Search This Blog

Thursday, 2 June 2022

TETEMEKO LA MOYO - 2

 





    Simulizi : Tetemeko La Moyo

    Sehemu Ya Pili (2)



    Gafla mazunguzo yale ya mjomba na mama ambayo yalikuwa ndio kwanza mabichi yakapita kichwani mwangu nikanza kujiuliza lakini kwanini naye mjomba ajilize kama mtoto kisa mwanamke, amemkosea nini mjomba?, maswali yalinikaba koo, majibu hayakuwa karibu ubongo wangu ulionekana nao kunisaliti, katika usaliti wa aina yake.

    ENDELEA.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zaidi ya nusu saa nilikuwa tiyari nimepoteza mule ndani ni kitafakari mazungumzo yale ambayo kwa kiasi kikubwa mjomba alikuwa akilalama kuhusu tabia mbovu aliyoanzisha mkewe mwishowe kumkimbia kabisa huku akimuachia mtoto.

    Mara nilianza kusikia sauti ya mama ikiniita, haraka nilijitoa mule ndani huku nikijiweka kwenye mtazamo mwingine, mtazamo ambao ingekuwa ngumu mama kujua hali yangu. Ilinibidi nijiweke vile, nilishamzoea mama yangu mara nyingi huwa ni mwepesi kubaini hali yangu, hivyo ingenisababishia maswali mengi ambayo kwa muda ule ningekosa majibu ya kumjibu. Baada ya kujihakikisha niko sawa nilijitoa ndani kana kwamba hakuna kilichokuwa kinanitatiza.

    Ukweli nilifanikiwa kumhadaa mama kabla ya kuniambia nimsindikize mjomba, jambo ambalo tiyari nilikuwa nalihitaji sana maana ndio ingeweza kunipatia walau majibu ya kile kilichokuwemo kwenye kichwa changu.



    Wakati huo, jua lilikuwa limebakisha masaa kadhaa kabla utawala wa giza kuingia katika usiku wa siku hiyo, hivyo miale ya jua ilikuwa imeshapoteza ubora wake, na kuleta nuru hafifu, na kuifanya kuwa jioni ya siku hiyo. Ni nyakati hizo ambazo maongezi ya mama na mjomba hayakuwa na uhai tena, baada ya kuagana hatimaye tulishika njia kutoka nyumbani kuelekea kilipo kituo cha daradara, ambazo zingemuezesha mjomba kufika nyumbani kwake kutokea mahali pale. Kituo cha daradara nacho hakikuwa karibu sana, kiasi kwamba ndio ilikuwa njia ya mimi kuweza kunipatia majibu ya maswali pindi ambapo nilipokuwa nayahitaji.



    Nilimuangalia mjomba katika jicho la kuibia ibia lakini bado alionekana hayuko sawa, mtazamo wake ulionekana kubabea mambo mengi ambayo yanamsumbua katika namna moja ama nyingine, fikra zangu muda huo ilikuwa ikipambana na juu ya kuuliza kile kilichokuwa ndani yangu, nilipima uzito wa lile jambo , uthubutu wa kuuliza ukanipotea huku nikikabwa kabisa , wakati huo ukimya ukitutawala miongoni mwetu baada ya maogezi machache hapo awali wakati tunatoka.

    Sikuwa mtu wa kupenda kushindwa nilipokumbuka kuwa sipendi kitu kinachoitwa kushindwa jambo. Haki nilijikaza na kuufukuza ukimya katika namna ambayo mjomba hakuitegemea. Swali zito lilinitoka na kumwelekeza mjomba katika hali ya kizembe mno ya kuuliza, swali ambalo sikutegemea uwenda ningepokea majibu katika hali isiyozuilika.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kiukweli kilio cha mjomba hakikuwa mbali, alilia sana, kilio ambacho kiliniumiza, si kupenda hali ile niliyokuwa nikiiyona nilijitamani kujilaumu, lakini sikuwa namna njiani pale, ilininibidi nigeuke mbembelezaji, niliitahidi kuzuia kilio chake, japo kwa muda kidogo kabla ya kuendelea na safari.



    Nikiwa sitegemei kama mjomba anaweza kuniambia chochote, baada ya kunyamaza, hatimaye alianza kunijibu lile swali langu niliokuwa nimeliuliza japo ilikuwa kwa ufupi isiyoleta tija kwa upande wangu. “Ni kweli hatukuwahi kuwa na matatizo hapo nyuma na shangazi yako kama ulivyoniuliza mpwa wangu, wewe ni bado sana, ujui jinsi maisha yalivyo kimsingi kuoa uyaone”, alimaliza mjomba. Majibu ambayo yaliongeza tu maswali upande wangu na kuleta mvutano wa kile nilichokuwa nikifikiri. Sikuwa na jinsi kuhusu kukua niyaone ni kweli nilikuwa nimeshakuwa na tiyari nilishaanza kuyaona. Hivyo sikutaka kuendelea na udadisi sana.



    Tuliendele kupiga hatua , bahati nzuri tulikuwa tumeshasogea sana karibu na kituo cha daradara. Na hata macho yetu yaliweza kukumbana na daradara ambazo nyingi zilikuwa zimejaza watu kuliko kawaida. Tulipiga hatua chache, hatimaye pua zetu zilikumbana na harufu ya kituo kile vizuri. Ilichukua muda kidogo katika uchaguzi wa daradara ambayo ilikuwa walau ina nafasi ya kumwezesha mjomba kusimaa. Baada ya kufanikisha hilo mimi niligueza kurudi nyumbani.

    ********

    Giza nalo lilikuwa linaingia rasmi, macho yangu yalishaanza kulipokea, ni nyakati ambazo nilikuwa, tiyari nimesharejea nyumbani. Mama akiwa anajishughulisha kuandaa chakula cha jioni, nilimchombeza kidogo katika hali ya kiutani , kama kawaida yangu. “Mama nawe” ilinitoka huku nikiweka mdekezo wa kitoto, “mmh nini nawe ushaanza kudeka?” maneno ya mama ya kapenya kwenye masikio yangu, katika hali ya kuuliza ambayo haikuwa ikihitaji majibu kwa lazima. Tuliendelea kuzungumza kidogo. Maeneno yake ya kaleta furaja, upande wangu nilijihisi mtu katika watu. Mama alikuwa akinifurahisha sana hata hali ya unyonge kwa wakati mwingine ilikuwa ikinitoke, kutokana na vijimaneno maneno vya mama kwa wakati fulani.

    Nilikuwa nikijisikia raha sana Mungu kunipa mama kama yule.

    Nilingia ndani, na kuketi sebuleni , taratibu na kiendea luninga iliyokuwa ikiangaliana nami bila kuwa na uhai. Nikibonyeza kitufe cha kuipa uhai, muda kidogo ilianza kubaliana na kile nilichokuwa nataka, nikiweka nayo ikatii.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Masikio yangu yakanza kusikia sauti ya luninga ile, huku macho ya kiona kile kilichomo ndani yake, ilikuwa ni nyimbo za wasanii wetu wa hapa nchini. Hapo kidogo zilizidi kuniliwaza na kupoteza fikra, ambazo zilikuwa zikinyanyasa kichwa changu. Muda nao haukuwa nyuma, uliendelea kwenda, nyakati hizo hurufu nzuri nzuri ambazo zilikuwa zinatoka jikoni, zilianza kunyanyasa pua yangu, huku tumbo nalo likiunguruma. Mama naye halishajua kuwa mwanae sina hali hata kidogo, muda mchache nilimwona akija, lakini katika namna nyingine.

    ********

    Siku ya safari iliwadia hatimaye mapema tuliacha ardhi ya Tanzania, wakati huo kabla ya hapo tulingia katika maombi mazito. Usiku wa kuamkia siku hiyo, maombi ambayo kwa upande moja ama mwingine yalizidi kunipa faraja kuhusu hali yangu. Tulimuomba Mungu atuwezeshe kufika salama ndani ya nchi ya India, na hata kuniwezesha afya yangu kuwa sawa. Hatimaye Mungu aliweza kujibu maombi yetu japo hayakuwa yote, kwa pamoja. Tuliweza kuingia India, baada ya masaa kadhaa angani ambayo sikuwa na uwakika sana yalikuwa mangapi.



    Hali ya hewa haikuwa na tofauti sana na nchini Tanzania kwa wakati ule, hivyo hakunisumbua kwa upande wangu, pia na mama. Tulikumbana na tabu kadhaa pale uwanja wa ndege lakini tuliweza kufanikiwa kumpata mtu ambaye alikuwa anajua lungha ya kingereza. Hivyo iliweza kutusaidia kufanya mawasiliano, hii ilitokana na wenyeji wengi wa nchi ya India hawakuwa na kifahamu kingereza, hata Kiswahili ambazo ndio lugha tulizokuwa tukizifahamu mimi na mama.



    Baada ya kufanikiwa kumpata dereva moja wa tesi pale uwanja wa ndege ambaye alikuwa akijiua kingereza vizuri, ilikuwa msaada mkubwa sana kwetu. Aliweza kutusaidia sana kuanzia siku ile ya kwanza hadi siku ya pili tulipoelekea hospitali, ambayo haikuwa mbali na sehemu ile tulipokuwa tumefikia.



    Siku hiyo ilianza ya kupendeza sana machoni mwetu, mwanga wa jua ilipenya ndani ya macho yetu na kuonesha fahari yake, hata kunifanya kuachia tabasamu ambalo ilikuwa nadra sana kwangu kuachia katika kipindi kama kile, tabasamu ambalo mwisho lilikuja kuchukizwa na siku ile iliyoanza katika, mnang’aro wa kupendeza na kuleta tumaini kwa upande wangu hakika ilikuwa kama inanikebehi.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ni kweli ilikuwa ikinikebehi, baada ya kufika katika hospitali ile ambayo tiyari tulikuwa na taarifa zake hapo awali, tulifanikiwa kumwona daktari mapema kuliko kawaida. Tulizungumza nae, huku tukiambatanisha vielelezo ambavyo, tulikuwa tumepewa kutoka kwa daktari aliyenitibu hapo awali. Maelezo yalijitosheleza kabisa, hatimaye niliingizwa katika chumba cha kufanyia uchunguzi. Uchunguzi ambao hakuchukua muda sana kutokana na tekenolojia yao, muda kidogo nilitolewa na kuelekezwa sehemu ya mapunziko, mapunziko ambayo hayakuchukua muda sana hatimaye, tulitwa pamoja na mama kuelekea chumba cha daktari.



    Nilishajua kuwa mambo yalikuwa tiyari yapo hadharani ni mimi tu na mama ndio tulikuwa tunasubiriwa ilikuweza kufahamu. Sikuonesha wasi wasi kama hapo awali, niliachia tabasamu la kivivu, tabasamu ambalo sikujua lilikuwa linamanisha nini?.

    Hatua kadhaa tulikuwa tunatazama na mlango wa chumba kile cha daktari, tulisubiri kidogo, kisha tukajitoma mule ndani, baada ya kupokea ruhusa. Kwa upole daktari yule, huku akitumia kingereza chepesi chepesi kuliko kawaida, niliweza kuyasikia maelezo yake vyema juu ya kile kilichopatikana baada ya uchunguzi ule katika mwili wangu.



    Kama vile nilikuwa nimemwagiwa na maji ya baridi mwili mwangu nilipoa gafla, sikuamini nilichokuwa na kisikia kutoka kwa daktari yule aliongea yakuwa moyo wangu ulikuwa umeharibiwa vibaya sana na ugonjwa ambao kitalaamu ulikuwa mgeni bado hakuwa na jina rasmi. Ambao ulikuwa umegundulika katika kipindi kifupi katika mwaka ulikuwa umepita. Bado wataalamu walikuwa wanaendelea kufanyia uchunguzi juu ya ugonjwa ule. Alizungumza mambo mengi sana , akigusia alichokuwa anakielewa kwa upande wake. Sababisho kuu katika uchunguzi wao wa awali likionekana , mahusiano ya mapenzi, mahusiano ambayo sababishi ni yale ambayo ni hasi kwa upande wa mwanamke na mwanaume. Vile vile alizidisha kuwa kitaalamu ule ugonjwa haukuwa na dawa iliyogudulika kuponesha moja kwa moja katika kipindi kile. Bali angenipa dawa ambazo ambazo zilikuwa na ubora ambao ungeweza kufanya afya yangu kuwa njema kwa kipindi kifupi.



    Alinisihi ya kuwa usijuhusishe kwenye mambo, ambayo kama nilikuwa nayapenda maisha yangu. Nilisikiliza kwa makini juu ya jambo lile lakini ni kama vile alikuwa akigongelea msumali kwenye mwili wangu. Maana maneno yake yalinichoma sana, sikuweza jua kuwa nitaweza vipi kuishi bila ya kupenda wakati tiyari Irine alikuwa akiishi kwenye moyo wangu. Niliteta na moyo wangu, lakini bado nao hakuwa na jibu sahihi. Mwishowe nilikubali, kwajili ya maisha yangu nitajitahidi kuwa mbali na hilo. Nilijisemea kimoyo moyo, nikiwa nimechoka kweli na yale majibu. Mama alinisihi sana niweze kuyazingatia yale kwa wakati wote, kwa upande wake, hakutaka kunikatisha tamaa, hakika alikuwa akijua kucheza na akili yangu, baada ya maneno yake ya kunitia faraja, nami nikiona kama hapakuwa na jambo zito lilikuwa likinikabiri.

    ************

    Naikumbuka vyema siku ile tulipoondoka nchini India. Nilinunua baadhi ya vitu kwa jili ya mdogo wangu Criss kutokana wakati wote alikuwa yupo kichwani mwangu. Na mimi mwenyewe nilinunua baadhi ya vitu vidogo vidogo kwa jili ya ukumbusho wa ile safari ijapokuwa haikuwa safari ya kutalii ila niliamua kufanya vile.

    Saa moja ya usiku tulitua katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere, na kuanza kunusa hewa ya Tanzania hakika. Nilijisikia raha ndani ya moyo wangu mno isiyokuwa na kifani.Nilijua punde tu ningeungana na mdogo wangu Criss.



    Wakati huo hawakuwa na taarifa yoyote ya kurudi kwetu, hivyo hakuna mtu aliyekuja kutupokea pale uwanja wa ndege. Tulikodi tesi kutokea pale uwanjani, kituo cha kwanza kilikuwa kwa mjomba baada ya dakika ndani ya tesi ile. Hatimaye tulifika hakuna aliyeamini ujio wetu, machoni mwao. Niliachia tabasamu kwa kila aliyekuwa akioniona alikumbana nalo, likaongeza furaha zaidi kwao huku mdogo wangu Criss alifurahi kupita maelezo. Hakika upendo wangu kwake ulikuwa ni chachu ya furaha yake. alinirukia mithili ya nyani, nami nikafanya jambo ambalo sidhani kama lingeweza kufutika ndani ya kumkumbuku yangu.

    ******

    Baada ya mama kuja katika ujio ambao, ulifanya kuridhisha tumbo langu, na chakula ambacho kilikuwa kitamu kupita maelezo. Muda machache tu nilijitoma ndani, nilipomaliza kula. Huku macho yangu kitalii, kwenye kile kitabu ambapo baada ya muda kutokana na kile kilichokuwemo. Mikono yangu haikuwa na nguvu tena ya kushika kitabu, ilitetemeka vibaya. Nilikumbuka vizuri siku ile ambayo kaka edy alilejea kutoka India akiwa pamoja na mama, ijapokuwa nilikuwa ni na miaka saba ila kumbukumbu yangu ilivuta vyema nikiwa kitandani pale. Nilishindwa kuendelea kusoma tena kilichokuwemo ndani ya kitabu. Nilijikuta kinanitoka kwenye mikono yangu na kudondoka hata pasipo kuelewa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Machozi yalianza kunitirika vyema kutoka kwenye macho yangu taratibu kuelekea kwenye mashavu yangu. Uchungu ulinishika vibaya nilikuwa kama mtu niliyepigwa viboko vikali katika makalio yangu uwenda kutokana na kosa fulani.

    Moyoni mwangu hasira alinishika vibaya mno nilitamani hata kumtafuna mtu ilinipoze hasira zangu. Kaka Eddy lilikuwa pengo kubwa ndani ya mwanya wangu hakika hakuna angeliweza kuliziba maisha yangu yote. Jinsi nilivyoikumbuka siku ile na pamoja zawadi alivyoniletea siku ile machozi yalizidi kunitirika nililia kimya kimya lakini haikutosha kupoza machungu yangu.



    Nilijikuta tu sauti ikitoka hakika ilikuwa mbaya ila haikunifanya ninyamaze. Zaidi ya nusu saa nililendele kilio kisichokuwa na mbelezaji. Baada ya muda nilinyamaza nikiwa sijui ilikuwaje ila nilichokumbuka vilio vya kwikwi vilinitawala kwa muda sana. Ni kiwa tiyari nimejitupa kitandani. usingizi ulikuja kunichukua, katika namna ya aina yake maana nikiwa katika nilisikia sauti kwa mbali ikiniiambia jambo.





    "Kajina maisha yako yapo hatarini kwa kiasi kikubwa, kuwa mbali kabisa na viumbe vinavyoitwa wanawake kaa mbali kabisa” kwa ukali sana sauti ile ilipitia nikiwa bado angali niko usingizini.

    Nilishituka kutoka usingizini kwa hali ya kugofya sana huku moyo wangu ukienda mbio vibaya.

    Nilijishangaa kwa nini hali ile inanijia na inahusiano gani na maisha yangu? au kuna jambo zito ambalo linakwenda kunitokea katika maisha yangu. Nilijiuliza huku nikijipatia majibu ya maswali yangu. Nilijionya mwenyewe huku nikijisema, “haiwezekani hata kidogo”.



    Machungu ndani ya moyo wangu yaliongezeka maradufu sikujua mwisho wa yote utakuwa nini?, kama chanzo bado kinanitatiza je huko mwisho kutatokea nini?. Bado hali ile iliniacha kwenye taharuki kali ndugu msikilizaji wasimulizi hii, Hakika kama kunajambo baya ambalo ningelijua mapema, lilikuwa linaenda kunitokea ndani ya maisha yangu, basi ningeliziua kuanzia pale.

    ********

    "Criss… Criss!, mwanangu upo kweli wewe au umelala asubuhi yote hii,” nikiwa bado nipo kimya sauti ya mama ilizidi kupenya kwenye vitundu vya masikio yangu, ikinitaka kuamka katika asubuhi ile, ikiwa mwanga wa jua, ulishaanza kuipendezesha siku katika namna nyingine.

    Niliitika ilikumjulisha kuwa nimeamka, wakati nikijivuta kivivu kutoka kitandani, ndipo niliposikia sauti ya mama tena ikinitaka nitoke nje.



    Nilinyanyua nikitokea pale huku macho yangu yakiwa bado hayajatoka na wenge la usingizi. Miale ya jua nayo ilinikabili punde na kuninyanyasa pindi nilipotoka nje, nilihisi macho yangu kuwa mazito vibaya hata sikuelewa nini kimenikumba ila nilianza kusikia maumivu kidogo kidogo kutoka kwenye mboni zangu. Nikiwa tiyari nimemfikia mama yangu pale alipokuwa amekaa.

    Maneno ya mama tu yalitosha kusawili kile nilichokuwemo kwenye macho yangu. “Kulikoni mwenzetu mbona macho yamevimba ulikuwa unalia nini usiku kucha?” . Mama alinuliza huku akiendelea kunitandika swali lingine wakati hata sijajibu, “au una tatizo ila unaonekana haupo sawa baba yangu hata kidogo?”.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maneno yale niliyasikia vizuri, wakati huo nipo kimya hata cha kujibu sina. Maneno yake yalinitia uchungu sana grafla nikakumbuka tukio lilotokea muda mfupi kabla sijapitiwa na usingizi usiku wa kuamkia siku hiyo.

    Nilijikuta machozi yakianza kunitiririka na kufatiwa na neno ambalo niliweza kulitamka kwa wakati huo. “Kwanini mimi mama?,’’ linanitoka kwa gadhabu ya hali ya juu. Hali yangu ilionekana wazi wazi kwenye mboni za mama kuwa haikuwa ya kawaida hata kidogo.



    Hapo sasa hata maneno ambayo niliyokuwa nikayatamka yalishindwa kutoka vizuri kwenye kinywa changu. Kwikwi zilifatia ikiendana na kilio cha uchungu nilichokuwa na kitoa.

    Hakika nilitamani dunia mzima kusiwe na wanawake ndani ya asabuhi ile, huku nikimpa nafasi ya upendeleo mama yangu. Nikiamini yeye pekee yake ndio alikuwa akistahiri kuwepo katika dunia kuliko viumbe hivyo.

    Na hata kwenda mbali zaidi huku nikiombea kama ikitokea vita hivi karibuni katika dunia basi viumbe hivyo viteketezwe kabisa maana vina roho mbaya, ilojaa chuki, usaliti tu kwenye mioyo yao. Wanapenda kujijali wao tu na si wenzao hata kidogo, watu wanamna hii hawafai hata kidogo. Nijisemea ndani ya fikra zangu kimya kimya huku nikiambatanisha na kilio kizito.

    Baada ya muda mrefu kidogo hasira zangu zilipungua na kasi ya kilio nacho nilichokuwa na kitoa kilipungua na hatimaye mama alifanikiwa kuninyamazisha. Na kutoa kauli iliyopenya vyema kwenye milindimo ya ngoma za masikio yangu, “aah hakika mama wee!, nilimpa haki yake kwenye kinywa changu kimoyo moyo kabla ya kuendelea kuongea.

    "Mwanangu nakupenda sana wewe ndio baba yangu si pendi nikuone unasononeka juu ya jambo lolote lile. Haya kwanza naomba uniambie nini kinakutatiza wewe maana nakuona haupo sawa kabisa?”, aliniuliza mama huku akiendelea tena kuongea. “Na kama kuna jambo linakusumbua wazi wazi ndani ya kichwa chako na omba uniweke wazi!” aliongea kwa msistizo.



    Nilisikiliza kwa makini yale maneno ya mama, huku nikiteta na moyo wangu nikiamini wazi kuwa mama yangu ni mtu mwenye upendo na mimi sana.

    Wakati huo nilitulia kimya, nikijishauri niweze kumwambia kilichokuwa kinanitatiza, niliona siku zote mficha maradhi mauti siku moja umuumbua. Nilijikaza kisabuni kunyanyua mdomo wangu ulionekana una mengi ya kuongea mbele ya macho ya mama na masikio yake, huku mama akivuta umakini kupokea maneno yangu haswa.

    "Mama maisha yangu yamekuwa hayapo sawa kabisa siku hizi mbili tatu, namkumbuka sana kaka Eddy mpaka leo, bado kaka Eddy ajanitoka hata kidogo nashindwa kumsahau kabisa yote kutokana na maisha tuliyokuwa tunaishi. Upendo wake kwangu ulikuwa zaidi ya vyote mama”, nilisita kidogo nikitazama kwa makini mama jinsi alivyokuwa akiyapokea yale maneno yangu, kabla ya kuendelea kuzungumza. “Angalia mama, hata vitabu vya dini vinasema tunatakiwa kusahau jambo ambalo limepita lakini kwangu imekuwa tofauti kabisa,

    angalia miaka kumi sasa. Lakini nimekuwa mgumu sana kusahau jambo linanitesa sana sijui kwa sababu tulizaliwa wawili?”, Nilimuliza mama swali la kizembe wakati nikiendelea kuongea, niliona hilo alikuitaji majibu niliendelea kuzungumza huku nikijibu mwenyewe. “Ilo sio tatizo mama upendo wake ndio tatizo sidhani kama atatokea kaka kama yule kwenye maisha yangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakika kaka Eddy alikuwa mtu bora sana kwenye maisha yangu si kwangu tu mama, hata wewe kwako!”. Mama aliendelea kunisikiliza kwa makini mno na namna yale maneno yalivyokuwa yakinitoka ndani ya kinywa changu, yalionekana wazi wazi yalikuwa yakimchoma mama na kumkumbusha mbali.

    Niliendelea kuongea ila hali ya mama alianza kubadilika kidogo kidogo, katika namna ambayo sikuitegemea kabisa ndugu msikilizaji.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog