Simulizi : Hofu
Sehemu Ya Tano (5)
Getonga akaupandisha uso na kuufikia uso wa Rensho, akakuta binti yule akiwa amefumba macho na kutoa tabasamu mwanana.
Maungo katika nguo ya Getonga yakaanza fujo, akaanza kusahau kama walichotaka kufanya kilikuwa ni tiba.
Akatamanika kingono.
Akaupeleka mkono na kumpapasa, ule ulaini wa ngozi ambayo hakuwahi kuiona ikipakwa mafuta ukamsaatajabisha!!
Rensho alikuwa na kila kitu kinachomfanya aweze kuitwa mrembo.
“Hata mama Eva hapa haingii ndani!!” Getonga alikiri…..
Getonga akaiamuru akili yake kufanya kama ilivyoagizwa, akaanza kumpapasa Rensho huku akiwa ameiondoa tayari bukta yake.
Wakati anamkumbatia ndipo akakutana na utofauti wa Rensho na ule wa mkewe mpenzi ‘mama Eva’.
Rensho hakuwa na joto hata kidogo, alikuwa wa baridi sana.
Nimelala na maiti!! Alijisemea Getonga huku akizidi kuzilazimisha hisia zake zisishuke kwa ni kwa kushuka hisia asingeweza kufanya lolote.
Hatimaye akalifikia eneo husika!!
Loh! Rensho alikuwa bado bikira…..
Getonga akastaajabu, lakini hapo hapo akakumbuka kuwahi kumsikia Kindo akidai kuwa yule Rensho aliwahi kufa na kuzikwa akiwa na miaka kumi tu. Lile wazo la kuwa analala na maiti likajirudia tena, lakini akaendeleza jitihada za kufanya kama alichoagizwa wakati huu alilazimika kufumba macho na kuvuta hisia za kuwa na mkewe kitandani!!
Rensho alikuwa hafanyi miguno wala hisia zozote zile, ni kama hakuwepo pale kabisa kimwili.
****
Jijini Dar es salaam, mheshimiwa waziri mkuu mstaafu na mwenzake mzee Nshomile wakiwa wako uchi wa mnyama waliamua kufikia maamuzi baada ya fumanizi lile ambalo lilimaanisha kuwa siri zao zote zilikuwa nje hatimaye. Na ilikuwa hatari sana kwa jambo hili.
Waziri mstaafu akaamua kumnyamazisha mkewe kwa namna waliyojua wao ndani ya kile chumba huku akitoa wazo la kumtafuta huyo mtu wa kuitwa Kindo.
“Tunaanzia wapi kumpata sasa…” aliuliza mzee Nshomile. Waziri msaafu akamwonyesha ishara kuwa wanatakiwa kuondoka.
Nshomile akatii amri….
Wakatoweka na kuacha miili miwili ndani ya chumba, mke wa waziri mstaafu na diwani ambaye alikuwa ametokwa uhai tayari.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
DAKIKA TANO BAADAYE!!
SAA KUMI ALFAJIRI.
Waziri mstaafu na mzee Nshomile walikuwa katika wodi moja wapo ndani ya hospitali ya taifa ya Muhimbili. Waliingia pale na kuruhusiwa muda ule kutokana na heshima kubwa aliyokuwanayo mheshimiwa waziri mstaafu.
Mavazi yao ya suti yalipendeza haswa.
Kwa waliowaona walinong’onezana kuwa harakati zote zile ni kwa sababu mheshimiwa anataka kuingia ikulu baada ya miaka kadhaa hivyo alikuwa katika kuisaka hali ya kushawishi umma ili apigiwe kura wakati wa uchaguzi mkuu.
Hawakujua kuwa walikuwa na lao jambo!!
Walipofika mapokezi waliomba kumwona mgonjwa aliyefikishwa hapo masaa machache yaliyopita aendaye kwa jina na John na cheo cha Inspekta.
Inspekta John Magege, ambaye vyombo vya habari usiku ule vilidai kuwa alikutwa akizurura akiwa na mavazi yake begani.
Ikasadikika kuwa ni Malaria kali ilikuwa imempanda kichwani.
Heshima ya waziri ikawapitisha tena bila kikwazo, licha ya muuguzi kudai kuwa mgonjwa alikuwa amechomwa sindano za usingizi. Walilazimisha wakaingia baada ya mheshimiwa kumpigia simu IGP ambaye alikuwa ni swahiba wake, IGP akawapa ruhusa.
Kweli walimkuta akiwa amelala kiutulivu sana.
Katika wodi ile alikuwa yeye ndiye mgonjwa pekee.
Waziri hakupoteza wakati, akaketi pembeni ya kile kitanda kisha akamshika kichwa Inspekta John ambaye hakuwa katika fahamu zake.
Akaanza kumuuliza maswali kadha wa kadha hasahasa juu ya muonekano wa Kindo na kama aliwahi kumuona hapo kabla.
Ajabu! Akiwa katika usingizi mzito aliyajibu maswali ipasavyo na kudai picha ya Kindo baada ya kuwa amekumbwa na lile janga ipo nyumbani kwake, akaelezea vyema kabisa mahali nyumba yake ilipo.
Picha ya Kindo! Ndo kitu pekee walichokihitaji wawili hawa maana walipomchukua mwanzo kwa ajili ya shughuli yao iliyoingia dosari hakuna hata mmoja aliyeikariri sura yake.
Hata mzee Nshomile licha ya kukutana na Kindo ana kwa ana hakukumbuka kuinasa sura yake akilini.
Hivyo walikuwa wakiihitaji kwa udi na uvumba!!
Maelezo yalipowatosha wakatoweka huku wakimpita muuguzi aliyekuwa ameuchapa usingizi jirani na eneo la mapokezi.
Ikiwa ni saa kumi na dakika zipatazo arobaini, walifunga safari hadi nyumba waliyoelekezwa na Inspekta John Magege.
Mlinzi hakuwa kikwazo kikubwa kwao, walimnyamazisha mara moja kisha wakaingia ndani, wakaziba sura zao ili kuondoa mlolongo wa kuhangaika kuwanyamazisha watu ambao walikuwa wamewatambua.
Sebuleni walimkuta mke wa John Magege akiwa bado yupo macho. Walipoingia akataka kupiga kelele, Nshomile akamrukia na kumziba mdomo, kisha swali moja tu.
“Chumba cha John kipo wapi?”
Huku akitetemeka akawaelekeza, waziri akaingia upesi na kutuliza akili kisha akaanza kuisaka ile picha hadi alipoipata.
Picha ikamrudishia kumbukumbu juu ya Kindo. Akaihifadhi katika suti yake kisha akatoka na kumpa ishara mwenzake.
Wakatoka!!
Saa kumi na moja alfajiri ulikuwa ni MSAKO KINDO.
Sura yake ikakaririshwa vyema katika akili za wawili hawa!!
Wakagawana maeneo ya jijini Dar es salaam kumsaka mtu anayefanana na hiyo sura ya Kindo.
*****
Rensho alianza kulalamika dakika kumi na tano baadaye, kisha akaanza kukoroma huku akijikunja huku na kule. Getonga hakumuachia aliendelea kupalangana huku jasho likimtoka.
Hakuwa akipata ladha yoyote ile kama alivyotegemea awali, ule ubaridi ukamfanya ajilazimishe tu kufanya alichokuwa akikifanya.
“Kindo….muhimu sana. Kindo Muhimu sana…… Kindo muhimu sana….” Rensho aliendelea kurudia yale maneno bila kuongeza neno jingine la ziada.
Getonga akatarajia mabadiliko lakini haikuwa hivyo, aliendelea kusisitiza kuwa Kindo ni muhimu sana.
Ghafla akatulia tuli kama alivyokuwa awali. Getonga naye akaacha kufanya alichokuwa anakifanya.
Hatimaye Rensho akayafumbua macho yake kichovu, kisha akaangaza huku na kule kama anayetoka kuamka.
“Nini kinatokea hapa …” aliuliza huku akijitazama na kisha kujifunika na shuka.
“Umesema KINDO MUHIMU SANA…” Getonga akamjibu.
“Kivipi muhimu…” akauliza swali lile ambalo lilionekana kuwa gumu kwa Getonga.
“Wewe ndiye umesema sio mimi…na hukutoa sababu…” alijitoa katika kujua akamrushia mpira.
“Ok! Ok ok…..hao hao…..hao….wanamtafuta oooh!! Sijui kama tutawahi aaargh wanatuua hawa…” Rensho alizungumza peke yake lakini akiwa na mashaka makubwa sana.
“Akina nani?”
“Washenzi walafi wa madaraka haramu.” Alijibu kwa ghadhabu.
“Kindo anamjua Salome…..sawa…Kindo ni muhimu sana. Kindo anajua kaburi ambalo nilizikwa miaka kama kumi na nne iliyopita..ooooh!! mbona tulimuacha Kindo sasa. Wanamtafuta hawa watu, wapo jirani kumpata ona…” alizidi kulalamika.
Jambo la kufa miaka kumi na nne iliyopita…lilimduwaza Getonga. Akajiuliza maiti gani huyu anaishi huku amezikwa kitambo kirefu?
Hakupata jibu!!CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Wakimpata Kindo wamenimaliza. Mimi wewe na familia yako,,,ooh! Wabaya watu hawa…. Kindo ni mtu muhimu sana.”
“Sasa tunafanyaje?” aliuliza Getonga kwa uoga.
“Tuondoke tukajaribu bahati.” Alitoa jibu huku akisimama wima, Getonga naye akasimama. Rensho akamkumbatia kwa nguvu kisha kama walivyotoweka na kufika Kahama wakatoweka na kuingia jijini Dar es salaam.
Walilifikia lile jumba ambalo walitokea mwanzoni na kuingia ndani Rensho akiwa mbele na Getonga nyuma. Moja kwa moja katika chumba alichokuea amefungiwa Kindo.
Lahaula! Kindo hakuwepo ndani yake!
Rensho akachoka, Getonga naye akasaidiana naye kuchoka huku akiifikiria familia yake.
Rensho alijaribu kuvuta hisia zote juu ya hili lakini hakuifanikiwa hata kidogo kupata ufumbuzi juu ya ni wapi alikuwepo Kindo.
“Watakuwa wamemkamata tayari….. tumekwisha ndugu yangu. Pole sana unaenda kuipoteza familia yako.” Rensho alimwambia Getonga pasipo kumtazama usoni.
Getonga akabaki kuduwaa asijue ni neno gani linaweza kuyabadili mambo haya.
Wakiwa bado wanashangaa mara ghafla kama upepo Rensho alipokea pigo kali katika mgongo wake. Ile Getonga anageuka kujiuliza kulikoni mara na yeye akachabangwa kofi kali usoni.
Akayumbayumba na kukaa chini huku maumivu yakitambaa mwili mzima.
Rensho alipojiweka sawa akakumbata na pigo tena kali katika mbavu zake.
“Mpumbavu mkubwa wewe ulidhani siku yako haitafika…..muonevu mkubwa wewe.” Sauti ya kike ikakoroma kutokea katika kigiza kidogo. Kisha ikaingia katika mwanga.
“Ulikosea sana kuamini kuwa sitakuwa na la kufanya, hayawani wa kike wewe. Na wewe Malaya wa kiume leo utajuta kuzaliwa..” alizidi kuonya yule mwanamke.
“Shit!” Rensho alitokwa na kauli ya mshangao, lakini haukudumu sana mshangao ule. Mara yule kiumbe mwingine wa kike akajirusha juu juu aliwa ameunyoosha mguu wake, Rensho akakinga mikono na kupangua pigo lile, maumivu aliyoyapata pale akakiri kuwa alikuwa anapambana na kiumbe hatari.
“We Malaya unaniangalia kama hunijui eeh!” Getonga akatupiwa swali na yule kiumbe.
“Rensho huyu nanmi sasa…”Getonga akamuuliza Rensho ambaye alikuwa ameanguka jirani kabisa na mahli alipokuwepo yeye.
“Anaitwa Queen huyu ni….”
“Alaa! Nd’o huyu…” Getonga akastaajabu na hapo akazikumbuka picha ambazo kumbe huyo aliwahi kumrushia azitazqme huku akidai kuwa ulimwenguni alikuwa msichana mrembo sana.
Kisha akalikumbuka ombi la yule kiumbe ambaye wakati wanakutana alikuwa na mguu mmoja huku akitokwa na harufu kali, pia hakuwa na sikio.
Sasa alikuwa mrembo haswa, na alikuwa na kila kiungo chake.
“Mbona sasa ana mguu..”
“Bwege amejibusti na Kindo huyu hapakuwa na mwanaume mwingine hapa…nilifanya makosa kumwacha Kindo hapa. Eeeh!! Tumekwisha sisi, anajua udhaifu wangu huyu atanisumbua sana.” Rensho alijilaumu huku akiwa hajajua ni kitu gani afanye.
“Wanaume ni washenzi sana nyie, washenzi wa kutupwa. Na wewe Rensho ukaona kwamba nitafaidi sana kuzaa na huyu bwana ukaamua uondoke naye… sasa ngoja nikuonyeshe tofauti yetu…” akasita kisha akageuka nyuma.. “Kin….. Kindo wee!” akaita kimahaba.
Na hapo akaingia kijana nadhifu haswa, kiatu chake kikiwa katika mng’aro mahsusi kabisa na alikuwa akitabasamu.
Akafika na kujiweka ubavuni mwa Queen.
Rensho na Getonga wakatumbua macho yao.
“Mtabaki huku kwa wafu sisi tunaondoka na kurejea ulimwenguni.” Alisema kwa nyondo.
Rensho akanyanyuka kwa hasira na kumvamia lakini akakutana na ngumi nzito ya begani akapiga mayowe na kumwangukia Getonga pale chini. Kisha Quue akamrukia tena kwa nguvu zote na kumchabanga teke kali gotini. Rensho akapiga mayowe makali.
“Umenivunjaaaaa!!”
“Huniwezi Rensho wewe ulikuwa wa wakati ule…. Na bado nitavunja na hicho kichwa” Alitamba huku akiufuta mkono wake uliompiga ngumi Rensho.
“Bila kitambulisho sitamuweza tutakufa….tutakufa tu!!” Rensho alimnong’oneza Getonga huku damu zikimbubujika mdomoni,
“Kwa hiyo….”
“Ngoja tuone anataka kutufanya nini…” alisema kwa kukata tamaa
Ilikuwa yapata saa kumi na moja na dakika hamsini za asubuhi ambapo mambo yalibadilika tena.
Ndani ya lile jumba akaingia kiumbe mwenye hasira kuu, Queen akiwa hajui lolote mara akachapwa teke la mgongoni akayumba kidogo na kutaka kujiweka sawa mara akachapwa ngumi kali ya uso akabaki kuona maluweluwe.
Punde Kindo akasikika akipiga kelele.
Getonga na Rensho waliokuwa wamekaa chini wakawashuhudia wanaume walioziba nyuso zao.
Baada ya udhibiti huo, wakazifunua nyuso zao.
Alikuwa ni waziri mkuu mstaafu na aliyemdhibiti Kindo alikuwa ni baba yake mzazi na Rensho. Mzee Nsomile!!
Rensho ana kwa ana na baba yake!!! Rensho alimtazama kwa hasira lakini pale alipo goti lilikuwa halifanyi kazi na mwili ulikuwa dhaifu. Hasira pekee nd’o ilimuongoza na kuamini kuwa anaweza kumdhibiti yule mzee.
Lakini alikuwa na maadui watatu, waziri, baba yake pamoja na mtumwa aliyesaliti utumwa Queen!!
HATARI!!!
Nianze na nani sasa? Alijiuliza Rensho huku akimlaani Queen kwa lile pigo ambalo lilitawanya goti lake na kumfanya ashindwe kusimama. Akapiga kite cha ghadhabu kuhu akiangaza macho huku na kule kama kuna namna ya kuweza kujinyofoa kutoka katika mikono ya watu wabaya.
“Laiti kama mguu ungekuwa unafanya kazi ningeweza hata kukimbia……lakini aah!! Huyu kaka na familia yake wangekufa vibaya.” Alizidi kuwaza na kuwazua.
Akiwa hajapata jibu sahihi, mara mzee Nshomile alimpiga Kindo kwa kutumia kiganja chake maeneo ya shingoni, akalainika na kupoteza fahamu. Kisha akamfuata Rensho na kusimama mbele yake.
Ili kuthibitisha hasira kali aliyonayo mbele ya yule binti akamuuliza swali moja.
“Mimi nani yako?” akahoji kwa hasira.
“Sikufahamu.” Rensho alijibu kwa jeuri huku akijua fika kuwa yule ni baba yake.
Mzee Nshomile bila kusogeza hatua nyuma akanyanyua mguu wa kulia akamtishia kama anamchabanga usoni. Rensho kwa kutumia mikono akajaribu kuzuia lakini ghafla ule mguu ukatua katika goti lililosambaratishwa na Queen. Rensho akapiga mayowe makali ya kutangaza maumivu.
Tendo lile la yule mzee kumsaga Rensho gotini likamtia hasira Getonga akafanya kujitingisha kidogo ili kutetea usalama wa Rensho lakini pale pale alikatwa kofi kali ya usoni, uso ukawaka moto na sekunde kadhaa mbele akaanza kutokwa damu puani.
“Mwanadamu mpumbavu wewe hauna la kutuzuia sisi…dunia hii ni yetu!” Waziri mstaafu ambaye alikuwa amemdhibiti Queen alisema kwa kejeli. Getonga akanyanyua macho yake wakagonganisha na yule waziri mstaafu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Whaaat…Gerlad Getonga Mosenya….. son of the bitch!!” akawaka kwa hasira yule mzee, Getonga naye akaduwaa hakutegemea kuwa yulew angeweza kuwa waziri mkuu mstaafu. Waziri ambaye aliwahi kuingia katika mzozo na gazeti ambalo Getonga alikuwa akiandikia makala.
Makala iliyomponda sana kuwa ni mbadhlifu wa fedha na maamuzi yake hayajanyooka, makala ambayo iliwapa nafasi wapinzani kukidhoofisha chama tawala.
Mafahari hawa wanakutana katika dunia nyingine. Ni aidha Getonga atoke hai na kwenda kuandika makala kuwa raisi mtarajiwa ni mshirikina amaafe ili kila kitu kiende salama.
“Njoo umshike huyu…mdhibiti kabisa” Waziri alimwamuru Nshomile naye akatenda vile mara moja.
Waziri akawa huru, akamsogelea Getonga ambaye alikuwa akivuja damu bado.
“Ulikuja huku pia kuchukua habari eeh!” Waziri alimdhihaki, kisha akaendelea, “ulinichafua magazetini enzi nikiwa waziri…nasikitika kuwa licha ya kukutanishwa na kupatanishewa ni kwamba hadi leo sijawahi kukusamehe nina hasira na wewe na leo nitazimisha ndoto zako zote ulizonazo mshenzi wewe.” Alizungumza kwa ghadhabu huku akiwa ameikaba shingo ya Getonga.
Na kwa kitendo cha sekunde chache tayari alikuwa amemchapa makofiu mawili makali. Damu ikazidi kuvuja huku Rensho akiishia kuumia tu asiweze kumsaidia Getonga.
“Babaaaa!” sauti ya mtoto mdogo ilisikika ikiita, matukio yote yakasimama.
Masikio ya Getonga yakatambua kuwa huyo ni Anitha alikuwa amesikia kilio chake kikuu cha maumivu.
“Nani huyo?” Waziri alimuhoji Nshomile.
“Kama ni mwanadamu nyonga mara moja…” alitoa amri Waziri . nshomile akiwa amemkaba Queen alikubali alichoelekezwa na wakaongozana kwenda sauti ya mtoto ilipotokea.
Queen alikuwa akimchukia Getonga lakini hakuwahi kumchukia mkewe na hasahasa yule mtoto, alimpenda sana.
Ile amri ya ukikamata nyonga ilimshtua na hasira zikampanda hakuwa tayari kushuhudia kifo cha yule mtoto.
Nshomile asiyekuwa na taarifa kabisa wala mategemeo katika lile tukio, alijikuta akimlegezea ukabaji Queen na kumpuuzia akimchukulia kama wanadamu wengine.
Hilo lilikuwa kosa kubwa sana kwa mzee huyu na ambalo lilizua varangati.
Queen aliinama ghafla na kujitoa katika mikono ya Nshomile, kisha upesi akakunjuka teke kali na kumchabanga mgongo akajibamiza katika vyuma vilivyokuwa mbele yake.
Hapohapo akamrukia tena na kumpiga ngumi ya kisogo kali sana, mzee Nshomile akaishia kuona maluweluwe na kuanguka chini.
Queen akamnyakua Eva (mtoto wa Getonga) na kisha akatimua mbio….. ile anafika mlangoni akatambua kuwa bado yeye si mwanadamu kamili na bado anamhitaji Kindo ili aweze kumrejesha tena katika ubinadamu. Akakata tamaa.
“Eva mpenzi…..” akamuita yule mtoto kwa sauti ya chini.
“Bee dada..” Eva akaitika kwa sauti ya kitoto.
“Naomba unisikie na ujaribu tu kunielewa sawa mama eeh! Unauona ule mlango pale..” akamnyanyua kichwa na kumuelekezea kule, “Kimbia nenda ukaufungue na uingie ujifiche pale, usilie wala usipige kelele hata kidogo…naenda kumleta baba sawa eeeh!!...sawa mamangu?” alimsihi kwa sauti tulivu ili aweze kuelewa.
Japokuwa alikuwa mtoto yale maisha ya utata yaliyokuwa yanaendelea katika jengo lile na kile kilio alichokisikia kutoka kwa baba yake tyari alitambua kuwa kuna hatari kubwa eneo lile.
Akafuata aliyoelekezwa!!
Eva akaanza kukimbia kuelekea ule mlango ulipokuwa, Queen alimtazama vyema ili afike kabisa na kujifungia nyuma ya ule mlango.
Tabasamu likamtoka kwa wepesi wa yule mtoto mdogo, akaufungua mlango, ile anatak kuingia ajifungie tu likatokea jambo ambalo lilivuruga utaratibu.
Katoka paka katika ficho lile, Eva akapiga kelele za uoga.
Queen akabaki kukodoa macho akimtazama jinsi Eva alivyokuwa anatapatapa.
Kelele za Eva zikamkurupua na mzee Nshomile kutoka pale chini, kabla Queen hajajua afanye nini alivisikia vishindo vya mwanadamu kusogea katika eneo lile. Akajipanga kumkabili…..
Ila mwenzake alikuwa amejipanga zaidi, mawenge yakamkumba baada ya kupondwa na kitu kizito kisogoni. Ile anaugulia maumivu akashtuka akiwa amebanwa mbavu zake mbili za chini kwa nguvu mno. Alijaribu kufyatuka lakini hakufanikiwa…maumivu yalikuwa makali mno.
Queen akaanza kulia kama mtoto mdogo. Lakini kama ile haitoshi akapigwa ngumi kali kiunoni, ngumi iliyopigwa kitaalamu kwa ajili ya kuvunja tu!
Queen akalainika na kumwangukia yule bwana huku akiendelea kuugulia.
Mzee Nshomile akamchukua begani kama mzigo tu usiokuwa na thamani yoyote, kisha akamfuata Eva pale alipo akamvuta mkono kwa nguvu sana Eva akaanza kulia.
“Mwache mtoto wangu nasema?” sauti kutoka katika ficho jingine ikatoka, Nshomile akaifuata kwa tahadhari akamkuta mama yake Eva (Anitha) akiwa amefungwa kamba mikono yake….. akamfungua na kumpa pigo moja la kulainisha.
Baada ya dakika kadhaa kwenye ukumbi wa mapambano alikuwepo Nshomile na mwenzake Waziri mstaafu huku mateka wao wakiwa wameongezeka idadi.
Rensho, Getonga, Kindo, Queen, Anitha (mke wa Getonga), Eva (mtoto wa Getonga). Ukumbi ulikuwa umechafuka damu. Ni Eva pekee ambaye alikuwa havuji damu.
*****
FAMILIA nzima ilikuwa ikimtazama Getonga, naye hakuwa na la kufanya zaidi ya kujisikia vibaya kukaidi ushauri aliopewa na mkewe kuwa ajiweke mbali kabisa na mambo ya uandishi wa habari za kipelelezi kwani ni hatari kwa maisha yake. Alimtazama Anitha mkewe akamtazama na Eva.
Machozi yakamtiririka kwa uchungu mkuu, uchungu wa kuamini kuwa baada ya vifo vyao kama kweli kuna mahali watakutana basi watamlaumu bila kumsamehe kamwe.
Ni heri wakutane duniani wakiwa hai, ataomba msamaha na maisha yao ya ndoa yataendelea.
“We kinyamkera ulidhani kuwaua wenzeti nd’o utatoka na wewe ukiwa hai ili ukatuaibishe dunia sivyo?” Waziri alimuhoji Rensho aliyekuwa hoi.
“Sasa utashuhudia vifo vya hawa rafiki zako mmoja baada ya mwingine halafu wewe utake usitake utatimiza ulichotakiwa kutimiza….na ukileta ubishi ni kifo cha moja kwa moja…wewe ni mtoto na utabaki kuwa mtoto tu..” Nshomile akaongezea.
Rensho hakujibu kitu alikuwa akihema juu juu tu kutokana na maumivu makali hasahasa ya goti lililotawqanyika.
“Queen, tunafanyaje sasa…’ hatimaye alimnong’oneza Queen, ambaye naye alikuwa hoi akiwa amevunjika kiuno.
“Wangetuachia hata dakika kumi tungebusti ila bila hivyo, naona tunateketea hapa…” alijibu akiwa amekata tamaa.
Mzee Nshomile alimfuata Eva akamshika mkono na kumvuta akasimama wima.
“Niue mimi umuache mwanangu hai…” Getonga akajikaza na kusema maneno yale ya kijasiri….
Waziri mstaafu akamrukia na kumchapa ngumi kali juu ya jicho, akachanika vibaya mno. Damu ikaanza kuvuja. Eva akaanza kulia kwa hisia kali za kuona baba yake akiteseka.
Waziri na mwenzake hawakujali hayo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Na wakati haya yakitokea ilikuwa yapata saa kumi na mbili alfajiri.
Rensho aliwatazama kwa uchungu mkubwa majeruhi waliomzunguka, alimuonea huruma hadi Queen ambaye alihusika katika kulisambaratisha goti lake wakiwa katika mapambano. Alijua kuwa wote hawana nguvu za kuwadhibiti watu wale lakini hata yeye alikuwa dhaifu sana…..
Rensho akajaribu bahati ya mwisho kabisa huku akijisemea nafsini mwake, iwapo hiyo nayo itashindikana basi tena atakuwa radhi kushuhudia vifo vya mateso kwa watu wale.
“Muulize Kindo…. Salome jina lake la kikabila ni nani…jibu muhimu na haraka” alimnong’oneza Queen, Queen naye akamnong’oneza Anitha, Anitha akamuuliza Kindo aliyekuwa hoi.
“Ndema” Kindo akamjibu kwa shida huku akiwa na dakika takribani kumi tangu arejewe na fahamu zake.
Jibu likamfikia Rensho!!
Akayafumba macho yake. Na kisha kuzua mtafaruku baada ya kuanza kupiga makelele.
“Ndema weee….Ndema weeeee amka Ndema….amka…mwili hauiwezi kuishi bila roho na hata roho haiwezi kuishi bila mwili….Ndema weeeee Ndema njoo sasa….. amka Ndema..”
“Pumbavu unasema nini wewe..” Waziri alimtusi kwa ghadhabu huku akimwendea kwa kasi.
Nshomile alikuwa anajiandaa kukikata kichwa cha Eva kwa kutumia kisu kikubwa.
Upepo haukuvuma sana hadi kusababisha milango kuvunjika. Hilo liliwashangaza wote hadi Rensho mwenyewe.
Lakini akaamini kuwa ukweli kabisa mwili hauwezi kuishi bila roho.
Baada ya mlango ule kuvunja katikati ya ule ukumbi akaingia mwanadada mwenye mimba…macho yake yalitangaza hasira kali sana, ujumbe ulikifikia kiumbe kilichokuwa katika tumbo lake.
“Salomeeee!!: Kindo alipiga kelele huku akijitutumua ainuke lakini yule alikuwa salome mwili tu, akili yake ilikuwa imevurugika vibaya mno na alikuwa anachemkwa na hasira.
“Wewe ni nani mwanamke…” waziri mkuu mstaafu alimuuliza. Lakini hakupata jibu badala yake Salome aliendelea kuangaza huku na kule.
Waziri akamfuata kwa fujo akidhani kuwa itakuwa rahisi kiasi kile.
Salome akajirudisha nyuma kidogo kisha akafyatuka kichwa kikali sana katika kinywa cha waziri, meno mawili ya mbele yakasalimu amri akayatema huku akiugulia maumivu.
Mzee Nshomile akajirusha ili kumsaidia waziri, Salome akajikunja kidogo lile teke kali likamkosa, akajizungusha hewani na teke la mzunguko, mzee Nsomile akainama likamkosa. Akataka kumpiga Salome ngumi katikati ya mapaja lakini alikuwa mwepesi sana akawahi kujirusha kisha kama afanyavyo kondoo akamfuata hewani kwa kutumia kichwa, ni heri aliwahi kukwepa kichwa kile kisikutane na kifua chake maana angepasuka pasuka kama ulivyopasuka ule mkono uliokutana na dhahama ile. Nshomile akaugulia maumivu, huku akisimama wina na kujaribu kumkabili Salome huku akiwa na majeraha.
Salome alikuwa hajasema neno lolote lile….tangu aingie katika kile chumba.
Waziri alijitutumua na kusimama akiwa nyuma ya Salome akaandaa shambulizi kwa kutumia chuma alichokiokota pale ndani.
Hakujua kama ni roho ipo katika utendaji na inaona kila kona.
Akakitupa kile chuma kwa nguvu, nia ikiwa kukitandika kisogo cha Salome….
Binti akainama chuma kikapita kwa kasi na kumtandika Nshomile usoni akatokwa na yowe kubwa kisha akaanguka chini.
Waziri akajirusha kwa kutanguliza miguu miwili mzima mzima ili kumuwahi Salome lakini haikuwa rahisi kama alivyodhani. Salome akakwepa kidogo kisha baada ya waziri kutua chini na yeye akajirusha hewani na kutua katika magoti yake.
Hapo akatokwa na ukelele mkubwa wa huku akiyasaga magoti ya waziri mkuu mstaafu.
Hali ikatulia huku Salome akiwa amefura kwa hasira kali sana.
“Wamalize wamalizeee….” Rensho alimsihi bSalome lakini akijua kuwa anazungumza na ile roho ndani yake.
“Sitaua mtu …” Salome alijibu. Rensho akawa mpole. Na wakati huohuo Salome alianguka chini na kutokwa na ile hali aliyokuwanayo akabaki kuwa Salome halisi.
Rensho alipogeuka kuangaza kushoto na kulia akagundua kuwa kuna watu walikuwa wamepungua…..
Kindo na Queen. Wako wapi hawa? Alijiuliza.
Na mara kindo na Queen wakaingia wakiwa katika afya zao imara.
Walikuwa wamebusti tayari.
“Kindo..” Salome aliita baada ya kumuona Kindo akiingia pale ndani.
Kindo akaingia katika mchecheto, ni kweli alikuwa akimpenda sana Salome kwa dhati. Lakini katika mazingira yale ili atoke salama ilikuwa lazima ajihusishe na Queen.
“Ni nani huyu kwani?” Queen alihoji.
“Huyo ni mume wangu..” Salome alitoa jibu……
“Shhhh! Komea hapo hapo mwanamke.”
“Hey! Jamani tunatakiwa kuwa wamoja jamani, ugomvi wa nini tena? Tunatakiwa kutoka humu ndani..” Rensho aliyekuwa amekaa pale chini alionya. Wakanyamza.
Lakini Queen alikuwa amefikiria jambo, hakuwa tayari kutoka mle ndani huku akijua kuwa Kindo si mali yake. Tayari alikuwa amekolea. Wivu wa kimapenzi ukaanza kumshambulia.
Na hapo akafanya tendo la kipuuzi kuliko yote aliyowahi kuyafanya.
Tendo lililomgharimu ila hakuipata nafasi ya kujuta.
Akawaza kumuua Salome ili abaki kuwa mmiliki halali wa moyo wa Kindo. Tayari alishatambua kuwa ile nguvu ambayo aliingia nayo mle ndani hakuwa nayo tena. Alikuwa ni mwanadamu wa kawaida tu.
Queen akitambua zaidi kuwa hakuna mwenye uwezo wa kumnyamazisha mle ndani hata Kindo mwenyewe hakuwa na sauti juu yake. Akamvamia Salome si katika namna ya ugomvi wa kike kike uliozoeleka. Huu ulikuwa wa aina yake…
Mapigano ya kiume! Queen akajirusha na kumtundika ngumi ya shavu salome, akatokwa na ukelele mkubwa huku akianguka chini.
“Queen acha, acha Queen…” alitoa onyo Rensho asiyekuwa na uwezo wa kusimama.
Lakini Queen badala ya kujibu akasimama na kumvaa Rensho akamtandika teke kali kifuani…. Rensho akapoteza fahamu palepale. Kimya kikatanda, Queen alikuwa ameiva kwa hasira. Kindo akajaribu kumtuliza.
Akamgeukia na kumtazama na macho yake mekundu yaliyokuwa yanang’ara kwa hasira.
“Ukae kimya Kindo…..hukuniambia kama una mahusiano na msichana yeyote kumbuka. Nyie wanadamu ni waongo lakini hapa ni mwisho wa mambo nasemaje Kindo ni aidha ufanye muujiza umeze maneno yako ama la nakinyonga hiki kiuchafu kinachojiita mkeo.” Alitoa karipio kali, Kindo akakumbuka kuwa hana wa kumlaumu zaidi ya ulimi wake. Ulimi uliopanga maneno matamu na kumjaza Queen.
Baada ya kuhakikisha kuwa kila mtu mle ndani alikuwa anamuogopa na Rensho akiwa amepoteza fahamu, akarejea kwa Salome. Lengo likiwa moja tu kummaliza kabisa.
Bila huruma akamkwinda na kumnyanyua kisha akamtupa kando, akaangukia tumbo huku akitokwa na kelele kubwa ambayo ilimzindua mzee Nshomile ambaye alikuwa amepotea kifahamu. Akakohoa huku akipepesa macho huku na kule. Hakuwa na nguvu tena.
Yowe la Salome lilimaanisha uchungu mkubwa sana. Uchungu usiokuwa wa kawaida.
Kisha akatulia tuli…..ule mtupo ulikuwa umeleta madhara makubwa sana. Lakini yawezekana kabisa kuumia kwake nd’o ilikuwa ponapona yake baadaye.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Damu ikaanza kumtoka kwa fujo kutoka sehemu zake za siri.
Mimba ilikuwa imeharibika!!
Damu ikazidi kutiririka, Queen akatambua kuwa amemuua Salome. Hakujua kuwa ile haikuwa mimba ya kawaida bali ilikuwa ni roho ya Rensho iliyohifadhiwa katika tumbo lile miezi kadhaa iliyopita. Roho iliyokuwa maalumu kwa ajili ya kumpa vyeo Rensho ambaye alikuwa ameandaliwa kuwa mwenyekiti kwa siku za usoni, roho ambayo Waziri na Nshomile walikuwa wakiisaka kwa hali na mali. Roho ambayo ingemuwezesha Rensho kuishi katika nafsi mbili, mwanadamu wa kawaida na pia katika dunia ya kimiujiza.
Damu ile ikavuja hatimaye ikamgusa Rensho!!
Bila mvua kunyesha radi kubwa ikapiga.
Kila mtu akaingiwa na hofu mle ndani, Rensho akarejewa na fahamu huku akijisikia imara maradufu. Na goti lake likiwa imara kabisa.
Alikuwa Rensho mpya, akalisikia lile joto la uhai…..tayari alikuwa ameipata roho yake.
Akasimama wima akitazamana ana kwa ana na Queen.
Queen akadhani Rensho aliyevunjika goti bado ni yule yule akamvamia aweze kumdhibiti, lakini yakawa maajabu ya mwisho aliyoweza kuyaona kabla hajapoteza uhai wake na kuteketea vibaya.
Alikutana na ngumi kali kutoka kwa Rensho, akapepesuka huku na kule kisha akaanguka chini na kuzimika moja kwa moja.,
Queen akapotea katika ramani ya uzima….
“We mzee kitovu cha Kindo kipo wapi? Ni swali moja na jibu moja tu….” Rensho akatupa swali kwa mzee Nshomile ambaye ni baba yake mzazi.
Kindo akaduwaa kusikia kitovu chake kikiuliziwa.
“Sihitaji ujifikirie katika hili mzee, ulikichukua kitovu chake akiwa na umri siku mbili tu. Na ulikichukua kwa sababu zenu za kishirikina ambazo leo zinawatokea puani. Natambua fitina zako zote ulizomfanyia Kindo ili kumvuruga na kuipoteza amani yake, kumuua mama yake mzazi…..na hata ujauzito wa Salome nadhani unajua nia yenu ilikuwa ipi. Washenzi kabisa, Salome aliwakosea nini mkampa mzigo huu. Mmemtesa Kindo mmemnyang’anya amani yake na kumpotezea marafiki zake….. baba mbaya kupita wote duniani, shetani mkubwa wewe. Na nilikuapia tangu siku ya kwanza uliponiingiza katika utawala huu kuwa ipo siku utalia na kusaga meno na hiyo siku ni leo sasa…..
Upesi nahitaji jibu….. kitovu cha Kindo kipo wapi?”
Mzee Nshomile alipatwa na aibu wakati Rensho akizungumza kibabe. Alijiumauma na hakujibu chochote kile. Kama kawaida ya Rensho haulizi mara mbili na ule upendo wa baba hakuwa nao tena.
Akajirusha na kumfikia akainama chini akaokota kile kisu kilichoandaliwa kwa ajili ya kumchinja Eva.
Ndani ya sekunde tano tu kilio kikubwa kikasikika.
Nshomile hakuwa na mkono mmoja!!!
“Ndani ya dakika mbili nitaondoa huo mguu…” akaonya Rensho huku mzee wake akiwa anaugulia maumivu na damu ikiruka na kumfanya Getonga aikwepe, Kindo akatokwa yowe la hofu.
“Katika jeneza lako mwanangu….”
“Komea hapo, usirudie kuniita mimi mtoto wako, unaruhusiwa kuzaa mwingine ukamuite hivyo, mnafiki mkubwa wewe. Mtoto wako na umetaka kuniua wewe leo…nyang’au wewe. Kwanza mtoto wako ulimzika zamani kabisa sio mimi ambaye nipo hai tena” alifoka Rensho huku macho yake yakiwa mekundu sana.
“Mwamshe huyo bwege mwenzako hapo chini upesi” Rensho akakoroma, Nshomile akamtikisa waziri mstaafu kwa kutumia mguu, yule jamaa akagutuka kutoka katika usingizi wa kifo.
“Uliuwauwa wabunge wangapi waliopaswa kushika nyadhifa ya uwaziri mkuu hadi ukateuliwa wewe shetani mwenye miguu miwili…. Aah! Ni swali na njibu upesi. Ukichelewa nakuondoa mkono kama mwenzako, kama shetani mwenzako.”
“Wanne….” Alijibu huku akitetemeka.
“Ni wapi umeizika akili ya raisi wetu hadi amekuwa wa kukuamini kiasi hicho katika madaraka yake?”
“Kwenye kaburi la mama yangu..”
“Ambaye ulimtoa kafara sivyo?” Rensho akakazia. Waziri akaona aibu kujibu.
“Getonga, hii ni makala nadhani sihitaji kukukumbusha kuwa wewe ni mwandishi. Hivyo usitazame kama mchezo wa kuigiza natambua unao uwezo mkubwa wa kufikiri na kukariri utajua namna ya kuandika.” Rensho alimgeukia Getonga na kumweleza kisha akafanya tabasamu kali. Tabasamu la ushindi.
“Mkatandaza HOFU mabaradhuli wakubwa nyie, nazitumia hizi nguvu zenu kuwaadhibu sasa shenzi nyie……sogea hapa wewe waziri mkuu, upesi!!” amri ikatoka. Waziri akajizoazoa hadi mbele ya miguu ya Rensho.
“Mkeo anajua kuwa wewe ni mshirikina?” akamuuliza kwa upole.
“Hapana hapana sijamwambia….”
“Tazama na uone aibu….. mkeo hajui mambo haya kwa sababu ni machafu. Anayajua diwani wenu yule niliyemtoa roho Kahama. Sasa na nyie nawatoa roho mnasemaje juu ya hili.” Aliuliza akimtazama waziri kisha akamtazama mzee Nshomile. Wote walikuwa wametepeta huku wakitetemeka sana.
“G yaone haya…” alimuonyesha Getonga kisha akatoa kicheko cha dharau kubwa.
Ilikuwa imetimia saa mbili na nusu asubuhi wakati haya yakitokea.
__________
NYUMBANI KWA WAZIRI.
___________
Yale masaa waliyokuwa wamemzimisha mkewe ambaye aliwafuma wakiwa uchi yalikuwa yameisha tayari, yowe alilotoa yule mwanamke liliwashtua watoto wake wakaimbilia eneo la tukio, walivamia kile chumba na kila mmoja akapigwa na butwaa kukutana na maiti ya diwani ikiwa imeharibika vibaya mno.
Mama alikuwa anazimia na kuzinduka huku akishindwa kusema neno lolote lile. Majirani walipata nafasi ya kuingia katika baadhi ya vyumba vya waziri huyo ambaye alisifika kwa wema wake na ukarimu.
Baadaye mwanamke aliweza kutoa ushuhuda juu ya kila kilichotokea hadi alipomuona mumewe akiwa uchi wa mnyama pamoja na mzee Nshomile.
Waandishi wa habari walizinasa picha na maelezo ya yule mama kwa ufanisi wa hali ya juu.
Ilikuwa patashika katika jumba lile, kila mmoja aliamini kuwa waziri alikuwa mshirikina. Lakini swali lilikuwa moja tu. Na ni nani aliyemuua diwani.
Waswahili wakasema kuwa ametolewa kafara.
Polisi wakafika eneo la tukio, chumba kikazungushiwa utepe wa kiusalama, hakuna aliyeruhusiwa kuingia ndani ya kile chumba tena hadi hatua za ziada zitakapochukuliwa.
Waziri na mzee Nshomile wako wapi? Hilo likawa swali.
Msako ukaanza…… msako madhubuti wa kuwatafuta watu hao.
Raisi wa jamuhuri alizipata taarifa hizi lakini bado alikuwa upande wa waziri mstaafu. Alijaribu kwa kila hali kuupinga ukweli. Akili yake ilizikwa muda mrefu bila yeye kujua.
“Akipatikana aletwe kwangu moja kwa moja..” alitoa amri hiyo. IGP akaipokea.
Msako ukaendelea!!
WAKATI MSAKO ukiendelea Rensho alikuwa amewapa amri wawili wale kuwa walitakiwa kutoka ndani ya nyumba ile na kukitafuta kituo cha polisi kilichopo karibu waweze kujisalimisha na kueleza bila kuficha maovu yao.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akawafungulia mlango huku akiwa onyo kuwa wakithubutu kudanganya atavipasua vichwa vyao.
Walifahamu kuwa anaweza na hakuwa akitishia hivyo walitii, mmoja akiwa hana mkono, mwingine hana meno. Wakatembea kwa shida huku wakianguka anguka.
Ndani ya dakika kumi walikuwa wamezingirwa na umati na watu wengi walimtambua waziri yule aliyewahi kuwa maarufu sana, kisha akafifia na kisha kuibuka tena akitabiriwa kuwa raisi wan chi mtarajiwa.
Simu zkapigwa katika vituo vya polisi juu ya unyama waliotendewa wawili hawa!!
Waliotoa taarifa hawakujua kuwa hao wanaoonekana kutendewa unyama, wenyewe pekee ni wanyama tosha.
Polisi wakafika eneo la tukio na kuwasomba mabazazi wale wasiokuwa na huruma. Moja kwa moja katika kituo kikuu cha polisi ambapo taarifa ya mauaji ya diwani mwanamke ilikuwa imefika pale huku msako mkali ukiendelea juu nya waliotenda mambo haya.
Ajabu kuu waliosadikika kutenda unyama ule walikuwa hoi zaidi!!
Kulikoni? Hilo nd’o swali walilojiuliza.
Taarifa zikafikishwa kwa IGP akaamuru waziri mkuu mstaafu afikishwe mbele yake upesi sana.
“Sawa afande!” mtoa taarifa akajibu kwa heshima.
_______
UPANDE WA PILI
________
Rensho akawakusanya watu wake akiiacha maiti ya Queen katika jumba lile, Salome alikuwa amerejewa na fahamu tayari. Rensho akambeba Eva ubavuni mwake. Safari ya kukitafuta kitovu cha Kindo na kuusaka mwili wa Rensho!!! Bila kusahau kuifukua akili ya raisi wa jamuhuri ambayo ilikuwa imezikwa katika kaburi la mama yake waziri mkuu mstaafu.
Utata wa mwisho kabisa ukazuka katika harakati hizi!!
Raisi wa jamuhuri ya muungano akazua HOFU!!
!
RAISI wa jamuhuri ya muungano alikutana na waziri mkuu mstaafu katika chumba cha siri kabisa cha kijeshi.
Alimkuta akiwa amepewa huduma ya kwanza.
Waziri mkuu mstaafu alitamani kudanganya lakini alipokumbuka kile kitisho kisichokuwa na masihara kutoka kwa Rensho alilazimika kusema ukweli mtupu.
Ukweli ambao raisi aliukataa kata kata akidai kuwa yule bwana amerukwa na akili tu. Hawezi kuwa amefanya kitu kama kile, eti aliua wabunge wanne akamuua na mama yake.??
Hapana!! Raisi alikataa katakata. Alikataa huku akitabasamu akimaanisha kuwa ule ni mzaha mkubwa kabisa usiotakiwa kutiliwa maanani kabisa.
“Lakini mkewe anadai kuwa amemuona kwa jicho lake akiwa uchi?”
“Hapana usikae kuamini maneno ya wanawake na wewe….hakuna kitu kama hicho….mambo ya wanawake. Wanafiki wanaota ndoto usiku wanasema waliona kitu na wanabisha hao. Wanawake we huwajui wewe, nilikwambia uoe ona sasa…hujui lolote kuhusu wanawake IGP” Raisi alizungumza maneno mengi huku akizidi kuegemea upande wa Waziri mstaafu.
“Hapana mkuu, nimeyafanya hayo yote na mke wangu ni shahidi wa kweli kabisa, naiomba serikali yako inihukumu.” Waziri alimsihi raisi wa jamuhuri.
Kisha IGP naye akakazia.
“Haya mkewe alikuwa anaota, vipi kuhusu maiti iliyokutwa ndani ya kile chumba mheshimiwa?”
“Waliiweka mahanithi waliomjeruhi, tena hili jambo nitalisimamia ipasavyo hivi vyama pinzani vinataka kutudhoofisha kiasi hiki. Na chanzo ni kwamba anataka kuwania uraisi..shenzi kabisa. siwezi kuyafumbia macho, kuna vyama vinatakiwa kufutiwa usajili kabisa, nadhani unaelewa ninachosema” Raisi alizidi kuwaka. Kwa asilimia mia akiwa anamtetea waziri mstaafu.
Siasa bwana!! IGP alijiwazia huku akitazama jinsi gani waziri mstaafu alikuwa katika hatia ya waziwazi.
“Waliohusika na tukio hili wanatakiwa wafikishwe mbele ya sheria mara moja!!” alitoa amri, amiri jeshi mkuu wa Tanzania.
IGP akatii!!
*****
RENSHO alimruhusu Eva, Anitha na Salome kuondoka kuelekea nyumbani huku yeye, Kindo na Getonga wakibaki kwa ajili ya zoezi la mwisho kabisa.
“Nilisikia unasema kuwa wana kitovu changu, mbona sielewi?” Kindo alimuuliza Rensho wakiwa wametulia eneo fulani nje kidogo ya jiji wakisubiri kigiza kiingine waweze kufukua makaburi mawili.
“Unapozaliwa kitovu kinakuwa kimeungana na mama. Hivyo lazima kikatwe nd’o unabaki na hicho kidogo. Basi kilipokatwa kile kitovu huyo mzee Nshomile alikichukua, lengo lake likiwa moja tu. Kukutengeneza na kisha kukutumia katika shughuli zao. Hivyo walitulia kwa muda mrefu wakiyafanya maisha yako kama yao, hukuwa na akili darasani Kindo, maisha yako na ya wazazi wako yamekuwa magumu tu..mwisho wakaamua wakutumie wewe kunitoa mimi….yaani kuirudisha tena roho yangu. Wakakuongoza kufanya mapenzi na Salome kisha kumpa mimba isiyokuwa mimba. Mimba ya kichawi…. Nia yao ile mimba kabla haijakomaa waitoe kishirikina na kisha kuniunganisha na yale mabonge ya damu nizaliwe upya. Nilitakiwa kupewa cheo.
Waliowaagiza kumuua Salome wakafanya makosa kwa kumbaka yule binti, na hapa nd’o siku ile ambayo unakumbuka damu ilianza kuvuja chumbani nikiwa pamoja na wewe…unakumbuka?” alimuuliza, Kindo akaikumbuka hiyo siku.
“Basi nd’o mambo yalipowaharibikia hapo na walikufa wengi, nilibahatika kubaki hai kutoka katika tukio lile kwa sababu moja tu, sikuwa na mwili wala roho. Sasa ningekufaje unadhani….mwili ulizikwa miaka mingi iliyopita na roho ilikuwa katika mwili wa salome kama mimba ya ajabu. Hivyo wewe ulikuwa wa muhimu sana…… wakakutia hofu maradufu. Wauaji wale wakaishika akili yako ili usiweze kutoa ushahidi wowote ule juu yao. Mshukuru Mungu wako kuwa upo hai hadi sasa.” Alimaliza Rensho.
“Na wewe unataka kujua juu ya kitambulisho….hakina maana tena kile kitambulisho. Nina roho yangu tayari, kile kitambulisho kilikuwa kwa sababu moja tu….iwapo mambo yakiwa magumu kabisa niende kujisalimisha kwa mkuu wetu, lakini sasa sitajisalimisha bali nitamuangamiza na popote anaponisikia anajua kuwa nitamuua tu….” Alisema kwa hasira.
Walizungumza mengi, wakapata chakula na hatimaye kigiza kikaingia.
Rensho akawashika mikono na kisha wakatoweka na kutokezea makaburini.
Kindo na Getonga walikuwa wanatetemeka haswa kujikuta makaburini wakati ule.
“Alikuwa anaitwa Magreth Hossana, tafuta kaburi lenye jina hilo haraka.” Rensho aliamrisha. Kwa kihoro Kindo na Getonga wakaanza kuangaza huku na kule wakilitafuta jina katika makaburi.
“Huyu hapaa…..” Rensho ambaye pia alikuwa akilitafuta lile kaburi aliwapigia wenzake kelele.
“Hapo hapo mlipo simama kama mlivyo mikono juu” sauti nzito ya kiume iliamrisha.
Kindo na Getonga wakasimama huku wakitetemeka. Kutahamaki walikuwa wamezingirwa mbele ya nyuma na kundi la wanaume wakiwa wamebeba bunduki mikononi mwao.
“Nyie ni akina nani?” jamaa mmoja mwenye ndevu nyingi aliuliza.
Kabla hawajajibu lolote sauti ya Rensho ikasikika.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nipo nao kwani vipi?” alitokeza akiwa katika vazi lake lilelile jepesi kabisa.
“Mnafanya nini hapa wakati huu?”
“Kwani nyinyi mnafanya nini hapa?” na yeye aliwauliza kwa jeuri. Kisha akaongezea, “Halafu hamjisikii vibaya wanaume wazima tena sita sijui mmetushikia bunduki watu tusiokuwa na silaha na hatuna neno baya na ninyi?” aliwachokonoa maksudi.
“Kaa kimya mwanamke…tutapasua vichwa vyenu sasa hivi mkileta dharau wachawi wakubwa nyie….” Alifoka jamaa mwingine mwenye kipara.
“Ok! Kwani mnataka nini labda…”
“Tunataka kujua nyie ni akina nani?”
“Wachawi tumekuja kuwaroga hizo Bunduki zenu zigeuke nyoka ikibidi……” Rensho alijibu kwa jeuri huku akitoa tabasamu hafifu.
Jamaa mwenye kipara akataka kumvamia Rensho, hapohapo akaifungua mikono yake na kisha kuifunga.
Mayowe yakatanda pale wale majingili walijikuta wakiwa wameshikilia nyoka mikononi mwao. Walipiga mayowe huku kila mmoja akitupa chini kitu ambacho hapo awali kilikuwa ni bunduki.
“Kuja hapa?” aliamuru walipokuwa wanakimbia. Wakatii na kurejea huku kila mmoja akipigwa butwaa tena. Zilikuwa ni bunduki.
Wakaziokota kwa uoga…..
“Sasa mtafanya kazi ndogo tu kisha mtaondoka…mnifuate haraka” akaamuru wakamfuata.
Wakalifikia kaburi la mama yake waziri mkuu mstaafu….
“Mtafukua na kutoa jeneza…” alitoa maelezo mafupi.
“Haraka!!” akaamuru. Wanaume waogopa kufa wakabaki kushangaa ni kwa namna gani watafukua kaburi lililojengewa.
“Mnaduwaa….wapuuzi sana nyie…haya nalitoa jeneza huko chini nikilitoa mmojawenu analifunua na kutoa hirizi nyekundu katika mwili wa marehemu.
Rensho hakuwapa nafasi ya kufikiri.
Kindo alikuwa amejikojolea tayari baada ya dada yule wa ajabu kubadili bunduki kuwa nyoka. Getonga yeye alikuwa akitokwa jasho kwa fujo.
Haikuwa sinema kweli jeneza likatoka na kuwa hewani, jambazi mwenye kipara akalivaa jeneza akafunua. Akaingiza mkono katika mifupa iliyosalia akatoka na hirizi.
“Wewe ni baba lao….” Rensho akamsifia huku akiichukua ile hirizi na kisha akaifungua, upepo ukavuma kidogo, jeneza likatoweka na hirizi nayo ikatoweka.
“Uwe huru raisi wa watu wema…..” Rensho akasema hakuna aliyemuelewa moja kwa moja.
“Mnaweza kwenda majambazi nawatakia kazi njema!” aliwaaga kiutani….
WAKATI HUOHUO!!
Raisi wa jamuhuri ya muungano alikurupuka kutoka kitandani, akili yake ambayo ilikuwa ngumu sana kukubali kuwa Waziri mstaafu si mtu mzuri ilikuwa imefunguka akajiona mjinga sana. Akampigia simu IGP na kumweleza kuwa waziri mstaafu hastahili huduma wala uangalizi wowote ule wa kiafya.
Na sheria ichukue mkondo wake!! Akaagiza.
Walau IGP aliweza kutabasamu.
Akili ya Raisi ilikuwa imefunguka hatimaye.
*****
Makaburi ya CITY katika wilaya ya Temeke, jeneza la mtoto mdogo lilikuwa juu tayari. Rensho alilifunua lile jeneza huku machozi yakimtiririka.
“Baba kumzika mwana, kiunafiki kalia
Kaujaza umati sana, mama yangu kazimia
Baba asiye maana, kaidanganya dunia.
Narudi kuangamiza, huruma ka mbali nami.
Waziri si muungwana, ushirikina watumia.
Ikulu wataka sana, bila huruma waua.
Yote sasa ni bayana, wafungwe miaka mia.
Narudi kuangamiza, huruma kaa mbali nami.
Rensho amka tena, Myaka kumi karibia.
U hai si mfu tena, najua unasikia.
Watu hawana maana, ukiwaona kimbia
Narudi kuangamiza, huruma kaa mbali nami.
Rensho aliimba lile shairi huku akibubujikwa na machozi. Kisha akaingiza mkono wake na kutoka na hirizi nyeusi. Akaifungua na kuitupa kwa Kindo. Kindo akajirusha nyuma huku akipiga kelele.
“Kitovu chako hicho unakikimbia tena….” Alishangaa Rensho kisha akaingiza tena mkono katika lile jeneza.
Akatulia kwa muda mrefu kisha akaliachia jeneza likaanguka mle kaburini.
“Getonga!” alimuita huku akiwa ameinama bado……Getonga akasogea kwa Rensho.
“Nifungue hirizi kiunoni mwangu…..” alimweleza, Getonga ambaye uoga ulikuwa umepungua alimfunua Rensho na kutoka na hirizi kubwa.
“Itupe kaburini, usiniulize niliivaa saa ngapi?”
Getonga akaitupa….
“MWISHO” alisema huku akitabasamu.
“Sasa ninalo joto la kike nina kila kitu cha kuitwa mwanadamu na sina ulinzi tena wa kishetani.” Alizungumza huku dhahiri akionekana kuwa na furaha kubwa.
“Tunalala kwa nani leo..wengine nd’o tunaingia kuyaanza maisha sasa…..vipi huku duniani lakini?” aliuliza Rensho huku wakiifuata njia na kutoka katika makaburi yale.
Getonga akashauri waende nyumbani kwake kwa sababu sio mbali sana. Wakatembea kwa miguu kufuata barabara. Kila kitu ambacho Rensho alikuwa kikiona laikuwa anauliza ni kitu gani. Kindo na Getonga wakafanya shughuli pevu ya kumjibu kila swali.
Hakika Rensho alikuwa mpya katika dunia!
Walifika nyumbani kwa Getonga, hawakumkuta Anitha lakini Salome alikuwepo nje ya nyuma. Salome akamkimbilia Kindo na kumkumbatia.
“Anitha yupo wapi?”
“Ameenda kwao”
“Na wewe mbona upo hapa nje!!” Getonga akahoji.
“Mwenyekiti anadai kuwa nyumba hii imefungwa na serikali…”
“Yupo wapi mjumbe?” aliuliza, Salome akanyoosha kwa kidole. Getonga akaelekea nyumbani kwa mjumbe, wakasalimiana kwa bashasha kubwa huku mjumbe akishangaa jinsi Getonga alivyokuwa amechafuka.
“Ni simulizi ndefu?” alimjibu.
“Polisi wanakutafuta lakini?”
“Ukweli upo wazi usijali kila kitu kitaenda sawa naomba unihifadhie hawa wageni wangu. Kwa usiku wa leo tu, naamini kuwa kesho nyumba yangu itafunguliwa na maisha yataendelea…” alimweleza kwa kifupi. Mjumbe akakubali kutoa msaada huo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
******
KIHITIMISHO!!!
SIKU iliyofuata mambo yalikuwa motomoto, magazeti yalilipuka kwa habari juu ya waziri mkuu mstaafu na maamuzi ya raisi juu yake.
Dar es salaam palikuwa na hekaheka, yule mwandishi aliyetoroka mahabusu kimiujiza alikuwa mtaani, na yule mshtakiwa mwenza aliyetoroka pamoja naye alikuwa amepatikana..
Mwanadada anayesadikika kuchuna ngozi za wanaume wawili alikuwa jijini Dar es salaam.
Mwanadada wa kuitwa Rensho huyu nd’o alitikisa jiji zaidi. Kila mtu alitaka kujua Rensho ni kimbe gani hadi akawa anatokea katika miili ya watu wakifa baada ya kuvuja damu kwa muda mrefu.
Inspekta aliyerukwa akili alikuwa timamu kabisa akizisikia habari hizi katika redio.
Wanawake waliokuwa wakivuja damu nao zilikuwa zimekoma kabisa.
Kwa kifupi kila mkazi wa Dar alikuwa na jambo la kuzungumza.
Maofisini kazi zilikuwa haziendi kila mmoja alitaka kujua nini hatma ya haya yote.
Mahakama ya hakimu mkazi kisutu, waziri mstaafu na mzee Nshomile walikiri makosa yao bila kupinga. Walikubali kuwa nyuma ya majanga yote yaliyotokea.
BAADA ya siku kadhaa hukumu ya kunyongwa hadi kufa ilikuwa halali yao.
Rensho na wenzake wakiachwa huru kabisa.
Anitha alirejea kwenye ndoa yake baada ya wazazi wake kumsihi sana asidai talaka kwani mumewe alikuwa kazini nd’o maana akajikuta akiingia katika mkasa huo na hata kama hiyo haitoshi kwa ushahidi wake mwenyewe ni kwa kiasi kikubwa alijaribu kuipigania familia yake.
Salome na Kindo wakarejea kuwa wamoja huku Rensho akiyaanza maisha yake kwa kuishi nyumbani kwao Getonga.
JIONI moja katika fukwe za coco maeneo flani nje kidogo ya jiji.
Kindo, Salome, Rensho, Anitha, Getonga na Eva walikuwa wameamua kukutana kwa ajili ya kusimuliana mawili matatu. Kila mmoja alisema lake juu ya mkasa walioupitia.
Getonga ambaye alikuwa amekaa kimya muda mrefu aliongea wa mwisho.
“Katika mikasa yote niliyowahi kupitia sijawahi kupitia mkasa wenye kutia HOFU kama huu, yaani kila nilipogusa ilikuwa ni hofu tupu….nadhani hata nikiwaandikia makala wasomaji na wao wataingiwa na hofu wakiwa wanaisoma… kwa kifupi huu mkasa nitauita HOFU”
“Amakweli HOFU” Salome alijazia na wengine wote wakakubali kuwa ule mkasa ulijaa HOFU.
“Ila yote juu ya yote ashukuriwe Mungu maana maisha yanaendelea!” Anitha alimalizia huku akimuegemea Getonga begani kimahaba.
“Baba HOFU nd’o nini?” Eva naye akauliza kitoto toto.
Kila mmoja akacheka kwa sauti ya juu.
Sauti zao za furaha zikamtoa katika hofu mwandishi wa simulizi hii na kuamua kuitua kalamu yake chini na kulifunika daftari ambalo nyuma kabisa liliandikwa neno moja tu…….
“MWISHO”
TOA MAONI YAKO SIKU HII YA LEO….
ASANTE KWA KUWA NAMI MWANZO HADI MWISHO…….
0 comments:
Post a Comment