Simulizi : Am Sorry
Sehemu Ya Nne (4)
ILIPOISHIA
Mara kwa mara alikuwa akielekea Muhimbili kwa ajili ya kumuona lakini hakuwa akipata nafasi na hata kama alikuwa akipata pamoja na wanafunzi wenzake, muda uliotolewa aliuona kuwa mfupi .
ENDELEA…
Ibrahim alimpenda Latifa , alihitaji kumuona akizinduka katika usingizi wa kifo na hatimaye kuzungumza naye kwa kumwambia ni kwa jinsi gani alikuwa akimpenda na kumhitaji . Hakuwa na nafasi hiyo tena , kipindi hicho, msichana huyo alionekana kama mfu kitandani .
Siku kadhaa zikapita , akasikia kwamba msichana huyo alikuwa amepelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu. Moyo wake ukanyong ’onyea mno, akakosa nguvu lakini pamoja na hayo , akaahidi kwamba asingeweza kumsaliti japokuwa hakuwahi kuzungumza naye.
Ilipopita miezi miwili, akapewa taarifa mbili , moja ilikuwa yenye kufurahisha lakini nyingine ilikuwa yenye kuhuzunisha . Yenye kufurahisha ilisema kwamba Latifa alikuwa amerudi nchini Tanzania lakini ile yenye kuhuzunisha ilisema msichana huyo alikuwa akihamishwa shule na kwenda kusoma shule moja ya kishua .
Taarifa hiyo mbaya ikaonekana kama mwiba moyoni mwake. Alishindwa kufahamu ni kwa sababu gani lilikuwa jambo gumu kwake kuonana na msichana huyo .
Baada ya wiki mbili , akaambiwa kwamba msichana huyo alianza masomo katika Shule ya St. Antony iliyokuwa Mbezi Beach .
“ Nitamfuata hukohuko tu , ” alijisema Ibrahim .
Hakutaka kuendelea kubaki katika moyo wa kipweke. Baada ya siku kadhaa akaamua kwenda shuleni huko kwa ajili ya kumuona msichana huyo . Alipofika katika geti la shule hilo, akaomba kuonana na Latifa , akakataliwa na mlinzi aliyekutana naye getini.
“ Hii siyo shule ya uswahilini, huku uzunguni , hebu nenda huko uswahilini ukaulizie kiuswahiliuswahili kama ulivyouliza, hapa ukija , unatoa taarifa kwa njia ya simu kwanza , ” alisema mlinzi huyo kwa kebehi kwani kila alipokuwa akimwangalia Ibrahim , alionekana kuwa na maisha mabovu .
****
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Makali ya Latifa darasani hayakupungua, kwenye kila mtihani alikuwa akionyesha kwamba uwezo wake ulikuwa wa juu mno, aliwaongoza wanafunzi wote kiasi kwamba wengi wakaanza kuanzisha bifu naye .
Wavulana walioendelea kumfuata, mmoja wao aliitwa Maliki Abdullahman. Alikuwa kijana mtanashati mwenye asili ya Kiarabu aliyetoka katika familia ya kitajiri, sura yake ilikuwa ya mvuto iliyowachengua wasichana wengi waliokuwa wakikutana naye barabarani .
Maliki alikuwa gumzo kila kona , wasichana walikuwa wakimsumbua kila siku lakini hakutaka kuwa na msichana hata mmoja. Darasani, uwezo wake haukuwa wa kawaida, alikuwa akikimbizana na Latifa japokuwa walikuwa wakisoma madarasa tofauti .
Aliwakataa wasichana wengi, hakupenda kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi lakini mara baada ya kumtia machoni Latifa , moyo wake ukamlipuka, hakuamini kama katika dunia hii hasa kwenye nchi ya Tanzania kungekuwa na msichana mrembo kama alivyokuwa Latifa .
“ She is so beautiful, I just want to be with her , I will never let her go, ” Ni mrembo mno, ninataka niwe naye , kamwe sitomuacha aondoke, ” alisema Maliki huku akimwangalia vizuri Latifa .
Msichana huyo akawa msichana wa ndoto zake, kila alipokuwa akielekea shuleni ilikuwa ni lazima kwenda katika darasa la kina Latifa kwa lengo la kumuona tu . Moyo wake ukatekwa, hakukuwa na msichana aliyeuteka moyo wake kama alivyokuwa Latifa .
Alijitahidi kumpiga picha kisiri na kuwa nazo kwenye simu yake , hiyo ikaonekana kutokutosha , alichokifanya ni kutafuta namba yake, alipoipata, akajitahidi kuwa karibu naye kimawasiliano lakini msichana huyo alikuwa mgumu kutekeka. “ Nifanye nini ? Ngoja nikamwambie ukweli . Mmh! Ila nitaweza kweli? Mbona naanza kumuogopa!” alijisemea Maliki.
Moyo wake ukashikwa na kiu zaidi , alijuta sababu ya kutoshuka garini siku ile na kwenda kuongea naye .
Moyo ukaanza kumuuma ! Hakujua nini kilikuwa ndani ya kijana yule !
SONGA NAYO .. .
Latifa aliishi kwenye mateso makubwa , kila siku akawa mtu wa mawazo tu akimfikiria kijana aliyekuja kumwangalia ambaye alitaka kuzungumza naye lakini hakuweza kushuka garini.
Siku ziliendelea kukatika, hamu aliyokuwa nayo moyoni mpaka ikaisha lakini hakufanikiwa kumuona Ibrahim tena . Aliendelea na maisha yake huku akiendelea kufanya vizuri katika masomo yake kwa kuwaongoza wanafunzi wote shuleni hapo .
Maliki, hakutaka kukata tamaa , kuna kipindi kikafika akaona ni bora kumfuata msichana huyo na kumwambia ukweli lakini hakuwa radhi kuendelea kupata mateso ya moyo . Alichokifanya katika siku ambayo alipanga kumwambia Latifa ukweli , akajiandaa vizuri, hakutaka kuonekana na kasoro yoyote ile , akajivisha ujasiri na kumfuata msichana huyo .
“ Hapana Maliki, sipo tayari kuwa na mvulana yeyote yule, ” alisema Latifa , alionekana kumaanisha alichokuwa akikisema .
“ Latifa, lakini mbona sioni tatizo lolote lile , kama kuna mtu ameuumiza moyo wako , ninataka kuwa daktari wako , niutibu na upone kabisa, nakuahidi kutokukuumiza , ” alisema Maliki huku akimwangalia Latifa machoni . Akamshika mkono ili asiondoke .
“ Maliki, let me go, I’m too young to take care of someone. I’ m just thinking of my studies , you met me here , you don ’t know where I came from, please, let me go, ” (Maliki , niache niondoke, mimi ni mdogo mno kumjali mtu . Ninayafikiria masomo yangu, ulinikuta hapa , hujui nimetoka wapi , niache niondoke ) alisema Latifa huku akimtaka Maliki amuachie mkono .
“ Laty ! What is your problem ? Should I say that I’m ready to die for you! Will this make you happy and trust me when I say that I love you?” ( Laty ! Tatizo lako nini? Natakiwa kusema kwamba nipo tayari kufa kwa ajili yako ? Hii itakufanya kuwa na furaha na kuniamini ninapokwambia kwamba ninakupenda!) aliuliza Maliki.
“ Let me go, ” ( Niache niondoke ) alisema Latifa , sauti yake ilitoka kwa juu tena yenye ukali mwingi .
Maliki akaogopa, ukali aliokuwa ameutumia Latifa ukamtisha , akajikuta akimuachia binti huyo na kuondoka zake. Alimwangalia msichana huyo huku moyo wake ukimuuma mno, hakuamini kama uwezo wake wote wa kuongea ambao aliutumia haukumsaidia hata mara moja na mwisho kukataliwa huku akijiona .
Huo wala haukuwa mwisho , alichokifanya ni kuanza kufuatilia kujua msichana huyo alikuwa akitoka kimapenzi na nani . Alifanya uchunguzi wake kwa siku kadhaa lakini hakubaini kitu chochote kile , aligundua kwamba msichana huyo alikuwa peke yake.
Latifa hakuyataka mapenzi , aliamua kuishi peke yake kwani kulikuwa na mambo mengi ya kufanya katika maisha yake. Aliendelea na maisha yake ya kuwakataa wanaume waliokuwa wakimfuatilia kila siku, japokuwa ulikuwa mtihani mzito lakini alihakikisha anafanikiwa.
“ Malkia Cleopatra. ...” alisikika sauti ya msichana mmoja akimuita jina lake la utani , Latifa akageuka , msichana yule akamsogelea.
“ Unasemaje Lilian?”
“ Kuna mvulana amenipa hii barua , amesema nikupe.”
“ Mvulana gani ?”
“ Wala simjui, nimekutana naye hapo nje ya shule , akanipa, akaniambia nikufikishie halafu akaondoka, ” alisema Lilian.
“ Mmmh!”
“ Unamjua?”
“ Hapana . Ni nani ?” aliuliza Latifa .
“ Sijui !”
Latifa akaichukua barua ile na kuanza kuifungua. Mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa kasi , mwili ukaanza kumsisimka, moyoni mwake alijua kwamba ni yule kijana aliyemuona siku ile . Alipoifungua barua ile , akaanza kuisoma, iliandikwa hivi. ..
Kwako Latifa
Nimekuwa nikikufuatilia kwa kipindi kirefu, u msichana uliyeuteka moyo wangu , nimekuwa nikiteseka kwa ajili yako kwa kipindi kirefu mno tangu ulipokuwa Sekondari ya Jangwani .
Najua haunifahamu , lakini unamkumbuka yule kijana aliyetaka kuzungumza nawe siku za karibuni? Yule kijana mchafu , asiyevutia lakini mwenye mapenzi ya dhati kwako?
Latifa, nimejaribu kila njia kukutana nawe lakini imeshindikana, sina njia nyingine ya kufanya zaidi ya kukuandikia barua hii kwa mwandiko huu mbaya .
Nilisikitika sana ulipopata ajali, kila siku nilikuwa mtu wa kukuombea dua ili upone na ninamshukuru Mungu kwa kukuponya na kukurudishia afya kama ulivyokuwa kabla.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilihuzunika kipindi cha nyuma ulipokwenda nchini India, naikumbuka picha yako ya mwisho kukuona ukiwa hospitalini, ulikuwa kimya huku sura yako ikionyesha kama haukuwa pamoja nasi.
Latifa, nina mengi ya kuzungumza lakini kubwa zaidi lililobeba hayo mengi, ni kwamba, ninakupenda mno, ninakupenda zaidi ya unavyofikiria.
Kama ningeulizwa ni kitu gani natakiwa kuwa nacho maishani mwangu sasa hivi , hakika ningekuchagua wewe .
Ninakupenda Latifa, sijajua ni jinsi gani naweza kulieleza hili, ila ukweli , ni kwamba nakupenda.
Ibrahim, Sekondari ya Azania.
Siku hiyo akasajiliwa kuanza masomo shuleni hapo huku akiwa na mtu wake wa karibu , mtoto wa bi Rachel aliyeitwa Dorcas .
ENDELEA NAYO .. .
Latifa akatokea kupendwa shuleni hapo kutokana na uzuri aliokuwa nao . Wanaume wengi walimtolea macho lakini hakukuwa na mtu aliyethubutu kumfuata. Hakukuwa na aliyefikiria kwamba msichana huyo alitokea nchini Tanzania , shule nzima walifikiri kwamba Latifa alitokea nchini Nigeria .
Hakukuwa na Mzungu aliyetaka kuanzisha uhusiano na msichana yeyote wa Kinaigeria , waliwafahamu wasichana hao , walikuwa wajanja na wengi wao walikuwa matapeli na kama ukiwa karibu nao , kuna siku wanakuibia kila kitu ulichokuwa nacho .
Ukaribu wa Latifa na Dorcas ukawapa wasiwasi zaidi, miongoni mwa watu waliokuwa wakorofi hata kuwasogelea alikuwa msichana Dorcas . Hakuwa msichana aliyewapenda wavulana , aliwachukia mno na chanzo cha kuwachukia kilikuwa ni jamaa aliyeitwa Michael Okonkwo , kijana wa Kinaigeria ambaye alimuibia vitu vyake vyote chumbani kwake zikiwepo fedha.
“ Kuwa makini Latifa, ” alisema Dorcas .
“ Makini na nini?”
“ Wanaume! Wanaume wa huku ni wabaya sana , ukizubaa tu , umelizwa, ” alisema Dorcas .
“ Usijali , nitakuwa hivyo .”
Dorcas hakutaka kuishia hapo , alianza kumsimulia mambo yote yaliyokuwa yakitokea shuleni hapo likiwepo suala la Wanaigeria kuwa wezi na matapeli wakubwa . Latifa akaogopa, hakutaka kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu yeyote yule .
Siku ziliendelea kukatika, alipoanza masomo ndipo watu walipojua kwamba mbali na uzuri aliokuwa nao , Latifa alikuwa mtu hatari darasani . Hakujali kama alikuwa katika ardhi ya ugenini , alichokuwa akikifanya ni kuwaongoza kwa alama nyingi darasani .
Ndani ya miezi sita tu , tayari jina lake lilikuwa miongoni mwa wanafunzi waliokuwa na kipaji darasani . Hakusoma sana , muda mwingi aliutumia chumbani lakini kila ulipokuwa ukija mtihani, Latifa alitisha kwa kupata alama za juu.
“ Nataka uhusiano naye , ” alisema jamaa mmoja, alikuwa mvulana mtanashati , Mhindi kutoka Jiji la Mumbai nchini India .
Liban alikuwa miongoni mwa watu waliovutiwa na Latifa , kila siku katika maisha yake alitamani kuwa karibu na msichana huyo . Alimpenda kwa moyo wake wote , hakuwa tayari kumuona msichana huyo akimkosa na ndiyo maana kila siku alikuwa akimtafuta katika rada zake .
Kuwa na Latifa halikuwa jambo dogo, hakuingilika kwa kuwa tayari alikwishaambiwa maneno mengi na Dorcas juu ya tabia za wanaume wengi shuleni hapo.
Moyo wake ulikuwa mgumu na hata Liban alipoanza kumchombezachombeza , Latifa hakuwa tayari .
Mbali na hilo , bado kichwa chake kilimfikiria mpenzi wake Ibrahim aliyekuwa nchini Tanzania . Hakutaka kumsaliti, alijitahidi kuutoa moyo wake kwa hali zote lakini si kumsaliti mvulana huyo . Japokuwa alikuwa kijana maskini , moyo wake ulikuwa na hamu ya kuishi naye milele.
****
Hakuwa na akili darasani , alifeli vibaya lakini mbali na akili hizo , Mungu alimpa kipaji cha uchoraji. Alipenda kuchora, kila siku katika maisha yake, asilimia kubwa alikuwa akitumia kuchora.
Alitafuta ajira magazetini , alikataliwa kwa kuwa hakuonekana kama alifaa kufanya kazi hiyo ya uchoraji. Ibrahim hakutaka kuishia hapo, aliendelea kuchora zaidi huku mbele yake akiyaona mafanikio makubwa .
Alichokifanya ni kutafuta sehemu maalum ya kufanyia kazi zake za kuchora. Hapo , akaandika bango kwa watu waliokuwa wakitaka kuchorwa , mteja wa kwanza kabisa kumpata alikuwa Nusrat, msichana wa Kipemba aliyefika mahali hapo na kutaka kuchorwa huku akiwa na mpenzi wake .
“ Kiasi gani ?” aliuliza Nusrat .
“ Elfu ishirini kwa mtu mmoja.”
“ Sawa. Chukua hii picha, naomba unichore hivihivi, picha iwe kwenye manila kubwa, nitakuja wiki ijayo kuichukua , ” alisema Nusrat huku akiingiza mkono mfukoni na kutoa kiasi hicho cha fedha na kumkabidhi Ibrahim .
Macho ya Nusrat hayakutulia , kila alipokuwa akimwangalia Ibrahim , alionyesha kwamba alikuwa na kitu fulani moyoni mwake , hakutaka kukiweka wazi kwani alionekana kuwa na hofu kubwa kwa kuwa tu mpenzi wake alikuwa pembeni yake .
Japokuwa hakutaka kuonyesha chochote kile , lakini ukweli ni kwamba alitokea kumpenda kijana huyo , hasa kipaji chake cha uchoraji ndicho kilichomdatisha zaidi .
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kile walichokijua kilikuwa ni kupendana tu pasipo kugundua kwamba ndani ya mapenzi, hakukuwa na furaha tu, kuna kipindi , watu hulia na kutamani kujiua au kuua kabisa .
ENDELEA NAYO .. .
Walihisi kwamba wao ndiyo walikuwa watu wa kwanza kupendana kama walivyokuwa wakipendana, muda mwingi walikuwa pamoja huku wakizungumzia mambo mengi ambayo kwa namna moja au nyingine yangeufanya upendo wao wa dhati uweze kukua na kuwa zaidi ya hivyo ulivyokuwa .
Siku zikaendelea kukatika huku miezi ikizidi kusonga mbele mpaka kufika siku ambayo wawili hao walimaliza masomo yao ya kidato cha nne na hivyo kukaa nyumbani. Waliitumia nafasi hiyo kufanya mambo mengi yakiwemo mapenzi.
Matokeo yalipotoka, Latifa alikuwa amefaulu vizuri lakini kwa Ibrahim , hakuwa amefanya vizuri kabisa. Alionekana kuwa na majonzi lakini mpenzi wake , Latifa ndiye aliyekuwa mfariji wake namba moja, kila alipokuwa akiyafikiria matokeo yale, Latifa alimsogelea, alimkumbatia na kummwagia mabusu mfululizo mashavuni mwake .
Kidogo, moyo wake ulijisikia afueni huku hata matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne yakaanza kupotea kabisa. Kwa sababu bi Rachel alikuwa na watoto wake waliokuwa wakisoma nchini Marekani , hivyo hakutaka Latifa aendelee kusoma nchini Tanzania , alichokifanya ni kuomba ruhusa kwa mzee Issa kwamba alitaka kumpeleka msichana huyo nchini Marekani kusoma.
“ Kwa hiyo unataka kumpeleka kwa Wazungu ?” aliuliza mzee Issa huku akionekana kutokuamini alichokuwa akikisikia . “ Ndiyo . Atakwenda kusoma katika shule wanayosoma watoto wangu , ” alisema bi Rachel .
“ Sawa, hakuna tatizo, ila mtoto mwenyewe atataka?”
“ Nitaongea naye .”
Hilo halikuonekana kuwa tatizo kwani hata Latifa alipofikishiwa taarifa hiyo , akakubaliana naye na hivyo kumwambia mpenzi wake , Ibrahim kwamba alitakiwa kuondoka nchini Tanzania na kwenda Marekani kusoma.
“ Mmmh!”
“ Nini tena mpenzi ?”
“ Wazungu wananiogopesha mno, hawatoweza kunilia tunda langu ?” aliuliza Ibrahim .
“ Najiamini, najitunza, hakuna kitu kama hicho, niamini, ” alisema Latifa na kumkumbatia Ibrahim.
“ Ila usiache kuchora mpenzi , naamini utafanya makubwa mno, ” alisema Latifa na Ibrahim kukubaliana naye .
Hakukuwa na kipindi alichokuwa na huzuni kama kipindi hicho, Ibrahim hakuamini kama furaha yote na ya kipindi chote ndiyo ilitakiwa kuishia wakati huo . Japokuwa Latifa alijitahidi kumwambia Ibrahim kwamba kusingekuwa na kitu chochote ambacho kingebadilika na angeendelea kulitunza penzi lake, Ibrahim hakuweza kuliamini hilo .
Usiku hakulala , mawazo yake yalikuwa kwa Latifa tu . Aliwasiliana naye kwenye simu na kumwambia juu ya wasiwasi wake wa kuporwa msichana wake lakini binti huyo aliendelea kumsisitizia kwamba alikuwa wake peke yake.
Siku hazikuganda, siku ya safari ilipofikia, Ibrahim akawa kama mgonjwa , mpaka ndege ya Shirika la Ndege ya American Airlines inapaa , tayari machozi yalikwishaanza kububujika mashavuni mwake.
Ndege ilichukua saa kadhaa kufika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Amsterdam ambapo walibadilisha ndege na kupanda nyingine iliyowapeleka mpaka katika Jiji la Atlanta nchini Marekani , sehemu ambapo Latifa alitakiwa kuanza masomo yake katika Shule ya St. Luis II iliyokuwa katikati ya jiji hilo .
Siku ya kwanza tu ambayo alipelekwa shuleni hapo, wanaume wote wakapigwa na butwaa, msichana mgeni, kutoka nchini Tanzania alionekana kuwa na uzuri usio wa kawaida. Alikuwa msichana wa Kichotara mwenye mvuto, hipsi zilizojaa na chini ya pua yake kuwa na kidoti kilichosindikizwa na vishimo viwili mashavuni mwake . Alimvutia kila mmoja.
Siku hiyo akasajiliwa kuanza masomo shuleni hapo huku akiwa na mtu wake wa karibu , mtoto wa bi Rachel aliyeitwa Dorcas . Kila alipokuwa , wanaume hawakusita kumwangalia kwa matamanio.
Japokuwa shule hiyo ilikuwa imekusanya wasichana wengi warembo wakiwemo Wabrazil na Wamexico, Latifa alionekana kuwatikisa wote. Wanaume wakapagawa, watoto wa kitajiri wakachanganyikiwa, hawakutaka kitu chochote kile , wao walimtaka Latifa tu .
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment