Search This Blog

Thursday, 2 June 2022

SAFARI YA MSITU WA SIRI - 4

 





    Simulizi : Safari Ya Msitu Wa Siri

    Sehemu Ya Nne (4)



    niliingia katikati kisha nikatulia tuli"" nilikaa kama dakika kadhaa sikusikia kitu chochote upande wa nje....nikaangaza angaza macho huenda nitaona upenyo wa kuona nje...gjafla nilimuona kiumbe yule kajitokeza huku akiangaza angaza macho uake huku na kule...alionesha kukata tamaa..niliona anainua mkono wake uliojaa matawi ya mti mkavu..kisha akaupeleka mpaka usoni akashika ule mshale niliomlenga jichoni..akauchomoa...alipiga kelele safari hii mngurumo uliongezeka..niliogopa sana nikaona anavunja miti iliyokuwa karibu yake...

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    nilijiuliza atakuwa amekasirika baada ya kunikosa eneo lile ndiyo maana anavunja miti.??



    niliogopa nikaanza kutokwa jasho...nilihisi joto kali sana wakati porini humo kulikuwa na upepo mwanana kutokana na miti mikubwa....nilijiuliza kiumbe huyu atatoka mda gani eneo hili ili niweze kuchoropoka hapa nikimbie nirudi nyumbani..."" kila nikichungulia sioni dalili yoyote ya kiumbe yule wa ajabu kuondoka eneo lile...niliishiwa nguvu nikakosa tumaini nilipochungulia nikaona amekaa...ingawa alikuwa amekaa lakini bado alionekana mrefu sana!!! mikono yake ilienea matawi yaliyoonekana kama yapo kwenye mti mkavu....kalikuwa na sura ya kutisha na macho yake yalikuwa mekundu...ukimtizama kwa harakaharaka unaweza ukasema ni mti..lakini alionekana kuwa na umbile la binadamu..



    niliwaza sana nini cha kufanya pia nilikuwa nahisi njaa kali..nilihisi kunamtu tumbini mwangu ananikatakata na kiwembe kwa jisi tumbo lilivyokuwa likiuma njaa...nikapata wazo kuwa nilibakiza mshale mmoja hivyo niurushe upande mwingine mshale ule...yule kiumbe akisikia kitu kinapita katika matawi ya miti ataondoka na kwenda ule upande aliosikia matawi ya miti yakitikisika na kutoa sauti...

    nilichukuwa mshale ule mmoja uliobaki taratibu nikauweka vyema kunako upinde kisha nikauvuta upinde na kuachia mshale juu ya matawi ya miti...mshale ule ulipokuwa unakwenda kwa kasi ulipita kwenye matawi ya miti na matawi yalitoa sauti kama kunamtu anakimbia huku matawi yakigusa mwili wake...

    kiumbe yule aliposikia hivyo"" ghafla alisimama na kuanza kukimbia muelekea ule upande niliorusha mshale...nilipohakikisha kiumbe yule yupo mbali nilitoka huku nazipiga hatua za kunyata kutoka kwenye kichaka kile miba ilinichoma lakini sikusikia maumivu...acho yangu niliyakodoa kwa makink kuangalia ule upande ambao kiumbe yu alielekea...



    ********



    Upande mwingine kule kijijini"" wanakijiji walionekana wakilia kwa huzuni kubwa ya kuwapoteza ndugu jamaa na marafiki"",, wanakijiji wengine waliendelea kujitokeza kutokea mafichoni"" mama yake David alikuwa akilia kwa uchungu juu ya mwanae David ......jamani mwangu Davi sijui kama nitakuona tena......kama utakuwa umekufa angalau tu japo nione maiti yako"""" uliniahidi utakuwa tegezi langu nitabaki na nani mie"" aliongea maneno hayo kwa uchungu huku akilia...kutokana na maradhi ya shinikizo la Damu ya kupanda yaliyokuwa yakimsumbua mama david na mawazo juu ya mwanae wa pekee..mama David alipoteza fahamu na kuanguka chini...

    hakuweza kupata msaada wowote alikuwa yeye peke yake mdani....

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *******



    kule porini David alinyata kwa hatua kama tatu hivi kisha akaanza kutimua mbio kwa kasi..alikimbia huku anatafuta njia ya kurudi nyumbani......alikimbia jasho lilimtoka aliona hata ule upinde hauna msaada tena kwake hivyo aliutupa... wakati anakimbia huku anaangalia kushoto kulia huenda akaweza kuona njia ya kurudi nyumbani....aligeuka nyuma kutazama labda kiumbe yule anamfuata...alipo geuza shingo kuangalia mbele ghafla alijingonga katikati ya paji la uso kwenye mti mkibwa uliokuwa mbele yake

    kisha akapasuka usoni akadondoka chini na kupoteza fahamu...



    *********



    kule kijijini watu walilia sana kila nyumba kulikuwa na msiba...inasikitisha sana kiumbe huyu hata hana huruma kwa watoto wadogo...tazama mwanangu kafa eee Mungu ulie juu tunakuomba utuepushie mbali maafa haya uwiii""" alisikima mama mmoja akilia kwa uchungu huku kamkumbatia binti yake wa miaka mitatu akiwa ameuwawa kwa kukanyagwa na yule kiumbe wa ajabu na kupasuka kichwa kabisa......



    Nyumbani kwa kinaDavid alionekana mama David bado yupo chini kapoteza fahamu...wakati akiwa katika hiyo hali ya kutokuwa na fahamu aliona vitu vingi alimuona mumewe enzi za uhai wake alimuona marehemu mama yake enzi za uhai wake kisha akamuona david akitafunwa na kiumbe yule wa ajabu alipiga kelele akimwambia yule kiumbe usimuuwe mwanangu...mara ghafla akastuka akapata fahamu..



    *******



    kule porini wakati huohuo aliozinduka mama David ndio wakati aliozinduka David....kisha David alibaki kalala hapo chini akitafakari ni nini kimemtokea..alihisi maumivu kwenye paji lake la uso alipojigusa sehemu ile aliona damu zikimtoka.

    UTATA UKAANZA.



    Ndipo kumbukumbu zikarejea alistuka sana...David alinyanyuka pale chini alipokuwa ameanguka na kupoteza fahamu kisha akaangaza macho huku na kule""" sehemu ile kimya kilitawala haikusikika sauti yoyote zaidi ya sauti za milio ya ndege wa porini....alianza kukimbia huku akiangalia mbele...huku macho yake yalikuwa yakitazama kwa tahadhali kubwa....alitafuta njia ya kuelekea nyumbani lakini hakufanikiwa kuipata....kutokana na njaa kali aliyokuwa naya David alipunguza kasi ya kukimbia na hatimae alianza kutembea lakini kwa tahadhali kubwa...."" ,, akili yake yote iliwaza nyumbani,, alikuwa akimfikiria sana mama yake...mama yangu sijui anaendeleaje? akiwa anatembea kwa mwendo wa kujivutavuta kama gari bovu...njaa ilimzidia hakuweza tena kuendelea kutembea alijisogeza chini ya mti mkubwa akaketi chini ya mti huo..kwa mbali aliona mti wa MKOMA"" alipotazama kwa makini juu ya mti ule aligundua kuwa mti ule ulikuwa unamatunda alinyanyuka pale chini kiufuata mti ule..aliupanda mpaka juu kisha akuchuma matunda na kuanza kula...alikula matunda yale kwa pupa alichuma moja baada ya jingine mfululizo alipohisi kuwa kashiba aliamua kupumzika huko huko juu ya mti""" mara ghafla mvua ikaanza kunyesha... kutokana na miti mikibwa kwenye pori hilo"",,,hivyo mvua ilinyesha kwa wingi mule porini....mvua hiyo iliambatana na upepo mkali sana na ngurumo za radi...David aliogopa sana alikumbatia tawi la mti huku mvua ikimnyeshea...mvua hiyo ilinyesha mfululizo bila kukata..na baada ya masaa mawili upita Bariri lilimzidia David hivyo hakuweza kuendelea kukaa kule juu ya mti aliamua kushuka mpaka chini alitafuta kichaka mara akakiona....alikimbia na kuingia ndani ya kichaka kile...kwa sababu matawi yalibanana kwenye kichaka kile hivyo basi,, maji hayakuweza kupenya kwa wingi kuingia ndani ya kichaka kile...ingawa yaliingia lakini siyo mengi kama ilivyokuwa kule juu ya mti"""

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ************



    upande mwingine""" kule nyumbani mama David alipata wasiwasi sana baada ya kuzinduka...mvua ile iliyokuwa ikinyesha ilimfanya awe na hofu juu ya mwanae david""" kisha akachungulia ule upande ambao pori lilikuwepo alistahajabu kuona mvua kubwa huku ukungu umetanda porini kule...ukungu ule uliweza kufunika hata miti isionekane kabisa....mama David alizidi kuogopa kwa sababu alimuona mwanae alikibilia porini huku akifuatwa kwa nyuma na yule kiumbe wa ajabu....jamani mwanangu sijui utakuwa na hali gani huko ulipo Davi wangu...nakuonea huruma sana mwanangu kwa nini unapata mateso haya angali ukiwa bado kijana mdogo.. Eee Mungu baba muhepushe mwanangu najambo lolote baya litakalo mkuta huko porini....mama david aliyasema maneno hayo huku akilia kwa uchungu mkubwa...kisha akaanza kusali..alipo maliza tu kusali ghafla mvua ile ilianza kupungua na ikakata kabisa....



    ********



    kule porini david alionekana bado yupo ndani ya kichaka kile kutokana na baridi kali david alitetemeka sana huku midomo yake ikijipigapiga kama mtu anayetafuna kitu ndani ya mdomo!!!!

    ingawa mvua ilikuwa imeacha kunyesha lakini david bado aliendelea kuwemo ndani ya kichaka kile wakati huo ilikuwa majira ya jioni..kutokana na wingu kubwa lililokuwa limetanda juu ya anga wingu hilo lilifanya kuonekane jioni zaidi kuelekea giza kuanza kuingia...David alitoka mdani ya kichaka kile kwa lingo la kuitafuta njia ya kurudi nyumbani alipotoka tu!!!"",,, ghafla alikutana uso kwa uso na kiumbe yule wa ajabu..



    macho yalimtoka David mapigo yake

    ya moyo yakaanza kupiga kwa kasi ya ajabu......aliogopa sana alihisi hajakubwa inamtoka....jasho lilimtoka wakati kulikuwa na baridi"" alijisemea moyoni laiti kama kiumbe huyu angejuwa nilivyochoka,,,angejua mama yangu bado ananitegemea,,, basi angenionea huruma angenibeba akanipeleka nyumbani kwetu.....wakati David anawaza hivyo"""" yule kiumbe wa ajabu alizipiga hatua kuelekea pale alipokuwepo david...""" kiumbe yule alimtazama David kwa macho ya umakini sana alijiuliza je? huyu ni nani aliyenisumbua kwa muda mrefu!!!!! kiasi hiki

    wakati huo david hakuwa na hata chembe ya hamu ya kukimbia kwa sababu alijua huo ndio mwisho wa maisha yake alianza kusali akimuomba mungu wake amsaidie....kiumbe yule alisogea mpaka akawa jirani kabisa na david alipomkaribia alimshika shingo kisha akamnyanyua... david...""",,david macho yalimtoka kutokana na mkono wa kiumbe yule aliukaza shingoni hivyo david alivuta pumzi kwa tabu....wakati huu david hakuogopa tena alikuwa tayari kwa lolote. aliamini hana ujanja tena....huo ndio utakuwa mwisho wa maisha yake.....



    ************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kule nyumbani mama david alikuwa na wasiwasi na uwoga ukatawala juu yake...alikuwa akimuwazia sana mwanae david baada ya kuona giza linanyemelea kuingia alafu david bado hajarudi nyumbani....mbaya zaidi hajui ni wapi alipo na je yupo salama?? Jamani mwanangu sijui uhali gani huko uliko alijisemea mama david huku machozi yakimtoka...aliamua kutoka nje aangaze angaze macho huenda atamuona david anarudi nyumbani"" mama david alikata tamaa akaamua kurudi ndani akaanza kusali alimuomba mungu amnusuru david asipatwe na jambo baya aweze kurudi nyumbani akiwa salama...

    baada ya kumaliza kusali..aliketi kwenye stuli akingojea huenda david akarudi...pia aliwaza kuhusu mdogo wake paul sijui atakuwa kaenda wapi ni siku ya pili sasa hajaonekana nyumbani!!!mama david hakuwa na amani mule ndani aliamua kutoka nje kisha akaanza kuzipiga hatua kuelekea kwa jilani yake.....alipofika alikuta familia ile ikiwa katika majonzi ya mtoto wao mdogo kufariki....jilani huyo ni yule mama aliyekuwa akilia kwa uchungu baada ya binti yake wa miaka minne kukanyagwa na yule kiumbe wa ajabu alipoingia kijijini hapo na kumkanyaga akapasuka kichwa...mama david alimuone huruma mama yule alikuwa akilia kwa uchungu mkubwa sana....kiasi ambacho alilia masaa mengi sana hivyo machozi hayakutoka tena....mama david alisikitika sana....hiyo iliamfanya na yeye kuanza kulia juu ya mwanae david..



    *********



    ule upande ule wa porini ,,""yule kiumbe wa ajabu bado alikuwa kamning'iniza david juu huku kashikiria baraabara kunako shingo ya david... kiumbe yule aliendelea kumtazama david kwa umakini wa hali ya juu ili aone ni nani huyu!!! na kwanini kanisumbua sana mpaka kusababisha nimepoteza jicho langu moja....baada ya kiumbe huyo wa ajabu kuwaza hivyo alimrusha david kwenye miti kisha david akadondoka chini akiwa hoi taabani""" kisha kiumbe yule akazipiga hatua kuelekea kule ambapo david kadondokea....alipomkaribia david alistahajabu sana baada ya kuona kiumbe yule anazipiga hatua kurudi nyuma huku akionekana kuingiwa na uwoga.....wakati david akiendelea kumtaza kiumbe yule wa ajabu alijiuliza je anataka kufanya nini!!!! mbona anarudi nyuma!!!? "" kumbe wakati david anakimbia kujihifadhi kwenye kichaka kile kwa ajili ya kujikinga mvua mkufu wake ulikatika na kuanguka chini kipindi anashuka juu ya mti ule wa matunda""" mkufu ule ulinasa kwenye tawi bila david kujua""""" ulikatika na kudondoka...kwa sababu david alichanganyikiwa na baridi lililompiga ukichanganya na ile mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha hakuweza kutambua kuwa mkufu ule haukuwepo shingo mwake.....



    ***********



    kiumbe yule wa ajabu alirudi nyuma baada ya kuona ule mkufu pale chini...kumbe kipindi anamrusha david aliangukia karibu na ule mkufu....hivyo David hakuweza kuuona mkufu huo kutokana na mawazo na cho yake yalikuwa yakimtazama kiumbe yule...

    kiumbe yule alizidi kurudi nyuma kisha akaanza kutimua mbio na kutokomea kusiko julikana..

    David alijiuliza sana kwani kaona nini mbona kakimbia!!!? kisha akanyanyuka na kuanza kutimua mbio huku ukono wake mmoja umeshikilia upande wa mbavu zake za kushoto.....hakuweza kuuchukua mkufu ule kwa sababu hakuuona....

    alitimua mbio mpaka akaanza kutoka nje kabisa ya msitu ule......kwa mbali alianza kuona mwanga alipotazama vizuri aligundua mwanga ule ni taa aina ya koroboi....aliona mwanga huo kupitia kwenye madirisha ya nyumba.....hapo akagundua kuwa hayupo mbali na kijijini kwao....aliendelea kutimua mbio bila kusimama...CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    hatimae akafika nyumbani.....alikuta mlango umerudishiwa tu...haukufungwa kwa komeo aliusukuma na kuingia ndani alistahajabu kukuta ukimya umetawala ndani humo.....aliita mama"" lakini mama yake hakuitika....alichukua kiberiti akawasha koroboi....alipomulika chumbani kwa mama yake aligundu mama yake hayupo...alistuka sana... alipapasa shingoni hakuona mkufu ule aliovalishwa na marehemu bibi yake"""" wakati akijiuliza umkufu huo utakuwa umedondokea wapi mara ghafla....



    ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

Blog