Search This Blog

Thursday, 2 June 2022

LOVE BITE - 1

 





    IMEANDIKWA NA : HUSSEIN O. MOLITO



    *********************************************************************************



    Simulizi : Love Bite

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Ni siku ya jumapili iliyokuwa na kila aina ya mchanganyiko wa watu kutoka sehemu mbali mbali walionekana kwenye kumbi za starehe.

    Wengi ambao walikua wanapenda taarab basi walijazana travertine hotel kuwaangalia jahazi.

    Kwa wengine wanaopenda bongo flavour basi walikutana bills,maisha,masai..Dar live na kumbi zingine zilikuwa na wasanii pendwa waliokuwa wanaburudisha week end hiyo.

    JOTHAN alikua anapendelea sana mixing za ma dj mbali mbali. Hivyo jumapili hiyo aliamua kwenda coco beach usiku huo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upepo mwanana uliokuwa ukipuliza huko coco beach na ukichanganya na big screen iliyokuwa inaenda sambamba na mixing za maana alizokuwa anazipiga dj huyo aliyezikonga roho za watu wengi waliokuwa pale, iilikuwa burudani tosha kwa waliohudhuria usiku ule.

    Jotham alipaki gari yake pembeni, alichagua kiti kilichukokuwa karibu na meza ya mwisho na kuagiza kinywaji alichokipendelea na kuendelea kufurahia mziki uliokuwa unaonyeshwa kwenye screen hiyo.



    Mara kwa mara madada poa walikuwa wanajipitisha pale alipo, lakini aliwachora tu na hakuwa na mpango nao.

    Baada ya dakika kadhaa, walitokea madada watatu waliokuwa wameingia pale coco beach na kuanza kutafuta mahali pa kukaa. Waliangaza meza nyingi zilikua na nafasi ya mtu mmoja au wawili tu na wao walikuwa na lengo la kukaa wote watatu kwenye meza moja.

    Baada ya kuangaza kwa muda, waliiona meza aliyokaa Jothan ikiwa na nafasi tatu za kukaa. Waliisogelea ile meza na walipokaribia tu kuifikia ile meza. Walishuhudia jamaa mmoja akiwa ameenda kukaa pale.

    “wewe kaka sogea sehemu yetu.” Aliongea mmoja kati ya wale wadada watatu baada tu ya kuifikia ile meza.

    “mbona hakuna alama yoyote kuwa mlikaa hapa. Hakuna vinywaji wala kitu chochote.” Aliongea yule jamaa huku akionyesha wazi kuvutiwa na ile sehemu iliyokuwa chemba lakini ikiwa inaonyesha vizuri ile tv.

    “ni vyema uwapishe kwa sababu waongeacho sio uongo.” Aliongea Jotham kumwambia yule jamaa. Hakuwa anapenda makelele ambayo alijua yatatokea baada ya mvutano huo wa kugombania ile sehemu.

    Yule jamaa akaamua kunyanyuka na kuwapisha wale warembo na yeye kwenda kukaa meza nyingine.

    “ahsante sana kaka, maana yule jamaa alitaka atubanie wakati sisi tumehangaika kutafuta meza tutakayokaa wote watatu”. Aliongea yule dada aliyeonekana kama kiongozi wao.

    Mavazi waliyovaa yalitosha kumshawishi mvulana yeyote rijali na kufanya iwe lazima macho ya matamanio kumtoka.

    Uzuri wa mabinti hao likuwa unashinda lakini huyo aliyekuwa kiongozi wao aliwazidi wenzake kwa kila kitu.

    Macho ya Jotham yaliona kila kitu kutoka kwa binti huyo mbichi. Chuchu zilitokeza kwa kujichora kwenye gauni ile nyepesi ambayo haikuwa na nguo nyingine ndani.

    “sikiliza oda zao, ziingize kwenye bili yangu” aliongea Jotham baada ya kumuita muhudumu aliyekuwa anamuhudumia toka afike pale.

    “ahsante.” Waliitikia wale madada baada ya kupewa ofa hiyo.

    Waliagiza vyakula na vinyaji walivyopendelea. Walipiga story za kawaida huku wakigongeana glass za vinywaji na kucheka.

    Jotham alikuwa kimya wakati wote huku akiwa bize kuangalia na kusikiliza mixing ambazo ndizo zilizomleta pale.

    Baada ya masaa kadhaa, alimuita muhudumu na kulipia bili yake.

    “ahsante kwa ofa yako.” Aliongea yule kiongozi wao baada ya Jotham kuwaaga.

    Jotham aliingia kwenye gari yake aina ya opah na kuondoka eneo hilo.

    Njiani alimkumbuka yule dada lakini aliishia kucheka tu kwakua hakuwa na hisia zozote za mapenzi juu yake. Zaidi alimtamani kuwa nae japo kwa usiku mmoja kwa jinsi alivyotoka. Hakika alikuwa na kila aina ya uchochezi wa kufanya ngono.

    Alifika kwake usiku mnene na kwenda kulala fofofo kutokana na usingizi uliojaa wakati huo.

    Asubuhi aliamka na uchovu tele na kwenda kuoga ili kujaribu kuupunguza uchovu aliokuwa nao. Alipomaliza kuoga. Alijiandaa tayari kwa kwenda kazini.

    Alisumbuka sana kuwasha gari lake lakini halikuwaka. Alipoangalia mafuta, aligundua kuwa wese lilikuwa limekata. Kwa kuhofia kuchelewa zaidi kazini, aliamua kwenda kituoni na kupanda daladala.

    Alifika kazini huku macho yake yakiwa mekundu yaliyoashiria kuwa bado alikuwa na usingizi.

    “mshikaji bora ukapate supu, maana hiyo harufu ya pombe uliyamka nayo ni noma. Utaongea vipi na bosi?” alishauri mmoja wa wafanyakazi wenzake aliyekuwa karibu naye.

    “poa, ngoja nielekee canteen basi.”

    Aliongea Jothan na kwenda canteen kupata supu ya mbuzi na chapati.

    Baada ya kunywa chai, alirudi na kuendelea na kazi.

    Saa nane ndio muda waliokuwa wanatoka kazini. Alienda kupata chakula cha mchana canteen na kuondoka zake kuelekea kituo cha daladala ambacho hakikuwa mbali na ofisini kwao.

    Alisubiri daladala kwa muda na kupanda gari iliyokuwa inaelekea mwenge kwa malengo ya kushuka kinondoni anapoishi.

    Usingizi ulichukua nafasi yake baada ya kupanda tu lile gari lililokuwa likisubiri abiria kwa dakika kadhaa pale kituoni

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya muda mrefu kidogo kupita, aliamka na kuangalia gari lilikuwa limefika wapi. Wakati akiwa anaanga angaza, macho yake yaligongana na yule mrembo aliyekuwa naye kwenye meza moja siku ya jana yake. Wote walikumbukana na kila mmoja akamuachia mwenzake tabasamu.

    Hapo alifanikiwa kumuona vizuri huyo msichana mwenye kila sifa ya uzuri.

    Usingizi uliendelea kumzonga Jotham na kujikuta anapitiwa na usingizi bila kuongea chochote na yule msichana.

    Gari lilifika mpaka mwenge na kupitiliza kituo alichokua anashuka Jothan. Aliamshwa na konda baada gari kushusha abiria wote.

    “tuko wapi hapa.” Aliuliza Jothan baada ya kuamka na kuangalia nje ambapo kulikua tofauti na mazingira anayoishi.



    “tumeshafika mwenge kaka.” Alijibu yule konda.

    Jothan aliangalia huku na kule na hakuona abiria yeyote aliyekuwa kwenye lile gari zaidi yake.

    Hakusikitika kupitishwa kituo, bali alisikitika sana kutochukua namba wala kujua jina la yule msichana aliyevutika naye zaidi baada ya kuonana nae kwa mara ya pili.



    Hakua na budi Jotham, zaidi ya kubaki ndani ya daladala na kugeuza nalo. Alipofika kinondoni kwa manyanya alishuka na kufuata njia ilyoelekea shule ya kambangwa secondary school na kupita chuo cha tumaini na kuingia nyumbani kwake ambapo hapakuwa mbali na pale.

    Hakuwa na hela nyingi sana, ila uwezo wa kula anachokitaka na kubadilisha nguo alikuwa nao.

    Alifika nyumbani na kujilaza kitandani kwake. Aliamka sa tatu usiku na kutoka kwenda sheli kununua mafuta kwenye kidumu kisha akaenda bar ya jirani na kupata chipsi kuku kisha akarudi nyumbani na kufungua tv na kuangalia yaliyomo.

    Saa tano usiku alianza kunyemelewa na usingizi,. Alizima tv yake na kwenda kulala.

    Alijikuta yupo na msichana yule mzuri kwenye fukwe za bahari wakipanga maswala yao ya kuoana. Alitoa pete na kumvisha mwanamke huyo mwenye kila aina ya sifa zilizompeleka Jotham kudata juu yake.

    Alikurupuka asubuhi na kugundua kuwa hali ile haikuwa halisi, bali alikua anaota.. aliangalia Alarm yake ambayo ilikuwa inalia wakati huo na kuizima.

    Alijiandaa na kupanda gari yake ambayo alishainunulia mafuta na kwenda nayo kazini kama kawaida.

    Baada ya mwezi mmoja kupita, Jothan alipata uamisho kikazi kwa miezi sita huko Morogoro.

    Alilaani ila hakua na jinsi kukubaliana na matakwa ya kazi. Ile ndoto ya kukutana tena na yule msichana iliyeyuka kwakua alijua kabisa kuwa kukaa kwake huko marogoro utakuwa mwisho wa kukutana tena na yule msichana kwa miezi mingi.

    Siku ya safari ilipofika. Alijiandaa na kupitiwa na gari la ofini kwao na kusafiri pamoja na wenzake waliopata uhamisho huo wa muda huko morogoro.

    Alifanya kazi huko kwa miezi mitatu na kupelekwa Arusha kwa ajili ya kumalizia miezi hiyo mitatu iliyobakia.

    Nia na madhumuni ni kuwafundisha kazi wafanyakazi wa mikoa hiyo kwakua ofisi yao ilikua imefungua matawi mapya katika mikoa hiyo.

    Zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya kurudi Dar, Jothan alipita barabara moja na kumkuta msichana mzuri akiwa ameshika tenga anauza maua. Moyo ulimlipuka ghafla na kujikuta anamsogelea yule dada bila kujitambua.

    “unauzaje maua” aliuliza Jothan huku akimuangalia binti yule mzuri ambaye alikua anatabasamu baada ya kumuona yeye pale.

    “shilingi elfu moja kwa kila moja.” Aliongea yule dada bila kumuangalia Jothan usoni.

    “nikitaka yote utaniuzia shilingi ngapi?” aliuliza Jothan huku akizidi kumtathmini binti yule huku akionyesha kufurahi na muonekano mzuri aliokuwa nao msichana huyo.

    “nisaidie kuhesabu, kisha nitajie idadi ili nikuuzie kwa bei ya jumla.”

    Aliongea yule dada na kumfanya Jothan kushangaa. Alijiuliza maswli ya haraka . labda hyule msichana hajui kusoma au alikua anamtega.

    “kwanini usiniambi tu, maana siyo mengi yaliyobaki.” Aliongea Jothan kwa sauti ya upole.

    “mi sioni kaka yangu.”

    Aliongea yule dada na kumfanya Jothan kupigwa na butwaa.

    “kweli???” aliuliza Jothan huku akiwa haamini alichoambiwa na yule dada.

    Kwa kumuonyeshea kuwa haoni, yule dada alivua miwani na kumuonyesha macho yake ambayo yalikuwa na watoto ndani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliingiwa na roho ya imani Jothan na kukiri moyoni kuwa yule dada alikua nahitaji msaada kwakua tatizo lake linatibika ila matibabu yake yalikuwa ghali sana.

    “unaishi mbali na hapa?” aliuliza Jothan baada ya kutoa noti ya shilingi elfu kumi na kuyachukua maua sita yaliyobakia.

    “si mbali na hapa, ni mtaa watatu hapo mbele.” Aliongea yule dada mwenye asili ya kichaga lakini asiyekuwa na lafudhi hiyo wala meno yake kuharibika. Ngozi yake ilikubali baridi na kuwa nyeupe yenye mvuto.

    “unaonaje kama nikikusindikiza?” aliuliza Jothan.

    “sawa”

    Alijibu yule dada na safari ya kuelekea kwao ilianza. Mwendo wa kuupapasa kwa fimbo ndio uliomfanya Jothan kuamini kuwa ni kweli huyo dada alikua kipofu.

    Alikaribishwa mpaka ndani na kukutana na mama yake huyo binti.

    “karibu baba,”alikaribisha mama yake yule dada na kuwapisha.

    “huyo ndio mama yangu wa peke, sina msaada mwengine zaidi yake.” Aliongea yule dada huku anatabasamu. Hakua anamuona Jothan ambaye wakati huo alikua anaumia juu ya msichana huyu ambaye alionyesha hali aliyokuwa nayo ameizoea.

    Aliaga baada ya kuongea na kupiga stori mbili tati ikiwemo maisha yao kwa ujumla.

    Alirudi kwenye nyumba waliyopangiwa na kumpa story rafiki yake anayekaa naye kwenye nyumba hiyo.

    “kwa hiyo unataka ufanyaje ndugu yangu,” aliuliza rafiki yake huyo baada ya kumpa mkanda mzima.

    “nitajitahidi kwa uwezo wangu wote ili BAHATI apone kabisa.” Aliongea Jothan na kumuonyesha rafiki yake ni jinsi gani ameguswa na mdada huyo.

    “kwa hiyo unampango wa kumchukua na kwenda naye Dar?” aliuliza rafiki yake huyo huku wakiendelea kula bisi zilizokuwa kwenye meza yao.

    “exactly” alijibu Jothan kiingereza kuonyesha msisitizo.

    Asubuhi ya siku ya pili, Jothan aliamka na kwenda tena kwa kina Bahati. Kabla hajafika, tayari alishamuana dada huyo mwenye juhudi na kazi yake akiwa barabarani kama kawaida yake akiuza maua.

    “mambo Bahati.” Alisalimia Jothan

    Kwakua sauti ya Jotham alikua ameshaijua, alimng`amua na kuachia tabasamu mwanana lililomuacha hoi Jotham.

    “safi” alijibu Bahati.

    Waliongea mengi na kubwa zaidi ni juu ya Jothan kumsaidia Bahati swala lake la macho. Bahati alifuraha sana na wote wakaenda kwa mama yake na kumpa taarifa zile njema.

    “nitashukuru sana mwanangu..mungu akuzidishie.”

    Aliongea mama yake Bahati na zoezi la kujiandaa kwa ajili ya safari ya Dar-es-salaam lilianza mara moja kwa kufua nguo zake chafu na kupanga zingine kwenye mabegi.

    “tutakupitia kesho saa kumi na mbili asubuhi.” Aliongea Jothan na kuaga.

    Bahati alipanga kila kitu chake akisaidiwa na mama yake tayari kwa safari ya kesho yake ambayo ilikuwa na matumaini makubwa kwake. Alisali na kumuomba mungu afike Dar salama na lengo la kufanyiwa upasuaji lifanikiwe kwa nguvu zake mungu wa viumbe vyote.



    Asubuhi na mapema gari ya kina Jothan ilimpitia Bahati na safari ya kuitafuta Dar-es-salaam ilianza.

    Njiani walipiga story na kucheka kama vile walikuwa wamezoeana muda mrefu au walikuwa wameshakutana kabla. Uchangamfu wa Bahati uliwapendeza watu wote waliokuwemo kwenye lile basi.

    Bahati alipendelea kukaa dirishani kwa ajili ya upepo. Lakini Jothan aliamini kuwa Bahati alikua anatamani pia kuona vilivyokuwa nje.

    Saa nane mchana walifika mombo na kupaki gari lao kwa ajili ya kupata chakula cha mchana. Waliokwenda haja walienda ilimradi safari ikiendelea pasiwe na usumbufu kati yao.

    “unapendelea chakula gani?” aliongea Jothan baada ya kuingia naye Bahati kwenye mgahawa huo.

    “kama kuna wali huwa napenda hata ikiwa na mboga yoyote.” Aliongea Bahati.

    Jothan alimuagizia wali na nyama ya kuku.

    “ahsante kwa chakula.” Aliongea Bahati baada ya kumaliza kula kile chakula.

    Baada ya hapo safari iliendelea na kufika ubungo saa kumi na mbili jioni. Safari ya kuwapeleka makwao ilianza na Jothan na Bahati walishuka kinodoni na kuingia ndani.

    Kutokana na uchovu wa safari, Jothan alimpeleka Bahati chumba atakachokuwa analala na kutoka nje kununua chakula watakachokula usiku huo.

    Baada ya kiza kutawla, Jothan alimpelekea chakula Bahati na kumuonyesha choo na bafu ambavyo vyote vilikua mule ndani kwenye kile chumba.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya mapumziko ya siku mbili, Jothan alimpeleka Bahati kwenye hospitali kubwa ya macho CCBRT kwa ajili ya upasuaji.

    Vipimo vilileta majibu mazuri kuwa kulikowa na uwezekano mkubwa wa kutolewa hivyo vitoto vya jicho na Bahati kona tena.

    Tarehe ya upasuaji ilipangwa kwa ajili ya upasuaji huo na Jothan alimpeleka Bahati ili apate huduma hiyo ambayo kama itafanikiwa itakuwa imempa maisha mengine kabisa mrembo huyo ambaye alikuwa haoni toka alipozaliwa..

    Muenendo mbaya wa utendaji kazi huko marogoro ndio uliomfanya Jothan kurudishwa tena mkoani humo. Alisikitika kumuacha mgeni wake katika hospitali kabla hajashuhudia matokeo ya upasuaji huo, lakini hakuwa na jinsi kwakua aliuachia uongozi jukumu la kumuangalia mgonjwa wake huyo.

    Miezi sita ilikatika akiwa huko Morogoro huku mawasiliano yakikosekana kati yake na Bahati. Hata alipouuliza uongozi wa kampuni yao walimwambia kuwa walikuwa wamempa kiasi cha hela baada ya kupona na tokea wamkabidhi hawakupata mawasiliano naye.

    Mawazo yalimsonga Jothan na hakujua kwanini Bahati aliamua kufanya vile. Baada ya uchumi wa kampuni hiyo kutengamaa na kupata uongozi uliokuwa ukipiga kazi kama ipasavyo, Jothan alirudi Dar kuendelea na majukumu yake ya kila siku.

    Alipofika nyumbani kwake palikuwa pamefungwa kama alivyo paacha. Aliingia ndani na kuikagua nyumba yake kwa macho kisha akaenda kulala kutokana na uchovu aliokuwa nao.

    Usiku wa jumamosi, aliamua kwenda club kwakua ni muda mwingi alikosa kwenda. Hivyo aliamua kwenda kupata mixing za ma dj wakubwa ambao wanajua kubadilisha nyimbo na kumfanya mtu aburudike na mpangilio wa nyimbo wanazoziweka kulingana na wakati.

    Wakati akiwa anaburudika na kinywaji chake huku akipata burudani nyingine akiwa kwenye kiti, mzuka alkampanda na kujikuta anaingia kati na kuucheza wimbo ulimvutia zaidi.

    Style alizocheza ziliwavutia wengi hadi baadhi ya wasichana walimfuata na kucheza nae. Aliifurahia sana hiyo siku na kurudi nyumbani akiwa na hamu ya kwenda tena siku ya jumapili.

    Kwakua alikua na likizo ya mwezi mzima kazini, hakuona tabu kulala mchana ili usiku akeshe tena kutokana na kuwa mziki ni starehe kubwa anayoipenda japokuwa siyo muimbaji.

    Siku hiyo alifika mapema na kutulia kwenye meza kwanza za nyuma na kuendelea kupata kinywaji na nyama choma kwa wingi.

    Wasichana wengi walimshobokea na kuomba ofa za bia. Kwakua Jothan alikuwa akiingia sehemu yoyote ya starehe huwa anakua amependeza mfukoni, basi hakuona shida kumwaga ofa mbali mbali kwa wanaomuomba bila kujali jinsia.

    Wakati disco likizidi kuchanganya. Kwa mbali kwenye mwanga hafifu Jothan alimuona msichana aliyemfananisha. Hakujiuliza mara mbili, alinyanyuka na kumfuata pale pale kwenye meza yao.

    Kadri alivyozidi kumsogelea, ndipo sura ya yule binti iliyozidi kumjia kichwani. Alimsogelea na kumuangalia kwa ukaribu zaidi.

    “kaka,tukusaidie nini?” aliuliza yule dada baada ya kumuona Jothan akiwa mbele ya meza yao amesimama na kumuangalia kupita kiasi.

    “sijui ndio wewe au nakufananisha?” aliongea Jothan huku akiwa haamini baada ya kumuona yule binti aliyekuwa kapendeza kupita kiasi.

    “kaka hizo swaga za kizamani kweli, za kuaza kufananishana mara sijui nilikuona wapi, achana na sisi bro” aliongea yule dada na kuwafanya wenzake kucheka.

    Kutokana na hadhi aliyokuwa nayo Jothan, alifedheheka kiasi na kumfanya akubali matokeo.

    Aliwaacha wale mabinti huku wakiwa wanamjadili na yeye kurudi kwenye siti yake. Ladha ya club ilipotea na kuamua kurudi nyumbani kwake.

    Alijitupa kitandani na kuwaza sana. Kwa jinsi alivyotekoa kufurahi kumuona tena yule msichana na majibu aliyopewa hata kabla hajajitambulisha yalimtia simanzi.

    “naweza kusema kuwa hawezi kunifahahamu, lakini hata sauti kashindwa kuitambua?... au kwa sababu sauti yangu ilikuwa ya kilevi?”

    Alijiuliza Jothan maswali mengi bila ya kuwa na majibu. Asubuhi ya siku ya pili alienda kupata supu maeneo ya karibu na kwao. Aliporudi alijitupa kitandani na usingizi ukamchukua mpaka saa kumi jioni. Njaa ilikuwa ina muuma sana. Aliamua kutoka na gari lake na kwenda kwenye Bar kubwa iliyokuwa msasani kwa ajili ya kupata chakula ambacho siku hiyo kilikuwa kinapikwa kwa ustadi mkubwa.

    Aliagiza oda yake na kuletewa baada ya muda kama wa dakika tano. Kabla hajaanza kula, kwa mbali aliisikia sauti ya yule mmsichana aliyekutana naye Club usiku wa jana yake. Alinyanyuka na kwenda kwenye ile meza ambayo alimkuta akiwa na rifiki yake mmoja wa kike.

    “samahani, wewe sio BAHATI!!!?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliuliza Jothan huku akiwa na uhakika asilimia zote kwakua alikua anafahamu fika kuwa yule ndiye mwenyewe kutokana na sauti yake na muanekano wake ingawaje kwa sasa alikuwa anavutia zaidi.

    “ndio mimi, umenijuaje?” aliuliza yule dada na Jothan aliachia tabasamu huku akitikisa kichwa chake.

    “ina maana Bahati hata sauti yangu huikumbuki?” aliuliza Jothan huku akiwa haamini kumuona Bahati akiwa na macho mazuri tena yaliyoongezewa uzuri na kope za bandia alizo bandika.

    “ningekuwa nakujua nisingekuuliza umenijuaje?” alijibu yule dada na kuendelea kuifyonza juice yake iliyosindikizwa na chpsi pamoja na nyama choma waliyokuwa wanakula yeye na rafiki yake.

    “nitakushangaa sana ukisema kuwa sauti ya Jothan hauikumbuki.” Aliongea Jothan na kubaki kumuangalia Bahati aliyepigilia mapigo ya ki sister duu.

    “WHO A JOTHAN BY THE WAY????”

    Aliuliza yule dada na kumfanya Jothan aondoke bila kuaga. Alienda counter na kulipia oda yake bila kuigusa na kuondoka zake.

    Hakuamini kuwa Bahati angewaza kuongea yale maneno mbele yake tena kwa nyodo wakati ni yeye ndie aliyemleta mjini na kumpa msaada wa kuyatibu macho yake baada ya yeye kuikubali hali ya ukipofu kutokana na kuwa kulikuwa na uhaba wa pesa nyumbani kwao.

    Jothan ilibaki kidogo tu agonge wakate anaendesha kutokana na mawazo yaliyochanganyikana na hasira kwa kile alichofanyiwa na Bahati.. Alijilaumu sana kwenda kula chakula pale na kuambulia maumivu. Alijuta kukutana tena na Bahati ingawaje mwanzoni alikuwa na hamu ya kuonana nae. Alifika nyumbani na kujilaza.

    ”who a Jonathan by the way??”

    Aliirudia ile kauli ya Bahati na kujikuta anashindwa kuamini kuwa yule ndie bahati halisi aliyemtamkia maneno yale.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog