Search This Blog

Wednesday, 1 June 2022

MAWIO NA MACHWEO - 5

 







    Simulizi : Mawio Na Machweo

    Sehemu Ya Tano (5)







    Maisha ya kibiashara yana mambo mengi sana ,hasa haya ya biashara za ushindani.Nasema haya kwa sababu,yule mshindani mwenzako aonapo unamzidi,huanza kutafuta njia za kukupoteza.Na ndivyo ilivyotokea.



    Wakati biashara yetu inazidi kunoga,ndipo Chris aliamua kujitoa kwenye kampuni yetu kwa kisingizio kuwa amechoka na anataka kustaafu.

    Tulimbembeleza lakini ilishindikana kutokana na msimamo wake katika hilo.Na zaidi alitaka share yake yote kama mkataba ulivyoandika.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tulikuwa hatuna jinsi zaidi ya kufanya atakavyo na hatimaye Chris aliondoka kundini huku akitaka pia na herufi za jina lake liondoke kwenye jina la kampuni yetu.



    Tukakaa kwa muda wa wiki moja tukijadiliana suala hilo.Share aliyochukua Chris ilikuwa ni kubwa sana,hivyo ilitubidi tupunguze wafanyakazi kwa muda ili turudishe hali ya kampuni.

    Baada ya kufanya hivyo,tulibadili jina la kampuni na kuitwa S and M Limited Company.Huku M ikichukua majina ya Mrwanda,Masai na Mendrovic na S ikimaanisha Solomon,Silvia na Saint.Kampuni ikaanza mwanzo kutoa huduma zake.

    ******************



    Sikuacha kumtembelea Mzee Said Soji.Na kuondoka kwa Chris,kulinijaza maswali kidogo,hivyo niliona ni bora nikamwone Mzee yule ambaye sasa umri ulikuwa unamtupa mkono.



    Nilipofika kwake alinipa chakula lakini nilikuwa sikitilii maanani zaidi ya kukichomachoma tu na kijiko. Ni kama alikuwa kichwani kwangu,kwani alioona hali ile,alianza kuongea maneno yake ya busara huku akianza kwa kunipa pole kwa kilichotokea katika kampuni yetu.



    “Kijana najua una matatizo sana na huko uelekeapo ndipo matatizo hasa yanapotokea.Yaani jinsi uendavyo mbele,na ndivyo uyakaribiapo matatizo.Cha msingi sasa hivi ni kukaa na kuangalia maisha yako tu!.

    Binaadam hata uumpe nini haridhiki,atatafuta njia na kuipata ili akuache wewe.Na ndivyo ilivyotokea kwako na kwa Chris.Umempa upendo mkubwa sana lakini bado akakuacha soremba. Sasa wapo wana mpango wa kuunda kampuni mpya,yeye na Mendrovic”.Alipofika hapo aliniangalia jinsi nilivyokuwa na mshangao usoni pangu hasa baada ya kusikia yale.

    “Ndio hivyo kijana,Chris amejiunga na Mendrovic Company.Cha msingi wewe angalia njia zako.Na najua lazima wataanzisha biashara inayofanana na yako ili mshindane,hapo sasa ndipo itagundulika ipi ni mdio na ipi ni hapana”.Mzee Said alizidi kluongea na kunifanya mimi nibaki bila neno zaidi ya kutafuna lips zangu kwa hasira.

    Niliondoka pale kwa mzee yule baada ya maongezi mengi sana yaliyonifanya nijengeke upya kifikra na kujipanga kwa ajili ya ujio wa Chris.

    ***********



    Kama nilivyotegemea,baada ya wiki moja,Chris akatangaza ujio wake mpya akiwa na Mendro Company.

    Chris alijiunga na kampuni ya Mjomba wa Miriam na shughuli walizoanza,zilikuwa hazina tofauti na za kwetu.

    Wafanyakazi wa kampuni yetu walishangaa sana lakini mimi wala sikuwa na mshangao kwani nilishajua ni nini kitakachojiri.



    Kwa mara ya kwanza,Chris akazalisha uadui kati yetu.Akawa ni mtu wa kuisakama kampuni yetu huku akiwa mstari wa mbele kutukana wafanyakazi wetu muhimu katika vyombo vya habari.

    Siku zote mwenye akili hukaa kimya na kumuacha mjinga ajiongeleshe mbele ya watu hadi akome.

    Kifupi sisi tulimuangalia na kumwona limbukeni tu!.



    Simu zetu akawa hapokei na hata akipokea anasingizia kuwa yupo mahala au yupo bize sana na maisha.Na alipoona tunazidi kumsumbua,aliamua kubadili namba zake ili asisikie kabisa mlio wa simu yake ukiita namba zetu.

    ************



    Biashara ikawa ushindani zaidi kuliko pale mwanzo.Chris akiwa ameondoka na mikakati yetu,aliifanya kampuni yake mpya aliyoitwa Mendro and Jengo Company Limited kuwa juu kupita maelezo.

    Bidhaa walizozitoa zilikuwa hazina tofauti na zetu hata kidogo.Na wao walikuja kasi zaidi kwa kuzipunguza bidhaa hizo bei na kufanya wananchi wengi waamie kwao.Hapo hali ikazidi kuwa mbaya kwetu na kuna baadhi ya wafanyakazi wasiyo na moyo wa uvumilivu waliamia kwa Chris na kuiweka kampuni ile juu zaidi,kutokana na kuondoka na njia zetu za kukuza biashara.



    Baada ya hali hiyo,tulikaa chini tena na kuanza kufikiria njia za kupambani ili kujikwamua na ushindani huo ulioletwa na kampuni ya Chris pamoja na Mjomba wa Miriam.n Hapo ndipo ulikuja muda wa kutumia elimu yetu.



    Mwenye elimu ya masoko aliongea mengi sana kuhusu kutafuta masoko duniani.Na mwenye elimu ya teknolojia,naye aliongea mengi kuhusu kutafuta masoko kwa kwa kutumia teknolojia zinazotuzunguka kwa muda ule.



    Hapo likaja wazo la kuanzisha mitandao ya kijamii ambayo ingehusisha zaidi mambo ya kibiashara na sisi kujitangaza katika hilo.Htukuishia hapo,tukaenda na kutafuta makampuni ambayo tungewekeza bidhaa zetu.



    Huko tulikutana na kampuni moja kutoka China,nayo iliingia ubia na kuanza kulitumia jina na lebo yetu kutengenezea bidhaa ambazo zilikuwa ni vitu vya ndani kama radio,luninga,pasi,vyombo na vitu vya namna hiyo.

    Hatukuishia hapo,tukaenda mbali zaidi na kuanzisha vituo vya matangazo kama radio na luninga,zote zikiwa na alama yetu.Pia mashule na hoteli kubwa hapa mjini,zilianzishwa kwa nguvu zetu sisi.

    *************

    Hatimaye kampuni ikarudi katika hali yakebaada kuwa katika kipindi cha mpito kilichodumu kwa miaka miwili.

    Ile kampuni ya akina Chris,ikarudi chini kwa kuwa waliishiwa njia ambazo zingewafanya washindane na sisi.Hapo sasa ikawa ndio tafrani na majanga.

    Tukawa tunawindwa kwa ndege au wanyama wa porini.Chris akawa nyoka kabisa,nyoka mwenye sumu kali.Kila mara akawa anataka kushuhudia tunalia,lakini ya MUNGU ni mengi na siku zote tulimwachia yeye.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***********

    Kila mmoja wa kampuni yetu,aliweza kuanzisha biashara zake binafsi na vitega uchumi mbalimbali.Nami kwa kuwa nilikuwa ni mpenzi sana wa kuwekeza,niliamua kufungua kituo cha kurekodia muziki au studio,na niliandikisha jina la kaka yangu ambaye alikuwa ana uwezo mkubwa sana wa kutengeneza mapigo ya muziki.

    Hapo nilifanikiwa sana na wazo hilo,na hata wasanii wa pale nyumbani,walikuja na unishukuru sana kwa hilo.

    **********

    Siku moja wakati tunashuka katika gari letu lile la kampuni,tukiwa tumetoka kwenye kikao cha biashara. Kwa mbele yetu ilitokea gari moja nyeusi,na kisha walishuka watu watatu nakuanza kutufyatulia risasi zisizo na idadi,jambo lililofanya umati wa watu kupiga kelele na kukimbia hovyo hovyo kama kundi la mbogo lililoona simba.

    Baada ya shambulio lile kutulia na watu wale kuondoka,ndipo na mimi nilinyanyuka pale nilipokuwa nimelala na kuwaangalia wenzangu.Wengi wao walikuwa salama lakini kwa upande Solomon alikuwa analia sana huku kaweka kichwa cha Silvia katika mapaja yake. Shati jeupe alilovaa Solomon,lilikuwa limelowa damu ya Silvia. Nilipoangalia vizuri,niligundua kuwa Silvia alikuwa kapigwa risasi tatu za kifuani,na pale alivyokuwa anaonekana alikuwa anapambana na mtoa roho huku akijaribu kumuhasa Solomon.





    “So…So…So….Soolo”.Silvia alikuwa akimuita Solomon kwa shida sana huku akipumua kwa kasi,jambo lililofanya mahala pale pazidi kujaa damu zilizokuwa zinavuja kutoka kifuani kwake.

    “Please,usiongee Sily,nakuomba usiongee”.Solomon alikuwa anamwambia Silvia huku akizidi kulia kwa uchungu. Wakati huo wale wafanyakazi wengine tuliyokuwa nao walikuwa wanaangaika kutoa taarifa polisi na hospitali.

    “Niache niongee Solo kwani nisipoongea hutonisikia tena kusikia nilichokusudia kukwambia”.Solomon akawa mpole na kuanza kumsikiliza Silvia maneno aliyokuwa anayaongea ambayo yalimtoka kwa shida sana. Bado niliendelea kuwaangalia huku machungu na jazba zikiwa zimenijaa kiasi cha kushindwa kufanya chochote kwa muda ule.

    “Solo,natangulia mume wangu. Naomba ukae na watoto wetu vizuri,nakuomba sana”.Silvia alianza kumpa wosia huo Solomon ambaye alimkatisha na kuanza kumkemea kwa maneno aliyokuwa anayaongea.

    “Embu nyamaza Sily. Wewe ni jasiri bwana.Kama uliweza kupambana na mengi ya nyuma,basi naomba upambane na hili japo kidogo,nakuomba Sily,nataka hawa watoto tulee wote,nakuomba”.Solomon alijikuta akiongea huku machozi yakizidi kum-miminika toka kwenye macho yake.

    “Nakubali Solo kuwa nimepambana na mengi,ila hili siwezi pambana nalo. Natangulia mme wangu kipenzi. Usimfanye kitu chochote anayehusika na haya,na ninakuomba usiwe kama Chris,usimuache Frank. Frank ndiyo nguzo iliyokukamata wewe,kama ukimuacha na yeye hatokuwa hana sifa ya kuitwa nguzo muhimu,kwa sababu kile alichokikamta kimeondoka. Nasema kamwe usimuache Frank atetereke peke yake,huyo ndiyo kila kwetu.

    Nakupe….pe…pe…eeeenda sa…aaaana So…oooo”.Kimya cha sekunde therathini kikatawala baada ya maneno hayo.Baada ya kimya hicho,kilichofuata ni yowe kubwa kutoka kwa Solomon akimlilia Silvia huku akiponda ponda vioo vilivyokuwa vimetapakaa pale chini. Ilikuwa ni uchungu mkubwa na machungu yaliongezeka baada ya madaktari kuja na kuthibitisha kuwa Silvia ameshaaga dunia.

    Ni machozi pekee ndiyo yalitawala kwa muda ule. Kwa upande wangu sikusita kukumbuka maneno ya utani aliyokuwa ananitania Silvia hasa siku ile nilipowapelekea taarifa kwa kuwaambia kuwa nampenda Miriam.

    Pia sikusahau pale alipokuwa anajitolea mfano wa mapenzi yake na Solomon,ambapo baada ya kutoa mfano huo alimgeukia na kumbusu. Sasa Silvia hakuwa na sisi tena.Utani wake hatuwezi kuuona tena,tabasamu lake nalo hatutaliona tena,ukweli alikuwa kaacha pengo kubwa kuanzia kwenye familia yake na kazini tulipokuwa tunafanya naye kazi.



    Baada ya mazishi,polisi walileta taarifa kuwa kifo cha Silvia kinahusiana na baadhi ya wapinzani wetu wa kibiashara hapa duniani,na moja kwa moja,mlengwa alikuwa ni Chris,ambaye hata msibani hakuonekana kabisa.Solomon hakutaka taarifa zaidi kuhusu mauaji ya Silvia.Hivyo aliomba kesi hiyo iachwe huku akiamini ilikuwa ni kazi ya MUNGU.Kesi ikazimwa na maisha mapya ya upweke kwa Solomon yakashika nafasi yake,huku faraja kubwa ikiwa kwa wanae wawili ambao wote walikuwa wa kike.

    Baada ya siku nne,ndipo Chris alikuja kwetu na kutupa pole, huku akisingizia kuwa hakuwepo nchini wakati hayo yote yanatokea. Akionesha hali ya uchungu na kuumia kwa sababu ya kifo cha Silvia,alienda hadi kwenye nyumba aliyopumzishwa Sily na kuweka mashada ya maua huku akionesha wazi kuwa kaumia na kifo kile.

    ***************

    Maisha yakaendelea na biashara nayo ikachukua nafasi yake japo Solomon alikuwa kaathirika sana baada ya kifo cha mkewe Silvia,hivyo hata ufanisi wake pale kazini ukapungua,jambo lililofanya Miriam ashike wadhifa wake kwa muda ili arudishe hali yake. Miriam akachukua nafasi ya umeneja wa uajasiriamali ambao alikuwa kaushikilia Solomon,na kitendo bila kuchelewa,akaanza kazi rasmi. Wakati huo nafasi ya Silvia ilichukuliwa na mfanyakazi mwingine ambaye tulimuamini sana hasa kwa taaluma aliyokuwa nayo.

    ************

    Japo Miriam alikuwa anafanya kazi kwetu,lakini muda mwingi sana alikuwa anaenda kwa mjomba wake na kukaa huko. Sikujua ni kwa nini na wala sikuwa na haja ya kumuuliza sana kwa sababu ile ndiyo familia yake.

    Mapenzi yetu hayakuwa nyuma hata kidogo. Yalizidi kupamba moto hadi watu wakawa wanaomba tufunge ndoa,lakini majibu tuliyokuwa tunawapa,yalikuwa ni kama kuwapa moyo tu!.Ndoa yaitaji moyo,ndoa yaitaji kujipanga wakati wa kuingia humo.Hayo ni mambo ya kuyasawazisha kabla ujachukua uamuzi wa kufunga ndoa.



    Kuna siku aliamua kuamia kwangu na kukaa kwa mwezi mmoja. Ndani ya mwezi huo tulifanya mengi kibiashara na kimaisha pia. Kila mara tulikuwa pamoja kama makinda ya njiwa,na kila mara alikuwa ni mtu wa kunihasa kuhusu maisha na siku ambayo yeye atadondoka. Mara nyingi niliuliza ana maana gani kuhusu maneno hayo,lakini hakunijibu hadi pale siku moja usiku ambapo ndio ilikuwa siku yake ya mwisho kukaa na mimi,alipofungua kinywa chake na kuanza kuongea maana ya maneno yake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alianza kwa kusema kuwa ananipenda sana,na kamwe asingependa kuona nateseka kwa ajili yake. Na mimi niliposikia maneno hayo nilimjibu kwa kumwambia kuwa nampenda sana pia. Nikiwa nadhani kamaliza maneno yake,nilishuhudia akinyanyuka pale kitandani na kukaa kwa ajili ya kuendelea kuongea.

    “Frank,natambua kuwa biashara yetu ni kubwa sana hapa nchini na duniani kwa ujumla. Biashara hii imetupa mali pamoja na umaarufu mkubwa sana duniani. Licha ya kutupa hayo yote,lakini biashara hii imetengeneza maadui wengi sana katika maisha yetu. Yule rafiki tuliyemtegemea kama rafiki,leo hii kageuka na kuwa adui anayetuwinda kama swala na chui wakiwa mbugani”.Akakaa kimya kidogo kama anafikilia jambo na kisha akatanua kinywa chake na kuendelea kuongea aliyokusudia.

    “Frank nataka utambue ni kiasi gani unawindwa hapa nchini kwenu. Wanajaribu kukuua lakini bahati inakuwa si yao. Kifo cha Silvia,kilikuwa kimekulenga wewe. Halikuwa kusudio lao kumuondoa Silvia duniani. Sily kaondoka badala yako Frank”.Hadi hapo nilikuwa kimya huku donge la mate linalowakilisha hasira,likiwa limenikaba kooni kama kiazi.

    “Lakini mama yangu,hayo yote wewe umeyajuaje?”.Nilimuuliza swali kwa upole angali nilikuwa najua ni nini alichomaanisha.

    “Kitendo cha wewe kuwa na mimi kila mahali,ndicho kinarefusha uhai wako. Wanaogopa sana kufyatua risasi kwa kuhofia wataniua na mimi. Mjomba wangu,mtoto wake na rafiki yako uliyekuwa unamuamini,kila siku wanakuwinda kwa bunduki na mabomu”.Miriam aliendelea kupasua jipu kuhusu ndugu zake hao,lakini ni kama alikuwa ananikumbusha tu! Mimi nilishayafahamu hayo muda mrefu sana.

    “Lakini kwani tumewafanya nini? Huu si ushindani wa kibiashara tu?Kwa nini wafanye hayo sasa!”Nilizidi kuuliza kama sijui kilichonyuma ya pazia.

    “Frank,kama nilivyowahi kukwambia hapo mwanzo kuwa yule mtoto wa mjomba aitwaye Yuri,alikuwa anataka anioe,baada ya kumkataa ndiyo ikawa chanzo za kuanzisha uhasama na wewe. Na uhasama huo ulikuwa mkubwa zaidi baada ya mimi kuhamia kwenye kampuni yenu. Na kwa kuwa Chris naye alikuwa ananitaka tangu zamani,basi naye akaona ni vema aamie kule ili iwe rahisi kunilaghai”.Miriam aliongea mambo yote ambayo aliyajua lakini lililonigusa ni hilo la Chris.

    “Ina maana Chris alikuwa anakusumbua hadi muda ule anahama!?”Niliuliza kwa hamaki.

    “Ndiyo Dadie. Lakini niliogopa kukwambia kwa sababu ya urafiki wenu,niliona kama nitawatenganisha na ndio maana nikaamua kukaa kimya”.Nilishindwa kuendelea kumuuliza Miriam baada ya majibu yake kwa maana ningefanya hivyo,hasira hata juu yake zingemfikia. Ni ujinga mkubwa sana kumficha jambo mpenzi wako mliyefanya mengi na zaidi mnatambulika hadi kwa wazazi wenu. Si vizuri kitu hicho wapenzi wasomaji wa hadithi hii.

    Hakuna jambo linalouma kama rafiki yako uliyedhani ni wa karibu kukufanyia matendo ya kifedhuri kama alivyofanya Chris. Kwa tabia aliyoifanya,nilijikuta namchukia mara zaidi ya mia kuliko hapo mwanzo.

    “Dadie. Usichukie kwa nilichokufanyia,ilikuwa ni lazima nifanye hivyo ili niokoe urafiki wenu. Nakuomba Frank,Dadie wangu,usichukie mpenzi wangu”.Miriam alijaribu kunitoa katika hasira zile kwa kunibebeleza huku akisugua sugua kifua changu.

    Nilikubaliana naye na kumuomba tulale kwa ajili ya kesho ambayo alitakiwa kurudi kwa mjomba wake alipokuwa anaishi. Baada ya hapo kilichofuata,ni kukumbatiana kwa kumbate ambalo nadhani ndilo lilikuwa kumbate la faraja kwangu. Licha ya kuwa la faraja,pia ndilo lilikuwa kumbate la mwisho katika safari yetu ya mapenzi mimi na Miriam tukiwa wazima na wenye viungo vyote.

    *************

    Kesho yake alirudi kwao na mimi kama kawaida nikaelekea kazini ambapo kwa wakati huo,Solomon alikuwa karudi katika hali yake ya mwanzo,hivyo kile kiti alichoshikiwa na Miriam,tayari alishakikalia tena. Sikutaka kuwaambia maneno aliyoniambia Miriam,lakini kila muda nilikuwa nawahasa sana wafanyakazi wenzangu kuhusu kuwindwa na makampuni mengine.

    Zaganda na Saint,wao waliendelea na kazi zao siku zote za maisha yao,walikuwa hawana wapenzi wala watoto.Bado waliamini kuwa wao ni vijana na wakati umri ulizidi kwenda.

    Nao sikuwa nyuma kuwaambia watafute watu ambao wangekuwa ni wapenzi wao,lakini kila muda walikuwa wananikatalia huku wakiniambia kuwa bado wanahitaji kula maisha yao.

    *************

    Ikapita wiki bila kumuona Miriam akija pale kazini. Wafanyakazi wenzangu maswali yote wakanitupia mimi. Na mimi sikuwa na jibu,kwani hata pale nilipopiga simu yake,ilikuwa haipatikani na nilipojaribu kumtumia barua pepe,nazo zilikuwa vivyo hivyo.

    Ukimya huo ukatimiza wiki ya pili.Hapo sasa kama kupenda ndipo niliamini kuwa napenda. Nikaanza kuteseka kwa fikra za kumfikiria Miriam,nilijiuliza mara kadha wa kadha kuhusu Miriam lakini sikupata jibu. Nilienda hadi kwa Mzee yule Mlinzi ambaye nilipenda sana kumtembelea nikipata muda.Alikuwa kazeeka sana mara ya mwisho nilipomtembelea,miaka sitini aliyokuwa kaimeza,ilitosha kabisa kumuita babu.Huyo ni Mzee Said Soji,baba wa mlinzi wa Mjomba wa Miriam,Mustapha Said Soji au Muphty.

    Nilikuwa najua mzee yule atakuwa na taarifa za Miriam alipoenda, kwa sababu mtoto wake alikuwa mara nyingi akimpa matukio yote yanayoendelea katika familia ile.

    MUNGU naye ana makusudi yake. Nilipofika maeneo anapoishi mzee yule,nilipata taaarifa kuwa kishakufa. Alifariki miezi miwili iliyopita kwa kupigwa risasi na watu wasiyojulikana. Hadi wanamaliza kuniambia,tayari nilishakata tamaa ya kumpata mwanamke wa moyo wangu,mwanamke ambaye alinifanya nisahau machungu ya nyuma. Miriam,ndiyo jina ambalo nililitamka baada ya kupanda gari langu na kuanza kupotea eneo lile.



    Nikakaa mwezi mzima bila kuonana na Miriam. Ule uwoga wa kwenda kwao kumuulizia,nikautoa na kuvaa ujasiri na kisha moja kwa moja nikaenda hadi kwa mjomba wake ambaye aliposikia kuwa namtafuta Miriam,alinifukuza kama mbwa pale kwake,na mbaya zaidi hata baba yake Miriam alikuwa hajibu ujumbe nazomtumia.

    Kama mapenzi hujui ni kiasi gani yanaumiza,basi ni muda huo ndiyo niliamini kuwa yanaumiza,tena yanaumiza kuliko yale ya mwanzo. Nilijikuta nayapambanisha maumivu ya My Rose na ya Miriam na nilichokuja kukigundua ni maumivu yote mawili kunitafuna. Sura ya Rose ilikuja usoni mwangu na kuniambia nisije kuwanyanyasa wanawake katika maisha yangu,na niuache moyo wangu upende tena. Kamwe nisije kusema kuwa siwezi penda tena.

    Mara baada ya sura na maneno ya Rose kupita.Ikaja sura ya Miriam,mwanamke ambaye nilimfungulia moyo wangu tena kama Rose alivyotaka. Nikampenda kwa moyo wote,nikamthamini kwa akili yangu yote,na nikamjali katika maisha yangu yote. Lakini sasa alikuwa hayupo na mimi tena,hata nikimpigia simu zangu hapokei wala kupatikana,barua pepe hazijibu,mawasiliano yote unayoyajua,yalikuwa hayafanikiwi kumpata Miriam.

    “Aaagh”.Nilijikuta napiga ukelele mkubwa na kurusha chupa iliyokuwa ina wiski,na moja kwa moja ikaenda kugonga kioo cha luninga iliyokuwamo sebuleni kwangu.

    Tayari mapenzi yalishanirudisha katika hali ya ulevi wa vinywaji vikali.Ulevi ambao niliapa kuwa sitakuja kuufanya katika maisha yangu. Lakini nitafanya nini? Na sheria zimewekwa ili zivunjwe.



    Akili na maisha yangu yakatawaliwa na vilevi. Wakina Solomon,Saint na Zaganda walijaribu kunishauri lakini ilikuwa ni kama mbuzi anapigiwa gitaa au wanajaza pipa kwa kisoda.



    Pombe ikawa pombe kwenye maisha yangu,hiyo yote niliamini ni njia ya kumsahau Miriam na sura ya Rose ambayo iliendelea kunitafuna fikra zangu kila kukicha.

    Kazi nayo ikazidi kudoda.Ofisini bila mimi,siyo ofisi,ni Solomon pekee ndiye alikuwa ana moyo wa kuwahamasisha wafanyakazi wengine waendelee kufanya kazi.

    Hali ikawa mbaya sana pale kazini,na ikawa mbaya zaidi baada ya kusikia kuwa Zaganda na Saint wamedai asilimia zao ishirini na tano kwa kila mmoja,na baada ya kuzipata wakaenda kuanzisha biashara zao. Hawakuishia hapo,wakachukua wafanyakazi muhimu wa ile kampuni na kuondoka nao kwa ajili ya kampuni yao.

    Hapo na mimi ndiyo hasira zikazidi na kama pombe,ndiyo zikawa pombe. Kila kukicha nilikuwa mtu wa vilevi vikali. Kampuni ikabaki chini ya Solomon ambaye kamwe hakutaka kuvunja ahadi ya Mkewe Silvia aliyompa kabla hajaaga dunia,lakini endapo Solomon angesipopata maneno yale kutoka kwa Silvia,basi na yeye angeondoka,nailikuwa ni harali yake kuondoka kwa sababu tabia niliyokuwa nimeianza,ilikuwa ni mbaya sana.

    Wale waliyokuwa wameingia ubia na kampuni yetu,nao mara moja walijiengua baada ya kupata taarifa ya matendo yangu mtaani na kazini.

    Hayo yote yalitukia ndani ya miezi minne tu!ya kutumuona Miriam.Kutomuona kwangu Miriam ndiyo lilibadili hayo yote.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kama hujui nguvu za mapenzi zinavyotesa,basi hayo uyasomayo ndiyo hasa mateso nayozungumzia. Kampuni ikashuka ubora,huku wakina Chris na kampuni yao,wakipanda kwa mbwembwe nyingi. Biashara waliyoanzisha wakina Saint na Zaganda,ilikuwa ni tofauti kabisa na ile ya mwanzo ya kampuni yetu,hivyo wala haikuleta upinzani kwa akina Chris japo ilikuwa ni kubwa.



    Kilichokuwa na mwanzo,huwa hakikosi kuwa na mwisho. Na sasa mwisho wetu nadhani ulikaribia. Hila na chokochoko za watu,zikatupeleka mahakamani kwa kosa la kuuza bidhaa za magendo na madawa ya kulevya. Serikali ndiyo hasa ilikuwa imetushitaki na vithibitisho vyote ilikuwa navyo. Madereva wetu pamoja na wafanyakazi wetu muhimu,ndiyo walikuwa wa kwanza kutoa uthibitisho huo.

    Walitushitaki kwa kusema kuwa wamekamata pembe za ndovu,ngozi za wanyama wa mwituni pamoja na hizo dawa za kulevya. Kwa ujumla kesi ilikuwa kubwa ambayo hatukuweza kuihimili kutokana na kukosa ushahidi wa kutosha.Hivyo kesi ile ilitushinda.

    Serikali iliamua kutuachia huru lakini walitupora hati zote za kusafiria,pamoja na zile za biashara tulizokuwa tumeanzisha.Yaani kwa kifupi waliamua kutufirisi hadi kilichobenki wakakiweka mikononi mwao. Umasikini kwa muda mfupi ukagonga hodi katika maisha yetu. Majumba,shule,mahotel na vituo vyote vya redio na luninga,wakachukua wao. Kila biashara ambayo tulimiliki kwa majina yetu,walichukua wao.



    Hapo ndipo nilitamani zaidi nipate lile kumbate la faraja kutoka kwa Miriam,lakini sikuweza kulipata kutokana na kupotea kwake. Sikujua hali ya Miriam,na wala sikufahamu yu wapi mpenzi wangu yule

    Na hapo ndipo niliamishia ulevi wangu wote kwenye pombe za kienyeji. Nikawa mlevi kupindukia,jambo ambalo lilifanya wazazi wangu kila siku kutoa machozi ya maumivu juu yangu.

    **************

    Ni siku moja ambayo Solomon alikuja na watoto wake kunililia kwa nifanyayo. Maneno yale yaliniingia kiasi kwamba nilishindwa hata nianzie wapi kuomba msamaha kwa yale yote niliyokuwa nimeyafanya. Solomon akiwa na wanawe alikuja hadi napoishi na kuanza kuniambia maneno haya.

    “Masai. Umekuwa na roho ndogo sana mdogo wangu. Embu ona mimi navyoteseka na hawa watoto. Angalia mwenyewe. Watoto walishazoea magari kwenda wanapotaka,leo hii nakuja nao kwa miguu hata maji ya kunywa ya kuwapa sina. Angalia mavazi yao wanayoyavaa,hawa ndiyo wanangu kweli Masai? Kwa nini unafanya haya?Sina ndugu mimi hapa mjini zaidi yako wewe,lakini wewe umeniacha nikihangaika na wanangu. Hivi mimi ningeamua kufanya haya uyafanyayo sasa hivi baada ya kifo cha Silvia,kweli ungefurahi? Kwa nini Masai,kwa nini nakuuliza?Nijibu Masai”.Kufika hapo Solomon alikuwa kapandwa na jazba hadi akanikwida shati langu ambalo sijui hata ni lini nililivaa.

    “Acha ujinga Masai.Huo ni utoto,ni utoto kabisa. Wewe mtu wako kapotea tu! Na ni kawaida yake tangu yupo chuoni,alikuwa anaweza kupotea hata mwezi mzima bila kuja chuo,ila baadae alirudi.Wewe hata huoni hilo,huna hata subira ya kusubiria aje. Unakunywa mapombe kila kukicha,pombe zenyewe siyo salama kwa afya yako. Wewe ni mtu gani Masai? Wewe wako kaondoka tu kwa muda,unakunywa mipombe hivyo,je mimi aliyeondoka daima katika upeo wa macho yangu,unataka nile mavi?Au unataka nifanyaje sasa. Nijiue? Hawa watoto watalelewa na nani?Acha upumbavu Masai.

    Wewe ni mpumbavu sana Masai,tena ni pumbavu la kwanza ambalo sijawahi kuliona dunia hii. Pumbavu lenye kipaji cha kuimba na kuandika maishairi,kucheza na mambo mengi ya kisanii,lakini linashindwa kutumia vipaji hivyo hata kutafuta senti za kuwapa wazazi wake. Mimi nina miaka arobaini na kenda sasa,unataka nifanye kazi gani ambayo itawafanya hawa watoto wale vyakula vinavyofaa?

    Hilo nalo huoni na wakati wewe una miaka therathini sijui na ngapi,bado kijana kabisa. Unashindwa hata kufanya chochote kwa ajili ya hawa watoto?Mbona mchoyo sana wewe Masai?Eeh! Mbona mchoyo wewe mtu? Ni mtu wa aina gani wewe?Kampuni imeteketea kwa ajili ya upuuzi wako,hilo hata huoni? Marafiki wote wametukimbia,hawataki hata kupokea simu zetu. Hilo nalo kwako hata halikuingii?”.Solomon alizidi kunipaka maneno ambayo kwangu yaliingia vizuri sana na kukaa sawa kwenye fikra zangu.

    Niliwaangalia watoto wale wawili wa Solomon na nilijikuta nalia na kuwafuata kisha nikawakumbatia huku nawaomba sana msamaha. Nililia sana siku ile,naweza kusema kilio kile kiliamsha ari mpya mwilini mwangu.Solomon alinihasa sana na kuniambia sasa ni wakati wa kuzoea maisha bila mapenzi na ya kula milo sita kwa siku.

    Nilimuahidi Solomon kuwasaidia kwa kila hali watoto wake ili warudi shule waliyoanza.Na kwa kumuonesha hilo,niliamua kuwachukua watoto wale na kuishi nao pale nyumbani kwetu,huku msaada mkubwa ukiwa kwa ndugu na wazazi wangu. Maisha yakarudi kama zamani,nikabadilika kitabia na sasa nikaamua kujiunga na ile studio niliyomfungulia kaka yangu. Ile haikuchukuliwa kwa sababu ilikuwa imeandikishwa jina lingine. Hivyo na mimi nikawa ndani ya studio hiyo.



    Ilikuwa kama utani pale nilipoingia na kuanza kujifunza kupiga mapigo ya muziki. Mara ghafla wasanii mbalimbali wakawa wanakuja pale na kufanya kazi na sisi. Na mimi hapo hapo nikaongeza bidii ya kuzidi kujifunza kupiga muziki huo wa Bongo Flava,na hatimaye nikawa mtaalamu wa mambo hayo. Haikuchukua muda sana,tukaanza kufahamika pale Dodoma,na baada ya kufahamika pale,jina letu likatoka na kuelekea Dar es Salaam. Hapo napo wasanii wakubwa kutoka mkoa ule,wakaanza kuja na kufanya kazi katika studio yetu. Jina likakua ghafla karibu Tanzania nzima.

    Kazi ile kiasi fulani ilibadilisha maisha yangu na ya Solomon akiwa na familia yake. Kaka yangu,ambaye alikuwa nguzo muhimu sana katika studio ile,kila siku alikuwa anabuni mapigo mapya ambayo yaliifanya studio yetu izidi kung’ara.



    Siku moja tukiwa mle studio,wakati huo kulikuwa hakuna wasanii waliokuja. Kaka yangu alikuwa anatengeneza mapigo ya muziki ambayo yalinivutia sana. Wakati anafanya hayo na mimi nikaanza kuyafuata mapigo yale huku nikiwa namuimba Miriam.Nilianza kulitaja jina lake na baadae nikaanza kuelezea maisha yetu tangu tulipokutana hadi aliponipotea. Ilikuwa ni mistari ambayo ilitengeneza hadithi ya mapenzi moja tamu sana. Kaka yangu alivutiwa sana na ile kitu,hivyo alinishauri kuandika na kukariri halafu niyarekodi mashairi yale.

    Nikafuata ushauri,na baada ya wiki moja,nikaingia studio na kurekodi mashairi niliyotunga. Wimbo niliuita Miriam. Ni wimbo ambao kwa muda mfupi uliotoka,ukapanda chati Tanzania nzima. Ulikuwa katika mahadhi tulivu lakini kwa mtindo wa kufoka foka,mtindo ambao hapa Tanzania washabiki hawaukubali sana kama ukiimba,lakini kwa upande wangu,nilikubalika vizuri sana.

    Huo ndio ukawa mwanzo wa usanii wangu. Nikapata na wazo la kufanya albamu nzima ambayo nilipanga kueleza kila kitu kilichotokea maishani mwangu. Na wazo hilo bila kupingwa,likapitishwa na kila mtu ambaye nilimpa malengo yangu kasoro wazazi wangu ambao waliniomba sana nisianze kuwachokoza wale waliotufirisi.Hilo mimi nililipinga na nilikuwa tayari kwa lolote katika maisha yangu.

    Kitendo bila kuchelewa,nikaingia kazini na kazi ikaanza ya kutunga mashairi na kuyakariri.



    Baada ya miezi mitatu,nikawa nimemaliza kazi ya kuandika maishairi na ya kuyakariri kabisa. Kazi iliyofuata ni kuanza kuingiza sauti katika mapigo ya muziki ambayo kaka yangu ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa kufanya hayo yote. Na kwa kiasi kikubwa tulifanikiwa kurekodi na kutengeneza albamu ambayo tuliita NYUMA YA PAZIA.

    Ni albamu pekee hapa Tanzania kuwahi kuwa na nyimbo nyingi zenye kusisimua. Albamu ilikuwa na nyimbo kumi na tano ambazo zote zilikuwa katika mtindo wa kufoka foka kiugumu (HARDCORE HIP HOP),mtindo huo ulikuwa ni wa kigumu kwa sababu ulikuwa hauogopi chochote wakati unautumika,kwa kifupi nilifichua mengi sana kuhusu maisha yangu na ile kampuni pinzani.

    Albamu ilipotoka kila mtu alipata nakala yake na kila mtu aliielezea jinsi alivyoona. Nyimbo zile kumi na tano zikabadilisha fikra za watu wengi ambazo zilikuwa zimepandikizwa vichwani mwao.

    Kuna wimbo kama SIYO KWELI. Huo ulielezea mambo yote waliyoyasema juu yetu hadi tukafirisiwa kuwa siyo ya kweli.Ni wimbo ambao ulichukua nafasi kubwa sana kwenye vituo vya redio na baadae tukatolea na video.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wimbo mwingine niliuita TUNAWAJUA.Wimbo huo ulisema wazi kuwa wale waliyotupa ile kesi tunawajua,huku ndani ya wimbo nikitumia baadhi ya maneno aliyoniambia Miriam ile siku ya mwisho wakati nipo naye. Katika wimbo huo niliwataja mjomba wa Miriam pamoja na Yuri mtoto wake.

    Wimbo mwingine,niliuita RAFIKI MSALITI.Wimbo huo ulikuwa moja kwa moja kwa Chris ambaye alisaliti biashara yetu kwa sababu ya fedha na mwanamke.

    BADALA YANGU,huo ukawa wimbo mwingine ulioelezea kifo cha Silvia. Wimbo huo nilisema kuwa kile kifo cha Silvia kilikuwa ni changu,lakini badala yake akaenda yeye. Nakumbuka baada Solomon kusikia hayo,naye akaniambia kuwa kila siku Chris anampigia simu ili ajiunge naye na awe tajiri kama zamani. Maneno hayo ya Solomon,yakatengeneza wimbo mwingine uitwao HUPATI KITU,ambapo humo na Solomon aliweza kuingiza sauti yake nzito na kuufanya ule wimbo kupendeza. Na ndiyo wimbo pekee niliyomshirikisha mtu mwingine.

    Wimbo mwingine ambao tuliupeleka hadi redioni kwa ajili ya kupata kupigwa,uliitwa KUNA NINI PALE?.Wimbo huo ulikuwa unauliza kuhusu lile ghorofa tulilokuwa tunasomea kuwa kuna biashara gani nyingine inayoendelea pale?Wimbo huo nao ulifanya vizuri sana.

    MTOTO WA KAKA YAKO. Wimbo mwingine ambao ulikuwa kama unamsema yule mjomba wake Miriam kwa kutaka kumuozesha mwanaye mtoto wa kaka yake.

    Sikusahau kumuelezea Mzee Said Soji katika wimbo wa MZEE MLINZI. Huu niliutunga kama kumuenzi mzee yule kutokana na ushauri wake pamoja na kazi yake.

    IPO SIKU.Nao ukawa wimbo mwingine ambao ulitupa matumaini ya kuwa ipo siku tutarudi kazini na kuendelea na majukumu yetu.

    S and M. Wimbo huu ukailezea kampuni yetu jinsi ilivyokuwa inapiga kazi ndani na nje ya nchi ya Tanzania.

    UPO NASI.Wimbo maalumu kwa Silvia na marehemu wote waliyotutoka katika mapambano ya kila siku.

    MIRIAM.Nao niliuweka katika albamu ile.

    SABABU NI NINI?.Wimbo huo uliuliza sababu ya sisi kufanyiwa yale yote.Je ni mapenzi,wivu au visa tu!

    TUSAIDIE.Ukawa wimbo kwa ajili ya kumuomba rais atusaidie katika janga linalotukumba.

    Watanzania na dunia kwa ujumla sasa ikafumbuka masikio na akili. Na pia allbamu hiyo ndiyo ikawa albamu bora kabisa Tanzania kwa mwaka huo.Na tunzo ikachukua.



    Jina langu likarudi kwenye chati sasa,lakini safari hii lilirudi kisanii zaidi.Kila nilipopanda jukwaani katika matamasha mbalimbali,mashabiki waliomba niendelee kuimba kutokana na mistari yangu kuwa na nguvu sana.

    Baada ya kuona kuwa nakubalika,ndipo nilichukua jukumu la kufanya maonesho nchi nzima. Na kwa kuwa tayari nilikuwa na jina na washabiki wengi,wadhamini wakajitokeza kwa wingi kwa ajili ya kudhamini tamasha langu hilo.Nikaalika na wasanii mbalimbali wa hapa Tanzania kwa ajili ya kusindikiza tamasha hilo.

    Kwa ujumla nilifanya vizuri sana kwa kila mkoa niyokuwa natembelea.Kila shabiki aliweza kuburudika kutokana na kazi ambayo nilikuwa naifanya.Mkoa wa mwisho ukawa ni DODOMA.Mkoa ambao ndiyo nilikuwa natokea na ndipo makazi ya studio yetu ilikuwepo. Na kwa mbwembwe nyingi,niliarika msanii mmoja kutoka nje ya nchi.

    Msanii huyo alitokea Marekani na baada ya kufika,tamasha likafanyika vizuri sana na kumalizika salama kabisa. Nakumbuka siku ya Tamasha jina tajwa lilikuwa ni Man’Sai,hadi yule msanii niliyemualika alikubali kwa jinsi nilivyofanya hadi wale washabiki wote wakabaki kulitaja jina langu.

    Kwa heshima aliyonipa,aliamua kurekodi na mimi nyimbo tatu ambazo zote ziliendelea kuwapondea wale maadui zetu.Msanii yule pia alikubali tufanye video ya wimbo mmoja ambayo angeichukua na kuipeleka katika vituo mbalimbali vya luninga vya nchini kwao na dunia nzima. Baada ya kufanya hayo yote,akarudi nchini kwao.



    Nusu ya mapato ya tamasha lile,nilimpa Solomon ili aendeleze maisha yake yake na ya watoto. Na nusu iliyobaki,tuligawana mimi na kaka yangu,huku mauzo ya albamu yangu,kiasi fulani niliipa familia yangu na kingine niliwapelekea watoto yatima kwenye kile kituo nilichoanzisha,ambacho nacho kwa muda ule kilikuwa chini ya serikali.Watoto wale walifurahi sana waliponiona na walikuwa hawataki hata niondoke,lakini ilinibidi nifanye hivyo.

    *************



    Siku moja wakati natoka kwenye shughuli zangu,ikiwa ni usiku wa saa mbili. Barabara ikiwa pweke kabisa,na huku mimi nikiwa natembea kwa miguu.Ghafla kwa mbele yangu ilitokea gari nyeusi na kupiga breki mbele yangu na kwa sauti ya juu wakaanza kuniamuru nifanye watakayo.

    “Simama kama ulivyo,na endapo ukijidai mjanja,tunaondoka na roho yako”.Iliamrisha sauti moja kutoka kwenye dirisha la lile gari.

    Niliposikia maneno hayo nilicheka cheko moja ya kebehi na kisha nikawajibu.

    “Kama kufa nimeshakufa muda mrefu sana,ila kwa sasa nimefufuka,msitegemee kama nitakufa kirahisi hivyo”.Baada ya kuongea hivyo,nililizunguka lile gari ambalo lilikuja kukaa mbele yangu. Baada ya kufanikiwa,niliendelea kunyoosha barabara kwa ajili ya kuelekea nyumbani.

    Nilipowapa mgongo walinifyatulia risasi karibu kabisa na miguu yangu wakidhani nitaogopa na kusimama lakini kwangu mimi ikawa kama wameniongeza spidi ya kutembea. Nikakaza mwendo bila uoga wala kugeuka nyuma. Ndipo jamaa wale ambao niligundua kuwa wapo watatu,waliamua kutoka garini na kunifuata.Niliposikia vishindo vyao,nikageuka ili niangalie wanachotaka kufanya.

    Waliponifikia,walianza kunitukana na kunikejeli. Hayo yote yalikuwa siyo kitu kwangu,lakini pale walipotukana wazazi wangu,ndipo nilipouanzisha moto. Nilipigana nao kwa muda kama wa dakika kumi,na kwa kuwa walikuwa wengi kuliko mimi,walifanikiwa kuniweka mikononi mwao kwa kunipiga na kitako cha bunduki maeneo ya kisogoni.Tendo hilo lilifanya nipoteze fahamu kwa muda nisiyoujua.



    Niliposhtuka nilijikuta kwenye chumba kidogo chenye mwanga hafifu pamoja na dirisha dogo moja ambalo lilikua juu kiasi cha kutoweza kulifikia ili nichungulie nje. Vilevile chumba kile kilikua kikitoa harufu kali ya uozo na kukiwa kumezagaa mifugo ya ajabu ambayo binadamu wa kawaida hawezi kuifuga. Panya,mijusi, mende, kunguni,funza,viroboto pamoja na wadudu wote uwajuao kwa kupenda mazingira machafu,walikuwamo humo. Mifugo ile hasa panya na mijusi walikua hawaogopi wala kuhofia kuuliwa na binadamu maana waliweza kusogea hadi puani mwangu na kuanza kuniramba na saa nyingine kuning'ata kabisa..

    Nakumbuka ilikuwa ni usiku sana wakati nimerudiwa na fahamu,hivyo sikujua ni vitu gani vinatoa harufu ile wala kuelewa pale ni wapi..

    Sikuweza kulala kirahisi kwa sababu viroboto,kunguni na mbu waliniandama mwilini pamoja na kuimba nyimbo nyingi sana zisizoeleweka masikioni mwangu, hasa mbu.



    Mida ya saa kumi alfajiri ndipo nilihisi napata usingizi baada ya mang'amu ng'amu mengi niliyopitia siku ile. Sikujua nilipataje usingizi ule lakini navyojua nililala na kuota ndoto nzuri sana nikiwa na Miriam tukipeana mambo mazuri na moto moto. Nikiwa ndani ya ndoto ile niligutushwa ghafla kwa kumwagiwa maji ya baridi jambo lililofanya nipige yowe kubwa kwa kutaja jina la Miriam ambaye alinijaa kichwani mwangu kupita maelezo.



    "Ha ha haa,Frank rafiki yangu wewe ni wa kulala na panya,kuliwa na mbu pamoja na viroboto?. Wewe ni wa kukaa na mizoga kama hii? {huku akipiga teke mguu mmoja wa binadamu kuja kwangu}. Embu ona mazingira uliyomo ndugu yangu. Eti na unaota kabisa upo na Miriam. Tajiri kama wewe, msanii, embu jione kwanza hapa ulipo". Yalikuwa ni maneno ya kwanza kuyasikia tangu niingie pale,na maneno yale yalitoka kwa mtu niliemfahamu kabisa.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Rafiki yangu Frank,kwa nini hukutusikiliza sisi baada ya kukupa lile onyo la kukufirisi?Siyo sisi tu! hata rafik zako na ndugu zako. Ona yanayokukuta sasa hivi,ni lazima ufe Frank,lazma ufe Jay Z ili tupumzike na matapishi yako". Aliendelea kuongea jamaa yule kwa msisitizo huku akisogeza uso wake karibu na uso wangu jambo lililofanya nigundue kuwa tayari kishamkabidhi roho yake shetani.





    Nilitabasamu kidogo na kisha nikafungua kinywa changu kwa mara ya kwanza tangu niingie pale.

    "Chris dogo langu,naona umevimba sana kichwa kisa umekuwa mlinzi wa shetani. Lakini hilo siyo kitu kwangu,hata nikifa kaa ukijua wapo wanaoujua ukweli wote ambao wewe unadhani haujulikani". Niliongea hayo kwa kujiamini jambo liliofanya Chris acheke kwa dharau na kisha akaendelea na maneno yake

    "Kijana naona dharau zimeanza,tayari nimeshakua dogo si ndiyo eeh! Sasa leo tutaona nani dogo humu ndani". Niligundua tayari Chris kishajaa gesi kwa hasira kutokana na maneno yangu maana toka kitambo alikuwa hapendi kuitwa dogo. Alichomoa bastola yake toka kiunoni na kisha kuielekeza kwenye kichwa changu na kunambia nisali sala yangu ya mwsho..



    Nilicheka tena lakini safari hii ni kwa sauti ya juu na kwa kejeli zaidi,kisha nikamwambia,

    "Chris, Chris dogo langu, fanya ufanyalo lakini huwezi kuupata moyo wa Miriam sababu wewe ni sura mbaya na moyo mbaya pia na huna mafani......". Sikumalizia kauli yangu,Chris tayari alishadakia kwa hasira zaidi

    "Sasa hapo ndiyo umeharibu kabisa na nabadilisha zoezi,hutokufa kwa risasi lakini cha moto utakiona,si wajidai unatema shombo? Ngoja tuone".. Alibwata Chris na kisha kutoka nje na aliporudi, alirudi na mabaunsa watatu wakiwa na mapanga mikoni mwao yakiwa yanang'aa kisawa sawa kuonesha kuwa yalikua ni makali hatari.

    Kabla hajafanya chochote,alikuja kwangu na kuanza kubwabwaja mambo mengine ambayo hata sikumuuliza.

    “Sikiliza Jiga. Watu wengi kama wewe hufa kutokana na kujua siri zetu,na ndiyo maana kihere here cha yule mzee mlinzi kwa kutaka kujua ni biashara gani nyingine inafanyika katika ghorofa lile,kilimpeleka kaburini”.Aliongea Chris ambaye alikuwa kasimama mbele yangu huku kashika ile bastola yake.

    “Kwa hiyo kisa ni biashara za kwenye lile ghorofa,ndiyo mkamuua Mzee Soji?”.Niliuliza kama nilikuwa sina jibu.

    “Siyo tukamuua,sema nilimuua. Nilimuua mimi peke yangu na kwa bunduki hii hii”.Alithibitisha maneno yake huku akiionesha ile bastola yake ndogo.

    Baada ya kuongea hayo,Chris aliwanong'oneza jambo wale mabaunsa na kisha alinigeukia na kuniuliza swali.

    “Jay.Ni kweli unataka kufa bila kuwaona watoto wako na Miriam?”

    “Miriam yupo wapi?”.Nilimuuliza Chris kwa hamasa ya kutaka kujua.

    “Yupo Urusi kwa baba yake.Na ana watoto mapacha na wote wa kiume. Kweli wewe jembe,lakini unakufa Jay”.Aliniambia Chris huku akiizungusha zungusha bastola yake.Nilicheka na kumjibu kuwa kwa sasa naweza kufa kwa sababu mwanamke nimpendaye,yu hai na ana watoto wangu.

    “Miriam siyo mwanamke wako,Miriam ni mwanamke wangu. Wewe ulinipora tu!”.Chris alibwata kwa hasira baada ya mimi kumwambia maneno yale.

    “Ha ha haaa. Eti nilikupora. Huna sumu Chris,sura mbaya kama hiyo huwezi kuwa na mtoto mzuri kama yule. Mimi ndiyo Jay Z na yule ni Beyonce,wewe mwenyewe ulitupa hayo majina,unakumbuka?”Nilimwambia Chris na kumfanya azidi kuwa na hasira.

    “Hapa nisije nikakupiga risasi za kichwa bure na wakati mimi nataka uyasikie maumivu halisi ya kufa”.Alipoongea hayo,akawaruhusu wale mabaunsa wenye mapanga kwa ajili yakufanya kazi yao.

    "Nadhani utaenjoy na kuwapa ushirikiano mkubwa jamaa zangu, kwa heri Handsome". Alimaliza Chris na kuanza kuondoka huku wale mabaunsa wakinisogelea na kushika miguu yangu.

    Hapo nilianza kukukuruka kwa nguvu nyingi japo nilikuwa nimefungwa kamba ngumu pamoja na pingu kwenye mikono yangu. Na nilizidi kurusha na mateke jambo lililofanya mmoja wa mabaunsa kunikalia kifuani na mwingne kushika mguu wangu wa kulia, huku mwingne akinyanyua panga lake juu na moja kwa moja likatua kwenye mguu wangu ule.

    Nilitoa yowe kubwa sana lakini halikufika popote sababu tayari nilikua na uzito mkubwa kifuani wa yule baunsa mwngine. Giza taratibu likaanza kutanda machoni mwangu,sauti ikazidi kupotea na matumaini nayo yakatoweka baada ya kuona mguu wangu mwingine unakamatwa kwa ajili ya kufanyiwa yale yale.

    Kifo karibu yangu,maumivu mwilini mwangu,matumaini kuokoka kwa wakati ule yakapotea. Ni MUNGU pekee niliyemkabidhi maisha yangu ayaokoe. Nilianza kusali kwa nguvu zote japo nilisema kuwa siogopi kifo. Sala zangu nadhani MUNGU alizisikia na kuzifanyia kazi kwa haraka sana.

    Wakati yule baunsa mwingine akiwa ananyanyua panga lake kwa ajili ya kuukata mguu wangu,ghafla mlango ule waliyoingilia ulibomolewa na kwa kishindo kikubwa kilichotua pale ndani,kiliwafanya wale mabaunsa kuacha zoezi la kuukata mguu wangu. Kishindo kile kilikuwa ni mwili wa Chris ambao uliingia mle ndani ukiwa hauna kichwa.

    “Wewe ndiye ulimuua baba yangu kwa sababu ya pesa,sasa leo na wewe mwisho wako umefika”.Ilikuwa ni sauti yenye hasira ikitokea kule mlangoni.Wale mabaunsa walikuwa wanatetemeka hasa ukizingatia walikuwa hawana siraha nyingine zaidi ya mapanga yao.

    Wakati bado walinzi wale wakiwa wanashangaa shangaa,kila mmoja niliona akidondoka huku damu zikiwatoka kichwani ambapo palikuwa na tobo kubwa lililotokana na risasi zilizopigwa kutokea kwenye kale kadirisha cha kile chumba.Sikujua ni nani aliyefanya vile,lakini sauti iliniita kwa jina la Jay Z na kuniuliza kama nipo salama,na mimi nikajibu kwa shida na kwa uchovu kuwa nipo salama.

    Baada ya jibu langu lile,waliingia jamaa wawili ambao niliwafahamu haraka sana.Walikuwa ni Zaganda pamoja na Solomon,wote walikuwa wameshikilia mapanga. Walininyanyua haraka na kuanza kunitoa nje. Pale mlangoni nilikutana na sura nyingine ikiwa imeshikilia bunduki kwa ukakamavu.Alikuwa ni Mustapha Said Soji,au Muphty,mtoto wa yule mzee mlinzi,na nahisi yeye ndiye alimuua Chris.

    Baada ya kutoka nje,pia nilikutana na Saint Kinala naye akiwa na bunduki,na moja kwa moja nikajua yule ndiye aliyewaua wale mabaunsa kupitia lile dirisha la kile chumba. Saint alikuja kuwasaidia wakina Solo kunibeba hadi getini.

    Lakini kabla hatujavuka lile geti,nyuma yetu zikaanza kufyatuliwa risasi nyingi sana.Huku nikiwa sielewi nini kinaendelea,nilimuona Solomon taratibu akianza kuregea na baadae kuniachia kabisa.

    Muphty aligeuka ghafla na kuanza kujibu mapigo ya risasi zile.Na baada ya muda,nilishuhudia walinzi watano wa jengo lile wakigaa gaa chini huku damu nyingi zikiwatoka. Muphty alimnyanyua Solomon na kumuweka begani,huku Saint na Zaganda wakinyanyua mimi hadi nje ambapo tulikuta gari likiwa linatusubiri.

    Dereva wa gari lile alikuwa ni kaka yangu ambaye alikuwa anatengeneza mapigo ya muziki katika studio yetu.Mimi na Solomon tuliwekwa siti za nyuma,huku Zaganda na Saint wakikwea kwenye bodi la pick up ile. Muphty yeye alikaa mbele na dereva.Safari ya kuondoka eneo lile ambalo lilikuwa ni pori kubwa sana ikachukua nafasi.

    “Masai…Masai…”.Ilikuwa ni sauti ya Solomon ikiniita kwa shida sana.

    “Naam kaka”.Na mimi nikaitika vivyo hivyo huku yale matambala na kamba niliyofungwa kwenye mguu ili damu zisiendelee kutoka,yakiwa yanafanya kazi kiasi chake.

    “Namuona Silvia ananipa mkono wake ili nimfate.Masai watoto wangu tafadhari”.Solomon aliongea hayo huku akiwa anapumua kwa kasi.

    “Usiseme hivyo kaka.Tutapona tu!”.Nilimpa moyo.

    “Hapana Masai.Nakufa kama mke wangu,na ninadhani atanisifu sana kwa nilichokifanya. Masai,nakuomba watoto wangu unitunzie,nakuomba Masai. Ukifika huko salama,nenda kafungue kesi tena ya kurudisha mali zetu,na ukifanikiwa nakuomba unisomeshee wanangu kwa kiwango chetu.Na kamwe usiwaruhusu wawe kama sisi. Tulifanya kosa kubwa sana kuwaamini marafiki,na mwisho wa siku ndiyo wametugeuka.

    Chanzo cha haya yote ni fedha na tamaa ya utajiri huku yakichochewa na wivu kutoka kwa marafiki hao.Wivu wa kutaka kumiliki kila kitu wakionacho,hadi mwanamke wa rafiki yako.Masai,usiwapeleke wanangu kwa njia hiyo”.Solomon alizidi kuongea japo bado ilikuwa ni kwa shida.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Masai,naomba uniahidi kuwa utawatunza wanangu.Niahidi sasa hivi”.Solomon aliweka msisitizo.

    “Nitafanya hivyo kaka”.Nilimjibu Solomon huku nikijaribu kumpooza kwa kumpiga piga begani.

    Alijibu asante,na baada ya jibu hilo alitulia tuli kabisa.Nilipomtikisa hakuitika na pale nilipomuita jina lake,alikaa kimya.Niligundua kuwa Solomon hakuwa na mimi tena.

    Nililia kwa sauti ya juu kuliko hata ile ya wakati nakatwa mguu. Ilikuwa ni machungu ndani ya uchungu,machozi ndani damu,kilio cha sauti ndani ya vita na matone ya jasho ndani ya baridi kali.

    Maumivu yaliyokuwa ndani ya moyo na mwilini mwangu kwa wakati ule,yalifanya nipoteze fahamu kwa muda nisiyoujua.





    Nilipozinduka nilijikuta nipo hospitali. Ilikuwa ni mida kama ya saa kumi na moja alfajiri. Watu walikuwa hawajaanza kuingia wodini,hivyo kulikuwa kimya sana.Nilivuta kumbukumbu na kukumbuka yote yaliyotokea nyuma.

    Hapo nikakumbuka kuwa nilikatwa mguu na wale wafuasi wa Chris,na baadae nikakumbuka jinsi Chris alivyokufa na mimi kuokolewa.

    Nilipofika kwenye kumbukumbu ya kifo cha Solomon,hapo machozi yalianza kunimwagika na kuanza kujipiga kifuani. Hiyo sikuona kama inatosha,nikaanza kurusha miguu pia,lakini ule mguu mmoja ulikuwa mzito sana,na nilipozidi kuurusha niliambulia maumivu. Huo ni ule mguu uliokuwa umekatwa na wale mabaunsa,sasa ulikuwa umenyofolewa kabisa na kubaki kipisi.

    Nilijikuta nazidi kulia maradufu ya pale mwanzo. Nililia kwa sauti ya juu kiasi cha kuwafanya wagonjwa wengine niliokuwa nimelazwa nao ile hospitali kuamka na kuanza kulalamika kuwa napiga kelele.Ndipo muuguzi aliyekuwa akinisamamia alikuja kunituliza na kuanza kunisihi huku akinipa matumaini mapya kuishi bila kiungo changu kimoja cha mwili.

    Yote kwa yote,yapasa kuelewa kuwa maisha yanaweza kwenda bila kuwa na baadhi ya viungo mwilini mwako. Kitu cha msingi ni binadamu kuelewa na kuwathamini wale ambao wana upungufu wa viungo hivyo. MUNGU ndiye kaniumba mimi na wewe,na MUNGU ndiye muweza wa kufanya yote katika maisha ya mwanadamu. Kama akiamua kuchukua kiungo chako,huchukua muda wowote.Na kama akiamua kukupa kilema tangu ulipozaliwa,basi pia hufanya hivyo. Usimdharau na kumkashifu kwa njia yeyote yule ambaye kapungukiwa viungo au kiungo cha mwili.

    ***************

    Baada ya kutulia kwa kunyamaza,yule muuguzi aliniambia ni mimi ndiye nilikuwa nasubiriwa kuamka ili nisaini karatasi ya kuwekewa mguu wa bandia,baada ya kile kidonda cha kukatwa mguu wangu kupona kabisa.Nilipomuuliza ni muda gani nimekaa pale,aliniambia ni wiki mbili,huku wiki moja nikikaa chumba cha wagonjwa mahututi.Hiyo ni baada ya kumwaga damu nyingi sana,na kule nilipopelekwa kulikuwa ni mbali sana,kwa hiyo walichelewa kunifikisha hospitali.



    Walikuja watu wengi sana pale hospitali kuja kunijulia hali pamoja na pole. Wengi walikuwa wanaamini kuwa nitatoka na kuendelea na maisha yangu. Na nilithibitishiwa kuwa Solomon naye alikufa siku ile baada ya kupigwa risasi mbili za mgongoni,ambazo zilitokezea kifuani na kupasua mishipa muhimu kwa ajili ya kupeleka damu.

    Licha ya wengi kuja kunijulia hali,lakini sikuweza kumuona Miriam wala rafiki zake na ujumbe wowote kutoka kwake. Kila siku nilingoja ujio wake,lakini hakuonekana hadi mwezi ukaisha.Nilikubali matokeo kuwa sitaweza kumuona tena.



    Baada ya wauguzi kuthibitisha kuwa nimepona kabisa,waliweka ule mguu wa bandia na kunipa fimbo maalum kwaajili ya kutembelea.

    ******************

    Nilirudi nyumbani baada ya kufanikiwa kuwekewa mguu huo.Nilipofika nilikuta ndugu na rafiki zangu wameniandalia sherehe ndogo ya kunikaribisha tena nyumbani. Tulisheherekea kidogo sherehe ile ili kusahau yaliyopita japo kamwe nisingeweza kuwasahau Solomon,Chris na Silvia. Ni watu niliyokuwa nawapenda sana.Watu ambao kwangu niliwafanya kama ndugu,lakini sikuwa nao tena.



    Malipo ya muovu,yakalipwa kwa kuuawa,na malipo ya shujaa kama Solomon na Silvia,nayo yalilipwa kwa kifo. Yote hayo ni kwa sababu walikuwa wanaokoa roho yangu,utapata rafiki gani kama hao katika dunia hii? Acha niwaite ni zaidi ya ndugu kwa heshima yao.



    Baada ya furaha kidogo kuja katika sherehe ile,ndipo dada yangu mdogo ,yule aliyesomea sheria mimi nilipoenda CBE, alienda kwenye jukwaa dogo lililoandaliwa pale nyumbani na kisha akaanza kuongea yaliyompeleka pale.

    Kwanza alianza kwa kumshukuru MUNGU kwa kutuleta pamoja eneo lile.Kisha baada ya hapo,alitoa sala kwa ajili ya marehemu wote waliotutoka katika dunia hii,huku wote tukiendelea kumsikiliza kwa makini.

    Baada ya kumaliza sala na baadhi ya maneno ya kuwashukuru waliohudhuria tafrija ile ndogo,aliniita pale jukwaani huku akiwa anatabasamu pana usoni mwake. Tabasamu ambalo kwangu liliamsha maswali kadha wa kadha hasa pale nilipofikiria mangapi nimeyapitia,na mangapi natakiwa kuyapita ili nitabasamu kama yeye. Kwa kifupi niliona kama ananitania kwa lile tabasamu.

    Baada ya mimi kupanda kwenye lile jukwaa,akawaita wenzake wawili,ambao alisema kuwa kasoma nao Sheria huko Mzumbe.

    “Kaka yangu mpendwa,au pacha wangu. Kwanza nimefurahi sana kwa kuwa leo hii tupo hapa pamoja”.Alianza dada yangu yule kuongea kwenye kipaza sauti,na wakati huo mimi nilikuwa naitikia kwa kupeleka kichwa juu na chini.

    “Nilisubiri sana ujio wako ili niweke wazi yanayoendelea katika dunia hii iliyojaa chuki na masimango. Chuki ambayo inawapoteza watu muhimu katika maisha yetu,chuki ambayo inaacha watoto wadogo wakiaangaika kutafuta msaada,chuki ambayo inapelekea watu waishi bila amani mioyoni mwao,chuki inayoleta uhasama baina ya watu na watu.Chuki yenye wingi wa maovu”.Dada yangu yule alikuwa akiongea safari hii bila kuweka lile tabasamu alilolionesha mwanzo,jambo lililonifanya niamini kuwa si kila tabasamu linaanisha kuwa mtu ana furaha bali ni katika kuiweka sura yake isijioneshe kama ipo katika huzuni au matatizo.

    Aliongea mengi sana baada ya mimi kupanda pale jukwaani. Lakini la muhimu zaidi alilosema kaniitia pale,ni kunipa taarifa kuhusu kampuni na mali tulizovuna kuachiwa huru baada ya ushahidi kukamilika na mimi kusubiriwa kwenda kuthibitisha yaliyonikuta.

    “Kaka. Kwa msaada mkubwa wa hawa rafiki zangu wawili,tuliweza kukata rufaa kuhusu ile kesi ya wewe kuporwa mali zako, na uzuri imeshasikilizwa na wale watuhumiwa Warusi tayari wamewekwa mikononi baada ya kupatikana na kesi nyingi nyingine. Ni wewe ulikuwa unasubiriwa kwa ajili ya kwenda kutoa ushahidi wa mwisho ili mali zote ulizofirisiwa na za kaka Solomon,kurudishwa mikononi mwako”.Dada yangu alinipa taarifa hizo,na baada ya taarifa hizo za ahueni,nilimshukuru kwa kumkumbatia kwa nguvu huku nikitoa machozi ya furaha pamoja na ya kuwakumbuka sana rafiki zangu waliyotangulia mbele ya haki. Nilitamani sana wangekuwepo na kuona mafanikio ya nguvu zetu,lakini hawakuwepo tena katika upeo wa macho yangu.

    **************

    Wiki iliyofuata nilipandishwa kizimbani ili kutoa uthibitisho kuwa yale yote yaliyosababishwa mimi kufirisiwa yalikuwa ni uongo. Nilipopanda pale,niliongea kidogo kwa kuwaeleza ukweli wa mambo. Na baadae nilitoa redio ndogo mfukoni na kuipa mahakama kwa ajili ya kuisikiliza.

    Walipoifungulia,walianza kuisikia sauti ya Chris ikinionya kwa yale niliyokuwa nayafanya na baadhi ya maongezi ya wale watu waliyoniteka.Maongezi ya wale watekaji yalikuwa ni kama kutoa taarifa kwa bosi wao kuwa wamefanikiwa kuniteka. Na hayo yote yalijirekodi wakati mimi sina fahamu.

    Kila siku maisha yangu nilijua kuwa nitatekwa na kuuawa,au kama si hivyo,chochote chaweza kunikuta kutoka kwa wabaya wangu. Hivyo wakati wowote nilikuwa natembea na kifaa cha kunakiri maneno kwa ajili ya ushahidi,na kweli nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

    Baada ya wale jamaa kutokeza na gari lao siku ile wakati narudi nyumbani,nilifungulia kile kifaa na kuanza kurekodi mambo yote yaliyokuwa yanaendelea baada ya mimi kutekwa. Maneno ya Chris,yalikuwa ndiyo msumali wa mimi kushinda kesi ile.Na mbele kabisa ya kanda ile niliyonakiri sauti za watu,kulikuwa na sauti ya Solomon akiniomba niwalee wanae kwa kuwapa elimu zaidi na matunzo yaliyo bora.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Baada ya kusikiliza sauti zile,walikuja mashahidi wengine watano kwa ajili ya kuweka ushahidi wa mimi kukandamizwa na kufirisiwa katika kesi ya kwanza. Mashahidi wale,walikuwepo siku ile wakati nafirisiwa,na ni hao ndiyo waliithibitishia mahakama kuwa nafanya biashara za magendo na kuuza madawa ya kulevya.

    Leo hii walikuwa upande wangu huku wakisema kuwa walishinikizwa kwa kupewa hela na Chris ili wanikandamize katika ile kesi yangu. Waliongeza kuwa,wale mashahidi wengine waliyonikandamiza siku ile,walikuwa wanakufa kila kukicha,tena vifo vya kikatiri na kutisha. Yote hayo,walisema yalifanywa na Chris na washirika wake.



    Baada ya kesi yangu kurindima na kuisha,ikaja kesi ya Mjomba wa Miriam na Yuri,kesi yao ilipangwa kufanyika siku moja na yangu. Hivyo nao wakapanda na kuanza kusomewa mashitaka yao. Wao walikuwa na mashitaka ya kuuza madawa ya kulevya,kuingiza silaha za moto nchini pamoja kuchukua watoto wadogo na kuwapeleka barani Asia kwa ajili ya kuwafanyisha biashara mbalimbali zikiwemo umalaya.

    Japo walikataa,lakini uwepo wa vithibitisho hivyo ulikuwepo .Na zaidi yule Muphty,ndiye alisimamia ushahidi ili Yuri na baba yake,wahukumiwe.

    Hatimaye,walipelekwa mikononi mwa serikali ya Urusi kwa ajili ya kuhukumiwa. Huku mali zao zilizokuwepo nchini,serikali yetu ikizigawa nusu kwa Urusi na nusu kubaki hapa.

    Kwa upande wangu,kampuni ilirudishwa mikononi mwangu na pia serikali ikanilipa fidia kama usumbufu nilioupata baada ya kufirisiwa.Hapo maisha mapya yakaanza huku nikiwa mlezi mkubwa wa watoto wa Silvia na Solomon ambao sasa walikuwa na miaka sita kila mmoja.

    **********



    Sikuwa mtu wa kutabasamu kama hapo nyuma,japo mali zangu zilirudishwa mikononi mwangu. Nilipoteza radha ya kuishi tangu zamani kutokana na ugumu wa maisha niliyoyapitia.

    Kazi ya kampuni ilianza tena huku ikiwa na wafanyakazi wapya na wale wa zamani. Zaganda na Saint,waliendelea na biashara yao.

    Niliwachukua rafiki wa dada yangu pamoja na dada mwenyewe na kuwaweka kama wanasheria wa mali zangu. Ile studio ya muziki,niliikuza na kuwa kubwa kiasi cha kufika uwezo wa kuchukua wasanii wanne kwa wakati mmoja. Yaani wasanii wanne waliweza kufanya kazi kwa wakati mmoja.

    **************

    Ni rafiki pamoja na ndugu zangu,ndiyo waliamua kunifanyia sapraizi kwa kuniwekea tafrija moja kubwa kiasi,ambapo waliita watoto yatima na wa mitaani kwa ajili ya kujumuika na mimi katika chakula cha usiku.Ilikuwa ni baada ya mwezi tu!Mimi kurudishiwa mali zangu,ndipo hayo yote yalitokea.

    Nilikuwa ni mtu wa furaha sana siku ile. Na baada ya kupata chakula,waliniomba nisimame na kuongea kidogo.

    Nilisimama na kuanza kwanza kumshukuru MUNGU kwa kunileta pale siku ile.Niliwashukuru wazazi,ndugu pamoja na watu wote waliyofika pale.Wakati naendelea kuongea hayo,mara nje kukaanza kusikika milipuko na kelele nyingi za watoto. Nilishindwa kuelewa ni nini kinaendelea hadi pale nilipotoka nje na kukutana na jambo lililonifanya nitoe machozi.



    Niliangalia juu na kuona milipuko ile ambayo ililipuka lakini sikuweza kuona vizuri kilichokuwa angani kwa sababu ya machozi yaliyokuwa yametanda machoni mwangu baada ya kuona watoto wengi wakiwa wameshikana mikono na kuimba wimbo wa siku ya kuzaliwa kwangu.

    Niliyafuta machozi yale na kuangalia juu na kukutana tena na milipuko ile angani ambayo inaitwa fataki. Ilikuwa ikilipuka inaandika “HAPPY BIRTHDAY FRANK”.

    Machozi yalizidi kunimininika sijui kwa sababu ya furaha au nini,lakini nilikumbuka mengi sana baada ya kugundua kumbe siku ile ilikuwa ni siku yangu ya kuzaliwa.

    Miaka thelathini na tano niliyokuwa naitimiza siku ile,ilikuwa si miaka ya kupitia maswahibu yale yote. Lakini MUNGU ndiye muweza wa yote,na nilimshukuru kwa kila jambo.



    Watoto wale wa mtaani pamoja na wale wa Solomon,waliendelea kuniimbia wimbo wa kuzaliwa huku wamenishika mikono yangu na taratibu waliniongoza kwenye jukwaa la ukumbi ule na kuniacha pale na wao kurudi walipokuwa wamekaa.

    Sasa watu wote ukumbini walitulia kimya wakiniangalia mimi na masikio yao yakiwa wazi kabisa kusikia ni nini nitakacho kiongea. Nilisogelea kipaza sauti,na bila kutegemea,sauti ya kwikwi ya kilio ilianza kusikika ukumbini mle kupitia spika zilizokuwa zimewekwa mle ndani. Ilikuwa ni sauti yangu ambayo sikutegemea kama itaweza kusikika vile.

    Nilijikaza sana nisiweze kuendelea,lakini mwisho wa siku ilikuwa ni kilio cha kweli kutoka kwangu. Watu walikuwa wametulia huku majonzi tele yakiwa yamewakumba kutokana na kilio changu,lakini kulikuwa hakuna hata mmoja aliyekuja kunisihi niache kufanya vile hadi pale nilipojikaza na kusema neno moja tu! La “ASANTENI”.



    Ukumbi mzima ulisimama na kanza kupiga makofi kwa ajili yangu na wakati huohuo watoto nao wakaanza kuimba wimbo maalum wa pongezi kwa ajili yangu.

    Ilichukua kama dakika tano kufanya hivyo,na baadae walitulia tena na kusubiri neno lingine kutoka kwangu. Safari hii nilikuwa nimeacha kulia hivyo sauti yangu ilikuwa tayari kwa ajili ya kuongea maneno niliyokuwa nimeyaandaa.

    Wakati nataka kuanza kuongea,mara mlango mkubwa wa ukumbi ule,ulifunguliwa kwa nguvu,na hapo nikamshuhudia Mzee mmoja mzungu mwenye mvi nyingi kichwani mwake akiingia huku kaongozana na wanajeshi watatu nyuma yake,na pembeni yake alikuwepo mwanamke aliyekuwa kabeba watoto wawili wa kiume.

    Watu ukumbini mle wote walibaki wakihamaki huku wakidhani tayari naingia tena matatani.Uwoga ukawaingia waalikwa pamoja na ndugu zangu kwa kuona kuwa tayari matatizo yanafufuka.



    Nilishuka toka pale jukwaani huku nikiwa naangalia kile kikundi kilichoingia kwa macho yenye hamaki. Nilijikuta nadondosha ile fimbo yangu ya kutembelea na kuanza kukimbia kwa kuchechemea huku nikilitaja jina la Miriam kwa sauti ya juu kabisa. Alishusha watoto aliyokuwa kawabeba na yeye akaanza kunikimbilia huku akiwa na tabasamu moja nililokuwa nimelikosa kwa muda mrefu sana.

    Alipofika,bila hata kujali kuwa mguu wangu mmoja ni mbovu,alinirukia na kunidandia huku mikono yake ikiwa imekumbatia shingo yangu. Nilijikaza nisidondoke,lakini haikuwezekana. Taratibu nilishuka chini na kwa upole kabisa tukalala pale chini huku kinywa cha Miriam kikiwa sawia kabisa na kinywa changu.

    “Koho koho kohoo”.Kikohozi cha Mzee yule mzungu kilitutoa katika dunia yetu tuliyoikosa kwa muda mrefu.

    Alikuwa ni baba wa Miriam,ambaye sasa alikuwa ni Rais mstaafu wa nchi ya Urusi,na alikuwa kaja pale kama mgeni mualikwa aliyealikwa kisiri ili mimi nisijue,yaani iwe kama sapraizi kwangu.

    “Umekuwa mzito sana Mamie wangu”.Nilimwambia Miriam huku bado akiwapale kifuani kwangu kana kwamba tulikuwa peke yetu.

    “Sitaki uchokozi Dadie”.Na yeye alijibu huku akilaza kichwa chake kifuni kwangu na kuendelea kulala.

    “Embu nyie nyanyukeni hapo,mnadhani chumbani nini?”.Baba wa Miriam aliingilia starehe yetu kwa kutuambia hayo kwa lugha ya kiingereza.

    Tulinyanyuka na bila kutegemea,tulikuta ukumbi mzima ukiwa macho pima kwetu. Aibu ikatawala nyuso zetu,mimi na Miriam.Lakini baadae tukazoea na kutoka katika hali ile ya aibu.



    Baada ya hapo. Aliwaita watoto wale ambao walikuwa na miaka miwili kila mmoja,kisha akawatambulisha kwangu kuwa ni watoto wangu. Mmoja alimuita Brown,jina la baba yangu na mwingine alimuita Ludovic jina la baba yake. Nilifurahi sana kwa majina yale,na ukweli ukiwaangalia walikuwa wamechukua asili ya watu hao. Yule Kulwa alikuwa wote ni baba yangu,na Doto alikuwa ni mzungu kama baba wa Miriam.

    Niliwafuata pale walipo na kuwakumbatia kwa nguvu sana huku machozi yakinitoka.

    “I am your father(Mimi ni baba yenu)”.Niliwaambia watoto wale ambao walikuwa kama hawaelewi chochote kinachoendelea.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Yes,Dadie. We miss you(Ndiyo baba. Tulikukumbuka)”.Alijibu yule Mzungu ambaye ni Ludovic au Doto,na baada ya hapo nao wakajiunga kwa kunikumbatia.

    Baada ya hapo. Nikanyanyuka na kumfuata Mzee Mendrovic,baba wa Miriam. Na kwa heshima kubwa niliinama na kubusu viatu vyake kuonesha ishara ya kumuheshimu.

    “Hapana Frank. Mimi ndiye nastahili kukufanyia hayo. Mambo uliyoyakanyaga,mimi sijawahi kuyakanyaga”.Mzee yule alininyanyua na kunikataza nisifanye vile.

    “Hapana baba,hii ni heshima ya utu uzima wako.Wewe ndiye umeniletea mwanamke wa maisha yangu,nastahili kukupa heshima hii”.Nilimjibu na kurudi tena chini na kubusu viatu vyake.

    Japo aliona aibu,lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kuacha nimalize nilichokusudia. Baada ya hapo,nilichukua fimbo yangu ya kutembelea na kwenda moja kwa moja kwa wazazi wangu na kumtambulisha mzee yule,kisha nikampeleka kwa ndugu zangu na baadae nikamaliza kwa watoto wa Solomon na Silvia,ambao waliitwa Hailey na Hellena. Miriam aliwakumbatia kwa furaha sana baada ya kuwaona watoto wale ambao walizidi kukua.



    Baba wa Miriam,alienda hadi pale jukwaani na kuniita mimi na Miriam.Na tulipopanda alitoa pete na kunikabidhi mikononi mwangu.

    “Frank. Pete hiyo nilimvisha mke wangu kama uchumba,naomba na wewe uitunze kama mimi nilivyoitunza”.Baada ya maneno hayo aliondoka pale jukwaani na kutuacha wawili sisi tukiwa tunatabasamu tu!.

    Nilicheka moyoni kwa kumuona yule mzee kama sijui vipi,alitufanya sisi watoto au sijui hatujielewi. Eti katuita wote wawili halafu ananipa pete mimi na kunihasa na anaondoka. Sasa Miriam alimuita wa nini kama kitu alichotaka kukifanya kilikuwa kinanigusa mimi tu!. Na alivyo na makusudi alikaa sehemu moja na wazazi wangu na macho yake yote yakawa yanasubiri kuona nitafanya nini.

    “Will you marry me?(Upo tayari kuoana na mimi)”.Nilipiga magoti huku nimeilekeza pete ile kwa Miriam na kumuuliza swali hilo.

    “Yes,I do Frank. (Ndiyo, nipo tayari Frank )”.Miriam alinijibu na kunyoosha mkono wake wa kushoto. Na mimi nikavisha pete kidole chake.

    Hapo ukumbi mzima ukalipuka kwa shangwe huku baba mkwe akiwa mstari wa mbele kupiga shangwe hilo.Nilinyanyuka pale nilipokuwa nimepiga goti moja kwa mguu wangu ule mzima na kumkumbatia kwa nguvu sana Miriam.

    Nilipomkumbatia,wimbo wa R.Kelly-The Storm Is Over ambao uliwekwa na DJ ulianza kuburudisha na kunifanya niamini kuwa kweli,hakuna jambo lisilokuwa na mwisho. Na wimbo ule ulinifanya nibubujikwe na machozi baada kugundua kuwa sasa majanga yale niliyoyapitia, yalikuwa yameisha.

    ****************

    “The storm is over now Miriam(Kimbunga/majanga yameisha sasa Miriam)”.Nilimwambia hayo Miriam huku nikiwa ndani ya suti nyeusi na Miriam ndani ya shela la harusi.

    Tulikuwa tumekumbatiana huku tunacheza wimbo huo wa R.Kelly kama kufungulia mziki baada ya harusi.

    Hayo yote yalifanyika baada ya wiki moja ya mimi kumvisha Miriam pete. Baba wa Miriam akishirikiana na Baba yangu bega kwa bega,walihakikisha ndoa ile inafanyika haraka iwezekanavyo. Na sasa nilikuwa mume halali wa Miriam naye alikuwa mke halali wa Frank Masai.

    “Yah,Dadie. The storm is over”.Naye alijibu na kulala kifuani kwangu.

    *************

    Kuhusu mjomba wa Miriam na Yuri mtoto wake. Wote walihukumiwa vifungo vya maisha jela. Na zile mali zao zilizogawanyishwa huku Tanzania na Urusi,zile za Urusi kwa kuwa zilikuwa Tanzania,basi akapewa Miriam kuzisimamia.

    HAYO NDIYO YALIKUWA MAWIO NA MACHWEO.Nikimaanisha kuchomoza kwa jua na kuzama kwa jua. Ila katika hadithi hii nilichukulia kama kuchomoza kwa jambo,na kuisha kwa jambo.



    *************



    Siku hiyo ilikuwa ni Jumamosi tulivu sana katika Mji ule wa Dodoma, ndege walirembesha anga huku miti ikilalamika kwa mvuto wa sauti yake kutokana na upepo mwanana uliokuwa unavuma kwa wakati huo. Watu walikuwa katika harakati mbalimbali za kufanya maisha yao yapendeze kama si kuvutia kabisa.



    Hatukuwa nyuma katika harakati hizo. Kama kawaida ya Jumamosi nyingine, nilipenda sana kutoka na familia yangu kwenda mahala tulivu na kujadili mambo mbalimbali ya kimaisha. Siku hiyo nilipanga kuipeleka familia yangu ya watoto wanne na mke wangu kwenye moja ya sehemu nilizokuwa nazimiliki. Sehemu hiyo ilikuwa na michezo ya kila aina kwa ajili ya watoto na kuwa na sehemu maalum kwa ajili ya wazazi kupumzika na kufanya mambo mengine.



    Tulienda huko siku hiyo mimi pamoja na familia yangu . Tuliwaacha wana wetu wale wanne,huku wawili tulikuwa tumeachiwa na marehemu Solomon na mkewe Silvia na wawili wakiwa wa kwetu na wote wanne walikuwa ni mapacha.Tulijitenga pembeni wanapokaa wazazi au walezi na tuliagiza vinywaji ili tuburudike. Tulikuwa hatuna cha maana kilichotupeleka pale zaidi ya kuwaleta watoto wafurahi.



    “Mme wangu,nilikuwa nimekumbuka sana hali hii ya kukaa pamoja na wewe, sikudhani kama ipo siku tutakuja kukaa hivi tena”. Alianza mke wangu Miriam kuniongelesha maneno yale aliyoyatoa kwa huzuni lakini ni kwa faraja pia.

    “Yashapita hayo mke wangu. Yalikuwa ni Mawio na Machweo tu!. Katika maisha watakiwa kujua kuwa unavoishi ni sawa na jua, yaani lina mawio (kuchomoza kwa jua) lakini hapa katikati kuna mengi sana hadi kufikia machweo (kuzama kwa jua), na ndiyo yale tuliyopitia”

    “Ha ha haaa, yaani dadie wangu hapo ndipo nakupendeaga.Husahau hata kidogo. Hiyo kusema maisha ni Mawio na Machweo ni mimi ndiye nilisemaga,ila hapo umeongeza vimisemo vingine, halafu unajua kuvielezea kabla hata hujaulizwa, nakupenda sana Frank wangu AKA Jay Z”. Aliongea Miriam baada ya mimi kumpa faraja ya maneno yangu yale machache lakini yamejitosheleza kihisia.

    “Mh! Na wewe bado umeling’ang’ania hilo Jay Z. Haya bwana my wife AKA Beyonce”. Na mimi nilimjibu kiutani na kusababisha wote tucheke na kuendelea kuwaangalia watoto wetu wakiendelea kufurahi pale kwenye bembea na wengine wakitereza na kutumbukia kwenye maji nakuanza kuogelea.



    “Dadie samahani”

    “Bila samahani Mamie wangu”. Alianza tena Miriam kuniongelesha na mimi nikaitikia.

    “Sijui kama nitakukera,lakini kuna jambo ambalo nilikuwa na hamu sana nilijue kuhusu wewe”.

    “Mh! Wife na wewe, hivi mimi naweza kukerwa na harufu ya chokoleti au ua waridi wakati ndiyo vitu vinavyonipa raha?. Wewe ndiye kila kitu, sema tu! Mama yangu”. Nilimpa uhuru Miriam wa kuongea jambo linaliomtatiza.

    “Asante mume wangu, na wewe ndiye kila kitu kwenye pumzi yangu. Kitu chenyewe niiiii …….”. Akawa kama ana sita kuendelea huku anatafuna kucha zake. Niligundua ni kitu cha siri au cha aibu ndiyo maana anashindwa kukitamka.

    “Wee Miriam wewe, hizo aibu umetoa wapi? Ha ha haaa,embu usinifurahishe. Ongea tu! Usiogope bwana. Si wajua kiasi gani navochukia ukiniogopa?”.Nilimtania kidogo Miriam na kumpa hamasa ya kuongea jambo lake.

    “Hivi na wewe mme wangu bado ujaachaga tu utani? Mimi sioni hata aibu, nilikuwa nakula kucha ili nikumbuke na niwaze wapi kwa kuanzia. Sasa hivi nimepata pa kuanzia.

    Dadie, una kumbuka siku ile nilipokuulizia kuhusu mpenzi wako wa nyuma? Ulipoaga na kuniambia ni hadithi ndefu,unakumbuka siku ille?”.Alianza Miriam kuongea suala linalomsibu baada ya kujitetea kuwa haoni aibu.

    “Yes, naikukumbuka sana siku ile na hadithi ile haiwezi kunitoka kichwani hata kidogo. Ni sawa na hii iliyonitokea hapa majuzi”.

    “Ehee,basi leo naomba unihadithie kilichokutokea hadi kikakufanya siku ile kupoa vile”.Alingeoa Miriam baada ya mimi kumjibu kuwa naikumbuka siku ile.Tukaendelea na maongezi.

    “Mh!We nawe, hujachoka kupata huzuni? Ujue ile inahuzunisha sana, na ndio maana siku ile nilipoa sana”.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Dadie bwana,mi sitaki. Nataka unihadithie hivyo hivyo hata kama ina huzuni hadi iishe. Isipoisha tutaendelea nyumbani”.

    “Ok mama yangu, ngoja nikuhadithie uridhike si wajua sipendi ukae na kisununu kwa ajili yangu?Sasa ngoja nikupe mkasa uliyonisibu mie”.

    “Ehee, we ndiye Baba Hailley sasa. Haya nipe hadithi hiyo”. Aliongea Miriam kwa furaha baada ya kumuambia kuwa nitamuhadithia mkasa mzima. Nilivuta pumzi ndefu na kuishushia na funda moja la ukweli la juisi ile ya ukwaju na kuanza kumpa hadithi ile Miriam.



    HAPA NDIYO MWISHO WA MAWIO







0 comments:

Post a Comment

Blog