekana kuwa kama
malaika.
“Can you speak English? (Unaweza kuongea Kingereza)” Filbert
alimuuliza msichana yule ambaye alikuwa ameongea lugha ya
Kifaransa.
“Yes. I can speak English (Ndio. Naweza kuongea Kingereza)”
Msichana yule alimwambia Filbert huku akionekana kuwa na
furaha.
Filbert akabaki kimya kwa muda, kila alipokuwa akimwangalia
msichana yule moyo wake ulikuwa ukijisikia hali ya tofauti sana, hali ambayo
aliwahi kuisikia mara moja tu tena katika kipindi ambacho alikutana na Amanda
katika jengo la Mlimani City. Kila alipokuwa akizidi kumwangalia msichana yule,
alikuwa akimfananisha na muigizaji wa filamu za utupu Marekani, Skin diamond
kutokana na urembo aliokuwa nao.
Je nini
kitaendelea?
Je msichana huyo ni nani?
Je Filbert ataweza
kufanikisha ndoto yake ya kuwa
rais?
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment