Search This Blog

Thursday, 2 June 2022

TETEMEKO LA MOYO - 3

 





    Simulizi : Tetemeko La Moyo

    Sehemu Ya Tatu (3)



    kama yule kwenye maisha yangu.

    Hakika kaka Eddy alikuwa mtu bora sana kwenye maisha yangu si kwangu tu mama, hata wewe kwako!”. Mama aliendelea kunisikiliza kwa makini mno na namna yale maneno yalivyokuwa yakinitoka ndani ya kinywa changu, yalionekana wazi wazi yalikuwa yakimchoma mama na kumkumbusha mbali.

    Niliendelea kuongea ila hali ya mama alianza kubadilika kidogo kidogo, katika namna ambayo sikuitegemea kabisa ndugu msikilizaji.

    ENDELEA.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yale maneno hayakuwa msumali tu kwangu na kumbe yalikuwa ya kichoma choma vibaya mno, namna nilivyokuwa nikiyaongea nilishangaa mama machozi ya kimtoka. Nilisita kidogo kumalizia yale maneno ambayo yalikuwa yakinitoka hata sikujua kama niliyapangilia ama la maana niliona yanakuja kwenye kinywa changu na kuyatamka tu.

    Nilikuwa kimya kidogo, nikiwa na mtazama mama kwa makini, nikitaka kusema jambo tena, ila kabla sijasema. Mama aliianza kuongea, maneno ambayo hakika sitakuja kuyasahau kabisa, najua mama yangu alikuwa akijua nini alichukuwa anakisema. "Criss mwanangu we ni tegemeo langu sana kwa sasa we ndio maisha yangu hakika mwanangu naomba uwe mbali sana na wanawake na kama utashindwa baba, kwa sababu najua sasa umekuwa mkubwa kwa sasa, basi baba yangu naomba ufanye uchaguzi sahihi. Yote kwajili ya maisha yako mwanangu nakupenda sana sipendi nikiona unapata tabu kama kaka yako Eddy.



    Sijui nini kilimtokea hakuwa mtu,wanawake tulimlea vizuri sana mimi na marehemu Baba yako. katika misingi mizuri ya dini kama tulivyokulea wewe, lakini baba kupenda hakuna mwenyewe upendo wa kimapenzi unakujaga pasipo mwenyewe kutegemea. Alisita kidogo mama huku akinitazama, nikiwa kimya tu. Macho yangu yaliweza kubainia maneno yake yalikuwa yana maana kubwa sana katika maisha yangu.



    Mama hakuishia hapo aliendelea baada ya kunitazama kwa muda kidogo “Siwezi kumlaumu kwa jambo hilo na jua Bibilia inasema vyema Mungu alituleta dunia kwa jili ya mapenzi yake, nasi hatuna budi tupendane, tuzaliane ilituijaze dunia.

    Ila mwanangu chunga mwanamke utayekuja kumpenda hakikisha ni wa namna tofauti na mwenye upendo wa dhati na wewe. Mama akuishia hapo,mara aliniuliza swali ni nikabaki nakodoa macho huku nikiliona nilikuwa katika mtihani mzito sana katika maisha yangu.

    Sikuwa na la kujibu maana sikuwa na jua juu ya jambo lile, halikuwa swali lingine bali lilikuwa likiwa likimuhusu kaka Eddy. Nilitulia ndugu msikilizaji nikabaki kimya, kabisa kimya ambacho kilifukuzwa na maneno ya mama, huku akiyatalawa mazungumzo kwa kiasi kwamba nilibaki kuwa msikilizaji.

    “Sikiliza mwanangu Criss, katika maisha ya kaka yako Eddy yana Siri nzito juu ya ndani yake, lakini kwa sasa sidhani kwa wakati wake wa wewe kuijua siri hiyo, wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi. lakini kwa si kwa sasa hivi nitakuwa na kubebesha mzigo sana na chuki zisiokuwa na sababu cha msingi mwanangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mama aliongea kwa hisia mno sana, maneno yale, niliyapokea katika mtazamo ulijaaa kidadisi kama kawaida, sikuiacha hiyo tabia yangu. Juu ya neno siri tena si siri ya kawaida ni nzito kidogo jambo ilo lilinza kuleta walakini kidogo ndani ya kichwa changu. Jambo gani hilo lililojificha juu ya kaka Eddy?, sasa ukawa mtihani ndani ya kichwa changu huku nikihitaji majibu yenye tija juu ya jambo lile huku likionenakana muhimu sana katika maisha yangu maana mama alishawaniambia lazima angeweza kuniambia lakini si kwa mapema kama shauku yangu ya kutaka kufahamu lile ilivyokuwa ikiniongoza.



    Jina la Irine likarudi kichwani kwangu, ndugu msikilizaji, ni huyo Irine ambaye niliweza kufahamu kwa uchache yalikuwa yakimuhusu japo kuwa sura yake ilishapotea siku nyingi kichwani mwangu. Niliitaji kumfahamu zaidi Irine, nilijiapiza kufatiria mwanzo mwisho kujua kilichopo nyuma ya lile.



    Wakati huo nilikuwa kimya nikiendelea kumsikiliza mama alichokuwa anasema ndani ya kinywa chake, ilikuwa si kawaida kabisa kumuona mama yupo kwenye hali ile. Kiukweli tangia kipindi chote cha likizo yangu, siku hiyo ilikuwa yupo tofauti sana hata hali ya uchangamfu ilimpotea. Jambo lile ilionekana wazi wazi lilimuumiza sana ndani ya moyo wake. Nilimjua mama si mtu wakupenda kuona mimi napata tabu, eti kisa kitu fulani.

    Furaha yangu ndio furaha yake ni hivyo hivyo huzuni yangu ndio huzuni yake.

    "Nadhani umenielewa usifikiri chochote mwanangu Criss nipo pamoja na wewe sahau chochote kuhusu haya unajua vyema umebakisha siku chache ufanye mtihani wako wa kumaliza elimu ya kidato cha sita hivyo jaribu kutulia kupunguza mawazo yasio kuwa ya msingi yatakuharibia mambo yako mwanangu umenielewa?”. Aliniuliza mama nami nikamjibua kwa kutikisa kichwa kuonesha nimeelewa kile alichokuwa anazungumza.



    Wakati huo muda ulishaenda sana, na hata jua lilianza kuchoma choma na kuongeza joto mwili, kuikaribisha mchana wa siku hiyo. Ni nyakati hizo ambazo mama aliniaga, na kuniachia pesa kidogo ya kufanya matumizi na yeye akilielekea kwenye mikutano yao ya kinamama.

    Nirejea chumbani kwangu punde mama aliponiacha, njaa haikuwa na sumbua tumbo langu, ijapokuwa nilikuwa sijapata kuingiza chochote ndani yake. Nilirudi ndani na kujitupa kitandani kwa mara nyingine.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikiwa kitandani kwangu nilitulia kimya ni kitafakari yale mama aliyoniambia muda mchache kabla ajatoweka kwenye macho yangu. Nikiwa nayafikiria yale mazungumzo mara nikakumbuka lile jambo la siri. Nikajiuliza mara mbili ni siri gani hiyo?. Fikra zangu zikaonesha kunisaliti, kabla ya kuleta tumaini, tumaini ambalo pekee fikra zangu zikinikumbusha naweza kulipata ndani ya kitabu alichokiandika mwenyewe kaka Eddy pasipo kulewa kilikuwa na maana gani katika maisha yangu.

    Macho yangu yakaanza kukitafuta wapi nilipokuwa nimekitupa, baada ya kumbukumbu zangu, kupotea mahari nilipokuwa nimekiweka. Maana nilipozoea kukiweka hakikuoneka. Mwanzoni niliona haitakuwa ngumu kukipata lakini kadiri muda ulivyokuwa unaenda ndio ugumu ulizidi kuongezeka. Nilichanganyikiwa kwa kweli ndugu msikilizaji.



    Kwa hasira na uchungu wa hali ya juu nilizidi kutafuta, ila muda wote ule sikuwa naangalia chini ya kitanda. Kitendo cha kuangalia chini ya kitanda hapo ndipo nilipopata kikiona kile kitabu, nikiwa hoi kwa utafutaji ule. Kwa sababu tiyari nilikuwa na jambo linaloniongoza sikuijali hali ile ya mwili wangu. Nikiwa na vuja jacho kutokana na saka saka ile. Haraka haraka huku nikiwa nimekodoa macho yangu kwa makini kutafuta ile sehemu haswa niliyoishia.



    Nilitaji kusoma neno kwa neno kwa muda huo kana kwamba kama kuna jambo la siri nzito kumuhusu kaka Eddy basi niweze kulitambua mapema. Kama nafsi yangu ilivyokuwa ikitaka kwa muda ule, niliamini uwenda jambo hilo ningeweza kulipata ndani ya kitabu kile kwasasabu fikra zangu zilifahamu kuwa tu kile kitabu kilikuwa cha siri na sidhani kama uwenda mama alikuwa anakijua maana yale yote yaliandikwa na kaka Eddy mwenyewe hayakuwa wazi mwanzoni. Na hata mimi kukipata kile kitabu sikutegemea kuhangahika hangaika kwangu ndiko kulifanya macho yangu yakutane na kile kitabu.

    Macho yangu yalikuwa katika ubora wake, baada ya muda kidogo, hatimaye nilifika ile sehemu ambayo nilikuwa nimeishia kuyasoma yalioandikwa ndani ya kitabu kile. Kwa hamasa ya kutaka kujua jambo niliongeza umakini katika macho yangu hapo sasa ilikuwa neno kwa neno.

    ************



    Nilimdaka vizuri, kuliko hata walivyokuwa wanategemea hakika, mwili wangu ulikuwa huko vizuri kuliko wakati ambao tulipokuwa tukielekea India.

    Nilikuwa mtu mwenye furaha sana, na hata hivyo nao walionekana wakifurahia ujio ule. Tukiwa nyumbani kwa mjomba, tuliandaliwa chakula, kiliongeza furaha zaidi kwa upande wa tumbo langu, ambalo nalo halikuwa limepata vyakula vya kinyumbani nyumbani yaani ya kitanzania kwa muda mwingi.

    Baada ya kula chakula pale, huku mimi nikiwa na Criss nikieendelea kumuliza mambo fulani fulani ya kitoto, alionekana akifurahi kila ni nilivyokuwa nikimtupia swali, kiukweli alitukumbuka sana si kidogo. Mama alizungumza na mjomba kwa dakika kadhaa, alafu tuliaga na kuelekea nyumbani nikiwa sambamba na mdogo wangu Criss. Kutokana hakukuwa mbali sana, kama dakika hamsini hivi tulikuwa tiyari tumefika nyumbani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tulikaribisha na ukimya pale nyumbani, kwa vyovyote vile ile hali ilikuwa ni lazima tungekutana nayo kwasababu hapakuwa na mtu pale nyumbani tuliishii mimi na mama pamoja na mdogo wangu Criss. Hayo ndio yalikuwa maisha yetu hatukuwa na mfanyakazi kama nyumba za za wanainchi wengi wa Tanzania. Mama akupendelea suala ilo kwetu kabisa sisi wenyewe ndio tulikuwa tukimaliza kila kitu.

    Tuliingia ndani na kuweka mambo sawa baada ya hapo tulilala kwa upande wangu nililala kweli sijui kwasababu ya uchovu wa safari au la ila nilijikuta tu ninaamshwa na mdogo wangu. Wakati huo jua lilishaanza kuchomoza, sikuamini kana kwamba jua lilikuwa lishaanza kuwaka vile. Taratibu nilijitoa kitandani na kwenda kuoga ilikuweka mwili sawa.

    ********

    Mazingira hayakuwa yamebadilika sana machoni mwangu baada ya siku chache, niliweza kuzoea hali ya pale, siku wa mtembeaji muda mwingi nilibaki ndani.

    Siku zilivyozidi kwenda hali yangu ilizidi kuimalika, na kuwa njema sana wakati huo sikuwa na wazo la mtu anayeitwa Irine, lilifutika kabisa ndani ya kichwa changu. Nilimsahau kwa kiasi kikubwa sana, moyoni mwangu hakuwepo tena mwanamke yule, na sikudhani tena kama angeweza kurudi tena kwenye maisha yangu katika namna ambayo sikujua kama ingenigharimu.



    Niliendelea kumsaidia mama katika miradi yake mbalimbali siku hadi siku. Miradi yake ilionekana kuimalika haswa, na harufu ya pesa ilianza kutunyemerea kama zamani. Hali ambayo ilitufanya tusahau kwamba tulitumia kiasi kikubwa hapo nyuma katika kupambana na afya yangu. Mama alinisifia sana, kwajinsi nilivyokuwa nikipambana na kumpa mbinu mbali mbali ambazo ziliweza kusaidia hali yetu ya kiuchumi kuimalika vizuri, kuliko kawaida. Nileendelea kusimami kwa makini mno mpaka kipindi ambacho ilinibidi niende chuo kufatiria masuala yangu ya masomo.



    Wakati huo karibia mwaka ulikuwa unakatika tangu ya tokee yale. Naikumbuka siku ile niliyopanga kwenda chuo kufatiria mambo yangu nilienda sambamba na mdogo wangu Criss, wakati huo nilikuwa nimeshafanya mawasiliano na Juma ambaye alikuwa rafiki yangu mkumbwa na kumpa taarifa kuwa ningefika maeneno yale muda wowote.

    Nilipofika mahali pale palikuwa kumebadilika kidogo tofauti na mwanzo. Nilionana na watu wengi kila moja alitukodolea macho kila nilipokuwa na tukikatiza si wadada si wakaka ambao wengi wao sikuwa na fahamiana nao. Nilizidi kusonga mahali ilipokuwa ofisi ya mkuu wa chuo huku nikiwa na mdogo wangu Criss ambaye yeye kazi yake ilikuwa kushangaa tu kila tulipopita ndani ya chuo kile.



    Moja kwa moja mpaka pale ofisini tulikaa kwa muda kidogo na hatimaye tuliingia ndani kuonana na mkuu yule, kabla sijasema hata kitu mkuu alinena kitu kilichonistua kidogo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Habari zako ninazo kijana wangu mapema tu nilipokea taarifa zako kutoka kwa mkuu wa kitengo chenu hapa chuoni pole sana kwa matatizo kijana wangu”, alisita kidogo huku akiendelea kunitazama nami nikiwa kimya kasha akaendelea kusema. “Maisha haya yana changamoto sana usimwamini mtu kabisa haswa hivi visichana vya hapa chuo.

    Vinatamaa sana havina mapenzi hata kidogo kijana wangu mimi nikama mzazi kwako lazima nikwambie ukweli kwasababu huku tumepitia sisi, nimefanya kazi hapa muda mrefu hivyo maisha ya chuo kwa jumla usione umri wangu huu na wajua vijana wengi hapa na maisha yao kwa ujumla”. Yule mkuu wa chuo aliongea bila kupepesa macho, maneno ambayo yalikuwa ni kama mwiba mkali kwangu. Ulikuwa mwiba kweli ambao ulinichoma na kutonesha kidonda changu ambacho tiyari kilikuwa kinakaribia kupona kabisa.



    Nilimtazama kidogo, nikafumba funda la mate mdomoni mwangu kisha nikamkabili kwa maneno ambayo nilijua yangeweza kubadilisha mada na kulekea kile nilichokuwa nimejia ndani ya ofisi yake,. “Aahh… nimekupata mkuu vizuri sana, kwa sasa nimesahau vitu vyote vya nyuma sasa naangalia maisha yangu maana familia inanitegemea” nilimaliza huku nikiachia tabasamu la kinafiki kwenye mtazamo wake.



    Mkuu alinyamaza kimya baada ya maneno yangu, huku akishighulisha mikono yake kupekua pekua mafaili fulani. Hata sikujua alikuwa anataka kunipa nini?,. Mara alitoa karatasi ambayo ilikuwa ni form nakunipa nilivyopewa tu nilijua niyakuomba kurudia mwaka kutokana na kupitwa masomo. Jambo lile nilishalitegemea kutokea sikuwa na wasi wasi,nilipokea kwa moyo moja. Kabla ya kunipatia meelekezo juu ya form ile.

    Tulitoka nje mimi na Criss nilitulia kidogo nakuanza kuijaza ile form dakika chache niliweza kuijaza vizuri kama inavyotakiwa. Nikamrudishia mkuu ambaye aliniambia nirudi baada ya wiki ili ile form aipeleke mahali husika. Nilimwelewa mkuu vizuri kile alichotakiwa kufanyika juu ya kuhakisha naendelea kupata elimu yangu.



    Tulitoka ofisini na kuanza kukatiza mitaa ya chuo taratibu mpaka ilipokuwepo darasa ambalo nilikuwa nikisoma nilipiga hatua huku nikiwa nimeshika mkono Criss. Hatua kadhaa tulifika darasani mule hakuna aliyeamini kila mwanafunzi wa darasa lile alishikwa na nafuraha isiyo na kifani. Kila moja alifurahi kuniona tena nikiwa kwenye afya njema kabisa hakuna aliyeamini juu ya ujio wangu katika nyakati zile. Kutokana na kukubalika darasani mule wapo baadhi ya wasichana walikuwa wakilia, vilio vya furaha. Si wasichana tu walikuwa wanafuraha ajabu juu ya ujio wangu hata wavulana nawo nyuso zao zilibeba furaha isiyo na kifani. Furaha ambazo kwa upande wangu niliziona za kawaida maana wachache ndio walikuwa wakijitokeza nyumbani na hata kuwasiliana nami juu ya afya yangu, hivyo niliona kama unafiki tu mbele ya macho yangu lakini sikuonesha wazi wazi.



    Nilichofanya nikumchukua rafiki yangu Juma ambaye tiyari nilishampa mapema taarifa ya kuwa ningekuwa pale, siku mbili nyuma.

    Tulitoka nje huku tukiendelea kuzungumza, kiukweli tulizungumza vitu vingi sana. Na hata Juma hakusita kunigusia habari za Irine kipindi chote ambacho mimi nilikuwa sipo vituko vyake. Haki na kili wazi hakuwa msichana ambaye mwanzoni nilizani bwana ndio amepanga niwe nae, nilimlaumu Mungu kunikutanisha na mwanamke yule huku nikiapa sitaweza kuwa na mwanamke yule hata ingekuwa kwa kushikiwa mtutu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tabia zake zilikuwa mbovu sana ndani ya chuo, kila mtu alifahamu nyendo za binti yule. Namna ambavyo Juma alivyokuwa akiniambia nilihusanisha na namna nilivyokuwa nikiingia chuoni pale kila mtu alivyokuwa akiniangalia hapo nilifahamu vyema kwanini nilikuwa naangaliwa sana hapo awali. Nilijuwa tu watu walikuwa wananisikitia kuling'ang'ania fupa ambalo lilikosa mlaji haki nilijiona mpumbavu muda wote kweli Irine hakuwa msichana wa aina yangu kabisa hakustaili kupendwa na mimi Juma aliendelea kuongea mengi hakika Juma alienda mbali sana.



    “Ahahh.. hiiiiii”, niling'ata meno kwa hasira, grafla nilisikia sauti ikiwa inaniita jina langu.

    Sauti ile ilipenya kwenye ngome zangu za masikio kudhihirisha ni jina langu lilikuwa likiitwa si mimi tu hata Criss mdogo wangu akisikia sauti ile wakati nikiendelea kumsikiliza Juma.

    Niligeuza shingo yangu kuangalia ni nani alikuwa akiniita, kugeuka tu mboni zangu zilikutana na taswira ya mdada ambaye sikuweza kumtambua vizuri hadi alipofika mahali pale tulipokuwa mimi Juma na mdogo wangu Criss. Nilimfahamu kwa sura jina lilikuwa limeshanitoka tiyari ni muda mwingi na vile sikuwa sana na mazoea na watoto wa kike hivyo nilishamsahau jina lake ila sura haikuwa ngeni kabisa.



    Muonekeano wa yule binti baada ya kutufikia na kuanza kuzungumza nae niliona vyema hakuwa anahamini ambacho anakiona mbele yake kamwe sura yake ilionekana imeshikwa na mfadhahiko mbele ya macho yangu hivyo niliongea na dakika chache na kutuacha pale mimi na juma tukiendelea kuongea jambo. Juma akanitupia swali, swali likaleta dhahama kwenye kichwa changu.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog