Simulizi : Jestina
Sehemu Ya Nne (4)
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Asubuhi taarifa ya kwanza ilikuwa ni kifo cha Mark, huku ikisema bado mauaji hayo hajulikani yanasababishwa na nani. Lakini kilichowashtua watu ni kwamba wote waliokufa walikuwa ni marafiki tokea zamani sana, hivo kukaibua maswali mengi sana. Kituo kimoja cha televisheni kiliomba kufanya mahojiano na mwalimu mkuu wa shule ambayo inaaminika kuwa wote waliokufa wamesoma pale.
"habari yako mwalimu"
"nzuri nashkuru"
"kwa jina naitwa Anita ni mwandishi wa habari kutoka J76 news chanel"
"mimi naitwa Anthon Dickson, ni mwalimu mkuu hapa"
"naam mwalim unazungumziaje matukio haya ya mauaji yanayoendelea hapa mjini hasa ukizingatia wote walipoteza maisha mpaka sasa ni wananfunzi wako"
"kwa kweli ni vigumu kueleza"
"kivipi mwalimu"
"unajua ndugu Anita hapa kulitokea kesi kubwa sana ya ubakaji kama utakuwa unakumbuka, ni takriban miaka kumi sasa imepita na inavosemekana kuna wananfunzi wamehusika na tukio hilo"
"unaweza kuwataja"
"hapana siruhusiwi kufanya hivo"
"na kwanini hasa ukawa unahisi kama mauaji yanayofanyika sasa ya uhusiano wowote na kilichotokea miaka kumi nyuma"
"Unajua tulivokuwa wadogo, tulikuwa tukisimuliwa mambo mengi sana ambayo wengi wetu hatuyaamini"
"kama yapi"
"kwa mfano najua utakuwa umesimuliwa kuhusu ulimwengu wa watu waliodhulumiwa"
"ndio lakini hizo ni hadithi za kufikirika tu"
"hapo ndio kwenye utata sasa na hilo ndilo linalotokea saa hivi, baada kufanyika tukio lile kesi ilipelekwa mahakamani lakini cha ajabu ilizimwa haraka na watuhumiwa wakaacha huru, kwa sababu haki haikupatikana, sasa aliedhulumiwa amerudi kuja kuitafuta haki kwa mikono yake kama tunavojua HAKI ISIPOPATIKANA KWA AMANI BASI ITAPATIKANA KWA VITA. Na hii ni vita ambayo hakuna mtu yoyote kati yetu anaeweza kuizua na kama huamini kama mizimu ipo heebu jaribu siku moja kuuwa halafu uachiwe huru uone kama hutokipata walichokipata hawa vijana walikufa"
Mwalimu mkuu alimaliza kuongea na kuomba kuondoka akaendelee na majukumu mengine ya kawaida. Na kwa sababu kipindi hicho kilikuwa hewani live kila mtu alishuhudia, "ni bora wafe tu ili watu wajue kama haki ya mtu ni mali", "pumbavu nani atakaa aamini upumbavu ule". "mmmh makubwa mi nlijua ni hadithi tu za kufikirika", hayo ni baadhi ya maneno yaliokuwa yakisemwa na baadhi ya watu kila pahali. Kwa kweli story ilikuwa ni hiyo tu kila kona unayopita, Alwin ni miongoni mwa watu waliokiona kipindi hicho na kufurahia sana majibu ya mwalimu, yalitosha kupeleke ujumbe kwa wote ambao wanacheza na haki za watu.
"jamani hali imezidi kuwa mbaya sasa" Jay aliongea katika kikao kifupi cha dahrura kilichoitisha baada ya kifo cha Mark. "sasa tunafanyaje" aliuliza Monica, "ah hatuna la kufanya, sisi tulitenda uovu huku tukifurahia bila kufikiria ni kiasi gani tulichowaumiza wengine" Jay aliongea akionekana kujuta sasa. "akah! we vipi sasa unajuta nini, mi nasema hapa cha msingi ni kumuua Alwin maana nahisi yeye ndie anetufanyia mchezo huu" alifoka Alex kwa hasira. "sasa umeona ulivokuwa huna akili unataka kurekebisha kosa moja kwa kutenda jingine" Jay alimjibu akionekana kuchukizwa na maneno ya Alex. "mi nlikwambieni huyo boya ni mtoto wa mama" aliongea Alex na kumkejeli Jay, "sawa mi ni mtoto wa mama, lakini mi naona bora tujiandae kufa tu maana hatujui anefuata ni nani" Jay aliongea na kuinuka kisha akaanza kutoka nje, "nenda huko na leo utakufa wewe, Jestina kama unanisikia leo Jay amejianda ukamuue sawa" aliongea Alex na kufanya mzaha.
Jay hakujibu kitu,wakati anatoka aliingia unyonge wa ghafla na kupatwa na homa kali sana iliomfanya aanguke barabarani. Wasamaria wema walipiga simu hospitali na punde gari ya kubebea wagonjwa ilifika na kumuawahisha hospitali. Alipofika tu alipatiwa huduma ya kwanza na kupelekwa chumba cha wagonjwa mahututi kutokana na hali yake kuwa mbaya sana. Familia yake ilifka akiwemo mkewe na mwanae wa kike mwenye umri wa miaka minne, lakini hawakuruhuisiwa kumuona kutokana na kuwa hali yake haikuwa nzuri. Hali hiyo ilimtia simanzi mkewe kumuona mumewe yupo katika hali mbaya sana lakini angefanyaje na alitakiwa kusubiri..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walisubiri mpaka jioni lakini hali yake haikuchanganya hico wakaambiwa waondoke na warudi kesho kwa ajili ya kumuangalia walikubaliana na daktaru na kuondoka. Kiza kilianza kuingia lakini bado hali ya Jay haikutengemaa kabisa "kwa kweli tumejaribu kadri ya uwezo wetu sasa ni muda wa kumuachia Mungu atende muujiza" aliongea daktari mmoja na wenzake wakamuunga mkono. Walizima vifaa vyote na kumuhamisha chumba, huko walimuunganisha na mashine ya kupumulia kwa ajili ya msaada maana hata pumzi ilikuwa ni ngumu kuvuta. Baada ya hapo walitoka wote na kumuacha chini ya uangalizi wa manesi.
"Jay.....amka" alisikia sauti ikimuamsha huku akitingishwa, kwa uvivu alifungua macho na mbele yake alikuwa Jestina amesimama akiwa na sura yake ya kawaida, sio ile ya kutisha. "najua umekuja kulipiza" aliongea Jay huku akiitoa mashine ya kupumulia, "lakini nina ombi moja tu kwako, naomba uniache mpaka kesho angalau nimuone mwanangu kwa mara ya mwisho kabla ya kuaga dunia" aliongea Jay kwa masikitiko makubwa. "kwanini ulikubali kushuhudia unyama ule" aliuliza Jestina huku uso wake ukianza kubadilika na kuwa wa kutisha. "kwa kweli siku ile sikutegemea kama kungetokea tukio kama lile" alijibu Jay kiunyonge, "lakini wakati linafanyika ulikuwa na uwezo wa kuzuia lisifanyika" aliongea Jestina akizidi kutisha. "hilo ndio linalonijutisha mpaka leo" aliongea Jay huku machozi yakianza kumtoka, "najua kama nimekukosea na niko tayari kulipa kwa nilolitenda, lakini naomba unipe siku moja tu japo nimuone mwanangu na mke wangu kisha njoo unimalize" Aliendelea kuongea Jay huku kilio kikipamba moto, alijaribu kujifuta lakini aliposusha mkono Jestina alikuwa kashaatoweka. "asante kwa kunikubalia ombi langu" aliongea huku akijiweka vizuri kitandani na kuendelea kulala.
Asubuhi mapema familia yake ilifika kumuona, "nini kimekusibu baba Sophia" aliongea mkewe huku akimuangalia kwa huruma, "hata mimi mwenyewe sijui, homa tu ilinishika ghafla" alijibu huku akilazimisha kutabasamu. "pole mume wangu" aliongea mkewe kumpiga busu katika paji la uso, "pole dady utapona" sauti ya Sophia iliskika huku akimpa pipi baba yake. Sophia alikuwa kafanana sana na baba yake, na alimpenda sana. "Sophia baby njoo nkwambie kitu" Jay alimuita mwanae na kumnong'oneza kitu, Sophia alitabasamu na kumrukia baba yake kisha akasema " wewe ni baba mzuri kuliko wote". Muda wa kutizama wagonjwa uliisha na familia yake iliaga na kuondoka huku wakiahidi kurudi kesho yake kwa ajili ya taratibu za kwenda nae nyumbani. Aliagana nao huku machozi yakimtoka maana alielewa hiyo ilikuwa ni siku yake ya mwisho duniani. Kutokana na hali yake kuimarika mashine za msaada wa kupumua ziliondolewa na kupelekwa chumba cha wagonjwa wa kawaida tu. Aliendelea kupata matibabu madogomadogo, lakini akilini mwake alikuwa akiwaona kama madaktari wanatwangaa maji kwenye kinu maana usiku wa siku hiyo ni usiku wa kifo chake.
Usiku hatimae ulifika na Jay alikuwa tayari kwaajili ya kufa tu maana alielewa kabisa ni aina gani ya mauaji anayofanya Jestina. "Jay, naona uko tayari kwa adhabu yako" alimsikia Jestina akimwambia wakati akiwa amepumzika. "ndio niko tayari kwa chochote" alijibu Jay huku akitetemeka, "Kwa vile umelitambua kosa lako na kulijutia, mimi sikuja hapa kukuuwa maana kwanza una mke anaekuthamini sana na pili una mtoto ambae bado anahitaji malezi yako na upendo wako kama baba yake" aliongea Jestina na kujitokeza mbele ya Jay akiwa katika umbile la kibinaadamu "lakini nataka ufanye kitu kimoja, usijaribu kutoa ushahidi kokote pale na pia nakupa siku tatu uondoke Mashvile na familia yako yote, nenda mbali sana na uwe baba mwema kwa mwanao na pia mume mwema kwa mkeo. Na jengine asijue hata mmoja miongoni mwa marafiki zako waliohusika na kifo changu. Mimi nimekusamehe na nakutakia maisha mema na yenye amani tele lakini kumbuka ukitovukwa adabu nitakurudia" alimaliza kuongea Jestina na kuoweka. Jay hakuamini kama kasamehewa maana alielewa kabisa kuwa Jestina alikuwa hataki masihara, alilala usingizi mzuri huku akijiapiza kufanya yote aliyoambiwa.
*******************
Mapema siku ya iliyofuata familia yake ilifika na taratibu za kutoka hospitali zikafanyika, baada ya kufika kwake alimueleza mkewe kuwa anataka kuhama Mashvile kwani amepata kazi nzuri nchini Italy. Aliwaeleza pia wazazi wake swala hilo na kwa vile yeye ndie aliekuwa analisha familia hakuna aliempinga, maandalizi ya safari yalifanyika kimya kimya bila hata rafiki yake mmoja kujua. Jioni yalikuwa yamekamilika na wote waliondoka mjini Mashvile "nakuahidi Jestina nitatekeleza yote ualionambia" aliongea maneno hayo kimoyomoyo wakati analipita bango liliandikwa KWA HERI MASHVILE.
"Oya Alex mtu wangu mbona tokea jana sijamsikia Jay" Patrick alimuuliza Alex ambae alikuwa bize akijaribu kumchora mwanadada mmoja ambe alionekana kudance vizuri sana, "ah mara mwisho niliskia kalazawa hospitali, lakini nahisi Jestina atakua kashampitia tayari" alijibu Alex na kuinuka kulekea katika ulingo wa kudance lakini nia na madhumuni yake ilikuwa ni kwa ajili ya yule mschana. "habari yako mrembo"
"safi tu".CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mimi naitwa Alex sijui mwenzangu"
"ahaa mimi naitwa Jessie"
"jina lako zuri, tunaweza tukasogea pembeni tukaongea mawili matatu"
"hamna shida"
basi walisogea mpaka counter na Alex akaagiza vinywaji kisha wakaanza kuongea, waliongea sana mwisho walionekana kukubaliana "oya Patrick wacha mi nitoke na shemeji yako" Alex alimuita Patrick na kumwambia, "oya mwanangu mtoto huyo mkali, kama vipi tupige tungo" Patrick alimnong'oneza Alex. "tulia mtu wangu mi naenda nae geto nikimaliza kula asali na kutwangia na wewe uje kuonja mtu wangu" aliongea na wakakubaliana.
Patrick alirudi kwenye dance floor huku Alex akiondoka na Jessie, "tunaenda wapi sasa" aliuliza Jessie, "ah nyumbani kwangu si mbali na hapa" alijibu Alex na kuzungusha mkono wake kwenye nyonga ya binti huyo. Mwendo ulikwa wa dakika tano tu hatimae walifika geto na kumkaribisha ndani. "kaa kitandani hapo nakuja" aliongea Alex na kuingia chooni, kumbe alikwenda kutega camera ili ajirikodi anavomkuna mrembo huyo. Alirudi na kumkuta tayari ameshavua nguo na kubakia mtupu, tamaa ya ngono ilimpanda Alex kujikuta anamvamia lakini kabla hajafikisha mdomo wake kwenye midomo ya mrembo huyo alijikuta akirushwa kwa nguvu.
Ghafla mrembo huyo alianza kubadilika, naam hakuwa mwengine isipokuwa Jestina. "wewe hujabadilika hata kidogo" aliongea kwa nguvu sana, "yaani bado wewe na yule mshenzi mwenzako mlikuwa mnafikiri kupiga mtungo" aliendele kuongea huku akimsogelea. "Jestina nisamehe" alianza kuomba msamaha, "umechelewa sana" alijibu Jestina na kupiga kofi la uso akimwachia alama za kucha. Alex aliweweseka lakini alipofungua macho hakumuona ila ghafla akamtokea kwa nyuma na kumchana mgongoni. Alex alipiga yowe la kuomba msaada lakini wapi hakuna lolote lilisikilikana nje ya chumba hicho. Jestina akatoweka tena na kumtokea mbel yake ila hakumgusa alimuangalia tu usoni na Alex mwenyewe akaokota kipande cha kioo na kunaza kujichana. Alipiga kelele kwa maumivu lakini alishindwa kujizuia mwisho alianguka chini, hapo Jestina alimsogelea na kumpiga kucha za shingo na kulitoa koromeo, aliacha ujumbe na kutoweka huku Alex akiwa chini akijaribu kuvuta pumzi ambayo haikua na pakupita mpaka mwisho akakata roho. Patrick baada kuona Alex hapigi simu aliamu kutoka na kumfata geto.
Kwa mwendo wa haraka Patrick alifka geto kwa Alex na kukuta mlango umefungwa lakini kila alipojaribu kugonga haukufunguliwa. Alisubiri kama dakika kumi kumi hivi ila bado kulikuwa kimya, mwisho alikumbuka kuwa ana ufunguo mwengine wa mlango huo lakinialipojaribu kuingiza kwenye kitasa uligoma hiyo ilikuwa ni ishara kuwa kulikua na ufunguo mwingine kwa ndani. Baada kuona jitihada zake zimegonga mwamba aliamua kutoa simu yake na kuandika ujmbe "poa mshkaji wangu tumekubaliana vipi na wewe unafanya nini, mbona mimi nikipata kama hivo tunapiga mtungo safi ila haina noma" aliutuma na kuondoka. Aliondoka na kuelekea nyumbani kwao, baada kufika alivua nguo zake na kwenda kujimwagia maji. Alimaliza na kutoka kurudi chumbani na hapo ndipo aliposhtuka kidogo maana suruali yake chini ilikuwa imeganda damu. Alitahidi kutafuta ni sehemu gani ameumia lakini hakuiona ndipo machale yakamcheza lakini akapotezea na kuingia kitandani.
Asubuhi mapema aliwahi kuamka nakwenda geto kwa Alex, alipofika alishtuka sana baada kuona michirizi ya damu ikitokea ndani ya chumba hicho. Alipiga kelele na watu wakaja kwa pamoja walisaidiana kuvunjia mlango na hapo ndipo wakakutana na mwili wa Alex umelela sakafuni huku ukiwa umetapakaa damu. Bila kuchelewa walipiga simu polisi na kutoa taarifa, ila alichokifanya Patrick ni kuchukua simu ya Alex na kuufuta ujumbe aliomtumia ili asije akaonekana yupo hatiani. Haukupita muda polisi walifika eneo la tukio na kuanza kufanya uchunguzi na katik tafuta yao walifanikiwa kuipata camera alioitega Alex na kuichukua kama sehemu moja ya ushahidi wao. Walimaliza kufanya uchunguzi na taratibu nyingine zikafuata ikiwa ni pamoja na kuupeleka mwili wa Alex hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
"tumefanikiwa kupata camera sehemu ya tukio" aliongea polisi mmoja na kumkabidhi Inspector Hans ile camera. Na yeye bila kuchelewa aliunganisha na computer yake na kuanza kuangalia, ilionyesha Alex akitoka chooni na alipofika kitandani alijirusha lakini hakuonekana mtu mwengine katika kitanda hicho. Lakini ghafla alichomoka kitandani na kujigonga ukutani kisha akaonekana kama akiomba msamaha lakini ghafla alipiga kelele na damu kuanza kumtoka. Waliendelea kuangalia video hiyo mpaka walipoona anachukua kioo na kuanza kujikata wenyewe mpaka akaanguka chini na ghafla akaanza kutoka damu shingoni kama ishara kuwa amekachinjwa, yakatokea maandishi ukutani "AMELIPA". Hapo camera ikaingia chenga na kuzima kabisa,askari wengi waliotizama ile video walishtuka sana hasa pale yalipotokea maandshi ukutani..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"mi si niliwaambia kama mauaji haya hayafanywi na mtu wa kawaida" aliongea Inspecta Hans na kuwaangalia wenzake "sasa mmeamini kama kuna mizimu duniani" aliendelea kuongea lakini alionesha kama kushtuka kidogo na kuamua kurudia kuingalia tena kwa mara ya pili lakini kwa makini zaidi, ndipo akagundua kama shape ya mschana kama iliokuwa inaakisi mwanga. Wenzake walimshangaa na kumuuliza mbona anaangalia tena. "hebu angalieni kwa makini hiyo video kwa mbali sana utaona kama shape ya mschana" aliwaambia na wote wakaikodolea macho ndipo wengi wakagundua kile alichokisema Inspecta Hans.
Alwin akiwa kwao alifutwa na askari kuombwa aende kituoni kwa ajili ya majadiliano, alikubali bila kinyongo na kuondoka nao. walifika kituoni na kuanza mazungumzo.
"kijana hebu tueleze kuhusiana na Jestina"
"mimi sina la kueleza"
"tunaomba msaada wako maana mauaji yamezidi na yantupa sifa mbaya kama kitengo cha polisi"
"sasa mimi niwaambie nini wakati kesi yake ilifikishwa kwenu miaka kumi iliopita lakini mkajifanya wababe kuipindisha sheria, kwa kupewa pesa mkanibambikia mimi"
"tusaidie basi tuweze kumdhibiti"
"hahaha mna kichaa kweli nyinyi, kiufupi mumechelewa sana amerudi mwenyewe kuja kuiweka sawa sheria na nyinyi hakuna mnaloweza kufanya kilichobaki nyie kaeni tu musubiri kukusanya miili ya atakao waua"
"kijana unajifanya jeuri si ndio" inpecta Brandon alifoka
"tena wewe haswaa umo katika list yangu" Alwin aliongea maneno hayo na ghafla alianza kubadilika na kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Naam walilipata jibu kumbe hakuwa Alwin bali alikuwa ni mwenyewe Jestina na aliamua kufanya hivo kumpa onyo Inspecta Brandon na polisi wengine juu ya mpango wa kupenda pesa na kupindisha sheria. Kushuhudia hivo Inspecta Brandon alianguka chini na kupoteza fahamu.
"mimi niliwaambia mkaniona namtetea Alwin, sikusema tu ila yalishaanikuta ndio maana nikawaambia haitasaidia hata kama mtamkamata Alwin kwa sababu Jestina ndie anaejibu ukimwita Alwin" aliongea Inspecta Hans, "unamaanisha nini kusema hivyo" aliuliza askari mwingine. "namaanisha kuwa Jestina anatumia sura ya Alwin, hivyo basi hata ukimhoji utaishia kukipata kama kilichompta Inspecta Brandon muda mfupi uliopita" aliposema hivo ndio wakakumbuka kama mkuu wao ameanguka, haraka walimbeba na kumuwahisha hosptali.
******************************
Ndege ilitua uwanja wa Mashvile, miongon mwa abiria walioshuka alikuwemo binti mmoja mrembo sana. Hakuwa mwengine isipokuwa ni mtoto wa Profesa Alexander Harison, Miryam. Baada ya miaka mingi sasa ndio anarudi nyumbani akitoka kuchukua masters katika udaktari akiwa kama daktari bingwa saikolojia. Alitoka nje ya uwanja na kuonana na baba yake mzazi "karibu nyumbani mwanangu" profesa aliongea huku akitanua mikono kama ishara ya kutaka kumkumbatia mwanae. Miryam kwa furaha aliruka na kumkumbatia baba yake. "umekuwa mkubwa mwanangu" aliongea profesa, "ah kawaida tu baba" Miryam alijibu na kuachia tabasamu na kuufanya uzuri wake uonekane vilivyo. "mie ningapata mtoto kama yule pia nisingefikiria kuoa mke mwengine", "dah yule mtoto ni mkali kupindukia kiasi profesa ampe kila anachotak", "sasa wewe unadhani acheze zawadi kama ile kutoka kwa muumba, kama angekuwa mwanangu angetaka hata dunia ningempa". Hayo ni maneo yalikuwa yakisemwa na walinzi walipokuwa wakimpokea mtoto wa bosi wao.
Waliingia kwenye gari na safari ikaanza, msafara huo ulikuwa ni zaidi ya ule wa raisi, ulikuwa na gari kumi zote aina Rolls royce nyeusi zikisindikizwa na pikipiki tatu mbele na tatu nyuma. Kwa kweli profesa alimpenda sana mwanae kiasi kwamba hakujali anatumia kiasi gani cha fedha kumhudumia tu. Alimpa kila alichotaka na hakusita kumwambia "WEWE NI LULU YA MAISHA YANGU". Mapenzi yake kwa mtoto wake hayakuwa na hayakufanana na chochote. Ila alijua ipo siku itabidi amkabidhi kwa mtu mwengine ili amlee, akimaanisha kuwa ipo siku mwanae pekee ataolewa na kuondoka nyumbani. Na kila alipoifikiria siku hiyo alihisi kama nusu na robo ya maisha yake atakua kayatoa, kuna baadhi ya wakati alijikuta akibubujikwa na machozi lakini angefanyaje na ndio mfumo wa maisha ulivo.
Walifika nyumbani na kupokewa kwa shangwe kubwa hasa ukizingatia anapokuwepo Miryam katika nyumba hio kila siku ni skukuu. Maana binti huyo kajaaliwa upendo wa hali ya juu sana kiasi kwamba wafanyakazi wote walikuwa wawazi katika kuongea nae, Ni mschana ambae hakujiona kwa uzuri wake na utajiri aliokuwa nao bali aliishi na watu wote kama sehemu ya familia yake. "Afadhali amerudi", "nakwambia huyu mtoto ni baraka ndani ya nyumba hii", "hata leo profesa aseme hana mshahara wa kutulipa basi mie nitafanya kazi bure ilimradi niwe karibu tu na Miryam". wafanyakazi wa kike hawakuwa nyuma katika kummwagia sifa binti huyo wa profesa maana aliuteka moyo wa kila mtu alikuwa ndani ya nyumba yao.
Kutokana na machofu ya safari, Miryam alioga na kupumzika. Upande wa Alwin alikuwa hafahamu chochote kuhusiana na ujio wa Miryam na hata profesa alikubaliana na mwanae kuwa asimwambie chochote..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sasa kutokana na kilichoonekana kwenye kamera askari wote waliamini kama kuzuia mauaji hayo ni sawa na kuzuia mawimbi baharini. Kila asakri aliamua kushughulika na mambo yake pasi na kuwaza tena njia za kumkamata muuaji, walijisemea "muache auwe tutakwena kukusanya mizoga". Jestina akiwa chumbani kwa Alwin ghafla hali ya hewa ilibadilika ghafla na kutoweka bila yeye mwenyewe kutaka, funga fungua alijikuta yupo kule katika ulimwengu wa waliodhulumiwa. "karibu tena Jestina" aliongea yule malkia, "mbona umenirudisha huku wakati sijamaliza kazi yangu" aliongea akionekana kuchukia kidogo. "kuna jambo nataka nikueleze kwanza ndio utarudi tena katika ulimwengu wa kibinaadamu" baada kusikia hivo kidogo akapoa. "Muda wako wa kukaa huko unakaribia kuisha" aliongea malikia na kumshtuwa kidogo Jestina, "si umenambia muda wangu utakwisha mpaka pale nitakapo wamaliza wote" aliongea Jestina kwa sintofahamu. "ndio, ilikuwa iwe hivyo lakini muda si mrefu utaanza kukutana na kikwazo" alijibu malikia, "na hicho kikwazo kitakufanya upumgukiwe nguvu za kuishi katika ulimwengu wa kibinaadamu", "nambie ni kikwazo gani hicho nikakiondoe mapema" aliaongea Jestina huku akianza kubadilika kwa hasira. "hutoweza kukiondoa hata uwe na nguvu kiasi gani hata mimi pia sikuweza kukiondoa wakati wangu" alijibu malikia akionesha ugumu wa kukiondoa kikwazo hicho. "basi nambie kikwazo chenyewe ni kipi" aliomba sasa Jestina, "MIRYAM" malikia alijibu huku akitetemeka.
"ah kumbe huyo tu" aliongea Jestina kwa dharau kidogo, "hiyo ni kutokana na mapenzi mazito aliokuwa nayo juu ya Alwin na jambo ambalo wewe hulijui ni kwamba Alwin anampenda sana Miryam japo hajawahi kumuona tokea azinduke, ila kwa sasa Miryam amerudi kutoka masomoni na akianza tu kuwasiliana na Alwin mapenzi yao yatamea tena jambo ambalo litamfanya Alwin aanze kusahau mambo mengine ikiwemo kisasi anachokusaidia kukikamilisha" aliongea malikia na hapo Jestina aliishiwa ujanja.
"lakini kuna kitu unaweza kukifanya ili kuendelea kubakia ulimwengu wa kibinaadamu" aliongea malikia, "kitu gani hicho". "usiwaingilia katika mapenzi yao wala usijaribu kumsogelea Miryam kwa ubaya maana katika ulimwengu hakuna vita kubwa kama ya mapenzi, pia hayohayo mapenzi ni amani ya kutosha" aliongea malikia. "sasa umesema wakianza kukutana mimi nitapoteza nguvu zangu" aliuliza Jestina, "utaweza kuwa nazo ikiwa Alwin atamueleza Miryam juu ya uwepo wa mzimu wako na kama atakubali bila kinyongo na kuamini kama ni kweli basi hapo utakuwa umeshinda maana hata nguvu zako zitaongezeka kwa sababu utakuwa na watu wawili ambao walikupenda sana kipindi cha uhai wako japo mwenyewe hukulifahamu hilo" alimaliza kuongea Malikia na kabla Jestina hajajibu chochote alitoweka na kurudi katika ulimwengu wa binaadamu. Alimkuta Alwin kalala fofofo, alisogea mpaka pembeni yake na kukaa. Alimuangalia kwa muda sana kisha akajilaumu kwa kumpa wakati mgumu sana kipindi cha uhai wake japo alimuonyesha ni kiasi alimpenda na kumjali, lakini kutokana na wivu wake wakimasomo hakutaka kumkubalia bali aliamua kumtesa kwa kutoka na mwanaume mwengine ambae baadae aliamua kumfanyi ukatili wa hali ya juu sana. Machozi yalianza kumtoka na kujikuta ni mwanamke asie na shukurania hata kidogo. Pia alikumbuka kipindi akiwa na urafiki na Miryam mschana ambae walitokea kupendana sana kutoka na tabia zao kuendana sana japo kiakili hakuwa na akili kama yeye "ama kweli kuwa na akili nyingi si kuwa na maarifa" alijisemea moyoni huku akihisi maumivu makali ya usaliti aliowatendea wawili hao pasi na kumthamini sana. Ila angefanyaje na ndio mambo yashaatokea hata kama angetaka kuyarekebisha isingewezekana maana tayari alishaaga dunia.
*****************************
Usiku uliingia huku maandalizi ya sherehe kubwa ya yakifanyika, ilikuwa ni sherehe ya kumkaribisha Miryam. Alwin akiwa kwao aliskia akiitwa na mama yake na aliposhuka alikutana na mtu asie mfahamu. Alikuwa na briefcase mkononi, "Mr Alwin huu ni mzigo wako" aliongea na kumkabidhi kisha bila kuongea kitu yeye aliondoka. Alwin alirudi chumbani kuufungua mzigo huo, alishangaa kuona kuna suti ya rangi ya maziwa au crem, viatu, tai nyekundu pamoja na funguo ya usafir. Pembeni kulikuwa na barua ndogo iliosema hivi.
"jiandae uje nyumbani kwangu by Profesa", yeye akiitwa na profesa huwa hafikirii mara mbili, aliingia chooni na kujimwagia maji. Alipomaliza alitinga suti alioletewa na kuning'iniza tai shingoni, alivaa viatu na kuchukua funguo lakini alipaongalia vizuri aliona saa moja matata sana na yeye bila kuchelewa aliitia mkononi na kuhakikisha kuwa amechukua kila kilicho ndani ya briefcase hilo. Alipojiridhisha yuko sawa alitoka chumbani kwake na kuelekea nje, aliwaaga wazazi wake na kutoka. Nje huko alikutana na gari moja ya bei mbaya aina ya Buggtti supersport vitesse ya rangi ya maziwa. Hakuuliza alibonyeza kitufe na kutoa loki, aliingia kwenye gari na safari ya kuelekea kwa profesa ilianza, kwa mwendo wa umakini zaidi alitumia dakika kama saba hivi kufika mjengoni kwa profesa..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alishuka gari na kumkabidhi funguo mlinzi aende akaiweke maegesho, "na sasa anaingia mgeni rasmi wa kwanza Mr Alwin Kelvin" MC alitangaza na ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe. "mmh jamani huyu kapendezaje", "wee jifanye mwendawazimu tu mali ya watu hiyo shosti". "sasa kwani mimi jiwe" hayo ni maneno waliokuwa wakiongea waschana wawili ambao walivutiwa sana ujio wa Alwin.
Basi aliekezwa meza kuu na kuambiwa akae kwenye kiti, "profesa kuna nini mbona unafanya sherehe" aliuliza Alwin "mambo matamu hayataki haraka" alijibu Profesa na hapo Alwin alielewa kuwa anatakiwa asiulize tena maswali. "na sasa tumkairbishe mgeni rasmi mwengine ambae pia ndie mlengwa mkuu wa sherehe hii Ms Miryam Alexander Harison" MC alitangaza tena na kuwafanya watu wachizike kwa makelele. Alwin alijikuta akitumbua macho kama mjusi aliebanwa na mlango huku akihisi hata moyo wake ulipunguza kasi ya mapigo, bila kujitmbua alijikuta akisemama na kuelekea kwenye ngazi ambapo Miryam alikuwa anashuka, hakuna aliemuuliza watu wote walitengeza njia ili apite bila kikwazo. "kwa kweli umependeza sana" alisema maneno hayo huku akimpa mkono Miryam, "asante hata wewe umependeza pia" alijibu Miryam. walitembea wawili hao huku wameshikana mikono utadhani ni mfalme na malkia wake mpaka kwenye meza.
**************************
Kimbembe kilikuwa kwa Patrick amabe alikuwa anapambana kutetea maisha yake, "Jestina najua nimekukosea naomba unisamehe", "ulikuwa na muda mwingi wa kutubu lakini hukufikiria hilo" Jestina aliongea kwa hasira mpaka radi zikawa zinapiga. Lakini ghafla alianza kupotea bila mpango, Patrick alipoona adui yake anapoteza muelekeo akaamua kutoka nduki. "Alwin nakuomba subiri japo kidogo nimalizane na huyu kwanza" aliongea katika moyo wake, na papo hapo akatoweka na kumtokea Patrick kwa mbele, bila kuchelewa alimpiga kucha za koromeo na kumuulia mbali. Alimpa kifo cha haraka makusudi ili asije akapoteza nguvu kabisa, Patrick alianguka chini kama mzigo huku damu nyingi zikimtoka shingoni. Taratibu Jestina alianza kutoweka kama vile unavofuta mchoro wa penseli kwa ufutio, nguvu zilinza kumuisha na kuanza kusikia maumivu makali sana. Aliona njia peke ya kujinusuru na kutoweka kabisa ni kwenda alipo Alwin na kumueleza yanayomkuta. Kwa nguvu zake kidogo zilizobakia alifanikiwa kutoweka na kutokea nyumbani kwa profesa. Na moja kwa moja alitokea mbele ya Alwin lakini alishangaa na kuona hata Alwin alikuwa hamuoni tena.
Alijaribu sana kumtokea mbele yake lakini hali ilikuwa ileile, kwa wakati ule Alwin alisahau kila kitu kiasi cha kuwa akili yake ilikuwa ikiutathmini uzuri wa Miryam tu. Baada kuona haonekani mbele ya Alwin, akaona njia pekee ya kuongea na Alwin ni kwa kutumia mwili wa mtu mwengine, alizunguka ndani ya ukumbi huo mpaka alipopata mtu wa kumtumia. Hapo aliuingia mwili huo na kuelekea alipo Alwin, "Alwin tunaweza kuongea kidogo" aliongea na kumfanya Alwin kugeuka lakini hakushughulika sana kwa sababu mwanamke aliemuita wala yeye hamjui. Alijaribu kumuita tena lakini haliilikuwa ni ile ile ndipo akaamua kumgusa mkononi, hapo Alwin alizinduka na kumgeukia kwasababu mwili wake ulikuwa wa baridi haswaa.
"Jestina unafanya nini hapa" aliuliza kwa sauti ya chini, "Alwin nakuomba nisikilize kwa makini sana" Jestina aliongea na kumvuta pembeni na kumueleza kila kitu. Alwin alishtuka kidogo baada kusikia vile, "subiri nikamwite Miryam" aliongea na kuondoka. "Miryam tunaweza kwenda kuongea varanda" nae Miryam hakukataa waliongozana mpaka varanda na kuanza kumueleza kila kitu, mwanzo Miryam alionekana kusita. "najua utakuwa huamini, subiri ni nimwite lakini nakuomba usipige kelele" aliongea Alwin baada kuona Miryam anakuwa mgumu kumuelewa. "Jestina jitokeze mbele yake ili akuone". Ghafla Jestina akatokea mbele ya Miryam "Mungu wangu, hivi ni kweli au nasinzia" yaliomtoka maneno hayo bila kujitambua. "Miryam nakuomba unisamehe kwa yale yote nlokukosea kwa sasa naomba unikubali kama rafiki yako kwa mara nyingine tena" aliongea Jestina huku akijitahidi asibadilike.
"Jestina mimi nilishaasahau hasa kama tuligombana mimi na wewe, siku ile nilitaka ufahamu tu kama ulikuwa ukiwaumiza watu wasio na hatia" Aliongea Miryam huku akimsogelea, "kama alivyoniambia Alwin kuwa umerudi kuja kuwalipisha waliokutenda basi mim niko pamoja na wewe" aliongea na hapo alikuwa karibu yake sana, aliamua kumshika mkono ili ajiridhishe kama kweli aliokuwa mbele yake. Alpomshika tu Jestina alitoweka na kumfanya Miryam ashangae kidogo "wow! Alwin its fantastic" aliongea huku akimkubatia Alwin kwa nguvu, "kama sheria ilishindwa kumpatia rafiki yangu haki yake basi mimi niko pamoja na nyinyi katika kuwateketeza wale wote waliohusika na kifo chake" Miryam aliongea lakini sauti yake ilikuwa imebadilika kidogo, Alwin alijitoa na kumwangalia "mbona unalia sasa" aliuliza kwa mshangao. "Alwin najua ulikuwa ukidhani namchukia sana Jestina, ukweli ni kwamba nilikuwa nampenda sana na ndio maana sikutaka apotee" aliongea Miryam kwa kwikwi. "usijali mpenzi wale wote waliohusika na kifo chake watalipa kwa maisha yao" Aliongea Alwin na kwa mara ya kwanza alimvuta Miryam na kukutanisha midomo yao au kama wanavyosema wengine "ROMANCE".
Kwa upande wa Jestina huo ulikuwa ni msimu mpya, maana alihisi mwili wake umepata uhai tena. Nguvu zake ziliongezeka mara dufu, wakati alizidi kutisha kiasi kwamba akikutokea tu kama unariho nyepesi basi unaweza kuaga dunia. Mvua ilianza kunyesha na radi zikawa zinapiga kwa nguvu sana hadi umeme ukazimika, "hahaha mlobakia jiandaeni" aliongea na kutoweka kisha hali ikarudi kuwa kawaida na umeme ukarudi..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alwin na Miryam walirudi uwanjani huku wakiwa wameshikana viunoni, moja kwa moja mpaka meza kuu. "Profesa" Alwin aliita kwa sauti ya chini, "sema Alwin" alijibu profesa huku akimuangalia. "nataka kukuibia kitu"
"wewe mtoto we, kitu gani hicho"
"ni kitu unachokipenda sana katika maisha yako" Profesa aliposikia hivyo akaelewa Alwin anamaanisha nini. Alisimama na kuelekea kwa MC kisha akachukua kipaza sauti na kuomba watu wamsikilize. "mabibi na mabwana naomba muniazime masikio yenu kwa dakika chache, ule muda niliokuwa nikiusubiria kwa hamu umefika, hatimae Mungu ameitika maombi yangu. Nawaomba wageni rasmi wasogee hapa jukwaani" aliongea na Alwin na Miryam wakainuka na kuelekea jukwaani. "napenda kumtambulisha kwenu rasmi Mr Alwin Kelvin ni mkwe wangu wangu kuanzia sasa" aliongea na ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe "hongera kijana na karibu katika familia" aliongea tena na kukumbatiana na Alwin kisha akairudisha mike kwa MC na kumwambia aendelee na ratiba.
Wakati wakiendelea na sherehe, aliingia mwanamke mwengine aliekuwa mzuri kupita maelezo. Vidume vyote vilianza kutokwa na mate ya kumtamani mwanamke huyo ambae alivaa nguo iliong'ara sana. Alitembea taratibu mpaka alipo Alwin na Miryam "hongereani sana" aliongea na hapo Alwin akashtuka baada kusikia sauti hiyo maana aliifahamu vilivyo kama ilikuwa ni sauti ya Jestina. "duh umebadilika" alikuta akiongea, "Jestina" Miryam aliita. "ndio mwenyewe" Jestina alijibu, Miryam alishindwa kujizuia na kumkumbatia bila kujali kama ule ni mzimu. Marafiki hao watatu waliongea na kufurahi sana, waliongea kama walivyokuwa wakiongea kipindi kabla hawajagombana. "Jestina nina ombi moja kwako" alikuwa Miryam, "lipo tena" aliuliza Jestina "ombi langu ni Matt, naomba umpe kifo chechenye maumivu makali sana" aliongea Miryam na kumfanya Jestina atabasamu kisha akajibu "usijali maana huyo dawa yako ipo kuzimu naipika".
"na mimi nina ombi moja" mara Alwin aliingilia, "haya lipi hilo" aliuliza Jestina. "nikipata mtoto wa kike nitamwita Jestina" aliongea na kutabasamu, "ah hilo si umwambie Miryam" alijibu Jestina, "mimi nimekubali" Miryam alijibu kisha wote wakacheka. "jamani muda wangu wa kuondoka umefika kwa hio tutaonana kesho" aliongea Jestina na wote walikubaliana. Alipiga hatua tatu ghafla umeme ukazima na uliporudi hakuonekana tena.
**************************************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment