Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

MREMBO ALIYEPOTEA - 3

 







    Simulizi : Mrembo Aliyepotea

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Furaha kubwa bado ilikuwa imetawala ndani ya moyo wa Jamila. Alijua sasa kile alichokitaka amekimaliza. Hofu ilianza kumnyemelea taratibu mwilini mwake kwani tayari akili yake ilimtatiza kitu cha kujibu endapo wakija chumbani kwao na kumkuta Alice amekufa. Chumba chote kilikuwa ni cha Jamila kwa kuranda randa usiku wote huku akiongea peke yake.

    “..Yees..!!, Sio mimi niliyemuua.., Mwalimu na wenzangu wote ni kwamba mimi… Noo.., nooo..Hiyo siwezi embu ngoja.. Ni kwamba nililala naye usiku vizuri sasa sijui nashangaa nimeamka tu asubuhi tayari ana damu nyingi puani mwake huku kanyolewa upara.. Hapana hapa nitakosea watashtuka hii hapana.. Mwalimu ni kwamba nimeshtushwa kuamka tu nakutana na mwili wa Alice ukiwa tapatapa huku damu zimemuenea kila sehemu. Siamini sana mambo ya kishirikina lakini mwalimu inawezekana.. Yees ..! cha kujibu nimepata…”

    Muda wote Jamila alikuwa ni mtu wa kujisemesha peke yake ni kwa jinsi gani atajibu maswali endapo kutakucha. Alijijengea taswira kwanza kwa washiriki wenzake watakavyoshtuka na hilo tukio na tena ni mara ya kwanza tu limetokea tatizo. Aliwaza sana mpaka mawazo yake yakampeleka kwa wahusika wenyewe wa hoteli.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “..Mhh lakini ninaweza kuumbuka hapa kwa maana watu wa hoteli wanaweza kusema kuwa hakujawahi kutokea tatizo kama lile na nikaumbuka bure. Na je wakimpeleka kwenda kumpima hospitali alama za mikono..?”

    Sasa mwili wa Jamila ukawa kama umepigwa ganzi kwa muda. Mwili wake ulikuwa tayari umeingia barafu tena lile la baridi. Alihisi hali ya hewa imebadilika kutokea joto mpaka baridi kali. Alichukuwa ule mkasi aliotumia kumnyoa Alice kisha akautupa kwa dirishani kupoteza ushahidi na kilichofuatia aliingia bafuni na kuchukuwa kipande cha sabuni alichokuwa akifulia shuka Alice na kisha kunawa mikono vizuri. Jamila aliamini kuwa kufanya hivyo kutachangia kwa kiasi kikubwa kutojulikana kama ni yeye alihusika katika mauaji ya Alice. Alirudi mpaka kitandani kwake nakunyanyua simu yake kwa mara nyingine huku akijaribu kuipiga namba ya John lakini ikawa vile vile kama mwanzo kuwa haipatikani. Aliangalia tena ile meseji aliyoituma kama ilimfikia lakini bado ikawa inaonesha iko hewani, muda wowote endapo John akiwasha simu yake itamfikia. Kutokana na uchovu aliokuwa nao Jamila kwa vitendo alivyomfanyia Alice usiku kutwa alijikuta usingizi ukianza kumnyemelea taratibu huku macho yake yakionesha dhahiri kuzidiwa na usingizi.



    *******



    Sauti za ndege wa porini wanaoishi mjini uku zikichochewa na mbwa wa mitaani ndizo zilikuwa zikiashiria kuwa imefika Saa kumi na mbili alfajiri. Kelele za milango za kufungwa na kufunguliwa nazo ziliwaamsha baadhi ya wapangaji wa hoteli. Jamila alikuwa mmojawapo kati ya watu waliokuwa wameamka asubuhi sana. Ule usingizi ulikokuwa umemptia usiku sasa ukawa wote ukawa umekatika huku macho akiyatoa sana kumuangalia mtu wa pembeni yake.

    “..Aliice..?? Alice..??”

    Mapigo ya moyo ya Jamila yalikuwa kasi zaidi huku yakichochea jasho kutiririka sambamba na mishipa pembezoni mwa shingo yake kumtoka. Alishangaa kumshuhudia Alice akiwa kajifunika shuka vizuri pembeni yake huku akionekana hana hata tone la damu. Jamila hakutaka kuamini mpaka akamfunua shuka lote nakumshuhudia Alice akiwa bado na nywele zake zile zile huku akikoroma kuonesha yupo kweye usingizi mzito sana..

    “..Ohh..!!, This is not serious..?? (Hii si kweli kabisa..??)”

    Jamila alijaribu kumuamsha Alice kwa kumtingisha labda huenda akashtuka. Kadri alivyomuamsha Alice ndivyo na Alice alikuwa akizidi kukoroma. Akili ya Jamila ikamuahama sasa akaacha zoezi zima la kumuamsha Alice na kukimbilia moja kwa moja mpaka bafuni kukagua vizuri kama ataziona zile damu zilizokuwa zikimwagika Alice usiku. Napo alipofika alikuta bafuni kweupe tena kusafi sana tu. Alichokifanya akarudi tena kwa mara ya pili mpaka pale kitandani. Alimgusa Alice mapigo yake ya moyo lakini yalikuwa yakidunda hivyo akaanza na kumuahamsha kwa mara nyingine tena.

    “Alice my love..??, Pliizz amka tujiandae twende mazoezi.. Alice..?? Alice..??”

    Kwa kuanza na jicho moja la kushoto na kisha la pii taratibu Alice akayafumbua macho yake yaliokuwa bado yamezungukwa na limbi la usingizi huku akimtolea macho yale Jamila.

    “..Niambiae Dada yangu..”

    “..Mhh Alice unalala wewe..?? yaani nimekuhamsha muda mrefu hata huamki mwenzangu..”

    “..Nahisi nilikuwa nimechoka sana hata hivyo..?”

    “..Ok.., Ingia bafuni basi kajiandae kwani muda si mrefu mwalimu atakuja kutuhamsha huku..”

    Jamila hakutaka kabisa kuamini kama aliokuwa akiongea naye ni Alice. Mpaka pale Alice alipoamka nakuchukuwa taulo kisha akaingia bafuni tayari kwa kuoga. Mapigo ya moyo ya jamila sasa yakawa yamepungua kasi yake. Alibaki akitafakari sana ndoto mbaya ambayo ilimtokea usiku wote. Alijitahidi kurudisha kumbukumbu zake mpaka usiku mara ya mwisho walipoongozana na Jamila mpaka chumbani kisha akafungua mlango. Na Alice alikuwa wa kwanza kuingia bafuni kuoga kisha alipigana kikumbo na Alice akiwa anatoka kuoga na kile kikumbo ilikuwa ni haraka haraka za yeye kwenda kutapika kwani alijisikia kichefu chefu sana. Na baada ya kurudi kutapika alimkuta Alice ameshalala hivyo na yeye akalala na ndipo ndoto za ajabu zikaanza kumtawala usiku kucha.

    “..Mmh..?? eti nimemuua Alice jamani..? hadi alitoka na damu nyingi puani mwake.. Allah niepushe na ndoto mbaya kama hizi..!!”

    Jamila alibaki akiongea peke yake huku akiinuka na yeye kitandani nakujifunga taulo tayari kupishana na Alice akitoka kuoga na yeye aende kuoga. Na ndani ya nusu saa tayari Alice na Jamila walikuwa wameshamaliza kujiandaa. Kila mmoja alionekana kuwa na furaha kwa mara ya kwanza kuingia kambini hapo. Siri kubwa juu ya ndoto mbaya alioiota Jamila usiku ilibaki moyoni mwake. Kamwe aliapa kutomwambia Alice wala mtu yeyote kwani alijiwekea imani mara nyingi ndoto kama hizo endapo atamwambia mtu basi huenda ikatokea kweli. Sasa Jamila akawa ni mtu wa kuonesha upendo wa hali ya juu kwa Alice. Hata wakati wa kujipodoa ni Jamila pekee ndio alipendekeza Alice atumie vitu vyake. Kutokana na miili yao kuwa sawa, Jamila alitoa trakisuti yake na kumkabidhi Alice avae vivyo hiyo na Alice.

    “..Alice..??, Pliizi nakuomba tuwe na urafiki wa karibu sana..!!, na pia sipendi urafiki wetu uishie hapa kwenye haya mashindano..”

    “..Ni sawa tu Jamila, hata mie nitafurahi endapo tukaendelea kuwa karibu na nadhani hata Baba yangu atafurahi pia kusikia nina rafiki wa karibu katika haya mashindano..”

    “..Kweli..??”

    “..Yap.., Ndio Jamila..!!, kwa jinsi ninavyomjua Baba yangu alivyomchangamfu yaani atafurahi huyoo..??”

    Jamila aliguswa sana na maneno ya Alice, alitamani sana siku moja aje amuone huyo Baba yake Alice. Alijihisi sasa mtu wa kumwambia siri zake zote za maisha ni Alice pekee.

    “..Alice kuna story moja nataka nikwambiae inanihusu mimi..??”

    “..Mmh..!!, umejuaje kama napenda sana story mie..??”

    “..Unapenda..? Basi hiyo ni true story ambayo imenitokea na mpaka sasa hivi inaendelea lakini kwa kuwa wewe ni rafiki yangu wa karibu najua utanipa ushauri mzuri sana.. Sasa sijui nikuhadithie kwa sasa hivi au jioni tena tukirudi kulala..??”

    “..Basi tufanye jiioni maana najua tu hapa utanikatisha utamu kama stoy za mwandishi Andrew Carlos yule wa Facebook..!!!”

    “..Kumbe na wewe unamjua enhee..??”

    “..Yaani wee acha tu.., mie story zake zinanifanya hata nakosa hamu ya kula chakula, kila muda nakodolea macho kwenye page ya uwanja wa simulizi tu nikijua ataendelea lakini anakuja kutoa baadaye, na akitoa tena ananiacha kwenye hamu ya kutaka kujua tena kinachoendelea, lakini story zake ni nzurii..”

    Wakiwa bado katika kupiga story Alice na Jamila mara hodi ikagongwa katika mlango wao. Alice alikwenda kufungua, alikuwa ni mwalimu wao.

    “..Haya.., haya muda umefika mpo tayari wote..”

    “..Ndio mwalimu tupo tayari..!!”

    “..Haya tuongozane kwenye basi nchni kabisa kisha tunaelekea Coco beach na tukitoka hapo tunarudi kujiandaa tayari kwa kwenda kituo cha watoto yatima Dodogodogo Centre kwa ajili ya kuwapelekea zawadi watoto yatima..”

    Pilika pilika za kutwa zilianzia hapo. Alice na Jamila walliongozana pamoja mpaka chini kupanda basi. Upendo aliokuwa akionesha Jamila dhahiri utajua ni ndugu na Alice. Walikaa siti moja katika basi na mapaka wanafika Beach Jamila alikuwa pamoja na Alice katika michezo mbali mbali na hata wakati wanarudi bado walikuwa wamejitenga na wenzao huku wakipiga sana story na kucheka peke yao. Muda wakupeleka chochote kwa watoto yatima pia Alice na Jamila walikabidhiwa Ndoo ya mafuta ya kupikia ambapo waliibebelea wawili mpaka wakakabidhi. Upendo ulizidi, walikula chakula cha pamoja na wale yatima huku Jamila akifanya vituko kuwafurahisha watoto na pia Alice alikuwa pembeni yake akimuiga Jamila. mpaka jion inafika Jamila na Alice walikuwa hoi kwa siku nzima na sasa wakawa wameshamaliza kula chakula cha usiku cha pamoja na wameelekea chumbani tayari kwa ajili ya kulala.

    “..Jamila..??”

    “.Niambie..??”

    “..Sasa ndio ule muda wetu muafaka ulioniambia, unakumbuka asubuhi uliniambiaje..??”

    “..Mmh Alice husahau..?? Ok, kwakuwa tupo kitandani nitakusimulia lakini usilale bwana mpaka nitakapomaliza sawa..?”

    “..Hee..?? kwenye story hata usingizi huwa sina mwenzako..!!”

    “..Basi nikwambie Alice, kwanza kifupi Baba yangu na mie ni msukuma ila Mama ni mhehe wa Iringa. Mapenzi yangu kwao yalikuwa ni maziuri tu kwa kuwa nilikuwa mtoto pekee. Walinidekeza kwa kunipa kila nilichokuwa nikikihitaji. Lakini kwa bahati mbaya nilipofikia kidato cha tatu nikaamua kuachana na shule. Na hii yote ni kutokana na kumpenda sana Nick. Wee..?? haya mapenzi wewe yasikie tu Alice. Basi Nick akanifanya niache shule niishi naye kwenye geto lake na kwa kitendo hicho kilimkera sana Baba yangu. Alifanya kila analoweza kumzuia Nick lakini mapenzi yalizidi kwani niliamua kumwambia Baba hadharani endapo anataka kunipoteza Duniani basi aendelee kumtesa Nick wangu.. Kile kitendo kilimuuizi sana Baba yangu nakujikuta wamenitenga yeye na Mama.. Nilihangaika maisha na Nick huku nikimtegemea Nick kwa kila kitu.”

    “..Kwan Nick alikuwa akifanya kazi..?”

    “..Hapana..!!, nyumbani kwao walikuwa na uwezo hivyo akawa anapewa hela nyumbani kwao na zinanisaidia kujkimu. Siku baada ya siku Nick wangu akaanza kubadilika nakujikuta anajiingiza katika madawa ya kulevya. Nilijitahidi kumrudisha Nick katika hali yake ya zamani lakini sikuwa na ujanja kwa kuwa hela alikuwa akipewa kwao na kukimbilia kwenye madawa. Ile hali ya Nick nikajikuta sina hela hata kidogo. Sina mtegemezi tena hivyo nikaanza na mimi kutafuta pesa huku nikiendelea mahusiano ya kimapenzi na Nick wangu japo si sana. Nilitanga huku na kule huku mpaka baadhi ya rafiki zangu waliponishauri nijiingize katika kuigiza filamu za kibongo. Napo nikaambulia kutambulika tu pale Mwanza lakini nikawa natembea na wanaume tofauti kisiri siri wanaoigiza na hata wengine watengenezaji na wasambazaiji wa hizi Cd za bongo muvi huku nikijilinda kwa kutumia kinga nakumtelekeza Nick wangu.

    “Mmmh..!!, pole mwaya kwa matatizo.., sasa ikawaje Jamila rafiki..?”

    “..Basi mpaka akatokea ndugu yangu mmoja akanishauri kwakuwa nina mwili mzuri tu naweza kujiingiza katika urembo na nikashinda. Nikaanza kutafuta fomu nakuingia rasmi katika mashindano haya ya urembo. Taarifa zikamfikia mpaka Nick wangu. Nikarudiana naye japokuwa alikuwa ameshaathirika na madawa sana ila niliapa nitakuja kufunga naye ndoa siku moja kwakuwa ndio mwanaume wangu wa maisha aliyenitoa usichana wangu. Nilipokuwa bado kambini kule Mwanza kabla hatujaingia katika mashindano alinifuata Jaji mmoja kisha akaniambia kuwa endaapo nitatembea nae yuko tayari kuniweka kuwa mshindi wa kwanza na hivyo kuja huku Dar. Na pia kama nitakuwa mshindi atanipa tena na mtihani mwingine wa kumzalia mtoto. Hapa ninapokwambia zoezi la kwanza nimefanikiwa kwani nililala naye nakumpa mapenzi nayeye akanitekelezea kama nilichokitaka hivyo nikawa mshindi wa kwanza.. Tatizo kubwa nilionalo Alice.., si unakumbuka jana usiku tulipishana bafuni..??”

    “..Ndio nakumbuka Jamila..!!”

    “..Basi nilienda kutapika na hapa najisikia kichefu chefu sana na hii yote ni dalili ya mimba Alice..”

    “..Kwahiyo inamaana tayari umeshika mimba Jamila..??”

    “..Ndio tena nahisi hivyo lakini kama ni mimba basi itakuwa ni ya mpenzi wangu Nick siyo yule Jaji..!!”

    Alice alikuwa akiifuatilia story hiyo kwa masikitiko makubwa huku akionesha kutikisa kichwa kwa kumsikitikia Jamila kwa yaliomkuta na kumpa pongezi kwa hapa alipofika.

    “..Kwa huyo huyo mtu aliokupitisha ukawa mshindi alikuwa akiishi huko huko Mwanza au..?”

    “..Hapana Alice, huyu mtu anaitwa John aliniambia anaishi na kufanya kazi huku huku Dar..”

    “..nani Jamila..??”

    Alice alioneshwa kushtushwa sana na jina la John. Akili yake moja kwa moja ilimpeleka mpaka kwa Baba yake wa kufikia, John. Hakutaka kuamini kabisa kama Baba yake angeweza kuwa na tabia hizo. Mapigo yake ya moyo sasa yakawa yanaanza safari kama vile gari lililokuwa likishuka kwenye mteremko mkali. Alijihisi jasho jembamba kumtoka, huku ile hali ya usingizi ikimuishia kabisa. Muda wote alikuwa akimkodolea jicho Jamila.

    “Mhh..!!, Alice mbona umebadilika ghafla my Dear..?”

    “Hapana Jamila, embu niambie kweli wala hata usinifiche. Umesema huyo mtu anatwa nani tena..??”

    “Si Johnson lakini wamezoea kumwita John..”

    “Huyo Johnson unaosema wewe ameoa..?”

    “Mh, kwa kwa mujibu wa maneno yake mwenyewe ameniambia kuwa hajaoa ila alipata mke wakaachana naye na kwa sasa anaishi na binti mdogo yupo sekondari..”

    Alice alishusha pumzi zake huku ile hali ya jazba aliokuwa nao akiituliza kwa muda. Jamila alitambua kuwa huenda Alice atakuwa anamfahamu John au labda pengine anamahusiano naye hivyo alijipa moyo nakunyamaza kimya kutokumwambia Alice juu ya huyo John mpaka siku wakishazoena zaidi ndipo amwambie ukweli.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    *****





    Wiki moja sasa ikawa inaenda kukatika tangu warembo wote kutoka mikoani wakae pamoja kambini ndani ya hotel ya Girrafe Green View. Karibu warembo wote wakawa tayari wameshazoeana ndani ya kambi. Wengi wa warembo walikuwa pea huku kila mmoja akionekana kushibana na mwenzake. Mazoezi mbali mbali kama ya kuvuta kamba, kucheza mpira wa ufukweni na hata kutembea pamoja kwenda kwenye viwanda na taasisi mbali mbali za kusaidia jamii ni kati ya vitu vilivyokuwa vimetia fora kwa baadhi ya warembo waliokuwa pamoja. Ule urafiki wa karibu sasa ukawa umezidi kwa Jamila na Alice. Alice alimpenda sana Jamila, walisaidiana kwa kila kitu. Alimchukulia Jamila kama ndugu yake wa karibu na kupeana ahadi nyingi za kimaisha ikiwa ni pamoja na kutokuachana mpaka kufa kwao ndipo na urafiki ufe. Mawasilianao ambayo Alice alikuwa akiyafanya na Mama yake wa kufikia, Janet sasa yakawa karibu na Jamila pia. Jamila alianza kumfahamu Janet haswa kupitia simu ya kiganjani ambayo alikuwa akipewa na Alice kuzungumza naye. Janet alimchukulia Jamila kama binti mtiifu na mwenye maadili na tena aliyefunzwa kwa kila kitu na wazazi wake. Upendo wa dhati kutoka kwa Mama yake Alice,Janet ulizidi kwani ni alikuwa mtu wa kwanza kabla ya John kumtembelea Alice pale kambini na kumpelekea vitu vidogo dogo. Kamwe hakutaka kumpelekea Alice peke yake kwani kila alichokuwa amekinunua basi ni kwa Jamila na Alice. Sasa Janet akawa ndani ya geti la hoteli ya Girrafe Green View huku akiwa na kibegi kidogo kilichosheheni zawadi mbalimbali akimsubiri mlinzi aliyemuomba akawaite Jamila na Alice. Punde akamwona Alice akija peke huku ameongozana na yule yule mlinzi aliyemuagiza.

    “..Mbona unakuja peke yako mwanangu..”

    Janet alishangaa kummuona Alice akija peke yake bila ya hata huyo rafiki yake wa karibu Jamila. Alitamani sana kumuona kwani alikuwa akimsikia tu kupitia simu ya kiganjani. Alipenda zile zawadi alizoleta awakabidhi wote wawili. Zilikuwa ni zawadi za nguo ambazo aliwakadiria kwani kwa jinsi waliyomuelezea kuwa wako sawa kwa kila kitu kuanzia kiuno, mabega na maumbile mengine.

    “Mama Jamila alitoka asubuhi na mapema nikiwa nimelala. Nilivyoamka sikumuona hivyo nilivyokuja kuitwa na mlinzi nimemtafuta wee bila mafanikio yeyote nadhani ataambiwa tu nipo huku na wewe hivyo atakuja. Na kwa jinsi alivyo na hamu ya kukuona?”

    “..Haya niambie mwanangu Alice maisha ya huku yanakwendaje..?”

    “Mama nahisi nimeshayazoe japo mwanzoni yalinipa wakati mgumu. Ujue safari hii tupo wengi sana tofauti na kipindi kile cha nyuma wakati nagombea pale Chang’ombe. Na kwa sasa hivi naona Mama kutakuwa na ushindani mkubwa sana kwani kila mmoja naona anasifa za kuwa mshindi. Yaani inafika kipindi Mama hadi natamani kukata tamaa kwa jinsi ninavyoshuhudia..”

    “Sasa mwanangu hapo ndipo pa kukazana. Siku zote unapoona kuna ugumu ndipo mafanikio huja. JItahidi kujituma sana mwanagu. Kila siku nimekuwa nikikuunganisha katika maombi. Nimekuwa nikikuombe sana na ipo siku amini utashinda tu..”

    “Asante sana Mama kwa maombi yako. Na vipi Baba anaendeleaje..?”

    “Baba yako anaendelea vizuri na nimekuwa karibu naye sana juu yako. Na wala usiwe na hofu kwani mipango yote anaimalizia tu hivyo unatakiwa ujitahidi na uwadhihirishie kuwa unaweza kuwa mshindi licha ya kufanyiwa mpango na Baba yako. Hapa kaondoka asubuhi kaelekea huko kazini kwao japo jumamosi kama ya leo huwa hawaendi. Kipindi hiki huwa wanakuwa na vikao vingi sana kuhusiana na hayo hayo mashindano. kwani ameshawahi kuja hapa kukuona zaidi ya kuwasiliana na wewe..??”

    “Hapana Mama..!!, sijawahi kumuona, huwa naongea naye tena mara chache sana huku akinisisitizia nijitahidi yeye ananifanyia mpango..”

    Alice alijihisi mwili wote kumsisimka. Alitamani hiyo wiki moja iliobakia ifike haraka ili atangazwe kuwa mshindi wa mashindano haya ya mrembo wa Tanzania. Aliongea na Mama yake mambo mengi sana juu ya mambo mbalimbali anayokabilana nao humo kambini. Ile siri aliyoambiwa na Jamila alitamani sana kumhaditihia mama yake lakini aliacha kutokana nakuona kuwa haina maana yeyote kwa mama yake huyo wa kufikia, Janet.





    *******





    Tangu warembo waingie kambini kwa mara ya kwanza John alionekana mtu mwenye kuchangaanyikiwa sana. Yale mapenzi ambayo alikuwa amepewa na Jamila mara ya mwisho katika hotel ya Savoy Jijini Mwanza sasa yakawa yanajirudia katika halmashauri ya kichwa chake. Alitamani sana atafute mahali wayarudie yale mapenzi lakini ilishindikana. Mawasiliano kwake na Jamila toka wameachana pale kambini siku ya kwanza tu yalikuwa ni magumu sana japokuwa John alikuwa na namba ya simu ya Jamila na kila akimpigia alikuwa hapatikani. Kazi nyingi ikiwa ni pamoja na maandalizi makubwa kwa ajili ya kilele cha mashindano haya ya kumtafuta mrembo wa Tanzania ndiyo yalimuongezea kumuweka John bize. Muda mwingine kuacha kabisa kupiga simu kwa Jamila huku mawazo yake akiyaelekeza kwenye u bize ambao atakuwa nao huko kambini Jamila. Kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele ndipo na akili ya John ailikuwa ikiharibika zaidi. Sasa wiki ikawa imeshatika bila ya John kumuona wala kumsikia Jamila.

    Wakati huo Jamila hakuumia sana kwa mapenzi ya John kwakuwa lengo lake lilikuwa ni kupata ushindi tu katika mashindano makubwa ya mrembo wa Tanzania. Siri kubwa mbili ambazo alikuwa amezitunza Jamila katika ubongo wake zilikuwa zikimuumiza sana. Siri ya kwanza ni mimba changa ambayo anayo na mhusika siye John bali ni mpenzi wake Nick aliokuwa akipendana naye sana japokuwa Nick aliharibiwa na madawa ya kulevya. Siri ya pili iliokuwa ikisumbua Jamila ni kuwa alishagundua kuwa Alice na John ni mtu na Baba yake sasa siri hiyo ikawa imejificha ndani ya moyo wake kwa kuizima simu yake nakuificha ili Alice asije akajua chochote. Wiki moja iliyokuwa imebaki ndio ilihamsha hisia tofauti kwa Jamila ambaye alikuwa sasa mawazo yake yote ni kuwasha simu yake na kumshawishi John aanze kuandaa mipango yote juu ya ushindi wake huo. Alidamka asubuhi na mapema kisha akaichukuwa simu yake nakumuacha Alice akiwa kapitiwa na usingizi halafu akatoka nje na kutafuta eneo lililokuwa kimya nakuwasha simu yake tayari kwa kumpigia John.

    “..Hellow my love..”

    “Jamila..? hata siamini..!!, unapatikana baby..? najua uko bize hapo kambini, lakini hata kunitafuta..??”

    “..Unajua nini mpenzi wangu, ni kweli nakuwa bize lakini saa nyingine nakosa hata muda wa kupiga simu na hapa ninavyokwambia tangu tumeachana sijaiwasha hata simu yangu kuwapigia nyumbani wala wewe mpaka hii leo.. Niambie sasa mpenzi wangu mipango yetu inaendaje..??”

    “..Kwa hilo usijali lakini nahitaji nilale na wewe tena nimekukumbuka sana na ninayamiss mapenzi yako.. fanya basi tuonane hata kama ni leo nipo tayari..??”

    “..mpenzi hilo wala usijali, lakini nina habari njema sana kwako..”

    “Mbona unanishtua inamaana tayari..?”

    “Tayari John, Tayari kweli, wee mwanaume mbegu zako hatari..??, hapa unaponiona naogopa kila muda nakimbia bafuni kutapika na kwa ushuhuda ngoja nije kutapika huko huko..?”

    “Kweli Jamila..”

    “Ndio, hapa unaponiona nina mimba nadhani ya wiki maana hicho kichefuchefu mpenzi wangu..??”

    Furaha ya ajabu ikaanza kujijenga ndani ya moyo wa John. Siku hiyo hiyo akawahi sana kudanganya ofisini kwao japo kulikuwa na kikao cha dharula kinachoendelea. Kwakuwa ilikuwa jumamosi na hakukuwa na foleni sana walipeana miadi na Jamila akatoroka pale kambini nakukutana naye hoteli ya Desert Palm iliopo sinza. Walifika kwenye hoteli asubuhi sana huku John akiwa na shauku ya kuufunua mwili wa Jamila kwa mara ya pili. Walifanya maongezi ya haraka haraka huku John akioneshwa kuufurahia kuuona mwili wa Jamila vilivyo. Ile hali ya kichefu chefu ilimtokea tena Jamila akiwa hotelini na John. Alitapika sana mule mule chumbani hali iliyompa faraja sana John na kusababisha kusisimka mwili wote. John sasa akaona ile ndoto yake ya siku nyingi juu ya kupata mtoto imetimia.

    “.. Sasa Jamila hesabu kuwa wewe ni mshindi wa mashindano haya ya mrembo wa Tanzania. Na kwa kuthibitishia hayo leo nahakikisha tukiachana naenda kuharibu akaunti yangu benki yote na kuwahonga majaji watakaokuwa wanaendesha shughuli yote. Nakupenda sana Jamila na nitunzie mtoto wangu kwani baada ya mashindano tayari nimekutafutia nyumba ambayo inakusubiri tu ufike nakuanza kuishi wewe na mwanangu huyo alioko tumboni..”

    “Asante mpenzi wangu, nakupenda pia. Wewe ndio kila kitu kwangu mpenzi wangu.. nikwambie kitu..?”

    “Niambie tu mpenzi wangu wewe ni kila kitu kwangu..”

    “Huwa mwenzio nakumiss sana, natamani niwe na wewe popote utakapoenda..”

    “Usijali mpenzi wangu..”

    John aliendelea kuongea kwa sauti ya chini chini na ya kimahaba huku akifungua pochi yake na kutoa picha yake ndogo ‘passpot size’ nakumpa Jamila.

    “hii nakuomba uhifadhi katika pochi yako ya kuwekea hela. Pliiz..!! ichunge sana asione mtu yeyote zaidi ya wewe kila unaponikumbuka..”

    “Asante my baby, mwaaaah..!!!”

    Jamila alionesha furaha feki huku akiibusu ile picha na kisha kuiweka kwenye pochi yake ya kuhifadhia hela kama alivyoambiwa na John. Ndani ya masaa mawili yalimtosha kabisa John kulala na Jamila pale hotelini kwa muda mfupi. Hela nyingi ambazo alikuwa amelipia John kwa kulala kwa muda mfupi na Jamila kisha kufanya naye mapenzi kwake hazikusikitikia zaidi ya kuwa na furaha juu ya mapenzi aliyopewa. Aliongozana na Jamila pale kwenda kwenye gari yake kisha wakapitia kwenye duka kubwa la nguo nakununuliwa nguo mbili tatu alizokuwa anazipenda. Baada ya hapo John alimsogeza Jamila mpaka karibia na hoteli ya Girrafe Green View ambapo ndipo kuliwekwa kambi yao Jamila ya miss Tanzania. Jamila alishuka ndani ya gari huku mkono mmoja kashikilia mfuko mkubwa uliokuwa na nguo zake alizonunuliwa na John na mkono wa pili ukiwa na pochi yake kubwa ya kuwekea hela. Sasa macho yake yakawa yamefika mpaka pale getini kwa mlinzi huku akimshuhudia Alice akiwa na Mmama ambaye hakumfahamu. Halmashauri yake ya kichwa chake ikafanya kazi kwa haraka mpaka akamgundua kuwa ni Mama yake na Alice kwani aliambiwa na Alice usiku kuwa atakuja asubuhi kuwatembelea. Jamila alitengeneza furaha ya ajabu iliyokuwa imepambwa na tabasamu feki huku akikaribia mpaka eneo lile la getini.

    “Jamila jamani waoooh..!! ulikuwa wapi shosti nimekutafuta mwenzio mpaka nimechoka na hapa unapoona ndio kwanza tulikuwa tunaagana na Mama yangu anataka kuondoka..”

    “..Mmhm..!!, mwenzangu si unajua tena kuna vitu nilienda kuchukuwa na niliona kukuhamsha asubuhi asubuhi haitakuwa vizuri kwani ni kwenda na kurudi na hata hivyo nilitoroka tu, vipi mwalimu hajaniulizia..?”

    “Hata hajakuulizia, si unajua leo jumamosi hivyo tunaachwa mpaka muda wa saa tano ndio tumeambiwa tutajikusanya tena tuwe pamoja kwa safari yeyote..”

    Ile furaha feki ambayo bado aliionesha Jamila sasa akailelekezea kwa Mama yake na Alice. Alimkumbatia kwa hisia zote huku akimpa maneno mazuri.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mama, tulikuwa tukikukumbuka sana na Alice. Na siku zote nilitamani sana nikujue Mama yangu kumbe ni wewe. Ujue kuongea kwenye simu peke yake hakutoshi Mama yangu sasa leo nimekujua na ukarimu wako. Asante kwa kuja kututembelea, karibu sana Mama..”

    “Asante sana mwanangu. Alice kaniambia mengi sana jinsi upendo wenu ulivyo. Nafarijika sana kuwa na wanangu karibu, cha msingi mfanikishe malengo yenu..”

    Mama yake wa kufikia na Alice, Janet alikuwa bado akiongea na Jamila. Muda wote Alice alikuwa bize pembeni yao akishangaa zile nguo ambazo Jamila amekuja nazo. Yale mazoea yao ya kuvaliana nguo sasa yakawa yamejijenga akilini mwa Alice, Alice alizitamani sana zile nguo nzuri alizokuja nazo Jamila. Aliziangalia mara mbili mbili huku akiendelea kukagua vitu vingine alivyokuja navyo Jamila. Na sasa alikuwa ameishika ile pochi ya Jamila akiikagua ndani yake.

    “..Jamila..?? , Jamilaaaaaaaaaaa..?”

     Alice alijikuta anadondosha ule mfuko pamoja na pochi mpaka chini huku mikono yake miwili akiielekeza katika mdomo wake. Alijihisi kasoro katika mwili wake. Uso wake ukawa tayari umeshabadilika huku ile mikunjo ya hasira ikichukuwa nafasi yake katika paji lake la uso. Alimuangalia Mama yake wa kufikia,Janet mara mbili mbili huku akishindwa kujiamanini kwa alichokishuhudia muda si mrefu. Alihamisha macho yake na kwa sasa akawa anamtizama Jamila ambaye hakugundua kitu chochote kinachoendelea. Mwili wa Jamila ukawa kama umemwagiwa na maji ama kunyeshewa na mvua, tena ile mvua yam awe. Alijihisi mwili kumtetemeka sana kwa kile alichokishuhudia na yeye. Ile sauti ya ukali iliokuwa ikilitaja jina lake sasa ikawa inamsogelea. Mwanzoni alijihisi huenda akawa ni Alice anamwita lakini akili na masikio yake yakaweza kutofautisha sauti ya Alice na ile iliokuwa inamwita. Ilikuwa ni sauti ya kiume ambayo bado ilikuwa ikiendelea kumwita. Jamila akaangalia pembeni yake huku akimwangalia mlinzi lakini akagundua naye si mlinzi aliyekuwa anamwita kutokana na yule mlinzi kuwa bize na kitabu cha ofisini akiandika.

    “Hapa mnafanya nini..?”

    Sasa ile sauti ikawa karibu na imeshaingia ndani ya masikio ya Alice pamoja na Jamila. Alikuwa ni mwalimu wao wa kambini. Kamwe alikuwa hapendi kuona washiriki wakijitenga na wenzao ama kutoroka. Alikuwa mkali sana na hata Jamila na Alice walikuwa wakijitahidi kutokufanya makosa mbele ya mwallimu wao huyo.

    “Hapa mnafanyaje nauliza..? Hapa ndio kambini..??”

    “Hapana mwalimu ni kwamba….”

    “Sitaki kusikia habari za kwama hapa..??”

    Yule mwalimu aliendelea kuwa mkali hali iliyowafanya Jamila na Aliice wajihisi kweli wanamakosa. Sasa Mama yake Alice akaingilia kati.

    “Samahani sana mwalimu, kwanza za saa hizi..?”

    “Salama tu..!!”

    “Nakuomba nikuombe msamaha mimi kwa niaba yao kwani mwenye makosa zaidi ni mimi hapa Mama yao. Na sikuwa nafahamu utaratibu wa hapa japo..”

    Akiwa katika kumjibu mwalimu wao huku akionesha kutetemeka. Alishangaa kukonyezwa na mlinzi wa zamu pembeni yake ambaye naye alihusika kwenda kumuita Alice kutokana na kukubali kuhongwa kiasi kidogo cha hela ambacho alikipokea kutoka kwa Mama yake na Alice.

    “Ndio hivyo mwalimu..”

    Mama yake alice aliamua kukatisha maongezi huku akimtolea macho mwalimu kujua atasemaje.

    “Ujue Mama. Hapa tumejenga utaratibu kwamba warembo wote wanaoingia hapa kambini si ruhusa kutoka. Lakini kutokana na maelezo yako na msamaha kawa kutokujua .Nimekuelewa hivyo nakuomba sana mzazi mwenzangu usije ukarudia tena…”

    “Sawa nashukuru kwa kunielewa mwalimu. Alice na Jamila mie naona niende..”

    “Sawa Mama msalime sana Baba ..”

    Waliongea kwa pamoja Alice na Jamila huku wakimwacha Mama yao akiondoka na wao kubaki na mwalimu wakirudi kambini.



    **************



    Taarifa juu ya mrembo aliyeshinda taji la Chang’ombe Alice Majaliwa mpaka kuingia kambini sasa ikawa imechukuwa sura mpya kichwani kwa Baba yake halisi Alice,Majaliwa pamoja na mkewe Juliana. Picha mbali mbali kupitia magazeti na hata habari kutoka kwa majirani waliokuwa wakiishi nao waliweza kuzitembeza taarifa mpaka kuwafikia moja kwa moja. Ingawa Mama yake halisi na Alice, Juliana alipigwa sana na mumewe kipindi cha nyuma wakati bado wanaishi na Alice hali iliyompelekea Mama huyo kutoroka na kumuacha Alice akiwa bado mdogo na baba yake nakufanyiwa vitendo vibaya vya kubakwa na mzee wake mpaka kufikia hatua ya Alice kumtoroka Baba yake akiwa bado mdogo nakutokomea kusikojulikana. Na sasa Mama yake halisi Alice,Juliana alikuwa wa kwanza kurudisha moyo kwa kurudi nyumbani kwake baada ya kuvumilia sana kwa kipindi cha mwezi mmoj na nusu akiwa kijijini kwao Kondoa. Alirudi nyumbani kwake kwa lengo moja tu nalo ni kuishi ama kumchukuwa na mwanae Alice. Alihuzunika sana baada ya kukuta Alice katoroka na kumuacha Baba yake akiwa katika hali mbaya ya kuishiwa nguvu kwa kutokula kwa siku tano. Tumbo lake lilikuwa limejaa pombe kali zile za kienyeji. Juliana hakuwa na kazi yeyote lakini kupitia kwa majirani na wasamalia wema alifanikiwa kumtibu mumewe mpaka akawa katika hali yake japokuwa tayari mwili wake Majaliwa ulikuwa katika hatari kutokana na kuingiliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi. Maisha yalizidi kuwa magumu zaidi. Baadhi ya majirani wakashauri wamtafute mtoto wao huenda wakapata msaada wowote kutoka kwake. Siku, wiki mpaka miezi ikakatika kwa kuhaha bila kuwa na dalili zozote za kumpata Alice kutokana na Jiji la Dar es salaam kuwa kubwa sana. Hatimaye baada ya kuhangaika kwa muda mrefu bila kuambulia chochote wakafanikiwa kuelekezwa ofisi za waratibu wa mashindano ya miss Tanzania. Walianzia safari yao ya kutoka Tandale kwa mtogole walipokuwa wakiishi kwa mguu mpaka Posta zilipo ofisi na kwabahati wakamkuta mlinzi ambaye aliwaelekeza moja kwa moja ofisini. Walimkuta mwakilishi mmoja wapo akiwa bado yupo ofisini na si mwingine bali alikuwa ni John Mapunda.

    “Samahani Baba eti hapa ndio ofisi za wale wanaoshiriki mashindano ya miss Tanzania..??”

    Majaliwa alijikaza na kumuuliza John kwa sauti ya upole huku kifua kikimbana kwa kukohoa. John aliwaangalia mara mbili mbili kwa jicho la dharau.

    “Ni nani kawaelekeza mje hapa..?? Hapa hatutoi msaada wa aina yeyote zaidi ya kujishughulisha na maswala ya urembo, kwani hamjaelekezwa hapo chini mapokezi..??”

    ”hapana Baba, hapo mapokezi hatukumuona mtu na ni mlinzi ndio katuelekeza hapa moja kwa moja. Sisi hatupo hapa kwa ajili ya msaada wa kifedha. Tupo hapa kwa shida moja tu..??”



    “shida gani..? wakati naona kabisa sura zenu zimekaa na ugonjwa . Maana namuona hata huyo mzee kababuka mwili wote huku kashikilia bahasha kubwa sijui ndio mafaili ya hospitali..?? Muwe waelewa hapa siyo hospitali jamani..? Na mlinzi yupi amewaruhusu nyie watu msiye na akili ya kufikiria..??”

    Hasira sasa zikawa zimempanda John na kuinuka katika kile kiti alichokuwa amekikalia huku akiinuka na kuranda randa mule ofisini. Alijua fika kuwa wanahitaji msaada tu wa kifedha kutikana na hali zao walizokuja nazo kuanzia miili yao mpaka mavazi. Juliana alikuwa amevaa khanga zilizopauka na kuchanika huku mumewe, Majaliwa akiwa katika vazi lenye rangi ya kahawia lililoshonwa shonwa kila pembe huku likiwa halina kola kabisa.

    “Baba sisi ni wazazi wa Alice majaliwa. Mimi ni Baba yake mzazi, naitwa Majaliwa.. Na tupo hapa kwa ajili ya kuonana na mwanetu Alice twende naye nyumbani..”

    John alipigwa na butwaa kwa muda. Hakutaka kabisa kuamini maneno yale. Kwanza kutokana nakujua kuwa Alice na marehemu Angel walikuwa mtu na mdogo wake na wala hawakuwa na wazazi na ndio maana Angel alizikwa chini ya manispaa. John aliendelea kukaa kimya kwa takribani dakika tano nzima huku akiendelea kuwatolea macho wazazi halisi wa Alice. Baba halisi wa Alice, Majaliwa alionekana kukasirika sana kwa kudhalilishwa kuwa ni omba omba. Aliitoa bahasha aliokuwa ameishika kisha akachomoa picha ndogo iliokuwa ikimuonesha Alice akiwa amebebwa na Baba yake huyo enzi za utoto huku pembeni yake akiwa mkewe, Juliana kisha ile picha akaiweka mezani kwa John kuhakikisha kuwa wao ni wazazi halisi wa Alice.

    “Alice mwenyewe huyu hapa Baba. Embu tunakuomba sana utuelekeze yupo wapi kwa sasa..?”

    John alibaki na kigugumizi kwa alichokiona kupitia ile picha. Ni kweli alikuwa Alice yule aliyemfahamu. Yule alice ambaye alimchukulia kama mtoto wake wa kufikia. Aliyeishi naye kwa muda mrefu tangu Angel afariki.

    “Embu niwaulize kitu wazee wangu..? Hivi mnajua Angel alipo..?”

    “Baba, sisi huyo Angel wala hatumjui kabisa. Sisi ni wazazi wa Alice ambaye unamuona katika hiyo picha..”

    “Sawa nimewaelewa. Ni kwamba hivi ninavyoonge leo ndio kilele cha mashindano haya ya miss Tanzania ambayo yatafanyika ukumbi wa Diamond Jubilee pale upanga. Kwa sasa hamtaweza kumuona huyo Alice mpaka mashindano yaishe usiku. Hivyo cha kuwasaidia tukutane wote usiku pale Diamond Jubilee kuanzia saa mbili..”

    “Ndio wapi huko baba..??”

    “Hampajui..? kwani nyie mnaishi wapi..?”

    “Baba sie tupo tunaishi Tandale kwa Mtogole na hapa unapotuona tumekuja mjiini kwa miguu kwani hata nauli yenyewe kwetu ni shida Baba..!!”

    “Sasa cha kuwasaidia hapa naondoka muda huu kwenda kwangu hivyo nitawapitisha hapo ukumbini mchana huu na itawabidi mpaka muda wa mashindano saa mbili usiku ufike. Kuhusu kuingia ukumbini msijali nitawasaidia kuingia na kuwatafutia sehemu nzuri tu ya kukaa wote wawili kwa kuwa hamna uwezo wa kulipia kiingilio..”

    Katika maisha ya John kamwe hakupenda kuwasaidia watu ambao hawana uwezo. Roho mbaya na ya kikatili aliyoumbiwa nayo sasa ikawa inajionesha kwa wazazi halisi wa Alice. Alijitahidi kuvumilia kwa kuwapakiza kwenye gari lake na kisha kuwapitisha mpaka hapo ukumbi wa Diamond Jubilee. Halafu yeye akaelekea kwake kujiandaa. Njia nzima ilikuwa ni ya ushindi kwa John. Furaha yake kubwa ilikuwa ni kwa Jamila ambaye alikuwa akimuumiza kichwa endapo akimpa ushindi, Alice atachukuliaje.

    “Asante sana Mungu kwa kunionesha njia. Alice achukuliwe tu na wazazi wake akaishi nao. Nashukuru mipango yangu sasa imekamilika na tayari nimewahonga majaji wote na hivyo namsubiria kwa hamu Jamila wangu kuwa mshindi usiku wa leo.”



    *************



    Ule urafiki ambao ulijijenga toka siku ya kwanza walipoingia kambini kati ya Jamila na Alice sasa ukawa umevunjika rasmi. Japo walikuwa wanakaa chumba kimoja lakini sasa wakageuka kuwa maadui kama vile chui na paka. Ni jamila ndio aliovunja uhusiano rasmi ambao ulikuwa ni wa kufa na kuzikana kati yao. Ilikuwa ni siku moja kabla hakujafikia kilele cha mashindano ya kumtafuta mrembo wa Tanzania. Dharau na kejeli kutoka kwa Jamila zilimchefua sana Alice. Jamila alijivunia kutembea na Baba yake Alice japo alitambua kuwa ni Baba yake mzazi halisi. Ile ahadi ambayo Jamila aliahidiwa kutoka kwa John kuwa mshindi wa kwanza katika mashindano ya mrembo wa Tanzania sasa ikawa imemuingia vilivyo masikioni mwa Alice. Alice alijiona mkosaji duniani. Aliumia sana moyo. Machozii mengi ya hasira yaliokuwa yakimtiririka mithili ya maji yanaofuata mkondo sasa yakawa yamesalimiana na sakafu yote. Nusu ya sakafu ilienea machozi ya Alice. Usiku kutwa alikuwa hana furaha wala kuamini kama Jamila angeweza kumgeuka na kutembea na Baba yake. Kumbukumbu zake zilimrudisha mbali sana toka alipoachwa na Dada yake wa kufikia marehemu Angel. Ndipo akamjua rasmi Baba yake wa kufikia, John. John alimuhaidi kumpenda kwa njia zote na kumfanya kuwa na furaha wakati wote. Tabasamu likaanza kutawala tena katika nyuso yake huku kumbukumbu zikimleta mpaka kwenye tukio alilofanyiwa na Baba yake huyo wa kufikia, John. Tukio la yeye kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya mrembo wa Chang’ombe lilimfariji. Kitendo cha yeye kutangazwa mshindi wa kwanza na kuzawadiwa nyumba pamoja na kiasi cha shilingi milioni mbili. Alijikuta yale maumivu yakipozwa na hilo tukio huku akiwa bado kwenye kona ya kitanda amesimama akimuangalia Jamila. Alijikuta hasira inamrudia tena kwa mara ya pili. Sasa akawa anaongea peke yake huku Jamila kapitiwa na usingizi hajitambui.

    “Baba kweli furaha yangu ulioniahidi ndio hii..?? Kwanini umeamua kunifanyia hivi Baba yangu..?”

    Uvumilivu wa wiki nzima aliokuwa akivumilia sasa ukawa umefikia tamati. Alice alijikuta akichukuwa simu yake nakuanza kubonyeza namba za simu kumpigia Baba yake wa kufikia,John. Simu iliita sana bila kupokelewa. Alijaribu zaidi ya mara tano lakini haikupokelewa. Halmashauri ya kichwa chake ikapambanua nakuamua kumpigia simu Mama yake wa kufikia, Janet. Akapokea ile simu.

    “Mama..??, najua wewe ni mzima tu wa afya..!!”

    “Vipi tena mwanangu kwani kuna nini..??”

    “Mama..?? Baba yangu uko naye usiku huu..??”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndio niko naye hapa kalala..!!”

    “Pliiz mama..!!, tena pliiz..!! embu nipe niongee naye..?”

    “Hapana mwanangu hata mimi ni mzazi wako waweza kuniambia tu. Tuliza kwanza hizo jazba ulizonazo kisha niambie nini kimekusibu mpaka unapiga simu usiku huu tena ukiwa katika hasira..?”

    Janet alioonesha kushtushwa sana na na ile simu iliopigwa na alice usiku. Katu hakuwahi kumsikia Alice akipiga simu usiku wa manane tena akiwa katika hali ya jazba. Pia Alice huwa hana tabia sana ya kumpigia simu baba yake zaidi ya kupitia kwanza kwa Mama yake hata kama anashida. Alichokifanya Janet, aliiweka simu yake sauti ya juu kisha akamuamsha mumewe apokee ile simu. Kwa usingizi ambao ulikuwa umemtawala John, alishtuka huku akiwa hajitambui vizuri nakupokea ile simu.

    “Enh hujambo mwanangu..??, vipi usiku huu nini tena..?”

    “Nakupenda sana Baba yangu. Najua unajua kesho ndio kilele cha mashindano yetu Baba. Nakuomba niwe mshindi nakuomba sana Baba yangu..”

    Alice alijikuta akiishiwa nguvu nakuongea maneno ambayo hakuyapangilia vizuri katika akili yake. Lengo lake kubwa ni kumwambia ukweli juu ya Jamila kuwa mimba aliokua nayo Jamila si ya kwake kama anavyodhania.

    “Mwanangu..?, kesho jitahiidi sana na tayari nimeandaa ushindi utaenda kwako..”

    Hasira kali zikamzidia Alice nakujikuta akiikata ile simu. Alikuwa ameshachoshwa na uongo wa Baba yake huyo wa kufikia, John. Aliona anadanganywa wakati ushahidi anao kwa Jamila. Alijikuta kile kidonda chake cha moyo kikizidi kuuma. Alichokifanya aliizima simu yake kisha akaenda moja kwa moja kwenye kabati la vipodozi. Kabati ambalo lilitawaliwa na vipodozi vyake na vya jamila. Aliichukua chupa ya paffyumu yake ambayo Jamila alikuwa akiipenda sana kisha akaipasua chini nakubakiwa na kipande cha chupa chenye ncha kali. Alisogelea mpaka eneo la kitanda pembeni kabisa alipokuwa amelala Jamila fofofo na kisha akauchukuwa mto na kumfunika nao Jamila usoni mpaka maeneo ya mdomoni. Jamila alitapatapa sana lakini kutokana na nguvu za hasira alizokuwa nazo Alice alijikuta akiuchukua mkono wake uliokuwa na kile kipande cha chupa nakukipeleka mpaka tumboni mwa jamila nakumchoma nacho. Alirudia hivyo hivyo kama mara tatu kuingiza tumboni na kutoa huku mkono mmoja akiwa na mto uliomziba Jamila uso na mdomo asiweze kutoa makelele.

    “Ehh mungu Baba nisamehe imenibidi kufanya hivi..!!”

    Alice alijikuta amejawa na ukatili kwa muda mfupi. Ule ukatili aliouchukia katika maisha yake sasa ukawa umemvaa. Tayari alikuwa ameshamaliza zoezi zima la kumchoma choma Jamila na kile kipande cha chupa katika tumbo. Jamila alikuwa ameshaaga dunia. Damu nyingi zilimtiririka puani mwake huku zikisambaa kupitia kwenye kitanda kilichokuwa kimetawala kwa mashuka meupe. Mwili wake ukaanza kubadilika rangi taratibu nakuwa nyeusi iliyochanganyikana na kijani. Ujasiri wa hali ya juu ukazidi kumtawala Alice. Alichukuwa shuka nakumfuta zile damu huku akichukuwa na shuka jingine kumfunikia taratibu kisha akauburuta mwili wa Jamila mpaka chooni na kumlaza katika sinki la kuogea. Alitoka chooni na kuufunga mlango kwa funguo ambayo ilikuwa ikining’inia mlangoni toka siku ya kwanza walipokabidhiwa chumba. Kimoyo moyo alishangilia kurejesha furaha yake ambayo ilitoka moyoni mwake kwa muda wa wiki nzima. Ile ndoto yake ya kuwa mrembo na kulitangaza taifa sasa ikawa imerejea rasmi katika kichwa chake.

    “Liwalo na liwe..!!, pumzika kwa amani Jamila. Najua ulitamani uwe mshindi kwa siku ya kesho lakini imenibidi kukuwahi kabla yangu..”

    Alice aliongea kwa sauti ya upole na ya kihuzini huku akiutupa ule ufunguo kupitia dirishani. Alitandika kitanda vizuri na wala hakutaka kulala tena zaidi ya kusubiri mpaka alfajiri itimie. Mpaka inafika alfajiri, Alice hakuwa na dalili yoyote ya woga wala usingizi katika paji la uso wake. Zoezi kubwa la kumuua Jamila alilofanya usiku wala halikumchosha zaidi ya kumpa nguvu zaidi.



    *******





    Asubuhi na mapema warembo wote walikusanyika pamoja kwa ajili ya kupata kifungua kinywa. Kila mrembo alionekana kuwa na wasiwasi kutokana n kufika kilele cha siku ya mwisho ya mashindano. Ile hamu ya chai iiwakuta warembo wachache huku wengi wao wakiiona chai chungu nakufikiria ushindi kwa usiku. Maswali ya papo kwa hapo ambayo warembo walijizoesha kumsumbua mwalimu wao kwa kumuuliza sasa wakaw hawataki tena kumuuliza zaidi ya kila mmoja kuyakremisha huku wengine wakiranda randa huku na kule ili mradi muda uende. Masaa kumi yalitosha sana kwa warembo kukaa pale katika hotel ya Girrafe Green View. Tayari giza lilikuwa likianza kutanda. Kila mrembo alikuwa tayari na mavazi ya usiku huo. Mavazi ya usiku, ya ufukweni na hata mavazi ya asili ndio yalikuwa mikononi mwa warembo wote. Alice alijikaza huku akishikilia mavazi mawili ya kwake na ya Jamila mikononi. Mwalimu wao aliyapitia moja baada ya jingine lakini alipofika kwa Alice alishangaa kumuona Alice akiwa na mavazi mawili mawili.

    “Mwenzako Jamila yupo wapi..??”

    Alihoji mwalimu yule wa warembo ambaye alimjua fika Jamila. Na wiki moja ya mwisho alikuwa akikwaruzana sana na Jamila kwa kutoroka huku akimpa onyo kila mara.

    “Hayupo mwalimu. Aliondoka jana usiku , lakini kaniambia atakuja tu hivyo niki..”

    Kabla Alice hajamalizia kujitetea alishangaa mwalimu wake huyo akidakia.

    “Embu lete hapa hizo nguo zake, lete..?? Tena mpumbavu kabisa. Yaani anakupa wewe kwa hiyo yeye hashiriki..? tena nimeshachoka na tabia zake sitaki tena kumsikia na akija aje aripoti kwangu na leo nitahakikisha hapandi jukwaani.. Wenzake wote wamefuata hapa mashindano yeye amefuata mashindano mengine. Sasa leo atalia nakurudi kwao Mwanza bila taji lolote..!!”

    Aliendelea kuongea yule mwalimu huku hasira kali zikimzidia kwa kitendo cha kuambiwa na Alice kuwa Jamila katoroka. Kila mmoja alishika mavazi yake nakupeleka mpaka kwenye basi lao. Zoezi liliofuata ni kukusanya funguo zote nakuziwasilisha kwa mwalimu wao kisha zikapelekwa moja kwa moja kwa meneja wa hoteli. Hali ya woga ikajirudi nakuanza kumtembelea tena Alice. Alijihisi huenda wakapita kukagua chumba kimoja baada ya kingine.

    “Najua nitaaibika tu nakupelekwa gerezani.., Na ndio mwisho wangu..,E eeh mwenyezi Mungu nisaidie..!!”

    Yule mwalimu alifanikiwa kuzikusanya funguo za vyumba vyote kutoka kwa wale warembo. Sasa akawaamuru warembo wote watangulie kwenye basi tayari kuelekea kwenye ukumbi. Muda wote Alice alikuwa akishindwa kuingia kwenye basi huku macho yake yote akiyaelekeza kwa mwalimu wake yule mpaka aliposimama na meneja wa ile hoteli. Alijitahidi kuangalia kwa makini japo hakusikia wanachoongea lakini wakiwa katika hali ya kukabidhiana ufunguo kati ya mwalimu na meneja mara yule mwalimu akawa kama anakitu amesahau, nakutoa sauti kali.

    “Alice..???, Aliceeeeee…??????”



     Mwili wa Alice ukawa kama umepigwa ganzi. Kile kitendo cha kuitwa na mwalimu wake kwa mbali kwake kikawa kama mtu aliyewekewa headphone masikioni. Akawa akiangaza tu kuwaangalia bila ya kuweza kusikia chochote.

    “we Alice si unaitwa kule na mwalimu..??”

    Mpaka mmoja kati ya washiriki wenzake alipomshtua kutokea kwenye basi Alice kuwa anaitwa ndipo akashtukaa.

    “Nani ananiita..?”

    “Kwani wewe humuoni mwalimu kule anakuita. Embu fanya haraka uende ili tuondoke..?”

    Yule mshiriki mwenzake alizidi kumsisitizia Alice aende. Alice akajihisi mapigo ya moyo kubadili uelekeo. Akili yake yote ikamuhama. Mawazo yake yakamrudisha mpaka usiku wake alipofanya lile tukio la kumuua Jamila kwa kutumia mto na chupa yenye ncha kali. Alijua ni wazi anachoitiwa huenda ni tatizo hilo hilo wameligundua.

    “Sio mimi..!! Sio mimi..!! Sio mimi..!!”

    Maneno mawili yakamkaa kichwani Alice huku akiongoza peke yake kuelekea walipo mwalimu na yule meneja huku akiyanena na kuyahifadhi akilini mwake. Hatua zaidi ya kumi na sita zilitosha kwa Alice kutoka lile aneo alilokuwapo mpaka kufikia sehemu waliposimama mwalimu wake na meneja wa hoteli ya Giraffe Green View.

    “Alice, nimekuita hapa kwa shida moja tu..?? Ni kwamba hapa tulipo mpaka sasa kuna pesa ambazo hawajamaliziwa wahusika waliotuhifadhi kwa muda wote huu toka tupo hapa kambini. Nimeshawapigia simu wanakuja hivyo itanibidi mimi kubaki mpaka watakapokuja hawa wenzangu ndipo tumalizane nao kwa kuwalipa kiasi kilicho baki. Sasa kwakuwa nakuamini wewe unafaa kuwa kiongozi kwenye msafara. Nakuomba uongozane na wenzako mpaka kambini na mkifika mtakutana na mwalimu Jacky si unamjua..?”

    “Sio mimi..!!, Sio mimi..!!”

    Alice akajibu jibu ambalo alikuwa ameliweka kichwani mwake huku akitetemeka. Kumbe muda wote ambao mwalimu alikuwa akimuelewesha Alice. Mawazo yake hayakuwa hapo. Mawazo yake bado yalikuwa mgando. Yalikuwa mgando kwa maneno mawili tu ambayo yalimkaa kichwani. ‘Sio mimi’.

    “Alice unanielewa nilichokumbia..? hiyo sio mimi unamaanisha nini enhh…? Embu fanya uende nao hao wenzako sawa..”

    “Sawa mwalimu..”

    Alice alishtuka na kujibu. Akakimbia mbio mpaka kwenye basi kisha akamuamuru dereva waondoke na safari ya kuelekea ukumbi mkubwa Dar Es Salaam, Diamond Jubilee ikaanza.



    ******



    Magari ya kifahari takribani ya thelathini yakawa yamepaki nje ya ukumbi wa Diamond Jubilee. Ukumbi ambao unauwezo wa kuingiza zaidi ya watu mia nane. Ukumbi ambao hutumiwa na watu wenye pesa zao kwa matamasha mbali mbali ya kidini na hata ya kijamii. Watu maarufu pia hupenda kuutumia ukumbi huu kwa shughuli zao binafsi. Muda wa saa moja na nusu usiku ukumbi ukawa umeshafurika zaidi ya watu mia tano huku wengine wakiwa mlangoni kwa kupita kutokana na foleni kuwa kubwa. Ni fainali ya mashindano ya kumtafuta mrembo wa Tanzania ambaye ataiwakilisha vilivyo Tanzania katika mashindano ya Dunia ndio sababu kubwa ya kujaa kwa watu huku kila mmoja akiwa na shauku ya kushuhudia mashindano hayo ni nani ataiwakilisha Tanzania. Pilika pilika za baadhi ya waandaaji huku na kule kuhakikisha kila mmoja anayeingia anakaa sehemu yake inayostahili kutokana na kiingilio alichokitoa. Viingilio vilipangwa kuanzia shilingi elfu themanini viti maalum na wale ambao uwezo wao ulikuwa mogo walitakiwa kulipa shilingi elfu hamsini.Washiriki wakawa wameshawasili huku wakiwa nyuma ya ukumbi tayari kwa kuyaanza mashindano. Kadri muda ulivyokuwa unasonga Alice akawa anazidi kuwa mpole. Mawazo kwake yakawa kama sehemu ya kumpotosha akili yake. Tabasamu ambalo alikuwa nalo sasa likaaza kufifia hata kabla mashindano hayajaanza.

    “Warembo, mimi naitwa Jacky, nipo hapa kwa sababu moja tu.!! sababu ya ninyi kuchuana kuonesha ni nani atafaa kwa usiku wa leo. Mbinu zote mnazijua. Sasa basi kuna fulana hizi hapa zimetoka katika kiwanda kinachotengeneza bia cha Tanzania brewaries limited (TBL) na kwa kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro. Kila mmoja naomba azivae na kuzifunga pembeni. Chini kabisa naomba warembo wote tuwe tumevaa kaptura fupi na pembeni yake kila mmoja anatakiwa kuivaa namba yake ya kushiriki.. sawa jamani..”

    “Sawa mwalimu.!!.”

    “Na baada ya hapo mtatakiwa kupanga mstari mmoja kuingia ukumbini kwa pamoja kwa ajili ya kutambulishwa kwa kila mmoja.”

    Maneno kutoka kwa mwalimu wao huyo yaliwaingia vilivyo washiriki wote. Kila mmoja akawa yupo haraka kuvaa nguo na kuchukuwa namba za kuweka pembeni. Bado Alice alikuwa nyumba nyuma kwa kila jambo. Mawazo yalimzidia sana, kila alichokiaona yeye kikawa kibaya kwake. Akatamani sana mashindano yaishe haraka sana nakutangazwa mshindi ili kile alichokifanya hotelini kisijulikane.

    “Namba ishirini ni ya Jamila Said yupo wapi..?”

    Aliongea yule mwalimu, Jacky huku akiwa kashikilia karatasi na namba akizigawa kwa washiriki mmoja mmoja pamoja na fulana.

    “Mwalimu huyo atakuja na taarifa za kutoroka kambini anazo Mwalimu wetu tuliyekuwa naye kambini hivyo hata na nguo zake za kushiriki anazo mwalimu..”

    Alice akaongea kwa kujiamini tena kwa msisitizo juu ya Jamila. Washiriki wote wakaguna kwani walikuwa wakijua fika tabia za Jamila za kutoroka ovyo kambini. Ndani ya dakika tano warembo wote zaidi ya thelathini wakawa mstari mmoja kungia ukumbini kwa kajili ya utambulisho. Namba zao za pembeni ya kiuno ndizo ziliwatambulihsa vilivyo. Alice alikabidhiwa namba ishirini na moja na namba ya Jamila ilikuwa imetayarishwa tayari nambari ishirini. Kwa mstari mmoja huku wakielekea jukwaa kubwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ******



    Wazazi halisi wa Alice, Majaliwa na mkewe Janet wakawa wamepata nafasi ya kuingia ndani ya ukumbi. Ni john ndiye aliyefanya mpango wote wa kuhakikisha wanaingia ndani na kupatiwa siti za heshima mbele kabisa. Kutokana na nyadhifa aliokuwa nao John, aliweza kumkabidhi mfanyakazi mwenzake jukumu la kuhakikisha wazazi hao wameingia ndani na kupatiwa siti za heshima. Pilika pillika zilimzidia John na mpango wake wote ukawa ni kuhakikisha Jamila anakuwa mshindi kwa usiku huu. Kile kiasi kikubwa cha hela ambacho aliwakabidhi majaji ndicho kilimuumiza sana akili na pia kumuondolea hofu kuwa moja kwa moja Jamila atapitishwa. Akili ya John ikawaza kuchanganyikiwa taratibu kwa kutokuona kinachoendelea. Akawa ni mtu wa kukaka na kusimama huku asielewe anachokifanya. Kila mfanyakazi aliyekuwa akifanya naye kazi akawa anamchukulia huenda yuko bize kikazi. John akainuka na kuelekea mpaka nyuma ya jukwaa baada ya kuona sura ya Jamila haipo miongoni mwa warembo waliopanda mbele pale kujitambulisha.

    “Jacky kuna mshiriki mmoja hayupo, na ni mwakilishi kutoka Mwanza anaitwa Jamila. Unataarifa naye..??”

    “yeah, nimeambiwa kuwa alitoroka kambini lakini hilo swala lipo chini ya mwalimu aliyekuwa nao kambini.. si una namba za mwalimu..”

    “ndio ngoja nimpigie..”

    Hasira kali zikawa zimeshateka uso wake huku akitoa simu yake mfukoni kwa kutetemeka. Mikono yake yote ikawa imeshaingia unyevu nyevu wa jasho. Akaiona simu kama ipo kwenye utelezi kwa jinsi alivyoishika. Kitendo cha kuzibonyeza namba kwake kikawa shida hivyo akampa Jacky.

    “Embu nitafutie jina la Joseph katika simu. Nimeandika Joseph office kwani kuna Joseph wawili humo..”

    John akawa akiongea kwa kutetemeka mdomo na mikono. Akatoa kitambaa na kujifuta. Jasho bado likazidi kutawala mwili wake. Macho yake yote yakawa bado ameyaelekeza kwa Jacky huku akimsikiliza atakachoongea.

    “Haipatikani..”

    “Unasemaje Jacky..”

    “namba ya Joseph haipatikani, au ana simu mbili..??”

    “Hapana bwana embu nipe simu..”

    John akaichukuwa simu kwa huku akihema juu juu nakurudia kuzipiga zile namba kwa mara ya pili. Jibu la kwanza na la pili likawa sawa, kuwa hapatikani. Mawazo yakaanza kuchukuwa sura mpaya katika ubongo wake na wazo kuu likawa ni kujua Jamila yupo wapi mpaka muda huu wa mashindano umefika. John akatoka nje kwa spidi kali moja kwa moja mpaka kwenye gari lake na safari ya kwenda hoteli ya Girrafe Green View ikaanza..



    *****



    Wafanyakazi wa hoteli ya Giraffe Green View walikuwa katika kufanya usafi wanguvu. Usafi wa kuhakikisha hoteli inarudi katika hadhi yake ya mwanzo. Zile harufi mbali mbali za vipodozi wakawa wanazifuta kwa kupulizia manukato maalum ya kwenye chupa. Tayari walikuwa wametoa mashuka takribani vyumba vyote kwa kuyafua. Na sasa wakawa wameingia katika chumba namba 26. Ndani yake walishuhuia kukutana na kipande cha chupa chenye ncha kali kikiwa kimelowana kwa damu. Mlango wa kuingilia bafuni nao ulikuwa na alama za vidole huku umefungwa. Woga ukawa umewatanda wafanyakazi wote wa hoteli huku wakiitana kukusanyika kushuhudia kuna kitu gani mule ndani. Wakiongozwa na meneja wao pamoja na mwalimu wa warembo ambaye bado alikuwa akisubiri wahusika waje kumalizia deni la hoteli .walifanikiwa kuvunja mlango wa kuingilia bafuni. Shuka kubwa lililovingilishwa mithili ya gogo au mizigo ya magendo likawa lipo machoni mwa mwalimu na meneja wa hoteli.

    “Hiki ni nini mwalimu..?”

    “Dahh hawa warembo sijui ndio wamefanya kitu gani yaani wana vituko sana..”

    Mwalimu aliongea kwa maneno ya kejeli huku wakifunua kile kitu kilikchuokua kimevingirishiwa shuka. Kadri wallivyokuwa wanakifungua ndipo na damu nyingi wakawa wakikutana nazo kupitia shuka hilo zikionesha kukauka.

    “Si jamila huyu..??? ndio Jamila mshiriki mmoja wapo wa mashindano haya..”

    Alihoji mwalimu kwa sauti ya mshangao huku akiendelea kushangaa. Wakaanza kuangaza huku na kule kuanzia chooni huku wakifuata alama mbali mbali za mikono ile walioikuta mlangoni. Wakafanikiwa kupata simu ndogo aina ya Samsung ambayo ilikuwa imezimwa nakutupiwa chini. Wakaanza zoezi zima la kuikagua namba moja baada ya nyingine ili kuweza kugundua ni ya mrembo gani kati ya washiriki waliokuwa wakiishi hapo. Walianza na upande wa picha ambapo waligundua picha nyingi zikimwonesha Jamila na Alice katika mapozi tofauti wakiwa humo chumbani na hata nje ya mazingira ya hoteli. Picha nyingi kati ya hizo zilikuwa ni za Alice.

    “Embu tujaribu kupiga namba za mwisho kupigwa katika hii simu..”

    Alihoji meneja wa ile hoteli huku mwili wake ukiwa umelowa kwa jasho zima kutokana na kushuhudia tukio lile. Walijaribu kuipiga namba ya mwisho. ikaonesha jina moja tu ‘Mama’ napo simu ikaita kwa muda lakini ikapokelewa baadaye sana.

    “Haloo mwanangu Alice..!!, vipi mmeshafika ukumbini..?”

    Ilikuwa ni sauti ya Mama yake wa kufikia na Alice, Janet..

    “Unaongea na meneja wa hoteli ya Girrafe Green View hapa. Samahani Mama sijui mwenye hii simu unamfahamu..?”

    “Ndio ni mwanangu anaitwa Alice..”

    “..Anhaa, sasa kuna tatizo limejitokeza, tunakuomba ufike hotelini hapa mara moja ila mwanao yupo katika mashindano..”

    Mama wa kufikia na Alice, Janet akashusha pumzi baada ya kuongea na simu. Akajua fika huenda Alice ameanza ule ugonjwa wake na atakuwa pengine amedondoka. Aliposikia tu yupo katika mashindano alijipa moyo kisha akamalizia kujiandaa kwa kuvaa gauni lake nakujipodoa. Akakodi taksi ikampeleka mpaka hotel ya Girrafe Green View.

    “Mama mbona unapitiliza tu kama mwenyeji hapa..?”

    Alihoji mlinzi wa getini baada ya Janet kupitiliza kuingia bila ya kumsemesha.

    “Naelekea mapokezi nahitaji kuonana na meneja haraka kaniita..”

    “Sawa Mama yangu hata kama ingekuwa unashida na Rais. Ulipaswa kuzingatia utaratibu kwanza. Hapa kuna daftari la wageni na pia napaswa kujua unapoelekea kwanza kuna tatizo kubwa limetokea huko na upande mzima wa hoteli umesimamisha shughuli zake..”

    “Unasemaje..??”

    Janet alitahamaki kwa mshangao.

    “Mama kuna binti amekutwa amekufa na mwili wake upo umepatikana chooni..”

    “Oohh Mungu wangu..!! atakuwa mwanangu Alice tu huyo..??, kwanini jamani..??, kwanini Mungu umemchukuwa mapema hivi. Ungemuacha hata basi ashiriki mashindano yake na ndoto zake zitimie. Uwiiiiiiiii…!!! Uwiiiiiiiii…!!!! Ataaaaa…!!!! Taaaaaa….!!!! Ataaaaaa….!!!!! uuuuuwwwiiiiiiii…”

    Janet akaanza kuangua kilio mbele ya mlinzi getini. Kilio alichokitoa kikahamsha hisia tofauti kwa wapiti njia pale hotelini. Akili yake ikawa imebadilika na kuhisi moja kwa moja amefichwa ukweli na meneja kuwa Alice yupo mashindanoni. Akajitupa mpaka chini nakuanza kutapa tapa mithili ya kuku aliyechinjwa upande mmoja akaachiwa. Akainuka nakuanza kuranda randa pale getini. Nguo zake zikachafuka ndani ya muda mfupi zikawa hazitamaniki huku nywele zote zikiwa zimeshasalimiana na mchanga wa chini.

    “Mwili wake upo wapi..? nipeleke nikamwone mwanaaaaaanguuu..??, Alice weeeeee…?? Aliiiiiceeee kwanini umekufa Aliceeeee..???”

    Janet akawa amezidiisha makelel zaidi hali iliyomfanya mlinzi amshike nakumuongoza moja kwa moja mpaka kwenye hotel walipo meneja.

    “Huyu hapa..”

    Aliongea mlinzi akimwambia meneja wa hoteli. Kwa pamoja meneja na mwalimu wa mashindano ya mrembo wa Tanzania wakageuza macho yao nakumuangalia Mama yake wa kufikia na Alice, Janet.

    “Mama huyu binti unamfahamu..”

    Janet bado akawa katika kuchanganyikiwa lakini alipofika tu nakushuhudia mwili siyo wa mtoto wake Alice. Akashusha pumzi akatoa leso huku kwikwi ikimbana.

    “Ndio namfahamu, anaitwa Jamila ni rafiki mkubwa wa mwanangu. Amefanya nini..??, kipi kimemsibu..?”

    “Hapa unapotuona hatujui chochote zaidi ya kuambulia kukuta chupa yenye ncha kali na pia tumboni mwa huyu binti amechomwa chomwa vibaya hali iliyompalekea kifo chake.. Sasa basi huyu binti alikuwa akiishi na mtoto wako, Alice na Alice tayari katangulia kwenye mashindano kushiriki kabla ya kugundua hili tatizo..”

    Janet akawa bado hajielewi elewi kwa kile anachoambiwa. Mawazo ya ajabu yakaanza kujijenga taratibu katika halmashauri ya kichwa chake. Akahisi huenda njama zimefanyika tu ili mtoto wakeAlice asiweze kushinda mashindano haya. Alifikiria vitu vingi bila ya kupata majibu. Akiwa bado katika dimbwi la mawazo ghafla akatokea mumewe,John akitoa macho huku nakule asielewe kinachoendelea.

    “Yupo wapi Jamila..??, Joseph..?”

    “Naam bosi..??”

    “Kuna mshiriki moja hayupo kule..!!”

    “My God..!! hiki ni nini..?? nani huyu..?”

    John alihoji alipoingia tu ndani ya hoteli. Hakuwa na hata salamu zaidi ya kufika tu kwa haraka haraka akimuulizia mwalimu wake juu ya Jamila alipo.

    “..Mwili wa Jamila huu bosi, Jamila katutoka hatuko naye tena..”

    “Jamila..? Jamila Said..? yule mrembo kutoka Mwanza..?”

    John akatahamaki huku akijihisi kuishiwa nguvu mwilini. Akahisi mwili kumtetemeka ghafla, wazo la kujua kuwa mkewe yupo pembeni likamtoka. Akili yote akaielekeza kwa Jamila ambaye mwili wake ulikuwa chini. Alichokifanya John aliinua mkono wake nakushika paji la uso la Jamila huku akiyaachia machozi ya uchungu yakimdondoka.

    “Jamila..? Jamila amka..? amka Jamila wenzako wameshaanza mashindano.. nani kakufanyia hivi..?, nawauliza ni nani kamchoma choma tumboni angali alikuwa na...”

    John akaanza kubadilika taratibu. Ile sauti ya taratibu ambao alikuja nayo. Ikaanza kubadilika nakuwa kali na ya juu. Akaanza kugomba kwa hasira. Akataka kutajiwa ni nani aliyehusika na mauaji ya Jamila. Kutokana na umati wa wafanyakazi wa hoteli waliokuwepo wakishuhudia ule mwili wa Jamila pale hotelini ulimfanya John asiweze kumtambua mkewe haraka.

    “Sasa bosi tumeikuta simu hii chumbani kwa huyu binti na kwa upelelezi mfupi tulioufanya tumegundua kuwa alikuwa akilala na Alice. Na hata mara ya mwisho ni Alice ndio aliyelala naye. Tumejaribu kupiga namba ya mwisho ya simu hii nakugundua kuwa iliongea na Mama yake na Alice na tumemuita kaja huyu hapa..”

    John akageuza macho yake kuangalia anachoambiwa. Macho yake yakakutana uso kwa uso na mkewe Janet. Hasira kali zikampanda. Akahisi huenda ni njama za Alice na Mke wake ndio waliosababisha mauaji hayo. Akajua ni wazi kutembea na Jamila lazima Alice atakuwa amejua na hivyo kushirikiana na Mama yake kumuua Jamila.

    “Mmeshapiga simu polisi.? Polisi wanatambua chochote juu ya tukio hili..?”

    “Hapana bado..”

    John akatoa s imu yake ya kiganjani nakuanza kubonyeza namba za msaada. Simu iliita kwa muda kisha ikapokelewa.

    “Unaongea na huduma ya msaada hapa tukusaidie nini..??”

    “Kuna tukio limetokea usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya Girrafe Green View na kumepatikana mwili wa binti ambaye alikuwa kambini na wenzake tayari kwa kushiriki mashindano yanayoendelea hivi sasa katika ukumbui wa Diamond Jubilee..”

    “Sawa. Dakika chache zijazo tutakuwepo hapo..”

    John akaikata simu kwa ghadhabu huku akishusha pumzi zake taratibu. Akaangaza macho yake kwa wafanyakazi wa ile hoteli waliokuwa wakiendelea kutoa macho mule kwenye chumba cha hoteli.

    “Jamani nawaombeni mpungue sasa, sihitaji kumuona mtu yeyote zaidi ya mhusika mkuu wa hoteli na hawa hapa wahusika waliokuja..”

    John akawa mkali kwa muda. Watu wakatii amri yake. Wakaanza kusambaa kila mmoja akienda sehemu yake ya kazi. Haikuchukuwa muda mapolisi wakawa wameshafika katika eneo la tuikio. Kiongozi wao alikuwa wa kwanza kufika chumbani hapo huku akihitaji maelezo ya kutosha kwa kilichotokea. Maelezo yakatolewa na meneja akisaidiana na mwalimu wa warembo,Joseph. Dakika kumi nzima zilitosha kuchukua maelezo ya kukamilika.

    “Wewe mmoja wapo utakuwa hatiani kutokana na ushahidi wa nambari za simu zilizopigwa mara ya mwisho kwako..”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakamfunga pingu Mama wa kufikia wa Alice,Janet. Wakauchukuwa mwili wa marehemu Jamila mpaka kituo cha polisi kuandikisha tena maelezo mengine kutoka kwa mke wa John. Walimuweka lokapu na baada ya hapo wakaanza safari ya kuelekea hospitali kuuhifadhi mwili wa marehemu.





    *******





    Ukumbi wa Diamond Jubilee Ukawa umeshafura watu zaidi ya mia sita huku wengi wao bado wakiingia. Mashindano ndani ya ukumbi yalikuwa yakiendelea. Warembo takribani ya thelathini kati ya thelathini na moja wakawa wameshapita kuonesha mavazi ya ubunifu. Nderemo na Vifijo vilichukuwa nafasi yake. Kila mrembo aliyepita jukwaani alikuwa na mashabiki wake. Wazazi halisi wa Alice, Majaliwa na Juliana wakawa wameshamgundua mwanao Alice. Uzuri uliojijenga katika mwili wa Alice ukawafanya kujiona na faraja sana moyoni mwao. Mashabiki waliokuwa wakimshangilia Alice na kumuita jina la bingwa ndio waliofanya kusisimka kwa wazazi wa Alice kila muda mashindano yalivyokuwa yakiendelea. Wakatamani sana mtoto wao,Alice aweze kuwagundua lakini kutokana na hali ya kutulia Alice awapo jukwani kukamfanya asiweze kujua kama wazazi wake wapo hapo. Baada ya kila mmoja kukamilisha kwa kupita na mavazi ya ufukweni, ya usiku na hata mavazi ya ubunifu. Kukatolewa burudani fupi huku majaji wakiendelea kupiga kura za kupata tano bora. Majaji walihangaika sana kuchambua kutokana na kula pesa yote ya John kwa kumuweka mshindi wa kwanza awe Jamila. Jamila hakuwepo katika orodha ya warembo walioshiriki na wakajaribu kumpigia simu John. Simu yake ikawa bize tu inaongea. Wakajaribu kila mara kuipiga ile namba huku mashindano yakiendelea lakini wakaambulia kutopatikana kabisa kwa namba hiyo ya simu. Sasa wakawa wameshakabidhi tano bora ya warembo kwa mgeni rasmi kwa ajili ya kupambanua na kumpata mshindi wa tano mpaka wa kwanza.

    “Mabibi na mabwana, wageni waalikwa, ndugu na washiriki wote wa mashindano sasa namkaribsha mgeni rasmi wa mashindano haya mheshimiwa Mbunge wa Ilala Ramadhan Komba aje kutangaza tano bora yetu..”

    Makofi, miluzi na hata makelele ya shangwe yakatawala ndani ya ukumbi huku kila mshiriki akiwa katika homa kali ya kutangazwa ama kuachwa. Mheshimiwa Ramadhan Komba akasimama akakabidhiwa kipaza sauti pembeni yake akiwa na karatasi ambayo iliandikwa kiufasaha kuanzia mshindi wa tano mpaka wa kwanza.

    “kwanza nitoe shukrani zangu kwa waandaaji kwa kunichagua kuwa mgeni rasmi wa mashindano haya. Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa mashindano haya tangu zamani. Najua ni sehemu mojawapo ya vijana wetu kuwapa nafasi ya kulitangaza taifa. Na pia ni njia mojawapo ya kujikwamua vijana haswa wa kike katika kujipatia ajira kupitia mashindano haya yanayoanzia mikoani. Labda nisitumie muda mrefu sana kutangaza kwani sina uzoefu na maswala ya u mc. Ningependa kutaja majina ya washiriki watano ambao wamefanikiwa kupita katika mashindano haya..,Mwanaidi Athuman,Mary enock,Alice Majaliwa,Jacqueline Gaspery na Josephina Winford..”

    Makelele yakatawala mara mbili na yalivyokuwa mwanzo. Majina yaliotajwa kila mmoja alionekana kuafikiana nayo. Warembo waliotaja wakasimama mstari mmoja huku waliosalia wakibaki pembeni kushuhudia nani ataibuka mshindi. Mgeni rasmi mheshimiwa Ramadhani Komba akapata fursa ya kukaa kwa muda huku majaji wakiendesha maswali kwa washiriki walipita katika tano bora.

    “Tunaanza na namba tano Mwanaidi Athumani uje happa mbele na uchukue kipaza sauti..”

    Mwanaidi akasogea mbele kidogo. Akashika kipaza sauti tayari kwa kujibu maswali.

    “Unachagua kiingereza Kiswahili..”

    “Nachagua Kiswahili..”

    “Ukiwa kama mshiriki wa mashindano haya ya mrembo wa Tanzania na ukiwa kama mshindi wa tano wa mashindano haya. Je unavyodhani nini msingi mkubwa wa kujikomboa vijana kama vijana katika janga hili la ajira..”

    “Asante sana Jaji. Kwanza shukrani kwa kufikia hatua kubwa hii ya mshindi wa tano kati ya washiriki thelathini. Najibu kama ifuatavyo. Msingi mkubwa wa kujikomboa kwa sisi vijana haswa ni Ujasiriamali. Kwa kupitia miradi midogo midogo ya kuianzisha sisi wenyewe kwa wenyewe tunaweza kujikomboa..”

    Makofi yalipigwa kwa Mwanaidi Athuman, akafuatiwa mshindi wa nne Mary Enock naye akaulizwa maswali kwa lugha ya kiingereza aliyoichagua. Sasa ikawadia tatu bora ambayo iliwakutanisha Josephine Winford, Jacqueline Gaspery na Alice Majaliwa. Kila mmoja alikuwa na sifa ya kuwa mshindi wa kwanza katika mashindano. Uzuri na umbo waliokuwa nao hawa tatu bora ni wazi unaweza kupeleka ushindi kwa wote. Mtindo wa maswali ukaendelea kwa mshindi wa tatu Jacqueline Gaspery. Na baada ya hapo akafuatiwa Josephine Winford. Mshindi wa kwanza akawa tayari ameshajulikana. Shangwe zikatawala kila kona. Alice akawa na bahati ya kupendwa na kila mmoja. Machozi ya furaha yakamtoka, akatembea jukwaani huku akiwapungia mkono watu waliokuja kwenye mashindano. Machozi ya furaha yakatawala usoni mwake hali iliyofanya kusahau mauaji alioyafanya usiku wa kuamkia siku hiyo. Viatu virefu alivyovaa vikimfanya atembee mbele kwa maringo sasa akawa ameshakikaribia kipaza sauti na kukishika tayari kwa kumsikiliza mgeni rasmi amuulize swali.

    “Unachagua Kiswahili ama kiingereza.?”

    “Amhhh..!! na prefer Swahili sababu its my national language..!”

    Ukumbi wote ukalipuka kwa makelele huku wakifurahia kusikia sauti ya Alice. Alice aliongea kwa kujiamini huku akisubiria swali atakaloulizwa. Macho yake yakaangaza huku na kule huku akiwa hana wasiwasi wowote. Mgena rasmi mheshimiwa Ramadhan Komba alikabidhiwa swali la kumuuliza mshindi wa kwanza wa mashindano haya Alice Majaliwa. Kitendo cha kuanza kuuliza swali tu, mara ghafla akatokea John ukumbini moja kwa moja mpaka kwa mc nakuchukuwa kipaza sauti huku jasho likimtoka.

    “Nashukuru kwa wote kuweza kuhudhuria mashindano haya. Taarifa ambazo zimetufikia punde ni kwamba mshiriki mmoja wapo kati ya thelathini na moja ambaye alikuwa katika orodha lakini hakupata nafasi ya kushiriki hatuko naye tena. Maiti yake imekutwa hotelini ikiwa imeviringishwa na shuka za hoteli huku tumboni ikimwonesha kuchomwa chomwa na kitu chenye ncha kali. Hivyo basi mashindano haya hayatatambulika kwa siku ya ya leo na tunayahairisha ramsi. Kamati ya miss Tanzania haitamtambua mshindi aliyepatikana kwa leo mpaka hapo tutakapowatangazia siku nyingine ya mashindano. Tiketi zenu mtabaki nazo mpaka siku nyingine na washiriki watakuwa wale wale walioshiriki leo kasoro wawili ambao ni marehemu Jamila Said na Alice Majaliwa ambaye tunamweka hatiani kuhusika na kifo cha rafiki yake waliokuwa wakilala pamoja huko kambini Jamila Saidi. Samahanini sana kwa kilichotokea..”

    “John akaweka kipaza sauti chini kisha akafuatana na polisi mpaka eneo alipokuwa amesimama Alice kwa kujibu maswali ya miss Tanzania. Wale mapolisi wakamfunga pingu Alice lakini kabla hawajamfunga Alice akawa ameshadondoka chini na damu nyingi kuanza kumtiririka zikitokea puani huku akitapatapa kwa kurusha miguu.



     Aloyce Kabula mtoto wa rais alioko madarakani nchini Rwanda. Anafanikiwa kuhitimu masomo yake ya utalii na urembo Napoli nchini Italy. Akiwa na miaka ishirini na saba Aloyce anasaidiwa kwa kiasi kikubwa na Baba yake kufungua chuo kikubwa cha masuala ya urembo kiitwacho Loyce beauty Training collage. Chuo kinapata mafanikio kikiwa chini ya Aloyce na kufikia wahitimu mia moja na ishirini kwa mwaka wa kwanza. Aloyce anapata pesa nyingi sana na umaarufu Rwanda nzima kupitia chuo chake cha Loyce.Akaona pesa na umaarufu havimtoshi mbele ya mwanamke nakuamua kutafuta msichana wa maisha yake ambaye atasaidiana naye katika kuiendeleza miradi yake sambamba na kumzalia mtoto. Ndoto yake kubwa ikawa ni kupata mrembo yeyote wa kiafrika kutoka nchi nyingine kwani kamwe hakupenda aoe msichana kutoka nchi yake ya Rwanda. Tanzania ni moja ya nchi ambazo Aloyce alikuwa akiziota sana maishani mwake. Alipenda sana ukarimu wa watanzania sambamba na uzuri na wa wanawake wake walivyoumbika. Mawazo yake moj kwa moja yakawa ni kupata mrembo mzuri atakayetoka nchini Tanzania.

    “Nahitaji ifanyike haraka iwezekanavyo na kwa njia yeyote..? swala la uraia nitajua mimi cha kufanya..!!”

    “Sawa bosi..”

    Aloyce aliwaamrisha walinzi wake wachukue gari na silaha kisha wapite boda mpaka Tanzania kwa ajili ya kumtafuta mrembo nambari moja Tanzania. Onesmo na Sheray ni kati ya walinzi waliokuwa wameteuliwa na Aloyce kuja nchini Tanzania wakipitia boda kuja kumtorosha mrembo nambari moja kwa uzuri Tanzania. Walikiweza Kiswahili kiufasaha na pesa waliopewa ilikuwa nyingi hivyo kuwarahisishia kazi ya kupenya boda mpaka kufika Tanzania. Wakiwa na silaha zao kwa siri siri Onesmo na Sheray wanafanikiwa kufika mpaka katika hoteli kubwa ya Girrafe Green View lakini siku hiyo hiyo waliofika ndio ilikuwa siku ya kilele cha warembo katika mashindano ya kumtafuta mrembo wa Tanzania. Furaha na tabasamu linawajaa Sheray na Onesmo siku nzima wanakaa hotelini huku wakisuka mipango kabambe ya kumpata mrembo wa Tanzania. Wakiwa ndani ya hoteli mara ghafla wanashtushwa na habari za kutokea kifo cha mshiriki mmojawapo katika hiyo hotel. Wanaenda kuhushudia huku wakiwa na masikitko makubwa.

    “Alice..!!, Alice ndio tampata.. na Lazima ikwende kwetu..”

    Sheray akamvuta Onesmo pembeni na kumnong’oneza jina la Alice baada ya kulisikia kwa meneja wa hotel akimhoji Mama wa Alice, Janet. Mipango mikubwa ikaendelea kufanywa kati ya Sheray na Onesmo. Wakafanya kila njia kuhakikisha Alice anakuwa mikononi mwao. Wakafuatilia tukio zima mpaka Janet anawekwa hatiani walikuwa wakifahamu. Mpaka inafika muda wa saa mbili za usiku tayari Mama wa kufikia wa Alice, Janet alikuwa mikononi mwa Onesmo na Sheray kwa pesa kidogo waliowahonga mapolisi wa kituo. Kutokana na maelezo waliyoyasikia hotelini wakawa wameshaamini kuwa Janet ni Mama kabisa wa Alice na hivyo atawasaidia huko waendapo.Wakawa tayari wakimsubiri mtu mmoja tu waliokuwa wameagizwa si mwingine bali ni Alice Majaliwa. Kitendo cha mapolisi kumuweka hatiani Alice majaliwa kikawa ni kicheko kikubwa sana kwa Onesmo na Sheray. Kazi kwao ikawa rahisi kuliko walivyodhani kutokana na mapolisi wale wale waliopokea pesa na kumuachia Janet sasa wakawa ndio waliomuweka Alice hatiani. Kiasi cha dola za kimarekani milioni moja kikawaingia tamaa kubwa mapolisi, wakagawana kila mmoja afe na chake. Wakapanga kila njia waweze kumuachia Alice endapo watafanikiwa kumuweka hatiani. Saa tatu za usiku Onesmo na Sheray huku kwenye gari wakiwa na Janet wakawa wameshafika nje ya ukumbi wa Diamond Jubilee wakimsubiri Alice. Wakapaki gari lao pembeni kabisa karibu na gari la polisi. Ndani ya muda mfupi kitendo cha mapolisi kutoka na Alice wakiwa wamembeba kikawa neema kubwa sana kwa Sheray na Onesmo. Wakawapokea polisi nakumfungua pingu Alice kisha wakampakiza kwenye gari lao nakutoka kwa mwendo kasi huku sauti ya John ikiendelea kusikika ndani ya ukumbi kwa mbali.

    “Mwanagu Alice..??, Amka mwanangu nipo pamoja nawe, amka mwanangu amka..??”

    Kwakuwa matatizo ya Alice Mama yake wakufikia,Janet alikuwa akiyajua ikawa rahisi kuanza kumpa huduma ya kwanza. Alianza kwa kumpepea na kumpa pumzi kupitia mdomoni mwake akiwa hajali zile damu zilizokuwa zikiendelea kumtoka Alice. Gari likaendelea kukatiza mitaa likitafuta barabara ya kuelekea morogoro huku malengo makubwa ni kupita Mbeya nakukatiza boda ya Tunduma.

    “Mama..??, Mamaaaa..????”

    Alice akashtuka akiwa hajielewi. Akanza kushangaa amezungukwa na watu ambao hawafahamu vizuri zaidi ya kumtambua Mama yake wakufikia, Janet.

    “Mwanangu Alice..??, pole mwanangu embu ngoja..!!”

    Janet aakawa ameshaziona damu nyingine zikiendelea kumtoka Alice. Akamfuta vizuri. Sheray ambaye alikuwa akiendesha gari ikambidi alisimamishe wote kwa pamoja na Onesmo wakaanza kumhoji Alice.

    “Hongera mekua mshindi kwa shindano yenu ya miss Tanzania..”

    “ooh ahsante.. asanteni sana..”

    Alice akawa hajitambui zaidi ya kuitikia huku mikono yake miwili akiilekeza katika kifua chake kwa mshangao wa furaha. Aliangaza pembeni huku na kule lakini kukawa giza sana hivyo hakuweza kujua yupo maeneo gani.

    “Mama nashukuru malengo yangu yametimia sasa, thanx Mama..!”

    Alice aliongea na Mama yake wa kufikia, Janet huku akimkumbatia. Kumbukumbu zote za kuanguka jukwaani mpaka kukamatwa kufungwa pingu na mapolisi hakuwa nazo. Alichokikumbuka ni mara ya mwisho kuambiwa amekuwa mshindi. Akalifanananisha tukio hilo kama lile alioshinda Chang’ombe. Alice akajiona huenda wanampeleka hoteli kubwa ya kifahari kwa ajili ya mapumziko yeye na Mama yake .



    *******CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    MISS TANZANIA AUA, MISS TANZANIA JAMBAZI, MREMBO AUAWA NA MISS TANZANIA, HII NDIO BONGO miss aua kisa awe mshindi, MISS TANZANIA ALICE MAJALIWA AUA NA YEYE KUJIUA, MREMBO WA MISS TANZANIA AKUTWA CHOONI AMEUAWA.. Ni baaadhi ya maneno yaliochukuwa sura katika ukurasa wa mbele wa magazeti yote. Asubuhi na mapema kila kijiwe cha kuuza magazeti kilijaa watu kushuhudia ni mrembo gani aliyeua na kujiua. Wapo waliohuzunika kwa kuuona mwili wa Jamila ukiwa hautamaniki. Picha kubwa iliomuonesha Alice akipita jukwaani ndio ikawasisimua wengi sana. Uzuri na umbo aliokuwa nalo Alice ni wazi utakataa kuwa hakuwa na kosa la kuua. Picha nyingi za kwenye magazeti zikaonesha tukio la Alice kuwa mshindi na nyingine zikaonesha kitendo ch Alice kudondoka nakuanza kutoa damu puani huku akitapatapa. Majonzi mengi yakatawala kwa kila msomaji wa magazeti. Radio na televisheni zikaripoti tukio zima la kuuawa kwa Jamila kama mshiriki mmoja wapo wa mashindano ya mrembo wa Tanzania akitokea Mwanza. Kamera za televisheni zikaonesha moja kwa moja mpaka hoteli ya Girrafe Green View na chumba namba 26 ambacho aliuawa Jamila. Masikitiko yakatawala Tanzania nzima hususani kwa wapenda urembo na waigizaji wa filamu. Wazazi halisi wa Alice wakawa hawajielewi na ni Baba Alice alikuwa wa kwanza kupoteza fahamu baada ya mtoto wake Alice kuambiwa anahusika kwa mauaji, Mzee majaliwa alipofikishwa hospitali ikagundulika amepooza upande mmoja kutokana na mshtuko. Kamati ya maandalizi ya mrembo wa Tanzania ikishirikiana na baaddhi ya viongozi wa nchi hata Rais wakaguswa sana na tukio zima, wakatoa salamu zao za rambi rambi.

    Taarifa juu ya kuuawa kwa Jamila zikazidi kupenya masikioni mwa watu haswa wale waliokuwa wakifuatilia maswala ya urembo. Jiji la mwanza likiongozwa na mkuu wa mkoa wa mwanza mheshimiwa Hussein Msangi alilipokea tukio zima la mauaji ya mrembo aliokuwa akiwakilisha Jiji lao la Mwanza Jamila Said kwa masikitiko makubwa. Hakuna hata aliyeweza kuamini kama Jamila ameaga dunia kutokana na umaarufu aliokuwa amejizolea pindi alipokuwa akiigiza filamu za bongo kwa jiji la Mwanza. Mpenzi wake Jamila wa kufa na kuzikana,Nicky kutokana na madawa ya kulevya kumuathiri kisaikolojia lakini akaonekana kuguswa sana na tukio la msiba. Yeye pamoja na wazazi wake wakakusanyika pamoja mpaka uwanja wa ndege tayari kwa kuupokea mwili wa marehemu Jamila Said. Ndani ya masaa mawili umati ukazidi kuongezeka ndani ya uwanja wa ndege wa jiji la Mwanza. Mapolisi wa Jiji la Mwanza walikuwa na kazi moja tu, kuzuia watu wasiingie zaidi uwanjani kwani wengi wao walitaka japo kulishuudia Jeneza kama ni kweli walioyasikia redioni na kuyaona katika televisheni na magazetini kuwa Jamila amefariki ni kweli ama la!

    Punde ndege ya kampuni ya Precision Airways ikashuka katika uwanja wa ndege wa Jijini Mwanza. Mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza wakajitokeza kuupokea mwili wa marehemu Jamila nakuupelekea mpaka nyumbani kwao. John akiwa mstari wa mbele huku akivalia suti nyeusi pamoja na viongozi wengine wa mashindano ya mrembo wa Tanzania wakalibeba jeneza kiufasaha nakuliingiza ndani ya gari spesho kwa kubebea maiti huku wakipanda kwenye gari na wazazi wa Jamila tayari kwa safari ya kuelekea Nyakato alipokuwa kwa wazazi wa marehemu Jamila. Msururu wa watembea kwa miguu mbele kabisa na nyuma yake baiskeli, zikifuatia piki piki, kisha bajaji na nyuma kabisa gari lililobeba maiti pamoja na gari la mkuu wa mkoa huku magari ya kawaida yakiunga foleni mpaka Nyakato alipokuwa akiishi Jamila na wazazi wake. Ndani ya Lisaa moja lilitosha kwa kumfikisha Jamila na kumzika moja kwa moja huku vili vikitawala kila pande.



    ***************************



    Ilikuwa ni asubuhi tulivu, dalili za mirindimo ya mvua ilikuwa ikiashiria kutoka katika anga. Ile dhahama ya wakulima kulima kwa kipindi kirefu bila kupata mazao yakueleweka sasa ikawa ukingoni. Mkombozi wao mvua ikaanza kunyesha eneo lote. Kila mmoja akaonekana kufurahia ujio wa mvua hiyo.

    Alice alikuwa ndani ya gari upande wa kushoto kwake alikuwa Mama yake wa kufikia,Janet na upande wa kulia kwake alikaa Onesmo na Sheray alikuwa derive siti ya mbele kabisa akiliendesha gari. Alice akaendelea kuvumilia umbali wa safari akiwa hajielewi elewi. Mawazo yake yakawa yamevurugika tofautti na alivyodhania. Wazo la yeye kupelekwa kwenye hoteli kubwa baada ya ushindi likatoweka akilini mwake baada ya kushuhudia safari ndefu isiyo na mwisho. Uvumilivu ukaanza kumshinda taratibu.

    “Mama tunaelekea wapi mbona sielewi chochote..??”

    “Mwanangu, unapaswa kutuliza akili na mawazo yako..”

    “sawa Mama lakini napaswa kujua tunapoelekea maana nashangaa safari ndefu isiokuwa na mwisho wakati mimi ni mshindi na nastahili nikapumzike mapema. Kama hiyo hoteli ni hoteli gani sasa hatufiki muda wote huo..??”

    Alice akaendelea kuwa mkali zaidi huku akiropoka kwa sauti ya juu akitaka kujua ukweli anapopelekwa. Hasira kali zilimshika. Mama yake wakufikia na Alice, Janet alijitahidi kumuweka Alice sawa kwa kumuelewesha kila kitu lakini Alice bado akaonekana kuwa mkali.

    “Onesmo huyo binti nataka nini mbona sumbufu..?”

    Sheray akahoji huku akiwa kasimamisha gari pembeni baada ya Alice kuanza kuongea kwa sauti ya juu.

    “Sikiliza Alice, hivi unajua ulichokifanya huko tulipotoka..? Unajua sisi ni wakina nani..?”

    “hapana..?”

    “Sasa ukweli ni kwamba huko ulipotoka umeua na umemuua mwenzako Jamila..Ni aibu kubwa umeifanya na hapa tulipo mwanangu tunafanya mpango wa kukutorosha ili kunusuru maisha yako mwanangu. Kumbuka nilikwambia kamwe sintokuja kukuacha maishani. Kinachotakiwa hapa ni tumuombe Mungu atufikishe salama.”

    Alice akaonesha kushtuka na jasho likianza kumtawala baada ya kuambiwa maneno kwa sauti ya utaratibu kutoka kwa Mama yake wa kufikia, Janet. Limbi la machozi likaanza kuchukuwa nafasi katika paji la uso wake hali ilioonesha kuguswa sana na maneno aliloambiwa juu ya kumuua Jamila. Roho ya huruma ikachukuwa nafasi katika moyo wa Alice. Akaona kumbe Sheray na Onesmo ni watu wazuri naa wanaojali utu kwa kumtorosha.

    “Mwanangu Alice acha kulia. Mie mwenyewe niliwekwa lokapu kwa kuhusika na mauaji yako kutokana na ile simu ulionipigia kwa mara ya mwisho na hawa ndio waliokuja kunioka kituo cha polisi na ndipo tukaja kukunasua na wewe. Lakini nasikia ulitangazwa kuwa mshindi wa mashindano ya mrembo wa Tanzania, ni wewe..?”

    “Ndio ni mimi Mama yangu..?”

    “Basi amini unaweza na utafika mbali tu katika maisha yako mwanangu kwani mwenyezi Mungu bado anakupenda..”

    “Asante Mama..”

    Muda wote Onesmo na Sheray walibaki kimya wakiwasiliza Alice na Mama yake wa kufikia, Janet. Safari Ikawa bado ikiendelea huku na maongezi ndani ya gari yakiendelea. Janet akamweleza mengi sana Alice kuhusu maisha. Alice akaguswa sana na maneno ya mama yake. Akajikuta mwili ukimtetemeka sambamba ni midomo yake kumcheza huku akisita.

    “Mama nakuomba nikwambie siri moja inayonitesa maishani..”

    “Niambie tu mwanangu kwani sina tena mtoto zaidi yako Alice, we ndio kila kitu kwangu..”

    “Mama najua unapata tabu nyingi kuishi na Baba. Najua umetokea kumchukia ana Baba na kama bado hujamchukuia nadhani nikikwambia utaanza kumchukia milele..”

    “Niambie mwanangu ni kitu gani hicho..?”

    “Mama..”

    “Ndio mwanangu..”

    Alice akavuta kwanza gauni lake aliokuwa amevalia mara ya mwisho kutangazwa mshindi kisha akalivuta mpaka kwenye paji la uso nakufuta mchozi sambamba na makamasi ambayo yalikuwa yakimteleza kutoka kwenye pua zake. Akawa yupo tayari kutoa duku duku lake moyoni alilolihifadhi kwa muda bila kujali Sheray na Onesmo watawasikiliza.

    “Mama baba hafai Mama.. Baba ndio chanzo cha matatizo yangu yote..”

    “Bado sijakuelewa mwanangu unamaana gani..??”

    “Kamwe maishani mwangu sikudhamiria kuua na wala niliapa sintokuja kumdhuru mtu yeyote hata kwa kucha lakini yote ameyataka Baba..?”

    Alice akaongea kwa hasira huku kwikwi ikimbana na pumzi kutaka kumkata. Mama yake akamuwahi nakumshika mdomo nakuanza kumpuliza huku akimsaidia kuhema. Akahema kwa haraka na kwa juu juu mpaka pumzi ikamrejea tena Alice.

    “Mwanangu Alice nakupenda sana punguza hasira, nakuomba unihadithie kwa utaratibu kwani natamani kujua kilichotokea mpaka kumchukia baba yako..”

    “Mama mimi naamini hakuna baba wa kweli duniani. Mungu amenijalia kupata baba, lakini kila baba ninayempata ananifanyia unyama. Ni siri kubwa sana iko moyoni mwangu na nitazidi kuwachukia baba wote duniani..”

    “Mwanangu Alice niambie kwanini uwachukie..”?? enhh..?? kwanini uwachukie wababa wote duniani?? Wamekufanya nini..??”

    “Mama amini usiamini nimezaliwa nikiwa na baba yangu tena akiwa mlokole haswa. Amenilea nakunisomesha mpaka darasa la saba ambapo uwezo wake ndipo ulipoishia. Tukaishi maisha ya tabu kwa kutegemea kukaanga na kuuza samaki kutoa kwa mama yangu. Baba yangu akaanza kubadilika sana, akawa analewa sana. Kila akirudi akawa anampiga mama japokuwa mama yangu hakuwa na kosa lolote. Nakumbuka mara ya mwisho baba yangu alirudi amelewa sana hali iliomfanya aingie ndani kwa hasira huku akimpiga mama nakumtukana matusi bila sababu yeyote. Alimpiga sana mama mpaka mama akafanikiwa kutoroka na kukimbilia pasipojulikana mpaka sasa.. Oooh mama.!! , mama yangu bado nakupenda popote ulipo. Nakupeeeenda maaamaaa..!!”

    “Ikawaje sasa..??”

    “Basi nikabaki naishi na baba yangu maisha yote. Nikiwa nampikia baba, namfulia huku nikiendeleza biashara aliokuwa akiifanya mama yangu ya kukaanga na kuuza samaki. Siku ya siku baba yangu akanipora hela zote za mauzo na kukimbilia kunywa pombe zake za kienyeji. Niliumia sana, niliumia kwa kutokujua hatma ya maisha yangu… iihhhhhhhhh..!! hhiiiii..!!”

    “Pole sana Alice, pole sana mwanangu. Ikawaje nakusikiliza bado..?”

    “Mama inatia uchungu sana. NIkaishi maisha ya tabu sana huku nikihakikisha baba yangu nampatia chakula haijalishi pesa Napata wapi. Nilihangaika kukopa huku na kule ili mradi nisimlaze baba yangu na njaa kwani hakuwa na sehemu ya kufanya kazi na hata akipata pesa kidogo alikuwa akipitia vilabuni na kunywa pombe za kinyeji na akifika nyumbani ni kutukana nyumba nzima. Mara ya mwisho nakumbuka nikiwa naishi na baba yangu, alinivamia kitandani mwangu usiku sana huku kashikilia mshumaa uliokuwa ukiwaka nakunibaka. Baba akaniondiolea bikra yangu ambao niliitunza mpaka kwa mwanaume atakayekuja kunioa. Baba akaniharibu sana sehemu zangu za siri. Damu nyingi zilinimwagika. Niliumia sana kwani alinitisha endapo nitatoa makelele angenichoma na mshumaa. Asubuhi yake ilivyo wadia baba akaenda kwenye mishuguhuliko yake napo ndipo nikapata nafasi ya kutoroka pale nyumbani. Ndipo nikayajua rasmi maisha ya mjini.. nikaapa kamwe sintokuja kumsamehe baba yangu maishani..”

    “Pole sana mwanangu Alice, pole sana. Sasa na baba yako John unamchukia kwanini wakati yeye ndiye aliyekupa ushindi wa Chang’ombe..?”

    “Mama kuna siri kubwa baba ameifanya. Amini usiamini nimemua rafiki niliekuwa nikimpenda sana sababu ya baba..”

    “Kwanini..?”

    “Mama..??, unakumbuka wakati baba yupo Mwanza mimi ndie nilikuwa katika kugombea taji la Chang’ombe. Kwa bahati nzuri na juhudi zake nikashinda na kupata nafasi ya kushiriki mashindano makubwa ya urembo. Mama kumbe kile kitendo cha mimi kushinda na baba kule Mwanza akawa keshampata Jamila na kampa ushindi wa kwanza baada ya kulala naye usiku kabla ya lile onesho. Jamila amekuja kambini akawa ananificha mpaka dakika za mwisho ndipo Jamila akaniambia wazi kuwa anatembea na baba na ameshahaidiwa ushindi kwenye mashindano makubwa kwa sababu ameshika mimba yake. Siku moja kabla ya mashindano hasira kali zikanijaa na si unakumbuka nilikupigia simu usiku kwanza. Na lengo langu lilikuwa nikumwambia baba ukweli juu ya mimba ya Jamila. Jamila alimwongopoea baba kuwa anamimba yake kumbe siyo mimba ya baba bali ilikuwa ni mimba ya mpenzi wake Jamila aliyemwacha kwao Mwanza anaitwa Nicky. Mama niliumia sana na hasira zikanizidia mpaka nikajikuta nimepasua chupa ya pafyumu chini na kisha kumuwahi nayo Jamila aliokuwa amelala nakumuua kwa ushenzi aliokuwa amefanya na pia nilihitaji kuwa mshindi wa mashindano hapa Tanzania ili ndoto zangu zitimie mama. Leo hii eti nimpende baba..? baba aliyetaka kuninyima ndoto zangu za kuwa mshindi kisa penzi la uongo alilopewa na Jamila..?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Janet akaguswa sana. Akachukuwa kitambaa nakujifuta machozi yalioanza kumlenga lenga. Alijihisi na yeye mkosaji duniani. Kitendo cha kutokuwa na uwezo wa kuzaa Janet akajichuklia ni tusi kubwa maishani mwake. Akajiona hafai kuitwa mwanamke duniani. Akajipa moyo konde.

    “Mwanangu Alice ipo siku Mungu atafungua njia amini. Ila si mara ya kwanza baba yako,John kunifanyia hivi. Alishawahi kunisaliti mara nyingo sana na hata mbele ya macho yangu nikishuhudia. Lakini nasema hayo yote ni maisha kamwe sintorudi nyuma. Atanikumbuka tu kwa wema nilioonesha kwake kwa kipindi chote..”

    Janet akamkumbatia Alice kwa uchungu huku wakiendelea kutolewa macho na Onesmo pembeni yao.



    ***** ***********



    Iliwachukuwa siku moja kusafiri kutokea Dar es salaam mpaka Kahama. Yale malengo yakupitia boda ya Tunduma yalishindikana hivyo wakabadili uelekeo. Wakawepo makutano ya Lusahanga. Usingizi ukamzidia Sheray ambaye alikuwa dereva njia nzima toka wanatoka Dar es salaam. Wakabadilishana na Onesmo akaenda siti ya mbele kushikilia usukani wakaanza kuzitafuta kilomita mia na sitini mpaka Rusumo. Sasa Alice akawa ameshajua ni wapi anapotoka na anapoelekea. Ni Janet ndio alipewa jukumu na Sheray kumwambia Alice sababu ya kutoroshwa kwake. Alice akawa hana kipingamizi kutokana na kukwepa kuwekwa gerezani kufuatia mauaji alioyafanya Dar. Mauaji ya kumuua mshiriki mwenzake kwenye mashindano ya urembo Jamila Said. Moyo wake ukawa na furaha iliyotawaliwa na amani ndani yake. Akapewa maneno mazuri na Janet akishirikiana na Sheray juu ya mambo atakayofanyiwa na mtoto wa rais wa Rwanda,Aloyce. Katika maisha yake Alice mpaka anafikisha umri wa miaka ishirini hakuwahi kuwa na mwanaume wala kushirikiana tendo lolote na mwanaume. Tangu baba yake ambake na kumtoa bikra Alice hakuwa akitamani kuwa na mwanaume yeyote maishani. Akayapokea maneno ya Janet na Sheray vizuri masikioni mwake huku akiwa hajiamini vizuri.

    “Sawa nimewaelewa nitajitahidi kutilia lakini nijuavyo ni vigumu kumpenda mtu ambaye hayuko katika fikra zangu.. nitafanyaje..?”

    “Hapana Alice, mapenzi huanza taratibu kwa kuzoeana kila mmoja na mwisho wa siku mnajikuta mmependana..”

    “Sawa mama nimewaelewa nitajitahidi kufanya usemavyo..”

    Janet na Sheray wakagongeana mikono na kisha wakagongeana na Alice huku siti ya mbele Onesmo akionesha tabasamu la ndoto zao za kumpeleka mrembo nambari moja Tanzania kufanikiwa. Akawa akiwaziwa heshima sambamba na mapesa watakayopewa na mtoto wa rais wa Rwanda, Aloyce. Onesmo akazidisha kasi ya gari kwa furaha aliokuwa nayo huku jua likizama na giza kuanza kuchukua nafasi yake..



    *****



    ITAENDELA

0 comments:

Post a Comment

Blog