Simulizi : Nakupenda Cindelela
Sehemu Ya Tano (5)
ILIPOISHIA
Wale magaidi wakaanza kuiongoza ndege kuelekea pasipojulikana,ndege ilichukua masaa mengi sana angani na taratibu wale magaidi wakaanza kuishusha ile ndege kwenye uwanja mkubwa na kwa mbali kulikuwa na miti mikubwa sana .miti ilikuwa imezunguka pande zote na kuonyesha kwamba ule msitu ulikuwa mkubwa sana
Wale magaidi waliwachukua Alex na Cindelela kisha wakawaingiza kwenye gari kwaajili ya kuwapeleka kwenye huo msitu,Ile ndege ili washwa tena na kuamrishwa ikaterekezwe mahali popote kwasababu haikutakiwa kuendelea kukaa pale
“nendeni mkaitelekeze baharini sababu najua watatusumbua”Vijana waliamrishwa na kuanza kutekeleza amri
“sawa mkuu”waliitikia kwa heshima na ukakamavu
Said na baadhi ya vijana wengine wakaingia kwenye gari na kuanza kuelekea kwenye huo msitu ili wakafanye walichokusudia kufanya.Walikimbiza gari kwa speed zote huku wakipongezana kwa ushindi walioupata sababu walihaidiawa pesa nzuri pindi watakapomaliza ile kazi ya kumuua Alex
“huyu jamaa inabidi tumuue akiwa yupo kwenye fahamu zake”saidi alisema
“kweli ili apatwe na uchungu ambao sisi tutaufurahia”alichangia mwingine
Walicheka huku wakigongeana mikono kwa ishara ya kufurahi na kupongezana,dereva aliendelea kuongeza speed huku akiwa makini sana katika kukwepa mabonde madogo madogo sababu huo msitu ulikuwa na mashimo mashimo katika barabara zake
Kwa kuangalia na macho tu ule msitu ulionekana unatisha sana sababu ulionekana kuwa na wanyama wakali sana.Haikujulikana huo ulikuwa ni msitu gani au ulikuwa upo katika nchi gani.Mtu pekee aliyekuwa anaujua huo msitu alikuwa ni Saidi na vijana wake sababu walionekana kuuzioea kwani walikuwa wanafuata njia kwa umakini
Cindelela alianza kufumbua macho yake taratibu sababu yalionekana kuwa mazito sana.Alianza kufumbua jicho la kushoto na kupepesa pepesa ndani ya lile gari walilolipanda.Aliogopa sana ule mwendo wa gari sababu ulikuwa wa kutisha sana.Cindelela aliamua kuangalia kushoto yake na kumuona kipenzi cha roho yake akiwa hajitambui hata kidogo
“Alex”Cindelela alihita kwa shida na hakupata jibu lolote kutoka kwa Alex kwani alionekana kuwa kimya sanaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Alex mpenzi wangu umekufa?na kama umekufa mimi utaniacha na nani Alex?na kwanini haujaniambia kwamba unakufa?Alex wewe ndiyo umenionyesha jinsi ya kupenda,wewe ndiyo umenifungua ubongo wangu wa kutomdharau mtu,kwanini unaniacha peke yangu Alex?naukuomba uamke mpenzi wangu nipo tayari tufe wote lakini siyo kukuacha uende peke yako”Cindelela alikuwa anazungumza maneno hayo huku akimtingisha Alex kwa nguvu japo alikuwa amechoka
Cindelela machozi yalimlowanisha uso wake kwani alikuwa analia kwa uchungu na kutamka maneno ambayo Alex angeyasikia angeamka na kama angekuwa amekufa basi angefufuka katika wafu ili aje kumkumbatia Cindelela wake na kumtoa kwenye yale majonzi mazito.Cindelela alilia japo sauti ilikuwa haitoki sababu ilikuwa tayari imeshakauka
Alex alikuwa asikii neno lolote kutoka kwa Cindelela kwani alikuwa kwenye usingizi mzito sana.Alex alikuwa hatambui lolote linaloendela hapo kwani alikuwa hatikisiki wala kufumbua macho yake japo mapigo yake ya moyo yalikuwa yanadunda poleple sana kuashiria kwamba bado yupo hai
Cindelela alimlaza Alex kwenye mapaja yake huku akimuangalia kwa macho ya huruma sana sababu hakujua kama Alex wake ataamka tena.Wakati Cindelela anawaza kuhusu Alex,Saidi na vijana wake walikuwa wanawaza pesa watakayoipata pindi watakapokamilisha kazi ile.Dereva alizindisha mwendo na kukata kona mbili tatu huku akiendelea kuingia ndani ya msitu
“bosi tumefanikiwa kumpata yule kijana”Saidi alisikika akiongea na simu
“safi sana vijana wangu,vipi na huyo mtoto wangu mpo nae?”mzee Jacobo aliuliza
“ndiyo tupo nae”Saidi alisema
“safi sana ila nataka mwanagu awe salama tu msije mkamfanya kitu chochote na kama ikiwezeka kijana mmoja anatakiwa aje nae huku arafu muendelee na shughuli yenu”alisema mzee Jacobo
“sawa mkuu”aliitikia Saidi samo hong chota na kukata simu
Alex taratibu alianza kurudisha fahamu yake na kufumbua macho yake.Aliangaza huku na kule na kumuona Cindelela akiwa amelala.Alinyanyua mkono wake na kumshika Cindelela kwenye mashavu yake,Cindelela alipoona ameguswa alishtuka na kufurahi sana kumuona Ale xyupo macho
“Nakupenda Alex”ilo ndiyo neno la kwanza kutamka
“Nakupenda Cindelela na sitokufa mpaka nikuvishe pete ya ndoa”Alex alisema na kumfanya Cindelela machozi yamtoke huku akilia kwa kwikwi
Alex nguvu zake zilianza kumrudia na kurudi katika hali yake ya kawaida japo kichwa alikuwa anakisikia kizito sana.Alipiga magoti na kuanza kumuomba mungu ili amnusuru yeye na mpenzi wake kwenye lile balaa lililokuwepo mbele yao.Cindelela nae alipipiga magoti ili kuungana na Alex katika maombi yale ya kumuomba mungu awanusuru na majanga yote yakliyopo mbele yao
Wakati Cindelela na Alex wakiendelela kumuomba mungu ili awaepushe kwenye janga lile,Saidi na vijana wake walikuwa wanashangilia ulaji wanaoenda kuupata baada ya kukamilisha kazi yao.Dereva nae alizidisha mwendo wa kuingia katikati yam situ kwani huo msitu ulikuwa ni mkubwa sana
Gari lilianza kuyumba yumba na kusikika mlio mkubwa wa tairi la mbele kupasuka.Kila mtu ndani ya lile gari alishtuka baada ya kusikia ule mlio wa tairi kupasuka.Gari liliseleleka na kudondoka pembeni ya barabara na kusikika milio ya watu ikiguna tu
Cindelela na Alex walikuwa wa kwanza kutoka huku wakionekana kuyumba yumba sababu ya kizungu zungu.Mungu aliwaepusha kwani hawakuwa na jeraha lolote katika miili yao japo lile gari lilipata ajali.Waliamua kukaa pembeni ya lile gari ili kuvuta pumzi na waanze safari ya kutoka ndani ya ule msitu
Walipoona kwamba vichwa vimetulia wakaanza kutembea kwa uvivu na kujikongoja.Hawakujua wanaelekea wapi kwani walikuwa hawajui njia yoyote ya kwenye ule msitu.Walizidi kutokomea huku wakimuomba mungu awaonyeshe njia ili watoke kwenye ule msitu mkubwa uliokuwa unatisha kupita mmaelezo
Walijitahidi sana kujikongoja mpaka ikafika kipindi njaa ikawa inawauma sana sababu walitembea kwa muda mrefu bila kupata chochote tumboni,Cindelela alionekana kuchoka zaidi sababu hakuwai kupitia hayo mazingira ya tabu.Alex alikuwa anamuonea huruma mpenzi wake kwani hakupenda ateseke wakati yeye yupo
“Cindelela mpenzi wangu naomba unisubiri hapa nikatafute chakula nikuletee”Alex alisema huku akimbusu Cindelela kwenye paji la uso
“Alex kwanini tusiende wote mpenzi wangu”Cindelela alisema
“Nakuonea huruma sana kwani najua haujazoea hizi shida naomba unisubiri nakuja muda siyo mrefu”Alex alisema
“sawa Alex ila nakuomba usichelewe”Cindelela alisema na kukaa chini ya mti huku hofu ikiwa imemtanda
Alex alimuacha Cindelela na akashika njia ya kuingia kwenye msitu ili kutafuta matunda au mnyama yeyote ambae anaweza akampata kwa urahisi.Alex alizunguka sana bila kufanikiwa mpaka akajikuta anakata tama
“ngoja nijaribu tena kutafuta sababu naweza nikampoteza kipenzi cha Roho yangu”Alex alisema huku akiendelea kuzunguka
Kwa mbali aliona miti mingi ikiwa imebeba matunda yaliyoonekana kuiva sana.Alex alisogea mpaka pale na kuanza kuchuma yale matunda baada ya kuyagundua kwamba ni maembe.Alex alichuma kwa wingi sana kiasi kwamba mpaka kubeba ilikuwa shida sana
Alipoona yanatosha alianza safari ya kurudi ili akampelekee mpenzi wake,moyoni alikuwa na furaha sana kufanya kitendo ambacho kitamfurahisha mpenzi wake wa kweli.Alex alipepesa macho baada ya kukaribia ule mti aliomuacha Cindelela.Alianza kutetemeka sababu Cindelela hakuwepo maeneo yale.Aliweka yale matunda chini na kuanza kuzunguka ili kumuangalia Cindelela
Mapigo ya moyo wake yalikuwa yanamuenda mbio mfano wa mtu alityetoka kukimbizwa muda mchache uliopita.Alex wakati anaendelea kumtafuta Cindelela alijikuta anashikwa begani na mtu ambaye alikuwa kwa nyuma yake.Alex alikuwa anageuka huku akitetemeka kwa hofu kubwa akidhani wale magaidi wamerudi tenaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alipogeuka nyuma akakutana na Sura nzuri sana ya msichana mrembo Cindelela ikimuangalia kwa macho ya kupendeza.Alex aliachia tabasamu zuri kasha akamkumbatia Cindelela na kumbusu shavuni
“mpenzi ulinitisha sana sababu nilijua umeshachukuliwa na wale magaidi au umeliwa na wanyama wakali”Alex alisema
“hapana mpezni wangu nami nilienda kukusaidia kutafuta chakula”Cindelela alisema
“aya umeniletea chakula gani?”Alex aliuliza
“Sijakuletea chakula ila nimefanikiwa kupata maji ya kunywa”Cindelela alisema
“asante na umewezaje kuyapata hayo maji?”Alex aliuliza
“me nimezunguka nikaona mto nikachota”Cindelela akasema
“nashukuru mpenzi wangu”Alex alisema na kumkumbatia kwa nguvu
Walirudi mpaka pale walipoacha maembe na kuanza kula taratibu huku wakifarijiana kwamba watatoka wote na kwenda kufunga ndoa.Walipoamaliza kupumzika wakaanza safari upya ya kutoka nje ya ule msitu ili watafute sehemu ya wazi ambayo wanaweza wakapata msaada
Walitembea kufuata mto kwani walijua huo mto utakuwa unafika mahali furani na kutakuwa na kijiji chochote karibu na huo mto.Walitembea kwa muda mrefu sana ikafika kipindi kila mtu alikuwa amechoka sana sababu walifika mabalia sana.Walifika sehemu moja ambapo kulikuwa na maporomoko ya maji
Maji yalikuwa yanadondoka kwa wingi sana sehemu hiyo na kufanya kuwe na sauti kali ya mngurumo wa maji.Cindelela na Alex waliipenda sana ile sehemu wakaamua kusimama ili kuangalia ile madhari japo walikuwa kwenye majanga mazito
“Alex hii sehemu ni nzuri sana”Cindelela alisema
“kweli mpenzi wangu hata mimi nimeipenda sna hiii sehemu”Alex alisema huku akionyesha hali ya wasi wasi sababu kitu kama hicho alishawai kukiota kwamba yupo kwenye maporomoko ya maji
“Alex nakupenda sana na sipo tayari uteseke wakati mimi nipo”Cindelela alisema huku akimsogelea Alex aliyeonyesha kuwa na wasiwasi
“Nakupenda pia Cindelela na wewe ndiyo mwanamke wa maisha yangu,naapa kwa mungu kwamba sitoweza kukuacha mpaka kufa kwangu”Alex alisema huku akitanua mikono ili ampokee Cindelela
Ghafla Alex alishangaa akisukumwa na mtu aisiyejulikana ametokea wapi.Alex alijikuta akidondoka chini na kuelekea kule maji yanapodondokea.Cindelela alishtuka sana kuona mpenzi wake amesukumwa na mtu ambaye akujua ametokea wapi.Aligeuza macho yake nyuma na hana kwa hana akakutana na mtu aliyeonyesha kukasirika sana
Cindelela aliogopa sana kuiona ile sura wakati alizani kwamba tayari yule mtu ameshakufa.Said samo hong chota alizidi kumkazia macho Cindelela kama anataka kummeza.Cindelela aligeuka kule alipodondokea Alex na kutaka kujitupa ili amfuate Alex lakini Saidi alimuwahi na kumshika mkono kwa nguvu kabla hata ajaruka
“Naomba uniache nimfuate mpenzi wangu”Cindelela alisema kwa uchungu huku akitaka kujinasua kwenye mikono ya Saidi
“yule siyo mpenzi wako,mpenzi wako yupo tayari na anasubiri kukuoa tu”Saidi alisema kwa nyodo
“huyo mwanaume unayemtaja mimi simjui kwani namjua Alex tu na nipo tayari kufa kwaajili yake”Cindela alisema huku machozi yakimtoka
Saidi alimbeba Cindelela na kuanza kuondoka nae kuelekea kule walipotokea.Saidi alikuwa na vijana wake wanne ambao nao walinusurika kwenye ile ajali ya gari kwani wawili walienda kuitupa ile ndege na watatu alibaki nao yeye,kati ya hao watatu mmoja ndiyo alikufa kwenye ile ajali,na wengine walibaki hai japo walionekana kuchubuka katika miili yao.Walimbeba Cindelela kwa pamoja na kuelekea kule gari lao lilipodondoka
“Inatakiwa huyu dada apelekwe nyumbani kwao ili akaonane na baba yake,kazi watafanya watu wawili arafu sisi tunaobaki tunatakiwa tukahakikishe kwamab yule kijana amekufa au la ”Alisema Saidi na kugawa majukumu kwa vijana wake
Wawili walipanda kwenye gari lingingine ambalo walikuja nalo wale vijana walioenda kuitupa ile ndege,safari ya kuelekea kwenyen kile kiwanja cha ndege ikaanza huku wakimuacha Saidi na vijana wengine wawili wakipanga mipango ya kwenda kumtafuta Alex
“Bosi inatakiwa tuufuate mto mpaka mwisho kama atakuwa amekufa tutaona mwili wake”alisema kijana mmoja
“sawa vijana wangu ngoja tuanze kazi”alismea Saidi na kuanza kuelekea kwenye yale maporomoko ili wauone mto na kuufuata
………………………………………………………………………………………………………………………….
Alex alipodondoka kwenye yale maporomoko moja kwa moja alitumbukia kwenye maji ambayo yalikuwa na kina kirefu sana.Kwakuwa ile sehemu ilikuwa ndefu sana Alex hakuweza kujigonga kwenye mwamba ila alizama mpaka chini.Alex alianza kuogelea kupanda juu ili apate pumzi hata kidogo
Alijitahidi mpaka akafika juu ya maji na kuanza kuogelea japo maji yalikuwa yanamshinda nguvu sababu yale maji yalikuwa yanaenda kwa kasi sana.Alex alikunywa maji mengi sana na kujikuta nguvu zikimuishia kabisa kwani alishachoka kuogelea na ule mto ulikuwa mkubwa sana
Alex aliona gogo likiwa linaelea huku likimpita karibu yake,Alinyoosha mkono na kulishika huku akivuta nguvu zake apate kulikumbatia.Alifanikiwa kulikumbatia na kukaa juu yake huku akiwa amelishikilia kwa nguvu zake zote.Gogo liliendelea kuelea huku likiwa limembeba Alex juu yake
Ilifika sehemu kasi ya maji ikaanza kupungua na kufanya lile gogo liwe linaelea kuelekea nje ya mto.Taratibu gogo likafika mpaka nchi kavu lakini Alex alikuwa hajitambui kabisa.Alex alikuwa hana fahamu yoyote kwa muda huo kwahiyo aliendelea kukaa juu ya ilo gogo bila kujua kwamba tayari alishafika nchi kavu
Muda ulivyozidi kwenda na jua nalo lilizidi kuongezeka na kumfanya Alex aanze kupata fahamu zake taratibu.Alipokuja kuzinduka alijikuta bado yupo juu ya lile gogo lakini alikuwa yupo pembezoni mwa maji.Alijibuliza na kujitupa kwenye udongo huku akijitahidi kutambaa kama nyoka kuelekea kwenye kichaka kimoja cha karibu apate kupumzika kwani bado alikuwa amechoka sana.Alitambaa kwa shida mpaka akakifikia kile kichaka na kuingia ndani yake
Kitendo cha Alex kuingia kwenye kile kichaka Saidi na vijana wake nao ndiyo walikuwa wanaingia kwenye maeneo yale huku wakiangaza macho yao kwenye ule mto.Walipofika pale karibu na Alex kijana mmoja alisita na kufanya Saidi na kijana mwingine wamuangalie kwa macho ya udadisi
“Subirini kwanza”Yule kijana alisema huku akiangalia chini baada ya kuona alama
“kuna nini?”Saidi aliuliza
“kuna kitu nimekiona”alisema yule kijana
“umeona nini?”Saidi aliuliza
“hauoni hizi alama kama kuna kiumbe kilikuwa kinatambaa?”aliuliza yule kijana
“kweli inaonekana kuna kiumbe kilikuwa kinatambaa na isije kuwa ni yule kijana amejificha kwenye hii sehemu”Alisema Saidi huku wenzake wakimsupport kwa kutikisa vichwa
“twende tukaangalie kama yupo hapo”alisema yule kijana na kuanza kuvuta hatua kuelekea kwenye kile kichaka alichojificha AlexCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Yule kijana alionekana kutembea kwa kasi huku akiwaacha wenzake nyuma kwani alitaka kuonekana shujaa mbele ya bosi wake,Alizifuata alama alizopita Alex na kuanza kuingia ndani ya kile kichaka.Saidi na kijana mwingine walikuwa kwa mbali wakimfuata mwenzao kwenye kile kichaka
Katika tukio la kushangaza aliibuka nyoka mkubwa sana na kumviringita yule kijana kwa kasi ya ajabu.Yule kijana alipiga kelele ambazo ziliwashtua wenzake na kuanza kukimbia kule alipoelekea yeye.Walimuona ndugu yao akiwa ameviringishwa na nyoka mkubwa huku akipanua mdomo kwa ishara ya kutaka kummeza
“Jamani nisaidieni nakufa”Yule kijana alikuwa anaomba msaada huku sauti za mifupa kuvunjika zikisikika
Saidi alitoa bastora yake aliyokuwa nayo mfukoni na kumpiga risasi yule nyoka,Yule nyoka alijikunjua na kuanza kutapatapa kisha akanyamaza kimya kwani alikuwa tayari ameshakufa.Walimsogelea mwenzao na kumkuta bado anaendelea kupumua kwa shida.Saidi alinyoosha bunduki yake na kumpiga risasi kichwani
“sasa mbona umemuua?”aliuliza kijana mwingine aliyekuwa nae Saidi
“sidhani kama anafaida yoyote sababu tayari ameshapoteza nguvu na hatutoweza kufanya kazi mbili kwa muda mmoja”alisema Saidi
“kazi mbili kivipi?”aliuliza yule kijana
“hatuwezi kumtafuta mtu kwenye huu msitu wakati tumebeba mgonjwa”Alisema saidi na kusimama juu
“kwahiyo tunafanyaje?”aliuliza yule kijana
“hapa inabidi tuufuate mto kwani yule kijana hawezi kuingia kwenye haya mapori sababu hana nguvu za kutembea,zile alama tulizokuwa tunaziona ni za huyu nyoka tuliyemuua”Alisema Saidi na kuanza kutembea kuelekea ule mto huku mwenzake akimfuata
Alex alipumua kwa nguvu kwani alikuwa kwenye kichaka cha jirani tofauti na kile alichotoka nyoka.Alimshukuru mungu kwa mambo mawili.Kwanza ni kutokuingia kwenye kile kichaka alichokuwa yule nyoka mkubwa,pili ni wale jamaa kuondoka maeneo yale bila kujua kwamba Alex yupo pale
Alex alikusanya nguvu upya na kuanza kutembea ili aone kama anaweza kutoka ndani ya ule msitu.Taratibu alianza kutembea kuelekea kusikojulikana huku akimuomba mungu amuongoze kwenye safari yake hiyo iliyojaa kiza sababu alikuwa hajui aanzie wapi na aishie wapi.Alex alitembea kwa muda mrefu sana huku kichwani kwake akilaumu na kuhisi Cindelela ndiyo chanzo cha yeye kufika katika hali ile
“Cindelela kwanini umenifanyia hivi? na ni nani huyo anaetaka nisikupende?Cindelela nitakupenda daima hata kama nitapita kwenye vikwazo gani ila tambua kwamba nakupenda sababu mapenzi tumeumbiwa sisi binadamu na wewe ndiyo chaguo la moyo wangu”Alex alisikika akisema huku akijikongoja kwa kutembea
Alitembea mpaka alipouona mti mkubwa na kuamua apumzike kwani njaa ilikuwa inamuuma sana kiasi kwamba mpaka kizungu zungu kilikuwa kinampata.Alikaa chini ya ule mti huku akiwaangalia ndege waliokuwa wanaimba kwa furaha.Alex alikuwa anatamani sana siku moja awe yeye na Cindelela wakiimba kwa furaha katika maisha yao ya ndoa lakini mambo yalishaonekana kwamba ni magumu sababu hakutegemea kutoka ndani ya huo msitu
Usingizi nao ulimpitia na kuja kushtuka muda ulikuwa umeenda sana
“Nakupenda sana Cindelela na sijawahi kupenda msichana kama ninavyokupenda wewe katika maisha yangu,Cindelela wewe ndiyo chaguo la moyo wangu .Akili yangu yangu,filkra zangu pamoja na nafsi yangu zote zipo kwaajili ya upendo wako,Cindelela naomba unipe japo nafasi katika moyo wako ili nipate japo Faraja ndani ya nafsi yangu,bila ya wewe kunipa nafasi sidhani kama kuna umuhimu wa mimi kuishi kwenye hii dunia wakati nakosa kitu nikipendacho”
“Cndelela mapenzi tumeumbiwa sisi binadamu wala hayajaumbiwa miti au mawe na ninavyosema nakupenda namaanisha kweli nakupenda kutoka ndani ya moyo wangu.Cindelela nimejitolea kwaajili yako na kila nitakalolifanya itakuwa kwaajili yako,Cindelela nakuomba unielewe ewe kipenzi cha roho yangu NIPO TAYARI KUFA KWAAJILI YAKO”……………………………………………………………………………………………………………….
Hiyo yote ilikuwa ni kumbukumbu ya Alex tangu siku ya kwanza kukutana na Cindelela mpaka alipofika ndani ya ilo pori.Alex machozi yalikuwa yanamtoka baada ya kumaliza kuvuta kumbukumbu ya matukio yote .Hakutaka kuamini kwamba Cindelela wake ndiyo anamkosa kilahisi namna ile
Akiwa juu ya mti alijaribu kuvuta usingizi ili aweze kulala kwani bado alikuwa na safari ndefu sana kesho yake ya kutoka ndani ya ule msitu mkubwa.Usingizi nao ulimpitia na kujikuta akilala kama mzoga.Usiku alishtuka sana baada ya kusikia sauti za wanyama wakali wakilia chini ya huo mti.Alijaribu kuwaangalia wale wanyama lakini hakufanikiwa kuwajua ni wanyama gani
Alex alisali na kujikabidhi mikononi mwa mungu ili amuepushe na mabalaa yote yatakayotokea katika ule msitu.Wale wanyama walitoka kwenye ule mti na kuelekea upande mwingine.Alex alipumua na kuendelea kulala huku akiwaza kesho aelekee upande gani
Asubuhi na mapema Alex alianza safari ya kutoka ndani ya ule msitu huku akitafuta sehemu yoyote ambayo inaweza kuwa inamakazi ya watu akapate msaada wowote
……………………………………………………………………………………………………………………..
Taarifa ya kupotea kwa ndege aliyoipanda Alex ilisambaa kwa kasi sana kwenye nchi ya Uingereza huku uongozi wa timu ukiwa umekosa amani kwani hawakujua kama Alex bado anaweza kuwa hai au la.Vikosi vingi vya usaklama vilitumwa katika bahari iliyosadikika kwamba hiyo ndege imedondokea ili kuokoa watu waliokuwemo mule
Baadhi ya viongozi wa timu walisafiri na vyombo hivyo ili kujua kama kijana wao nae yupo katika ndege hiyo au la,Wazamiaji walizamia katika hiyo bahari na kuanza kutoa maiti zilizokuwepo kwenye ile ndege kisha wakawa wanaziweka katika vyombo vingine arafu wanapeleka juu
Maiti zote zilikaguliwa lakini maiti ya Alex na Cindelela hazikuonekana,Pia hakukuwa na maiti za vijana wengine sita.Kila mtu alikuwa anajiuliza hao wengine watakuwa wameenda wapi sababu maiti zao zilikuwa hazionekani pale.Hakuna aliyekuwa anajua lolote kwamba hao vijana waliopotea walikuwa ni magaidi na ndiyo waliowateka Cindelela na Alex
Taarifa hizo zilifika sehemu nyingi sana kwani zilikuwa zinasambaa kwa kasi duniani kote.Wazizi wa Alex walipopata taarifa hiyo walisikitika sana kwani hawakujua ni vipi watampata mtoto wao.Kila siku walikuwa wanasali ili mungu amuepushe mtoto wao kwani yeye ndiyo alikuwa nguzo kwenye familia hiyo.Nyumba kubwa waliyokuwa wanaishi kwa sasa ilijengwa kwa hela za Alex,pia walifungua miladi mingi sana ambayo ili wafanya wawe matajiri kwani walikuwa wanaingiza pesa nyingi sana kwa kipindi hicho
“mungu naomba umuepushe mwanangu kwani bado hatujui kama yupo hai au amekufa kama yupo hai naomba umlinde na mabalaa yote”mama yake na Alex alikuwa anamuombea mtoto wake kila siku
Taarifa hizo pia zilimfikia dokta ambaye alikuwa anamtibu Cindelela na ndiye mtu wa kwanza kujua uhusiano kati ya Alex na Cindelela.Dokta alipozipata hizo taarifa alisikitika sana kwani alijua ni kiasi gani Alex na Cindelela walivyokuwa wanapendana japo aliwashuhudia kwa siku moja tu,siku ambayo Cindelela na Alex waliunda mapenzi yao pale hospitali
Dokta aliingia kwenye mafaili yake na kuanza kutafuta namba ya mzee Jacobo ili amtaharifu kwamba kijana yule aliyemtolea Cindelela figo amepotea baada ya ndege kudondoka baharini.Dokta hakujua kwamba mzee Jacobo ndiyo anahusika na ishu nzima ya Alex.Alifanikiwa kuipata namba ya Mzee Jacobo na kuanza kuipigaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“hallo”dokta alisema baa ya simu kupokelewa
“hallo nani mwenzangu”Alihitika mzee Jacobo
“mimi ni dokta kutoka katika hospitali ya St Thomas London”dokta Alisema
“okey daktari nimefurahi sana kunipigia,vipi kulikuwa na tatizo lolote?au huyo kijana aliyemsaidia mwanangu amejitokeza akitaka hela yake nimpe niitume sasa hivi”alisema Mzee Jacobo
“hapana huyo kijana hajaja hapa ila nilitka kukuambia kwamba huyo kijana amepata matatizo”alisema Dokta
“Mungu wangu!!!!! Amepata matatizo gani tena?”aliuliza mzee Jacobo
“yeye ni miongoni mwa watu waliopata ajali ya ndege”alisema Daktari
“ajari ya ndege ipi?”aliuliza mzee Jacobo
“ile ya ndege iliyotumbukia baharini”alisema dokta
“huyo kijana anaitwa nani?”aliuliza Mzee Jazobo
“anaitwa Alex na maiti yake haionekani wakati maiti za watu wengine zimeonekana”Alisema dokta
“Anaitwa nani tena!!!!1?”aliuliza mzee Jacobo kwa mara ya pili huku akionekana kushangaa
“anaitwa Alex pia ni mchezaji mpira katika timu moja iliyopo haopa Uingereza na ndiyo kijana anayetembea na mwanao Cindelela,nimekuambia hivi ili umsaidie ssababu yeye alimsaidia mwanao na yule kijana ni mpole sana,nimesikitika sana kupotea kwake”Dokta alisema bila kujua kwamba mtu anayemuambia ni mtu aliyetaka kumuua Alex bila kujua kwamba ndiyo kijana aliyemtolea Alex figo
Mzee Jacobo masikio yake yaliziba kwa muda baada ya kusikia kwamba Alex ndiyo kijana aliyemtolea Cindelela figo moja.Alisimama kama sanamu huku chozi likimdondoka sababu hakuamini kwamba kijana anayetaka kumuua ndiyo kijana aliyeokoa maisha ya mwanae.Mzee Jacobo alikata simu na kuanza kupiga simu ya Saidi ili amuambie kwamba asimuue Alex
Kila akijaribu kupiga namba ya Saidi ilikuwa haipatikani,alijaribu mara kwa mara bila mafanikio yoyote.Mzee Jacobo alianza kutetemeka kwani alijua anasababisha kifo cha mtu asiyekuwa na hatia
“Eeeh mungu naomba umnusuru huyo kijana kwani sikujua kwamba ni mtu mwema kwangu,naomba umuepushe na kifo kwani nakiri yeye ndiyo anastahili kumuoa mwanangu na siyo mtu mwingine yeyote”Mzee Jacobo alisema huku akitoka nje ya nyumba yake kwani alionekana kuchanganyikiwa
Hali ya mzee Jacobo ilianza kubadilika gafla kwani alishajua amefanya makosa makubwa sana kutaka kumuua mtu ambaye aliokoa maisha ya binti yake bila kujua.Moja kwa moja alikaa kwenye kiti kilichokuwa kwenye garden yake na kuanza kufikiri ni jinsi gani atamasaidia yule kijana sababu kila akijitahidi kumpigia Saidi ili asimuue Alex namba yake ilikuwa haipatikani
“sasa nifanyaje ili nimsaidie huyo kijana sababu najua lazima Saidi amuue”mzee Jacobo alikuwa anajisemea mwenyewe kama kichaa
Kwa mawazo aliyokuwa nayo hakujua kama mkewe yupo nyuma yake anasikiliza anavyoongea mwenyewe.Mzee Jacobo mwili ulianza kumtetemeka sababu alikuwa anaogopa dhambi kubwa ambayo ilikuwa inataka kuja mbele yake.Dhambi ambayo aliipanga lakini siyo kwa kijana aliyemsaidia binti yake kurudisha uzima wake
“Eeh mungu naomba umlinde huyo kijana kwani sikujua kama ndiyo yeye aliyemsaidia mwanangu”alijisemea mzee Jacobo na kushangaa akishikwa bega kwa nyuma
Alipogeuka alikutana na sura ya mke wake ikimuangalia kwa macho ya udadisi sana.Mzee Jacobo alishtuka kidogo kwani hakujua kama mke wake alikuwa anasikia maneno yote aliyokuwa anayaongea mwenyewe
“Mume wangu nadhani kuna kitu kinakusumbua na unatakiwa uniambie sababu mimi ni mkeo”Mkewe alimuambia
Mzee Jacobo hakuwa na lakujitetea sababu mkewe alishaonyesha dalili ya kujua kila kitu kinachoendelea.Ilibidi awe mkweli na kumueleza mkewe kila kitu kilichotokea kuhusu huyo kijana mpaka simu aliyoipokea kutoka kwa Daktari.Mkewe alikuwa anasikitika sana huku machozi yakiwa yanamtoka sababu alimuonea huruma sana Alex kwani hakuwa na hatia yoyote
“mume wangu hivi huyo kijana akifa na Cindelela akaja kujua wewe ndiyo umesababisha unadhani utamuambia nini?”mkewe aliuliza
“mke wangu sijui hata nifanyaje kwani nahisi nitampoteza mwanangu”Mzee Jacobo alisema
“kinachotakiwa ni kukusanya watu wako wengine ili muende kumsaidia huyo kijana sababu yupo kwenye hatari kubwa sana,na kumbuka huyo ndiyo mkwe wangu ninayemfahamu naomba umsaidie mkwe wangu”mke wa mzee Jacobo aliongea kwa uchungu sana
“lazima nimsaidie”alisema mzee Jacobo huku akimkumbatia mkewe kumfariji
Mzee Jacobo alichukua simu yake na kumpigia kijana wake mwingine ambaye alikuwa miongoni mwa vijana wa Saidi ili ampe taarifa ya kuacha kumuua Alex
“Hallo bosi”alisema huyo kijana baada ya kupokea simu
“Paul mpo wapi kwa sasa?”aliuliza mzee Jacobo
“sisi tupo Tanzania na tupo pamoja na mwanao ila saidi na vijana wengine wawili tumewaacha msituni”alisema yule kijana
“wao wanafanya nini msituni?”mzee Jacobo aliuliza
“bado wanamtafuta yule kijana ili waakikishe kama amekufa au la?alisema yule kijana na kumfanya mzee Jacobo jasho limtoke baada ya kusikia maneno yale
“mungu wangu kwani mlimfanyaje?”aliuliza mzee Jacobo
“Mara ya mwisho alitupwa kwenye maporomoko ya maji na kusema ukweli hawezi kupona sababu kule chini kuna mawe mengi sana.Japo kazi ilikuwa na ugumu lakini tumeifanya vizuri bosi “alisema yule kijana bila kujua yale maneno yalikuwa yanamchoma mzee Jacobo
“kwahiyo atakuwa amekufa?!!!”aliuliza mzee Jacobo kwa kuhamaki
“ndiyo pale hawezi kupona kabisa”alisema yule kijana
“fika nyumbani tutaongea vizuri”alisema mzeeJacobo na kukata simu
Mapigo ya moyo wa mzee Jacobo yalikuwa yanaenda mbio sababu ya ile taarifa aliyoipata kwamba Alex amefariki dunia.Alikaa kwenye kiti huku akimsubiri yule kijana ambaye alikuwa anakuja na mtoto wake.Pale kwenye kiti palikuwa hapakaliki kwani kila muda alikuwa anaangalia getini kama kuna mtu anaingia na gari
Baada ya masaa mawili vijana waliwasili na gari huku wakiwa pamoja na Cindelela ambaye alikuwa hajitambui hata kidogo.Walishuka na kumuingiza ndani ya nyumba ili waje kuzungumza na mzee kuhusu Alex.Walikwenda mpaka pale alipokuwepo mzee na kumsikiliza anataka kuwaambia nini sababu alionekana tofauti kabisa na mwanzo
“tumefika mzee”alisemayule kijana
“kaeni chini”alisema mzee Jacobo huku akiwa kwenye hali ya utofauti
“sawa bosi”waliitikia na kukaa kwenye viti
“mnasema kweli yule kijana anaweza kuwa amekufa?”aliuliza mzee Jacobo
“ndiyo mkuu hatuwezi kukudanganya”walisema wale vijana
“mnaweza kunipeleka huko?”mzee Jacobo aliuliza
“ndiyo tunaweza lakini sasa hivi muda umeenda sana”Alisema yule kijana
“hapana nahitaji kwenda hata kwa ndege ya kukodi”alisem a Mzee jaocbo
“sawa mzee tunaweza kwenda”alisema yule kijana
Mzee Jacobo alitoka pale kwenda kujiandaa na hiyo safari,alimuaga mkewe ambaye alikuwa na Cindelela.Kabla hajaondoka Cindelela aliamka na kumkuta baba yake yupo kwenye harakati za kutaka kuondoka
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“baba”Cindelela alihita
“nam mwanangu”alihitika mzee Jacobo
“naomba umsaidie Alex wangu baba,sidhani kama nitaweza kuishi kwa raha kama nitamkosa Alex,baba naomba ukamsaidie Alex kwani wanamtesa bila hatia yoyote”Cindelela alisema kwa uchungu na kufanya mzee Jacobo na mkewe machozi yawadondoke
“Usijali mwanangu nitamsaidia”mzee Jacobo alisema na kumbusu mwanae shavuni kisha akaondoka
Mzee Jacobo aliweka maanani yale maneno aliyoambiwa na mtoto wake,Pindi atakapokuta Alex amekufa basi atakuwa ameshampoteza mwanae kipenzi.Mzee Jacobo alijitahidi sana kusali kimya kimya ili asije akakuta suala kama lile sababu itakuwa ni jambo la kusikitisha kama Alex akiwa amekufa.Walipanda kwenye ndege na safari ya kuelekea kwenye ule msitu ikaanza
…………………………………………………………………………………………………………
Alex alikuwa bado yupo kwenye wakati mgumu sana kwani alikuwa hajui wapi anapaswa kwenda iliatoke ndani ya huo msitu mkubwa.Alijitahidi sana kutembea lakini alikuwa haoni mafanikio yoyote kwani hakukuwa na makazi ya watu hapo karibu zaidi ya kuwa na miti mingi
“kwanza hapa ni nchi gani?”Alex alijiuliza mwenyewe bila kupata jibu
Aliendelea kujikongoja taratibu huku akipata muda mwingine alikuwa anapumzika sababu ya kuvuta pumzi.Siku ya pili ilikuwa inakatika bila kupata mafanikio yoyote ya kuona mtu karibu na ule msitu.Usiku kama kawaida yake alitafuta mti uliokaa vizuri na kupanda ili apate kujipumzisha
Kelele za wanyama waliokuwa ndani ya msitu huo zilikuwa zinamtisha sana Alex na kujikuta akitetemeka kwa uoga aliokuwa nao.Alikuwa anaangaza Juu ya huo mti ili aangalie kama kutakuwa na wanyama wanaopanda kwenye miti kama chui na wanyama wengine lakini alikuwa mahali salama kwani hakukuwa na myama yoyote juu ya ule mti
Mungu alisaidia usiku ukapita salama bila Alex kupata madhara yoyote kutoka kwa wanyama wakali waliokuwepo ndani ya huo msitu.Alipoona pamekucha kabisa aliamka na kuanza safari yake ya kutoka ndani ya huo msitu huku akijitahidi kubashiri njia za kutoka
Saidi na yule kijana mwingine aliyebaki naye walikuwa katika harakati za kumtafuta Alex ili wamuue kabisa kwani kwa dalili zilivyokuwa zinaonyesha kwamba Alex alikuwa hai sababu maiti yake hawakufanikiwa kuiona kwenye maji.Walitembea kando kando ya ule mto huku wakiangalia pande zote kama wataweza kumuona Alex
Kwa mbali walifanikiwa kumuona mtu akitembea kwa kujikokota huku akiufuta ule mto kwani alikuwa na dhumuni la kwenda kunywa maji.Saidi na mwenzake walijificha ili kujua ni nani yule anayeenda kunywa maji pale kwenye mto.Walipoangalia vizuri alikuwa ni Alex ndiyo anaenda kunywa maji kwani alionekana anakiu sana sababu aliyavamia maji kwa pupa na kuanza kunywa
“hapa tunaenda kumkamata kwa urahisi sana sababu anaonekana amechoka sana”Saidi alisema na kuanza kusogea pale alipokuwepo Alex
Alex alikuwa hajui kama kuna watu wanamyemelea ili wamkamate,yeye aliendelea kunywa maji sababu alikuwa na kiu sana mpaka koo lake lilikuwa limemkauka sana.Bila hata kupoteza muda Saidi na kijana wake walimvamia Alex na kuanza kumpiga ili kumregeza nguvu zake asije akaleta shida
Alex alijitahidi sana kujitetea lakini alishindwa nguvu na wale magaidi, kwahiyo Alex alibaki kuwa mpole akisubiri kupata hukumu yake kutoka kwa Said Samo hong Chota.Saidi na mwenzake walimbeba Alex na kuingia nae kwenye msitu ili wamuue.Walimfunga kwenye mti na kuanza kumchapa fimbo kwa nguvu na kusababisha Alex alie kwa uchungu sana huku akiomba msaada
“huyu hatumuui haraka haraka ila tunamuua kwa mateso mazito”Alisema Saidi na kuendelea kumchapa fimbo
Alichukua prize na kuipeleka kwenye sikio la Alex kisha akaanza kuliminya kwa nguvu huku akifurahia Alex anavyopiga kelele za uchungu akiomba msaada.Saidi hakuishia hapo alichukua tena ile prize na kuanza kuminya vidole vya Alex kwa nguvu na kuvifanya vianze kutoa damu
Alex alipiga sana kelele mpaka sauti ikaanza kumkauka lakini Said samo hong wala hakuwa hata na chembe ya huruma.Saidi kichwani mwake alikuwa anafikiria pesa atakayoipata pindi atakapokamilisha mauaji yale.Said aliendelea kumtesa Alex kwani hataka amuue moja kwa moja bila ya kumtesa
Wakati Saidi anaendelea kumtesa Alex Mzee Jacobo na wale vijana wawili nao walikuwa wanakatisha maeneo yale baada ya kuzunguka kwa muda mrefu sana kwenye ule msitu.Mzee Jacobo alisikia kelele kwa mbali na kuamua kusimama ili asikilize zile kelele zilikuwa zinatokea wapi
“mmesikia kelele za mtu akiomba msaada?”aliuliza mzee Jacobo
“ndiyo tumesikia bosi”Alijibu kijana wake
“naomba twende asije kuwa ndiyo huyo Alex mwenyewe”Alisema mzee Jacobo huku akianza kuelekea mashariki ambapo kelele zilikuwa zinatokea
Wakati wanakaribia kwenye lile eneo lenye kelele mara wakasikia mlio wa bunduki ukisikika kutoka maeneo yale.Mzee Jacobo alishtuka sana na kujua kwamba Alex atakuwa tayari ameshapigwa bunduki na kufa fa kwani zile kelel hazikusikika tena.Walianza kutembea kwa haraka huku mzee Jacobo alisali kimoyo moyo kwani hakutaka Alex afe sababu alijua lazima atampoteza Cindelela pindi atakapopata taarifa kwamba Alex amekufa.Jasho lilikuwa linamtoka huku miguu ikitetemeka
Presha aliyokuwa nayo mzee Jacobo ilikuwa haielezeki sababu kama Alex akifa mtoto wake lazima awe kwenye matatizo makubwa.Kwa kipindi hicho Cindelela ulikuwa umuambii kitu zaidi ya Alex kipenzi chake.Pindi atakapomkosa Alex basi atakuwa amepoteza maisha yake kwa kifo au kwa kuugua uchizi
Mzee Jacobo alikuwa anakumbuka sana maneno aliyokuwa anaambiwa na mtoto wake wakati anaondoka.Maneno yale yalizidi kumchoma na kumfanya aongeze kasi ya kuelekea kwenye lile pori walilosikia sauti ya risasi ikilia.Mzee Jacobo alianza kuingiwa na hofu sana kwani ukimya ulitawala sana maeneo yale na fikra zake zote zilienda kwenye kifo cha Alex
“eeh mungu naomba nimkute hakiwa hai”mzee Jacobo alijisemea kimoyoni
Mzee Jacobo na vijana wake wawili waliingia kwenye lile pori na kukuta hali ikiwa tofauti na jinsi walivyofikiria.Walimkuta kijana momoja aliyekuwa na Saidi akiwa amelala chini huku akivuja damu nyingi sana kichwani.Walipomchunguza walikuta amepigwa risasi ya kichwa na kufa pale pale
Walipeleka macho yao pembeni na kukuta Saidi wala Alex hawapo maeneo yale.Mzee Jacobo alitoa bunduki yake na kuanza kuelekea kwenye kwenye njia moja ambayo ilionyesha kwamba Saidi na Alex walipita.Mzee Jacobo alijitahidi kukimbia Japo alionyesha umri wake umeenda sana lakini kila alipokuwa anafikiria maisha ya mwanae alikuwa anaongeza kasi ili akamuokoe Alex ambaye ndiyo tulizo la mtoto wake
Wale vijana aliokuwa nao mzee Jacobo walishhangaa sana kumuona mzee Jacobo akiwa anakimbia kuliko wao,lakini walikuwa hawajui nini kilikuwa nyuma ya pazia sababu mzee Jacobo hakuwaambia dhumuni lake la kumuokoa Alex kwani alijua lazima watamgeuka na wasingemleta kwenye huo msitu.Mzee Jacobo aliendelea kukimbia huku akiangalia wapi walipopita Saidi na Alex
Kwa mbali alimuona Saidi akiwa amembeba Alex kwenye Mabega yake huku akionekana kutembea kwa kasi sana,Haikujulikana anampeleka wapi sababu kama angetaka kumuua angemuua tangu huko alipokuwa.Mzee Jacobo baada ya kumuona Said akiwa na Alex alizidisha mwendo ili amfikie
Mzee Jacobo alipiga risasi juu na kumfanya Saidi asimame pale pale sababu alijua ni mapolice ndiyo wamekuja kumkamata,Alipogeuka nyuma alimuona mzee Jacobo na vijana wengine wawili wakimfuata pale aliposimama.Saidi alishangaa sana kumuona mzee Jacobo kwani hakutegemea kumuona mzee Jacobo hakiwa pale sababu kazi ya kumuua Alex ilikuwa bado haijakamilika
“bosi unatafuta nini huku?”Saidi aliuliza
“nimekuja kumchukua huyo kijana sababu hastahili kufa”Alisema mzee Jacobo
Saidi pamoja na wale vijana wengine walishangaa sana kwani hawakutegemea kusikia neon kama lile kutoka kwa mzee Jacobo ambaye kipindi cha nyuma alitilia mkazo sana suala la kumuua Alex.Saidi alitikisa kichwa kwa ishhara ya kukataa maneno ya yule mzee na kuona yule mzee ameingiwa na uchizi wa muda mfupi
“mzee wewe ndiyo unaongea maneno hayo?”Saidi aliuliza
“mimi ndiyo nazungumza tena nikiwa na akili zangu timamu,naomba huyo kijana aachiwe huru.Mimi ndiyo niliyetoa majukumu ya kumuua kijana huyo na ni mimi ndiyo nasitisha hayo majukumu siku ya leo”Mzee Jacobo alisema huku akimtazama Alex aliyekuwa kwenye bega la Saidi
“mzee unajua kwa sasa tupo kwenye hatari ya kupoteza maisha ya watu zaidi ya mia kwenye ndege tuliyoitupa baharini,unadhani tukimuacha huyu kijana hawezi kututaja kwamba sisi ndiyo tuliyofanya yale mauaji?”aliuliza Saidi
“liwalo na liwe ila nataka niokoe maisha ya binti yangu”alisema mzee Jacobo huku akimsogelea Saidi ambaye alikuwa anarudi nyuma
“mzee usijaribu kusogea sababu nitafyatua risasi ya kichwa kwa huyu kijana na utampoteza kabisa”alisema Saidi huku akirudi nyuma
Saidi alishika bunduki yake imara huku kidole chake kikiwa sehemu ya kufyatulia risasi.Said hakuwa na masihara yoyote kwani kama akimuacha Alex atakuwa amejipalilia makaa ya moto kwenye maisha yake sababu Said alikuwa anatafutwa kila mahali na lile tukio la kudondosha ndege lingekuwa ndiyo kihama chake kwani uchunguzi ulikuwa bado unaendelea
“Boss naomba urudi nyuma kabla sijamuua huyu kijana”Saidi alisema huku akielekeza bunduki yake kwenye kichwa cha Alex
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“hapana Saidi huyo kijana hatakiwi kufa”Mzee Jacobo alisema
“naanza kuhesabu sitaki unifuate,moja,mbili,taaaaaa”Kabla hajamalizia alishangaa kitu kikimuuma kwenye shingo yake kwa kasi ya ajabu
Saidi alimdondosha Alex chini na kuanza kuangalia kitu gani kimemuuma kwenye shingo yake.Macho yake yalikutana na nyoka aina ya Black mamba akiwa kwenye tawi la karibu katika mti aliokuwa nao karibu.Saidi alianza kulia kwani alikuwa anamjua fika yule nyoka ni Hatari sana kwani inasemekiana yule nyoka akikung’ata huwezi kuchukua muda mrefu unapoteza maisha
Said alianza kupepesuka na kuanza kupiga risasi hovyo kwani hakutaka kufa peke yake.Risasi alizozipiga ziliwapata vijana wake na kudondoka chini huku risasi moja ikimpiga mzee Jacobo kwenye mkono wake wa kulia sababu aliruka pindi saidi alipokuwa anapiga zile risasi
Mzee Jacobo alitumia nafasi hiyo kufyatua risasi mbili zilizompata saidi kwenye kifua chake na kudondoka papo hapo,Mzee Jacobo aliinuka na kuanza kuwaangalia wale vijana wengine na kuona bado wanapumua.Aliwafyatulia risasi na kuwamaliza hapo hapo sababu hakutaka kuwaacha hai kwani wangearibu mipango yake
Mzee Jacobo baada ya kuhakikisha kwamba wale wote wamekufa alimsogelea Alex na kuanza kumuangalia kama amepoteza maisha au la.Alimuangalia kwa makini na kugundua kwamba Alex bado anapumuana yupo hai,Alimuinua na kuanza kumkokota kutoka nje ya ule msitu wenye kutisha.Japo mzee Jacobo hakuwa na nguvu sana pia alikuwa na jeraha kla risasi kwenye mkono wake lakini alijitahidi sana kumkokota Alex kwani bila kurudi na Alex maisha ya mtoto wake yangekuwa kwenye hatari kubwa sana
Mzee Jacobo alikuwa anamuomba mungu wafike salama sababu Alex alionekana kuwa na hali mbaya sana.Mzee Jacobo alitoa simu yake ya upepo na kuanza kupiga kwenye kitengo cha msaada ili walete Helikopta kwani asingeweza kutembea na Alex mpaka nje ya hule msitu kwani wote walionekana wapo kwenye hali mbaya sana
Ndani ya masaa kumi Helikopta iliyokuwa na watu ndani yake ilitua ndani ya huo msitu kasha watu watatu waliovalia mavazi ya kijeshi walishuka na kuanza kuelekea kule walipokuwepo Alex na mzee Jacobo.Waliwafikia na moja kwa moja wakawapeleka kwenye Helikopta na safari ya kuelekea Tanzania ikaanza
Hali ya Alex ilikuwa mbaya kuliko hali aliyokuwa nayo mzee Jacobo kwani mpaka muda huo Alex alikuwa hajitambui.Mzee Jacobo alikuwa anamuangalia Alex kwa huruma sana huku dokta akiendelea kumpa huduma ya kwanza ndani ya ile Helikopta.Mzee Jacobo alikuwa anamuomba mungu Alex asife sababu Hkutaka kumpoteza mwanae
“mungu naomba usimchukue huyu kijana”Mzee Jacobo alisema kimoyomoyo
Helikopta ilishuka chini na moja kwa moja gari la wagonjwa mahututi lilifika pale na kumpakia Alex ili wampeleke hospitali kufanyiwa matibabu.Gari lilikuwa linaendeshwa kwa kasi huku likipiga king’ora kufanya magari mengine yasimame kulipisha.Moja kwa moja Gari liliingia kwenye hospitali ya Aga khan na moja kwa moja Alex alichukuliwa na kuwaishwa wodini ili akapate matibabu
Mungu alikuwa mwema kwani Alex baada ya kupewa matibabu ya uhakika fahamu zilianza kumrudia polepole japo alikuwa na hali mbaya kwahiyo walikuwa wanampa vidonge vya usingizi ili alale muda mrefu.Mzee Jacobo nae alikuwa kwenye hali nzuri sababu hakuwa na jeraha lingine zaidi ya Risasi tu iliyompiga kwenye mkono kwahiyo ariruhusiwa kuondoka nyumbani
Mzee Jacobo alipofika nyumbani hakutaka kumuambia kitu chochote mwanae kwani alikuwa anataka kuhakikisha Alex anapona vizuri ndiyo amuambie mwanae kwamba mpenzi wake yupo hospitali.Hakutaka kuonana hata na mwanae sababu aliogopa kuulizwa swali lolote kuhusu Alex kwani hayo maswali yangekuwa ni ya lazima kutoka kwa Cindelela
“mume wangu”mke wa mzee Jacobo aliita
“niambie mke wangu”alisenma mzee Jacobo
“unajua kwamba Cindelela hajala siku ya pili sasa”Mkewe alisema
“kwanini?”mzee Jacobo aliuliza
“mwanangu anateseka sana sababu kila muda anazungumza kuhusu Alex tu,nikimpa chakula hataki anasema mpaka atakapomuona Alex ndiyo atakula hicho chakula,naomba tumpeleke huko hospitali ili tuipoze roho yake sababu mwanangu anateseka sana”alisema mke wa mzee Jacobo huku machozi yakimtoka
Mzee Jacobo aliposikia hali ya mwanae na yeye machozi yakaanza kumtoka huku akiinuka kuelekea kwenye chyumba alicholala Cindelela.Machozi yaliendelea kumtoka zaidi alipoona hali ya mwanae iliyokuwa mbaya sababu ya kutokula na mawazo aliyokuwa nayo juu ya Alex
“baba Alex yupo wapi?”ilo ndiyo lilikuwa neon la kwanza kutoka kwenye mdomo wa Cindelela
“mwanangu leo nakupeleka ukamuone Alex”mzee Jacobo alisema huku akimkumbatia mwanae
“kweli baba?,kwani Alex hajafa?”Cindelela aliuliza maswali mawili mfululizo
“mwanangu, Alex ni mzima na leo naenda kukupeleka ili ukamuone”alisema mzee Jacobo
“asante baba nashukuru sana”Cindelela alisema huku tabasamu likimtoka kwenye mdomo wake
Mzee Jacobo alitoka kwenda kufanya maandalizi ya kumpeleka Cindelela hospitali ili akamuone Alex.Baada ya muda kidogo Cindelela akawa ndani ya gari la baba yake wakielekea hospitali.Cindelela alionyesha furaha sana kwani hakutegemea kama Alex angepona katika yale maporomoko ya maji,Vilevile alikuwa ahamini kama ni kweli Alex atakuwa amepona alidhani labda baba yake anamdanganya.Kwahiyo Cindelela alikuwa njia panda na alitaka kuhakikisha yeye mwenyewe kama Alex amepona kweli
Mzee Jacobo na Cindelela walifika hospitali kisha wakashuka na kumuacha Dereva.Moja kwa moja walienda kwenye chumba alicholazwa Alex.Kabla hawajaingia mzee Jacobo alimuangalia binti yake kisha akatabasamu na kufungua mlango ili waingie
Macho ya Cindelela yalimuona Alex akiwa amelala kwenye kitanda huku watu watano wakiwa wamemzunguka.Cindelela alianza kutembea kwa madahaa kuelekea kwenye kitanda alicholala Alex.Kwa mwendo aliokuwa anatembea na viatu vyake vilivyokuwa vinalia watu waliokuwemo kwenye kile chumba wakageuka kumuangalia yeye
Moja kwa moja Cindelela alipiga magoti pale kwenye kitanda na kumbusu Alex kwenye paji la uso.Kitendo kile kiliwafanya watu wamshangae kwani hawakumjua yeye ni nani kwa Alex.Miongoni mwa watu wale walikuwa ni wazaizi wa Alex ambao walipata taarifa kwamba mtoto wao amelazwa pale hospitalini
“Wewe ni nani?”mama yake na Alex aliuliza
“mama mimi ndiyo mpenzi wa Alex naitwa Cindelela,na Alex ni mtu muhimu sana kwenye maisha yangu kuliko kitu chochote kile”Cindelela alisema huku machozi yakimtoka
Mama yake na Alex hakuwa na neno lingine zaidi ya kumkumbatia Cindelela.Mzee Jacobo alimuhita baba yake na Alex na kuanza kumuambia kila kitu kuhusu Alex na Cindelela lakini hakutaja kama yeye ndiyo mtu aliyetaka kumuua Alex.Mwisho wa maongezi yao yalifikia kwenye suala la kuwaozesha Alex na Cindelela ili wawe mke na mume
“inatakiwa mipango tuianze mapema tu pindi Alex atakapokuwa vizuri kabisa”Mzee Jacobo alisema
“Kweli pia nashukuru sana kukufahamu mzazi mwenzangu”alisema baba yake na Alex
Urafiki mkubwa ulitengenezwa kati ya mzee Jacobo na baba yake Alex.Cindelela alikuwa hajui kitu chochote kama wazazi wake walishaanza kuzungumzia swala la ndoa yao,yeye alikuwa na hamu ya kumuona Alex akiwa na nguvu zake
“Cindelela”Alex alihita polepole na kumfanya Cindelela ageuke kwa haraka
“Alex kipenzi changu umeamka?asante mungu”Cindelela alisema kwa furaha
Alex alifumbua macho yake yote na kuanza kumuangalia Cindelela aliyekuwa mbele yake.Taswira ile ilimrudisha nchini Uingereza ambapo Cindelela alikuwa anaumwa nay eye alikuwa anamuangalia kama yeye anavyoangaliwa sasa.Alex alitabasamu na kumuangalia Cindelela ambaye bado alikuwa anamshangaa Alex
“Siwezi kufa mpaka ahadi yetu itakapotimia”Alex alisema na kumfanya Cindelela atabasamu huku machozi yakimtoka
“nakupenda sna Alex”Cindelela alisema huku akimkumbatia Alex
Baada ya siku kadhaa Alex alipona kabisa na kuwa kama zamani.Cindelela alifurahi sana kwani maisha yao ya furaha yalianza upya.Kila mahari walikuwa wote sababu kila mmoja hakutaka kumuacha mwenzake awe peke yake
“Cindelela nilikuwa nakuambia kwamba Alex anakupenda sana ebu cheki mlivyopendezea”Wit alitania siku moja akiwa na Cindelela pamoja na Alex
“sikujua kama Alex ndiyo mwanaume wa maisha yangu ila kwa sasa nampenda sana na namtambua kama yeye ndiyo mume wangu mtarajiwa”Cindelela alisema huku akitabasamu
“nadhani kwenye harusi yenu watu wataniona kichaa jinsi nitakavyokuwa”Wit alisema huku akicheka
“ndiyo usubiri sasa siku siyo nyingi”Cindelela alisema huku Alex akibaki kimya
Wakati Cindelela,Wit na Alex wakizungumza hayo wazazi wao walikuwa wapo kwenye mipango ya harusi.Kila mzazi alipania kwani walitaka kuifanya ile harusi iwe ni ya kihistoria.Taarifa za kuoa kwa Alex zilifika mpaka kwenye uongozi wa timu ya Birmingham city.Uongozi wa timu ulitoa kiasi kingi cha pesa ili kufanikisha harusi ile
“Swala la ukumbi nitalishughulikia mimi”Alisema waziri nishati na madini ambaye alikuwa rafiki mkubwa sana wa Mzee Jacobo
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mimi nitajitolea usafiri wa watu wote watakaoenda kwenye iyo harusi pia nitajitolea Gari itakayowabeba maharusi”alisema mfanya biashara mmoja maarufu sana aliyekuwa anajulikana kwa jina la Joseph Muhando
Kila mtu alikuwa anatoa ahadi yake juu ya ile harusi kwani ilipangwa kuwa ni harusi ya kihistoria katika nchi ya Tanzania.Cindelela na Alex walitamani sana siku hiyo ifike sababu kila mtu alikuwa na shauku ya kufunga ndoa hiyo.Vitu vyote vilikamilika na kila mtu alikuwa tayari kwa harusi hiyo ambayo ilionekana kuwa na Presha kubwa sana kwa watu
Siku chache kabla ya harusi kufungwa Mzee Jacobo alipokea simu kutoka kwa mzee Thomas ambaye waliweka ahadi kwamba mwanae atamuoa Cindelela.Simu ile haikuwa ya kheri lakini kwa maelezo kutoka kwa mzee Jacobo yalimfanya mr Thomas akubaliane kwani Cindelela alikuwa na mapenzi mazito kwa Alex
“hapo nimekubali bila kinyongo na kuhusu mwanangu nitamuelewesha tu,acha wanaopendana waowane”alisema Mr Thomas
Mzee Jacobo alifurahi sana kusikia vile kwani hakutegemea ka mr Thomas atakubaliana na jambo lile.Mzee Jacobo alipata amani ya moyo ambayo ilimzidishia hali ya kufanya maandalizi ya harusi.Mambo yote yaklikamilika na ni masaa tu ndiyo yalikuwa yannasubiriwa ili ndoa ifungwe
“Cindelela sasa unaenda kuwa mke wangu wa halali “Alisema Alex
“nani nafurahi kwani naenda kukuhita mume wangu”Cindelela alisema
Nje ya kanisa katoriki la St Joseph lililopo posta kulikuwa na umati mkubwa wa watu wakiwa nje ya kanisa ilo wakisubiri kuona tukio ambalo wengi wao walikuwa wanalisubiria kwa hamu sana.Magari ya kifahari yalikuwa yamepaki nje huku maaskari wengi sana wakiwa wamezunguka kanisa zima kulinda usalama wa watu na mali zao
Kelele zilisikika kwa wingi baada ya kuonekana farasi wawili wakikokota kigari kilichobeba maharusi.Kila mtu alikuwa anarusha maua kwa ishara ya kuwabariki katika ndoa yao.Alex na Cindelela walikuwa wanapunga mikono kwa watu huku wakiachia tabasamu zuri na la kupendeza
Walishuka kwenye kile kigari na wakaanza kuvuta hatua kuelekea ndani ya kanisa.Kwa wale waliobahatika kuwa ndani walishangilia sababu Cindelela na Alex walipendeza sana kuanzia mavazi yao mpaka muonekano wao.Ndani ya kanisa kulikuwa na viongozi wengi ambao walikuja kumpa support kiongozi mwenzao
Bila kupoteza muda misa ilianza na kila mmoja alikuwa makini kusikiliza ibada,Watu wote walikuwa wanasubiri kipindi cha kuvalisha pete na kuhapa.Walisogea mbele na kusimama kwa kuangaliana.Pete za zililetwa pale mbele na wapiga picha walikuwa makinisana kusubiri tukio ilo muhimu
“Alex umekubari kumuoa Cindelela na kuwa mke wako wa ndoa?,mtasaidiana kwenye kila jambo?na mtakuwa pamoja mpaka kifo kitakapowatenganisha?Pri aliulza
“Ndiyo nimekubali”Alex alijibuu na kumvisha Cindelela pete
Watu walipiga makofi huku wakina mama wakipiga vigelegele kwani walifurahi sana.Cindelela nae alipoulizwa alijibu kama Alex alivyojibu na kufanya shangwe zisikike upya.Mpaka misa inahisha Alex na Cindelela walikuwa ahawaamini kama tayari wameshakuwa mume na mke
“hii ndiyo ndoto niliyokuwa naiota siku zote na kweli imetimia”Alex alisema huku akimkumbatia Cindelela
Misa ilipoisha watu wote wakaanza kuelekea ukumbini kwaajili ya kujumuhika katika sherehe ya kuwapongeza maharusi.Alex na Cindelela walipandishwa kwenye gari haina ya Hammer kwaajili ya kuelekea kwenye ukumbi wa sherehe.Baadhi ya viongozi nao walikuwa wanaelekea kwenye ukumbi huo ili kukamilisha tukio lile lililokuwa linasubiriwa kwa muda mrefu
“Ndani ya ukumbi mkubwa wa YORK CITY GARDEN watu walionekana kujaa kusubiri maharusi waingie ili harusi ianze.Mc maharufu ajulikane kwa jina la Enock kobelo alionekana akiwachangamsha watu waliokuwepo pale ukumbini kwa maneno yake ya hapa na pale
“Sasa wageni waalikwa tunaomba tusimame ili kuwaruhusu maharusi wetu waingie ukumbini na tuanze ratiba yetu”Mc alisema na kila mtu aliyekuwemo mule ndani alisimama kwaajili ya kuwapokea maharusi
Maharusi waliingia ukumbini na watu walikuwa wanashangilia kiwa makofi na vigelegele.Watu maarufu walikuwa wengi sana kwenye harusi hiyo akiwemo Waziri mkuu wa nchi ya Tanzania Mh Christopher Magali.Pia kulikuwa na mawazili wengi pamoja na wabunge bila kukosa wafanya biashara maarufu
Harusi ilienda kama ilivyopangwa huku Alex na Cindelela wakipewa zawadi nyingi ikiwemo nyumba mbili za kifahari zilizopo pembezoni mwa bahari ya hindi.Japo Alex kwa kipindi hicho alikuwa na hela za kutosha kutokana na kazi yake ya uchezaji mpira.Zawadi zilikuwa nyingi sana Lakini zawadi nyingine ilikuwa ni kwenda nchini Marekani kwaajili ya fungate
Mpaka harusi inaisha kila mtu alikuwa ameridhika na ile sherehe kwani ilikuwa ni babkubwa kutokana na kuchangamka sana kupita maelezo.Alex na Cindelela baada ya Harusi walilala hotelini kwaajili ya kujiandaa kwanmi kesho yake walihitajika kusafiri kuelekea Marekani kwaajili ya fungate
Cindelela na Alex walisafiri kwenda Marekani kwaajili ya fungate la harusi yao.Walifikia ndani ya Jiji la NEW YORK na kuanza kula raha kwa kutembelea sehemu mbalimbali za kihistoria.walikaa mwezi mmoja ndani ya jiji ilo huku wakistarehe katika fukwe mbalimbali
“Alex mbona sijisikii vizuri”Alisema Cindelela
“ujisikii vizuri kivipi?”Alex aliuliza
“nahisi kichefuchefu”Cindelela alisema
“siyo swali la kuuliza mambo yameshajipa”Alex alisema huku akicheka
Walipoenda kupima ni kweli Cindelela alikutwa na ujauzito kwahiyo walikuwa wanasubiri mtoto tu.Baada ya fungate lao kuisha walirudi Tanzania kwaajili ya kujiandaa kurudi nchini Uingereza kuendelea na masomo huku Alex akiendelea na kazi yake ya uchezaji mpira kwani alikuwa anaipenda kutoka moyoni mwake
Wote wawili walirudi nchini Uingereza na kuendelea na shughuli zao za kimasomo.Kitu kilichomsikitisha Cindelela ni baada ya kusikia kwamba baba yake anashikiliwa na police kwani alikuwa ni muhusika lile tekio la ndege kudondoka na.Baada ya uchunguzi wa muda mrefu ilibahinika ni kweli kwamba mzee Jacobo anahusika kwahiyo alitakiwa kuhukumiwa kifungo cha maisha
“naomba niongee na mwanangu kabla sijapelekwa gerezani”mzee Jacobo alisema
Cindelela alipelekwa kwaajili ya kuongea na baba yake kwani ilionekana ana jambo la siri anataka kumuambia
“Cindelela mwanangu”mzee Jacobo alihita
“Abee baba”Cindelela alihitika
“naomba umpende Alex kwani yeye ndiyo mwanaume pekee anayekupenda katika dunia hii,pia mtunze mama yako kwani najua nitakuwa nimemuacha kwenye hali mbaya ya majonzi.Najutia maamuzi yangu ya kutaka kumuua Alex bila kujua yeye ndiyo chanzo cha uzima wako.ila usisahau kumpenda Alex kama anavyokupenda wewe”mzee Jacobo alisema huku machozi yakimtoka
“sawa baba nitafanya ulivyoniambia”Cindelela alisema huku akifuta machozi
Mzee Jacobo alifungwa kifungo cha maisha japo alikuwa ni waziri wa mambo ya nje.Cindelela na Alex waliendelea kuishi nchini Uingereza huku wakisubiri kittoto kilichopo tumboni mwa Cindelela kizakliwe ili kiongeze furaha katika maisha yao
“mke wangu nitafurahi sana tukipata mtoto wa kiume ili tumuite jina la ushindi”Alex alisema
“kweli mume wangu na mungu atajalia tumpate huyo”Cindelela alisema
Siku zilipita na atimae miezi tisa ilitimia tangu Cindelela alipopata ujauzito.Cindelela alipelekwa hospitalini kwaajili ya kujifungua.Cindelela alifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume na kumfanya Alex afurahi sana kwani Alihisi ndoto zake zimetimia
“mke wangu nimefurahui sana”Alex alisema
“hata mimi nimefurahi mume wangu,aya unataka tumpe jina gani mtoto wetu?Cindelela aliuliza
“nataka tumuite mshindi lakini tunaliweka kwa kingereza’Alex alisema
“unamaanisha tumuite VICTOR?”Cindelela aliuliza
“Ndiyo mke wangu”Alex al;isema
“apo sawa kwani ni jina zuri na nategemea mtoto wetu atakuwa mshindi siku zote”Cindelela alisema
“Nakupenda sana Cindelela mke wangu”Alex alisema
“Nakupenda pia Alex mume wangu na mungu atakuwa na sisi kwenye maisha yetu yote”Cindelela alisema na kumkumbatia Alex
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“NAKUPENDA CINDELELA MKE WANGU”alisema Alex
“VICTOR,VICTOR,VICTOR ebu zima taa bwana ulale hiyo story nyingine utandika kesho kwasasa unatakiwa upumzike ili uupoze ubongo wako”ilikuwa ni sauti ya bibi yangu mpendwa ikiniambia kwamba niache kuandika story kwa muda huo kwani ilikuwa ni usiku sana
Kiukweli nilipoangalia saa ilikuwa nisaa kumi kasoro dakika kumi na mbili,Nikaamua kuzima computer yangu ili nilale kesho niamke na nguvu mpya ya kuandika Story nyingine tena ambayo ni mwendelezo wa simulizi hii ya Cindelela
MWISHO
0 comments:
Post a Comment