Simulizi : Akirudi Tumuue
Sehemu Ya Pili (2)
DAKIKA ishirini baadaye, Sarah alikanyaga breki nje ya nyumba kubwa, ya kisasa, Ada Estate, Kinondoni. Muda mfupi baadaye yeye na Kasha walikuwa sebuleni. Ilikuwa ni sebule pana na iliyopendeza kutokana na kufurika samani zenye thamani kubwa. Kwa sekunde au dakika kadhaa Kasha alikuwa akijiuliza ni vipi Sarah ameweza kuyamudu maisha kwa kiwango hicho.
Huku akiendelea kuduwazwa na ubora wa sebule hiyo, mara Sarah alimzindua: “Unatumia kinywaji gani?”
Kasha alifikiri kidogo kisha akajibu, “Nikipata bia baridi nadhani roho itasuuzika.”
“Bia gani?”
“Tusker.”
Sarah alitokomea chumbani na kurejea baada ya muda mfupi, mikononi akiwa na sinia ambalo juu yake zililala chupa nne za bia. Dakika tano baadaye, koo la kila mmoja likiwa limeshapitisha mafunda kadhaa ya vinywaji hivyo, hatimaye Sarah alisema, “Kasha, pole sana kwa misukosuko iliyokukumba. Uniwie radhi kwa kutowasiliana nawe katika kipindi chote cha kesi yako. Nadhani unaujua udhaifu wetu, sisi wanawake; mwenye nyumba hii nd'o aliniteka...”
Alizungumza kwa zaidi ya dakika tano. Hatimaye Kasha naye akapata fursa ya kuzungumza lakini yeye hakuwa mzungumzaji sana. Alijali kumpa picha halisi ya jinsi alivyofanikiwa kuwa huru. “Usijali,” baada ya maelezo yake, alisema. “Pamoja na mikikimikiki yote lakini leo niko huru. Lakini sijui kama unaitambua mbinu niliyoitumia hadi nikawa huru.”
“Kwa kweli, sijui.”
“Hujui?!” Kasha alimtazama Sarah kama asiyeamini.
“Sikutanii, Kasha,” Sarah alisisitiza.
“Ok, nitakueleza.”
“Itakuwa vizuri.”
Zikamchukua Kasha dakika kadhaa akimsimulia Sarah jinsi alivyowatoka askari pale mahakamani. Hata hivyo, miongoni mwa kanuni za Kasha pale anapomsimulia mtu yeyote jambo lolote ni kutoweka kila kitu bayana, na hakuwa tayari kuitengua kanuni hiyo hata kwa mtutu wa bunduki.
Mwishoni mwa simulizi yake kwa Sarah, alikumbana na swali, “Enhe, halafu ukaenda wapi?”
Ni hapo alipoamua kutokuwa mkweli. “Nilibana hapahapa Dar,” alijibu. “Sikuona umuhimu wa kutoka nje ya jiji. Tukio nililolifanya lilikuwa kubwa, hivyo huenda ningekamatwa kirahisi.”
Sarah aliguna kwa mshangao. Akamkazia macho Kasha. Hatimaye akahoji, “Kwa hiyo uliishi wapi? Gesti?”
“Sikuwa na pesa ya kuniweka gesti kwa miezi yote hiyo miwili.”
“Kwa hiyo uliishije?”
“Nilifichwa na mtu kama wewe, mwenye kujiweza kama wewe,” Kasha alijibu huku akiachia tabasamu la mbali.
“Haya bwana we, hongera,” Sarah alisema huku akibibitua midomo. “Kwa hiyo hadi leo uko na huyo mkeo?”
“Mbona unanipa mke mapema ivo?” Kasha aliendeleza masikhara. “Yule alijitolea tu kunipa hifadhi, basi! Si zaidi ya hilo. Na leo nd'o nimetoka kwake, moja kwa moja. Nategemea ufadhili mpya kutoka kwako.”
Kwa mara nyingine Sarah aliguna. “Kasha! Si nimekwambia kuwa sasa mimi ni 'mtu' wa mtu?”
“Acha hizo, Sarah,” Shaka alimponda. “Kwani huyo jamaa mwenyewe yuko wapi?”
“Ametoka.”
“Akinikuta hapa atakuelewaje?” Kasha akalifuta lile tabasamu lake.
“Kwa leo hawezi kukukuta.”
“Hawezi kunikuta! Kwa nini?”
“Kwa sasa hayupo.”
“Mbona sikuelewi?”
“Ni kweli hujanielewa. Nitakuelewesha.”
“Poa.”
**********
BAADA ya Kasha kutiwa mbaroni, Sarah alihofia hata kwenda kumjulia hali. Alihisi kuwa kitendo cha kuonyesha sura yake katika kituo cha Polisi kingemponza. Angekamatwa na kuunganishwa na kesi iliyomkaabili mpenziwe. Hivyo, kwa uchungu mkubwa akaamua kutowasiliana naye kwa namna yoyote ile japo bado alimpenda na alimhitaji.
Kwa jumla Sarah alikuwa mzuri wa sura na umbile. Ni weusi wake wa kutakata, macho yanayoshawishi na kifua kilichobeba matiti ya ukubwa wa wastani, matiti yaliyoshiba ndivyo vilikuwa vigezo vilivyowafanya wanaume wakware wamkodolee macho ya matamanio.
Isitoshe, alijaaliwa mapaja makubwa, makalio makubwa na teketeke, ambayo pia yalimsababishia kero na usumbufu kutoka kwa wakware. Wengi wao aliwapa majibu ya kistaarabu lakini ya kuwakatisha tamaa. Ni wengi, siyo wote. Mwanamume mmoja, yeye alikuwa na moyo wa jiwe, pamba masikioni. Safari mbili za awali alizombembeleza Sarah aliambulia majibu kama ya waliotangulia.
Hakukata tamaa. Akajaribu mara ya tatu na ya nne, akitumia lugha laini sanjari na kumpa pesa nyingi ambazo aliamini kuwa ni ulimbo mzuri wa kuwanasa wanawake warembo. Naam, hatimaye alifanikiwa, Sarah akajikuta akiridhia kuupitisha usiku kucha nyumbani kwa bwana huyo.
Jambo moja lilimsukuma Sarah kufikia uamuzi huo. Aliutambua uzito wa kesi iliyomkaabili Kasha, kwa hali hiyo hakujipa matumaini kuwa Kasha atakiepuka kifungo cha miaka thelathini au maisha. Je, ataendelea kukaa hivihivi bila ya mwanamume hadi lini?
Hakuwa tayari kuendelea kuishi katika hali ya upweke. Alihitaji mtu wa kumliwaza, mtu wa kumfanya ajisikie kuwa na yeye ni binadamu kama binadamu wengine wanaoyafurahia maisha. Hivyo, alipolifikiria suala hilo la kuondokana na upweke, akajumlisha na pesa alizopewa na bwana huyo, uamuzi wa kumtema Kasha ukatwaa nafasi nafsini mwake, uamuzi ambao aliutekeleza bila ya kusita. Akamweka kisogoni.!
Ndiyo, Kasha alitapikwa, nafasi yake ikachukuliwa na mtu huyo ambaye hali yake kiuchumi ilikuwa njema kupindukia. Mtu huyo aliitwa Machibya. Makazi yake yalikuwa Kinondoni Ada Estate ambako alijenga nyumba ya ukubwa wa wastani, iliyopendeza. Alikuwa ni daktari katika hospitali moja kubwa iliyomilikiwa na tajiri wa Kiarabu wa nchini Yemen.
Kwa mwaka mmoja ambao alikuwa ameshafanya kazi katika hospitali hiyo, tayari akawa ameshapata nyumba hiyo, na kununua magari mawili ya kuringia; Honda Civic na Mercedes Benz. Na alipobaini kuwa tayari Sarah yuko katika himaya yake, hakutaka apate shida. Alimnunulia gari dogo, jeusi aina Nissan Laurel.
Maisha yakaendelea kuwanyookea hadi Machibya alipofungua hospitali yake binafsi eneo la Mikocheni 'B' na akaamua kuachana na ajira ya kwa yule Mwarabu wa Yemen. Na katika kuboresha huduma kwenye hospitali yake, alilazimika kusafiri mara kwa mara ng'ambo ya nchi ambako alichukua zaidi ya wiki mbili kabla hajarejea.
Kwa siku hii ambayo Kasha na Sarah walikuwa nyumbani kwa Machibya, mwenyewe alikuwa nchini Canada, na kuhusu hilo, Sarah hakumficha Kasha.
“Yuko Canada?” Kasha aliuliza kama vile hajamsikia Sarah vizuri.
“Ndiyo.”
“Tangu lini?”
“Ana kama wiki mbili hivi.”
“Kurudi?”
“Labda Jumamosi ya wiki ijayo.”
Kasha alifikiri harakaharaka. Siku hiyo ilikuwa ni Jumatano. Jumamosi moja ingepita kabla ya ile iliyodaiwa na Sarah kuwa ndiyo siku ambayo Machibya angerudi. “Kuna kama siku kumi ambazo hatakuwa amerudi, si nd’o maana’ake?” hatimaye alihoji.
“Yeah.”
“Hebu n'ambie, utashindwa kunipa hifadhi kwa siku mbili, tatu hizi ambazo hayupo?”
Jibu la swali hilo lilikuwa mbali kwa upande wa Sarah. Takriban dakika nzima ilipita ukimya ukiwa umetawala. Sarah alikuwa akifikiria uwezekano wa kumsaidia Kasha. Moyoni aliamini kuwa atakuwa amejitia matatizoni endapo atamhifadhi mtu ambaye huenda anasakwa na vyombo vya sheria kwa tuhuma za kuua na kutoroka akiwa chini ya ulinzi.
Hata hivyo, penzi kwa Kasha bado lilijikita moyoni mwake. Japo ni jambazi, hilo halikuwa tatizo akilini mwa Sarah. Bado penzi lilikuwa na nafasi kubwa, penzi lililotokana na faraja ya maneno na vitendo kila siku enzi za uhusiano wao. Ni penzi hilo lililomfanya aamue kumpa hifadhi Kasha japo kwa masharti.
“Uwezekano huo, upo,” alisema. “Lakini hebu fikiria, serikali bado haina usongo na wewe?”
Kasha alimtazama kidogo Sarah na kubaini kuwa anasita kuchukua uamuzi wa kumhifadhi. Hakujali. Badala yake alijibu kwa swali: “Kwa ile ishu ya mahakamani?”
“Ndiyo,” Sarah alijibu kwa msisitizo. “Ulitoroka na uliua. Unadhani watakuwa wamekusahau?”
“Siwezi kujua.”
“Sawa, lakini usijipe imani kuwa wamekusahau, Kasha,” Sarah alikazia. “Hakuna tena uzembe katika Jeshi la Polisi. Na usiombe faili lako likaibuliwa huko lilikochimbiwa, likatua mezani kwa afande mmoja mpenda sifa; nakuapia, utasakwa kama mhaini!”
Kicheko cha dharau kilimtoka Kasha. Akauliza, “Kwa hiyo, Sarah, nitambue kuwa uwezekano wa wewe kunipa hifadhi ni mdogo sana? Unawaogopa askari?”
Sarah alimtazama huku kakunja uso kwa mbali. “Kama wewe nd'o ungekuwa mimi usingeogopa au kusita-sita?”
Kasha hakujibu. Kwa mara nyingine alicheka, safari hii kicheko hicho kikiwa cha mbali huku akiyahamisha macho yake kutoka usoni pa Sarah na kuyazungusha sebuleni humo.
Ukimya ukapita tena. Hatimaye Sarah akauvunja ukimya huo. “Ok, niko tayari kukuhifadhi,” alisema. “Lakini uhakikishe kuwa hutoki-toki humu ndani. Yaani usionwe na mtu mwingine yeyote katika siku mbili, tatu utakazokaa hapa; sawa?”
Lilikuwa ni sharti dogo sana kwa Kasha. Huku akiachia tabasamu la mbali, akasema, “Ondoa shaka, Sarah. Kila kitu kitakwenda kama unavyotaka. Usihofu kitu.”
*** *** *** *** *** ***
KICHEKO cha dharau kilimtoka Kasha. Akauliza, “Kwa hiyo, Sarah, nitambue kuwa uwezekano wa wewe kunipa hifadhi ni mdogo sana? Unawaogopa askari?”
Sarah alimtazama huku kakunja uso kwa mbali. “Kama wewe nd'o ungekuwa mimi usingeogopa au kusita-sita?”
Kasha hakujibu. Kwa mara nyingine alicheka, safari hii kicheko hicho kikiwa cha mbali huku akiyahamisha macho yake kutoka usoni pa Sarah na kuyazungusha sebuleni humo.
Ukimya ukapita tena. Hatimaye Sarah akauvunja ukimya huo. “Ok, niko tayari kukuhifadhi,” alisema. “Lakini uhakikishe kuwa hutoki-toki humu ndani. Yaani usionwe na mtu mwingine yeyote katika siku mbili, tatu utakazokaa hapa; sawa?”
Lilikuwa ni sharti dogo sana kwa Kasha. Huku akiachia tabasamu la mbali, akasema, “Ondoa shaka, Sarah. Kila kitu kitakwenda kama unavyotaka. Usihofu kitu.”
**********
NI saa 2:30 usiku. Hii ilikuwa ni siku ya pili kwa Kasha ndani ya nyumba ya Machibya. Tayari alikwishaoga na sasa alikuwa sebuleni, katika sofa lilelile alilokalia jana mara tu alipokaribishwa na Sarah. Macho yake yalikuwa kwenye kioo cha televisheni ambako muziki ulioporomoshwa na kundi fulani la wanamuziki wa kizazi kipya ulikuwa ukionyeshwa. Kwa kiasi fulani burudani hiyo ilimtia faraja.
Alikuwa peke yake ndani ya nyumba hiyo tangu asubuhi baada ya Sarah kuondoka. Na ilimlazimu kufuata makubaliano yake na Sarah, kwamba asionekane hadharani. Kwa jumla hakupaswa kuonwa na mtu yeyote mwingine!
Kukaa ndani kama mtu aliyeswekwa kizuizini, kwake ilikuwa ni kero kubwa, lakini afanye nini? Ilimlazimu kufanya hivyo katika kuepuka madhara yanayoweza kumpata kama atakiuka utaratibu huo.
Hadi kufikia saa 6 mchana, tayari bia nne zilikwishapenya tumboni mwake huku akijiliwaza kwa kutazama vipindi mbalimbali vya televisheni.
Saa nzima baadaye alihisi uchovu ukimwingia. Bia zilikwishafanya kazi yake. Usingizi ukamvaa kwa kasi. Alizinduka saa 10 jioni. Alipotupa macho kwenye stuli akaiona chupa ya bia ambayo hajaimaliza. Lakini sasa hakuwa na haja nayo tena. Ni njaa iliyochukua nafasi. Akakumbuka kuwa kuna nyama ya kuokwa ndani ya jokofu.
Hakuchelewa, aliitwaa na 'kuishambulia.' Kisha akashushia na lita nzima ya maji baridi. Sasa akajisikia vizuri. Akaingia katika chumba alicholala jana yake. Humo akatwaa sabuni katika kijibegi chake kidogo na kuelekea bafuni. Siyo kwamba ndani ya bafu hilo hakukuwa na sabuni. La. Zilikuwamo, tena za aina mbalimbali, zote zikiwa za manukato.
Kasha hakuwa na mazoea ya kutumia sabuni za aina hiyo. Mara chache alizowahi kuzitumia alikumbwa na vichefuchefu, hivyo aliamua kutumia sabuni za kawaida, zile ambazo hutumiwa zaidi kwa kufulia nguo au kuoshea vyombo vya chakula.
Sabuni hii ya KUKU ni miongoni mwa sabuni alizozishabikia na kuzipenda. Dakika kumi baadaye alitoka bafuni huku akijisikia yu timamu kimwili na kiakili. Akarudi sebuleni ambako aliketi katika sofa lilelile na kushika rimoti ya televisheni. Akabonyeza-bonyeza hadi akaipata stesheni aliyoihitaji.
Akatulia akitazama mfululizo wa muziki wa kizazi kipya huku, mara chache akiwa ameizamisha akili yake katika muziki huo, na kwa kipindi kirefu mawazo yake yakiwa katika kujikwamua na 'ufungwa' huo sambamba na kujikwamua upya kimaisha.
Muda ulikwenda hadi ikatimu hiyo saa 2:30 usiku. Hatimaye saa 3 ikakanyaga. Yeye hakujali. Alijiamini. Japo Sarah alikuwa hajarejea, hata hivyo hakuwa na wasiwasi. Alitambua kuwa hiyo ni nyumba ya mwanamume mwenzake, Machibya. Lakini hakutaka kujenga hisia kuwa huenda Sarah kamlaghai kuwa Machibya yuko safarini Canada kumbe yuko hapohapo Dar.
“Hata akiwa amenidanganya, hawaniwezi,” hatimaye alijikuta akinong'ona kama kichaa. Akakunja ngumi na kuongeza, “Nitamdhibiti huyo bwana'ake. Kufumaniwa siyo kigezo cha kumnyong'onyesha mfumaniwa. Unaweza kufumania na mfumaniwa akakushikisha adabu. Kama huyu malaya atakuwa ameniuza, basi sitauzika! Na hapo ndipo atakaponijua… Nitawaonyesha yeye na huyo hawara yake kuwa mimi ni nani!”
Kufikia hapo akaachia tabasamu dhaifu lakini la kujiamini. Akaunyanyua mguu mmoja na kuupachika juu ya mwingine. Mara kicheko kifupi, kicheko cha chini, chenye taswira ya hasira iliyojikita moyoni, kikamtoka.
Sasa akawaza jinsi atakavyopiga hatua moja mbele katika kuondokana na 'ufungwa' huo na jinsi atakavyopiga hatua kadhaa mbele kimaisha. Zilimchukua takriban dakika tano akiwaza hili na lile. Hatimaye akapata ufumbuzi.
**********
SARAH alikanyaga breki za gari nje ya geti saa 3:45 usiku. Ilikuwa ni nyumba ya kisasa, yenye uzio mkubwa, huku geti la mbele likiwa ndilo kiingilio rasmi kwa yeyote mwenye haja ya kuingia humo.
Machibya hakupenda kuajiri mlinzi kwa kuwa aliona hakuna umuhimu wa kufanya hivyo. Alichofanya katika kuimarisha ulinzi wa nyumba yake ni kutandaza umeme katika seng'enge zilizopandikizwa juu ya ukuta kuilinda nyumba yake. Getini aliweka kitasa maalumu ambacho yeye na Sarah ndio walioweza kukifungua kwa kutumia kifaa maalumu cha kielektroniki, kifaa kidogo kilichojaa katika kiganja cha mkono lakini kikiwa ni cha kisasa.
Kwa kutumia kifaa hicho, Sarah hakupata shida kulifungua geti hilo kabla hajaingia na gari lake la kifahari, Nissan Laurel dogo, jeusi lililokuwa na mvuto mkubwa machoni mwa yeyote ajuaye magari mazuri. Muda mfupi baadaye alikuwa sebuleni.
“Vipi, nimechelewa sana?” alimuuliza Kasha.
“Sana, baby,” Kasha alijibu. “Nimekuwa mpweke sana. Tangu asubuhi hadi saa hizi niko ndani tu.”
“Pole sana, baby. Us'jali. Lakini bia si zimekuliwaza kidogo?”
“Kwa kiasi fulani,” Kasha alijibu huku mchanganyiko wa mambo ukimzingira kichwani.
Aliwaza jinsi atakavyozungumza na Sarah juu ya suala lililomsumbua kichwani. Hakujua kama Sarah atamwelewa na kuafikiana naye. Kama hatamwelewa wala kuafiki, ni dhahiri Kasha atakuwa ameumbuka. Itakuwa ni aibu kubwa. Na hapo ndipo huenda hifadhi yake ikavunjwa rasmi!
Isitoshe, kwa usiri mkubwa, Sarah anaweza kuwatonya askari ambao watakuja kumzoa kama mzoga. Hisia hizo zilimfanya aamue kuusaka ujasiri. Ndiyo, awe na ujasiri wa kupanga maneno kitaalamu na kutokuwa na soni ya kumwambia Sarah hicho alichopanga kumweleza.
Akilini mwake aliamini kuwa, ili wazungumze kwa utulivu, lazima wawe na bia mbele yao. Hivyo, alichokoza: “Vipi unajihisi uchovu?”
“Kwa nini?”
“Kutokana na mahangaiko ya kutwa nzima.”
Sarah alitabasamu kwa mbali. “Ni kweli. Lakini ni uchovu mdogo tu.”
“Keti basi upumzike. Uchovu utakutoka, na hasa kama utashushia bia bariiidi.”
Sarah alicheka kidogo. “Yeah, hapo umesema.”
Sarah alijitupa sofani. Lakini punde tena akanyanyuka na kulifuata jokofu ambako alitoa bia moja na kumgeukia Kasha. “Na wewe?”
“S'o mbaya kama nitaongeza moja.”
Sarah akatwaa chupa nyingine na kumfungulia Kasha.
Hawakuishia bia moja, moja. Saa nzima baadaye Sarah alikuwa ameshashusha bia tatu tumboni huku Kasha akimalizia ya pili. Sasa Sarah alichangamka. Aibu zikamtoka. Maongezi yaliyofuata hayakuvihusisha vinywa pekee, la. Hata mikono yao iliongea kwa namna yake, maongezi yaliyowapa faraja waliyoihitaji.
“Sarah,” kuna wakati Kasha alimwita.
Sarah hakuitika. Yale waliyokuwa wakiyafanya yalimteka akili kwa kiasi kikubwa. Hakuhitaji kuzungumza, alihitaji starehe.
“Sarah,” Kasha alirudia, safari hii akiikwanyua mikono ya Sarah iliyokuwa ikitalii hapa na pale maungoni.
Ni zuio hilo lililoirejesha akili ya Sarah kwa Kasha. Akaunyanyua uso na kumtazama, macho yake yakionyesha bayana kuwa kuna jambo zaidi alilolihitaji, jambo litakalomfikisha kileleni mwa starehe hiyo waliyoianza.
Kasha hakuwa na tatizo lolote. Japo siyo kwamba alimhitaji sana Sarah kimapenzi, hata hivyo hakuona kama ilimstahili mtu kama yeye, mwanamume aliyekamilika kila idara, kulala ndani ya jumba kubwa na mwanamke mrembo, Sarah, wawili tu, huku kila mmoja akitumia chumba chake.
Alichukulia kuwa kwa mwanamume yeyote afanyaye hivyo kwa zaidi ya siku moja, tena akiwa na mwanamke ambaye siku zilizopita walikuwa wakikesha usiku takriban kila siku kwa raha zao, atakuwa amemdhalilisha mwanamke huyo. Hivyo, usiku huu wa siku ya pili aliamua kumshinikiza Sarah, wakumbukie.
“Kwa nini umeamua kunitenga, Sarah?” hatimaye Kasha alimuuliza.
“Kukutenga?” Sarah hakumwelewa. “Una maana gani kuniuliza hivyo?”
“Hujui kuwa kunilaza usiku kucha peke yangu ni kunitenga?”
Tabasamu la mbali likamtoka Sarah. “Kwa hiyo unatakaje?” hatimaye alihoji.
“Huu uwe usiku wetu. Tuwe mwili mmoja, tuziridhishe nafsi zetu kwa raha zetu.”
Sarah hakuwa na kipingamizi. Kati yao hakuna aliyekuwa mgeni kwa mwenzake. Walifahamiana, walijuana. Mara kadhaa, kabla Kasha hajakamatwa na Polisi, walishaangukia kitanda na kufanya yale waliyodhamiria kuyafanya, nafsi zao zikiburudika kwa kila kitendo walichokitenda.
Hivyo, muda mfupi baadaye walikuwa chumbani, ndani ya kile chumba mahsusi kwa wageni, chumba ambacho Kasha alikitumia kwa malazi tangu alipofika hapo. Humo walifanya mengi na kuzungumza mara chache, pumzi, ubunifu, juhudi, maarifa na utundu maradufu vikiwa vigezo vilivyowafanya waendelee na kuendelea. Hawakuwa na nafasi ya kujadili lolote, walikuwa na nafasi ya kufanya lolote!
Hudaiwa kuwa mapenzi ni uchafu lakini siyo uchafu wa mwili na mavazi. Sarah na Kasha walidhihirisha hilo wakiwa kitandani, mavazi yao yote yakiwa yamejitenga na miili yao. Kuna wakati Kasha aliutumia ulimi wake kubusu, kuramba na kunyonya kwa ari kubwa kila alipohitaji na alipoamini kuwa palipaswa kufanyiwa ziara hiyo.
Sarah naye hakuwa nyuma. Alijua kuitumia mikono yake kupapasa na kutomasa kitaalamu ilhali ulimi wake wa moto ukinyonya kwa utaratibu unaosisimua na kufyonza kwa namna iwezayo kumtia mtu uchizi kwa burudiko la kipekee. Hatima ya yote ilikuwa ni kuisulubisha miili hiyo katika namna iliyoonyesha kuwa kila mmoja alitaka kumdhihirishia mwenzie kuwa yuko juu zaidi.
Kuna wakati yowe dogo jembamba lilisikika, likiambatana na sauti ya kike ikimwaga sifa kwa kukitaja mfululizo kiungo fulani huku miguno mizito na uropokaji wa kimahaba uliotoka kwa sauti ya kiume nao ukipokea mara chache.
Hata hivyo, pamoja na kufanyiana hayo yote, bado kichwani mwa Kasha kulikuwa na jambo lililomsumbua, jambo ambalo hakutaka ifike asubuhi nyingine bila ya kuliweka bayana kwa Sarah. Alitaka autumie usiku huohuo kumdokeza Sarah kisha kumshawishi akubaliane nalo.
Taa ya rangi ya bluu ikiwaangazia nuru hafifu, nuru waliyoipenda, Kasha na Sarah waliendelea kulala kitandani hapo huku wakitazamana kwa macho yaliyoridhika kwa kile walichokifanya muda mfupi uliopita. Wakati huo pia mikono yao haikutulia, Sarah alikuwa akimpapasa Kasha katika paji la uso huku Kasha akiutelezesha mkono wake katika milima na mabonde ya mwili ule mwororo wa Sarah.
Hatimaye: “Sarah,” Kasha aliita kwa upole, macho yake yakimtazama Sarah, sawia. Tazama yake ilionyesha kulikuwa na jambo zito alilotarajia kumweleza Sarah.
*****HAYA WAPENZI HAO WAMEKULA RAHA TANI YAO. SASA KASHA ANA DUKUDUKU. ANATAKA KUMWAMBIA KITU SARAH. JE, ATAMWAMBIA? NA KAMA ATAMWAMBIA, WATAELEWANA? KAZI IPO. TUONANE
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment