Search This Blog

Thursday 2 June 2022

NAKUPENDA CINDELELA - 2

    Simulizi : Nakupenda Cindelela

    Sehemu Ya Pili (2)

    ILIPOISHIA

    “Cindelela”Alex aliita

    “beee”Cindelela alihitika huku akionekana kumuonea Alex aibu

    “Nalazimika nikuambie ukweli japo ni mara ya pili tumeonana”Alex alisema

    “niambie tu ukweli gani?”Cindelela aliuliza huku akiwa makini kusikiliza Alex anataka kusema nini

    SONGA NAYO

    “Cindelela sidhani kama nitakuwa nimeutendea haki moyo wangu kama sijakuambia ukweli unaoutesa moyo wangu”Alex alisema huku akimuangalia Cindelela kwa umakini

    “kaka bado sijakuelewa unamaanisha nini”Cindelela alisema

    “Cindelela namaanisha kwamba nakupenda na bila ya wewe sidhani kama kuna kitu kitawezekana,Cindelela akili yangu umetokea kuiteka sana na muda mwingi umekuwa ukiniumiza kichwa kwa kukufikiria wewe.Nakupenda sana Cindelela nakupenda na nitazidi kukupenda”Alex aliongea huku akimuangalia Cindelela ambaye alionekana akiona aibu kwa yale maneno

    “asante sana kwa kunipenda”ilo ndiyo lilikuwa jibu kutoka kwa Cindelela

    “Cindelela naomba unipe japo nafasi katika moyo wako,naomba niwe mpenzi wako japo uipoze roho yangu kwa machugu ninanyopata”Alex alisema

    “kaka samahani sana siwezi kuwa na wewe na sidhani kama itatokea mimi kuwa na wewe na usije ukanyanyua mdomo wako na kuongea neon kama ilo please naomba uniache kama nilivyo”Cindelela aliongea bila mzaha wowote

    Alex alionekana kama amepigwa na shoti ya umeme sababu hakuamini kama angepata jibu kama lile kutoka kwa msichana ambaye anampenda kwa moyo wake wote.Machozi yalitaka kumtoka Alex lakini alijikaza kiume ili asionekane dhaifu mbele ya msichana,alitamani sana kunyanyua mdomo wake ili aongee neon jingine lakini aliogopa kupewa maneno ambayo yangeuumiza moyo wake

    “Cindelela naomba unielewe japo kidogo,naomba unipe hata jibu la NDIYO ili kuufurahisha moyo wangu,nakuomba sana unikubalie ombi langu”Alex alisema huku akionekana wazi kwamba anaumia moyoni mwake

    “kaka kama kweli wewe unanipenda sawa,ila tambua kwamba mimi sikupendi hata kidogo na ukiendelea kunifuatilia nadhani tutaonana wabaya.Kuna utofauti mkubwa sana kati yangu na wewe na hata nikiwa na wewe nadhani itakuwa kituko sana”Cindelela alisema huku akimpandisha Alex na kumshusha

    Alex aliumia sana moyo wake na kujikuta machozi yakimdondoka bila kutegemea sababu kitu alichokiongea Cindelela kilimuumiza sana moyo wake.Utofauti hali ya maisha ndiyo uliofanya Cindelela amkatae Alex bila hata ya kujua kama kweli anampenda au anataka kumchezea,Alex aliinama chini huku hasiamini kama msichana aliyeongea maneno yale ni Cindelela

    Baada ya dakika kadhaa Wit alikuja pale kwenye meza na kukuta hali ya hewa ikiwa imebadilika sababu kila mtu alikuwa amejiinamia upande wake,Wit hakujua nini kinachoendelea pale sababu Alex alikuwa kimya ameinama huku Cindelela akiwa busy anabonyeza simu yake

    “Wit naomba tuondoke”Cindelela alisema huku akisimama na kuanza kuelelkea kwenye gari

    “Alex nini kimetokea?”Wit aliuliza baada ya kuona Alex akiwa amejiinamia

    “Wit tutaongea baadae”Alex alisema na kuondoka

    Wit aliendelea kushikwa na bumbuwazi sababu hakuelewa nini kimewakuta ,alilipia vyakula na kuanza kuelekea kwenye gari.Ndani ya gari alimkuta Cindelela akiwa amejiinamia peke yake,Wit alimuamuru dereva aendeshe gari na kuondokaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Wit umepanga kuniuza rafiki yangu?”Cindelela aliuliza kwa uchungu

    “kwanini unasema hivyo Cindelela?”Wit nae aliuliza

    “wewe umeniacha na Yule kaka ili anitongoze”Cindelela alisema

    “Cindelela Yule kaka anakupenda sana na sidhani kama kuna mtu anateseka juu yako kama Alex,Cindelela Alex ni kijana mzuri sana na sidhani kama ana nia mbaya na wewe”Wit alisema

    “Naomba unisikie mimi simpendi hata kidogo na sidhani kama nitakuja kumpenda sababu hatuendani hata kidogo”Cindelela alisema

    “Cindelela hali yake ya umasikini isikufanye umdharau uwezi kujua atakusaidia nini hapo mbeleleni,Cindelela mbona mimi namuheshimu Alex na namchululia kama watu wengine?”Wit alisema kwa uchungu

    “Wit kama wewe unamuheshimu huyo Alex kwanini usiwe nae?’Cindelela aliuliza

    “kwakuwa amekupenda wewe haina haja ya mimi kuwa na yeye ila kama angenifuata mimi sidhani kama ningemjibu kama wewe ulivyofanya”Wit alisema

    “Wit naomba yaishe”Cindelela alisema na kukaa kimya

    …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

    Alex alipanda kwenye gari na kujikuta kama mtu aliyepungukiwa na kitu kwenye mwili wake sababu alijiona kama mzigo uliokosa muelekeo.Akiwa ndani ya gari maneno ya Cindelela yalikuwa yanajirudia kwenye akili yake na kusababisha machozi yamtoke kwa kujiona kama mkosaji mbele ya mwenyezi mungu

    “eeh mungu kwanini umeniumba masikini”Alex alisema bila kujua kama kwenye gari kuna abiria wengine

    Watu wote wa kwenye gari waligeuka na kuanza kumuangalia Alex alivyokuwa anajiongelesha mwenyewe.watu wengine walimuonea huruma sababu walikuwa hawajui nini anachokiwaza na kwanini ameongea vile.Wengine walimuona kama kichaa kinataka kumuanza

    “hivi ni watu wote ndiyo wanafanyiwa kama mimi?hivi mapenzi yanaangalia utajiri au umasikini?mbona nilishawai kusoma simulizi moja ya Jamaa aliyetokea kumpenda mwanamke mchafu na masikini wa kutupwa,tena simulizi hiyo inaitwa KWANINI JULIANA?ikiwa imetungwa na Victor Dismas.Kwanini Cindelela ameshindwa kufanya kama alivyofanya Julius kumpenda msichana ambaye haeleweki japo mwisho wake uliishia kubaya?Hata iweje nitakupenda Cindelela na nitafanya kila kitu mpaka uwe wangu”Alex alijisemea mwenyewe

    Alex alijikuta kushtuka akiwa kimara temboni alikuwa ameshapitishwa kituo kimoja ,Alitelemka kwenye gari na kuanza kupita njia za mkato mpaka kimara suka kasha akaanza safari ya kurudi kwao maeneo ya gorani.Japo alijitahidi kupunguza mawazo lakini kichwa kilishindwa kutoa mawazo kwa msichana Cindelela,wakati anaendelela kutembea akashtuka kusikia simu yake inaita na mpigaji alikuwa ni Wit

    “Hallo Alex”Wit alisema baada ya kusikia simu imepokelewa

    “hallo Wit”Alex alijibu

    “Alex samahani kwa yote yaliyotokea najua utakuwa umeumia sana ila mimi nipo bega kwa began a wewe mpaka pale mabo yatakapo kaa sawa”Wit alisema kumpa moyo Alex

    “hapana Wit wala nisikusumbue sababu hata ufanyaje hauwezi kubadilisha hali yangu ya umasikini na kumfanya Cindelela anipende,wewe pumzika na asante sana kwa kunijali ila tutaendelea kuwasiliana”Alex alisema

    “Alex usiseme hivyo na kwanini unakata tamaa mapema?”Wit aliuliza

    “lazima nikate tama sababu ya yale majibu niliyojibiwa na sijui kama itakuja kuwezekana kumpata Cindelela japo nampenda kwa moyo wangu wote”Alex alisema kwa uchungu

    “usijali Alex nitakusaidia kumpata”Wit alisema na kukata simu

    Alex aliumia sana moyoni lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na ukweli,Japo Cindelela alionyesha kwamba hampendi lakini Alex alipata matumaini kidogo kutokana na yale maneno ya Wit.Wit alijitahidi sana kumfanya Aex asijisikie Vibaya sababu alikuwa jambo zuri kumtenga mtu kutokana na hali aiyokuwa nayo

    Siku ziliendelea kukatika huku Alex akiongeza juhudi katika masomo yake sababu alijua fika kwamba mapenzi yameshamshinda.Mpaka Alex namaliza kidato cha nne hakufanikiwa kumpata msichana Cindelela zaidi ya kuwasiliana na Wit mara kwa mara.Alex alipomliza kidato cha nne aliamua kujiingiza kwenye masuala ya soka japo ndoto yake kubwa ilikuwa kusoma na kuwa kiongozi katika nchi ya Tanzania sababu alitaka kuwasaidia watu wenye matatizo mbalimbali

    Majibu ya kidato cha nne yalitoka na Alex alifanikiwa kupata daraja la pili ,kitu kilichofanya wazazi wake wafurahi kupita maelelzo sababu walikuwa wanamtemeea mtoto wao kwani ndiyo alikuwa ni mtoto wa pekee .Japo nyumbani kwao walikuwa na uwezo wa hali ya chini lakini wazazi wake waliamua kumpatia zawadi ya kumpongeza mtoto wao kwa kufahulu kidato cha nne

    Baba yake na Alex alikuwa mkulima katika mkoa wa pwani katika wilaya ya kibaha,Aliamua kukata sehemu ya shamba lake na kumkabidhi mwanae ili maisha yatakapomuendea vizuri ajenge nyumba katika eneo ilo,Alex alifurahi sana kupata zawaidi ile kutoka kwa baba yake na kuhaidi kwamba atafanya vizuri katika masomo yake ili abadilishe hali ya nyumbani kwao

    “baba na mama nashukuru sana kwa zawadi mliyonipatia lakini bado sijaridhika na hapa nilipo nahitaji kufika mbali sana na hapa”Alex aliwaambia wazazi wake

    “tunashukuru sana mwanetu na tunakuombea kwa mungu ili ufikie malengo yako uliyojipngia”Mama yake alisema

    Alex alimshukuru sana mungu kupata wazazi wenye ukarimu japo hali ya maisha yao yalikuwa ya chini,alijitahidi sana kuwapenda na kuwaheshimu wazazi wake sababu yeye ndiyo alikuwa ni mtoto wa pekee na endapo atafanya jambo ambalo litawakera wazazi wake litasababisha mtafaruku mkubwa sana kwenye maisha ya familia yao

    Alex alifanikiwa kupangiwa shule ya Benjamini ili kuendelea na masomo yake ya kidato cha tano na cha sita.Shule ya benjamini ilikuwa ya mchanganyiko na ilikuwa maeneo ya ilala katika jiji a Dar es salaam.Alex alifurahi sana kuanza maisha ya kidato cha tano sababu alijua hiyo iauwa njia moja wapo ya kufanikisha malengo yake

    “Lazima nifanikishe malengo yangu ili niisaidie familia yangu na jamii kwa ujumla”hayo yalikuwa maneno ya kila siku kutoka kwenye kinywa cha Alex

    Maisha yaliendelea huku Alex akiwa serious na masomo yake hata mambo ya mpira alishasahau sababu yeye alitaka kitabu ndiyo kimtoe.Katika darasa la HGL Alex alionekana hana mzaa hata kidogo hasa kwenye suala la masomo,baadhi ya wanafunzi walikuwa wanamtania kwamba ametumwa na kijiji chao ili akikomboe na ujinga

    Japo Alex alikuwa busy na masomo lakini kichwani bado alikuwa na kumbukumbu ya msichana mrembo Cindelela.Alex alijitahidi sana kutoa mawazo kwa Cindelela lakini alishindwa sababu bado alikuwa anampenda.Kila alipokuwa anamkumbuka Cindelela machozi yalikuwa yanamtoka kutokana na maneno aliyoambiwa na Cindelela

    “mh lazima nipigane ili nitoke kwenye ili janga la umasikini”Alex alijisemea mwenyewe

    Katika shule ya Benjamini kulikuwa na timu ya mpira wa miguu ambayo ilikuwa inashiriki ligi kuu Tanzania bara.Ashanti ni timu ambayo ilikuwa inatumia uwanja wa shule ya Benjamini kwa kufanyia mazoezi .Alex alianza kuvutiwa sana na mazoezi waliyokuwa wanayafanya katika uwanja hule na yeye alikuwa ni mmoja ya watu waliokuwa wanatazama yale mazoezi kila siku hasa muda wa jioni

    Siku moja Alex aliamua kumfuata kocha wa timu hiyo na kumuomba kushiriki katika mazoezi waliyokuwa wanayafanya,Bila kipingamizi yule kocha alimkubalia na Alex alianza kufanya mazoezi katika timu hiyo.Kwa muda mfupi alioanza mazoezi Alex alikuwa anaonyesha uwezo wa hali ya juu hasa katika kupachika mabao na kusababisha viongozi wa timu hiyo waanze kusugua vichwa katika kumsajili

    “Alex wewe ni mchezaji mzuri sana na ningependa uichezee timu yetu”kocha alimuambia Alex siku moja wakiwa wanatoka mazoeziniCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “asante sana kocha ila mimi kwa sasa mabo ya shule yamenibana sana ila nitakapomaliza shule nadhani nitajiunga na timu yenu kwa sasa naomba niwe nafanya mazoezi tu”Alex alisema

    “sawa Alex ila ni vizuri kama ukiongeza juhudi na kutokulewa sifa sababu nimeshaona nyota yako itang’aa sana siku za usoni”Kocha alimuambia Alex

    “nashukuru kocha kwa maneno yako”Alex alisema na kuagana na kocha kisha akaondoka

    Maisha yalikuwa yanaendelela huku Alex akiwa anajituma darasani na kwenye mazoezi ya timu.Lakni kama unavyojua kwenye mafanikio apakosi wafitini,na ndiyo kitu kilichomkuta Alex kwenye timu ya Ashanti baada ya wachezaj wenzake kumfanyia majungu na kusababisha Alex afukuzwe kwenye timu kwa kuonekana kwamba ni mtovu wa nidhamu

    Roho ilimuuma sana Alex lakini alimuomba mungu na kuendelea na masomo yake kama kawaida huku akiongeza juhudi katika kusoma.Mara moja moja alikuwa anawasilina na Wit ili kujua hali aliyokuwa nayo Cindelela sababu bado alikuwa yupo kwenye akili yake.Alex alifanikiwa kumaliza kidato cha sita na kukaa nyumbani huku akisubiria matokeo yatoke.Katika kipindi hicho chote cha kusubiri matokeo Alex alikuwa anacheza mpira wa mtaani katika timu ya mtaani kwao

    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..

    Nchini England kulikuwa na timu inayojulikana kwa jina la Birmingham City Football Club iliyopo katika jiji la Birmingham.Club hiyo ilianza mnamo mwaka 1875 kama Small Health Allience lakini ilipofika mwaka 1943 timu hiyo ambayo ni ya tatu kumilikiwa na kampuni ilibadirika na kuitwa Birmingham city baada ya kuitwa majina kadhaa huko nyuma.

    Birmingham ambayo ilikuwa inatumia uwanja wa St Andrew’s kama uwanja wake wa nyumbani ilipata pigo la kushuka daraja na kuanza kushiriki ligi daraja la kwanza inayojulikana kwa jina la Championiship.kitu icho kiliwauma sana viongozi wa timu hiyo na kujiona kama wao ni chanzo cha timu hiyo kufanya vibaya katika timu yao

    Jopo la viongozi lilikutana ndani ya chumba cha mkutano ili kujadili ni kitu gani kilichosababisha mpaka timu yao kushuka daraja na ni mbinu gani wafanye ili waweze kuipandisha tena timu yao daraja.Kikao kilianza huku kila mtu akisugua kichwa ili atoe wazo ambalo kila mtu atalihafiki na kulifanyia kazi

    “Nadhani kila mtu anaipenda timu yetu na kitu kidogo sana ndiyo kimetufanya tushindwe kubaki ligi kuu na sasa tunahitaji kurudi kwa mbinu yoyote ile”alikuwa ni Peter Pannu ambaye ni director akizungumza maneno hayo na kusababisha wote watikise kichwa kukubaliana nae

    “sasa tufanyaje ili uzembe kama hule usijirudie?”director Ryan Yeung aliuliza

    “hapa ni kufanya utafiti wa kitu gani tulichokosea nyuma”Panos Pavlakis alisema

    “lakini kumbukeni kwamba timu yetu ilikumbwa na wachezaji wengi sana ambao walikuwa majeruhi hasa kipindi cha kumaliza ligi”alisema Shui Cheong Ma ambae alionekana kimya muda wote

    “sasa Tunafanyaje”director Peter Pannu aliuliza

    “tunahitaji kupata wachezaji wenye nguvu na uwezo wa kupachika mabao”Shui Cheong Ma alisema watu wote wakatikisa kichwa kukubali

    “Je hao wachezaji tutawapata wapi na ukiangalia timu yetu imepata hasara kubwa sana na kusababisha pesa nyingi kupotea”Peter Pannu alisema

    “Tunatakiwa kwenda Africa au America Kusini sababu kule ndipo kuna wachezaji wenye nguvu na wanapatikana kwa bei ya chini”Shui Cheong Ma alisema na kusababisha wengine wampe support kwa kutikisa vichwa

    “basi jukumu hili tunamuachia chief scout Malcolm Crosby afuatilie na baada ya muda mchache atatupa majibu lakini mimi pendekezo langu la kwanza aende Africa sababu nimeona wachezaji wengi wanaocheza hapa kutokea Africa wanaonyesha uwezo wa hali ya juu”Alisema Peter Pannu

    Kikao kilifungwa na jukumu lote aliachiwa mkurugenzi wa usajili Malcolm Crosby ili azunguke popote anapopajua ili atafute wachezaji amabo watafaa kwenye timu yao.Malcolm alitafuta baadhi ya vijana kwaajili ya kuzunguka nao katika bara la Africa ambapo ndipo walipoambiwa waanzie

    “Africa ni kubwa sana sasa sijui tutaanzia nchi gani?”aliwauliza vijana wake

    “hapo ndipo tatizo lilipo ila mimi ningependa tuende East Africa sababu nilishawahi kutembea katika nchi ya Tanzania “alisema kijana mmoja

    “je unadhani huko tutapata tunachokifuata?”Malcolm aliuliza

    “ndiyo wapo wachezaji wengi sana wenye vipaji natuamini malengo yetu yatatimia”Yule kijana alisema

    “sawa ngoja tuandae safari”Malcolm alisema

    Baada ya siku mbili safari ya Malcom kuelekea Tanzania ilianza kwa dhumuni la kwenda kutafuta wachezaji ambao wataisaidia timu yao.Dhumuni la kwenda nchini Tanzania ni kupata wachezaji wazuri na wabei rahisi ambayo hauwezi kuwalipa wachezaji wa uingereza

    Alex aliumia sana moyoni lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na ukweli,Japo Cindelela alionyesha kwamba hampendi lakini Alex alipata matumaini kidogo kutokana na yale maneno ya Wit.Wit alijitahidi sana kumfanya Aex asijisikie Vibaya sababu alikuwa jambo zuri kumtenga mtu kutokana na hali aiyokuwa nayo

    Siku ziliendelea kukatika huku Alex akiongeza juhudi katika masomo yake sababu alijua fika kwamba mapenzi yameshamshinda.Mpaka Alex namaliza kidato cha nne hakufanikiwa kumpata msichana Cindelela zaidi ya kuwasiliana na Wit mara kwa mara.Alex alipomliza kidato cha nne aliamua kujiingiza kwenye masuala ya soka japo ndoto yake kubwa ilikuwa kusoma na kuwa kiongozi katika nchi ya Tanzania sababu alitaka kuwasaidia watu wenye matatizo mbalimbali

    Majibu ya kidato cha nne yalitoka na Alex alifanikiwa kupata daraja la pili ,kitu kilichofanya wazazi wake wafurahi kupita maelelzo sababu walikuwa wanamtemeea mtoto wao kwani ndiyo alikuwa ni mtoto wa pekee .Japo nyumbani kwao walikuwa na uwezo wa hali ya chini lakini wazazi wake waliamua kumpatia zawadi ya kumpongeza mtoto wao kwa kufahulu kidato cha nne

    Baba yake na Alex alikuwa mkulima katika mkoa wa pwani katika wilaya ya kibaha,Aliamua kukata sehemu ya shamba lake na kumkabidhi mwanae ili maisha yatakapomuendea vizuri ajenge nyumba katika eneo ilo,Alex alifurahi sana kupata zawaidi ile kutoka kwa baba yake na kuhaidi kwamba atafanya vizuri katika masomo yake ili abadilishe hali ya nyumbani kwao

    “baba na mama nashukuru sana kwa zawadi mliyonipatia lakini bado sijaridhika na hapa nilipo nahitaji kufika mbali sana na hapa”Alex aliwaambia wazazi wake

    “tunashukuru sana mwanetu na tunakuombea kwa mungu ili ufikie malengo yako uliyojipngia”Mama yake alisema

    Alex alimshukuru sana mungu kupata wazazi wenye ukarimu japo hali ya maisha yao yalikuwa ya chini,alijitahidi sana kuwapenda na kuwaheshimu wazazi wake sababu yeye ndiyo alikuwa ni mtoto wa pekee na endapo atafanya jambo ambalo litawakera wazazi wake litasababisha mtafaruku mkubwa sana kwenye maisha ya familia yao

    Alex alifanikiwa kupangiwa shule ya Benjamini ili kuendelea na masomo yake ya kidato cha tano na cha sita.Shule ya benjamini ilikuwa ya mchanganyiko na ilikuwa maeneo ya ilala katika jiji a Dar es salaam.Alex alifurahi sana kuanza maisha ya kidato cha tano sababu alijua hiyo iauwa njia moja wapo ya kufanikisha malengo yake

    “Lazima nifanikishe malengo yangu ili niisaidie familia yangu na jamii kwa ujumla”hayo yalikuwa maneno ya kila siku kutoka kwenye kinywa cha Alex

    Maisha yaliendelea huku Alex akiwa serious na masomo yake hata mambo ya mpira alishasahau sababu yeye alitaka kitabu ndiyo kimtoe.Katika darasa la HGL Alex alionekana hana mzaa hata kidogo hasa kwenye suala la masomo,baadhi ya wanafunzi walikuwa wanamtania kwamba ametumwa na kijiji chao ili akikomboe na ujingaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Japo Alex alikuwa busy na masomo lakini kichwani bado alikuwa na kumbukumbu ya msichana mrembo Cindelela.Alex alijitahidi sana kutoa mawazo kwa Cindelela lakini alishindwa sababu bado alikuwa anampenda.Kila alipokuwa anamkumbuka Cindelela machozi yalikuwa yanamtoka kutokana na maneno aliyoambiwa na Cindelela

    “mh lazima nipigane ili nitoke kwenye ili janga la umasikini”Alex alijisemea mwenyewe

    Katika shule ya Benjamini kulikuwa na timu ya mpira wa miguu ambayo ilikuwa inashiriki ligi kuu Tanzania bara.Ashanti ni timu ambayo ilikuwa inatumia uwanja wa shule ya Benjamini kwa kufanyia mazoezi .Alex alianza kuvutiwa sana na mazoezi waliyokuwa wanayafanya katika uwanja hule na yeye alikuwa ni mmoja ya watu waliokuwa wanatazama yale mazoezi kila siku hasa muda wa jioni

    Siku moja Alex aliamua kumfuata kocha wa timu hiyo na kumuomba kushiriki katika mazoezi waliyokuwa wanayafanya,Bila kipingamizi yule kocha alimkubalia na Alex alianza kufanya mazoezi katika timu hiyo.Kwa muda mfupi alioanza mazoezi Alex alikuwa anaonyesha uwezo wa hali ya juu hasa katika kupachika mabao na kusababisha viongozi wa timu hiyo waanze kusugua vichwa katika kumsajili

    “Alex wewe ni mchezaji mzuri sana na ningependa uichezee timu yetu”kocha alimuambia Alex siku moja wakiwa wanatoka mazoezini

    “asante sana kocha ila mimi kwa sasa mabo ya shule yamenibana sana ila nitakapomaliza shule nadhani nitajiunga na timu yenu kwa sasa naomba niwe nafanya mazoezi tu”Alex alisema

    “sawa Alex ila ni vizuri kama ukiongeza juhudi na kutokulewa sifa sababu nimeshaona nyota yako itang’aa sana siku za usoni”Kocha alimuambia Alex

    “nashukuru kocha kwa maneno yako”Alex alisema na kuagana na kocha kisha akaondoka

    Maisha yalikuwa yanaendelela huku Alex akiwa anajituma darasani na kwenye mazoezi ya timu.Lakni kama unavyojua kwenye mafanikio apakosi wafitini,na ndiyo kitu kilichomkuta Alex kwenye timu ya Ashanti baada ya wachezaj wenzake kumfanyia majungu na kusababisha Alex afukuzwe kwenye timu kwa kuonekana kwamba ni mtovu wa nidhamu

    Roho ilimuuma sana Alex lakini alimuomba mungu na kuendelea na masomo yake kama kawaida huku akiongeza juhudi katika kusoma.Mara moja moja alikuwa anawasilina na Wit ili kujua hali aliyokuwa nayo Cindelela sababu bado alikuwa yupo kwenye akili yake.Alex alifanikiwa kumaliza kidato cha sita na kukaa nyumbani huku akisubiria matokeo yatoke.Katika kipindi hicho chote cha kusubiri matokeo Alex alikuwa anacheza mpira wa mtaani katika timu ya mtaani kwao

    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..

    Nchini England kulikuwa na timu inayojulikana kwa jina la Birmingham City Football Club iliyopo katika jiji la Birmingham.Club hiyo ilianza mnamo mwaka 1875 kama Small Health Allience lakini ilipofika mwaka 1943 timu hiyo ambayo ni ya tatu kumilikiwa na kampuni ilibadirika na kuitwa Birmingham city baada ya kuitwa majina kadhaa huko nyuma.

    Birmingham ambayo ilikuwa inatumia uwanja wa St Andrew’s kama uwanja wake wa nyumbani ilipata pigo la kushuka daraja na kuanza kushiriki ligi daraja la kwanza inayojulikana kwa jina la Championiship.kitu icho kiliwauma sana viongozi wa timu hiyo na kujiona kama wao ni chanzo cha timu hiyo kufanya vibaya katika timu yao

    Jopo la viongozi lilikutana ndani ya chumba cha mkutano ili kujadili ni kitu gani kilichosababisha mpaka timu yao kushuka daraja na ni mbinu gani wafanye ili waweze kuipandisha tena timu yao daraja.Kikao kilianza huku kila mtu akisugua kichwa ili atoe wazo ambalo kila mtu atalihafiki na kulifanyia kazi

    “Nadhani kila mtu anaipenda timu yetu na kitu kidogo sana ndiyo kimetufanya tushindwe kubaki ligi kuu na sasa tunahitaji kurudi kwa mbinu yoyote ile”alikuwa ni Peter Pannu ambaye ni director akizungumza maneno hayo na kusababisha wote watikise kichwa kukubaliana nae

    “sasa tufanyaje ili uzembe kama hule usijirudie?”director Ryan Yeung aliuliza

    “hapa ni kufanya utafiti wa kitu gani tulichokosea nyuma”Panos Pavlakis alisema

    “lakini kumbukeni kwamba timu yetu ilikumbwa na wachezaji wengi sana ambao walikuwa majeruhi hasa kipindi cha kumaliza ligi”alisema Shui Cheong Ma ambae alionekana kimya muda wote

    “sasa Tunafanyaje”director Peter Pannu aliuliza

    “tunahitaji kupata wachezaji wenye nguvu na uwezo wa kupachika mabao”Shui Cheong Ma alisema watu wote wakatikisa kichwa kukubali

    “Je hao wachezaji tutawapata wapi na ukiangalia timu yetu imepata hasara kubwa sana na kusababisha pesa nyingi kupotea”Peter Pannu alisema

    “Tunatakiwa kwenda Africa au America Kusini sababu kule ndipo kuna wachezaji wenye nguvu na wanapatikana kwa bei ya chini”Shui Cheong Ma alisema na kusababisha wengine wampe support kwa kutikisa vichwa

    “basi jukumu hili tunamuachia chief scout Malcolm Crosby afuatilie na baada ya muda mchache atatupa majibu lakini mimi pendekezo langu la kwanza aende Africa sababu nimeona wachezaji wengi wanaocheza hapa kutokea Africa wanaonyesha uwezo wa hali ya juu”Alisema Peter Pannu

    Kikao kilifungwa na jukumu lote aliachiwa mkurugenzi wa usajili Malcolm Crosby ili azunguke popote anapopajua ili atafute wachezaji amabo watafaa kwenye timu yao.Malcolm alitafuta baadhi ya vijana kwaajili ya kuzunguka nao katika bara la Africa ambapo ndipo walipoambiwa waanzie

    “Africa ni kubwa sana sasa sijui tutaanzia nchi gani?”aliwauliza vijana wake

    “hapo ndipo tatizo lilipo ila mimi ningependa tuende East Africa sababu nilishawahi kutembea katika nchi ya Tanzania “alisema kijana mmoja

    “je unadhani huko tutapata tunachokifuata?”Malcolm aliuliza

    “ndiyo wapo wachezaji wengi sana wenye vipaji natuamini malengo yetu yatatimia”Yule kijana alisema

    “sawa ngoja tuandae safari”Malcolm alisema

    Baada ya siku mbili safari ya Malcom kuelekea Tanzania ilianza kwa dhumuni la kwenda kutafuta wachezaji ambao wataisaidia timu yao.Dhumuni la kwenda nchini Tanzania ni kupata wachezaji wazuri na wabei rahisi ambayo hauwezi kuwalipa wachezaji wa uingereza

    Kwa maajabu aliyoyafanya Alex pale uwanjani yalimfanya mr Malcom apatwe na kitete cha kumchukua bila kuangalia mechi inayofuata.Mr Malcom aliondoka na vijana wake huku akiwa amefurahi sana kuona lengo lake likakaribia kufanikiwa sababu aliona kwamba Alex ndiyo mtu pekee anayefaa kwenda nae Uingereza

    Mr Malcom aliifika hotelini ambayo walifikia awali kisha akawahita vijana wake ili wazungumze mambo mawili matatu ambayo yatawasaidia katika mchakato wao uliokuwa unaendelea

    “nadhani leo ndiyo tumeona mchezaji ambaye anafaa kuondoka na sisi”Mr Malcom alisema

    “yes ila tunahitaji muda zaid wa kumuangalia”alisema kijana wake

    “mimi sina shaka na mchezaji yule sababu amekaa kimpira na anajua kuuchezea mpira pia anajua kufunga inatakiwa tufanye haraka kabla timu nyingine azijamfuata”alisema Mr Malcom

    “sawa mkuu tumekuelewa”walisema vijana wake

    “basi zoezi la kumfuatilia yule kijana lianze mapema”Alisema Mr malcom huku akifuta miwani yake

    Kikao kilifungwa na kila mmoja alirudi kwenye chumba chake kwaajili ya kulala ili kesho waanze kazi ya kumfuatiklia AlexCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

    Katika kichwa cha Cindelela hakuwa na wazo lolote linalomuhusu Alex japo Wit aikuwa anajitahidi kumueleza kuhusu Alex.Cindelela alikuwa hataki kabisa kusikia jina Alex au jina la mwanaume yoyote sababu alikuwa hataki mpenzi kwa muda huo mpaka pale baba yake atakapomuambia kwamba wakati umefika wa kupata mchumba

    “Cindelela kwanini unamchukia Alex?”Wit alimuuliza siku moja wakiwa shuleni

    “siyo kama namchukia ila sidhani kama tunafanana katika maisha na unajua baba yangu uwa hapendi niwe na maraifki wa chini”Cindelela alisema

    “kwani watu wenye hali ya chini wapoje?, na kwanini baba yako anawachukia?hivi assume ndo ingekuwa ni wewe ungefanyaje”Wit aliuliza maswali kwa mkupuo

    “Wit siwezi kukujibu swali hata moja na sitoweza ila hadithi zako za Alex ziishie hapa sitaki kuzisikia tena kwenye masikio yangu”Cindelela alisema kwa ukali kidogo

    “basi rafiki yangu tusije tukagombana kwa vitu vidogo ila kumbuka uwezi jua ni mtu gani anayekupenda”Wit alisema huku akimuangalia Cindelela aliyeonyesha kukasirika

    Cindelela hakutaka kujibu tena zaidi ya kunyanyuka pale alipokuwepo na kuanza nkuondoka huku akimuacha Wit akiwa anamuangalia.Wit hakuamini kama Cindelela angefanya kitu kama hicho sababu yeye ndiyo alikuwa rafiki yake kipenzi pale shuleni na sehemu yoyote,Wit alitikisa kichwa kwa ishara ya kusikitika kisha akainuka na kuelekea upande alioelekea Cindelela ili akamuombe radhi sababu amemkosea rafiki yake

    “Alimkuta Cindelela akiwa amekaa ndani ya darasa lisilokuwa na watu huku akiwa ameinama chini,Wit aliingia ndani ya ilo darasa na kukaa karibu na Cindelela.Alimshika bega huku akimuinua kichwa ili amuambie kitu kilichomleta mule ndani

    “Samahani sana rafiki yangu kama nimekuudhi”Wit alisema kwa upole sana

    “Wit naomba uniache mambo ya mahusiano naomba uniachie mwenyewe na mwambie huyo Alex kwamba mimi simpendi na sitokuja kumpenda”Cindelela aliongea kwa ukali mpaka Wit alishtuka

    “sitokuambia tena kuhusu Alex nadhani imeshatosha”Wit alisema kwa upole huku akiegemeza kichwa cha Cindelela kwenye kifua chake

    “nimekusamehe rafiki yangu”Cindelela alisema

    “nashukuru sana kipenzi”Wit alisema huku akitabasamu

    Waliendelea na mazungumzo mengine mpaka muda wakwenda nyumbani ulipofika .kipindi hicho walikuwa wanasoma kidato cha tano na ndiyo walikuwa wanaingia kidato cha sita.Cindelela hakutaka kuwa na mzaa kwenye masomo sababu alikuwa anaingia kwenye kidato cha hatari.Kidato kitakachokusafishia njia ya kuingia chuo kikuu

    Cindelela na Wit waliagana na kila mmoja aliingia kwenye gari lao kwaajili ya kuelekea nyumbani kwao.

    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..

    Siku ziliendelea kukatika kuelekea pambano la fainali kati ya Bulula fc ambayo anaichezea Alex na timu pinzani ilikuwa France corner.Pambano lilikuwa linasubiriwa kwa hamu sana kwani kila mmoja alikuwa anania ya kuchukua ubingwa wa wilaya ili kujiwekea heshima.Alex alikuwa hatulii sababu yeye ndiyo alikuwa tegemezi kwenye timu yao na ukicheki mabeki wote wa timu pinzani walikuwa wamekamia ili asipate bahati ya kufunga goli

    Siku ya mechi ilipofika na ndiyo siku ambayo selikari ya jamuhuli ya muungano wa Tanzania ilitangaza mataokeo ya kidato cha sita kwa kupitia wizara yake ya elimu.Alex alikuwa na mawazo mawili katika kichwa chake,wazo la kwanza alitaka akaangalie matokeo kabla ya mechi,wazo la pili aangalie matokeo baada ya mechi.Aliamua kujikaza kisabuni na kuelekea kwenye internet café ili aangalie matokeo yake kabla ya kuelekea uwanjani

    Mwili ulikuwa unamtetemeka wakati anafungua shule aliyomalizia ili aangalie matokeo yake.Alifika mpaka kwenye jina lake na macho yake yakaona division two ya kumi na moja.Alex hakuamini macho yake na kuamua kurudiarudia kuangalia kama ni kweli,Alipoona kwamba ni kweli aliamua kupront yakle matokeo na ili aendelee na mambo nyingine

    Alex alitoka pale na kwenda kujiunga na wenzake kwaajili ya kuelekea uwanjani .Wlikodisha gari aina ya costa na safari ya kuelekea uwanjani ikaanza.Ndani ya gari Alex alikuwa kimya huku akimshukuru mungu kwa kumfanikisha katika mitihani yake,lakini Alex bado alikuwa anawaza m,echi iliyokuwepo mbele yake sababu ilikuwa ni muhimu na ni ngumu sana

    Walifanikiwa kufika uwanjani mapema na kuanza kupasha misuli yao kwaajili ya mpambano wa kukata na shoka.Mashabiki nao walikuwa wakiimba kuwapa support wachezaji wao ili wapambane mpka mwisho.Alex kila alipokuwa anauangalia mpira alikuwa anaufananisha na msichana mrembo Cindelela kwahiyo muda wote alitamani awe anaumiliki yeye tu

    Refa alianza kuhita wachezaji katikati ili mpambano uweze kuanza kwani muda ulikuwa umeshawadia.Mr Malcom na vijana wake nao walikuwa wameshafika uwanjani ili kumtazama Alex kama atafanya vizuri kama kwenye ile mechi ya kwanza.Roho za wachezaji wote zilikuwa zinaogopa sababu walikuwa wamepaniana sana

    Mpira ulianza kwa kasi ya ajabu huku timu ya Alex ikishambuliwa sana na kusababisha wachezaji waanze kupoteana uwanjani,Walijitahidi kupambana kufa na kupona kiasi kwamba beki wao mmoja aliumia na kumuingiza mchezaji mwingine.Alex kila alipokuwa anapata mpira mabeki walikuwa wanamkaba kwa nguvu na kumpokonya mpira kitu kilichomfanya Mr Malcom awe anaangalia pembeni

    Mpaka mapumziko yanafika hakuna timu iliyofanikiwa kuliona lango la mwenzake.Kila timu ilienda kukaa kwenye upande wake ili waweze kujadili na kusawazisha makosa ya kipindi cha kwanza.Captain wa timu ya Bulula alisimama na kuanza kuongea na wenzake

    “Inatakiwa sasa hivi tucheze kwa kushambulia ila Alex usisimame kama namba tisa sasa hivi inatakiwa usimame kama namba kumi sababu wewe unauwezo wa kuchukua mpira na kupiga chenga”Captain aliesema

    Waliongea mengi mpaka refa alipopuliza filimbi kwaajili ya kipindi cha pili kuanza,wachezaji wote waliingia uwanjani na kipindi cha pili kikaanza.Timu ya Alex walionekana kubadilika kwani walikuwa wanamiliki sana mpira huku Alex akionekana mtu muhimu sababu alikuwa anamiliki mpira na kupiga chenga kisha anatoa pasi kwa wachezaji wenzake

    Alex alikuwa anaufananisha ule mpira na msichana mrembo Cindelela ambaye alikuwa anam,penda kuliko kitu chochote.Kila muda Alex alionekana na mpira huku akijaribu mashuti kadhaa langoni.Ilipofika dakika ya sabini na tano Alex alipokea pasi nzuri kutoka kwa mchezaji mwenzake.Alex alipiga chenga watu wawili kisha akampasia mchezaji mwingine na kukimbia kwa mbele kidogo,yule mwenzake wala hakuwa na mbwembwe kwani alipiga pasi tena kwa Alex na kufanya one two safi sana.Alex alimtoka beki mwingine na kubaki yeye na goli kipa kisha akatisha kama anapiga shuti na kufanya kipa aruke upande wa kulia,Alex alipiga taratibu hule mpira upande wa kushoto na kufanikiwa kuipatia timu yake bao safi

    Uwanja ulilipuka kwa kelele sababu ilo goli lilionekana kama dhahabu kutokana na mchezo wenyewe kuwa mgumu sana.Mr Malcom alikuwa anatabasamu huku akipiga makofi baada ya kushuudia Alex akiinyanyasa timu pinzani.Moto wa Alex uliendelea kwani alipiga mashuti mawili ambayo yaligonga mwamba na kufanya Mr Malcom awe anainuka mara kwa mara

    Refa alipuliza kipenga cha mwisho kuashilia kwamba mpira umeisha,Mashabiki wote walimkimbilia Alex kisha wakambeba juu juu huku wakiimba kwa furaha.Mr Malcom aliwahita vijana wake ili awape maagizo

    “naomba mkamuhite yule kijana niongee nae”Mr Malcolm aliwaambia vijana wake

    “mkuu subiri kwanza wamalize kupewa zawadi zao”kijana wake alisema

    Zawadi zilianza kutolewa na alex alipewa zawadi ya mfungaji bora katika mashindano hayo,Timu yao ilipata zawadi ya jezi seti mbili,kikombe pamoja na pesa taslimi shilingi milion moja.Kila mtu alifanikiwa zawadi hizo na shangwe ziliendelea kwenye uwanja huo baada ya zawadi kutolewa

    “samahani tunaomba kuongea na wewe pembeni”Alex alishtuliwa na alipokuwa kwenye shamla shamla za ushindiCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “sawa tunaweza kwenda”Alex alisema huku akisogea pembeni

    Wale vijana walimpeleka kwa Mr Malcom ili akaongee nae.Mr Malcolm alianza kuongea na Alex dhumuni alilomuhitia na kumuelekeza kila kitu kinavyokwenda.Alex hakuamini kama ni yeye amechaguliwa kwenda Uingereza kucheza mpira wa kulipwa.Lakini Alex alikuwa njia panda sababu bado alikuwa ana nafasi ya kuendelea na masomo

    “kijana mpira unalipa sana kuliko hata kazi nyingine hasa katika nchi za ulaya,na bahati hii wapo wengi wanaitafuta lakini wanaikosa “Mr Malcom alisema huku akimuangalia Alex

    “naomba nafasi ya kufikiria kwanza”Alex alisema

    “tunakupa usiku wa leo ukazungumze na wazazi wako na kama itawezekana tupe mawasiliano yako ili kesho tuje kuzungumza na wazazi wako”Mr malcolm alisema

    Alex aliwapatia namba za simu kisha akatoka na kwenda kujichanganya na wenzake ili kuseherekea ushindi.Mr Malcolm na vijana wake waliondoka kuelekea hotelini ili kupumzika na kupanga mipango ya kesho yake.Mr Malcolm alionekana mwenye furaha muda wote sababu alijua ndoto za kumpata mchezaji zimeshatimia

    Asubuhi na mapema Mr Malcolm alimpigia simu Alex ili awaelekeze nyumbani kwao,Alex aliwaelekeza na safari ya kuelekea kimara suka ikaanza ili kwenda kuzungumza na wazazi wa Alex.Walifika kimara suka na kumkuta Alex stand kisha wakampakiza ili waelekee nyumbani kwao.Walifika kwa akina Alex na kupokelewa vizuri kisha wakaingia ndani.Baadhi ya watu walishangaa kuona wazungu wakiingia nyumbani kwakina Alex sababu lilikuwa ni tukio geni pale mtaani

    “nadhani mtoto wenu ameshawaambia kila kitu kuhusu sisi”Mwenyeji wa Mr Malcolm alisema

    “ndiyo ametuambia ila bado hatujahafiki”Alisema baba yake na Alex

    “kwanini hamjahafiki?”Aliuliza yule mwenyeji wa Mr Malcolm

    “tunahitaji mwanetu asome kwanza ili aje kutusaidia katika maisha yetu”Alisema baba wa Alex

    “mpira wa uingereza unalipa sana kuliko hata kusoma ila kama kusoma atasoma tu huku akiendelea kucheza mpira”alisema yule mwakilishi wa mr Malcolm

    “atasomaje huku anacheza mpira?”Aliuliza baba yake na Alex

    “Timu itagharamia masomo yake katika chuo cha Birmingham univeristy huku akiendelea kucheza mpira”Alisema muakilishi wa Mr Malcolm

    “hapo nimekubali kwa roho moja”baba yake na Alex alisema na kufanya Alex afurahi kupita maelezo

    Michakato ya kukata vibali vya kusafifiria ikaanza kufanyika kwa haraka sana.Ndani ya siku kadhaa kila kitu kinachomuhusu Alex kilikuwa tayari na safari ilikuwa imeshaandaliwa.Alex alikuwa ahamini kama ni yeye ndiyo anaondoka kuelekea ulaya kusoma pamoja na kucheza mpira.Alex alitamani sana kumtafuta Cindelela japo amuambie neno la mwisho sababu ilionekana kama ndoto kwa wao kuonana.Lakini Alex alikuwa anaogopa kumtafuta sababu alishaonywa,alimtafuta Wit kwenye namba yake lakini alikuwa hapatikani kwa muda huo

    Mpaka Alex anafika uwanja wa ndege kwaajili ya safari hakuamni kama ni yeye ndiyo anaingia ndani ya ndege kwaajili ya kwenda ulaya.Alex alimshukuru sana mungu kwa kumfungulia milango na kumjazia baraka japo alikuwa anaumia kila alipokuwa anamkumbuka Cindelela.Alex aliagana na wazazi wake pale uwanjani huku machozi yakimtoka sababu alizoea kuwa nao karibu

    Alex na kijana wa Mr Malcom walipanda ndege kwaajili ya kuondoka huku wakimuacha Mr Malcolm na kijana mwingine sababu bado walikuwa na jukumu la kwenda kutafuta wachezaji wengune katika nchi nyingine

    Ndege ilipaa na kuacha ardhi ya Tanzania ikimuaga Alex na kumtakia Kheri huko aendako

    Alex alikuwa anafurahi sana ndani ya nafsi yake sababu alipata fursa mbili kwa wakati mmoja.Fursa ya kwanza ilikuwa ni kucheza mpira katika timu ya Birmingham city na fursa nyingine ilikuwa ni kwenda kusoma katika chuo cha Birmingham university.Hakuna siku ambayo Alex alitegemea kama kitatokea kitu kama icho kwenye maisha yake sababu alikuwa mtu wa chini sana kiuchumi

    “kweli mungu ni mkubwa leo na mimi nipo ndani ya ndege kuelekea ulaya!!!”Alex alikuwa anajishangaa mwenyewe wakati yupo kwenye ndege

    Walitumia masaa mengi sana angani huku Alex muda mwingi alikuwa anautumia kwa kulala sababu ya uchovu wa kukaa muda mrefu sana.Katika kichwa chake alikuwa anawaza ni jinsi gain atakavyosakata soka kwa moyo wake wote huku akiendelea na masomo yake kama kawaida

    “mungu nisaidie ili nikafanye maajabu huko niendako sababu nataka kuikomboa familia yangu katika umasikini tuliokuwa nao”Alex alikuwa anajisemea mwenyewe kila alipokuwa anakumbuka hali ya nyumbani kwao

    Walifanikiwa kufika katika uwanja wa ndege wa Birmingham-Shuttlesworth International Airport uliopo katika jiji la Birmingham,Walianza kushuka kwenye ndege huku Alex akiona utofauti wa hali ya hewa katika nchi hiyo na nchi ya Tanzania.Kulikuwa na baridi la wastani sababu kipindi hicho kilikuwa ni cha majira ya joto

    Walikamilisha kila kitu pale uwanjani na kupokelewa na wenyeji wao ili kuwapeleka katika hoteli kwaajili ya mapumziko ili kesho yake waelekee kwenye makazi ya timu hiyo.Alex muda wote macho yake yalikuwa nje akiangalia jinsi lile jiji lilivyokuwa linapendeza tofauti kabisa na jiji la Dar es salaam ambalo ametoka

    “mh sisi tupo nyuma kimaendeleo”Alex alijisemea huku akitikisa kichwa

    Mpaka wanafika katika Hotel ya HAMPTON INN&SUITES BIRMINGHAM Alex alikuwa hajagandua macho yake nje sababu alikuwa anavutiwa na jiji ilo,Walishuka kwenye gari kisha wakaanza kuingia ndani ya hotel ili kupata chumba kwaajili ya mapumziko ili kesho yake waanze michakato ya uelekea kwenye makazi ya club

    Alex aliingia kwenye chumba cha hotel na kujikuta akishangaa shangaa sababu hakuwai kuingia kwenye chumba kizuri namna hiyo.Alex alijitupa kitandani ili apate kupunguza uchovu wa safari sababu alikuwa na masaa mengisana angani.Haukuchukua muda mrefu Alex alipitiwa na usingizi mzito uliomchukua masaa mengi mpaka kuja kushtuka

    Alex alishtuliwa na sauti ya simu iliyokuwa inahita kwenye chumba chake,Alex aliinuka na kwenda kuipokea ili kujua nani anaepiga

    “hallo”alisema baada ya kupokea simu

    “hallo hapa ni Reception kuna mgeni wako anahitaji kukuona”upande wa pili ulisema

    “ok mwambie aje chumbani”Alex alisema na kuweka simu mezani

    Baada ya dakika kadhaa mlango wa chumbani kwake alisikia unagongwa alifungua na kukutana na yule mwenyeji wake aliyemleta katika nchi hiyo ya Uingereza.Alimkaribisha ndani na kukaa kwenye masofa yaliyokuwepo kwenye kile chumba kikubwa ili kusikiliza ujio wa yule mwenyeji wake

    “nimekuja kukuangalia na kukuambia kwamba kesho asubuhi nitakuja kukuchukua ili tuelekee kwenye makazi ya club sababu wanahamu sana ya kukuona”yule mwenyeji alisema

    “sawa utakuja kunichukua saa ngapi?”Alex aliuliza

    “asubuhi nitakuwa hapa kwaajili ya kukuchukua”Yule mwenyeji alisema

    “sawa nitakuwa tayari”Alex alisema

    “sawa ila twende nje kwaajili ya kupata chakula kisha nikuache uendelee kupumzika”Yule mwenyeji alisema

    “basi ngoja nioge ndiyo tutoke”Alex alisema huku akisimama

    Alex aliingia bafuni na kuoga kwenye bafu ambalo hata hakutegemea kama siku moja itatokea kuingia,yeye alishazoea kuingia na ndoo bafuni lakini humo ndani alikutana na dish kubwa ambalo alitakiwa kuingia.Alex alimaliza kuoga kisha akatoka na kubadilisha nguo haraka haraka sababu hakutaka kumchelewesha mwenyeji wake.

    Walitoka nje na kuanza kuelekea kwenye restaurant ya hotel hiyo ambayo haikuwa na watu wengi sana,walikaa kwenye meza moja na muhudumu alifika haraka sana kuwasikiliza wanahitaji nini.Yule mwenyeji alichukua menu na kuagiza chakula anachokipenda,kasheshe lilikuwa kwa Alex kutokana na ugeni wa kwenye nchi hiyo alikuwa hajui achague chakula gani sababu majina hakuyazoea.Alichagua chakula kimoja wapo baada ya kuona neno chicken lilimaanisha kuku

    Vyakula vililetwa na wakaanza kula huku wakiongea mambo tofauti tofauti ili kubadilisha mawazo,yule mwenyeji alikuwa anamshauri mambo mengi sana kuhusu maisha ya pale Uingeleza ili asije akapoteza kitu kilichomleta pale

    “kijana ukifanya vizuri katika mpira nadhani utatokea kuwa maarufu sana na ukiwa maarufu utakuwa unawindwa sana na watoto wa kike,kama unavyojua mazoezi na wanawake ni vitu viwili tofauti kabisa”Yule mwenyeji wa Alex alisema

    “Nimekuelewa na mimi kilichonileta hapa nitakizingatia”Alex alisema huku akiwa makini sana

    “sawa me nitakutakia kila la kheri kwenye majaribio yako natumaini utakuwa ni miongoni mwa wachezaji wazuri”Alisema mwenyeji wa Alex

    Walimaliza kula na Alex alirudi chumbani kwake ili kupumzika kwaajili ya kesho kuelekea ndani ya club ya Birmingham.Alex alikaa kitandani huku akiangalia movie katka screen kubwa iliyokuwa kwenye chumba chake.Alex alirudisha mawazo yake Tanzania na kuona sura nzuri ya msichana mrembo aliyesukumana nae siku ya kwanza katika shule ya LoyolaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alex alimkubuka msichana Cindelela na kujikuta kama ubaridi ukipenya kwenye mwili wake sababu hakujua kama atakuja kumuona tena katika maisha yake sababu wapo mbali kwa kipindi hicho,Alex machozi yalikuwa yanamtoka kila alipokuwa anakumbuka majibu aliyojibiwa na Cindelela sababu yalimkatisha tamaa na hakutegemea kama siku moja itatokea kumpata Cindelela

    “Cindelela lazima utakuja kwenye himaya yangu”Alex alijisemea mwenyewe

    Alex aliajikuta usingizi ukimpitia na kulala fofofo sababu bado alikuwa na ule uchovu wa safari.Alikuja kushtuka asubuhi na kuamka kitandani ili ajiandae sababu ya kuja kuchukuliwa kuelekea kwenye makazi ya timu.Alijiandaa haraka haraka na kukaa tayari kwaajili ya kuja kuchukuliwa

    Haukupita muda mrefu mlangio wake uligongwa na alipoenda kufungua alikuwa ni yule mwenyeji wake amekuja kumchukua Kwaajili ya kuelekea kwenye makazi ya Club.Walitoka pale chumbani na kuingia kwenye gari kisha safari ikaanza.Alex alikuwa anaongea na mwenyeji wake huku macho yake yakiwa nje ili kutazama jiji ilo vizuri sababu lilikuwa linamvutia sana kwenye macho yake

    Baada ya muda wakawa tayari wameshafika kwenye makazi ya club hiyo kwaajili ya kufanya mazungumzo na kumpima Afya yake ili waangalie kama atawafaa katika timu yao.Alex aliingizwa moja kwa moja kwenye chumba cha mikutano ili kuongea na uongozi wa timu.Alex alikutana na vijana wengine kumi ambao nao wametoka sehemu tofauti tofauti kwaajili ya majaribio ili wachujwe na kubaki wachache ambao watajiunga na timu hiyo

    Wote walikaa tayari kwaajili ya kuanza hicho kikao ambacho hakikutakiwa kiwe cha muda mrefu,kikao kilianza na watu wote walikuwa makini kusikiliza

    “habari za asubuhi ndugu wachezaji,kama mlivyoambiwa kwamba timu yetu inavyohitaji wachezaji kutoka katika nchi tofauti tofauti ili kuimarisha timu yetu kwaajili ya kupanda ligi kuu kwa mara nyingine tena.Tumepita katika nchi zenu na kuchagua wachezaji ambao watashirikiana nasi katika kuiimarisha timu yetu katika mashindano tofauti.Siyo kila mchezaji aliyekuja hapa ataendelea kuwa na sisi wapo wengine ambao tutawarudisha nyumbani kama uwezo wao ukiwa mdogo katika kucheza mpira”Alisema Peter Pannu ambae ni director

    “Mtafanya majaribio ya siku tatu kuanzia kesho chini ya uangalizi wa benchi zima la ufundi na wale watakaoonyesha uwezo wa hali ya juu tutabaki nao hapa ila wengine tutawarudisha mlipotoka sababu hii ni awamu ya kwanza na wengine bado wanakuja,Kwa awamu hii tutachagua wachezaji watatu kati ya ninyi kumi mliokuwa hapa”aliongeza Mr Peter pannu

    Wachezaji wote waliokuwepo pale walivuta pumzi sababu hawakutegemea kama kutakuwepo na mchujo watakapofika hapo kwenye club.Alex alijihisi kufakufa sababu hakujua kama atafahulu katika mchujo sababu wale wenzake aliowaona walikuwa na maumbo makubwa na walikuwa wanaonyesha kwamba wapo vizuri kwenye mchezo wa soka

    “acha nipambane nao sababu japo nchi yangu haina umaarufu sana kwenye mchezo wa soka”Alex alijisemea mwenyewe

    Alex alikuwa na haki ya kuogopa sababu wale wenzake wote walikuwa wametoka katika nchi ambazo zilikuwa zimeendelea kwenye mchezo wa soka.Wapo waliotoka Nigeria,Cameroon,Ivory cost ambazo zote zinajulikana katika ulimwengu wa soka.Alex yeye ametoka kwenye nchi ambayo haipo hata kwenye nafasi mia moja katika viwango vya fifa

    Kikao kiliisha na kila mtu alipelekwa kwenye chumba chake kwaajili ya kesho kuanza mazoezi ya mchujo.Alx alikuwa anawaza mengi sana na kikubwa alilokuwa analipinga ni kushindwa katika majaribio kwani alikuwa hataki tena kurudi Tanzania wakati ameshafika kwenye nchi ambayo ingemletea mafanikio yakeCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Asubuhi na mapema wachezaji wote kumi walikuwa ndani ya uwanja wa WAST HILLS TRAINING GROUND ambao ulikuwa unatumika kwaajili ya mazoezi ya timu hiyo.Alex alikuwa anaingia ndani ya uwanja wa majaribio kwaajili ya kuonyesha uwezo wake wa soka.Alex alikuwa anavuta kumbukumbu ya maisha aliyokuwa anaishi Tanzania machozi yalikuwa yanamtoka huku akiingia uwanjani

    “hapana lazima nipambane sitakiwi kurudi kule nilipotoka na kama nikirudi ndoto za kumpata Cindelela zitaishia hapo”Alex alijisemea huku akifuta machozi

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog