Search This Blog

Wednesday, 1 June 2022

IT'S HAPPENING - 5

 







    Simulizi : It's Happening

    Sehemu Ya Tano (5)





    Siku moja batuli akiwa anarudi kutoka shuleni, aliona nyumba ipo kimya tofauti na siku zote. Alipotupa macho kitandani, alimuona yule mtoto mchanga akiwa kalala peke yake. Alipika chakula na kula. Muda wote huo hakumuona Tulisa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya muda mtoto aliamka na kuanza kulia sana. Alimchukua na kumnyanyua, chini ya ile khanga aliyofuniikiwa mtoto aliona kikaratasi kidogo chenye maandishi.



    Alimbembeleza mtoto na kumpikia uji na kukichukua kile kikaratasi na kukianza kukisoma.



    “rafiki yangu Batuli, naomba unisamehe sana kwa kukuachia mzigo. Mimi siwezi kushudia mwanangu anavyokufa kwa ugonjwa uliompata.

    Nimepata lifti ya kwenda Dar-es-salaam. Nawapenda wote, ila naenda kutafuta maisha mjini, nikifanikiwa nitakuja tena. Ila kama itachukua muda mrefu ndio hivyo. Nasikitika kukuacha rafiki yangu mpendwa na sina cha kukulipa ila mungu atakuandikia fungu lako. Kama mwanagu akiwa hai, usisahau kumuhadithia maisha niliyoyapitia mama yake. Mwambie asinichukie ila anisamehe kwa kosa nililomtendea. Nawatakia maisha mema.”



    Ile karatasi ilimtoa machozi Batuli. Hakuweza kuirudia kuisoma. Alijua kuwa rafiki yake ameamua kumpa mtihani mkubwa na hakujua afanye nini.



    Kutokana na ulezi, Batuli alikatisha masomo yake na kuamua kumlea mtoto huyo wa rafiki yake kwa mapenzi mazito huku akimuombea mungu aweze kupona matatizo yake.

    Mungu alimjaalia mtoto huyo waliyempa jina la HUSSEIN akapona na ukuaji wake ukiendelea vizuri.



    Baada ya miaka kumi na tisa, Hussein alikuwa mvulana mkubwa na mwenye kipaji kikubwa cha kucheza mpira, kuandika stori, kuigiza na kuimba.

    Tabia nzuri ndio iliomlea na kuwa mtoto wa kuigwa na kila mtu huko kijijini kwao.



    Hakufanikiwa kuendelea na secondary japokuwa alifaulu vizuri kutokana na maisha magumu waliyokuwa wanaishi.



    Aliyetumia jina la Batuli, alionekana ni Aunt Ezekiel baada ya miaka hiyo. Nafasi ya Hussein alicheza Hussein mwenyewe.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *******************

    Wakati wanaendelea kuangalia hiyo movie mpaka hapo ilipofikia, Jaqueline Wolper alishindwa kuvumilia kuendelea kuiangalia hiyo movie. Alitoka na kuingia chumbani kwake. Brenda alishangaa kumuona mama yake akiwa ameacha kuangalia ile Movie wakati ilikuwa ni movie nzuri tena inayosisimua.



    Aliisimamimsha ile movie na kumfuata mama yake chumbani kwake. Alishangaa kumuona mama yake akilia kwa uchungu huku akiikumbatia mito yake.

    “mama, mama..” aliita tulisa huku akimtikisa mama yake ambaye alikuwa analia kwa kwikwi wakati huo.



    “nia..che,,Brenda.” Aliongea Jaqueline Wolper huku machozi yanamtoka.



    Brenda alimuacha mama yake na yeye kwenda kuendelea kuiangalia hiyo movie.

    **********************



    Alionekana Chuchu Hans akiwa mjini Dar huku akiwa anatoka kwenye duka la nguo na kuzingukwa na waandishi wa habari mbali mbali.

    “super star Tulisa, unaweza kutuambia nini malengo yako katika mwaka huu katika tasnia hii ya bongo movie?” aliuliza muandishi mmoja wa habari.

    “malengo yangu ni kufanya kazi bora ili nichukue tuzo za Oscar. Hiyo ndio ndoto yangu kuu kwa mwaka huu.” Alijibu Tulisa huku akiwa amezungukwa na waandishi wa habari waliomzonga mpaka akakosa hewa..



    “vipi, una malengo ya kuzaa mtoto mwengine zaidi ya huyu Felister tunayemjua??” aliuliza muandishi mwengine wa habari.

    “mtoto niliye naye ananitosha sana. Kama kuzaa ningezaa mapema sio hivi sasa mtoto wangu ameshafikisha miaka kumi saba.” Alijibu Tulisa na kuingia kwenye gari lake huku waandishi wa habari wakilizunga lile gari na kumgongea kwenye kioo.



    *****************

    Alitoka chumbani C.Wolper na kumfokea mtoto wake.

    “itoe hiyo movie… sitaki kuona ukiiangalia.” Aliongea Jaqueline na kuanza kulia tena.

    “niambie tu mama, kuna nini katika hii movie.” Aliuliza Belinda na kumfuata mama yake alipoenda kukaa..



    Alimbembeleza sana na kufanikiwa kumnyamazisha mama yake. Jaqueline alimuanga lia mwanaye na kumshika mkono. Kwa uchungu alimkumbatia mwanaye huku analia na kumwambia maneno yaliyomuacha hoi Belinda



    “HUSSENI NI MTOTO WANGU”



    Aliongea C. Wolper na kumuacha mwanaye kwenye bumbuwazi.



    “kila ulichokiona katika maisha ya Tulisa na Batuli, ndio maisha yangu ya nyuma niliyoishi kabla sijaja huku Dar-es-salaam.” Aliongea C.Wolper na kuonyesha ishara za kusikitika kwa alichokifanya.



    “kwa hiyo mama wewe ndio Tulisa aliyezungunziwa kwenye hii Movie?” aliuliza Brenda.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “kweli damu ni nzito kulika maji, mwanangu kaamua kunitafuta mama yake kwa njia ya kunikumbusha maisha yangu ya zamani.”



    Aliomgea Wolper na kumuangalia mwanaye ambaye wakati huo alikuwa yupo katika wakati mgumu kutokana na taarifa zile za ghafla ambazo hajawahi kuzisikia hata kwa Bahati mbaya.



    Safari ya kuanza kumtafuta mtoto wake ilianza siku ya pili yake tu baada ya usiku huo kupita bila usingizi.

    “niambie wangu.” Ilisikika sauti upande wa pili baada ya kupokea simu ya Jaqueline Wolper.

    “namuulizia Hussein mine. Upo nae hapo?” aliuliza Wolper.

    “umekiona kilivyo kifaa?... huyo ni mali ya Jerusalem.. ongea lengine.” Aliongea JB bila kujua dhumuni la mwana dada huyo mrembo.

    “acha utani bwana, nina shida naye binafsi.” Aliongea Jaqueline Wolper akiwa katika hali ya umakini ili mradi JB afahamu kuwa hakuwa kwenye mzaha.

    “hapa hayupo, si unajua yupo kwenye mapumziko mafupi nyumbani kwake kabla hajaingia location kwa ajili ya kitu kingine.” Aliongea JB huku akionyesha wazi kumtambia mwenzae ambaye bado movie yake hajaikamilisha.

    “mcheki hewani, mwambie nina shida naye leo hii.” Aliongea C.Wolper na kumfanya JB akate simu. Baada ya dakika mbili. Alipiga tena.

    “vipi?” aliuliza Wolper baada ya kupokea simu.

    “hapatikani.” Alijibu JB baada ya kujaribu kumpigia mara kadhaa.

    “nitumie namba yake.” Aliongea Wolper. Bila hiyana alimtumia namba ya Hussein kupitia meseji.



    Jaqueline alijaribu kumpigia Hussein kwa dakika kadhaa, lakini namba yake bado haikupatikana. Zoezi la kumtafuta kwenye simu lilidumu siku nzima bila ya mafanikio. Siku iliyofuata, Wolper alidamka asubuhi na mapema na kwennda nyumbani kwa JB.



    “naomba nipeleke anapoishi.. nina shida naye kweli.” Aliongea Wolper baada ya kuonana na JB na kusalimiana.

    “shida yenyewe hutaki kuniambia.. unafikiri nitakusaidiaje?” aliongea JB na kumuangalia Wolper ambaye alionyesha wazi kuwa hayuko sawa.

    “utafahamu kila kitu wangu, ila kuonana nae Hussein ni jambo zuri zaidi.” Aliongea Wolper na kumfanya JB kukubali kumpeleka mahali anapoishi Hussein.



    Walikuta kufuli liki nin`ginia mlangoni kuashiria kuwa hakuwepo chumbani kwake.

    “samahani, hivi Hussein ana muda gani hajalala hapa?” aliuliza JB baada ya kumuona mpangaji mwenzake akitoka chumbani kwake.

    “mbona ni wiki sasa sijamuona. Hata kufuli lake halijawahi kutikisika toka alipoondoka.” Alitoa majibu dada huyo yaliyowafanya waangaliane JB na Jaqueline.

    “tena nilimuona kabeba begi kubwa.. nikahisi itakuwa anasafiri tu.” Aliongeza yule dada na kuwafumbua masikio. Waliaga na kuondoka.zao.



    “itakuwa kaenda wapi??.. au u super star ndio umeanza kumpa kiburi?” aliongea JB huku akionyesha wazi kukasirishwa kwa kitendo kile cha kusafiri bila kuagwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jaqueline alirudi nyumbani kwake na kuanza kufikiria ni nini afanye ilimradi akutane na mtoto wake huyo aliyemdhania kuwa amepoteza maisha muda mrefu.



    Wazo la kwenda kijijini kwao lilipitishwa na halmashauri ya kichwa chake. Alianza kupanga nguo zake tayari kwa safari.



    “una uhakika atakuwa huko kweli?” aliuliza Belinda.

    “sina uhakika, ila fikira zangu zinaniambia kuwa yupo huko.” Aliongea Wolper na konyesha kuwa hakuwa na raha kabisa mpaka kiu yake ya kukutana na mtoto wake itimie.



    Siku ya pili yake, alitia gari yake mafuta full tank na safari ya Tanga ilianzia hapo. Alifanikiwa kufika kijijini kwao saa nane mchana.



    Alifunga vioo vyake vilivyokuwa na Tinted ili mradi asisumbuliwe na watu mbali mbali kijijini hapo.



    Safari yake iliishia nje ya nyumba ya marehemu rafiki yake. Alishuka na baadhi ya watu waliomuona walishindwa kuamini kuwa yeye ndio Wolper waliokuwa wanamuona kwenye Tv.



    Wolper alibisha hodi bila mafanikio, aligeuka nyuma na kuona kundi la wanakijiji likiwa limekusanyika kumshangaa yeye.

    Alimfuata mzee mmoja na kumsalimia.



    “samahani, eti wenyeji wa hii nyumba, bado wanaishi kweli?” aliuliza Wolper na kuwafanya watu walikowa karibu na yule mzee aliyeulizwa kuzidi kushangaa.

    “Batuli tumemzika hivi karibuni.. na mtoto wake hatujui alipokwenda. Maana baada ya mazishi ya mama yake tu na yeye akatoweka hapa kijijini.”

    Aliongea yule mzee maneno yaliyomchoma Wolper na kumfanya aishiwe nguvu. Machozi yalimlenga lenga na baadae yalimshinda na kudondoka huku akijitahidi kuyafuta.

    “kwani una undugu nae?” aliuliza mzee huyo baada ya kuona mapokeo ya msiba ule kwa Wolper.

    Alishindwa kuongea zaidi alianza kulia hali iliyowafanya watu waliokusanyika pale kumuonea huruma.



    Walimpeleka makaburini na kumuonyesha kaburi la rafiki yake.



    “Batuli, naomba unisamehe kwa yote niliyokutendea. Sijawahi kukulipa fadhila hata siku moja licha ya kutulea mimi na mwanagu. Sijawahi kukukumbuka hata siku moja japokuwa nimekuwa na uwezo kifedha. Wewe ulikua zaidi ya wazazi wangu walionifukuza nyumbani na ukaamua kunipokea. Ulijinyima wewe na kuhakikisha napata mimi ili mimi na mwanagu tuwe salama…. Sina jema nililokutendea. Leo nimeyakumbuka yote haya baada ya ujumbe mzito uliompa mwanangu juu ya ukweli kuhusu maisha yangu. Nisamehe huko ulipo na sitachoka kukuombea kwa mungu akufutie madhambi yako…nisa meheeee Batuliiii”

    Jaqueline Wolper alilia sana na kugala gala. Wanakijiji waliofahamu ukweli na kumuonea imani sana Wolper.



    Walimpa pole na kumtoa eneo lile.

    Mariamu alikua mmoja kati ya wanakijiji waliokuwa pale. Machozi yalimtoka baada ya kuthibitisha ukweli wa mpenzi wake juu ya alichomwambia awali. Alirudi nyumbani kwao huku machozi yakilowanisha mashavu yake.



    Baada ya siku tatu , Jaqueline Wolper alirudi Dar-es-salaam. Aliamua kuandaa mkutano na waandishi wote wa habari hapa Tanzania na nchi jiirani.



    “nimeamua kuwaita ili mripoti taarifa hii muhimu katika maisha yangu. Kwanza kabisa napenda kutengua kauli yangu niliyosema kuwa nina mtoto mmoja.” Aliongea Wolper na kufanya ukumbi mzima kuguna.

    “nina watoto wawili. Ukiacha huyu Belinda mnayemjua, yupo mtoto wangu wa kwanza wa kiume niliyemzaa nikiwa na umri wa miaka kumi na nne tu. Kutokana na udhaifu wa mtoto na magonjwa yaliyomuandama, niliamua kumtelekeza kijijini kwa rafiki yangu na mimi kuja huku mjini kutafuta bahati yangu. Ndipo nilipompata M.r Poul Nyange ambaye ndio baba wa Brenda na kuninyooshea njia yangu ya kuwa msanii. Dhumuni la kuwaita, na ruhusa yangu kurusha live maelezo yangu kwa watu wa redio na tv, ni kumuomba radhi mwanangu. Nampenda sana na nipo tayari hata kumpigia magoti kwa makosa niliyomfanyia. Sina raha mama yake, nimeenda kijijini kumtafuta na nimemkosa. Nilichombulia ni maumivu tu kwa kupata taarifa za kifo cha rafiki yangu ambaye amamlea mwanangu. Kama unanisikia popote ulipo. Mama yako nakupenda na nakuhitaji nikuone hata kwa dakika moja nikuombe msamaha. Najua kila kilichoandikwa kwenye movie ya NO ONE KNOWS TOMMOROW ulikuwa unalenga kunifikishia ujumbe ili nikutambue. Nimekujua mwanangu Hussein. …. Nisamehe mwananguuuuu….”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jaqueline Wolper alishindwa kuendelea kuongea zaidi kutokana na machungu aliyokuwa nayo moyoni. Si yeye tu, bali ukumbi mzima ulizizima kwa majonzi na baadhi yao walianza kulia kutokana na ukweli huo uliowaumiza wengi.



    Wakati Jaqueline Wolper akiwa chini analia huku akibembelezwa na baadhi ya wasanii wenzake, kwa mbaali watu walizisikia hatua za watu watatu zikiingia pale ukumbini kupitia red capet iliyokuwa inaelekea kwenye stage.



    Mara ukumbi wote ulinyanyuka na kuanza kupiga makofi huku wakishangilia hali iliyomfanya Jaqueline Wolper kuinua kichwa chake na kuangalia mbele. Alipigwa na butwaa baada ya kumuona Aunt Ezekiel na JB wakiingia huku wamemuweka HUSSEIN katikati.



    Alinyanyuka na kuchomoka mithila ya mshale na kwenda kumkumbatia mwanaye huku akilia kilio cha Kwikwi.



    “nisamehe mwanangu.”

    Alilia Wolper na kumuangalia mwanaye ambaye nae alikua analia pasipo mfano.alichomoka Hussein mikononi mwa mama yake na kukimbilia stejini.

    Tukio hilo liliwashangaza watu wote baada ya kumuona Hussein akiokota mike huku akilia.

    “siwezi kukusamehe mama mpaka ukubali adhabu nitakayokupa.” Aliongea Hussein huku akilia kwa uchungu.

    “nipo tayari mwanagu kwa adhabu yoyote.” Aliongea Wolper huku analia. Ukumbi wote ulibaki kimya kusikiliza adhabu atakayo itoa Hussein.



    “adhabu yangu…… NJOO UNIKUMBATIE KAMA MWANAO UNIPENDAYE KWA DHATI KWAKUA NAKUPENDA ZAIDI YAKO.”



    Maneno hayo yalimfanya Jaqueline Wolper kumkimbilia tena mtoto wake na kumkumbatia. Ukumbi wote ulipiga makofi.

    Belinda nae hakuwa nyuma. Na yeye akaenda kumkubatia kaka yake huku wote nyuso zao zikionyesha kuwa na furaha lakini mashavu yalikuwa yamelowana macozi ya furaha.

    Waandisha wa habari nao hawakusubiri. Taarifa ile ilitambaa kwa kasi ya upepo na kila kona ya Africa na dunia kwa ujumla walipata habari ile ya Msanii bora wa kike Africa kuwa na mtoto aliyetengana naye kwa miaka 20.



    Familia hiyo ilitimia kwa Hussein kuamua kurudi kijijini na kumchukua mpenzi wake na kwenda kumtambulisha kwa mama yake. Mariamu alikua anaona kama ngekewa kukutana na Jaqueline Wolper na kutambulishwa kuwa ndio mama yake mkwe. Bila kusubiri, sherehe kubwa iliandaliwa na mama yake Hussein kwa ajili ya kumvisha pete ya uchunba Mariamu. Mama yake Mariamu naye alialikwa mjini na kushiriki sherehe hiyo ya aina yake iliyokuwa na wasanii wa fani mbali mbali waliofurika kitu ambacho hakijawahi kutokea Tanzania.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndoto za Hussein na mama yake zinatimia baada ya Jaqueline Wolper kutetea taji lake na Hussein kuchukua tuzo za mtunzi bora wa hadithi afrika. Pia alichukua tuzo za oscar kama muigizaji bora chipukizi



    IT`S HAPPENING

    THE END************



0 comments:

Post a Comment

Blog