Simulizi : It's Happening
Sehemu Ya Nne (4)
Maisha ya kuishi pale kijijini yalikuwa magumu kwakua alihisi upweke sana kila akimkumbuka mama yake aliyekua anamtunza na kufanya lolote kwa ajili yake.
Alilia kila siku na kumuomba mungu ampunguzie mitihani. Sasa alibaki njia panda. Hakutaka kuendelea kuishi pale kwakua alikua na dukuduku la kutaka kumwambia ukweli Jaqueline Wolper kuwa yeye ni mtoto wake pia akilikumbuka Jiji la Dar lilivyomfunza hakua na hamu nalo hata kidogo.
Baada ya arobaini ya mama yake kumalizika, alimuaga mpenzi wake kuwa ameamua kurudi Dar kwa mara nyingine ili akutane na mama yake na ampe habari zile kwakua mwenye siri ile alibaki yeye na Mariamu peke yake.
“safari njema. Ila kumbuka kuwa sijamuona mvulana yeyote hapa kijijini niliyempenda kama wewe mpenzi wangu. Usihadaike na jiji japokuwa umeniambia kuwa wewe umeshajifunza na tayari umashayashinda majaribu ya mji huo.” Aliongea Mariamu maneno yaliyomfanya Hussein amshike bega na kumuomba awe na amani.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“chukua hii simu, mi nitapata nyingine mjini na nitachonga line nyengine. Hii itasaidia kudumisha mawasiliano kati yetu.” Aliongea Hussein na kumkabidhi Mariamu ile simu yake.
“ahsante mpenzi wangu,” aliipokea kwa mikono miwili na Hussein akaanza safari peke yake ya kurudi tena Dar kwa mara ya pili.
Alipanda gari na kufika Dar saa kumi jioni. Alipanda daladala na kushuka manzese na kwenda kwenye gesti ya bei rahisi na kujituliza hapo.
“hivi kipaji cha kutunga stori ninacho, kwanini nisiwapelekee mastaa ili wazitungie filamu??”
Alijiuliza Hussein huku akiwa kitandani kwake. Aliona ujinga kulala. Aliamka na kuanza kutunga hadithi ambayo itamshika mtu yeyote na kushawishika kuinunua story yake.
Alikaa kwa muda akitafakari cha kuandika. Mwisho wa siku akalipata jina la hadithi yake. Aliamua kuandika jina la story hiyo NO ONE KNOWS TOMMOROW
******************
Vipande vya tukio zima la usaili viliunganishwa na kuwa mkanda mmoja na kupelekewa Jaqueline Wolper kwa ajili ya kumbu kumbu zake. Waliuangalia na ilipofikia kipande cha Hussein Jaqueline Wolper alianza kucheka hata kabla Hussein hajaingia.
“muangalie huyu mtoto alivyoleta kituko kwenye usaili.” Aliongea Wolper akimwambia mwanae Belinda waliokuwa wote sebuleni wakiingalia ile cd.
“kha!.. kumbe ni huyu.?” Alishtuka Belinda baada ya Kumuona Hussein kwenye ile cd.
“vipi kwani, unajuana nae?” aliuliza Jaqueline Wolper kwa mshangao.
“huyu mkaka ana moyo mzuri sana. Ndiye aliyenisaidia nilipoporwa na kibaka.” Aliongea Belinda na kumfanya mama yake ashangae.
“yaani huyu ndio ulisema unatamani uonane nae tena?...ana nini sasa?. Wewe hujui matapeli wa hapa mjini. Walikuwa wanalengo la kukuibia wote hao ndio maana alijifanya kukusaidia ili umpe chochote.” Aliongea Wolper huku akionyesha wazi kumdharau Hussein.
“usiseme hivyo mama.”
Belinda alionyesha wazi kukerwa na kauli ya mama yake.
“si ulisema mapolisi walikuja kumkamata?.. kama sio kibaka na yeye ni nani?”
Aliongea Wolper na kumkera mwanaye ambaye aliondoka na kwenda chumbani kwake na kumuacha mama yake akiendelea kuangalia ile cd.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Zoezi la kuwatafuta wasanii watakao shiriki katika filamu mpya ya Jaqueline wolper lilikamilika na watu waliopatikana walianza mazoezi. Katika watu hao, rafiki yake Hussein nae alikua mmoja kati ya waliopita ngwe zote za mashindano.
“hallow my queen of Jerusalem.” Aliongea Jacob Stephane baada ya Jaqueline Wolper kupokea simu.
“safi tu, niambie.” Aliongea Wolper kwa mapozi.
“unaweza kuja nyumbani kwangu muda huu kuna ishu nataka tuongee.” Aliongea JB na kumfanya C.Wolper kujifikiria kidogo.
“siwezi kuja mine,..niko bize balaa.” Aliongea Wolper huku akionyesha wazi kuwa hawezi kutoa pale.
“poa, ila nilikuwa nataka nifanye na wewe kazi yangu katika mwezi huu.” Alifunguka JB nia yake ya kumuita nyumbani kwake.
“sorry bonge la bwana, siku hizi sifanyi kazi zinazotoka nje ya kampuni yangu.” Aliongea C.Wolper huhku akionyesha kuwa hayuko tayari kushiriki movie hiyo.
“ ni scene tatu tu zinazokuhusu mine.” Aliongea JB ili kumuonyesha ni jinsi gani alivyokuwa anamuhitaji.
“nielewe brother , sina muda wa kufanya kazi za nje.” Aliongea Jaqueline na kukata simu.
Mawasiliano ya C.Wolper na wasanii wenzake yalipungua sana hasa ikitokea ishu za kazi.
Ubize wake ulikuwa mkubwa kwakua kwa sasa alikua anahitaji kutoa movie kali ili jina lake libaki kuwa hewani kama lilivyo sasa.
******************
Hussein alikaa gesti kwa muda wa wiki moja huku akiendelea kutafuta mahali pa kupeleka hadithi yake hiyo baada ya kumaliza kuandika. Juhudi zake zilizaa matunda baada ya kwenda kwenye tamasha la wasanii linalofanyika kila jumamosi viwanja vya lidas club.
Huko alijitosa kwa msanii mkubwa mwenye kila aina ya mbwe mbwe na anayesifika kwa kucheza movie za serious comedi. Bila hiyana, Haji Salumu al-maarufu kama mboto alimkutanisha na JB.
Alipata nafasi ya kusikilizwa na kupewa contact ili wakutane siku ya pili yake ofisini kwake.
Siku hiyo alimuomba mungu sana amsaidie ili afanikiwe lengo lake. Alivaa nguo zake zilizokuwa nzuri kidogo alizonunua kutokana na pesa za pole alizopewa na wanakijiji. Kwa kutumia simu ya kibandani, alielekezwa ofisi za kampuni ya Jerusalem ilipo na akafanikiwa kufika.
Alikaribishwa vizuri mapokezi na kuambiwa asubiri kwakua mkurugenzi alikua na mgeni ndani.
“bosi, kuna kijana hapa amejitambulisha anaitwa Hussein, amesema eti ana apointiment ya kukuta na wewe leo hii.” Aliongea secretary baada ya kumpigia simu JB.
“yeah.. mwambie aingie.”
Aliruhusu JB na Hussein aliingia na kusalimiana nae.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“story yako inahusu nini kabla sijaisoma.” Aliuliza JB ili ajue maudhi ya stori yenyewe.
Hussein alimuhadithia maudhui ya ile hadithi yake yaliyomvutia mno JB na kumuhakikishia kuwa ni lazimma ataicheza hiyo story.
“kumbe kuna vipaji vizuri tu mtaani,.. wewe unaweza kucheza hiyo nafasi ya mtoto uliyyemuelezea???” aliuliza JB baada ya kuvuta picha ya mtu anayetakiwa kucheza kama muhusika mkuu.
“ndio,.. naweza kuigiza kuliko hata kutunga hadithi.” Aliongea Hussein baada ya kupata mwanya wa kujielezea kipaji chake kingine.
“kesho njoo mazoezini kwetu. Acha hii story nimpe mtu aiandikie scripti.”
Aliongea JB na kumfanya Hussein aondoke kwa furaha.
Kesho yake alienda mazoezini na kupangiwa vipande mbali mbali vya hisia. Ubunifu wa maneno na uvaaji wa uhusika katika kila kipande alichopewa kilimfurahisha sana JB na kumuona anafaa kabisa kucheza movie zake.
Walipomaliza mazoezi Hussein alimuelezea ukweli JB kuwa hana pa kuishi zaidi ya gesti ambapo hata hela zilianza kumuishia na alikua anategemea sana sanaa kwa sababu hakua na kazi nyingine. JB alimuelewa na kumkaribisha nyumbani kwake.
Hela alizo lipwa kwa ajili ya story na hela yake ya kucheza hiyo movie vilimuwezesha kupanga chumba na kununua vitu muhimu vya ndani.
Alinunua simu, na cha kwanza kufanya ni kuwasiliana na mpenzi wake Mariamu na kumpa taarifa juu ya mwangaza unavyoanza kujitokeza kwenye maisha yake.
“nakutakia kila la kheri katika mafanikio yako. Sababu najua kuwa mafanikio yako wewe ndio mafanikio yetu wote.”
Maneno ya mpenzi wake yalimpa moyo na kujiapiza kutomsaliti msichana huyo aliyekuwa naye kwenye kipindi chote cha shida.
Baada ya mazoezi ya kutosha, Hussein alipelekwa dukani kuchagua nguo kadhaa kwa ajili ya scene za hiyo movie. Walianza kuchukua vipande vya movie hiyo na kuimaliza huku wakiwa wote wamekifurahia kipaji cha ajabu cha Hussein. JB alikiri kipaji cha Hussein kuwa kilikuwa cha aina yake. Alikuwa na hisia zinazoweza kumtoa mtu machozi kwa vipande vyote vya manyanyaso alivyovicheza.
Movie hiyo ilikamilika na Posters zilibandikwa kila kona ya jiji na baadhi ya magorofa yaliwekwa matangazo makuwa yenye Picha ya Hussein, Aunti Ezekiel na Chuchu Hans.
“jamani huyu mkaka namjua, alishawahi kuniuzia viatu kule kariakoo.”
Hayo maneno yalitamkwa na wadada wengi waliowahi kumuona Hussein kipindi alichokuwa ana hastle.
Jina la kampuni ya Jerusalem lilifanya movie hiyo kusubiriwa kwa hamu kubwa kutokana na watu kujua kazi za JB huwa zinawakosha wengi. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kampuni ya Steps Entertainment ndio ilikuwa na kazi ya kuisambazi hiyo movie nchini na nje ya nchi.
Movie ilipotoka iligombaniwa kama njugu na kumpa matokeo mazuri Hussein na wenzake walioifanya kazi hiyo.
“wangu, umeiyona movie yangu?” aliuliza JB baada ya kumpigia Jaqueline Wolper simu.
“ndio nimeichukua muda huu.. nitaiangalia muda si mrefu.”
Aliongea Jaqueline na JB akakta simu. Wolper alishangaa sana kumuona Hussein kwenye cover la mbele ya ile cd. Alitamani kumuangala yule mtu aliyeleta vituko kwenye usaili wa movie yake.
Alimsubiri mtoto wake aliyempeda na alipofika aliiweka ile cd na kuanza kuangalia ile movie ya NO ONE KNOWS TOMORROW.
Matangazo yalirushwa na movie ilipoanza alishangaa kidogo jina la muhusika mkuu. Aliitwa Hussein Molito, jina hilo la Molito lilimshtua kidogo. Lakini alipotezea na kuendelea kuangalia hiyo Movie na alipenda kuona ilivyoandikwa BASED ON TRUE STORY.
********************
Inaonekana familia moja masikini huko Tanga kijijini, mtoto wa kike aliyetumia jina la Tulisa alikua anaenda shuleni, huko alikutana na Rafiki yake Batuli na kuingia wote darsani.
Wakati mwalimu akiwa anaendalea kufundisha, Tulisa alikua anasinzia kila wakati. Hali iliyomfanya rafiki yake kuwa na wasi wasi na Tulisa.
Walipotoka shule, Batuli aliamua kuvunja ukimya.
“mbona hivyo rafiki yangu?.” Aliuliza Batuli walipokuwa njiani.
“sijui Batuli, siku hizi nachoka sana. Najisikia hamu ya kula vitu vichachu pia baadhi ya vitu nilivyokuwa navipenda zamani, hivi sasa sivipendi. Kila wakati najihisi usingizi umenijaa tu rafiki yangu.” Aliongea Tulisa na kumfanya rafiki yake amuangalie kama vile anamkagua.
“rafiki yangu hiyo ni mimba, ukubali ukatae.” Aliongea Batuli baada ya kusikiliza maongezi ya Tulisa.
“wee??....baba ataniua Batuli,.. nifanyeje?” aliongea Tulisa huku akili yake ikionyesha kuchanganyikiwa kupita kiasi.
“chamsingi we nenda kwa huyo Omary na umwambie kuwa wewe ni mjamzito. Hakuna njia nyengine,” aliongea Batuli huku akionyesha wazi kumuonea huruma rafiki yake.
“nitaafanya nini mimi oooh.”
Tulisa alianza kulia na nguvu za miguu zilimuishia na kuamua kukaa chini.
“ila mimi nilikuonya mazoea na yule mkaka. Lakini hukunisikia. Acha kulia Tulisa, kwani kulia kwa sasa hakuwezi kukusaidia chochote.” Aliongea Batuli na kujaribu kumbembeleza rafiki yake huyo aliyekuwa katika hali ya utatanishi.
“mi nimefanya mara moja tu, tena nilimkatalia sana, sema kanilazimisha sana.” Aliongea Tulisa huku akionnyesha ni jinsi gani anavyojutia kitendo kile.
“ndio hivyo. Unaambiwa hata mara moja hiyo hiyo unaweza kupata mimba.”
Aliongea Batuli na kumbeleza rafiki yake na kumnyanyua na safari ya kuelekea kwa muhusika wa ile mimba ilianza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“vipi tena, mbona mmoengozana humu mwenzako analia, kuna tatizo gani.” Aliongea Omary baada ya kumuona Tulisa akiwa ameongozana na Batuli.
“ulichokuwa unamlazimisha mwenzako kufanya kile kitendo matunda yake ndio haya, mwenzako ana mimba na wewe ndio utajua pa kuipeleka.” Aliongea Batuli huku akionyesha wazi kumchukia Omary toka mwanzo.
“kama ana mimba aipeleke huko kwa waliompa sio mimi, tena msiniletee uchuro hapa.” Aliongea Omary na kumfanya Tulisa ashtuke.
“Omary unasemaje?” aliuliza Tulisa kwa uchungu.
“kusikia umesikia sema hicho ni kiburi. Yaani wamekataa wote huko uliowapelekea ndio umemuona Omary ndio bwege mtozeni wa kukubali hiyo mimba. Nenda kamtafute aliyekupa mimba hiyo. Hapa ukija uje ukiwa unataka msaada wa kumchagulia mtoto wako jina lakini sio kuniletea mzigo. Maisha yangu yenyewe mzigo halafu mnataka kuniongezea mzigo mwengine?.. nendeni msiniletee kiwingu hapa,.”
Aliongea Omary na kufunga mlango wake. Tulisa alianza kuangusha kilio cha haja kilichomfanya rafiki yake kumchukua na kuondoka nae.
Alitumia muda mrefu kumbembeleza na baadae akampa wazo.
“nenda kamwambie mama yako, atajua nini cha kufanya.” Aliongea Batuli huku akiwa amejaa huzuni kwa kilichomkuta rafiki yake.
“mama atamwambia baba, ndio yale yale tu. Nitauliwa mimi. Baba yangu mkali sana”´aliongea Tulisa na kumfanya rafiki yake kushusha pumzi ndefu.
“sasa unataka kufanyaje?” aliuliza Batuli baada ya kuona kila wazo analompa analipangua.
“naona bora nikatoe tu basi.” Aliongea Tulisa huku akimuangalia rafiki yake.
“mimi sikushauri hicho kitu. Kwanini ushiriki dhambi ya kuua kiumbe cha mungu bila hatia. Unajua atakuja kuwa nani huyu mbeleni?... hiyo dhambi ya kuzini hujaitubu unataka kuongeza madhambi mengine. Tuliza moyo rafiki yangu. Hii ni mitihani tu unayopaswa kupambana nayo na sio kuikimbia. “
Aliongea Batuli maneno yaliyomfanya Tulisa kukubali ushauri wa rafiki yake.
Alienda nyumbani kwao huku akiwa na simanzi kubwa.
“vipi mwanangu, kwema huko shuleni?” aliongea mama yake Tulisa baada ya kumuona mwanaye akiwa katika hali tofauti na aliyoizoea.
“hapana mama,.. nipo sawa tu.” Aliongea Tulisa huku sura yake ikionyesha wazi kuwa alikuwa na huzuni.
“wewe ni mwanangu na najua kila nukta ya hatua ya furaha yako na kila nukta ya uelekeo wa huzuni yako. Bila shaka mwanangu una kitu kina kusumbua.” Aliongea mama yake kwa upole na kumfanya Tulisa aangalie chini.
“ni kweli mama, ila sijui utanifikiriaje, ila sikupanga mimi iwe hivyo.” Aliongea Tulisa na kumfanya mama yake amuangalie kwa umakini mkubwa.
“UNA MIMBA??”
Aliuliza mama yake na kumfanya Tulisa ashtuke na kumuangalia mama yake ambaye alishaanza kubadilika. Aliamua kuitikia kwa kutikisa kichwa.
“sasa wewe unajua fika kuwa maisha yetu yalivyokuwa magumu. Halafu unajua kuwa baba yako ni mkali na anaweza hata kukutoa roho kama akiyabaini haya?.. hujifikirii?.. utajua mwenyewe.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliomgea mama yake na kumuacha Tulisa pale nje na yeye akaingia ndani kwa hasira.
Usiku wa siku hiyo alikuwa na mawazo sana. Kutwa aliyafikiria maneno ya Omary aliyekuwa akimrubuni kwa kumpa hela, zawadi na madaftari ya shule na kujifanya alikuwa na lengo jema kwake.
“Tulisaaaaa… wewe mwanaharamu amka”
Tulisa alisikia sauti ya baba yake ikiita kwa kugomba. Aliamka na kufungua mlango. Kabla hajasimama sawa sawa mlangoni. Alikutana na kibao cha nguvu kutoka kwa baba yake huyo.
“shenzi kabisa wewe, haya kusanya nguo zako nenda kwa huyo mwanaharamu mwenzako mpumbavu wa akili wewe. Tena toka kabla sijakuumiza mbwa we.”
Maneno makali yalimtoka baba yake Tulisa. Mama yake hakua na kauli yoyote pindi mzee huyo awapo na hasira. Alijua kuwa kuinunua kesi ilikuwa ni rahisi endapo atajaribu kumtetea mwanae.
Tulisa alikusanya nguo zake na kuondoka usiku ule kuelekea kusiko julikana huku mama yake akimuangalia kwa huruma. Mzee wake alitoka na kwenda kufunga mlango baada ya Tulisa kutoka.
“kama na wewe unamuonea huruma, mfuate” aliongea baba yake Tulisa kwa hasira na kumuangalia mke wake. Mama Tulisa hakujibu kitu zaidi ya kwenda chumbani kwake.
Kilio cha Tulisa kilibaki moyoni huku machozi yakionyesha ushirikiano mkubwa kwa kuya lowesha mashavu yake.
Safari ilimfikisha kwa rafiki yake Batuli. Alifunguliwa mlango na kupewa shuka na rafiki yake na kumuacha alale mpaka asubuhi.
“niambie, tunaenda shule au?” aliulza Batuli baada ya kujiandaa tayari kwa safari ya shuleni.
“siwezi kwenda, si unajua hali niliyokuwa nayo. Nitagundulika na wanafunzi wenzangu watanicheka.” Aiongea Tulisa na kumuangalia rafiki yake kivivu.
“poa,.. sasa nikiulizwa na mwalimu nisemeje?”aliuliza Batuli.
we mwambie kuwa toka tulivyoachana jana hujaonana na mimi.” Aliongea Tulisa.
“haya, baadae.”
Aliongea Batuli ambaye kipindi hicho alikuwa darasa la saba na Tulisa alitanguliwa darasa moja na rafiki yake huyo.
Huo ndio ukawa mwisho wa Tulisa kwenda shule na kuamua kuishi kwa rafiki yake huyo anayejitegemea baada ya wazazi wake wote kufariki.
Waliishi maisha magumu kwa kipindi chote huku wakitegemea kilimo cha mahindi ambacho kiliwasaidia kukidhi mahitaji machache tu.
Miezi ilisogea mpaka Tulisa alipojifungua. Kutokana na baridi kali na kutokuwa na usalama wa kutosha kwa kitoto hicho kichanga, kilikumbwa na ugonjwa wa degedege. Hali hiyo iliwachanganya sana Tulisa na Rafiki yake Batuli.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Waliuguza hadi wakajua kuwa yule mtoto lazima atapoteza uhai kwakua afya yake ilitetereka sana.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment