Simulizi : Safari Ya Msitu Wa Siri
Sehemu Ya Tano (5)
Mara ghafla mlango ulisukumwa kumbe alikuwa ni mama ya david...alikuwa anaingia ndani""" ni baada ya kutoka kule kwenyenyumba ya jilani..alikuja anakimbia kwa shauku ya kutaka kumuona mwanae yupo katika hali gani.....bila shaka huyu aliyewasha koroboi ni David"" alijisea moyoni huku anaipiga hatua ya mwisho kuingia ndani...alifurahi sana akamkumbatia mwanae....pia david alifurahi sana kumuona mama yake kwa mara nyingine tena......mama david alilia kwa furaha hakuamini kama mwanae angerudi salama kutoka mikononi mwa kiumbe yule wa ajabu.kisha aliingia haraka chumbani akachukua matunda na kumpelekea mwanae..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
aliamini kuwa david hajala kitu chochote tangu alipomkimbia kiumbe yule wa ajabu na kutokomea porini..David aliyapokea matunda yale...alianza kuyashabulia kama ngedere kaona tunda la msimu. kisha david akaanza kumsimulia mama yake yale yaliyomkuta huko porini"",, mama yake alikuwa akimtaza david kwa sura ya upole na macho ya huruma...kisha akanyanyuka na kutoka nje. alichukuwa maji na kuyapeleka bafuni...alipomaliza kumuandalia david maji ya kuoga alirudi ndani...wakati huo david alikuwa ameshamaliza kuyala matunda yale...mayake alimwambia nenda kaoge nimeshakuwekea maji kule bafuni....david alimtazama usoni mama yake kisha akajisemea moyoni "NANI KAMA MAMA!!! hakika wewe ni mtu bora kwangu...mekuwa ukinijali na kunipenda sana...nakuombea kwa Mungu akupe maisha marefu...nakupenda sana mama....kisha david akanyanyuka na kuelekea bafuni
Baada ya kumaliza kuoga alirudi ndani alipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwake kisha akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi....kutokana na uchovu aliokuwa nao.. hazikupita dakika nyingi....alisinzia
**********
Asubuhi palipokucha David alidamka mapema na kuanza kumsaidia mama yake kazi ndogondogo"",, alichukua shoka na kuanza kupasua kuni wakati anapasua kuni alikuwa anaimba wimbo.....""wimbo ule ni wimbo aliokuwa anapenda sana kuuimba marehemu bibi yake....aliendelea kupasua kuni kwa kutumia shoka...alipomaliza aliingia shambani akaanza kuchimbua viazi vitamu ili mama yake akiamka avipike kwa ajili ya chai ya asubuhi.......baada ya kumaliza kuchimba viazi vile alitoka shambani akaelekea jikoni kisha akatika na mfuko akarudi shambani ili kuvikusanya vile viazi alivyovichimba kisha alivipeleka jikoni""""" kisha alichukuwa madumu mawili yenye ujazo wa lita 20 pamoja na jagi akaanza kuzipiga hatua kuelekea kisimani.....wakati akiwa njiani alipata wazo kuwa kisimani ni mbali sana ni kama kilomita mbili hivi"""
wanakijiji walipenda kuchota maji ya kisima hicho kwa sababu yalikuwa masafi kupindukia....kuliko maji ya MTONI.......lakini kutokana na umbali hivyo David aliamua kuelekea MTONI kwa ajili ya kuteka maji...
alipofika hakutaka kuchelewa alianza kuchota maji kwa kutumia jagi na kuyamimina ndani ya dumu.....kutokana na maji ya mwanzoni kuwa machafu aliamua kukunja suluali na kuingia ndani ya MTO kama hatua kadhaa.....alichota maji na kuyamimina ndani ya dumu....alifanya hivyo mpaka dumu la kwanza likajaa kisha akalinyanyua na kulipeleka nchi kavu"",, akachukua dumu jingine na kuelekea tena MTONI .......alianza kuchota maji na kuyamimina ndani ya dumu.....mara ghafla aliona mamba anakuja kwa kasi ya ajabu mamba yule alionekana alikuwa na njaa kali sana!!!! David alianza kutimua mbio kutoka MTONI humo ingawa hakuwa mbali sana na nchi kavu...alitumia nguvu nyingi kukimbia kutokana alikuwa ndani ya maji hivyo hakuweza kukimbia kwa kasi...alitazama nyuma ili kuangalia mamba yule kafika umbali gani kutoka pale yeye alipo...ghafla aliteleza kwenye jiwe lililokuwemo ndani ya maji akadondoka tubwiii!!!!! Mara ghafla David alipiga kelele
david alinyanyuka haraka akakimbia.....alitumia nguvu nyingi sana kwa sababu alikuwa anakimbia ndani ya maji...yule mamba alikata tamaa baada ya kuona windo alilokuwa akiliwinda limeshatoka ndani ya maji na kukimbilia nchi kavu....David alikimbia umbali kama wa mita mia sana na urefu wa kiwanja kimoja cha mpira wa miguu..kisha alisimama na kugeuka nyuma....hakuamini kilichotokea.....alikuwa akitetemeka kutokana uwoga wa hali ya juu..huku haja ndogo ikimtoka mfululizo....alirudi kuchukua lile dumu lililokuwepo mchi kavu"" ni dumu lile alilolijaza maji mara ya kwanza kisha akalipeleka nchi kavu.....hakutaka kuchelewa alilibeba na kuliweka begani kisha akaanza safari ya kurudi nyumbani.....haikumchukua muda sana akawa amefika....alimkuta mama yake ameshamuandalia chai na viazi vitamu....""" david hakutaka kumsimulia mama yake kile kilichotokea"",,, kwa sababu alijua mama yake ana shinikizo la damu ya kupanda na kushuka...hivyo kama angemsimulia huenda yakatokea mambo mengine.....alikunywa chai na baada ya kumaliza.....ataka kwenda porini kiwinda lakini alikumbuka upinde wake aliutupa baada ya kuchanganyikiwa juu ya yule kiumbe wa ajabu kule kwenye msitu wa siri...""" david alifadhaika sana alianza kumkumbuka mjomba wake kisha akawaza sijui nimwambie mama kama Mjomba Paul kauwawa na yule kiumbe wa ajabu!!!!! hapana sio leo ipo siku nitamwambia...alijisemea hivyo moyoni....
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**************
kule upande wa jikoni mama david alionekana akizichochea kuni kwenye jiko la mafiga matatu...
mama david alichukua picha mbili kisha akaketi kwenye stuli alizitazama picha zile huku sira yake ikionekana kuwa na majonzi""",, ni picha ya marehemu mume wake..na ile picha nyingine ni picha ya marehemu mama yake.....wakati akiangalia picha hizo david alikuwa akizipiga hatua kuelekea ule upande wa jikoni alipokuwa mama yake...david alifanya hivyo baada ya kumuona mama yake kashikilia zile picha hivyo alijua mama yake huwa anaangalia picha hizo pale anapokuwa na mawazo....hivyo david alienda pale ili kumfariji mama yake...alipodika alianza kucheza bila muziki wowote alicheza mama yake alipomtazama alicheka sana kisha akamwambia yani unavituko kama marehemu baba yako....alikuwa mcheshi sana """alisema mama david huku akitabasamu....kisha david akamkaribia na kumkumbatia.....ghafla david alijipapasa shingoni""" ni baada ya kuiona ile picha aliyokuwa ameishikilia mama yake kwa mkono wa kulia ni picha ya bibi yake....david ilibidi amueleze mama yake...""mama mkufu wangu alionivalisha marehemu bibi ulipotelea kule mstuni.....alafu bibi aliniambia nisiuvue mkufu huo na popote niendapo niwenao......alisema eti mkufu ule ni hazina ambayo nilisubiliwa niwe mkubwa nipewe...ndio maana bibi alinivalisha....
*******
Mama david alistuka....aliona david akivalishwa mkufu ule lakini hakujua maana yake ,,,yeye alijua ni zawadi tu ambayo bibi yake kajisikia kumpa mjukuu wake.....kisha kumbukumbu ikamrudia alikumbuka miaka ya nyuma kipindi cha usichana wake miaka 30 iliyopita...sikumoja alitoka shule na kumkuta bibi yake david ameanguka shambani na kupoteza fahamu.alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kuanguka kifafa.........mama david alikimbia mpaka kwa jirani kuomba msaada lakini hakukuta mtu yeyete katika nyumba ile ya jirani....aliamua kurudi haraka mpaka kule shambani alipokuwepo bibi yake david
ghafla alikuta kazinduka huku kashika mkufu...mama david alistahajabu sana kwani hakuwahi kumuona mama yake na mkufu huo...alipomuuliza mama huo mkufu umeutoa wapi....bibi yake david alimwambia hata mimi sijui lakini kipindi nipo katika hali ya kutokuwa na ufahamu nilimuona babu yako..kisha akanipa mkufu akasema ni kinga...."""kinga hii nije kumpa mjukuu wangu.......wa kiume atakaye zaliwa....ni hazina
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**********
baada ya kumbukumbu hiyo kumrudia mama david ilibidi amwambie ukweli mwanae kuhusu mkufu huo..david baada ya kusikia hivyo alistuka kisha akajisemea moyoni liwalo na liwe kama ni kinga lazima nirudi kule mstuni nikautafute mkufu....
david alinyanyuka bila kumuongelesha mama yake kisha akaanza kuzipiga hatua....jamani mwanangu unaenda wapi!!!? nakusihi usiende kule mstuni yule kiumbe wa ajabu atakudhuru!!!! david aligeuka nyuma kisha akajibu kwa sauti ya upole samahani mama yangu kipenzi lazima niende..kisha akaanza kutimua mbio kuelekea mstuni......alikimbia na baada ya muda alianza ukingia kabisa kunako msitu wa siri ni msitu ambao hakuna binadamu anayejua kuna nini ndani yake kwa sababu hakuna mtu wala mnyama aliye wahi kuingia mstuni humo kisha akatoka hai....
wakati david anazipiga hatua huku macho yake yakiwa makini kutazama chinini huenda atauwona mkufu huo aisee hakuamini kilichotokea mara ghafla..
david hakuamini kilichotokea....alikutana uso kwa uso na kiumbe yule wa ajabu... david aliogopa alibuni mpango wa kumtoroka kiumbe yule.... najuta kwa nini nimerudi huku porini"" alijisemea David aligeuka nyuma na kuanza kutimua mbio kurudi alipotoka"" baada ya hatua kadhaa alistuka alisita kukimbia akasimama,, kumbe aliuona ule mkufu ukiwa chini alifurahi sana akauokota kisha akaendelea kutimua mbio.... mara ghafla yule kiumbe wa ajabu alitokezea mbele yake huku sura yake ikionekana kujawa hasira za hali ya juu....david alikumbuka maneno ya bibi yake kwamba mkufu huo asiuvue awenao popote pale aendapo ni kinga kwake...punde kiumbe yule alimnasa david na kumpiga kwa kutumia mkono wake uliojaa matawi kama mti....david alirushwa na kipigo kile akadondoka mbali damu zilimtoka puani na mdomoni alipotaka kunyanyuka alishindwa.. kiumbe yule wa ajabu alimsogelea david kisha akamnyanyua na kumrusha kando...kisha kiumbe yule wa ajabu akazipiga hatua kuelekea kule alipodondoka david.. alimnyanyua mpaka juu jirani kabisa na uso wake.... alimtazama kwa jicho lake moja lililobaki... kisha akamrusha mbali david alidondoka na kutumbukia nda na shimo"""" ni shimo lile alilotumbukia mara ya kwanza siku ile kipindi anakimbia... david alipofika upande wa chini ndani ua shimo hilo alipoteza fahamu....
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**********
kule nyumbani kwa kinaDavid alionekana mama david akimuomba Mungu amnusuru mwanae David...
Mara ghafla david alipata fahamu"" alipoangaza angaza macho aligundua kuwa shimo hilo ndio lile shimo alilotumbukia sikuile hivyo basi anaijua njia ya kutokea upande wa nje. aliponyanyuka alihisi maumivu makali kichwani... alijikongoja kuifuta njia iliyokuwa chini kwa chini ya aridhi alifanikiwa kuona ule upenyo wa kutokea upande wa nje... alitoka kisha akaanza macho yake huku na kule....alipohakikisha kua yule kiumbe wa ajabu hayupo eneo hilo aliamua kutimua mbio.. alitimua mbio bila kujua ni wapi anaelekea... alikimbia umbali mrefu mara akaanza kutoka nje ya msitu huo...alifurahi sana"""mara ghafla kiumbe yule wa ajabu alijitokeza mbele yake david alistuka sana haja kubwa ikamtoka kwa uwoga wa hali ya juu...david alipotaka kutimua mbio kiumbe yule alimnasa david...... alipotaka kuuvaa mkufu ule ulimponyoka na kudondoka chini... kumbe kipindi mkufu huo unadondoka uliangukia kwenye mguu wa kiumbe huyo wa ajabu"""ghafla kiumbe yule alimuachia david...kisha kiumbe yule alianza kupukutika kama vumbi iliyokung'twa kwa kitambaaa... alipukutiaka mpaka akaishilia.. ghafla msitu ule ulibadilika giza lililokuwa limeufunika msitu ule lilipotea pakawa na nuru....wanyama walionekana ndani ya msitu ule hata kule kijijini nuru ile ilionekana kule mstuni.... David alistahajabu sana aliuokota mkufu wake na kutimua mbio kurudi nyumbani kwao..
punde alifika nyumbani akamsimulia mama yake yote yaliyotoke huko mstuni... mama yake alifurahi sana... david alipotoka nje alikuta mkusanyiko wa wanakijiji upande wa mbele wa nyumba yao walipomuona david walisema kwa kupaza sauti
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
DAVID SHUJA..DAVID SHUJAA ...DAVID SHUJAA.....
**************************************************
***MWISHO**
0 comments:
Post a Comment