IMEANDIKWA NA : VICTOR DISMAS
*********************************************************************************
Simulizi : Nakupenda Cindelela
Sehemu Ya Kwanza (1)
“Nakupenda sana Cindelela na sijawahi kupenda msichana kama ninavyokupenda wewe katika maisha yangu,Cindelela wewe ndiyo chaguo la moyo wangu .Akili yangu yangu,filkra zangu pamoja na nafsi yangu zote zipo kwaajili ya upendo wako,Cindelela naomba unipe japo nafasi katika moyo wako ili nipate japo Faraja ndani ya nafsi yangu,bila ya wewe kunipa nafasi sidhani kama kuna umuhimu wa mimi kuishi kwenye hii dunia wakati nakosa kitu nikipendacho”
“Cndelela mapenzi tumeumbiwa sisi binadamu wala hayajaumbiwa miti au mawe na ninavyosema nakupenda namaanisha kweli nakupenda kutoka ndani ya moyo wangu.Cindelela nimejitolea kwaajili yako na kila nitakalolifanya itakuwa kwaajili yako,Cindelela nakuomba unielewe ewe kipenzi cha roho yangu NIPO TAYARI KUFA KWAAJILI YAKO”.
Maneno hayo yote alikuwa anazungumza kijana Alex ambae alionekana kuchoka huku njaa ikimuuma sana,Alex alikuwa ameegemea kwenye mti huku macho yake yakiangalia na kuona ndegewaliokuwa wanatua kwenye huo mti huku wakiimba nyimbo za furaha.Nyimbo zote walizokuwa wanaimba wale ndege huku wakirukaruka kwenye miti Alex aliziona kama kelele kwenye masikio yake sababu ya njaa na uchovu aliokuwa nao
Alex aliinuka pale alipokuwepo na kujaribu kuelekea katikati ya msitu ili apate japo matunda ambayo yangeweza kuipoza njaa aliyokuwa nayo,alijitahidi kutembea kwa uhangalifu huku akitazama juu ya miti kama anaweza kuona mti wowote wenye matunda.Alex bado alikuwa na msongo wa mawazo kichwani kwake sababu alikuwa ahamini kama ndiyo yeye aliyekuwepo ndani ya msitu hule wenye kutisha sana
Alex alitembea kwa muda mrefu sana mpaka akahisi kuchoka sababu macho yake yalikuwa yanafunga kutokana na njaa aliyokuwa nayo,Alex aliamua kukaa chini ya mti mmoja ili kupumzika sababu alikuwa na uchovu ambao ulimshinda kuendelea na safari ya kutafuta chakula.Haukupita muda mrefu usingizi nao ulimpitia pale pale chini bila hata kujitambua,kutokana na uchovu aliokuwa nao Alex alijikuta amelala kama samaki wanayemuhita pono
Puu puu puu ndiyo sauti iliyomshtua Alex kutoka usingizini huku akikurupuka kwa woga kutokana na ile sauti aliyoisikia,Alex aliogopa sana kusikia sauti ya kishindo kutoka juu ya ule mti sababu alikuwa hajui ni kitu gani kilichodondoka,Alex alikaa pembeni na kufikicha macho yake ili kujua ni kitu gani kilichodondoka kutoka katika hule mti aliokaa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alex hakuamini macho yake baada ya kuona maembe makubwa matatu yakiwa mbele yake tena yameiva vizuri ,Alex alianza kutoa tabasamu japo lilikuwa tabasamu hafifu sana.Kutokana na njaa aliyokuwa nayo alianza kuyasogelea yale maembe huku mate yakimdondoka kutokana na uchu wa kupata chakula,alipeleka macho yake juu ya hule mti na kukuta maembe mengi yakiwa juu ya hule mti tena mengi yakionekana yameiva
“Asante sana Mungu wewe ndiyo kila kitu kwangu na wewe ndiyo utanilinda mpaka pale nitakapotoka ndani ya huu msitu”Alex alisema huku akiyaokota yale maembe
Alex alianza kuyafakamia yale maembe kwa haraka kisha akachukua vipande vya miti na Kuanza kuangua maembe mengine kwaajili ya akiba ya usiku,Alex alipata maembe mengi sana kwasababu ya uhodari wake wa kuyaangua.Alivua shati lake na kuyaweka yale maembe huku yeye akiwa amebakia na Vest peke yake,alitoka pale kwenye mti na kuendelea na safari ya kutoka katika hule msitu mkubwa pende zote
Usoni Alex alikuwa na sura ya uchovu na upole sababu alikuwa haujui wapi anaelekea,Alex alitamani japo akutane na mtu yoyote katika hule msitu ili ampe msaada sababu alikuwa anaogopa kutembea peke yake kwenye hule msitu uliokuwa unatisha sana.Usiku nao ulikuwa unaingia huku hofu nayo ikizidi kutanda moyoni mwake sababu huo msitu ulikuwa na wanyama wakali sana, wanyama ambao wanahatarisha maisha ya binadamu.Alex alitafuta mti mkubwa sana na kupanda juu yake ili aweze kulala sababu aliogopa kulala chini kutokana na wanyama waliokuwa wanazunguka katika huo msitu hasa nyakati za usiku
“eeh mungu naomba unilinde katika kila kitu ninachokipitia,naomba unilinde na mambo yote mabaya sababu bila ya wewe kutuma malaika zako mimi siwezi kufanya chochote”Alex aliongea kwa uchungu huku machozi yakimdondoka
Alichukua yale maembe yake na Kuanza kula moja huku machozi yakiendelea kumtoka,Alex alijitahidi kuvuta kumbukumbu ili ajue ni kitu gani kilichosababisha mpaka yeye afike kwenye ule msitu mkubwa
“Ewe mwanamke nikupendae na nitakae kupenda mpaka mwisho wa maisha yangu,nimefanya haya yote kwaajili yako ili nipate japo nafasi katika moyo wako,NAKUPENDA SANA CINDELELA na nitakupenda mpaka tone la mwisho la damu yangu”Alex alisema huku machozi yakimtoka
Alex kila alipokuwa anamkumbuka Cindelela machozi yalikuwa yanamdondoka japo alikuwa anajikaza kiume,Cindelela ndiyo lililokuwa chaguo lake sababu aliweza kuiteka nafsi yake ndani ya muda mfupi,lakini Alex kila alipokuwa anakumbuka kilichotokea mpaka anafika ndani ya huo msitu alikuwa Anatokwa na machozi,machozi yauchungu machozi ya uzuni pamoja na machozi ya manyanyaso
“upo wapi Cindelela wangu?uko wapi ewe kipenzi cha roho yangu?”
…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
Ilikuwa ni ijumaa iliyotulia huku hali ya mawingu ikionyesah kwamba muda wowote mvua inaweza kunyesha.Wanafunzi katika shule ya Mbezi inn walionekana wakiwa kwenye pilikapilika kila mtu akiwa na mambo yake aliyokuwa anayafanya muda huo,wengine walikuwa madarasani wanajisomea,wengine walikuwa wanapuga story sababu walimu hawakuwa madarasani muda huo,Baadhi ya wanafunzi watoro walikuwa wanatafuta mbinu za kutoroka shule
Tofauti na wanafunzi wote alionekana mwanafunzi mmoja akipitisha daftari kwa wanafunzi wenzake ili ili kukusanya michango sababu siku hiyo walikuwa na mechi kati yao na shule nyingine,Mwanafunzi huyo alikuwa anapita kwa mwanafunzi mmoja mmoja na kumuomba mchango wake,wapo waliokuwa wanatoa pia wapo waliokuwa wanakataa wakisema hakuna faida yoyote watakayoipata katika mechi hiyo.
“Janeth tusaidie mchano wako sababu leo tuna mechi na shule ya Royola,mchano wako unaweza kutusaidia katika kuwapa maji wachezaji wetu”Kijana Alex alikuwa anamuambia mwanafunzi mwenzake
“hivi Alex mnajua kama tumewachoka?ninyi kila mechi mnayoenda kucheza lazima mtufuate na kutuomba mchango,kwani shule haiwapi hela?”Janeth alimuuliza Alex huku akivuta daftari lake ili asome
“siyo hivyo Janeth support tunayoipata shule ni ya usafiri tu,na sisi tukishinda mechi hii tutakuwa tumeitangaza shule yetu”Alex alisema kwa unyenyekevu wa hali ya juu
“sawa shika hii ila iwe mwanzo na mwisho kuja kuniomba michango ya mechi”Janeth alitoa shilingi elfu moja na kumkabizi Alex
“asante sana kwa mchango wako dada Janeth mungu akubaliki”Alex alisema na kuipokea ile hela
Alex aliendelea kukusanya michango kwa wanafunzi wengine .wanafunzi wengi walikuwa wanampatia michango Alex kutokana na uhaminifu mkubwa alionao na alikuwa siyo mtu wa tama,mpaka inafika saa sita na nusu Alex alikuwa ameshajikusanyia hela za kutosha ambazo zingewasaidia katika safari yao
“Namuhitaji captain wa timu ya shule”alisema Mwalimu wa michezo
“nipo hapa Mwalimu”Alex aliitika na kumfuata Mwalimu pale aliposimama
“Nifuate ofisini kwangu”Mwalimu alisema na kuondoka
Walitoka na kuelekea ofisini kwa Mwalimu sababu kuna vitu alitaka kumuambia.Walifika na kukaa kwenye viti huku Alex akisubiri kuambiwa ni kitu gani ameitiwa pale
“Alex wachezaji wote wapo vizuri?”ilo ndilo lilikuwa swali la kwanza kuoka kwa Mwalimu
“Ndiyo Mwalimu wote wapo vizuri kasoro mimi nasumbuliwa na maralia”Alex alisema
“Mungu wangu!!! Kwahiyo hauna uhakika wa kucheza meci ya leo?”.Mwalimu aliuliza kwa kuhamaki
“Mwlimu itategemea kama timu ikizidiwa sana naweza nikaingia uwanjani”Alex alisema huku akionyesha kweli anaumwa
“Hapo sawa sababu shule nzima inakutegemea wewe katika upachikaji wa magoli sasa usipocheza nadhani itakuwa kituko,ila nenda kawaambie wachezaji wote pamoja na washangiliaji waliotoa michango ifikapo saa nane wawe pale uwanjani kwaajili ya Kuanza safari”Mwalimu alisema huku akichezea kalamu yake
“sawa Mwalimu”Alex alijibu na kusimama
Alex alitoka ofisini kwa Mwalimu na kwenda kuwatangazia watu madarasani kuhusu muda wa kuondoka pale shuleni na wapi wanahitajika kuwepo,muonekano wa Alex ulikuwa ni wa kushangaza kwa wanafunzi wenzake kutokana na mavazi yake ya shule kuwa chakavu japo alijitahidi kujiweka nadhifu ili na yeye awe kama wenzakeCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa muonekano aliokuwa nao Alex baadhi ya wanafunzi walikuwa wanamtenga na kumuhita chokoraa japo na wao walikuwa wanasoma shule yenye tabaka moja.Wanafunzi wengine walikuwa wanampenda kutokana na ukarimu aliokuwa nao pamoja na ucheshi mbele za watu.Wale waliokuwa wanamtenga ni wale wanaojiita masister duu na mabrother men wa shule
Ilipofika saa nane kamili ilipofika wanafunzi wote walikuwa wamekusanyika katika uwanja wa shule ili waanze safari ya kuelekea katika shule ya Royola,kila mchezaji alikuwa amepania mechi hiyo sababu alitaka kuonyesha uwezo wake aliokuwa nao.Magari mawili aina ya coaster yaliwasili katika uwanja huo na kupakia wachezaji pamoja na washangiliaji,ndani ya gari kila mtu alikuwa anaongea lake huku akijitapa kwa maneno
“Mimi leo lazima nifunge magoli mawili”alijitapa Devi
“Wewe Devi utaniweza mimi?,mimi leo lazima niwe nyota wa mchezo kwa kutupia goli tatu kama Messi”alijitapa mwananfunzi mwingine ajulikanae kwa jina la Bernad
“Ninyi chezeni tu mimi naenda kuangalia watoto wazuri,si unajua warembo wengi ni wakishua tofauti na shuleni kwetu”Alisema Enock huku akitabasamu
Wanafunzi wote walicheka sababu hawakutegemea kupata wazo kama lile kutoka kwa Enock,Story zilinoga sana ndani ya gari huku kila mtu akiongea la kwake kuhusu mechi hiyo,wengine walikuwa wanaimba nyimbo za kujitamba ilimradi ilikuwa vurugu tu ndani ya gari.Tofauti na wanafunzi wengine Alex alionekana kuwa tofauti sana na wanafunzi wengine sababu yeye muda wote alikuwa kimya huku akitafakari kama ataweza kucheza mechi hiyo
“Alex mbona umepooza sana?”aliuliza Enock
“nipo kawaida ndugu yangu”Alex alijibu
“nakuona haupo kawaida na nilivyokuzoea sababu umekosa amani”Enock alisema
“Nawaza kama nitaweza kucheza mechi ya leo au la sababu bado naumwa sana”alisema Alex huku akionekana kupooza kweli
“Hapana Alex wewe lazima ucheze kumbuka wewe ndiyo tunakutegemea katika ufungaji sasa usipokuwepo nani atafunga magoli?”aliuliza Enock
“kwenye kikosi nimewapanga Devi na Bernad kama washambuliaji,nadhani watafanya vizuri kama n inavyotegemea ila kama wakizidiwa sana inanibini niingie mwenyewe”alisema Alex
“sawa tunakukubali Van persie wetu”alitania Enock
Wote walicheka na kutulia tuli huku kila mtu akiwa anawaza la kwake,gari liliongeza kasi na baada ya nusu saa wakawa wameshafika katika shule ya Royola na kila mwanafunzi alishuka kwenye gari huku wakifurahi kufika katika shule hiyo nzuri sana.Walipokelewa vizuri na wanafunzi pamoja na walimu wa shule hiyo ambao walionekana wakalimu sana kwa wageni wao
Macho ya wanafunzi wa Mbezi inn walikuwa yanaangalia madhari ya shule hiyo ambayo yalikuwa tofauti sana na shule wanayosoma wao.Macho ya Alex yalikuwa yanaangalia hule uwanja jinsi ulivyokuwa mzuri na wakuvutia ambao ulikuwa tofauti sana na uwanja wa shule yao
“mh yani mimi niache kucheza mpira kwenye uwanja mzuri namna hii?”Alex alijiuliza mwenyewe huku akipiga hatua kuzunguka zunguka kidogo
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Mbezi inn walianza kuzunguka zunguka katika shule iyo ili kuangalia mazingira ya shule.Macho ya Enock yalikuwa busy kuangalia wasichana warembo waliokuwa wanakatiza kwenye macho yake
“Ebwana eeh!!cheki toto lile lilivyoumbika “Hayo ndiyo yalikuwa maneno aliyokuwa anasema Enock kila alipokuwa anakutana na msichana mzuri
Kijana Alex alikuwa peke yake akizunguka baadhi ya maeneo ya shule hiyo japo kusafisha macho yake,Alex alipita kwenye kila darasa akiangalia jinsi yalivyokuwa mazuri na yakuvutia,Alex alikuwa anatabasamu kila alipoona kitu kilichokuwa kinamfurahisha
“Jamani kaka mbona unanigonga?”Alex alisikia sauti nyororo ikimuuliza na kufanya masikio yake yazibuke huku mwili wake ukisisimka
Alex alipogeuka kuangalia amemsukuma nani,moyo ulimripuka baada ya macho yake Kukutana na binti mrembo akiwa amesimama pembeni yake huku akionyesha kukasirika.Binti huyo alikuwa na kila sababu ya kuitwa mrembo sababu alikuwa na vigezo vingi sana katika uzuri wake
Msichana yule alikuwa na sura nzuri sana tena ya kuvutia iliyokuwa na macho ya wastani,pua iliyochongoka huku ikiweka muonekano mzuri kati ya macho na mdomo wake.Mdomoni alijaliwa lipsi nzuri za kufanya awe na tabasamu zuri lililosababisha vishimo vidogo kwenye mashavu yake kila alipokuwa anacheka au kutabasamu
Japo alikuwa amevaa nguo za shule lakini umbo lake zuri lilionekana vyema kutokana na hips zake kutaka kutoka kwenye skirt yake aliyoivaa,japo alikuwa anaonekana bado ni mdogo kiumri lakini uzuri wake ulishajionyesha wazi katika kila macho ya mwanaume aliyemuona,weupe wake wa wastani nao uliongeza nakshi katika uzuri wake.Alex alikuwa ameganda kama sanamu akimuangalia Yule binti aliyesimama pale pembeni yake huku huyo binti nae akiwa amemkazia macho Alex
“Kaka mbona unanishangaa wakati nakuambia umenisukuma?”Yule dada alimuuliza tena Alex baada ya kuona amezubaa
Alex aliendelea kumshaangaa Yule binti sababu ya uzuri aliokuwa nao na kila dakika zilivyokuwa zinaenda Alex alizidi kuchanganyikiwa na uzuri wa Yule binti.Japokuwa Yule binti alikuwa amekasirika lakini Alex aliona kama mzaa sababu hasira zake ziliongeza uzuri wake
“kaka ina maana haunisikii?”Yule binti aliuliza tena
“Samahani dada nilikuwa mbali sana kimawazo,naomba unisamehe”Alex alisema kwa upole huku matamshi yakiwa yanasita kutoka
“sawa ila usitembee kama upo peke yako njiani kumbuka kuna watu wengi unapishana nao”Yule dada alikuwa anaongea huku akianza kuondoka
“samahani dada naweza kujua hata jina lako?”Alex aliuliza
“naitwa Cindelela?”Yule dada alijibu
“kweli una sifa zote za kuitwa Cindelela”Alex alisema huku akimuangalia kwa makini sana
“kwanini unasema hivyo?”Cindelela aliuliza
“uzuri uliokuwa nao na sifa nilizokuwa nazisikia kutoka kwenye hadithi ya Cindelela sidhani kama mnapishana sana japo wewe unaonekana umemzidi sifa”Alex alimsifia
“kaka unamasihara sana ila naomba nikuache kuna sehemu naenda”Cindelela alisema na kuondoka
Yule binti aliondoka huku akimuacha alex kwenye simanzi kubwa sana sababu hakutegemea kama atakutana na binti mrembo kama Yule.
“hivi naota hama ni kweli?”Alex alijiuliza baada ya kubaki peke yake
Alijizoazoa pale alipokuwa na kuanza kuondoka ila moyoni alishaanza kutawaliwa na fikra za Yule binti sababu alishaanza kumpenda sana kutoka moyoni
“Lazima nimtafute kwani nahitaji kumfahamu kiundani “Alex alijisemea
Alex aliamua kurudi walipokuwepo wenzake ili wapange mikakati ya mechi sababu muda huo ulikua ni saa tisa na nusu na ifikapo saa kumi mechi ndio inaanza .Saa kumi kamili ilipofika wanafunzi wa shule ya loyola walianza kujitokeza mmoja mmoja katika uwanja wa shule hiyo ndani ya saa kumi na dakika ishirini uwanja wote ulijaa wanafunzi wakisubiri mechi ianze na kushuudia kandanda safi kutoka kwa wanafunzi wenzao
Macho ya alex yalikua hayatulii sababu muda wote alikua akiangaza pande zote ili angalau aweze kumuona Cinderela kwa mara nyingine tena
“Sijui atakua amekaa upande gani?”alex alijiuliza
Refa alipiga filimbi kuashiria mpira Kuanza .Mpira ulianza kwa kasi huku kila timu ikishambulia kwa kasi katika lango la timu pinzani.Alex alikua makini sana kufuatiilia mchezo ule kwani muda wowote anaweza kuingia endapo timu yake itazidiwaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati alex anaendelea kuangalia mpira kwa mbali alifanikiwa kumuona CInderela akiwa amekaa na rafiki zake wakiangalia mpira,moyo wa Alex ulilipuka sana kumuona Yule binti mrembo ambae alishaingia kwenye moyo wake.mrembo aliyesababisha mtafaruku katika nafsi yake ndani ya muda mfupi
“I must do something”(lazima nifanye kitu).alex alijisemea huku akitabasamu
Mpira ulienda mapumziko huku magoli yakiwa bila kwa bila sababu mechi ilikua ngumu sana na kila timu ilikuwa inalinda lango lake ili wasiruhusu goli kuingia,wachzeaji wa Mbezi inn walikaa upande wao huku Mwalimu wao akiwapa maelekezo ya kufanya watakaporudi kipindi cha pili
“Alex fanya mpango uingie kwani naona tumezidiwa”Mwalimu wa michezo alisema
“sawa Mwalimu”Alex alisema huku akivaa jezi yake japo alionekana hana raha.
Refa aliita wachezaji waingie kwa ajili ya kipindi cha lala salama,Alex nae aliingia uwanjani huku macho yake yakimuangalia msichana Cinderela aliyekuwa katikati ya rafiki zake,Alex moyo wake ulikuwa unafurahi kila alipokuwa anamuona Cindelela akitabasamu huku akiongea na wenzake
“ngoja nionyeshe uwezo wangu wote katika soka sababu naweza kuteka hisia za mashabiki wa hapa”Alex alijisemea huku akipasha misuli yake
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku shule ya Loyola wakishambulia kwa kasi katika lango la Mbezi inn,Loyola walibahatika kugongesha miamba mara tatu bila kupata bao na kufanya uwanja uripuke kwa shangwe huku wakiimba nyimbo za kujisifu
Alex alipata mpira uliotoka kwa beki wa kulia na kuanza kuwapiga chenga mabeki watatu wa Loyola kisha akabaki yeye na goli kipa,Alex alipiga shuti moja kali sana lililomshinda kipa na kuingia golini moja kwa moja wavuni.Kelele zilisikika kwa wanafunzi wa Mbezi inn huku wakilitaja jina la Alex kwenye kila wimbo wa kusifia ,kasi yake haikuishia hapo kwani Alex alikua anawanyanyasa mabeki wa Loyola mpaka wakamkata kwenye eneo la hatari na kusababisha Mbezi inn wapate penalty
Refa akaweka penalty na mpigaji alikua Alex mwenyewe,Alex alimuangalia kipa kisha akapiga shuti moja kali liliongia wavuni na kufanya matokeo yasomeke mbili kwa bila
“That boy is a best player and super sub ,I cant belive if there is talented man in Tanzania like that boy”alisikika Mwalimu wa shule ya Loyola akimsifia Alex
“he is playing like lionel messi”alisikika Mwalimu mwingine.
Dakika ya themanini na nane Mbezi inn walipata kona iliyochongwa kiufundi kutokea upande wa kushoto, mpira ulitua kwenye kichwa cha Alex kilichofanya mpira kugonga mwamba na kutinga wavuni,watu walipiga kelele hata wanafunzi wa Loyola walishangilia goli lile sababu lilionekana ni la ufundi wa hali ya juu
Mpaka refa anamaliza mpira Mbezi inn walikuwa wameshinda goli tatu kwa sifuri,watu wengi walijazana kumshangilia Alex kwa ushindi alioupatia timu yake na kuonekana yeye ndiyo shujaa wa mechi.Sio wanafunzi wa Mbezi inn peke yake waliokuja kumpongeza Alex hata wanafunzi wa Loyola walikuja kumpongeza kwani alionyesha kandanda safi tofauti na walivyofikiria
Macho ya Alex hayakutulia sababu alikuwa anaangalia kila pande ili amuone msichana aliyetokea kumpenda ghafla.kwa mbali aliweza kumuona binti mrembo Cinderela akiwa anaagana na mwenzake kisha akapanda kwenye gari aina ya V8 na kuondoka.Alex hakuamini macho yake baada ya gari alilopanda msichana mrembo Cinderella likiishiria getini na kumfanya moyo wake ujawe na simanzi
“jamani wanafunzi wa Mbezi inn tunatakiwa kwenye gari ili tuondoke”ilisikika sauti ya Mwalimu wa michezo ikisema
wanafunzi wa Mbezi inn walianza kuingia kwenye magari waliyokuja nayo ili kurudi shuleni kwao , kijana Alex mawazo yake bado yalikuwa kwa msichana Cinderella ambaye ndiyo ilikua mara ya kwanza kwa wao kuonana lakini alitokea kumpenda kuliko kitu chochote
“hapana lazima nirudi hapa niweze kuonana na Cinderella”Alex alijisemea mwenyewe
Gari la shule ya Mbezi inn wakati linaondoka wanafunzi walikua wanashangilia huku wakitaja jina la Alex kama ndiyo shujaa wa mchezo hule.Alex mwenyewe alikua kimya sana sababu alikua anauwaza uzuri aliokua nao msichana Cinderella
“vipi Alex wenzio tunafurahi wewe upo kimya?”Enock alimuuliza
Kaka yani acha tu nilichokiona nakijua mwenyewe”alex alisema kwa hisia kali
“kwani umeona nini?”Enock aliuliza
“Enock nimemuona msichana mzuri sana ambae sikutegemea kumuona katika maisha yangu”alex alisema
“kaka acha fix huyo msichana yukoje mpaka useme hvyo”Enock aliuliza
“Enock msichana niliyemuona ni mzuri kuliko wasichana wote niliowahi kuwaona na kwa kweli nimempenda sana hata mungu mwenyewe analijua hilo na kama ni shetani hatakuwa amesababisha hivi basi atakuwa amefanikiwa kwa asilimia kubwa sana.Enock kama itatokea siku Yule msichana akawa kwenye mapenzi yangu nadhani nitatoa sadaka iliyokuwa juu ya uwezo wangu”Alex alifunguka kwa hisia kali
“kweli Alex Leo umepatikana,wewe si ndiyo unajifanya ga mgumu kwa mademu?,ebu angalia Angel alivyokupenda wewe ukamchomolea na kusema utaki msichana,vipi leo imekuawaje ?”Enock aliuliza
“kaka Yule msichana nimetokea kumpenda ghafla na anavyoonekana ni mstaarabu kuliko ninavyofikiri,mpaka sasa sijui ni kitu gani kimesababisha nimpende Yule msichana wakati hata simjui hata kidogo na sijui kama atakubali kuwa wangu japo najipa matumaini ya kumpata”Alex alisema kwa utulivu wa hali ya juu
“aya bwana yangu macho naona unataka kufungwa na wazee wa kishua”Enock alisema
Walienda na story mpaka walipofika shuleni huku wakishangilia kwa ushindi walioupata,kwa kuwa giza lilishaingiza Alex aliamua kurudi nyumbani kwao maeneo ya suka gorani ambapo alikuwa anaishi na wazazi wake.Alex aliporudi nyumbani alioga na kukaa sebuleni kwao kwaajili ya chakula cha usiku,Alipomaliza kula aliingia chumbani kwake ili atafute usingizi sababu alikuwa amechoka kutokana na ile mechi waliyocheza
Alex alijitahidi sana kutafuta usingizi lakini ilikuwa inashindikana kutokana na mawazo yake kumfikiria Cindelela,hata yeye mwenyewe alikuwa ajielewi kwanini ametokea kumpenda ghafla Yule msichana wakati ndiyo kwanza ilikuwa mara ya kwanza kwa wao kuonana
“Hapana siwezi kukubali lazima nimtafute Cindelela lazima nieleze hisia zangu kwake,mh ila hakinikataa je?”Alex aliongea huku akiandika kwenye Diary yake iliyokuwa pembeni mwa kitanda chake
Asubuhi kulipokucha Alex alienda shule kama kawaida na kujichanganya na wanafunzi wenzake ambao waliokuwa wanampa support,wanafunzi wengi walipomuona Alex walipiga kelele kwa furaha sababu yeye ndiye mtu aliyeipatia ushindi shule yake.Masomo yaliendelea kama kawaida huku Alex akionekana kutokujali sifa alizokuwa anazipata kutoka kwa wanafunzi wenzake yeye mawazo yake ypte yalikuwa yanamuwaza msichana Cindelela ambaye aliuteka moyo wake
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..
Kwa upande wa Cindelela alikuwa hana hata moja analoliwaza kuhusu Alex,yeye muda mwingi alikuwa anafanya mambo yake ya kujisomea na muda mchache aliokuwa anaupata alikuwa anabiga story na rafiki zake ili kubadilishana mawazo
“Cindelela”Aliita rafiki yake
“Niambie Witness”aliitika
“Siku zile niliona ulikuwa unaongea na Yule kijana aliyefunga magoli matatu kwenye mechi,vipi mnafahamiana?”Witness aliuliza
“hapana hata simfahamu”Cindelela alijibu kifupi
“sasa mbona milikuwa mnaongea muda mrefu?”Wit aliulza tena
“Wit unapenda kunidadisi sana!! Yule kijana ilitokea bahati mbaya alinisukuma ndiyo maana tukaanza kuongea lakini hakuna chochote kuhusu kufahamiana”Cindelela alijibu kwa kirefu
“kumbee!! Me nilidhani mnafahamiana lakini kwa dalili zinavyoonyesha Yule kijana atakuwa na kitu moyoni sababu muda wote macho yake yalikuwa yanakuangalia wewe na hata alipoingia uwanjani akugandua macho yake kwako”Witness alisema huku akitabasamu
“mhh!!! Mimi sijui chochote na mambo ya huyo kijana tuyaache sababu hatuhusu”alisema Cindelela
Waliendelea kupiga story nyingine huku wakicheka kwa furaha,walikuwa wanapiga story ili kusubiri waje kuchukuliwa na magari kwenda nyumbani,Haikuchukua muda mrefu gari ya kina Cindelela iliwasili pale shuleni na kumpakia Cindelela ili arudi nyumbani
“Bye Wit”Cindelela alisema huku akipanda kwenye gari
“bye Cindelela tutawasiliana”Wit alisema
Baada ya Cindelela kuondoka Witness nae alikuja kuchukuliwa na gari yao na kuondoka,hayo ndiyo yalikuwa maisha ya kila siku kwa watot hao wawili kutokana na hali za wazazi wao kuwa nzuri
Cindelela alikuwa na maisha mazuri sababu alikuwa ni mtoto wa kipekee katika familia ya mzee Jacobo na mke wake maria,mzee Jacobo alikuwa ni waziri wa mambo ya nje katika nchi ya Tanzania huku mkewe akiwa ni daktari mkuu katika hospital yao binafsi ambayo ilikuwa inashughulika na magonjwa tofauti tofauti
Kutokana na azi walizokuwa wanazifanya maisha yao yaklikuwa mazuri sana sababu walikuwa wanapata kila kitu walichokuwa wanakitakakatika maisha yao.Wzazi wa Cindelela walimpenda sana binti yao sababu yeye ndiyo alikuwa ni mtoto wao pekee katika familia yao na ndiyo lilikuwa tegemeo lao la baadae katika maisha yao.Walijitahidi sana kumpa kila kitu alichokuwa anakitaka ili aje kufanikiwa katika maisha yake ya baadaeCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-
Mzee Jcobo alikuwa hana uwezo wa kupata mtoto tena sababu ya ajali ya gari aliyoipata nchini Sweden akiwa katika shughuli za kimataifa,Ajali ile ilifanya kupoteza nguvu za kiume kutokana na operation aliyofanyiwa karibu na viunga vya uzazi ili kunusuru maisha yake.Siri hiyo ilibaki kwake na kwa mkewe hakuna hata mtu mmoja aliyekuwa anafahamu kama mzee Jacobo hawezi kupata mtoto tena
Fikra za mzee Jabobo,mapenzi yake yote pamoja na mawazo yake yalikuwa kwa mtoto wake wa pekee na kipenzi chake Cindelela sababu ndiyo lilikuwa jicho lake alilokuwa analitegemea
"mwanangu nakupenda sana na kila kitu ninachokifanya nafanya kwaajili yako,nakuomba usije kuniangusha mwanangu,mambo ya wanaume achana nayo kabisa sababu wanaume watakuaribia maisha yako ambayo nayatengeneza kwa gharama kubwa"baba yake alikuwa anamsisitizia
"usijali baba sitokuangusha na nakupenda sana baba yangu"
Hyo ndiyo yalikuwa mazungumzo yao ya kila siku wanapokaa kama familia.Kutokana na uzuri aliokuwa nao Cindelela wazazi wake walikuwa wanaofia sana wanaume kwahiyo walijitahidi kumpatia kila kitu ili asije kutegeka na wanaume wa nje ambao wanajifanya wana pesa,Wazazi wake walimuwekea ulinzi pale shuleni kwa kuchagua baadhi ya walimu ili wamfatilie Cindelela katika kila jambo alilokuwa analifanya
............................................................................................................................................................................................................................................................................................
Mpaka mwezi unakatika Alex hakupata bahati ya kuonana na Cindelela kwa maa nyingine,Tabu aliyokuwa anaipata Alex kutokana na kutomuona Cindelela kwa mara nyingine ilikuwa haielezeki sababu ubongo wake wote ulikuwa umeshaganda na kusitisha kufanya kazi nyingine zaidi ya kumuwaza Cindelela.Mawazo yalikuwa yanapishana kichwani mwake huku akipanga mbinu za kutaka kumuona yule binti mrembo Cindelela
"Enock rafiki yangu siku zinazidi kukatika bila kumuona Cindelela sijui nifanye nini"Alex alikuwa anamuomba swahiba wake
"mh!! labda twende shuleni kwao tunaweza tukamuona"Enock alishauri
"sidhani kama itawezekana tena kuenda kwenye shule hile"Alex alisema huku akionyesha kukata tamaa
Wliongea mengi sana huku wakipanga mipango ya kwenda katika shule ya Loyola ili wakapate nafasi ya kuonana na Cindelela na kumueleza hisia zake kwake,kila mpango waliokuwa wanapanga ulikuwa unashindikana mpaka mwezi mwingine ulipokatika bila ya Alex kumuona Cindelela,Kichwani mwa Alex alishajua kama haitotokea tena kwa yeye kumuona tena Cindelela msichana anayempenda.Siku moja Alex aliitwa na mwalimu wa michezo ofisini kwake sababu kuna jambo alitaka kumuambia na yeye kama captain wa shule lazima ausishwe,Alex alifika kwenye ofisi ya mwalimu na kukaa kwenye kiti ili amsikikilize kitu alichomuitia
"Alex nimekuita hapa kwasababu moja,kuna barua ya mechi imekuja hapa shuleni kwetu kuna shule inataka mechi na sisi"mwalimu alisema
"shule gani mwalimu?"Alex aliuliza
"Loyola wameomba mechi ya marudiano na sisi si unakumbuka mechi ya kwanza tuliwafunga"Mwalimu alisema huku akitabasamu
Moyo wa Alex ulimlipuka baada ya kusikia taharifa ile kutoka kwa mwalimu wake wa michezo,Alex hakutegemea kama itatokea siku Loyola wakaomba mechi na shule yao sababu ya tofauti wa madaraja,Loyola waliomba hiyo mechi ili kulipa kisasi kutokana na kipigo cha aibu walichokipata kutoka kwenye shule ya mbezi inn
"Vipi Alex tuwakubalie?"mwalimu aliuliza
"mwalimu inabidi tuwakubalie sababu wanajitahidi sana kuleta upinzani"Alex alisema huku akionyesha kufurahi kupita kawaida
Mipango ya mechi iliandaliwa vizuri mpaka siku ya mechi ilipowadia,wanafunzi wote wa shule ya mbezi inn walikuwa wanatamani masaa yaende ili wajikute tayar wapo kwenye shule ya Loyola,wakati wanafunzi wengine wakiwa wanatamani kwenda kucheza mpira Alex yeye alikuwa na mawazo tofauti kabisa na wanafunzi wenzake.Alex alikuwa anatamani kwenda kumuona msichana Cindelela ambaye alikuwa anampenda kuliko kitu chochote katika moyo wake, msichana aliyetokea kuichanganya akili yake na kuifanya kama zezeta wa mapenzi
"Nakupenda sana Cindelela"Alex alikuwa anajisemea kila alipokuwa anamuwaza Cindelela
Wanafunzi wa mbezi inn waliingia kwenye magari kwaajili ya safari ya kuelekea kwenye shule ya Loyola,safari ilianza huku wanafunzi wakiwa wanashangilia huku wakiimba nyimbo za majigambo kama walizokuwa wanaimba siku ya kwanza,Alex kama kawaida yake yeye alikuwa kimya akimfikiria Cindelela na kama atapata nafasi ya kumuona,mpaka wanafika kwenye shule ya Loyola Alex alikuwa hajitambui sababu alikuwa anapanga maneneo ya kumuambia Cindelela pindi atakapo muona
"Alex wewe haushuki kwenye gari?"Alex alishtuliwa na swali aliloulizwa na rafiki yake
Alipoangalia vizuri akakuta wanafunzi wenzake wote walishashuka kwenye ilo gari na tayari walishakaa kwenye vikundi vikundi wakiimba nyimbo za majigambo,Alex nae alishuka kwenye gari na kuamua kujichanganya na wenzake
"Wit wit umemuona yule kijana aliyefunga magoli matatu kwenye mechi iliyopita?"alisikika mwanafunzi wa shule ya Loyola akimuambia Wit ambae ndiyo rafiki mkubwa wa Cindelela
Kila mwanafunzi wa shule ya Loyola alikuwa anamuangalia Alex alipokuwa anatembea,wapo waliokuwa wanamfuata na kuzungumza nae mambo mawili matatu ili kumdadisi,Alex alipokuwa anapiga story na wale wanafunzi kwa mbali alimuona rafiki yake na Cindelela akiwa amekaa na mwanafunzi mwenzake wakiongea,Kwakuwa Alex alishapata bahati ya kumuona yule dada akiwa na Cindelela katika ile mechi ya kwanza alishatambua fika kwamba yule atakuwa ni rafiki wa Cindelela.Taratibu Alex akaanza kuelekea pale alipokuwepo Wit
"Samahani dada naweza kuongea nawe pembeni?"Alex alimuuliza
"yah tunaweza kuongea"Wit alijibu huku akisimama pale alipokuwepo
Walisogea pembeni na ili wazungumze,Wit alikuwa anamuangalia Alex kuanzia juu mpaka chini ila kwa kuibia ibia,muonekano aliokuwa nao Alex ulikuwa kituko kwenye macho yake lakini alijitahidi kumvumilia sababu Alex alionekana kuwa na kitu kikubwa sana kilichokuwa kwenye moyo wake,Wit aliamua kukunjua moyo wake ili amsikilize Alex alikuwa anataka nini.kwa wanafunzi wenzake walikuwa wanamshangaa Wit kusimama na Alex sababu walikuwa hawaendani hata robo, hata wanafunzi wa shule ya mbezi inn walikuwa wanamshangaa Alex kusimama na msichana mrembo tena kwa kujiamini,Wengi wao walidhani Alex anamtongoza Wit lakini hawakujua nyuma ya pazia kuna nini
"dada kuna mtu namuulizia hapa"Alex alisema
"mtu gani?"Wit aliuliza
"anaitwa Cindelela"Alex alijibu
"Namfahamu sana na ni rafiki yangu mkubwa sana"Wit alisema
"je naweza kumuona?"Alex aliuliza
"kwa leo hajaja shule ila naweza kukupatia mawasiliano yake,kwani wewe unashida nae gani?"Wit alimuuliza Alex huku akimuangalia kwa makini
"Dada nisiposema ukweli nahisi kama nitakuwa nautesa moyo wangu,na ni bora hata nikuambie wewe ili kama ikishindikana kuonana au kuwasiliana na Cindelela unaweza ukanifikishia ujumbe wangu hata kama ukitamka neno moja la kuashiria nampenda,kusema ukweli tangu siku ya kwanza nilipokutana na Cindelela katika shule hii moyo wangu umetokea kumpenda sana na ninavyosema nampenda namaanisha ukweli,sitojali utofauti tuliokuwa nao ila nitajali matakwa ya moyo wangu,endapo siku nikapata nafasi kutoka kwa Cindelela nadhani ulimwengu wote utajua kama kweli nampenda,nipo tayari kufanya lolote ili niwe na Cindelela"Alex al;isema kwa kirefu tena kwa hisia kali sana maneno yaliyomfanya Wit atokwe na chozi la uzuni
"Lakini kaka unahisi kama Cindelela anaweza kukubali?unajua kama Cindelela ni mtoto wa waziri?unajua kama Cindelela amezuiliwa mengi kuhusu wanaume?na je Cindelela ataridhika na hali yako uliyokuwa nayo?"Wit aliuliza maswali kwa mfululizo
"Dada mapenzi hayausiani na hayo yote uliyoliza ial kama moyo wake utaridhia kuwa na mimi sidhani kama kuna kitu kitashindikana"Alex alisema
"kaka nimependa sana ujasiri wako,ujue hata wanaume wa hapa shuleni kwetu wanamuogo[pa sana Cindelela sababu ya uzuri wake pamoja na utajiri wa wazazi wake.Kwa ujasiri uliokuwa nao hata mimi nimetamani sana uwe rafiki yangu"Wit alisema huku akitabasamu
"Naomba unisaidie mawasiliano yake au unipatie namba zako niweze kuwasiliana nae"Alex alisema
"mimi nitakusaidia ila kazi ni ngumu sana"Wit alisema
"kazi ngumu kivipi?"Alex aliuliza
"Cindelela ni msichana wa tofauti sana na huwa hapendi makuu,Cindelela alishawai kushiriki katika mashindano ya umodo katika shule yetu na kufanikiwa kushinda,tangu aliposhinda wanaume walikuwa wanapishana kila mmoja alikuwa anamtongoza lakini Cindelela amewakataa wote na kuhapa kwamba hawezi kuwa na mwanaume sababu wanaume wote ni waongo,ila nisije kukukatisha tamaa unaweza kujaribu bahati yako"Wit alisema na kufanya Alex abubujikwe na jasho
"oya Alex njoo tuingie uwanjani mpira unakaribia kuanza"Mchezaji wa mbezi inn alikuwa anamuita Alex
"naomba unipatie namba zake kabla sijaingia uwanjani"Alex alimuambia Wit
"siwezi kukupa namba zake ila wewe unipe namba zako kisha mimi nitakutafuta,kitu kingine ninachoweza kukusaidia ni kwambaCindelela amejiunga kwenye mtandao wa facebook na anatumia jina la Cindelela Jacobo unaweza kumuomba urafiki,mimi nipoi nyuma yako kwenye kila kitu unachokifanya na jina langu naitwa Witness"Wit alisema
"sawa nashukuru mimi naitwa Alex samahani kwa kutojitambulisha mapema"Alex alisema
Alex alimtajia Wit namba zake kisha akanakili jina analotumia Cindelea kwenye Diary yake,baada ya hapo akaenda kujichanganya na wenzake huku akimuacha Wit akimtazama na kutabasamu
Baada ya dakika kadhaa mechi ilianza huku kila timu ikilishambulia lango la wapinzani wake,mpaka kipindi cha kwanza kinaisha hakuana timu yiliyofanikiwa kupata bao la kuongoza japo kulikuwa na kosa kosa za hapa na pale,Kipindi cha pili kilianza huku kila timu ikiingia kwa morali ya kutaka kupata ushindi,mechi iliendelea kuwa ngumu mpaka ilipofika dakika ya sabini na sita Alex alipoipatia timu yake bao la kuongoza japo alikuwa analindwa sana na mabeki wa timu ya Loyola.Mpaka mechi inaisha mbezi inn walipata ushindi wa goli moja kwa bila na kufanya Alex aibuke kidedea kwa mara ya pili tena
Hakuna mtu aliyeamini kama kuna Mtanzania anaweza kusakata soka kiasi kile,Tofauti na watu walivyokuwa wanafikiria kuhusu Alex kwamba anapenda soka kuliko kitu chchote ila jibu lilikuwa hapana,Alex alikuwa anampenda Cindelela kuliko kitu chochote.
Wanafunzi wa mbezi inn walianza kupanda kwenye magari yao na safari ya kuelekea shuleni ikaanza,Kichwani mwa Alex alikuwa anafikiria jambo moja tu ji jinsi ya kujiuga na katika mtandao wa facebook ili aweze kuwasiliana na Cindelela.Gari lilipofika kimara suka Alex alishuka na kuanza kuelekea barabara ya zamani,Alipofika njia panda ya Gorani kwa mbele akaona kibao kimeandikwa MWANAMUONGA INTERNET CAFE,hapo akili ya Alex ikacheza na wazo la kwenda kufungua mtandao wa facebook
"acha nifungue leo ili nianze kumtafuta"Alex alijisemea huku akielekea kwenye ile internet cafe
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alex aliingia ndani ya internet café na kukuta baadhi ya watu wakiendelea na mambo yao huku wakiwa kimya sana sababu ya ubusy waliokuwa nao,Alex aliamua kwenda kwa muhusika ili nae apate japo computer moja iliyokuwa wazi afanye mambo yake
“samahani mzee unaweza kuniunga na mtandao wa facebook?Alex aliuliza
“je una email address?”Yule mzee nae aliuliza
“hapana sina”Alex alijibu
“sasa inakubidi ufungue email address then ndiyo nikuunge na facebook”Yule mzee alisema
“itanicost shilingi ngapi?”Alex aliuliza
“shilingi elfu moja tu”Yule mzee alisema
“sawa wewe fungua tu”Alex alisema na kukaa kwenye kiti ili mzee alekebishe mambo
Yule mzee alianza kumfungulia Alex email mpaka ilipokamilika kisha akamuunganisha na mtandao wa facebook,Alex alifurahi sana kuona mambo ya kuunganishwa na mtandao wa facebook yameshakamilika,ila Alex alikuwa na jina moja tu lililokuwepo kichwani mwake na si lingine lilikuwa jina la Cindelela
“sasa mzee naomba unitafutie mtu mmoja anaitwa Cindelela Jacobo”Alex alisema huku akitabasamu
Yule mzee akaanza kusearch lile jinaalilotajiwa na Alex kisha wakakaa kusubiri matokeo,Yalitokea majina matatu yaliyofanana na lile jina,lakini Moja kwa moja Alex macho yake yakaona picha ya mtu aliyekuwa anamtafuta.Mapigo ya moyo ya Alex yakaanza kuenda mbio baada ya kuona ile picha ya msichana aliyetokea kumpenda kuliko kitu chochote
“samahani mzee unaweza kumuomba urafiki huyu dada?”Alex aliuliza
“ndiyo naweza ila wewe ulisema unataka kujiunga na mtandao wa facebook tu na siyo vitu vingine,we uoni kama ninawateja wengi wanahitaji huduma?”Yule mzee aliuliza kwa hasira kidogo
“samahani mzee wangu naomba unisaidie katika ilo tu”Alex alisema
“sawa”Yule mzee alisema huku akibonyeza kwenye sehemu iliyoandikwa Add a friends
Baada ya kumaliza ile kazi alimlipa Yule mzee hela yake kisha akatoka nje ili arudi nyumbani kwao,Alex mpaka anaenda kupanda gari la kuelekea nyumbani kwao maeneo ya kimara gorani kichwani bado alikuwa na mawazo kwa msichana Cindelela.Alex alijipa matumaini kidogo sababu alikuwa na njia angalau ndogo ya kuwasiliana na Cindelela endapo akikubali kuwa rafiki yake kwenye facebook
“Hivi kwanini nimetokea kumpenda ghafla huyu msichana?hivi kuna mtu alishawahi kupenda kama ninavyopenda mimi?”Aex alijiuliza maswali bila kupata jibu
Watu waliokuwa kwenye gari walikuwa wana mshangaa sana Alex alivyokuwa anajichekesha mwenyewe mfano wa mtu anayeumwa ugonjwa wa akili.Alex alifika nyumbani kwao na kula chakula cha usiki kisha akaingia chumbani kwao ili kulala
Asubuhi na mapema Alex aliamka na kuanza kufua nguo zake ili baadae apate muda wa kupumzika sababu ilikuwa siku ya jumamosi,baada ya kumaliza kufua nguo zake alipata kifungua kinywa kisha akachukua daftari lake ili apate kujikumbusha mambo yote waliyosoma wiki hiyo
Alijitahidi sana kusoma lakini mambo yalikuwa hayaingii kichwani sababu muda wote mawazo yake yalikuwa kwa Cindelela ,mpaka inafika jioni Alex alikuwa hajatafutwa kwenye simu na Witness kitu kilichompa wasiwasi huenda ombi lake la kuomba namba ya Cindelela litakuwa limekataliwa
“Yule dada atauwa amenidanganya nini?”Alex alijiuliza bila kupata jibu
Hadi Alex anaingia kulala hakuna simu yoyote iliyoingia kuoka kwa Witness ambaye alimuhaidi kwamba atamsaidia kufanikisha ili kumpata Cindelela.
Asubuhi ya jumapili ilipofika nako mambo yalikuwa yaleyale hakuna namba mpya iliyoingia kwenye simu yake wala message kutoka kwa Witness,alikaa sehemu na rafiki zake huku akihesabu masaa yanavyokwenda na muda huo ulikuwa ni mchana
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
Upande wa Cindelela hakuwa na wazo lolote kuhusu mtu anayeitwa mwanaume,yeye aliendelea na shughuli zake nyingine kama ilivyokuwa kawaida yake.Lakini kuna siku wakati anatoka kuoga alikuta missed call tatu kwenye simu yake,Alipoangalia nani aliyepiga alikuta ni rafiki yake kipenzi Witness.Cindelela aliamua kumpigia Wit ili ajue alikuwa na shida gani
“Hallo”Witness alisema baada ya kupokea simu
“niambie best mzima wewe?”Cindelela aliuliza
“mimi mzima nimekumiss mumy”Wit alijibu
“nimekumiss pia kipenzi changu aya niambie mumy”Cindelela alisema
“Best kuna kitu nataka nikuambie”
Niambie tu best ni kitu gani?Cindelela aliuliza
“unamfahamu kaka mmoja anaitwa Alex?”Wit aliuliza
“Alex yupi?”
“Yule kaka anayesoma shule ya mbezi inn waliokuja kucheza mechi na sisi”Wit alisema
“sidhani kama namfahamu”Cindelela alisema
“ni Yule kaka uliyekuwa unaongea nae siku ya mechi pale shuleni”Wit alisema
“okey nimemkumbuka,vipi amefanyaje?”Cindelela aliuliza
“ameniomba namba zako”
“namba zangu za nini?”Cindelela aliuliza
“ameniambia anashida na wewe”Wit alisema
“hapana usimpe sababu sijui ana nia gani na mimi”Cindelela alisema
“sidhani kama ana nia mbaya na wewe sababu anaonekana mstarabu saba wala hana shida kaka wa watu”Wit alisifia
“ngoja nifikirie kwanza sababu siwezi kukurupuka”Cindelela alisema
“sawa best ila kuna ishu nyingine nataka jumapili unisindikize mlimani city kuna vitu vya nyumbani naenda kununua”Wit alisema
“usijali best nitakusindikiza wala usijali”Cindelela alisema
…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
Alex wakati anaendelea kupiga story na rafiki zake alishangaa simu yake ikiwa inaita na namba iliyokuwa inapiga ilikuwa namba mpya,akili ilikuwa inawaza labda atakuwa ni Wit ndiyo anapiga,alitoka pembeni na kupokea ile simu
“Hallo”Alex alisema baada ya kupokea simu
“hallo Alex mzima wewe?”ilikuwa ni sauti nyororo sana ikimuuliza Alex
“me mzima nani mwenzangu?”alex aliuliza
“mimi Witness”Wit alijibu
“Jamani kumbe Wit niambie”Alex alisema
“sikia Alex leo nitakuwa na Cindelela maeneo ya mlimani city kama unaweza nakuomba uje uongee nae”Wit alisema
“nitajitahidi”Alex alisema huku akionyesha wasiwasi
“sawa Wit nitakuja”Alex alisema
“sawa ila usichelelwe”Wit alisema na kukata simu
Alex alipomaliza kuongea na simu alikaa pembeni na kuanza kujiuliza maswali kama aende au la,wenzake waliendelea kumkodolea macho Alex sababu alionekana kama amepagawa
“Hapana nafasi ya kuzungumza na Cindelela ndiyo hii sidhani kama nitapata tena nafasi kama hii,lakini wakitaka niwanunulie vitu mimi hela natoa wapi?”Alex alijiuliza mwenyewe bila kupata jibu kamili
Taratibu alishika njia ya kwenda nyumbani kwao ili kujiandaa kwaajili ya kwenda kukutana na Cindelela,Alipofika nyumbani akachagua nguo ambazo zingemfaa kwenda kukutana na yule msichana aliyetokea kumpenda,kila nguo aliyokuwa anachagua aliona kama haimpendezi kutokana nyingi zilikuwa zimechakaa na hazifai kwa mtoko wa kwenda kukutana na motto mzuri kama Cindelela
“bwana liwalo na liwe navaa nguo yoyote”Alex alijisemea huku akielekea bafuni kuoga
Alipomaliza kuoga alirudi chumbani kwake fasta fasta na kuanza kujiandaa ili atoke,alivaa nguo na kujiangalia kama yupo vizuri.Aliporidhika alitoka na kuanza safari ya kuelekea stand ili apate usafiri wa kumpeleka suka,bahati ilikuwa upande wake sababu alipofika barabarani akakuta gari nalo ndiyo linataka kuondoka,Alidandia na safari ya kuelekea kimara suka ikaanza
Alipofika suka alishuka na kupanda daladala ya kuelekea mwenge,Alex alitamani gari lipae sababu aliona kama anachelelwa kwenda kukutana na Cindelela.Japo ilikuwa ni siku ya jumapili lakini walipofika ubungo wakakuta foleni kubwa iliyosababishwa na roli lililopasuka tairi,Alex hakutka kujiuliza mara mbili alishuka kwenye gari na kukimbia mpaka ubungo darajani kasha akapanda gari jingine
“Alex ukifika hapa jifanye kama sijakuhita”Message iliingia kwenye simu yake kutoka kwa Wit
“sawa wala usijali kwani nyie mmeshafika?”Alex aliuliza
“ndiyo tumefika na tupo hapa shoplite(kwa sasa ni Nakumat)”Wit alijibu kwa sms
“nakuja”alex alijibu
Ilichukua dakika chache Alex akawa ameshafika mlimani city na kushuka kwenye gari,aliingia ndani ya jingo la mlimani city na kuanza kushangaa shangaa pale ndani.Alinyanyua simu yake na kumpigia Wit ili ajue yupo wapi kwa sasa
“Wit nipo hapa nje”Alex alisema baada ya Wit kupokea simu yake
“Tusubiri tunakuja muda siyo mrefu”Wit alisema
Alex alikaa kwenye kiti akiwasubiri watoke huku moyoni akiwa na hofu ya kuongea na Cindelela,Alex alijitahidi kupanga maneno ya kuongea na Cindelela ili asije akaboronga pindi atakapopata nafasi.Maneno yalikuwa hayapangiki na kujikuta hofu ikiendelea lumtanda sababu alikuwa anajua nni kitakachokuja mbele yake endapo atakapoongea pumba
Macho ya Alex yalishtuka baada ya kumuona Cindelela akiwa ameongoza na na Wit wakitoka katika jengo la Shoplite.Mapigo ya moyo yalianza kumuenda mbio huku akionekana wazi kutetemeka baada ya kumuona msichana mrembo na aliyekuwa anampenda kwa dhati akiwa anakuja mbele yake.Alex alijikuta tumbo linamuuma ghafla huku kijasho chembamba kikimtoka kwa hofu
“mambo Alex”Wit alimsalimia
“poa”Alex aliitika huku jasho likiwa linamkauka japo kulikuwa na Ac ya kutosha
“mambo kaka”Cindelela nae alimsalimia
Ile sauti ilimfanya Alex awe kama ameshanganyikiwa sababu hakujua ajibuje ile salamu,Alex alitamani kujibu marahaba,salama,sijambo au poa lakini mdomo ulikuwa mzito sana kwenye kuongea,Alijitahidi kumkazia macho na kuamua kujibu salamu ya Yule binti mrembo
“poa Cindelela mzima wewe?”Alex alijibu na kuuliza swali
“kweli unakumbukumbu hadi leo jina langu lipo kichwani mwako” Cindelela alisema
“Alex naomba tutafute sehemu tukae”Wit aliongea na kuanza kutoka nje
Alex na Cindelela wakaanza kumfuata nyuma mpaka alipoenda kukaa kwenye mgahawa mmoja uliokuwepo pale nje.Mhudumu alipofika Cindelela na Wit waliagiza chakula na vinywaji huku Alex akisema yeye ajisikii kula kitu chochote.Alex alikuwa anaogopa jumba bovu sababu hakuwa na hela yoyote zaidi ya hela ya nauli
“Alex wala usiogope mimi nitalipa kila kitu”message iliingia kwenye simu ya Alex ikiwa imetoka kwa Wit
Alex alipumua kidogo huku akimtazama Wit aliyekuwa mbele yake,Wit alimpa ishara Alex ya kutokuhofia kitu chochote sababu yeye yupo kwaajili yake.Kwa ujasiri Alex aliagiza juisi peke yake na kuanza kunywa huku wakipiga storyCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“sorry jamani naingia toilet”Wit alisema huku akisimamapale kwenye kiti
Wit alitoka pale na kukunja kona mbili tatu kasha akaenda sehemu na kukaa chini,Alichukua simu yake na kuanza kuandika Message kwa Alex
“Alex hiyo ndiyo nafasi niliyokupa ili useme maneno yako yote sababu ukiikosa leo nadhani utaipata mwakani”Wit alituma hiyo message
Alex alipokea hiyo message na kuanza kuisoma huku akitabasamu sababu alikuwa anaitaka hiyo nafasi kwa muda mrefu.Alex alitawaliwa na hofu kila alipokuwa anamuangalia Cindelela ambaye alionekana busy akila chakula.Cindelela alipokuaja kuinua macho alikutana na Alex akimtazama kama kuna kitu anataka kusema
“mh tatizo nini?”Cindelela aliuliza
“hakuna tatizo”Alex alijibu
“mbona unaniangalia sana mpaka umesahau kunywa hata hiyo juisi?”Cindelela aliuliza
“Cindelela laiti ungejua kitu kinachoniumiza moyo sidhani kama ungeendelea kuuliza swali hilo”Alex alisema kwa utulivu mkubwa
“kitu gani kinachokuumiza moyo?”Cindelela aliuliza huku akiwa amemkazia macho Alex
“Cindelela”Alex aliita
“beee”Cindelela alihitika huku akionekana kumuonea Alex aibu
“Nalazimika nikuambie ukweli japo ni mara ya pili tumeonana”Alex alisema
“niambie tu ukweli gani?”Cindelela aliuliza huku akiwa makini kusikiliza Alex anataka kusema nini
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment