Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

KAHABA KUTOKA CHINA - 4

 





    Simulizi : Kahaba Kutoka China

    Sehemu Ya Nne (4)





    Ilipoishia



    wakakata kona kulia, wakachukua barabara ya vumbi ambayo ilitokea katika barabara ya Ally Hassan Mwinyi na kutokomea kusipojulikana huku wakiwaacha watu waliokuwa pale Macho kutokuelewa kama kulikuwa na utekaji ambao ulikuwa umefanyika mahali pale kutokana na uharaka ambao ulifanywa katika kutekeleza kitendo kile.



    Songa nayo sasa...



    Swali ambalo lilitoka kwa Mpelelezi Deogratius Mariga likamfanya Rose kunyamaza kwa muda na kuanza kufikiria jambo. Si kwamba katika kipindi hicho hakumfahamu mwanaume ambaye alikuwa amezaa nae mtoto Lydia, alikuwa akimkumbuka sana ila hapo alionekana kama kupigwa bumbuwazi kwa kuulizwa swali ambalo hakulitegemea.

    “Baba yake ni kijana fulani anaitwa Joshua” Rose alijibu na kisha kunyamaza.

    “Mara yako ya mwisho kukutana nae ilikuwa lini?” Mariga aliendelea kuuliza maswali.

    “Miaka mitano iliyopita” Rose alitoa jibu ambalo likamfanya kila mtu kushtuka.

    “Miaka mitano iliyopita?”

    “Ndio”

    “Mbona kipindi kirefu sana?” Mpelelezi Zemba akaingilia kwa kuuliza swali.

    Hapo ndipo ambapo Rose akaamua kuelezea kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha yake ya nyuma. Hakutaka kuficha kitu chochote kile, kila kitu ambacho alikuwa akielezea, machozi yalikuwa yakimtoka, historia ya maisha yake hasa ile ya usagaji ilionekana kumuwekea doa kubwa moyoni mwake. Alipomaliza, kila mmoja akashusha pumzi ndefu.

    “Umepata kitu chochote hapo?” Mpelelezi Zemba alimuuliza Mariga.

    “Kidogo. Inawezekana huyo baba yake atakuwa amehusika katika utekaji” Mariga alijibu.

    “Yeah! Inawezekana lakini kama nina mashaka kidogo” Zemba alijibu.

    “Mashaka gani tena?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hivi baba anaweza akamteka mtoto kweli?” Zemba aliuliza.

    “Inategemea”

    “Hebu subiri. Naomba nikuulize kitu kimoja Rose. Uliwahi kupigana na huyo kijana, Joshua?” Zemba alimuuliza Rose.

    “Hapana”

    “Hata kutoleana maneno mabaya?”

    “Hapana”

    “Duh! Mbona kazi inaonekana kuwa kubwa sana” Mariga alisema huku akionekana kukata tamaa.

    Waliendelea na mahojiano zaidi na zaidi, mpaka saa moja linakatika, kila mmoja alikuwa na uhakika kwamba Joshua ndiye mtu ambaye alikuwa amehusika katika utekaji wa mtoto Lydia. Walichokifanya ni kusimama na kisha kuaga huku wakiahidi kurudi siku inayofuatia. Wakaondoka sebuleni hapo na kisha kuingia ndani ya gari lao.

    “Hebu subiri” Mariga alimwambia Zemba

    “Kuna nini tena?”

    “Kuna kitu nimehisi”

    “Kitu gani?”

    “Kuhusu mtu wa upande wa pili”

    “Yupi?”

    “Huyo Peter”

    “Kuna kipi umehisi?”

    “Hauoni kwamba nae anaweza kuwa amehusika?”

    “Mmh! Sidhani. Lakini hakuna tatizo. Tukamhoji maswali kadhaa kuhusu huyo mtu kwanza” Zemba alimwambia Mariga na kisha wote kuanza kurudi ndani ya nyumba ile.

    Awamu ya pili ya maswali ikaanza tena mahali hapo, katika awamu hii maswali mengi yalikuwa yakihusiana na Peter tu. Katika kila neno ambalo alikuwa akiongea kuhusiana na Peter, kila mmoja akaanza kutengeneza kitu chake kichwani mwake. Mpaka wanamaliza dakika ishirini za mahojiano, kila kitu kikaonekana kuwa wazi na wala hakukuhitaji maswali zaidi.

    “Kila kitu kipo tayari. Mtekaji kashajulikana” Mariga alimwambia Zemba.

    “Nani kamteka mtoto wangu?” Rose aliuliza.

    “Peter”

    “Peter?”

    “Ndio”

    “Mmejuaje?”

    “Alikuwa akijua kwamba mtoto ni wake, si ndio hivyo?”

    “Ndio”

    “Katika sifa zote ulizotuambia kuhusu yeye, maelezo ya mlinzi wa getini wa nyumba hii, mlinzi wa shule ile ya Sheng Shung pamoja na dereva, ameonekana kuwa na alama hizo hizo. Au nimekosea Zemba?” Mariga alisema na kumuuliza Zemba.

    “Haujakosea. Mtekaji atakuwa huyu huyu” Zemba alisema.

    “Sasa kwa nini kamteka mtoto wangu?” Rose aliuliza huku akianza kulia tena.

    “Ni kwa sababu anajua kwamba mtoto ni wake na hajamuona kipindi kirefu. Hilo tu” Mariga alimjibu Rose.

    Hakukuwa na cha kuchelewa, kila kitu kikaonekana kuwa wazi kwa wakati huo na ukweli ulikuwa umekwishajulikana kwamba Peter ndiye ambaye alikuwa amehusika na utekaji ule, kwa maana hiyo walitakiwa kumtafuta. Kilichofanyika ni kupiga simu katika kituo cha polisi cha Mwenge na kisha kuwapata taarifa juu ya Peter ambaye alikuwa akihisiwa kuhusika katika utekaji wa mtoto Lydia, utekaji ambao ulianza kuvuma sana jijini Dar es Salaam.

    “Mkifika na kumkuta, kitu cha kwanza muwekeni chini ya ulinzi kwa mahojiano maalumu” Mpelelezi Mariga alimwambia polisi ambaye alipokea simu kituoni.

    “Hakuna tatizo”

    “Cha msingi ngoja tusubiri hapa hapa ili kama itatokea wamempata na kumuweka chini ya ulinzi twende na Rose mpaka huko” Mariga alimwambia Zemba na kisha wote kutulia kochini wakisubiri wapigiwe simu.

    *****

    Lydia alikuwa akiendelea kulia ndani ya gari lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alionekana kujali kitu chochote kile, kitu ambacho walikuwa wakikijali katika kipindi hicho ni kuelekea katika hospitali ya Mikocheni B kwa ajili ya kumuonyeshea Bwana Edward mjukuu wake ambaye alikuwa akitaka kumona kila siku.

    Muda wote Ezekiel alikuwa amemkamata Lydia vilivyo katika siti za nyuma. Huku Peter akiendesha gari lile. Peter hakuonekana kuzijali kelele za Lydia kwa kuamini kwamba kuna kipindi kingefika, kipindi ambacho mtoto huyo angenyamaza kabisa na wao kuendelea na mambo mengine. Japokuwa kutoka Masaki mpaka Mikocheni B hakukuwa na umbali mkubwa lakini kutokana na foleni za hapa na pale walieza kutumia muda wa dakika arobaini na tano na ndipo gari lile likaanza kuingia katika eneo la hospitali ile.

    Bado Lydia hakuwa amenyamaza, alikuwa akiendelea kulia kama kawaida. Hawakutaka kuteremka, moja ya sheria za hospitalini hapo ilikuwa ni kutokupiga kelele, hawakutaka Lydia aendelee kupiga kelele za kilio na wakati walikuwa na uhitaji wa kuingia ndani ya hospitali ile katika muda huo wa saa kumi, muda ambao ulikuwa ni wa kuwaona wagonjwa.

    Lydia alilia mpaka akanyamaza, wakateremka na kisha kuanza kuelekea ndani ya hospitali ile huku Peter akiwa amembeba mikononi mwake. Moja kwa moja wakaelekea katika kile chumba alicholazwa Bwana Edward, walipofika, hata mama yake, Bi Stella alikuwepo ndani ya chumba hicho akiwa amekuja kumjulia hali mume wake.

    “Baba….” Peter alimuita baba yake ambaye alikuwa amelala kitandani pale.

    “Mjukuu wangu. Mjukuu wangu yupo wapi?” Bwana Edward alimuuliza Peter.

    “Huyu hapa. Nimekuja nae baba kama nilivyokuahidi” Peter alimwambia baba yake, Bwana Edward.

    Japokuwa alikuwa mgonjwa aliyeonekana kuzidiwa, akayageuza macho yake pembeni na kisha kuanza kumwangalia mtoto ambaye alikuwa amesimamishwa pembeni yake, mtoto ambaye alikuwa akiangalia kwa macho yaliyokuwa na uoga.

    “Hatimae nimemuona mjukuu wangu. Nimemuona mjukuu wangu Peter” Bwana Edward alimwambia Peter huku kwa mbali maachozi yakianza kumlenga.

    Bwana Edward akaonekana kuwa mwingi wa furaha, hakuamini kwamba katika kipindi hicho alikuwa amefanikiwa kumuona mtoto ambaye aliamini kwamba alikuwa mjukuu wake, kwa tabu sana akauinua mkono wake na kisha kuupeleka shavuni mwa Lydia na kisha kuanza kulishika shika shavu lake, moyo wake ulikuwa na furaha kupita kawaida.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Peter nae akaonekana kuridhika, kila alipokuwa akimwangalia Lydia, moyoni mwake alikuwa akijisikia amani kupita kawaida, hakuamini kwamba mara baada ya miaka mitano kupita siku hiyo ilikuwa ni siku nyingine ya kumuona mtoto wake, mtoto aliytoka katika kiuno chake.

    “Lydia. Nyamaza Lydia. Mimi ni baba yako” Peter alimwambia Lydia ambaye alikuwa akianza kulia tena.

    “Nataka kurudi kwa mama yangu” Lydia alimwambia Peter.

    “Utarudi. Mimi ni baba yako Lydia…mimi ni baba yako” Peter alimwambia Lydia ambaye hakuonekana kuelewa zaidi ya kuendelea kulilia kurudi kwa mama yake.

    “Nimeridhika. Kwa sasa hivi nipo tayari hata kufa. Nimeridhika kumuona mjukuu wangu” Bwana Edward alimwambia Peter huku akionekana kukata tamaa kitandani pale.

    Hawakutaka kuondoka mahali pale, kwa Peter, alikuwa akijisikia faraja moyoni mwake, kitendo cha kumuona Lydia ambaye aliamini kwamba ni mtoto wake kilikuwa kimempa faraja kubwa kupita kawaida. Muda wote alikuwa amemshika Lydia, hakutaka aondoke mikononi mwake, alikuwa akitamani kuwa pamoja nae katika kipindi chote.

    Huku wakiendelea kuwa katika furaha kubwa juu ya uwepo wa Lydia mahali hapo, mara mlango ukafunguliwa, dokta mkuu pamoja na polisi wanne wenye bunduki wakaingia ndani ya chumba hicho. Kitu cha kwanza wakawaweka wote chini ya ulinzi.

    “Mpo chini ya ulinzi” Polisi mmoja aliwaambia huku akiwa amewanyooshea bunduki.

    “Chini ya ulinzi! Kwa kosa gani?” Peter aliuliza huku akijifanya kushangaa.

    “Utekaji”

    “Utekaji? Hapana, sijamteka, huyu ni mtoto wangu, nilichokifanya ni kumchukua na si kumteka. Toka lini baba akamteka mtoto wake?” Peter alijibu na kisha kuwauliza swali ambalo likaonekana kuwa kama dharau kwa polisi wale.

    ****

    Polisi wakaonekana kuwa na hasira, majibu ya Peter yakawafanya kuvimba kwa hasira kupita kawaida, wakawafuata mahali pale walipokuwa na kisha kumfunga pingu pamoja na Ezekiel na kisha kuondoka nao mahali hapo kuelekea kituoni. Bi Stella akabaki akilia tu, hakuamini kama mtoto wake ambaye alikuwa anampenda kwa wakati huo alikuwa amewekwa chini ya ulinzi wa polisi na kupelekwa polisi huku akitakiwa kufikishwa mahakamani siku za usoni kutokana na kukabiliwa na kesi ya utekaji.

    Polisi hawakuondoka bila Lydia, nae wakamchukua na kisha kuelekea nae kituoni. Wakawapigia simu mpelezi Mariga na Zemba na kuwaambia kwamba walikuwa wamekwishampata mtoto pamoja na watuhumiwa kwa hivyo mama wa mtoto huyo alitakiwa kufika kituoni kwa ajili ya kumchukua mtoto wake na mambo mengine kufuata.

    Katika kipindi chote hicho Peter alikuwa akilalamika tu kwamba hakuwa amemteka Lydia kwa sababu asingeweza kumteka mtoto wake mwenyewe. Polisi hawakutaka kumuelewa kabisa, walichokuwa wakikifanya ni kuendelea kumpeleka katika kituo cha polisi kwa ajiliya maelezo mengine.

    Wala hawakuchukua muda mrefu, wakafika katika kituo cha Osterbay ambapo huko ndipo walipotaka ahifadhiwe kabla ya mambo mengine kuendelea zaidi. Polisi wote wakaonekana kufurahia, hawakuamini kama kazi ya kumkamata peter ilikuwa ni rahisi namna ile, walibaki wakipongezanana tu.

    “Huyu atakuwa anajifunza utekaji” Polisi mmoja aliwaambia wenzake huku akicheka kidharau.

    “Hahaha! Kwa nini?” Polisi mwingine aliuliza.

    “Mtu unafanya utekaji hata masaa mawili hayajapita, umekamatwa. Huyu atakuwa akijifunza utekaji” Polisi yule alijibu.

    Peter na Ezekiel waliendelea kubaki kituoni hapo mpaka saa kumi na mbili kipindi ambacho Rose akafika mahali hapo akiwa pamoja na wale wapelelezi na Bi Lucy. Kitu cha kwanza ambacho alikuwa akikitaka mahali hapo ni kuona mtoto wake tu, Lydia akaletwa, akamchukua na kumbeba huku akilia.

    “Huyo kijana mwenyewe yupo wapi?” Rose alimuuliza polisi aliyekuwa pale kaunta.

    “Yupo ndani. Anasubiria kesi yake”

    “Naweza kumuona?”

    “Subiri kwanza” Polisi yule alimwambia na kisyha kuingia kwenye chumba kimoja.

    Rose alibaki mahali pale huku akimwangalia mtoto ake, Lydia. Hakuamini kwamba Lydia alikuwa amepatikana baada ya kutekwa ndani ya muda mchache. Kila alipokuwa akimwangalia, alikuwa akijisikia kulia kwa furaha.

    Katika kipindi hicho hasira za Rose zilikuwa kwa Peter, mapenzi yote ambayo alikuwa nayo juu ya Peter katika kipindi hicho hayakuwepo tena, alikuwa akimchukia sana na chuki yake ilizidi zaidi mara baada ya kumteka mtoto wake. Rose alikuwa akitaa kuongea na Peter kwa sababu alikuwa akitaka kumwambia ukweli juu ya mtoto Lydia ili asiwe anajiwekea uhakika kwamba Lydia alikuwa mtoto wake kama alivyokuwa akijipa uhakika huo kila siku.

    “Subiri kwanza” Polisi yule alimwambia Rose mara baada ya kurudi kutoka katika chumba kile.

    Wala haukupita muda mrefu, ni ndani ya dakika kadhaa, polisi ambaye alionekana kuwa kiongozi wa kituo kile akatokea mahali hapo, akaanza kumwangalia Rose, uso wake ukaonyesha tabasamu kubwa. Kwa sababu Rose alikuwa akitaka kuongea nae kidogo hakutaka maongezi yafanyikie mahali hapo, akamwambia kuelekea katika chumba kile pamoja na Bi Lucy.

    “Unataka kuongea nae? Kuhusu nini?” Polisi yule, Bwana Pawasa aliuliza.

    “Kuna mambo fulani nataka kumwambia” Rose alijibu.

    “Mambo gani?”

    “Kama kumpa taarifa”

    “Juu ya nini tena? Yaani unataka kuongea kwa amani na mtekaji wa mtoto wako?”

    “Yeah! Nimeomba mkuu”

    “Hakuna tatizo. Ila utatakiwa kuongea nae mbele yetu” Bwana Pawasa alimwambia Rose ambaye akakubaliana nae.

    Polisi mmoja akagizwa kwenda kumfungulia Peter mlango wa sero na kwamba alikuwa akihitajika mahali hapo. Peter akatoka huku akionekana kukasirika, akapelekwa katika chumba kile, macho yake yalipogongana na macho ya Rose, akaonekana kutoa tabasamu kubwa.

    Miaka mitano ilikuwa imepita tangu kipindi cha mwisho kabisa kuuona uso wa mwanamke huyo ambaye alikuwa amesimama mbele yake, mapenzi ambayo alikuwa nayo katika kipindi cha nyuma bado yalikuwepo moyoni mwake katika kipindi hicho. Kila alipokuwa akimwangalia Rose, Peter alikuwa na uhakika kwamba Rose ndiye ambaye angeongea ukweli juu ya kile kilichokuwa kimetokea, yeye ndiye angeongea ukweli kwamba Lydia alikuwa mtoto wake na hivyo hakumteka, alikuwa amemchukua tu.

    “Rose…!” Peter aliita huku akionekana kutokuamini.

    “Kwa nini ulimteka mtoto wangu Peter?” Lilikuwa swali lililotoka kwa Rose huku uso wake ukionekana kuwa katika hali ya hasira.

    “Sikumteka Lydia” Peter alimwambia Rose.

    “Kumbe ulifanyajae?”

    “Nilimchukua kama mtoto wangu”

    “Hapana Peter, Rose si mtoto wako na kamwe hatokuwa mtoto wako” Rose alimwambia Peter.

    “Lydia ni mtoto wangu Rose. Haukumbuki siku ile ambayo tulifanya mapenzi na kisha mimba kuingia. Haukumbuki kila kilichotokea kwetu ndani ya chumba changu na maneno ambayo uliniambia?” Peter aliuliza huku akionekana kuwa na uhakika kwamba Lydia alikuwa mtoto wake.

    “Lydia sio mtoto wako Peter” Rose alimwambia Peter huku watu wengine wakiwa kimya ndani ya chumba kile.

    “Ni mtoto wangu. Hata kama tutaachana na kuwa tofauti bado Lydia atakuwa mtoto wangu. Hautoweza kuubadilisha ukweli Rose” Peter alimwambia Rose.

    “Ila kwa nini ulimteka Lydia?”

    “Baba alitaka kumuona mjukuu wake kabla ya kufariki” Peter alijibu.

    “Sasa ndio umchukue Lydia?”

    “Ndio. Baba alikuwa akitaka kumuona mjukuu wake” Peter alimwambia Rose.

    “Nisikilize Peter. Lydia si mtoto wako” Rose alimwambia Peter ambaye kwa mbali akaanza kutokwa na machozi.

    “Si mtoto wangu?”

    “Ndio”

    “Kivipi?”

    Swali hilo ndilo lililomfanya Rose kuanza kuhadithia kile ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha yake ya nyuma katika kipindi ambacho wavulana wengi walikuwa wakimfuatilia kwa kumtaka kuwa na mahusiano nae. Katika stori hiyo, aliongea mambo mengi sana ila hakutaka kugusia kuhusiana na usagaji, alimuelezea sana Joshua mpaka siku ambayo alifanya nae mapenzi na hatimae mbegu kuingia katika mfuko wake wa uzazi.

    Kila mtu alikuwa ametegesha sikio akisikiliza kwa makini. Kadri Rose alivyokuwa akielelezea na ndivyo ambavyo Peter alivyozidi kutokwa na machozi zaidi na zaidi. Moyoni aliumiza, aliuhisi moyo wake kuchomwa na msumali uliokuwa na ncha kali tena uliokuwa wa moto kupita kawaida. Miguu yake ikapatwa na ganzi, akaihisi ikilegea na kisha kuchuchumaa huku machozi yakiwa yameloanisha sana mashavu yake.

    “Haiwezekani Rose. Haiwezekani Rose” Peter alimwambia Rose huku akionekana kutokuamini kile ambacho alikuwa amekisikia.

    “Huo ndio ukweli Peter, sitaki kukudanganya. Lydia si mtoto wako. Ni mtoto wa Joshua” Rose alimwambia Peter.

    “No…No…No Rose. Hapana. Lydia ni mtoto wangu. Hebu mwangalie alivyofanana na mimi. Hapana Rose, huyu ni mtoto wangu. Ni mtoto wangu” Peter alisema kwa sauti huku akilia kama mtoto.

    “Huo ndio ukweli”

    Kwa jinsi Peter alivyokuwa akionekana mahali pale, kila mtu aliyekuwa ndani ya chumba kile akaingiwa na huruma, hata Bi Lucy mwenyewe alijisikia maumivu, katika maisha yake hakuwahi kumuona mtu ambaye alikuwa akilia kwa uchungu kama alivyokuwa akifanya Peter. Rose akashindwa kuvumilia zaidi, nae alikuwa akizidi kutokwa na machozi. Akaanza kumfuata Peter, alipomfikia, akamkumbatia.

    “Usilie Peter. Naomba usilie” Rose alimwambia Peter huku nae akilia.

    “Umeniumiza Rose. Kwa nini haukuniambia kama mimba haikuwa yangu?”

    “Nilihofia. Nilihofia kukuumiza na nilimhofia baba yangu”

    “Hata kama Rose. Umeniumiza sana. Nimeingia katika matatizo kwa sababu ya kumteka mtoto ambaye si damu yangu, Baba yangu anakaribia kufariki, amemuona Lydia akaridhika kwa kuamini kwamba amemuona mjukuu wake. Mungu wangu! Kwa nini umenifanyia hivi Rose?” Peter alimwambia Rose na kumuuliza.

    “Sikuwa na lengo la kukumiza Peter. Naomba unisamehe kwa kila kitu”

    “Ni ngumu Rose. Ninachokiamini ni kwamba Lydia ni mtoto wangu. Hata kwa vipimo vya DNA, nipo tayari kupimwa lakini Lydia ni mtoto wangu” Peter alimwambia Rose.

    “Kama unataka kupima, sawa. Hakuna tatizo. Nipo tayari upimaji ufanyike ili uamini zaidi” Rose alimwambia Peter.

    Hayo ndio makubaliano ambayo yalikuwa yamefanyika mahali hapo kwamba ilikuwa ni lazima vipimo vya DNA vifanyike na hatimae ukweli ujulikane zaidi moyoni mwa Peter. Kwa Peter bado hakuwa akiamini kwamba Lydia hakuwa mtoto wake, kitu alichokuwa akikitaka ni kuufahamu ukweli na wala hakuwa tayari kumuacha Lydia aondoke na wakati kwa kiasi fulani alikuwa akiamini kwamba alikuwa mtoto wake.

    “Kama mpo tayari hakuna tatizo. Ila kwanza itatakiwa kufanyika kitu kimoja” Bwana Pawasa aliwaambia.

    “Kitu gani?” Rose aliuliza.

    “Ni lazima tumpate huyo mtu ambaye unasema kwamba ni mzazi halali wa mtoto huyu”

    “Joshua?”

    “Ndio” Bwana Pawasa alijibu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    Joshua alikuwa akiishi kwa wasiwasi sana toka siku ya mwisho ambayo alinusurika kufanyiwa kitu kibaya na Bwana Shedrack ambaye alionekana kuwa mwingi wa hasira. Kuanzia siku hiyo maisha yake yakabadilika kabisa, aliutambua vilivyo utata ambao alikuwa nao Bwana Shedrack, utata ambao alikuwa akiwafanyia vijana wengine ambao walikuwa wakimtaka binti yake, Rose.

    Joshua alijua fika kwamba alikuwa amekwishaingia katika uhasama mkubwa na mzee huyo ambaye bado alikuwa akimtafuta kila siku. Hali ikazidi kuwa mbaya kwake kitu kilichompelekea kufanya jambo moja ambalo aliliona kuwa sahihi katika kipindi hicho, kutafuta chumba kingine na hatimae kuhama katika mtaa huo.

    Katika kipindi ambacho alikuwa akitafuta chumba katika mtaa mwingine, alikuwa akichelewa kufika katika kile chumba chake kitu ambacho kilimfanya kuingia saa nane usiku katika kipindi ambacho aliona kwamba Bwana Shedrack asingeweza kuja kumuulizia. Maisha yake ya wasiwasi yalindelea zaidi na zaidi, kila siku alikuwa mtu wa kujificha ili kuukimbia uso wa Bwana Shedrack ambaye alijua fika kwamba bado alikuwa akimtafuta.

    Siku zikaendelea kukatika huku akiendelea kuishi maisha ya kujificha mpaka pale ambapo akakamilisha mipango yake ya kuhama na kuhamia Kijitonyama, huko akaweza kuishi kwa amani, hakutaka watu wengi wapafahamu alipokuwa amehamia zaidi ya rafiki yake, Ally ambaye alikuwa akiishi chumba cha jirani katika nyumba ile aliyohama.

    Maisha huko yakaendelea zaidi, muda mwingi Joshua alikuwa akimfikiria Rose. Japokuwa makubaliano yao ambayo walikuwa wameyaweka yalikuwa ni kuzidi kuwasiliana katika kipindi ambacho wasingekuwa pamoja lakini katika kipindi hicho hali ilikuwa tofauti kabisa, Rose hakuwa akipatikana simuni jambo ambalo lilikuwa limemuweka Joshua kwenye wakati mgumu sana.

    Joshua hakutaka kukata tamaa, kila siku alikuwa akijaribu kumtafuta Rose simuni lakini matokeo yalikuwa ni yale yale na wala hayakuweza kubadilika kabisa, kwamba Rose hakuwa akipatikana kabisa. Ukiachana na Rose, wakati mwingine alikuwa akiifikiria mimba ambayo alikuwa nayo Rose, kiu ya moyo wake katika kipindi hicho ilikuwa ni kumuona mtoto ambaye angezaliwa na Rose, mtoto ambaye alikuwa ni damu yake.

    Joshua hakujua ni mahali gani ambapo alitakiwa kumuulizia Rose na hatimae kumpata. Alipokuwa akikumbuka mengi ya nyuma ndipo hapo alipoonekana kukumbuka kitu kwamba mara ya mwisho ambayo alikuwa akiagana na Rose alimwambia kwamba alikuwa akienda kuishi kwa rafiki yake ambaye alikuwa akiishi katika hosteli iliyokuwa maeneo ya Sinza makaburini.

    Baada ya kulikumbuka hilo, Joshua hakutaka kuendelea kubaki chumbani kwake, alichokifanya ni kuanza kuelekea katika hosteli hiyo ili kuangalia kama angeweza kumpata mpenzi wake, Rose. Ndani ya daladala Joshua alikuwa na mawazo tele, alikuwa akimkumbuka sana mpenzi wake, Rose, alikuwa na hamu kubwa ya kuliona tumbo lake ambalo lilikuwa limembeba mtoto wake.

    Daladala ambayo alikuwa ameipanda kuelekea Sinza haikuchukua muda mrefu, akafika Sinza Makaburini ambapo moja kwa moja akateremka na kisha kuanza kuangalia huku na huko kana kwamba alikuwa akimtafuta mtu fulani. Mbele yake kulionekana kuwa na nyumba za kawaida tu, hakuona kama alikuwa ameiona hosteli yoyote ile mbele ya macho yake. Alichokifanya ni kuwasogelea vijana ambao walikuwa pembeni na kisha kuanza kuongea nao.

    “Mambo vipi!” Joshua aliwasalimia vijana wale ambao wakainua vichwa vyao kutoka katika drafti walilokuwa wakilicheza na kumwangalia Joshua.

    “Poa” Vijana wale waliitikia na kisha kuyarudisha macho yao katika drafti lao.

    “Samahani kidogo. Naomba niulize swali moja” Joshua aliwaambia vijana wale ambao wakaacha kucheza drafti na kisha kuanza kumwangalia usoni.

    “Uliza tu”

    “Kuna hosteli yoyote hapa karibu?” Joshua aliuliza huku akiangalia huku na kule.

    “Hosteli? Mmh! Hapa ninachokijua ni kwamba kuna hosteli moja tu, tena ya wasagaji ipo hapo nyuma” Kijana mmoja alimjibu Joshua ambaye akaonekana kushtuka.

    “Hosteli ya wasagaji?”

    “Yeah! Hosteli ya wasagaji. Mbona umeshtuka sana kaka? Demu wako anaishi humo nini?” Kijana mmoja alimuuliza huku uso wake ukionyesha tabasamu.

    “Hapana. Kuna mtu nataka kwenda kumuulizia”

    “Nae anaishi humo?”

    “Hapana. Nadhani alikuja mara moja tu”

    “Basi sawa”

    Kijana mmoja akaanza kumuelekeza Joshua mahali ambapo hosteli hiyo ilipokuwa ikipatikana, baada ya kuona kwamba maelekezo ambayo alipewa yalikuwa yamemuingia kichwani, akaondoka mahali hapo. Joshua akaanza kuzifuata njia zote ambazo alikuwa ameelekezwa mpaka macho yake kutua katika nyumba moja kubwa ambayo iliandika MARIA HOSTEL.

    “Nadhani ndio hapa” Peter alisema na kisha kuanza kulisogelea geti. Alipolifikia, akaanza kuligonga.

    Msichana mmoja aktokea na kisha kulifungua geti lile na macho yake kutua usoni mwa Joshua. Tabasamu kubwa likatoka usoni mwa msichana yule, sura ya uchangamfu ambayo alikuwa nayo Joshua ikaonekana kuziteka hisia zake kwa kipindi kifupi sana.

    “Karibu” Msichana yule alimkaribisha Joshua.

    “Asante. Samahani, kuna msichana nimekuja kumuulizia” Hoshua alimwambia msichana yule.

    “Msichana yupi?”

    “Anaitwa Rose”

    “Rose! Rose yupi?”

    “Alikuja kumuona msichana fulani mahali hapa”

    “Msichana yupi?”

    “Anaitwa Irene”

    “Mmmh!”

    “Kuna nini tena?”

    “Kuna Irene wengi sana mahali hapa”

    “Ninayemfahamu mimi ana makalio makubwa kwa nyuma, si mrefu sana, ni mweupe. Nilimuona siku moja tu akiwa na msichana wangu” Joshua alimwambia msichana yule.

    “Daah! Huyo msichana anaitwa Irene Godfrey”

    “Ok! Nadhani ndiye yeye! Nimemkuta?” Joshua aliuliza.

    “Alifariki wiki iliyopita” Msichana yule alitoa jibu ambalo lilimchanganya sana Joshua.

    “Alifariki?” Joshua aliuliza huku akionekana kuchanganyikiwa na jibu lile.

    “Ndio. Ni wiki imepita toka afariki”

    “Alikuwa anaumwa?”

    “Hapana. Aliuawa”

    “Daah! Kwa hiyo hata wewe haujui msichana wangu atakuwa amekwenda wapi?”

    “Hapana. Msichana mwenyewe sijawahi hata kumuona” Msichana yule alimwambia Joshua.

    Joshua akaonekana kuchoka kupita kawaida, maneno ambayo aliyazungumza msichana yule yakaonekana kumlegeza sana. Hakuamini kama kweli katika kipindi ambacho alikuja ndani ya hosteli ile alimkosa Rose, msichana ambaye alikuwa akitamani kumuona katika kipindi hicho. Joshua akabaki kimya kwa muda huku akionekana kama mtu ambaye alikuwa akijifikiria kitu fulani kichwani mwake. Kuondoka alikuwa akitamani kuondoka lakini hata kubaki napo alitaani kubaki, hakujua afanye nini.

    “OK! Nashukuru” Joshua alimwambia msichana yule na kisha kuondoka mahali hapo.

    Akili yake haikukaa sawa kabisa katika kipindi hicho, yule mtu ambaye alikuwa amemfuata ndani ya hosteli ile alikuwa amemkosa na hakujua ni kwa namna gani angeweza kumpata mtu huyo, Rose. Moyoni hakujisikia kuwa na furaha kabisa, muda wote alionekana kuwa na majonzi kupita kawaida. Kitendo cha kumkosa Rose kilimaanisha kwamba asingeweza kumuona tena kwani hata kwenda kumuulizia nyumbani kwao lingekuwa suala gumu kutokea.

    Kuanzia siku hiyo Joshua hakuonekana kuwa na furaha, muda mwingi alionekana kuwa mpweke. Joshua hakutaka kuendelea na kazi katika kipindi hicho, kitu alichoamua ni kuanza kufanya biashara tu. Mara kwa mara alikuwa akitoa mizigo ya viazi mkoani Mbeya na kisha kuileta jijini Dar es Salaam na kuiuza kitu ambacho kilionekana kumpatia fedha ambazo zilionekana kumtosha.

    Joshua hakuonekana kuridhika, mara kwa mara alikuwa akibadilishabadilisha biashara kutokana na misimu kadhaa ya mazao kwa jinsi ilivyokuwa ikienda katika kipindi husika. Kujituma kwake, kuangaika kwake pamoja na kujitolea muda wake mwingi katika kufanya biashara vilikuwa vitu ambavyo vilimfanya kujipatia kiasi cha fedha na kisha kuanza kujenga nyumba yake mwenyewe.

    Kila siku Joshua akawa mtu wa kuingiza fedha, kila siku akawa mtu wa kupokea oda za watu mbalimbali ambao walikuwa wakitaka mazao husika katika kipindi husika cha mazao fulani. Kutokana na kuwa na fedha za kutosha, wanawake nao hawakubaki nyuma, kila siku walikuwa wakijitahidi kwa nguvu zao zote kutaka kumuingiza Joshua katika mikono yao.

    Joshua hakuonekana kuwa mwanaume mwepesi kukamatika na wasichana hao, kila siku mawazo yake yalikuwa kwa msichana wake, Rose ambaye alikuwa mjauzito. Moyoni mwake tayari alijihesabia kuwa baba na hivyo hakutakiwa kuangaika na wasichana wengine ambao walikuwa wakiendelea kujigonga kwa kasi. Japokuwa alikuwa mbali na Rose lakini kila siku moyo wake ulikuwa ukimwambia kitu kimoja kwamba msichana Rose bado alikuwa mpenzi wake na kama ingetokea siku wakaonana basi angeweza kumwambia wafunge ndoa na hatimae kumlea mtoto wao pamoja.

    Mwaka wa kwanza ukakatika na mwaka wa pili kuingia. Mwaka wa pili ukaisha na mwaka wa tatu kuingia lakini wala Joshua hakuweza kumuona msichana wake, Rose. Moyo wake uliendelea kuwa na maumivu makali, mawazo juu ya Rose na mtoto wake yalikuwa yakimwandama kila siku katika maisha yake. Kuna wakati alikuwa akijifikiria kumchukua msichana mwingine na hatimae kufunga ndoa lakini kila alipokuwa akimfikiria zaidi Rose, wazo hilo lilikuwa likimtoka kwa wepesi sana kichwani mwake.

    Mwaka wa nne ukaingia lakini bado hali iliendelea kuwa vile vile, hakuweza kumuona Rose. Maisha ya nyumbani kwake yalionekana kuwa si mazuri japokuwa alikuwa na kila kitu. Nyumba yake kubwa hakuiona kuwa na thamani, gari lake la kutembelea hakuliona kuwa na thamani na hata biashara zake pia hakuziona kuwa na thamani katika kipindi hicho. Rose pamoja na mtoto wake ambaye wala hakuwahi kumuona ndio walikuwa watu ambao walionekana kuwa na thamani kuliko kitu chochote katika maisha yake kwa wakati huo.

    Mpaka mwaka wa tano unaingia, bado hali haikuwa imebadilika, iliendelea kuwa vile vile. Joshua akaonekana kuchoka, Joshua akaonekana kukata tamaa kuendelea kusubiri, uamuzi ambao alikuwa ameamua kuuchukua katika kipindi hicho ni kutafuta msichana ambaye alionekana kufaa kuwa mke. Hilo halikuwa tatizo kwake, kwa sababu wasichana walikuwa wengi waliokuwa wakimfuatilia, akaanza kuwafikiria wasichana kadhaa, wasichana ambao aliamini kwamba walikuwa wametulia na kisha kuanza kuwachuja.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zaidi ya wasichana kumi na mbili wakaja kichwani mwake, akaanza kumfikiria mmoja baada ya mwingine. Mchujo ulikuwa mkali kichwani mwake mpaka pale ambapo alimpata mmoja ambaye akaonekana kufaa kuwa mke wake, huyu aliitwa Debora.

    Kwa haraka sana Joshua akachukua simu yake na kisha kuanza kulitafuta jina la Debora, alipolipata akaanza kumpigia simu. Lengo lake katika kipindi hicho lilikuwa ni kupanga miadi na Debora waweze kuonana sehemu fulani ambako huko angemwambia ukweli kwamba alikuwa akitaka kumuoa kwa sababu alikuwa msichana ambaye alimuona kufaa kuishi nae na kumzalia watoto pamoja na kutengeneza familia iliyokuwa na upendo.

    Debora alipoambiwa kukutana na Joshua, kwanza moyo wake ukafurahi, hakuamini kwamba mwanaume yule mwenye pesa, mwanaume ambaye alikuwa akimfikiria kila siku ndio ambaye alikuwa amempigia simu na kutaka kuonana nae. Hiyo ikaonekana kuwa bahati kwa Debora, bahati ambayo kamwe hakutakiwa kuiacha ipite.

    “Kesho saa ngapi?” Debora alimuuliza Joshua simuni.

    “Saa moja usiku. Utakuwa na nafasi?”

    “Ndio. Muda wote nina nafasi. Wewe tu Joshua” Debora alimwambia Joshua.

    “Kama muda wote una nafasi, kwa nini tusifanye hata leo saa kumi na moja na nusu jioni?” Joshua aliuliza.

    “Hakuna tatizo. Panga pa kukutania” Debora alimwambia Joshua.

    “Naomba tuonane pale Travertine hotel. Nina mengi ya kuongea nawe siku ya leo” Joshua alimwambia Debora ambaye bila shaka akakubaliana nae.

    Siku hiyo ikaonekana kuwa siku njema kwa Debora, muda mwingi alikuwa akijifikiria ni aina ya mavazi gani ambayo alitakiwa kuyavaa siku hiyo. Kila vazi ambalo alikuwa akilifikiria aliliona kutofaa kuvaliwa siku kama hiyo. Alitamani kuonekana mpya machoni mwa Joshua, hata kama katika kipindi cha nyuma alikataa kuwa wake, siku hiyo alitaka kuhakikisha kwamba mwanaume huyo anakuwa wake na hatimae mambo mengine kufuata.

    Saa kumi na moja na dakika ishirini Debora alikuwa akiingia ndani ya eneo la hoteli ya Travertine. Macho yake yalipotua usoni mwa Joshua ambaye alikuwa amekaa katika moja ya viti vilivyozunguka meza iliyokuwa na vinywaji, tabasamu pana likaonekana usoni mwake. Joshua akainuka kutoka kitini na kisha kumsogelea Debora na kumbusu shavuni.

    “Unanukia vizuri” Joshua alimwambia Debora ambaye alikuwa akitabasamu tu.

    “Asante”

    “Manukato gani tena?” Joshua alimuuliza debora.

    “La Laspinho” Debora alijibu.

    “Mmh! Yananukia vizuri sana”

    “Hata wewe pia unanukia vizuri pia”

    “Najua. Ila sikushindi wewe Debora” Joshua alimwambia Debora.

    Hapo hapo Joshua akamuita mhudumu ambaye akafika mahali hapo na kisha kumuagiza vinywaji. Siku hiyo kwake ikaonekana kuwa siku maalumu ambayo alitakiwa kuzungumzia suala moja tu, ndoa na kisha kumsikiliza Debora angesema nini juu ya hilo. Kwake, hakuwa na wasiwasi kabisa, kitu ambacho alikuwa akikiamini ni kimoja tu kwamba msichana Debora asingeweza kukataa katika kipindi ambacho angemwambia ombi la kuwa mke wake wa ndoa.

    “Atakubali tu” Joshua alijisemea katika kipindi ambacho alikuwa akinywa juisi huku akimwangalia Debora.









    Wote walibaki wakiangaliana kwa macho ya kimahaba, katika kipindi hicho kila mtu alionekana kuvutiwa na mwenzake, walikuwa wakiangaliana huku wakipeana tabasamu kuonyesha ni jinsi gani walikuwa wamevutiana. Mpaka chakula kinaletwa mahali hapo, kila mmoja alikuwa akitumia muda wake kumwangalia mwenzake kwa macho ya kisiri. Ni kweli walikuwa wamependana, ni kweli katika kipindi hicho kila mmoja alionekana kuvutiwa na mwenzake.

    Joshua alijua fika kwamba msichana Debora alikuwa akimpenda sana na alikuwa akimpenda zaidi ya alivyokuwa akifikiria lakini katika kipindi hakujua ni kwa jinsi gani alitakiwa kuanzisha mazungumzo yake kumwambia Debora kwamba alikuwa akitaka sana awe mke wake wa ndoa. Katika macho yake, Debora alionekana kuwa mwanamke mzuri, mwanamke ambaye alistahili kuwa na mtu kama yeye, mtu mwenye pesa za kununulia kila alichokuwa akikitaka.

    “Hallooow” Joshua aliita mara baada ya kuona ukimya umetawala mahali hapo.

    “Hallow” Debora aliitikia na kisha kuanza kucheka.

    Moyo wa Joshua ukamlipuka, damu yake ikaanza kuzunguka kwa kasi mwilini mwake, tabasamu ambalo alikuwa amelitoa Debora likaonekana kumtetemesha moyo wake kupita kawaida. Uzuri wa Debora ukaonekana kuwa mara nne ya ule uzuri ambao alikuwa nao, tabasamu lile likaonekana kuuteka zaidi moyo wa Joshua. Akajikuta akizidi kumpenda Debora, akajikuta akizidi kumpenda msichana huyo ambaye katika kipindi hicho alionekana kuwa mzuri hata zaidi ya Malkia wa kipindi kirefu kilichopita, malkia ambaye alikuwepo katika nchi ya Misri, malkia aliyeweza kuolewa na kaka zake wa damu, malkia mrembo ambaye alikuwa akijulikana kuwa mrembo zaidi ya wanawake wote duniani, malkia Cleopatra.

    “Debora” Joshua alijikuta akiita kwa sauti ya chini, sauti ambayo ilielezea kile kilichokuwa moyoni mwake.

    “Abeee” Debora aliitikia kwa heshima zote.

    “Nilisahau kukwambia kitu kimoja” Joshua alimwambia Debora ambaye alikuwa akitabasamu muda wote hali iliyomfanya Joshua kuchanganyikiwa zaidi.

    “Kitu gani?”

    “Umependeza mno Debora. Nani alibuni hayo mavazi yako?” Joshua alimuuliza Debora ambaye akaacha kula na kisha kuanza kujiangalia.

    “Nilinunua dukani wala hayakubuniwa na mwanamitindo yeyote yule” Debora alijibu huku akiendelea kuliangalia vazi alilokuwa amelivaa.

    “Hivi kwa uzuri wote huo Debora, kweli kuna wanaume walishindwa kuja kwako na kukwambia kwamba wanakupenda?” Joshua alimuuliza Debora.

    “Walikuja wengi”

    “Ukawaambiaje baada ya kukwambia wanakupenda?”

    “Nilichukulia kawaida tu kwa sababu sikuwa tayari kuolewa wala kuingia katika mahusiano” Debora alitoa jibu ambalo kwa kiasi fulani likamfanya Joshua kubadilika.

    “Haukuwa tayari kuingia kwenye mahusiano?” Joshua aliuliza huku akionekana kushtuka kidogo.

    “Yeah! Ilikuwa zamani”

    “Ila sasa hivi iko vipi?”

    “Kwa sasa nipo tayari” Debora alitoa jibu ambalo likamfanya Joshua kushusha pumzi nzito.

    “Nimelifurahia jibu lako” Joshua alimwambia Debora ambaye tabasamu halikumuisha usoni mwake.

    Muda wote huo Joshua alikuwa akizunguka huku na kule. Japokuwa alikuwa akipiga stori nyingi lakini alikuwa akitaka kufika sehemu moja tu, sehemu ambayo ilikuwa ni kumwambia kwamba alikuwa akimpenda. Maongezi yake katika wakati huo yalifanana na mtu ambaye alikuwa akitaka kwenda Afrika Kusini, ila njia alizokuwa akipita ni kuelekea Kigoma, kuingia Burundi na Kongo na mwisho wa siku kusafiri tena kuelekea Zimbabwe na kisha kuingia nchini Afrika Kusini.

    Maongezi yake yalikuwa marefu sana na wakati kulikuwa na njia fupi, njia ambayo ingemfanya kufika pale alipokuwa akitaka tofauti na muda ambao alikuwa akiutumia kuzunguka huku na kule. Japokuwa moyo wake ulikuwa ukiamini kwa aslimia mia moja kwamba Debora asingeweza kupindua lakini badio alikuwa na kijihofu moyoni mwake, siku hiyo alishangaa kuona ujasiri wote ambao alikuwa nao moyoni mwake ukiwa umempotea kabisa.

    “Kuna kitu ningependa kukwambia jioni ya leo” Joshua alimwambia Debora.

    “Kitu gani?” Debora aliuliza swali ambalo lilimfanya Joshua kushusha pumzi ndefu na nzito.

    “Nimetokea ku…….” Joshua alisema lakini hata kabla hajamalizia sentensi yake, simu yake ya mkononi ikasikika ikianza kuita.

    Akanyamaza, alichokifanya ni kuichukua simu ambayo ilikuwa mfukoni mwake na kisha kuanza kuangalia kioo, namba ilikuwa ngeni kabisa. Hakuonekana kujali sana, alichokifanya ni kuipokea simu na kisha kuipeleka sikioni.

    “Hallow” Joshua aliita huku akionekana kujiamini.

    “Unaongea na kituo kikuu cha polisi cha Osterbay” Sauti ya upande wa pili ilisema.

    “Polisi?” Joshua aliuliza huku akionekana kushtuka.

    “Ndio. Polisi”

    “Kuna nini tena. Mbona umenitisha?”

    “Unahitajika kituoni” Sauti ya upande wa pili ilijibu.

    “Mungu wangu! Kituoni kufanya nini tena? Kuna baya lolote nililolifanya? Mbona kila siku ninalipa kodi kila ninapoleta mizigo yangu!” Joshua alisema huku akionekana kuwa na hofu.

    “Unahitajika mahali hapa. Upo wapi kwa sasa?” Sauti ya p[olisi iliuliza.

    “Nipo Magomeni”

    “Sawa. Tunahitaji ndani ya dakika thelathini uwe umefika mahali hapa” Polisi yule alimwambia.

    “Kuna amani afande?”

    “Ndio. Hautakiwi kuhofia kitu chochote kile”

    “Oooopppsss..! Nakuja” Joshua alisema na kisha kukata simu.

    Amani yote ambayo alikuwa moyoni mwake ikaonekana kupotea, simu ambayo ilikuwa imeingia kutoka polisi ikaonekana kubadilisha hali yote ya furaha ambayo alikuwa nayo na kuingiwa na hali ya hofu. Kwanza kabla hajaongea chochote kile na Debora akaanza kufikiria kuhusiana na biashara zake ambazo alikuwa akizifanya, alionekana kuwa na hofu kila wakati.

    Akaanza kuwafikiria madereva ambao walikuwa wakiendesha magari yake kwa kuona kwamba inawezekana walikuwa wamesafirisha mirungi pamoja na bangi na hivyo magari yake kukamatwa na yeye kuhitajika kituo cha polisi. Kila kitu ambacho alikuwa akikifikiria mahali hapo kikaonekana kumtia hofu, hakukuonekana kuwa na amani hata mara moja.

    “Kuna nini tena?” Debora alimuuliza Joshua mara baada ya kukata simu.

    “Simu kutoka polisi” Joshua alisema huku akionekana kuwa mnyonge.

    “Wamesemaje?”

    “Wananihitaji sasa hivi” Joshua alimjibu debora.

    “Mmmh! Kiamani au?”

    “Alivyosema ni kiamani lakini sidhani. Hiyo ni mbinu mpya wanayoitumia polisi pindi wanapotaka kukukamata” Joshua alimwambia debora.,

    “Sasa unahisi kuna kitu gani kimetokea huko?”

    “Mmh! Sijui. Yaani hapa naanza kufikiria biashara zangu. Hawa madereva wangu watakuwa wamefanya kitu. Haiwezekani iwe hivi. Nimefanya biashara kwa miaka zaidi ya mitatu, sijawahi kuitwa na polisi kituoni” Joshua alimwambia Debora.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Inabidi uende kuwasikiliza kwanza”

    “Mmmh! Sijui nifanye nini. Ngoja nikupeleke nyumbani kwanza” Joshua alimwambia Debora.

    Mazungumzo yalikuwa yamekwishaingia doa, katika kipindi hicho zile hali za mapenzi ambazo walikuwa nazo katika kipindi kifupi kilichopita zikaonekana kupotea. Badala ya mzunguko wa damu wa Joshua kuwa mkubwa kutokana na hisia za kimapenzi alizokuwa nazo juu ya debora, katika kipindi hicho mzunguko ule ukabadilika, haukuwa ukizunguka kwa kasi kwa sababu ya hisia za kimapenzi, ulikuwa ukizunguka kwa kasi kwa sababu moyo wake ulikuwa umejawa na hofu kubwa.

    Walipotoka mahali pale, wakaingia ndani ya gari na kisha kuanza kumpeleka Debora Mwananyamala alipokuwa akiishi. Ndani ya gari kila mmoja alionekana kuwa kimya, hofu kubwa bado ilikuwa ikiendelea kuutawala moyo wake, hakuamini kwamba kulikuwa na polisi ambao walikuwa wakikuita kituoni kiamani, kichwa chake kiliamini kwamba kila polisi ambaye alikuwa akikuita kituoni alikuwa akikuita kwa sababu ulikuwa umefanya kosa fulani na hivyo walikuwa wakitaka kukukamata kirahisi bila kuangaika kutembea mpaka kuchoka au kuchoma mafuta ya gari lao.

    “Safari njema Joshua. Kuwa makini barabarani” Debora alimwambia Joshua mara baada ya kumteremsha katika mtaa wa mwananyamala maeneo ya Komakoma.

    “Hakuna tatizo. Take care” Joshua alimwambia Debora.

    Joshua hakutaka kupoteza muda wake mahali hapo, japokuwa alikuwa na wasiwasi mwingi lakini hakuonekana kuwa na jinsi, ilimpasa kwenda katika kituo cha polisi kujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea. Njiani, kama kawaida yake hakuonekana kuwa na furaha kabisa, kitu ambacho kilimfanya kumuita Debora na kuongea nae katika kipindi hicho alikuwa ameachana nae huku akiwa hajamwambia kile alichotaka kumwambia, hiyo ilimuuma sana.

    Kutoka Mwananyama Komakoma mpaka katika kituo cha Osterbay wala hakikuwa mbali, akafika na kisha kuanza kueleka katika kaunta ya kituoni hapo. Alipofika, akajitambulisha na kumwambia polisi aliyemkuta katika kaunta ile kwamba alikuwa amepigiwa simu na kuambiwa alikuwa akihitajika katika kituo hicho.

    “Wewe ndiye Joshua?” Polisi yule aliyekuwa kaunta alimuuliza.

    “Ndio mimi”

    “Sawa. Ingia ndani ya chumba hicho” Polisi yule alimwambia Joshua ambaye alionekana kuwa na wasiwasi zaidi.

    Maneno aliyoambiwa kuingia ndani ya chumba kidogo kilichokuwa katika kituo kile yalionekana kumuogopesha zaidi. Kwanza akageuka nyuma na kisha kuangalia nje, polisi kadhaa walikuwa wametulia katika viti vyao wakipiga stori tu. Katika kipindi hicho ni wazo moja tu ndio ambalo lilikuwa likimjia kichwani mwake, wazo lililomtaka akimbie mahali hapo na kurudi alipotoka.

    Kitendo cha kuambiwa kwamba aingie ndani ya chumba kile kilionekana kama kujikamatisha kirahisi na kizembe sana, kujikamatisha katika hali ambayo hakutarajiwa kuifanya kabla. Kichwa chake kikawa kikiuliza maswali yasiyokuwa na majibu, moyo wake ukagawanyika, upande mmoja ulimwambia aingie lakini upande mwingine ulikuwa ukimkataza kufanya hivyo kwa kuwa lilikuwa kosa ni sawa na kuliwasha pipa kwa petroli na wewe kujiingiza mzima mzima.

    “Samahani afande. Kuna usalama?” Joshua alimuuliza polisi yule huku akianza kutokwa na kijasho chembamba.

    “Mbona unaogopa?”

    “Dada, hakuna mtu anayekuwa na amani mara anapoambiwa anahitajika polisi. Unakuwa na amani gani na wakati kitendo cha kuingia hapa tu umebakiasha hatua moja ya kueleka jela? Yaani ukitoka hapa unakwenda mahakamani na kisha kuingia jela kwenyewe. Naomba uniambie. Kuna amani?” Joshua alimuuliza polisi yule.

    “Yeah! Kuna amani” Polisi yule alimwambia Joshua.

    Japokuwa alikuwa amehakikishiwa amani lakini moyo wake ukaopnekana kulipinga hilo. Kwa hatua za taratibu zilizojaa wasiwasi akaanza kusogea ndani ya chumba kile, alipoufikia mlango, akaingia.

    Macho yake yakatua kwa mwanamke mmoja, mwanamke ambaye alikuwa na uhakika kwamba alikwishawahi kumuona sehemu fulani kipindi kirefu kilichopita, ukiachana na mwanamke huyu, pembeni kulikuwa na mwanamke mwingine wa Kichina. Joshua akaonekana kushtuka, mwanamke ambaye alikuwa amemuhitaji kwa muda wa miaka mitano, leo hiyo alikuwa mbele yke akiwa amebeba mtoto, akajihisi furaha kubwa moyoni mwake, wasiwasi wote ambao alikuwa nao ukaonekana kupotea ndani ya sekunde moja, kwa kasi ya ajabu, mwanamke yule akamuweka mtoto chini na kumsogelea na kisha kumkumbatia huku kila mmoja akianza kulia.

    “Rose….Rose…Rose…” Joshua aliita huku akiwa amekumbatiana na Rose na machozi yakimtoka.

    “Joshua. Joshua mpenzi. Hatimae nikutana na wewe” Rose alimwambia Joshua.

    Kila mtu akabaki kimya mahali pale wakiwaangalia wapendao hao ambao walikuwa wakilia huku wakiwa wamekumbatiana. Kukutana kwa mara nyingine lilikuwa ni tukio ambalo hakulitegemea mtu yeyote yule katika kipindi hicho, kwao ukaonekana kuwa kama muujiza, wakati mwingine wote walionekana kuwa kama wapo ndotoni ambapo baada ya muda kidogo wangeamshwa na alamu za simu zao kwa ajili ya kuendelea na shughuli zao nyingine za kila siku.

    “Hivi ni wewe Rose?” Joshua alimuuliza Rose akiwa amemtoa kifuani mwake, akawabaki akimwangalia.

    “Ni mimi. Ni mimi Joshua” Rose alimwambia Joshua na kisha kukumbatiana tena.

    Siku hiyo ikaonekana kuwa furaha kubwa katika maisha yao, hakukuonekana kuwa na mtu ambaye aliamini kile ambacho kilikuwa kimetokea mahali hapo, kwao, bado ilionekana kuwa kama ndoto moja kubwa ambayo ingewasisimua katika maisha yao yote.

    “Mtoto…” Joshua alisema na kisha kumwachia Rose.

    Macho yake yakatua usoni mwa Lydia ambaye alikuwa amesimama pembeni kabisa ya miguu ya mama yake huku ane akiangalia kile ambacho kilikuwa kikitokea. Hakujua sababu ambayo ilimpelekea mama yake kukumbatiana na mwanamume ambaye hakuwa akimfahamu kabisa. Joshua akachuchumaa na kisha kumwangalia Lydia usoni.

    “Malkia wangu” Joshua alimwambia Lydia huku akimwangalia, machozi yalikuwa yakiendelea kumtoka, akashindwa kuvumilia, akajikuta akimkumbatia Lydia ambaye akaanza kulia huku akitaka aachiwe kutoka katika mikono ya baba yake, Joshua.







    Sauti ya kilio cha Lydia bado ilikuwa ikiendelea kusikika mahali hapo. Mtu ambaye alikuwa amemkumbatia hakuwahi kumuona, hakuwa akijua kabisa kama yule ndiye alikuwa baba yake mzazi, mwanaume ambaye hakuwa ameonana nae katika kipindi chote cha maisha yake. Rose alikuwa akiwaangalia wote wawili huku akiendelea kutokwa na machozi, kila alipokuwa akimwangalia Joshua kumbukumbu za siku za nyuma, siku ambazo alikuwa akiwasiliana na Joshua na kufanya mapenzi zilikuwa zikimjia kichwani mwake.

    Siku hiyo, watu wa familia moja walikuwa wamekutana mahali hapo, Joshua hakuonekana kuamini kwamba simu ile ambayo alipigiwa na polisi alikuwa akihitajika mahali hapo kwa ajili ya kuonana na mwanamke ambaye alimpa ujauzito pamoja na mtoto wake, Lydia.

    Alipoona kwamba kamkumbatia vya kutosha mtoto wake, akasimama na kisha kuwaangalia watu ambao walikuwa mahali pale. Kilichomshtua, rafiki yake, Ally alikuwepo mahali hapo, akamfuata na kisha kumpa salamu kwa kupeana mikono na kuwaangalia polisi waliokuwa mahali pale na kuwasalimia.

    “Kuna nini tena? Mbona polisi hivi?” Joshua aliuliza huku akionekana kutokuelewa kitu chochote kile ambacho kilikuwa kikiendelea mahali hapo.

    “Naomba ukae kwenye hicho kiti mara moja” Polisi, Bwana Pawasa alimwambia Joshua ambaye akavuta kiti kilichokuwa pembeni na kisha kukikalia.

    “Unamjua msichana huyu?” Lilikuwa swali la kwanza ambalo lilitoka kwa Bwana Pawasa akimuuliza Joshua.

    “Yeah! Huyu alikuwa msichana wangu” Joshua alimjibu.

    “Alikuwa msichana wako. Ina maana kwa sasa si msichana wako?” Bwana Pawasa alimuuliza Joshua.

    “Hiki ni kitu ambacho kinahitaji mazungumzo. Nilipotezana nae kwa miaka mitano, siwezi kusema kwamba bado ni msichana wangu kwa sababu sifahamu kama ameolewa na mtu mwingine au amempata mvulana mwingine. Ninachokifahamu ni kwamba mara ya mwisho naachana nae, alikuwa msichana wangu” Joshua alimwambia Bwana Pawasa huku watu wote mahali pale wakiwa kimya wakimsikiliza.

    “Na unamfahamu huyu mtoto? Bwana pawasa alimuuliza Joshua huku akimnyooshea kidole Lydia.

    “Kwa kumuona, ndio kwanza namuona leo” Joshua alijibu.

    “Kwa hiyo haumfahamu”

    “Yeah! Simfahamu”

    “Sasa kwa nini umemkumbatia kwa furaha?”

    “Kwa sababu ya hisia”

    “Hisia gani?”

    “Kwamba ni mtoto wangu” Joshua alijibu.

    “Kipi kilichokufanya kuhisi hivyo?” Bwana Pawasa alimuuliza huku akiwa amemkazia macho.

    “Katika kipindi ambacho nilitengana na Rose, alikuwa mjamzito” Joshua alijibu.

    “Kwa hiyo unadhani haya ndio matunda ya ujauzito aliokuwa nao?”

    “Ndio. Ninahisi hivyo”

    “Ok! Ngoja nikuulize swali jingine la msingi. Kipi kilikufanya kujua kwamba ujauzito huo ulikuwa wako?” Bwana Pawasa alimuuliza.

    “Siku ya kwanza na ya mwisho kufanya nae mapenzi, aliniambia kwamba alikuwa katika siku hatari za kupata mimba. Kwa sababu kila mmoja alikuwa katika hisia kali za kufanya mapenzi, tukashindwa kujizuia. Tukafanya” Joshua alimwambia bwana Pawasa.

    Kila kitu ambacho alikuwa akikielezea Joshua mahali hapo watu wote walikuwa kimya wakimsikiliza. Maswali ambayo alikuwa akiulizwa mahali hapo yalikuwa yakijbiwa kikamilifu, alikuwa akitoa majibu ya kuridhisha kiasi ambacho kila mtu mahali hapo akaonekana kumuelewa.

    “Na utasemaje kama akitokea mwanaume mwingine na kusema kwamba huyu mtoto ni wake. Utakubaliana nae?” Bwana Pawasa alimuuliza Joshua.

    “Kiukweli ni ngumu sana kukubaliana nae” Joshua alijibu.

    “Kwa sababu gani?”

    “Ni kwa sababu Rose alinimbia kwamba siku ile tuliyokuwa tukifanya mapenzi alikuwa katika siku zake za kushika ujauzito” Joshua alijibu.

    “Hilo hatukatai. Kipi kinachokufanya kuamini hilo? Au alikudanganya, au ulimpa mimba lakini mimba yako aliitoa au mimba kuharibika. Kipi kinachokufanya kuamini kwamba hili ndio tunda la ujauzito uliokuwa umempa Rose?” Bwana Pawasa aliuliza swali ambalo lilimfanya Joshua kukaa kimya kwa muda kama mtu ambaye alikuwa akifikiria jibu la kutoa.

    “Sidhani kama anaweza kufanya hivyo” Joshua alijibu.

    “Kwa nini haudhani kwamba anaweza kufanya hivyo? Unamwamini kwa asilimia mia moja au?” Bwana Pawasa alimuuliza Joshua.

    “Basi tu, kwa hapo sina jibu, ila sidhani kama anaweza kufanya kitu kama hicho” Joshua alimwambia Bwana Pawasa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maelezo ambayo aliyatoa Joshua yakaonekana kumridhisha kila mtu mahali hapo, kilichofanyika ni kwa Bwana Pawasa kumuagiza polisi mmoja kumfungulia Peter ambaye alitakiwa kufika mahali hapo. Katika kipindi ambacho Peter alikuwa akielekea mahali hapo, ikaonekana kama bahati, sauti ya mama yake ikasikika katika kaunta, polisi ambaye alikuwa katika kaunta ile akamruhusu kuingia katika chumba kile.

    Macho ya Bi Stella yakakutana na watu kadhaa ambao walikuwa ndani ya chumba kile, hakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea mahali hapo, hakukuwa na mtu aliyekuwa akimfahamu zaidi ya mtoto wake, Peter, Rose pamoja na mtoto ambaye aliamini kwamba alikuwa mjukuu wake, Lydia.

    “Karibu mama” Bwana Pawasa alimkaribisha Bi Stella.

    “Asante. Nimekuja kumuona mtoto wangu” Bi Stella alimwambia Bwana Pawasa ambaye nae alimtaka kukaa chini na kusikiliza kile kilichokuwa kikiendelea mahali hapo.

    “Peter. Unamjua huyu kijana?” Bwana Pawasa alimuuliza Peter huku akimnyooshea kidole Joshua.

    “Hapana”

    “Joshua, unamjua huyu kijana?”

    “Hapana” Joshua alijibu huku akimwangalia Peter.

    “Mpaka hatua hii mmekwishatuchanganya sana, tena mtu ambaye anatufanya kutuchanganya ni Peter” Bwana Pawasa aliwaambia.

    “Kuna nini tena?” Bi Stella alijikuta akiuliza.

    “Ok! Unamfahamu huyu mtoto?” Bwana Pawasa alimuuliza Bi Stella huku akimnyooshe kidole Lydia.

    “Ndio. Ni mjukuu wangu” Bi Stella alijibu.

    “Ok! Nimekuelewa. Umejua vipi kama huyu ni mjukuu wako?” Bwana Pawasa alimuuliza.

    “Mtoto wangu, Peter aliniambia”

    “Tatizo lile lile. Tumerudi tena kwa Peter yule yule” Bwana Pawasa alisema.

    “Kwani kuna nini kinaendelea?” Bi Stella aliuliza huku akionekana kutokuelewa kile kilichokuwa kikiendelea mahali hapo.

    Hapo ndipo ambapo Bwana Pawasa alipoanza kuelezea kile kilichokuwa kikiendelea mahali hapo, kila kitu ambacho alikuwa akikielezea kilionekana kumuingia sana Bi Stella ambaye alionekana kutokuamini kile ambacho alikuwa akikisikia kwa wakati huo. Akabaki akimwangalia Rose kwa macho yaliyojaa chuki kubwa, hakuamini kama mtoto ambaye alikuwa ameonyeshewa kwamba alikuwa mjukuu wake kumbe hakuwa mjukuu wake.

    “Kwa hiyo mmekubaliana nae?” Bi Stella aliuliza.

    “Nani?”

    “Rose”

    “Ndio. Ila Peter hakutaka kukubaliana nae. Alichoamua ni kwamba vichukuliwe vipimo vya D.N.A” Bwana Pawasa alimjibu Bi Stella.

    “Hata mimi naona hilo ndio suluhisho ambalo linatakiwa kufanyika” Bi Stella alimwambia Bwana Pawasa.

    “Ila katika vitu vyote itawapasa mkubaliane na kitu kimoja”

    “Kitu gani?”

    “Kama ikitokea ikagundulika kwamba mtoto si wa Peter, tutasema kwamba alimteka mtoto na si kumchukua kama alivyodai kwani si mtoto wake. Ila kama ikionekana kwamba ni mtoto wake, basi tutakubaliana kwamba alikuwa amemchukua mtoto wake na si kumteka. Umenielewa?” Bwana Pawasa alimwambia Bi Stella.

    “Mmmh! Nimekuelewa”

    “Sawa. Vipimo vitafanyika leo hii hii” Bwana Pawasa aliwaambia.

    “Hospitali gani?”

    “Hakuna mtu anayetakiwa kufahamu. Ni siri yetu. Kuna dokta wa hospitali fulani ndiye ambaye atachukua vipimo” Bwana Pawasa alimjibu Bi Stella.

    Tayari mambo yakaonekana kuanza kuwa magumu mahali hapo, uamuzi ambao alikuwa ameuchukua Bwana Pawasa ulionekana kuwa uamuzi mmoja mkubwa ambao ungeweza kumpoteza Peter ambaye angeshtakiwa kwa kosa la kumteka mtoto tena kwa kutumia bunduki. Bi Stella hakuonekana kujali, kitu ambacho alikuwa akikiamini ni kwamba Lydia alikuwa mtoto wa Peter.

    Peter hakunyamaza, kila wakati alikuwa akidai kwamba Lydia alikuwa mtoto wake maneno ambayo yalionekana kumchanganya hata Joshua mwenyewe ambaye alibaki akiwa hajui kama mtoto Lydia alikuwa mtoto wake au wa Peter kama alivyodai.

    Baada ya dakika kadhaa, wakatolewa ndani ya chumba kile na kisha kutakiwa kuingia katika gari aina ya difenda tayari kwa kuelekea katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo ili kugundulika mzazi halisi wa mtoto Lydia.

    “Una uhakika ile mimba ya kipindi kile ndio iliyomtoa mtoto huyu?” Joshua alimuuliza Rose huku akionekana kuwa na hofu.

    “Nina uhakika”

    “Sasa inakuwaje kuhusu mtu huyu?”

    “Baba alitaka niolewe na Peter, nikawa kwenye mahusiano nae, tukafanya mapenzi. Ili kumfanya asiwe na wasiwasi na baba asinigombeze kwa chochote kile, nikamdanganya kwamba siku ambayo nilifanya nae mapenzi ilikuwa ni siku ambayo mimba iliingia ila nilimdanganya, tayari nilikuwa na mimba yako” Rose alimwambia Joshua.

    “Nimekuelewa. Kwa hiyo hapa jamaa hana chake?”

    “Hana chake. Niamini mpenzi”

    “Nakuamini kwa asilimia mia moja” Joshua alimwambia Rose.

    “Nikuulize swali”

    “Niulize tu”

    “Unanipenda?”

    “Zaidi ya miaka mitano iliyopita” Joshua alimwambia Rose

    Safari ya kwenda hospitalini bado ilikuwa ikiendelea, kitu walichokifanya polisi ni kimoja tu mahali hapo. Hawakutaka watu hao watumie usafiri wao wenyewe kwani kwa kufanya hivyo wangeweza kufanya kitu chochote kile kama kuleta ushawishi kwa madaktari kwa kuwaahidi fedha au kitu kingine na ndio maana walitaka waende nao kuelekea katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kutumia gari lile la polisi.

    Walipofika huko, Bwana Pawasa akaonana na Dokta Iqram Maduro ambaye alimuelezea kila kitu kilichokuwa kimetokea na dokta huyo kuahidi kuwanyia vipimo wote, vipimo ambavyo vilistahili kufanyika. Dokta Iqram akaanza kumuita mama na mtoto wake, Rose akainuka na kisha kuelekea katika chumba maalumu na baada ya hapo, Peter na Joshua kufuata. Walichukua takribani dakika ishirini, wakatoka ndani ya chumba kile na kutakiwa kukaa katika benchi.

    Hakukuwa na mtu ambaye alionekana kuwa na amani, kila mmoja alionekana kutokujiamini mahali hapo. Japokuwa Joshua alikuwa amepewa uhakika na Rose kwamba mtoto alikuwa ni wa kwake lakini katika kipindi hicho hali ya kujiamini ikamtoka kabisa moyoni mwake, alionekana kama mtu ambaye alikuwa akisubiri majibu ya damu yake ili kugundulika kama aliathirika au la. Wala haukupita muda mrefu, dokta Iqram akatokea mahali hapo huku akiwa na karatasi, hofu zikaongezeka mioyoni mwao.

    “Kila kitu tayari” Dokta Iqram aliwaambia.



    *****

    Kila mmoja alikuwa kimya katika kipindi hicho wakimwangalia dokta Iqram ambaye alisimama mbele yao huku akiwaangalia na mikononi mwake kukiwa na karatasi kadhaa. Kwa Joshua, Peter, Bi Stella pamoja na Rose walionekana kuwa na wasiwasi, majibu ya vipimo vya D.N.A ndiyo ambayo yangeweza kuwapa uhakika kwamba Lydia alikuwa mtoto wa nani.

    Polisi, Bwana Pawasa akasimama na kisha kumsogelea dokta Iqram na kisha kumuomba zile karatasi, alipopewa akaanza kuziangalia, aliziangalia kwa sekunde kadhaa na kisha kuyapeleka macho usoni mwa Joshua, alipoyatoa, akayapeleka macho yake usoni mwa Peter, hakuridhika, napo akayatoa na kuyapeleka usoni mwa Rose, wote hao walionekana kuwa na wasiwasi mkubwa.

    “Nashukuru dokta kwa msaada wako” Bwana Pawasa alimwambia dokta Iqram kabla ya kusema nani alikuwa mzazi halali wa mtoto Lydia.

    Bwana Pawasa alionekana kama kuchelewesha mambo mahali hapo, kila mtu alikuwa akitaka kujua kile ambacho watu walikuwa wamekisubiria sana mahali hapo, kitendo cha Bwana Pawasa kuchukua karatasi zile na kutokuzungumza nao chochote kilizidi kuwaongezea presha watu wale.

    “Mtoto ni wa Joshua” Bwana Pawasa aliwaambia huku akianza kumpa Peter karatasi zile ahakikishe.

    Mapigo ya moyo yakaongeza kasi mwilini mwa Joshua, hakuonekana kusikia vizuri kile ambacho alikuwa amekiongea Bwana Pawasa. Huku akionekana kutokuamini, akampokonya Peter karatasi zile na kisha kuanza kuziangalia kwa makini. Ni kweli, vipimo vyake vya DNA vilikuwa vimeendana na vipimo vya DNA vya Lydia.

    Joshua akashindwa kuvumilia, akasimama na kisha kumfuata Rose na kumkumbatia kwa furaha. Kitu ambacho walikuwa wakitegemea kutokea ndicho kilikuwa kimetokea kwa wakati huo. Mara baada ya miaka mitano kupita bila kuonana, leo hii walikuwa wameonana kwa mara nyingine, ndani ya siku ambayo ilikuwa na utata mkubwa kuhusianana mtoto wao Lydia lakini mwisho wa siku kila kitu kilikuwa kama kilivyotakiwa kuwa.

    Kwa Peter, mambo yalikuwa tofauti kabisa, majibu ambayo yalikuwa yametangazwa yakaonekana kumuumiza kupita kawaida. Hakuamini kama alikuwa amefanya kazi kubwa ya kumteka mtoto Lydia na wakati hakuwa mtoto wake wa kumzaa. Akajutia muda wake, akajutia kila kitu ambacho kilikuwa kimefanyika mpaka kuhakikisha kwamba Lydia anatekwa na kumpeleka kwa baba yake, Bwana Edward ambaye alikuwa hoi kitandani.

    Mpaka katika kipindi hicho Bwana Edward alikuwa na uhakika kwamba alikuwa amemuona mjukuu wake kabla ya kifo chake, hakuwa akifahamu kama kulikuwa na utata mkubwa juu ya mtoto yule ambaye alikuwa ameletewa hospitalini pale.

    “Nafikiri kila kitu kimekamilika. Kwa maana hiyo Peter utafikishwa mahakamani kwa tukio la utekaji ambalo ulilifanya” Bwana Pawasa alimwambia Peter huku akimtaka mmoja wa polisi waliokuwa mahali pale wamfunge pingu.

    Kwa Bi Stella hilo likaonekana kuwa kama pigo moja kubwa katika maisha yake. Mume wake alikuwa hoi kitandani, mtoto wake pekee, Peter ndiye ambaye alikuwa njiani kuelekea gerezani kwa kile alichokuwa amekifanya. Moyo wake ukawa kama umekufa ganzi, hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya hili kumuokoa mtoto wake asifikishwe mahakamani ambapo baada ya hapo angeishia gerezani.

    “Naomba mumsamehe” Bi Stella alimwambia bwana Pawasa.

    “Mmepoteza muda wetu, yaani mmepoteza sana. Kwanza kwa kumuangalia tu huyu mtoto na Joshua, wala hakuna kuuliza swali, wamefanana vile vile ila nyie mkajidai wabishi” Bwana Pawasa alimwambia Bi Stella.

    “Naomba mumsamehe mtoto wangu” Bi Stella aliendelea kuomba msamaha.

    “Hilo suala gumu sana, hili tukio alilolifanya limefika mpaka makao makuu na jalada lake kuandaliwa, hicho ni kitu kisichowezekana kabisa” Bwana Pawasa alimwambia Bi Stella.

    Ule ukaonekana kuwa kama msiba mmoja mkubwa kwa Bi Stella, hakuamini kama katika kipindi hicho yeye ndiye ambaye alikuwa akipitia mambo yote yale. Alipokuwa akimwangalia mtoto wake, Joshua, alikuwa akilia kama mtoto huku akihitaji kusamehewa kwa kila kitu alichokifanya. Polisi hawakuonekana kumuelewa kabisa, kitu ambacho walikuwa wakikifanya ni kutekeleza wajibu wa kazi yao tu.

    Walipofika nje wakawapandandisha kwenye gari na kisha kuanza safari ya kurudi kituoni. Muda wote Joshua na Rose walikuwa wameshikana mikono huku wakionekana kuwa na furaha tele. Bi Lucy mpaka katika kipindi hicho hakuongea kitu chochote kile, alikuwa akifuatilia kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea.

    Katika kipindi ambacho walikuwa garini kuelekea katika kituo cha polisi cha Osterbay, muda mwingi Peter alikuwa amekiinamisha kichwa chake chini akilia. Kila wakati alikuwa akijuta kwa kile ambacho kilikuwa kimetokea, hakuamini kwamba mwisho wa kila kitu ungekuwa namna ile. Katika kipindi hicho lawama zake zote alikuwa akimpa Rose kwa kile ambacho alikuwa amekifanya cha kumdanganya kwamba kabla Lydia hajazaliwa ule ujauzito ulikuwa wa kwake. Njia nzima kwake ilionekana kuwa ya mkosi, katika kipindi hicho alijua fika kwamba alikuwa akielekea gerezani kufungwa kwa kitendo kile alichokifanya cha utekaji wa mtoto Lydia.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Kila kitu kikaonekana kufanyika kama kilivyotakiwa kufanyika. Peter na Ezekiel wote walihukumiwa kwa kufungwa gerezani kwa miaka kumi kutokana na kitendo cha utekaji ambacho kilitafsiliwa kama ugaidi mahakamani, tena mbaya zaidi walikuwa wametumia bunduki. Kwa Bwana Edward ambaye alikuwa hoi hospitalini, nae akafariki katika maumivu makali. Kwa Joshua na Rose, wakakubaliana kukaa chini na kupanga maisha yao ya baadae. Hawakutaka kuishi kama wapenzi, walichokuwa wamekiamua kwa wakati huo ni kutaka kuishi kama mume na mke.

    Wakafanya mipango ya kufunga ndoa, kwa sababu Joshua alikuwa na fedha za kutosha, hilo kwake halikuonekana kuwa tatizo hata mara moja. Walichokifanya ni kwenda kuonana na Bwana Shedrack ambaye akaonekana kutokuwa na jinsi zaidi ya kuwapa baraka zote kwamba waoane na Mungu awatangulie katika maisha yao huku akiwataka wasahau kila kitu ambacho kilitokea katikamaisha ya nyuma.

    Baraka zile zikaonekana kuwa baraka kweli, kamati ya harusi ikaandaliwa na hatimae michango ikaanza kukusanywa huku taarifa zikaanza kusambazwa kwamba Joshua na Rose katika kipindi hicho walikuwa wamechoka kuishi maisha ya peke yao hivyo walikuwa njiani kufunga ndoa. Kwa ndugu jamaa na marafiki, hiyo kwao ikaonekana kuwa jambo kubwa na zuri ambalo vijana wengi walitakiwa kuchukua hatua kama hiyo, baada ya miezi miwili watu hao wakafunga ndoa na kuishi kama mume na mke.

    Maisha yao yakawa ya furaha, kitendo cha kufunga ndoa na kuishi pamoja kikaonekana kuwafurahisha na kuwapa matumaini mapya katika maisha yao ya ndoa. Hawakutaka kumtenga Lydia na Lee, waliwaacha watoto hao pamoja waendelee na maisha yao kama kawaida, kwenda katika shule ya St’Marys pamoja na shule ya kichina ya Shung Sheng.

    Lydia ndiye alikuwa mtu pekee ambaye alikuwa akiwaunganisha kwa kila kwa wakati huo, kwao, yeye ndiye alikuwa furaha yao, walimpenda kupita kawaida huku wakimpa kila kitu ambacho alikuwa akikihitaji. Ndani ya miaka yao mitano ya ndoa yao, wakapata watoto wawili mapacha, pacha wa kiume walimpa jina la Erick na wa kike kumpa jina la Erica.

    Watoto hao wakazidi kuwaunganisha zaidi na zaidi, wakawaweka pamoja zaidi, wakawapa furaha ambayo walikuwa wakiihitaji katika kipindi hicho. Miaka iliendelea kusonga mbele mpaka kukatika miaka mingine mitano, wakawa wamefikisha muda wa miaka kumi tangu wafunge ndoa na kuwa mume na mke.

    Kwa sababu Lydia alikuwa akijua kuzungumza lugha ya kichina kama mchina, shule ikaamua kumgharamia kwa kila kitu ili aelekee nchini China kwa ajili ya kusoma zaidi. Hilo lilikuwa ni ombi ambalo lilifikishwa mbele ya Bwana Joshua na mkewe, Bi Rose. Hakukuwa na kipingamizi chochote kile, katika maisha yao walitamani sana mtoto wao aendelee kupata elimu zaidi, hivyo alitakiwa kwenda nchini China kwa ajili ya kuiendeleza elimu yake kwa muda wa miaka mitano.

    Katika siku ambayo Lydia alikuwa akiondoka ndani ya nchi .pamoja na Lee kuelekea nchini China kwake ilikuwa ni majonzi makubwa, hakuamini kama katika kipindi hicho alikuwa akienda kuishi mbali na wazazi wake, watu ambao walikuwa nae karibu kwa kila kitu. Hakukuwa na jinsi, kitu ambacho kilikuwa kikitakiwa kutokea hakikuwa na budi kutokea, katika miaka yake kumi na tano, alitakiwa kuondoka nchini Tanzania na kuelekea nchini China kuendelea kusoma.

    Lee ndiye ambaye angebaki kuwa mtu wake wa karibu katika kipindi hicho, kusingeweza kutokea mtu yeyote yule ambaye angekuwa nae karibu zaidi ya Lee ambaye kwake alikuwa kama ndugu yake. Baada ya kuagana na kila mtu katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Juliaus Kambarage Nyerere, wakaelekea katika ndege ya Air Qatar na kisha baada ya muda ndege hiyo kupaa, safari ya kuelekea nchini China kwa lengo la kusoma ikawa imeanza wakati huo.

    ****

    Katika kipindi cha nyuma kabla ya Lee kuondoka Bi Lucy alionekana kuwa na wakati mgumu, katika kipindi hicho alikuwa akiifikiria sura ya bandia ambayo alikuwa ameivaa, sura ambayo alikuwa ameibadilisha zaidi ya mara ishirini mpaka kufikia katika kipindi hicho. Kila siku alikuwa akifikiria kama lilikuwa jambo sahihi kumwambia Lee kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea katika kipindi cha nyuma au la. Bi Lucy hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya lakini hakuwa na jinsi, alichoamua ni kumuita Lee ambaye katika kipindi hicho alikuwa na miaka kumi na nane.

    “Nataka ufahamu kila kitu kuhusiana na mimi siku ya leo” Bi Lucy alimwambia Lee ambaye alikuwa kimya akimsikiliza.

    Uso wa Bi Lucy ukaanza kubadilika, macho yake yakaanza kuingiwa na wekundu hali iliyoonyesha kwamba machozi yalikuwa yakimlenga. Lee hakujua ni kitu gani ambacho Bi Lucy alikuwa akitaka kumwambia kwa wakati huo, alichokifanya ni kuanza kumbeleza mama yake aache kulia na kisha kuzungumza kile alichokuwa akitaka kuzungumza.

    Alichokifanya Bi Lucy ni kuanza kumuhadithia Lee kila kitu kilichotokea katika maisha yake ya nyuma pamoja na mumewe, Zhan ambaye alikuwa waziri wa Afya nchini China. Bi Lucy hakutaka kuficha kitu chochote kile, alimuhadithia kila kitu mpaka fedha ambazo zilikuwa katika benki kuu ya Tanzania

    “Kwa hiyo hii sura niliyoizoea si sura yako?” Lee aliuliza huku akionekana kushtuka.

    “Ndio. Hii si sura yangu halisi, hii ni sura ya bandia ambayo nimekuwa nikiivaa kwa sababu sikutaka wananchi wa China kunifahamu kwani wangeweza kuniua pia” Bi Lucy alimwambia Lee.

    “Sasa mbona kila siku inaonekana mpya na haina tatizo kabisa. Hivi sura ya bandia inaweza kukaa usoni kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi na nane?” Lee aliuliza huku akionekana kushangaa.

    “Nimekuwa nikiibadilisha mara kwa mara sura hii kwa kuagiza kutoka nchini China” Bi Lucy alimwambia Lee.

    “Utajificha mpaka lini mama?” Lee alimuuliza mama yake, Bi Lucy.

    “Mpaka nitakapokufa”

    “Haiwezekani. Kuna kipindi kitafika na utatakiwa kuwa huru” Lee alimwambia mama yake.

    “Wewe unavyoona ni kipindi gani?”

    “Kipindi nitakapokuwa rais wa China”

    “Unataka kuwa rais wa China?”

    “Ndio. Kwa gharama zozote zile nitataka kuwa rais wa China” Lee alimwambia Bi Lucy.

    “Kama unataka kuwa rais wa China, haina budi ni lazima ukasome nchini China”

    “Hilo si tatizo. Nitakwenda kusoma huko na ningependa kwenda na Lydia” Lee alimwambia mama yake.

    “Kwa sababu gani?”

    “Huwa siangalii hapa mama. Huwa ninaangalia maisha yangu ya baadae. Kila ninapoangalia, naona kabisa Lydia atakuja kuwa msaada wangu mkubwa sana hapo baadae kuupata urais wa China” Lee alimwambia Bi Lucy.

    “Mmmh! Mbona unanichianganya”

    “Hautakiwi kuchanganyikiwa mama. Kila kitu kipo kwenye mipango. Ngoja niende na Lydia nchini China tukasome, muda ukifika, utagundua kwamba Lydia alikuwa msaada wangu mkubwa katika kuupata urais wa China. Nikishakuwa rais, utakuwa huru, nikishakuwa rais, tutapata fedha zaidi. Niamini mama” Lee alimwambia mama yake, Bi Lucy.

    :”Naliamini hilo. Ila umemwambia Lydia kitu chochote kuhusiana na hilo?”

    “Hapana. Sitomwambia. Ndio kwanza ana miaka kumi na tano. Nataka mpaka atakapofikisha miaka ishirini ndio nitamwambia mipango yangu” Lee alimwambia Bi Lucy.

    “Sawa. Hakuna tatizo”

    Huyo alikuwa Lee, kijana aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kuchezea kompyuta katika maisha yake. Kila siku alikuwa ni mtu wa kushinda na kompyuta yake chumbani huku akifanya mambo mbalimbali. Kompyuta ikaonekana kuwa rafiki yake mkubwa ambaye hakutaka kumuacha katika kipindi hicho, alikuwa akiamini kila kitu kilikuwa rahisi kufanyika duniani kama tu utaishirikisha kompyuta yako.

    Kutokana na kuwa mzoefu mkubwa wa kutumia kompyuta yake hasa mambo ya network, Lee alikuwa akitumia mitandao bila kulipia kitu chochote kile. Katika maisha yake hakuwa akilipia gharama zozote zile. Alikuwa akitumia simu bure, alitumia internet bure na hata Dstv alikuwa akitumia bure kabisa bila mtu yeyote kugundua hilo.

    Pamoja na hayo yote, Lee alikuwa mwizi wa mitandaoni. Wateja wa kampuni za simu mara kwa mara walikuwa wakilalamika kwamba fedha zao zilizokuwa kwenye akaunti zao za simu zilikuwa zikiibiwa, hakukuwa na mtu ambaye alifahamu kwamba Lee ndiye alikuwa katika mchakato mzima. Kwake, maisha ya wizi kwa kutumia kompyuta ndio ambayo alikuwa akiyafanya sana, kuiba benki kwake halikuonekana kuwa tatizo, alikuwa akichukua kiasi kikubwa cha fedha na kisha kukihifadhi katika akaunti zake zaidi ya sita.

    Katika maisha yake, alijiona kuwa na uhitaji wa fedha kuliko kitu kingine, alijua fika kwamba kama ulitaka kuwa rais wa nchini China basi kwanza ilikupasa kuwa na fedha nyingi ili baadae uweze kuupata uongozi huo wa juu. Hiyo ndio sababu ambayo ilimpelekea kuwa mwizi wa mitandaoni, kitu alichokuwa akikihitaji ni kupata fedha tu.

    Aliuhitaji sana urais wa nchi ya China, alihitaji kuiongoza nchi hiyo ambayo ilimuua baba yake kwa sababu ya wizi wa mamilioni ambao alikuwa ameufanya. Lee akaonekana kama kuridthishwa, nae akatamani kufanya wizi katika nchi hiyo. Wizi ambao alikuwa akitaka kuufanya haukuwa kama ule wa baba yake aliokuwa akiufanya, wizi ambao alikuwa akitaka kuufanya ni wizi wa kuiba kwa kutumia kompyuta, wizi wa kuingiza codes katika kompyuta za benki na makampuni makubwa na kisha kuiba.

    Hilo kwake wala halikuonekana kuwa tatizo. Katika umri ambao alikuwa nao alijua fika kwamba angekwenda kufanya kila kitu alichokuwa akikitaka kukifanya. Ndoto yake kubwa ilikuwa ni kuwa rais wa China, rais wa kwanza mwizi kuitawala nchi ya China. Pamoja na hayo yote, hakuona kama angeweza kukamilisha kila kitu endapo asingemshirikisha Lydia. Lydia kwake akaonekana kuwa kila kitu, bila Lydia aliona kwamba asingeweza kufanikisha malengo yake aliyojiwekea ya kuwa rais wa nchi ya China. Katika kila kitu ambacho alipanga kukifanya kuwa rais wa nchi ya China, Lydia alikuwa mtu wa kwanza katika mipango yake.

    Katika kipindi ambacho walikuwa wakisafiri kuelekea nchini China, mawazo ya Lee yalikuwa yakifikiria kuwa rais wa China tu, hakutaka kufikiria kitu kingine kwa wakati huo, alikuwa akitaka kuwa rais tu. Kwake, hilo likaonekana kuwa jambo jepesi sana, jambo ambalo lisingekuwa na tatizo lolote lile, ila pamoja na hayo yote, Lydia ilikuwa ni lazima aingie katika mipango yake ili aweze kuwa rais wa China katika miaka ya baadae.

    “Nitakuwa rais tu. Lydia hatoweza kukataa kufanya nitakachotaka akifanye” Lee alijisemea katika kipindi ambacho safari ya kuelekea nchini China ikiendelea.

    *****

    Walitumia masaa ishirini na mbili mpaka kufika nchini China ndani ya uwanja mkubwa wa Kimataifa wa Beijing. Hali ya hewa ilikuwa tofauti sana na ndani ya jiji la Dar es salaam, baridi lilikuwa kali miilini mwao japokuwa kwa wachina hali ile ilionekana kuzoeleka sana. Kwa wote wawili wakabaki wakiyashangaa majengo pamoja na mandhali ya nchi ya China kwani wote katika kipindi hicho ndio ilikuwa mara ya kwanza kukanyaga katika nchi ya China.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakaanza kutembea pamoja na abiria wengine kuelekea katika mlango wa kuingia ndani ya jengo la uwanja huo ambapo mabegi ya abiria yalikuwa yakipekuliwa na kisha kuyachukua na kuanza kupiga hatua kutoka nje. Walipofika nje, wakakuta vijana wawili ambao walikuwa wameshika mabango yaliyoandikwa majina yao na kisha kujitambulisha kwamba wao ndio waliokuwa watu ambao walikuwa wakisubiriwa na vijana wale. Wakachukuliwa na kisha kuanza safari ya kuelekea shuleni.

    Njiani, kila mmoja alikuwa akiangalia majengo mazuri pamoja wingi wa watu ambao ulikuwa ukionekana mitaani, kila kitu ambacho kilikuwa kikioneana katika macho yao kilionekana kuwa kigeni kilichojaa mvuto mkubwa. Kichwani mwa Lee katika kipindi hicho alikuwa akifikiria kuhusu kuiongoza nchi hiyo ambayo ilikuwa miongoni mwa nchi kubwa duniani, bado alikuwa na hamu ya kuwa rais wa nchi ile kwa ajili ya kuiba fedha na kuendelea na maisha yake.

    Hakutaka kuwa rais wa China kwa sababu ya mambo mengine, kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kuwa rais wa China na kisha kuiba fedha za serikali. Katika kila mipango ambayo alikuwa ameipanga, Lydia alikuwa amekaa katikati, asingeweza kuitimiza kama Lydia asingekuwa daraja la kufikia katika sehemu anayotaka kuwa katika kipindi cha mbele.

    Gari likachukua barabara ya 6th Ping ambayo ilikwenda moja kwa moja mpaka ikaungana na barabara kubwa ya Wei Wei ambayo ilikwenda hadi katika shule moja kubwa, shule ambayo ilikusanya watoto wa hatua ya kwanza mpaka wale wa high school, shule kubwa iliyokuwa ikijulikana sana nchi China, Shengh Weng, shule iliyokuwa upande wa kaskazini mwa jiji la Beijing ambayo pia kulikuwa na chuo kilichoitwa kwa jina hilo hilo.

    Geti lilipofunguliwa, gari likaingizwa na kisha kuteremka. Kila mmoja alibaki akiangalia mazingira mazuri ya shule hiyo, wanafunzi walikuwa wengi huku kila mmoja akionekana kuwa bize akifanya mambo yake. Hawakutakiwa kusimama na kushangaa shangaa tu, wakachukuliwa na kisha kupelekwa ofisini ambapo huko wakaandikishwa kujiunga na shule hiyo na kisha kupelekwa katika vyumba ambavyo walitakiwa kuvitumia.





    Japokuwa alikuwa na miaka kumi na tano lakini Lydia alionekana kuwa na uzuri kupita kawaida. Umbo lake lilionekana kuwa umbo la kimiss ambalo lilikuwa likiwachanganya sana wanaume ambao walikuwa wakimwangalia katika kila kipindi ambacho alikuwa akitembea. Ngozi yake nyeusi ikaonekana kumuwekea mvuto zaidi, wanafunzi wote weusi wa kike ambao walikuwa wakisoma shuleni hapo hawakuwa wakionekana kuwa na mvuto kama aliokuwa nao Lydia.

    Upole wake, ukimya wake nao ulikuwa chachu kwa wanafunzi wengi ambao walikuwa wakimwangalia, kila alipokuwa akipita, wanaume walishindwa kujizuia, walijikuta wakitoa salamu bila kupenda. Umri wake haukuwa mkubwa lakini mwili wake ulikuwa mkubwa kiasi ambacho watu wengi walifikiri alikuwa na miaka kumi na nane.

    Wachina wengi wakaonekana kuanza kuomba urafiki kwa msichana Lydia lakini jambo hilo kwa Lydia lilionekana kuwa gumu katika kipindi hicho. Mtu ambaye alikuwa nae karibu sana alikuwa Lee, kila alipokuwa akitoka darasani, Lee alikuwa pembeni yake kiasi ambacho kikawafanya wanaume wa Kichina kumuona Lee kuwa mtu mwenye bahati ambaye alikuwa amempata Lydia bila kutumia nguvu yoyote ile.

    Mavazi yake ya shule hiyo iliyokuwa ikivaa sare ndio ambayo yalionekana kumdatisha kila mwanaume. Kwa wanafunzi wengine wa kike hasa wa Kichina wala hawakuwa wakitamanisha, hii iliwezekana kuwa na ngozi zao kuwa na mvuto, lakini kwa wanafunzi weusi wa kike kama Lydia, ilikuwa ni balaa. Kila mwanafunzi wa kiume alikuwa akitamani kuwa na Lydia, hawakuwa wakikifikiria kitu kingine vichwani wao zaidi ya kufikria ngono tu kwa kuona kwamba wanawake wengi ambao walikuwa wametoka Afrika walikuwa na miili iliyojaa joto.

    Kila mtu alikuwa akimwangalia Lydia kwa macho ya mahaba, hawakujua ni kwa namna gani ambayo ingewafanya kumpata Lydia ambaye alionekana kuwa karibu sana na Lee. Upole wake ukamfanya kutokuzoeana sana na wanafunzi wengine shuleni hapo, kitu ambacho alikuwa akikipenda kwa wakati huo kilikuwa ni kusoma tu.

    Kwa Lee, yeye kama yeye alionekana kuwa mkali toka wiki ya kwanza ambayo aliingia ndani ya shule hiyo kusomea IT (Information Technology), masomo yahusuyo kompyuta. Uwezo wa lee ulionekana kuwa tofauti na wanafunzi wengine kiasi ambacho mpaka walimu walikuwa wakishangaa ni kwa jinsi gani mtu huyo alikuwa na uwezo wa namna hiyo.

    Baada ya wanafunzi kuona kwamba Lee alikuwa na kitu cha ziada kichwani, wakaanza kumgeuza mwalimu wao jambo ambalo Lee alilifanya bila kuangalia jinsia au rangi. Kujituma kwake kwa ajili ya wanafunzi wengine kukaonekana kumpa sifa sana shuleni pale, wanafunzi wakaanza kumtangaza kwamba alikuwa miongoni mwa wanafunzi ambao walikuwa wakipenda sana wenzao wajue kama ambavyo wao walivyokuwa wakijua.

    Kwake, hilo likaonekana kuwa jambo zuri ambalo alikuwa akilitaka sana katika kipindi hicho. Alijua fika kwamba hata kabla ya kufika huko mbeleni na kuwa rais wa nchi hiyo, alitaka kuhakikisha kwanza anachukua uongozi wowote shuleni hapo. Hayo ndio yalikuwa malengo ambayo alikuwa amejiwekea, malengo ambayo aliyaona ni lazima yatimie.

    Mwaka wa kwanza ukakatika, bado Lee alionekana kuwa mkali na aliendelea kujitoa kwa ajili ya wanafunzi wengine. Kila alichokuwa akikifanya, walimu walijivunia kuwa na mtu kama yeye. Jina lake likazidi kuwa kubwa, japokuwa shule ilikuwa na wanafunzi zaidi ya elfu ishirini na tano lakini wanafunzi wengi wakaanza kumfahamu kutokana na kile alichokuwa akikifanya.

    Maisha yaliendelea zaidi, mwaka mwingine ulipoingia, Lee akaanza chuo katika shule hiyo hiyo ambayo kwa sehemu nyingine ilikuwa ikitumika kama chuo, na hiyo ilitokana na mapendekezo ya serikali ambayo ilitaka litengwe eneo ndani ya shule hiyo kwa ajili ya chuo, mchakato ambao ulitiwa chachu na rais wa kipindi hicho, Bwana Hong Teng mnamo mwaka 2003, katika kipindi ambacho nchi ya China ilikuwa imeongezeka wasomi huku jiji la Hong Kong likitaka kujigawa na kuwa nchi.

    Chuoni hapo, bado Lee hakuonekana kurudi nyuma, alikuwa akiwadhihirishia wachina wenzake kwamba alikuwa moto wa kuotea mbali katika kipindi hicho. Kichwani mwake, kila alipokuwa akikaa alikuwa akiifikiria kompyuta yake, kila alipokuwa akikaa alikuwa akifikiria kuwa rais wa China kwa ajili ya kuiba fedha tu.

    Baada ya mwaka mmoja mwingine kupita, Lee akaona kwamba alitakiwa kuanzisha kitu fulani, kitu ambacho kingewakusanya wanafunzi na wanachuo karibu zaidi, hapo ndipo alipoanzisha mtandao wake ambao ulikuwa kama facebook, mtandao alioupa jina la WorkSpace, mtandao ambao ungekuwa unatumika katika chuo hicho tu.

    Mtandao ule ukaonekana kuanza kuvuma chuoni pale, Alikuwa amechukua kipindi cha miaka miwili mpaka mtandao ule kukamilika. Hiyo ikaonekana kuwa njia bora kwa wanachuo na wanafunzi kuwasiliana kumbe katika kichwa chake bado Lee alikuwa akifikiria mambo mengine kabisa.

    Wizi ndio ambao alikuwa akitaka kuufanya katika kipindi hicho. Mtandao ulikuwa ukijisajili kama ulivyokuwa ukitumia mtandao wa facebook. Katika kipindi cha kujisajili, ilikuwa ni lazima uweke namba yako ya simu, bila kuweka ulikuwa hauwezi kujisajili. Katika namba ya simu ambayo ulikuwa ukiiweka, ulikuwa na uamuzi wa kuifanya ionekane au isionekane, huo ni uamuzi wako ila katika kipindi cha kujisajili, ilikuwa ni lazima uweke namba ya simu kwa ajili ya kukutumia code ambazo ulipaswa kuingiza ili uendelee na usajili wa akaunti yako ya WorkSpace.

    Kila mtu alipokuwa akiweka namba ya simu, moja kwa moja ilikuwa ikienda katika email ya Lee, sehemu ambayo ilimfanya kuchukua namba yako ya simu na kisha kuanza kuitafuta line yako, yaani simu yako hata uwe wapi, ilikuwa ikimwambia kupitia namba ya line yako. Hatua iliyofuata ilikuwa ni kuanza kuipekua simu yako bila wewe kujua, akawa anaangalia sehemu zote ambazo namba yako iliwahi kuandikwa kama kwenye benki au sehemu nyingine.

    Alipoona kwamba namba yako ilikwishawahi kuandikwa benki na kuingizwa kwenye kompyuta, alikuwa akicheza na kompyuta mpaka kuijua namba yako ya akaunti ya benki. Alipoijua, hiyo ikaonekana kuwa kama mafanikio makubwa kwako, akawa anaingiza codes zake za wizi, akaunti yako inajileta, namba zako za siri zinatokea na anaangalia kiasi cha fedha na kukuibia bila wafanyakazi wa benki kufahamu.

    Hiyo ndio njia ambayo alikuwa akiitumia Lee, kichwa chake kilikuwa kikifikiria sana fedha, wanachuo hawakuonekana kulifahamu hilo, kwao waliona kama mapinduzi makubwa ya mtandao wa Facebook, walijivunia sana kuwa na mtandao wao ambao ungewafanya kuwa karibu zaidi bila kujua kwamba nyuma ya pazia kulikuwa na mchezo mchafu ambao ulikuwa ukiendelea.

    Kila siku kazi ya Lee ilikuwa ni kuwaibia fedha wanachuo na wanafunzi wa kawaida ambao walibaki wakilalamika kwa uongozi wa benki bila kujua kwamba Lee alikuwa nyuma ya kila kitu. Ni ndani ya miezi miwili tangu mtandao huo utumike, tayari alikuwa ameingiza kiasi cha dola milioni mbili huku nyingine zikizidi kumiminika katika akaunti zake za siri, akaunti ambazo benki zilionekana kama zimekufa kumbe zilikuwa hai ila alichokifanya ni kubadilisha codes za akaunti zake kificho.

    Mtandao wa WorkSpace uliendelea kushika kasi kila siku, wanachuo walizidi kujiunga zaidi na zaidi. Wanachuo wa vyuo vingine waliposikia kwamba kulikuwa na mtandao mwingine kama wa Facebook ambao ulikuwa ukipatikana katika chuo hicho, wakamuomba Lee aupanue zaidi mtandao huo, Lee hakuwa na shida, akafanya kama wanachuo walivyotaka iwe.

    Kama kawaida yake, kila siku akaunti zake zikawa zinacheka sana, fedha zilikuwa zikimiminika kupita kawaida. Lee akaonekana kuleta mapinduzi makubwa kwa nchi ya Marekani kutokana na mitandao mingi ya kuchati kumilikiwa na wamarekani. Kwa Lee hiyo ikaonekana kuwa furaha kwake, hata serikali ya China ilipomtaka kuutanua mtandao huo zaidi na zaidi nchini kote, Lee akafanya hivyo.

    Hapo ndipo ilipokuwa balaa katika akaunti zake, akaanza kuingiza kiasi kikubwa cha fedha jambo ambalo alisababisha matatiozo makubwa kwa benki mbalimbali. Benki nyingi zikafungwa kwa sababu walionekana kuwa wezi, walionekana kuwaibia wateja wao fedha katika akaunti zao bila kujua kwamba kulikuwa na mwanachuo ambaye alikuwa nyuma ya kila kitu, huyu alikuwa Lee, kijana ambaye alikuwa ameanzisha mtandao wa kuchati huku lengo lake likiwa ni kuwaibia watu fedha kutumia kompyuta tu kwa kuingiza codes chache ambazo zilimuingizia fedha.

    Zaidi ya wananchi milioni kumi wa China wakawa wamejiunga na mtandao huo wa kuchati, mtandao ulionekana kuwa mzuri sana ambao uliwafanya watu kuwa karibu sana. Mtandao ule wa WorkSpace ukazidi kuwa zaidi. Nchi ya Japan nao wakataka kunganishwa, Lee akafanya hivyo, nchi ya Mongolia nao wakahitaji, Korea, Thailand na nchi nyingine wakahitaji, lee akawaunganisha na mpaka kutapaa katika bara lote la Asia. Baada ya kipindi kichache, Lee akawa milionea, aliingiza fedha nyingi kihalali kutokana na matangazo ila fedha nyingi zaidi aliziingiza kwa njia isiyokuwa ya halali hata kidogo.

    ****

    Kila siku ndoto zake zilikuwa ni zile zile, kuwa rais wa nchi ya China na kisha kuiba fedha nyingi ambazo zilikuwa zikitengwa kwa maendeleao ya nchi ya China. Japokuwa Lee alikuwa amepata mafanikio makubwa lakini wala hakuweza kuacha chuo, kila siku alikuwa mtu wa kusoma kwani bado alijiona kwamba hakuwa amefikia mafanikio kabisa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya miezi kadhaa, Lee akatakiwa kuhama katika chuo hicho na kuhamia katika chuo kikuu cha China, Beijing. Hiyo ikaonekana kuwa kama taarifa mbaya kwake, alikuwa amewazoea watu wengi sana katika chuo kile alichokuwa akisoma katika kipindi hicho ila pamoja na hayo yote, hakuwa na jinsi.

    Siku moja kabla ya kuondoka katika chuo hicho, Lee alitumia muda mwingi sana kuongea na Lydia ambaye bado uzuri wake ulikuwa ni zaidi ya kipindi cha nyuma. Kwa sababu Lydia alikuwa amekwishafikisha miaka kumi na nane, Lee akaanza kumwambia kuusiana na lengo ambalo alikuwa amejiwekea, kuwa rais wa nchi ya china.

    “Nataka kuwa rais wa China” Lee alimwambia Lydia ambaye kwa kiasi fulani alionekana kushtuka.

    “Unataka kuwa rais wa China?”

    “Ndio. Au wewe unaonaje?” Lee alijibu na kisha kuuliza.

    “Hakuna tatizo. Ila itabidi ujipange sana, si unajua hii nchi kubwa” Lydia alimwambia Lee.

    “Hilo halina tatizo. Nitafanya kila linalowezekana mpaka nifanikiwe. Kwanza nahitaji fedha zaidi” Lee alimwambia Lydia.

    “Hilo nalo la msingi sana”

    Kwanza katika kipindi hicho, Lee alikuwa akimsoma sana Lydia huku kichwa chake kikifikiria kama lilikuwa jambo sahihi kumwambia Lydia kile ambacho alikuwa amekifikiria au la. Huo kwake ukaonekana kuwa mtihani mkubwa sana, katika maisha yake, hakupenda kuwaamini wanawake kutokana na usiri mdogo ambao wangeweza kuwa nao mioyoni mwao. Alijua fika kwamba ni wanawake wachache ndio walikuwa na moyo wa kutunza siri, kuifanya siri kuwa siri.

    “Nataka unisaidie” Lee alimwambia Lydia.

    “Nikusaidie nini?”

    “Kupata urais” Lee alimjibu Lydia.

    “Mungu wangu! Nikusaidie kupata urais? Nitakusaidia vipi sasa?” Lyidia aliuliza huku akionekana kushtuka.

    “Wewe ni msichana mrembo sana Lydia”

    “Nalifahamu hilo”

    “Naamini kupitia urembo wako utanisaidia sana” Lee alimwambia Lydia.

    “Kivipi?”

    “Usiwe na wasiwasi. Kila kitu nitakwambia hapo baadae, cha msingi kwanza acha muda usonge mbele” lee alimwambia Lydia.

    Maisha bado yalikuwa yakiendelea zaidi, kila siku Lydia alikuwa mtu wa kujiuliza tu kwamba ni kwa namna gani angeweza kumsaidia Lee katika kile alichokuwa akikitaka amsaidie. Ni kweli alijijua kwamba alikuwa mrembo sana ila hakujua kwamba Lee angeutumia vipi urembo ule kwa ajili ya kumsadia kupata urais wa nchi ya China.

    Katika mwaka wa nne toka awe nchini China, hapo ndipo Lydia akampata mwanaume ambaye alimuona kufaa sana kuwa mpenzi wake, huyu alikuwa mwanaume kutoka barani Afrika katika nchi ya Kenya, Pierre Mbade. Mapenzi ya watu hawa wawili yalianza kimasihala sana lakini mwisho wa siku wote wawili wakajikuta wakiwa katika mapenzi ya dhati. Kutokana na umaarufu wa urembo ambao alikuwa nao Lydia, chuo kizima wakafahamu kwamba watu hao wawili walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi.

    “Nataka tukishamaliza chuo mwaka ujao turudi Afrika na kwenda kuoana” Pierre alimwambia Lydia huku akionekana kutokujiamini kama alikuwa amepata msichana mrembo namna ile.

    “Usijali. Tutafanya hivyo tukifika huko” Lydia alimwambia Pierre huku akiachia tabasamu pana.

    Kwao, mapenzi yakaonekana kuwa kila kitu kwa wakati huo, muda mwingi walikuwa pamoja huku wakifanya mambo mengi kama wapenzi. Pierre akachukua nafasi hiyo kuutoa usichana wa Lydia na kuyafanya mapenzi kuchanganmka zaidi na zaidi. Japokuwa mapenzi yao yalikuwa yakiendelea kama kawaida lakini bado kwa Lydia kichwa chake kilikuwa kikifikiria mambo mengi, hasa jambo ambalo Lee alikuwa amemwambia.

    Kwa upande wa Lee, akahamia katika chuo kikuu cha nchini China, Beijing. Kila mwanachuo ambaye alikuwa akisikia kwamba Lee angehamia katika chuo hicho alikuwa na hamu kubwa ya kumuona mtu huyo ambaye katika kipindi hicho alikuwa na jina kubwa katika bara zima la Asia. Katika kipindi ambacho alikuwa analiingiza gari lake la kifahari katika mazingira ya chuo, wanachuo wakaanza kuelekea kule gari lilipokuwa likiegeshwa, katika kipindi hicho, kila mtu alikuwa na shauku ya kumuona Lee, alifananaje na alikuwaje.

    Lee alipoteremka kutoka garini, wanachuo zaidi ya mia saba wakatoa simu na kamera zao na kisha kuanza kumpiga picha. Kwao, Lee alionekana kuwa maarufu sana katika kipindi hicho, mtandao wa WorkSpace ambao alikuwa ameuanzisha ulionekana kumpa jina kubwa na fedha nyingi bila watu kugundua kwamba nyuma ya pazi, Lee hakuwa mtu mzuri kabisa kutokana na wizi aliokuwa akiufanya.

    Kila aliyekuwa akimuona Lee katika kipindi hicho akaonekana kutokuamini kabisa, kwao, Lee alionekana kuwa kama malaika wa baraka ambaye alikuwa ameshushwa ndani ya chuo hicho. Lee alionekana kuwa tofauti sana na watu wengine ambao walikuwa na majina makubwa, kwake, umaarufu haukuwa kitu chochote kile, alitaka kuonyesha upendo mkubwa kwa kila mtu kwani huko mbeleni alikuwa na kitu kimoja cha kufanya, kutaka urais wa nchi ya China.

    Kabla hajaanza kuelekea ofisini, Lee akaanza kuongea nao, watu waliokuwa na maswali wakaanza kuuliza, Lee akawa huru kujibu kila swali, watu wakaonekana kuvutiwa nae. Mpaka katika kipindi ambacho anaelekea ofisini, bado watu walikuwa na shauku ya kutaka kusikia mengi kutoka kwake.

    Siku hiyo ndio ikawa siku ambayo Lee alikuwa ameingia ndani ya chuo hicho. Wanachuo wengi ambao walikuwa na akaunti katika mtandao wa kijamii wa WorkSpace wakaanza kuandika kuhusiana na ujio wa Lee ndani ya chuo kile huku wengine wakidiriki kusandika kwamba walijisikia kupata faraja sana kumgusa Lee na wengine wakisema kwamba walikuwa wakiumwa lakini mara baada ya kuliona gari la Lee linaingia, wakapata nafuu, pale walipomgusa tu, wakapona kabisa.

    Lee akawa mtu maarufu sana, kwa kila mchina ambaye alikuwa akisikia kwamba Lee alikuwa amehamia katika chuo kikuu cha nchini China, Beijing, kila mtu akatamani kwenda na kumuona. Kama kawaida yake, Lee hakuwa na mbwembwe, hakuwa na maringo hata mara moja. Alikuwa akiongea na watu wote, hakumbagua hata mara moja kwani alijua fika kwamba alikuwa na safari ndefu mbele yake.

    Waandishi wa habari hawakutaka kukaa kimya, tayari waliona kwamba katika kipindi hicho jina la Lee ndio ambalo lilikuwa kubwa sana, wakataka kuongea nae. Tofauti na watu wengine maarufu ambao walikuwa wakihitaji fedha katika kila kipindi ambacho walikuwa wakiitwa katika televisheni kwa ajili ya kuhojiwa, kwa lee wala hakutaka kulipwa, alikuwa akitaka kuhojiwa bure.

    “Ilikuwaje mpaka ukaanzisha mtandao wa WorkSpace?” Lilikuwa moja ya Sali ambalo yalitoka kwa mwandishi wa kipindi kile.

    “Nilikuwa ninahitaji kuwaweka watu karibu zaidi, watu wawe marafiki, wazoeane, watembeleane, wanaotaka kuwa kwenye mahusiano basi waingie kwenye mahusiano” Lee alijibu.

    “Kuna kingine zaidi ya hicho?”

    “Yeah! Unajua hii lugha ya Mandarian ndio lugha inayoongewa na watu wengi duniani kuliko lugha yoyote ile, katika mtandao wa WorkSpace, pia unaweza kuchagua lugha, mandalian imekuwa lugha ya kwanza. Kama unavyoona, kuna Kiswahili pia” Lee alimwambia mwandishi.

    “Na ni nani alikuandikia lugha ya Kiswahili?”

    “Mimi mwenyewe”

    “Wewe mwenyewe? Unajua Kiswahili?”

    “Yeah! Ninaifahamu sana lugha hiyo”

    “Umeijuaje?”

    “Nilizaliwa nchini China ila maisha yangu kwa miaka mingi nimekulia Afrika katika nchi ya Tanzania. Huko ndipo nilipoijua zaidi lugha hii” Lee alimwambia mwandishi wa habari.

    Kwa sababu kituo cha televisheni cha CCTV kilikuwa kikiangaliwa na watu wengi katika nchi za Asia, zaidi ya watu milioni hamsini walikuwa wakiangalia kipindi kile. Lee alikuwa ameelezea mengi sana ambayo yalionekana kuwagusa watu wengi sana. Katika baadhi ya mambo ambayo alikuwa ameyaongea, hakutaka kuwa mkweli, hakutaka watu wafahamu kama alikuwa mtoto pekee wa Zhan, mwanaume ambaye alikuwa waziri wa Afya katika kipindi cha nyuma, mtu ambaye aliuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kufanya ufisadi huku mke wake kutoroka. Wachina na watu wengine wakamuelewa kwa kila alichokisema..

    Siku zikaendelea kusonga mbele mpaka katika kipindi ambacho chuo cha Beijing kilipotaka serikali mpya kutokana na wale waliokuwepo kumaliza muda wake. Watu wakajitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kugombania nafasi mbalimbali mahali hapo. Lee akaona hiyo kuwa nafasi, alijiona kuwa na kila sababu ya kuwa rais wa chuo achukue mafunzo na baadae kuwa rais wa nchi ya China, akachukua fomu.

    Wanachuo wakaonekana kufurahia kupita kawaida, kitendo cha Lee kuchukua fomu ya kugombania urais wa chuo kilionekana kuwa kitu kilichowapa furaha kupita kawaida. Watu wengine ambao walikuwa wamechukua fomu za kuwania urais chuoni hapo walikuwa na kazi ya kufanya kampeni mpaka kuhonga lakini kwa Lee, kampeni yake kubwa ilikuwa ni kwenye mtandao wake wa WorkSpace, hata wale wanachuo ambao hawakuwa wakifika chuo walikuwa wakiziona kampeni zake ambazo alikuwa akiendelea nazo katika mtandao ule.

    “Ngoja niwe rais wa chuo kwanza kabla ya kuwa rais wa nchi hii” lee alijisemea huku akionekana kujiamini kwamba ni lazima angeshinda uchaguzi huo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Je nini kitaendelea?

    Je Lee ataweza kufanikisha lengo lake la kuwa rais wa chuo?



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog