Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

AM SORRY - 5

 





    Simulizi : Am Sorry

    Sehemu Ya Tano (5)



    ILIPOISHIA

    Japokuwa hakutaka kuonyesha chochote kile, lakini ukweli ni kwamba alitokea kumpenda kijana huyo , hasa kipaji chake cha uchoraji ndicho kilichomdatisha zaidi . ENDELEA .. .

    Nusrat alikuwa msichana mrembo aliyevutia kwa kila kitu, macho yake malegevu, umbo lake la kimisi na hipsi zilizojaa vilizidi kuongeza uzuri wa muonekano wake huku akiwa ndiyo kwanza ana miaka ishirini .

    Japokuwa alipewa siku maalum kufika mahali hapo kuchukua picha yake , kwake ilionekana kuwa ngumu kusubiri. Alitokea kumpenda mno Ibrahim na asingekuwa tayari kuendelea kusubiri kwani kila siku moyo wake ulikuwa kwenye mateso makali . Alichokifanya ni kuanza kuelekea kule alipokuwa akichorewa picha yake .

    Kila siku alipofika hapo, alikuwa mtu wa kupiga stori tu huku muda mwingi akitumia kukaa mikao ya hasarahasara ili aweze kumpagawisha Ibrahim . Kwa kijana huyo ilikuwa ni shida mno lakini akaamua kuvumilia kwani aliwajua wasichana vilivyo .

    “ Unajua sana kuchora, hivi ulijifundisha au kipaji ?” aliuliza Nusrat .

    “ Kipaji tu . Mungu aliniumba nikiwa hivi, ” alijibu Ibrahim.

    “ Hongera sana wangu, unajitahidi sana , ” alisema Nusrat .

    Kila siku akawa mtu wa kutoa pongezi tu kwa kijana huyo . Hakukuwa na siku ambayo hakwenda mahali hapo na kujifanya akiulizia picha.

    Alivumilia mno mpaka kikafika kipindi ambacho hakutaka kuendelea kuwa na uvumilivu , aliamua kuufungua mdomo wake na kumwambia ukweli jinsi alivyokuwa akijisikia , kwamba alimpenda mno na hakuwa akilala kwa ajili yake .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ibrahim alivyoambiwa, hakushtuka , alilitegemea hilo kwani dalili za mvua zilikwishaanza kuonekana kwa mawingu kutanda angani , hivyo akachukulia suala hilo kuwa kawaida sana .

    “ Umechelewa mno Nusrat , nina mtu tayari , ninampenda na ananipenda , ” alisema Ibrahim .

    “ Haiwezekani , sidhani kama nimechelewa Ibrahim. Nimetokea kukupenda, siwezi kukaa kimya kwani ninausababishia moyo wangu maumivu mazito , naomba uwe wangu , hata ukinifanya kuwa mtu wa pili, nitakuwa tayari kwa hilo lakini si kukukosa, ” alisema Nusrat huku akionekana kuwa na uhitaji wa kuwa na kijana huyo .

    Msimamo wa Ibrahim ulikuwa uleule kwamba hakutaka kuwa na binti huyo kwa kuwa tayari alikuwa na mpenzi wake aliyeahidiana naye mambo mengi , Latifa .Siku zikaendelea kukatika, Nusrat hakukoma, alijua kwamba alikataliwa lakini hakutaka kuchoka, kila siku alifika mahali hapo na kuendelea kumwambia kijana huyo maneno matamu kwa kuamini kwamba kuna siku moyo wake ungebadilika na kukubaliana naye.

    Alipoona kwamba Ibrahim anaendelea kuweka msisitizo kwamba alikuwa na mpenzi wake , hapo ndipo alipotumia njia nyingine ambayo aliamini angefanikiwa kwa urahisi mno, akaanza kutumia zawadi .

    Kila alipofika hapo , alikuwa na vitu mbalimbali ambavyo alimwambia kijana huyo kwamba vilikuwa ni zawadi kwake kutokana na kazi nzito aliyokuwa akiifanya kwa kumchorea picha yake.

    Siku za kwanza ilikuwa ngumu kukubaliana na msichana huyo lakini baada ya kulia sana huku akilalamika kwamba hakuwa akithaminiwa, Ibrahim akaamua kuzipokea zawadi hizo kama fulana, chokleti na hata wakati mwingine kuletewa fedha.

    Taratibu Nusrat akaanza kuyabadilisha maisha ya Ibrahim , kiasi kikubwa cha fedha alichokuwa akimpa, alikitumia katika kuyaendeleza maisha yake kwa kununua vitu vingi vya ndani na hata kulipia kodi ya chumba alichokuwa amepanga baada ya kuhama nyumbani.

    Kukataa kwake kuwa mpenzi wake , mwisho wa siku msichana huyo akasisitiza kwamba wawe marafiki wa kawaida ili kumtoa wasiwasi , Ibrahim akakubaliana naye pasipo kugundua kwamba hiyo ilikuwa moja ya njia aliyoitumia msichana huyo kumteka .

    Urafiki ulipokua , Nusrat akaanza kumuomba Ibrahim mitoko mbalimbali . Hilo wala halikuwa jambo gumu, kwa kuwa walikubaliana kwamba walikuwa ni marafiki tu , kijana huyo hakuwa na wasiwasi wowote ule.

    Kuwa karibu na Nusrat , kutoka na kwenda sehemu mbalimbali , kupokea zawadi zake na hata kuwa naye bize kwenye simu kuongea naye nyakati za usiku kukaanza kuubadilisha moyo wa Ibrahim . Taratibu akaanza kumsahau Latifa huku akiupa nguvu msemo usemao ‘Fimbo ya mbali haiui nyoka’ .

    Baada ya ukaribu wao kudumu miezi miwili, mambo yakabadilika , wakaanza kubusiana na mpaka kubadilishana mate kitu kilichoufanya moyo wa Ibrahim kuanza kumsahau kabisa Latifa, na miezi minne ilipokatika , akasahau kama alikuwa na msichana aliyeitwa kwa jina la Latifa, penzi la Nusrat likauteka moyo wake .



    Liban hakutaka kukata tamaa hata mara moja, alimpenda sana Latifa na hivyo asingeweza kukaa kimya na kuona msichana huyo akipita . Kila siku shauku yake kubwa ilikuwa ni kuzungumza naye lakini hakuweza kuipata nafasi hiyo .

    Latifa hakuwa msichana mwepesi, hakuwa kama wasichana wa Kizungu ambao ukiwaambia kwenda kula chakula cha usiku , basi hukubaliana nawe . Kwa Latifa, alitamani kuishi kama Mtanzania kwa kuamini kwamba lingekuwa jambo gumu kupatikana kwa kuwa alilelewa kama Mtanzania .

    “ Nampenda sana Latifa , ” alisema Liban.

    Ni kweli moyo wake ulichanganyikiwa mno, japokuwa alipata nafasi ya kusoma na msichana huyo darasa moja lakini hakuwahi kupata nafasi ya kuzungumza naye . Msichana huyo alionekana kuwa siriasi sana .

    Siku zikaendelea kukatika mpaka Liban aliposema kwamba imetosha , kama kuteseka aliteseka mno na katika kipindi hicho ulikuwa ni muda wa kumwambia ukweli tu , kama atakubali, awe mpenzi wake na kama atakataa , basi abaki na maumivu yake moyoni.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ Ninakupenda Latifa , ” alisema Liban kwa sauti ndogo aliyohakikisha kwamba aliitoa kimahaba.

    “ Najua, unafikiri nilikuwa sijui! Najua sana .”

    “ Nashukuru. Kwa hiyo inakuwaje ?”

    “ Kuhusu nini ?”

    “ Kuwa nami.”

    “ Haiwezekani .”

    “ Kwa nini?”

    “ Nina mpenzi wangu, nampenda, namjali na kumthamini, mbaya zaidi , siwezi hata kumsaliti, ” alisema Latifa .

    Hakuwa muongeaji sana , alipoona kwamba amemaliza kile alichokuwa amekizungumza na Liban, akasimama na kuondoka zake . Maneno yale ya Latifa yalikwenda na maumivu makali moyoni mwa Liban , hakuamini kama angeweza kuambiwa maneno yenye kuchoma kama yale .

    Alimwangalia Latifa alivyokuwa akiondoka, alionekana mrembo hasa lakini hakuwa na cha kufanya, kama kukataliwa , tayari alikuwa amekwishakataliwa, ikambidi awe mpole tu .

    Siku zikaendelea kukatika, japokuwa kwa upande wa Tanzania , Ibrahim aliamua kuanza uhusiano wa kimapenzi na msichana mwingine lakini kwa Latifa hakutaka kabisa kufanya hivyo , hakujua kilichokuwa kikiendelea, hakujua kwamba mwanaume yule aliyempa moyo wake na kumsisitizia kwamba alitakiwa kuwa nao makini tayari alianza kuwa na mwanamke mwingine.

    Alimpenda mno, hakuwa akikaa zaidi ya saa moja pasipo kumbukumbuka . Kila alipoziangalia picha za Ibrahim , aliuhisi moyo wake ukiwa kwenye uhitaji mkubwa wa kuwa naye. Hakutaka kujaribu kumsaliti . Kwa jinsi alivyokuwa akimpenda, alihisi kwamba alikuwa akionekana kila alipokuwa , yaani Ibrahim alikuwa akimfuatilia vilivyo .

    Darasani aliendelea kuongoza mpaka mwaka mzima unamalizika na matokeo kutoka , Latifa alikuwa amefanya vizuri kuliko wanafunzi wote shuleni hapo , matokeo yake yakawa ni ya alama za juu na kufunika alama zilizowekwa na genius Michael Rudzic , Mrusi aliyewahi kusoma shuleni hapo mwaka 1967 ambaye alishikilia rekodi ya kufaulu kwa alama nyingi.

    “ This is impossible , ” ( Hii haiwezekani) alisikika mwalimu mmoja mara baada ya kupata matokeo ya mitihani ile .

    “ She has the highest scores than what Rudzic got in 1967 , she has broken the Rudzic ’s record and make her own record , ” ( Ana alama za juu zaidi ya alizopata Rudzic mwaka 1967, amevunja rekodi ya Rudzic na kuweka rekodi yake mwenyewe , ) alisema mwalimu huyo huku akionekana kutokuamini , ikambidi avue miwani yake na kuyaangalia vizuri matokeo yale.

    Huo ndiyo ulikuwa ukweli , mara baada ya rekodi ya mwanaume genius kutoka nchini Urusi kudumu shuleni hapo kwa miaka mingi , hatimaye msichana kutoka Afrika, tena katika nchi iliyojiita Maskini , Tanzania alikuwa amefanya vizuri na kuvunja rekodi hiyo.

    Moto wake ulimuogopesha kila mtu , wanafunzi wengine wakaanza kumtolea macho kwa kuona kwamba msichana huyo alikuwa na akili za ziada. Mpaka shule zinafungwa nchini Marekani kwa kujiandaa na majira ya joto , tayari Latifa alijipatia umaarufu mkubwa shuleni hapo.

    “ Tunarudi Tanzania , ” alisema Dorcas .

    “ Asante Mungu! Sasa ni wakati wa kumuona tena mpenzi wangu , nilimkumbuka sana , Mungu, naomba moyo wa kumpenda mara mia zaidi ya nilivyokuwa nampenda kipindi cha nyuma , ” alisema Latifa huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana.Kwa wakati huo , aliuhisi moyo wake kuwa kwenye mapenzi makubwa zaidi ya kipindi kilichopita , alimpenda mno Ibrahim na hakuwa tayari kumpoteza ,



    Moyo wake ulijawa na upofu, hakujua kile kilichokuwa kikiendelea nchini Tanzania , mvulana aliyekuwa akimpenda na kumthamini, mvulana aliyempa thamani kubwa ya moyo wake , aliyemfanya kumkataa Liban , wakati huo alikuwa kwenye mapenzi ya dhati na msichana wa Kiarabu , Nusrat .
    SONGA NAYO …
    Latifa alikuwa mtu mwenye presha kubwa , kitendo cha kufika nchini Tanzania leo, kesho tu akaanza kumtafuta Ibrahim kwenye simu . Ilikuwa kazi kubwa kwani kila namba aliyokuwa akimpigia miongoni mwa zile alizokuwa nazo , hakuwa akipatikana .
    Ilimuumiza mno, alitaka kumuona mpenzi wake kwa kuamini kwamba kwa kipindi hiki alikuwa mzuri zaidi , yaani tofauti na jinsi alivyokuwa kipindi cha nyuma . Hakuacha , kila siku alikuwa akimpigia lakini matokeo yalikuwa yaleyale , hakupatikana.
    “ Au alibadilisha namba? Hapana , inawezekana amezima tu , ” aliwaza na kujijibu mwenyewe.
    Si kwamba hakupafahamu alipokuwa akiishi kijana huyo , alipafahamu lakini kitu cha kwanza alichokitaka ni kumfanyia ‘surprise ’ juu ya uwepo wake nchini Tanzania kwa kuamini kwamba angeshtuka mno.
    Baada ya kukaa kwa siku mbili pasipo simu yake kupatikana , hapo ndipo alipoamua kwenda nyumbani kwao , Manzese kwa ajili ya kumuulizia, kwani tayari alikwishahisi kuna jambo baya lilikuwa limetokea .
    “ Hayupo , alitoka na msichana mmoja hivi, demu wake , ” alisema msichana aliyemkuta katika nyumba hiyo ya kupanga .
    “ Unasemaje ?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “ Amegonganisha magari nini ?”
    “ Unamaanisha nini ?”
    “ Kwani wewe nani ?”
    “ Naitwa Latifa .”
    “ Basi siyo wewe , yule anaitwa Nusrat, ni mzuri kama ulivyo wewe japokuwa umemzidi kidogo tu , ” alisema msichana huyo .
    “ Sijakuelewa unamaanisha nini .”
    “ Kwani wewe ni nani kwake ?”
    “ Mpenzi wake .”
    “ Kwa hiyo ana mademu wawili !? Mmoja Muhindi na mmoja Mwarabu, kweli jamaa noma, ” alisema msichana yule .
    “ Bado anaishi hapa?”
    “ Hapana , alihama , kahamia Magomeni .
    Latifa hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo , akasimama na kuelekea ndani ya gari lake , hata kabla hajaliwasha, akauegemea usukani wa gari lile na kuanza kulia. Moyoni aliumia, hakuamini kile alichokuwa amekisikia kwamba mpenzi wake , aliyempenda , aliyetumia muda mwingi kwa ajili yake, leo hii alikuwa katika uhusiano na msichana mwingine .
    Alilia na kulia , muda wote alikuwa akijutia uamuzi wake wa kuwa na Ibrahim kiasi kwamba kuna wakati alijiona kuwa mtu mjinga asiyestahili kupenda wala kupendwa .
    “ Kwa hiyo ana mademu wawili !? Mmoja Muhindi na mmoja Mwarabu, kweli jamaa noma, ” maneno ya dada yule yakajirudia kichwani mwake na kumfanya kuumia zaidi .
    “ Haiwezekani , ” alisema Latifa na kuteremka garini.
    Akamfuata msichana yule na kumuomba amuelekeze alipokuwa amehamia , kwa kuwa hakuwa anapafahamu, akamuelekeza sehemu aliyokuwa akifanyia kazi yake ya kuchora, Latifa akarudi garini na kuanza kuelekea huko .
    Hakuwa makini barabarani, kichwa chake kilikuwa kimevurugika mno, mapenzi aliyoyapenda na kuyathamini , leo hii yalimfanya kubadilika na kuwa kama chizi . Alipofika karibu na Ubalozi wa Marekani , ilibakia kidogo tu agonge, bila utaalamu wa dereva mwenye gari ndogo, tayari angesababisha ajali .
    “ Mungu wangu ! Ni nini hiki?” alijiuliza huku akijishangaa .
    Aliendesha mpaka karibu na eneo ulipokuwa Ukumbi wa Maisha Klabu ambapo kulikuwa na wachoraji wengi wa picha za kubandikwa ukutani. Hakutaka kuteremka, alibaki garini akianza kuangalia huku na kule kuona kama angeweza kumuona Ibrahim .
    Wala hakuchukua muda mrefu , mtu aliyekuwa akitaka kumuona maeneo hayo , alifanikiwa kumuona , alikuwa amekaa chini huku akichora kama kawaida yake . Japokuwa aliambiwa maneno mengi , lakini akajikuta akifarijika , kwa mbali uso wake ukaanza kuwa na tabasamu pana.
    Maneno yote aliyoambiwa na msichana yule yakaanza kupotea na kumuona mtu mbaya ambaye hakutaka kuuona upendo wake na Ibrahim ukiendelea kama kawaida. Huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana, akaushika mlango kwa ajili ya kuteremka .
    Hata kabla hajafanya hivyo , mara akamuona msichana mmoja mrefu , mrembo mwenye nywele nyingi mpaka mgongoni akitembea kumfuata Ibrahim , akaacha kutoka garini na kuangalia kwa makini .
    Msichana yule alipomfikia Ibrahim , akamfumba macho kwa nyuma kama wafanyavyo watoto na kisha kumbusu shavuni .
    Yalikuwa ni zaidi ya maumivu , yalikuwa ni zaidi ya moto mkali uwakao . Moyo wake ukawaka moto, akahisi kama kulikuwa na mtu aliyemfuata huku akiwa ameshika msumari wa moto kisha kuuchoma moyo wake.


    Mara baada ya kuondoka kuelekea nchini Marekani huku akimuacha mpenzi wake , Ibrahim nchini Tanzania . Anaporudi, anakuta Ibrahim akiwa na msichana mwingine kitu kinachomuumiza mno.
    SONGA NAYO ….
    Latifa alichanganyikiwa mno, kitendo cha kuona mpenzi wake aliyempenda na kumthamini akiwa amezama katika mapenzi ya mwanamke mwingine, moyo wake ulimuuma mno. Akaliegesha gari lake katika eneo la maegesho ya magari nyumbani kwao na kisha kuteremka. Akaanza kutembea harakaharaka kuufuata mlango wa kuingia ndani kwao . Mashavu yake yaliloanishwa na machozi yaliyokuwa yakimbubujika kwa maumivu makali .
    Kwa kuwa hakukuwa na mtu mwingine ndani ya nyumba zaidi ya mfanyakazi wa ndani, akaingia chumbani kwake .Akakifuata kitanda, akakikalia na kuuchukua mto na kuuegemea huku akijifuta machozi yaliyokuwa yakimbubujika . Taswira za tukio lililopita ziliendelea kujirudia kichwani mwake kama mkanda wa filamu na kadiri alivyoendelea kukumbuka, aliumia zaidi .
    “ Ibrahim ....nimekufanya nini mpenzi ? Kwa nini umeamua kuniumiza hivi ? Kwa nini mpenzi ? Naomba unionee huruma, rudi kwangu , ninaumia , naomba uje kunifariji , ” alisema Latifa huku akilia kama mtoto .Huo ulikuwa mwanzo wa maumivu yake makali . Alimpenda sana Ibrahim na hakutaka kuona akiondoka kirahisi mikononi mwake. Alikumbuka kwamba alipoteza muda wake mwingi kumfikiria , aliwakataa wanaume wengi kwa ajili yake , leo kuona akiondoka mikononi mwake, tena kirahisi namna ile , lilikuwa jambo gumu mno.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Alichokifanya, siku iliyofuata akaondoka na kurudi kulekule Osterbay, sehemu iliyokuwa na wachoraji wengi, alitaka kumuona kwa mara nyingine Ibrahim kwani hakuamini kama kile kilichotokea jana kilikuwa cha kweli.
    Alipofika hapo, akamkuta Ibrahim akiwa peke yake, akateremka garini na kuanza kumsogelea . Kitendo cha Ibrahim kumuona msichana huyo , akakunja sura yake, hakufurahishwa na uwepo wake mahali hapo.
    Ibrahim hakumpenda Latifa , kitendo cha kusogelewa, akaanza kumtukana msichana huyo . Alimtukana na kumdhalilisha kwa kumuita m ****** kumshobokea mtu asiyempenda. Latifa aliumia sana lakini neno moja tu ndilo alilokuwa akimwambia kwamba alimpenda.“ Ninakupenda , ” alisema Latifa huku akilia kama mtoto na watu wakiwa wamesogea kuangalia kilichokuwa kikiendelea .
    “ Huna hadhi ya kutembea na mimi , mbona unakuwa na shobo wewe binti , hebu jiangalie, una hadhi ya kutembea na mimi? Kama nilishawahi kutembea na wewe hiyo kitambo tu , sahau, hebu toka niendelee na kazi yangu , ” alisema Ibrahim kwa sauti ya juu , watu wote waliokuwa wakipita njia, wakasimama na hata waliokuwa wakiyaendesha magari yao, walipoliona tukio hilo, wakasimama na kuwaangalia .
    “ Ninakupenda ..... ”
    “ Mimi sikupendi . Tokaaaaaaa. ...”
    “ Ninakupenda , ninakupenda Ibrahim , naomba usinifanyie hivi, kumbuka tulipotoka, kumbuka ulivyokuwa nyuma , yakumbuke maisha yako Ibrahim, msichana uliyenaye hakupendi, hata kama angeikuta hali uliyokuwa nayo zamani asingekupenda, Ibrahim , naomba ukumbuke, naomba vuta kumbukumbu mpenzi wangu , ” alisema Latifa .
    “ Nani mpenzi wako ? Mimi mpenzi wako ? Hebu toka huko , unaniambia kuhusu historia inanihusu nini?” alisema Ibrahim kwa dharau, tena akiona sifa kwa watu waliowazunguka.“ Dada nenda zako tu , huoni aibu hilo limwanaume linavyokukashifu, ” alisikika msichana mmoja akiongea , alionekana kushikwa na hasira .
    Bado Latifa hakuwa radhi kuondoka mahali hapo. Maneno aliyoongea Ibrahim yalimuumiza mno lakini hakutaka kuondoka kirahisi . Alijua fika kwamba mvulana huyo alikuwa akimpenda mno ila kutokana na uwepo wa Nusrat ndiyo uliombadilisha moyo wake .




    Latifa , msichana aliyekuwa na uwezo wa darasani , anajikuta akiangukia katika mapenzi na kijana aitwaye Ibrahim ambaye baadaye alikuja kumuacha solemba baada ya kupata msichana mwingine wa Kiarabu . Latifa anaumia sana , hana jinsi, anarudi nchini Marekani kusoma, anapofika katika Chuo cha UCLA , anakutana na mvulana aliyekuwa akimtaka sana , huyu aliitwa Liban .
    SONGA MBELE …
    Huo ulikuwa mwanzo wa ukaribu wao, wawili hao, Latifa na Liban walikuwa pamoja kila sehemu walipokuwa. Walisoma darasa moja huku kila walipokuwa wakiingia darasani , walikaa karibukaribu hali iliyowafanya wanaume wote kugundua kwamba wawili hao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi .
    Hiyo haikuwa kazi nyepesi kwa Liban , ni kweli alimpenda mno Latifa lakini kila alipoingizia suala la uhusiano wa kimapenzi , Latifa hakutaka kukubaliana naye , bado maumivu ya Ibrahim yaliendelea kukumbushwa moyoni mwake.
    Siku ziliendelea kukatika, Liban hakutaka kusikia wala kuelewa , kila alipoambiwa sitaki , hakukata tamaa , aliendelea kumwambia zaidi na zaidi mpaka Latifa akachoka na mwisho wa siku, bila kulazimishwa , akajikuta akianza kubusiana na kijana huyo na hatimaye midomo yao kugusana , kilichofuata ni kubadilishana mate.
    “ Ninakupenda Latifa , ” alisema Liban , alimkazia macho msichana huyo , hisia kali za kimapenzi zilionekana machoni mwake.
    “ Ninakupenda pia, lakini ...”
    “ Lakini nini ?”
    “ Naomba usiniumize , ” alisema Latifa kwa sauti ya chini .
    “ Siwezi kufanya hivyo , siwezi kukufanya kama huyo mpumbavu , ” alisema Liban huku akiachia tabasamu pana.
    Liban akawa mtu mwenye bahati mno, wanaume wengi chuoni hapo UCLA walijaribu kumfuatilia Latifa lakini walikataliwa, kitendo cha Liban kumchukua kiliwaumiza wanaume wengi.
    Latifa hakutaka kuliacha penzi la Liban , kwa kipindi kichache alichokuwa naye alimfanya kujisikia amani moyoni mwake , ile furaha ya mapenzi ambayo watu wengi walikuwa wakiizungumzia, ikaanza kuingia moyoni mwake.
    Siku zikaendelea kukatika, mpaka mwaka huo unakatika na mwaka mwingine kuingia , wawili hao waliendelea kuwa pamoja huku kila mmoja akimpa mwenzake ahadi ya kuoana na kuishi pamoja.
    Mwaka wa pili ulipomalizika, wakati wa likizo ndipo Liban akamwambia Latifa kwamba angependa aende naye nchini India kwa ajili ya kuwaona wazazi wake na hatimaye waweze kufunga ndoa kwani umri ulikuwa unaruhusu .
    Latifa hakuamini , hakumkatalia Liban, walikuwa wamebakiza mwaka mmoja tu wamalize chuo hivyo hiyo ikaonekana kuwa nafasi yake kujiandaa kwa ajili ya ndoa, baada ya wiki moja, wakapanda ndani ya ndege na kuelekea India.
    Safari kutoka nchini Marekani mpaka India ilichukua saa ishirini na saba ndipo ndege ilipoanza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi uliokuwa katika Jiji la New Delhi. Ndege iliposimama , abiria wakaanza kuteremka na kuelekea nje ya uwanja huo na kwenda kuchukua mizigo yao.
    “ Uliwaambia wazazi wako kuhusu mimi?” aliuliza Latifa huku uso wake ukitawaliwa na tabasamu pana.
    “ Hapana , ila niliwaahidi kwamba nitawafanyia sapraizi.”
    “ Mmmh!”
    “ Usiogope kipenzi, wewe twende tu , watafurahi sana mana ’ke walinisisitiza sana kuhusu kuoa , ” alisema Liban huku akionekana kuwa na furaha tele.
    Walipofika nje ya uwanja huo , wakachukua teksi na kuanza kuelekea katika Mtaa wa Aurangzeb uliokuwa hapo New Delhi, mtaa ambao wanaishi matajiri wakiwepo waigizaji kama Aksey Kumar na Sunil Shetty .
    Kutokana na wingi wa magari na Bajaj barabarani, walichukua nusu saa mpaka kufika katika mtaa huo .
    Teksi ikaelekea kwenye nyumba moja ya kifahari na kuanza kupiga honi , geti likafunguliwa na gari kuingizwa .
    Wasichana wawili waliokuwa ndugu zake Liban wakalikimbilia gari hilo kwani walikuwa na taarifa kwamba kaka yao angefika nyumbani hapo siku hiyo.


    Msichana mrembo , Latifa amejikuta akipata maumivu makubwa baada ya kuachwa na mpenzi wake , Ibrahim . Huku akiwa kwenye maumivu hayo , anampata mwanaume mwingine wa Kihindi ambaye anampeleka kwao, India, cha kuhuzunisha, hata ndugu wa mwanaume huyo wanamkataa .
    SONGA NAYO …CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Latifa alitia huruma , kila muda Liban alipokuwa akimwangalia, alitamani kulia , hakukuwa na siku ambayo alimuonea huruma mtu kama siku hiyo. Moyo wake ulimpenda mno msichana huyo , kwake , alikuwa kama pumzi .
    Alikuwa tegemeo kubwa mpaka kumpa ahadi kwamba angemuoa na kuwa mama wa watoto wake, lakini mwisho wa siku, ndugu na watu wengine wa karibu hawakumtaka msichana huyo .
    Alitamani kubadilisha matokeo , ndugu zake wakubaliane naye na kuondokana na dhana potofu kwamba Latifa alikuwa na laana kutokana na mchanganyiko wake wa rangi . Ndugu wale hawakutaka kunyamaza , bado waliendelea kulalamika kwamba Liban hakutakiwa kuwa na mwanamke kama Latifa .
    Latifa hakutaka kuendelea kubaki nyumbani hapo, alichokifanya ni kusimama , akachukua mabegi yake na kuondoka nyumbani hapo . Kitu kibaya ambacho kilimshangaza sana ni kwamba Liban hakuweza kumfuata, yaani ni kama mwanaume huyo alikubaliana na wazazi wake.
    “ Ninawachukia watu wa nchi hii , ” alisema Latifa huku akilia kama mtoto .
    Alitembea barabarani huku kichwa chake kikiwa chini, machozi yalikuwa yakimbubujika, kadiri alivyojitahidi kuyafuta, hayakukata, yaliendelea kutoka zaidi na zaidi .
    Safari yake hiyo ikaishia mbele ya hoteli kubwa ya Mumbai , hapo ndipo alipoamua kuchukua chumba, hakutaka kukaa sana , akapanga kuondoka kurudi Tanzania siku inayofuata .
    ****
    Mapenzi yalikuwa motomoto , Ibrahim na Nusrat walijiona kuwa miongoni mwa wapenzi waliokuwa wakipendana kwa dhati kuliko watu wowote wale katika dunia hii . Muda wote walikuwa pamoja, walitaniana na kubusiana kila walipokuwa.
    Kila mmoja kichwa chake kilifikiria ndoa tu , walipita vizingiti vingi vya wazazi, ndugu , jamaa na marafiki na mwisho wa siku, wote hao walikubaliana kufunga ndoa.
    Kwa Ibrahim , furaha iliongezeka zaidi , kila alipokuwa akikaa, alimfikiria msichana huyo ambaye kwake alionekana kuwa kila kitu . Baada ya siku kadhaa kupita, Ibrahim akajikuta akianza kuwa karibu na mwanaume mmoja, alionekana kuwa mzee wa makamo , alikuwa na ndevu nyingi zilizokuwa na mvi, alionekana kuchoka hali iliyoonyesha kwamba maisha yalimpiga sana .
    Alikutana na mzee huyu wakati akielekea Posta kwa ajili ya kukamilisha michoro yake ambayo alitakiwa kumkabidhi Balozi wa Uingereza kama zawadi pekee kutoka kwa Watanzania kabla ya kuelekea nchini mwake .Alipokutana na mzee huyo aliyekuwa ombaomba barabarani, akajikuta akifunga breki na kuteremka. Hakujua sababu iliyomfanya kuwa na huruma kiasi hicho, alionekana kuvutiwa na mzee yule, akaufungua mlango na kuanza kumfuata.
    “ Naomba unisaidie hela ya kula , ” alizungumza mzee yule, mavazi yake yalikuwa yamechakaa sana .
    “ Chukua hii , ” alisema Ibrahim huku akimkabidhi mzee yule noti ya shilingi elfu kumi .
    Hakutaka kukaa sana , ndani ya gari , alikosa amani, kila wakati alikuwa akimfikiria mzee yule ambaye kwake alionekana kuwa na uhitaji mkubwa. Hakutaka kuficha hisia zake , akampigia simu Nusrat na kumwambia kuhusu mzee huyo .
    “ Ni vizuri kusaidia watu wasiojiweza , ” alisema Nusrat.
    Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa urafiki baina ya mzee ombaomba na Ibrahim . Mara kwa mara alikuwa akimfuata na kuzungumza naye mambo mengi ambayo kwa Ibrahim , yalimsisimua sana .
    “ Kwa hiyo ikawaje mpaka ukawa ombaomba?” aliuliza Ibrahim , alitegesha masikio yake kumsikiliza mzee yule ambaye pasipo kutegemea, akaanza kububujikwa na machozi, swali aliloulizwa, likazifanya kumbukumbu zake kurudi nyuma , akaanza kulia .
    “ Naomba unihadithie mzee wangu , ” alisema Ibrahim.
    “ Ni stori ndefu mno.” “ Hata kama , naomba unihadithie, nini kilitokea ?”
    “ Ni mambo mengi , ila moja la msingi , usimfanye mwanamke kulia kwa ajili yako , hiyo ni laana iliyonifanya niwe hapa, ” alisema .


     Nipo hapa kwa sababu ya chozi la mwanamke , nipo hapa kwa kuwa nilimfanya mwanamke kulia. Hakika ningejua kama haya yangetokea, hakika ningemfanya kuwa na furaha milele, nisingeruhusu kuliona chozi lake, ” alisema mzee yule, akanyamaza, akakiinamisha kichwa chake chini , akaanza kulia tena .
    “ Nyamaza mzee . Lakini kwa nini unaniambia hivi?”
    “ Ni kwa sababu wewe ni rafiki yangu, sipendi upate majanga kama niliyoyapata mimi, natamani uje kuwa na furaha maishani mwako , ” alisema mzee yule .
    “ Maneno yako yananitisha .”
    “ Si kwamba nakutisha , ila nakwambia njia za kufanikiwa , njia za kuiepuka laana maishani mwako , ” alisema yule mzee .
    “ Usijali mzee , nitakuwa nikija mara kwa mara , ” alisema Ibrahim na kuondoka . Moyoni mwake hakuweza kukumbuka chochote kuhusu Latifa japokuwa maneno yale yaliutesa sana moyo wake.
    *****
    Kama kulia alilia sana lakini hakikubadilisha kitu, kila kitu kilichokuwa kimetokea , kilitokea na hivyo alitakiwa kusahau kila kitu . Alipofika jijini Dar es Salaam , Latifa akapokelewa kwa shangwe kwa kuwa alifanikiwa sana katika elimu yake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Alikuwa msichana mwenye uwezo mkubwa mno, alijijengea heshima chuoni kutokana na uwezo wake kielimu . Kila mtu akajivunia kuwa na mtu kama yeye hasa katika familia ya bi Rachel .
    Siku zikaendelea kwenda mbele mpaka pale alipotakiwa kurudi tena chuoni nchini Marekani , akarudi zake . Huko chuoni hakukutana tena na Liban, mwanaume huyo alikuwa amehama chuo na kuelekea katika Chuo cha Mumbai nchini India, hakurudi tena Marekani .
    Uzuri wa Latifa ukaendelea kuwa gumzo , hakujua ni nani aliwaambia watu kile kilichotokea, baada ya wiki kadhaa tu , kila mmoja alifahamu kilichoendelea nchini India na hivyo kumpa pole sana .
    “ Naomba kuuliza swali , ” alisema Latifa , walikuwa darasani walipokuwa wakisoma .
    “ Uliza, ” alisema profesa huku akiiweka vizuri miwani yake, kila mtu alimheshimu Latifa, hivyo kila alipoinuka na kutaka kuzungumza kitu, watu wote walikuwa kimya .
    “ Mtu wa kwanza kutengeneza gari , alifikiria kuhusu gari tu na wala hakufikiria kwamba kuna mtu angekuja na kutengeneza ndege , si ndiyo?” aliuliza Latifa .
    “ Ndiyo !”
    “ Hivi kwa nini huyu mtu aliyekuja na kugundua ndege hakufikiria kutengeneza gari lenye miguu kumi badala ya minne?” aliuliza Latifa .
    “ Unamaanisha nini ?”
    “ Nataka kufahamu tu . ”
    “ Mmmh! Sijui kwa nini hakufikiria hilo .”
    “ Sawa. Lakini , kama Alexander Bell aligundua simu ya mezani , kwa nini mtu aliyegundua simu ya mkononi asingegundua simu za aina nyingine zinazotumia waya ?” aliuliza Latifa.
    “ Pia sijui.”
    “ Kuna chochote unachojifunza kutokana na maswali yangu?”
    “ Hapana . Unamaanisha nini?”
    “ Kama jopo la madaktari duniani walikaa kwa ajili ya kutafuta dawa za kuua kansa iliyokomaa, wakakosa , hivi hatuwezi kuwa kama mtu aliyegundua ndege na simu za mkononi? Yaani namaanisha kwa kwenda mbele na kufikiria kitu kingine zaidi ?” aliuliza Latifa.
    “ Unamaanisha nini ?”
    “ Najua umeshajua ninachokimaanisha. Ninataka kutengeneza dawa za kuteketeza kansa katika dunia hii , ” alisema Latifa kwa kujiamini.
    “ Unasemaje ?”
    “ Hiyo dawa itaitwa Morphimousis , nikwambie kitu profesa ? Itakwenda kuokoa maisha ya watu wengi, niamini. Hii ndiyo nafasi ya kuwa bilionea ili yule Ibrahim na Liban wanitafute , ” alisema Latifa , ghafla machozi yakaanza kumbubujika, wanachuo wote walikuwa kimya.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    MWISHO


0 comments:

Post a Comment

Blog