Search This Blog

Wednesday, 1 June 2022

IT'S HAPPENING - 3

 







    Simulizi : It's Happening

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Siku ya usaili ilifika na watu wengi kutoka sehemu mbali mbali walijitokeza kujaribu bahati zao. Hussein na rafiki yake waliwasili na kupanga foleni ili na wao wakajaribu bahati zao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zamu ya hussein kuingia kwenye chumba hicho kilichopambwwa vizuri kwa ustadi na hewa mwanana ya air condition ikileta kiubaridi mule ndani. Camera nyingi zilikizunguka kile chmba.

    Majaji watatu walikuwepo. Vicenti kigosi, Wema Sepetu wakiongozwa na chief judge wao Jaqueline Wolper ndio walio simamia zoezi zima.

    “action”

    Hiyo kauli alipewa Hussein baada ya kuingia tu mule ndani. Moyo ulimuenda mbio sana baada ya kumuona mama yake pale mbele. Alishindwa kufanya lolote zaidi ya kumtazama huku machozi yakianza kumlenga lenga.

    Majaji walishangaa kumuona mshiriki huyo ambaye waliamini labda hajui hata maana ya action.

    “action maana yake kitendo…. Haya kwa Kiswahili, anza.”

    Aliongea Vicenti Kigosi na kuwafanya majaji wenzake kucheka.



    Hussein hakuweza kuvumilia, machozi ya uchugu yalimtoka na kutolewa na mabaunsa waliokuwa wakilinda usalama baada ya kuambiwa atoke bila ya yeye kutii amri hiyo.



    Hussein alitolewa nje na kila mtu aliyekuwa kwenye usaili ule alimshangaa kumuona analia kwa kwikwi huku mabaunsa wakimsukuma ili aondoke eneo lile.



    Hakujua kwa nini ilimtoke hali kama ile, ila uchungu wa mama yake ambaye alionekana kama binti mdogo kabisa kutokana na mavazi na muonekano wake, basi machungu ya maisha magumu anayoyaishi ndio sababu iliyomfanya ashindwa kujizuia na badala yake kumwaga machozi hadharani.



    Aliondoka Hussein na kurudi chumbani kwake. Alijitupa kitandani na roho yake ilikuwa na nyakati mbili tofauti kwa wakati mmoja. Kwanza moyo wake ulimuuma baada ya kugundua kuwa mama yake hamjui kabisa, pili yeye binafsi alifarijika kumuona mama yake kwa mara ya kwanza. Alitegemea kushinda lile shindano ili awe karibu na mama yake. Ila hali ambayo hata yeye alishindwa kuizuia ilimjia na kumfanya ashindwe kufanya lolote.



    Baada ya masaa matatu, Rafiki yake alirudi huku akiwa na furaha baada ya kufanikiwa kupita kwenye mchujo wa kwanza.



    “niambie mwana.” Alisalimia Hussein baada ya kumuona rafiki yake akiwa na furaha kupita kiasi.

    “nimepita mwanangu, hapa nilipo nimefarijika maana katika watu ishirini waliotakiwa kwa mchujo wa kwanza nimebahatika kuwemo.” Aliongea rafiki yake huyo.

    “mwanangu nahisi halikuwa zali langu.” Aliongea Hussein kwa uchungu.

    “hata mimi mwenyewe nilishangaa jinsi ulivyotolewa wakati tulipokuwa tizi tulikua tunakamua vizuri tu.” Aliongea rafiki yake huyo bila kujua ni jinsi gani alikua anamuumiza Hussein.



    “sidhani kama Robby unaweza kuamini nitakacho kuambia.. Jaqueline Wolper ni mama yangu mzazi kabisa.” Aliongea Hussein na kumfanya Robby acheke.

    “mwanangu punguza stress, maana naona mpaka unataka kuchanganyikiwa.” Aliongea Robby huku akionyesha wazi kuwa maneno ya Hussein hayakumuingia akilini kabisa.



    “ukubali ukatae, ila ipo siku utakuja kuamini nikuambiacho.” Aliongea Hussein na kumuangalia Robby ambaye alikua anavua viatu vyake na kuchukua ndala.

    “ngoja nikaoge, maana wewe huna jipya zaidi ya kupigana fiksi tu hapa. Mwenyewe akihojiwa anamtaja mtoto wake wa pekee wa kike Miss Belinda. Sasa wewe wa wapi?” aliongea Robby na kutoka nje.



    Jina la Belinder lilimjia kichwani na kumkumbuka dada aliyekutana naye kule kariakoo siku za nyuma. Kwa mbali picha ilimjia kwa jinsi binti huyo alivyokuwa mweupe na anayotaka kufanana na Jackline Woliper.



    Hapo hakubisha. Alijua kuwa yule msichana atakua ndie motototo wa mama yake tu ambaye Africa nzima inamtambua mtoto huyo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alilala na kumsubiri rafiki yake atoke bafuni ili amuulize jinsi huyo mtoto wa Jackline Wolper alivyo.

    “sasa, unaweza kunielekeza jinsi huyo mtoto wa Wolper alivyo?” aliuliza Hussein baada ya Robby kutoka kuoga.



    “hata picha zake ukitaka nakuonyesha.” Aliongea Robby na kumfanya Hussein kunyanyuka kitandani alipolala na kukaa kitako.

    “nionyeshe basi nimuone.”



    Aliongea Hussein na Robby akachukua simu yake na kuingea internet na kuanza kuperuzi kurasa kadhaa na kuigia kwenye blog ya Wolper na kumuonyesha Hussein picha kadhaa za Jackline alizopiga na mwanae Belinda.



    Hapo hussein aliziamini fikra zake. Moja kwa moja. Sura ya mtoto mzuri aliyemsaidia

    mkoba wake na kumfanya yeye kufikishwa polisi kwa mara ya kwanza ndio ndio yule dada yake wa kuzaliwa tumbo moja na mama yake.



    Siku tatu baadae, safisha jiji waliwavamia wafanya biashara wadogo waliokuwa wakifanya biashara zao pembeni ya barabara. Walivamia na kukamata baadhi ya mali za wafaya biashara hao. Hussein na Robby ni moja kati ya wahanga hao. Hawakujua wafanye nini na kodi ilikua inakaribia.



    Siku zilizidi kwenda huku akiba ndogo waliyokuwa nayo wakiendelea kuimaliza kutokana na kutokua na kazi wala njia nyingine ya kupata hela.



    Ugumu wa maisha uliwatembelea hali iliyowafanya wauze vitu vya ndani. Kodi ilipofika. Walikubali kuachia chumba na kila mmoja atafute njia yake.



    Akiwa kwenye dimbwi la mawazo, aliwaza vitu vingi mpaka mawazo potofu ya kujiunga na uporaji pia yalimsogelea kichwani mwake.

    Kila siku alifuatwa na mtu mmoja alijitambulisha jina la Philipo na kumshauri ajiumge na kundi lao.

    “kwani nyinyi mnajishughulisha na nini?”

    Aliuliza Hussein huku akionyesha kuwa alikuwa tayari kumfuata huyo mtu aliyekuwa akimfariji kwa kumwambia kazi yao ina hela na yeye anayo nafasi ya kujiunga nayo.



    “hili kundi ni kikosi kazi. Yaani hatuchagui kazi na mwisho wa siku ni kutoka na mkwanja.”



    Alifafanua yule mtu ambaye walizoeana muda mfupi kwakua walikuwa wanakaa wote mtaa mmoja kabla yeye kuachia kile chumba..



    Hussein hakuona ubaya kujiunga na kikosi kazi na kupelekwa kwa mkuu wao. Alikutana na wavulana wenye rika kama lake wakiwa si chini ya kumi na tano. Wengine wakiwa na alama kila sehemu. Walikuwa wanaishi kweye gofu moja la nyumba iliyotelekezwa muda mrefu.



    Hussein alipewa kanuni na masharti ya kundi hilo. Alifundishwa jinsi ya kung`oa sight mirror na vitu mbali mbali kwenye magari na kumpelekea bosi huyo ambaye aliwalipa papo hapo.



    Baada ya kuhudumiwa sehemu ya kulala na chakula kwa muda wa siku tatu. Alitakiwa na yeye aingie kazini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ugeni wa kazi hatari ya kwenda kuiba ndio uliomfanya hussein kujikuta kwenye mikono ya polisi baada ya kushtukiwa wakati wanafanya uhalifu huo.

    Alipelekwa selo ya watukutu kwa ajili ya kushikishwa adabu.

    Hakua na jinsi, zaidi ya kukubali matokeo yoyote kwakua alikamatwa na kidhibiti. Alijua ndoto zake za kukutana na mama yake ndio zinaishia jela.



    Akiwa ndani Hussein alikua analia tu huku akijutia uamuzi wake wa kujiingiza kwenye kikundi cha uporaji na wizi wa vipuri vya magari.



    Alipewa adhabu ya viboko viwili kila siku asubuhi na viwili jioni. Adhabu hiyo ilidumu kwa wiki nzima ambayo alikaa huko selo ya kuwafunza tabia nzuri watoto waliopotea.



    “kwanini umeamua kujiingiza katika vikundi vibaya kama vile wakati sura yako haifanani na vitendo unavyovifanya.” Aliuliza dada mmoja ambaye alikuwa mkuu kwenye ile selo.

    “sio mimi mama yangu, ni ugumu wa maisha tu. Halafu ndio mara yangu ya kwanza kuiba. Sijawahi hata siku moja.” Aliongea Hussein huku analia kuonyesha ni jinsi gani anavyojutia kufanya tendo hilo.



    “sasa kama wananchi wenye hasira kali wangekukamata, unafikiri wangekuuliza na mara yako ya ngapi umeiba?.. wangekuua na stori za Hussein zingeishia hapo. Nadhani kama ni funzo umeshapata, mimi nimeamua kukusaidia kwa sababu umekuwa mtiifu na nimepata picha kuwa wewe ni mwema sema makundi maovu ndio yamekuharibia sifa yako. … unaishi wapi?

    Aliongea yule mama huku akionyesha wazi kuwa alikua anataka kumuachia siku ile. Alishtuka baada ya kuambiwa maneno yale na yule mama na kumfanya Hussein kumshukuru mungu kwa kumsaidia kutoka mule ndani.

    “hapa Dar sikai tena. Nataka kurudi tu Tanga.” Aliongea Hussein huku akionyesha wazi kukata tama na jiji hili lililojaa kila aina ya mambo yafurahishayo na kuumiza moyo.



    Yule askari akamruhusu Hussein baada ya taratibu za kumtoa kukamilika. Alimpa nauli ya kurudi kwao kama alivyotaka mwenyewe kwakua hakua na hamu tena ya kuendelea kukaa Dar-es-salaam.



    Hakua na haja ya kwenda kule kwenye kundi la kikosi kazi kwa ajili ya kuchukua nguo zake, alikubali kurudi Tanga na nguo zake alizopewa baada ya kutoka mule ndani. Huku akiwa na hela kiasi alizopewa na yule mama ambaye alikuwa askari mkuu pale.



    Simu ya mkononi ndio kitu pekee ambacho angeweza kusema amekichuma Dar-es-salaam. Zaidi ya hapo ni kumuona mama yake mzazi na mdogo wake wa kike ambao wote hawakumtambua.



    Uamuzi wa kurudi Tanga haukua na pingamizi kichwani kwake kwakua hakua na pa kuanzia.

    Alienda ubungo na kupata basi la Simba mtoto ambalo lilibakiwa na siti chache.

    Safari ya kurudi Tanga ilianza huku Hussein akiwa haamini kama angechomoka pale Polisi kutokana na kujionea watu wanavyotolewa hela na ndugu zao ili watoke.

    Tena kwa kesi yake ya wizi ndio kabisaa, alijua kuwa lazima angepanda kizimbani na kuhukumiwa kwenda jela kabisa.



    Hamu yote ya kukutana na mama yake ilimtumbukia nyongo na kuyakumbuka maneno ya mpenzi wake Mariamu. Alijuta kwenda Dar japokuwa alifarijika na kupata mafunzo mengi jinsi ya kuishi na marafiki na maadui.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande mwengine alikubali kuwa kuishi mjini peke yake ni form six. Maana mafunzo aliyoyapata toka anaikanyaga ardhi ya Dar-es-salaa ni makubwa tena yakiwa yamempa ujasiri wakuishi popote. Hakuwahi kufikiria kuwa kwa jinsi alivyokuwa akijitahidi kuishi maisha ya utii wa sheria kijijini kwao angeweza kwenda polisi siku moja. Lakini Dar ameenda mara mbili kwa kipindi kifupi.

    Kubwa zaidi ambalo hakulitegemua ni kuwa alikua nay eye kwenye kitabu cha kumbukumbu ya mapolisi ya watoto watukutu wanaojiingiza kwenye wizi. Hiyo ilimuumiza lakini alijua yote yalichangiwa na ugumu wa maisha ambayo alishajichokea na alikua tayari kwa lolote.

    Alishukuru kuwa hakujiingiza kwenye uvutaji bangi, ulevi wala kutumia madawa ya kulevya. Aliamini kuwa kama angeendelea kuwa katika kundi lile basi vyote hivyo angetumia hata kwa lazima kutokana na wanakikundi wote walikuwa wanatumia vilevi hivyo.

    Mawazo ya kuiacha Dar hayakumuumiza kichwa kutokana na kujihisi uhuru baada ya kukaa ndani kwa wiki moja. Alitamana gari iondoke haraka kwakua alishaikinai Dar japokuwa jambo lililomleta hakufanikiwa kwa asilimia nyingi.



    Kama maombi yake yalisikilizwa na dereva. Dakika tano baadae alipiga honi kuwashtua abiria waliokuwa wakisua sua pale chini wapande basi tayari kwa safari.



    Alitia gia na gari ikanza kutoka ubungo kwa mwendo wa kinyonga kutokana na wingi wa gari uliokuwa eneo hilo.



    Baada ya kufika maeneo ya mbezi hakukua na magari mengi, basi lilianza kwenda kwa kasi huku kichwa cha Hussein kikiwa na mawazo mengi zaidi ya yale aliyokuwa aliyokuwa nayo wakati anaenda Dar-es-salaam.



    Alifika Tanga jioni na kushuka kijijini kwao salama. Alianza kulikata pori kuelekea na kulekea nyumbani kwao. Kabla hajafika kwao, basi aliamua kwenda kwa mpenzi wake ili aonane nae kwa sababu ni muda mrefu hajamuona.



    Alipofika kwa kina Mariamu, alimuona kwa mbali akiwa amekaa peke yake huku akionekana kukosa furaha. Hussein alijua bila shaka atakuwa anamuwaza yeye hivyo alijitokeza uwanjani na kupiga uluzi ulio`mshtua Mariamu na kuangalia mbele. Kama mshale, Mariamu alichomoka na kumfuata Hussein na kumkumbatia huku machozi yanamtoka.



    “usijali mwanamke wa maisha yangu. Wewe ndio wangu na wengine hawana nafasi kwangu.” Aliongea Hussein huku akijaribu kumpooza mpenzi wake ambaye bado alikua analia kwa kwikwi.



    Mwanzoni alijua kuwa kile kilio kilikua kwa ajili ya kumkumbuka sana au hakuamini kuwa anaweza kurudi. Lakini kilio kile hakikukoma kwa muda mpaka Hussein akajua kuwa kuna kitu kingine kilichomliza mpenzi wake.



    “niambie basi mpenzi wangu umepatwa na nini… unaniacha njia panda mwenzako unapolia bila kunipa sababu inayokuliza.” Aliongea Hussein huku akiwa na hofu kubwa kutokana na kuwa hajawahi kumuona mpenzi wake akiwa analia vile kwa uchungu.



    “mama… mama..Hussein.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliongea maneno hayo Mariamu na kumkumbatia Hussein tena kwa uchungu huku akimminya kwa nguvu kuashiria uzito wa machungu aliyokuwa nayo.

    Hussein alijua bila shaka kumetokea msiba kwa mama yake Mariamu. Aliamua kuchukua jukumu la kumbembeleza Mariamu ambaye kwa wakati huo alishindwa kuongea kutokana na kilio cha kwikwi alichokuwa analia.



    Mara akapigwa na butwaa alipomuona mama yake Mariamu akitoka ndani. Alishangaa kwa sababu alionekana mzima na hakuwa na hali yoyote ambayo ingemfanya Mariamu kumlilia vile.

    “pole mwanangu kwa kuondokewa na mama yako.” Aliongea mama yake Marimu na kumfanya Hussein atambue kuwa kile kilio kilikua kinamuhusu yeye.



    “Hussein, …..Hussein!!”

    Hayo maneno yalimtoka Mariamu baada ya Hussein kutoka pale alipo mbio na kuelekea nyumbani kwao haraka. Alishangaa kuona watu wengi wakiwa wamejaa nyumbani kwao. Alipofika tu, baadhi ya majirani walimsogelea na kuanza kumpa pole. Wakati wote huo alikuwa kama amepigwa sindano ya ganzi. Hakuhisi chochote zaidi ya kushangaa tu manbo yanavyokwenda.

    “pole mwanangu, hii yote ni mitihani ya dunia. Kuwa na moyo wa kiume kwa kuvumilia katika huu mtihani mzito uliokupata.”



    Aliongea mzee aliyekwenda kumpokea na kuzidi kumchanganya Hussein. Alikuwa kama mtu ambaye hajielewi wa jinsi alivyokuwa anatoa macho tu bila ya kuongea chochote. Kila dakika iliyokwenda, tafsiri za huzuni zilijijenga kwenye moyo wake baada ya kuona kila mtu aliyekuwa pale kwao alimpa pole na kumuonea huruma.



    Wanawake waliokuwa wakiishi karibu na nyumba hiyo walizidi kuzidisha kilio baada ya kumuona Hussein akiwa amefika pale.



    Alichukuliwa Husein na kupelekwa kwenye chumba kilicholazwa maiti ya mama yake, hapo ndio machozi ya uchungu yalianza kumtoka baada ya kumuona mama yake huyo aliyemlea toka kichanga amepoteza maisha. Kilio cha sauti kilimtoka na kufanya watu wamtoe nje na kumbembeleza sana.

    Ilikuwa kazi kubwa sana kumtuliza Hussein ambaye alikua analia kwa sauti huku akuyataja mambo aliyokuwa akifanyiiwa na mama yake ambayo hakuna mtu atakayeweza kuyabeba mamba hayo hata kama atakuwa analipwa.

    Kilio chake kilimgusa kila mtu na kufanya hata waliokuwa wanambembeleza na wao kuumia moyo na wao kuanza kuungana nae kulia.



    Siku ya pili yake ndio siku ya mazishi ya mama yake Hussein. Walienda makaburini wanaume kwakua yule mama alikuwa muislamu. Shekhe alitoa maelezo machache na kuwakumbusha watu wafanye ibada kwakua kila nafsi lazima itaonja umauti.



    Huku machozi yanmtoka. Hussein alikuwa mtu wa kwanza kutia dongo kaburini na wengime wakafuata na kumaliza mazishi hayo.



    “POLE!!!”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hilo neno lilisikika kwa kila mtu akimuambia Huusein aliyebaki kama yatima kwakua hakumjua baba yake kabisa.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog