Simulizi : Nakupenda Cindelela
Sehemu Ya Nne (4)
ILIPOISHIA
Alex nae aliinuka na safari ya kuelekea alipolazwa Cindelela ikaanza,Alex alijikuta mwili wake ukitetemeka huku jasho likimtoka mpaka mwenyewe akawa anajishangaa kwanini kitu kama kile kinatokea.Daktari alishika mlango wa chumba special alicholazwa Cindelela kwaajili ya kuufungua ili waingie ndani
SONGA NAYO
Alex aliendelea kutetemeka mpaka akawa anajishangaa kwanini hali kama ile inamtokea.Kuna kitu kilikuwa kinamuambia Alex kwamba aondoke hapo haraka sababu anaweza kupata tatizo la ghafla kutokana na hali aliyokuwa nayo.Alex aliamua kumshikia mkono daktari ili kumuambia jambo
“samahani dokta kicha changu sikielewi elewi na sijui ni kwanini hali kama hii inanitokea”Alex alimuambia daktari ambae alikuwa ndo anaufungua ule mlango ili waingie ndani
“kwani huyu mgonjwa ni nani yako?”Dokta aliuliza
“mgonjwa sina uhusiano nae wowote zaidi ya kuwa ni mwanafunzi mwenzangu”Alex alisema
“sasa mbona naona hali yajko imebadilika sana tangu tumeanza kuondoka pale ofisini”dokta alisema huku akirudi nyuma
“mimi mwenyewe najishangaa sana kwanini natokewa na hali hiii”Alex alisema
“nisubiri nakuja”Dokta alisema na kuondoka
Dokta alitoka pale na kumuacha Alex akiwa amesimama pale pale akiwa ajielewi vizuri,baada ya dakika tatu daktari alirejea pale huku akiwa ameshika chupa ya maji mkononi mwake.Alimpa Alex ile chupa ya maji na kumuambia ayanywe yote sababu alionekana na presha ya kwenda kumuangalia mgonjwa.
“aya tunaweza kuingia”dokta alisema baada ya kuona Alex hofu yake imeshaondoka
Waliingia mule chumbani na kwa mbali Alex aliona mtu amelala kwenye kitanda akiwa anaangalia juu huku kawekewa kifaa cha oxygen ili kimsaidie kupumua.Miguu ya Alex ilianza kuwa mizito kutembea sababu kila akiiangalia ile sura alikuwa anaifahamu.Dokta alikuwa anamshangaa Alex sababu alikuwa anatembea pole pole huku akiburuza miguu yake
Alex machozi yakaanza kumtoka baada ya kukaribia kwenye kile kitanda na kumkuta aliyelala pale ni msichana anayempenda kuliko wasichana wote kwenye huu ulimwengu.Japo Cindelela alimjibu majibu ya kashfa na fedhea lakni Alex akupunguza upendo wake kwa Cindelela sababu ndiyo ulikuwa upendo wake wa kwanza tangu afikie umri wa utu uzima
“Cindelela mungu anamakusudi na sisi na ametukutanisha hapa ili kila mtu ajue kwamba milima haikutani lakini binadamu wanakutana.Cindelela nakupenda kwa moyo wangu wote japo mimi ni masikini wa mali lakini leo naweza nikawa tajiri katika kurudisha uhai wako.Eee mungu nashukuru kwa kunikutanisha tena na mwanamke ambae nampenda kutoka ndani ya nafsi yangu na naomba umrudishie uhai wake kwa mara nyingine tena”Alex alisema na kumbusu Cindelela kwenye paji la uso
Kipindi hicho chote Dokta alikuwa amekodoa macho sababu alikuwa hajui Alex anazungumza nini kwani Alex alikuwa anatumia lugha Kiswahili kuongea na Cindelela ambaye amepoteza fahamu.Kile kitendo cha kumbusu na yale machozi yaliyokuwa yanamtoka Alex, dokta alijua kwamba kuna kitu kinaendelea kati ya wale wawili
Walitoka pale wodini na kuelekea kwenye ofisi ya daktari ili wajue ni kitu gani cha kufanya ili warudishe uhai wa Cindelela sababu alikuwa kwenye hali mbaya sana.Walikaa kwenye viti ili wazungumze namna ya kufanya ili kumsaidia Cindelela katika hali aliyokuwa nayo
“Alex unamfahamu yule dada?”Dokta alimuuliza Alex
“ndiyo namfahamu sana”Alex alijibu
“ni nani yako?”dokta aliuliza tena
Alex alimuambia daktari kila kitu kilichotokea huko nyma kuhusu yeye na Cindelela lakini akamwambia asije akamueleza mtu kitu chochote hasa wazazi wake na Cindelela.Alex hakutaka kabisa wazazi wa Cindelela wamfahamu kuwa yeye ni nani wala kumuona hata sura yake
“Alex upo t6ayari kumsaidia Cindelela?”dokta aliuliza
“mimi nipo tayari lakini nahofia kama italeta madhara yoyote kwenye hali yangu ya kucheza mopira”Alex alisemaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-
“Hapana hali yako itaendelea kama kawaida na utaendelea kucheza mpira kama mwanzo,wapo watu wengi sana wanaishi wakiwa na figo moja lakini bado wanaendelea na shuguli zao kama kawaida” Dokta alimuambia Alex
“Kwasababu ni huyu mwanamke sina budi kufanya hivi lakni naomba nipate idhini kutoka kwenye uongozi wa timu ili waniruhusu “Alex alisema
Alex alichukua simu na kuwapigia viongozi wa timu yake ili wamruhusu kutoa figo.Japo uongozi uliweka ngumu lakini Alex akaweka msimamo wake na kwa kusaidiana na daktari walifanikiwa kuwashawishi sababu ilionekana hakuna madhara yoyote.Kikubwa walichokifanya ni kuweka siri baina ya uongozi na Alex mwenyewe kwani hawakutaka suala lile lifike kwa waandishi wa habari
“Alex tunahitajika tufanye haraka ili tunusuru maisha ya umpende”Dokta alisema na kumfanya Alex achanganyikiwe kusikia neon umpendae
“okey me nipo tayari”Alex alisema
Dokta alitoka na kwenda kuzungumza na madaktari mwengine kwaajili ya kuanza upasuaji wa haraka.Manesi walipeleka vifaa vyote kwaajili ya upasuaji unaotakiwa kuanza.Alex alichukuliwa na moja kwa moja akapelekwa kwenye chumba cha upasuaji.Ndani ya chumba icho kulikuwa na madaktari sita waliovalia mavazi ya kijani wakiwa tayari kwa kufanya operation mbili,ya kwanza ni kumtoa Alex figo moja nay a pili ni kumuwekea Cindelela figo kutoka kwa Alex
Alex alilazwa kwenye kit6anda huku akitetemeka kwa hofu baada tya kuona visu na mikasi vikiwa pembeni yake.Alichomwa sindano ya usingizi na taratibu kiza kikaanza kutanda kwenye macho yakeAlex alipotelea kwenye usingizi mzito na kufanya madaktari waanze kazi yao kwa harakalakini kwa umakini mkubwa sana
Operation ilichukua muda mrefu sana mpaka kukamilika sababu ilikuwa ni ya watu wawili.Baada ya operation kuisha Alex alichukuliwa na kupelekwa kwenye chumba kingine tofauti na Cindelela sababu Alex alisema kwamba hataki mtu mwingine yoyote ajue kama yeye ndiyo aliyejitolea ile figo mpaka pale Cindelela atakapopata fahamu
Siku zilikatika huku hali ya Alex ikiendelea vizuri na kwa upande wa Cindelela alishaanza kufumbua macho na kurudisha fahamu yake japo siyo sana.Kabla Cindelela ajapata fahamu Alex alikuwa anachukuliwa na kupelekwa alipolazwa Cindelela kisha anarudishwa chumbani kwake
“Ni nani aliyejitolea kumpa mwanagu figo?”Mzee Jacobo alimuuliza Daktari
“Kuna kijana mmoja hivi ila kwa sasa hayupo hapa sababu amerudishwa alipokuwa”Daktari alidanganya
“na kuhusu malipo yake je?”Mzee Jacobo aliuliza
“amesema asilipwe kitu chochote kwani amejitolea kwa mapenzi yake mwenyewe na siyo kwaajili ya pesa”Daktari alisema
Mzee Jacobo alishangaa sana kuona mtu amejitolea figo bila ya kutaka malipo yoyote yale.Alijiuliza sana huyo mtu atakuwa ni nani sababu ameonyesha moyo wa upendo sana kwa binti yake
“Dokta naomba hata unielekeze kwa huyo mtu ili nikampatie shukrani zangu”mzee Jacobo alisema
“huyo mtu amesharudishwa Tanzania”Dokta alisema na kumfanya mzee Jacobo azidi kuchanganyikiwa baada ya kusikia huyo mtu ni mtanzania
Siku zilikatika na hali ya Cindelela ikawa inaendelea vizuri kiasi kwamba akawa anaweza hadi kuongea.Mzee Jacobo na mkewe walitakiwa kurudi Tanzania ili wakaendelee na majukumu mengine ya kitaifa sababu hali ya mtoto wao ilikuwa inaendelea vizuri sana
“dokta kwani mimi nilikuwa naumwa nini?”Cindelela aliuliuliza siku moja walipokuwa na daktari
Dokta alimuambia kila kitu kilichotokea lakini alificha kutaja jina la mtu aliyejitolea figo kwa ajili ya kurudisha uhai wake
“Dokta naomba unitajie huyo mtu aliyejitolea kwaajili yangu,tafadhari dokta nipo tayari kumpa zawadi yoyote atakayoitaka sababu amejitolea maisha yake kwaajili yangu”Cindelela alisema akimuambia daktari
“Subiri kwanza binti ukipona vizuri nitakuletea huyo mtu”dokta alisema
“kwani bado sijapona vizuri?au huyo mtu aliyejitolea kwaajili yangu amekufa mnanificha?”Cindelela alionekana kuchanganyikiwa na kuuliza maswali kama kichaa
“kwa hali aliyokuwa nayo huyu binti nikimleta Alex anaweza kupata matatizo mengine sababu lazima apatwe na mshtuko”dokta alijisemea mwenyewe
“Dokta mbona haunijibu?”Cindelela aliuliza huku machozi yakimtoka
“basi nitamleta wala usijali”Dokta alisema na kuondoka ili kumuacha Cindelela apumzike
Cindelela alikuwa anajiuliza sana ni mtu gain aliyejitolea kwaajili yake.Hamu ya kutaka kumuona kijana huyo ilifika kooni na kufanya muda wote awe anamsumbua daktari ili amlete huyo kijana amuone.Pindi Cindelela anapokuwa usingizini Alex alikuwa anachukuliwa na kupelekwa kumuona Cindelela
“Dokta kwa sasa mimi nimepona naomba umlete basi huyo kijana,na kama amekufa naomba mnipeleke kwenye kaburi lake nikampe shukrani yangu”Cindelela alisema
“Usijali leo nitamleta umuone sababu umeshapona kabisa”Dokta alisema
Dokta alichukua simu na kupiga ili Alex aletwe pale wodini kumuoa Cindelela.Cindelela moyo wake ulianza kufurahi sababu alikuwa na hamu sana ya kumuona huyo mtu aliyejitolea ili yeye apone.Muda wote macho yake yalikuwa yanaangalia kwenye mlango ili amuone huyo kijana wakatia anaingia
Alex baada ya kupewa taarifa kuwa anatakiwa kufika kwenye chumba alicholazwa Cindelela,haraka haraka alianza kuelekea mpaka kwenye kile chumba na kusimama mlangoni kwa dakika moja bila kufanya kitu chochote.Alishika mlango na kuanza kuusukuma ili aingie ndani ya kile chumba alkicholazwa Cindelela
Alex alisimama kwa muda pale mlangoni huku akitaka kuingia ndani ili akaonane tena na Cindelela.Mapigo ya moyo yalikuwa yanamuenda mbio sababu alikuwa anawaza kama Cindelela bado ataendelea na hule msimamo wake au laa.Taratibu alianza kufungua mlango na kuanza kuvuta hatua moja ndani ya ule mlango huku akitabasamu
Cindelela hakugandua macho yake pale kwenye mlango sababu alikuwa anataka kumuona mtu aliyesababisaha mpaka yeye kuwa hai kwa kipindi hicho.Cindelela alipokuwa anaona mlango ukifunguliwa alizidi kukodoa macho ili kumuona ni kijana gani ataingia mule ndani ya chumba
Cindelela alipigwa na bumbuwazi baada ya kumuona Alex akiingia ndani ya kile chumba huku akitabasamu kwa furaha,Cindelela hakutaka kuamini kama mtu anayemuona pale ni Alex aliyemkataa siku nyingi wakiwa nchini Tanzania.Tararibu machozi yakaanza kumtoka kila Alex alipokuwa anamsogelea pale Alipokuwa
“Am sorry Alex(Samahani Alex)”Ilo ndiyo lilikuwa neon la kwanza kumtoka Cindelela huku machozi yakimtoka kwa wingi na kusababisah uso wake ulowe machozi
“Sorry for what Cindelela?I forgot everything and I am here to open new page with you because God taught you how life goes ,please don’t cry Cindelela Am here for you(Samahani ya nini Cindelela?,nimeshasahau kila kitu na nipo hapa kufungua ukurasa mpya na wewe kwasababu mungu ameshakufundisha maisha yanaendaje,tafadhari usilie Cindelela nipo kwaajili yako)”Alex alisema kwa hisia kali huku machozi yakimtoka kama maji kwenye uso wake
Dokta alipoona vilio vinazidi sana akaamua kutoka nje ili kuwaopisha kwani hata yeye machozi yalikuwa yanamlenga kwasababu Alex alishamuambia kila kitu kilichotokea nyuma.Kwa ujasili na mapenzi aliyoonyesha Alex kwa Cindelela hata dokta mwenyewe aliyanshangaa kutokana na majibu ya kashfa aliyojibiwa Alex
“Cindelela mimi bado nakupenda sana na nipo tayari kwa lolote hata kama ni kupoteza uhai wangu kwaajili yako.Nkuomba unipe japo nafasi ndani ya moyo wako ili na mimi niridhike sababu najiona kama sijakamilika bila ya kuwa na mtu kama wewe”Alex alisema huku akikaa kwenye kitanda alicholala Cindelela
“Alex”Cindelela aliita kwa kusitaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Please niambie Cindelela kama una….”Alex alijikuta akizibwa mdomo na kiganja cha Cindelela mpaka mwili wake ukasisimka kwani alikuwa ajamalizia kusema alichokusudia
“Nakupenda Alex wala sina budi kusema maneno hayo sababu kwa uliyonionyesha tu inatosha kuonyesha kwamba unanipenda kwa moyo wako wote na mimi nakuhaidi kukupenda mpaka mwisho wa uhai wangu.Alex narudia tena NAKUPENDA SANA”Cindelela alisema na kumkumbatia Alex kwa nguvu na kufanya Alex mapigo ya moyo yawe yanamuenda mbiyo mfano wa mtu aliyetoka kukimbizwa na kundi la majambazi
Moyo wa Alex ulilipuka kwa furaha na kujikuta ni mshindi katika vita aliyokuwa anapambana.Mara ya kwanza hakutaka kuamini kama aliyetamka maneno yale ni Cindelela mwenyewe.Alimtoa kichwa chake pale kwenye bega na kumshika mabega yake huku akimuangalia usoni ili amtazame kwa umakini kama ndiyo yeye anayetamka maneno yale
“Alex naomba uniamini ninachosema,nipo tayari kuwa na wewe sehemu yoyote utakayoenda na nahapa sitokuacha milele”Cindelela alisema
“Nashukuru sana Cindelela kwa kunipa amani ya moyo wangu,Amani ambayo niliikosa kwa muda mrefu sana,Amani iliyonitoka tangu nilipokutana na wewe kwa mara ya kwanza.Hakika mungu ni waajabu na ninapasa nimshukuru”Alex alizungumza na kupeleka macho yake juu kwa ishara ya kumshukuru mungu aliye juu
Waliongea mengi sana huku Alex akionyesha furaha ya ajabu na kujikuta yupo ndani ya bustani ya Edeni akiwa amezungukwa na wanyama wazuri waliokuwa wanafurahia upendo wao huku miti na maua ikitoa harufu nzuri ya kupendezesha upendo kati yake na Cindelela
“Alex unatakiwa umuache mgonjwa kwa muda mfupi kisha utakuja kuzungumza nae baadae kidogo sababu leo ataruhusiwa kuondoka”Alex alisikia sauti ya Daktari ikimuambia
Alex alimbusu Cindelela shavuni na Cindelela nae akarudisha mapigo kwa busu zuri lililomsisimua Alex.Kama daktari alivyomuambia Alex alitoka nje na kwenda kukaa sehemu ili aitwe tena kuzungumza na Cindelela sababu hamu yake ilikuwa bado haijaisha
Alex alionekana kuchekacheka mwenyewe kama mtu anayeugua uchizi sababu hakutegemea kama juhudi zake zimezaa matunda na kufanikiwa kukipata kitu akipendacho.Kwa mtu aliyekuwa anamuangalia Alex kwa muda mrefu angejua kwamba kijana huyo anaugua uchizi lakini mambo yalikuwa ni tofauti.Alex amepata kitu alichokuwa anakitaka ndiyo maana muda wote alikuwa na furaha
Alex alikuja kuitwa na manesi kwaajili ya kwenda kuonana na Cindelela kwa mara nyingine kwani Mzee Steven alishakuja kumchukua kwaajili ya kurudi nae katika jiji la Birmingham kuendelela na masomo yake.Mzee Steven alipomuona Alex alifurahi sana japo alikuwa hajui ni kitu gain kilichokuwa kinaendelea kati ya Alex na Cindelela
Mzee Steven ambae ni rafiki wa baba yake Cindelela alikuwa anamfahamu Alex ni mwanafunzi katika chuo cha Birmingham University ambacho anafundisha,Vilevile alikuwa anafahamu kwamba Alex ndiyo raisi wa wanafunzi pale chuoni.Alikuwa hajui kama Alex ndiyo kijana aliyejitolea figo kwa Cindelela na kwasasa wameshakuwa wapenzi
“Wewe ni kiongozi mzuri sana sababu umekuja kumuangalia mwanafunzi mwenzako anaendeleaje siyo siri nimefurahi sana’Alisema mzee Steven bila kujua chochote
“Nilipaswa kufika hapa sababu huyu ni mwanafunzi mwenzangu pia tunatokea katika nchi moja”Alex alisema bila kuweka bayana kwamba yeye ndiyo aliyejitolea figo kwaajili ya Cindelela
“okey sisi ndiyo tunarudi chuoni vipi na wewe si ndiyo unaelekea huko?”Mzee Steven alimuuliza Alex
“na mimi ndiyo narudi kwani nilikuja huku kwaajili ya kumuangalia mgonjwa tu”Alex alijibu
“basi tutakuwa kwenye ndege moja”alisema mzee Steven
“ndiyo”alijibu Alex
Wakati yote yanazungumzwa Cindelela alikuwa anaangalia tu bila kuchangia neon lolote.Alex alitoka pale na kwenda kuonana na Daktari ili waagane na kurudi kwao.Waliongea maneno machache na kubadilishana namb a za simu kwani tayari walishajenga urafiki japo kwa muda mfupi tu
Alex alitoka na kuungana na wkina Cindelela kwaajili ya kuelekea uwanja wa ndege.Muda wote Alex alikuwa anamuangalia Cindelela kwani bado alikuwa ahamini kama ni kweli Cindelela ameshakuwa mpenzi wake.Ndani ya ndege walifanikiwa kukaa pamoja na Mr Steven alikuwa mbali.
Cindelela aliweka kichwa chake kwenye kifua cha Alex huku akitabasamu na kufanya vishimo vya mashavu viwe vinamtoka.Cindelela alikuwa anasikilizia mapigo ya moyo wa Alex yakikimbia kwa kasi mkama treni ya umeme
“Alex wewe ni wangu na sitokupoteza katika maisha yangu nisamehe kwa yote niliyokukosea kwani sikujua kama binadamu tunaweza kukutana sehemu ambayo hatukuweza kutegemea.Kila nikikuangalia nahisi kama nilifanya dhambi kubwa sana kwako”Cindelela alizungumza kwa uchungu na kufanya Alex machozi yamdondoke
“Cindelela mimi nimeshasahau kila kitu kilichotokea nyuma na hapa nilipo moyo wangu ni mweupe wala sina kinyongo na wewe mpenzi wangu”Alex alisema huku akimtazama Cindelela
“nashukuru sana Alex kwa kunisamehe na mimi nakuhaidi sitokufanyia kitu kibaya katika maisha yangu yote”Cindelela alisema na kumkumbatia Alex
“Usijali mpenzi wangu”Alex alisema
“Alex umefikaje huku?”Cindelela aliuliza
Alex alimuambia mchakato mzima uliomfanya mpaka yeye kufika katika jiji hilo.Cindelela alikuwa anamuangalia Alex kwa makini wakati anazungumza maneno yale
“Alex ni wewe ndiyo mchezaji aliyeandika NAKUPENDA CINDELELA wakati anafunga goli?”Cindelela aliuliza
“ni mimi niliyeandika vile lakini nilikuwa sijui kama upo katika nchi hii”Alex alisema
“Alex nakushukuru sana na kweli unamapenzi ya kweli kwangu”Cindelela alisema huku akipata joto zuri katika mwili wa Alex
Walifika kwenye jiji la Birmingham na kila mtu alielekea kwenye nyumbani kwake.Hawakutaka mzee Steven ajue kitu chochote kinachoendelea baina yao kwani walitaka mapenzi yao yawe siri mpaka pale watakaporudi Tanzania.
“John hauwezi amini kama huyo mwanamke mnayemuhita Alice ndiyo Cindelela niliyekuwa nakuambia siku zile”Alex alikuwa anamuambia rafiki yake
“acha masihara”Alisema John
“Siyo masihara icho ni kitu cha ukweli na siku siyo nyingi utaanza kutuona pamoja kwani tayari…..”Alex aliishia hapo hapo
“Tayari nini Alex?”Aliuliza rafiki yake
“nitakuambia siku nyingine”alisema Alex
Waliendelea na story nyingine huku muda mwingine Alex alichukua simu yake na kumpigia Cindelela ili kumjulia hali.
“Alex nataka nimpigie simu Wit ili nimuambie kama mimi na wewe tumekutana huku”Cindelela alisema
“aya ukimaliza utaniambia “Alex alisema
Walipokata simu Cindelela akampigia Witi ili amuambie kama amekutana na Alex nchini Uingereza
“Wit kusema ukweli dunia ni ndogo sana na usije ukamdharau mtu kwa jinsi alivyo”Cindelela alisema baada ya Wit kupokea simu yakeCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“kwanini unazungumza hivyo?”aliuliza Wit
“Wit hauwezi amini kwamba ni Alex nipo nae hapa Uingereza na ni mtu maarufu katika jiji la Birmingham kuliko unavyotegemea”Alisema Cindelela
“Cindelela nadhani kichaa kinakupanda,Alex si yule kaka uliyekuwa unamdharau na kumuhita masikini sasa huko Uingereza anafanya nini?”Wit aliuliza
“kwasasa Alex ni mchezaji mpira maarufu katika jiji ili pia ni mwanafunzi katika chuo ninachosoma mimi na ndiyo raisi wa wanafunzi”Cindelela alisema
“Wewe umekosa maneno ya kuniambia”Wit alisema
“nitapiga picha Arafu nitakutumia”Cindelela alisema na kukata simu
Mapenzi kati ya Cindelela na Alex yalianza kupamba moto huku kila Alex anapokuwepo Cindelela na yeye yupo hapo hapo.Ktika kila mechi anayocheza Alex Cindelela alikuwa hakosi hata mechi moja kwani yeye ndiyo ilikuwa chachu ya Alex kupata magoli na kuonyesha T shirt yake iliyoandikwa NAKUPENDA CINDELELA
Wlipiga picha nyingi sana na kumtumia Wit aliyekuwepo Tanzania.Muda mwingine Alex alikuwa anapata fursa ya kuongea na Wit huku akimshukuru sana kwa msaada aliokuwa anampa mwanzoni
Kwa jinsi mapenzi yao yalivyokuwa yanakuwa kwa kasi na kufanya jiji zima lijue kwamba Alex anampenzi aitwae Cindelela.Vyombo vya habari navyo havikuwa nyuma kurusha picha tofauti tofauti za Alex akiwa na Cindelela kwenye mapozi ya kimapenzi
“Jamani wanapendezana sana”ilisikika sauti yam dada wa kizungu akisifia wakati Alex na Cindelela wakiwa wameongozana
Taarifa za mahusiano kati ya Alex na Cindelela zilimfikia Mr Steven na kuamua kumpigia simu mzee Jacobo ili kumpasha habari kwamba mwanae anatoka na kijana mmoja ajulikanae kwa jina la Alex
“Haiwezekani hivi nitamuambia nini mr Thomas na mwanae”Alifoka mzee Jacobo
“kwani kuna nini?”aliuliza Mr Steven
“Sikia mimi na mzee Thomas ni marafiki wakubwa sana na nilishamuhaidi kwamba mtoto wake lazima aje kumuoa Cindelela sababu tunataka kuunganisha urafiki wetu ili tujenge undugu”alisema mzee jacobo
“Kwahiyo unafanyaje wakati mwanao ndiyo tayari yupo na huyo kijana?”mr Steven aliuliza
“kwani huyo kijana ni nani?na kwanini awe na mwanangu?hivi anajua mimi ni nani?siwezi kuruhusu hayo mahusiano arafu nikaharibu undugu wangu mimi na Mr Thomas.Lazima nimfanye kitu huyo kijana”alifoka mzee Jacobo na kukata simu
Mzee jacobo alikasirika sana hasa baada ya kusikia mtoto wake anatoka na kijana mwingine wakati yeye alishamuandalia mwanae mwanaume ambaye atakuja kumuoa.Mzee Jacobo na Mr Thomas walikuwa ni marafiki wa muda mrefu sana japo Mr Thomas alikuwa na asili ya Sweden
Urafiki wao ulitengenezwa siku moja wakati mzee Jacobo alipoenda nchini Sweden kwa ziara ya muda mrefu.Huko ndipo alipokutana na Mr Thomas kisha wakajenga urafiki mkubwa sana ambao uliwafanya wawe kama ndugu.Kwakuwa mr Thomas alikuwa na mtoto wa kiume na mzee Jacobo alikuwa na mtoto wa kike ambaye ndiyo Cindelela walipanga kwamba watafanya liwezekanalo ili Cindelela aje kuolewa na mtoto wa Mr Thomas ili kuuendeleza undugu wao
Kwa hizo taarifa alizozipata kwamba Cindelela anatembea na kijana mwingine tofauti na mtoto wa mzee Thomas ilikuwa ni kama fedhea kwake ndiyo maana mzee Jacobo alionekana kuchanganyikiwa sana baada ya kupata ile taarifa kutoka kwa Mr Steven
“Ilo swala sitoweza kurikubali litokee”Mr Jacobo alisema kwa nguvu bila kujua kama mke wake yupo karibu yake
“kuna nini mume wangu?”mkewe aliuliza
“si huyu mwanao anataka kuniaibisha”Mzee Jacobo alisema
“anakuaibisha na nini mume wangu?mkewe aliuliza
“nasikia amepata mwanaume huko alipokuwa”Alisema mzee Jacobo
“wewe nani amekuambia hivyo?”mkewe aliuliza
“ameniambia mr Steven”Mzee Jacobo alisema huku akiwa amekunja sura na jasho zikimtoka
“sasa mume wangu sidhani kama kuna haja ya kupinga sababu Cindelela siyo mtoto tena.Kama ni kweli wamependana ni vizuri kama wakija kujitambulisha hapa kwetu ili tujue mahusiano yao “mkewe alisema
“Hivi wewe mwanamke una kichaa?,sitaki tena kusikia upuuzi wako,unadhani nitamuambia nini Mr Thomas?unajua ahadi gain tuliyopanga na Mr Thomas?”Aalifoka mzee Jacobo
“kwani huyo mr Thomas ni nani mpaka aingilie mahusianio ya mtoto wako?”aliuliza mkewe
“nilishapanga kwamba Cindelela atakuuja kuolewa na mtoto wa Mr Thomas “alisema
“mume wangu naona unachanganyikiwa,na elimu yako yote bado unampangia mwanao mwanaume wa kumuoa?hivi wewe wazazi wako walikupangia unioe mimi?Muache mtoto na maamuzi yake”Mkewe alisema na kushangaa akipokea kibao cha uso na kufanya adondoke kitandani
Kwa hasira alizokuwa nazo mzee Jacobo hakutana kuongea neon lingine zaidi ya kuchukua simu yake na Kumpigia Cindelela ili amtaadharishe kuhusu huyo kijana.Kila alipokuwa anapiga simu aliambiwa simu haipo hewani,mzee Jacobo alijaribu mara kwa mara na kujikuta akikata tamaa ya kuendelea kupiga simu kwa mwanae
“huyo kijana lazima nimkomeshe”alisema Mzee Jacobo huku akipiga ngumi kwenye ukuta
……………………………………………………………………………………………………………………..
Mapenzi ya Alex na Cindelela yaliendelea kusambaa kwa kasi kwani kila mtu ndani ya jiji ilo alikuwa anajua kwamba Alex na Cindelela ni wapenzi.Sehemu yoyote uliyokuwa unamuona Alex Cindelela nae alikuwa pembeni yake sababu walipenda sana kuongozana pamoja
Picha mbalimbali zilikuwa zinasambaa kwenye mitandao kuhusu Alex na Cindelela wakiwa kwenye mapozi tofauti tofauti.Picha hizo zilisambaa na kumfikia mzee Jacobo kitu kilichomuongezea hasira na kumfanya aanze kupanga njama mbaya sana juu ya Alex
“Alex mpenzi wangu lini tunarudi Tanzania?”Cindelela aliuliza siku moja wakiwa katika mgahawa mmoja wakipata kifungua kinywa
“bora umeniuliza sababu natamani sana nikapaone nyumbani kwetu,siku siyo nyingi tunafunga chuo na kipindi hicho ligi itakuwa imesimama kwahiyo nitaomba kurudi nyumbani ili nikawaone wazazi wangu”Alex alisema
“natamani sana turudi wote ili nikakutambulishe nyumbani kwetu nadhani watafurahi sana kukuona”Cindelela alisema
“Kama watanipokea vizuri nitafurahi sana ila naomba usiwaambie kitu chochote kuwa mimi ndiyo nimekutolea figo”Alex alisema kwa umakini
“wala usijali mpenzi wangu ila mimi natamani sana hata kesho turudi Tanzania sababu nataka nimuonyeshe Wit kama kweli nakupenda”Cindelela alisema
“Usijali mpenzi wangu tutarudi”Alex alisema na kumbusu Cindelela kwenye shavu lake
Siku zilikuwa zinaenda huku mapenzi nayo yakiwa yanapanda kwa kasi sana.Katika interview zote alizokuwa anahojiwa Alex na vyombo vya habari,alikuwa hakosi kutaja jina la Cindelela
“tunapenda sana kujua kwanini kila ukifunga goli kuna maandishi unayaonyesha kwenye t shrt yako ya ndani?”Alex aliulizwaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“yule ndiyo mtu anayesababisha mpaka mimi napata magoli mengi sana uwanjani”Alex alijibu
“kivipi wakati wewe ndiyo unayecheza mpira?”Alex aliulizwa swali jingine
“kila nikiwa uwanjani nakumbuka sana tabasamu lake pia nakumbuka sana maneno yake matamu anayoniambia juu ya kuongeza juhudi katika kucheza mpira,Cindelela ni mtu anayenifanya niwe na amani muda wote,yeye ndiyo mtu aliyenifanya mpaka niwe katika timu hii sababu bila yeye nisingekuwa na juhudi za kufika katika nchi hii”Alex alisema
“kwani yeye ndiyo amekuleta katika nchi hii?”Alex aliulizwa
“Ilo swala tutazungumza siku nyingine”Alex alisema na kumaliza mahojiano
Alitoka nje na kuongozana na Cindelela ili kuelekea sehemu walikopaki gari.Wakati Alex anatembea kwabahati mbaya alijikwaa na kuinama chini.Hiyo ilikuwa pona yake kwani wakati anainama chini mlio wa risasi ulisikika na risasi mbili zilipita juu yake
Hali ya hewa ilibadilika ghafla sababu kila mtu alikuwa anakimbilia upande wake ili kukimbia kifo.Alex alimshika mkono Cindelela kwa nguvu zote na kuanza kukimbilia upande mwingine ili kujificha.Mapigo ya moyo wa Cindelela yalikuwa yanaenda kwa kasi sana sababu hakijua ni nani aliyekusudiwa kuuwawa na zile risasi
Baada ya muda kidogo hali ilionekana kuwa shwali na watu wakaanza kujitokeza waliopojificha.Mwili wa Alex ulishakufa ganzi kwani hakujua ni nani aliyekuwa anataka kumuua na kwanini alikuwa anataka kumuua?.Kikubwa alichokuwa anashukuru ni kule kujikwaa kwake kwani ndiyo kulisababisha akwepe zile risasi
Police walifika eneo lile na kuanza kuhoji watu kuhusu kitu kilichotokea,Kila mtu alionekana kutaja jina la Alex kwamba ndiyo mtu aliyekuwa analengwa na zile risasi.Police walimfuata Alex na kuanza kumuhoji mwaswali ili awaambie ni gain kimetokea mpaka watu wanataka kumuua
“mimi hata sielewi sababu nimejikuta tu risasi zikipita juu yangu”Alex alisema
“kwani unaugomvi na mtu yoyote?”Alex aliulizwa
“hapana sina ugomvi na mtu yoyote “Alex alijibu
“twende kituoni ili tukakuhojizaidi”
Alex alichukuliwa yeye na mpenzi wake kisha wakapandishwa kwenye gari la police ili wakahojiwe zaidi.Alex alisema kila kitu anachokifahamu lakini hakuweza kumtaja mtu yoyote mwenye ugomvi nae sababu kwa kipindi hicho alikuwa hana mkwaruzano na mtu yoyote.Alipomaliza kuhojiwa Alex alitoka nje kwaajili ya kurejea nyumbani kwake ili akaangalie nini cha kufanya kwani hofu ilishaanza kumtanda kwenye kichwa chake.Akiwa ndani ya gari alishangaa kuona simu yake ikiita kwa private namba,aliiangalia sana ile simu na kuamua kuipokea ili ajue ni nani anayepiga
“hallo”Alex alisema baada ya kupokea simu
“Hallo kijana mwenzangu napenda nikutaadharishe kwamba uachane na huyo binti kwani anatakiwa awe mke wa mtu hivi karibuni na usipofanya hivyo nadhani unatamani kufa”ilikuwa ni sauti ya mwanaume ikizungumza kwa rafudhi mbaya ya kisomali
“unasemaje?Alex alipayuka kwa nguvu huku jasho zikimtoka
Simu ilipokatika Alex hakujua afanye nini kwani hakuwa akielewa chochote,Kijasho kilikuwa kinamtoka sababu hakujua ni nani anayefanya mchezo ule wa kumtishia.Aligeuza macho yake pembeni na kumuangalia Cindelela ambaye naye alikuwa amemkodolea macho ya udadisi akitaka kujua ile simu inahusu nini
“Alex mbona unatetemeka?”ilo ndiyo lilikuwa swali la kwanza kutoka kwa Cindelela
“Simu mpenzi”Alex alisema kwa uoga
“simu imefanyaje?”Cindelela aliuliza tenja
Alex alimuambia Cindelela maneno yopte aliyoambia na mtu aliyempigia.Cindelela hakutajka kuamini kama ni yeye ndiye aliyekuwa anazungumziwa kwenye ile simu iliyopigwa.
“Cindelela kwani wewe unamchumba?”Alex aliamua kuuuliza
“hapana mimi sina mpenzi mwingine zaidi yako Alex”Cindelela aliongea huku akimkumbatia Alex
“sasa mbona wananiambia niachane na mwanamke niliyekuwa nae kwani anahitajika kuwa mke wa mtu hivi karibuni?”Alex alimuuliza Cindelela
“Alex mimi sijui chochote”Cindelela alisema kinyonyonge
“Basi liwalo na liwe ila naapa sikuachi acha tu waniue”Alex alisema
“Nakupenda Alex na ili swala lazima nilifikishe kwa Dady kwamba kuna watu wanataka kumuua mpenzi wangu”Cindelela alisema
Ndani ya kipindi kifupi Alex alikuwa anakosa rah asana japo Cindelela alijitahidi kumfariji kwa kuwa nae karibu.Kila siku Alex alikuwa anapokea simu za vitisho vikimtaka amuache Cindelela.Taarifa hizo zilifika mpaka kwenye uongozi wa timu na kuamua kumuwekea Alex ulinzi kila alipokuwa anaelekea
Taratibu mashambuliuzi zidi ya Alex yalianza kupungua na kumfanya Alex aanze kujisikia tena Amani.Baada ya muda kidogo Alex alikuwa huru na uongozi wa timu ukaamua kuwatoa walinzi sababu hakukua tena na vitisho zidi yake.Mapenzi yake na Cindelela nayo yalizidi kusonga kwa kasi kwani ilifika hatua walianza kupanga mipango ya kuoana hata kabla hawajawasiliana na familia zao
“Cindelela mimi kwetu hawana shida kabisa labda nyumbani kwenu”alisema Alex
“Alex hakuna mtu atakayeleta kipingamizi sababu mimi ndiyo nimeamua kukupenda na sitokubali mtu yoyote apinge mapenzi yetu “Cindelela alisema
“Cindelela lazima tupate baraka za wazazi wote wawili”Alex alisema
“Ndiyo lakini hawatoweza kunipangia niwe na nani”Cindelela alisema
“mh basi yaishe manake tumeshaanza kuweka gundu wakati hata bado hatujaenda kuwaambia”Alex alisema
“sawa mpenzi wangu”Cindelela alisema
Mipango ya kurudi Tanzania ikaanza kupangwa sababu kipindi hicho kilikuwa cha likizo na ligi ilikuwa imeshasimama.Alex alikuwa na hamu sana ya kwenda kuwaangalia wazazi wake sababu kilishapita kipindi kirefu sana bila kuwaona wazazi wake.Vilevile Alex alikuwa na hamu sana ya kwenda kuwaona wazazi wa Cindelela ili wamtambue kwamba ni mkwe wao
Siku ya kuondoka Alex na Cindelela walielekea uwanja wa ndege na moja kwa moja safari ya kurudi nchini Tanzania ikaanza.Moyoni Alex alikuwa na furaha sana kurudi Tanzania sababu alipakumbuka sana.Aliwakumbuka sana rafiki zake pia alikumbuka maisha ya nyumbani kwao japo walikuwa wanaishi kwa dhiki
“Cindelela natamani sana tufike nyumbani”Alex alisema
“hata mimi kwani nimepakumbuka sana”Cindelela alisema
“Cindelela tukifika tu sitotaka tupoteze muda,nataka nikuoe kabisa uwe mke wangu wa ndoa”Alex alisema huku akitabasamu
“Hata mimi nina hamu sana ya kuwa mke wako Alex”Cindelela alisema
Waliongea mengi sana mpaka Alex akapitiwa na usingizi,Usingizi ulimchukua na kujikuta yupo katikati ya ndoto,ndoto ambayo alishawai kuiota Hapo awali kabla ajawa na Cindelela
Alex alikuwa anaota yupo katika maporomoko ya maji huku mbele yake alionekana Cindelela akimuangalia kwa macho yenye mahaba japo alikuwa amechoka sana
“Alex nakupenda sana na sipo tayari uteseke wakati mimi nipo”Cindelela alisema huku akimsogelea Alex aliyeonyesha kuwa na wasiwasi
“Nakupenda pia Cindelela na wewe ndiyo mwanamke wa maisha yangu,naapa kwa mungu kwamba sitoweza kukuacha mpaka kufa kwangu”Alex alisema huku akitanua mikono ili ampokee Cindelela
Ghafla kabla Cindelela hajamfikia pale alipokuwa alijikuta Akisukumwa kwenye yale maporomoko.Alex alishtuka kwenye usingizi huku akihema kwa nguvu na kufanya watu wote waliokuwa kwenye ile ndege wamshangae.Jasho zilikuwa zinamtoka kwa wingi huku akionyesha hofu ya waziwazi iliyokuwa ndani yake
“Alex nini kimetokea mbona umeshtuka hivyo?”Cindelela aliuliza
“Nothing Cindelela(hakuna kitu Cindelela)”Ale alisema huku akijifuta jasho
“Alex naomba uniambie ukweli mimi ni mpenzi wako”Cindelela alisema huku akimuangalia Alex kwa macho ya hurumaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nimeota mpenzi”Alex alisema
“umeota nini mpaka ushtuke hivyo?”Cindelela aliuliza
“Ndoto ya kawaida nitakuambia tukifika”Alex alisema
“Sawa mpenzi wangu ila usilale tena usije ukaota nimeolewa na mtu mwingine”Cindelela alisema kwa utani na kufanya Alex acheke
Cindelela aliegemesha kichwa chake kwenye kifua cha Alex huku wakiendelea kuongea.Kichwa cha Alex kilikuwa hakijatulia sababu ile ndoto ilimchanganya sana kutokana na ile ndoto aliyoiota kwa mara ya pili.Alex alijiuliza maswali mengi sana lakini baadae akaamua kupuuzia sababu ilikuwa ni ndoto tu isiyokuwa na maana yoyote
……………………………………………………………………………………………………………………..
Mr Jacobo baada ya kuhakikisha kwamba mwanae anatembea kweli na kijana ajulikanae kwa jina la Alex aliamua kutafuta mbinu za kumuangamiza Alex.Alitafuta baadhi ya vijana ili waweze kumuua Alex.Alikodisha muuaji maarufu kutoka katika nchi ya Somalia akijulikana kwa jina la Saidi chota samo hong
Said chota samo hong alikuwa ni muuaji maarufu sana katika bara la Africa kwani aliweza kufanya mauaji mbali mbali ndani ya nchi ya Somalia na nje ya nchi hiyo.Saidi alikuwa na vijana wake sita ambao walikuwa wanamsaidia katika kazi zake alizokuwa anazifanya
Mzee Jacobo alimtafuta Said ili aweze kumuua Alex sababu ile kazi kwa saidi ilikuwa ni nyepesi sana.Walikubaliana kila kitu na kuanza mipango ya kufanya mauaji bila kujulikana na mtu yoyote kama Mzee Jacobo anahusika
“Naomba mnifanyie kazi yangu kwa uangalifu mkubwa sana sababu mnajua mimi ni nani katika serikali ya Tanzania,Endapo ikija kujulikana mjue vichwa vyenu vitakuwa halali yangu”Mzee Jacobo aliwatisha vijana wa saidi
“usijali bosi uwa tunafanya kazi kwa uangalifu mkubwa sana”walijinu
“sawa mnaweza kwenda”Mzee Jacobo alisema
Saidi na kundi lake waliingia ndani ya nchi ya Uingereza ili kukamilisha mauaji ya Alex,Picha zote walishazipata kwahiyo ilikuwa rahisi kwa wao kumjua Alex sababu maelekezo yote walishapewa.Walianza kumfuatilia Alex hatua kwa hatua mpaka siku moja alipoingia kwenye kituo cha television kwaajili ya interview
Wakati Alex anatoka na kuelekea kwenye gari lake vijana wa Saidi walifyatua risasi lakini zilimkosa Alex hasa baada ya kujikwaa na kuinama chini.Vijana wa Said walivyoona vile wakaamua kujificha na kutokomea sehemu isiyojulikana
Mzee Jacobo alipata Taarifa kwamba Alex wamemkosa na risasi,Hasira zilimpanda sana mzee Jacobo na kuwatukana sana wale vijana sababu walikuwa wanaleta mzaa kwenye kazi.
“Jamani naomba mfanye kila muwezalo huyo kijana asiwe Duniani”Mzee Jacobo alisema
“usijali bosi kazi itakamilika hivi karibuni”alisema Saidi
Mipango iliendelea kupangwa huku wale wauaji wakijaribu mbinu tofauti ili kumuangamiza Alex.Mzee Jacobo alipata taarifa juu ya ujio wa Cindelela na Alex katika nchi ya Tanzania na mtu aliyempa hizo taarifa alikuwa ni Cindelela bila kujua kwamba baba yake ana nia mbaya na mpenzi wake
“Saidi fanyeni mpango mpango wa kuingia kwenye ndege atakayopanda Alex na Cindelela kisha mfanye niliyowatuma”Mzee Jacobo aliwapa maagizo vijana wake
“usijali bosi”Saidi alijibu
Siku ya siku saidi na vijana wake waliingia kwenye ndege aliyopanda Cindelela na Alex.Baadhi walikaa karibu na Alex huku wengine wakiwa mbali na eneo lile ili kuangalia usalama wa ile ndege.Walikuwa wanaonyeshana ishara kwamba kazi inatakiwa kuanza muda siyo mrefu
Alex na Cindelela walikuwa hawajui kitu chochote kinachoendelea kwani wao walikuwa na hamua sana ya kurudi Tanzania wakafanye mipango ya kufunga ndoa na kuishi kama mume na mke japo bado walikuwa na umri mdogo
Kwa mbali walianza kusikia harufu ya moshi uliopulizwa juu na watu waliojifunga vitu katika pua zao.Watu ndani ya ndege walianza kukooa kwa nguvu huku wakidondoka chini na kufanya ile ndege ikose hali ya utulivu kwani sababu kelele za kuomba msaada zilikuwa zinasikika
Alex alichukua shati lake na kujifunika kwenye pua yake na Cindelela alifanya hivyo hivyo kama Alex alivyofanya.Walikuwa wanaona baadhi ya watu wakidondoka na kupoteza fahamu sababu ile dawa iliyopulizwa ilikuwa ni kali na ilikuwa inaleta usingizi mzito sana
Wale magaidi waliingia mpaka kwenye chumba cha rubani na kisha wakawaweka chini ya ulinzi.Ndege nzima ilishakuwa chini ya ulinzi na wale magaidi wakaanza kuiongoza kupeleka sehemu wanapopataka wao
“ninyi ni wakina nani?”Alex aliuliza kwa hasira
“unataka kujua sisi ni wakina nani?”Alijibu saidi kwa kuuliza
“ndiyo nataka kujua ninyi ni wakina nani na kwanini mtuteke?”Alex aliuliza
“hahaha sisi ni watu tuliyokuja kuchukua roho yako”Saidi alisema na kumpulizia Spray kwenye pua yake
Alex macho yake yakaanza kufunga taratibu na kuanza kupoteza fahamu kisha akadondoka chini na kutulia kimya.Cindelela alianza kulia kama mtoto mdogo na kujikuta akipoteza fahamu sababu alijua huo ndiyo ulikuwa mwisho wa Alex
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment