Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

HOFU - 3

 





    Simulizi : Hofu

    Sehemu Ya Tatu (3)





    “Hebu ngoja umesema ni redio Tumaini ndo wametangaza… ngoja hebu..” Getonga akachukua simu yake na kumpigia rafiki yake aliyekuwa anafanya kazi katika kituo hicho cha redio. Akamuuliza juu ya ukweli wa habari hiyo.

    “Taarifa imeletwa na muhudumu wa hoteli fulani hivi na kisha kuthibitishwa na polisi juu ya tukio hilo. Maajabu zaidi aliingia na mwanamke lakini amekutwa akiwa peke yake. Ni balaa kaka..” alijieleza wakati huo simu ikiwa katika spika za nje. Wakisikiliza wote wawili.

    “Wamekuta kitambulisho cha mwanamke huyo ambaye sasa ndo anatafutwa… anaitwa Maria Paul…”

    “Whaat!!!” akashtuka Getonga.

    “Unamfahamu ama?” Anitha akauliza.

    “Ahhmm! Jina sio geni hilo….” Akajibu kwa hofu Getonga.

    Wivu!! Wivu ukajitundika katika moyo wa Anitha. Akaondoka bila kuaga, amani ikatoweka tena!!



    Halafu akarejea ghafla akiwa ameukunja uso wake haswa!!

    “Jana uliondoka na gari na umerudi bila kuwa nalo.. umeliacha wapi G… eeh.. umeacha wapi gari?” Anitha akahoji huku akiwa ameshika kiuno. Macho yake makali yasiyokuwa na chembe yoyote ya mzaha yakiwa yanatazama uso wa Getonga unavyopigwa butwaa baada ya kusikia swali lile ambalo hakulitarajia.

    Mungu wangu wee!! Akasimama na kushika kichwa chake. Anitha akayahamisha macho yake kumfuata Getonga. Kisha akasonya na kuendeleza malalamiko.

    “Baba Eva…. Gari umemwachia nani yako leo… nangoja jibu”

    “Yaani huwezi amini…”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Siwezi amini kuwa umelisahau kwa hawara wako mpya…” Anitha akamalizia kauli.

    “Mama Eva… ni nini hicho sasa unaleta hapa….”

    “Sikuelewi hata kidogo, jana umechelewa kurudi usiku, sikulalamika, umenikumbatia unanukia marashi ya kike mi nakutazama tu… sasa na gari halipo… baba Eva ni nini hiki…ni nini lakini?” anitha akashindwa kuendelea kulalamika akaanza kulia kwa kusina akiwa amejiinamia kwenye kochi.

    Nafsi ikamsuta Getonga akakumbuka kuwa alikuwa jirani sana na Maria usiku uliopita na pia wakati maluweluwe ya Eva kujitokeza Maria alimkumbatia kwa nguvu. Bila shaka nd’o wakati aliomuachia marashi.

    Je ajishushe na kuanza kuelezea mkasa juu ya Maria? Ili aweze kuelezea juu ya kusahau gari lake likioshwa mahali!! Lakini kwa kusema yote haya bila shaka atalazimika kusema juu ya Eva kuonekana na kisha kutoweka na kama hii haitoshi lazima autaje mkasa wa Kindo na mama yake kuuwawa kinyama.

    Eva hatanielewa hata kidogo!! Getonga alisalimu amri kimya kimya.

    Akapiga hatua kadhaa na kumfikia Anitha kisha akamshika bega, ghafla Anitha akakipangua kiganja chake na kukitupilia mbali.

    “Nenda ukawashike hawara zako ambao unawahonga magari….. ndio hao unaowahonga magari nenda ukawashike…. Gerlad Getonga… wanaume wanaumee… pete ya ndoa kidoleni unaenda kwa mahawara, unawahonga na…”

    “Stooop Anitha!! Nyamaza…. Hujui usemalo. Eva ametoweka tunatakiwa kujiandaa na kwenda kutafuta ufumbuzi huu sio muda wa kugombana….”

    “Niache nizungumze mume wangu, Eva alipotea ukiwa na hawara zako, kupotea kwake ni pigo kwa ajili ya usaliti wako… oooh Eva mwanangu weee… Eva weeee..” akashindwa kuendelea na kuanza kuangua kilio. Getonga akamkabili na kuanza kumbembeleza.

    “Gari lipo car wash… nililiacha huko… tunaongozana wote tunalichukua na kisha tunaenda polisi. Sina hawara mke wangu!! Nakupenda.” Getonga akajitetea. Anitha akamkumbatia kwa nguvu huku akishusha maneno kadhaa ya kumsihi Getonga asimsaliti.





    ****



    HABARI mbili zikazidi kukichanganya kichwa cha Getonga. Akashindwa aanze na lipi kwanza na lipi lifuate baada ya.

    Anitha alikuwa amegeuka mbogo, hakutaka kushaurika na upuuzi kuwa gari lilikuwa linaoshwa likasahaulika na kisha kupotea hazikumwingia akilini hata kidogo. Akapigia mstari majibu yake ya awali kuwa mumewe amelitoa lile gari kwa ajili ya hawara wake. Getonga alijaribu kusihi lakini hakusikilizwa tena, Anitha akapanda taksi na kutoweka.

    Getonga akabaki kuduwaa huku akilikumbuka vyema tukio la kuacha gari likioshwa kisha akaenda katika chumba cha Maria ambapo hakumkuta. Baada ya pale akafanya safari ya kwenda kwa mama yake Kindo ambapo mabalaa rasmi yalianzia.

    Gari aliloliacha likioshwa halikuwepo tena na mkewe hataki kusikia habari hiyo.

    Habari ya pili ilikuwa juu ya kifo cha Sam, kifo cha aina ileile ya kuvuja damu. Hili lilimvuruga kabisa Getonga na kuona mipango yake yote ikienda mlama. Akafikiria kwenda kutoa taarifa polisi juu ya gari lake kuibiwa katika mazingira yale ya kuoshwa, lakini akaamini kuwa polisi wanaweza kumpotezea muda zaidi bila kujali mwanaye wa pekee Eva yu katika mikono ya watu wabaya.

    Asa aanzie wapi? Hilo likawa swali zito zaidi.

    Akataka kwenda mahali ambapo tukio la kifo cha Sam limetokea, lakini akasita baada ya kutembea hatua kadhaa, akakumbuka jambo la muhimu zaidi kwa muda ule.

    Wanawake? Wanawake na wivu wao!!! Kengere ya hatari ikalia katika kichwa chake. Akamuwaza Anitha na kuhisi kuwa anaweza kufikia hatua mbaya ya kujiua kutokana na hisia zake potofu!!

    Upesi akapanda taksi na kuamuru apelekwe maeneo ya nyumbani kwake kwa mwendo mkali kabisa. Dereva akabuni njia zake za panya na safari ikaanza!!

    Baada ya dakika thelathini Getonga alikuwa anatelemka garini baada ya kuwa amelipa pesa iliyotakiwa.

    Kichwani mwake alikuwa amepitisha maamuzi ya kumweleza Anitha kila kitu juu ya mauzauza yanayoendelea, aliamua hivi kwa kuamini kabisa Anitha angeweza kuathirika kisaikolojia iwapo hali itaendelea kuwa vilevile.

    Nyumba ilikuwa tulivu sana, na milango ilikuwa imefungwa kwa ndani.

    Wanawake!! Sasa hapa hataki niingie ama? Akajiuliza huku akiangaza huku na kule namna ya ziada ya kuweza kuingia ndani.

    Hapakuwa na namna!!

    “Anitha… Anitha mama yangu…..” alianza kusihi Getonga huku akijaribu kuchungulia huku na kule bila mafanikio ya kumwona mkewe. Akazunguka upande wa jikoni, akachungulia hakuona kitu, akazunguka upande wa stoo, bado hakuona kitu, bado aliendelea kuita kwa bidii huku akiomba msamaha, moyo wake ulishatawaliwa na hofu juu ya mkewe kujiua. Jambo ambalo aliliwaza awali na kisha kuchukua maamuzi ya kurejea nyumbani.

    “Bwana Gerlad Getonga!!” sauti nzito ilimshtua kutoka upande wake wa kushoto. Akageuka upesi akiwa ametaharuki akakutana na sura ya mwenyekiti wa mtaa.

    “Mzee Magesa, kuna taarifa zozote juu ya mwanangu.” Akamuuliza huku akijua kabisa hapakuwa na uwezekano wa mwanaye kupatikana kwa njia za kipolisi ama kipelelezi.

    “Hapana Getonga, na si hilo lililonileta hapa. Nimejaribu kupiga simu yako haikupatikana na namba ya mkeo haipokelewi sijui kwanini..”

    “Kuna tatizo gani mkuu….”

    “Mkeo alipiga kelele za kutisha sana huku akiwa amejifungia ndani ya nyumba, hakijulikani ni nini kinaendelea…nimepewa taarifa na jirani yenu nami nikajaribu kuwasiliana nawe bila mafanikio..” sauti nzito iliendelea kuporomoka.

    Kengere ya hatari ikalia kwa mara nyingine tena katika kichwa cha Getonga. Akaondoka bila kuaga hadi katika dirisha linaloelekeza chumbani kwake na mkewe. Alijaribu kuchungulia pasi na mafanikio, pazia zito lilikuwa limeziba kabisa. Alitapatapa huku na kule bila mafanikio, na mwisho wakakubaliana kuuvunja mlango.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwenyekiti akisikiliza uamuzi wa Getonga akawaruhusu vijana waliokuwa wanashirikiana katika kutafuta namna ya kuingia ndani ya nyumba ile kuuvunja mlango.

    Zoezi likamalizika, mbiombio Getonga akiwa anahema juu juu na hofu ikiishi katika damu yake akamsaka mkewe huku na kule.

    Hatimaye akakifikia chumba chao!! Akausukuma mlango, ukafunguka kidogo sana kisha ukawa mzito kama kwamba kuna kitu kimewekwa maksudi kiweze kuuzuia, akaendelea kuusukuma ukawa unasogea kidogo kidogo. Waliposhirikiana wakaufungua.

    Getonga akaingia ndani, kitu cha kwanza akatazama upande wa kushoto aweze kujua ni kitu gani kilichokuwa kinauzuia mlango usifunguke.

    Macho yakaongezeka ukubwa ghafla, kiganja kikawahi kuuziba mdomo usipige kelele.

    Ushuhuda wa ajabu, pua ya mkewe ilikuwa imepasuka vibaya na damu zilikuwa zimetapakaa katika marumaru pale chumbani.

    Mikono ilikuwa imesambaa kushoto na kulia, mguu mmoja ukiwa na kiatu na mwingine ukiwa peku.

    Amekuwaje huyu jamani eeeh!! Getonga alianza kulalamika peke yake.

    “Gerlad Getonga…” sauti nzito ya mwenyekiti wa mtaa ilimuita. Akageuka kumtazama, lakini sauti nzito hakuwa na habari naye bali macho yake yalikuwa yamekodoa kutazama kitanda cha Getonga.,

    Getonga akajisogeza kwa kusuasua hadi akakifikia kitanda.

    Hapa uvumilivu haukuwepo tena kwa alichokiona, alipiga kelele moja kisha akalainika na kudondoka chini. Ile pua iliyovunjika ya mkewe haikuwa inatisha kama hali iliyokuwa pale kitandani.

    Akajikongoja na kuinuka tena, kwa kutumia magoti akajivutavuta hadi akakifikia kitanda, akazidi kutumbua macho yake katika kitanda chake kilichovikwa shuka jeupe.

    Kipande cha gauni kilikuwa kimefunuliwa na kilikuwa kimebeba vitu vya kutisha na kuduwaza huku vikileta mateso ya nafsi. Pembeni yake kulikuwa na karatasi.

    “Eva…..Eva….” akaanza kuita huku akitetemeka, mwenyekiti wake hakuwa amepata la kusema bali kuungana na Getonga katika mshangao ule.

    Getonga, akanyoosha mkono wake uliokuwa unatetemeka ili aweze kushika kile kilichokuwa katika kipande kidogo cha gauni ili aweze kujihakikishia kabisa kama hofu yake ni sahihi ama la!!

    Naam!! Hayakuwa mauzauza bali hali halisi kabisa, vidole viwili vilivyokuwa vimetapakaza damu katika kile kipande cha gauni vilikuwa vya mtoto wake wa pekee. Eva!

    Kama mtoto mdogo, Getonga alianza kuomboleza kwa sauti ya juu huku akijirusha huku na kule. Mwenyekiti akasaidiana na majirani kumdhibiti Getonga asije akajidhuru.

    Na wakati huo simu ilikuwa imepigwa polisi tayari.

    Getonga akajilaumu kwa kusita kumweleza mkewe ukweli juu ya kilichotokea usiku wa siku iliyopita, sasa mambo yanazidi kuongezeka na stori inazidi kuwa ndefu ya kuelezea…..

    Getonga akajikuta kwa wakati mmoja akipoteza vitu vingi; mtoto wake, amani, uaminifu kwa mkewe na kubwa zaidi akajikuta amenunua hofu bila kulazimishwa!!



    Polisi walifika baada ya muda mfupi kutoka katika kituo kilichokuwa jirani. Anitha akakatiwa PF3 na kukimbizwa hospitali upesi, Getonga akaandamana na msafara ule. Polisi wakaimarisha ulinzi pale chumbani pasipo kugusa kitu chochote kile.



    ***



    “Gerlad Getonga, kuna mtu yeyote anakudai kaka, ama umekosana naye siku za karibuni?” mwenyekiti alimuuliza wakati wakiwa nje ya hospitali wakisubiri muda wa kwenda kusalimia wagonjwa.

    “Hapana, sina madeni na sijagombana na mtu….kwani nini?” alijibu na kupandishia swali jingine huku akionekana kuvutiwa na swali lile.

    “Getonga wewe ni rafiki yangu sana ujue…siwezi kusikia jambo nisikueleze. Umeniunga mkono sana wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, nakumbuka kila kitu….” Akasita kidogo akakohoa kulainisha koo kisha akaendelea, “Kwa tetesi ni kwamba yale maandishi yaliyoachwa kitandani yalikuwa yameandikwa kwa lugha ya kiarabu, na kwa wale wanaoielewa lugha wanadai kuwa yale maneno kwa Kiswahili ni “UNANICHELEWESHEA”…..sasa ni kitu gani unamcheleweshea huyu shetwain hadi afanye unyama ule… eeh!” alimaliza mwenyekiti.

    Getonga akashusha pumzi kwa nguvu, akajishika kiuno.

    “Hawa watu wa hivi ni wabaya sana anaweza kufanya mambo mabaya zaidi kwa mtoto wako… kama lipo ambalo hujawatimizia tafadhali bwana we fanya kutimiza….usibishane nao we wape.” Mwenyekiti alizidi kutilia mkazo kauli yake.







    ASUBUHI waliyooingoja kwa ajili ya Anitha kuruhusiwa kutoka hospitali haikukucha vyema, wakati Getonga akijipa matumaini kuwa atazungumza na mkewe kinagaubaga hadi amuelewe na kisha wawe kitu kimoja waungane katika kumsaka Eva. Kuna kundi la watu wanne lilikuwa linamsaka kwa udi na uvumba kwa ajili ya mahojiano, baada ya kumkosa nyumbani kwake walipata taarifa kuwa anaweza kuwa yu hospitali ambapo mkewe alikuwa anapata matibabu.

    Wakaandamana kuelekea maeneo hayo ya hospitali!!



    Mwenyekiti wa mtaa alikuwa amesinzia lakini Getonga angali macho akitafakari juu ya kipindi hicho kigumu cha mpito anachopitia. Taswira ikanasa katika vidole viwili kutoka katika mkono wa mwanaye, akauma meno kwa hasira huku akijipiga piga miguu yake sakafuni.

    Nani huyu anayenifuatilia lakini kwa mara nyingine? Alijiuliza asiwepo hata mtu mmoja wa kumjibu.

    Mara simu yake ya mkononi ikaanza kuita, kwa sababu alikuwa amezima sauti basi ilitoa mwanga pekee kumpa taarifa hiyo. Akaitazama na kugundua ilikuwa namba mpya.

    Wanataka kunipa pole hawa!! Aliwaza kisha akairejesha mfukoni bila kuipokea.

    “Gerlad Getonga…….” Sauti laini ya kike ilimuita, akageuka upesi akakutana na watu wanne wakiwa wamemnzunguka.

    “Uumh! Naam…” akaitika.

    “Upo chini ya ulinzi na unahitajika kituo cha polisi Chang’ombe muda huu…” sauti ya kiume ikaamuru.

    Sauti hii ikamtoa mwenyekiti katika usingizi, akayapikicha macho yake kisha akapiga mwayo.

    “Kuna nini hapa…” akauliza. Getonga hakuwa na la kujibu, hata wale viumbe wanne ambao walitambulika kuwa maaskari na wao hawakuwa na la kumjibu.

    Mmoja akachomoa pingu na kuikamata mikono ya Getonga ambaye alijaribu kuikwepesha na hapo akajihalalisha kupokea kofi zito mgongoni. Hata kabla maumivu hayajamwisha tayri mikono yake ilikuwa imeunganishwa katika pingu.

    “Kituo cha polisi Chang’ombe…. Unaweza kufika kesho maana kwa muda huu hauna la kusaidia..” polisi wa kike akamwonya mwenyekiti wa mtaa ambaye alitaka kuandamana na Getonga ajue kulikoni.



    ****



    Bunduki? Mauaji? Ujambazi?.... haya yalikuwa maswali yaliyokisumbua kichwa cha Getonga wakati yupo nyuma ya vyuma vya selo. Katika makosa makubwa aliyowahi kufanya maishani mwake basi hili alilolifanya lilikuwa kubwa lakini la kizembe kupita yote aliyowahi kufanya.

    Uzembe katika kutoa taarifa!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alitambua fika kuwa gari lake limetoweka katika mazingira ya kutatanisha, hakuna mtu yeyote aliyetambua wapi lilipo. Lakini bado hakutoa taarifa polisi. Hadi polisi wamekuja kumkamata kwa kesi mbaya ya kukutwa na bunduki katika gari lake ambalo limefanya ujambazi huku roho nne za wananchi wasiokuwa na hatia zikipotea.

    Kwa sababu gari ni lake na leseni pamoja na kadi vimelithibitisha hilo basi aidha muuaji ni yeye ama anawafahamu walioua!!



    ASUBUHI majira ya saa nne mpelelezi wa kesi iliyomuhusu Getonga tayari alikuwa amewasili. Getonga akatolewa kwa ajili ya kuchukuliwa maelezo, kila swali aliloulizwa aliliona kama jipya sana kwake.

    Umiliki wa bunduki?

    Kushirikiana na majambazi?

    Alichoweza kujibu ni kwamba mara ya mwisho kulitumia gari lake ni pale ambapo alilipeleka kituo cha kuosha magari. Zaidi ya hapo hakulitumia tena. Mpelelezi akamrudisha mahabusu huku akimwonya kuwa kama hatakuwa mkweli basi hukumu yake itakuwa mbaya sana.

    Getonga akabaki katika kustaajabu, Eva, Anitha na sasa yeye muhimili mkuu wa familia yu matatani na hana namna ya kujinasua.



    MAJIRA ya saa mbili usiku baada ya mahabusu kuhesabiwa Getonga alijibanza katika kona moja ya chumba kile. Alikuwa mtulivu kabisa akijaribu kushtuka kutoka usingizini huenda alikuwa katika ndoto mbaya, lakini kila alivyoyafumbua macho alijikuta yupo rumande.

    Akatoa tabasamu la karaha!!

    Milango ikafunguliwa kisha matusi ya hapa na pale kutoka kwa maaskari yakamsindikiza mtuhumiwa mwingine mgeni katika rumande ile. Mahabusu wazoefu wakaanza kumsumbua na kumzongazonga hapa na pale, wengine wakimwomba sigara wengine wqakitaka awape pesa na wakorofi zaidi walimlazimisha aende kulala jirani na choo.

    Getonga aliyatazama yote haya katika mwanga hafifu!! Akangoja majibu ya yule mtu anayesumbuliwa lakini la! Hakujibu lolote. Akajipenyeza hapa na pale ili apate mahali sahihi pa kuketi.

    “Unaenda wapi wewe? Nimesema utalala chooni huko?” alikoroma mahabusu mbabe. Yule mtu mgeni hakuyajali maneno yake, akazidi kujipenyeza tu bila kujali lolote.

    “Unanikanyaga we bwege…” akabwatuka mwingine, bado yule bwana hakujali na hata hakuomba radhi.

    Hakusema neno lolote lile. Getonga naye akawa anamshangaa sasa!

    “Nyie mnamchelewesha naona, mapombe yake anakuja kutusumbua sisi….” Mtuhumiwa mwingine akayasema haya huku akiruka hatua kadhaa kisha akamgusa yule mgeni begani. Na hapo hapo akamfyatua teke kiunoni.

    Yule bwana akajikunja kwa maumivu watuhumiwa wengine wakashangilia. Na hapo akageuka upesi akarusha mkono wake ngumi ikampata yule mbabe usoni, akapepesuka na kuanguka chini huku akigumia kwa maumivu.

    Miguno ikasikika kutoka kwa watuhumiwa!! Yule bwana hakujali, hatimaye akaketi pembezoni mwa Getonga ambaye naye alikuwa anamuhofia huyo bwana asiyesema neno lolote lile. Ni kama alikuwa hasikii na pia hana uwezo wa kuongea.

    “Bro….” Getonga alijaribu kumwita yule mgeni baada ya kuwa ameukalia mkono wake kwa muda mrefu bila kujua na sasa ganzi ilikuwa inamshika.

    Mgeni hakugeuka!!

    Getonga akajaribu kujitoa kwa nguvu ndipo yule bwana akajitikisa kidogo, Getonga kwa sababu alikuwa ametumia nguvu kujitoa basi kile kitendo cha kuachiwa akajikuta akimpiga kichwa mwenzake wa pembeni ambaye alitaka kumwijia juu kisharishari kabla mgeni hajamnasa kofi zito katika paji la uso na kumwacha akibung’aa badala ya kuugulia maumivu.

    “Oya wanakuja…wanakuja mwana!!” kwa mara ya kwanza yule mgeni akaanza kuzungumza huku akiwaaminisha watu wote mle ndani kuwa makini na kile anachokisema.

    “Mnasikia…hao wamekaribia hao hapo…” alizidi kusihi!!

    Watuhumiwa wengine waliokuwa mahabusu wakabaki kumshangaa yule bwana ambaye sura yake haikuwa inaonekana kutokana na giza.

    Alipoona hakuna anayemuelewa aliruka hovyo hovyo huku akiwakanyaga wenzake akakimbilia katika matundu ya milango ya chuma ambayo ikifunguliwa basi mtuhumiwa anaweza kutoka nje, mlango huu upo jirani na mapokezi.

    “Afandee…nyie maafande acheni kulala, anaku….wanakuja hao…eeeh!! Wanakuja….” Alipiga makelele hovyohovyo na alikuwa kama anayetaka aeleweke.

    “We bwege ulijifanya hujui kuongea sasa unapiga makelele huko eeeh!! Kesho utanieleza fala wewe…” afande alifoka baada ya kugundua kuwa mtu ambaye aligoma kutaja majina yake baada ya kukamatwa akizurura usiku akiwa na panga sasa anazungumza.

    “Afande….wanakuja niamini mimi….” Akasihi yule bwana huku sauti yake ikiwa kama anayetaka kulia.

    Alipomaliza kauli hii kila mmoja aliweza kuusikia upepo ulioanza kuvuma.

    “We fala unaita mvua eeeh!!” afande akabwatuka bila kufanya jitihada zozote za kuyafanyia kazi maneno ya kijana yule mahabusu.

    Upepo huu ukamshtua Getonga, aliwahi kuushuhudia mahali. Siku ambayo Eva anajitokeza na kisha kupotea, pia siku ambayo mama yake Kindo aliuwawa.

    Getonga akasimama upesi aweze kwenda kumwona huyo mtu anayelalamika ni nani…..

    Akaruka hovyohovyo na yeye.

    Ana kwa ana wakagonganisha macho na Kindo!!

    “Wamefika tayari…. Na we hutaki kuwapa vitu vyao ona sasa…ona…..” alilalamika Kindo. Getonga akabaki kuduwaa!!

    Mara likafuata tukio jingine la kustaajabisha!!

    Mapokezi zikaanza kusikika kelele zisizo na kifani, vishindo vikubwa vikubwa vya mianguko ya kabati navyo vikasheheni.

    Watuhumiwa wote kila mmoja alikuwa anang’ang’ania kuwa palke mlangoni ili aweze kuona nini kinatokea. Lakini ghafla wote wakauogopa ule mlango na kuanza kukimbia huku na kule baada ya mkono wa mwanadamu kupenya pale mlangoni huku ukiwa unavuja damu. Kisha mwili wa askari ukajibamiza pale mlangoni ukatoka na kurudi tena kwa kasi huku ukizidi kupondeka pondeka.

    Ilikuwa ni kama kuna mtu alikuwa anambamiza pale lakini ajabu mtu huyo hakuonekana!!

    Taharuki ikatanda kila kona, Getonga akamvaa Kindo na kumhoji ni kitu gani kinatokea.

    Kindo akarejea kuwa Kindo yuleyule asiyeweza kusema maneno mengi zaidi akaendelea kujiongelea akisema.

    “Rensho…Rensho!!”

    Kila swali liloulizwa alijibu Rensho!!

    Hakuwa mkorofi tena, hakuwa msemaji tena!!

    Utata!!



    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    MWENYEKITI wa mtaa hakutaka kumshtua Anitha kwa kumpa taarifa juu ya Getonga kushikiliwa na polisi kwa makosa makubwa makubwa likiwemo la mauaji. Alitulia tuli akimweleza kuwa Getonga yu katika harakati za kumsaka mtoto wao, Anitha aliyekuwa mnyonge muda wote alikubaliana na yule mwenyekiti kuwa alitakiwa kutulia nyumbani ale vizuri sana ili mwisho aweze kurejea katika afya yake murua.

    Kitu kikubwa alichofanya mwenyekiti ni kumpa Anitha binti yake mkubwa ili aweze kuishi naye kwa kipindi hicho alichotakiwa kuwa chini ya uangalizi. Alifanya hivi ili kumweka mbali Anitha na maneno ya majirani ambayo yanaweza kumsababisha akaipoteza amani tena.

    Anitha alikuwa mtu wa simanzi muda wote, hakumuwaza Getonga bali Eva mwanaye. Kila alipovikumbuka vile vidole viwili alijikuta akiangua kilio huku Bertha binti wa mwenyekiti wa mtaa akifanya jitihada za kumbembeleza.



    Siku ya pili baada ya kutoka hospitali, Bertha akiwa jikoni anapika na yeye akiwa sebuleni anatazama filamu alipata ugeni wa ghafla.

    Mgeni mwanamke ambaye hakukumbuka kuwa ni ustaarabu kubisha hodi kabla ya kuingia ndani. Yeye akaingia bila hodi!!

    Tabasamu tele mdomoni mwake!

    Hakusalimia, akaketi!!

    Hawara wake Getonga!! Anitha akawaza kisha akauficha uso wake usionekane kuwa katika hasira.

    “Kuna mzigo wangu mumeo alikuachia hapa…maana mi hata si mkaaji nataka kuondoka zangu…” aliuliza binti yule huku akiukunja mguu wake na kuacha mapaja meupe nje. Anitha akajihisi hasira, akatamani kutukana lakini akasita.

    “Hee dada kwani we bubu ama?”

    “Sijaelewa swali lako ujue…” Anitha akaweza kujiongoza akili yake akauliza kwa utaratibu.

    “Mume wako…Gerlad Getonga amekuachia mzigo wangu kabla hajaenda huko polisi?”

    “Sijaonana naye na hakuniambia kama kuna mgeni atakuja hapa…” akajibu Anitha. Yule mgeni akaanza kucheka kwa sauti ya chini, vishimo katika mashavu yake vikaonekana, na mzigo wa matiti kifuani mwake ukawa unarukaruka wakati anacheka. Anitha akajisahau kuwqa alikuwa amekereka macho yake yakaitazama shingo ya yule dada, akayatamani madini aghali aliyovaa shingoni.

    “Mna visa kweli, yaani mumeo bwana daah!! Kwa hiyo hamshirikishani madeni yenu eeh!!”

    “Dada sikuelewi kabisa, mambo ya mimi kushirikishana naye ama kutoshirikishana naye wewe yanakuhusu nini..nimesema hakuna mzigo wowote alioacha hapa…” akajibu kwa ukali.

    Yule dada akashtuka kisha akasimama wima na yeye akiwa amechukia. Midomo ikimtetemeka!!

    “Pete si umeona haina umuhimu eeeh!!” akasema, huku akimtazama anitha. Anitha naye akajitazama kidoleni.

    Maajabu!! Hakuwa na pete kweli, akaduwaa.

    “Kama pete haina umuhimu, nitachukua na hicho kidole chake ndo utajua umuhimu wake nyau wewe!!” alifoka huku sura yake ikiwa nyekundu kwa hasira.

    Anitha akaanza kutetemeka huku macho yakiwa yamemtoka pima!!

    “Akija mwambie Rebeca wa Nshomile alikuja kufuata mambo zake….” Akatoa kauli hiyo huku akitoka nje na kuubamiza mlango kwa nguvu mno.

    Anitha akapiga mayowe, Bertha akakurupuka kutoka jikoni mbiombio mpaka sebuleni. Akamkuta Anitha akiwa katika taharuki kali.







    “Wifi…… kuna nini eeeh!!” Bertha alimuuliza huku akiangaza huku na huko huenda kuna kitu ambacho kinamtisha Anitha, na kama kipo na yeye aweze kujihadhari mapema.

    Hakuna chochote alichofanikiwa kukiona!!!

    “Atanikata kidole….atanikata kidole…amechukua pete…” alibwatuka Anitha huku hofu ikizidi kutanda na Bertha asielewe ni kitu gani kinachozungumziwa.

    “Nani eeh!! Nani…”

    “Mwanamke…Rebeka anaitwa Rebeka…”

    “Rebeca gani? Tuliza akili yako tulia kabisa hakuna kitu kama hicho lakini….” Akasita Bertha huku macho yake yakikitazama kidole kisichokuwa na pete kidoleni.

    Imeenda wapi sasa? Akajiuliza….

    “Amechukua Rebeca ….amechukua..”

    “Ni nani yako huyo Rebeca?”

    “Simjui na sijui alichukua muda gani….” Anitha aliendelea kujibu huku akitetemeka waziwazi.



    ****



    KIINI MACHO CHA AJABU!!



    ASKARI waliokuwa lindoni nd’o walikuwa wa kwanza kugundua hali hii ya sintofahamu. Hapakuwa na mtu yeyote mapokezi na makaratasi yalikuwa shaghalabaghala, jambo ambalo si la kawaida hata kidogo taarifa ya dharula ikatolewa upesi. Namba za maaskari wawili waliokuwa mapokezi zikatajwa na mara moja ukaanza msako usiokuwa na mafanikio ya haraka.

    Ulinzi wa dharula ukawekwa kwa umakini kabisa kabla selo hazijakaguliwa na kukutwa zikiwa salama kabisa bila purukushani yoyote ile ambayo ingeweza kuleta mashaka kuwa kuna mahabusu aliyejaribu kutoroka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Makaratasi yaliyosambaa huku na kule yalikusanywa pamoja na daftari kubwa kabisa ambalo ni maalumu kwa ajili ya kuandikishia orodha ya mahabusu wanaoingia kila siku.

    Wakati upelelezi wa kipi kilichotokea pale ukiendelea C.I.D mpelelezi Gasto aligundua jambo jingine. Ilikuwa baada ya kuhitaji kuendelea kuchukua maelezo kutoka kwa mtuhumiwa wa mauaji na ujambazi kwa kutumia silaha.

    Aliifikia milango ya chuma ya mahabusu ile na kuita mara moja jina la mtuhumiwa.

    “Gerlad Getonga!!” alirudia kwa sauti ya juu zaidi. Kimya!

    Hakuna aliyejibu huku mahabusu wakitazamana wao kwa wao na kuulizana kuwa ni nani mwenye jina hilo.

    Baada ya kuita mara nne bila kupata mrejesho wowote, afande Gasto akiongozwa na askari mwenye dhamana ya kufunga na kufungua mahabusu kwa siku ile aliingia ndani na kumtazama mahabusu mmoja baada ya mwingine.

    Gerlad Getonga hakuwa ndani!!

    Ametoka vipi kwenye vile vyuma? Ama ameshirikiana na hao maaskari waliotoweka? Haya yalikuwa baadhi ya maswali yaliyowachanganya askari wote waliopewa taarifa hii akiwemo inspekta Mujuni mkuu wa kituo kile.

    “Ita majina mahabusu wote huenda ni wengi hawamo!” alitoa amri inspekta.

    Majina yakaitwa kwa kufuata orodha iliyokuwa katika lile daftari kubwa.

    Tofauti na Gerlad Getonga ikafahamika kuwa mahabusu mwingine ambaye hakuandikwa jina lake na sababu za kutoandikwa jina zikaainishwa kuwa aligoma kusema chochote

    “Alikamatwa kwa kosa gani?”

    “Uzururaji… uzururaji afande!!” askari mmoja alijibu huku akisoma katika lile daftari.

    Ukimya ukatanda kwa sekunde kadhaa, Inspekta Mujuni akijikuna kichwa kwa kutumia kalamu yake maaskari wengine wakitazamana bila kusema neno lolote.

    Mlango wa ofisi ya mkuu wa kituo ulipogongwa ndipo fahamu zilimkaa sawa na kuuliza kwa shari aliyepo mlangoni anataka nini? Badala ya kujibu, aliyekuwa mlangoni akaendelea kuugonga mlango!

    Inspekta akampa ishara askari mmoja kuwa aufungue mlango. Upesi akatii.

    Alipoufungua akakutana na filamu ya kutisha, sura moja ya kutisha sana na laiti kama yasingekuwa mavazi yake basi asingeweza kujulikana yeye ni nani zaidi ya mzimu uliokuja kuwatisha maaskari.

    Namba yake ya utambulisho begani ikamtambulisha kuwa ndiye mmoja wa maaskari waliokuwa wakisakwa ili waelezee ni kitu gani kimetokea usiku pale kituoni.

    Uso wake mweupe ulikuwa umegeuka mwekundu, mashavu yalikuwa yamevimba huku yaliwa yamekwanguliwa na kuacha michirizi mizito ya damu, macho yalimvimba kana kwamba amepigwa ngumi kali za usoni. Mikono yake mwembamba ilikuwa imevimba huku na yenyewe ikiwa imekwanguliwa haswa. Udenda ulimtoka hovyo mdomoni huku ukiambatana na damu nzito.

    “Jenny…..umekuwaje eeh!!” Askari mmoja wa kiume alimuuliza, lakini hakujibiwa kitu zaidi ya kutumbuliwa macho tu.

    “We Jenny wewe…” Inspekta Mujuni naye alijaribu bahati yake kwa sauti iliyojaa uoga. Jenny hakujibu kitu na huyu naye akaishiwa kuangaliwa tu na macho yaliyokodolewa.

    “Mwenzako yupo wapi… eeh afande Kassim yukwapi?” Inspekta akapandishia swali jingine zito.

    Jenny akainama na kuruhusu damu izidi kumtoka kinywani.

    “Piga simu upesi huduma ya kwanza… tunatakiwa kufanya jambo hapa…” amri ikatoka.

    Wakati askari akibofya namba kadhaa kupiga simu. Jenny aliyekuwa ameinama alinyanyua kichwa chake hakutambua kama tabasamu lake alilojaribu kutoa lilionekana kama kilio cha kukera, yeye pekee ndiye aliyejua kuwa alikuwa katika kutabasamu.

    Kwa mara ya kwanza akafunua kinywa chake, huku damu ikimtoka kwa wingi akajilazimisha kuzungumza hivyohivyo.

    “Anataka mali yake aondoke zake….” Akaitoa kauli ile kisha akalegea askari wakawahi kumdaka kabla hajaanguka chini. Wakamweka chini taratibu.

    Na hapo ndipo alipoichafua ofisi nzima.

    Akaanza kukohoa kila akikohoa anarusha damu!!

    Jitihada za kumsaidia ziligonga mwamba. Walifuta damu kwa leso lakini ilikuwa sawa na kazi bure tu!!



    Huku mapokezi askari mwingine wa kike alikuwa katika tatizo jingine mwanadada ambaye hata jina alikuwa hajajitambulisha alikuwa ameenda kituoni pale kuelezea shida yake katika namna ya kupayuka bila kueleweka anasema nini, kwa jinsi askari yule alivyokuwa amechanganyikiwa na hali iliyomkumba askari mwenzao hakuweza hata kumsikiliza. Yule dada hakukoma kuzungumza aliendelea kusema huku akirukaruka huku na kule kudhihirisha jinsi alivyotishwa na taarifa ile.

    Wakati wakiendelea kutoelewana, mlango wa mkuu wa kituo ukafunguliwa na maaskari kadhaa walikuwa wameubeba mwili wa Jenny.

    Mwili huu ulipoonwa na yule mlalamikaji pale mapokezi mayowe yakaanza upya.

    “N’do huyu…..mamaaaa nakufaaaa…” alipiga mayowe makubwa. Askari mmoja akawahi kumdhibiti na kumlazimisha atulie.

    “Wewe ni nani?”

    “Naitwa Anitha ……huyu amekuja kunitishia amani nyumbani kwangu, ananitishia kuniua mimi….anataka nimpe kitu nisichokijua…” Anitha akajibu huku akiwa bado ametaharuki na asiamini kile alichokuwa anakiona.

    “Amekuja saa ngapi?”

    “Kama dakika arobaini na tano zimepita…. Ni huyu sijamfananisha hata namba zake begani nilizikariri, na niliziandika hapa..” akaonyesha mkono wake.

    Kweli kabisa, namba za Jenny zilikuwa katika mkono wa Anitha.

    Maajabu haya!! Jenny alienda vipi kwa Anitha na kisha akafika kituo cha polisi bila kuonwa na watu wengine nje!!

    Ilistaajabisha.

    “Kwa nini umekimbilia kituo hiki?”

    “Nahitaji kuzungumza na mume wangu, kama kuna lolote linaendelea anifahamishe siwezi maisha haya ya mashaka…”

    “Mume wako? Mume wako anakuwaje hapa. We ni mke wa askari..”

    “Hapana mume wangu yupo mahabusu hapa hapa nimeambiwa.”

    “Jina nani?”

    “Mimi?”

    “Hapana yeye?” askari akajibu…

    “Gerlad Getonga!!” Anitha akatoa utambulisho.

    Kimya kikubwa kikatanda, Inspekta akabaki mdomo wazi. Maaskari wengine wakabaki kuguna.,

    “We ndo mke wa Gerlad Getonga?” aliuliza huku akiwa haamini.

    “Ndio afande!”

    Askari mmoja mwenye papara akajikuta akiropoka kuwa Getonga ametoroka na anatafutwa na jeshi la polisi.

    Anitha akatumbua macho kisha akalegea na kuanguka chini huku akipoteza fahamu papo hapo.

    Na hakuzinduka katika dunia ya kawaida hadi aliposafiri kwenda nchi asiyoijua… nchi iliyojaa mauzauza ya aina yake!!



    ***CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Milango haikufunguka lakini mwanadada mrembo kupindukia aliingia katikati ya kundi la mahabusu. Macho yake makali yakamtazama mahabusuy mmoja baada ya mwingine. Wakasalimu amri na kuketi chini kisha kusinzia kabisa.

    Kasoro watu wawili tu nd’o waliobaki na fahamu zao.

    “Rebeca…. Rebeca ulikufa Rebeca…” Kindo alizungumza kwa kitetemeshi cha uoga. Yule mwanadada akaanza kucheka huku akimkaribia na kumkaba koo. Kindo akakodoa macho yake asijue nini cha kufanya. Hata Gerlad naye hakuwa na la kumsaidia alikuwa ametingwa na hofu huku akishuhudia maajabu makubwa kupita yote aliyowahi kuyaona katika ujana wake.

    “Wewe na wewe….” Yule dada alisema kwa sauti ya chini lakini yenye amri akasita kisha akaendelea, “Leo ninaondoka na nyie, naondoka nanyi usiku huu, hilo sio ombi hii ni amri yangu na hakuna wa kuitengua!! Wanadamu huwa mnajifanya mnajua sana kutengua amri, hii yangu haitenguki na kama ukiitengua basi elewa kuwa kuna gharama utalipa….wewe (akimtazama Gerlad Getonga), ukiitengua amri hii kwa namna yoyote ile basi mkeo na mtoto wako watakuwa sadaka yangu, nitawang’oa macho kucha, na masikio yao. Na utayala kama chakula chochote kile kiliwavyo!!!” akasita na kumwacha Getonga aingiwe na maneno yale.

    “Halafu wewe dogo (akimtazama Kindo), nitang’oa kichwa chako na kisha kumpelekea mama yako makaburini huko akione kilivyokuwa kibaya. Halafu kiwiliwili chako nitakisaga katika mashine ya kusagia nyama na kisha huyu mwenzako atakunywa kama mtoli… si unaujua mtoli nyau wewe!!” alitoa karipio. Hakuna aliyejibu chochote.

    “Ooooh!! Nimeukumbuka mtoli jamani… dah!” akasema kwa utulivu kisha akafanya tabasamu na kumalizia tena kauli yake, “Nitakusaga na kukufanya mtoli”

    “Tunaondoka sasa hivi… dakika hii hii…” alimalizia hiyo kauli huku akiwa amewakamata mikono Kindo na Getonga. Wakalisogelea lile geti ambalo hata mtoto mdogo hawezi kupita. Rebeca alizidi kulikaribia.

    Getonga akatarajia kuwa watakwama pale, lakini haikuwa sahihi. Wakapenya kana kwamba hakuna geti pale. Wakaongozana huku wakiipita ile maiti iliyopondeka vibaya ya askari wa kiume. Wakamfikia askari wa kike ambaye alikuwa hoi kabisa.

    Rensho akamnyanyua kwa mkono mmoja huku akimwachia Kindo huru, akamsogeza hadi nje na kisha akampa maagizo.

    “Unaenda nyumbani kwa Anitha muda huu huu, mwambie kuwa nitafuata kidole changu kama hayupo tayari kunipa mzigo alioachiwa na mumewe. Msalimie sana…” alimaliza kutoa maelekezo. Yule askari akiwa anatokwa damu sura imemvimba alipiga hatua kama msukule akienda sehemu ambayo hajawahi kufika, akienda kufanya jambo asilolijua.

    Rensho na akina Kindo wakapita katika vichochoro kadhaa na kutokea katika jumba kubwa la kifahari!!! Wakaingia ndani na mageti yakajifunga!!

    Rensho akatoa kicheko!!

    Akazidi kuwaongoza hadi katika vyumba viwili tofauti, kila mmoja akiingizwa katika chumba chake.

    Milango ikafungwa!!









    “Mwanadamu…..we mwanadamu…” sauti inayokoroma ilimshtua Getonga kutoka katika dimbwi la usingizi uliokuwa umemtwaa. Akapikicha macho yake na kukutana na sura ambayo hakuelewa kama ni ya mwanaume ama mwanamke. Akayashusha macho yake chini kidogo akabaini kuwa kiumbe kilichokuwa mbele yake kilikuwa na mguu mmoja tu, na mwingine ulikuwa umekatika kabisa.

    “Amka ule!!” sauti ile ikaamrisha kwa kukoroma vilevile.

    “Sijisikii kula…” akajikuta ametokwa na jibu lile huku akijaribu kujizuia asitaharuki zaidi..

    Kile kiumbe kikaanza kucheka kwa sauti ileile inayokoroma kisha kikazungumza, “Ukikitaa kula sasa utaishia kula masikio yako ana vidole vya mikono yako….mwanadamu ewe mwanadamu!! Bora ule”

    Getonga akashtushwa na kauli ile kutoka kwa kiumbe kile. Lakini kabla hajaendelea kile kiumbe kilitoweka na kurejea baada ya dakika tano.

    “Tazama…tazama kisha nikueleze jambo..” kiumbe kilirusha picha kadhaa katika chumba alichokuwa amefungiwa Getonga.

    “Nini hiki?” aliuliza baada ya kutazama. Zilikuwa picha za msichana akiwa katika mikao tofauti tofauti. Alikuwa anavutia sana kumtazama.

    “Niliwahi kuwa mrembo sana, mrembo kupita wasichana wengi sana. Nilipoletwa huku nikauthamini urembo wangu, nikasusia chakula. Nilichoambulia ni kula sikio langu….” Akasita na kugeuka upande wa kuume, Getonga akashuhudia tundu dogo bila kuwa na sikio, mwili ukamsisimka akauma meno yake.

    Yule kiumbe akaendelea, “nilikula vidole vya miguu yangu, na hatimaye nikala mguu wangu…… kufikia pale nilijuta lakini nilikuwa nimechelewa tayari… je mtanashati kama wewe unataka yakutokee kama yaliyonitokea mimi…mwanadamu eeh mwanadamu!!” akamaliza huku akiwa amemkazia macho Getonga.

    “Na hata jina langu lilikuwa zuri sana, niliitwa Queen nilipokuwa mwanadamu…”

    “Ulipokuwa mwanadamu? Kwani sasa wewe ni nani?” hatimaye Getonga aliuliza.

    “Mimi si mwanadamu tena bali mnyonyadamu…” alijibu kwa ujasiri kisha akacheka kidogo. Getonga akashindwa kuuzuia mkojo uliokuja ghafla.

    Akajikuta anajikojolea!!

    “Nakufananisha ama nimewahi kukuona mahali?” kile kiumbe kilisema hayo huku macho yake yakiwa yamekaza kuutazama uso wa Getonga.

    “Wewe ulikuwa nani duniani kwani?”

    “Mwandishi…nilikuwa mwandishi..”

    “Hapana sijakutana nawe katika uandishi lakini mimi na magazeti wapi na wapi, ni sehemu gani labda pengine umewahi kuishi…..”

    “Dar, Mwanza, Iringa, Mbeya, Kigoma, Musoma na Pwani….” Alijibu Getonga kwa umakini kabisa akitarajia kuwa kiumbe yule anaweza kuwa msaada.

    “Sijaishi mkoa hata mmoja kati ya hiyo. Yawezekana mnafanana tu… lakini haya macho haya….haya macho yamewahi kunitazama…. Na sio mara moja….tumewahi kukutana hakika” Alizidi kuvuta hisia, Getonga akifanya juhudi za kumwomba Mungu amkumbushe kiumbe yule ni wapi wamewahi kukutana….

    Haikuwa hivyo, kiumbe akatoweka akiamini kuwa amemfananisha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Getonga akabaki mwenyewe tena akijiuliza ni kitu gani yule mwanadada wa kujiita Rensho alikuwa akikitaka kutoka kwake.

    Wanyonya damu?? Ana maana gani huyu kiumbe



    ***



    Milango ilifunguliwa chumba kingine, yule kiumbe aliyedai kuwa aliitwa Queen akiwa duniani alikuwa anaendelea kusambaza chakula kwa watu kadhaa waliokuwa katika jumba hilo. Hapakuwa na chakula cha ziada zaidi ya nyama na mboga za majani na matunda mchanganyiko. Haikujulikana ni nyama ya mnyama yupi.

    Katika chumba alichoingia ndipo alipopata jibu na upesi aliufunga ule mlango na kuanza kurukaruka na magongo yake hadi akakifikia chumba alichokuwa amefungiwa Getonga!!

    “Mwanadamu…eeh mwanadamu….” Akaita. Getonga akajongea mlangoni.

    “Sasa nimejua ni wapi tumewahi kukutana…..tumewahi kukutana katika macho yako ya pili duniani..”

    “Macho yangu ya pili duniani? Sikuelewi?” alihoji huku akiwa anatetemeka.

    “Ukiogopa unazidi kufanana naye…”

    “Nani sasa?”

    “Eva…. Unamjua Eva wewe?”

    “Eva mtoto wangu…Eva, yupo wapi mwanangu?? Namtaka mwanabgu!”

    “Yupo katika maandalizi ya mwisho ya kunyonywa damu, amenawiri vya kutosha na malikia ana kiu kubwa sana… na ana hasira wanadamu wanamkera sana” alijibu kiumbe yule. Getonga akalegea na kuketi chini.

    “Mwanadamu…njoo hapa njoo…” kiumbe sasa alinong’ona, Getonga akiwa hajui la kufanya alijisogeza karibu. Na hapo akatambua bayana kuwa yule kiumbe alikuwa ananuka sana na aliponyanyua kinywa azungumze ndipo harufu ilizidi kuwa mbaya.

    “Mshukuru Mungu wako kuwa ni mimi niliyefyeka vile vidole vyake viwili….nikafanikiwa kuyaona macho yake vizuri..na sasa nimeyaona hayo macho kwako na kukutambua kuwa ni baba wa kiumbe kile. Mwanadamu!! Mwanadamu, kwani upo tayari kufa na kuiacha familia yako ikiteseka? Ama unafurahia kuona mwanao asiye na hatia anateseka namna hii katika ulimwengu mchafu kama huu?” alihoji yule kiumbe huku macho yakiwa maangavu kabisa.

    “Sitaki, nisaidie nitoke humu ndani!! Na kwanini mmekata vidole vya mwanangu eeh!!”

    “Kila mmoja anataka kutoka humu ndani lakini hajui cha kufanya ili atoke…lakini wewe unalo la kufanya ili utoke…”

    “Lolote nitafanya nisaidie!!” alijibu Getonga huku hofu ikiwa inazidi kumtawala.

    “Hautatoka kwa utanashati wako, lakini kama ukifanikiwa kutoka basi ni kwa sababu moja tu…nimempenda sana mtoto wako na siko tayari kushirikisha macho yangu kumtazama akiuwawa mbele yangu.. kama ukikamatwa akauwawa ukiwa naye wewe ni sawa juu yako, lakini sitakuwa tayari kushiriki walau kuiona maiti yake. Mtoto wako anakupenda sana lakini wewe humpendi mwanao, licha ya wakati mgumu kama huu anakupendeni sana wewe na mama yake…. Yeye si kama watoto wengine akilia alilie mama tu, huyu analilia baba na mama…. Ni wa pekee sana.” Kwa sauti ya chini kabisa yule kiumbe alinena na Getonga.

    “Ni usiku wa kesho kutwa nd’o unaweza kutoka lakini unatakiwa uniahidi kama utaweza kutimiza masharti yangu na kisha nikupe masharti yako. Kwanza jibu maswali yangu mawili….” Akaweka kituo kisha akavuta pumzi na kuendelea.

    “Unapafahamu Kahama?”

    “Ndio napafahamu!!”

    “Umepafahamu vipi?”

    “Niliwahi kuishi kule…” akajibu Getonga.

    “Ahaa hebu sogea karibu yangu zaidi..” kiumbe kikamsihi Getonga, naye akatii huku akitetemeka. Lakini safari hii haikuwa kwa amani. Kiumbe kikapitisha mkono wake upesi katika tundu lililokuwa kila baada ya nondo moja. Mkono uliokomaa ukalichapa shavu la Getonga na kumbamiza ukutani, akatokwa na yowe kubwa.

    “Pumbavu sana wewe, unadhani hapa tupo duniani unanidanganya mimi kama wasichana wenu mnaowadanganya huko? Dakika tano zilizopita umejibu kiufasaha sehemu ambazo umewahi kuishi Tanzania, Kahama haikuwa katika orodha, sasa nakuuliza juu ya Kahama unasema umnewahi kuishi huko. Mwanaume mwongo sana wewe, huenda hata humpendi mtoto wako shenzi kabisa…tena …” akakoma kidogo, akarudi nyuma na kuchukua ufunguo mkubwa akaufungua ule mlango. Akamkuta Getonga bado yupo chini, akamnyanyua na kumweka vyema kisha akamtandika kofi kali katika paji la uso kisha akamziba mdomo asiweze kupiga kelele. Maumivu yakasambaa kwa kasi huku akitetemeka.

    “Yaani unanidanganya mimi wakati nataka kukusaidia…”

    Akambamiza ukutani huku akiwa amemziba mdomo, sasa akiwa hana magongo bali amesimamia mguu mmoja tu, akampiga kichwa kifuani, Getonga akalainika na kuketi chini huku akishindwa kusema neno nisamehe…likaishia hewani!!

    “Tena ngoja niwahishe tarehe yenu ya kunyonywa damu shenzi wewe!!! Kumbe malikia yupo sawa kuwachukia wanadamu” Kiumbe kikatoweka kwa ghadhabu!!

    Getonga aliyasikia maumivu yakitambaa mwili mzima, hakuamini kama kiumbe yule alikuwa na nguvu na maamuzi ya kikatili namna ile. Getonga akajutia uongo wake, huku akipata fursa ya kukumbuka maisha halisi ya duniani.

    “Laiti kama wanawake mia kama hawa wamwagwe duniani..wanaume tutaacha uongo kwa kweli…” kisha akatabasamu baada ya wazo hilo.



    “Kisa umejua kuwa nakupenda wewe na mwanao ndo unaanza kuninyanyasa wewe mwanadamu kwa kunionyesha uongo wako mapema, ama kwa sababu si mrembo tena….” Getonga akashtuka kuisikia sauti ya kukoroma pale mlangoni!!

    “Naomba usinidanganye tena tafadhali, sijisikii kufanya nilichotaraji kufanya, nahitaji urejee kwa mkeo, nahitaji umtunze mwanao…… ni kweli unapafahamu Kahama?”

    “Napafahamu kwa jina tu lakini sijawahi kuishi…nisamehe”

    “Nimekusamehe…na je unamfahamu mwanadada anayeitwa Salome??”

    “Nimekutana na Salome wengi sana, sijui ni yupi unayemuulizia?” alijibu kwa nidhamu huku akiwa palepale chini.

    “Salome mtoto wa mzee Wilbard… Salome Wilbard umewahi kusikia jina hilo”

    “Hapana sijawahi lakini nawajua akina Salome wengi…”

    “Salome mjamzito….ujauzito wake una miezi miwili sasa ama mitatu!! Je unamfahamu Salome mjamzito?”

    “Aaah!! Naweza kuwa namfahamu lakini nisijue kama ni mjamzito, nawajua akina Salome kadhaa…” alijibu kwa umakini Getonga.

    “Salome ndiye atakayekuweka huru kwa sababu Salome ndiye aliyekuingiza katika matatizo haya wewe na mwenzako huyo bwege ambaye hawezi kuzungumza.” Sauti ya kukoroma ilitoa maelekezo yale.

    “Salome? Salome ameniingiza mi matatizoni…Salome gani huyo?” Getonga alijiuliza huku akili yake ikifanya kazi kwa mwendokasi mkubwa mno.

    “Nampata wapi huyo Salome nimtie adabu zake!!” akauliza huku akiwa ametaharuki.

    “Yupo Kahama sasa…. Mnapajua nyie wenyewe wanadamu… hata malikia wetu anamtafuta, alikuwa anakutafuta wewe amekupata sasa amebaki Salome ili aweze kutimiza mambo yake.”

    “Mambo yake? Na ananitakia mimi nini? Na mtoto wangu je?” alizidi kuuliza Getonga.

    “We unamwekea kauzibe kuna mambo zake unazificha na kumsababishia ashindwe kutambulika, na huyo Salome naye anamweka matatani sana na kumfanya akose amani!!” alijibu kwa utulivu.

    “Maskini weee mimi nina nini chake sasa kama sio uonevu huu jamani eeh na Eva wangu mie..” akaanza kulia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Acha kuwa bwege kama mwenzako unalialia tu… ulipokichukua kitambulisho chake anachokitumia katika safari zake na mikutano uliona sifa eeh sasa unalia lia nini? Mtoto hadi anakatwa vidole we umekomalia tu kitu usichokijua” kiumbe akamgombeza Getonga, na hapo akili ya Getonmga ikafyatuka na kuwa kama mwendawazimu. Akakumbuka kuwa aliwahi kuwa na kitambulisho ambacho hakuwahi kutazama jina limeandikwa nani na picha ni ipi. Mbaya zaidi hakumbuki ni wapi aliwahi kukihifadhi.

    “Ukipate kitambulisho, umpate Salome mwenye ujauzito wa miezi miwili Kahama, na kubwa la mwisho unatakiwa kuhakikisha humu tumboni mwangu unaniachia mtoto pia, hata mimi ni mwanamke nahitaji kuwa na katoto kazuri kama Eva!! Baada ya hayo utakuwa huru. Kwaheri!!” kiumbe kikamaliza na kutoweka zake!!

    Getonga akabaki katika mtihani mgumu kupita yote maishani mwake.

    Hajui kitambulisho kilipo, hamjui Salome wa Kahama. Halafu anatakiwa kumjaza ujauzito kiumbe yule wa maajabu, mwenye mguu mmoja, asiyekuwa na sikio moja, sura mbaya, na mwenye harufu mbaya.

    Getonga akajisikia kichefuchefu alipojenga taswira juu ya kifua cha kiumbe yule na harufu yake chafu….akajizuia asitapike.







    WAKATI Getonaga akijiuliza iwapo afanye mapenzi na kiumbe yule wa ajabu ajiitaye mnyonya damu ama aache litokee janga la kuipoteza familia yake. Katika kijiji kimoja maeneo ya Ushirombo nje ya wilaya ya kahama kulikuwa na kikao kikubwa sana kilichoshirikisha watu watatu, mmoja akiwa mwanamke.

    Mzozo ulikuwa mkubwa sana, wanaume wawili ambao walikuwa wakimzidi umri yule mwanamke waliongea kwa amri baada ya lugha ya awali ya hiari kuonekana kugonga mwamba.

    “Magdalena acha ubishi mdogo wangu… tambua mimi ni kaka yako niliyekuachia titi na wewe ukanyonya na kunenepa hivi. Mimi ni wa kwanza kuona jua… na nilishaona hapa hatari ambayo itatokea. Sawa sijasoma lakini mimba gani ile ya kuvuja damu kila siku. Mtu hajui alipotoka hajui hata jina lake we umeng’ang’ania tu na huo ulokole wako. Mbona huyo mchungaji kama ana moyo mzuri kwanini yeye asimchukue akae naye kwake…. Wakati mwingine hii mikosi ya kukosa mume unajileteaga mwenyewe” alitema maneno lafudhi ya kisukuma ikishika kasi yake.

    “Kaka nakuheshimu sana, nawe niheshimu kama mdogo wako na kubwa zaidi niheshimu kama mwanamke!!!” alikemea yule mwanamke yeye hakutawaliwa na ile lafudhi.

    Mwanaume aliyekuwa kando alikohoa kidogo kisha naye akaingia katika maongezi.

    “Vielimu hivi… yaani jasho lilitutoka sisi tukalima mpunga wewe ukaenda shule lakini leo hii elimu yako inakufanya ujione wewe nd’o wewe. Laiti kama baba na mama wangekuwepo wangekukataa na kukupa radhi nasema…. Hutaki kytusikiliza kaka zako. Mchungaji anakudanganya kila siku kuwa ni wema kutunza watu usiowajua, haya umemtunza huu mwezi wa tatu sijui, mara hospitali mara mavazi. Yote juu yako, mchungaji hakusaidii mbona. Haya utasema hizo pesa ni za kwako…. Sisi hazituhusu. Lakini usalama wa ukoo wetu. Wewe unafuga mtu huko Kahama majanga yanatupata sisi.

    Magdalena yaani elimu yako haijakusaidia lolote hadi leo dada yangu….” Alisema kwa upole yule mwanaume huku akitikisa kichwa.

    “Kwani kaka.. nyie mlitaka nifanye nini labda….maana sijaelewa nia yenu.”

    “Umwondoe nyumbani kwako….. aende mbali kabisa na ukoo wetu.”

    “Haya nitamuondoa..”

    “Kila mara unasema hivyo… kama anakushinda twende tutamuondoa kistaarabu tu!!”

    “Nitamuondoa mwenyewe!! Kwaherini na asanteni kwa ushauri, kuhusu lile shamba la mpunga, nitatuma pesa mnunue yale madawa…” alitoa kauli hiyo ikiwa ya mwisho kisha akasimama na kutoweka hadi katika gari lake.

    Safari ya kurejea Kahama mjini!!

    Ilikuwa yapata saa kumi na moja za jioni!!!



    ******



    Muda huo huo mjini Kahama!!!



    Katika jumba bovu ambalo lilijengwa likaishia kati ujenzi ukakoma baada ya mwenye nyuma hiyo kuuwawa migodini. Kulikuwa na jambo…… wanaume wawili walikuwa wakihangaika kumtua mwanamke ambaye alikuwa amepoteza fahamu.

    Waliyakumbuka vyema masharti waliyopewa na mganga wa jadi juu ya utajiri waliokuwa wakiuhitaji.

    Mganga aliwatuma ngozi ya mwanadamu! Wawili hawa ambao madawa ya kulevya na ugumu wa maisha ulikuwa umewachanganya walijadiliana kisha kura yao ikaanguka kwa binti ambaye alikuwa amezoeana nao. Binti ambaye ni kama hakuwa timamu sana kiakili na hakujulikana ni wapi anatokea. Wengine walisema ni msukule unaishi katika nyumba ya mtu kwa masilahi binafsi wengine wakadai nd’o dawa ya utajiri ya mwanamama aliyekuwa akiishi naye.

    Vijana hawa wakaona kuwa huyu alikuwa mtu sahihi wa kumchuna ngozi kwa masilahi yao.

    Wakamwekea dawa za usingizi katika pipi, akauvaa mkenge wakamtorosha hadi katika jumba lile kubwa.

    Sasa hakuwa na fahamu kabisa walimngoja mtaalamu wa kuchuna ngozi aweze kulifanya zoezi lao likamilike. Hawakuzungumza chochote kile kila mmoja alikuwa ana hofu juu ya hili walilotaka kulifanya.

    Wakati wakimngoja mchunaji, mwanaume mmoja akaanza kuupapasa mwili ule usiokuwa na fahamu!!!

    “Maskini ana mimba halafu!!” akajisemea huku akimpapasa bado, mara masikio mara mapaja, mwisho akamfunua nguo yake.

    Titi zilizosimama wima zikamdhihaki, akazibinya kidogo. Yule aliyekuwa ametulia akaingiza mkono wake maungoni na kujiweka sawa, tayari alikuwa ameingiwa na matamanio.

    Mwisho wakashirikiana na kumvua nguo zote kisha wakakubaliana kumuingilia zamu kwa zamu hadi mchunaji afike.

    Mwili usiokuwa na fahamu ulikuwa umetulia vilevile ukiwa umefumba macho!!!



    ****

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    KENGELE ya hatari ikagonga katika kichwa cha Rebeca wa Nshomile akiwa katika kitanda chake chenye thamani kubwa sana, alijihisi kuwashwa washwa na mapigo yake ya moyo yakaanza kwenda mbio. Alijaribu kuinuka akae vyema lakini usingizi nao ukazidi kumsisitiza arejee kitandani.

    “Amka Renshooo hatari!!!” akajikaza na kusema kwa nguvu, kisha akaketi kitako.

    “Amka Renshooo!!” akasema kwa sauti ya juu tena.



    Ndani ya mji wa Kahama mwili wa msichana aliyetaka kubakwa ukatikisika kidogo. Yule mbakaji akasita kubaka akamtazama iwapo atafumbua macho na kuwatambua.

    “Suka…Suka.. anataka kuamka, mdunge sindano atazijua sura zetu huyu…” mbakaji akamwambie mwenzake ambaye alichukua sindano na kuvuta maji katika kichupa walichokuwa wameambatana nacho. Akavuta ya kutosha. Kisha akamuinamia yule binti.

    Akamgeuza.

    “Mh! Ana kalio la maana duuh!!” akajisemea huku akimsuguasugua tayari kwa kumdunga sindano.

    “I love KINDO…..sijui nd’o bwanake huyu…duh!! Jina la bwana linaandikwa hadi takoni aisee! Huyu demu noma aisee…..halafu hapo unakuta bwana’ke ndo alimgeuza akamchora huu ujinga…halafu wakaachana bora hata tumchune tu hii ngozi maana hawezi kuolewa na mtu mwingine huyu. Eti? Nani mpumbavu wa kukubali kuoa mwanamke amechorwa jina la mtu”

    “Oya acha maneno mengi choma sindano mi nipande bwana mizuka inapanda sana.” Alisihi bwana aliyekuwa uchi.

    Jamaa mwenye sindano akainama tena akampapasa yule binti.



    Jijini Dar es salaam katika jumba lisilojulikana lilipo Rensho akatetemeka tena na kisha akapiga kelele kuu.

    “Amkaaaa Rebecaaaaa…..amkaaaaa”



    Wakati huohuo yule binti aliyekuwa amepoteza fahamu mjini Kahama akanyanyuka kwa nguvu sana na kumpiga kichwa yule bwana mwenye sindano kisha akaikwapua ile sindano upesi na kumdunga nayo uumeni yule aliyekuwa uchi.

    Mshikemshike!! Jamaa akatoa mayowe makubwa, binti akiwa uchi akasimama wima tena akarusha teke kali katika korodani za yule aliyekuwa uchi akapoteza fahamu palepale huku akigumia kwa maumivu makali. Yule aliyebaki akataka kukimbia, msichana akamdaka na kuikamata shingo yake akaizungusha kwenda katika upande usiokuwa wa kawaida.

    Kilichofuata hapo ni kile ambacho wawili hao walipanga kufanya kwa yule msichana.

    Binti akazichuna ngozi zao katika mwendo wa haraka kuliko kawaida bila kusema neno lolote.

    Baada ya hapo akatoweka akitembea kwenda sehemu asiyoijua, hakuwa na hofu yoyote ile na alikuwa hajitambui, alizidi kwenda mbele tu hadi aliposimama katikati ya barabara akitetemeka baada ya kushtuliwa na honi kali za gari na breki.

    “Mungu wangu…..” dereva mwanamke akapiga kelele huku akishika breki kwa wepesi aweze kumnusuru yule binti.

    “Mungu wangu nini hiki….” Akataharuki baada ya kukutanisha macho na mwanamke akiwa uchi wa mnyama katikati ya barabara huku nguo zake zikiwa begani.

    Ile sura ni kama aliifananisha lakini alipofumba na kufumbua tena yule aliyetaka kugongwa hakuwepo barabarani.

    “Mamaweeeeee!!” alipiga kelele huku akiendesha gari hovyohovyo huku akilitaja jina la Mungu….

    “Mh! Ni mtu kweli ama nilikuwa nawaza tu mimi….” Alijiuliza Magdalena baada ya kupata utulivu kiasi, mapigo ya moyo yakiwa hayajerejea bado katika hali yake ya kawaida.

    “Sio Martha yule?” alijiuliza kwa sauti, akimfananisha yule binti barabarani uchi kama binti ambaye kaka zake walikuwa wakimsihi amwondoshe pale nyumbani kwake kwa sababu ni mikosi. Jina Marha ni yeye aliyempatia baada ya binti yule kushindwa kukumbuka lolote juu ya historia yake

    Magdalena akajiaminisha kuwa ni yale maneno makali ya ndugu zake yaliyomletea picha ile ya ajabu.

    “Ningeweza kuangusha gari kijinga tu kumbe hakuna lolote hata!!” aliwaza kisha akapuuza yote yaliyotokea.

    “Na haya ni maono kabisa, yule binti simwondoi nyumbani kwangu, akina kaka wakichukia wao wachukie tu!! Tena wasipende kufuatilia maisha yangu, yaani watu wasiosoma bwana ni shida…imani mbovumbovu zimejaa kichwani mwao” alilaani Magdalena huku akiendelea kuendesha gari lile.

    Hakujua kuwa huo ulikuwa mwanzo kizungumkuti, utata na hofu kuu!!

    Laiti angejua!!!!.........



    ****



    Jijini Dar es salaam ndani ya ficho lisilofahamika wapi linapatikanika, baada ya kutulia Rensho alisimama akapiga hatua kadhaa mwisho akakifikia chumba alichokuwa amehifadhiwa Gerlad Getonga. Kichwani mwake alijua kabisa kuwa alisafiri maili kadhaa na alipigana na kundi la watu ili kuusalimisha uhai wake, lakini hakujua ni wapi uhai wake umehifadhiwa. Jambo ambalo lilimkera kuishi kwa mashaka na hofu.

    Nani huyu anayeshiriki katika uhai wangu!!! Nataka kuishi shenzi zake. Halafuhayo mabazazi yalitaka kumfanya nini yale maana kama yalimlewesha hivi. Sijui mwannaume sijui mwanamke huyo….

    Maswali lukuki yakakighafirisha kichwa chake. Akapandwa na hasira



    “We fala Salome yupo wapi na kitambulisho changu kipo wapi….” Aliuliza kwa shari kuu huku akimtazama Getonga.

    Getonga akajivika ujasiri hakujibu lolote akatabasamu.

    “Nakuuliza wewe….Salome yupo wapi, nahitaji kujua alipo na pia kitambulisho changu. Hivi wanadamu mbona wabishi nahitaji kuondoka hapa… bado mnaning’ang’ania tu….” Alifoka kwa sauti ya juu sana.

    “Simjui salome na wala kitambulisho sikijui…” alijibu kwa utulivu. Rensho akatoweka bila kusema neno lolote.

    Na baada ya kuda geti likafunguliwa, Gerlad akashikwa mkono na watu asiowajua na kuongozwa kuelekea mahali.

    Giza likatawala kisha akaufikia mwanga….

    “Jibu moja la kipumbavu naondoa hii pua ya mkeo!!” alikuwa ni Rensho akiwa amemning’iniza Anitha mke wa Gerlad Getonga katika mbao nne imara akiwa amefungwa kamba.

    Getonga akapigwa na butwaa!!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Kitambulisho, pili Salome anapatikana wapi… hakuna jibu nachinja. Huwa sionyi mara mbili!!!” Rensho akazungumza kwa sauti ya chini!! Na wakati huo akahamishia kisu kuelekea katika shingo ya Salome.

    Getonga akatamani kusema lolote ajuala lakini bahati mbaya hakuwa akijua lolote!!!

    Mshikemshike!!!



    **GETONGA hajui lolote na bado natakiwa kujibu maswali.. kama hana majibu haipo nafasi ya kujitetea ni mkewe kuuwawa kwa kuchinjwa!!



    ITAENDELEA!!!



0 comments:

Post a Comment

Blog