Search This Blog

Thursday, 2 June 2022

SAFARI YA MSITU WA SIRI - 2

 





    Simulizi : Safari Ya Msitu Wa Siri

    Sehemu Ya Pili (2)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya miezi minne(4) kupita David aliaza kurudi katika hali yake ya kawaida ya uchangamfu.. lakini mwili wake ulionekana kupungua kutokana muda mwingi alikuwa anawaza juu ya kifo cha bibi yake...mbaya zaidi pale anapokumbuka ucheshi/mafundisho ya maisha pamoja na hadithi za kale alizokuwa akisimuliwa na marehemu bibi yake'''hiyo ilimfanya ashindwe kula chakula vizuri kila siku""" na hatimae mwili wake ulipungua kwa kiasi kikubwa alionekana kukonda....

    *********

    kijana David alipenda kuutumia muda wake mwingi kudadisi mambo kwa kuwauliza maswali mbalimbali watu waliomzidi umri..hivyo alifahamu mambo mengi zaidi...pia alikuwa nakipaji cha kujua jambo kwa haraka hata kama kaelekezwa bila vitendo" hiyo iliwastahajabisha watu wengi pia

    kutokana na nidhamu,,ukarimu,,uchapakazi, unyenyekevu.. tabia nzuri aliyokuwa nayo David ilimfanya watu wote wampende hapo kijijini...

    na kwa jinsi alivyokuwa mweupe kwa kufata rangi ya mama yake alionekana handsome na mwenye mvuto...hivyo mabinti wengi wa kijijini hapo walijingonga na kujipitisha pitisha nyumbani kwa kinaDavid kila wakati ilimradi tu",,wamuone david hata kama hakuna jambo la msingi.. walitamani kila mmoja wao amilikiwe na David



    lakini David hakuwajali wasichana hao.....

    paul ambae ni mjomba wake david" baada ya kuona David ameshakuwa kijana"aliamua kumfundisha. jinsi ya kuwinda" pia alimpa mbinu za kumnasa mnyama kwa kutumia upinde na mshale....kijijini kwa kinaDavid jamii yao walikuwa wafugaji hivyo hivyo David hakufahamu chochote kuhusu kilimo""

    kadri David anavyozidi kukuwa ndivyo alizidi kuwa muwindaji hodari...alitokea kuwa mtu mwenye shabaha sana",, kila aliporusha mshale hakuna mshale uliopotea alihakikisha analenga shabaha yake baraabara...pindi" anapokuwa mawindoni

    David alikuja kuwa moto wa kuotea mbali kwa uwindaji....mjomba wake alimsifu sana pia alijivunia kuwa mwalimu bora wa David kwenye uwindaji"".....sikumoja mama yake David aliugua ghafla...

    hivyo walimkimbiza haraka Kwenye kituo cha afya cha kijiji hicho....walimfanyia vipimo ndipo alipogundulika kuwa Anashinikizo la damu ya kupanda(HIGH BLOOD PRESSURE)

    daktari aliyekuwa zamu siku hiyo alikuja kisha akauliza ndugu wa mgonjwa huyu wako wapi?? David baada ya kusikia hivyo alisimama haraka.. mjomba wake alimzuia kisha akaenda yeye ndipo daktari huyo akamwambia paul maradhi yanayomsibu Dada yake...paul alisikitika sana..kisha daktari akasema lakini hali yake sio mbaya sana tumemwekea Dripu hivyo anaendelea vizuri...hapo nafsi ya Paul ikatulia...

    *******CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakati huo David akiwa kasimama kwa nje jirani kabisa na mule alimoingia mjomba wake"",huku alikionekana ni mwenye shauku sha kutaka kujua kinachoendelea pia kujua mama yake amepatwa na tatizo gani..

    punde alimuona mjomba wake akitoka mule ndani..alimfuata kwa haraka..vipi mjomba" mama anaumwa nini??? anaendeleaje?? daktari kasemaje? hivi kweli mama atapona?? David aliuliza maswali hayo mfululizo... Ndio atapona pia sasa hivi anaendelea vizuri paul alijibu" huku akizipiga hatua za mwendo wa taratibu naweza kumuona:? aliuliza David" hapana yupo kwenye uangalizi wa daktari hivyo tutaruhusiwa kumuona badae...

    david alibaki kimya. kisha wakaondoka kurudi nyumbani kwaajili ya kuandaa chakula cha mgonjwa.)

    ******

    Baada ya muda kidogo walifika nyumbani",,David alichukua kuni akawasha jiko haraka kisha akaanza kuandaa chakula kwa ajili ya mama yake....wakiti akifanya hivyo pia alikuwa akimuomba Mungu mama yake apone apate afya njema...

    *******

    Paul alimuaga David kuwa anaelekea porini kwaajili ya uwindaji" kisha akaondoka zake kwa lengo la kwenda kutafuta kitoweo.

    Baada ya chakula kuiva alipakua chakula hicho ilikuwa ni ndizi pamoja na nyama ya swala...kisha akaanza safari ya kuelekea kituo cha Afya kule alipolazwa mama yake...alizipiga hatua kadhaa kisha akakumbuka" hueanda zikahitajika pesa kwaajili ya malipo ya matibabu hivyo basi aliingia chumbani kwa mama yake kisha akaliinua godoro hilo la pamba juu ya kitanda kilichotengenezwa kwa miti. alifanya hivyo kutokana alikuwa akijua mama yake huwa huweka pesa zake mahala hapo",,alitoa kiasi cha shilingi elfu thelathini zilizokuwa na mchanganyiko wa elfu moja moja zikiwemo mia tano mia tano na shilingi elfu mbili mbili...alizichukua pesa zile kisha akaondoka zake kuelekea huko alipolazwa mama yake...alizipiga hatua za haraka haraka na baada ya muda kidogo alifika.. alielekea moja kwa moja kwenye wodi aliyolazwa mama yake...aliingia alikuta mama yake kalala..alipoitazama dripu ilionekana imekaribia kuisha...alimuamsha taratibu kwa kumtikisa...punde mama David aliamka..alifumbua macho na baada ya kumuona Mwanae alitabasamu" wakati huo David alionekana mwenye sura iliyojaa majonzi...kisha akasema unaendelea mama? "nimekuletea chakula ni ndizi na nyama ya swala je utaweza kula kwa wakati huu?? David alimuuliza mama yake"" ndio mwanangu nitakula sasa hivi" kisha akanyanyuka na kukaa kitako.. David akampa chakula mama yake akala mama David alionekana kukifurahia chakula kile kisha akamwambia David unajua kupika,, umepika chakula kitamu sana"" umenikumbusha marehemu baba yako wakati mwingine alikuwa akinisaidia kupika..alikuwa akiingia jikoni wee anapika mahanjumati hatari" David alitabasamu kisha akasema Natamani baba yangu angekuwa Yuhai...punde daktari aliingia na kumjulia hali mama David.

    ******

    Dripu iliisha kisha daktari aliitoa dripu ile", na baada ya masaa manne kupita Mama David aliruhusiwa kwenda nyumbani...waliondoka kuelekea nyumbani.

    walipo fika nyumbani David alimuaga mama yake kuwa anaenda porini kule alipokuwepo mjomba wake mawindoni...mama David hakuwa na pingamizi alijibu ni sawa...kisha David akaondoka zake kuelekea porini.....

    alitembea umbali wa kama kilometa nne hivi kisha akafika sehemu ile ambayo paul anapenda kuwinda maeneo hayo aliita mjomba" kwa kupaza sauti..sauti ya David ilisikika vizuri masikio mwa Paulo kutokana na Mwangwi hivyo sauti ilijirudia rudia"" mjomba aliitika kisha David alielekea upande ule ambao sauti ilitokea..

    alimuona mjomba wake..Loh! yani leo mawindo magumu yani wanyama hawapatikani eneo hili kabisa tangu nilipokuja sijafanikiwa kuona mnyama hata mmoja..alisema Paul",,

    walikaa takribani masaa matatu bila kuona mnyama yoyote akitokeza eneo lile..

    nabaada ya muda kidogo kupita Paulo aliamua wagawane maeneo. alisema mimi nitaelekea upande ule na wewe utaelekea upande mwingine tujaribu labda tutafanikiwa kuona wanyama..

    David aliona wazo hilo ni zuri kisha akafanya kama mjomba wake alivyosema""

    *******CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    David alizipiga hatu kuelekea upande mwingine...alijitahidi kutazama kwa umakini lakini hakuona dalili ya mnyama yoyote kuonekana eneo hilo....aliamua kusonga mbele zaidi pia hakufanikiwa kuona chochote...alikumbuka maneno ya bibi yake enzi za uhai wake alimwambia"

    ((((katika maisha yako usioende kukata tamaa yakupasa uwe na subira katika kila jambo)))

    hivyo basi kauli hiyo ilimjenga vyema David kisaikorojia....

    alikuwa ni mwenye subira hakukata tamaa mara kwa mbali alimuona mnyama alipotazama kwa makini aligundua kuwa ni Swala...alifurahi sana"" uso wake ulionekana kujawa tabasamu...alinyata kwa hatua za taratibu ili swala yule asimuone...David alinyata unaweza kusema ni mtu mwenye mafunzo ya kininja.....alipo mkaribia alitoa mshale mmoja kwenye (PODO) lililokuwa mgongoni kisha mshale ule akauweka kunako upinde.. kabla hajarisha mshale ule...ghafla swala yule alikimbia na kuelekea mbele zaidi.. David alifadhaika sana hakukata tamaa alimfuta mnyama yule kule alipoelekea....alipoangazaangaza macho alimuona swala yule...David akanyata tena kwa maranyingine tena alipomkaribia swala yule alikimbia na kutokomea porini zaidi....David hakukata tamaa aliamua kuingia katika pori hilo kwaajili ya kumfuatilia swala yule huenda atamuona...

    *********

    Upande wa pili alionekana paul akiendelea kutafuta mawindo lakini hakuna dalili yoyote ya mnyama kutokeza hatimae paul alikata tamaa kisha akaamua kurudi pale walipokuwepo mwanzo.... alikaa katika jiwe moja akimsubiri David arudi huenda atakuwa amefanikiwa kunasa mnyama yoyote"" paul alikuwa akimuamini sana David katika uwindaji na haijawahi kutokea hata sikumoja David kutoka mawindoni bila kurudi na kitoweo..... alimsubiri lakini hakuona dalili ya David kutokeza eneo lile ndipo alipoamua kupaza sauti..alimuita David bila mafanikio yoyote aliamua kwenda kumtafuta ule upande alioelekea David pia hakumuona...alimtafuta pande zote bila mafanikio ya kumuona David...

    paul alikata tamaa..akajisemea moyoni atarudi tuu wacha mimi nirudi zangu nyumbani...

    **********

    Upande mwingine David aliinekana akizidi kuingia ndani ya pori...." pori lile lilionekana kuwa na msitu wenye miti mikubwa sana..mara ghafla alimuona swala yule,, kwa sasa swala yule hakuwa mbali na pale alipokuwepo David..kisha alivuta unde ule kumlenga swala yule....ile anataka uachia mshale swala alitimua mbio na kutokomea ndani zaidi kunako msitu huo...

    David alichukia sana....akaamua kuingia ndani zaidi kunako msitu huo....mara ghafla kilipita kiumbe mbele yake kwa kasi ya hajabu akuweza kukitambua kiumbe kile.



    Alistuka! sana kisha akawa katika hali ya umakini zaidi,, ikasikika sauti yenye mngurumo wa ajabu ambao hakuwahi kusikia sauti ya mnguromo huo tangu kuzaliwa kwake.... alipotazama kwa mbele aliona kunamnyama"" ,,alipomtazama vizuri" aligundua kuwa ni NGIRI. alisogea taratibu ili kumnasa mnya yule..mara ghafla..mnyama yule alipitiwa na kiumbe cha ajabu ambacho hata David hakukiona viziri wala hakuweza kutambua ni kiumbe cha aina gani!''',, kiumbe kile kilitenganisha katikati ya mwili wa yule NGILI. nakisha kutoweka na upande mmoja ambao ni sehemu ya kuanzia tumboni kuelekea nyuma.. kikaacha upande mmoja ambao ni sehemu ya kuanzia tumboni kuelekea kichwani...Damu zilimrukia David aliogopa sana..baada ya kuona hivyo alitimua mbio bila kujua ni wapi anaelekea alikimbia huku ameushikilia baraabara upinde wake",,



    *******



    baada ya kukimbia umbali mrefu huku akiwa anatokwa na damu kwenye baadhi ya sehemu za mwili wake..majeraha hayo aliyapata kwa sababu alikuwa anapita kwenye vichaka vyenye miba pasipo yeye kujua kutokana na hofu na uwoga aliokuwanao hivyo hakuweza kuhisi maumivu hata kidogo kwa wakati ule,, "" alipunguza mwendo kisha akatazama nyuma huenda akakiona kiumbe hicho....lakini hakuona chochote..

    wakati David anakimbia kwa ajili ya kuokoa maisha yake kumbe ndio alikuwa anazidi kuingia ndani zaidi kunako msitu ule,,"" alipotaamaki hakuweza kukumbuka ni njia ipi aliyoingianayo hivyo alikuwa kama mtu aliyepotea njia...

    alitembea kwa hatua za kunyata huku CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akigeuza-geuza shingo yake kila upande,,"" alifanya hivyo mara zote kipindi anazipiga hatua...mara kiumbe kile cha ajabu kikapita tena" mbele yake kwa kasi ya ajabu david hakuweza kukitambua kiumbe hicho kutokana kilikuwa kinapita kama upepo( vup)

    aliingiwa na uwoga kisha mapigo yake ya moyo yalianza kupiga kwa kasi ya ajabu....aliamua kutimua mbio,, safari hii alikimbia huku anapiga kelelele...nakufaaaaa!!! nisaidieni..aliomba msaada pasipo mafanikio yoyote...alipiga kelele hizo ili kama kuna mtu yupo karibu na maeneo hayo aweze kumsikia huenda akampa msaada...Lah!hasha!!"",,

    kelele zile hazikusaidia chochote"",, hakuna mtu aliyesikia kelele zile kwa sababu David alikuwa ndani zaidi kunako msitu ule hivyo kelele zile hazikuweza kutoka nje ya msitu",,



    ************



    Hakuna binadamu yeyote aliyewahi kuingia kwenye MSITU huo kisha akatoka Yuhai",, inasadikika kuwa ndani ya msitu huo ,, kuna kiumbe wa ajabu.

    inasemekana miaka mingi iliyopita"",, yapata takribani zaidi ya miaka mia moja kulikuwa na watu",,jamii ya kabila la ""WACHEDA"" watu hao walikuwa wakiabudu mti""..Mti huo ulikuwa Katikati ya mstu..ambapo David yumo....

    watu hao jamii ya kabila la WACHEDA waliuita Mti huo MUNGU wao.. hivyo walikuwa wakifanyia makafara na matambiko,,""na kuomba katika mti huo... ilitokea siku moja kuna mtu mmoja alikwenda msituni humo na kuukata mti ule...baada ya kuukata..alipata lahana muda huohuo"" kisha alibadilika na kuwa kiumbe wa ajabu...Tangu siku hiyo hakuwahi kuonekana tena...hata ndugu jamaa na marafiki zake hawakuwahi kujua ni wapi alipokwenda hivyo alibakia msituni humo maisha yake yote...basi

    kuanzia sikuhiyo alikuwa anauwa chochote kinachoonekana kuingia kwenye msitu ule...alifanya hiyo kwa Wanyama na Binadamu mpaka kizazi chaJamii yote ya kabila la WACHEDA kilikwisha nakutoweka kabisa...



    ************



    David alikuwa katika wakati mgumu sana na hatari kubwa ndani ya msitu ule..alichoka kukimbia akaamua kupumzika chini ya mti..baada ya dakika kadhaa aligundua kuwa hapo alipoketi sio salama..yani pako wazi sana hivyo alihofia kuwa huenda kiumbe kile kitamuona kwa urahisi na kumdhuru..

    alijisogeza huku anatambaa utadhani mtoto wa miezi tisa""",,,David alijisogeza kunako kichaka kidogo ili ajifiche.. lakini kabla hajafanya hivyo..ghafla kiumbe kile kikajitokeza tena"" kikapita kwa kasi ya ajabu!! David alinyanyuka haraka kutoka pale chini kisha akaanza kutimua mbio tena...alikimbia sana huku asijue nini cha kufanya...wakati anakimbia mara ghafla alikanyaga sehemu iliyotitia akadondoka kisha akatumbukia ndani ya shimo refu sana Tiiiiiiii akapoteza fahamu



    alipozinduka alishangaa kujikuta amelala chini alipatazama upande wa juu aligundua kuwa yumo ndani ya shimo...sasa nimefikaje humu alijiuliza David....ndipo kumbukumbu ikarudi alikumbuka kuwa alikuwa anamkimbia yule kiumbe wa ajabu ambaye hata yeye mwenyewe hakufanikiwa kukitambua kiumbe kile...aliogopa sana alipotazama vizuri aliona kama unauwazi sehem akaamua kupita kwenye uwazi huo..... aliifuata njia hiyo ambayo ilikuwa iko chini ya aridhi....wakati anazipiga hatua alikuwa anajiuliza maswali njia hii itatokezea wapi??? lakini alijipa moyo bila shaka hili ni handaki hivyo basi lazima kutakuwa na njia ya kutokezea nje..baada ya kuwaza hivyo alianza kuzipiga hatua za harakaharaka..kutokana na giza lililokuwemo humo ndani ya hiyo njia ya nini kwa chini ya aridhi...David alijingonga gonga kwenye kingo za njia ile...

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    **************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog