Simulizi : Love Bite
Sehemu Ya Tatu (3)
ILIPOISHIA……….
Mawazo yalirudi tena kwenye ile picha na kuamua kuificha bila kuichoma moto kama alivyotaka mwanzo kufanya. Badala yake alienda sehemu ambayo kulikuwa na hati ya nyumba yake na kuiweka ile picha katikati. Ni kweli Prisza alikuwa anampenda na hawakuwahi kuachana. Ni muingiliano tu wa maisha ndi uliowatenganisha. Moyo wake aliona kama si haki kuichoma ile picha kwakua bado alikua na nafasi ndani ya moyo wake japokuwa kuonana na msichana huyo ni ngumu sana. Hata alipomaliza chuo alijitahidi kumtafuta bila mafanikio. Mpaka muda huu anajitegemea ni kipindi kirefu cha miaka sita tuko walipokutana na Prisca kwa mara ya mwisho.
Mawazo ya msichana huyo wa kwanza katika maisha yake yalimchanganya kichwa na hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali matokea na kuanzisha ukurasa mwengine wa maisha yake kwenye mapenzi na shani
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya usafi huo wa kabati lake, aliamua kujilaza kitandani na usingizi ukamchukua.
SONGA NAYO…………
Siku ya pili yake Jothan alienda kazini kama kawaida. Alifanya kazi zake na baada ya kurudi kazini alimkuta Shani amejaa tele nyumbani kwake.
“karibu mume wangu “ alikaribisha Shani na kumfuata Jothan na kumpokea mizigo yake.
“ahsante.” Aliongea Jothan na kumkabidhi mizigo yake Shani.
“una oga kwanza au unakula ndio uende kuoga?” aliuliza Shani baada ya kurudi pale alipokuwa Jothan.
“vyovyote tu mke wangu. Maana nahisi joto na hata njaa pia ninayo.” Aliongea Jothan na kumfanya Shani atabasamu.
“kaoge kwanza, maana ukiwa vizuri hata chakula kitashuka barabara.”
Alishauri Shani na mawazo yake yakapitishwa moja kwa moja na Jothan. Alipotoka kuoga Jothan, alirudi mezani na kukuta Shani ameshaandaa mapocho pocho ya kila aina yaliyochafua meza.
“unajua mke wangu, hata niwe na njaa vipi, kama wewe upo nyumbani basi hudiriki kuitunza hiyo njaa kwa sababu unajua sana kupika mke wangu. Muda mwengine naomba nipate na njaa ya ajabu ili nikifakamie kisawasawa chakula chako.”
Aliongea Jothan na Shani akabaki anatabasamu na kumuangalia Jothan kwa mapozi.
Mapenzi moto moto kutoka kwa Shani yalizidi kupamba moto. Muda wote Shani alijitahidi kumuweka Jothan kwenye kundi la wanaoyafurahia mapenzi. Jothan alijisikia raha kutokana na Shani kila wakati kutokana na mauzo anayoyapata kuwa na msichana High classic.
Walitamani kila saa wawe karibu na kulishana ndio style iliyowavutia watu wengi waliowashuhudia wawili hao walionyesha kupendana sana.
Siku moja Jothan akiwa anatoka kazini, ghafla aliona gari likiwa limepaki pembeni na kuna msichana akihangaika kulishughulikia lile gari. Jothan alipaki gari lake pembeni na kushuka kwa ajili ya kutoa msaada.
Alipomfika eneo la tukio, yule dada aligeuka kumuangalia Jothan na wote wakajikuta wanapigwa na butwaa.
“JOTHAN!!” aliita yule dada kwa sauti kubwa iliyoambata na mshangao mkuu.
“PRISCA!!” hata jothan naye alilitaja jina la yule msichana na kumfanya Prisca kujiachia na kupitisha mikono yake mgongoni mwa Jothan kupitia kweye makwapa yake kama ishara ya kumkumbatia. Jothan naye akampokeaa vizuri kwa kuzungusha mikono yake kwenye kiuno namba 6 cha Prisca.
Baada ya kusalimiana, wakaona haitoshi. Waliacha gari zao pale pale na kutafuta sehemu tulivu na kukaa kwa ajili ya kupigiana story mbili tatu kutokana na kukumbukana kupita kiasi.
“ ahsante mungu kwa kunikutanisha na kipenzi changu jamani,.. jothan milima haikutani ila binaadamu tunakutana. Leo hii kauli hiyo ndio naikubali kwa asilimia zote.” Aliongea yule dada huku akionyesha furaha ya wazi juu ya Jothan ambaye wakati huo alikua na tabasamu la usoni lakini kichwani alikua kwenye msongo wa mawazo. Anampenda Prisca lakini kwa sasa Shani amechukua nafasi kubwa kwenye moyo wake kutokana na kumpa kila anachokihitaji tena kwa wakati.
Alikiri kuwa kwa sasa Prisca alizidi uzuri na kumfunika hata Shani. Maana Shani alikuwa ameridhika na kuzidi kuwa mnene kiasi japokuwa sio kigezo cha kupunguza uzuri wake.
Ila Prisca alikuwa mwembaba lakini aliyekuwa na figa iliyojichonga kama glasi ya wine.
Kwenye kiuno alikuwa mnene na kufaya hipsi zake kuonekana sana. Pia kijungu cha wastani kilichotupiwa huko nyuma ndio kilizidi kumpa maksi zaidi na kumfanya azidi kuonekana special na wanaume wote wanaojua viwango vya wanawake wazuri na wenye mvuto katika muonekano wa macho ya marijali.
Kiuno kilichoingia ndani na muinuko wa kibinda ndio kilitengeneza namba 6. kiuno hicho mungu kawapendelea wasichana wachache sana. Hata wachina wameshindwa kutengeneza dawa ya kutengeneza kiuno hicho.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sura ya mviringo iliyokuwa na macho yenye kilevi bila ya kunywa kileo chochote ndio kilikuwa kivutio kingine. Ukiachana na weupe halisi ambao ulikuwa kiasi na kufanana na maji ya kunde, pia vijisima vidogo mashavuni vilivyojitokeza kila akifanya tendo lolote liliousumbua mdomo wake vilimfanya mtu yeyote kutamani kumuangalia usoni.
Uso uliombwa na haya mbele ya mwanaume ndio ulikuwa kivutio hasa kwa mvulana mwenye kutafuta mtu wa kuweka ndani na kuoa kabisa.
Mambo yote hayo ndiyo aliyokutana nayo Jothan baada ya kukutana na Prisca kwa mara nyingine baada ya muda mrefu.
Hata yeye mwenye alikutana na majaribu hayo aliyoyafananisha na majaribu ayapatayo mwanamke mjane baada ya kusikia sauti ya mwanaume tajiri aliyekuja kumfariji na kwa kumuahidi kumuoa na kuwa tayari kuwalea watoto wake.
Alijikaza kiume na kujaribu kuyaficha madhaifu yake yaliyomkumba na kujifanya yupo kawaida.
“Hata mimi nimefurahi kukuona, za miaka?” aliongea Jothan na kumuangalia Prisca ambaye alikua na furaha wakati wote huo toka wameonana.
“vipi, leo maaskari hawaji??” aliuliza Prisca na kucheka.
“leo hakuna mwanafunzi hapa..au wewe mwanafunzi?..maana siku ile nilikataa kuwa mimi ni mwanafunzi halafu wewe ukajitambulisha kuwa mwanafunzi.” Aliongea Jothan na kufanya kicheko kitawale kwa sekunde kadhaa kati yao.
“tumetoka mbali sana Jothan, leo naona kabisa kuwa mungu katufanya tusahau kipindi chote ambacho hatukua pamoja.” Aliongea Prisca huku akionyesha wazi kuwa bado alikuwa na mawazo ya mapenzi juu ya Jothan.
“hata mimi naona kama vile hatukuonana siku mbili kwa jinsi siku ya leo ilivyofukia mashimo ya miaka mingi niliyoishi bila kuiona sura yako.” Aliongea Jothan na kumuangalia Prisca aliyekuwa na kila kitu cha kutalii umuangalipo usoni.
“nikuulize swali Jothan?”
Aliongea Prisca na kumfanya Jothan kushangaa kidogo baada ya kuombwa ruhusa ya kuulizwa kitu.
Alifikiria kwa nukta kadhaa kisha akaruhusu kusikia kitu alichotaka kuuliza Prisca.
“umeshaanzisha uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwengine zaidi yangu?”
Aliuliza Prisca swali hilo huku akiwa kawaida na kuonyesha wazi kuwa lile swali linahitaji majibu sahihi na yenye utashi juu yake. Jothan hakuamini kama swali lile lingekuja mapema kabla hajaliandalia maandalizi yoyote ya kujibu.
Ubongo wake ulikimbia kwa kasi kutafuta jibu la kumpa kati ya ukweli au kumuongopea kwakua wakati huo swala la kumuepuka au kumpotezea msichana huyo aliyeonja penzi lake toka hajakuwa sister du kama hivi sasa.
Elimu ya msichana huyo na maisha mazuri anayoishi pia vilikuja kwenye ubongo wake na kufanya machaguo kuwa mengi. Yaani kama ni mtihani, basi lile swali lilikuwa katika mfumo wa matiple choice tena lililokuwa na mfumo wa A,B,C,D,E na F..
“sina.”
Alijibu Jothan huku moyo wake ukimuuma kumkana Shani.
“wooh… ni wazi hii couple Mwenyezimungu amekuwa akiismamia kwa kipindi kirefu. Unajua kuwa hata mimi nilikuwa naamini kuwa kuna siku tutakuja kuonana tena. Ndio maana sikuona uzito wowote kuwakataa wanaume wengi huku nikiwa sijui ni lini tutakutana. Roho ingeniuma sana ungeniambia kuwa kuna mwengine umeshampa moyo wako.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliongea Prisca bila kujua kuwa huo ndio ulikuwa ukweli wenyewe. Maneno hayo yalimfanya Jothan ajione kuwa hakuwa na makosa kumuongopea kwa sababu angemwambia ukweli chochote kingeweza kutokea na kusababisha maongezi ya amani kati yake na Prisca kutoweka.
“unataka kuniambia kuwa mpaka hivi sasa hauna mtu mwengine aliyerithi mikoba yangu?” aliuliza Jothan kimitego.
“hakuna… yaani toka uliponiacha sijaguswa na mtu mwengine. Yaani hata kama ungekuwa umenifunga luku basi zingesoma unit zile zile ulizoziacha.” Aliongea Prisca na kumfanya Jothan kutabasamu.
Waliongea mengi na kila mmoja alifurahia uwepo wa mwenzake pale. Waliachana baada ya kumrekebishia Prisca gari lake na kila mmoja kupata mawasiiliano yote ya mwenzake. Waliachana na ahadi ya kukutana naye tena walikubaliana kuwa watapeana taarifa kwenye simu.
Siku hiyo iliwekwa kwenye Diary ya Jothan ambaye alikuwa anatemba nayo kwenye mkoba wake wa kazini.
Usingizi ulikuja ukiambata na ndoto iliyojirudia kuanzia mwanzo hadi pale walipoachana. Aliamka asubuhi na kukuta Shani ameshamuandalia maji ya moto kwa kuwa asubuhi hiyo ilikuwa na kiubaridi kidogo. Alipoamka tu aliletewa nguo za bafuni pamoja na mswaki ambao ulisha wekwa dawa kabisa.
Alipokuwa bafuni mawazo yaligeuka upande wa pili na kumfanya amuwaze pia Shani kwa jinsi alivyokuwa akitimiza wajibu wote kama mke bora anavyotakiwa kufanya. Kila aliloliwaza kutendewa na msichana basi Shani alikuwa wa kwanza kufanya hata kabla hajaambiwa fanya.
Hayo na mengine mengi ndio yalimfunga Jothan na kuyatuliza macho yake kwa wasichana wengine na kumfanya kuwa mtiifu kwa kurudi nyumbani mapema.
Na kama anataka kupata moja moto maja baridi basi hutoka na mpenzi wake huyo ambaye alimfanya kuinjoy kwa kuwa sehemu nyigi walizoingia hakukua na mtu mwenye demu mkali kama wake.
Alimaliza kuoga huku kichwani hakujua jibu nini kati ya A au B. kuna wakati alitamani kuyaweka kuwa yote ni majibu. Kuna wakati alitamani arushe shilingi ila alishindwa kumjua nani amuweke mwenge na nani amuweke bichwa.
Prisca ndio msichana waliyebikiriana kwakua yeye hakuwahi kufanya mapenzi kabla kutokana na ulinzi thabiti wa wazazi wake alipokuwa anasoma. Na Prisca ndiyo yeye aliyekata utepe.
Shani ndio mpenzi wake wa ukubwani ambaye anamuonjesha matamu ya ndoa hata kabla hajafikia maamuzi ya kuoa. Hata sasa anaanza kuonekana na kitambi kidogo kwa sababu ya raha azipatazo kwa mpenzi wake huyo.
Japokuwa walikuwa wapenzi kwa kipindi kirefu, lakini hawakuwahi kukaa pamoja hata wiki moja kwa sababu kila mmoja alikuwa anaishi na wazazi wake.
Ila Shani na yeye wamekuwa wakilala pamoja mara tatu kwa wiki.
“itakavyokuwa ndio hivyo hivyo.” Aliongea Jothan baada ya kuona anaisumbua akili yake bila majibu sahihi.
Siku waliyo ahidiana kukutana kati ya Jothan na Prisca iliwadia huku kila mmoja akiwa amewasili bila kukosa huku wakiwa wamejitupia vitu vya thamani kila mmoja.
Make up na mpangilio wa nguo alizovaa Prisca zilimfanya kuonekana katika muonekano mwengine wa kuvutia zaidi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jothan hakuamini kuwa ndiye yeye alikuwa analala kwenye kifua cha yule msichana zamani. Pia hakuamini kuwa huyo msichana ndiye aliyekuwa akilipigania penzi lake miaka yote japokuwa walikuwa hawajaonana miaka mingi.
Walikutana huku kila mmoja akiwa ameshuka kwenye gari lake na kwenda kwenye hotel moja yenye hadhi hapa Dar. Walipata chakula cha mchana na baadae wakaenda kwenye swimming pool kuogelea.
Hamadi !,
Macho yalimtoka Jothan baada ya Prisca kuvua nguo zake na kubaki na nguo ya ndani huku juu kukiwa na sidiria ndogo iliyobana maziwa yake na kuyafanya yapande juu na kuonekana sehemu kubwa ya maziwa iliyoteganishwa na msitari mmoja kati kati kuwa wazi.
Jothan hakuona ubaya kuvua nguo na yeye na kubaki na boxer na kujumuika naye kwenye swimming pool huku wakiwa peke yao eneo hilo lililokuwa na mabwawa mengi ya kuogelea.
Waliogelea na kujikuta michezo yote wanacheza. Kuanzia bembea, mpira wa pete na mwisho wakamaliza na mchezo usio hitaji kocha wala mashabiki japo kuwa unapendwa na watu wengi hapa duniani. Ukiwa mtoto unaambiwa kuwa mchezo huo ni mmbaya lakini ukikuwa bila kufundishwa unajikuta unacheza huku ukijilaumu kwa nini hukuanza kucheza toka mwanzo.
Hawakujua walitumia muda gani kwakua taa za ile hotel ziliwaka muda wote na kufanya mtu asitambue wakati kama hajaangalia saa.
Mndinyo wa kitanda murua cha hotel hiyo ndio sababu iliyowafanya kudumu muda mrefu huku kila mmoja akiwa ame miss raha za mwenzake.
Mechi hiyo ya marudiano ilikuwa kali na kila mmoja alikiri kuwa walihitaji kuwa karibu na kucheza kila mara.
Baada ya muda, Jothan aligutuka kuwa hiyo siku ndio siku Shani alikuwa analala kwake. Aliamka fasta na kutupa macho yake kwenye saa ya ukutani
“MUNGU WANGU…. SAA SABA USIKU?”
Alishtuka kimoyo moyo na kutaja alichokiona kwenye saa. Aliamka ili aenda kuoga kwa ajila ya kwenda nyumbani kwake.
“vipi darling, unaenda wapi tena… mwenzio nahitaji kimoja tu cha mwisho.”
Alidakwa mkono kimahaba na Prisca aliyekuwa ameyarembua macho yake na kuonyesha ishara zote za kuhitaji kipindi cha pili baada ya mapumziko.
“najisikia uchovu ndio maana nilikua nataka kwenda kuoga.” Aliongea Jothan huku akiwa na wasiwasi mkubwa juu ya Shani kugundua usaliti alioufanya siku ile.
“twende wote babie, tukirudi mpango mzima au…” aliongea Prisca na kumfanya Jothan azidi kuchoka.
“poa.. twende.”
Alikubali kishingo upande na wote wakaenda kuoga na uchokozi alioufaya Prisca huko bafuni ikiwafanya mchezo huo kuanzia huko huko bafuni na kumalizikia kitandani wakiwa hoi na usingizi wa muda wote waliokuwa wakicheza cheza ulikuja na kuwafanya wapate usingizi mnono.
Saa nne asubuhi ndio waliachia kitanda na kwenda kuoga. Walipofungua mlango walikutana na wahudumu waliokuwa wakigonga kwa ajili ya kufanya usafi. Walieda kupata supu kutokana na kupotelewa na nguvu nyingi masaa kadhaa yaliyopita.
Baada ya hapo. Walijiandaa na kila mmoja akapanda kwenye gari lake huku Prisca akionyesha wazi kuwa aliufurahia uzinduzi wa uhusiano yao uliofanyika kwenye kitanda cha hotel ya SERENA.
Jaothan akiwa kwenye gari lake, aliiona simu yake aliyoiacha makusudi kwa ajili usumbufu pindi awapo na Prisca. Alikuta missed call zaidi ya kumi na tano na sms sita zote zikiwa za Shani na zikionyesha kuwa na wasi wasi juu ya usalama wake.
Alihuzunika sana kwa kosa alilolifanya japokuwa hakupanga kulala nje.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maisha ya kuendesha mioyo miwili hakuwahi kuishi na tayari kwa siku hiyo aliona adha yake na kutamani kuchuja na kuwa na mmoja tu. Ni nani ambaye angestahili kubaki na ni nani atoke ndio swali lililokosa majibu kwakua wote alikuwa anawakubali kwa wakati wao.
Alivyolala na Prisca alikuwa kama alikuwa anamfungua kwa mara ya kwanza hali iliyomfanya aamini kuwa hakutumika muda mrefu. Aliona sio sawa kumuacha msichana huyo mwenye ndoto naye nyigi za maisha yao toka walipokuwa wanasoma.
Na Shani hakustahili kutendewa unyama wowote kwakua hata yeye hajawahi kumfanyia unyama wowote zaidi ya kumfariji anapokuwa ana huzuni na daima aliisimamia furaha yake hata ikibidi kuenda kinyume na matakwa ya dini kwa kukubali kuishi nae bila ndoa.
Akiangalia kila mmoja alionyesha kumpenda kwa wakati wake na hawakuwa tayari kumuachia.
Ila yeye swali la NIMPENDE NANI lilimsumbua kuliko hata DIAMOND.
Aliamua kuwasha gari lake na kuelekea nyumbani.
“oooh.. ahsante mungu. Umekumbwa na nini kipenzi changu?.” Aliongea Shani baada ya kuupokea mkoba wa Jothan. Hali hiyo ilimshangaza Jothan kwakua hakutegemea mapokezi kama yale.
“samahani mke wangu, sikukupa taarifa kuwa ofisini kuliandaliwa warsha na nikaenda kwa kudhani itaisha siku hiyo. Hata hivyo simu yangu niliisahau kwenye gari na kunifanya nisizione missed call zako mapema.” Aljiuma uma Jothan mbele ya Shani ambaye wakati huo ndio kwanza alikuwa anamvua viatu baada ya kukaa kwenye moja ya masofa yaliyokuwa pale sebuleni.
“sawa mpenzi wangu. Nimefarijika tu wewe kurudi salama.. maana nilikuwa na wasi wasi juu ya uzima wako tu.” Aliongea Shani na kumuonyesha Jothan jinsi anavyomjali.
“samahani sana mpenzi wangu, nitajaribu kukupigia simu kwa kila siku nitakayochelewa kurudi nyumbani.”
Aliongea Jothan na kukiri kuwa amefanya makosa makubwa ambayo hata yeye mwenyewe hakuyategemea.
Siku hiyo ilipita kwa Jothan kulala muda mrefu kutokana na uchovu wa jana yake. Asubuhi aliamka na kukuta ameandaliwa nguo za kuvaa kwa ajili ya kwenda kazini zikiwa zimepigwa pasi kabisa. Aliwekewa maji ya uvugu vugu kwa ajili ya kuoga kisha kifungua kinywa matata kilikuwa tayari mezani kinamsubiria yeye tu.
“ashante mke wangu.” Alishukuru Jothan baada ya kumaliza kunywa chai.
“usijali mume wangu, nakutakia safari njema. Take care honey.” Aliongea Shani na kumfungulia mlango wa gari Jothan.
Jothan alifika kazini mapema na kufanya kazi zake kama kawaida. Saa nane alitoka kazini na kurudi nyumbani. Alikuta ameandaliwa chakula cha mchana mezani lakini Shani hakuwepo kwakua ilikuwa ni siku ya kwenda kwao. Alijihisi mpweke na alitamani Shani angekuwepo kwake moja kwa moja. Alikata shauri baada ya kula chakula na kuamua kumtafuta mpenzi wake kwenye simu.
“hallow” alipokea Shani kwa mapozi.
“I miss u babie, unaweza kuja tutoke baadae kidogo tukale mbuzi maeneo ya Facebook pub?” aliongea Jothan.
“noo babie, leo nimeenda kwa mama. Sio vizuri kuonyesha tabia mbaya mbele yake ya kurudi usiku. We vumilia babie. Kesho tutakuwa wote.” Aliongea Shani kwa pozi zilizomfanya Jothan kushindwa kukata simu hata kama maneno ya msingi ya kuongea nae yameisha.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“basi sawa. Sijui lini utanipeleka kwa mama.” Aliongea Jothan huku anatabasamu.
“si wewe mwenyewe tu hujaamua. Ukiamua hata leo nakuleta huku.” Aliongea Shani huku akionyesha wazi kuwa alikua anacheka.
“nitakuja tu mine, si unajua mambo mazuri hayahitaji haraka.” Aliongea Jothan na kukata simu.
Siku ya pili yake walitoka pamoja na kwenda kula bata maeneo hayo na kurudi mida ya saa tano usiku.
Alipokuwa kazini, alisikia simu yake ikiita kwa mlio tofauti. Kabla hata hajasoma jina la mpgaji wa hiyo simu. Tayari alishamtambua kwakua aliihifadhi namba ya mtu huyo kwa mlio tofauti kwa makusudi.
“haloo.” Aliipokea ile simu.
“haloo babie, I miss u.” sauti nyororo ya kike ilisikika upande wa pili.
“I miss u too Prisca, niambie.”aliongea Jothan huku akiangalia wafanya kazi wenzake waliokuwa bize wakifanya shughuli zao.
“hata kunitafuta wangu,.. yaani kama uliniroga mwenzako siku ile. Yaani sijielewi mpaka hivi leo.” Aliongea Prisca kwa sauti ya mahaba.
Jothan aliangalia na kuona soo kuendelea kuongea maneno yale mbele ya wafanyakazi wenzake.
“sema nini babie, nitakupigia nikiwa free. Now nipo kazini halafu nina kazi nyingi.” Aliongea Jothan kwa sauti ya chini.
“sawa wangu, baadae.” Aliitkia Prisca na kukata simu.
Jothan alifanya kazi zake na kurudi nyumbani kwake. Baada ya kupata chakula cha mchana, alijitupa kitandani na kuchukua simu yake na kumpigia Prisca.
“haya lete maneno.” Aliongea Jothan baada ya Prisca kupokea simu.
“nina hamu ya kuonana na wewe babie… sihitaji kuwa mbali na wewe hata kwa dakika moja kwa jinsi nillivyozimika mbaya.” Aliongea Prisca kwa sauti iliyomshinda mwana dada wa kipindi cha ala za roho kinachoruka usiku kwenye kituo cha clouds fm. Sauti ilipenya vizuri kwenye masikio ya Jothan na kuhisi labda Prisca alichanganya sauti ya Loveness love (Diva) na wema sepetu.
“tupange week end, sababu katikati ya wiki ni majanga.” Aliongea Jothan.
“poa, ijumaa si ulisema unatoka mapema. Unaonaje kama tukikutana siku hiyo.” Aliongea Prisca na wazo lake likapitishwa moja kwa moja na Jothan.
Siku ya ijumaa ilipofika. Jathan alimpa taarifa Prisca na wakakutana maeneo ya Peacock hotel iliyopo maeneo ya mnazi mmoja.
Jothan alifika na kumkuta Prisca alishafika muda mrefu kidogo na tayari alishaagiza kinywaji na alikua anakunywa taratibu.
Alipofika, alipokelewa kwa kukumbatiwa na Prisca na kupewa mabusu matatu matakatifu kwenye mashavu yake na moja likiwa sawia mdomoni mwake. Baada ya salamu hiyo adhimu. Walimuita muhudumu aliyekuja haraka na kumpa oda yao.
“tuchukue chumba sasa hivi au baadae?” aliuliza Prisca baada ya kumaliza kula.
“hapana, leo sijisikii vizuri kabisa na sipo tayari kushiriki tendo lolote Prisca.” Aliongea Jothan na kumfanya Prisca apigwa na butwaa. Maana alijiandaa kabisa kupata mechi nyingine siku hiyo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“kwanini babie….unaumwa???” aliuliza Prisca kwa mshangao.
“siumwi, ila mayo wangu unanisuta kila siku nikiongea na wewe kwenye simu au nikikutana na wewe. Najihisi sifanyi fair kwa nikitendacho.” Aliongea Jothan huku sura yake ikionyesha wazi kuwa hakuwa na furaha ingawaje aliingia kwa muonekano wa mtu aliyefurahia uwepo wao pale.
“jamani, tatizo ni nini wangu, mbona una nifumba fumbo ambalo sijui nitalifumbua vipi?...naomba uniambie ukweli kuliko kuniweka mwenzako kwenye uzio wa alama ya kuuliza.” Aliongea Prisca huku akionyesha wazi kubadilika kutoka katika hali ya furaha aliyokuwa nayo mwanzo na kuungana na Jothan.
“Prisca, hivi bado unanipenda?” aliuliza swali Jothan lililomfanya Prisca apigwe na bumbuwazi kwakua hakulitegemea lile swali.
“nakupenda sana tena zaidi ya niwezavyo kuelezea kwa ulimi wangu. Ndio maana nikaweza kukaa kipindi kirefu bila ya kuwa na mtu mwengine japokuwa ni wengi walikuwa wanakuja kunitongoza na bado sikuona umuhimu wa kuanzisha mapenzi mapya kabla mapenzi yako wewe na mimi kufa.” Aliongea Prisca na kumuangalia Jothan aliyekuwa makini kumsikiliza.
“hata mimi nakupenda Prisca, ila mimi ni msaliti na sio mwema kwako hata kidogo. Cha kwanza nimekuwa muongo kwa kukuongopea toka siku ya kwanza tulipokutana kwa mara ya pili ukubwani. Cha pili sistahili kuwa wako kwakua tayari nimeshakuharibia mipango na malengo yako kwa kipindi krefu Prisca.” Aliongea Jothan huku akionyesha wazi kuwa alikuwa katia wakati mgumu kufunguka yale yaliyomjaa moyoni.
“sikueliwi Jothan.. naomba nidadavulie uyasemayo.” Aliongea Prisca huku akionyesha kuchaganyikiwa.
“kwanza naomba unisameha Prisca kwa haya nitakayokuambia. … nilifanya makosa makubwa siku ile kwa kutokuambia ukweli kuwa tayari nina msichana na ninaishi naye. Nampenda sana ingawaje sikuweza kutoka kwenye mitego yako siku ile kwakua wewe ndio wa kwanza kukaa moyoni mwangu na chembe chembe za upendo juu yako ndizo zilizonisukuma mpaka kukuongopea na kukuambia kuwa sina mtu. Siwezi kuweka mafahari wawili kwenya zizi moja. Na kumuacha Shani ni kitu kisichowezekana kwakua ananionyesha mapenzi zaidi ya niliyowahi kufikiria mapenzi kuwa hivyo. Maamuzi yangu ni kwamba. Kuanzia leo sahau kuwa na mimi ni mpenzi wako…. Niwie radhi kwa hili.”
Aliongea Jothan huku machozi yakimlenga lenga. Hakika ni uamuzi mgumu aliouchukua kwakua aliamini ilikuwa ni mtihani mkubwa katika mapokezi ya mlengwa. Alipoinua macho yake kumtazama Prisca, tayari mashavu ya prisca yalishalowana kwa machozi huku macho yakiwa mekundu. Kilio cha kwiki kilianza kusikika na kumfanya Jothan kuingiwa na imani baada ya kumtaza mpenzi wake huyo anaye amua kumuacha bila kosa lolote.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment