Simulizi : Safari Ya Msitu Wa Siri
Sehemu Ya Tatu (3)
huko nyumbani kwa kina david....alionekana paul ameanza kuingiwa na wasiwasi...inamaana mpaka sasahivi david hajarudi atakuwa amepatwa na nini?? alijiuliza paul ambae ni mjomba wake David...wakati huo mama David alikuwa amepumzika chumbani kwake...alikuwa kasinzia kutokana na zile dawa alizopewa kule kituo cha afya zilimpelekea mwili wake kuregea hivyo tangu mda ule alikuwa bado kalala...
**********CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Paul aliamua kurudi kule porini kumtafuta David""",,alimtafuta kwa muda mrefu sana bila mafanikio yoyote....paul aliwaza huenda David labda kaingia kwenye ule msitu ambao ni MSITU WA SIRI"" ,,,watu wa kijiji hicho waliuita msitu huo hivyo...kwa sababu hakuna binadamu yeyote anaejua chochote kuhusu msitu ule...kwa sababu hakuna mtu aliyeingia msituni mule akatoka salama hivyo ilibaki kuwa siri ya msitu...aaah kama atakuwa kaingia msituni mule Masikini David wangu sijui kama Yusalama"",, aliingiwa na wasiwasi akanza kuita kwa kupaza sauti...aliita hivyo mpaka sauti ilikauka....
hatimae alianza kuingia ndani ya msitu ule ili kumtafuta David huenda atamuona
***********
upande mwingine alionekana David bdo yupo ndani kwenye njia ya handaki lile...kwa mbali alianza kuona mwanga"" alipotazama kwa makini aliona ni mwanga wa Jua....akaanza kuzipiga hatua za haraka haraka kuelekea kunako mwanga huo...alipoukaribia aliona njia ikionesha upande wa nje aliona miti alifurahi sana kuisha akaifuata njia ile ili atoke nje....kabla ya kutoka aliona kitu" akakitazama kwa makini ndipo alipoona kiumbe wa ajabu..kiumbe huyo alitisha sana alikuwa anafanana na mti...ukikitazama ni mti kabisa",, lakini alikuwa na umbile la binadamu...nilistuka nikaingiwa na uwoga....huku ikiambatana na vijampo vya mfululizo (phu phu phu) nilijiuliza inamaana hiki ndicho kile kiumbe kilichokuwa kinapita kwa kasi ya ajabu mbele yangu au????kisha nikaanza kuangaza angaza macho yangu nilipo tazama kwa mbali nilistuka kuona mafuvu na mifupa mingi ya binadamu......kisha niliona mti ule ukitembea kuelekea upande niliokuwepo...wakati huu niliweza kuona vizuri mti ule waajabu ulikuwa ukitembea.....niliogopa sana nikajua leo ndio mwisho wa uhai wangu....nikafumba macho...nilipofumbua macho sikumuona kiumbe yule waajabu""" kumbe alikuwa kapitiliza na kuelekea mbele zaidi..niliogopa kutoka kisha nikaamua kubaki hapohapo....nilikaa kwa muda kama wa lisaa limoja nilipoona pako kimya nikaamua kutoka ili niondoke eneo lile"",, kabla sijafanya hivyo. niliona yule kiumbe wa ajabu anarudi huku ameninginiza kiwiliwili cha binadamu...kiwiliwili hicho kilionekana kuanzia upande wa tumboni kuelekea kichwani...bila kuwa na sehemu ya chini yani kiuno na miguu....niliogopa sana."" ,, kiumbe kile kilipokuwa kinasogea nilistuka sikuamini macho yangu kwa kile nilichokiona.....niliogopa zaidi baada ya kuona kiwiliwili hicho kilikuwa ni cha..
niliogopa zaidi baada ya kuona kiwiliwili cha Mjomba.....nilifumba mdomo kwa kiganja changu ili nijizuie kupiga kelele""mwili wangu ulipatwa na ganzi ghafla....nililia kwa uchungu...
""mjomba wangu wa pekee inamaana siokuona tena"" nilijisemea moyoni kishaniliona kiumbe kile cha ajabu nyenye muonekano wa mti...kimerusha kiwiliwili kile cha mjomba paul..kwenye yale mafuvu pamoja na mifupa ya binadamu""' Tiiiii...kisha kiumbe kile kikaondoka.. nilikaa kwa dakika kadhaa pasipo kuona dalili yoyote ya kiumbe kile kurudi eneo"""" lile niliamua kuchoropoka haraka kutoka kwenye handaki lile kisha nikaanza kutimua mbio nilikimbia pasipo kujua naelekea wapi... kwa mbali niliona mtu kalala chini nikaanza kunyata nilipokaribia...nilistuka kuona kiwiliwili ambacho hakuna upande wa juu...yani kuanzia tumboni kuelekea kichwani....nilipotazama vizuri niligundua kuwa ni cha mjomba paul niliogopa zaidi mara ghafla nikasikia kishindo kikubwa nilipotazama niliona kile kiumbe kikija upande wangu....niliogopa nikaanza kutimua mbio......mara ghafla niliteleza nikatumbukia kwenye maporomoko yaliyokuwa yakielekea mtoni... Chubwiii......
********
nilipokuja kuibuka upande wa juu nilikiona kile kiumbe...kilionekana kukasirishwa na kitendo kile cha mimi kutoka eneo lile....niliogelea hatimaye nikatoka kwenye mto ule kwa sababu nilikuwa natumia nguvu nyingi kuogelea nilijikuta nimelala pembezoni mwa kingo za mto huo....
nilipokuja kuzinduka ilikuwa ni usiku...kwa sababu sikuwa na saa hivyo basi sikuweza kutambua kuwa ilikuwa ni sangapi....niliogopa sana nikaamua kupanda juu ya mti mkubwa....
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
************
Kule nyumbani alionekana mama David.....akijiuliza maswali yasiyokuwa na majibu...inamaana mpaka sasahivi Mwanangu David atakuwa wapi?? alijisemea hivyo moyoni""
ni kweli haijawahi kutokea hata sikumoja David kutokuwepo nyumbani mpaka muda huo....mama David akatoka nje kuelekea kwenye nyumba aliyokuwa akilala mdogo wake ambaye ni Paul huku kwa mali zilisikika kelele za ngoma""" ngoma ile iliashiria kuwa kunamtu anaoa siku ya kesho hivyo basi watu huwa hukusanyika kwa pamoja kisha wanacheza ngoma hiyo na kunywa( karinya). yani pombe ya kienyeji""".....mama david alizipiga hatua kwa lengo la kumuuliza paul kuhusu David...alipogonga mlango..........Paul hakuitikia alipotazama vizuri aligundua mlango umefungwa....aliwaza akasema au watakuwa wameenda kwenye Ngoma??? mmh!!!! lakini mbona hawakuniaga?
mama David alibaki na alama ya mshangao kichwani mwake...kisha akarudi ndani....
*********
Kule porini David alipanda juu ya mti.....ili kujipumzisha na kutakapokucha aanze kuitafuta njia ya kurudi nyumbani...kutokana na baridi kali David hakuweza kupata usingizi alibaki macho wazi"" palipoanza kukucha alitelemka chini kutoka juu ya mti ule kisha akanza kuzipiga hatua huku akitazama kushoto kulia nilitembea kwa hatua na macho ya tahadhali..mara ghafla nikaona kunakiumbe kimepita kwa kesi mbele yangu..nilisimama kisha nikaokota kipande kikubwa cha mti...kisha nikajiweka mkao wa tahadhali.....mara ghafla kilijitokeza kiumbe kile""" kisha kikaanza kunifuata pale nilipokuwa nimesimama..... niliogopa nikawa narudi nyuma mara ghafla nikajikwaa kwenye mizizi ya miti nikadondokea makalio....wakati huo mapigo yangu ya moyo yalikuwa yakipiga kwa kasi..niliogopa nikajua leo ndio mwisho wa maisha yangu...kisha kiumbe kile kilisogea mpaka pale nilipokuwa nimeangukia...nilifumba macho kwa kuogopa mara sikuhisi dalili yoyote ya kiumbe kile kunigusa...nilipofumbua macho niliona kiumbe kile kikirudi nyuma huku kikiangalia kifuani kwangu...
nilitahamaki kisha nikajiangalia kifuani kwangu...sikuona kitu zaidi ya Mkufu alionipa bibi....kwa kunivalisha mkufu huo sijawahi kuuvua tangu marehemu bibi aliponivalisha miaka mingi iliyopita...kiumbe kile kilirudi nyuma na hatimae kikatokomea.....nilisimama nikaanza kutimua mbio....nilikimbia umbali mrefu kiasi...niliiona njia ya kurudi nyumbani nilifurahi sana....nilianza kuingiwa na amani na nikapata matumaini ya kurudi salama nyumbani....mara kwa mbali naona watu wakikimbia ovyo kila mtu alipita njia yake......mara ghafla niliona mti ulie umeingia kijijini kwetu..
niliona wanakijiji wakikimbiahuku na huku kila mmoja alipita njia yake....niliingiwa na wasiwasi kuwa mama yanguatakuwa hatarini... nilitimua mbio kuelekea nyumbani..wakati nakimnia watu walinishanhaa..na kuniona kuwa nimechanganyikiwa...kwanini nikimbilie kule kwenye hatari wakati wao wanakimbia kwaajili ya kwenda kujificha ili waokoe usalama wa maisha yao"",,
nilikimbia nikaingia mpaka ndani huku naita MAMA MAMA..... nilipotazama vizuri sikumuona mama nikaamua kutoka nje... nilisikitika sana kuona maiti nyingi za wanakijiji zikiwa zimetapakaa chini kama mchanga"" nilizitazama maiti zile ili niangalie kama miongoni mwa maiti zile huenda nikamuona mama yangu"" nilitazama maiti moja hadi nyingine kwa umakini zaidi...ndipo nikagundua kuwa hienda mama yangu bado Yuhai.....nikakimbia nisijue naelekea wapi....mara kwa mbali nilimuona mama nilifurahi sana nikaita mama kwa kupaza sauti lakini mama hakunisikia kutokana alichanganyikiwa juu ya kiumbe huyu wa ajabu kwa kuuwa watu...
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
******
nilipoona haisikii sauti yangu nikaamua kukimbia kuelekea ule upande aliokuwa mama...mara ghafla nilimuona kiumbe yule akimfuata mama alikuwa nyuma kama hatua kumi hivi...niliogopa sana...nikapaza sauti tena nikaita mama..mama..ghafla kiumbe kile kikaacha kumfaya mama kikasimama..kikageuza shingo kutazama ule upande niliopo...kiumbe yule alinitazama kisha akaendelea kumfuata mama...nilimuonea huruma mama yangu alikuwa anakimbia huku kanga zikimdondoka....
nikatoa mshale nikauweka kwenye upinde nikauvuta kwa nguvu zangu zote huku nikikumbuka mjomba paul alipokuwa akinifundisha jinsi ya kulenga kitu kikiwa mbali bila kukikosa...nilivuta kisha nikaachia mshale ule""" ulienda moja kwa moja mpaka kwenye mgongo wa kiumbe yule...kutokana na umri mdogo niliokuwa nao nilitumia guvu nyingi kuuvita upinde ule na baada ya kuachia mshale nilidondoka chini nikaishiwa nguvu...
"" kiumbe yule alipiga kelele za umivu kwa mngurumo mkubwa sana mpaka nikaogopa....nilikodoa macho nikaona kaacha kumfuata mama yangu kisha akaanza kuja ule upande niliokuwepo...!!!! nilipoona hivyo nilinyanyuka pale chini nikaanza kutimua mbio kuelekea kwenye nyumba yetu..niliiparamia mlango nikaingia ndani na kujifungia....
nilisikitika sana kuona nyumba yetu iliezekwa kwa nyasi hivyo itakuwa rahisi kiumbe yule kuninasa....pia niliwaza kama akifika hapa atahadibu nyumba ili aninase hivyo nyumba itabomoka na tutakosa makazi ya kuishi.....
********
baada ya kuwaza hivyo niliamua kufungua dirisha ili nitoke nje...kutokana na dirisha kuwa juu sana nilishindwa....nikaamua kutoka nje kwa kupitia mlangoni....nilipotazama mbele yangu niliona kiumbe yule wa ajabu kakaribia kabisa hakuwa mbali na nyumba yetu...nilitimka mbio hata sijui naelekea wapi!!!!!
wakati nakimbia niliwaza nikimbilie msituni nikajifiche...kiumbe yule wa ajabu atanifuata""hivyo mama yangu pamoja na wanakijiji watapata muda mzuri wa kutafuta maficho wajifiche pia nitakuwa nimeokoa maisha ya wanakijiji waliobakia....
*********
nilikimbia huku napumua pumzi ya kutweta na mapigo yangu ya moyo yaliongezeka kupiga kwa kasi..niligeuka nyuma kutazama yule kiumbe yupo umbali gani nilistahajabu sikumuona kiumbe yule...nilipoona hivyo nikaongeza kasi ya kukimbia...ghafla alijitokeza mbele yangu...nilitoa mshale haraka nikauweka kunako upinde na kuachia mshale ule...ulikwenda moja kwa moja mpaka kwenye jicho la upande wa kushoto mwa kiumbe huyo...alipiga kelele zenye mgurumo mkubwa mpaka ndege waliokuwepo juu ua mti walionekana wakiruka kukimbia mngurumo ule..
kisha kiumbe yule alikimbia na kutokomea...nilijipa moyo nikajisemea moyoni kumbe dawa yako ni mshale jitokeze tena uone....kisha nikatoa mshale mwingine nilipogusa kwa juu kwenye PODO ile ya kubebea mishale niliishiwa nguvu baada ya kuona ulibakia mshale mmoja pekee... kumbi kipindi nakimbia mishale mingine ilidondoka.....
wakati bado nimesimama naangaza angaza macho huenda kiumbe yule labda atajitokeza...ghafla niliona JOKA kubwa likitokea kichakani mwiliwangu ulisisimuka kwa uwoga nikapiga hatua kurudi nyuma huku namshangaa nyoka yule kwa ukubwa alionao""CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nilijikwaa kwenye kipande cha mti uliokuwepo chini nikadondoka..kumbe kipindi nadondoka ndio wakati kiumbe yule alikuwa akinirukia ili atenganishe kiwiliwili changu kati kwa kati...alijigonga kwenye mti mkubwa uliokuwa pembeni yangu...kisha mti ule ukavunjika na kudondoka chini.. nilinyanyuka pale chini na kianza kutimua mbio nilikimbia kwa kasi hata sikujua naelekea wapi"" nikaona kichaka nikakivaa kichaka kile bila kujali"" kichaka kile kilikuwa na miba mirefu lakini sikuwwza kusikia maumivu miba ilipotoboa ngozi yangu kwa wakati ule..
******
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment