Simulizi : Tetemeko La Moyo
Sehemu Ya Tano (5)
Roho yangu haikuwepo tena dunia, kwa muda ule, maana nilipojitoma ndani, sikuona faida ya kuishi katika dunia. Dunia ambayo katika jicho la kawaida niliona hainitaki kabisa, Kiukweli niliamua kufanya maaumuzi haya, huku nikimsihi Mungu.
ENDELEA.
********
Yalikuwa maneno ya mwisho ndani ukurasa wa kitabu kile, maneno ambayo sasa yaliuponda sana moyo wangu, huku yakiniweka katika hali nyingine, hali ambayo kwa mara ya kwanza nilikuwa sikuwahi kuijua kama sababu ya kifo cha kaka yangu mpendwa, sababu ambazo mara kadhaa nilikuwa nikimuuliza mama lakini hakuwahi hata siku moja kuniambia kilikuwa kimetokea nini katika miaka kadhaa iliyokuwa imepita. Ni kweli kaka Eddy aliamua kujitoa roho yake mwenyewe yaani kunyinyonga kutoka na mapenzi, hakika alikuwa amependa sana, katika namna ya ajabu sana mpaka kufikia maamuzi yale, ambayo mwanzoni ilibaki kuwa siri ambayo si kuwa naitambua.
Ni kiwa kitandani pale nilianza kutoa shutuma kali kwa Irine kama vile nilikuwa nimewahi kumwona, nikiamini moja kwa moja yeye ndio sababu ya kifo kile. Na kama alikuwa hampendi kaka kwanini alikubali kuwa nae?, hakika nilijiuliza maswali ambayo yalizidi kuongeza gadhabu katika mwili wangu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sasa kitanda kilikuwa mwiba mkali, mwiba unachoma katika kila pande za mwili wangu, sikutamani kuendelea kuwa juu yake, niliamua kujitoa na kuelekea nje ya chumba change. Wakati huo kutoka kwangu nilikaribisha na harufu nzuri ya chakula. Huku tabasamu pana la mama likinikaribisha, kabla ya kuniambia ya kuwa muda si mrefu alikuwa akitaka kuja kunigongea iliniweze kupata chakula. Ni kama vile nilikuwa nimeota kutoka kwangu kwa muda ule. Na mimi sikutaka kuonesha tofauti yoyote niliachia tabasamu liliojaa upendo kwa mama yangu.
Siku ilikuwa tofauti sana, mara nyingi huwa mama anachelewa kula lakini siku hiyo tulijumuhika pamoja katika meza ya chakula, huku akiyatawala maongezi muda wote wa chakula, maongezi ambayo yalinipa faraja sana na hata kusahau machungu ambayo yalikuwa yamejenga ndani ya mwili wangu. Nilikula sana tofauti hata na kawaida, na kama ilivyo kwenye upande wa kupika mama hakuwahi kuniangusha hata kidogo. Chakula kilikuwa kitamu haswa, kadiri nilivyokuwa naona kama naridhika kula lakini utamu wa chakula kile, ulinifanya niendelee kula tu.
Hatimaye tumbo langu lilionekana kuzidiwa na hali ya kuendelea kula hivyo niliona wazi ningesabisha raha kuwa karaha muda wowote. Hivyo zoezi la kula lilinishinda huku nikimuahidi mama ya kuwa kesho asabuhi ningekiamkia chakula kile mapema sana, nilikuwa nikiogea katika hali ambayo ilifanya mama kutoka na kicheko kizito tukiwa pale, huku akinichombeza na maneno ya utani kama kawaida yake.
Tuliendelea kukaa mezani pale kwa muda kidogo baada ya kuamaliza kula. Hatimaye mama aliniaga kulekea chumbani kwake, niliamua kukaa pale sebuleni kwa muda kidogo huku nikitazama runinga, kidogo iliweza kunipotezea mawazo kadhaa yalikuwa yanapita kichwani mwangu, kiukweli nilikuwa na mawazo kadhaa wa kadhaa ya kinitawala kichwani mwangu japo nilijaribu kupambana nayo kiume lakini yalionekana kuniandama sana.
Runinga nayo ilionekana kushindwa kupambana na mawazo yangu, ambayo kiasi kikuwa nilikuwa nikifikiria kuhusu kaka, ni kweli alikuwa amepotea katika kifo ambacho kwa mtu wa kawaida unaweza ukadhani ni cha kizembe lakini kwa upande wangu niliumia mno.
Niliamua kuingia chumbani kwangu, kwa wakati huo muda ulikuwa umeenda sana, kutokana na uchovu wa mawazo yalikuwa yakinitawala nilivyoweka tu mwili wangu juu ya kitanda, usingizi wa aina yake ulikuja kunichukua.
Na kunifikisha asubuhi ambayo ilianza kwa kupendeza sana machoni wangu, hakika kama ilivyoanza kwa kupendeza, siku ilisha kwa kupendeza pia kwa upande wetu.
Niliendelea kukaa nyumbani, siku nazo hazikuchelewa hatimaye likizo yangu iliisha na kurejea shuleni wakati wote mama hakuwahi kuniambia chochote kuhusu kaka Eddy juu ya siri na mimi sikutaka kumgasi niliamini wazi tiyari nilikuwa nimeshafahamu hiyo siri ambayo mama allikuwa akitaka kuniambia, hivyo sikutaka kujishungulisha sana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilirejea shule ikiwa imebakiza miezi michache ilituweze kufanya mtihani wangu wa mwisho. Taratibu nilianza kupoteza habari za kaka Eddy, kadiri siku zilivyokuwa zinaenda shuleni pale. Nilijua juu ya kufikiri suala kama lile lingiweza kunipotezea katika masomo yangu. Japo mwazoni ilikuwa ngumu lakini kutokana na jambo ambalo lilikuwa linanikabili, mbeleni mambo yale yalianza kupotea. Huku nikiendelee kupambana sana katika kuipigania Elimu yangu kwa kiasi kikubwa.
Ikiwa imebaki wiki tatu kabla ya kufanya mtihani, katika mchana moja. Nikiwa na tafakari ya kile nilichokuwa nimekisoma ndani ya siku hiyo. Nilishangaa tu nikipewa taarifa na moja ya mwanafunzi mwenzangu ambaye tulikuwa tumezoena sana. Taarifa iliyokuwa ikinihitaji kuelekea ofisini kuona na mwalimu Rajabu, ambaye tulikuwa tumezoena sana kuokana na kufanya vizuri sana katika somo lake la historia. Sikujua sababu ya wito katika namna moja ama nyingine lakini siku hiyo ilionekana tofauti.
Nilivuta pumzi ndefu huku akili yangu ikijenga hofu ndani yake. Ni hiyo hofu ambayo sikujua kama ingeleta machungu sana katika mwili wangu na kuongeza uchungu maradufu juu ya viumbe viitwavyo wanawake, uchungu ambao kwa muda mwingi ulikuwa umeshapotea na kusaulika kabisa ndani ya mwili wangu.
Nikiwa ndani ya hali ya sintofahamu, miguu yangu iliongoza kuelekea ofisini, katika moja ya ofisi ambayo tiyari kichwa changu, kilikuwa kinaongoza miguu vilivyo, hatimaye nilikaribisha na ukimya wa hali ya juu, ukimya ambao ulitokana na kutokuwepo walimu wengi ndani ya ofisi ile, huku wachache wakionekana kuwa bize na shunguli zao. Ilinibidi nielekea moja kwa moja katika meza ya mwalimu Rajabu. Ambaye alinikaribisha katika namna ambayo, nilianza kuhisi uwenda kunajambo zito lipo ndani yake, ambalo kwa kiasi kikubwa lilikuwa linanihusu mimi haswa. Fikra zangu zikaanza kupambana na muonekano ule wa mwalimu Rajabu, huku nikiomba kusiwe na jambo baya lolote ambalo lingeniweka katika hali ambayo sikuwahi kuitegemea.
Ni kweli mwalimu Rajabu alikuwa ana jambo zito ambalo lilikuwa likinihusu sana.
Aliongea kwa upole sana mwalimu kuliko hata kawaida yake, huku akinisihi niwe mvumilivu katika kipindi kama kile, maongezi ambayo kaisi kikubwa yalikuwa yanamuongelea mama yangu, kutokana na simu aliyopokea kutoka kwa mjomba wangu. Ni hiyo simu iliyokuwa ikieleza hali ya mama baada ya kufanyiwa mambo ambayo kiukweli yalionekana dhahiri upande wangu hayakuwa madogo hata kidogo na mke wa mjomba, ajabu sasa sikujua chanzo cha yale yote, nikakumbuka vyema kabla sijaondoka nyumba katika miezi miwili na nusu iliyokuwa imepita kulikuwa na hakuna maelewano mazuri kati ya shangazi na mjomba, huku mjomba akidai kukimbiwa na mwanamke huyo, kimbilio kubwa likiwa kwa mama.
Moja kwa moja nilijiua wazi uwenda katika matatizo yale ya mjomba na mke wake, itakuwa ndio chanzo cha mama kuingia katika matatizo. Nililani vikali mwanamke yule huku nikijenga gadhabu kali ambayo muda ilikuwa imepotea dhidi ya viumbe viitwavyo wanawake, nikijiapiza kufanya kitu juu ya kile.
Kiukweli hata sikuweza kuendelea kumsimkiliza tena mwalimu licha ya kuniambia mjomba alitoa tu taarifa zile si kwajili ya mimi kwenda nyumbani bali nikunijulisha jinsi mambo yalivyo. Nadhani alikuwa amekosea sana maana akili yangu ilikuwa mbali sana. Nilijiuliza maswali mengi ambayo majibu yake yalikuwa mbali, kwa wakati ule.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Huku mwalimu Rajabu akiendelea kunisihi sana nisiweze kuwaza jambo lile, uwenda mambo yatakuwa sawa muda si mrefu. Lakini maneno yake nilivyokuwa nikiyapiama kwenye mizani ya kichwa changu, yalionekana dhahiri mama anaweza kuwa katika hali ambayo haikuwa si nzuri hata kidogo. Kingine kibaya ambacho kilinitia shaka, mwalimu Rajabu alionekana kama kuna jambo ananificha katika maongezi yake.
Nilimwitia mwalimu katika namna ambayo ilikuwa ni kama kumlizisha tu kwa muda ule. Huku akili yangu ikiwaza kutoroka shule ilikuweza kwenda nyumbani mapema iliniweza kujua hali ya mama. Kutoka na shule haikuwa mbali sana na nyumbani yaani ilikuwa katika ndani ya mkoa ya Dar es salaam, ambapo nyumbani kwetu ilikuwa chanika yenyewe ikiwa kigamboni. Haikunipa shida sana katika zoezi la kutaka kuondoka ndani ya shule. Japo kuwa sikuwahi kutoroka hata siku moja lakini njia zote ambazo wazoefu wakutoroka shule nilikuwa nazijua vilivyo.
Baada ya kutoka ndani ya ofisi ile, huku akili yangu ikiwaza kufanya jambo lile hakunichukua muda sana, nilimuendea rafiki yangu moja na kumwambia suala lile ambalo lilikuwa linanikabiri na uzuri mara nyingi huwa ananisikiliza sana. Hata nilivyomwambia jambo lile hakuleta kipingamizi. Huku akinisihi niweze kurudi shuleni mapema sana kutokana na mtihani ambao ulikuwa unanikabili katika majuma kadhaa ya mbele.
Alinisadia sana, ndugu yule katika kukamilisha zoezi langu la kutoroka, japo nilikuwa na ujasiri hakika kidogo ilijenga hofu kwenye mwili wangu, hofu iliyoletwa na kukumbuka habari za wahuni ambao huwa mara nyingi wanakaa nje kwajili ya kuvizia wanafunzi ambao mara kadhaa hutoroka, katika mpango ambao mwalimu mkuu aliweka katika kuthibiti utorokaji wanafunzi shuleni pale. Ambao watu hao wakifanikiwa kukamata wanafunzi wanawaleta shule na kupewa elfu hamsini kwa kila mwanafunzi moja. Hakika ilinipa hofu katika kufanya zoezi langu lile, lakini nilipomkumbuka mama yangu ujasili ulinipanda, huku liwalo na liwe likinitwala kichwani mwangu.
Uzuri mungu alikuwa upande wangu japo kuwa hapakuwa na giza, kutokana siku hiyo ilikuwa mchana ambayo ilikuwa ikienda jioni hivyo hata haikuweza kunisaidia kwa wale ambao walikuwa wakilinda wanafunzi. Mungu tu ndio alifanikisha lile mpaka na ingia kwenye gari la kuelekea Kongowe ambalo lingine fikisha kwenye gari mbagala hapo ningepata gari za Gongo la mboto kisha kupanda gari za nyumbani Chanika, hakuna kitu kibaya chochote ambacho kiliweza kunitokea, nilishukuru Mungu sana kwa mara nyingine.
Safari haikuwa ndogo kabisa ndani ya siku hiyo, kutoka na kubadilisha magari kadhaa huku foleni za hapa na pale zikiikabili safari yangu. Ila hatimaye nilingia nyumbani huku sasa yangu ya mkononi ikionesha vyema saa tano juu ya alama, ndio pua yangu ilikuwa ikininusa hali ya hewa ya pale nyumbani.
Huku nikipokelewa na giza na ukimya ulikuwa ukionesha dhahiri yakuwa mama hakuwepo pale, hilo nalo liliongeza hofu ndani yangu, nikiangalia muda ulikuwa umeenda sana wazo la kwenda kwa mjomba kwa muda ule lilikatishwa. Na juu ya kupata usafiri wa kunitoa pale na kunipeleka nyumbani kwa mjomba, ambapo kulikuwa mbele ya chanika, maana mjomba yeye alikuwa akikaa Masaki ambayo ni mbele ya Chanika.
Akili yote haikuwa kabisa, hakika niliendelea kumlani shangazi kwa jambo ambalo wazi lilikuwa likionekana ni kubwa kufikia mama kuhitaji uangalizi ambao mpaka muda ule sikuwa na jua ya kwamba ni hospitali au nyumbani kwa mjomba.
Hakika mungu alikuwa upande wangu katika jambo lile japo nilikuwa nimechanganyikwa sana kutokea shuleni lakini sikuweza kusahau funguo za nyumbani, ambazo nilikuwa na miliki maana mama alishanizoesha kuniachia funguo, huku yeye akibaki na funguo zingine. Nilitafakari kidogo nikajitoma ndani baada ya kutoa mahali funguo nilipoziweka.
Kweli baada ya kufanya zoezi la kufungua mlango, nilikaribisha ndani huku nikiziendea taa ilikuweza kunipa mwanga ndani mule, taa nazo hazikuwa na hiyana zilikubali nami na kuanza kunikaribisha. Katika namna ambayo sikuitegemea. Nyumba ilikuwa imebadilika sana, kulionekana dhahiri uwenda kulitokea purukushani ambayo haikuwa ya muda mrefu sana maana, vitu havikuwa katika mpangilio wake kabisa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-
Hali ile nayo ikadhidi kuleta dhahama kwenye kichwa changu, huku nikijenga taswira ya jambo ambalo lilikuwa kama giza ndani ya fikra, hakika fikra zilionekana kunisaliti maana hazikuniletea jibu sahihi kwa nyakati kama zile, si hivyo tu hata usiku nao ulikuwa mrefu sana kwa upande wangu.
Uchungu ulikuwa umenikamata vilivyo, huku taswira ya mama ikininyanyasa ndani ya usiku ule, na kili wazi upendo nilikuwa nao dhidi ya mama yangu hakuwa na kipimo ndugu msikilizaji.
Hatimaye asabuhi, ambayo ilikuwa kama mwaka ndani ya usiku. Iliingia katika namna ambayo hakunihitaji hata kuoga zaidi ya kubadili nguo, na kuongoza balabala, kuelekea kituoni, kuangalia gari ambazo zingeniwezesha kufika kwa mjomba. Sikupata tabu sana, baada ya dakika kadhaa nilikuwa ndani ya gari, ambayo hakutumia muda mwingi hatimaye niliwasili, nyumbani kwa mjomba. Huku nikaribishwa na ukimya ambao, nao ulizidi kunijengea hofu kwenye kichwa changu, kiukweli nilishanganyikwa maana, hata miguu yangu haikuweza kusimama nikiwa pale.
Nilinyongonyea, kabisa sikuwa na nguvu ndugu msikilizaji, hata muda ulivyokuwa unaenda nikiwa nje ya nyumba ya mjomba sikujua, nilishangaa tu jua likiniwakia nikiwa pale lakini halikuwa na tija kabisa kwenye mwili wangu.
Wakati nikiwa kwenye tafakari nzito, ni nyakati hizo ambao kidogo nilipokea tumaini ambalo lilikuwa limeshapotea kwa upande wangu, hakika nilifulizia maswali mia kidogo mjomba ambaye alikuwa mbele yangu, maswali ambayo sikumbuki kama mjomba alinijibu au la. Nilichokumbuka tu mjomba alinisihi nitulie kwa muda ule, na ikiwezekana niweze kurudi shule mara moja, jambo ambalo kwa upande wangu halikuwepo kabisa. Kuhusu kurejea shuleni huku sielewi hali ya mama hilo lilikuwa jambo ambalo hakika nisingiweza kulifanya hata ingekuwa kwa kupigwa ama.
Baada ya mjomba kuona nilikuwa nikileta ukinzani kwa kile alichokuwa anaongea, alinisihi ni msikilize kwanza, nami sikubisha nilimpa nafasi ya kujieleza, maneno ambayo kamwe yalizidi kuongeza hasira kwangu na kuapa kufanya jambo baya dhidi ya shangazi, ambalo sikuwahi kufikiria uwenda lingiweza kutimia katika namna ambayo ingenigharimu kwa kiasi kikubwa.
Ukweli tulifika hospitali baada ya mvutano dhidi yangu na mjomba kuangalia hali ya mama ambaye, niilibaini haikuwa nzuri kwa wakati ule kutokana na shambulio alilofanya shangazi, la kujeruhi vibaya maeneo ya upande wa kushoto wa kifua chake maeneo sahihi yalipokuwa moyo wake. Kutokana na dai lake la kuwa ndio chanzo cha ndoa yake kuvunjika dhidi ya mjomba wangu. Niliumia sana kutokana na jambo lile huku nikijiapiza kufanya kitu, kwa vyovyote vile ningefanya.
Najua chuki nilizokuwa nazo dhidi ya viumbe viitwavyo wanawake, ndio ilikuwa chanzo ya kufanya yale yote, hata kama shangazi alikuwa amefanya kosa lakini sikupaswa kuhukumu kwa namna ile. Wakati mama yangu aliweza kupona mapema ila mimi nilijichukulia mamlaka ya kufanya hukumu. Ukweli kabisa nilihusika katika kifo cha shangazi lakini sikusudia kufanya mauaji.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lakini sikuwahi kufikiria uwenda kwenye jambo langu lile zito ningesaidiwa na kiumbe ambaye katika maisha yangu niliwatoa thamani viumbe vyote vya jamii yake. Naichukia nafsi yangu sana, chuki zisiokuwa na msigi ndio ilikuwa chanzo yote yale, naweza sema maumivu ya moyo ya kaka yangu kipenzi Eddy ndio yalinifanya nifike kule.
Hakika nimejifunza kitu kwenye kesi yangu ile. Mwanamke aitwaye Catty ndio alikuwa amenisaidia sana katika jambo lile. Sasa niliamua kuliweka wazi kila moja aweze kuelewa kitu ambacho kilikuwa kipo nyuma ya jambo lile. Wanafunzi wenzangu, mama yangu, mjomba yangu aweze kuelewa nini chanzo cha yale yote.
**************
Yalikuwa maneno yangu ya mwisho juu ya mambo yalikuwa yamenitokea miaka kadhaa ya nyuma, maneno ambayo katika siku ile nilipokuwa nikiyatoa yalimtoa mama yangu chozi sana.
Hakika mama yangu alitambua kiasi gani moyo wangu ulivyokuwa ukimthamini kaka yangu pamoja nae. Najua aliteseka sana, katika muda wote nilivyokuwa ndani katika kesi iliyokuwa ikinikabili ya kuuwa, lakini baada ya msaada mzuri wa mwanasheria Catty, niliweza kuachiwa huru kwa kosa lile huku likihesabika kama ni kosa la kuua bila kukusudia. Yale yote yalinifanya nijifunze jambo katika maisha yangu yote nanyi ningependa mjifunze kupitia mimi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment