IMEANDIKWA NA : SHIWAWA BINASALAAN AL JABRY
*********************************************************************************
Simulizi
: Am Sorry
Sehemu Ya Kwanza (1)
Msichana mrembo mwenye asili ya Kihindi, Nahra Patel alikuwa akilia huku akikimbia kwa kasi kuelekea barabarani . Jasho lilikuwa likimtoka, alikuwa akihema kwa nguvu, alionekana kuchoka, lakini hakutaka kusimama.
Japokuwa miguuni hakuwa na viatu na alikuwa akikimbia katika sehemu zilizokuwa na miba, Nahra aliendelea kusonga mbele, cha ajabu hata miba haikuweza kumchoma na kama ilimchoma, hakuwa akisikia maumivu yoyote yale.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Machozi yalikuwa yakimbubujika mashavuni mwake, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali, hakuamini kama msichana mrembo ambaye alisifiwa na wanaume kwamba alikuwa mithili ya malaika, leo hii alikuwa amefukuzwa kama mbwa na mwanaume ambaye kila siku alimuita ‘ndoto ya maisha yake’ .
“ Deo, mimi? Hapana , kwa nini ? Nimekufanya nini?” aliuliza maswali mfululizo lakini hakupata jibu lolote.
Alipofika barabarani, akatulia chini , pembezoni kabisa mwa barabara hiyo na kuanza kulia huku akiwa amekiingiza kichwa chake katikati ya mapaja yake .
Machozi yalikuwa yakimbubujika tu , kila alipokuwa akikumbuka namna alivyokimbizwa na mwanaume aliyemchukulia kama mume wake wa baadaye, moyo wake ulimuuma mno.Hakuwa na sehemu ya kwenda na wala hakuwa na fedha . Wazazi wake hawakutaka kumuona kabisa kwa sababu alikuwa amebeba mimba ya kijana mwenye ngozi nyeusi wakati alikuwa Mhindi .
Mapenzi yake ya dhati, kung ’ang ’ania kwake kuwa na Deo ndiyo kulimfanya leo kuwa katika hali hiyo . Hapo barabarani alikuwa mtu wa kujuta tu , kila alipokuwa akikumbuka maisha aliyopitia, alibaki akimlaani Deo.
“ Ubungo buku .. .Ubungo buku , ” ilisikika sauti ya kondakta wa daladala .
Nahra akainua uso wake na kuiangalia daladala iliyosimama mbele yake , akasimama na kuanza kuifuata, alipoifikia akaingia ndani na kuondoka .
Ndani ya gari , kila mwanaume alikuwa akimwangalia Nahra kwa matamanio, alikuwa msichana mrembo wa Kihindi ambaye alikuwa na sifa zote za kuitwa ‘ Malkia Cleopatra’ . Kwa sababu ilikuwa ni usiku na gari halikuwa na taa ndani, hakukuwa na mtu aliyeyaona machozi yake japokuwa uzuri wake ulionekana.
“ Unalia nini tena Kajool ?” aliuliza mwanaume aliyekaa naye , alimuita jina la muigizaji maarufu wa kike wa filamu za Kihindi, Nahra hakutaka kujibu swali hilo , bado kilio chake cha kwikwi kilikuwa kikisikika.
Kuanzia hapo Kibaha mpaka anaingia Dar es Salaam, alikuwa mtu wa kulia tu , kumbukumbu za maisha aliyokuwa akiishi kwa Deo zilikuwa zikijirudia kama mkanda wa filamu kitu kilichomuumiza mno na kumfanya azidi kulia .
Mpaka daladala linaingia Ubungo , tayari ilikuwa saa tatu usiku , Nahra akateremka na kusimama kituoni na watu waliokuwa wakisubiri usafiri.
“ Niende wapi ?” alijiuliza Nahra, jibu lililokuja ni kwamba alitakiwa kwenda kwa wazazi wake waliokuwa wakiishi Masaki .
Baada ya dakika kumi , akapanda daladala iliyokuwa ikielekea Masaki na safari ya kuelekea nyumbani kuanza . Kama kawaida , bado alikuwa mtu wa kulia tu , kilio chake cha kwikwi hakikuisha , baada ya dakika thelathini , akafika nje ya geti la nyumba yao, akaanza kugonga .
“ Nahra, umefuata nini , baba yako ataniua , ” aliuliza mlinzi aliyefungua geti.
“ Naomba niingie , nataka kuonana na baba, ” alisema Nahra .
“ Hapana , naogopa Nahra . Siku ile alitaka kunipiga risasi, siwezi kukuruhusu , ” alisema mlinzi huyo .
“ Ninataka kuingia ndani Chichi , niache niingie nikaongee na baba yangu , ” alisema Nahra huku akianza kulia tena .
Msimamo wa mlinzi ulikuwa uleule, hakutaka kumruhusu Nahra kuingia ndani. Baada ya kulazimisha sana tena kwa kusukumana, Nahra akafanikiwa kuingia ndani ya eneo la nyumba yao. Akaanza kuufuata mlango na kuanza kuugonga.
Baada ya dakika tano, mlango ukafunguliwa na wazazi wake wote wawili kutoka ndani kwani mlango uligongwa kifujofujo . Macho yao yalipotua kwa binti yao aliyekuwa akilia huku akiomba msamaha , baba yake, mzee Patel akaonekana kubadilika , akakunja uso kwa hasira.
“ Umefuata nini hapa? Umefuata nini wewe mbwa?” aliuliza mzee Patel, Nahra hakujibu kitu, alichokifanya mzee huyo ni kurudi ndani, kama kawaida yake alikuwa ameikumbuka bunduki yake .
Mama yake , bi Aishani alimtaka Nahra aondoke kwa kuwa alijua fika mumewe alifuata bunduki lakini Nahra hakutaka kuondoka , alikuwa tayari kupigwa risasi na kufa , ila si kuondoka nyumbani kwao .

Bado msimamo wa Nahra ulikuwa palepale, hakutaka kuondoka mahali hapo, alikuwa radhi kumuona baba yake akimpiga risasi na kufa lakini si kukubali kirahisi kuondoka nyumbani kwao .
Bado alikuwa akilia , alijiona kunyanyaswa kwa kile kilichokuwa kimetokea , kitendo cha kutengwa na ndugu zake kisa alikuwa na mimba ya mtu mweusi kilimuumiza mno. Hakukuwa na mtu aliyemuelewa , hata mama yake, mtu pekee aliyekuwa akimuonyeshea mapenzi ya dhati , katika suala hilo alikuwa tofauti naye .
Mlango ukafunguliwa, mzee Patel kutoka huku mkononi akiwa na gobole , alichokifanya, huku akionekana kutetemeka kwa hasira , akamnyooshea Nahra gobole lile tayari kwa kumfyatulia risasi.
“ Niue tu , we ’ niue baba, ila jua kwamba nilimpenda Deo na nisingeweza kumuacha , kama mnaona nilifanya makosa, wewe niue kwani hata wewe utakufa tu , ” alisema Nahra , alikuwa amepiga magoti huku akilia kama mtoto .
Bila bi Aishani kulipiga gobole lile , basi risasi iliyotoka ingeweza kumpiga Nahra kifuani . Mdomo wa gobole ukaenda pembeni , risasi ikatoka na kupiga ukutani. Japokuwa mtoto wao alikuwa amefanya makosa yaliyoonekana kuwa makubwa kwa kuzaa na mtu mweusi lakini hakuwa radhi kumuona Nahra akipigwa risasi na kufa .
“ Punguza jazba, ” alisema bi Aishani huku akimsihi mume wake asimuue Nahra.
“ Usinizuie , niache nimuue huyu m ****** ametudhalilisha sana , acha nimuue, ” alisema mzee Patel huku akionekana kuwa na hasira mno.
Bado Nahra alikuwa aking ’ang ’ania kubaki mahali hapo, hakuwa na pa’ kwenda usiku huo , kama walivyokuwa wazazi wake , hata ndugu zake wa Kihindi walikuwa wamemtenga , sababu ilikuwa ni ileile ya kuzaa na mwanaume mweusi.
Mbali na ndugu zake, mwanaume aliyekuwa amempa mimba, Deo alikuwa amemfukuza nyumbani kwake . Hakutaka kuondoka mahali hapo, kama kuuawa , alikuwa tayari kufa lakini si kuondoka nyumbani kwao .
“ Chichi , mtoe huyu mbwa mara moja, ” alisema mzee Patel, mlinzi akasogea mahali hapo na kumshika Nahra, akaanza kumbeba juujuu.Japokuwa hakuwa akipendezwa na jambo lile lakini hakuwa na jinsi, alitekeleza amri ya bosi wake kwamba Nahra alitakiwa kutolewa nje kinguvu .
“ Niacheeee, nimesema niacheeee , nimesema sitokiiiiiiiii, ” alisema Nahra huku akipiga kelele .
Hiyo wala haikusaidia , Chichi akafanikiwa kumtoa Nahra nje ya nyumba hiyo . Kwa sababu mvua ilikuwa imeanza kunyesha na ardhi ilianza kulowanishwa na maji , Nahra hakujali , akakaa chini na kuendelea kulia .
Katika maisha yake yote , hicho ndicho kilikuwa kipindi kigumu kuliko vyote , hakuamini kama kweli wazazi wake walimfukuza kama mbwa kisa tu alizaa na mwanaume mweusi. Hata kama alikuwa Muhindi , akajikuta akianza kuwachukia Wahindi wote kwa kile alichokuwa amefanyiwa.
“ Sitorudi tena nyumbani na sitorudi tena kwa Deo, acha niendelee na maisha yangu , ” alisema Nahra na kisha kusimama, akaanza kuondoka .
Alitembea kwa mwendo wa taratibu, mvua kubwa iliendelea kumnyeshea na kumlowanisha lakini hakuweza kusimama sehemu kwani nyumba zote za Masaki zilikuwa za kifahari zilizokuwa na uzio mkubwa.
Wakati mwingine alikuwa akijuta kupewa mimba na Deo kwa kuwa tu jamii yake ilimtenga lakini kuna kipindi aliona kwamba hakutakiwa kujilaumu , kile kilichokuwa kimetokea , kilishatokea hivyo alitakiwa kusonga mbele.
Dakika ziliendelea kusonga mbele , mpaka anafika kituoni , tayari ilikuwa ni saa tano usiku , akakaa hapo na kuanza kusubiri gari japokuwa mkononi hakuwa na fedha yoyote ile . Baada ya dakika thelathini , daladala ndogo (Hiace ) ikasimama hapo na kupanda .
Safari ya kuelekea Magomeni ikaanza , hakuwa na ndugu yeyote lakini kitu pekee alichokuwa akikitaka ni kufika huko tu . Mawazo yalimtawala, hakujua ni sehemu gani alitakiwa kwenda kuishi.
Deo alikuwa kimya chumbani mwake, machozi yalikuwa yakimbubujika mashavuni mwake , hakuamini kile kilichokuwa kimetokea , kumfukuza Nahra nyumbani kwake kilikuwa ni moja ya kitendo kilichomuuma mno.
Alimpenda Nahra kwa mapenzi ya dhati, hakuwa tayari akimuona msichana huyo akipata tabu yoyote ile, japokuwa alikuwa msichana wa Kihindi, kwake haikuwa tatizo , alikuwa akimpenda hivyohivyo .
Wazazi wa Nahra walionekana kuwa tatizo kwake . Mara baada ya kumpa mimba msichana huyo na kuhamia kwake kwa kuwa wazazi wake walimfukuza , wazazi hao wakawatuma wanaume wawili waliokuwa na bunduki, walichokuwa wakikitaka ni kuona Deo akimfukuza Nahra nyumbani hapo, vinginevyo , wangemuua .
Huo ulikuwa mtihani mkubwa maishani mwake , alimpenda Nahra , hakutaka apate tabu yoyote ile, kitendo cha kuambiwa amfukuze msichana huyo kilikuwa kigumu, akakataa .
Watu hao walipoona kwamba kitu hicho hakikufanyika, wakarudi kwa mara ya pili, wakati huu walionekana kuwa na hasira zaidi , kila walipokuwa wakimwangalia Deo usoni, waliyakumbuka maneno ya mzee Patel ambaye aliwaambia wamuue tu .
“ Kijana , fanya tunachokwambia . Tumeagizwa tuje kukuua , hatuwezi, tunakuonea huruma. Fanya hivyo , tunakupa siku moja ya ziada, kesho tukija, tunakuja na sura tofauti , ” alisema mwanaume mmoja huku akimwangalia Deo usoni.
Kwa jinsi walivyoonekana , kwa maneno yao yaliyokuwa yakitoka midomoni mwao ilionyesha kabisa watu hao walikuwa wamemaanisha kile walichokuwa wamekiongea , Deo akakubaliana nao.
Siku hiyo usiku ndiyo ilikuwa siku ya kumfukuza Nahra nyumbani hapo. Alifanya hivyo huku moyo ukimuuma mno, kila alipokuwa akimwangalia Nahra , alijisikia huruma , moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali.

“ Nahra, naomba unisamehe, sikutaka kukufukuza, wazazi wako ndiyo waliolazimisha kufanya hivi, ninakupenda Nahra, ” alisema Deo huku akimuona Nahra akikimbia , machozi yalikuwa yakimtoka msichana huyo , baada ya hapo, hakujua Nahra alielekea wapi, usiku huo kwake ukawa wenye mateso mengi .
“ Nitamtafuta tu , ” alisema Deo huku akijipa uhakika kwamba angemuona tena Nahra aliyekuwa na mimba yake.
***
Hakuwa na sehemu ya kwenda, sehemu pekee ambayo aliifikiria kwa wakati huo ilikuwa ni katika bustani iliyokuwa Magomeni Hospitali, ambapo hapo ndipo alipotaka kupatumia kama chumba chake kwa usiku wa siku hiyo .
Alipofika mahali hapo, akatafuta sehemu ambayo kwake ilionekana kuwa nzuri na kujilaza. Usingizi ulikuwa mgumu kupatikana , bado moyo wake ulimuuma mno, machozi yaliendelea kumbubujika kila alipokuwa akikumbuka hali ya kutengwa iliyokuwa ikitokea katika maisha yake .
Usiku wa siku hiyo ulikuwa ni usiku wa shida, kutokana na sehemu hiyo kuwa na miti mingi na visima vilivyochakaa vilivyokuwa na maji , mbu walikuwa wengi na walimuuma usiku mzima lakini hakutaka kujali , aliendelea kulala .
Ilipofika alfajiri , saa kumi na mbili , alikuwa macho , akainuka na kuanza kuondoka bustanini hapo. Sehemu pekee ambayo alikuwa akiifikiria kwa wakati huo ni kwenda kwa mwanaume wa Kihindi ambaye alikuwa akimpenda ila alimkataa kwa kuwa alikuwa na Deo, huyu aliitwa Mithun.
Hakujua mwanaume huyo angempokeaje , hakujua kama angemkaribisha au kumfukuza, alitaka kujaribu na aliuweka moyo wake kukubaliana na hali yoyote ambayo ingetokea huko .Baada ya kutembea kwa miguu kwa zaidi ya dakika ishirini, akafika Kariakoo katika Mtaa wa Twiga na kuifuata nyumba moja ya ghorofa na kuanza kuugonga mlango .
Wala hazikupita sekunde nyingi , mlango ukafunguliwa, mtu aliyeufungua alikuwa mwanaume ambaye alimfuata mahali hapo kwa ajili ya kuongea naye , mwanaume wa Kihindi ambaye sura yake ilipendezeshwa na ndevu zake nyingi , alikuwa Mithun.“ Nahra.. ..” aliita Mithun huku akionekana kushangaa.
“
Naomba unisamehe Mithun, ninahitaji msaada wako , ” alisema Nahra huku akianza kulia tena , hakukuwa na kitu alichokuwa akikihitaji mahali hapo zaidi ya msaada .
“ Nahra, kuna kitu ulisahau kwangu ?” aliuliza Mithun kidharau .
“ Hapana Mithun, naomba unisaidie.”
“ Naomba uondoke nyumbani kwangu . Kwanza unanuka, una siku ngapi hujaoga? Hebu tokaaa , nenda kwa huyo Mwafrika wako na sitaki kukuona mbele ya macho yangu . Tokaaaaaa , ” alisema Mithun kwa sauti ya juu, kilio cha Nahra kikaongezeka zaidi .
Moyo wake uliumia, hakuamini kama maneno yale aliyoyasikia yalitoka kwa mtu kama Mithun, mwanaume ambaye kila siku alimwambia kwamba alikuwa miongoni mwa wasichana waliokuwa na mvuto duniani.
Mithun hakutaka kusimama mlangoni hapo, alichokifanya ni kurudi ndani na kuufunga mlango. Machozi yaliendelea kumbubujika Nahra, moyo wake ulikuwa mgumu kuamini maisha aliyokuwa akiyapitia kipindi hicho, akajikuta miguu ikikosa nguvu na kukaa chini .
Kilio kikaanza kusikika mpaka majirani waliokuwa ndani ya vyumba vyao wakatoka kuangalia ni nani aliyekuwa akiwapigia kelele , walipoona Nahra analia tu huku akiwa amefungiwa mlango, wakamwambia aondoke.
Akaiona dunia ikiwa imemgeukia , hakuona mahali ambapo angeweza kupata msaada , kitendo cha kubeba mimba ya mtu mweusi tayari kilibadilisha maisha yake kwa ujumla . Nahra akasimama na kuanza kuondoka , alipokuwa akielekea , hakuwa akipafahamu.
“ Nitakwenda wapi mimi? Bora nikajiue tu , siwezi kuendelea kuishi, ” alijisemea Nahra huku akipiga hatua kuelekea nje ya ghorofa hilo .
Huo ndiyo ulikuwa uamuzi alioufikia, hakutaka kuendelea kuishi tena , mateso na maumivu aliyokuwa amepitia yalitosha kabisa kumfunza, hivyo alitaka kujiua kwa kuamini kwamba angekwenda kupumzika.
Akaanza kukimbia kuelekea Kariakoo Relini huku lengo lake kwa wakati huo likiwa ni kwenda Mivinjeni. Hakukuwa na kitu alichokuwa akikifikiria zaidi ya kujiua tu , alitaka kuiondoa roho yake kwa kulala kwenye reli na treni kupita juu yake .
Mara baada ya kufika Kariakoo Relini, akachukua Barabara ya Kilwa na kunyoosha nayo kama alikuwa akienda bandarini. Alipofika Mivinjeni, akaanza kuelekea katika reli iliyokuwa chini ya daraja .
“ Nitajiua tu , ” alijisemea Nahra na kujibanza sehemu huku akisubiria treni ipitie na yeye kulala relini . Aliyachoka maisha yake hiyo ndiyo sababu iliyomfanya atake kujiua siku hiyo .
“ Poooooo, ” ilisikika honi ya treni ya mizigo , alipoisikia honi hiyo, akachungulia kwa jicho moja. Treni ya mizigo ilikuwa ikija kwa kasi, ilikuwa imetoka kituoni na kuanza safari yake , alipoiona treni hiyo kwa mbali , Nahra akasubiri mpaka ikaribie na ndiyo aende kujilaza relini na hatimaye aweze kufa na kuyaepuka mateso aliyokuwa akiyapata .
“ Nisamehe Mungu! Mateso yamezidi, acha tu nijiue ili wazazi wangu wapumzike, wasinichukie tena . Pia nisamehe kwa kukiua hiki kiumbe kinachojitengeneza tumboni mwangu. Mungu, sifanyi hivi kwa kupenda, najua unayajua maisha ninayopitia , ” alisema Nahra huku treni ile ikiendelea kusogea zaidi .
Nahra aliendelea kuisubiria treni ambayo ilibakisha kama hatua mia mbili kabla ya kufika pale alipotaka kujilaza. Kichwa chake kilitawaliwa na mawazo tele, alikuwa tayari kujiua lakini si kuendelea kuishi kwa mateso kama aliyokuwa akiishi.

“ Bora nife tu , sina haja ya kuendelea kuishi, ” alisema Nahra .
Kifo ndicho kilichokuwa kikifikiriwa kichwani mwake, moyo wake uliona kwamba endapo angejiua basi angeweza kwenda kuishi kwa amani katika sehemu nyingine tofauti na alivyokuwa akiishi duniani.
Baada ya sekunde kadhaa, treni ilikuwa mbali kama hatua mia moja, alichokifanya Nahra, akakimbilia relini na kujilaza . Machozi yalikuwa yakimtoka, hakuamini kama maisha yake yote aliyokuwa akiishi , mwisho wa siku alikuwa amefikia hatua ya kujiua .
“ Nisamehe Mungu, sikupenda kujiua, ila sina jinsi. Acha nife na mwanangu aliyepo tumboni , ” alisema Nahra , treni ya mizigo ilikuwa ikija kwa kasi na ilibakisha hatua arobaini tu za miguu ya binadamu kabla ya kumkanyaga. Muda wote treni ilikuwa ikipiga honi lakini Nahra hakutoka relini , alidhamiria kujiua kwa kukanyagwa na treni hiyo.
ILIPOISHIA..
Treni ya mizigo ilikuwa ikija kwa kasi , Nahra aliyafumba macho yake , uamuzi aliokuwa ameuchukua kipindi hicho, ulionekana kuwa wa muhimu kuliko kitu chochote kile. Treni ilikuwa imebakiza umbali wa hatua hamsini za miguu ya binadamu kumfikia .
ENDELEA. ..
Machozi yalikuwa yakimbubujika Nahra , treni ya mizigo ilikuwa ikiendelea kusogea kule alipokuwa amejilaza . Hakujuta moyoni mwake kwa hatua aliyokuwa ameifikia , kwa wakati huo , kifo, kwake kilionekana kuwa muhimu zaidi ya uhai .
Huku treni ikiwa imebakiza kama hatua thelathini za miguu ya binadamu na huku Nahra akiendelea kulala relini pale na macho yake yakiwa yamefumba, ghafl akashtuka akishikwa mikono na kuanza kuvutwa.
Akayafumbua macho yake kuangalia ni nani aliyekuwa amemshika . Macho yake yakatua kwa kijana mchafumchafu, aliyevalia pensi ya jinzi chakafu huku mdomoni akiwa na sigara .
Kwa kuwa yule mwanaume alikuwa na nguvu na Nahra hakuweza kupingana nazo , akajikuta akitolewa katika reli na treni kupita kwa kasi .
“ Unataka kujiua?” aliuliza jamaa yule huku akimwangalia Nahra kwa mshangao.
“ Ungeniacha nife , sitaki kuishi, naomba uniache nife, ” alisema Nahra wakati akilia kama mtoto huku akitaka kurudi relini .
“ Kuna nini tena ? Mbona msichana mrembo unataka kujidedisha? aliuliza kijana yule huku akimwangalia Nahra usoni.
Kwake, Nahra alionekana kuwa mzuri kuliko mwanamke yeyote aliyewahi kumuona machoni mwake, kitendo cha kutaka kujiua kilimshtua mno, hakuamini kama msichana mzuri kama alivyokuwa alipaswa kujiua .
Nahra hakusema kitu, alibaki akilia tu . Bado moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali , kiu ya kutaka kujiua iliendelea kubaki moyoni mwake. Lawama zake zote zilikuwa kwa mwanaume huyo aliyemtoa relini , hakujua ni aina gani ya maisha aliyokuwa akiyapitia , hakujua ni jinsi gani moyo wake ulikuwa kwenye chuki kubwa dhidi ya ubaya aliokuwa ametendewa na wazazi wake na hata ndugu zake.
“ Kuna nini Mhindi wewe?” aliuliza mwanaume yule.
“ Nataka kufa .”
“ Kwa nini? Umechoka kula ugali ?”
“ Hapana kaka , nataka kufa .”
“ Hebu kwanza tutoke hapa, unaweza kuniletea msala, ” alisema mwanaume yule na kuanza kuondoka mahali pale .
Wakatoka sehemu ile karibu na reli na kwenda juu kulipokuwa na daraja ambapo walivuka na kuanza kutembea pembezoni mwa Barabara ya Kilwa huku wakielekea Kariakoo Relini.
“ Kuna kitu gani kinaendelea?” aliuliza mwanaume yule.
Hapo ndipo Nahra alipoanza kusimulia kile kilichokuwa kimetokea maishani mwake toka alipoanza kuwa na mahusiano na Deo, alipofukuzwa na wazazi wake na hata ndugu zake ambao hawakutaka hata kumuona .
Historia ya maisha yake ilimshtua mwanaume yule aliyejitambulisha kwa jina la Issa , naye akajikuta akianza kuwachukia Wahindi . “ Kwa hiyo hauna pa’ kuishi?” aliuliza Issa .
“ Sina. Sina chochote katika maisha yangu. ”
“ Basi poa , kama vipi wapotezee tu , twende tukaishi gheto kwangu , ” alisema Issa. “ Unaishi wapi?”
“ Tandale Kwa Mtogole.”
“ Mmmh!”
“ Nini tena ?”
“ Gari unapandia wapi ?”
“ Hahah! Hapa hakuna gari , tunakwenda kwa ngondi tu , tunazama hapo mbele , tunaibukia Jangwani , tukizama tena Magomeni , tunaibukia Tandale, dakika tano tu , tupo gheto , ” alisema Issa huku akicheka.
Kutoka katika maisha ya fedha aliyokuwa akiishi, leo hii , kila kitu kilikuwa kimebadilika . Japokuwa Issa alionekana kijana mhuni asiyekuwa na chochote, lakini hakutaka kukataa kwenda kuishi kwake . Hakuwa na kitu, huyo Issa aliyeonekana kuwa mhuni , kwa matatizo aliyokuwa nayo , kwake alionekana kuwa msaada mkubwa .

Walichukua zaidi ya dakika thelathini, wakafika nyumbani hapo. Chumba kilikuwa shaghalabaghala, hakukuwa na mpangilio hata mmoja, kilionekana kwamba kwa zaidi ya mwezi mzima hakukuwa na usafi wowote ambao ulifanyika ndani ya chumba hicho .
Nahra akashusha pumzi ndefu, muonekano wa chumba kile ulionekana kumchosha mno. Aliyaonea huruma maisha yake , hakuamini kama kuanzia siku hiyo , mwanaume huyo aliyekuwa radhi kumsaidia tayari alikuwa amemkaribisha ndani ya chumba chake kisichokuwa na mvuto wowote ule.
“ Hapa ndiyo gheto , karibu sana mrembo , ” alisema Issa huku akiachia tabasamu pana.
“ Mmmh! Kuzuri , ” alisema Nahra, harufu mbaya ya chumbani mle , ikaanza kuiumiza pua yake . Hilo wala hakujali sana , alichokuwa akikihitaji ni sehemu ya kuishi tu .
ITAENDELEA

0 comments:
Post a Comment