Simulizi : Hofu
Sehemu Ya Pili (2)
Alipotoa komea mara mlango ukasukumwa ndani kwa nguvu, akajirusha kando akiamini ni vurugu za rafiki zake baada ya kupata pesa.
Lakini macho yakashuhudia kitu tofauti. Kiumbe kisichotambulika sura yake kikivuja damu katika kichwa chake, mikononi na uso usionekana walau kidogo kiliangukia magoti, kisha huku kikikoroma kikatokwa na maneno machache sana.
“Mmeniu….uua…”
Kisha mdomo ukatangulia ardhini, na mwili wote ukafuata kwa kishindo. Kiumbe kile kikahema kwa nguvu mara moja kisha kikatulia tuli!!
Sam akatokwa na yowe la uoga, na alipoitazama saa yake akaingiwa uoga zaidi.
Ilikuwa saa nane usiku!!!
___
KIZA kilichotanda katika macho yake kilianza kufifia na baadaye ikafuata nuru baada ya mauzauza ya hapa na pale. Alijaribu kuunyanyua mkono wake lakini ulikuwa mzito hakuweza!!
Akayahisi maumivu mguuni mwake, akatamani kulalamika lakini midomo ikawa mizito kufunguka. Akabaki kulalamika katika nafsi kisha akajikakamua na kisha kujinyanyua kwa nguvu zote.
Akafanikiwa kukaa kitako, harufu ya ubani na udi kwa mbali ikafuatia katika pua zake.
Mara ya mwisho alikuwa anamkimbia Maulid na hatimaye akajikwaa katika bonde na kupoteza fahamu lakini hayupo tena bondeni, amevikwa suti ya gharama na yupo mahali asipopajua.
“Nipo wapi hapa?” aliuliza kwa sauti ya chini ilhali yupo peke yake. Hakuna wa kumjibu!!
Mara mlango ukafunguliwa, wakaingia wanaume wawili walipotazamana wao wakatabasamu na kutoweka. Baada ya sekunde nyingi kidogo akaingia mzee mtu mzima.
Baba yake Rensho!!
Mauzauza!!
Safari hii hakuwa katika sura yake ya kikaidi ambayo inasadifu kauli yake ya kupigana vita vya Kagera.
“Kindo… Emmanuel Kindo….mkwe wangu mwenyewe huyooo… dume la mbegu.” Mzee Gaspar Nshomile alimsifia huku akichanua tabasamu mwanana. Tabasamu lile likaifungua akili ya Kindo upya. Kabla mzee Nshomile hajamtembelea pale nyumbani kwake na kumweleza juu ya mahusiano baina yake na mwanaye kuna mahali aliwahi kumuona miaka kadhaa nyuma tena akiwa katika mavazi ya aina ile ya suti za bei mbaya.
Nilimuona wapi huyu mzee? Kindo alijiuliza huku akizidi kujilazimisha kukumbuka. Lakini hakupata kumbukumbu zaidi ya aliyokuwanayo….
Mzee Nshomile akatoweka akimwacha Kindo katika dimbwi la mawazo. Mlango ukafungwa tena!!
Baada ya dakika takribani tano wakaingia wale wanaume tena, wakamuamuru Kindo asimame, aliposuasua wakamsaidia kunyanyuka.
“Mnanipeleka wapi lakini? Mimi nimewakosea nini jamani ndugu zangu…. Na hapa ni wapi jamani…” aliuliza maswali mfululizo lakini hakuna hata aliyekaribia kumjibu.
Wakamwongoza hadi katika chumba kingine, wakaufungua mlango na kumsukumia ndani ya chumba hicho kisha wakafunga kwa nje wakizipuuzia kelele alizowapigia za kuomba msaada.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
HOFU NDANI YA CHUMBA.
Macho ya Kindo yalishuhudia mandhari ya kuvutia, japo alikuwa anatetemeka alikiri kuwa chumba kile kilikuwa cha kifahari. Alitazama kabati akatazama marumaru, akakitazama na kitanda….. hapo macho yakasita, kitanda kile kikubwa hakikuwa kitanda pekee.
Palikuwa na kiumbe juu yake, kiumbe laini kabisa upande wa mgongo uliokuwa wazi, kisha ile nguo laini ambayo kilijivika kiumbe kile ilifanya umbo lake lililokatika vyema na kuichora miinuko miwili katikati ya umbo lake kuonekana vyema. Mgongo wake ulifunikwa kiasi na nywele ndefu nyeusi.
Mapigo ya moyo ya Kindo yakaongezeka kasi, hofu ikahama na kuingiwa na matamanio kiasi flani. Alikiri kuwa yule binti alikuwa ni mrembo zaidi ya Salome wake.
“We we ni nani….” Aliuliza kwa sauti ya chini kabisa Kindo bila kufanya hatua yoyote ile mbele. Kile kiumbe kikatoa sauti ya chini pia ya kicheko.
“Unacheka wakati nakuuliza we ni nani na hapa mmenileta kufanya nini?” akahoji kwa ukali…. Kile kiumbe kikacheka tena na sasa kikajigeuza taratibu na kuuonyesha uso wake kwa Kindo.
Asalalee!! Kifua cha yule binti kilibeba mzigo mdogo kabisa wa matiti na hapakuwa na njitihada zozote za kuyaziba. Kindo uroho ukamwingia, akasahau kuwa hajapata jawabu la kwanini amevalishwa suti, akakutana na mzee Nshomile na sasa yu pamoja na yule binti katika chumba asichokijua.
Macho ya Kindo yakabaki kutumbulia kifua cha yule binti.
“Kindo umekuwa mkaka kweli…..” kauli ya kimahaba kutoka kwa yule binti ikarejesha wasiwasi.
Amenijuaje huyu kiumbe!! Aliduwaa Kindo.
Akanyanyua macho yake kumtazama yule mwanadada.
Akamuta anatabasamu na vishimo vidogo vikaonekana katika mashavu yake.
Sura ngeni kabisa!!
“We ni nani na umenijuaje…” alihoji Kindo.
“Emmanuel Kindo….. si ndo wewe jamani ama… hivi ulishaacha kukojoa kitandani hahahahah!!” sauti laini ikazidi kumjaribu Kindo.
Kukojoa kitandani!!! Huu msamiati ukamduwaza, ni kitendo cha miaka mingi iliyopita alipokuwa mtoto mdogo bado.
“Hivi ulifaulu kuingia form one maana ulikuwa na akili we mtoto…”
Huyu ni nani lakini jamani!!! Kindo alizidi kuhamanika.
“Wewe ni nani nakuuliza? Nitakujeruhi usipojieleza na hatakuwepo wa kunifanya lolote…” alikaripia Kindo huku akijikaza na kupiga hatua kumsogelea.
Binti yule akacheka sana kisha akasema, “Yaani ulikuwa unapigwa nakusaidia mimi kila siku leo hii unipige looh! Unafurahisha Kindo wewe….”
Lahaula!! Kindo akaruka nyuma na kujibana ukutani akimwacha yule binti akiwa anacheka hadi kutokwa na machozi.
Kindo alizidi kujigandamiza ukutani, kijasho cha uoga kikimtoka.
“We Re…Rebeka wewe…..we Rebeka…..” Aliita huku akizidi kujigandamiza ukutani…
Kindo alikuwa amekutana na ajabu zito na mauzauza ya aina yake, macho yake yalikuwa yakimtazama mtoto wa zamani ambaye alizikwa akiwa na miaka kumi tu! Alizikwa akasahaulika enzi hizo na kisha akafutika katika vichwa vya waliomjua baada ya miaka kadhaa.
“Kindo mkeo amefariki pole sana!!” Kindo akaikumbuka kauli ya mzee wake ambaye alikuwa amezoea kumwita Rebeka kuwa ni mke wa mwanaye.
Yule mtoto yu hai sasa akiwa mbele ya Kindo, si mtoto tena bali mtu mzima.
“Ulikufa Rebeka…..ulikufa..” sauti yenye kitetemeshi cha uoga ilizidi kutoka katika kinywa cha Kindo.
“Hata wewe unakufa muda si mrefu!!” yule binti akamjibu kwa furaha kabisa.
“Noo.. usiniue Rebeka usiniue…” alisihi.
“Sina ujanja Kindo lazima niku…..” akasita kisha akatega sikio kama anayesikiliza kitu.
“Anakuja… anakuja Kindo… anakuja…”
“Nani…eeh!” Kindo akauliza, lakini hilo likawa swali la mwisho kabla yule binti hajaanguka chini ghafla na kuanza kuvuja damu puani na masikioni!! Kindo akataka kukimbia lakini mlango ulikuwa umefungwa kwa nje.
Akahaha huku na kule, likaja tukio kubwa zaidi. Kile chumba kilichokuwa kisafi na cha kuvutia kikapatwa na joto kali sana na kisha kama mvua inavyonyesha nje, ndivyo damu ilivyoanza kunyesha ndani ya kile chumba.
Kindo akapagawa, hakuna alichoona tena zaidi ya damu nzitonzito. Akajaribu kukimbia pasi na uelekeo akateleza na kuanguka chini, mdomo wake ukitangulia sakafuni.
Akatulia kama Rebeka!!
____
MKUTANO haukuanza kwa wakati kwa sababu alisubiriwa mtu mmoja ambaye alikuwa kiungo muhimu sana kwa siku hiyo. Wajumbe wengine walikumbwa na pepo la wivu kutokana na mafanikio ya muda mfupi ya mjumbe mwenzao.
Kila mmoja alimfikiria Yakuza Wenje na kutamani kusimama katika nafasi yake kwa wakati huo, waliamini kuwa kwa mafanikio aliyoyapata katika jambo la msingi kama lile basi ilikuwa siku yake ya neema na kujazwa mapesa na kugeuka kuwa tajiri mkubwa kabisa.
Muda ulizidi kusonga mbele na bado muhusika hakufika, hivyo mishumaa haikuwashwa kumaanisha kuwa mkutano ulikuwa haujaanza rasmi.
Minong’ono ya hapa na pale kutoka kwa wajumbe haikuisha, walikuwa wakilalamikia tabia ya Yakuza kutojali muda inawaharibia wengine ratiba zao. Malalamiko hayakupata wa kuyajibu, wengine wakavuta midomo yao kimanung’uniko lakini hii haikusaidia.
Ghafla, tofauti na utaratibu wa siku zote mlango unaotumiwa na wajumbe kuingia katika ukumbi ule na wakiwa wanaamini kabisa kuwa amesalia mjumbe mmoja tu kuingia, ukafunguliwa kwa pupa.
Yakuza huyo!! Kila mmoja akawaza na kutoa miguno ya kukereka.
“Washa mishumaa… washa mishumaa upesi!!” sauti iliyokatika taharuki kali iliamuru, wajumbe wakaitambua kuwa ilikuwa ya katibu wao. Mambo yalikuwa tofauti kabisa tena yasiyofuata utaratibu!!
Wakawasha mishumaa yao, na kwa mara ya kwanza taa kali ya katibu wao haikuwashwa na wakaweza kuiona sura yake kwa mara hiyo ya kwanza.
“Mambo yamevurugika… mambo yamevurugika wajumbe…” alianza kuelezea huku akihema juu juu.
“Eti…”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mambo si mambo tunatakiwa kujilinda na kuchukua hatua za haraka haraka kabla jambo hili halijatudhuru wote….” Akakohoa kisha akavuta pumzi na kuzitoa kwa nguvu kisha akaendelea, “hatujui wapi pa kuanzia lakini Yakuza ameharibu mambo yetu tayari. Yakuza ametuweka katika hatari kubwa sana na hadi dakika hii hapokei simu yake ya mkononi… halafu tulichomwagiza hajakifanya ametulaghai” akasema kwa ukali, wajumbe wakaguna kwa mshangao.
“Kiumbe hakijulikani kilipo…… hakijulikani kilipo wajumbe …..” alipoimaliza kauli hii aliendelea, “Watolewe upesi na kulindwa, mkawatoe upesi jamani……” akasihi, na kisha wote wakabaki kimya wakiutazama mlango uliofunguka ghafla kisha upepo mkali ukaanza kuvuma!!
Woga ukatawala, wajumbe kila mmoja akalalamika ajuavyo huku wakijaribu kutiana moyo kuwa ile ni hali ya kawaida.
“Pereza… kafunge mlango haraka!!” katibu akatoa amri kuu…. Pereza ambaye alikuwa kamati ya ulinzi alisimama huku akijutia cheo chake. Hofu ilikuwa inaishi naye, akajitutumua kiume akaufikia mlango akaanza kupambana na upepo akiuvuta mlango ndani.
Mara upepo ukakoma ghafla!!
“Aaah!!” wakaduwaa wajumbe!! Pereza akacheka ki9fedhuli kisha akajitapa, “Nimeuamrisha ukome….” Akajaribu kuuvuta mlango, mlango haukusogea.
“Chibe…. Upesi njoo tusaidiane…” Pereza akaamrisha, msaidizi wake akajongea kiukakamavu mlangoni. Akaushika mlango kinguvu.
“Nenda ukausukume kwa nyuma mi navuta mbele.” Pereza akaamuru. Chibe ambaye ni mjumbe na pia makamu katika kamati ya ulinzi akatii. Akazunguka nyuma ya mlango.
“Mamaaaaa… nakufaaaaa” Chibe akatokwa na ukulele wa ghafla. Pereza akaruka pembeni kimazoezi kisha na yeye akaenda nyuma ya mlango kutazama nini kinamtokea mwenzake huko nyuma.
Hakumkuta!!
“Watoe vyumbani ….mkawatoe vyumbani upesi….” Katibu alihamasisha juu ya Kindo na Rebeka kutolewa vyumbaniu, sasa kila mjumbe alihaha huku na kule.
“Funguo haupo… funguo!!” mjumbe mmoja alilalama.
“Pereza… funguoooo!!” katibu aling’aka.
Pereza akaduwaa, kisha mdomo ukabetuka wakati anajibu, “alifunga Chibe na hayupo hapa tena….”
“Fuck!! Fuck! Fuck….!!” Aliropoka katibu mkuu.
Mihangaiko hiyo ikawa kama imeruhusu ule upepo wa maajabu kuanza kuvuma tena. Safari hii hakuna aliyeweza kuuzuia tena. Ukavuma hadi ndani.
Na hapo ukabadilika haukuwa upepo wa kawaida tena. Ukaleta joto badala ya ubaridi, na mvua yake haikunyesha nje ikanyesha ndani, si mvua salama ya maji bali mvua ya aina yake.
Mvua ya damu!!
Upepo haukuja na ile damu, ile damu ilitoka kwa wajumbe. Upepo ulivuma ukianza na katibu, ukambamiza huku na kule bila kumruhusu kutulia, damu zikamvuja kila kona. Upepo huu wa maajabu ni kama ulikuwa na mikono mingi sana, ukanyanyua mjumbe mmoja baada ya mwingine na hatimaye wote wakawa angani wakibamizwa katika kona hii na ile.
Damu zao zikageuka kuwa mvua iliyosababishwa na upepo ule.
Na janga lililotokea katika nyumba hiyo lilizua kizaazaa nchi nzima!!
Kila aliyesikia tukio hilo akajawa na HOFU!!
****
MSHAHARA aliokuwa anapokea kwa shughuli ya kukata majani katika nyumba ya kizito ulikaribiana na ule wa wafanyakazi wanaolipwa katika ofisi nyingine.
Mshahara huu uliyafanya maisha yake kuwa mazuri, akaihudumia familia yake ya mtoto mmoja na mke, akapanga nyumba nzuri na baada ya mwaka mmoja akanunua gari ambalo hakutaka tajiri wake ajue.
Hakubadili muonekano wake wa mavazi, na kila siku akaendelea kuonekana maskini na mnyenyekevu sana. Hii hali iliimarisha kibarua chake.
Kama ilivyo kawaida yake Kelvin Mgonja, siku hiyo aliwahi tena kazini asubuhi sana akitarajia kuhudumia nyasi za bosi wake mapema kisha aingie katika shughuli nyingine.
Tofauti na siku nyingine ambapo mlinzi humfungulia geti upesi upesi. Siku hii ya maajabu alibisha hodi hadi akaingiwa na kero ya kuwa mwajiriwa katika nyumba ile.
Hadi inatimu saa mbili asubuhi hapakuwa na dalili yoyote ile ya kufunguliwa geti. Ilipofika saa tatu asubuhi wasiwasi ukaanza kumwingia, haikuwa kawaida ya bosi wake kulala hadi saa hizo.
Au anaumwa!!! Kelvin alijiuliza huku akijaribu kusaka upenyo aweze kuchungulia. Hakuupata upenyo wa kujua nini kinaendelea ndani ya nyumba ile.
Majira ya saa tano asubuhi Kelvin akaenda kutoa taarifa katika serikali za mitaa juu ya hali ile inayoendelea nyumbani kwa bosi wake. Kwa sababu alikuwa mtu mzito na anayefahamika mwenyekiti alikurupuka na kuacha shughuli zake nyingine, akawachukua wanamgambo watatu wakaongozana naye pamoja na Kelvin hadi nyumbani kwa Patrick Massawe kijana ambaye alitarajiwa kugombea ubunge baada ya miaka miwili na alikuwa na asilimia zote za kuchaguliwa.
Hali aliyoiacha Kelvin bado haikubadilika, hapakuwa na mlinzi getini.
Mwenyekiti wa mtaa akajaribu kupiga simu ya Patrick, ikaita bila kupokelewa. Hali hii ikazidisha hofu!!
Mwenyekiti kwa kutumia wadhifa wake akaruhusu wanamgambo waruke lile geti na kutua ndani ya ile himaya. Wanamgambo wakajitutumua wakachumpa ndani ya ile himaya . mwenyekiti na Kelvin wakaendelea kungoja nje!!
“Tazama kila pande!! Kuwa makini zaidi…” mwenyekiti akaamuru jeshi lake lililokuwa ndani.
Kimya kikatanda kwa takribani dakika kumi, kisha mlipuko wa kelele za hamaniko.
“Mamaweee… tunakufaaa…. Mamaaaa” vilio vya wanamgambo vilisikika, kisha wakaliparamia geti, wakatua upande wa pili hawakutulia wakaendelea kukimbia.
Mwenyekiti na Kelvin nao wakaanza kukimbia huku wakipiga kelele kana kwamba wanajua nini kilichowasibu wenzao.
Wanamgambo walipopata akili ya kutulia huku wakihema juu juu wakasimulia juu ya hali iliyokuwa ndani ya ile nyumba ya mheshimiwa Patrick Massawe.
“Damu, damu kila kona……maiti kila upande…. Ni balaa…” alijieleza mmoja wao kisha mwingine akatikisa kichwa kuunga hoja mkono.
Mwenyekiti akatoa taarifa polisi!!
Baada ya nusu saa nyumba ya Patrick ilikuwa imezingirwa na utitiri wa askari. Wakafanya utendaji wao, geti likavunjwa komeo lake likabaki wazi wakati miili zaidi ya kumi ikitolewa katika jumba hilo huku waandishi wa habari wakifanya jitihada zao katika kupiga picha hapa na pale.
Lilikuwa tukio la kustaajabisha!!
Patrick Masawe alikuwa mmoja katika ya waliopoteza uhai katika tukio hilo!!
***
AKIWA katika nyumba ya kulala wageni huku hofu ikiwa imemtawala juu ya tukio lililotokea majira ya saa nane usiku nyumbani kwake na jingine lililotokea saa tisa usiku. Kutembelewa na mgeni anayevuja damu kisha akapoteza maisha mbele yake huku akisema neno moja tu ‘mmeniua’. Sam alikuwa akihaha kujiuza huku na kule kitandani na kujiuliza ni nani alikuwa mtu yule maana alivyokuwa anavuja damu sura yake haikuweza kuonekana hata kidogo.
Tukio lile likamfanya afunge safari ya ghafla kwenda nyumbani kwa rafiki zake, nia yake kuwashirikisha wenzake ili wafahamu usiku huohuo ni kitu gani sahihi wanatakiwa wafanye juu ya ule mzoga.
Huku akakutana na kubwa kuliko.
Don na Deniss walikuwa maiti wenye aibu kabisa, walikuwa uchi huku damu zikitapakaa kila mahali. Bila shaka walihangaika kabla ya kufa.
Sam akatimua mbio hadi alipoipata nyumba ya kulala wageni, akajifungia ndani huku akili ikicheza huku na huko na kusababisha aukose usingizi kabisa.
Do na Deniss wamekufa wakiwa uchi na huko nyumbani kwake ametembelewa na mgeni ambaye ni kama alichagua kufia nyumbani kwake.
Maskini Don na Deniss, au wamechoma visu kwa sababu ya pesa? ..lakini mbona walikuwa wanaelewana sana hawa rafiki zangu!! Sam alijiuliza kwa utulivu huku akizidi kutafuta chanzo kikuu.
Lakini, yaani wachomane visu wakiwa uchi… uchi wa mnyama… hapana!! Kuna kitu, ama niseme kuna mtu amewaua!! Alizidi kujiuliza na kujipatia majibu kwa sauti ya juu.
Mtihani!!
Asubuhi na mapema akawasha runinga iliyokuwa pale chumbani ili aweze kubaini kama taarifa juu ya yule mtu aliyefia nyumbani kwake zimevifikia vyombo vya habari pia alihitaji kujua ni kitu gani kimewaua Don na Deniss kama kipo.
Habari zilikuwa za siku iliyopita na hapakuwa na habari mpya kabisa.
Sam akaizimisha runinga na kuendelea kujilaza, usingizi ulipomnyemelea akapiga simu mapokezi na kumzuia mfanya usafi asihangaike na chumba chake katika suala la hilo muda ukifika.
Majira ya saa saba alipowasha tena runinga akakutana na habari mpya asiyoijua hata kidogo. Kila kituo kilizungumzia juu ya mauaji ya kutisha katika nyumba ya mzee Patrick Masawe.
Picha zilionyeshwa huku kituo kikiomba radhi kwa picha zile, hakika walikuwa sahihi kuomba radhi kwa sababu zilikuwa zinatisha haswa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mwingine hana mguu, mwingine mkono, jicho na miili mingine ikiwa ni viwiliwili pekee bila vichwa.
BAADA YA SIKU TANO
HABARI ya mauaji yale ikiwa imezoeleka, vifo vya Don na Deniss vikiendelea kupepelezwa na kifo cha Yakuza Wenje nyumbani kwa Samson kukimweka kijana yule matatani, na jeshi la polisi lilikuwa likimsaka na kuwaamisha wananchi kuwa kupatikana kwa Samson utakuwa ufumbuzi mkubwa wa janga hilo la ghafla lililotokomea na roho nyingi.
Wakati haya hayajatulia na Sam akiwa hana dalili ya kupatikana. Ahueni nyingine ikapatikana.
Kijana aliyekutwa akiwa mahututi ndani ya jumba lile ambalo roho lukuki zilipotea sasa alianza kupata nafuu. Aliweza kujitikisa kidogo kisha akafumbua macho yake na kubaki akiduwaa.
Uangalizi wa madaktari ulichukua nafasi kubwa ili kuokoa maisha yake ili aweze kutatua utata huo uliogubika.
Jitihada zikazaa matunda, afya yake ikaimarika. Lakini alikuwa kimya bado asiseme lolote. Na alipokuja kusema neno moja la kwanza neno hilo likakikamata kinywa chake na kuwa neno lake la kila siku.
“Rensho!!” nd’o neno pekee aliloweza kulitamka.
Baada ya picha zake kusambaa magazetini, akatambulika kuwa aliitwa Emmanuel Kindo.
Mama yake Kindo akahojiwa na kudai kuwa huyo Rensho anayetajwatajwa na Kindo, alikuwa ni mwanamke ambaye mwanaye alitarajia kuoana naye siku za usoni na hakujua jingine la ziada tena hadi mwanaye alipokutwa na janga hilo akiwa ndani ya suti.
***
SIKU zilizidi kukatika na Sam akiendelea kuishi maisha ya kujificha. Hakuwa na ujanja mwingine wa kujitoa katika kesi iliyounganishwa na kutajwa kuwa yote inamuhusu yeye.
Katika kujificha huku, alitawaliwa na taswira mbili, moja ya yule binti akimlalamikia na ile ya pili ikiwa ya yule bwana mwenye kuvuja damu akimlilia na kisha kukata roho.
“Au walivyombaka…” Sam alipitiwa na wazo hilo kisha akalikumbuka tukio la Don na Deniss kumwingilia kinguvu yule binti kabla ya kumtosa katika mkondo wa maji fahamu zikiwa zimemtoka tayari. Binti yule alimlilia sana Sam awe msaada kwake lakini hiyo ilikuwa ngumu sana kwa sababu Don na Deniss walikuwa na bunduki na kiubavu walimzidi Sam
Sam akalazimika kuwa mpole, Don na Deniss wakatimiza haja zao kwa kujirudia mara kadhaa na kisha kumtosa katika maji yule binti.
Hata kabla hawajalipwa pesa yao linatokea janga hili la kutisha Don na Denny wanakufa huku wakiwa uchi!!
Yakuza naye anakufa na anayetuhumiwa kwa hili ni Sam ambaye yupo mafichoni.
Yule binti ni nani hasa!! Sam akajiuliza, huku kwa mbali akiamini kuwa huenda yule binti akawa na ushahidi wowote wa kumweka huru tena.
Akakusudia kumtafuta, lakini mara akakata tamaa kwa kuamini kuwa iwe isiwe lazima yule binti alipoteza uhai siku ileile.
Akaamua kuanza harakati zake za kusaka chanzo cha yote haya kwa kuanzia kukutana na mpenzi wa Don.
Akaifanya safari majira ya usiku kabisa!!
Bila taarifa akaingia mitaa ya Temeke mwisho, akapita nyumba kadha wa kadha akaifikia nyumba ya Sarah aliyojengewa na Don enzi za uhai wake. Sam akaugonga mlango taratibu sauti ya Sarah ikajibu huku ikitokea ndani, akamuuliza ye ni nani anayegonga mlango.
“David..” akadanganya ili Sarah aweze kufungua. Kweli akafungua!
Sam akaingia ndani akimuacha Sarah akiwa katika mshangao wa hali ya juu…..
“Shem, tulia tuzungumze sijaja kwa ubaya na unayoyasikia yote katika vyombo vya habari ni uongo mtupu!! Mimi naweza kumuua Don, mimi naweza kuutoa uhai wa Deniss… Sarah nawe uliamini hivyo…” alihoji kwa kusihi. Sara badala ya kujibu akabaki kutoa machozi tu!!
“Sarah, hapa kuna jambo zito sana limejificha ambalo si la kawaida. Mimi sijaua…. Nashindwa hata kuelezea nini kinatokea.”
“Shem, sijaamini kuwa ni wewe uliyeua na sitakaa niamini. Lakini ni kitu gani sasa hiki kinanitokea baada ya kifo chake.,…,”
“Kitu gani tena….” Alihoji Sam kwa umakini.
“Naota ndoto, au niseme kuwa niliota ndoto gani hata sijui… msichana hivi amejilaza haonekani sura yake bali mapaja tu, halafu anavuja damu. Niliposhtuka…..” akasita akaanza kulia, Sam akaenda kumyamazisha.
“Usilie sasa shem ndo maana mimi nimekuja hapa ili tujue la kufanya… si unajua natafutwa eti nimeua mimi…”
“Najua….” Alimalizia Sarah!!
“Sawa ikawaje baada ya ndoto..”
“Nikaingia katika siku zangu ghafla…. Yaani ghaflka na …na hazijakata hadi leo…” akalia kwa sauti ya juu wakati anamalizia kauli yake.
“Unatokwa damu?.... mbona…eeh..”
Badala ya kujibu Sara akabaki kulia tu asijue kipi cha kujieleza zaidi.
“Hata kazini siendi mara kwa mara… yaani damu inanitoka sana…. “ akasita kisha akaendelea, “bora basi ingekuwa inatoka tu…. Yaani inatoka halafu nakuwa nanuka shem nanuka vibaya…”
Sam akakisikia kichwa chake kikivurugika haswa!! Hii ilikuwa habari mpya zaidi tena tatanishi.
“Hivi Sam, Don na Deniss walifanya nini kwani?”
“Deniss ameingiaje tena hapa kwani….”
“Maria naye aliota….” Alisema kwa sauti ya chini.
“Heh! Maria mpenzi wake Deniss?”
Sara akatikisa kichwa kuafikiana na Deniss.
Sam akachoka!!
“Shem….kwani Don alikuwa anafanya kazi gani? Wewe ni rafiki yake mkubwa tafadhali usinifiche!!” Sara akauliza swali ambalo lilikuwa la ghafla sana.
“Nani, Don!!” Sam akauliza kipumbavu huku akipepesa macho huku na kule kumkwepa Sara.
“Don, alikuwa anafanya biashara zake tu mikoani… alikuwa mfanyabiashara.” Sam akajibu huku akitetemeka wazi wazi.
“Nilidhani alikuwa dereva tu wa magari makubwa!!” Sara akakebehi huku akikumbuka kuwa awali Don aliwahi kumweleza kuwa yeye ni dereva.
Aibu zikamkumba Sam!! Hakujibu chochote. Sarah akaanza kulia kilio cha chinichini, kisha akamlalamikia Sam kwa kumdanganya. Sam alihofia kumweleza waziwazi kuwa walikuwa majambazi na tukio lao la mwisho kikazi zaidi walikumbana na binti safarini wakamteka na kisha kufanya waliyomfanyia.
“Ni kweli shem Don ni dereva wa magari makubwa, hilo la biashara alinionya nisikueleze, nasikitika nimepitiwa nimesema….” Sam akaupigilia msumari kisha akaupaka rangi uongo wake ukawa ukweli. Sarah akaamini!!
***
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
VIDOLE vyake vilikigonga kichwa chake mara tatu, kisha akaitoa miwani yake akaipangusa vyema na kuibandika machoni. Akaivuta meza yake ikatoa ukelele kidogo. Kisha akatoa bahasha yenye ukubwa wa A3. Kabla hajaifungua na kuitazama vyema akavunja kijiti kidogo na kujichokonoa meno yake kisha akabeua.
Akaivamia bahasha na kuigeuza chini juu, juu chini. Kila kilichokuwa ndani yake kikamwagika mezani. Zilikuwa picha nyingi sana zinazoelezea tukio moja matata sana la mauaji katika nyumba ya kifahari ya bwana Patrick Massawe aliyekuwa mbunge mtarajiwa.
Picha hizo ambazo zilihitaji Inspekta shupavu kama yeye kuzitazama zilipigwa na mpiga picha ambaye anajua haswa nini maana ya picha. Zilipigwa kwa umakini mkubwa na ukaribu wa kuridhisha!!
Akapitia moja baada ya nyingine.
Mh! Akakumbwa na mguno baada ya kukutana na picha ambayo ilikuwa tofauti, akaisogeza vyema machoni pake!!
Mwanamke amejilaza chini amekunja miguu yake katika mtindo wa ‘nne’ yaani paja moja limekaa juu ya paja jingine.
Inspekta akameza funda dogo la mate kisha akauingiza mkono wake katikati ya mapaja yake na kuyaweka mauongo yake sawa kwani tamaa zilishamwingia.
“Pumbavu yaani natamani maiti? Ila…. Ila alikuwa mrembo sana aisee…. Kwa hiyo huyu alikufa bila kuwa na jeraha ama?”
Akanyanyua simu yake ili amuulize anayehusika…. Baada ya kuingiza namba za muhusika na kupeleka sikioni hapo hapo simu yake ikaita, akashtuka na kutaka kuirusha kando, alipoitazama aliyekuwa anapiga ni mtu muhimu.
“Jambo Inspekta! Uchunguzi wa alama za vidole umeonyesha kuwa kuna vidole vya mwanamke katika miguu na mikono ya miili yote kasoro miili miwili tu, yule ambaye yupo hai na mwili wa yule msichana pekee katika tukio hilo…”
“Zuia miili isizikwe.. na yule fala anayesema Rensho Rensho ameweza kusema zaidi…”
“Hapana hajasema neno la ziada tena….”
Simu ikakatwa!!
“Mwanamke aue watu kinyama namna hii… mbona balaa hili..” alijisemea huku akirejesha zile picha katika bahasha.
Na huyu mwanamke ambaye hakuguswa ni kwa nini hakuguswa!! Wazo lilisafiri katika kichwa chake wakati anaufunga mlango wa ofisi yake, akaingia garini na kuendesha hadi hospitali ambayo maiti zilikuwa zimehifadhiwa zikiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Ilikuwa tayari saa tano asubuhi wakati anazima injini za gari yake mbele ya hospitali.
Maaskari waliopishana naye walisaluti, akazipuuzia salamu hizo akaenda moja kwa moja kwa askari mkuu wa ulinzi aliyepewa jukumu lile, akamwomba waongozane akauone mwili wa msichana asiyejeruhiwa.
Moyoni alitamani sana kuiona sura ya maiti yule ambaye alimsababishia matamanio katika picha na kusababisha mauongo yake muhimu kunyanyuka ghafla, pili alitaka kujua ni kwa nini hajadhurika hata kidogo, na tatu alihitaji kujua kama aliwahi kumwona mahali ama la kuikariri sura ile kwa ajili ya kuanza upelelezi mapema.
Waliongozana hadi mochwari baada ya klufuata hatua zote muhimu. Muhudumu wa mochwari akaliendea jokofu ambalo alikuwa amehifadhi ule mwili wa yule binti asiyekuwa na jina.
Akavuta kwa nguvu, akakutana na maiti nyingine tofauti akafunga upesi huku akidhani kuwa alikosea namba ya sanduku. Akaangaza huku na kule na kuvuta jingine huko napo akakutana na hali ileile ya mwili mwingine.
“Kijana unapoteza muda!!” Inspekta akakoroma huku akirusha mikono yake huku na kule. Yule kijana mwenye upara wa kimaskini akaendelea kuhaha bila mafanikio.
“Hayupo…. Hayupo pale alipohifadhiwa!!” alijibu huku akitetemeka.
“Hayupo! Una maana gani kijana, unaleta utani…utani na serikali.” Inspekta akatoa miwani yake usoni na kumkazia macho yule bwana aliyekuwa anatetemeka tu.
“Alikuwa sanduku gani?” Inspekta akamgeukia afande kwa swali lile, afande akanyoosha kidole kuelekea ile sehemu sahihi kabisa ambayo hata bwana kipara alikuwa anaamini.
“Na ni nani alikuwa zamu jana ya kulinda hapa..”
“Afande Christopher…” alijibu kwa nidhamu ya hali ya juu.
“Kahakikishe kuwa hayupo huyo maiti ili tumpigie simu Chris haraka….”
Askari akaruka hatua nne kubwa za kikakamavu akalifikia jokofu na kulivuta, Inspekta akimtazama kwa makini.
“Mamaaaa!!” akatokwa na ukelele mkubwa wa hofu!
Inspekta akasita kukurupuka, zaidi akajipa umakini.
“Ni nini…” akahoji huku mapigo yake ya moyo yakienda kasi sana.
Askari alikuwa anatetemeka bado huku ameyatumbua macho yake, mzee kipara alikuwa anashangaa tu!
“Askari ni nini hapo?” akakoroma tena.
“Afande… njoo ujionee afande…..”
“Nimekuuliza ni kitu gani hapo?” akakaripia.
“Afande… afande Christopher…”
“Whaaat!!!” akaruka na kulifikia lile jokofu, akakutana na mwili wa askari ambaye alikuwa anatokea kituo chake, alikuwa ametulia tuli ndani ya jokofu la kuhifadhia maiti na yeye akiwa maiti tayari.
Alikuwa ameingia sehemu ambayo awali alihifadhiwa mwanamke mapaja wazi asiyekuwa na jina.
“Hii inawezekanaje askari…”
“Sielewi hata kidogo afande!! Sielewi..”
“Weka walinzi wa kutosha hapa na kisha nimkute huyu sungura pori kituoni, upesi!!” aliamuru huku akimtazama mlinzi wa mochwari kwa jicho lililojaa chuki.
“Lakini mimi…afande….” Hakumalizia kauli yake akajikuta akiona maluweluwe kadhaa mbele yake. Alikuwa amepokea kofi barabara katika shavu lake.
Inspekta akatoka nje akiwa mwenye ghadhabu vilevile, akachukua simu yake na kubofya namba kadhaa.
“Upo nyumbani…..aah… sawa nakuja!!” akamaliza na kuirejesha mfukoni. Akachukua gari lake na kutoweka.
****
KATIKA kipindi cha miaka miwili ambayo wamekuwa katika mahusiano ya kiwiziwizi hakuna kipindi kigumu alichokuwa anapitia kama wakati huo.
Kuwachanganya wanaume wawili hilo kwake halikuwa tatizo hata kidogo kwa sababu penzi lake alilitoa kimasilahi zaidi na isitoshe kwa wakati huo alikuwa amebaki na mpenzi mmoja, lakini hii hali ya utofauti katika mwili wake ilimkosesha raha kabisa Maria.
Aliwaza nani wa kumshirikisha jambo hilo kwa ukaribu zaidi, aliamini kabisa hakuna hata rafiki yake mmoja awezaye kumvumilia na kumsikiliza kwa kina na kisha kumshauri vizuri.
Kwa ukaribu zaidi akamfikiria mama yake mzazi, mama Maria!
Akapanga siku hiyo aende kumtembelea nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Luis. Akajipanga kuanzia asubuhi kwa safari hiyo, lakini wakati anaanza kuvaa akapokea simu kutoka kwa Kisembe, hapakuwa na maongezi marefu. Kisembe alihitaji kuonana naye haraka iwezekanavyo hapohapo nyumbani kwake.
Utamu wa pesa za kuhongwa ukageuka uchungu katika hali hii hakuwa na lolote la kupinga, kwani alimjua vyema Kisembe asivyokuwa na dogo.
Maria akaketi kitandani na kuchukua kioo akaendelea kujipamba kiuchovuuchovu hadi hapo aliposikia mlango ukigongwa.
Akajongea kufungua, akaingia ndani bwana Kisembe kwa fujo akairukia midomo ya Maria iliyokuwa inameremeta!!
Maria akampokea kwa kujilazimisha mzee huyu. Wakakutanisha ndimi, wakakokotana hadi chumbani, Kisembe akamtupa Maria hapo na kisha akaanza kuyaondoa mavazi yake kwa fujo.
“Mpenzi….nipo katika siku zangu please!!” maria akasihi lakini Kisembe hakuacha kuondoa nguo zake.
Hakuna neno alilosikia kwa wakati huo, alikuwa amejiandaa kwa shughuli ile ya chumbani.
Maria alitaka kujieleza zaidi lakini Kisembe tayari alikuwa kifuani kwake akimtomasa huku na kule.
“Kisembe bwanaa… yatachafuka mashuka Kisembe acha!! Acha basiii” aliendelea kusihi Maria.
Kisembe mwenye nguvu akambana Maria na kuondosha nguo zake.
“Umeanza kunifanya mimi mtoto eeh… unadhani tarehe zako sizijui… haya kuna nini hapa….” Kisembe alimbana Maria kwa swali hilo.
Lahaula!! Maria kujitazama, hakika hakuwa na yale mauzauza ya kutokwa damu mfululizo. Kisembe hakumpa muda wa kushangaa akamvamia kwa fujo.
Alishaizoea sura ya Maria, haikumpa hisia tena. Akafumba macho na kujenga ile picha ya marehemu, lakini akajitahidi awezavyo zile damu zisiingie akilini mwake, alimsikia Maria akiguna tu kama kawaida yake wawapo sirini.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“N’talala hapa leo!!” baada ya kumaliza awamu ya kwanza Kisembe alimweleza Maria. Maria akajitetea kimahaba kuwa mama yake amemuita nyumbani hivyo lazima aondoke.
“nimesema nitalala, sio kwamba nitalala na wewe..” Kisembe akajibu kwa hasira kidogo. Maria akakubaliana naye, akaingia kuoga upya.
Kisha akamuaga na kutoweka!!
***
Alianza kwanza kuukosa usingizi akiwaza namna ambavyo maiti ya yule binti imetoweka hospitali, akawaza pia ni kwa namna gani yule askari wake mtiifu ameuwawa na kuwekwa katika jokofu bila mtu yeyote kugundua hilo.
Aligeukia tena upande mwingine, mara akajihisi kubanwa mkojo.
“Aaargh Maria naye na hili linyumba choo cha nje….mi sitoki, nakojoa katika beseni akija ataenda kumwaga…” alilalamika huku akisimama na kupapasa bila kuwasha taa. Akalipata beseni akaliweka katika mlengo sahihi, akaanza kumwaga haja zake.
Mkojo mrefu!
Mkojo gani huu! Alijiuliza huku akihisi waziwazi kuwa hakuna dalili ya mkojo ule kukatika, akajaribu kuubana lakini haikuwezekana. Akajisogeza akiwa na beseni lake katika kitufe cha kuwashia taa. Akawasha!!
Asalaale!! Beseni jeupe lilibeba mkojo mwekundu…. Haukuwa mkojo ule zilikuwa ni damu.
Macho yakamtoka pima Kasembe.
Akajitahidi kuzibana damu hizo zisimtoke, na hapo akaisikia sauti ile ya Maria iliyokuwa inamlilia kuwa yupo katika hedhi asimuingilie lakini hakukoma akamuingilia bila kuona japo chembe ya damu.
Kasembe baada ya kufanikiwa kuidhibiti ile damu kidogo, akavaa nguo zake hovyohovyo. Akatoka nje na kuingia ndani ya gari lake, nia yake ikiwa kuwahi huduma hospitali yoyote ile…
Haikuwa nyepesi kama alivyoweza kudhani!!
Asubuhi ya siku iliyofuata taarifa za kustua nchi zikatapakaa.
Inspekta Juma Kisembe amekutwa amekufa baada ya kuvuja damu nyingi akiwa ndani ya gari lake kando kando ya barabara ya Mandela jijini.
Inspekta alikuwa akivuja damu katika sehemu zake za siri!!
Kifo kama cha mume mwenzake kwa binti Maria, Dennis!!
***
MWANDISHI AJIINGIZA KWENYE UTATA WA HOFU!!
EBOLA….. watafiti wakatoa taarifa kuwa Inspekta Kisembe amekufa kutokana na ugonjwa huo.
Ebola? Vyombo vya habari vikahoji!!
Ebola gani hiyo iliyomtoa damu sehemu moja tu!! Ebola humfanya mgonjwa avuje damu katika kila tundu lililopo katika mwili wake.
Hii Ebola ya Inspekta mbona ya aina yake!!
“Kwa hiyo tuwatangazie wananchi kuwa kuna mlipuko wa gonjwa hilo hatari!!” mwandishi wa habari akamchimba msemaji wa jeshi la polisi.
“Kutokana na taarifa ya daktari amesema yawezekana ni Ebola maana ugonjwa mwingine haujaonekana…”
“Lakini hata Gonorea nayo humtoa mtu damu mkuu, huoni taarifa ya gonjwa la ebola bila kuthibitishwa ni sawasawa na kuwajengea wananchi hofu makusudi!!” mwandishi akamchimba zaidi, kisha bila kumpa muda wa kujibu akaongezea jingine, “ na hawa wenzetu akiwemo bwana Patrick Masawe na wao wamekufa vifo vya aina hii… na hadi sasa maiti hazijakabidhiwa kwa ndugu na kilichowaua hamjakisema wazi, mbona hiki kifo cha mzee Kisembe ufumbuzi wake umepatikana upesi sana mheshimiwa?” mara simu ikakatwa!!
Mwandishi hakujisumbua kupiga tena maana alijua imekatwa maksudi na hata mpata hewani tena msemaji huyo aliyezidiwa na mzigo wa maswali ya kuthibitisha uhakika wa kifo cha inspekta Kisembe.
Hiyo ilikuwa kawaida ya wakubwa wakiulizwa maswali magumu!!
Mwandishi yule akajinyoosha katika kochi alilokuwa amekaa, kisha kitu kikamkuna ghafla kuwa asipuuzie tukio hilo la inspekta kufa katika hali ya kustaajabisha.
Akautazama ukuta kisha akafumba macho baada ya kuiona picha kubwa ya msichana mrembo kiasi ambaye amepauka haswa. Mwandishi akamkumbuka Nadia, akaukumbuka mkasa wa Usilie Nadia ulivyokuwa wa kusisimua, kitabu chake ambacho kilimpeleka Musoma na kisha kuishia Mwanza.
Akageuka upande mwingine akakutana na picha nyingine iliyobuniwa haswa na kupendeza, maandishi yakasomeka ‘Anti Ezekiel.’ Akalikumbuka tukio hili katika hekaheka zake za uandishi.
Tukio ambalo almanusura liondoke na uhai wake, badala yake mkewe na mama yake mzazi wakapotelea katika tukio hilo.
Tukio hilo la kugundua mkakati kabambe wa kuusambaza ushoga katika nchi ya Tanzania kwa kuwateka watoto wadogo wa kiume kisha kuwahifadhi katika ngome iliyojengwa ardhini na kuwafundisha tabia za kishoga.
Ufumbuzi huu ulimfanya kuwa mtu maarufu na wa kuheshimiwa!!
Akainama chini na kuzidi kuwashwa kufuatilia tukio la kifo cha inspekta wa polisi na watu zaidi ya kumi na tano. Wote kwa kutokwa damu nyingi!!
Lazima kuna kitu hapa!! Aliwaza Gerlad Getonga, mtunzi wa vitabu vya Usilie Nadia na kisha akaandika kitabu cha kihistoria kile cha Anti Ezekiel, mkasa wa kweli kabisa uliotaka kuondoka na roho yake huko Iringa.
Alitamani sana kumshirikisha mkewe Anitha, lakini akatambua kuwa lazima atakutana na vikwazo vikali, kwa sababu tukio la Michigan ambapo mkasa wa Anti Ezekiel ulimalizia wote waliponea chupuchupu.
Getonga akaitazama picha ya Eva mtoto wake, machozi yakamlenga lenga alipofikiria kuwa atamuacha kwa muda wakati akilifuatilia kwa ukaribu tukio hilo.
“Hapa hakuna hatari yoyote bila shaka ni katukio kadogo tu..” alijipa moyo huku akipita maamuzi ya kufuatilia mkasa huu tofauti na waandishi wengine!!
Getonga akaondoka bila kuaga, tayari alikuwa na vifaa vyake muhimu kwa ajili ya kazi hiyo.
Laiti kama angejua kuwa tukio lile sio dogo kama adhaniavyo ni heri angejiepusha nalo!!!
Hakujua kuwa madhara yake ni ya papo kwa hapo zaidi ya yaliyomkuta wakati akifuatilia mkasa wa Anti Ezekiel.
Akajiingiza kichwakichwa pasi na hofu yoyote!!
****
Alikuwa amejitahidi na kuachana na matumizi ya sigara, lakini pombe hakuweza kuiacha. Angalau kwa siku chupa mbili kwa ajili ya kuichangamsha akili yake kisha anaendelea na mambo mengine halafu jioni anajumuika katika vijiwe vya kahawa.
Jioni hii akiwa amemaliza mizunguko ya siku hiyo akitumia usafiri wa pikipiki binafsi alikuwa amevuna mambo kadhaa ambayo yalimpa mwanga juu ya wapi anaweza kuanzia.
Katika daftari lake dogo akaandika mambo hayo kwa ufupi sana. Ambapo yeyote hata mkewe akilikwapua daftari lile hakuna ambalo angeweza kuambulia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kindo- Mwendawazimu anayetamka neno moja tu! =Rensho. Huyu SIMJUI
Maria- inasemekana alikuwa hawara yake Inspekta. =SIMJUI
Sarah- Rafiki kipenzi wa Maria. =SIMJUI
Kijana- alionekana katika nyumba ya Maria usiku. =SIMJUI
“Kila mtu simjui! Duh pagumu hapa” Alijikuta akisema kwa sauti ya juu.
“Unataka kumjua nani?” sauti ya Anitha ikamkurupua kutoka katika mawazo yake.
“Baba naye kwa kuongea mwenyewe loooh!!” sauti ya kitoto ya Eva ikapeperusha swali la Anitha, wakajikuta wakicheka huku wakimtazama Eva akijifinyafinya uso wake.
Getonga akarejea katika mawazo yake tena!! Akalitazama daftari lake na kuendelea kusoma.
Deniss- alikuwa hawara wa Maria. =AMEKUFA!!
Inspekta Kisembe- alikuwa hawara wa Maria. = AMEKUFA
“Mahawara nao wote wamekufa!! ” akajiuliza safari hii hakutoa sauti nje.
Kuna kitu hapa!! Akamaliza kwa kujipigia makofi, Eva na Anitha wasijue lolote linaloendelea.
Usiku huu ukapita Getonga akijipongeza kwa kujua mambo kadhaa ambayo hakuyajua.
Asubuhi alichelewa kuamka!! Na alipoamka alikutana na mkewe akiwa anacheka.
“Nini tena wewe kucheka asubuhi asubuhi..”
“Waandishi mna mambo nyie dah siwawezi. Ila nashukuru hata ulivyojiweka mbali na mambo hayo.”
“tumefanya kituko gani tena.”
“Si mwili wa Inspekta huyu aliyekufa kwa ugonjwa wa Ebola….”
“Nani, Inspekta Kisembe ama…”
“Ehee huyohuyo… eti nimesikia magazetini kuwa kuna raia wanadai kuwa marehemu amekutwa na maneno gani sijui kwa hiyo inasemekana ni u-freemanson umemuua dah!! Maiti hana la kujitetea kwa kweli…” alisema haya huku akiwa bado anatabasamu.
“Maneno tena? Wapi” Getonga aliendelea kuhoji kwa shauku.
“Rensho sijui Renshi…ila wamesema ni jina lenye herufi sita kwa hiyo ni Freemason…. Kweli hamna dogo waandishi…”
Gerlad Getonga akauficha mshtuko wake, akaguna na kuendelea na shughuli za kusafisha kinywa chake.
Rensho!! Hilo neno nimewahi kulisikia wapi? Akajiuliza kimya kimya huku akitamani kujiandaa upesi akanunue hilo gazeti linalodai kuwa Inspekta alikutwa na alama.
Baada ya kuoga alirejea chumbani, akachukua kidaftari chake kidogo
Mstari wa kwanza kabisa wa harakati zake akakutana na neno.
Kindo- chizi anayetamka neno Rensho pekee.
Upesi akaongezea maneno chini yake.
Rensho ni nani? Kisha akakihifadhi tena.
****
Gari dogo aina ya Toyota Carina lilisimama katika maegesho ya magari yasiyokuwa rasmi maeneo ya Kariakoo mtaa wa gerezani. Vioo vikashushwa na aliyekuwa anaendesha gari hilo.
Akaangaza huku na kule akiwa ameinyoosha shingo yake akaona alichohitaji kukiona, kisha akairudisha gari nyuma kidogo akaiingiza barabarani. Akaendesha kwa muda mfupi akafikia sehemu ya kuosha magari!!
Akaliacha gari likiwa linaoshwa pale, akaingia mtaa wa tatu kutoka pale. Akaifikia nyumba ambayo siku iliyopita alielekezwa kuwa Maria alikuwa anaishi pale. Akiwa na kofia yake ya pama kichwani akajiundia uenyeji, hakutaka kumuuliza mtu yeyote yule juu ya mahali anapoelekea.
Akaufikia mlango na kuanza kugonga! Hakupata majibu na bado hakukata tamaa akaendelea kugonga kama yu mwenyeji sana wa eneo lile.
Baada ya kujihakikishia kuwa hakuna mtu wa kuufungua ule mlango, mwandishi huyu mashuhuri Gerlad Getonga akaamua kukishusha kitasa ili ahakikishe kuwa Maria aliufunga kabla hajaondoka. Mlango ukafunguka, akatazama kushoto na kulia. Hapakuwa nna mtu anayemtazama, akaanza kuita jina la Maria huku akiingiza kichwa chake ndani katika mfumo wa kuchungulia.
Chumba hakikuwa na mwanga sana, lakini kile kitendo cha kuufungua mlango tu na kuangaza huku na huko akakutana na kitambulisho. Upesi akainama na kukikwapua kisha akauegesha mlango tena na kutoweka akiwa anajiamini kabisa ili kuleta imani kwa yeyote yule ambaye atakuwa amemtazama.
Hakujua kwa nini amechukua kile kitambulisho na hakujua ni cha nani lakini huo ukawa mwanzo wa hekaheka ya ajabu kabisa!! Lakini hakujua kuwa alichelewa sana kugundua.
****
HAKIKA alionekana kama mwendawazimu!
Jinsi alivyovaa, jinsi alivyokuwa akihangahika kuchorachora huku na huko. Mwanamama mtu mzima alikuwa jirani na kijana huyo.
Gerlad Getonga akawasalimia wote wawili. Kabla mama hajajibu, yule mwendawazimu kimtazamo akaropoka maneno ambayo yalikuwa muhimu sana kwa Getonga.
“Rensho….Rensho!!”
Getonga akatikisa kichwa kisha akamsalimia mama tena, mama akajibu kwa upole kabisa akiwa na dalili zote za kukata tamaa.
“We nawe unataka unisumbue na maswali kama wenzako halafu upotee usirudi tena… hamna la kunisaidia nyie watu sijui waandishi” alilalama baada ya Getonga kujitambulisha kuwa ni mwandishi wa kujitegemea na anataka wazungumze naye juu ya tukio lilomsibu mwanaye.
Jibu lile lilimkwaza lakini alitumia utashi wa hali ya juu kumshawishi yule mama mzazi wa kijana aitwaye Kindo kuzungumza naye.
Ukumbi ukabaki kuwa wa mama Kindo
“Najuta kuitwa mama, lakini mbaya zaidi najuta kuzaa kisichokuwa chema!” akasita kisha akakaa sawa na kuendelea, “Kindo hakutaka kunisikiliza mimi, kaamua kufunga ndoa na huyo Rebeka sijui. Nikamkataza katakata na kumweleza wazi kuwa binafsi sijaridhia suala lake la kumuoa huyo binti na kuachana na Salome. …..” mama akasita tena na kumgeukia mwanaye aliyekuwa akitazama kitu asichokijua.
Kindo asiyesema neno zaidi ya ‘Rensho’ alikuwa anatetemeka huku akiwa amekodoa macho yake, Getonga naye akafuatisha macho ya mama ana wote kusaidiana kumtazama Kindo.
Amekuwaje huyu naye!! Mama mtu alijiuliza.
Na hapo likatokea tukio la ajabu kabisa liliwaduwaza wawili hawa. Kindo akaanza kuzungumza!!
“Mpe….mpe… mpe upesi…mama mpeni…mpeni mama.. kaka mpe upesi.” aliyasema haya huku akimtazama Getonga…. Badala ya kushtuka Getonga alifanya tabasamu, kwani aliamini kuwa Kindo ameanza kurejewa na fahamu zake tena, hivyo atanufaika naye hasahasa kwa kufanya mahojiano na mwanadamu pekee aliyetoka akiwa hai katika tukio la kustaajabisha na wanadamu zaidi ya kumi na nne kuuwawa kinyama na kilichowaua kisijulikane popote.
“Mama, wakija waandishi wengine usiwaruhusu kuongea na Kindo sawa.. watamvuruga akili yake. Mimi kama nilivyokwambia nina nia ya kukusaidia.
“Sawa mwanangu… nita…” mama akakatishwa na kelele za Kindo tena, “Mpe upesi nasema.. mpe kama kipo.. mpe..” alitoa karipio Kindo, Getonga akatabasamu huku akizidi kuamini kuwa ni fahamu zinamrejea Kindo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Na hekaheka za kukata na shoka zikaanzia hapa!!
Kindo akamvagaa na kumwangusha chini huku akimkaba kwa nguvu sana shingo yake huku akimsihi kwa maneno hayohayo kuwa ampe kama kipo.
Getonga akakakamaa na kujitoa katika mikono ya ya Kindo kwa juhudi zote, akahema juu juu huku akimtazama Kindo na kutoamini kitu kilichotokea. Kabla hajapumua vizuri na kujiweka sawa tena mara alimwona Kindo akizidi kuyakodoa macho, halafu akaanza kukifuatilia kitu ambacho Getonga hakukiona.
Na wakati huo alimuona mama yake akiingia ndani!!
“Mpe kaka.. mpe …mpe anaomba …mpe…” aliyasema haya kwa sauti ya chini, Getonga hakuelewa kitu. Lakini sasa alikuwa ameanza kuingiwa na hofu!!
Wakati huohuo zikasikika kelele ndani ya nyumba ya mama yake Kindo, alikuwa akilia kuomba msaada. Getonga akatoka mbiombio mpaka ndani kutazama kulikoni. Hapakuwa na kelele tena.
Akakutana na sebule isiyotamanika kuitazama, hata kama ni filamu ya kutisha lakini hii ilikuwa maradufu.
Kichwa katika stuli, mguu mmoja ukining’inia darini, paja likiwa sakafuni, na..na…….
Ilitisha kutazama vinginevyo. Damu mbichi ilikuwa imetapakaa!!
Mama Kindo alikuwa ameuwawa kinyama ndani ya sekunde kadhaa!!
Riadha aliyotimka Getonga mwenye kitambi cha pesa hakuwahi kukimbia namna ile, alijikwaa akaanguka akasimama, akaongeza mwendo. Akapotea njia na kujirekebisha tena, akajitapikia lakini hakujali!!
Kila aliyemtazama alihisi kuwa yawezekana ni kibaka ama anayerukwa na akili. Lakini hakuna aliyemjali, kila mmoja alikuwa na shughuli zake.
Hii ikawa siku ambayo Getonga asingeweza kuisahau aidha kwa kuishi ama kwa kuwa kuzimu.
Ukawa mwanzo wa moyo kudunda kwa kasi kila mara, mwanzo wa kuikosa amani ya nafsi na mwanzo mwingine wa kuishi kama kivuli, kivuli kinachoogopa na kuogopwa pia!!
Mwanzo wa kujutia maamuzi!!
*
***
MBIO kali za Getonga ziliishia katika teksi ambayo ilimpeleka nyumbani kwa Maria. Safari hiii hakujali iwapo kuna watu wanamtazama ama la! Aliufikia mlango moja kwa moja na kugonga kwa fujo ili aweze kufunguliwa.
Badala ya mlango kufunguliwa alishangaa kusikia kitasa kikifungwa.
Yumo! Alijisemea na hapo hapo akausukuma kwa nguvu mpaka ndani. Akamkuta Maria akiwa ametaharuki na akiwa ameanguka chini baada ya kusukumwa ghafla bila kutarajia, alikuwqa amenyanyua mikono yake juu kama anayesihi na kuomba msamaha.
Kwa mawazo yake aliamini kabisa kuwa mbele yake alikuwa ni askari.
“Maria…..” Getonga akamwita huku akiwa anaurudishia mlango vyema. Maria hakuitika na badala yake aliendelea kutetemeka tu .
“Nini kinatokea hapa Maria….mimi ni mtu mwema huna haja ya kuogopa.. nahitaji kuzungumza na wewe Maria…” Getonga aliendelea kusihi huku akiwa anamkazia macho Maria ambaye alikuwa akitazama beseni, macho ya Getonga yakahama na kulifikia lile beseni.
Macho yakaongezeka ukubwa wake kwa sababu ya kukodoa.
“Maria, damu za nini hizo ndani ya chumba chako…. Maria ni wewe unaye… ni wewe Maria…..” Getonga alisema kama anayesuta…. Maria akapata nguvu ya kuzungumza.
“Sijui lolote kaka yangu… sijui nd’o nimeingia hapa ndani… sijui kitu..” alijitetea huku akisimama na kuketi kitandani….. kisha akaendelea, “Kama utaamua kunikamata, utakuwa tu umeamua kakangu, yaani mimi sijui lolote lile nimeingia humu ndani na kuikuta hali hii, haki ya Mungu naapa.” Alijitetea huku sauti yake ikitetemeka.
“Maria, sijaelewa kitu hebu niambie ni kitu gani kimetokea hapa kwa ufupi maana mchana nimeukuta mlango huu ukiwa wazi. Ni nani alikuwa humu ndani? Ukweli wako utakuweka huru..”
Maria akajikuta katika kilio cha kimya kimya kisha akajikaza na kuzungumza, aliamua kuzungumza ukweli kwa sababu alikuwa matatani tayari katika jambo asilolijua hata kidogo.
Akauelezea ujio wa inspekta Kisembe nyumbani kwake pia akaielezea hali yake ya kuvuja damu bila kikomo na maajabu yaliyotokea baada ya kukutana na Kisembe.
“Yaani ilikuwa ajabu, wakati natarajia kuaibika mbele ya Kisembe na kisha kuchafua mashuka nikajikuta nipo sawa kabisa bila hata tone la damu……” akaendelea kujieleza hadi jinsi alivyoondoka na kumwacha Kisembe mle ndani na hapo aliporejea nd’o anakutana na hali hiyo ya damu kuwa katika beseni lake la kuogea.
Getonga alimsikiliza kwa makini huku mapigo yake ya moyoi yakiongeza kasi na wakati mwingine kupungua, hasahasa alipokikumbuka kifo cha kutisha kupita vyote alivyowahi kuvishuhudia.
Kifo cha mama Kindo!!
“Na unamfahamu vipi Samson? Na mara yake ya mwisho kuja hapa ni lini..”
“Sam ni mpenzi wangu pia, ana majuma matatu tangu aje hapa mara ya mwisho…angeweza kuja siku za hivi karibuni lakini alipata janga la kuwapoteza rafiki zake wawili, afande huwezi amini kuwa na hao rafiki zake wamekufa kwa kupoteza damu….”
“Unamaanisha wamekufa kama Inspekta Kisembe sivyo?” Getonga akakolezea.
“Nini? Inspekta amekufa? Lini? Wapi eeh!! Mungu weee!!” Maria alitaharuki kusikia taarifa hiyo kwa mara ya kwanza katika masikio yake. Akahaha huku na kule, Getonga akamtuliza na kisha kumpa hali halisi juu ya tukio hilo la maajabu.
“Maria, nahitaji kuonana na Sam usiku huu huu… hii hali si ya kawaida na ni lazima jibu lipatikane upesi kabla mauaji hayajaendelea. Ninauhitaji sana ushirikiano wako” Getonga akamsihi Maria kwa upole sana.
Wakaelewana nna kuondoka wakiiacha ile damu ikiwa palepale. Wakaufunga mlango kwa kitasa.
****
CHUMBA kilionekana kidogo na godoro alilozoea kuliita mke wake wa pili lilionekana kumkera siku hiyo, halikuwa laini kama siku zote na halikunesanesa.
Alijigeuza huku na kule ili aupate usingizi lakini hali ilikuwa tete. Hakuupata usingizi.
Kila alipofumba macho alikutana na picha ya ajabu sana mnachoni mwake, damu nzito katika beseni!! Chumbani kwa mpenzi wake wa siku nyingi.
Na kwa jinsi alivyozizoea damu, alitambua mara moja kuwa ile ilikuwa damu ya mwanadamu. Swali moja likabaki kumuumiza kichwa, ni mpenzi wake ameuwawa ama ni yeye ameua. Wakati anataka kulipuuzia hili inakuja picha ya yule dada wa kubakwa na akina hayati Don na Deniss.
Sam akaukosa utulivu, akasimama na kuliendea jokofu akachukua maji ya baridi, akaketi katika sofa na kuamua kuwasha luninga aweze kutazamna mawili matatu.
Mlango wake ukagongwa!!
Askari! Akajiweka katika tahadhari kubwa na kisha kujutia maamuzi yake ya kuamua kulala nyumbani kwake siku hiyo. Upesi akaupeleka mkono wake kiunoni na kuitoa bastola yake.
“Sam…..” sauti ya kike ikaita. Akaitambua mara moja kuwa ilikuwa ya Maria!! Lakini hakufanya papara kufungua mlango, akaendelea kuvuta subira. Alitambua fika kama ni Maria kweli basi atajua la kufanya ili aingie ndani. Hakika ndani ya sekunde kadhaa mlango ukafunguliwa.
Maria alikuwa na funguo za ziada!!CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sam kutokea katika eneo la uficho akatambua kuwa Maria hakuwa peke yake. Jambo ambalo lilimtatiza, na ghafla akakurupuka akiwa na bunduki yake mkononi akawaelekezea wawili wale.
Maria akazungumza kwa niaba ya Getonga, akaelezea kwa ufupi juu ya ujio wao. Sam akaridhika na mazungumzo yake akaitua bastola yake na kuungana katika mazungumzo yenye amani tele.
Sam akasimulia tukio la kubakwa kwa binti wakiwa katika shughuli zao za kinyang’anyi, akaelezea matukio yaliyofuata baada ya hapo kwa rafiki zake kupoteza uhai katika namna ya kustaajabisha.
“Mbaya zaidi hata mzee Yakuza naye alikutwa amekufa..”
“Yakuza nd’o nani?”
“Huyo nd’o aliyetuagiza tumuue yule binti…”
Ni kwanini aliwaagiza mfanye vile labda..”
“Hakika hatukumuuliza maana kazi yetu sio kujua bali kutenda tu!!”
“Getongaaaa!! Getongaaaa!!!........” sauti kali kutoka nje ikasikika, Sam akagutuka kwa kudhani wamezingirwa na maaskari. Akaikwapua bunduki yake na kumwelekezea Getonga. Upesi akanyanyua mikono juu kwa usalama wake., Maria aliduwaa asijue nini kinaendelea.
Na mara ukaanza kuvuma upepo wa maajabu, upepo unaoleta kero ya joto badala ya kuleta ahueni ya ubaridi.
“Mpatie anachotaka!!” sauti ikasikika tena. Wote mle ndani wakatazamana.
“Sam, huna haja ya kutumia bunduki yako, si mimi, wewe wala Maria anayejua nini kinaendelea hapa…..” Getonga akamuonya Sam. Akaishusha bunduki yake.
Mara vikasikika vishindo kutoka chumbani, wakastaajabu tena. Sam akaiweka sawa bunduki yake na kuelekezea katika korido inayotokea chumbani.
Maajabu ya mwaka!!
Akatokea mtoto mdogo ambaye ni Getonga pekee alikuwa anamtambua.
“Babaaaa…. Mpatie aniache mi sipapendi huko baba. Babab mi nataka kwenda shule sitaki hukooo anaponipeleka baba…” sauti ya kitoto ya Eva ilizungumza na baba yake ambaye alikuwa amekodoa macho tu.
“Babaa…” Eva alisihi tena.
“Anataka nini… na ni nani? Eeh nani….” Aliuliza kwa pupa.
Badala ya kupata jibu, upepo ukaanza tena kuvuma, ukalifunua gauni la Eva na kisha ukavuma zaidi na kumwangusha Eva chini!!
“Mamaaa!!” sauti ya Eva ikasikika kwa mara ya mwisho katika masikio ya Getonga!!
Upepo ukakoma, na hapo ukaanza msako wa kumtafuta Eva ndani ya kile chumba. Walimtafuta hadi katika kabati la vyombo na chini ya viti lakini hakuwa Eva, sauti yake wala gauni lake.
Getonga alipagawa haswa!
Ndani ya muda mfupi aliojiingiza katika tukio asilolijua anakumbana na mambo mazito ya kutisha.
Simu yake yta mkononi iliita na kumrejeshea fahamu kuwa alikuwa hajaishika kwa muda mrefu.
Alikuwa ni mkewe!!
Akaipokea upesi upesi!!
“Nikimpiga mwanao usinilaumu!!” sauti ya Anitha mkewe ilisema kwa kiburi.
“Amefanya nini tena….”
“Mimi naandaa chakula mezani yeye ameenda sijui wapi kucheza na hadi sasa hajarudi. Mi leo namchapa kwa kweli…”
“Alikuaga na kukwambia anaenda wapi…”
“Kaondoka na watoto wenzake hapa na hajasema hata anapoenda..” alizidi kulalamika Anitha, kisha akasita na kugeuza mazungumzo, “we nawe mbona unahema juu juu kwani ukwapi hadi muda huu…”
“Nipo hapa wapi hapa….najiandaa kuja nyumbani…” alijiumauma. Anitha akakata simu!!
Getonga akaketi chini kama zoba, jasho likiwa linamtoka kwa wingi!! Eva wake alikuwa matatani huku akimsihi kitu asichokijua!! Ile sauti ya Eva kulalamika kuwa anataka kusoma hataki kwenda huko kwingine ilizidi kumpagawisha!!
Majuto yakaanza kujengeka katika fikra zake.
Akajuta kuwa kiherehere!!
“Sam, kesho nitakuja na gari langu twende pamoja hadi huko lilipotokea hilo tukio labda japo sidhani lakini twende labda itasaidia. Kumbuka hili ni kwa ajili yetu sote, wewe unasakwa na polisi na pia kusumbuliwa na sura ya huyo binti katika fikra zako, pia Maria unavuja damu bila kikomo. Halafu mimi kama mlivyoona kwa macho yenu waziwazi nimempoteza mtoto wangu wa pekee. Eva! Kwa hiyo hili sio jambo la kupuuzia hata kidogo.” Getonga alisihi kisha akaaga.
Maria akataka kuondoka naye, Sam akamzuia na kumsihi walale wote maana anaogopa sana. Maria akakubali!!
Lakini wakakubaliana kuwa hawatalala katika nyumba ile bali nyumba ya kulala wageni. Hii ni kutokana na tukio la mauzauza lililojitokeza. Hawakuwa wapenzi bali mtu na shemeji yake lakini hawakujali kuhusu hilo
Wakakubaliana kukutana siku iliyofuata saa tatu asubuhi kwa ajili ya safari!!
***
WANGEUPATA vipi usingizi wakati mtoto wao haonekani? Anitha alimlaumu Getonga kuwa kwa kuchelewa kwake basi mtoto akawa huru sana na kwenda anapotaka, Getonga hakutaka kujitetea maana alimjua vyema mkewe.
Walihangaika huko na huko bila mafanikio, Getonga hakusema lolote juu ya yale mauzauza kwa kuhofia kumpoteza mkewe kwa shinikizo la damu. Hata katika kituo cha polisi hakusema lolote juu ya yale mauzauza.
Kitandani Anitha alimgeuzia mgongo mumewe na hakutaka kuguswa hata kidogo, aliendelea kulalama huku akimmwagia lawama Getonga, sasa akaenda mbali zaidi na kudai mumewe ana hawara huko nje na hii nd’o mikosi.
Getonga alijisikia hasira kali sana lakini hakutaka kujibu mapigo kwa kuhofia kuipoteza amani kidogo iliyobaki kwa ukimya wake.
Usingizi ukampitia Anitha na kuleta amani kidogo kwa Getonga! Akabaki na maswali mawili tu, asubuhi kuendelewa kumsaka Eva kwa kuzuga ama aandamane na Sam kuelekea eneo la tukio.
Usingizi ukampitia bila jibu!!
Asubuhi akawahi kuamka ili kumkimbia Anitha kitandani. Akaenda sebuleni na kywasha runinga. Hakuwa na la kuangalia kwa muda ule lakini alifanya kama geresha tu.
Anitha aliamka na kiburi chake kama kawaida, akamsalimia mumewe huku ameuvuta mdomo na masikioni akiwa amepachika ‘earphone’!! Getonga akatabasamu bila kujibu chochote.
Anitha akiwa chumbani akajisikia vibaya kuipoteza amani ndani ya nyumba. Akaona hakuna maana kumkasirikia mumewe kwa tukio la kupotea mtoto.
Ataanza vipi kuzungumza naye sasa?
Akakumbuka taarifa aliyotoka kuisikia katika redio yake aliyokuwa nayo masikioni muda wote. Akakiendea kioo na kuunda tabasamu lake mwanana, kisha akaenda sebuleni huku mapigo ya moyo yakimwenda mbio.
“Waandishi yawezekana mpo sahihi eeh!” akaanzia hapo, Getonga akamtazama, akaendelea. “Kafa mwingine na chata ya Inspekta, mwaka huu freemason lazima watumalize….”
Getonga akavuta umakini. Anitha akajisogeza karibu yake na kumsimulia tukio jingine la mtu kufa kimaajabu kwa kuvuja damu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hebu ngoja umesema ni redio Tumaini ndo wametangaza… ngoja hebu..” Getonga akachukua simu yake na kumpigia rafiki yake aliyekuwa anafanya kazi katika kituo hicho cha redio. Akamuuliza juu ya ukweli wa habari hiyo.
“Taarifa imeletwa na muhudumu wa hoteli fulani hivi na kisha kuthibitishwa na polisi juu ya tukio hilo. Maajabu zaidi aliingia na mwanamke lakini amekutwa akiwa peke yake. Ni balaa kaka..” alijieleza wakati huo simu ikiwa katika spika za nje. Wakisikiliza wote wawili.
“Wamekuta kitambulisho cha mwanamke huyo ambaye sasa ndo anatafutwa… anaitwa Maria Paul…”
“Whaat!!!” akashtuka Getonga.
“Unamfahamu ama?” Anitha akauliza.
“Ahhmm! Jina sio geni hilo….” Akajibu kwa hofu Getonga.
Wivu!! Wivu ukajitundika katika moyo wa Anitha. Akaondoka bila kuaga, amani ikatoweka tena!!
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment