Search This Blog

Thursday, 2 June 2022

TETEMEKO LA MOYO - 1

 





    IMEANDIKWA NA : YONA FUNDI



    *********************************************************************************



    Simulizi : Tetemeko La Moyo

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Ukumbi ulivutia katika namna isiyoelezeka, kiukweli waandaji wa idara ya mapambo walifanya kazi yao ipasavyo. Tofauti hata nilivyokuwa nikidhani. hakika kulivutia katika macho ya kila moja aliyekuwa amefika sehemu ile. Uzuri si idara ya mapambo tu iliyofanya kazi yake ipasavyo lahasha kila moja alifanya kazi yake vile nilivyohitaji mimi na mpenzi wangu Irine ndani ya siku ile. Katika siku ambayo Irine wangu , alikuwa akitimiza miaka kumi na tisa. ni hiyo miaka aliyotufanya ilitufanya tuwe pale kwa muda ule kusherehekea pamoja na ndugu na jamaa wengine. Yote niliyafanya mimi kwajili ya upendo wangu na thamani yake ndani ya moyo wangu. Irine kwangu alikuwa zaidi ya kila kitu. Muda mfupi tangia uhusiano wetu ulipoanza siku zote nilijitahidi mara ya kufanyia mambo mazuri yote kuonesha thamani yake kwangu kama wafanyavyo wanaume wengine kwa wenzawao. Hakika sikuwahi kufikiria ipo siku nitakuja kufikia katika namna hii ambayo isiyoelezeka. naichukia nafsi yangu, naiichukia sana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku hiyo ilipendeza sana uzuri kila moja aliyepata mwaliko,alifika kwa wakati husika. Si wanafunzi wenzetu katika chuo chetu si marafiki wengine kila moja alifika kwa wakati huku wakiwa wamependeza kuliko kawaida. Hali ile ilinogesha sana siku hiyo, sijui niseme nini kwa upande wangu nilikuwa na furaha isiyo elezeka. Nilionekana wazi wazi kwenye taswira ya uso wangu dhahiri , na hata kwa upande wa Irine ambaye aliyetufanya tuwe pale muda ule naye alionekana mtu mwenye furaha kupita maelezo. Hakika hakuna aliyetamani kuisha kwa siku ile kila mtu aliyekuja pale alijiskia yupo sehemu tofauti sana kutokana na hali ya ukumbi wenyewe. Kulipendeza sana ,nakshi naskhi za mule ndani ziliwavutia wageni waalikwa , walikula wakanywa vinywaji kila aina ya vyakula na vinjwaji walivyokuwa wanavipenda

    Siku hiyo ilikuwa ni muhimu sana katika namna mbili ya kwanza ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa Irine wangu. Pili nilimvisha pete ya uchumba. ilikuwa kwasababu upendo wangu nilihitaji kila mtu ajue nijinsi gani ninavyompenda msichana yule kutoka ndani ya moyo wangu nasi vinginevyo.



    Hakika nilikuwa nimepagawa sana na mwanamke yule maana nilikuwa tiyari kujitolea chochote kwajili yake. Nakumbuka hapo awali sikuwahi kupenda na sikuwa mshirika wa dhahama hii. Akili yangu haikuwa ikifahamu nini maana ya mapenzi, nilikuwa nikiyangalia katika mtazamo usikuwa na maana mbele ya kichwa changu. Mtazamo uliloleta majibu mengi chanja tofauti na hasi kwa upande wangu.

    Kila mtu aliyekuwepo alishuhudia tukio lile kwa macho yake mawili , ijapokuwa kipato changu kilikuwa cha kati na hata wazazi wangu ilanilijibana bana huku na huku. Kutimiza yote yale ndani ya siku ile. Nilijichanga sana hatimaye nilifanikiwa kuyafanya yote yale bila mchango wa mtu yoyote.

    **********

    Yapata mwezi moja umepita tangu yatokee yote yale nikiwa bado nipo kitandani nauguza majeraha katika mwili wangu niliyoyapata muda mfupi tu baada ya kumalizika sherehe ya kipenzi changu Irine. Niliumia vibaya sana sehemu za ubavuni kwenye zangu mbavu ,vile vile nilivunjika mguu hivyo , nilikuwa mtu wa kulala kitandani muda wote mpaka sasa tangia ajari ile iliyosabishwa na dereva wapikipiki niliyoipanda muda mfupi tu baada ya kuagana na Irine nilipoenda kumrudisha hosteli.

    Sasa yalikuwa yamejirudi katika kichwa changu. Nikiwa kitandani, yaliongeza maumivu makali niliyasikia kwenye mwili wangu. Maumivu ambayo hayakuwa tu yakisababisha na majeraha yale niliyokuwa nimeyapa lahasha maumivu yalichanganyika na mateso ya moyo. Moyo ambao tiyari ulikuwa ushasalitiwa katika akili ya kawaida. Macho yangu hayakuweza kumwona Irine kwa kipindi chote hicho , walau wangeweza teta na moyo wangu. ilikuweza kuupa faraja pindi yangemuona Irine.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Namna nilivyokuwa nimeyakumbuka yale yaliniumiza sana sikuamini juu ya yote yale niliyomfanyia Irine siku si nyingi zilizopita ameshindwa hata kunijulia hali hata kwenye simu yangu. Maana kama kufika nyumbani kwetu ilikuwa tatizo hata hilo ameshindwa baada ya wiki tu nilipopokea simu yake katika kile nilichoona unafiki katika masikio yangu. uvumilivu ulinishindwa nilibanwa na kilio cha chini chini , nikiwa juu ya kitanda ambacho hakikuwa na hiyana kama binadamu. kiliofariji mwili wangu kwa wakati wote. lakini sasa kilishindwa kunibembeleza katika kilio. Kilio kilichochanganyika na majuto ndani yake.

    Hali yangu ilibadilika grafla mwili ulikosa nguvu ,nikajikuta mboni zangu zinapoteza taswira. Weusi ulitawala takatika vishimo vya macho yangu , masikio yalikuwa mazito sikuweza hata kujua anayeingia wala anayetoka ndani ya chumba changu. Hata sauti bembelezi ya kitoto ya mdogo wangu Criss haikupata tena nafasi kwa wakati huo. Ni huyo Criss mdoggo wangu mbaye mara nyingi hupenda kucheza karibu na kitanda changu.katika namna niliyokuwa nikiona ni faraja kutokana na hali yangu.

    ***********

    Hata sikuelewa nipo wapi baada ya muda ambao nilihisi ni mfupi baada ya kutokea hali ile. Nilishangaa nilipofumbua mboni za macho yangu shuka jeupe lilikuwa limeufunika mwili wangu huku kibaridi cha mbali kilikuwa kinapenya ndani ya mwili wangu ulikuwa unatoa vimaji maji ambavyo dhahiri ilitokana na hali nilikuwa nikisikia ndani ya mwili wangu. niliangaza kidogo baada ya macho yangu kuipata nuru kwa mara nyingine. Kichupa kidogo cha wastani kikiwa kinaning'ing'inia juu ya kitanda kidogo tofauti na cha kwangu , ilitosha kabisa kufahamu pale ni nilipo kwa muda ule ,kwa uhakika kabisa kuwa mahali pale kulikuwa hospitali. si kufahamu wakati sahihi nilikuwa nimefika mahali pale na chanzo cha mimi kuwa pale. Nilijiuliza maswali ambayo hayakuwa na majibu ya wazi kwenye kichwa changu, akili ilikuwa bado imeganda kabisa.Wakati nikisubiri jibu nilihisi kama kitu kipo kwenye mkono wangu. Kabla hata sijaangalia vizuri nini kipo mkononi mwangu, nilimuona mama yangu akiwa anaongea na mtu ambaye kwa muonekano tu nilijuwa wazi ni daktari. Maongezi yao yalipenya vizuri kwenye ngoma za masikio yangu. kwa uhakika kabisa masikio yangu yalikuwa katika ubora wake. ubora ambao ulipotea muda mfupi kabla ya kuwa eneo lile.Daktari yule aliongea kitu ambacho kiukweli hakikuningia akili kabisa. Na si mimi hata mama yangu nilivyomuona nilibaini kuwa jambo lile hakuwa anakubaliana nalo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Si kuwa tiyari hata kidogo kwa kile kilichokuwa kinaendelea, nilijua wazi sasa ni muda wa mama kuaangahika, huku ikiwa si ya chini ya mwezi moja tu pesa nyingi sana alitumia kwajili yangu hii leo suala la kwenda India kwa jili ya uchunguzi wa moyo wangu. Lilikuwa geni kabisa masikioni mwangu. Hapo awali sikuwahi kuugua maradhi ya moyo hata kidogo.na hata huku nyuma hakuna mtu ambaye ndani ya ukoo wetu ama familia yetu alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo. Hivyo juu ya kweli kwamba moyo wangu huenda una matatizo kama daktari alivyoshauri , punde tu kabla hata haijafika miezi sita liwe imepatikana ufumbuzi , tena nje ya nchi haikuniingia akilini hata kidogo.Wakati huo nikiwa bado nitaendelea na dawa kwa jili ya kupunguza maumivu yale kwa muda mfupi. Ijapokuwa ni kweli nilihisi mabadiliko muda mfupi kwenye upande wa kushoto wa kifua changu eneo sahihi ulipo moyo wangu. Ila bado niliona hali iliyokuwepo mbele si nzuri hata kidogo.nilitamani kupingana na maneno ya yule daktari, lakini ni kaona ni sawa na ujinga tu. ujinga wa kupingana na mtu ambaye alikuwa akipambana na kuikoa afya yangu. Fikra zangu zikaonekana kubariana na lile kwa kinyongo . Ni kinyongo cha ambacho nilichajua hakuwa na njia nyingine zaidi ya kutumia pesa. Hali yetu kiuchumi sasa ndio likawa tatizo si kwamba mbaya ilikuwa mbaya sana ila kidogo ingeleta shida kwa namna moja ama nyingine.



    Nilitulia kimya kama vile nilikuwa sijui jambo lolote liliokuwa likiendelea ,ni kiwa bado nipo kitandani chumbani mule, huku nikisikilizia maumivu makali ndani ya mwili wangu. Pande zote zilivuta kuliko kawaida , ila nilijikaza kiume si kutaka kuonesha udhaifu kama baadhi ya wagonjwa wengine pindi wapatapo maumivu makali utawasikia tu hiiiiiiii... ohhooo nakufa !!!!! mama mie nakufa !!!!! mara uwiii Mungu wangu nisaidie!!!!!!. Kwa upande wangu nilikuwa kimya huku nikiwa nimeyafumba macho yangu kusikilizia maumivu kimya kimya.

    Nilihisi mwili wangu ukiguswa guswa maeneo ya usoni kama baadhi ya watu wanavyofanyaga kupima hali ya mgonjwa .



    Nilifumbua macho yangu taratibu hayakuchelewa kuona mtu aliyekuwa akifanya vile. Hakuwa mwingine bali alikuwa ni Mama yangu taswira yake ndani ya mboni za macho yangu ilitambulika vizuri. Sura yake ilionesha wazi wazi kuwa alikuwa akipata maumivu makali kutokana na hali yangu.

    "Pole Eddy utapona mwanangu " nilimsikia vyema mama akiyatamka ndani ya kinywa chake huku yakifatiwa na maneno yakunitia moyo. Alionekana bayana tu kuwa ana mashaka na hali yangu, wakati huo aliendelea kuongea maneno mazuri yakunitia nguvu.

    Muda ulienda hatimaye kile kichupa cha wastani kilichokuwa juu ya kitanda changu kilionekana kuishiwa maji. Ambayo niliyaona ya kitiririka kuelekea katika moja ya mkono wangu huku yakiwa yanapita kwenye kama kabomba chemba sana kuelekea ndani ya mwili wangu. Kupitia tundu dogo lilotobolewa kwenye mkono wangu ikiunganisha sehemu ya juu ya kichupa kile kuelekea kwenye wangu mwili kwa tararibu , kadiri yalivyokuwa yakienda hali yangu ilianza kurudi kama mwanzoni kabla sijafikishwa eneo lile pale nilipojikuta na kosa nguvu na nuru kupotea kwenye macho yangu. Lakini sikujua kilikuwa kichupa cha ngapi?, ila mwenendo wake ulinirudishia nguvu zangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jioni baada ya hali yangu kuonekana kidogo imerudi sawa daktari hakuona haja ya mimi kuendelea kubaki alichofanya nikutupatia ruhusa. Na kumpatia mama maelekezo pamoja na kumpatia dawa kwajili yamatibabu yangu. Nilishuhudi mama yangu zikimtoka pesa nyingi sana hapakuwa namna yoyote yeye ndio alikuwa mtu pekee wa kuyatenda yale. Wakati hakukuwa na mtu ambaye angeweza kusaidiana bega kwa bega na mama katika ugonjwa wangu . Baba ndio alikuwa mtu pekee ambay angemsaidia mama katika hali ile lakini alikuwa tiyari ameshakufa katika miaka miwili iliyopita. Kipindi ambacho hata nilikuwa sijamaliza elimu yangu ya kidato cha sita.

    Mtu pekee katika familiya alikuwa ni mama si kwamba ndugu hawakuwepo lahasha ilitokea hali ya kutoelewana baina ya ndugu zake baba. Pindi alipofariki ilikuwa katika ile hali ya ndugu kutaka kutudhurumu haki yetu kama watoto na pamoja haki yake mama kama mke wa marehemu. Baada ya zoezi la kurithi mali za baba kutatuliwa na mahakama ndipo uhusiano wetu ulipovunjika. Na kwa upande wa ndugu zake mama hali zao zilikuwa ni za chini na kiasi kikubwa walimtegemea mama yangu kwa kila kitu.



    Wiki tu baada ya kuruhusiwa hospitalini hali yangu iliendelea kuimalika siku hadi siku majeraha nayo yalianza kupona , huku nikiwa chini ya uangalizi wa mama. Alihakisha na kula vizuri na pata dawa kwa wakati, miezi mitatu ilipotimia majeraha yote yalipona kabisa huku yakiniachia makovu sehemu za mwili wangu, kama kumbukumbu. na kwa upande wa moyo wangu ulitulia kabisa naweza kusema zile dawa zilinisaidia kabisa.



    Kwa kipindi chote kile si kuweza kupata habari yoyote iliyomhusu Irine hata nilipowasiliana na baadhi ya marafiki zangu hawakuwa wananipa taarifa zake. Nilijua wazi wananificha ila sikutaka kufatiria sana kutokana na hali yangu ilivyo. Ukizingatiwa mama kipindi chote nilipokuwa najiuguza aliniambia daktari ameshauri nisiwe mtu wa mawazo muda wote. ingeweza kunisabishia madhara ndani ya moyo wangu. Na kingine zaidi alichokuwa akisisitiza ni suala la kuwa mbali na mambo ya mapenzi yangechangia sana kunifikirisha nakujikuta anapata upinzani mkali kutoka kwenye moyo wangu. Hivyo nilijaribu kuepuka sana jambo lolote linalohusisha mawazo ndani ya kichwa changu kabisa. Ijapokuwa Irine alikuwa akinijia sana ndani ya kichwa changu katika namna isiyoelezeka.

    ************

    Criss!... Criss!....Criss!!!, nilisikia vizuri sauti ya mama ikiwa inanita ikitokea nje wakati nikiwa bado nikiwa naendelea kusoma kijitabu kile kilichoandikwa na Kaka miaka kadhaa. Niliiumia sana, huku bado nikiwa na shauku maisha ya kaka yalikumbwa nanini na kwanini Kaka aondoke kipindi ambacho nahitaji msaada wake kwajili ya maisha yangu? niliendelea kujiuliza maswali wakati huo sauti za mama zilizidi kupenya kwenye ngome za masikio yangu. Nilificha haraka haraka kijitabu kile ili hata kama mama akija asijue nilikuwa nafanya nini ndani. Niliona sehemu sahihi ni chini ya kitanda. Nilikiweka haraka na kutoka nje....

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Huku kwa hamaki nilibamiza mlango wangu maana nilishajua mama m anaweza kuwa amekasilika kutokana na kitendo cha kuniita muda mrefu. Kutoka tu macho yangu yaligongana na ujio wa mjomba hapo nilifahamu kuiita kote kule kwa mama ni juu ya ujio wa mjomba.

    " Muda wote mwanangu Criss ulikuwa unafanya nini cha ajabu huko chumbani?”, punde tu niliponiona mama alianza kwa kuniuliza swali, kabla hata sijajibu aliendelea kuzungumza. “Haya nenda uchukue chupa ukamletee mjomba wako soda .Nilifanya kama mama alivyoniambia huku tiyari mjomba alishaipokea salamu yangu ambayo nilitoa kwa sauti ya chini wakati mama akiendelea kuongea. Kwa muonekano wa mjomba nilihisi ujio ule haukuwa wakawaida maana si kawaida yake kuja nyumbani katika siku kama. Mara nyingi huwa ujio wake unakuwa na angalua kuna jambo muhimu. Kutoka na mama yangu huwa mtembeleaji mkubwa wa ndugu zake, na sisi wengine. Hivyo ujio ule ulinifanya nitake kujua ni jambo gani haswa lilomleta mjomba nyumbani, roho ya kiudadisi ilikuwa bado ikinitawala.



    Nilingia ndani nikachukua chupa ya soda ya kampuni ya pespsi na kuelekea dukani kwa Mangi. Wakati huo nilimuacha mama akiwa anazungumza na mjomba, mazungumzo ambayo nilikuwa nikitaka kuyafahamu kwa udi na uvumba . Maana ugeni ule ulishanijengea fikrandani ya kichwa change , fikra ambazo hazikuwa na majibu sahihi kwangu.

    Miguu yangu haikuwa nyuma baada ya kutoka ndani nilipiga hatua ambazo hazikuwa nyingi hatimaye ni nilikuwa tiyari nimelifikia duka la Mangi na kwa bahati nzuri hakukuwa na foleni kama siku nyingine. Niliagiza mara moja na kurudi nyumbani kwasababu hakukuwa mbali hata si kuchelewa kufika nikampatia ile soda mjomba. Taratibu mjomba aliendelea kuinywa huku akien-delea kuzungumza na mama.



    Nilijivuta pembeni kidogo, na walipokuwa wakizungumza na kuketi, na kuyatega masikio yangu, masikio nayo hayakuniangusha kwa mbali yaliweza kuyasikia mazungumzo yale. Mazungumzo ambayo kadiri nilivyokuwa nikiyasikia ndipo roho yangu ilianza kupambana na maumivu makali, hakika roho ilikuwa ikiniuma mno kutoka na kile ambacho mjomba alikuwa akizungumza. Yalinifanya kwa mara nyingine nivichukie nichukue viumbe vinavyoiitwa wanawake hasirani kwa katika maisha yangu.

    Nilinyanyuka pale nilipokuwa nimeketi, si kutaka tena kuendelea kuyasikia yale, wakati huo mjomba alionekana myonge sana. Unyonge ulikuwa ukichangiwa na kile ambacho alikuwa akisema kwa mama. Hata nilipokuwa naingia ndani macho yangu yaliona wazi wazi hali ile.



    Niliamua kujifungia mlango kimya ndani ya chumba changu, taratibu nakienda kitanda, kitanda kikanipokea chenye hakikuwa na hila kama wanadamu wengine, kilikubali kuupa faraja mwili wangu. Mawazo nayo haykuwa mbali, punde nilipojipunzisha ni kifakari maneno yale ya mjomba nayo yakaona ni muda muafaka wa kunisurubu. Kweli yalifanikiwa, muda mchache yalianza kunitoa machozi, hali iliyoniongezea hasira dhidi ya viumbe vinavyoiitwa wanawake. Ni laani vikali, nadhani hata niliweza kumkufuru Mungu kwa kwenda mbali zaidi, niliwatoa thamani kabisa viumbe hivyo, na hata kumweka mama yangu katika aina nyingine ya jinsi na si jinsia ya viumbe hivyo, hakika kichwa change kilikuwa maji. Maji yalipoteza uelekeo na sasa yalikuwa yanaenda sehemu isiyojulikana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya muda kidogo, hasira zilivunipungua ni kakumbuka bado nilikuwa na kazi ya kusoma kijitabu kile kilichoandikwa na kaka katika miaka kadhaa iliyopita . nikaishughulisha mikono yangu kupambana kule nilipokuwa nimekiweka, hapakuwa pengine nilikuwa nimekihifadho chini ya godoro. Sekunde kadhaa mikono yangu ilikuwa tiyari imekamata vizuri, ikiendelea kutafuta sehemu niliyokuwa nimeishia, macho nayo bado yalikuwa katika ubora wake, yaliweza kuona vizuri maandishi yale.

    *******

    Siku kadhaa mbeleni jambo lile linishinda kabisa kwa namna nilivyokuwa nikimpenda Irine katika maisha yangu, iliniwia vigumu sana kusahau penzi lake. Kiukweli moyo wangu ulimpenda kweli, hapo nikanza kuikumbuka siku ambayo kwa mara ya kwanza nilipoonana nae. Si kujua Mungu anakusudio gani ndani ya maisha yangu katika siku hiyo. Ilikuwa kama siku nyingine ziendazo dunia lakini tofauti yake akili yangu ilikuwa tiyari haikuwa na mpango wa kutoka juu ya kitanda cha hosteli nilipokuwa nimelalia. Ilitokana na kimvua cha wastani kilichokuwa kimepiga siku nzima ndani ya siku hiyo na kuleta kiubaridi ndani ya jioni ya siku hiyo, hali ambayo ilinifanya niendele kubiringita ndani ya kitandaa. Lakini baada ya muda niliamua kujitoa eneo lile, nilijishangaa tu hata wazo la kwenda cafe area.



    Hivyo baada ya kushindana na fikra zangu nilijukuta miguu yangu inatoka ndani na kuongoza maeneo yale. Nilipofika eneo lile niliingia na kuagiza chakula kama kawaida yangu, na kuelekea meza ambayo mara nyingi huwa naitumiaga eneo lile. Muda kidogo baada ya kukaa muhudu alilete chakula nilichokiagiza.

    Wakati naendelea kula walikuja wadada kama watatu hivi karibu ilipokuwa meza yangu na kuketi katika moja ya meza ambayo haikuwa mbali na nilipoketi mimi. Sikuwajali kama kawaida yangu, niliendelea kula. Kwa mbali nilikuwa nikiyasikia mazungumzo ya wadada wale. Balaha lilikuja pale walipokuwa wakiendelea kuzungumza. Maana kuna sauti ya moja kati ya wale wadada ilikuwa ikipenya sawia ndani ya ngoma za masikio yangu. Na kuleta hali ya tofauti kidogo, hali ambayo kamwe sikuwahi kufikiri kama ingeliniacha na maumivu makali ndani yake.



    Hata sikujua sauti ile ilikuwa inalengo gani pale mwanzoni maana kwasababu kupenya kwake ndani ya masikio yangu ilikuwa ukiupa moyo wangu faraja kwa muda mfupi. Nilijihisi kusisimuka sana ndani ya mwili wangu, msisimko ambao kwamwe sikutaka tamani ache kunisisimua tangia nilipoanza kuisikia. Ilinibidi nigeuke kuelekea sauti inapotokea hakika macho yangu hayakuamini kile nilichokuwa nikikiona, nadhani yalikuwa katika dhahama nyingine, ni hiyo dhahama ambayo imeghalimu maisha yangu kwa kiasi kikubwa.



    Nilihisi kama nipo ndani ya ndoto vile, katika jioni ile, haki ilikuwa ni ndoto ambayo ilikuwa imekuja bila ya kuyafunga macho yangu labda kuwemo kwenye usingizi.

    Uzuri wa yule msichana hakika uliendana vyema na sauti iliyokuwa ikimtoka kinywani mwake. Mungu alimpa kila kitu si sauti tu sura nzuri, umbo zuri la wastani , huku mashavu yake yakipambwa na vishimo viwili , kimoja upande wa kulia wa shavu lake na kingine upande wa kushoto wa shavu lake. Zilipamba vyema urembo wa msichana yule, na kuleta utofauti na wanadamu wengine, hakika Mungu alimuumba katika utulivu wa hali ya juu utulivu ulisabaisha kuleta burudani kwenye mboni za macho yangu punde nilipoigeuza shingo yangu kufatisha sehemu ilipokuwa ikitoka sauti ile ya mwanadamu yule.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kumjua msichana aliyekuwa akiitwa Irine ndani ya ubongo wangu. Mwanzoni si kuwa nalijua jina ilo kabisa, kutokana nilivutiwa naye nilifanya juu chini kufatiria habari zake. Na baada ya purukushani katika siku mbili tatu hatimaye niliweza kulifahamu vyema jina hilo, pamoja na baadhi ya vitu ambavyo nilikuwa niliviona vya msingi katika kukamlisha hadhima yangu juu ya msichana yule. Sikupata shida sana kutokana na umarufu wangu, na watu kunithamini sana ,na hadhi niliyokuwa nayo ndani ya chuo. Vyote hivyo vilitokana na uwezo wangu wakukimbia katika mbio fupi kuliko mtu mwingine chuoni pale katika mashindano mbalimbali.



    Ulikuwa kivutio kikubwa sikuwahi kuwa na mpinzani kabisa . Ilo lilinijenge jina kwa kiasi kwamba ilinifanya niwe rahisi kupata habari zake. Kwasababu rafiki zake walinitambua vyema, sikupata tabu hata pale nilipoenda kuzungumza nawo kwa lengo la kutaka kujua habari zake walinipa ushirikiano mkubwa sana. Muda mchache niliweza kumfahamu vyema ndipo malindo yangu yalipoanza ,na hatimaye Irine aliingia kwenye imaya yangu.

    *********

    Mambo yote yaliyo tokea kipindi cha nyuma kidogo yalinifanya wazo la Irine kututoka kichwani mwangu, siku hadi siku kuwa gumu zaidi. Wakati huo afya yangu ilikuwa imelejea kama zamani , licha ya daktari kusisitiza nisifikirie chochote kile haswa kitu kiitwacho mapenzi kwa kipindi chote nikiwa bado najiuguza kabla sijaenda India aliposhauri juu ya uchunguzi zaidi kuhusu moyo wangu.



    Penzi lake kwangu lilikuwa kama vile penzi la kipofu, nilipagawa sana na msichana yule, sidhani kama ulikuwa upendo wa kawaida, nilihisi uwepo wa nguvu za giza katika jambo lile, Lakini fikra zangu hazikuwa zikikubali moja kwa moja, hata kunakipindi nilijilaumu sana lakini mwishowe nilijikuta nikijipuuza mwenye na Irine akirudi tena ndani yangu. Na kujipongeza ya kuwa nilikuwa na mapenzi ya dhati na binti huyo , licha ya kutoonesha kunithamini kipindi chote nilichokuwa nikiugua niliamini ipo siku ningeweza kumweka sawa na kurudi katika upande wangu. Juu ya kuwa anipendi suala hilo halikuwa likipata nafasi kwangu.

    Nikikumbuka maneno yake, hata nguvu zilikuwa zikiniishia. Kuna baadhi ya siku macho yangu yalikuwa ya kivimba na kuwa mekundu kutona na kilio ambacho hakikuwa na mbembelezaji.



    Nilikuwa nikishikwa na uchungu sana kila nikimfikiria msichana yule hata ilifika kipindi mama yangu alikuwa anapoteza furaha baada ya kubaini hali yangu. Mama hakuwa akifurahishwa na hali ile ilikuwa ikijitokeza upande wangu lakini hakuwa namna.

    **********

    Zilipita wiki tano baada ya kupona majeraha yote , grafla hali yangu ilianza kubadilika mwili ulianza kukosa nguvu na maumivu madogo yalianza kujitokeza eneo la kushoto la kifua changu ambapo ulipo wangu moyo. Hali yangu ya kimwili kijumla ilianza kudhoofu tofauti na mwanzoni.

    Nilimueleza mama jinsi nilivyokuwa na jisikia na hata hali yangu ilivyokuwa ikibadilika, kumbe hata yeye aliiyona. Maskini mama alianza kutafuta pesa kwajili ya kutibiwa na kibaya zaidi haikuwa hapa nchini, bali nje ya nchi kutokana hali ile ambayo daktari alishaiyona kabla na alishasema nini cha kufanya mapema. Mama aliangaika pekee yake sehemu mbali mbali hadi kule mzee alipokuwa akifanyia kazi ila bado hakufanikiwa kupata pesa ya kutosha, angalau walimpa pesa kidogo lakini zilikuwa hazitoshi kugharamia safari ile pamoja na matibabu ndani ya nchi ya India.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilimbidi Mama auze moja ya nyumba yetu ilitoachia marehemu baba , aliuza tu ilimladi iliaweze kufanikisha matibabu yangu yalikuwa yanaitajika kwa namna yoyote ile, maana mambo yalionekana yangeweza kuwa mabaya kadiri siku zilivyokuwa zinaenda.

    Mipango ya safari ilipangwa haraka haraka baina yangu na mama ambaye ndio alikuwa akinisimamia mwanzo hadi mwisho katika ugonjwa wangu. Na tulipo hakikisha mipango imekaa sawa mama alimchukua mdogo wangu Criss na kumpeleka kwa mjomba iliakakae kipindi chote ambacho tutakuwa hatupo. Tusingeweza kwenda naye licha umri wake kuwa mdogo lakini ilitubidi kwasababu ya pesa kuwa haitoshi ilitulazimu. Sikupenda hata kidogo litokee lile kwasababu upendo wangu dhidi ya mdogo wangu. Macho yangu hayakuwa tiyari kuipoteza taswira yake ijapokuwa ni kwa muda mfupi ila kitendo kile kiliniuma sana.

    **********



    Maneno yale yalikuwa yameandikwa na kaka Eddy, ndani ya kijitabu kile yaliniingia kisawasawa kwa mara nyingine. Moyoni mwangu nilizidi kupata hasira juu ya viumbe viitwavyo wanawake moja kwa moja nilijua tu uwenda Irine ndio chanzo cha ugonjwa ule wa kaka na safari ya kuelekea huku India. Katika mwanzo ule ambao mpaka leo umebaki kuwa historia isiyofutika kichwani mwagu, huku ikiendela kunisurubu na kuniachia maumivu makali katika kila pembe ya mwili wangu.



    Gafla mazunguzo yale ya mjomba na mama ambayo yalikuwa ndio kwanza mabichi yakapita kichwani mwangu nikanza kujiuliza lakini kwanini naye mjomba ajilize kama mtoto kisa mwanamke, amemkosea nini mjomba?, maswali yalinikaba koo, majibu hayakuwa karibu ubongo wangu ulionekana nao kunisaliti, katika usaliti wa aina yake.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog