Simulizi : Am Sorry
Sehemu Ya Pili (2)
ILIPOTOKA
“Mmmh! Kuzuri ,” alisema Nahra, harufu mbaya ya chumbani mule , ikaanza kuiumiza pua yake . Hilo wala hakujali sana , alichokuwa akikihitaji ni sehemu ya kuishi tu.
ENDELEA. ..
Kadiri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda mbele ndivyo ambavyo moyo wa Deo ulizidi kuuma , hakuamini kama tayari msichana aliyekuwa akimpenda kwa moyo wote , Nahra hakuwa mikononi mwake.
Moyo wake ulikuwa katika majuto, japokuwa alipewa vitisho vya kuuawa endapo tu asingemfukuza Nahra lakini kumuachia likaonekana kuwa kosa kubwa kwake kwani hata kama angemchukua na kuondoka naye kwenda kuishi sehemu nyingine, aliamini watu hao wasingeweza kumpata .
Hakutaka kukaa nyumbani, alijiona kuwa na uhitaji mkubwa wa kumtafuta msichana huyo aliyeondoka nyumbani kwake usiku wa saa mbili . Alichokifanya siku hiyo ni kuondoka nyumbani. Sehemu ya kwanza ambayo ilimjia kichwani mwake ni kwenda kumuulizia nyumbani kwao , Msasani .
Alipofika huko , mtu wa kwanza kabisa kuonana naye alikuwa mlinzi, Chichi .
“ Namuulizia Nahra , ” alisema Deo huku akionekana kutokuwa sawa .
“ Daah ! Deo, hata salamu?”
“ Nimechanganyikiwa kidogo . Mambo vipi!”
“ Poa. Nahra hayupo.”
“ Hayupo ! Si alikuja hapa jana usiku ? Chichi , usinifiche bwana , mimi mweusi mwenzako , naomba uniitie Nahra , ” alisema Deo huku akionekana kutokuwa sawa kabisa , alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa .
“ Deo, siwezi kukuficha kitu , mbona zamani nilikuwa nakuitia freshi tu . Jana Nahra alikuja hapa home, mdingi wake akamtimua kama mbwa, ” alisema Chichi .
“ Unasemaje ?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Ndiyo hivyo . Mzee katili sana , alimfukuza kama hamjui . Hapa unaweza kuniletea msala , mzee akikuona anaweza kukuua na kunifukuza kazi, kama vipi wewe nenda tu , ” alisema Chichi .
“ Sawa. Haina noma, niende wapi sasa? Nikamtafutie wapi ?”
“ Sijajua . Popote pale wewe nenda tu , ” alisema Chichi, akaingia ndani na kufunga geti .
Deo akabaki akiwa hajui ni mahali gani alipotakiwa kwenda muda huo , bado alikuwa amechanganyikiwa mno na hakujua mahali alipokuwa msichana wake aliyekuwa na ujauzito wake .
Hakuwa na jinsi, kwa sababu alitakiwa kuondoka na hapo nyumbani ndiyo ilikuwa sehemu pekee ambayo aliamini angeweza kumkuta Nahra , akaondoka zake na kurudi nyumbani huku uso wake ukiwa na huzuni mno.
***
Maisha hayakuwa ya kawaida hata mara moja, kuishi na mtu ambaye hakuwa na malengo yoyote yale zaidi ya kuendekeza pombe na kuishi kwa kutumia kuuza vyuma chakavu, yalikuwa ni maisha magumu kupita kawaida.
Issa hakuwa mwanaume aliyekuwa akimhitaji , lakini kwa wakati huo , hakuliangalia hilo, aliona ni bora kuishi naye hivyohivyo tu .“ Wewe kula tu , usijali, utaendelea kuishi hapa, ” alisema Issa.
Tofauti na matarajio yake , Issa hakumtaka kimapenzi hata siku moja, kila siku walikuwa wakilala wote lakini hakukuwa na siku aliyokuwa akimgusa kitu kilichomfanya Nahra kufikiria vibaya. Marafiki wa Issa hawakukauka, uzuri wa Nahra ulikuwa gumzo mtaani, kila wakati, wanaume walikuwa wakifika hapo na mtu pekee waliyekuwa wakitaka kumuona alikuwa Nahra tu .
Issa alikuwa mkali kwa kila mwanaume aliyekuwa akimtaka Nahra , hakutaka mtu yeyote amuingilie msichana huyo na wakati alikuwa kwenye ngome yake . Wapo waliokuwa wakimfuata kwa pesa ili awaunganishie awe nao lakini vyote hivyo , Issa aliendelea kukataa .
Siku ziliendelea kukatika, miezi ikasonga mbee mpaka tumbo la Nahra kuanza kuonekana . Hapo , Issa aliendelea kuhangaika zaidi , hakutaka kukaa nyumbani, alijitahidi kutoka kwenda mihangaikoni ili kuhakikisha kwamba chakula cha kutosha kinapatikana kwa ajili ya Nahra aliyekuwa mjauzito .
Baada ya miezi tisa kutimia, Nahra akajifungua mtoto mzuri wa kike ambaye alimpa jina la Latifa. Japokuwa alikuwa mtoto mdogo, uzuri wa sura yake haukuweza kujificha, alipokuwa akicheka, akitabasamu na hata kulia , bado uzuri wake ulikuwa palepale.“ Amechukua sura yako , mmmh! Katoto kazuri , ” alisema Issa huku akimwangalia Latifa .
“ Asante.”
“ Kwa hiyo ndiyo baba yake alimkataa?”
“ Ndiyo .”“ Duuh ! Makubwa . ”
Kila alipokuwa akimwangalia mtoto wake , Latifa, Nahra aliumia, mawazo juu ya Deo yakaanza kumtawala. Moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makubwa , hakuamini kama mtoto aliyekuwa amezaliwa alikataliwa na baba yake.
Siku zikaendelea kukatika na mawazo kuzidi kumuumiza . Latifa alipofikisha kipindi cha miezi miwili tu , Nahra akaanza kuvuta sigara na kunywa pombe za kienyeji , hakufanya hayo kwa kuwa alipenda bali alitaka kuyaondoa mawazo juu ya Deo. Sigara na pombe hazikumpenda , ndani ya miezi mitatu tu afya yake ikaanza kubadilika .
Mwili uliendelea kupungua kila siku , sehemu yake kubwa aliyokuwa akiishi kwa wakati huo ilikuwa klabuni tu. Japokuwa Issa alikuwa mlevi na mvutaji sigara mzuri lakini kwa Nahra alionekana kuwa zaidi yake .
ENDELEA. ..
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Uzuri wake haukupungua japokuwa mwili wake ulichoka mno kutokana na unywaji wa pombe za asili na uvutaji sigara . Maisha yake yakazidi kupoteza dira , wale watu waliokuwa wakimfuatilia, hawakumfuatilia tena , walevi aliokuwa akinywa nao klabuni ndiyo waliokuwa wakimchukua na kufanya naye mapenzi.
Kwa sababu hakuwa na fedha, mlevi yeyote yule aliyemsaidia kiasi cha shilingi mia mbili kwa ajili ya kununua kikombe kimoja cha gongo , naye alikuwa akimuweka kwenye foleni ya kufanya naye mapenzi usiku ndani ya choo cha klabuni hapo.
Kwa Latifa, hakupokea malezi bora, kila siku alikuwa akiachwa nyumbani na hata kama ilitokea siku mama yake kumchukua na kwenda naye klabuni , alipolilia maziwa , alipewa kiasi cha pombe kunywa.
“ Wewe mwanamke , utamuua huyo mtoto ! Unampa gongo !” alisema mlevi mmoja kwa mshangao.
“ Bwana achana na mimi , usifuatilie maisha yangu, fanya kilichokuleta , ” alisema Nahra huku akiona kila kitu alichokuwa akikifanya kilikuwa sawa .
Walevi wengine hawakupenda kuona jambo hilo likiendelea kutokea , walichokifanya ni kumwambia Issa ambaye alionekana kuchukizwa na kitendo hicho na hivyo kumchukua Nahra na kumpeleka kwa dada yake, Semeni aliyekuwa akiishi Manzese Midizini .
Pombe zilizidi kumkolea Nahra mpaka kufikia kipindi ambacho hakuwa akirudi nyumbani, sehemu yake ya kushinda na hata kulala ilikuwa klabuni tu . Issa alikuwa kwenye wakati mgumu, japokuwa alimchukua mwanamke huyo kwa ajili ya kumsaidia lakini kwa kipindi hicho, kwa kiasi fulani alikuwa akijuta .
Kila siku ilikuwa ni lazima kumfuata Nahra klabuni na kumrudisha nyumbani, japokuwa lilikuwa zoezi gumu kwake lakini hakuwa na jinsi, alifanya kila kinachowezekana kuhakikisha Nahra analala nyumbani kwake .
Mwaka wa kwanza ukakatika na mwaka wa pili kuingia , ulipokatika, mwaka wa tatu ukaingia . Nahra aliendelea kubaki katika hali ya ulevi mkubwa na mpaka mwaka wa tatu unaingia , tayari alikuwa mnywaji mkubwa kuliko wanywaji wote waliomtangulia.“ Mtoto wangu yupo wapi ?” aliuliza Nahra , mwili wake ulikuwa umekonda mno huku ukiwa na vipele vingi .
“ Yupo kwa dada yangu. Ameanza shule , usihofu kitu chochote kile , ” alijibu Issa .
“ Nataka kumuona mtoto wangu , ” alisema Nahra.
“ Utamuona tu . Usijali .”
“ Lini?”
“ Wewe unataka lini?”
“ Leo.”
“ Kwa leo haitawezekana . Tufanye keshokutwa, ” alisema Issa .
Mwezi wa kwanza ukakatika toka amuulizie Latifa, mwezi wa pili na wa tatu ikakatika na hatimaye kumalizika mwaka mzima . Afya yake iliendelea kuzorota huku vipele vikiendelea kumsumbua mwilini mwake .
“ Twende hospitalini, ” alisema Issa .
“ Hapana . Siwezi kwenda .”
“ Kwa nini?”
“ Naogopa sindano .”
“ Hapana . Utakwenda tu .”
Afya ilikuwa yake lakini lakini kwenda hospitalini ilikuwa mbinde. Alichokifanya Issa ni kumbeba na kuanza kuondoka naye . Muda wote Nahra alikuwa akilalamika kwamba hakutaka kwenda hospitalini lakini Issa hakutaka kujali , aliendelea kumbeba mpaka walipofika katika Hospitali ya Halmashauri, Tandale.
“ Apelekwe Muhimbili kwa vipimo zaidi , ” alisema DK. Mariamu.
Issa hakuchoka , kwa sababu alikuwa na kiasi fulani cha fedha, akachukua Bajaj na safari ya kuelekea Muhimbili ikaanza . Walipofika huko , vipimo vikachukuliwa na Nahra kuonekana kuwa na ugonjwa hatari wa UKIMWI .
Hiyo ilikuwa taarifa mbaya kwake , msichana aliyekuwa na mvuto mkubwa kiasi cha kuwatetemesha wanaume wa Kihindi, leo hii alikwisha kabisa na kuambukizwa ugonjwa hatari wa UKIMWI .
Nahra alilia sana lakini kilio chake hakikubadilisha kitu, mtu pekee ambaye kwa kipindi hicho alikuwa akimfariji alikuwa Issa tu .
Siku zikaendelea kukatika, vipele vikaongezeka na hata mwili uliendelea kupungua zaidi mpaka kufikia hatua kupauka kabisa. Hizo zote zilikuwa dalili za ugonjwa huo hatari na mwisho wa siku nywele zake kuanza kunyonyoka.
Nahra alikwisha kabisa, aliharibika na kila siku alikuwa mgonjwa . Japokuwa kila siku alitamani sana kwenda klabuni kulewa lakini kwa hatua aliyokuwa amefikia , hakuwa hata na nguvu za kuweza kusimama . Akawa mtu wa ndani tu .
“ Ninakufa Issa , ninataka kumuona mtoto wangu, ” alisema Nahra huku akitia huruma kitandani.
Issa hakuwa na cha kufanya, ni kweli kwa muonekano aliokuwa nao alionekana kutokuwa na muda mrefu kuendelea kuishi, alichokifanya ni kwenda kumchukua Latifa na kumletea.
Itaendelea katika toleo lijalo , usikose nakala yako.
Alikuwa amefanana naye kwa kila kitu kuanzia uzuri na hata ngozi ya mwili .
Nahra alibaki akimwangalia mtoto wake tu , machozi yakaanza kumtoka pale alipokumbuka kwamba alikuwa mfu aliye hai .Mwili uliendelea kupungua kila siku , sehemu yake kubwa aliyokuwa akiishi kwa wakati huo ilikuwa klabuni tu. Japokuwa Issa alikuwa mlevi na mvutaji sigara mzuri lakini kwa Nahra alionekana kuwa zaidi yake .CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Nahra alibaki akimwangalia mtoto wake tu , machozi yakaanza kumtoka pale alipokumbuka kwamba alikuwa mfu aliye hai .
Issa hakuwa na cha kufanya, ni kweli kwa muonekano aliokuwa nao alionekana kutokuwa na muda mrefu kuendelea kuishi, alichokifanya ni kwenda kumchukua Latifa na kumletea . ENDELEA. ..
Nahra alikuwa amefanana naye kwa kila kitu kuanzia uzuri na hata ngozi ya mwili . Nahra alibaki akimwangalia mtoto wake tu , machozi yakaanza kumtoka pale alipokumbuka kwamba alikuwa mfu aliye hai.
Huo ukawa muendelezo wa mateso aliyokuwa akiyapata , mara kwa mara alikuwa akiletewa mtoto wake na kuanza kumwangalia , moyo wake ulimuuma, alikuwa akiyauma meno yake kwa hasira na kuwapa lawama zote wazazi wake na Deo ambao walimfanya kuwa hivyo .
Kila kitu kikabadilika, mtu pekee aliyekuwa akiyaangalia maisha yake ya mateso kitandani pale alikuwa Issa tu . Siku zikakatika , mwili ulizidi kukonda na vipele kuongezeka, kwa kumwangalia tu , usingeweza kubaki kimya, machozi yangekulenga na kusema kwamba Nahra alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakipitia mateso makubwa .
“ Issa, kama nitakufa , naomba umsomeshe mtoto wangu mpaka chuo kikuu , ” alisema Nahra huku akionekana kukata tamaa .“ Usijali , nitajitahidi, hata kama nitakosa fedha, nitakopa tu .”
“ Issa, nilikwishawahi kukuelekeza nyumbani, si ndiyo?”
“ Ndiyo .”
“ Utaweza kupakumbuka ?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Nafikiri nitaweza.”
“ Basi hapo ndipo utakapotakiwa kwenda endapo utapata tatizo lolote kuhusu fedha, ” alisema Nahra .
Siku hiyo aliongea kwa shida sana , ilipofika saa saba mchana, mateso aliyokuwa akiyapata kitandani yakaisha na kukata roho . Huo ukawa msiba mkubwa kwa Issa, alibaki akilia sana lakini machozi yake hayakuweza kubadilisha kitu chochote kile .
Alichokifanya ni kuelekea nyumbani kwa kina Nahra, japokuwa alielekezwa juu kwa juu lakini alifanikiwa kufika huko . Mtu wa kwanza kabisa kumpa taarifa za msiba alikuwa mlinzi wa getini, Chichi ambaye aliwapelekea taarifa wazazi wake Nahra .
“ Acha afe , tulimwambia azae na mtu mweusi , ” alisema mzee Patel , Mhindi aliyeonekana kuwa na roho mbaya . Japokuwa Wahindi wengine walipewa taarifa kuhusu msiba wa Nahra lakini hakukuwa na mtu aliyejitokeza kwenda huko , walibaki majumbani mwao wakiendelea kuyafurahia maisha.
Kitendo alichokifanya Nahra cha kukubali kuzaa na mtu mwenye ngozi nyeusi, Deo kiliwachukiza mno, hawakutaka kumuona , hawakumpenda na hata hawakutaka kuufikiria uzao wake , kwao , uzao wa Nahra ukawa ni uzao wenye laana.
Baada ya kila kitu kumalizika na Nahra kuzikwa, Issa akawa na jukumu kubwa na zito la kumlea mtoto Latifa . Kila alipokuwa akimwangalia, moyo wake ulimuuma mno kwani sura yake ilimkumbusha Nahra.
“ Wazazi wa Nahra wana roho mbaya sana , wamemkataa Nahra na uzao wake wote , ” Issa alimwambia dada yake , Semeni aliyekuwa na jukumu la kukaa na Latifa.
“ Kisa?”
“ Kazaa na ngozi nyeusi, ni hatari sana .”
Mwaka wa kwanza ukakatika na wa pili kuingia , Latifa aliendelea kukua huku uzuri aliokuwa nao ukiendelea kuonekana zaidi , ulipofika mwaka wa pili, watu wakaanza kupigishana kelele kwa kudai kwamba Latifa angeweza kuwa mwanamke mrembo kuliko wanawake wote duniani, uzuri wake ulimdatisha kila mtu .
“ Aiseee! Kama malaika!” alisema jamaa mmoja, alikuwa akimwangalia Latifa .
“ Kwani ushawahi kumuona malaika?” jamaa mwingine akauliza huku akicheka.
“ Sijawahi, lakini huyu kama malaika.”
Uzuri wa Latifa ukawa gumzo Manzese nzima , kila mtu aliyekuwa na hamu ya kutaka kumuona mtoto mzuri alikuwa akiambiwa kwenda nyumbani kwa Semeni kumuona Latifa .
Mwaka wa tatu ulipoingia , Latifa akaanzishwa shule ya chekechea . Katika shule hiyo , kulikuwa na watoto wengi kutoka uswahilini ambao walikuwa na fujo mno, ila kwa Latifa, bado ukimya wake ulikuwa ukiendelea kama kawaida.
Mbali na ukimya wake, walimu wakagundua kitu kimoja kwamba Latifa hakuwa mtoto wa kawaida, uwezo wake ulikuwa ni wa juu kabisa . Yeye ndiye alikuwa mwanafunzi wa kwanza kujua kusoma na kuandika japo kwa mwandiko mbaya .
Uwezo wake huo ukawashangaza walimu wote, hawakuamini kama kungekuwa na mtoto ambaye angeweza kufanya vitu hivyo kwa haraka kama alivyokuwa Latifa. Hata mitihani ya shuleni hapo ilipokuwa ikija, Latifa alikuwa akiongoza jambo lililowafanya walimu kumpeleka darasa lingine la juu kwani uwezo wake ulikuwa ni wa kitofauti kabisa. Kwa kifupi tungesema Latifa alikuwa ‘genius ’.
Mpaka anaanza darasa la kwanza , Latifa alikuwa mtoto mwenye uwezo mkubwa darasani , katika kila mtihani, alikuwa akifanya vizuri kitu kilichowashangaza sana walimu kwani hakukuwa na mwanafunzi aliyewahi kusoma shuleni hapo huku akiwa ana akili nyingi kama Latifa.
Mbali na uwezo wake darasani , Latifa alikuwa mtoto mrembo ambaye usingeweza kumwangalia mara moja na kuyahamisha macho yako . Mchanganyiko wake wa rangi ulivichanganya vichwa vya watu wengi kiasi kwamba wengine wakatabiri kuwa angekuwa miongoni mwa wasichana watakaokuja kuitikisa nchi ya Tanzania .
Miaka ilikatika zaidi , mpaka Latifa anaingia kidato cha kwanza katika Shule ya Wasichana ya Jangwani , uzuri wake uliendelea kuwatikisa watu wengi wakiwepo wavulana waliokuwa wakisoma katika Shule ya Wavulana Azania .
“ Kuna demu nimekutana naye , ni mkali balaa , anasoma hapo Jangwani , aisee huyo demu ni shida, ” alisikika mwanafunzi mmoja akiwaambia wenzake .
“ Yupo vipi?”
“ Mhindi si Mhindi , Mswahilini si Mswahili , ni noma.”
“ Hahaha ! Utakuwa unamzungumzia Latifa .”
“ Latifa! Latifa yupi?”
“ Kuna msichana wa kidato cha kwanza , ni mzuri ile mbaya , halafu ana akili kinoma, hakuna anayeweza kumfikia, ” alisema mwanafunzi mwingine .
Stori juu ya uzuri wa Latifa ndizo zilizokuwa zikisikika tu , uzuri wake uliendelea kumdatisha kila aliyekuwa akimwangalia. Watu wakazidi kuambiana kuhusiana na Latifa kiasi kwamba binti huyo akaanza kupata umaarufu katika shule hizo mbili .
****
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Miongoni mwa wanafunzi waliokuwa wakimpenda Latifa alikuwa Ibrahim Musa, kijana mtanashati aliyekuwa akisoma katika Shule ya Azania . Kila siku alipokuwa akisikia stori kuhusu Latifa , Ibrahim alikuwa akiusikia moyo wake ukitetemeka kwa furaha.
Mapenzi juu ya msichana huyo yakamtawala, kila alipokuwa akikaa , alimfikiria Latifa na hata katika kipindi cha kuondoka shuleni hapo, hakuwa tayari kuondoka mpaka pale alipokuwa akimuona msichana huyo .
Kwa mwaka mzima Ibrahim alikuwa akiendelea kumfuatilia Latifa, wavulana wengi walimfuata msichana huyo lakini mwisho hakukuwa na mvulana yeyote ambaye alikubaliwa.
Kila alipokuwa akiwaangalia wavulana ambao walimfuata Latifa na alipojiangalia yeye , alijiona kutokuwafikia hata mara moja. Hakuwa mvulana tajiri, alitoka katika familia masikini ambayo haikuwa na mbele wala nyuma .
Ibrahim alikuwa kama Latifa , japokuwa alikuwa kijana masikini lakini alikuwa na uwezo mkubwa darasani , katika kila mtihani aliokuwa akifanya, aliongoza kwa maksi nyingi kiasi kwamba alikuwa gumzo kwa walimu wote .
“ Nataka kuwa daktari, ila daktari bila kuwa na mke mrembo haiwezekani, Latifa atanifaa , ” alisema Ibrahim . Moyo wake uliendelea kuumia kila siku, kumfuata Latifa na kumwambia ukweli alikuwa akiogopa sana . Mwaka mwingine ukaingia na kupita , mwaka wa tatu ulipoingia , Ibrahim akashindwa kuvumilia , hakuwa tayari kujiona akiteseka na wakati kulikuwa na mtu ambaye angeweza kuyatuliza mateso yake ya moyo.
Siku hiyo alikuwa amejipanga vilivyo , alivalia nadhifu huku akiwa amevipiga kiwi viatu vyake . Aliipanga siku hii kuwa maalumu kuzungumza na msichana huyo , kumwambia kila kitu kilichokuwa kikiusibu moyo wake.
Baada ya kufika shuleni, hakutaka kutoka darasani , alivumilia mpaka muda wa kutoka . Kadiri muda ulivyozidi kwenda mbele, mapigo yake ya moyo yakawa yanaongeza kasi ya udundaji, alipenda kuonana na Latifa lakini moyo wake ulijawa hofu kubwa .
Baada ya kengele ya kutoka , moja kwa moja akaelekea nje ya shule na kusimama barabarani. Macho yake yalikuwa katika geti la shule ile ya wasichana , alikuwa akimsubiria Latifa tu .
“ Leo lazima kieleweke , siondoki mpaka nimuone, ” alijisemea Ibrahim .
Dakika ziliendelea kusonga mbele huku wanafunzi wakiendelea kutoka , alikuwa kama mtu anayewahesabu wanafunzi hao , mpaka mwanafunzi wa mwisho anatoka, Latifa hakuwepo .
“ Mmmh! Hajafika au alipita ila sikumuona ?” alijiuliza Ibrahim .
Hakutaka kuvumilia kusimama nje, alichokifanya ni kuelekea ndani ya shule ile na kukutana na walinzi, akaanza kuwauliza kuhusu Latifa, kwa sababu alikuwa maarufu, halikuwa tatizo.
“ Hauna habari nini?” aliuliza mlinzi mmoja.
“ Habari gani ?” aliuliza Ibrahim kwa mshangao.
Unajua nini kilichompata Latifa ? Usikose wiki ijayo.
“ Latifa alipata ajali asubuhi, nimesikia hali yake mbaya sana , aligongwa na gari hapo Jangwani na amepelekwa hospitalini huku akiwa hajitambui. Tetesi zinasema kwamba anatakiwa kusafirishwa kupelekwa India kwa matibabu zaidi kwani fuvu lake limetikisika , ” alisema mlinzi yule, Ibrahim akaonekana kuchanganyikiwa.
“ Unasemaje ?” aliuliza Ibrahim kwa mshtuko.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment