Simulizi : Hila
Sehemu Ya Tano (5)
SUZAN aliposhtuka kutoka katika usingizi asiojua alisinzia kwa muda gani alikutana na sura ambayo alikuwa akiifahamu vyema kabisa kutokana na kumwona baba yake akihangaika nayo mara kwa mara.
Alikutana ana kwa ana na mwanadamu anayetafutwa auwawe kisha kichwa chake kikatwe na kutumwa uholanzi kikaketi makumbusho ya BvB wakati anaunywa mvinyo wake anakitazama na kutabasamu.
Ana kwa ana na Samweli Mbaule.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Macho yalimtoka pima Suzan, akataka kupiga kelele lakini ghafla kijana aliyehitimu mafunzo ya JKT akamkaba koo lake kwa ustadi mkubwa.
“Bila shaka haujawahi kufa!! Sipendekezi leo iwe siku yako ya kwanza kufa, maana ukifa leo hutapata bahati ya kukutana name tena tukitabasamu….. kuwa mtulivu mtoto wa kike mimi si muuaji lakini najua kuua….” Sam alikoroma huku macho yake yakiwa mekundu.
Sam, kwa mara ya kwanza alikuwa ameamua kunywa pombe ili kujipa ujasiri wa jambo ambalo alikuwa ameamua kufanya.
Akamwachia binti yule kisha akajipekua na kutoka na simu mfukoni mwake.
Ni kama alitegemea kile ambacho binti yule alikuwa amepanga kufanya. Kwa ncha za macho yake akamtazama jinsi alivyokuwa na akili mbovu.
Mara ghafla binti akachomoka akaufikia mlango na kuanza kukimbia huku akipiga kelele.
Sam akaanza kwa kutabasamu kisha akacheka kidogo, halafu likaja cheko kubwa.
Naam! Alikuwa na kila sababu za kucheka kwa sababu binti yule hakujua kuwa mwandishi wa habari ni jasusi vilevile!
Anazijua mbinu!!
Sam akauendea mlango na kuufungua kisha bila papara akatoka nje. Akamkuta binti yule akihaha huku na kule. Hakujua wapi aende, Sam akawasha tochi yake na kummulika.
“Rudi ndani dogo, au nd’o unataka kwenda kuliwa na fisi huko.”
Suzan alibaki kuduwaa, mahali walipoingia mchana ambapo palikuwa jirani na barabara ya kwenda Morogoro. Hapakuwa mahali hapa alipokuwa wakati huu. Baridi kali iliyopenya katika ngozi yake baada ya kutoka nje nayo ilimduwaza zaidi na kukiri kuwa alikuwa eneo tofauti na Dar es salaam.
Ama kweli nipo mikononi mwa muuaji hatari! Binti yule akakiri huku akirejea taratibu alipotoka.
Sam akamfungulia mlango naye akaingia!
Kwa utulivu Sam akachukua simu na kupiga namba kadhaa na kuweka sauti ya juu katika spika.
“Nani mwenzangu?” ikasikika sauti upande wa pili. Suzan akaanza kulia baada ya kuiskia ile
sauti….. ilikuwa ya baba yake mzazi.
Sam alikuwa amempigia IGP.
“Samwel Mbaule nazungumza. Na anayelia ni mwanao wa mwisho na pekee wa kike kama sikosei.”
“Nini unasema wewe mwendawazimu, Sam nitakuua vibaya we kijana nitakatakata vipandevipande ujue. Namwomba huyo mtoto mara moja….. namwomba kabla sijauruhusu mkono wa dola ukushughulikie
“Kwani ulipowaruhusu wanikamate nikiwa Tanga walikupa jibu gani? Anyway, ni kweli utanikatakata lakini usiponisikiliza kwa makini nitakuomba kesho uwe tayari kulikuta sikio la mwanao Tanga mjini, Kichwa Ubungo stendi ya mabasi, mguu mmoja Mwanza, Macho yote mawili Arusha mjini, na utumbo utaukuta kituo cha mabasi yaendayo Mugumu Serengeti yakitokea Musoma. Aah! Vingine hautavipata maana nitakula, mfano ulimi wake, na ana makalio mazuri… nitakula yote. Ukishaniua utayakuta hayo tumboni mwangu…” Sam alizungumza kwa utulivu mkubwa lakini aliye katika hasira kuu.
Hasira ya ukombozi.
Wakati akitapika maneno yale, Suzan alizidi kulia kwa sauti ya juu.
Na mara ikasikika sauti ya mke wa IGP akimuuliza mumewe ni kitu gani kinaendelea.
Ama kwa hakika IGP alidata akawa mpole haswa na kutulia tuli huku akiamini kuwa Sam hakuwa akitania.
“Ni kitu gani unataka hadi umguse mwanangu, nitakuua Sam. Nitakuua kwa mateso.”
“Nahitaji wewe na raisi wako mkiri maovu yenu na kuisafisha Tanzania yetu…”
“Maovu? Maovu gani we mpuuzi?”
“Ukiendelea kutumia lugha za kipumbavupumbavu nitakata simu na siku nikipatikana nitakuwa nakupa pole ya kuzika kiungo kimojakimoja cha mwanao huku kifo chake kikiwa moja kati ya vifo vya kutisha vilivyowahi kutokea Tanzania.” Sam alikoroma tena.
IGP akakiri kimyakimya kuwa alikuwa amekutana na kichwa kibovu kupita vyote alivyowahi kukutana navyo, na mbaya zaidi mtoto wake alikuwa mikononi mwa kichwa kibovu.
“Ninakusikiliza ni kitu gani unataka, Sam unafikia hatua ya kumgusa hadi raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania….”
“Mmeigeuza Ikulu kama gesti mnaingia tu kizembezembe kufanya mambo yenu ya kiharamia. Mafisadi wakubwa nyi, mnawaacha askari polisi wakiishi katika nyumba za mabati zilizogawanywa kwa maboksi ndani yake, vyoo havitamaniki. Eti mnataka kwa maisha yale waache kula rushwa, mnavimbisha matumbo yenu na kuvaa suti za gharama ya juu. Naomba nikate simu nitakapopiga tena nitahitaji kujua msimamo wako.
Ole wako uzunguke na kuanza kuunda mpango wowote ule wa kumwokoa mtoto wako, IGP sina utani na sijawahi kutaniana na wewe… utaokota viungo katika mikoa niliyokutajia….. kuwa mtulivu na makini katika hili. Kumbuka huyu ni mtoto wako pekee wa kike na sio mtoto wenu wewe na huyo Saidi anayejiita raisi…..alamsiki IGP” Sam akamaliza na kukata simu kisha akaizima.
Akamtazama binti yule mrembo akiwa anabubujikwa na machozi. Akamwonea huruma lakini hakuonyesha jambo hilo machoni. Alitamani sana kumweleza kuwa yeye si muuaji wala mtu mbaya lakini alitambua kuwa ule haukuwa wakati muafaka kufanya vile.
“Nilichomwambia baba yako nitakifanya kwa vitendo, huenda ni mapema kuliko nilivyomwahidi.” Sam akamweleza yule binti kisha akafungua mlango na kutoka nje huku akiufunga mlango ambao alikuwemo yule binti.
*****
VURUMAI likakolea nyumbani kwa IGP, mkewe akawa mbogo akitaka kujua ni kitu gani kinaendelea kwa mwanawe pekee wa kike.
IGP alitamani kumweleza juu ya maelekezo ya Sam juu ya kinachoendelea lakini alilikumbuka onyo la Sam juu ya kuwa makini ili aisije kusababisha kifo kibaya kwa mwanaye.
IGP alitambua wazi kuwa kwa kumweleza mkewe kila kitu angekuwa amevujisha siri na hapo zingesambaa na kisha kumkera Sam ambaye angechukua maamuzi ya kumuua mtoto wake.
Mambo ya wanawake aliyajua!
Alipofikiria aina ya kifo ambacho Sam alikuwa amemwelezea alisisimka na kumweka Sam katika daraja la watu hatari sana wanaotakiwa kuogopwa.
Akataka kuwasiliana moja kwa moja na raisi, lakini akakumbuka kuwa Sam alimsisitiza kuwa mtoto ni wake yeye na si mtoto wake yeye na raisi kwa pamoja. IGP akakiri kuwa alikuwa amewekwa kikaangoni.
Kwa usiku ule asingeweza kuupata usingizi, kwa sababu mkewe alikuwa haishi kulia na kulalamika bila kukoma.
IGP akasimama na kuvaa suruali yake.
“Unaenda wapi baba Suzani…” Mkewe akamuhoji.
“Naenda kufuatilia hii simu iliyonipigia….” Alijibu IGP kinyonge kisha akaondoka.
Akawasha pikipiki yake na kuondoka, wazo la aende wapi lilikuja akiwa juu ya pikipiki yake. Akabadili uelekeo baada ya kupita mataa ya Magomeni akiwa anatokea Kimara akaamua kuunganisha moja kwa moja hadi feri. Akakiwahi kivuko akaingia yeye na pikipiki yake. Akavuka hadi upande wa pili.
Kisha akaendesha kwa kasi akafika mahali alipokuwa anahitaji.
Alipokelewa kwa mitutu ya bunduki na askari wanne waliokuwa wakiilinda nyumba ile. Lakini baada ya kuvua kofia ngumu aliyokuwa amevaa wote walishusha bunduki zao chini na kisha kumpigia saluti kikakamavu, yeye akajibu kizembe.
“Robert yupo ndani?” aliuliza huku akiegesha pikipiki yake kando. Askari mmoja akamsaidia. Na mwingine akamkimbia ndani kwenda kumwamsha mzee Robert Masawe mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi.
Baada ya dakika kumi wawili hawa walikuwa wamejitenga kando wakiwa katika mazungumzo mazito sana.
“Masawe.. Sam atamuua yule mtoto, we unajua Masawe nimehangaika sana hadi kupata mtoto wa kike, hivi nitaweza kuishi tena unadhani. Masawe nimekimbilia kwako naomba unishauri kabla sijaamua kumkabili raisi kama itabidi…” IGP alijieleza huku akiwa anaukosa utulivu wa akili yake.
Masawe alikuwa msikivu huku moyoni mwake akiwa anatabasamu pana sana. Aliamini kuwa ile barua pepe aliyoituma kwa Sam hatimaye alikuwa ameifanyia kazi.
Lakini kitu ambacho hakukitarajia ni Sam kumteka mtoto wa IGP. Hapo akakiri kuwa wapo vijana wanaoweza kupambana kwa ajili ya taifa lao.
“IGP hili jambo sio la kukurupukia hata kidogo, maana kosa moja litagharimu uhai wa mtoto. Raisi wetu unamjua vyema si mtu wa kutunza jambo kifuani mwake, ukimwambia atakurupuka na kupiga simu Marekani ili apate msaada wa CIA… atakapofanya hivyo na kisha Sam agundue kuwa anafuatiliwa na watu hao haki ya Mungu nakuapia tutamzika Suzan.” Masawe alimweleza IGP na kila alipokuwa akitaja neno ‘kifo’ IGP alikuwa akiukunja uso wake na kujipigapiga kifuani.
“Sasa mi nafanya nini… maana amedai kuwa tumfichue BvB mara mimi na raisi tuache ufisadi.. sielewi hata jambo moja Masawe naapa na ukweli mtupu kwa jina la mama yangu aliyetangulia mbele za haki. Masawe sijui lolote mimi….” Na hapo IGP kashindwa kuzungumza akaanza kutokwa machozi na kisha kilio cha kwikwi.
Amakweli penzi lina nguvu ya ajabu. Robert Masawe hakuamini hata kidogo kuwa IGP shupavu kama yule anaweza kulia kama mtoto mdogo. Lakini pia akapata mwanga kuwa yawezekana ni ukweli mtupu kuwa IGP hajui lolote bali anaishi tu kwa amri za raisi wa nchi.
Robert akampigapiga bega IGP na kumsihi awe mtulivu na anyamaze ili waweze kujua ni kitu gani wanatakiwa kufanya.
“Kwani wewe unamjua BvB huyo ambaye unatakiwa kumfichua.”
“Nimewahi kumsikia tu lakini siijui hata sura yake….”
“Kuna siri zozote raisi anafanya na wewe labda.”
“Hapana Masawe mimi ananiamuru na ninafanya atakavyo lakini sina siri naye.”
“Na vipi kuhusu Sam kusakwa auwawe, unajua lolote lililojificha hapo. Kwanini auwawe…. Unahisi hakuna uhusiano na jambo lolote unalolijua?” Masawe akamuhoji kwa utulivu.
“Masawe, kila kitu anajua raisi mimi naamrishwa tu na unajua sitakiwi kupinga hovyohovyo….” Alijibu huku akilalamika IGP. Masawe akatambua kuwa anachosema ni ukweli mtupu.
“IGP naomba nikueleze jambo ambalo nadhani litaweza kuleta majibu mawili, ni kifo cha mwanao ama uhai wake tena.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Aaah! Masawe usiniambie kuhusu Suzani kufa.. acha Masawe najisikia vibaya mno…” alilalamika IGP.
Na hapo mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi akamweleza Masawe juu ya kile anachojua ama kuhisi juu ya sintofahamu ya hila zinazoendeshwa kimyakimya na serikali. Ubadhilifu wa pesa na ufisadi uliokithiri.
“Steven Marashi kijana wetu yule unadhani amekufa kifo cha kawaida…. Si bure IGP. Unachotakiwa kufanya wewe kama wewe sasa kwa ajili ya mwanao, zungumza na Sam akikupigia simu zungumza naye kwa upole kabisa. Mwambie upo tayari kufanya atakavyo yeye na ikiwezekana hata kushirikiana naye.
“Sasa Masawe..” akasita kuzungumza aliisikia simu yake ikitetema, akajipekua akaitoa na kukutana na namba mpya.
“Nani mwenzangu….”
“Dady please! Please Dady, help me. Ataniua huyu, mpe anachotaka baba… nakuomba.” Sauti ya Suzan ikasikika ikilalamika.
IGP akataka kupasuka kwa hasira iliyochanganyikana na mshtuko.
“Upo wapi Suzan, anataka nini huyo eeh!”
“Anataka wewe na mheshimiwa raisi mseme ukweli na kisha kujivua madaraka ikiwezekana.”
“Nini anasema ukweli upi anataka, nieleze mwanangu nipo tayari kwa lolote ili wewe uwe na amani… nini anataka huyo.”
“Dady… amezungumza nami kwa kirefu sana, BvB ni nani baba, ni nani huyo? Na vipi kuhusu Masele….. ulichokitangaza juu yake una uhakika nacho baba. Tafadhali baba nisaidie nitakufa….” Suzan alijieleza upesiupesi, maneno ambayo yalimchanganya IGP vibaya mno.
“IGP natoweka kwa sasa lakini nitakayopiga kwako itakuwa simu ya mwisho. Ubia mlio nao na mtu wa kuitwa mzee Matata si sahihi kwa nchi yetu, na yeyote yule wa kujiita BvB hana nafasi katika nchi hii huru, kesho nitahitaji kujua nini hatma ya mchumba wangu Tina, maana kama si jeshi lenu kumziba mdomo basi najua unafahamu alipo. Ikiwa ataendelea kufichwa ili aisiseme ukweli basi na mimi nitaendelea kubaki na mwanao hadi siku nitaamua kumuua….” Akamaliza Sam na kukata simu.
IGP akataka kutia neno lakini hakubahatika!
Simu ikawa imezimwa!
IGP akazidi kuchanganyikiwa, Masawe akamtuliza na kisha akamweleza jambo ambalo lilikuwa na maana kubwa sana kwake kwa usiku ule.
Masawe akaelezea juu ya vile vichwa vine vya wazungu vilivyokutwa nje ya nyumba ya waziri wa nishati na madini, Mathias Obhare.
Akamueleza kuwa wale wanne ni watu walewale ambao waliagizwa hospitali ya Lugalo na mzee Matata kama madaktari kuokoa maisha ya Gama, kitu ambacho hakikuwa kweli hata kidogo. Taarifa hiyo Robert hakumweleza IGP kuwa alipewa na nani lakini dokta Mosha ndiye aliyemweleza kwani alikuwepo usiku ule wa mchezo ule.
IGP akashtushwa na taarifa ile lakini Robert akamsihi afanye mambo yake taratibu kichwani lakini kasi kimatendo ili aweze kujua kuna jambo gani linaendelea kati ya raisi na mzee Matata na baada ya hapo atapata jibu.
IGP akaagana na mrakibu msaidizi Robert Masawe huku akiahidi kuwa makini kwa kila hatua yake.
*****
Siku iliyofuata zikiwa ni siku mbili tangu vichwa vine vya wazungu vikutwe nje ya nyumba ya waziri wa nishati na madini.
IGP aliamua kuitumia siku hiyo kwa ajili ya kujua kuna nini kati ya mzee Matata na raisi wan chi. Alikusudia kufanya jambo lile la hatari kabisa kwa maslahi ya mtoto wake ambaye yupo mikononi mwa Mzee Matata. Kwa kuupata ukweli basi angeweza kumshawishi Sam aweze kumwacha huru mwanaye pasipo kumdhuru.
Alikuwa ameyapanga maswali yake vyema jinsi ya kumwingia mtu yule mzito. Akajipanga kumnyenyekea na kumwagia sifa za kutosha ili aweze kuuingia mkenge na kuyasema maneno ambayo alikuwa akiyahitaji.
Wakati huu hakuondoka na pikipiki bali gari yake.
MATATA MATATANI
MZEE MATATA kama ilivyokuwa kawaida yake, kila mambo yanapoharibika alikuwa anajipooza hasira zake kwa kumwadhibu Tina ambaye alikuwa mateka wake. Alikuwa akifanya hivyo kwa kuamini kuwa mchumba wa Tina ndiye aliyekuwa nyuma ya haya yote.
Na hata baada ya kuuwawa wazungu wanne ambapo mzee Matata aliamini kuwa mkono wa Sam unahusika, alikivamia chumba cha Tina kwa lengo la kumwadhibu. Na adhabu aliyoipanga siku ile ilikuwa kubwa zaidi, alipanga kuuondoa uhai wa Tina.
Lakini kabla ya kuuondoa uhai wa binti yule aliwaza kuzimalizia hasira zake kwa kumbaka na baada ya hapo amuue kwa namna yoyote ile.
Kitu ambacho alisahau ni kwamba siku ile alivyoitwa na raisi ghafla huku akiwa amechanganywa na simu kutoka uholanzi, aliondoka na kusahau kufunga kile chumba.
Na ni upenyo huo ambao Tina aliutumia vyema ili aweze kujikomboa. Nafasi ambayo ilibadili kila kitu.
Mzee Matata alifika na mkanda na kuanza kumchapa Tina huku akimuuliza maswali yasiyojibika.
Kisha akamuamuru avue nguo zake zote.
Amri hii ilimtisha Tina na kuona kama mpango wake unataka kuharibika. Hakuwa tayari kuvua nguo kirahisi namna ile kama Matata alivyotaka. Na hapo akaamua kucheza na hisia za Matata.
Mwanamke mwanamke tu!
Tina akaitoa nguo yake ya juu.
Matiti yakabaki kumtazama mzee Matata. Tina akalitazama koo ya mzee Matata akaliona linapanda juu na kushuka.
Mate ya tamaa yamemezwa! Akajisemea huku moyo wake ukitabasamu kwa jinsi mzungu yule alivyokuwa akienda kuuvaa mkenge.
Hapohapo Tina akamvamia mzee Matata, kwa maksudi kabisa akayaruhusu matiti yake kukichoma kifua wazi cha yule mzee.
Mzee Matata akatokwa na neno tamu la kimahaba kwa lugha ya kiingereza. Wakati mzee Matata anaanza kupagawa, Tina alikuwa kwenye akili zake timamu kabisa na alitambua kuwa zile zilikuwa dakika zake za mwisho za kujitetea.
“Mkeo hawezi kuja kuchungulia jamani…” Tina akahoji kwa sauti nyororo katika masikio ya mzee Matata.
Mzee yule akacheka kama bwege!
“Nipo na mlinzi tu hapa, yupo getini huko… vua basi mpenzi… yaani ukinipa vizuri nakuachia uondoke…” Matata akabubujikwa na maneno, joto la mtoto wa kingoni lilikuwa limeondoka na utimamu wake.
Naam kama alivyoamriwa kuvua nguo, Tina akaingiza mkono katika nguo yake ya ndani, akaibetua kama anayetaka kuivua, wakati huo mzee Matata akiwa amejikita katika kulambalamba matiti ya Tina.
Mkono wa kuume wa Tina ukaendelea kuhangaika katika chupi, wakati ule mwingine ukiwa unampapasa na kumfinyafinya mzee Matata.
Mkono wa kuume ukaibuka na kisu kidogo ambacho Tina alikipata ndani ya ile nyumba siku ambayo mlango ulisahauliwa wazi.
“Mzee Matata… I love you sana baby wangu!” Tina akamdhihaki mzee Matata, kisha akauzamisha ulimi wake katika sikio baridi la mzee Matata.
Pumzi za yule mzee zikapanda juu, wakati zinashuka Tina naye akaushusha mkono wake katika tumbo la yule mzee.
Uchovu wa tamaa za kimwili, na makali ya kisu kikali, mzee Matata akashindwa kupiga kelele akaanguka chini. Tina akamrukia na kuzamisha tena na tena katika tumbo lile kubwa. Damu ikamrukia usoni lakini hakujali.
Alikuwa na roho ya kinyama!
Naam! Na alikuwa sahihi, maana hata yeye alitendewa unyama haswa.
Mzee yule akatokwa na kelele hafifu kisha akaanguka chini huku akifanya jitihada za kuzuia utumbo wake usimwagike chini.
Tina alibaki akiwa amekishikilia kisu kile huku akingoja yeyote yule atakayejitokeza mbele yake na amwangamize.
Hakuna aliyejitokeza!!
Akiwa vilevile alitoka hadi nje, akamwona mlinzi getini akiwa ameshika kirungu tu. Muonekano wa Tina ulikuwa kama mzimu tu, alikuwa ametapakaa damu na nywele zake zilikuwa zimetimka hovyo.
Na kwa jinsia livyokuwa amekonda, mlinzi alikuwa na haki ya kukimbia.
Tina akatoka mbio huku akikitupa kile kisu, barabara nzima alionekana kama kichaa kwa jinsi alivyokuwa. Lakini ni nani wa kujali jijini Dar kila mtu akaendelea na mihangaiko yake.
Tina akazidi kuambaa na kupotelea mbali huku mapigo yake ya moyo yakiwa yanadunda sana. Kadri alivyozidi kukimbia alikuwa akizidi kuona watu wakipungua, hilo lilimfurahisha sana lakini hakujua ni wapi anapoelekea ikiwa ni salama ama la!
Aliyakumbuka yote aliyowahi kushuhudia katika jumba lile.
Aliwahi kumwona raisi wa nchi katika jumba lile. Hili nd’o jambo lililomsisimua zaidi. Na pia kumfanya ahofie kukutana na polisi. Maana ikiwa raisi alikuwa akifika katika jumba lile basi bila shaka anafurahia vitendo vilivyokuwa vikifanyika pale ndani.
Kwa kukamatwa na polisi angeishia kurejeshwa kulekule alipokuwa ametoroka.
Alipenya asijue anapoelekea hadi pale aliposikia akiamrishwa kusimama. Mkojo ukataka kumtoka Tina.
Akatamani kukimbia lakini akahofia kuzua jambo jingie, kwanza mwili wake ulikuwa dhaifu bado. Na kitendo cha kukimbia ilikuwa kuhalalisha kuwa yeye ni mkosefu.
___
UOGA ulimvaa IGP baada ya kuikaribia nyumba ya mzee mazoea ya kumtetemekea mzee huyu yalikuwa yanamtafuna. Ilikuwa heri kuikaribia ikulu kuliko kulikaribia jumba lile la tajiri yule kutoka magharibi.
IGP alijiuliza ataanza kumuuliza maswali gani ili walau aweze kuupata mwanga juu ya nini kinachoendelea kati yake na raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Uoga wake ulienda kando baada ya kukumbuka kuwa alitakiwa kuujua ukweli ili kuuokoa uhai wa mtoto wake pekee wa kike ambaye kutoweka kwake kulikuwa kumeipoteza amani ndani ya nyumba yake.
Wakati akiwaza haya IGP alimtilia maanani msichana aliyekuwa akitembea upesiupesi huku akionekana mwenye hofu. IGP alitaka kujishughulisha naye lakini akatambua kuwa hilo halikuwa la msingi sana kwake kwa wakati ule badala yake alitakiwa kutilia maanani upelelezi wake.
Akatelemka garini na kulifikia geti ambalo nusu lilikuwa wazi na nusu likiwa limefungwa.
Akalisukuma huku akitarajia kukutana na mlinzi ambaye atamweleza ikiwa mzee Matata yupo ndani ama la kwa sababu awali alikuwa amempigia simu na haikupokelewa.
Pale mahali anapoketi mlinzi hakukuta mtu! Akatembeza macho yake huku na kule bado hakuambulia kitu, akashusha pumzi na kutazama chini. Na ghafla akayakodoa macho yake katika marumaru iliyokuwa imetapakaa katika ua wa nyumba ile.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akainama na kutazama kwa makini. Akajihakikishia kuwa ile ilikuwa ni damu. Akajaribu kutazama ni wapi ilikuwa imetokea, akayaona madoa kadhaa kuelekea ama kutokea kwenye nyumba ya mzee Matata.
IGP akaichomoa bastola yake kiunoni upesi na kuishika kwa umakini kabisa kisha akanyata kufuata alama zile zilizoachwa na damu.
Akafika hadi mlangoni, kabla ya kuingia akachukua simu yake ya upepo na kutoa taarifa za hali ya hatari kwenye nyumba anayoishi mzee Matata.
Kisha akaupiga teke mlango uliokuwa wazi, akataraji kukutana na kiumbe hai lakini haikuwa hivyo, akazidi kuifuatilia ile damu.
Naam! Akakifikia chumba ambacho hakikuwa na michirizi bali dimbwi la damu.
Na aliyekuwa anaogelea katika dimbwi lile alikuwa mzee Matata ambaye ulimi ulikuwa umemtoka nje.
IGP akapiga simu ya dharula na kuhimiza kikosi cha huduma ya kwanza kifike upesi. Na hata kabla hajakata simu alizisikia gari za polisi zikifunga breki nje ya geti. Akakumbuka kuwa alipiga simu kabla hajaingia ndani kuhitaji msaada wa dharula.
Mwili wa Matata ukachukuliwa na kupelekwa hospitali upesi huku ile nyumba ikiwekewa ulinzi mkali na upelelezi ukiwa unashika hatamu juu ya nani aliyeshiriki katika tendo lile.
IGP alikuwa amepagawa zaidi kwa sababu hakuwa amefanikisha kusudi lake la kumtambua mzee Matata kiundani hasahasa mahusiano yake na raisi wa nchi. Kitu ambacho kilimaanisha alikuwa anamsogeza mwanaye mpenzi hatua moja zaidi katika umauti. Hakujua atajitetea vipi ili aeleweke na kupewa muda zaidi wa kuutafuta ukweli.
Hofu yake ikamtisha mkewe na mdogo wake wa kike ambaye alikuwa akiishi nyumbani kwake.
Akaanza mkewe kilio cha kwikwi, mdogo wake naye akafuatia. Kisha kikawa kilio kikubwa. Wakawa wanaomboleza kifo cha Suzan.
IGP alijaribu kuwakanya lakini hakuweza kuzimisha kilio chao, simu zikapigwa kwa ndugu na jamaa. Ni kama walikuwa wanaalikwa pale ili kusaidia kupaza sauti za vilio.
Mkewe akaenda mbali zaidi na kumpigia simu raisi wa nchi ambaye walikuwa na mawasiliano ya karibu. Akamweleza kuwa Suzan amekufa lakini IGP hataki kusema ukweli kwa sababu anamjua mtekaji wa mwanaye.
IGP alichukizwa na tabia ya mkewe ya kutokuwa mvumilivu, lakini kwa hali aliyokuwanayo asingeweza kumrekebisha.
Akiwa yu chumbani mara simu yake ikaita, akatambua moja kwa moja kuwa atakuwa ni raisi anataka kupata uhakika iwapo ni kweli maneno aliyoelezwa na mke wake. IGP alijifikiria sana maswali ya mitego atakayokutana nayo huku akilikumbuka na onyo la Sam kuwa asije akathubutu kumshirikisha raisi juu ya jambo lile. Akaipuuzia simu ile hadi ikakatika.
IGP akataka kuizimisha simu yake lakini akahofia kuzua jambo jingine kubwa kuliko hili ambalo lilikuwa linatoke.
Simu yake ikaita tena.
Akaipokea kwa utulivu huku akijiahidi kuwa hatazungumza lolote la maana na raisi zaidi ya kumwambia kuwa ampe muda.
“IGP…..” akataka kujitambulisha lakini sauti ya upande wa pili ikamkatisha.
“Nakutambua mkuu, tunakuhitaji Makongo jeshini. Kuna tukio linakuhitaji wewe, ni sasa hivi tunakuomba tafadhali. Kijana wetu yupo nje ya nyumba yako unaondoka naye sasa hivi mkuu. Luteni K” Upande wa pili ukazungumza na kisha simu ikakatwa.
IGP akaghafirishwa na amri ile aliyopewa lakini amri za jeshi zote ni sahihi hivyo alijiandaa na kuondoka akiacha kilio nyuma yake huku mkewe akisisitiza kuwa anataka kuiona sura ya mwanaye kwa mara ya mwisho walau aweze kuaga.
IGP hakujibu kitu!
Akatoka nje na kupokelewa na mwanajeshi ambaye alikuwa katika magwanda yake rasmi.
Wakaondoka kwa kutumia gari alilokujanalo yule mwanajeshi.
Punde tu baada ya kuingia ndani ya ile gari, walitokea mafichoni wanajeshi wengine wawili vijana. Wakamshurutisha IGP kuwapatia simu zake zote, akatii bila kuleta ubishi. Na hakuzungumza lolote hadi walipofika Makongo jeshini. Akaingizwa katika chumba ambacho kilikuwa na viti vine, akaamriwa kuketi katika kiti kimojawapo.
LUTENI K :IGP unamfahamu vipi mzee Matata….” Alikumbana na swali kutoka kwa mjeshi aliyeitwa Luteni K.
IGP:Mwekezaji kutoka nje.” Alijibu kwa ufupi.
LUTENI K: Ni hilo tu unalofahamu…”
IGP:Mengine nimeryasikia kama tetesi tu hivyo siwezi kuyatumia kama majibu.”
LUTENI K :Mfano wa hizo tetesi…”
IGP:Mzee Matata ni mojawapo wa mafisadi na mnyonyaji katika nchi hii…”
LUTENI K :”Baada ya kusikia hizo tetesi umewahi kuzifanyia kazi.”
IGP:N’do nilikuwa naanza kufuatilia nikakutana na tukio la Mzee Matata kujeruhiwa ama kujijeruhi bado sijaelewa.”
LUTENI K:Unamfahamu binti anayeitwa Tina…”
IGP:Wapo wengi sijui Tina yupi
Luteni K hakujibu kitu badala yake alitoa amri kisha mbele yake akaletwa binti ambaye awali akiwa ndani ya gari lake wakati akienda kwa mzee Matata alimuona akiwa anahangaika mtaani huku akiwa na hofu.
Alikuwa ni Tina!
“Umewahi kumwona binti huyu…” Luteni akampiga swali IGP, hakika haikuwa mara ya kwanza wala ya pili kumuona. Akakiri kumwona masaa machache kabla ya kushuhudia tukio la kujeruhiwa kwa mzee Matata.
“Nimewahi kumwona… lakini sijui iwapo anaitwa Tina.”
“IGP huyu anaitwa Tina, na anadai anao ushahidi kuwa raisi wa nchi ni msaliti. Na kama yeye ni msaliti basi wewe lazima utakuwa kibaraka wake. Jeshi limekasirika sana, na halijaanza kukasirika sasa hivi, miaka hii mitano ya mwisho ya utawala wenu imekuwa migumu sana kwa jeshi. Chakula ni cha shida na hakuna ile hali ya kujaliwa zaidi ya kutuchukua na kutubwaga nchi zenye vita na kwenda kufia huko kwa kigezo kuwa tunasaidia kurejesha amani. Baada ya kufa familia zetu zinateseka na kuishia kuyalaumu makaburi yetu.
Sasa nimekuita hapa baada ya mawasiliano ya dharula na wenzangu.. tunach….” Kabla hajaendelea simu ya IGP iliyokuwa mikononi mwa mwanajeshi aliyeenda kumchukua iliita.
_____
MAKAMBAKO, NJOMBE.
SAM alikuwa katika mfadhaiko wa hali ya juu sana, alimwona IGP kama mpumbavu asiyejijua kama yeye ni mpumbavu. Kitendo cha kusikia kuwa mzee Matata yu mahututi baada ya kujeruhiwa kwa visu tumboni akiwa nyumbani kwake ilimaanisha kuwa ule ulikuwa mpango madhubuti uliosimamiwa na Raisi ambaye amegundua kuwa mambo yanaenda mrama.
Na angejuaje ikiwa IGP hajamweleza juu yake?
Alijiuliza na hapo akakumbwa na pepo mchafu ambaye awali alimfanya kama utani lakini sasa alimaanisha.
Sam akajifikiria kumuua Suzan kisha ikiwezekana na yeye ajiue akaungane na Tina wake ambaye hadi wakati ule aliamini kuwa amekufa.
Sam akaingia katika nyumba ambayo aliijenga kijijini kwa baba yake, ambayo ndani yake alikuwa amemuhifadhi Suzan. Kabla ya kufanya lolote alichukua pombe kali na kuigida katika kipimo alichoona kimemtosha.
Baada ya hapo akachukua panga ambalo lilikuwa linang’ara kutoka na upya wake.
Nakata kiungo kimoja baada ya kingine, kisha napiga picha nawatumia waandishi… lazima niwatese kama walivyonitesa wao! Alijisemea Sam huku uoga ukiwa mbali naye.
Alitaka kutimiza dhambi ile kisha ajiue lakini alitamani kuisikia sauti ya IGP ikilia kwa uchungu wakati atakapokuwa anamsikiliza mwanaye akilia wakati kiungo kimoja baada ya kingine kikitolewa.
Sam akajiapiza kuwa hatasikiliza uongo wowote kutoka kwa IGP badala yake yupo tayari kukisikiliza kilio chake tu.
Akatoka tena nje akalitazama jua lilivyokuwa linaanz akuchomoza lakini lisiweze kushindana na baridi.
“Nisamehe baba… nakuja kwa Tina wangu…” alizungumza na anga, kisha akajihisi kama amebarikiwa kufanya vile.
Akaingia na kulichukua panga kali katika mkono wake, akamvamia Suzan na kumziba mdomo.
Kisha akamfunga kamba imara kabisa!
Kitu kizuri ni kwamba nyumba ile ilikuwa imejitenga mbali sana kutoka kwa wanakijiji wengine hivyo hakuwa na mashaka yoyote endapo Suzan atapiga kelele.
Baada ya kumfunga vyema, akachukua simu yake na kuiwasha kisha akampigia IGP.
Simu ikaita muda mrefu na hatimaye ikapokelewa.
”Picha za mtoto wako … aah sorry picha za viungo vya mtoto wako nimeamua sitavisambaza Tanzania nzima badala yake nitawatumia waandishi wa habari ili waweze kujaza katika kurasa za mbele za magazeti yao. Na nimekupigia simu hii ili uwe unamsikia mwanao kila hatua yake ya kukaribia umauti, sikupi nafasi ya kuzungumza naye lakini nakupa nafasi ya upendeleo kumsikia akiwa analia kilio cha mwisho… pumbavu mkubwa wewe. Ni shauri lako sasa iwapo utakata simu ama la…..”
Sam hakusubiri IGP ajibu kitu chochote akaiweka ile simu kando, na kisha akalichukua panga lake kali. Akamtazama Suzan kisha akamsogelea na ghafla akaliachia panga kwa kasi kubwa likamfikia.
Suzan akatokwa na yowe kubwa lenye mchanganyiko wa hofu na kila aina ya uchungu.
Sam akamtukania mama yake. Akalinyanyua tena, awali alimpiga kwa kutumia ubapa lakini sasa aliyaweka makali katikati. Akaushika mkono wa yule binti na kuutandaza vyema wakati huo alisikia simu yake IGP akilalamika maneno ambayo hakuyasikia.
Sam akalinyanyua panga ili aweze kufyeka vidole vya Suzan mara akagutushwa na kitu.
Hakuamini macho na masikio yake!
****
IGP alikosa uvumilivu baada ya tamko lile la Sam, alikuwa kama mwehu akamrukia Luten K bila kujua kwa nini amemrukia.
“Anamuua mtoto wangu… luteni nisaidie anamuua.. luteni sina mtoto mwingine wa kike… luteni sijui lolote kuhusu maasi ya raisi. Mimi si kibaraka luteni natii amri za jeshi. Mkubwa hakosei!! Wajua Luteni wajua….” Alilalamika IGP huku akilia kama mtoto na kamasi zikimtoka.
Luteni K alibaki katika mshangao asijue nini cha kufanya. Anamsaidia vipi wakati iliyopo mbele yake ni simu na si mtu.
Alijaribu kumtuliza lakini IGP alikuwa kama mwendawazimu, mara akimbie huku mara ajikune hapa mara pale.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakika alikuwa amechanganyikiwa!!
Akiwa na simu yake hana hili wala lile zaidi ya kukisikia kilio cha mtoto wake ambaye alikuwa anaugulia kipigo kutoka kwa Sam.
Mara ghafla alishtuka akikwapuliwa ile simu na binti ambaye haikuwa mara ya kwanza kumuona. Alikuwa ni binti ambaye alimuona akihaha huku na kule barabarani wakati anafika kwa mzee Matata kisha akamchukulia kuwa ni mwendawazimu na kumpuuzia.
Sasa binti yule alikuwa ameishika simu yake huku kila mtu pale ukumbini akimkodolea macho.
“Sam…. Sam kama unanisikia please acha unachotaka kukifanya… kiache na unisikilize mimi Sam…. Saaam!!” alizungumza yule dada kwenye simu kwa sauti ya juu.
MAKAMBAKO, NJOMBE TANZANIA.
Sam akaisikia ile sauti iliyokuwa na maana kubwa kwake, sauti ambayo kwa mara ya mwisho aliisikia ikilalamika kwa wivu kabla hajatoweka na maaskari na hakuwahi kumuona tena. Upesi akasita kile alichokuwa anakifanya, akaikwapua ile simu na kusikiliza kwa makini.
“Tina….. Tina ni wewe mpenzi wangu… Tina nihakikishie kuwa ni wewe… nihakikishie Tina.” Sam alizungumza huku akiwa katika mgawanyiko wa taharuki mbaya.
Na hapo akaisikia sauti kutoka upande wa pili ikijibu. Wakati inajibu wakajikuta wote kwa pamoja wakizungumza.
“Moyo wangu ukatua kwako, nafsi ikakiri kukuhitaji. Nitaziheshimu hisia zako, nitakupa penzi langu lote. Na Mungu atulinde hadi kesho itakapokosa kesho nyingine”
Hakika alikuwa ni Tina na Sam. Maneno hayo hakuyafahamu mtu mwingine bali wawili hawa tu.
Naam! Machozi yaliyotiririka Njombe yakatiririka katika jiji la Dar es salaam pia.
Sam na Tina walibubujikwa machozi ya furaha!
“Naomba usifanye lolote ulilotaka kulifanya…”
“IGP nd’o alikuwa amekuteka?” Sam aliuliza, Tina akakanusha. Na kumsihi afanye hima kurejea jijini Dar es salaam kwani kuna mambo anatakiwa kuyajua upesi sana.
“Kesho nakuja! Nitakuja na Suzan ikiwa tu utaniambia wewe bila kushurutishwa kuwa nije.”
“Sam sijashurutishwa na mtu yeyote. Njoo Dar es salaam.” Tina akasisitiza.
Baada ya hapo simu ikakatwa!
Luteni K akabaki kumshangaa Tina bila kusema chochote. IGP alitamani kusema neno lakini akakosa la kusema mbele ya Tina, akamsogelea na kupiga magoti mbele yake ili amshukuru.
IGP akiwa analia kama mtoto mdogo, Tina akajisikia fadhaa sana. Na yeye machozi yakamtoka, akapiga magoti na kumkumbatia IGP.
KIKOSI KAZI KAMILI.
UWANJA wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere ulikuwa umetapaa mamia ya watu, kila mmoja akitambua ni jambo gani lililompeleka pale. Wengine kupokea wageni wao na wengine kusafiri lakini wapo pia ambao hawakuwa na kazi bali walienda kuketi na kuvuta hewa safi inayopatikana maeneo yale.
Muda ulizidi kusonga huku hekaheka zikiongezeka na kupungua. Ndege ilipotua pirika ziliongezeka na pia wakati anakaribia kupaa.
Ndege ya shirika la kimataifa ilitua majira ya saa kumi alasiri. Pirika pirika hazikuwa nyingi sana kama ambavyo ilikuwa kwa mashirika ambayo yanafanya safari za ndani pekee.
Abiria waliowasili hawakuwa wengi sana. Hivyo iliwapa wepesi hata watu waliokuja kuwapokea kuwapata kirahisi.
Baada ya muda kidogo alitoka mgeni ambaye alikuwa akisubiriwa kwa hamu na makundi matatu pale uwanjani.
Wa kwanza ni wale walioenda kumpokea kwa ajili ya kumfikisha ikulu ambapo alikuwa na mazungumzo na raisi, hawa walikuwa watu watatu na mmoja kati ya hao alikuwa ni kijana kutoka usalama wa taifa.
Kundi la pili lilikuwa jeshi la mtu mmoja tu, huyu hakuwa makini katika macho yake lakini akili yake ilifanya kazi maradufu. Baada ya wageni wale kupokelewa ndipo akatambua kuwa yawezekana mtu anayemuhisi akawa ndiye yule aliyepokelewa.
Huyu alikuwa ni Yakubu Gama, hakuwa akiijua sura ya BvB lakini uwepo kijana kutoka usalama wa taifa ambaye aliwahi kufanya naye kazi kabla hajakumbwa na dhahama na kisha kutangazwa kuwa alipoteza uhai.
Alizifuatilia nyendo za kijana yule hadi pale walipompokea mzungu aliyekuwa amejivika kofia ya pana huku akiwa hana mzigo wowote zaidi ya bahasha ndogo mkononi mwake. Hawakupoteza muda wakatoweka na kuingia katika gari.
Gama hakuwa na papara alingoja waondoke kwanza ndipo aanze kuwafuatilia ili ajue ni wapi wanaelekea na iwapo itabidi aweze kuzusha vurumai na kuupata muafaka. Kitu ambacho aliombea sana kisitokee ni mgeni yule kupelekwa ikulu moja kwa moja. Kwani kwa kufanya vile alijua asingeweza kuipenya ngome na kuingia na hata kama angefanikiwa basi mwisho wake ingekuwa umauti.
Gama aliingia katika gari aliyokuwa amekuja nayo, lakini kabla hajaanza kuwafuatilia aliona kundi jingine ambalo lilikuwa na watu wawili. Walikuwa wakipeana maelekezo fulani ambayo hakuyasikia lakini walikuwa wakinyooshea mkono gari lililokuwa linatoweka.
Gama akatulia kidogo, akatoa sigara yake na kuanza kuvuta akiwategea watu wale waanze kuondoka kwanza.
Walipoingia katika gari yao naye akawasha na kuwafuata kwa tahadhari kubwa huku akiyaruhusu magari mengine mawili yamtangulie ili kuondoa dhahania kuwa anawafungia tela watu wale.
Uwepo wa yule kijana makini wa usalama wa taifa ulimfanya Gama aongeze umakini ili asiweze kushtukiwa.
_____
HOSPITALI ambapo alikuwa amelazwa Mzee Matata hali ilikuwa tulivu sana, madaktari walikuwa wamemrejesha katika chumba cha wagonjwa wa kawaida akiwa ametolewa katika kile cha wagonjwa mahututi na wakati huu alikuwa akipumua bila kutumia mipira maalumu.
Na alikuwa amezuia kufanyiwa mahojiano yoyote yale na askari polisi ama yeyote aliyetakiwa kujua juu ya nini kimemsibu.
Mpelelezi wa kesi ile ya mzee Matata kujeruhiwa akaishia kuandika jina la mjeruhiwa bila maelezo yoyote katika faili lake. Mzee Matata hakutoa maelezo yoyote yale.
Aliifanya Tanzania kama ya kwake vile!!
Alichotegemea ni kwamba baada ya kupata nafuu ataenda ikulu kuzungumza na raisi juu ya kilichomtokea na baada ya hapo basi yeyote aliyehusika na hata asiyeuhusika ataishia jela.
Hakujua kuwa maji yameanza kuzidi unga hivyo kuna kila dalili ya kula ugali mbichi.
Nje ya chumba alichokuwa amelazwa mzee Matata. Alikuwepo mwanamke ambaye alikuwa hafahamiki kama alikuwa amekuja kusalimia mgonjwa ama kuna daktari alikuwa akimngoja. Na hakuna ambaye aliweka mashaka yoyote juu yake.
Utaanza vipi kuweka mashaka kwa mtu bila sababu ya msingi.
Baada ya kukaa muda mrefu alisimama na kwenda pembeni kidogo akatoa simu yake na kubofya namba kadhaa akawa amepiga mahali. Akazungumza kwa kifupi kisha akarejea kuketi pale kwa takribani dakika tatu halafu akasimama na kutoweka.
Alikuwa amemaliza kazi yake mwanamke yule wa kinyakyusa.
Mama lao!!
****
SIMU aliyoipiga mama lao ilipokelewa na Yakubu Gama. Mama lao alimweleza kuwa kuna wageni walikuwa wameingia hospitali na anahisi mmojawao anaweza kuwa ndiye BvB. Mama lao hakutaka maswali, akakata simu na kuondoka.
Wakati mama lao anaondoka alipishana na mzee ambaye alikuwa anatembelea mkongojo, almanusura wakumbane wakati wakipishana. Mama lao akampuuza na kuendelea na safari zake.
Mzee yule akageuka na kumtazama mama lao kisha akatikisa kichwa bila kusema neno lolote.
Akaendelea kutembea taratibu huku mkongojo wake ukimpa egemeo kila anavyopiga hatua mbele.
Mama lao akaendelea mbele zaidi, wakati anataka kukata kona mara akakumbana na wanaume watatu, hawa hakuweza kukwepana nao, akajikuta akigongana na mmoja wao.
Akavutwa mkono kisha akakaripiwa na wanaume wale huku wakimsihi aongeze umakini wake wakati anatembea.
Mama lao akaomba radhi! Wakamwacha akaenda zake.
Mama lao alipofika nje akachukua tena simu yake ili aweze kuzungumza na Gama na kumtahadharisha juu ya mazingira kamili yalivyo pale hospitali hasahasa alichokiona kwa nje. Lakini wakati huu simu ya Gama haikuwa ikipatikana, mama lao akasonya kisha akatafuta usawa mzuri ambao anaweza kuona kila kitakachokingia na kutoka pale hospitali. Alihitaji kumwona Gama ili awahi kumtahadharisha kuwa ameona gari la wanajeshi nje ya ile hospitali hivyo huenda kuna ulinzi mkali wa kijeshi unaendelea.
Wakati anasubiri pale kwa takribani dakika kumi, mara hekaheka zikaanza pale hospitali. Wagonjwa wakawa wanapiga kelele huku kila mmoja akitafuta mahali pa kukimbilia. Mama lao akiwa nje alilitazama tukio lile na wala asijishughulishe nalo hata kidogo.
Wale wanaume watatu ambao walikuwa wameufungia tela msafara mdogo uliokuja kumpokea mtu waliyeamini kuwa ni BvB. Walikuwa wamejipanga kwa ajili ya kwenda kumtia nguvuni BvB na kikosi chake akiwemo yule mwanausalama wa taifa ambaye Gama alikuwa akimuheshimu kwa umachachari wake.
Wanaume wale waliingia moja kwa moja katika kile chumba alichokuwa amelazwa BvB. Moja kwa moja wakafika na kumtia nguvuni yeye na kikosi chake huku wakiwaonyeshea bunduki.
Wale wanajeshi hawakuwa wakimtambua vyema yule mwanausalama kuwa nyuma ya Steven Marashi na Yakubu Gama ni yeye aliyekuwa akiaminika kuwa na uwezo binafsi zaidi aliyebakia.
Kijana yule upesi alijirusha na kuipiga teke bunduki ile huku yule mzungu anayeaminika kuwa ndiye BvB aklimfyatua teke kali ambalo lilimwondoa ndani ya kile chumba hadi kufika nje, akafikia miguu ya kile kizee kilichokuwa kikitembelea mkongojo.
Kizee kile hakikushtuka, kikabaki kimetulia kama ki usingizini.
Mapambano ya haja yakaendelea mle ndani. Mara ghafla yule kijana wa usalama wa taifa ambaye anaunga mkono maovu ya serikali alifika na kumzoa yule mwanajeshi ambaye alikuwa ameangukla miguuni mwa yule mzee.
Kisha akamtupia ndani na akaufunga mlango.
Hapo ndipo likatokea tukio la kusisimua.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Yule mzee kwa kutumia goti lake akaurukia ule mlango na kutua ndani akiwaacha watu wote katika taharuki kubwa.
Hakujihangaisha na wale wazungu bali alijitupa na kumuwahi yule mwanausalama. Mwanausalama akakwepa pigo lile, lakini hakudumu katika kukwepa kule akapokea pigo jingine katika mnyumbuliko ambao aliutambua kuwa ni watu wawili tu walikuwa wanaweza kunyumbulika namna ile.
Kabla hajajiuliza sana mzee yule akaivua kofia yake na kisha akatokwa na tabasamu la ghadhabu.
Alikuwa ni Yakubu Gama katika muonekano wa tofauti kabisa. Kijana yule akajiona kama anayepambana na mzimu, maana alijua wazi kuwa Gama alikufa.
Hilo likamfanya aishiwe mbinu, Gama hakusema neno akamwingia na mapigo mengine matatu, yote yakapenya kisha pigo la nne lilikuwa lile lililomdhoofisha yule dada mkaidi Suzi. Pigo la ngumi ya kifo.
Likamwingia mbavuni, mwanausalama akasalimu amri akatua chini. Wanajeshi wale walikuwa wameelemewa kwa vipigo kutoka kwa yule mwanausalama hivyo ni macho yao pekee yaliyoweza kufanya kazi na kumshuhudia kiumbe yule wa ajabu akigawa adhabu ya maana.
Punde mlango ule ulivamiwa na hapo wanajeshi lukuki wakazama mle ndani.
Bunduki zao mikononi, wakawaweka chini ya ulinzi watu wote mle ndani.
Yakubu Gama akiwa mmoja wao.
Yakubu alianza kuingiwa hofu kuwa huenda ameingia matatani lakini mara macho yake yakangongana na Luteni mtukutu Lutei K.
“Nilijua tu kuwa huwezi kuwa ulikufa kirahisi vile Gama.” Luteni ambaye alikuwa akifahamiana na Gama alizungumza huku akitabasamu.
“Mfunge huyu bwana pingu!” Luteni akaamuru, na pale BvB akafungwa pingu, na washirika wake nao wakafungwa pingu.
****
KIHITIMISHO
Redio ya taifa ilikuwa ikisikilizwa na asilimia zidi ya sabini nchini kote kuanzia asubuhi. Luteni K alikiongoza kikosi cha wapiganaji wote katika kipindi maalumu cha kulitangazia taifa hila kadha wa kadha ambazo zimekuwa zikifanywa na raisi wa nchi ambaye hakupatikana kwa njia ya simu na wala mkewe hakuwa akijua wapi alipokuwa ameenda.
Luteni K aliwatambulisha kwa majina wale wapiganaji. Christina Elisha ‘Tina’, Steven ‘ven’ Marashi(marehemu), Samwel ‘Sam’ Mbaule, Yakubu Gama, Robert Masawe, Dokta Macho, John Masele, Lilian Mishele ‘Lili’na Sekela Ambindwile ‘Mama lao’.
Akayaelezea mengi juu yao na kwa namna ambayo kila mmoja amefanikisha kufichuliwa kwa mkataba mbovu kupita yote uliowahi kutiwa saini nchini Tanzania.
Mkataba wa kugawa ardhi nono ya Tanzania kwa mtu binafsi kwa sababu tu ya msaada wake kifedha.
Mkataba huo ulifichuliwa katika mkanda ambao hayati Steven Marashi aliurekodi siku akiwa ikulu bila mtu yeyote kumshtukia. Mkanda ambao baadaye Lili alitumwa na watu wabaya kumlaghai Steven na kisha kuuchukua, lakini kwa uzalendo wa Lili akajivika ujasiri na hakuufikisha mkanda ule kwa watu wabaya badala yake akaufikisha mikononi mwa Tina ambaye naye aliuchimbia ardhini katika hali ya usalama na leo hii umekuwa ushahidi mkubwa kabisa.
Luteni alimwelezea kila mmoja na hatimaye akatoa tamko kuwa nchi ilikuwa inashikiliwa rasmi na jeshi la Tanzania, na hakuna namna yoyote ya kumtambua raisi kwa sababu aliitwa kujitetea na wala hakujitokeza.
Wakati Luteni akiendelea kuzungumza kuna ujumbe uliletwa na kukatisha mazungumzo yake maana ilikuwa ulikuwa ujumbe wa lazima.
Naam! Akaupokea ule ujumbe, ujumbe wa kifo cha raisi ambaye alikutwa amejinyonga katika hoteli ya hadhi ya kawaida kabisa, huku nyuma akiacha ujumbe mfupi kabisa ‘NISAMEHE TANZANIA’.
Taarifa ile ikamfikia Mathias Obhare ambaye alikuwa hoi hospitali, shinikizo la damu likapanda zaidi. Jitihada za madaktari zikagonga mwamba.
Na yeye akapoteza uhai wake akaenda kuungana na Raisi wake ambaye walishirikiana katika hila.
Baada ya kutoka katika studio za redio ya taifa, kule nje zilikuwa ni shangwe za aina yake, mamia kwa maelfu ya watanzania walingoja kuziona sura za mashujaa wale. Hakika jitihada zao zilikuwa zimewasisimua mno na wale waliokata tamaa wakapata nguvu tena.
Umati ukawapokea kwa shangwe kubwa. Wote kwa pamoja wakawapungia mikono kwa ishara ya kukunja ngumi na kuitupa juu. Watanzania nao wakafanya vilevile.
_____
Majira ya saa kumi jioni, makaburi ya Kinondoni. Kundi la mashujaa lilikuwa limeenda kuweka shahada la maua katika kaburi la Steven Marashi.
Ilikuwa huzuni kubwa kuwa yule aliyezianzisha harakati alikuwa amekufa bila kuyaona matunda, lakini kwa John Masele na Sam lilikuwa jambo la kawaida kwa sababu waliamua kutambua mpiganaji kama sweta.
Na sweta lile lilikuwa limechanika!
Baada ya kufanya dua fupi, Lili alizungumza jambo ambalo liliamsha simanzi.
“Natamani ungekuwepo katika mchezo huu mume wangu, baba yangu, kaka yangu na nguzo yangu ewe Steven….. nalikumbuka cheko lako na kila kitu chako. Steven hebu kuwa kama umejificha basi mpenzi wangu, hebu kuwa kama upo kwenye mchezo tu na baadaye mchezo utaisha kama huu wetu ulivyoisha kwa furaha tele, najisikia vibaya sana kila nikiziona herufi ‘SLM’ nakumbuka siku ambayo uliziunganisha na kunitamkia bayana kuwa na ziungane daima lakini wapi sasa mbona umeondoka sasa ‘Steven Lilian Marashi’ na sasa nimebaki ‘S’ peke yangu.
Steven naamini umejificha naomba nikisema neno nawe ujitokeze……” Akanyamaza kidogo kisha akamalizia, “KOMBOLELA STEVEN MARASHI…..”
Na hapo akajikuta akiangua kilio kikubwa, ikawa kazi ya wenzake kumbembeleza.
Naam! Kombolela zote ziliweza kuwafichua watu walipojificha lakini kasoro hiyo moja tu haikuweza kumfufua Steven!
Wakaondoka huku nyuma wakiliacha kaburi la Steven Marashi.
“Niamini mimi….. huko alipo Steven anatabasamu …” ilikuwa sauti ya IGP ambaye alinusurika kutupwa katika orodha ya wasaliti na bahati ikawa kwake kuangukia kwa watu safi ila walioshurutishwa tu kutumika bila kujua.
Naam! Baada ya utulivu wa kutosha jeshi lilitangaza kura ya ndio na hapana ya kumwingiza ikulu, John Masele.
Kura zikapigwa na kwa asilimia zaidi ya 80 watanzania wakapiga kura ya ndio. Hatimaye yule mwanamapinduzi akaingia madarakani!
Tanzania mpya ikazaliwa kwa matumaini mapya kabisa.
Lili hakutaka kuingia kwenye siasa kabisa badala yake yeye alimvuta mama lao kando na kumsisitiza kuwa akicheza filamu ya mapigano atauza sana Tanzania. Mama lao hakuamini lakini baadaye ikawa kweli mama lao akakubali kuingia katika masuala ya filamu, filamu yake ya kwanza kuchezwa ikawa ni ile riwaya ambayo iliandikwa na mmojawapo wa watunzi mahiri Tanzania ambaye baada ya mjumuiko wa tukio lile aliandika riwaya akaiita HILA… Riwaya iliyovuta sana umakini wa watanzania, wengi wakaisoma ili wajue ambacho hawakuwa wakikijua.
Filamu ya HILA ikampa mama lao tuzo lukuki.
Baada ya tunzo hizo, mwandishi ambaye alikuwa likizo kwa muda mrefu akafanya mahojiano na mama lao. Huyu alikuwa ni Samweli Mbaule.
Katika mahojiano yale walizungumza mengi sana, na mwisho wa maongezi yale mama lao hakuishiwa visa vyake.
“Ulikuwa umejificha sana Sa, watu wakasema hautajihusisha tena na mambo ya uandishi wa habari… nimekufichua hatimaye… KOMBOLELA SAM!!”
Sam akabaki kucheka tu asiwe na la kusema!!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MWISHO!!
0 comments:
Post a Comment