Simulizi : Am Sorry
Sehemu Ya Tatu (3)
ILIPOISHIA
Hakutaka kuvumilia kusimama nje, alichokifanya ni kuelekea ndani ya shule ile na kukutana na walinzi, akaanza kuwauliza kuhusu Latifa , kwa sababu alikuwa maarufu, halikuwa tatizo .
“Hauna habari nini?” aliuliza mlinzi mmoja.
“Habari gani ?”
SONGA NAYO .. .
Ibrahim aliyasikia mapigo ya moyo wake yakidunda kwa nguvu , hofu ikamuingia, akajikuta akianza kusali kimoyomoyo mlinzi yule asimpe taarifa mbaya kuhusu Latifa kwa kuamini kwamba moyo wake ungemuuma sana .
“ Latifa alipata ajali asubuhi, nimesikia hali yake mbaya sana , aligongwa na gari hapo Jangwani na amepelekwa hospitalini huku akiwa hajitambui. Tetesi zinasema kwamba anatakiwa kusafirishwa kupelekwa India kwa matibabu zaidi, ” alisema mlinzi yule, Ibrahim akaonekana kuchanganyikiwa.
“ Unasemaje ?” aliuliza Ibrahim kwa mshtuko.
“ Ndiyo hivyo , yaani leo watu wamemmisi sana , si unajua demu yule alivyokuwa mkali, ” alisema mlinzi yule.
Ibrahim hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, alihisi kuchanganyikiwa sana , alichokifanya ni kuanza kutimua mbio kuelekea Muhimbili. Kwa kumwangalia , alionekana kama chizi, mapenzi yaliuendesha moyo wake kupita kawaida.
****
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ulisikika mlio mkubwa wa gari , watu wakapiga mayowe, msichana aliyekuwa amegongwa na gari akapiga kelele , alipaishwa juu na alipoanguka chini , akaanguka vibaya, hakutikisika, hapohapo akatulia tuli .
Damu zilikuwa zikimtoka mfululizo , shati lake jeupe alilokuwa amelivaa, lilikuwa ni vigumu kujua kama lilikuwa jeupe , lilitapakaa damu hali iliyoonyesha kwamba msichana huyo alikuwa ameumia vibaya.
Watu waliokuwa pembezoni mwa barabara wakaanza kumfuata, dereva aliyekuwa amemgonga na gari , hakukimbia , akateremka na kumfuata mahali pale alipoangukia . Kila mtu aliyemuona msichana huyo , alishika kinywa chake kwa mshtuko , hakukuonekana na dalili kwamba msichana huyo alikuwa mzima .
Kilichofanyika ni kumbeba na kumpeleka katika gari lile lililomgonga na safari ya kuelekea Muhimbili kuanza . Hakukuwa na mtu yeyote aliyegundua kwamba msichana aliyegongwa alikuwa Latifa, uso wake ulijaa damu huku akiwa ameumia vibaya kichwani.
“ Mungu wangu ! Huyu atakuwa amekufa, ” alisema jamaa mmoja.
Alipofikishwa hospitalini, akachukuliwa na kupelekwa katika chumba cha upasuaji . Kitu cha kwanza alichofanyiwa ni kuwekewa mashine ya hewa safi.
“ Inatupasa tufanye kitu vinginevyo anaweza kufa , ” alisema Dk . Thomas Lyaruu, alikuwa bingwa wa upasuaji hospitalini hapo.
“ Kitu gani ?”
“ Mapigo yake ya moyo yapo chini , nipe CPR, ” alisema Dk . Lyaruu.
Hapohapo mashine ya kushtulia mapigo ya moyo, Cardiopulmonary Resuscitation ( CPR) ikaletwa na moja kwa moja kuanza kuyashtua mapigo ya moyo ya Latifa ambayo yalikuwa chini mno.
Kila kitu kilichokuwa kikifanyika mahali hapo, kilifanyika kwa harakaharaka, baada ya kuona kwamba mapigo yake ya moyo yanaanza kurudi katika hali yake, wakamtundika dripu na kuanza kuisikilizia hali yake.
Tayari wanafunzi walikwishaanza kukusanyika hospitalini hapo, kila mmoja alionekana kujawa na majonzi kufuatia taarifa waliyokuwa wameisikia kwamba mwanafunzi mwenzao aliyekuwa akisifika kwa urembo shuleni , Latifa alikuwa amepata ajali mbaya ya gari .
Hali iliyokuwa ikiendelea hospitalini hapo ilizidi kuwatia hofu wanafunzi kiasi kwamba kila mmoja akabaki akisali kimoyomoyo ili Mungu atende muujiza na hatimaye aweze kurudi katika hali yake ya kawaida.
“ Mpelekeni kwenye chumba cha upasuaji , tunatakiwa kuanza kazi mara moja, ” alisema Dk. Lyaruu.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, wakamtoa katika chumba kile cha dharura na kumpeleka katika chumba cha upasuaji na kazi kuanza mara moja.
“ Ubongo wake umetikisika, hili ni tatizo kubwa , hebu subirini, muandaeni , nitarudi sasa hivi kuanza naye , ” alisema Dk. Lyaruu.
Dk. Lyaruu akatoka ndani ya chumba hicho na baada ya dakika chache, alikuwa kwenye chumba kikubwa ambacho kilikuwa kikitumika kwa kufanyia mikutano au vikao vya dharura .
Jopo la madaktari lilikuwa limekutana, wote walikuwa mahali hapo kwa ajili ya kuizungumzia hali aliyokuwa nayo Latifa ambayo ilimshtua kila mmoja. Baada ya kufanyiwa uchunguzi, ripoti zikawekwa mezani na kuanza kujadiliwa .
“ Ni ajali mbaya , ripoti zinaonyesha kwamba ubongo wake umetikisika na damu kuvilia, kuna vitu vitatu vinaweza kutokea kama tusipofanya kitu fulani , kitu cha kwanza mgonjwa anaweza kuwa kichaa, anaweza kupoteza kumbukumbu , anaweza kupata kifafa , lakini mbaya zaidi , anaweza kufariki, ” alisema Dk . Lyaruu, madaktari wote walikuwa kimya wakimsikiliza .
Itaendelea wiki ijayo .
“ Kwa hiyo ili kuyaokoa maisha yake, ni lazima tulifungue fuvu lake, tuitoe damu hiyo , kama tutashindwa , haina budi kumsafirisha kuelekea nchini India, ” alisema Dk Lyaruu, kila mmoja ndani ya chumba kile akashusha pumzi ndefu.
Kuna vitu vitatu vinaweza kutokea kama tusipofanya kitu fulani. Kitu cha kwanza mgonjwa anaweza kuwa kichaa , anaweza kupoteza kumbukumbu, anaweza kupata kifafa, lakini mbaya zaidi , anaweza kufariki ,” alisema Dk. Lyaruu, madaktari wote walikuwa kimya wakimsikiliza . ENDELEA …
Ilikuwa ni taarifa mbaya ambayo hawakutegemea kuisikia kipindi hicho, msichana mdogo ambaye alipata ajali na kuletwa hospitalini hapo alipatwa na tatizo kubwa lililoashiria kifo chake endapo tu asingeweza kutibiwa kwa ufasaha.
Alikuwa msichana mdogo mno kupata mateso kama yale aliyoyapata. Msichana mrembo , mwenye akili nyingi , leo hii alipata ajali mbaya na kuufanya ubongo wake kutikisika .
“ Kwa hiyo ili tuyaokoe maisha yake, ni lazima tulifungue fuvu lake, tuitoe damu hiyo , kama tutashindwa , haina budi kumsafirisha kuelekea nchini India, ” alisema Dk Lyaruu. Kila mmoja ndani ya chumba kile akashusha pumzi ndefu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kikao cha dharura kikafungwa na kila mtu kuondoka ukumbini hapo. Vichwa vyao vilikuwa vikifikiria ni kitu gani kilitakiwa kufanyika ili Latifa aweze kupona na kurudi katika hali ya kawaida.
Hawakutaka kumuona akichanganyikiwa au kumbukumbu yake kufutika , hawakutaka kumuona akipatwa na ugonjwa wa kifafa, mbaya zaidi , hawakutaka kumuona akifariki dunia, walitaka kumtibu na mwisho wa siku awe kama alivyokuwa kabla .
“ Dokta, nini kinaendelea?” aliuliza mwanamke mmoja, alikuwa ni yule dereva aliyemgonga Latifa kwa gari .
“ Subirini kwanza , kuna kitu kinatakiwa kufanyika, ” alijibu Dk . Lyaruu huku akionekana kuwa na haraka.
“ Nipo radhi kutoa kitu chochote kile , ninahitaji huyu mtoto apone , naomba mumsaidie , ” alisema mwanamke yule.
Alionekana kuchanganyikiwa, kitendo cha kumgonga Latifa na gari kilimchanganya. Kila alipokuwa akikaa, hakutulia , alisimama na kuzunguka huku na kule, alionekana kama chizi .
Sehemu hiyo ya kusubiria kuwaona wagonjwa hakuwa peke yake, zaidi ya wanafunzi thelathini walikuwepo mahali hapo huku kila mmoja akitaka kumuona Latifa , msichana mrembo ambaye alikubalika , leo hii alikuwa hospitalini huku akiwa hajitambui .
Baada ya dakika ishirini , madaktari watatu na manesi wanne wakaingia ndani ya chumba cha upasuaji ambapo alikuwepo Latifa . Walipofika, kitu cha kwanza wakashikana mikono kwa kumzunguka Latifa na kisha kuanza kumuomba Mungu kwa dini zao ili aweze kuwasaidia katika upasuaji uliokuwa unakwenda kufanyika ndani ya chumba hicho.
Kitu cha kwanza walichokuwa wakikihitaji ni kumuingiza katika mashine kubwa iliyokuwa na kipimo kiitwacho Magnetic Resonance Imaging (MRI ) . Hicho kilikuwa kipimo maalumu ambacho hutumika katika kuangalia ni sehemu gani ya ubongo wa mwanadamu iliyokuwa imevilia damu.
Hiyo ndiyo ilikuwa hatua ya kwanza kabisa ambayo walitakiwa kuichukua ndani ya mashine ile . Kikamera kidogo ambacho kiliunganishwa na kompyuta iliyokuwa chumbani mule ikaanza kuchukua kile kilichokuwa kikionekana.
Kila daktari akashtuka, hawakuamini kama donge la damu ambalo lilivilia ndani ya ubongo wa Latifa lilikuwa kubwa kiasi kile . Japokuwa waliwahi kupokea wagonjwa wengi wa tatizo kama lile lakini hawakuwahi kumpata mgonjwa aliyekuwa na donge kubwa la damu kama ilivyokuwa kwa Latifa .
“ Hapa kazi ipo, sidhani kama itawezekana , ” alisema Dk . Pius, alikuwa mtaalamu wa upasuaji hospitalini hapo .
“ Ooppss…! Sikujua kama damu inaweza kuwepo kwa wingi kiasi hiki. Hili ni tatizo kubwa, inatakiwa ahamishwe haraka kwenda kwa wataalamu zaidi, vinginevyo , anaweza kufariki, ” alisema Dk . Lyaruu.
Hospitali ambayo ilikuwa vichwani mwao kwa haraka sana ni Ganga Medical Center iliyokuwa nchini India, huko ndipo alipotakiwa kupelekwa kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji ambao ungegharimu zaidi ya dola elfu kumi , zaidi ya shilingi milioni ishirini .
“ Ni fedha nyingi, atazipata vipi?” aliuliza Dk. Lyaruu.
“ Labda tukazungumze na yule mwanamke aliyemgonga, tukishindwa , tuwaruhusu waandishi wa habari wa Gazeti la Uwazi waitoe taarifa yake gazetini , naamini ataweza kupata kitu chochote kile , ” alisema Dk . Pius.
Walichokifanya ni kumfuata mwanamke yule ambaye muda wote alikuwa mtu wa kulia tu . Walipomwambia kwamba Latifa alitakiwa kusafirishwa nchini India kwa ajili ya matibabu, akakubaliana nao kulipia kila kitu , si milioni ishirini tu , hata ingekuwa mia moja, alikuwa radhi kufanya hivyo .
Mawasiliano na Hospitali ya Ganga yakaanza kufanyika. Mtoto mwenye sura nzuri , aliyekuwa na akili darasani , aliyetoka katika familia ya kimasikini ambapo mama yake alifariki kwa ugonjwa wa Ukimwi , alihitaji kupelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu ya kuondoa donge kubwa la damu kwenye ubongo, kila kilichokuwa kikiendelea , alikuwa kwenye usingizi wa kifo, hakuwa akifahamu chochote kile .
“Atakufa?” aliuliza Bi Rachel .
“Hapana , hawezi kufa, Mungu wetu ni mkuu , atamponya tu,” alisema Dr . Munil ambaye alionekana kuwa na imani kubwa .
ENDELEA NAYO …
Bado Latifa aliendelea kuwa kitandani hapo, ukimya ulikuwa ni sehemu ya maisha yake ya kila siku, hakuwa akizungumza kitu chochote kile na hata kula alikuwa akila kwa kutumia mipira maalumu ambayo iliunganishwa tumboni mwake.
Kila siku ilikuwa ni huzuni kwao , kwa Bi Rachel , moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali mno, kila siku alikuwa akimuomba Mungu aweze kumponya binti huyo ili moyo wake urudi kwenye amani kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma .
Wiki zikakatika na hatimaye mwezi wa kwanza kumalizika , bado Latifa aliendelea kuwa kitandani pale. Mwezi mwingine ulipoingia , kidogo kwake ikaonekana kuwa nafuu , akaanza kwa kukunja vidole vya mikono yake , manesi waliokuwa ndani ya chumba hicho hawakutaka kubaki humo , wakatoka kwa kasi kumfuata Dk . Munil na kumwambia kile kilichokuwa kimeendelea chumbani.
“ Kuna nini?” aliuliza Dk . Munil.
“ Dokta, dokta, mgonjwa ameanza kukunja vidole vyake , ” alisema nesi mmoja huku akihema kama mtu aliyekimbia umbali mrefu .
“ Mgonjwa gani ?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Latifa. ”
Dk. Munil hakutaka kubaki ofisini kwake , kwa kasi ya ajabu akachomoka na kuanza kuelekea katika chumba alichokuwemo Latifa .
“ Kuna nini?” aliuliza Bi Rachel ambaye alikuwa nje ya chumba kile .
“ Subirini.”
“ Kwa nini tusubiri? Manesi walitoka wakikimbia, wewe unatuambia tusubiri! Kuna nini?” aliuliza Bi Rachel huku Issa akiwa pembeni akimsikiliza.
Dk. Munil hakujibu swali hilo, akaingia ndani kwa ajili ya kujihakikishia kwa macho yake. Alipofika ndani ya chumba hicho, moja kwa moja macho yake yakatua kwa Latifa aliyekuwa kitandani, akayapeleka macho yake katika vidole vyake , kwa mbali vilikuwa vikitikisika .
“ Amepona, ” alijikuta akisema Dk . Munil huku akipiga magoti chini na kumshukuru Mungu.
Alichokifanya Dk . Munil ni kumuita Bi Rachel na Issa ndani ya ofisi yake na kuanza kuwaambia kile kilichokuwa kimetokea ambacho kwao kilionekana kama muujiza mkubwa.
Kila mmoja alijikuta akimshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyokuwa ameyafanya . Baada ya siku mbili , Latifa akaanza kufumbua macho yake na baada ya siku chache mbele, akaanza kuongea japo kwa sauti ya chini kabisa.
“ Hakupata tatizo lolote?” aliuliza Bi Rachel .
“ Hakupata. Tulitegemea angeweza kusahau kila kitu lakini haikuwa hivyo , tukahisi kwamba angeweza kupata ukichaa lakini haikuwa hivyo pia, ni mzima wa afya , hili ni jambo la kumshukuru Mungu, ” alisema Dk . Munil.
“ Kwa hiyo ni lini hali yake inaweza kutengemaa kabisa?”
“ Hivi karibuni, nadhani baada ya wiki moja. ”
“ Tunashukuru sana .”
Waliendelea kusubiria hospitalini hapo huku kila mmoja akitaka kuona Latifa akirudi katika hali yake kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma . Kadiri siku zilivyozidi kwenda mbele ndivyo ambavyo hali yake iliendelea kuwa vizuri na baada ya wiki moja iliyosemwa , akaanza kuongea kama kawaida.
“ Ilikuwaje?”
“ Ulipata ajali.”
“ Mungu wangu !”
“ Ila tunashukuru Mungu umepona .”
“ Kwa hiyo hapa nipo hospitali gani ? Agha Khan? Mbona Wahindi wengi?”
“ Hapana . Hapa upo India.”
“ Mmmh! Na wewe nani ?” alimuuliza Bi Rachel .
Hakutaka kuficha , moyo wake ulikuwa ukimsuta kila alipotaka kukaa kimya. Hapo ndipo alipoamua kumwambia Latifa ukweli juu ya kila kitu kilichokuwa kimetokea . Moyo wa Bi Rachel ukaanza kumpenda Latifa. Katika maisha yake yote, alikuwa amepata mtoto mmoja tu ambaye kwa wakati huo alikuwa nchini Marekani akisoma. Jina la mtoto huyo aliitwa Godwin .
Mara baada ya kumzaa mtoto huyo , kwa bahati mbaya Bi Rachel akapata ajali mbaya ya gari akiwa na mume wake aliyefariki dunia palepale huku yeye akiharibika kizazi chake na kutokuweza kubeba mimba tena .
Akaishia kuwa na mtoto mmoja tu , hakupata mwingine tena , huyo ndiye mtoto aliyekuwa akimpenda. Kitendo cha kuwa karibu na Latifa kikamfanya kutamani kuendelea kuishi na msichana huyo , hakujua Latifa alikuwa nani , hakujua kama ana wazazi wake au la , kitu alichokuwa akikitaka ni kuishi naye tu .
“ Nitamuomba niishi naye, nimsomeshe , nitatumia hata utajiri wangu wote ili mradi afike pale ninapotaka afike . Halafu nilisikia wakisema kwamba yeye ni genius, kama ni kweli , nitampeleka Marekani katika shule ya watoto wenye vipaji akasome , nadhani huko maisha yake yatabadilika , ” alijisema Bi Rachel , kila alipokuwa akimwangalia Latifa , alijisikia furaha moyoni mwake.
Waliendelea kubaki nchini India mpaka pale Latifa aliporuhusiwa tayari kwa kurudi nyumbani. Hakuwa amepata tatizo lolote lile ambalo lingemfanya kuwa na ugonjwa wowote , iwe kifafa, kusahau au kupoteza maisha.
Alipokuwa amehadithiwa kile kilichokuwa kimetokea , alibaki akilia huku akimshukuru Bi Rachel kwa msaada aliompa ..“ Ninataka kuishi na Latifa , ” alisema Bi Rachel , alikuwa akimwambia Issa .
“ Haiwezekani , bado tunahitaji kukaa naye zaidi, akikuakua , tutakuruhusu uje kumchukua , ” alisema Issa .
“ Na mama yake yupo wapi ?”
“ Ni stori ndefu sana , kuna siku utajua , kitu cha msingi, acha tuendelee kukaa naye hapa , ukitaka kumuona , usihofu chochote kile , unakaribishwa sana , ” alisema Issa .
Tayari kwa mtazamo wa haraka aligundua kwamba Latifa alikuwa fedha , hakutaka kumruhusu kuondoka mahali hapo kwani alijua kwamba endapo Bi Rachel angeamua kumchukua basi asingeweza kuwasaidia.
Mwanamke huyo alikuwa tajiri, alikuwa na kiasi kikubwa cha fedha, alimiliki vituo vya mafuta , super market na biashara nyingine zilizokuwa zikimuingizia fedha kila siku. Maisha yake yalitawaliwa na fedha, hakuwa na shida, aliishi maisha aliyotaka kuishi siku zote .
Alichokifanya Bi Rachel ni kubadilisha maisha ya Issa , dada yake na Latifa pia . Mara kwa mara alikuwa akiwatumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuwaendeleza katika maisha yao ya kila siku. Baada ya kuhakikisha kila kitu kimekaa sawa , akamhamisha Latifa katika Shule ya Jangwani na kumhamishia katika Shule ya St . Antony iliyokuwa Mbezi Beach.
Hakutaka msichana huyo apate tabu yoyote ile , alitaka kumsomesha mpaka atakapofikia levo ya juu kabisa . Shuleni huko , Latifa alionekana kuwa mwiba , uzuri wake ulimpagawisha kila mvulana aliyekuwa akimwangalia .
Wasichana wenzake waliokuwa wakivuma kwa uzuri shuleni hapo wakaanzisha bifu na yeye, waliuogopa uzuri wake kwa kudhani kwamba angeweza kuwachukulia wavulana wao .
“ Ninamchukia huyu kinyago , simpendi kweli, sijui kwa nini amehamia hapa, ” alisema msichana mmoja, aliitwa Theresa aliyekuwa miongoni mwa wasichana waliokuwa wakitesa kwa uzuri shuleni hapo .
“ Achana naye shoga, asikuumize kichwa, hakuna atakayeweza kutuchukulia watu wetu , ” alisema msichana mwingine .
Uzuri wa Latifa haukuishia hapo bali ulikuwa mpaka darasani , hakukuwa na mwanafunzi aliyekuwa akimfikia kwa uwezo mkubwa aliokuwa nao . Japokuwa wasichana wengi warembo darasani hawakuwa na makali lakini kwa Latifa hali ilionekana kuwa tofauti kabisa.
Walimu walibaki wakimshangaa , hawakuweza kuamini kama kulikuwa na mtu aliyekuwa na akili nyingi kama alivyokuwa Latifa. Katika masomo yake yote shuleni hapo , alipata alama ya A kitu kilichomfanya kuwa mwanafunzi wa kwanza katika shule hiyo kufaulu kwa kiwango hicho kikubwa .
“ Hapa ni kusoma tu , mapenzi baadaye, ” alisema Latifa kila alipokuwa akifuatwa na wavulana, kwake , masomo yalikuwa chaguo la kwanza.
****
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ibrahim alikuwa kwenye wakati mgumu , muda mwingi alikuwa mtu wa mawazo , hakuamini kama kweli msichana aliyekuwa akimpenda alipata ajali na hivyo kipindi hicho alikuwa hoi kitandani huku akiwa hajitambui .
Mara kwa mara alikuwa akielekea Muhimbili kwa ajili ya kumuona lakini hakuwa akipata nafasi na hata kama alikuwa akipata pamoja na wanafunzi wenzake , muda uliotolewa aliuona kuwa mfupi .
Alimpenda Latifa, alihitaji kumuona akizinduka katika usingizi wa kifo na hatimaye kuzungumza naye.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment