Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

HOFU - 4

 





    Simulizi : Hofu

    Sehemu Ya Nne (4)





    Na baada ya kuda geti likafunguliwa, Gerlad akashikwa mkono na watu asiowajua na kuongozwa kuelekea mahali.

    Giza likatawala kisha akaufikia mwanga….

    “Jibu moja la kipumbavu naondoa hii pua ya mkeo!!” alikuwa ni Rensho akiwa amemning’iniza Anitha mke wa Gerlad Getonga katika mbao nne imara akiwa amefungwa kamba.

    Getonga akapigwa na butwaa!!

    “Kitambulisho, pili Salome anapatikana wapi… hakuna jibu nachinja. Huwa sionyi mara mbili!!!” Rensho akazungumza kwa sauti ya chini!! Na wakati huo akahamishia kisu kuelekea katika shingo ya Salome.

    Getonga akatamani kusema lolote ajualo lakini bahati mbaya hakuwa akijua lolote!!!

    Mshikemshike!!!



    Zilikuwa ni sekunde takribani thelathini zilibaki ili Getonga ashuhudie kifo cha mkewe na hakujua iwapo Eva mtoto wake naye atauwawa kwa mtindo huohuo.

    “Rebeka….” Getonga aliita kwa sauti ya juu kiasi. Rensho akageuka kumtazama.

    “Huyo mama ukishamuua na kitambulisho kisipatikane utakuwa umesaidia nini?”

    “Gerlad Getonga na siasa zako tangu utotoni nikikuruhusu kuzungumza utanishinda tu…. I need my ID” Rensho aling’aka. Kisha akaongezea “Na nahitaji pia kujua Salome yupo wapi….”

    “Kuhusu kitambulisho kiukweli sikijui lakini ukinielekeza kilivyo naweza kukusaidia kutafuta, na kuhusu Salome yupo Kahama ukiniruhusu vilevile naweza kukusaidia kumsaka….”

    Maneno yale yakamtuliza Rensho kidogo, akashusha kisu na kisha kumkaribia Getonga waweze kuzungumza kiurafiki.

    Rensho akaamua kuwa mpole zaidi na hatimaye akaamua kumweleza Getonga mambo kadha wa kadha juu ya utata uliotanda.

    Getonga alikuwa msikivu sana akisikiliza historia ya maajabu ya mtoto aliyesemekana kuwa alikufa ulimwenguni na kuzikwa ilhali alikuwa mzima katika ulimwengu mwingine.

    “Wanadamu ni wabaya sana..watazame na uwaache hivihivi na siwapendi kabisa. hata wewe wasingekuwa mke na mtoto wako ningekuua siku ile ulipokwenda kwa mama yake Kindo kufuatilia jambo hili, hakuna kitu sipendi kama kufuatiliwa!!” akasita kidogo kisha akamtazama Getonga machoni kwa sekunde kadhaa. Macho yake yakaanza kujaa hofu ghafla, akakosa amani na mara akaanza kutokwa na kauli za ajabu ajabu.



    “Shit!!!” ghafla Rensho alishtuka huku kile kisu kikimtoka na kuanguka chini, aliyumba kama anayesukumwa na mtu asiyeonekana, aliwahi na kuushika mti uliokuwa jirani naye.

    “Amkaaaa Renshoooo!!!” alipiga kelele huku akitapatapa huku na kule.

    “Amka watashtukiaa!!” alitokwa na ukelele tena.

    Getonga akabaki kushangaa.

    Hakujua kuwa Rensho yu katika mapambano makali sana.

    ****



    MAGDALENA aliegesha gari eneo maalumu ambalo huwa analitumia kila siku kutokana na ufinyu wa eno katika nyumba aliyokuwa akiishi. Kisha akautwaa mkoba wake na kujizoazoa hadi nyumbani kwake.

    Tofauti na siku zote kukuta Martha amepika chakula ama la yupo jikoni katika hatua za mwishomwisho. Siku hii palikuwa kimya sana.

    “Martha weee!!” akaita kwa sauti yake iliyojaa upole.

    Kimya!!

    Akaita tena kwa sauti iliyoanza kupanda juu. Lakini bado ukimya ulitanda. Magdalena akautua mkoba chini na kwenda kutazama nini kimemsibu Martha chumbani kwake.

    Alifika na kukigonga chumba lakini hapakuwa na jibu, akaelekeza jicho lake katika kitundu cha kuingizia ufunguo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kitanda kilikuwa tupu, akataka kuufungua mlango lakini upepo wa ghafla uliobamiza milango na madirisha ukamfanya aghairi na kwenda kupambana katika kufunga mlango mkuu na madirisha.

    Upepo huu ulikuwa wa ajabu sana, ni kama ulikuwa ukipambana naye asiweze kufunga mlango, alijaribu kusukuma bila mafanikio, upepo ule wenye baridi na vumbi ukamzidi nguvu kama masihara, upepo ukaingia na kutokea dirishani. Kisha hali ikawa shwari……

    Magdalena akatoka nje kutazama ni madhara gani yamejiri kwa jirani zake, lakini akastaajabu kuwa wengine walikuwa wameketi nje wanasukana. Na wengine walikuwa wametingwa jikoni wakipika.

    Mh!! Upepo gani huu Mungu!! Alijiuliza huku akirejea tena ndani, akajitupa kwenye kochi, akawza juu ya hayo mambo mawili yaliyomtokea kwa kipindi kifupi sana.

    Kwanza kumkosakosa msichana barabarani akiwa uchi, kisha upepo mkali uliopoa ghafla.

    Hapohapo jicho lake likatua mlangoni, akaona kiatu cha Martha, akakumbuka kuwa kabla ya upepo kuvuma alikuwa chumbani kwake akifanya jitihada za kumtazama nini kinamjiri, hakumuona kitandani na alipotaka kufungua mlango ndipo upepo ukaanza kuvuma.

    Magdalena akasimama kiunyongeunyonge akakiendea chumba tena, akafika na kukifungua moja kwa moja.

    “Oh! My God…” akatokwa na mshtuko. Alikuwa anatazamana na Marha akiwa amelala uchi wa mnyama kitandani, na alikuwa hoi kweli.

    Dakika kadhaa zilizopita hakuwa kitandani, sasa amelala hoi bin taabani.

    “Mshenzi atakuwa ameingiza mwanaume humu ndani…. Walikuwa wanafanya mapenzi amemficha sasa anajifanya amelala..” akawaza Magdalena kisha akakisogelea kitanda na kuanza kumtikisa yule binti ambaye alimbatiza jina la Martha.

    “I love KINDO” Magdalena aliyaona maneno yale katika makalio ya Martha. Akaendelea kumtikisa.

    “Kindo jina kutoka Iringa hili… Kindole…” alipitisha wazo hilo katika kichwa chake kilichokuwa kimevurugwa haswa.

    “We Martha wewe…..” aliita huku akiangaza huku na huko kama upo uwepo wa mtu mwingine ndani ya kile chumba.

    Dakika tatu baada ya jitihada za kumuita bila mafanikio, Magdalena aliamua kulifikisha jambo lile kwa mjumbe!!

    Wakaongozana hadi nyumbani ili waweze kujua ni kitu gani kimemsibu Martha.



    Wakati Magdalena anafika kwa mjumbe na kumweleza juu ya hali ya mwanaye kitandani. Ni wakati huohuo jijini Dar es salaam, mwanadada mrembo wa kuitwa Rensho alikuwa amefumba macho akihaha kupiga kelele za kumuamsha Martha kwa namna yoyote ile. Aliita kwa nguvu sana huku kila anayemtazama akiduwaa.



    Mjumbe na Magdalena waliporejea wakamkuta Magdalena akiwa sebuleni ameketi akiwa na mavazi yake, mkononi akiwa na dawa za kutuliza maumivu.

    “Shkamoo mama…shkamoo mjumbe.” Alitoa salamu ile kwa kujiamini lakini akionekana kuwa hayupo sawa.

    “Marahaba Martha….. we mama na huyu hapa? Wanawake mbona mnatutia presha hivi sisi, nimezeeka jamani mimi” alilalamika mjumbe.

    Magdalena alikuwa amekodoa macho tu akimtazama Martha hakuamini hata kidogo kuwa ndiye huyu ambaye hakuwepo kitandani kisha akaonekana kitandani akiwa hoi usingizini na sasa yupo sebuleni.

    Hofu ikatanda waziwazi!!

    Mjumbe aliondoka akiwa amejaa ghadhabu kubwa. Akamlaani Magdalena kwa kumpotezea wakati na kumtia hofu pasipo na sababu.

    “Martha umekuaje mama…eeh!” alimuuliza walipokuwa wamebaki wawili.

    “Kichwa kinaniuma mama…..”

    “Pole mwanangu. Tangu muda gani una hali hii.”

    “Yaani tangu nilale mchana sijaamka hadi sasa hivi.”

    Mh! Tangu mchana wakati sijamkuta kitandani huyu…..

    “Martha hakuna kitu sipendi kama kudanganywa katika maisha yangu..” alionya Magdalena huku akitetemeka kwa hasira, wazo lake lilikuwa palepale kuwa Martha ni muongo. Na siku hiyo atakuwa aliingiza mwanaume ndani ama la alienda kwa mwanaume mahali.

    “Sikudanganyi mama..nililala tu na sijatoka nyumbani.” Martha alijibu kwa upole.

    Magdalena alisimama na kuzunguka huku na kule kisha akamvaa Matha tena.

    “Niambie ukweli jioni hii kabla hujaigiza kuwa umesinzia kitandani uchi, ulikuwa unafanya nini?”

    “Mama sijawa sehemu yoyote na sijatoka kabisa….. kichwa kimeniuma sana.”

    “Ok! Hebu ngoja….” Alisema na kuiacha ile kauli ikielea hewani akaingia chumbani ili aweze kuhakikisha ni kitu gani Martha anamficha.

    Alipokifungua chumba tu… kitu cha kwanza kugundua kilikuwa ni kiatu cha kiume.

    “Mwanaharamu mkubwa huyu!!” akatokwa na kauli nzito huku akikibeba kile kiatu.

    “Nahesabu hadi tatu..wewe kidume uliyejileta ndani ya nyumba hii kuzini na binti yangu kama hujajitokeza. Naita polisi na utajuta kwa kitendo ulichokifanya.” Alitoa karipio kwa sauti ya juu sana iliyojaa kitetemeshi.

    Martha akiwa sebuleni akaiona dalili ya mama yake huyo wa kufikia kurukwa na akili. Mwanaume gani ndani ya chumba chake. Ni jambo ambalo halikumuingia akilini kabisa.

    Akaona isiwe tabu, akasimama na kuelekea chumbani kwake.

    “Mama….”

    “Nani mama yako mshenzi wewe… Martha kukupenda kote kule leo hii unaniletea mwanaume ndani ya nyumba yangu. Ulitaka nikupendeje wewe. Matha nimekuokota huna hili wala lile wewe eeer” alizungumza kwa uchungu mkubwa.

    “Mama mimi na wanaume wapi na wapi?”

    “Hiki kiatu cha kwako eeh!! Cha kwako nakuuliza?” Magdalena alimwonyesha kile kiatu kwa kumsuta. Matha alipokana kuwa hakijui akawa ametibua hasira za Magdalena.

    Kipigo kikachukua nafasi!!

    Magdalena alipiga kama mwizi!!



    Jijini Dar es salaam, Rensho akaanza kuingiwa na hofu ya usalama wake.

    “Renshooo atakuuua…. Pigana wewe….” Alipiga kelele huku akianguka chini na kugaagaa.

    Alikuwa akiunguruma kama mbwa aliyejeruhiwa ama mwenye hasira.



    Mjini Kahama, Martha ambaye ni Salome. Akaudaka mkono wa mama yake wa kufikia, akaanza kuuviringisha, yule mama hakuamini. Akaanza kujitoa lakini hakuweza, Martha akarusha mkono na kumnasa kibao kikali yule mama.

    “Martha unanipiga mimi…” aliliza na asiamini kinachotokea. Martha hakumjibu, akauzungusha mkono kwa nguvu zaidi mama akapiga mayowe yalkiyoambatana na mlio wa mkono kuvunjika.

    Teke zito likamtoka Martha na kusambaratisha mbavu kadhaa katika ubavu wa yule mama na palepale akapoteza fahamu.



    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    KESI mbili zikapata muunganiko na kushabihiana.

    Wanaume wawili wamekutwa wamechunwa ngozi nje kidogo ya mji wa Kahama. Katika eneo la tukio vimekutwa viatu vitatu, viwili vikiwa vinafanana na kimoja kikikosa mwenzake.

    Kiatu kilichokosa mwenzake kimekutwa maeneo ya kahama mjini katika nyumba ya mwanamke anayedai kujeruhiwa na binti yake wa kufikia, na kiatu hicho kilikuwa chumbani mwake.

    Mwanamke huyo aliyejeruhiwa vibaya huku akivunjwa mkono wa mbavu mbili alifahamika kwa jina la Magdalena na anadai anayeweza kujua wapi kile kiatu kimetoka anakwenda kwa jina la Martha.

    Mama yule akaongeza kuwa katika makalio ya yule binti kuna jina KINDO hivyo kwa namna moja ama nyingine anaweza kuwa anahusika kufahamu huyu binti ni nani na anapatikana wapi.

    Mahakama ya wilaya haikuwa na uwezo wa kusikiliza kesi ile ya mauaji. Kesi ikahamishiwa jijini Dar es salaam

    Martha akaanza kusakwa kwa kesi ya mauaji na kisha kuchuna ngozi za mwanadamu.

    Kindo akahusishwa katika kusaidia upelelezi!!



    Wakati kesi hii ikishika kasi.

    Getonga na Rensho walikuwa wasafiri katika basi la abiria kutoka Dar es salaam kwenda Kahama kwa sababu moja tu ya kumsaka Salome ili Rensho aweze kuuchukua uhai wake na kurejea katika maisha yake bila kumsumbua mtu tena.



    KIZAAZAA kikubwa kikaanzia hapa!!!.



    Rensho alikuwa gumzo punde tu baada ya kupiga hatua na kuingia ndani ya basi lile. Mavazi yake na manukato aliyopulizia yalimfanya awe wa kipekee katika safari ile.

    Wanaume walimtamani pasi na kujua kuwa hakuwa wa ulimwengu huu!!

    Getonga pekee ndiye aliyefahamu fika kuwa alikuwa ameongozana na mwanamke ambaye alizikwa akiwa na miaka kumi tu, akasahaulika na matanga yakakaa. Lakini ajabu yu hai tena.

    Kichwani mwake Rensho yalipita maswali mengi sana juu ya namna ya kukabiliana na huyo dada wa kuitwa Salome mjini Kahama. Hamu yake ilikuwa kurejea alipotoka.

    “Ulisema kitambulisho umekihifadhi wapi?” Rensho alimuuliza Getonga kwa sauti ya chini kabisa.

    “Kitakuwa nyumbani katika nguo zangu, sikuwahi kukitazama hata siku moja. Na hata ukiniuliza kipo vipi sina la kujibu.”

    Rensho akafanya tabasamu hafifu na kisha kuendelea kuuchapa usingizi katika siti aliyokuwa ameketi. Getonga yeye alikuwa anasoma gazeti alilonunua.

    Robo saa baadaye mwanaume mwenye sauti ya juu ya kukoroma aliwasalimia abiria kwa ujumla na asijali iuwapo wamemjibu ama la. Kisha akakohoa kuweka koo sawa.

    Na hapo akaanza kuhubiri neno Mungu, akakemea mambo kadha wa kadha akawasihi watu kumtukuza Mungu maana ufalme wake umekaribia. Asilimia hamsini ya abiria walimsikiliza na kumtilia maanani huku wale wengine wanaoamini kuwa dini imegeukia biashara hawakujishughulisha naye hata kidogo.

    “Wengine wamelala kabisa, mwanadamu unaweza vipi kulala bila kumtukuza Mungu. Imeandikwa kesheni mkiomba maana ufalme wa mbingu unakaribia…..” sauti ile ikapaa zaidi na kupasua ngome za Rensho. Kutoka katika usingizi wake akaitambua ama kuifananisha ile sauti.

    “Getonga na huyu ni mmoja wao….” Alimweleza huku akiwa amefumba macho.

    “Mh! Unaota mapema yote hii…” Getonga alijibu huku akitabasamu na akilini akijisemea “Hadi majini nayo yanaota….balaa!!”

    “Gerlad Getonga, sioti nimefumba macho, na huyu ni mmoja wao..anataka kutoa kafara watu wote katika basi hili. Washenzi sana hawa…. Washenzi G…..mimi si mkorofi ila sitaki kushirikiana na watu hawa nataka kurudi nyumbani….” Rensho akasema huku bado akiwa amefdumba macho. Kwa maongezi yake Getonga akagutuka kuwa yule binti hakuwa katika ndoto. Akamtilia maanani!!

    “Ni nani unayemzungumzia…”

    “Huyu anayepiga hizo kelele katika lugha ya maajabu…” alijibu kwa utulivu. Kisha akaongezea, “Atawasimulia wenzake kitakachomtokea. Akisema fumbeni macho tuombe nishike bega unitikise kwa nguvu, usiipoteze nafasi hiyo maana hamtafika Kahama salama, wote mtakufa!!” alizungumza kisha akatulia tuli.

    Getonga akabaki katika kuduwaa asiamini kabisa kama Rensho yupo sahihi, alimtazama yule bwana aliyevalia suti ya bei ya kawaida tu anayepiga kelele na kutokwa jasho.

    Mbona kama mtu wa Mungu huyu!!! Alijisemea. Na wakati huohuo yule bwana akawaomba abiria wote wafumbe macho waweze kuomba.

    Getonga hakutaka masuala ya majuto ni mjukuu, akaamua kufanya Rensho alivyotaka na hapo likazuka sekeseke maridhawa ndani ya basi.

    Wakati huo walikuwa katikati ya Mlandizi na Kibaha.

    Baada ya kutikiswa bega, Rensho aliruka kama mtu aliyeshtuka kisha akajirusha na kuikaba shingo ya yule aliyejiita mtu wa Mungu. Yowe la hofu likamtoka na kile kitabu cha dini kikamtoka mkononi.

    Rensho bila kuiachia koo ya yule muumini, akaivuta suti yake kwa nguvu. Wakati huo abiria wengine walikuwa wamemsogelea Rensho wakiamini ana mapepo.

    Lahaula!! Hirizi kubwa nyekundu ikaonekana kifuani mwa yule jamaa. Wasafiri waliokuwa na viherehere wakarudi nyuma na kukanyagana walipoiona hirizi ile. Wanawake wakaanza kupiga mayowe wanaume wakawa wanatetemeka. Dereva naye akasimamisha basi.

    “Ni nani aliyekuagiza humu??” hatimaye Rensho akauliza swali lile akiwa na ghadhabu. Yule bwana aliyekuwa amekodoa macho alijaribu kufinya macho hapa na pale kama namna ya kujitetea lakini Rensho alikuwa makini zaidi, kwa zaidi ya miaka kumi alikuwa ameishi katika yale maisha ya giza na bado alikuwa hajatoka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Amakweli Rensho hakuwa mtu wa kuuliza mara mbili!

    Ghafla akamwachia yule jamaa na hapohapo akamrukia teke kali kifuani mwake, jamaa akajibamiza katika viti na kutua chini kwa nguvu huku akipasuka vibaya mno.

    “Nshomi….Nshomi…..” alijibu hatimaye huku akivujwa damu.

    Baada ya kupata jibu lile, Rensho mwenye ghadhabu alimrukia tena kwa nguvu pale chini, akamkaba koo kwa nguvu kisha likafuata tukio la maajabu ambalo lilileta hofu zaidi.

    Rensho huku akipiga kelele nyingi sana akaivuta ile hirizi, na hapo ukatokea mlipuko mkali. Moshi mweusi ukatanda katika ile basi.

    Hakuna abiria aliyemuona mwenzake, moshi ulikuwa unanuka vibaya sana.

    Mayowe yakatanda kila kona na wakati huu hadi wanaume nao walilia wakiita mama zao. Utata!

    Getonga alikiri kuwa mkasa huu ni zaidi ya yote aliyowahi kupitia katika uandishi wake. Maana huu wa sasa ulimweka ye mwenyewe katika mazingira ya kuishi kwa uoga wakati wote bila kujua nini hatma ya yote haya.

    Baada ya takribani dakika kumi, kila mmoja alimtazama mwenzake kama kituko, alikuwa mweusi tii!! Kwa sababu ya ule moshi.

    Kasoro Rensho tu ndiye alibaki katika mng’ao wake wa awali.

    “G…” Rensho akamuita Getonga kisha akamshika mkono. Wakatoka nje ya basi ambapo raia wema walikuwa wamezunguka hapa na pale kufuatilia kuna nini kinatokea.

    “Nawatakia safari njema!!” Rensho alizungumza huku akitoweka na Gerlad. Yule jamaa wa kuhubiri hakuonekana tena, Rensho alikuwa ametuma salamu zake huko ajuapo. Salamu kwa njia ya kuua….

    Abiria walikuwa kimya wakati Rensho na Getonga wakitoweka.

    Hatimaye wakaishia porini.



    “Nishike kwa nguvu..muda umetuacha sana…” Rensho alimuelekeza Getonga ambaye hakuwa na kipingamizi akafanya kama anavyotakiwa.

    Kufumba na kufumbua, walikuwa wanatazamana na bango lililoandikwa KARIBU KAHAMA.

    Getonga alianza kuyazoea haya mauzauza.

    Msako ukaanza usiku uleule!!



    ****



    Jijini Dar es salaam, kesi kutoka mjini Kahama ilionekana kuoana vyema na tukio ambalo limewahi kutokea jijini Dar es salaam takribani mwezi mmoja na ukiwa umepita.

    Mpelelezi wa kesi ile kutoka mjini Kahama aliikabidhi kwa wapelelezi wa jijini Dar es salaam kwa minajiri ya kushirikiana katika kulitatua hili.

    Inspekta John Magege aliisoma vyema kesi ile akahusisha na nyingine kadhaa ambazo zimejitokeza jijini Dar es salaam.

    Kindo! Hili ndilo jina ambalo lilitokea Kahama na pia Dar es salaam.

    Akalikumbuka tukio la mauaji makubwa katika nyumba ya mheshimiwa mbunge mtarajiwa, mauaji ambayo chanzo chake hakikujulikana zaidi ya kupitishwa kuwa Ebola ndiyo imewaua.

    Katika kesi hii Inspekta Magege alitakiwa kushirikiana na mpelelezi wa kwanza kabisa wa kesi iliyotokea jijini Dar es salaam. Inspekta Kisembe.

    Lakini bahati mbaya Kisembe naye alikufa hata kabla kesi haijafika popote. Alikufa kwa kuvuja damu!

    Alipokumbuka hili mwili ukamsisimka.

    Alikuwa anayo nafasi ya kujiingiza katika kesi hii ama kuiacha kwa wapelelezi wapya kabisa. lakini akachagua kuendelea na upelelezi huo. Upelelezi wa kumsaka msichana aitwaye Matha ambaye anajihusisha na kuchuna ngozi za wanadamu.



    Inspekta John akiwa ndani ya gari lake binafsi aliamua kuifanya kesi hii katika utaratibu wa hali ya juu sana.

    Wakati natoka kazini bila kumpa mtu taarifa yoyote aliamua kufuatili ile nyumba ambayo yalitokea mauaji ya kutisha huku akipona mwanaume mmoja tu wa kuitwa Kindo huku akisema neno moja tu… “RENSHO!” tena bila kukoma.

    Aliiendesha gari yake kwa umakini na utulivu mkubwa hadi akaifikia ile nyumba ambayo hakuna mtu alikuwa akiishi tena bali mlinzi wa serikali aliwekwa pale kulinda hadi ufumbuzi utakapopatikana.

    “Inspekta John Magege…” alijitambulisha kwa mlinzi ambaye alikuwa ananuka pombe za kienyeji wakati ule. Mlinzi akamruhusu kuingia ndani.

    Kwanza akaikagua nyumba vyema kuanzia nje kabla hajaufikia mlango na kuufungua…..

    Nzi wakaruka wakipishana naye na wengine kumzunguka.

    “Mh! Nzi hadi leo…” alijiuliza wakati akiungua mlango zaidi. Nia yake alitaka kufananisha ripoti iliyoandikwa na marehemu Inspekta Kisembe na mazingira halisi juu ya vifo vile vya kutatanisha.

    Akapiga hatua ndani, nzi wakazidi kusikika wakipiga miluzi kutokea katika chumba kingine. Inspekta John akasita kuendelea mbele akatamani kumuuliza mlinzi swali, akapiga hatua mbele kisha nyuma tena.

    Akatoka nje hadi kwa mlinzi!!

    “Mpo makini na ulinzi wa jengo hili ama?”

    “Makini sana afande!!”

    “Hakuna watoto wanaruka humu ndani na kuacha vinyesi. Not watoto peke yao hata watu wazima….” Alihoji Inspekta.

    “Hapana, kila dakika kila sekunde tupo hapa kulinda. Na kwa uzio huu hawezi kiumbe kuruka ili aje kumaliza haja zake humu. Haiwezekani hata kidogo afande!!” alipinga mlinzi wakati huu akiwa makini zaidi. John akalisaili eneo lile na kukiri kuwa hakuna kiumbe awezaye kuruka ule uzio kwa ajili ya kumaliza haja zake mle ndani.

    “Kwani kuna nini afande!!?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akaondoka bila kujibu swali la mlinzi ambalo lilikuwa muhimu. Muhimu sana.



    “Badala anijibu na mimi nimwambie ninachokijua katika jumba hili…. Aah! Shauri zake bwana na u-inspekta wake. Yaani watu wakiwa na vyeo eti hawataki kuulizwa maswali..” alilaani yule mlinzi huku akiketi katika eneo lake tena. Gobole lake akilifanya egemeo.



    JOHN aliingia moja kwa moja ndani tena, akapenya hadi kule ambapo awali alisikia nzi wakivuma.

    Safari hii alisikia na sauti zikiunguruma kwa chini sana mle ndani.

    “Pumbavu zao hawa walinzi wameipangisha hii nyumba…” alijisemea huku akitembea kwa kunyata.

    Hatimaye akaanza kusikia neno moja moja…

    “Ametuzidi ujanja……. Atatuua yule….” Moja ilikuwa sauti ya kiume na nyingine ikiwa ya kike.

    “Wamepangisha majambazi humu. Pumbavu sana….” Akajipapasa mahali inapoishi bunduki yake, akakumbuka kuwa aliiacha ndani nya gari yake.

    Sauti zikazidi kunong’ona, sasa alianza kuifahamu sauti mojawapo. Na lile wazo lake kuwa kuna watu wamepangishwa mle ndani likaanza kuyoyoma.

    “Tatizo hatuwezi tena kujua alipo…… atatuua kimyakimya akitoka katika lile tumbo la Kahama. Yaani akitoka kila mmoja aanze kuchimba kaburi lake mapema… ila wewe nilikueleza kabisa kuwa yule nani yule……”

    “Shhhh!! Sio muda wa kulaumiana huu, yule nani sijui nani sio wakati wake…ishu ni moja tunafanya nini?? Limeshatokea hilo?” mwanamke alihoji kwa hamasa.

    “Hivi huyu kitambi naye ameendaje kwenye basi bila kulikagua.. huenda angemjua na kumkamata kabla hajauwawa.” Mwanaume bado alikuwa katika kulalamika.

    “Makamu anakuja muda gani maana hapa sio salama, tunatakiwa kuuchukua huu mzoga tuondoke.” Mwanamke aliulizia na hapohapo upepo ukaanza kuvuma, upepo wenye ubaridi wa hali ya juu. Upepo ule ukapenya ndani kama kimbunga.

    Inspekta John akashikwa na kigugumizi iwapo atoke nje ama aendelee kubaki. Ujasiri ukamsukuma kubaki, akapiga hatua moja na kuchungulia, akakutana na migongo ya watu wawili. Lakini chini ulikuwa mwili uliotokwa na uhai. Bila shaka nzi walijileta kwa sababu ile.

    Akina nani hawa? Mbona sauti kama…..hata mwili nao kama wa…..oooh!! ni yeye huyu ni yeye…anafanya nini humu jamani. Mungu wangu…” alitaharuki Inspekta John. Mara ule upepo ukakoma.

    John akatoa simu yake mfukoni aweze kupiga picha walau moja tu ya umuhimu sana.

    Akaseti simu yake isitoe mwanga wakati wa kupiga ile picha na wala isitoe mlio wowote.

    Upesi akaitega vyema!! Akiwa makini kabisa.

    Lakini kosa moja tu likamgharimu. Simu yake haikuwa imewekwa katika ukimya na muda huohuo mkewe alimpigia simu maana usiku ulikuwa unaingia na hajarejea nyumbani!!

    Simu ikapiga kelele.





    ******



    Maeneo ya Nyihogo ndani ya mji wa Kahama. Getonga na Rensho walichukua chumba kwa kutumia pesa aliyokuwanayo Rensho na Getonga asijue ni wapi ameitoa.

    “Yule bwege wa kujifanya mchungaji alikuwa na pesa sana…” Rensho alijisemea wakati wakiwa ndani ya chumba walichokuwa wamechukua. Getonga alimtazama bila kusema neno lolote.

    “Saa sita kamili usiku niamshe we jamaa, nd’o muda mzuri wa kumsaka huyo Salome….. kwa wakati huu siwezi kujua pa kuanzia…we bwege ungekuwa umenipa kitambulisho changu hata nisingehangaika hivi!!”

    “Nitakuamsha!!” Getonga alijibu kwa upole.

    “Chukua simu yako katika pochi humo…ama ilete hiyo pochi hapa” akazungumza Rensho. Kisha akachukua kipochi chake na kuitoa simu ya Getonga. Getonga aliduwaa na kutaka kuuliza ile simu imefikaje pale lakini akahofia kumkera Rensho. Akaipokea.

    “Ole wako uwasiliane na mtu kabla hatujamaliza kilichotuleta..,.. nimekupa useti alarm tu ya kutuamsha saa sita basi!!”

    Getonga akafanya kama alivyoamrishwa! Wakati Rensho anapitiwa usingizi aliukunja mguu wake na kuuweka juu ya mwingine, mapaja yake meupe na laini yakachungulia nje.

    Getonga akazikumbuka ndoto za marehemu kadhaa ambao walikuwa wakiota mwanamke mwenye mapaja meupe kisha ameyaacha nje huku akiupandisha mguu mmoja juu ya mwingine.

    Nalala na jini leo!! Getonga alijisemea huku hofu ikimtawala zaidi



    ****



    Jijini Dar es salaam, kabla Inspekta John Magege hajatambua ni kitu gani afanye baada ya simu yake kutoa mwanga. Wale watu tayari walishamshtukia na yule mwanamke akawahi kumdaka.

    “Inspekta John Magege!! Kipi kimekuleta huku. Mtoto mdogo kama wewe…” yule mwanamke alimuuliza baada ya kumtambua.

    “Lakini hata usingekuja bado tungekutana tu… asante kwa kujileta mwenyewe kwa wakati…” mwanaume alimtazama kwa kebehi na kumwambia maneno yale, Inspekta aliyekuwa ameketi chini alijikakamua na kuzungumza, “Mpo chini ya ulinzi wa…” kabla hajamaliza alishtukia akikwanguriwa vibaya mno na kitu ama mnyama asiyemjua.

    Sekunde nne nyuma alikuwa mzima wa afya na uso unaong’ara lakini sekunde nne baadaye alikuwa akiugulia maumivu makali na uso wake ulikuwa unatokwa damu.

    Kama ni kiumbe basi alikuwa ni paka.

    “Hakuna amri za jeshi katika chumba hiki bwana mdogo…na kwa vile umetutambua basi naweza kukuahidi kuwa uhai wako upo mikononi mwako…. Kiburi kitakufanya umfuate huyu mwenzetu alipokwenda..” mwanaume mwenye kitambi alimkoromea huku akimwonyesha maiti ya mwenzao ambaye aliagizwa kwenda kusaka damu kwa kuleta ajali ya maksudi katika basi. Bahati mbaya akakutana na Rensho akaambulia kifo.

    “Watu wengine bwana…juzijuzi tu kilikuwa ki-koplo sasa kupandishwa cheo na kuwa Inspekta nd’o kujifanya unajua kufuatilia kila kitu….shenzi taipu.” Mwanamke alimsimanga inspekta John.

    “Haya hatupotezi wakati hapa….Mafaili ya kesi hii yapo wapi na upelelezi wako umefikia wapi Inspekta.” Bwana mwenye kitambi akaunguruma. Inspekta John akanywea na kutambua kuwa watu hawa hawakuwa wa kuwatishia neno ‘mpo chini ya ulinzi’. Akalazimika kujibu. Alijibu kila alichokuwa anakijua huku watu wale wakimsikiliza.

    Baada ya maelezo yake, wale watu wakanasa mambo mawili makuu.

    Kindo, yule mtu aliyepona katika sekeseke la mauaji yale makubwa alikuwa bado hai huku akimtaja RENSHO….

    Pili kuna msichana mjini Kahama anayedhaniwa kuwa ni mchuna ngozi amekutwa na maneno katika makalio yake.

    “I love KINDO”.

    Huu ulikuwa mwangaza tosha, watu wale wakatoweka pale upesi na kukubaliana kukutana katika nyumba ya makamu mwenyekiti wao baada ya muda mfupi.

    “Huyu naye….” Mwanamke aliuliza huku akimtazama Inspekta John

    “Mfunge tu asije akatusumbua baadaye…” mwanaume alijibu, John hakuelewa walimaanisha nini. Alimtazama yule mwanaume ambaye anamfahamu vyema akitegemea huruma yake lakini haikuwa hivyo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya nusu saa Inspekta John akiwa amevua suruali yake na kuitupia begani huku shati lake akilichomekea katika kibukta kifupi alichovaa, alitoka mle ndani akiwa anacheka tu.

    Mlinzi alimuona kuanzia mbali…. Hakutaka kulisubiri lile balaa. Akajificha aweze kuona ni kitu gani kinamtokea yule mbwana mjivuni wa cheo.

    Kupitia alipojificha alimuona Inspekta akilipita gari lake na kuendelea kwenda mbele akiwa anacheka vilevile kama alivyotoka.



    ****



    Ulikuwa ni mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi maalumu kwa ajili ya mfungo wa takribani mwezi mzima kwa ajili ya toba kwa dini ya kiislamu.

    Waziri mkuu mstaafu ambaye pia alitajwa sana kuwa ni mtarajiwa katika kugombea nafasi ya uraisi baada ya miaka minne alikuwa chumbani kwake huku nje kukiwa na mamia ya wananchi ambao walikuwa wamekuja kufturu. Ilikuwa kawaida ya bwana huyu kufanya jambo hilo kwa wanachi si chini ya miamoja kwa siku. Tangu mfungo ulipokuwa umeanza.

    Kwa siku nyingine alikuwa akiungana nao na kula pamoja lakini siku hii hakuonekana kabisa, hadi alivyoingia baadaye sana na kuwapungia mkono tu huku akionekana kuwa mwenye haraka sana.

    Baada ya muda ugeni mwingine ulifuata, akaingia diwani wa kata yao na mwanaume mwingine ambaye alisemekana kuwa atakuwa meneja kampeni wakati wa uchaguzi.

    Hayo yote yeye mwenyewe muheshimiwa hakuwahi kuyathibitisha na kila alipoulizwa alicheka tu na kusema watu wasubiri muda.

    Ndani ya chumba kimoja, watatu hawa walikutanika na kuhakikisha chumba kimefungwa kabisa.

    “Nshomile….. weka mipango mezani sasa.” Muheshimiwa waziri mkuu mstaafu Kimune Mune alimuuliza mwenzake. Yule diwani akakaa vyema akisubiri Nshomile aweze kuzungumza.

    “Mipango iliyokuwepo ya mimi kumuagiza marehemu ndani ya lile gari, tulitaka kumridhisha muwezeshaji ili aweze kuingia katika vita hii na atusaidie kutukamatia huyo Rensho na ku…”

    “Mshomile hayo yamepita tayari tuweke mkakati wa usiku huu huu ikiwezekana….” Diwani alimkatisha Nshomile ambaye ni baba mzazi wa Rensho.

    “Hapa la msingi zaidi ni kwenda Kahama…tukimpata huyo binti mwenye alama ya Kindo makalioni lazima atatueleza Kindo yupo wapi, tukimpata Kindo lazima tu atatuelekeza ni wapi Salome yupo, akikamatwa yule ni kuondoa kile kiumbe tumboni, kwisha habari yake Rensho hapo…. Mtoto mdogo kama yule anatusumbua hivi..” alitoa maelezo yake kwa kujiamini kabisa.

    “Na kile kibwana Inspekta umekifunga vizuri kweli asije akatuharibia, si unajua ninavyojulikana mimi.” Kimune Mune, waziri mkuu mstaafu alihoji.

    “Magazeti ya kesho kutwa zitawekwa picha zake nd’o utajua kama bado ni inspekta ama ni mtu wa kupelekwa Milembe huko akakae na vichaa wenzake.” Mzee Nshomile alijibu kwa nyodo huku akiachia tabasamu hafifu.

    “Haya tuna masaa kadhaa ya kufanya jambo hili, mke wangu nimemwambia hatuhitaji usumbufu tuna kikao cha muda mrefu..kwa hiyo tunaondokea hapa na tutarudi wote kukutana hapahapa. Tunaondoka sasa!! Tukumbuke kuwa tukifanya mzaha, IKULU tunaikosa na hicho kitoto tulichokilea sisi kitatuabisha hadharani!!” Waziri mstaafu aliamuru. Kila mmoja akajiandaa na kutoweka katika njia walizozijua wao.

    Majira ya saa tano usiku walikuwa mjini Kahama wakirandaranda huku na kule. Waligawana sehemu za kufanyia msako ule usiku. Kwa nguvu zao za maajabu kila mmoja akiwa na jina Kindo mkononi akilisaka ni wapi lilipo.

    Hawakuchoka watatu hawa licha ya kuruka hapa na pale bila mafanikio, hatimaye katika kitongoji cha Nyahanga nje kidogo ya eneo la kahama mjini. Diwani mwanamke alihisi Kindo aliyoiandika ikivutana kuelekea mahali, akaifuatisha hadi katika bonde moja, akashuka huko kwa kasi akalifukuzia windo lake, mbwa walibweka sana lakini hakuwajali.

    Hatimaye akafikia mahali na kukuta mtu akiwa amejifunika.

    Akamfunua haraka. Ana kwa ana akakutana na mwanamke mwenye ujauzito unaoonekana waziwazi, alikuwa amelala mithiri ya mtu aliyepoteza fahamu ama amekufa kabisa.

    Alianza kumtikisa kwa nguvu bila mafanikio, hatimaye akamfunua nguo zake akamgeuza nyuma… kwa utulivu kabisa kayaweka macho yake sawa akisaidiwa na ile mbalamwezi iliyokuwa inang’ara haswa. Akalisoma jina Kindo katika makalio ya yule dada..

    “Maskini na kimimba chake….” Alijisemea yule diwani mwanamke huku akimvisha tena mavazi yake.

    Sasa naondokaje naye wakati amezimia sijui amelala!! Alijiuliza.



    Katika hoteli waliyolala Kindo na Rensho ile simu ikalia kumaanisha kuwa muda ulikuwa umefika. Kindo akamtikisha Rensho kidogo tu akaamka na kuruka kisha akasimama wima.

    “Shenzi taipu wamenisogelea wajinga hao…. Wamenisogelea….. wapo wapo….” Alihamanika Rensho kisha akaufungua mlango na kutoka nje. Huku nje alikimbia kidogo kisha akatoweka kabisa.

    Sekunde kadhaa akawa katika jalaa lililokuwa bondeni kabisa.

    Yule diwani akiwa anajihangaisha kumwamsha Salome pale chini.

    Rensho akawasili na hakuwa na wakati wa kupeana salamu, akaruka hewani na kumchapa teke kali la shingoni yule diwani. Hakumpa nafasi ya kujibu mapigo wala kufanya sala yao haramu ya kupotea kimiujiza. Akaruka tena na kumchabanga ngumi kinywani, diwani akatema damu. Akayumba na kumwangukia Salome ambaye wqakati huu alishtuka na kusimama wima, akabaki kuduwaa akishuhudia wanawake wawili usiku wa giza kama ule wakipigana makonde.

    Rensho akataka kumuwahi Salome lakini diwani naye akajirusha na kumkamata miguu yote miwili Salome akatua chini kama gunia. Diowani akamrukia na kumkata kofi kali sana la mgongoni, Rensho akajikunja kwa maumivu na hapohapo akafanikiwa kuutoa mguu mmoja akaurudisha juu kisha ukatua katia sikio la yule diwani. Diwani akalegea na kumwachia yule binti….

    “Mlinionea vya kutosha shenzi zenu!!” akasema Rensho huku akiangaza ni wapi Salome yupo tena.

    Hisia hazikumpa kabisa.

    Laiti kama angejua kuwa Salome ana maandhishi yale, wala asingekawia kumtia mikononi. Lakini hakujua juu ya hilo.

    Hasira za salome kumponyoka mikoni mwake akarejea kuzimalizia kwa yule diwani. Akamkaba shingo yake kwa nguvu kisha……kisha akaikaba hirizi yake na kuichomoa kwa nguvu zote.

    Nshomile na waziri mstaafu wakatambua kuwa hali si shwariu. Homa ya jiji Rensho ameharibu tayari.

    Kila mmoja akakimbia kivyake.

    Majira ya saa tisa na nusu usiku walikuwa ndani ya kile chumba.

    Chini ulikuwepo mwili wa diwani wa kata. Alikuwa maiti tayari.

    Nshomile na waziri mstaafu, walikodoa macho tu wasiamini kile walichokuwa wanakiona!!

    KIZAAZAA!!!







    MASAA MANNE YALIYOPITA!!

    JIJINI DAR!



    NAFSI ya mama Magege mke wa waziri mkuu mstaafu hakuwa na amani kabisa. uvumilivu wake alihisi unamponza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wasiwasi ulioishi katika nafsi yake, kwa siku hii ulikuwa juu zaidi.

    “Mume wangu na huyu diwani wana ajenda gani ya siri eeeh!!” alijiuliza huku wivu ukichukua nafasi kubwa zaidi.

    Alijigalagaza kitandani lakini hakupata usingizi.

    “Yeye si ndo mume wangu…… nataka kujua ni kitu gani hicho wanachozungumza ambacho mimi sitakiwi kujua. Kama ni siasa mbona alipokuwa waziri tulikuwa tunaandamana kila sehemu?” alijiuliza tena safari hii kwa sauti huku akirusha miguu yake na kulivuruga shuka.

    Uvumilivu ukakomea pale akasimama wima na kuelekea katika chumba ambacho mumewe alikiita cha siri, kwa ajili ya kuzungumza mambo nyeti kabisa ya kisiasa ili aweze kuingia ikulu baada ya miaka minne.

    “Ikulu unataka kwenda unapanga mipango na diwani? Upuuzi huu wasinifanye mjinga mimi…na yule mzee Nshomile..macho yake yamejaa uongo uongo tu…shenzi kabisa…” aliwaza huku akipiga hatua kukielekea kile chumba.

    “Mh! Lakini akinishtukia itakuwaje doh! Watanidharau eeh!! Wivu wa uzeeni huu….. mwee!!” alijionya wakati anataka kuyumbisha mawazo yake.

    Lakini nafsi nyingine ikamshinikiza aende liwalo na liwe.

    “Wakinishtukia nazuga kuwa nilikuwa naenda stoo!!” Mama Magege akapata cha kuongopa iwapo atafumwa akiwa karibu na eneo hilo ambalo waliliita eneo la faragha kuu ya kisiasa.

    Uoga ulimuingia kadri alivyozidi kukisogelea kile chumba….awali alitegemea kusikia majibizano baina ya watatu hao walioingia katika kile chumba. Lakini ajabu ukimya ulikuwa wa kutisha sana.

    Ilikuwa yapata saa saba na dakika kadhaa za usiku.

    Hatimaye akakifikia kile chumba. Kwa kumbukumbu zake ni kuwa mle ndani hakuna godoro wala kitanda zaidi ya makochi na meza kubwa.

    Ukimya huu!! Wanafanya nini? Alijiuliza. Huku akiwa ametega sikio lake mlangoni.

    Hata kukoroma hamna? Alijiuliza.

    Pepo la wivu likasemezana naye kuwa mumewe yupo anafanya mapenzi na diwani!! Ujasiri wa kufungua mlango kisharishari kwa nia ya kufumania ukamuingia.

    Akausukuma mlango…..

    Mlango ukagoma kufunguka. Akajaribu kushusha kitasa.

    Hapo ukakubali amri, akasukuma kwa nguvu!!

    Kimya!! Hakuna mshtuko wowote.

    “Ahaa!! Wananichezea kamchezo eeh!! Kuna mlango mwingine wamejitengenezea kwa ajili ya kufanya uasherati wao. Wanapita bila mimi kujua… pumbavu!!!” alihamaki mama Magege, akaanza kusaka mlango huo wa ziada. Alihaha huku na kule bila mafanikio. Hapakuwa na tundu wala mlango wowote wa ziada.

    “Washenzi hawa wamenipitaje hawa eeh!! Magege umepita wapi wewe na wanaharamu wenzako??” alijiuliza huku akifunga kanga yake vizuri. Akatoka nje kuchungulia ni kwa namna gani wangeweza kutoka bila yeye kujua. Hakuiona hiyo namna.

    “Tutaona nani mjanja leo…..” alizidi kuhamaki na kuamua kufanya jambo ambalo baadaye liligeuka kuwa mshikemshike na mwanzo wa kufumbuka macho yake.

    Mama Magege akaamua kujificha nyuma ya nlile kochi kubwa kabisa ambalo aliamini kuwa hawezi kuonekana. Aliamua kufanya hivyo ili aweze kumuumbua mume wake.

    Akajituliza pale bila kukata tamaa aliamini fika kuwa watarejea kabla hapajapambazuka na kuzuga kuwa walikuwa katika chumba hicho kwa muda wote ule.

    Subira yavuta heri!!

    Naam! Ukafika wakati wa kupata matokeo ya subira….

    Ile subira ikaleta shubiri!!!



    Kitu kikaanguka kwa nguvu ndani ya kile chumba na kiza kikatanda ghafla.

    Mama Magege kule alipojificha akatokwa na mayowe bila kutarajia huku akijikurupua kutoka mafichoni.

    Alihaha huku na huko, hofu ikamfanya ausahau hata mlango ulipokuwa.

    Akaituliza akili yake na kujiona mpuuzi wa mawazo kutokana na alichokuwa akikifikiria.

    “Naogopa nini sasa?” alijiuliza……

    Lakini kupitia dirisha akaona mwanga nje…

    “Mbona umeme upo sasa halafu hu….” Kabla hajamalizia kauli yake chumba kikapata mwanga.

    “Au kuna shoti…” alijisemea tena na jicho lake likahama hadi sakafuni.

    “Mamaweeeeeee!!” alipiga makelele kwa sauti ya juu sana. Alikuwa anatazamana ana kwa ana na mwili uliokuwa uchi huku ukivuja damu. Mwili wa Diwani!!

    Nguvu zikamwisha mwilini!!

    Akalegea na kujikuta akiketi pembeni ya ule mwili akiwa hana la kufanya.

    Ghafla likatokea jingine kubwa!!

    Hajui kama walitoka ukutani ama walitoka darini!!

    Mume wake mpenzi na mzee wa kuitwa Rensho walitokeza ndani ya kile chumba wakiwa uchi wa mnyama!!

    Wakatazama jicho kwa jicho!!

    Mama Magege akapoteza fahamu wakati waziri mstaafu na Nshomile wakitumbua macho.

    Rensho alikuwa amezua balaa haswa!!!



    ****



    KAHAMA!



    Chumba cha hoteli wilayani Kahama, Getonga akiwa amefanikiwa kupata lepe la usingizi alishtukia akiangukiwa na kitu kizito kifuani. Akajaribu kujigalagaza huku akipiga kelele lakini akaishia kupiga kelele katika kifua chake.

    Alikuwa amezibwa mdomo!!

    Na hata amacho yalipopata ufahamu vyema alitambua kuwa alikuwa ana kwa ana na mwanamke mwenye macho mekundu na hasira kali.

    Alikuwa ni Rensho!!

    “Salome kanipotea…dakika mbili nimemuona na dakika mbili baadaye kapotea… tunafanyaje sasa… na wale wajinga wanamsaka…” alizungumza Rensho. Na wakati huo aliuachia mdomo wa Getonga.

    Getonga akashusha pumzi kwa nguvu!!

    “Sasa mbona umenivamia hivi Rensho hujui naweza kufa….”

    “Heri yako unayewaza kufa. Mimi nawaza kufufuka sasa. Nataka kurudi katika asili yangu!!” alijibu Rensho huku akikaa kitako.

    “Halafu ukiogopa unafanana na kile kitoto chako aisee!!” Rensho aliongezea huku akikaa vyema katika kitanda.

    “Yah! Tunafanana sana….” Alijikaza Getonga na kujibu.



    “Tunafanyaje juu ya kumpata Salome.” Akawa makini tena Rensho na kuuliza.

    Getonga akatulia kwa muda kisha akajibu awezavyo.

    “Ren.. mimi ninachofahamu juu ya Salome ni kwamba ni binti ambaye alikuwa safarini, akatekwa kisha kubakwa na vijana wawili kati ya watatu waliomteka. Yule kijana ambaye hakufanya huo unyama ndo alinisimulia. Walipomaliza wakamtupa katika korongo moja ili afe kama walkivyokuwa wameagizwa na mkuu wao…. Baada ya hapo sijui lolote kuhusu Salome ndugu yangu. Yaani vinginevyo mimi unanionea tu….” Alijieleza kwa huzuni kuu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mh! Huu ni utata mkuu na ni hatari kwangu na hatari kwako. Wewe usiseme nakuonea wakati umefanya njama ukachukua kitambulisho changu…. Ok! Tunatakiwa kuangalia namna ya kuiepuka hii hatari, kwangu mimi si tatizo kurudi kuwa mtumishi wao lakini wewe watakuua na familia yako yote…..” alikoma kidogo na kuutazama uso wa Getonga jinsi ulivyotaharuki.

    “Tunatakiwa kushirikia katika kumbukumbu hizi walau tujue jambo moja ama mawili juu ya Salome. Tukishayajua hayo tu basi huu mchezo tunaumaliza mara moja kinabaki kitambulisho tu…. Tena tunatakiwa kuwa makini kabla yule bwege wa kuitwa Nshomile hajampata Salome. Yaani akimpata tu, jiandae kufa kikatili kwa kuchommwa moto kiungo kimoja baada ya kingine…aisee majamaa yanaua vibaya yale kaka yangu. Yaani yanakata mkono yanauchoma, yanakata kamguu yanachoma…” Rensho akamaliza kwa kucheka cheko la kupendeza, wakati Getonga alikuwa ametumbua macho yake kwa hofu kuu.

    “He! Unakodoa mimacho…nd’o hivyo wanavyokuua……” akamnaga, kisha akabadilika tena, “Ok! Kaka, usiku huu tunatakiwa kufanya jambo….unatakiwa uni’busti’”

    “Ku’busti’ nd’o nini jamani…” aliuliza kinyonge.

    “Unibusti nikumbuke walau mambo kadhaa juu ya huyo Salome….”

    “How..”

    “Umesema?” Rensho akahoji….alikuwa hajaelewa lugha iliyotumika.

    “Aaah! Namaanisha kiaje sasa.”

    “Kirahisi tu na vigumu vilevile…..” akavuta pumzi kidogo kisha akalalamika kuwa anahisi njaa, kisha akaendelea “Unatakiwa kufanya mapenzi na mimi……” akasita tena na kumtazama Getonga usoni.

    “Usishtuke kusikia mapenzi, lakini unatakiwa kuwa makini nikupe maewlekezo. Wakati unafanya mapenzi na mimi sharti ni moja tu, hakikisha unanisikiliza nitakachokuwa nasema na ukinukuu..huo nd’o utakuwa mwanga wetu, hivyo hutakiwi kunifanya kama mkeo ama hawara yako yoyote yule, na kujikuta ukipoteza akili yako yote usijue ni nimezungumza nini…..” Rensho akashusha pumzi na kuweka kituo akimsubiri Getonga aseme lolote.

    Getonga alikuwa amepagawa kiakili, akaikumbuka ndoto ya Maria kuwa anaota mtu anatokwa damu, akakikumbuka kifo cha Inspekta Kisembe kufa huku akivuja damu baada ya kutoka nyumbani kwa Maria, kifo cha Sam nacho kikamchanganya, Don na Dulla walikufa kwa kuvuja damu…bila shaka baada ya kutoka kufanya ngono. Sasa anaambiwa ashiriki katika ngono na mtu huyu.

    Hofu, uoga na kila aina ya mawazo ikamtawala kijana huyu mwandishi maarufu anayesakwa jinni Dar kwa kosa la kutoroka rumande alipokuwa akikabiliwa na kesi nzito ya kushirikiana na majambazi huku gari yake ikikutwa na silaha za kivita.

    “Aah! Rensho mbona sasa hiyo ngumu jamani..”

    “Ok! Basi nadhani ni rahisi kufa kile kifo nilichokwambia…..usiku mwema mi nalala.” Rensho akajibu kwa jazba kisha akageukia upande mwingine.

    Nimeyakoroga!! Alijisemea Getonga huku akijiuliza lipi ni sahihi.

    Kubembeleza!! Ni hili aliliona sahihi zaidi. Akaingia katika zoezi hilo.

    “Ren, nahisi hujanielewa tu, unajua kabisa sitaki kufa na sitaki kushuhudia familia yangu ikifa namna hii. Nilichokuwa nataka ni walau kuuliza maswali mawili matatu, halafu ukinijibu tu tunafanya utakavyo kwa manufaa yetu!!” alizungumza kwa sauti iliyojaa ushawishi.

    “Hapo sasa umenena…. Neno moja lenye maana. Haya uliza?”

    “Ni madhara gani nitayapata nikikosea masharti.”

    “Utakufa kwa kuvuja damu!!” Rensho alijibu kama suala la kawaida kabisa. kisha akamalizia “kisha nami nitapata ujauzito usiokuwa na kikomo utanitesa hadi nitakaposalimu amri… kitu cha msingi kuwa makini…na kwanini ujiandikie kukosea wakati nimeshakueleza??”

    Getonga alikuna kichwa, maji alikuwa ameyavulia nguo tayari hakuwa na haja ya kuyaogopa. Aidha yawe machafu ama masafi ni lazima ayaoge tu.

    Kichwani mwake kilichomchanganya ni ule uzuri wa Rensho.

    Je? Ataweza kujiongoza akili yake, ule uhondo na kusikia maneno atakayosema.

    Kitanzi kilikuwa katika kichwa chake na chaguo pia lilikuwa ni lake!! Aidha kujiua ama kukitengua kitanzi kile.

    Mtihani mkubwa sana!!!

    Wakati anawaza haya, Rensho alizitoa nguo zake zote na kulala chali kitandani,.

    Ebwana wee!! Matiti kifuani hayakujua nini maana ya kulala tangu yasimame yalikuwa vilevile, rangi yake ya chungwa iliyafanya na yaonekane kama chungwa lakini katika mfano wa embe dodo, kile kiuno kilikuwa mahali pake na kilibeba lile tumbo dogo la Rensho katika namna ya kipekee huku mapaja ya wastani yakishangilia hali ile. Chini ya magoti alikuwa na michirizi fulani kama iliyoleta ukijani ukichunguza kwa mbali. Michirizi ya huba.

    Getonga akaupandisha uso na kuufikia uso wa Rensho, akakuta binti yule akiwa amefumba macho na kutoa tabasamu mwanana.

    Maungo katika nguo ya Getonga yakaanza fujo, akaanza kusahau kama walichotaka kufanya kilikuwa ni tiba.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akatamanika kingono.

    Akaupeleka mkono na kumpapasa, ule ulaini wa ngozi ambayo hakuwahi kuiona ikipakwa mafuta ukamsaatajabisha!!

    Rensho alikuwa na kila kitu kinachomfanya aweze kuitwa mrembo.

    “Hata mama Eva hapa haingii ndani!!” Getonga alikiri huku unafiki akiweka kando…..



    **GETONGA katika mtihani…. Anatakiwa kum’busti’ RENSHO…..

    Akikosea masharti tu… wamekwisha!!!!



    ITAENDELEA…



0 comments:

Post a Comment

Blog