Simulizi : Anti Ezekiel
Sehemu Ya Tatu (3)
SOTE tulitazamana bila shaka kila mmoja akiwaza lake juu ya kinachoendelea.
“Kwa hiyo baba alikuwa anasema ukweli juu ya Michigani eeh!!” alijisemea nami nikamuunga mkono kuwa kuna uwezekano mkubwa sana kuwa mzee wake alikuwa sahihi juu ya ubaya wa Michigani japo hakuwa anaweza kuielezea vizuri.
“Mwanangu Justin jamani. Kwa hiyo wamemuua ama?” aliniuliza kana kwamba mimi ni wakala wa hiyo Michigani na ninajua kila kitu. Sikumjibu kitu akaendelea kuzungumza na nafsi yake!!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilitumia fursa hiyo kumweleza juu ya mazungumzo baina yangu na mama. Nikamweleza ukweli juu ya namna alivyopotea anitha, na nikafikia hatua ya kumweleza hata zile picha alizonitumia Anitha kabla hajakamatwa na yeyote yule ambaye mimi simfahamu.
“Picha ya mtoto?? Picha ya mtoto kama huyo usemaye ilikuwa inapatikana maeneo fulani ndani ya Michigani, sasa ukiniambia kuwa Anitha alikamatwa ama alipotelea eneo hilo nashindwa kukuelewa maana miezi tisa iliyopita Michigan iliteketea” Jojina alinijibu baada ya kumweleza juu ya picha katika barua pepe aliyonitumia Anitha kabla hajakamatwa na watu waliovaa suti nyeusi!! Wawili nyuma yake na wawili mbele yake!!
Majibu ya Jojina yakasababisha jambo tunalolifanya liwe kama mchezo wa maigizo usiojulikana wapi unaanzia na wapi unapoishia.
“Kwa hiyo hapa mjini hakuna tena sehemu kama hii!!”
“Haipo kwakweli ujue sambusa zangu napeleka kila kona ya mji lazima ningekuwa nafahamu picha hiyo!!” alinijibu kwa kujiamini.
Hayo yakawa mazungumzo yetu ya mwisho kabla kimya hakijatanda na kila mmoja kusinzia!!
****
Asubuhi nilikuwa nimeamka na wazo kichwani!! Nikamshirikisha Jojina akanielewa bila shaka naye akaunga mkono!!! Kwa sasa na yeye alikuwa mhanga katika mambo niliyokuwa napitia, Jojina aliamini kuwa ni kweli mtoto wake naye alichukuliwa katika tetesi za Michigani na mazingaombwe yake.
Akaamua kuungana rasmi na mimi huenda njia nitakayopitia inaweza kuwa suluhu yake pia.
Lililomhamasisha zaidi ni suala la mimi kumuona Dulla ambaye alikuwa mpenzi wake akiwa hai!! Wakati alidhani kuwa ni marehemu.
Majira ya saa moja asubuhi tulikuwa ndani ya basi kuelekea mjini Morogoro!! Tulitaka kuwashuhudia hao viumbe ambao walikuwa wakingojewa nyumbani kwetu kwa ajili ya kuuleta mwili wangu tayari kwa maziko, mwili ambao unasadikika kutokuwepo tena na sasa walikuwa wakija na taarifa tu rasmi kwa wazazi wangu!!
Nilikuwa nimejivika kofia kubwa kama kawaida kuificha sura yangu!!
Majira ya mchana tulikuwa Morogoro tukipata chakula katika mgahawa usiokuwa na mlundikano wa watu!! Baada ya hapo kwa mwendo wa miguu tukaanza kupita mtaa mmoja hadi mwingine tukipatafuta kwa hadhari kubwa nyumbani kwetu nilipozaliwa. Hapakuwa mbali sana kutokea stendi ya Msamvu, hivyo ilituchukua dakika chache tu kuwasili katika eneo lile.
Tuliukuta umati mkubwa ukiwa pale nyumbani, nilisikitika sana kuona kuwa wale watu wote wamelishwa sumu na kuamini kuwa mimi nimekufa na huku nikihusika na mauaji na pia nikihusika katika kulawiti.
Lakini huenda umati ule ulijazwa zaidi na tukio la msafara wa kuleta maiti yangu nyumbani kupata ajali na kisha mtu mwingine kufa huku jeneza likiingia katika korongo na maiti kutoweka.
Nilifanikiwa kuwaona watu wawili ambao nilikuwa nafahamiana nao. Wote walikuwa waandishi wa habari!! Nilijisikia kwenda kuwasalimia lakini hofu ya kujizulia mambo magumu zaidi ikanikwamisha.
Jojina alikuwa makini kabisa kuangaza huku na kule, nia ya kuja naye pale ni kupata uhakika iwapo hiyo Michigani ni kweli inahusika na mikasa yote tunayopitia na tuliyopitia ama Michigani ni kitu kingine.
Iwapo atamuona mtu yeyote ambaye awali aliwahi kumwona Michigani nilimsihi anijuze kwa wakati ile tujue nini cha kufanya.
Namba yangu ya simu ilikuwa nyingine tena na aliyeitambua alikuwa ni Jojina pekee. Tulipoufikia umati tukatengana, kila mmoja akaenda upande wake huku tukipeana ahadi kuwa baadaye tutakutana kwa ajili ya kupeana taarifa juu ya nani kaona nini.
Zaidi ya wale waandishi wa habari kadha wa kadha watu wengine niliofanikiwa kuwaona ni ndugu wa karibu, lakini wao hawakunitambua!!
Nililiona kundi la watu likimuhoji mama yangu, aina ya nywele zao ilinipa majibu mara moja kuwa wale ni askari. Mama alikuwa anafanya viapo mara kwa mara, bila shaka kuna swali walikuwa wanamuuliza na kila alivyojibu wanadhani anadanganya.
Swali gani jingine kama si juu yangu??
“SAA MBILI USIKU, GIRAFFE HOTELI CHUMBA NAMBA 18 NITAACHA WAZI INGIA KWA TAHADHARI KABATINI”
Ulikuwa ujumbe kutoka kwa Jojina. Nikausoma na kuuelewa.
Hoteli ile ilikuwa inajulikana sana hivyo sikuhangaika, nikajihesabia mida hadi ukafika huo wakati. Roho ilikuwa inadunda na kuhisi kusalitiwa lakini kwa sababu niliamua kumuamini Jojina nilipiga konde moyo.
Nikaanza kwa kuupenyeza umati hapa na pale hadi nikafika mahali mama yangu ameketi peke yake chini ya mti akilia kwa maumivu makubwa!!
Nilimgusa begani akageuka lakini sikuifunua kofia.
“Mama mimi Sam, usionyeshe dalili za kushtuka!!!” nilimwambia kwa utulivu, lakini kama kawaida ya wanawake nimemsihi atulie yeye akasimama wima.
“Mamaaa!!” nilimsihi, akabonyea tena chini.
“Usijishughulishe na mimi wakati huu tunapoongea.” Kweli akatazama mbele.
Nikamweleza kwa ufupi sana juu ya wakati ambao ninapitia, nikamwomba aniombee sana kwa Mungu!! Sikumjibu maswali yake yote, lakini nikamweleza kuwa naenda kulala na siku inayofuata nitamtafuta tuzungumze.
Nikampatia mkono wangu, akajikumbushia mazoea yake ya miaka nenda rudi!!
Akaubusu!!
Nikaondoka.
Muhudumu alikuwa anakula wakati mimi naingia pale ndani, akajiweka sawa aweze kunisikiliza. Nikaulizia vyumba akanieleza kuwa vipo, nikamsihi anipatie chumba upesi, akafanya hivyo.
Baada ya malipo nikapewa funguo wangu !!!
Badala ya kwenda chumbani kwangu, nikaenda chumba namba 18. Kweli nikalikuta kabati kubwa kabisa. Nikafungua na kuingia ndani yake.
Nikajipekua na kukuta dhana zangu kadhaa nilizonunua kabla ya kuingia pale zikiwa sawa.
Kisu kidogo na nyembe kadhaa kwa ajili ya kujilinda!! Iwapo litatokea lolote.
Likakatika saa la kwanza lakini la pili halikukatika mara wakaingia wanaume wanne mle ndani. Kupitia kitundu kidogo nikawa nawatazama, kabati lilikuwa limefungwa kwa ndani na funguo nikiwanayo mimi.
“Huyu mwanamke kumbe aliacha wazi, yukwapi kwani?”
“Analewa huko nimemwacha!!” ilijibu sauti nene kutoka kwa mtu mwenye kipara, sikuweza kuwaona vyema.
Waliketi na kuanza mazungumzo palepale.
Mwongeaji mkuu akiwa mwenye kipara!!
“Dulla eeh huu ujio wa ghafla ni kwako mshkaji wetu, na ishu ni moja tu, wanawake Dulla angalia wasije wakakuponza tena, huyu mwanamke huyu we unadai anakufahamu sijui, angalia Dulla wasije majamaa wakakutoa muhanga. Si unajua huyo bwege mwandishi amemvuruga kabisa bosi sasa hivi na haoni hatari kuua. Sasa wewe endekeza mambo ya wanawake halafu mwisho wakuchomeshe jamaa akumalize. Usije ukasema hatukukwambia, kama unaona tunaingilia uhuru wako Dulla sawa lakini kama unajipenda acha hizi mambo.” Alizungumza kwa sauti ya chini wenzake wawili wakawa wanatikisa vichwa kukubaliana naye.
“Yaani ipo hivi sawa huyu mwanamke hatoki humu ndani, nd’o mwisho wake sifanyi ujinga tena kama wakati ule wa Michigani ya juu ile.” Aliposema kauli hii vicheko vikatawala kisha maongezi ya hapa na pale. Kabla yule msemaji hajaingiza maongezi mengine.
“Hivi huyu bwege wa kujiita mwandishi hajui kuwa atakufa kifo kibaya sana akicheza. Yaani angezijua hasira za jamaa dah bora hata ajinyonge kuliko kuingia mikononi mwa bonge waiti.” Alisema kwa masikitiko bwana mwenye kipara, kisha akainama na hapo nikaweza kumwona Dulla. Alikuwa ni yuleyule mtekaji wa mke wangu.
“Mkewe anaipata suluba aisee hadi huruma. Halafu yule msaidizi akajifanya kumtetea siku ile kaambulia vinao na matusi, Bonge waiti ni habari nyingine jamani.” Dulla alizungumza, na baada nya hapo ikasikika hodi mlangoni. Sauti ya kilevi.
“Oya Malaya wako huyo, hakikisha unafanya tulivyozungumza Dulla. Anakujua sana huyu demu.” Kipara alimnong’oneza Dulla na maneno yale yakaonekana kumuingia.
Mlango ukafunguliwa, wale mabwana watatu wakatoka nje na ndani akabaki Dulla, kisha akaingia mama lao. Alikuwa amelewa chakari kimtazamo, aliyumbayumba huku akiimba nyimbo anazozijua yeye mwenyewe. Niliendelea kuyatazama haya yanayoendelea huku nikijiuliza juu ya Michigani na mkasa unaoendelea.
Bonge waiti!! Huyu ni nani katika mlolongo huu wa kustaajabisha!!
Taa haikuzimwa na jicho langu likaendelea kushuhudia mambo machafu kusimulia kati ya Dulla na Jojina. Lakini nililazimika kutazama huku nikichukua tahadhari nisije kugusa chochote kile ambacho kinaweza kutibua mipango yetu.
Ni vyema kuwa niliendelea tu kutazama kinachoendelea, maana ningeacha na kuona aibu huenda lingetokea baya na kisha nikajutia muda wangu!!
“Jojina, ujue nakupenda sana.”
“We wala hunipendi na kama unanipenda mbona ulinikimbia.” Alijibu Jojina kilevilevi.
Dulla akamtazama yule mwanamama jinsi anavyosinzia na hapo nikamuona akichukua mto, akawa anasitasita lakini hatimaye akaushusha na kuufunika uso wa Jojina kisha akaukandamiza.
“Jojina lazima ufe ili niendelee kuishi kwa amani nisamehe…nisamehe inanibidi tu kukuua kabla mimi sijauwawa.” Alisema huku akiwa anauma meno yake.
Akili ikafanya kazi harakaharaka, mikono ikiwa inatetemeka nikauzungusha funguo, na kisha kulikanyaga kabati kwa nguvu. Dull hakujiandaa kuupokea mshtuko huo, akaacha mara moja kile alichokuwa anafanya na sasa akawa anatazamana moja kwa moja na mtu ambaye yeye binafsi anaamini kuwa ni dhaifu na huenda alijinyonga tayari.
Mama lao alikuwa akihema kwa nguvu huku akikohoa bila kikomo.
Sikumpa nafasi ya kuzubaa zaidi, nikajirusha na kumkaba huku nikivuta picha ya mke wangu na mwanangu mpenzi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Wewe wewe!!” alianza kunisonta kwa kidole chake. Lakini sikutishika nikajivuta nyuma na kumwangushia kichwa kimoja, akatokwqa na yowe la uchungu, nikataka kumpiga ngumi lakini akaniwahi akanikanyaga teke la tumboni.
Kisha zikafululiza ngumi mbili tatu, nikaanza kuona mawenge!!
Lakini zile zikawa ngumi za mwisho. Ikajha ile sababu ya muhimu kabisa niliyokuwa naingoja ya Jojina kuitwa mama lao!!
Nikiwa chini nikamuoa akimnyanyua Dulla juu juu. Kisha akamnasa vibao kama mtoto mdogo, na mkong’oto uliofuata pale ni yeye pekee anaweza kusimulia maumivu iwapo angepata nafasi ya kusimulia.
Lakini hakupata nafasi hiyo!!
“Justin yuko wapi?” aliuliza kwa jazba huku akiwa amemuunganisha Dulla mikono yake vyema.
Mama lao alikuwa mama kweli!!
Dulla akaanza kujiumauma, mama Lao akamweka sawa kisha akatuliza kisigino chake katika korodani za Dulla. Yowe likamtoka na mimi nikasisimka.
“Unasema ama husemi wewe mpumbavu.” Alifoka mama lao.
“Sijui alipo sijui chochote dear, mimi ni kibaraka tu nisamehe…”
“Kwanza koma kuniita dear, wewe kibaraka wa nani?”
“Bonge…bonge waiti…..”
“Nd’o nani na yupo wapi na ni shughuli gani mnajihusisha nayo?” alimbana swali.
Dulla badala ya kujibu akajitoa katika himaya ya Jojina na kujaribu kujitetea huku na kule.
Jojina alikuwa macho haswa, mimi binafsi sikujua nimekidondosha kile kisu muda gani lakini yeye alikikwapua kutoka kilipokuwa, Dulla akajikuta akigumia kwa maumivu, kisu kikiwa kimezamishwa mgongoni!!
“Hivi unajifanya umafia wangu umeusahau eeh!!” sasa alizungumza huku akikizungusha kile kisu kama akayechokonoa.
Mama lao alikuwa katili haswa!!
Dulla alikuwa anapiga kelele lakini zote ziliishia katika kiganja cha mama lao. Alikuwa amemziba vyema.
Maumivu aliyokuwa akiyapata hata wewe unaweza tu kuyakadiria!!
Mashuka yalikuwa yanazidi kuwa mekundu na mama lao hakujali hayo. Sura yake ilikuwa imechafuka kwa ndita zilizotangaza hasira.
“Justin mtoto wangu yupo wapi?” aliuliza tena kisha akamwacha Dulla azungumze.
Lakini hakuzungumza na badala yake alianguka na kupoteza fahamu!!!
“Bwege atatiharibnia akizinduka shenzi kabisa anazo picha zangu niliwahi kumpa.” Alisema Jojina kisha akafanya nisichotarajia.
Akazamisha kisu katika upande wa moyo wa Dulla.
“Kalale kwenye moto wa jehanamu muuaji mkubwa wewe.” Alisema kwa hasira. Kisha akasimama kitandani akavua nguo zake zote zilizolowana damu.
Akauendea mkoba wake akachukua nguo nyingine akavaa.
“Twen’zetu!!” alisema na hapo tukatoka nje.
Jojina akiyumba kama mlevi!!! Na hapo nikapata jibu kuwa kumbe hakuwa amelewa bali alikuwa mtaalamu katika kuigiza.
Nilimtazama kwa wasiwasiu mkubwa, sikujua kama anaweza kuwa jasiri kiasi hiki mwanamama huyo.
Alimpataje Dulla? Na alimshawishi vipi hadi kumuamini tena??
Hayo yalikuwa maswali niliyotarajia kumuuliza tukishafika nje ama kwenda popote pale na kuwa huru!!!
“Sam, najua unajiuliza tunaanzia wapi eeh!! Usijali mpenzi wangu, mimi naifahamu Iringa vyema. Na kama kweli kuna kitu kibaya huko michigani nitajua tu!! Nakuhakikishia kuwa kama mwanangu mimi Justin, mwanao, mkeo, na Anitha wako salama basi watatoka salama. Hukuwahi kujua kwanini naitwa mama lao, lakini utajua hatua kwa hatua…” aliniambia huku akinibinyabinya kiganja cha mkono wangu
***JIFUNZE: Hakuna mwanamke aliyehifadhi tumboni mwake, Malaya, jambazi ama muuaji.. kwa miezi tisa kisha akamzaa.
Mazingira nd’o huzaa tabia hizi, mwanadamu huongozwa na mazingira na nyakati. Katika maisha yetu kuna nyakati zinakuja na kutulazimisha kusema uongo ilimradi tu kukomboa kitu flani, na zinakuja nyakati za hasira na chuki na kutusukumia dhambini.
Ni kumwomba mungu tu atupe mioyo ya ujasiri sana!!!
Nilibaki katika mshangao kwa muda nikiendelea kujiuliza yule mwanamke ni wa aina gani. Awali nilidhani kuwa ni msema sana tu kutokana na haiba aliyoionyesha siku tulivyosafiri naye kutokea jijini Dar es salaam, mara ya pili tukakutana naye akiwa anauza sambusa na bajia, hapa akazidi kunishangaza lakini ninazidi kumfahamu.
Sasa namtambua kama mama lao!!
Hakika alikuwa mama lao!!
“Mabwege wamelewa wale hawajui kama mwenzao kajifia huko ndani shenzi kabisa!!!” Jojina alizungumza kama anayesema mwenyewe, nikageuza shingo na kuwaona wale jamaa waliovaa suti waliokuwa wakimsihi Dulla amuue Jojina. Kulingana na mavazi aliyokuwa amevaa Jojina, mavazi tofauti kabisa na yale aliyokuwa amevaa awali, ilikuwa ngumu kwa mtu yeyote kuweza kumtambua. Kasoro mimi tu!!
“Sam, umeyaokoa maisha yangu! Sikutarajia kama ungeweza kushawishiwa na ujumbe ule mfupi niliokutumia ukajileta kichwa kichwa katika chumba kile!! Vipi tungekuwa tumepanga kukuua labda, ama vipi ungegundulika kuwa upo ndani ya chumba kile!!
Umekuwa jasiri sana kujileta katika mdomo wa kifo bila hofu. Na sit u kujileta katika mdomo wa kifo, bado ulikuwa jasiri ulipoona yule bwana anataka kuniua hukuvumilia ukatoka ndani ya maficho na kumkabili. Ni wanadamu wachache sana wawezao kujihatarishia maisha yao kama wewe ulivyofanya.” Jojina alikuwa akininong’oneza kwa sauti ya chini huku akinivutia katika kifua chake. Tulikuwa nyumba ya kulala wageni tayari.
Nilimjibu kizembezembe huku nikijifanya usingizi umenitawala, nikambusu midomo yake kisha nikageukia upande wa pili nikimwacha jojina akipitisha mikono yake kutokea mgongoni mwangu na kisha kuiunganisha kwa mbele!! Akanikumbatia.
****
ASUBUHI majira ya saa nne, tulikiachia chumba. Mama lao akiwa amevaa kama alivyokuwa amevaa usiku uliopita huku mimi nikiwa nimebadili na kuvaa kaptula na fulana kubwa, kichwani nikiwa na kofia kama ilivyo kawaida tangu niingie matatani.
Safari yetu ilikuwa ya kuvizia maeneo ya nyumbani kwetu ili tuweze kujua ni kitu gani kinachoendelea, tulitambua fika kuwa lazima taarifa juu ya kifo cha Dulla zilikuwa zinafahamika kwa wenzake na kama kuna lolote litakuwa limeendelea basi mwanzo wake ni pale msibani.
Tuukuta umati mkubwa tofauti na siku ya kwanza, jambo hili halikuwa la kawaida hata kidogo, ni kweli msiba huu ulikuwa na utata ndani yake lakini haukuwa utata wa kuvuta umati mkubwa kiasi kile.
Tukajichanganya katika makundi kwa tahadhari kubwa!!
Jojina alikuwa wa kwanza kuchezwa machale, akiwa amevalia wigi kichwani lililombadili sura yake alinivuta katika kundi fulani kisha tukawapa migongo kama hatuna habari nao.
“Hawa polisi walichofanya ni uonevu, haiwezekani mara amekufa mara msafara umepata ajali, sasa wanasema sijui kuna wadau wake mama yake anawajua??? Huu ushenzi huu!! Mama ambaye hata Dar hajawahi kwenda anajua nini sasa.” Alilalamika bwana mmoja, nikageuka kumtazama sura ilikuwa ngeni.
“We! Bora tu unyamaze maana hii serikali yetu hii ukionekana tu unatetea jambo basi. Chanzo eti jana pale mazikoni mama amekataa kata kata kuwa mtoto wake ajafa na siku ile usiku alipopiga mayowe kuwa ameisikia sauti ya mwanaye. Hapo tu nd’o tatizo likaanzia siku aliyodai kuwa amemsikia kesho yuake nadhani nd’o ikatokea ajali. Kwanini serikali isikubane isitoshe huyu mwenyekiti wa mtaa ana chuki binafsi na familia ya marehemu.” Alinong’ona kijana mwingine na yeye sikuwa nikimfahamu. Maongezi yao yakanipa mwanga kuwa mama yangu alikuwa matatani.
“Sam…jikaze usipaniki utaharibu!!” Jojina aliwahi kugundua azma yangu maana kuna chembechembe za wazimu zilianza kunipanda kichwani na kujisikia nikikabiliwa na mzimu wa lolote na liwe. Ni heri Jojina aliniwahi kisha akanishika mkono na kunitoa mahali hapo.
Mama yangu alikuwa kila kitu kwangu!! Almanusura nimponyoke Jojina na kukimbia lakini ukakamavu wake aliweza kunihimili, sikuweza kufanya lolote.
“Sam, unatakiwa utambue kitu kimoja. Tupo katika mapambano ambayo hakuna ajuaye tunapambana. Hatuna msaada na jeshi letu linazidi kuporomoka, ameondoka Anitha, Mama Eva, Mzee Matata sijui, sasa ameondoka mama, ukiiruhusu akili yako kujikita katika wazimu basi ujue kuwa nitabaki peke yangu!! Siwezi kupambana peke yangu Sam siwezi hata kidogo, wewe ukiharibu tu tambua kuwa utajikuta umefungwa kamba wewe, Anitha, mama, Eva, mama Eva na mimi pia halafu nani wa kumfungua mwenzake, ama nd’o unataka kuanza kumlilia Mungu ilihali amesema jisaidie nami nitakusaidia, unataka kujiingiza katika janga maksudiu. Janga ambalo mwanga wake tumeanza kuuona, tunatambua kuwa kuna Michigani, tunajua kuhusu Anti Ezekiel kiasi fulani, tunalo la kusema kuhusiana na kindo. Halafu wewe unataka kuharibu.
Sam kwa jinsi walivyokusaka kwa muda mrefu nadhani unajua kuwa wakikukamata ……wakikukamata Sam. Si umezikwa kiuongouongo, wale watakuzika kweli. Mbaya zaidi Sam, hawa watu akina Bonge waiti wanaonekana kukubalika samba serikalini kwa lolote lile wanalodanganya. Sam unatakiwa kuwa imara, ni mimi na wewe iwapo hatatokea mwingine wa kutuunga mkono tunalo jukumu la kumwokoa mama, Eva, mama Eva, Justin kama yupo hai mwanangu, Anitha na wengine wote wenye haki.” Jojina alinieleza haya kwa hisia kali. Kila mstari wa neno lake ulikuwa ni fimbo inayoumiza, aliusema ukweli mtupu. Nikapepesa macho nisitazamane naye usoni lakini yeye alizidi kunikazima macho ili maneno yaniingie.
Jojina!! Jojina alikuwa Anitha mwingine!!
“Nimekuelewa sana dada yangu!!” niliamua kukubali yaishe.
“Tunaondoka dakika hii kuelekea Iringa ama popote pale lakini sasa hivi tunaondoka tukiwa na lengo moja tu kuitafuta Michigani popote ilipo, kumtafuta Bonge waiti kama kweli yupo, tunaondoka kwenda kuisaka amani!!!” alizungumza katika namna ya kuamrisha sasa hakunitazama machoni.
Nikatii!!CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tukaongozana mpaka stendi, bahati nzuri magari ya kuanzia safari Morogoro kwenda Iringa yalikuwepo mengi tu.
Tukaingia katika basi lililokuwa linakaribia kuondoka!!
Dakika kumi baadaye likaanza safari. Tulikuwa tumepata siti mbili za mwisho nyuma kabisa!!
Hatukujali kuhusu hilo. Kama kawaida tukaandikisha majina ya kughushi!!
Kimya kilitanda, hatukusemezana chochote kile. Kwa takribani dakika thelathini, sijui Jojina alikuwa anafikiria nini, lakini mimi nilikuwa nawaza juu ya Kusadikika iitwayo Michigani, mahali palipovunjwa na kuteketezwa sasa tunapatafuta, nikamuwaza pia Ezekiel wakati huu nikimfananisha na mzimu wa ajabu uliojileta katika maisha yangu!!
Ezekiel! Ezekiel asiyejulikana! Aidha yu hai ama amekufa.
Dakika chache baadaye gari likasimama na kuegesha pembeni.
“Kuchimba dawa mapema hivi!!” hatimaye Jojina akatokwa na neno la kwanza.
“Vibofu havifanani aisee.” Nikamjibu kiutani, akatabasamu.
Lile tabasamu halikudumu sana, akataka kusema neno lakini akaishia kutanua tu mdomo na asiseme chochote.
Sikujua nini kimemsibu.
Baada ya sekunde kadhaa sikuwa na haja ya kuuliza tena kulikoni!!
“Iwapo unajua kuwa umeandikisha jina lisilokuwa lako katika tiketi yako, jisalimishe mapema kabla haujapekuliwa!! Narudia tena, iwapo unajua umeandikisha jina lisilokuwa lako katika tiketi uliyonayo tafadhali ndugu jisalimishe mapema nje ya basi kabla upekuzi haujaanza!!” sauti kali ya kiaskari iliamrisha.
Jojina alijisajiri kama Prisca na mimi nilijisajiri kama Rama.
Majina feki!! Mungu wangu!! Kuna nini tena?
Nilimtazama Jojina alikuwa akijaribu kujificha asionekane kama anayeshangaa, lakini macho yangu yalipotua katika kifua chake niliweza kushuhudia jinsi moyo wake ulivyokuwa unadunda kwa kasi.
Sote tulikuwa tumepagawa, hasahasa mimi ambaye sura yangu ilikuwa takribani katika magazeti yote nchini. Vipi wakiniona hawa maaskari. Bila shaka nd’o safari ya jela na kifo moja kwa moja.
“Sam, zama chini zama wajinga watakagua, ingia nitakufukina na sketi yangu fanya fasta.” Jojina alininong’oneza. Sikungoja zaidi maana kama ni hatari tayari tulikuwa hatarini.
Nikazama chini wakati abiria wengine wakiwashangaa askari waliokuwa wakitoa lile tangzo na wengine wakijishughulisha katika kujisalimisha mbele.
Nikajibana na hatimaye Jojina akatanua miguu nikawa chini ya himaya ya miguu yake miwili, joto kali likanitoa jasho lakini bora joto, jinsi nilivyojibana chini ya viti vile niliumia sana mgongo!! Miguu ya Jojina ilikuwa inatetemeka haswa.
Tulikuwa matatani!!
“Wanakagua tiketi Sam. Omba Mungu sana” Jojina aliinama na kunong’ona nikamsikia lakini sikujibu, akazidi kutetemeka.
Zikapita dakika kadhaa akanong’ona tena.
“Sam wanayo picha sijui ni picha ya nani, hawakagui tiketi mafala hawa wanakagua sura Sam. Ni hatari Sam” Jojina akazidi kunitia hofu.
Niliendekea kudumu katika hali ile bila kujitingisha wala kukohoa. Hofu niliyokuwanayo katika mazingira haya ilikuwa mara kumi ya hofu ya siku moja iliyopita nilipokuwa kabatini nikiwasubiri akina Dulla, na hofu hii ilizidi ile hofu ya kumuona Jojina akiua mtu.
Wakati naitafakari hali inayonikabiri nmara nikaisikia sauti ya Jojina tena, safari hii ilizungumza kwa uoga zaidi.
“Sam…tumekwisha….mafala wana picha yangu aisee kumbe wananitafuta mimi!! Jiweke safi Sali sala zako za mwisho, wanatuua hawa!! Hawatuachi Sam”
Kauli hii haikuwa kavu, iliambatana na mkojo!!
Yule mwanamama jasiri alikuwa anajikojolea, ule mkojo wa moto kutoka kwa Jojina ukatua vyema katika uso wangu!! Nikataka kujitikisa lakini nikahofia kuharibu zaidi.
Hakika Jojina alikuwa ameogopa sana.
Na kama alivyosema kuwa tumekwisha ni kweli alimaanisha, maana jasiri akifikia hatua ya kujikojolea basi ujue amenyanyua mikono juu…
***KUMBUKA!! MUNGU alitumia ubunifu wa hali ya juu sana kuliko ubunifu wowote uliowahi kutokea popote pale, kipindi anamuumba mwanadamu. Alimpa kila kitu, lakini akamnyima uwezo wa kujua nini kitatokea katika sekunde moja ijayo mbele yetu.
Kwa sababu hatujui lijalo, ni vyema kujiweka tayari kila muda ikiwa hatujui siku wala saa!!!
Sikukarahishwa na ile mikojo ya mama lao badala yake fikra zangu ziligandiana maneno ya Jojina ambaye n’do alikuwa shuhuda wa kila kinachoendelea.
. . Alikuwa amekiri kuwa hatuna ujanja na tumekamatika. Niliisikia na kuiona vyema mikono yangu jinsi ilivyokuwa ikitetemeka, nilijaribu kujiimarisha lakini sikuweza.
. . “Wewe kaza uso wako nitazame!!!” niliisikia sauti ya askari ikiamrisha, Jojina akazidi kutetemeka, sasa hakuwa akijikojolea tena, bila shaka mikojo ilijiishia katika kibofu!! . .Mimi ndo nilikuwa kwenye mashaka zaidi.
. . Niliiona miguu ya yule askari ikiwa imesimama imara mbele ya siti ya mwisho kabisa, bila shaka alikuwa akiwakagua akina Jojina.
. . Niliusikia mkono wa Jojina ulishuka kwa kasi na kuanza kunipapasa, alinishika sikio mara anishike kichwa!! Nikajiuliza kulikoni na bado sikufanya jitihada za kumzuia asinipapase. Sikujua anachokihitaji ni kipi. Mara akanishika pua na hatimaye akapanda juu kidogo akainyofoa miwani katika macho yangu.
. . Nilistaajabu nisijue kama hii ni hofu inasababisha ama ni kipi kinamsibu mwanamama huyu!! Nilikuwa namwomba Mungu afanye muujiza wowote ule na ile iwe ndoto. Tatizo ni moja tu!
. . Mungu hapangiwi kazi!! Yeye huombwa tu. Nami nikalazimika kuomba huku nikitarajia majibu ya haraka haraka.
. . Hatimaye miguu ile ikageukia upande aliokuwa ameketi Jojina. Hofu ikaongezeka maradufu.
. . “Kwani kuna nini hapa jamani!!!” nniliisikia sauti ya Jojina, sikujua anamuuliza nani.,
. . “Tiketi yako ipo wapi mwanamke??” sauti kali ya kiaskari ilijibu.
. . “Tiketi…tiketi yangu mimi….. Joshua, we Joshua….. mpe kondakta tiketi yake.” Jojina alijibu nikabaki kuduwaa kule chini nisijue nini kinaendelea baina yao.
. . Jojina aliendelea kusema maneno maneno, bila shaka aliyajua mwenyewe mimi nikabaki katika fumbo!!!
. . Kimya kikatanda, nikamsikia yule askari akisonya na mara akageuza na kuondoka zake. Nilistaajabishwa sana na muujiza huo.
. . “Usitoke…vumilia huko huko!!!” alinong’ona Jojina, nami nikajizi kujikaza. Gari likawashwa!! Safari ikaendelea na kile kilichotokea kikabaki kuwa cha kutetwa ndani ya basi.
Baada ya dakika kadhaa Jojina aliniruhusu nitoke kule chini, hii ni baada ya abiria kadhaa kuwa wameuchapa usingizi wasijue kama nilitokea kule chini.
. . “Jojina umewalaghai kitu gani wewe mwanamke!!” nilimuhoji kwa sauti ya chini.
Akaanza kwa tabasamu kisha akanieleza kitu kilichonifanya niamini kuwa si lazima uende shule ndipo uwe na uwezo mkubwa wa kimaamuzi kama wa mama lao.
. . “Yaani nilikuwa najua kuwa sitaweza kuchomoka hapa, yaani kitu nilikuwa nimesahau ni kwamba Dulla huwa ana picha zangu tena nyingi tu, na wale jamaa waliniona nikiwanaye na mbaya zaidi aliwatambulisha kwangu. Hivyo ule mzoga kwa namna yoyote ile lazima skendo za kuua ziwe juu yangu. Sasa nikajibweteka kimawazo nikiaqmini ni wewe wanakusaka. Alikuwa pale hivi siti ya nne nd’o nikaiona picha, wacha nichachawe mtu mzima!! Yaani nikajua tumekwisha. Aliponikaribia zaidi nikaamua kama ni kufaacha nife kishujaa, ndo pale nikakupapasa nikakutoa miwani yako harakaharaka nikaitundika katika uso wangu. Aliponifikia nikaanza kujisemesha, jamaa akaniondoa miwani, aisee kitu nilichofanya najua mwenyewe, nikabenjua macho yangu, hii bolti nyeusi ikapotea ikabaki hii nyeupe, hii michezo naijua sana tangu zamani, wakati nabenjua nilikuwa napapasa huku na kule na mara nimkamate mkono, mara nimshike kifua. Nadhani unajua kilichotokea hapo, wasafiri bila kutumia aki;li wakaanza kukoroma kuwa mimi sina uwezo wa kuona tena wakitumia lile neno kali kabisa, kipofu!! Askari akaishiwa hamu, akanirejeshea miwani yangu machoni, nikayaweka macho yangu sawa na kumwona jinsi alivyokuwa na wasiwasi. Lakini nadhani ile picha nikiwa na kipara na uhalisia huu nikiwa na wigi umemwacha hoi. Kipofu mwenye wigi, wakati picha ni mtu anayeona akiwa na kipara.
. . Akasonya na kuondoka zake!! Sam siamini hata kidogo kama…….” Akasita kuzungumza, akaniegemea na kunong’ona, “kuna bwege anatuchora….” Aliniambia na kisha akanionya kuwa nisifanye jitihada zozote za kupepesa macho.
. . “Pita upesai nenda kamwombe kondakta,,, mwambie ninaumwa tumbo….pameharibika Sam hapa nenda haraka.” Akanisihi, upesi nikasimama na kupita nikafanya hima na kumfikia kondakta. Nikamsihi kama nilivyoelekezwa, nikalalamika sana juu ya mgonjwa wangu asiyeweza kuona anaumwa tumbo.
. . Kondakta akanielewa, nikarejea na kumchukua Jojina katika namna ileile ya kumwongoza mimi mbele yeye nyuma, akiigiza kuwa hana uwezo wa kuona. Wakati huu niliweza kumtilia mashaka yule mtu ambaye Jojina alidai kuwa hana nia nzuri, nilimwona akinong’ona na mwenzake. Nikajifanya sijui lolote linaloendelea.
. . Tulipoufikia mlango mimi nikiwa mbele kama kawaida mara tukasikia sauti kali ikiamrisha.
. . “Ninakutilia mashaka wewe mama usiyeweza kuona. Simama hapo hapo ulipo!! Nayaongea haya kwa mamlaka niliyopewa na jeshi la polisi Tanzania.” Niliskia miguu ikiishiwa nguvu, nikaanza kutetemeka. Lakini haikuwa hivyo kwa mama lao.
Ghafla akanisukuma nikatangulia nje.
. . “Saaaam poteaaaaa!!!” ndo neno pekee alilotoa, akatupa miwani huko, akaikunja sketi yake. Akili ikafanya kazi vyema sikulemaa, mwanamama anakimbia sijapata kuona, kumbe ule unene ni gelesha tu.
Nikaanza kufuata nyuma, huku nyuma zikawa zinasikika kelele za abiria. Yule askari sikuisikia sauti yake. Na niisikie ili iweje tena.
. . Nikapenya kila alipopita Jojina, mimi nyuma.
. . “Simama la sivyo nafyatua risasi!!!” ilisikika sauti kwa mbali, almanusura nisimame kama yasingekuwa maneno ya Jojina.
. . “Sam usisimame hakuna kitu hapo Sam kimbia.” Alinisisitiza pasipo kugeuka nyuma. Maneno yake yakanitia wazimu wa kukimbia nikakazana zaidi. Hakika hatukujua ni wapi tunakwenda!!
. . Taratibu nilianza kuchoka, na bado nilisikia vishindo kwa nyuma. Jojina alikuwa ameniacha tayari na vile tulikuwa tukipenya katika majani sikuweza kumwona kabisa. Hofu ikaanza kutanda, dalili za kukata tamaa zikanikumba.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
. . “Jojinaaa…..Jojinaaa..” nilianza kuita lakini sikujibiwa.
. . “Simama kimburu Kenge, shenzi kabisa simama.” Sauti iliamrisha kwa nyuma. Nilikuwa nimechoka, nikasikia miguu ikigongwa kwa nyuma, nikayumbayumba kisha kama mzigo nikatua chini.
. . Meno yangu yakauma nyasi!!! Nikajitahidi kugeuka nikakutana na mwanaume akiwa ameshikilia pingu. Alikuwa anahema juu juu, ni yuleyule mwanaume ambaye tulikuwanaye ndani ya gari. Alikuwa ananitazama kwa jicho kali.
. . “Shetani mkubwa!!!” nikasikia sauti nyingine ikasikika ikitokea katika majani!!! Mimi na yule mwanaume mwenye pingu tukatahamaki, lakini hatukudumu sana mara yule mwanaume akaaguka chini akijishika kichwa, nikaona jiwe kubwa pembeni yake. Na hapo akatokea yule mama aliyejikojolea ndani ya gari.
. . Jojina kwa mara nyingine!!!
. . “Mshenzi mkubwa wewe ukipona nenda kamweleze mkuu wako wa kazi kuwa kuna watu wabaya anawafuga huko.” Alikoroma mama lao. Lakini huyo mtu aliyepewa nafasi ya kupona akataka kuleta ujanja, ambao Jojina aliutegemea kumbe, akasimama na kurusha teke, mama lao akaingiza mkono wake katika sketi yake, akatoka na jiwe jingine kazuga kama analirusha yule askari akajificha kwa kutumia mikono miwili huku akiruka kando.
. . Jojina akatabasamu wakati yule bwana anaitoa kinga yake usoni, hapohapo akalivurumisha lile jiwe.
. . Nilibahatika kuona meno kadhaa yakitoka katika kinywa cha yule bwana. Kufikia hapo mama lao hakuwa akizuilika.
. . “Auaye kwa upanga……” alisema huku akitua juu ya mwili wa yule bwana anayevuja damu, “Atauwawa kwa upange vilevile” akamalizia huku akiishika ile pingu na kuanza kumcharaza nayo yule bwana usoni.
. . Kila alipoituliza paliumuka kisha damu!!
. . Akapiga kwenye taya, akapiga paji la uso!! Akapiga kila kona!!!
. . Kisha mbio zikaendelea. Kidogo nilikuwa nimepumzika. Nikaweza kukimbia zaidi, wakati huu tukiwa sambamba na mama lao Jojina.
. . “Niliwahi kuwa mwanariadha shule!!” alisema bila kunitazama.
. . Sikumjibu.
. . Hapakuwa na mtu anayetufuatilia kwa nyuma!!!
. . “Hivi unajua tunapoelekea lakini?” Jojina aliniuliza, hapo tukajikuta tunapunguza mwendo taratibu huku kila mmoja akikumbwa na kiwewe.
. . “Hata sijui ndugu ujanja wangu mimi Morogoro mjini tu Msamvu, Kihonda basi!!” nilimjibu na hatimaye tulikuwa tumesimama.
. . Jojina akajipekua na kutoka na simu yake katika koba lake ambalo hakuwahi kulitua hata mara moja tangu tuliposhuka garini na kuanza kutimua mbio.
. . “Simu imezima chaji aisee tungeweza hata kutumia ramani ya simu kama ingeweza kufaa.” Akasonya kisha akairudisha simu yake mkobani.
. . Tukaendelea kutembea kuelekea mbele bila kufahamu kama ni salama ama hatari.
. . “HIFADHI YA TEMBO MIKUMI” Kibao kikatukaribisha baada ya mwendo mrefu.
. . “Mungu wangu tupo mbugani Sam!! Mbugani Mikumi hapa…” aliweweseka Jojina nami nikapagawa. Hapakuwa na ngojangoja zaidi tukaanza kukimbia kuelekea uelekea mwingine, tukapishana na makundi ya Swala, na kwa mbali kabisa tukaiona barabara. Tukaukaza mwendo zaidi hadi tulipoifikia ile barabara.
. . Ilikuwa barabara ya vumbi, na ilikuwa bahati yetu tena tukaonana na wanadamu. Tukauliza na kupewa uelekeo wa barabara ya kuelekea Iringa, tukakaza mwendo, miguu yangu ilikuwa hoi sana lakini sikukubali kuonekana lelemama.
. . “Sam hawa jamaa tunaopambana nao hawa wananikumbusha hekaheka za Tunduma huko.” Jojina akaanzisha maongezi, walau mwendo na maongezi wapunguza uchovu.
. . “Tunduma? Harakati zipi tena huko.”
. . “Wakati ule wa uchunaji ngozi bwana!! Yaani kuna mdogo wangu fulani hivi kidogo achunwe ngozi, mwanamama nikaingia ‘front’ kutetea damu aisee, yaani mafunzo ya mgambo niliyopitia yananibeba sana mara kwa mara. Nikamjua jamaa anayewafahamu mabwana waliomteka dogo, aisee akajifanya mbishimbishi, nilimpiga ngumi mbili akalegea huko nikamkamata, nikamuwasha vibao ka’ vinne hivi wacha apagawe!! Nikamzuga kama nampiga teke akasema atanipeleka, nikamshika ile staili inaitwa Tanganyika jeki, yaani nikamkamata suruali yake huku nyuma nikamyanyua akawa anatembelea vidole. Moja kwa moja hadi eneo la tukio, saa nane usiku hiyo mwanamke barabarani. Nimeficha kisu huku kwenye pindo la sketi, tumbili yeyote ajiweke mbele yangu nafyeka korodani zake namtia uhanithi mimi!!, nikafika pale, nikatia mkwara na jamaa akiwasihi, mbona walimtoa ndani, walikuwa nd’o wanajiandaa na safari ya kwenda Zambia wakamchune ngozi….nikaondoka naye mabwege wananishangaa tu!! Chezea mama lao wewe!!!” alimaliza simulizi hii kwa majigambo, nikamkodolea macho wakati huo tukiwa barabarani tayari.
. . Kichwani nikakiri kuwa huyu Jojina alikuwa na mengi zaidi ya nilivyomtambua.
. . Baada ya muda tukafanikiwa kuelewana bei na lori la mbao lililokuwa linaelekea Mafinga, Jojina akawa siti ya mbele mimi nikawa nyuma huku na vijana wengine.
. . Safari hii haikuwa na mushkeri wowote ule.
. . Tukafika Iringa mjini majira ya saa nne usiku!!
. . Tukatembea kwa miguu kuitafuta nyumba ya Jojina.
. . Tukaifikia nyumba vyema, lakini mazingira haya yalikuwa tofauti kidogo!! Ni kama kuna aidha ukarabati ulikuwa umefanyika ama la yale makazi kuna mtu aliongeza ama kupunguza kitu.
. . Naam!! Tulipoufikia mlango palikuwa na kufuri!!
. . Nani amefunga sasa? Wakati sisi tulikuwa tukitumia kitasa cha kawaida!!
. . Hatukungoja usiku ule upite, tukazunguka kwa nyuma na kuifikia nyumba ya mmiliki wa nyumba zote pamoja na chumba alichokuwa amepanga mama lao!!
. . Mwenye nyuma alikuwa hajalala, kuna mambo ya faragha alikuwa anashughulika nayo na mkewe na bila shaka ujio wetu ulimshtua sana!!!
. . “Kulikoni Jojina…” aliuliza kwa sauti tulivu.
. . “Mimi n’do niulize kulikoni kama ni kodi yako nilimaliza mapema tu vipi tena kufuli jipya mlangoni kwangu!!”
. . Mwennye nyuma akaduwaa kabla hajauliza.
. . “Wewe mwanamama wewe mbona mnataka kunivuruga sasa. Si wamekuja kaka zako hapa na dada zako wengine kudai kuwa unahama wewe, tena wamekuja na simu yako wewe kuwa haurudi tena hapa. Tena kizuri zaidi walikuja na mwenyekiti wa mtaa na mjumbe, mimi nikawaruhusu wakachukua mizigo yako kuwa wanakuletea huko ulipo, sijui kwa mume wako wewe!! Mi hayo sijui na hapa wakaacha vitu vichache tu!!!” alijibu kwa kujiamini baba mwenye nyumba.
. . “Mungu wangu weeeee!! Bahasha!!!” ndicho kitu cha kwanza kabisa kukumbuka kuwa tulikiacha ndani ya chumba kila kabla ya kusafiri!!!
. . Jojina akalegea na kushuka chini.
. . Akakaa!!
. . Nikaungana naye katika fedheheko hili!!!
. . Bila kithibitisho kile ni wapi zaidi pa kujitetea?
. . Tumekwisha!!!!
. . Nilikiri kimoyomoyo!!!
***
. . Mwenye nyumba alilazimika kutushangaa tu asijue nini kinatusibu, ni kama tulikuwa tumechanganyikiwa vile. Mzee yule akiwa na koti lake kubwa aliganda mlangoni akitutazama.
. . “Mna nini kwani vijana wangu, eeh Jojina ni nini kwani?” hatimaye aliuliza.
. . Jojina akamtazama kwa jicho linaloashiria kukata tamaa akataka kusema neno lakini akaishia kufungua kinywa tu na lisitoke neno lol.ote lile. Baridi ilikuwa kali na kiza kilikuwa kimetanda. Nilitamani kumweleza mwenye nyumba juu ya hofu yetu lakini nikahamisha na kuuliza swali.
. . “Kwani wamekuja lini hawa watu!!”
. . “Leo asubuhi tu!! Yaani hata majirani watakuwa hawajasahau, yaani saa nne hivi walikuwa hapa. Mbona wastaarabu sana ndugu zako wale mi sidhani kama wanaweza kuwa wamekufanyia kitu kibaya!!”
. . “Ndugu zangu wapi mzee, umewahi kuona nimekutambulisha ndugu yangu hata mmoja hapa tangu mzee wangu yule marehemu, sina ndugu ni vibaka tu hao hawana lolote…vibaka kabisa!!” alilalamika Jojina huku akipigapiga mikono katika ardhi na miguu akiirusha huku na kule. Alikuwa amevurugwa sana na jambo lile.
. . Nikamsogelea na kumnong’oneza, “Hapa si mahali sahihi hata kidogo. Kama walikuja hapa asubuhi basi wanaweza kurudi muda wowote ule nakwambia. Hawa si vibaka watakuwa nd’o hao akina anti Ezekiel.”
. . Jojina akatumbua macho yake, huenda hakuwahi kuwaza jambo kama lile. Akasimama wima. Wakati anasimama mzee naye alikuwa ameuacha mlanngo na kupiga hatua zaidi mbele.
. . “Sasa vibaka gani hao wa kuacha makochi, kabati na kila kitu cha thamani na kuchukua sijui picha ganigani hizo Jojina, kweli nd’o vibaka walivyo!!” alizungumza kwa sauti ya chini katika namna ya kusihi.
. . Suala la vitu walivyoiba likazua mjadala upya na ni hapo ambapo Jojina aliungana nami kuamini kuwa wale hawakuwa vibaka bali ni watu wanaotutambua vyema na kuna kitu walikuwa wanatafuta. Kipi zaidi ya picha za Dulla!!!
. . La!! Si picha ya Dulla pekee na bahasha!! Bahasha yenye picha na nakala nyingi ambazo bado ni fumbo.
. . Bahasha yenye ufunguo uliochakaa!!
Nikasimama wima baada ya kukumbuka vitu hivyo, na hapo nikamuuliza yule baba mwenye nyumba.
. . “Na kitanda wameacha?”
. . “Hawajachukua kitu zaidi ya hizo picha na makaratasi mengine!!” alinijibu huku akituona kama watu ambao tuna wazimu vichwani mwetu.
. . Sisi hatukujali, na wakati huo Jojina naye alikuwa amesimama. Akaomba chumba kifunguliwe, baba mwenye nyumba akataka kugoma Jojina akamgeuzia jicho nkatika namna ya kutangaza shari. Akaingia ndani na kurejea na funguo.
. . Akatukabidhi tukaondoka kuelekea kule chumbani, ni upande ule pia ilikuwepo stoo ambayo alidai kuwa baadhi ya vitu vya Jojina vilihifadhiwa mle.
. . Jojina akaingia chumbani mimi nikazama stooni, kila mmoja akitafuta bahasha nachochote kile kingine ambacho kitaweza kutusaidia katika kufanikisha azma yetu ya ukombozi.
. . Giza lilikuwa linatusumbua kuweza kuona vitu barabara, lakini tulilazimika hivyohivyo. Nilivuta makochi huku na kule, nikavuta vyombo na chochote ambacho nilihisi kingeweza kunisaidia mbele ya safari.
. . Lile giza ambalo tulikuwa tunalichukia mara lilitoweka ghafla, lakini si kwamba ulikuwa ni umeme umewaka la! Hapakuwa na kibatari wala mshumaa na hata taa za kandili hazikuwa jirani.
. . Nikautafakari ule mwanga!! Nikajivuta hadi dirishani na kutazama miale yake inapoanzia.
. . Ama!! Zilikuwa ni taa za gari. Tena si gari moja, zilikuwa gari mbili.
. . Nikajisogeza dirishani zaidi katika nondo niweze kutambua zile gari usiku ule wa manane zinataka kitu gani maeneo yale.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
. . Nani angenieleza? Hakuwepo!!
. . Vinginevyo nitoke nje na kujisogeza eneo lile. Jambo ambalo sikuwa tayari hata kidogo kulifanya.
. . Mara nikasikia kishindo nisijue kinatoka wapi. Mhanga wa nyoka akigusana na ujani…….hiyo inajulikana. Nikaanza kuingiwa hofu nisijue ni kitu gani nahofia.
. . Mara ghafla kiza cha awali lakini cha sasa kikiwa kinene zaidi kwa sababu nilikuwa nimeathirika na ule mwanga.
. . Nikatamani sana ule mwanga ungeendelea kidogo maana nilikuwa nimeona kitu cha rangi ya kaki. Ni kama bahasha vile.
. . Nikajiundia matazamio ya wapi nilipokiona, mithili ya mtu asiyeweza kuona nikaanza kupiga hatua moja baada ya nyingi nikipapasa huku na kule huenda ile ingeweza kuwa bahati kuu zaidi kupata kutokea.
. . Nikapapasa vibaya nikatengua vyombo kutoka katika beseni, zaikazuka fujo!! Nikajikinga, bahati nzuri sikudhurika, nikaendelea mbele, nikapapasa tena huku na kule, wakati huu ikawa safari ya viti kuporomoka, katika kujikinga na kuruka huku na kule nikaparamia kochi na kuanguka chini. Viti kadhaa vikatua juu yangu.
. . Nikajikaza sikupiga mayowe, nikaanza kufanya jitihada za kujinyofoa kutoka katika hali ile. Lakini haikuwa rahisi, nikiwa nimesahau kabisa juu ya kishindo cha kwanza nikasikia kishindo cha pili, mara cha tau na cha nne. Vishindo vilikuwa vinajongea kuja katika chumba kile.
. . Mungu wangu!! Nikapagawa na kuanza kujinyofoa kwa pupa. Hali hii haikusaidia.
. . Nikiwa bado katika sintofahamu, mara nikaona mwanga mdogo kutokea dirishani, na ili kunidhibiti nisitokwe na mayowe nikasikia sauti ya chini kabisa ikinong’ona.
. . “Wamekuja mabwege, wako wengi kweli wamembana baba mwenye nyumba huko, tokea dirishani usirudi nyuma wanaua wale.” Ilikuwa sauti ya Jojina.
. . “Joji…Jojina…nimebanwa na makochi nisaidie nipo huku chini.” Nililia kwa uchungu uliochanganyika na uoga, na mara nikakatisha kauli yangu, jicho langu liliiona bahasha ile iliyonipelekea kubanwa na makochi yale.
. . “JItahidi u..” sikumwacha amalizie.
. . “Jojina bahasha hii hapa…..hii hapa Jojina.” Nilimsihi wakati huo vishindo vikizidi kusogea na sauti ya baba mwenye nyumba ikisikika ikilia.
. . Niliukaza mkono wangu nikajitahidi hatimaye nikaishika ile bahasha. Nikaanza kuivuta mara nikawasikia wakiwa wamefika.
. . Nikajikuta nachagua moja tu!!
Jojina aipate bahasha kama wataniua mimi yeye atausaka ukweli. Nikatumia nguvu zangu za mwisho nikajinyanyua kwa uchungu mkubwa viti vikaparanganyika, nikainyofoa bahasha nikairusha dirishana, niliuona mkono wa Jojina ukiidaka vyema, na hapo kochi kubwa likatua vyema usawa wa paja langu na kunikandamiza vyema.
. . Hapa sikuweza kujizuia nikatokwa na yowe la uchungu!!
. . Mara miale mikali ikanimulika machoni, matusi makali makali ya nguoni yakafuata baada ya hapo.
. . “Huyu ni nani ulisema hajaja mtu kimburu wewe!!” sauti hii iliambatana na kilio kutoka kwa baba mwenye nyumba.
. . Ulikuwa msala wa aina yake!!
. . Tochi ziliwashwa na kuzimwa katika macho yangu hivyo kunivuruga nisiweze kuona chochote kile.
. . “Kill him!!” nikaisikia sauti nyingine ikiamrisha kwa ghadhabu. Nafsi yangu ikakubali kwa shingo upande kuwa sikuwa na namna cha muhimu ni kumwombea Jojina aweze kunitendea haki huku nyuma na hatimaye nizikwe kwa heshima zote kama mpigania ukombozi.
. . Ukombozi nisioujua hadi nakufa!! Iliniuma sana.
. . Mara wale watu wakavamia mle ndani, wakaanza kupangua vitu kwa harakaharaka, hata walipofanikiwa kunifikia hakika nilikuwa hoi.
. . Lakini hawakujali, wakanikwapua na kunirusha nje.
. . “Samson… Samson!!!” niliisikia sauti ikiniita, nikajaribu kutazama nikakutana nna mwanga wa tochi, sikumtambua ni nani. Lakini alijawa na dharau wakati akilitaja jina langu. Bila shaka alinijua vyema, nikiwa nahaha huku na kule mara kiatu kikatua katika upande wa nyuma wa shingo yangu na uso ukajivuta kwa nguvu kisha ukatua katika ardhi, maumivu yakatambaa mwili mzima nikaishia tu kutoa mguno wa maumivu. Nilipojilamba pembezoni mwa midomo yangu nikaipata ladha ya chumvi, nilitambua kuwa natokwa damu, lakini kabla sijatulia vyema nikasikia kiatu kikiisambaza pua yangu!!
. . Naam!! Damu zikaanza kuchuruzika na maumivu makali yakanifanya nilie kama mtoto!!
. . “Jack eeh hebu msake huyu Malaya lazima wapo wote wajinga hawa” aliamrisha na pale wakatoweka wanaume wawili, niliweza kuona miguu yao.” Nilianza kupatwa na mashaka walipoondoka na kuelekea ule usawa ambao Jojina alikuwa. Nikaendelea kuugulia maumivu pale chini. Sasa nilikuwa nikilindwa na wanaume wawili. Hawakusema lolote na mimi, bila shaka walingoja watuunganishe wote pamoja na Jojina waweze kutuadhibu. Adhabu gani nyingine kama si kuuwawa?
. . Ile hali ya kuamini kuwa baada ya muda mfupi nitakuwa maiti iliniathiri sana, donge la hasira likanikaba na nikahisi machungu ya kuonewa yakilidondosha chozi langu kutoka katika maficho ya macho yangu.
. . Nauwawa kabla sijaonana na mke wangu na mbaya zaidi kabla sijaonana na Anitha, sijaonana na Eva mwanangu pekee.
. . Nikalegea na kuikumbatia ardhi nikiisihi iwapo ina uwezo wowote kwa wakati ule na inisaidie niepukane na uonevu ule.
. . Lakini ardhi haikunisikia vyema, ikazidi kuimeza damu iliyokuwa ikinitoka puani. Mgongo ulikuwa unauma na kiuno vilevile. Niligeuka kumtazama baba mwenye nyumba, mwanga wa zile tochi ukanisaidia kumwona jinsi kinywa chake kilivyosambaratishwa vibaya, taya ilikuwa imelegea na kuangukia upande wa kushoto, udenda uliochanganyikana na damu ulimiminika kutoka katika kinywa chake. Sikumtazama mara mbili licha ya kuonekana kama anayetaka kuniambia neno fulani.
. . Nilipougeuzia uso wangu upande mwingine nikakutana na kivuli kikubwa chenye umbo kama la mnyama.
. . Mara kile kivuli kikapiga hatua kubwa mbili na kisha kikapaa.
. . Kilipotua na jamaa mmoja kati ya wawili waliokuwa wakitulinda akaanguka chini na hapo kile kivuli kikatangaza uhai wake na ubabe uliopitiliza.
. . Kivuli kikabweka!!!
. . Lahaula!!! lilikuwa jibwa kubwa mithili wa yale majibwa ya polisi!!!
. . Nikageuka kumtazama baba mwenye nyumba alikuwa anajilazimisha kutabasamu. Nikastaajabu lakini nikahisi kuwa lazima kuna jambo linaendelea na yeye analijua.
. . Na hapo nikamsikia akitokwa na sauti kwa kujilazimisha, alijilazimisha kwa sababu kuu moja tu!!!
Sababu alitaka kujiokoa yeye na mimi pia.
. . “Simbaaa…..umaaa!!!!” alisema kisha akarudi chini na kutulia tuli!!!
. . Ebwana eeh!! Hivi kumbe mbwa wana hatari kiasi hicho. Yule bwanha aliyekuwa chini alijikuta akishambuliwa kwa kasi ya ajabu, yule mbwa alikuwa anajua nini maana ya kuuma!!
. . Dakika mbili zilitosha kumnyamazisha yule bwana.
. . Yule mwenzake aliyekuwa amesimama wima bado alianza kuhaha akiitisha ile mbwa kwa mawe, lakini haikutetereka. Alibahatika kuiponda kwa jiwe moja lakini kwa mara ya pili ilikuwa kazi bure.
. . Jibwa likajirusha na kung’ata shingo!!! Jamaa akaanguka chini, jibwa likaanza kumrarua kwa fujo.
. . Lilipohakikisha ametulia tuli likageuka na kutazamana ana kwa ana na mimi!! Hofu ikaanza!!!
. . Macho ya jibwa lile yalikuwa yanang’ara haswa!!
. . Kauli ya kwamba ukilijua jina la mbwa basi hakutishi niliduwaa haikufanya kazi, niliita jina la Simba lakini mbwa yule alionekana kuwa mwenye hasira kali zaidi, aliunguruma kisha akaendelea kunisogelea. Mapigo ya moyo yakazidi kwenda kasi na amani ikatoweka tena.
. . Mara akaanza kubweka, nikafanya kosa kutishia kuwa naweza kupambana naye kwa kumtisha kama namfukuza. Jibwa likatanua kinywa na bila shaka alitaka kufanya shambulizi!!!
. . Nikaamini kuwa ng’ombe wa masikini hazai ni usemi sahihi kabisa. Nikakiona kifo tena mbele yangu. Nguvu nazo zilikuwa zimeniishia.
. . **UJUMBE! Kukata tamaa nd’o asili ya mwanadamu, hasahasa akishafanya jitihada zake binafsi pasi na kumshirikisha mtu!! Lakini je? Kukata tamaa ni suluhu ya kujikwamua kimaisha, ama kufanikiwa lolote lile?
. . Wanadamu wengi hushindwa kutimiza ndoto zao kwa sababu ya pepo hili la kukata tamaa.
. . Ili ufanikiwe katika maisha ni lazima ulishinde pepo la kukata tamaa lakini vinginevyo katika kila vita ulimwenguni wewe utakuwa wa KUSHINDWA TU!!
Utashindwa vita ya kuupinga umasikini, utashindwa vita ya kudharauliwa na mwisho kabisa utashindwa vita kuu ya KUSHINDWA KUIONGOZA AKILI YAKO!!!
. . TAFAKARI!!
“Acha simba!!!” ikaamrisha sauti kali. Nikapepesa macho ili nijionee ni nani huyo!!
Na hapo akatokea MAMA LAO akiwa na tabasamu usoni na rungu kubwa mkononi!!
Alikuwa anatokwa damu mdomoni lakini hakuwa na kitu kinachoitwa wasiwasi tena, akaanza kutembea zaidi.
Alikuwa anachechemea!!
. . “Mama lao…” nikajikuta natokwa na sauti yenye kitetemeshi.
. . “Tuondoke hapa Sam. Wajinga wana mtandao mpana sana hawa. Simama Sam jikaze simama tupotee hapa.” Alinisihi Mama lao, lile jibwa lilibaki kutikisa mkia, bila shaka lilimjua vyema Jojina na mbwa akojuaye….
Hakuna kilichoharibika.
. . Nikajikaza nikasimama wima, mbwa huyu hakuwa na madhara tena kwangu ilhali Jojina alikuwa amemkaripia tayari.
. . Nikajikongoja huku nikiyasikia maumivu ya kiuno bado. Lakini ilikuwa heri maumivu haya kuliko kuuwawa kabla sijatimiza azma yangu.
. . Sikujua kama mwendo wangu ulikuwa mdogo kiasi cha kumkwaza Jojina, hakusema na hata angesema isingesaidia kuniongezea mwendo mgongo ulikuwa unauma sana, na si hivyo tu hata nilipojaribu kukimbia yale maumivu ya kinywa kilichopasuka yalisababisha kichwa kiwe katika maumivu makali sana. Jojina alinitazama kwa huruma huku akizidi kukaza mwendo.
. . Mara akasimama ghafla kisha akachuchumaa, nikamfikia nikiwa nashangaa.
. . “Panda mgongoni Sam… panda upesi” aliniamuru, ni kitu ambacho sikukitarajia hata kidogo lakini hakuwa na masihara hata kidogo, akarudia kauli yake safari hii kwa kuamrisha.
. . Nikajiweka mgongoni, Jojina akasimama kama kifaru akaanza kutimua mbio mimi nikiwa mgongoni. Usiku wa giza tukielekea anapopajua yeye. Niliyafumba macho yangu kukabiliana na uchungu niliokuwa nikiusikia. Kichwa kilikuwa kinauma haswa!! Lakini haukuwa wakati muafaka wa kulalamika.
. . Mama lao akaendelea kutimua mbio.
. . “Taksiii….Taksiiii msaada tafadhali mgonjwaaa!!” aliita kwa nguvu baada ya kuziona taksi kadhaa zikiwa zimeegeshwa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
. . Dereva moja akawahi upesi akaufungua mlango wa teksi yake. Hapo sasa nilikuwa nimefumbua macho nikishuhudia filamu hii ya aina yake.
. . “Tupeleke Stendi ya mabasi…” aliamuru Jojina na hapo nilikuwa siti ya nyuma na yeye akiwa pembeni yangu.
Dereva alibaki kuduwaa ni kama hakuwa akiamini kama tulikuwa na pesa ya kumlipa, Jojina akaling’amua hilo, upesi akajipekua na kutona na noti nyekundu akamlipa dereva.
Akatia gari moto tukatoweka…njia haikuwa mbaya sana hivyo wakati huu nilipata fursa ya kutambua kuwa kinywa kilipasuka japo si vibaya sana lakini shingo ilikuwa inauma sana bila shaka yule bwana aliyenipiga mateke.
. . Stendi haikuwa mbali, tukapewa pesa yetu iliyosalia na kutelemka, wakati huu nikijikongoja mwenyewe. Kila kitu katika suala la maamuzi nikamuachia Jojina maana walau yeye alikuwa na unafuu.
. . Sikujua alikuwa na maana gani usiku mnene kama ule kuamua safari ya kuja stendi lakini hakuniacha niumie akili kutafakari sana, mara akaita teksi nyingine.
. . “Tupeleke Gangilonga” akatajiwa bei akalipa.
Ukimya ukatawala kwa takribani dakika kumi na tano. Tukatelemka mahali ambao Jojina aliamua yeye.
. . Teksi ilipoondoka tukatembea kwa mwendo wa miguu hadi katika nyumba kubwa kiasi iliyozungukwa na majani mengi, bila shaka ni kutokana na watu kutoishi eneo lile kwa muda mrefu.
. . Jojina alivyofika pale geti lilikuwa limefungwa na hakushtuka ni kama kitu alichokitarajia.
Akachumpa ukutani akatua upande wa pili. Kisha akafungua geti dogo na kuniruhusu niingie ndani.
. . “Miezi sita sijakanyaga hapa aisee.” Alisema neno la kwanza tangu tufike pale. Sikuchangia chochote.
Akaniongoza hadi ndani, uzuri wa Iringa hakuna vumbi kali sana, badala yake vipindi vya baridi huchukua nafasi kubwa zaidi hivyo hapakuwa na madhara ya vumbi.
. . “Hapa hakuna umeme wala nini Sam.” Alizungumza tena, nikamuunga mkono kwa kumweleza kuwa hilo si tatizo cha muhimu usalama wetu.
. . Akapapasa huku na kule akaibuka na mshumaa, kisha akavuta kumbukumbu na kupapasa sehemu nyingine akaibuka na kiberiti na kisha kutengeneza mwanga hatimaye.
Nikaketi naye akaketi katika makochi chakavu yaliyokuwa pale ndani.
. . “Baba yangu alikufa maskini lakini walau alijenga kibanda hiki kwa taabu.” Akaanzia hapo, hili halikunigusa sana. Nilitamani kusikia juu ya namna tulivyoweza kuokoka.
Nikaamua kumuuliza.
. . Akatabasamu kidogo kisha akaketi vyema!!
. . “Sam, yaani japokuwa huwa siendi katika nyumba za ibada hata miezi sita ama mwaka lakini nimeamini kuwa Mungu huwa hamtupi mja wake…. Lakini najiuliza iwapo nami ama sisi ni waja wake. Maana nikiwa katika kile chumba changu nikaisikia sauti ya baba mwenye nyumba ikilalamika, na kuna watu walikuwa wakitoa karipio. Nikasitisha nilichokuwa nafanya, simu yangu nilikuwa nimeweka katika chaji. Nikainyofoa kwanza nikaiweka katika mkoba wangu. Nikatuliza akili, mara nikaona mwanga wa gari. Mwenye nyumba wangu hana gari, nikajishtukia na kuheshimu machale yangu kuwa hapa mambo yanaanza kuharibika, nikapitia dirishani mbiombio nikakimbia hadi nyuma ya nyumba ambapo sauti hizo zilikuwa zinatokea. Nikasikia wakimuuliza juu yangu iwapo nimerudi, kisha wakamuuliza iwapo amewahi kuniona na mgeni. Nikasikia wakimuuliza iwapo anaifahamu sura fulani katika picha ambayo najua tu ni yako hakuna mwingine. Mwenye nyumba akakiri kuwa nilikuwa nimerejea tayari. Lakini hakukubali kiwepesiwepesi badala yake walimpa kipigo kwanza nd’o akalainika.
. . Alipokubali kuwaongoza kuja upande wa kile chumba changu na stoo pia ndipo nikashtuka na kuja mbiombio upande ule, nikakuita hukuitika, nikawasha tochi nd’o pale ukanipa ile bahasha!!! Wajinga wakavamia pale mimi haraka nikadidimia chini.
. . Sam niliumia sana nilipowashuhudia wakikupa kipigo kiasi kile, bahati nzuri ndani ya chumba changu tofauti na simu nilichukua pia kile kirungu changu cha mgambo si nilikwambia nilipita huko, kiukweli hicho kirungu niliwadhulumu.
. . Nikajiuliza sasa mimi na kirungu nitakusaidia kitu gani mie. Wakakutukana matusi mazito, nikatamani kukimbia lakini ningeweza vipi kukuacha ufe hivihivi.
. . Nikatamani kupiga kelele lalini mwenzangu we, sisi wahehe ni waoga sio siri, yaani unaweza kupiga kelele asitokee hata mtu mmoja sasa hapo ni kipi kama si kujitafutia kufa burebure.
. . Nikataka kuwakabili kwa kirungu lakini kweli wanaume wanne kwa kirungu kimoja, si matusi hayo!!
. . Nikajikuta naketi chini, na hapo nikakumbuka jambo la muhimu kupita yote na siajui tu niliwaza vipi kuhusu mbwa wa kufugwa wa baba mwenye nyumba. Yule mbwa huwa hana masihara, baba mwenye nyumba alipewa na wazungu fulani hivi rafiki zake. Nikavamia banda nikalifungua, uzuri ananitambua yule mbwa!!
. . Nikamvuta hadi nyuma ya nyuma, ghafla nakutana na wanaume wawili kati ya wanne nikatambua kuwa kazi sasa imeanza.
. . Nikamwachia mbwa akala sahani moja na bwana mmoja halafu mimi na kirungu dhidi ya mwanaume asiyekuwa na silaha, Sam nilimrukia, akanipiga teke mbavuni yule bwege, nikajikaza nikafyatuka na rungu nikalituliza hapa (akagusa utosi wake) jamaa akalainika bila kupiga kelele, chini!!. Ile nageuka namkuta mwenzake akitapatapa pale chini damu inamruka, nikammulika nikahisia kuwa uhai ulikuwa unafanya urafiki naye. Nikamrukia kwa ghadhabu, kabla sijamfikia nikajikwaa nikaanguka chini, nilipoamka hasira zote kwa yule bwana, na yeye nikamtandika rungu kwenye paji la uso. Bila shaka kajifia yule we tungoje taarifa ya habari tu. Kuja kusimama wima tena simwoni mbwa. Nikataka kumwita kwa sauti ya juu lakini nikahofia usalama maana nilitambua fika kuwa wale wanaume wawili wapo bado kule mbele. Nikaanza kunyata taratibu gizani ili nitambua kulikoni, nd’o hapo nikaisikia sauti ya baba mwenye nyumba ikimwamrisha mbwa kushambulia!! Walau amani ikarejea japo niliendelea kunyata, hadi wakati nafanikiwa kufika ndipo namuona yule mbwa akitaka kukushambulia nikamzuia…Sam Mungu ametupangia jambo fulani amini!! Hili tukio halikuwa la kuokoka kirahisi namna hiyo hata kidogo.” Jojina alimaliza na kushusha pumzi kwa nguvu, nami nikashusha pia kama tuliambizana kufanya vile kwa pamoja.
. . “Sam nadhani tunatakiwa kupumzika halafu kesho twende Makanyagio. Lazima tuanzie huko.”
. . “Makanyagio? Nd’o wapi huko??”
. . “Kweli wewe mgeni Iringa nimeamini. Huko ni sehemu maarufu sana kuna makaburi kule, kama unakisikia chuo cha Mkwawa basi ndo kuelekea hukohuko.” Alimaliza kisha akasimama, lakini mimi sikuwa na usingizi. Jojina akaleta godoro la pamba ambalo lilikuwa linatoa harufu ya uvundo akalitandika pale sebuleni.
. . “Tutalala hapa maana huko chumbani hapalaliki kuna harufu sana.”
. . “Popote tunalala Jojina.” Nilimuunga mkono.
Akajitupa na baada ya muda alikuwa anakoroma, nilijaribu kujilazimisha kulala lakini hata usingizi haukujileta jirani nami.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikapata wazo la kujishughulisha na bahasha na yaliyomo.
Maana swali juu ya hawa watu walikuwa wanatafuta nini na mbona wameacha ile bahasha lilikuwa linanisumbua.
Nikaichukua bahasha kutoka katika kiti alichokuwa ameketi Jojina.
. . Nikashtuka na mapigo yangu ya moyo yakaongeza mwendo kasi. Bahasha ilikuwa nyepesi sana tofauti na ilivyokuwa awali wakati inabeba picha na makorokoro mengineyo.
. . Nikaanza kutetemeka nikiamini kuwa ule ushahidi nilioupigania kwa muda mrefu umetoweka, nikaingiza kwa uoga mkono ndani ya ile bahasha. Hapakuwa na makaratasi mengi sana.bali karatasi moja tu!!
. . Nikalichomoa upesi. Lilikuwa karatasi tofauti kabisa na yale ambayo yalikuwa ndani ya bahasha ile awali.
Nilianza kumwamsha Jojina awe shahidi lakini bahati mbaya hakunisikia hata kidogoa alikuwa amezama katika dimbwi la usingizi.
. . Nilijaribu kuiweka akili sawa labda si bahasha ninayoitazamia, lakini ilikuwa ni ile na sasa haikuwa na kitu ndani yake.
. . Nikafungua ile karatasi kwa makini nitambue kama nayo ni moja kati ya zile za awali lakini hapana hii ilikuwa tofauti.
Nikajongea katika mshumaa, nikaanza kuisoma.
Hofu ikatanda maradufu, ulikuwa mwandiko wa kike.
. . “Sam kama huu ujumbe utakufikia, fanya kila uwezalo uniokoe Sam. Nimefanya kila jitihada nijitoe katika mikono ya watu hawa lakini jitihada zimegonga mwamba. Nakuandikia ujumbe huu nikiwa nimekata tamaa kabisa ya maisha na sina uhakika kamaq utaupata ujumbe huu, Sam yanayotokea huku hayasimuliki hata kidogo kwa maandishi, ninayoyashuhudia huku nilipo ni mazito mimi na wewe hatuyawezi bila msaada wa watu wengine, lakini hao watu wengine ambao nawasema wote wapo katika upande wa watu hawa. Sam kama ukiona ni ngumu sana kuniokoa, amini kuwa nimeridhia kufa. Wewe funga safari ondoka katika nchi hii, nenda mbali Sam maana ukiingia huku hautatoka Sam. Jiondokee uende mbali labda utapata msaada kutoka kwa watu wengine huko wasiokuwa wenyeji wa ardhi hii.
Natamani sana walau ningejua huku nilipo ni wapi lakini bahati mbaya sina hata kitu kimoja cha kufananisha eneo hili. Na bora ningekuwa natulia sehemu moja, hawa jamaa wananihamisha kila leo. Nimeuza utu wangu Sam na nimeshiriki penzi na huyu bwana ambaye kama ni mkweli atakufikishia ujumbe huu, ameshindwa kabisa kunivujishia siri za humu lakini amesema kuwa hapendezwi na mambo ya humo na atakushirikisha. Nimeamua kumwamini kwa sababu sina namna na hata nisipomwamini mimi ni wa kufa tu Sam wangu!!! Sama kama itakuwa sawa naomba umsikilize huyu bwana, macho yake hayadanganyi hata kidogo, na laiti kama pasingekuwa na vifaa vya kurekodia humu ndani angeweza kunieleza jambo nami nikakuandikia.
. . Sina thamani yoyote zaidi ya uhai nilionao, nimejirahisisha kimapenzi mara kadhaa ili niweze kuokoka lakini haijasaidia. Nimejirahisisha kwa huyu bwana pia, sijui kama nitafanikiwa ame nimeshindwa!!!
. . Samahani kwa mwandiko huu mbaya, nimeyaandika haya nikiwa katika giza, narudia tena kama huyu bwana ni mkweli basi alifanya hila ya kuzima taa na kuzuia kamera kuweza kunirekodi, nikafanikiwa kukuandikia haya.
Sam, kama sitafanikiwa kupona nifikishie salamu hizi kwa mama yangu mwambie nampenda sana, pia mwambie mzee Matata katika maisha yake ajifunze kumsikiliza mtu kabla hajaamua kumuhukumu. Hii itasaidia kuokoa wengi.
. . Akupendaye!!!
. . Anitha
Barua ilimalizika nisijue kama imemaridhika, maneno yaliyoandikwa ndani ya barua ile yalikuwa mazito sana. Nikamkumbuka yule bwana aliyekuwa akinibinyia macho kila mara nilipofanikiwa kutazamana naye, sikuweza kupata jibu la moja kwa moja iwapo ni yeye aliyeagizwa na Anitha kunifiikishia ujumbe ule.
. . Nikakumbuka pia jinsi yule mbwa alivyomng’ata shingoni na labda kuondoka na uhai wake.
. . Labda alikuwa mtu mwema!!! Macho yake yalijawa na huruma yule mtu!!!
. . “Jojina….” Sasa nikamkanyaga kwa nguvu, akaamka. Nikamshirikisha juu ya nilichokutana nacho katika bahasha tuliyosadiki kuwa ina nyaraka zetu za kutuongoza.
. . Kama nilivyoduwaa na yeye akaduwaa vilevile. Akaisoma barua na kuimaliza.
. . “Sam, hawajatuchezea akili hawa tujiingize mkenge!!!”
. . “Hapo n’do pagumu pa kuamini na pagumu zaidi kukataa.” Niliishia kujibu kwa sauti ya chini.
. . “Inawezekana kumbe Anitha yupo hapahapa Iringa eti!” akaniuliza swali la kizembe kabisa. Sikumjibu badala yake nikabetua midomo.
. . Hakuna aliyelala tena!!!
. . Bahasha iliyokuwa na zile takwimu nyingine za muhimu ikawa imepotea katika namna ile ya kustaajabisha.
. . . . . . ****
. . SAA MBILI asubuhi tulikuwa maeneo ya Makanyagio, Jojina alikuwa kiongozi kama kawaida. Kwa mtazamo alionekana kuipoteza kumbukumbu ya nyumba ambayo alikuwa anataka twende, mbaya zaidi alilisahau hata jina la mzee wa makamo ambaye alihitaji twende kuonana naye.
. . “Ujue nimekuja huku mara ya mwisho mwaka juzi ule, sasa watu wamejenga majumba yao huku, siikumbuki nyumba hata kidogo. Na jina nd’o limenitoka sasa.” Alilalamika, tayari ilikuwa saa saba.
. . Hadi majira ya saa kumi na mbili hatukuwa tumefanikiwa kwa lolote.
. . Tukarejea Gangilonga kisirisiri usiku mnene.
. . Jojina alijituliza peke yake akivuta kumbukumbu hii mara ajaribu kubinyabinya kichwa chake. Nilimsikitikia sana maana macho yake makubwa yalikuwa mekundu, akachukua kipande cha mkaa na kuandika chini herufi A hadi Z akidhani kwa kuiona herufi fulani atakumbuka jina la mzee huyo ambaye sikujua alihitaji nini kutoka kwake.
. . Bado hakulikumbuka jina!!
. . Angeweweza kukumbuka hata majina ya watoto wake lakini bahati mbaya hakuwahi kuwa na mtoto wa kumzaa.
. . “Sam…Sam….. “ Ghafla Jojina aliniita, nikiwa nimeduwaa akanishika mkono na kunivuta kuelekea chumbani.
. . “Baba alikuwa anaandika namba za simu katika kitabu fulani hivi…..” alizungumza huku akianza kupekuea maboksi kadha wa kadha na mimi nikamsaidia. Haikuwa kazi nyepesi kulikuwa na harufu kali sana isiyostahimilika. Lakini tulilazimika kujikaza.
. . Saa nane usiku na dakika kadhaa nikafanikiwa kupata kijitabu kidogo rangi ya kijani. Jojina akapiga kelele kushangilia. Kilikuwa chenyewe, upesiupesi akapekua majina.
. . “Mzee Madati huyu hapa!!!” akakutana na jina ambalo alilihitaji.
. . Tukalala tukiwa na jina hilo vichwani mwetu!!!
. . Mzee Madati!!!
. . . . UTATA MPYA WA ANTI EZEKIELI
. . KAMA ilivyokuwa siku iliyopita maeneo ya Makanyagio, tulihangaika kuuliza huku na huku hatimaye tukaipata nyuma iliyojificha sana tukaelezwa kuwa hapondipo anapatikana mzee Madati. Ajabu sasa kila ambaye alituelekeza alitutazama kwa mashaka, wakati mimi nilikuwa na kofia ya pama na miwani kichwani na Jojina naye alijifunika vyema na wigi lake asiweze kuonekana.
. . Tuliwakuta akinamama watatu wakiwa wanatwanga majani ambayo mimi sikuyafahamu. Nikawasalimia kwa Kiswahili lakini hawakunijibu.
. . Jojina akawasalimia kikabila, mimi nikabaki kimya nisiambulie neno hata moja.
. . Hata yeye hawakumjibu vilevile.
. . “Tunahitaji kuonana na mzee Madati….” Alizungumza Kiswahili hatimaye. Bado wale wanawake hawakujibu kitu. Mmoja wao akaingia ndani, na baada ya hapo akatoka kijana moja mrefu mwenye macho mekundu.
. . “Samahani tunahitaji kuonana na mzee Madati!!” alisema kwa unyenyekevu Jojina lakini yule kijana hakuguswa na unyenyekevu huo.
. . Akatutazama na kutuuliza ni ipi shida yetu.
. . Jojina alishindwa aanze vipi kujielezea shida yake kwa mtu baki kiholela namna ile, nikamwona akianza kukunja ndita nikatambua anataka kuzua zogo. Nikamkanyaga mguu, akatambua dhima yangu. Akatulia
. . “Kaka tuna shida kubwa sana ambayo ni yeye tu wa kuisikiliza.” Alisema Jojina kwa sauti ya chini kabisa.
. . “Mnatoka wapi.”
. . “Gangilonga!!”
. . “Mbona unajibu wewe tu mwenzako yupo kimya, we jamaa unatoka wapi?” alikoroma yule kijana. Mara nikamwona Jojina akitokwa na tabasamu na hapo akatokwa na kauli iliyoleta urafiki.
. . “We Geza wewe yaani ujue nilikuwa nimekusahau kabisa, mwone mtoto mdogo unakoroma hivyo!!!”
. . Yule kijana akashtuka kuitwa jina lile.
. . “Ndema mie!!” Jojina akajitambulisha kwa jina jipya. Kumbe lilikuwa jina lake la ukoo.
. . Sura ya yule kijana ikajawa na tabasamu si yeye tu na wale akinamama wakaanza kuzungumza, wakamsemesha Jojina kikabila naye akawajibu. Wakakiri kuwa alikuwa amebadilika sana.
. . Tukakaribishwa ndani!!
. . Mzee Madati alikuwa mahututi kitandani!!!
. . Ilisikitisha kumtazama, lakini nd’o ilikuwa hali yake haswa.
. . Jojina akazungumza kwa muda mrefu sana na ile familia kwa kikabila. Baadaye akaninong’oneza.
. . “Ile homa ya Ezekiel inamwondoa mzee Madati.” Kauli fupi lakini nzito sana.
. . Nikatamani kuuliza lakini hatukuwa huru kiasi kile.
. . Jioni hiyo tukapata fursa ya kuzungumza na mzee Madati alipokuwa ameamshwa kwa ajili ya kunywa uji pamoja na dawa.
. . Alichukua muda sana kumkumbuka Jojina, lakini alipomkumbuka ilikuwa shangwe tele. Alizungumza naye juu ya baba yake ambaye alikuwa marehemu tayari.
. . Akatuelezea namna alivyochukuliwa na watu asiowafahamu wakamlaghai kuwa wanataka kununua shamba lake hivyo aende kuzungumza na bosi wao.
. . “Nilipofika wakaniuliza iwapo nafahamiana na mzee wako Ndema, mimi nikakubali upesi tu na hapo ili kufanya biashara iende haraka nikawaeleza kuwa nauza kipande changu kwa sababu ya kusimamia kesi ya mzee wako. Wakanipongeza sana kwa utu wangu kisha wakaniuliza matumaini ya kushinda kesi. Ndema unajua jinsi gani mimi na baba yako….(akasita akakohoa sana) kisha akaendelea… mimi na baba yako tangu utoto ni chanda na pete. Kwanini nimwombee mabaya, nikawaeleza ukweli kuwa naamini kuwa ile kesi kuna watu wenye fitina wameitengeneza.
. . Ndema, awali nilikuwa nimekataa kata kata kunywa kahawa yao, niliikataa kata kata lakini baada ya sote kuchangamka na kuonekana kufahamiana. Nikanywa ile kahawa yao ya moto nyeusi.
. . Nd’o nikajipa tiketi ya maswaibu haya, nakufa najiona na mzee wako wakamuua wajinga wale….. Ndema na wewe kijana kaa mbali kabisa na Anti Ezenaninani sijui, Anti nani yule…msijihusihe kabisa na hao…mi wameniua na ninyi watawaua ”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
. . “Baba usiseme hivyo!! Hautakufa hata tafadhali, kwani wenyewe wanapatikana wapi ili tuangalie uwezekano wa kuwachukulia hatua.” Jojina aliuliza kwa upole kabisa.
. . “Akina nani tena jamani?” mara mzee Madati aliuliza kwa sauti ya kukoroma.
. . “Si hao watu wabaya waliokuwekea hiyo kahawa. Na huyo Ezekiel ni nani tena maana…” Aliuliza Jojina huku akimpoozea uji mzee Madati.
. . “Kahawa gani tena?” alihoji huku akiwa katika kubung’aa.
. . Na hapo wale wanawake wakatueleza kuwa mzee Madati ana tatizo la kusahau na hapo hawezi kukaa sawa tena ilikuwa bahati kubwa sana kwetu amesema nasi kwa muda mrefu.
. . Hawakuwa katika utani!!
. . Tulijaribu zaidi ya mara kumi lakini mzee Madati alikuwa haonyeshi ushirikiano, na baadaye akasinzia.
. . Akaondokea kuwa katika hali ile hata siku iliyofuata na nyingine tena, hakuonyesha ushirikiano nasi tukabaki katika utata mtupu.
. . Mzee Madati naye anamtambua huyo Ezekiel.
. . Kulikoni? Ama ni mzimu huu unatuzunguka kwa ajili ya kuja kuyavuruga maisha yetu? Niliwahi kujiuliza.
. . Lakini kuna kitu mzee Madati anajua kuhusu Anti Ezekiel.
. . SIKU YA NNE hatukwenda tulibaki mafichoni. Lakini tukifanikiwa kununua gazeti mjini.
. . Hapakuwa na habari yoyote ile mpya. Sikuzungumziwa hata kidogo katika kurasa za mbele, bila shaka walitaka kuwaaminisha watu kuwa nimeuwawa.
. . Wakati najiaminisha hivyo, mara nikakutana na habari ambayo bila shaka katika siku kadhaa nyuma ilikuwa ikiunda vichwa vya habari lakini sasa ilibakia kuwa habari ya kawaida.
. . “Mama aliyefukua kaburi la mwanae na kuutoa mwili kisha kuuchoma amegundulika kuwa na matatizo ya akili……..” habari ile ilitaja jina la mama yangu mzazi!!
. . Nilichoka!!
. . Mama yangu amefukua kaburi langu akautoa mwili na kuuchoma?? Haya yalikuwa maigizo kabisa tena yaliyokosa waigizaji wazuri.
. . Hawa watu walikuwa wanatumia pesa!!
. . Waligundua kuwa Dulla aliuwawa mjini Morogoro. Wakajiaminisha kuwa mama lao hawezi kuwa muhusika.
. . Wakati huo wakijua fika kuwa mimi bado nipo hai. Kile kifo wakakihusisha na uwepo wangu, bila shaka walimbana mama awaambie kama tuliwasiliana, mama akagoma.
. . Wakatumia pesa kumuuzia kesi nzito, kisha wakatumia pesa tena kumhonga daktari ampime mama akili na kisha wakayanunua majibu kwa pesa zao.
. . Daktari akalipa fadhila kwa kuandika kuwa mama yangu mimi ana matatizo ya akili.
. . Akatolewa rumande na kutupwa hospitali ya vichaa Mirembe.
. . Hakika ilistaajabisha.
. . Machozi yakanitoka!!!
. . Jojina akasogea karibu yangu na kuanza kunibembeleza!!!
. . “Jojina, wamemchukua Mama Eva, wamemchukua mama Eva, Anitha ndo huyu anatoka kutuandikia barua hajui kama atapona ama atakufa, wametaka kukuua Jojina, sasa wamemchukua mama yangu, walimuua baba yako, wamemchukua mtoto wako.. ni kipi sasa wanataka. Mi siwezi kuishi hivi kwakweli siwezi kabisa.si bora nife sasa eeh bora nife” nilijikuta nakaribia kufanya kufuru. Jojina akaingilia kati.
. . “Ufe wewe ili mama ateseke huko bila kuwa na msaada wowote, kufa kwako ni kumkimbia Eva mtoto wako, aibu ilioje Sam. Unawaza kufa, basi sikuwa na haja mimi ya kumuua yule askari kule porini, sikuwa na haja yoyote ya kujiingiza katika utata huu, ni heri ungeniacha nikiwa nauza bajia na sambusa zangu kuliko huku uliponileta. Ungeniacha sasa. Haya si unataka kufa!!!
. . Naomba unirudishe uliponitoa, nirejeshe stendi na kapu langu la bajia na sambusa lakini usisahau kitu kikubwa kabisa. Naitaka amanmi yangu ambayo umeipoteza!!!” Mama lao Jojina alikuwa amekasirika haswa. Lakini sio hasira zilizozungumza, aliyoyasema yote yalikuwa kweli tena kweli tupu. Nikakumbwa na aibu nikatamani kuomba msamaha lakini Jojina hakuwa tena pembeni yangu!!! Alikuwa ameelekea chumbani.
. . Nililazimika kumfuata, ikawa zamu yangu kumbembeleza kutoka katika kilio chake.
. . Nilimsihi sana, hatimaye akanikumbatia miili yetu ikagusana na kila mmoja kujikuta akivuta pumzi ya mwenzake. Baridi kali la Iringa likatusababisha tutamani kuendelea kukumbatiana.
. . Kilichotokea baada ya hapo hakuna aliyekitazamia kuwa kitatokea.
. . Tulikurupuka asubuhi kila mmoja akiwa utupu!!!
. . Hakuna aliyeanzisha mazungumzo juu ya ajali iliyotokea usiku.
. . UJUMBE: DUNIA haitendi hali hata siku mojua, WANADAMU wamejaaliwa kasumba ya unafiki!! Usitarajie wanafiki waishio katika dunia isiyotenda haki wanaweza kukuhurumia hata siku moja!!! Jiwekee akiba ya uaminifu, usiumwage uaminifu wako kwa kila nafsi.
Dunia isipokutendea haki usiililie dunia bali mlilie aliyeiumba dunia!! Yeye pekee nd’o mtenda haki…….
. . . . **SAM anafikia maamuzi mabaya ya kufikiria kufa akidhani kufa ndo suluhu ya matatizo… JOJINA anamtia moyo!!
. . . . **WATU WABAYA wamemharibia uelekeo na mama yake SAM……..vipi kuhusu mzee MADATI NAYE??
.....**Sam amefanya mapenzi na mamalao>>>>>>
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment