Simulizi : Chaguo Langu Ni Wewe
Sehemu Ya Pili (2)
Siku hiyo alifika mapema tofauti na waatoto wengine,kwa vile kulikuwa na watoto wachache waliokuwa wakianza kucheza michezo yao uwanjani hapo Jongo aliona heri ajitafutie sehemu aketi na kumsubili rafiki yake Shamsa.Muda wote Jongo alipokuwa amefika hapo akiwa amekaa pale chini ya mwembe yake yakivuta hisia huku na huko labda atamuona rafikiye lakini haikuwa hivyo Shamsa hakuonekana. Licha ya watoto wengi kuanza kujazana katikati ya uwanja huo mkubwa lakini hakuonekana mpaka baadae Jongo akiwa amejiinamia huku akiwa mwenye masikitiko kutokumuona yule rafiki aliyemchangamsha siku iliyopita. Jongo akiwa amejawa na udhuni juu ya kutokumuona rafikiye aliyemtegemea kukutana nae tena siku hiyo.Ghafla alistuka aliposikia kitu kikimtambaa shingoni mwake haraka alijipangusa kwa kutumia mkono wake,wakati akijiweka sawa alihisi tena kama kuna mtu nyuma yake,haraka Jongo alizungusha fimbo yake na kuelekeza kule alipohisi kitu kikimfuata.Alirejesha tena fimbo yake,zikapita kama dakika moja alisikia tena kitu kikimtambaa shingoni mwake haraka Jongo aliruka huku akigeukia kwa nyuma na kuipeleka fimbo yake safari hii akiwa wima amesimama.
“Aisee! muoga sana wewe?”
“Alla! Kumbe ni wewe shamsa?”Jongo alihamaki baada ya kusikia sauti ya shamsa
“Yes, ni mimi Shamsa Samir “Shamsa alimjibu huku akiangua kicheko kilichomuacha hio Jongo
“Kwanini unanitisha sasa?”Jongo aliuliza kwa hamaki
“Nilitaka nijue kitu kutoka kwako” Shamsa alijibu huku akicheka
“Kitu gani Shamsa”Jongo alimmtupia swali linguine
“Kama una hisia….na sasa nimefahamu hilo”
“Na sasa umefahamu lipi kwa utafiti wako?”
“Kweli unazo hisia tena nzito sana yaani kabla sijakugusa umeshajua kama kuna mtu aliyekuwa akikufuata?”
”Ndio hivyo lazima nifahamu ilo kama wewe unavyomuona mtu wa karibu yako aliyekuwa mwema na mmbaya nami nAweza kulifahamu hilo”Jongo alimjibu
“Aisee! upo vema sana “
“Yaani hata wewe ukae mbali yangu lakini nikisikia sauti yako tu nishakufahamu kama ni wewe”Jongo alimwambia
“Ni vema ukiwa hivyo ili kupambana na maadui pindi wanapotaka kukudhuru”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku hiyo Shamsa alipokuwa akija uwanjani hapo aliwakuta mwenzake wameshafika na kuendelea kucheza michezo yao wale wenye kamba waliruka, wenye mpira walicheza ili mladi kujiridhisha roho zao kama tabia za watoto zilivyo. Kwamba mbali alimuona Jongo ameshafika na kuketi pale chini ya mwembe,kama kawaida aliwapa mpira watoto wengine naye alikwenda kule alipokuwa amekaa Jongo.Alipofika hapo hakutaka kuwa na haraka,alijifikilia na kuamua kumtega Jongo,Hakutaka kukaa karibu na Jongo ila alitaka kumstua.Shamsa alipofika hapo alizunguka huku akinyata mpaka nyuma ya mwembe huo ambapo Jongo alikuwa ameegemea,haraka Shamsa akaokota jani la mwembe huo lililokuwa limedondoka jirani yake na kulishika mwanzo wa jani hilo na kulipeleka nyuma ya shingo ya Jongo.Kwa vile Shamsa alitumia ncha ya jani hilo kulipitisha shingoni mwake, Jongo alistuka ghafla na kujipangusa kisha akatulia.Shamsa alipoona Jongo akiendelea na mambo mengine alimlipitisha tena jani hilo safari hii kwa nguvu kidogo kisha alikimbia haraka mpande wa pili ndio Jongo alipoona kitu kisicho cha kawaida hakanyanyuka na kugeuka nyuma haraka huku fimbo yake mkononi ikipapasa huku na huko.Haraka Shamsa alianza kucheka na kujitokeza mbele yake,Jongo alinywea baada ya kusikia sauti ya Shamsa,hakuwa na budi akaamua kuketi tena chini ya mwembe huo huku akiwa amefedheheka kinamna.Siku hiyo waliongea mambo mengi wakafahamiana na kutambua kuwa ni wenyeji wa mikoa tofauti huku Shamsa akiwa ni mzigua kutoka Tanga huku Jongo akijitambulisha kuwa ni mzaliwa Morogoro kabila lake likiwa mluguru.Shamsa alimwambia Jongo siku hiyo alionekana kufika mapema tofauti na siku zote alizokuwa akiwai kufika.Jongo hakumjibu upesi kutokana na kujisia aibu Fulani hivi,ila Shamsa alijua yote hayo kwa sababu yake yeye ndio maana alionekana Jongo kuchangamka tofauti na siku zote.
“Unaoneka siku hizi mwenye furaha ya wazi sijui kwanini”Shamsa alimuuliza baada ya kumuona Jongo akiwa kimya akitabasamu
“Kwa sababu yako, Shamsa wewe ni rafiki mwema kwangu”Jongo alimwambia
“Nashukuru kama kwa ajiri yangu kukufurahisha”
“Shukurani zije kwako rafiki mwema”Jongo alimwambia
“Nami nazipeleka kwa mungu muumba ashukuliwe”
“Aminii”
“Hivi uliniambia unasoma shule gani vile?”Shamsa alimuuliza
“Majengo….ni hapo tu jilani na mnala wa voda
“Hivi unasomaje hapo nawe uoni kwani kuna walemavu?”Shamsa aliuliza maana hakuwa akijua kama shule hiyo walemavu wapo pia
“Kuna mwalimu wetu anaitwa Uweso yeye uja kila siku kutufundisha sisi walemavu wa uwoni”
“Aisee! Kumbe shule hiyo ina walemavu?
“Ndio Shamsa ila tupo wawili tu mimi na mwenzangu, tunatumia mashine za brela kusomea”Jongo alimfafanulia
“Hongera sana, unasoma darasa la ngapi”
“Darasa la tano sasa sijui wewe unasoma darasa la ngapi?
“Mwaka huu naingi darasa la nne katika shule hiyo hiyo ya majengo”
“Karibu sana rafiki mwema Shamsa”Jongo alimkaribisha
“Nashukuru sana rafiki yangu….tupo pamoja”
Shamsa na Jongo waliongea mambo mengi wakiwa wamekaa peke yao mwembeni hapo, wakasahau michezo iliyowaleta pale ,siku hiyo ilikuwa kwa mazungumzo tu sijui walipanga hama hawakutarajia.Shamsa alisahau kabisa kucheza na wenzake hata hivyo hawakuwa na mda nae wao waliendelea kucheza na kuruka ruka kama kawaida yao hawakumjali Shamsa wala Jongo.Muda uliwadia saa kumi na mbili iligonga kwa adhana kusikika msikiti wa jilani na uwanja huo kuwa taarifu wakazi wa maeneo hayo wajongee masjid kumsujudia mtume.Watoto waliopo pale uwanjani wana kawaida yao,adhana ikisikika wanajua moja kwa moja muda umefika kurejea majumbani mwao na ndivyo ilivyotokea watoto walianza kutawanyika na kurejea majumbani mwao.Shamsa na Jongo nao waliagana huku Shamsa akimshika mkono Jongo na kumuongoza njia kisha walipofika mbele kutokea njia nyingine iliyompeleka Shamsa nyumbani kwao waliagana hapo na Jongo aliongoza njia inayoelekea nyumbani kwao huku akiwa mtu mwenye furaha isiyoelezeka.
**********
“Shkamoo baba”Shamsa alimsabahi baba yake baada ya kufika nyumbani
“Marhabaha...ujambo binti yangu?”
“Sijambo baba”Shamsa alijibu huku akikaa kwenye sofa karibu na baba yake
“Wewee….ala! Nenda kakoge kwanza, angalia miguu yako ilivyokuchafuka”Mama yake alimsema
“Jamani mama naenda, ila nilikuwa namsalimia baba kwanza”Shamsa alisema huku akinyanyuka
“Jamani nini kwani mwenyewe ujioni miguu ilivyo umechafuka vilivyo”
“Sawa…..mama lakini hata sio michafu”Shamsa aliongea wakati akielekea mlango wa kutokea uwani mwa nyumba hiyo.
“Na ujisugue vizuri maana wewe”Mama yake alimwambia huku akimsindikiza na macho yake.
Shamsa alioga na kujisafisha vizuri bafuni mle kisha alitoka na kuingia ndani ya chumba chake.Baada ya dakika tano Shamsa alitoka akiwa amevalia upande wa kanga na blauzi ya mikono mirefu. Akiwa ameketi sofani pale alipokuwa amekaa kwa mara ya kwanza alimsogelea baba yake na kuanza kuzungumza nae kile kilichokuwa moyoni mwake.Maana baba kwa mtoto ni tablet iliyoshindiliwa na msumali mirefu yenye king’ang’anizi.Wakati Shamsa akitaka kuzungumza na baba yake,mama yake alikuwa makini akimsikiliza na kumshangaa kitu gani alichokuwa akitaka kumwambia na kumzonga baba yake usiku huo.Wakati Shamsa akianza kuongea kwa mkato mkato lakini mama yake alielewa kitu ambacho mtoto wake alitaka kuzungumza.Bi.Ramla alimtupia jicho kali sana mtoto wake alihisi utoto ndio uliokuwa ukimsumbua mpaka kufikia kumwambia baba yake juu ya huko anapokwenda kucheza.Kwanza mama yake alijua maongezi ya mtoto wake yatahusu juu ya masomo na shule aendayo,lakini haikuwa hivyo yeye alithamini sana mchezo kuliko masomo.Licha ya uzembe wake juu ya masomo lakini alikuwa na uelewa mkubwa sana kwenye masomo yake,alikuwa akishika nafasi ya pili darasani.Ndio maana wazazi wake walikuwa wakimuacha acheze anavyotaka lakini darasani hawakutaka ashuke kimasomo zaidi ya kupanda mpaka siku nyingine alifikia nafasi ya kwanza darasani......CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kipindi hicho Shamsa alizungumza na Baba yake alimuuitikia tu huku akizungusha kichwa lakini hakuwa na uelewa anachozungumza mtoto wake, aliona alichokuwa akizungumza kilikuwa hakina maana yoyote kwake.Shamsa alimwambia ya kwamba “Baba nimeenda kucheza na kupata mchumba, anampenda hadi mama” mwanamke au mwanaume huyo rafiki yako?” Bwana Samir alimuuliza mtoto wake, Mwanaume baba tena anatembelea fimbo” Shamsa alisema. “ Bwana Samir akapiga moyo konde na kupotezea kwa kauli ya mtoto wake,hakutaka kumuuliza chochote mkewe akaona Shamsa alikuwa bado mtoto sana mwenye umri wa miaka kumi alafu leo apate mchumba huko wanapocheza ni maajabu haya.Aliendelea na kazi zake huku akiendelea kumuitikia mtoto wake kwa kuzungusha kichwa.Alipoona Shamsa amemzunguka sana huku akiwa afanyi kazi zake kwa amani akaamua kunyanyuka na kuingia zake ndani huku akimuacha mke na mtoto wake wakimshangaa.Bi.Ramla alimwangalia mtoto wake kwa jicho la unaona sasa, Shamsa alishangaa sana pale alipomuona mama yake akimwangalia,bila kupepesa mara moja akajua kauli aliyoitoa itakuwa imemtatiza sana baba yake na alimwangalia mama yake na kumsogelea karibu kisha akamwambia.
“Mama Rafiki mwenyewe wa kiume ambaye ni mlemavu wa uoni anayeitwa Jongo, pia naye ni mwenyeji wa mkoa huu sasa anasoma katika shule ambayo kesho mimi nakwenda kuanza”Shamsa alimwambia mama yake baada ya kumuona akiwa amefura
“Lakini mwanangu kwanini ukuniambia tangu mwanzo mpaka uje kusema mbele ya baba yako?
“Hapana mama naona yote ni kheri juzi tu ndio nimejuana nae ni rafiki tu wakawaida”
“Sawa sasa ni rafiki ulivyosema ni mchumba,ujui kama umemuuzi baba yako?”
“Hapana mama nimetania tu niwasikie wazazi wangu mtasema nini”’
“Umefanya makosa sasa unaona mpaka baba yako amekasilika”
“Sio mchumba wangu kweli mama natania”Shamsa alijitetea
“Sasa tutafanya nini ili baba yako harudi kwenye hari ya kawaida”
“Mwambie anisamehe mama sina mchumba mie”Shamsa alimwambia mama yake
“Usirudie tena kulopoka lopoka tu”mama yake alimkanya
“Sawa mama nimekuelewa”Shamsa alishukuru na kuelekea chumbani mwake huku mama yake akinyanyuka na kuingia chumbani.
************
Angali Shamsa akiendelea kuwaza,usiku ulizidi kukoma mbu nao waliendelea kumtafuna kwa furaha.Angani kulikuwa baridi na upepo uliojaa ulikuwa ukivuma.Alizidi kujikunyata kwenye kitanda maridhawa akijikinga dhidi ya upepo wa baridi uliokuwa ukimiminika kimyakimya.Macho yake hayakuweza kuona mbali na pale alipokuwa amejistiri kutokana na kiza kushida uoni wa mboni zake.Hakujua siku iliyofuata atakwenda na nani shuleni hapo,alitamani usiku ukuche kuwai kuamka na kwenda shuleni ili kukutana na rafiki yake Jongo.Shamsa aliwaza mambo mengi kutokana na kuelewa jinsi ya kufika shuleni hapo alijua moja kwa maoja shule atakayokwenda kusoma ndiyo atakayokuwa anafundisha mama yake.Usiku ulikuwa umekwenda Shamsa akiwa bado kitandani mawazo mengi kichwa na usingizi ukamchukua akalala fofofo mpaka asubuhi.Shamsa aliamshwa na mama yake akaamka na kujiandaa kwa ajili ya kuwai shuleni.Ilipofikia saa mbili asubuhi yeye na mama yake wakatoka nyumbani na kulekea shuleni,muda wote Shamsa alikuwa mtu mwenye furaha moja kwa moja mawazo yake yalienda na kuzama juu ya kijana Jongo alimfikiria sana Jongo na sasa akajua lazima anakwenda kuonana na Jongo shuleni hapo.
Baada ya mwendo wa nusu saa walifika waliona mbele yao kukiwa na kibao cha msingi kilichoandikwa Manispaa ya Nyegenzi Shule ya msingi Nyakabungo mkoani mwanza.Shamsa alijua sasa shule anayotakiwa kusoma ndio hiyo na sasa anakwenda kuanza.Bi.Ramla alikwenda moja kwa moja mpaka ofisi ya mwalimu mkuu akiwa na Shamsa pembeni yake,alipoingia tu mle ndani Bi.Ramla alianza kumsalimia mwalimu mkuu ambaye ni mwanamama wa makamo na kisha kumpatia kitambulisho pamoja na makalatasi ambacho yanadhibitisha anatakiwa kufundisha katika shule hiyo.Pia Ramla alitoa kalatasi kadhaa toka ndani ya mkoba wake na kumkabidhi Mkuu huyo,akazipitia kisha akainuka na kumtaka Bi.Ramla amfuate.Waliongozana mpaka sehemu ya chumba kimoja kilicho kati ya jengo hilo mwanamke huyo alifungua mlango kwa funguo aliyokuja nayo tokea kule ofisini.Mlango ukafunguka nao wakazama ndani,muda wote Bi.Ramla alikuwa amemshikilia mwanae aliyeonekana kuwa na shauku kubwa ya kutaka kuingia darasani.
“Mama Ramla…mtoto jina lake nani?”Mama huyo alimgutusha Ramla macho yake yakiwa juu ya meza kubwa uliyokuwepo ofisini humo.
“Anaitwa Shamsa Samir Nassoro”Bi.Ramla alijibu
“Anasoma darasa la ngapi”Aliendelea kumuuliza mwanamke huyo huku akiangalia kalatasi yenye maelezo kwa hiyo
“Darasa la nne” Bi.Ramla alijibu
“Fomu pamoja na maelezo yake nimeyaona na kuyapitia sasa mimi na wewe tunaelekea ofisi ya waalimu kisha nitampeleka Shamsa darasani”
“Haina tatizo nashukuru sana”Bi.Ramla alimwambia
“Usijali tupo pamoja na karibu sana”
Bi.Ramla aliongea na mwalimu huyo kisha akampeleka upande wa pili wa jingo hilo ambapo ndipo ilipokuwa ofisi ya waalimu wote, Bi.Ramla akatambulishwa na mwanae akapelekwa darasani ambapo alishangaa pale alipowakuta watoto wengi ndio wale aliokuwa akicheza nao pamoja kule uwanjani Laah! Alishangaa na furaha angali mdomoni,ila hakumuona rafiki yake wa ubani Jongo.Shamsa aliudhunika sana moyoni mwake ila alijiapiza na kujipa moyo na kusubili mpaka muda wa kurejea nyumbani utakapowadia aende kumuuliza hapo ndipo atakapolipata jibu kama anasomea shuleni hapo au nyingine.
*******CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Shamsa na Jongo waliwahi kufika sana kuliko watoto wenzao waliokuwa wanacheza katika uwanja huo.Wao walikua wanacheza kwa furaha na kuongea huku wakigongana mikono ikawa ni desturi ya wawili hao kupenda kuongea peke yao uwanjani hapo.Siku zilikatika kwa mazoea yao kushamili,furaha na buraha ilitawala na kuchanua kwenye nyuso zao,walishikana na kuzunguka pamoja kama makinda wawili. Siku moja Shamsa alifika lakini Jongo hakufika alijipa subira na kusubili kwa muda lakini Jongo hakutokea siku hiyo Shamsa alikuwa mpole kila wakati wenzake walimwambia wacheze pamoja lakini yeye akujali nafuu yake ilikuwa Jongo.Hakuweza kula wala kulala sababu ya Jongo, hakusoma wala kuandika kisa hakumtia machoni Jongo looh! Shamsa siku mbili tu alikuwa amepungua mwili wake sababu ya Jongo.Wenzake walijitahidi kumchangamsha ili kuondokana na mawazo ya Jongo lakini ilishindikana Shamsa akaona maneno mengi kwa wenzake akaamua kuondoka uwanjani hapo na kurejea nyumbani.
Siku iliyofuata Shamsa alikwenda shuleni kama kawaidi aliingia kila darasa kumtafuta Jongo lakini hakumuona aliambulia patupu ata alipojaribu kuwauliza wanafunzi wa darasa hilo aliambiwa kuwa Jongo anasoma katika shule hiyo ila yafikia siku mbili Jongo hakuonekana shuleni na wengine hawakupajua nyumbani kwao.Muda wa kurejea nyumbani uliwadia,wanafunzi wote walirejea majumbani mwao,Shamsa aliangaza huku na uko labda atamuona lakini wapi mawazo yalimdanganya.Muda wa kucheza ulipowadia Shamsa alifika mategemeo yake yakiwa kuonana na Jongo sasa yaliyeyuka pia siku hiyo Jongo hakutokea tena upweke ulimtawala alikaa peke yake chini ya mwembe huo akimfikiria Jongo.Shamsa hakutumia muda mwingi kukaa maeneo hayo aliondoka na kurudi nyumbani kwao,Bwana Samir na mkewe walimuona mtoto wao akiwa kwenye hali hiyo waliamua kumuuliza kulikoni mtoto kuwa katika hali hiyo, Shamsa hakusema kitu chochote wala akujibu alipitiliza mpaka chumbani kwake na kujitupa kitandani.Bi. Ramla hakujua kitu gani kimempata mtoto wake,alimfuata mpaka ndani na alipomuuliza kama anaumwa,alijibu hakuwa mgonjwa na mama yake alizidi kumdadisi ili kujua kitu gani kimempata mwishowe Shamsa akamdanganya mama yake kuwa amepigana na rafiki yake aliyekuwa wakigombea mpira.Bi.Ramla alicheka kisha akamtaka mwanae kuwa na amani,Shamsa hakumwambia ukweli juu ya hali aliyokuwa nayo kumkosa kijana Jongo.
Siku nyingine tena Shamsa alikwenda kucheza ila hakumwona Jongo akamua kuwauliza wenzake kama kuna anayepajua nyumbani anapokaa Jongo.Watoto wengi waliokuwepo uwanjani hapo walimshangaa baada ya kumsikia msichana kama Shamsa akimuulizia kijana Kipofu.Yalikuwa ni maajabu kwao kwani kutokuwepo Jongo kwa siku tatu uwanjani hapo watoto wale waliona nafuu kwao,hawakupenda kabisa uwepo wa Jongo uwanjani hapo walimuona binadamu aliye na kasoro.Kijana mmoja aliyekuwa akikaa karibu na nyumbani kwa kina Jongo akamuelekeza ilipo nyumba ya mama Jongo,kwa uwelewa wake haraka alitambua njia ya kumfikisha katika nyumba aliyoelekezwa ndipo nyumbani kwa kina Jongo.Shamsa hakutaka kuchelewa aliongoza njia na kuifuata barabara na kisha kukata kulia,kama alivyokuwa ameelezwa.Njia nzima Shamsa alimuwaza Jongo,hakujua huko anapokwenda kama atafanikiwa kumuona au atakuwa amedanganywa nyumba na vijana wale wasiompenda Jongo,aliwaza yote hayo kichwani mwake. Kwavile hapakuwa mbali na pale uwanjani, dakika sita tu alifika mbele ya nyumba aliyokuwa imepakwa rangi ya kahawia, Moja kwa moja Shamsa alitambua nyumba hiyo ndio alipoelezwa ndipo anaipokaa Jongo.Alisogea mpaka karibu na mlango wa kuingilia ndani ya nyumba hiyo, yenye baraza ndogo, akiwa pale kibarazani ili kubisha hodi, kabla mkono wake uliokuwa amekunja vidole vyake ili kutaka kugonga. Ghafla mlango huo ukafunguliwa na kukutana uso kwa uso na Mama wa makamo akiwa anatoka ndani, Shamsa hakumjua ni nani aliyekuwa mlangoni, akiwa akitetemeka moyo wake ukienda kasi akamsalimia.
“Shkamoo…..mama”Shamsa alisalimia
“Marhabaha ujambo mtoto mzuri”Mama Jongo alimjibu
“Jongo yupo?”Shamsa aliuliza
“Mmmh! Hee yupo, vipi kwani?”
Shamsa hakumjibu alichofanya yeye ni kumhulizia Jongo kama amemkuta au kama anakaa nyumbani hapo, Mama yule alishangaa kwani ahikuwai kutokea hata siku moja awe mtoto au mkubwa kuja kumulizia mwanae. Mama Jongo akamjibu “Ndio yupo ila anaumwa” Shamsa alifurahi kusikia majibu hayo kutoka kinywa mwa mama huyo,aliongea tena haraka “Samahani mama naweza kumuona” Mama Jongo akamkaribisha ndani na macho yake yakimwangalia mtoto huyo’’Shamsa alipita ukumbini moja kwa moja mpaka sebuleni alimuona Jongo amelala kwenye kochi moja la watu wawili lililokuwepo pale sebuleni.Alienda moja kwa moja huku macho yake makali yakitua pale alipolala Jongo,Shamsa kwa huruma alijua Jongo anaumwa sana alimkalibia na kisha akamuhita “Jongo…!” japo alikuwa anaumwa lakini Jongo hakuweza kuisahau sauti ya Shamsa haraka aliitika kwa kumwita jina “Shamsa…!”Shamsa aliitika “Yes Jongo” Jongo alihoji “Umewezaje kufika nyumbani?”Shamsa alimjibu nimeona kimya nikaamua kukuulizia kwenu ndio maana nipo hapa’’Shamsa alifurahi sana muda wote ule mama Jongo alikuwa pembeni anawaangalia wawilia hao wakiongea kwa furaha.....
Muda wote Shamsa na Jongo walikuwa sebuleni wakiongea hili na lile,baadae mama Jongo alimtaka anyanyuke ili anywe uji.Jongo aliposikia sauti ya mama yake alimuitikia na kumtaka mama yake amtambulishe kwa rafiki yake.Kweli muda si muda Jongo akaanza kumtambulisha Mama yake kwa Shamsa wote walifurahi kwa pamoja wakapeana mikono kwa bashasha na Shamsa alimsaidia Jongo kunyanyuka na kukaa vizuri kwenye kochi ili anywe uji.Mama Jongo alikuja na kikombe cha uji alipotaka kumnywesha Jongo ,Shamsa aliomba apewe yeye kikombe cha uji na kumnywesha Jongo,Mama Jongo alimwangalia na kisha akamuuliza kama ataweza kumnywesha mtoto mwenzake.Shamsa alimuhakikishia ataweza ndio Shamsa alichukua kikombe kutoka mikononi mwa Mama Jongo na kumnywesha Jongo.Jongo alikunywa uji kwa amani akijua aliyekuwa akinywesha alikuwa Shamsa mpaka alipomaliza alirudisha Kikombe kwa Mama Jongo na kuendelea kucheza nae kuongea nae mpaka muda wa yeye kurudi nyumbani aliaga na kumuahidi Jongo atakuja tena kesho yake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kesho yake alifika alikwenda shuleni kama kawaida walikutana huko huko, kila wakati na muda wa mapumziko Shamsa ahisikiapo kengere ukimbilia darasa anaposoma Jongo na Mariamu ambao wote ni walemavu. Shamsa akiingiapo darasani humo umkuta Mariamu na Jongo wakiwa wamesogeleana wakisoma pamoja anakeleka sana,ikafikia kipindi akawa anamchukia Miriamu,Jongo alielewa kutokea kwa hali hiyo lakini hakuwa na jinsi.Kila siku Shamsa hakuchoka kuwa karibu na Jongo wakawa wanaongea na kucheza mpaka Siku alipopata nafuu Jongo walifika uwanjani kwa watoto wenzao wanapokuwa wakicheza kila siku.Walikuwa pamoja mpaka walipomaliza shule, Jongo alichaguliwa kusoma Shule ya watoto walemavu sababu ya ulemavu wake wa huoni na Shamsa alisoma kwingine tofauti na Jongo.Waliendelea na masomo huku wakiwasiliana na kukutana kwa ajiri ya masomo yao kila siku mpaka wakafikia kidato cha pili na kuufanya mtihani wao kwa mafanikio makubwa na kufanikiwa kuingia kidato cha tatu.Shamsa alikuwa msichana aliyepevuka kiakili na kimwili hata Jongo nae alikuwa mvulana sharobalo mwenye umbo matata linaloweza kumchanganya mwanamke yoyote atakaye bahatika kumtiha machoni mwake.Kutokana na ukaribu uliozoeleka kutoka kwa wawili hao hali ilikuwa tete kwa Shamsa juu ya Jongo,alikuwa amezimika kimahaba,alimpenda sana Jongo toka ndani ya moyo wake,kila siku zilinavyozidi kwenda ndivyo Shamsa alivyozidi kumpenda Jongo ila hakudhubutu kuufungua mdomo wake na kumwambia kwani hisia zake alizionesha wazi juu ya kijana Jongo mwenye ulemavu wa macho.
“Hee! Jamani hee msibomoe nyumba zetu bora mtulipe kwanza”ilikuwa sauti ya mama Jongo
“Kulipwa mtalipwa ila mnapewa utaratibu jinsi ya kukabiliana na bomoa bomoa itakayoanza hivi karibuni”Mwenye kitu aliwaambia wananchi hao waliokuwa ofisini hapo
“Siliza mwenye kiti…sisi wengine hatuna nyumba za kukaa zaidi ya hapo unapopaona sasa unafikiri mkitoa hapo mtatupeleka wapi na kutulipa hamtaki”
“Kweli kabisa wananchi tunaonewa sana ardhi ni zetu wenyewe alafu serikali inaingilia kati na kututaka tuondoke sasa tutakwenda wapi? Mwengine alidakia
“Mie siondoki mpaka niwaone waje kubomoa”
“Kweli kabisa jirani heti tupo barabarani…watu wenyewe hawaitengenezi hiyo barabara yenyewe miaka yote ipo vile vile wanatuonea tu hawa”
Wananchi walilalamika serikali kuwataka wazibomoe nyumba zao zilizokuwa kandokando ya barabara kwani barabara hiyo ilitakiwa kupanuliwa na kuongezwa ukubwa.Mama yake Jongo naye alikuwepo, akililia haki yake ya kulipwa ndipo aondoke ndani ya nyumba hiyo.Hakuwa peke yake walikuwa watu wengi sana nyumba zao zilikuwa zimepigwa herufi ya X kwa sababu ya kuwa zimejengwa barabarani. Aiku hiyo waliambiwa kitakapokuja kijiko cha kubomoa wasilalamike kwa ajiri ya kazi hiyo.Siku zilizidi kwenda Mama Jongo aliendelea kufuatilia pesa yake na akafikia muda maalumu wakalipwa pesa zao ili waondoke ndani ya nyumba hiyo.Mama Jongo alikuwa na wakati mgumu sana hakujua ataenda wapi kwa wakati huo alikaa na kufikiria aliamua kutafuta kiwanja au kununua kabisa nyumba maeneo ya nyumbani kwao alipotokea Morogoro.Baada ya siku mbili tatu aliwaulizia ndugu zake wanaoka Morogoro kufanikiwa kupata nyumba kubwa kwa kiasi cha milioni kumi na mbili.
Hakutaka kupoteza muda alipopata taarifa ya kwamba amefanikiwa kupata nyumba hivyo alihama kimakazi na kuamia mkoani morogoro akiwa na mtoto wake Jongo.Huo ndio ulikuwa Mwisho wa kuonana kwa wawili hao, Shamsa na Jongo wenyewe walikutana kabla ya kuagana na kuhaidiana kukutana tena kama mungu akijaalia.Shamsa alilia sana kila wakati alimfikilia sana Jongo alijilaumu kwa nini hakumwambia dhamira yake kwani alimpenda sana Jongo na sasa ameondoka huku atakuwa na kwa wasichana wengine.
********
Siku ya siku iliwadia ya Mama Jongo kuondoka, ndugu na majirani walisaidiana kupakia vyombo kwenye gari.Ilikuwa siku ya majonzi makubwa kwa Shamsa na Jongo, hakuna aliyejua ukweli kilichowaliza watoto wao.Shamsa alimlilia Jongo alijua huo ndio ulikuwa mwisho wao kuonana, watu wengi waliwabembeleza na kuwatuliza lakini Shamsa wala hakuwasikiliza alimsihi Jongo hasiondoke.Wakati yote hayo yakiendelea Mama yake Shamsa alizipata taarifa kutoka kwa majira zake wakimtaka aende kumwangalia mtoto wake jinsi anavyo mlilia Jongo.Mama yake alishangaa haraka alitoka na kuelekea huko alipoelekezwa ndipo mwanae alipokuwa.Bi.Ramla alienda huku kichwani mwake akiwa na mawazo kibao kuhusu yale aliyoambiwa na majirani kuhusu mtoto wake Shamsa,alipofika hapo alishangaa akiwa mbele ya nyumba moja kati ya nyumba zilizopo katikati ya mtaa wao.
“Shamsa ….mwanangu vipi tena?” Bi.Ramla alibwabwaja huku akimfuata mwanae kule aliko
“Mama Jongo…mama anaondoka”Shamsa alianza kulia upya
“Hee! Mwanangu nyamaza basi nasi tutaondoka mbona unalia kama mtoto”
“Jongo mama ananiacha”Shamsa alilia kama mtoto
“Sasa Binti yangu unacholilia ni kitu cha ajabu sana…embu nyamaza jamani”
“Namtaka Jongo Mama ni rafiki yangu wa muda mrefu sana”Shamsa alibwabwaja huku akiendelea kulia
“Basi nyamaza twende nyumbani sasa”Mama Shamsa alimshika mkono mwanae na kuanza kumvuta kuelekea nyumbani.
***********
Baada ya Jongo Mama yake kuondoka Shamsa aliendelea kuishi nyumbani kwao na wazazi wake huku akiwa hana raha kama zamani, mama yake alijua hali hiyo kutokana na kuondoka kwa kijana Jongo hila hakuwa na la kufanya juu ya uwamuzi wa mzazi wa Jongo kuondika.Kila siku alilia na kuomboleza juu ya kijana Jongo, hakujua atampata wapi tena kijana anayempanda kana huyo.Arusha ni kubwa hakujua ataanza vipi kusafiri mpaka mkoa huo kumtafuta Jongo ila alijiapia lazima siku moja waonane tena na Jongo.Siku zilizidi kwenda Shamsa alizidi kupungua kimwili huku kiakili akiwa hajakaa sawa.Kila wakati aliweuka na kumkumbuka Jongo kwani alimpenda sana kuliko kitu chochote.....
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku zinavyozidi kwenda ndivyo hali ya Shamsa alivyozidi kuwa mbaya,Bi.Ramla alishangaa sana ila zaidi baba yake Bwana Samir ndio kabisa maana hakujua kitu gani kilichokuwa kimemsibu mtoto wake mpaka kupatwa na hali ya kukonda na kudhoofika.Kila siku Bwana Samir alikuwa akiketi chini na kumuuliza mtoto wake kitu gani kilichokuwa kikimsababishia kuwa katika hali hiyo,Shamsa hakuweza kumjibu baba yake kwani kila wakati kilio tu, ndio ilikuwa kazi yake pekee.Siku moja Uzalendo ulimshinda Bi.Ramla alipoona hali ya mtoto wake inavyozidi kuwa mbaya alihamua kumueleza ukweli wa jambo mume wake kuhusu Binti yao Shamsa.Bwana Samir alimsikiliza mkewe kwa umakini kisha Samir hakutaka kumuona mtoto wake akipotea katika masomo yake kwani tayari ilifikia wiki nzima bila Shamsa kutokea shuleni kama ilivyo kawaida yake sababu ya uchovu aliokuwa nao juu ya mawazo.
Siku iliyoata Bwana Samir alirudi nyumbani akiwa ameongozana na Mama mmoja wa makamu, Mama huyo alikuwa mnene kidogo mwenye sura pana na macho yake yalikuwa makubwa kama goroli. Muda wote mama huyo alionekana akitabasamu, usoni wake uliwaka kutokana na tabasamu hilo meno yake meupe yote yalionekana.Siku hiyo Bwana Samir alimletea mtoto wake mwana saikolojia baada ya kuafikiana na mkewe nini cha kufanya juu ya hali hiyo.Ndipo walipoamua kumtafuta mwana Saikolojia kuzungumza na mtoto wao ili kumjenga na mtengeneza kiakili na kimwili.Siku hiyo walipofika Bwana Samir na mgeni huyo waliingia moja kwa moja mpaka chumbani kwa Shamsa na kumkuta akiwa amelala usingizi,bila kuchelewa Bwana Samir alimuhamsha na kutaka kuzungumza nae.Shamsa aliamka na kukaa kitandani huku macho yake yakiwa yamekodolea mama huyo aliyekuwa amevaa miwani usoni mwake huku lile tabasamu lake mwanana alilichanua sawia.
“Shamsa binti yangu…nimekuletea Anti hapa anataka kuzungumza nawe”
“Sawa baba sijui anataka nini? Shamsa alimtupia swali baba yake
“Anataka kukuweka vizuri kisaikolojia binti yangu”
“Yes! Shamsa ujambo mdogo wangu?”Dada huyo alimsalimu
“Sijambo shkamoo!”Alimsalimia
“Marahaba unaendeleaje?”Mama huyo aliuliza
“Mmmh….kwani uliambiwa naumwa?”
“Hapana sio kwamba unaumwa…”
“Kumbe kinachokusumbua nini? Baba yake aliwai kumuuliza
“Lakini baba mimi siumwi kitu”
“Sasa kwa nini unadhoofika namna hiyo wewe, kitu gani kinachokusumbua sema basi?”
“Bwana Samir nimeshakijua kinachomsumbua mtoto wako hivyo niachie mimi nifanye kazi yangu atakuwa anasumbuliwa na saikolojia huyu”
“Haa! Baba anataka kunifanya nini? Shamsa alihamaki baada ya kusikia maneno hayo
“Usijali binti hakuna kitu kibaya juu yako zaidi ya kuzungumza nawe tu ndio dawa yake”
Muda wote Shamsa akiongea na baba yake pamoja na yule mwanasaikolojia Bi.Ramla alikuwa akiwasikiliza kwa umakini huku akitikisa kichwa chake kwa masikitiko makubwa juu ya hali aliyokuwa nayo mtoto wake. Alimuona Bwana Samir akitoka ndani ya chumba hicho na kumuacha Shamsa akiwa na Mama huyo aliyejulikana kwa jina la Janeth.
Wakati Bi.Janeth akianza kuzungumza na Shamsa Bwana Samir na mkewe walikuwa chumbani kwao wakizungumza kuhusu hatima ya mtoto wao.Hawakutaka kukaa mahali hapo kutokana na kumchanganya mtoto wao juu ya yale anayoambiwa.Hivyo waliamua kumuacha ndani humo akiwa na mwanasaikolojia huyo.Wakiwa ndani ya chumba hicho wanawake wawili ambao ni Bi.Janeth na Shamsa wakizungumza juu ya hali aliyokuwa nayo na kwa vile Bwana Samir alikuwa amemueleza kila kitu mama huyo juu ya kile kinachomsibu mtoto wake.
Shamsa alikuwa kimya akimwangalia na kumsikiliza yale Bi Janeth aliyokuwa akimwambia kuhusiana na urafiki wake kwa Jongo.
Upendo ni neno la kiswahili linalojumlisha idadi kadhaa ya hisia, kuanzia mahaba, pendo hata upendo wa Kimungu.Ni kwamba kitenzi "kupenda" kinaweza kurejea aina za hisia, hali na mitazamo tofautitofauti, kuanzia ridhaa ya jumla ya kitu unachokipenda mfano utamwambia mama yako “napenda chakula hiki”, hapo utakuwa umeshapata hisia juu ya chakula hicho.Mvuto mkali kati ya binadamu ni mapenzi kwa mfano utamsikia mama yako akisema “Nampenda mume wangu”. Umuhimu wa matumizi na maana, pamoja na utata wa hisia zinazohusika, hufanya kuwe na ugumu katika ufafanuzi, hata kulingana na hali nyingine za kihisia uliyonayo juu ya kijana huyo.
Ukifikiria unaweza kugundua mapenzi kwa kawaida yanarejea hisia za ndani zisizoelezeka, tena za kudumu kwa mtu mwingine. Hata hivyo, maelezo haya pia yanashirikisha hisia tofauti, kutoka kuwa na urafiki wa kimahaba hadi ukaribu wa kihisia kwa mwanaume kupelekea kutokea kitendo cha mapenzi.Ndio maana wazazi wako wanapenda kuwa karibu nawe ili usiingie katika mkumbo huo, kwani kiingia huko utaaribikiwa zaidi ya hapo ulipofikia.Kuna mapenzi ya aina mbalimbali husimamia mafungamano kati ya akili zako na moyo, kutokana na umuhimu wake mkuu katika saikolojia, ni mojawapo ya maudhui yanayopatikana sana katika kupenda.
Ingawa desturi au chanzo cha mapenzi ni suala ambalo hujadiliwa mara kwa mara, sura tofauti ya neno hili zinaweza kuwekwa wazi kwa kuamua nini si mapenzi.Kama njia ya kawaida ya kuonyesha hisia chanya ni aina kubwa ya kupenda kupitiliza, mapenzi kwa kawaida hugonganishwa na mazoea kupita kiasi.Kama pendo ambalo linaegemea zaidi kwenye uhusiano wa kirafiki kuliko wa kingono, mapenzi kwa kawaida hugonganishwa na tamaa na kama uhusiano kati ya watu, unaohusisha mahaba, pia urafiki wa ukaribu zaidi, ingawa neno mapenzi linaweza kutumika pia kwa urafiki wa karibu katika njia fulani fulani lakini usiwe wa kupitiliza.Wakati yanapojadiliwa kidhahania, mapenzi kwa kawaida yanarejelea pendo kati ya watu, hisia alizonazo mtu kuhusu mtu mwingine. Mapenzi mara nyingi yanahusisha kutunza au kujiainisha na mtu au kitu, ikiwa ni pamoja na nafsi ya mtu.Aidha, katika tofauti za kiutamaduni katika kuelewa mapenzi, mawazo kuhusu upendo pia yamebadilika sana kadiri ya wakati.
Baadhi ya wanahistoria wanahusisha dhana za kisasa za mapenzi ya kimahaba na Ulaya wakati au baada ya Karne za Kati, ingawa kuwepo kwa mahusiano ya kimahaba kabla ya wakati huo kunaonyeshwa na ushairi wa kimapenzi wa kale na sio ya sasa utaaribika binti.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kutokana na utata wa dhahania ya mapenzi, mjadala juu ya mapenzi kwa kawaida hupunguzwa hadi maneno yaliyopitwa na wakati, na kuna mithali kadhaa kuhusu mapenzi, mojawapo ikiwa ile ya watoto wadogo. Pendo hushinda mambo yote ambapo mhusika anakuwa hawezi kufanya kitu zaidi ya kuwa na msongo wa mawazo kama ulivyo wewe, hivyo basi unatakiwa uhachane na mawazo hayo uende shule ukasome na sio kumuwaza mtu ambaye ujui alipotokea.Mapenzi kati ya watu wawili ni hisia za nguvu kuliko kumpenda mwingine kwa jumla.
Mapenzi yasiyotuzwa ni hisia za mapenzi ambazo haziwezi kulipwa au kurudishwa. Mapenzi kama haya yanaweza kuwepo kati ya wanafamilia yako tu na sio kwa marafiki. Pia kuna matatizo kadhaa ya kisaikolojia yanayohusiana na mapenzi.Katika historia ya mtu na dini ndizo taaluma ambazo zimeelekeza sana suala la mapenzi. Mapenzi yamegawanyika katika sehemu tatu zinazolingana ambazo ni tamaa, mvuto na pendo. Tamaa huwafunua watu kwa wengine, mvuto wa kimahaba huwahamasisha watu kuzingatia nishati yao kwa kuhusiana kingono na pendo linahusisha kustahimili mwenzako au mtoto kwa muda wa kutosha.
Tamaa ni hamu ya mwanzo ya ngono ambayo inahusisha kutolewa kwa wingi kwa kemikali. Athari hizi huwa hazikai zaidi ya wiki chache au miezi michache.Utafiti uliofanywa hivi karibuni na wanasayansi umeonyesha kuwa kadiri watu wanavyoendelea kupendana, ubongo huwa unatoa aina fulani za kemikali, ikiwa ni pamoja na 'pheromones', 'dopamine', 'norepinephrine', ambayo hufanya kazi sawa, kuchochea kiini cha furaha kwenye ubongo na kusababisha ongezeko la mapigo ya moyo, kupoteza hamu ya kula na kulala, hisia kali za msisimko juu ya mtu huyo. Utafiti umeonyesha kwamba hatua hii kwa jumla hudumu kuanzia mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu. Nakubunia nadharia ya miraba mitatu ya mapenzi Bi.Janeth akaendelea na akasema mapenzi yana vipengele vitatu tofauti ambavyo ni urafiki, kujitoa, na uchu. Urafiki ni aina ambayo watu wawili huambiana siri na mambo kadhaa kuhusu maisha yao binafsi. Kuwajibika, kwa upande mwingine, ni matumaini kuwa uhusiano huo ni wa kudumu. Aina ya mwisho na inayopatikana sana ni mvuto wa kingono au uchu. Mapenzi ya uchu ni kama yanavyoonyeshwa katika kupumbazwa kimapenzi pamoja na mapenzi ya kimahaba. Aina zote za mapenzi hutazamwa kama mchanganyiko tofauti wa vipengele hivi vitatu.Shamsa alikuwa amenyamaza tuli akimsikiliza kwa umakini mkubwa sana Mwanasaikolojia huyo.Alikuwa amkimueleza hali aliyokuwa nayo kuhusu kijana Jongo, kuondoka kwake kumekuwa na madhara makubwa sana katika familia yake, kwani kipindi hicho alitakiwa ajitahidi kusoma ili aweze kufaulu mitihani yake.
Baada ya kuzungumza Bi.Janeth aliaga na kuondo huku Bwana Samir akiwa mtu mwenye furaha baada ya kumuona mtoto wake akiwa mwenye tabasamu mwanana lililochanua kwa huba.Bi.Ramla alifurahi zaidi pale alipoingia chumba cha mtoto wake na kumkuta Shamsa akiwa mwenye tabasamu pana usoni mwake huku mikononi mwake akiwa ameshikilia kitabu kilichoandikwa “Mahusiano katika maisha yangu”Bi.Ramla alikiangalia kitabu hicho mara mbili mbili kisha akamfuata mahali pale alipokuwa amekaa mtoto wake.Hakujali kumsingikiza mgeni aliyekuja kumpa ushauri mtoto wake badala yake Bwana Samir ndio aliyemsindikiza mgeni huyo.
“Vipi Mwanangu…umemuonaje mwalimu?” Bi.Ramla aliuliza kwa mbwembwe
“Sawa tu mama …nimemuelewa na amenishauri vizuri sana”Shamsa alijibu kwa furaha
“Hongera mwanangu kama umemuelewa unatakiwa ufuate ushauri wake sasa mama”Bi.Ramla alisema
“Rakini mama ndio basi tena kuonana na Jongo, kwanini nisionane nae hata siku moja tu?”
“Lakini mwanangu si umemsikia mshauri alivyosema…hutakiwi kuwaza sana na kulazimisha kitu wakati mungu hajakupangia”Bi.Ramla alisema
‘Sawa mama nimekuelewa nitafuata ushauri wenu nyote”
“Vizuri mwanangu unatakiwa usome sasa hachana na vitu visivyokuwa na msingi kwako”
‘Sawa nimekuelewa mama”
Baada ya mazungumzo kwa mzazi na mwanaye yalikuwa ya furaha hata pale Bwana Samir naye aliingia chumba humo na kuendelea na mazungumzo yao.Bwana Samir na mkewe walimsihi mtoto wao kuwa na amani siku zote na kurejea shuleni ili kuweza kufanya mtihani wake wa kidato cha nne.Shamsa hakuwa na kinyongo aliweza kuwasikiliza kwa umakini mkubwa wazazi wake kwa vile ushauri wa Bi.Janeth kumuingia akilini hakuwa na namna alikubaliana na wazazi wake kisha kwa pamoja wakakumbatiana na mtoto wao.
***********
Ulikuwa mwaka wa pili sasa tangia Jongo na mama yake wahame mji wa Mwanza.Shamsa akiwa kidato cha nne hakiwa hajui chochote kinachoendelea juu ya kijana Jongo,hakuwa na mawasiliano nae wala kuzisikia habari zake.Muda wote alipenda kuwa pamoja na marafiki zake.Hakika hakupenda kuwa karibu na wanaume kwani alijua madhara yake juu ya kuwa na ukaribu nao kwani alifundwa na Bi.Janeth kutokuwa karibu na wanaume hao kimazoea.Siku zilikimbia kama mwewe angani mwaka wa pili ukafikia Shamsa kuingia kidato cha nne.Alisoma kama kawaida mpaka ikafikia kipindi cha kufanya mtihani wa kidato cha nne, alifanya mtihani wake na kuushinda vyema kwa harama za juu .Shamsa akafaulu kuingia kidato cha tano katika shule ya sekondari Mwika iliyopo mkoani Moshi. Aliendelea na masomo ya sekondari huku akiwa msichana mrembo mwenye shepu ya kumpagawisha mwanaume yoyote aliyetokea mbele ya macho yake.Shamsa alikuwa mtoto pekee katika familia ya bwana Samir na mkewe Bi.Ramla.Shamsa alikuwa mwenye sura nzuri macho makubwa ya kuregea hakika alikuwa mzuri wa kuvutia.Kipindi cha kuanza masomo,Shamsa aliondoka Mwanza na kuelekea mkoani Moshi.Aliondoka akiwa mtu mwenye mawazo sana hakujua jinsi gani atakaa mbali na wazazi wake,Zaidi kilichokuwa moyoni mwake ni kuonana na kijana Jongo aliyeondoka miaka miwili iliyopita.Alianza masomo yake Mjini Moshi lakini muda wote alionekana mtu mwenye mawazo hata waalimu pamoja na wanafunzi wenzake walijua ila hawakuwa na namna ya kumhoji kuhusiana na tatizo hilo.
Shamsa aliendelea na masomo yake kwa muda wote wa miaka miwili na kukaa bila kurudi Mwanza kwani Mama yake hakutaka mtotowake arejee nyumbani angali bado akiwa hajamaliza masomo yake .Hivyo kipindi chote hicho alisoma bila kurejea.Hata kipindi cha likizo hakuruhusiwa kurudi mwanza badala yake alikwenda kwa dada yake aliyekuwa akiishi dare s salaam.Kidato cha tano akamaliza akaingia kidato cha sita kwa furaha huku akijua muda wa kumaliza masomo unawadia ili kurejea nyumbani kwa wazazi wake...
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati huo Shamsa akikalibia kumaliza kidato cha sita alikuwa akisumbuliwa sana wanaume mbalimbali hasa wanafunzi wenzake walimtaka kimapenzi.Katika kidato cha sita kulikuwa na kijana mmoja mtanashati anayeitwa Rashid,Kijana huyu hakutaka kuvumilia, hakuwa radhi kuuonamoyo wake ukiteseka na wakati mtu ambaye angempa pumziko alikuwepo katika dunia hii.Hakutakiwa kusubiri, aliogopa kuchoka na hivyo akapanga siku ya kumfuata Shamsa kwa ajili ya kumwambia ukweli jinsi moyo wake ulivyojisikia.Alijipanga sana muda wa kutoka darasani, akaanza kujivuta kwa ajili ya kuzungumza na Shamsa.Hakuwa nafasi, wakati yeye akitaka kumsogelea msichana huyo mrembo na kumwambia ukweli, tayari wanaume mbalimbali waliwai kumfuata Shamsa na kumtaka kimapenzi.
Moyo wake uliumia mno,hakuamini kama ingeshindikana kabisa kuzungumza naye.Hakavumilia,akasubiri siku nyingine amfuate na kumwambia shida yake.Rashidi alikuwa mtoto wa bilionea mkubwa ambaye alitokea kumpenda msichana Shamsa.Utajiri mkubwa aliokuwa nao baba yake ulionyesha dhahiri kwamba hakuwa na hadhi kubwa kwa msichana Shamsa.Hakutaka kujali hilo,alipomfuata Shamsa utajiri wake aliuweka pembeni alitanguliza mapenzi kwani aliamini kwamba pesa zisingeweza kununua mapenzi,hata kama angekuwa na pesa kiasi gani angeishia kununua ngono na si upendo.
“Kumbe kwa staili hii sitaweza kuongea naye,ngoja nitafute namba yake ya simu”aliwaza.Hilo ndilo alilolifanya,kaitafuta namba ya msichana huyo.Kuipata haikuwa kazi kubwa,watu wengi walikuwa nayo,alipoipata tu,akatafuta siku na kumpigia simu kwa lengo la kuonana naye.
“Wewe nani?”Aliuliza Shamsa baada ya kupokea simu
“Rashidi!”
“Okay! Nikusaidie nini Chidi?”Aliuliza Shamsa
“Kuzungumza na wewe”
“Kuhusu?”
“Stori tu za kawaida”
“Samahani! Sina muda kaka yangu!”
“Shamsah!
“Naomba unielewe! Sina muda!” Alisema Shamsa kisha akakata simu
Hakukoma, hata siku iliyofuata aliendelea kumsumbua na kumtumia meseji nyingi mno.Hayo ndio yalikuwa maisha yake na baada ya wiki mbili, ili kuepusha usumbufu Shamsa akakubaliana na Rashidi na kuonana naye.
“Tuonane wapi?”Aliuliza Shamsa
“Bwalo la shule basi”
“Hapana sihitaji kuonekana kwa mtu yoyote yule, labda twende nje ya shule”
“Sawa Sema wewe basi, au kama vipi tuonane darasani siku ya jumapili”
“Sawa”
Siku ya jumapili ndani ya darasa, walikuwa wamekaa meza ya nyuma kabisa na pale walipo walikuwa wamezama ndani ya maongezi.Rashid alimwambia shida yake Shamsa hakuwa tayari kumuelewa kwani mawazo yake yote kwa wakati huo yalikuwa kwa Jongo, ambaye hakujua mahali alipokuwa kwa wakati huo. Shamsa alijiapia lazima amtafute Jongo popote alipo na kumuweka mikononi mwake.Wakati Rashid akiendelea kumueleza shida yake,wala Shamsa hakuwa na habari naye,mapenzi yote ndani ya moyo wake yalikuwa juu ya kijana Jongo,hakika chaguo lake lilikuwa ni Jongo hakuwa mwengine.Ikafikia kipindi Shamsa akachoka kumsikiliza Rashid kwa maneno aliyokuwa akiambiwa na kijana huyo aliona kama mkuki uliochoma moyoni mwake.Lakini Rashid hakuchoka kumbembeleza na kumpa ahadi nzuri,hata hivyo Shamsa hakutaka kuendelea kumsikiliza hivyo alinyanyuka kitini kisha akakusanya vitabu vyake na kuondoka.Rashidi alijalibu kumzuia Shamsa asiondoke lakini alichelewa tayari msichana huyo alikuwa ameshaondoka ndani ya darasa hilo na kurejea hosteli.
*******
Kijana Jongo wakati akiahamia mkoani morogoro na mama yake hakika ilikuwa majonzi makubwa kwake baada yam kutengana na rafiki yake wa kipekee Shamsa.Hakujua kama hapo alipofikia atapata rafiki atakayempenda kama Shamsa.Mama yake alikuwa na wakati mgumu sana kumbembeleza mtoto wake juu ya kuondoka Mwanza na kumuacha yule ampendaye.Baada ya siku mbili tatu Jongo alipelekwa shule ya sekondari Kigurunyembe kuendelea na masomo yake akiwa kidato cha tatu.Jongo aliendelea na masomo yake akiwa mremavu wa macho,wataalamu mbalimbali waliendelea kufika shuleni hapo ili kuendelea kumfundisha Jongo.Wakati Jongo akifundishwa peke yake alijiona mnyonge,mkiwa mwenye simanzi juu ya uhuru wa kucheza na watoto wenzake.Hapo ndipo mawazo yalipojirudia juu ya msichana yule dada aliyekuwa akicheza nae pamoja mjini mwanza,alijipa moyo na kujisemea lazima amtafute popote pale Shamsa ili awe karibu naye.
Jongo alisoma na kuhitimu kidato cha nne huku akiwa kijana mtanashati mwenye kuvutia, kipindi chote hicho Jongo kutengana na Shamsa hakuna hata mmoja kati yao aliyewai kumpigia simu mwenzake.Ingawa walikuwa hawana simu kipindi wakiwa sekondari hivyo baadae Jongo alipewa simu na mama yake ili aweze kuwasiliana na watu wake wa karibu.Hata hivyo licha ya Jongo kuwa na simu lakini mawasiliano yake kwa Shamsa yalishindikana kwani hakujua jinsi gani ataipata namba ya Shamsa kwa wakati huo.Hata hivyo hakukata tamaa alizidi kumuweka moyoni msichana huyo mrembo.Alijifikiria kuandika barua hili aweze kuituma kwa anuwani ya shuleni kwao lakini alipokumbuka ya kwamba kwa kipindi hicho tayari Shamsa ameshamaliza masomo yake ya kidato cha nne sasa atakuwa ameamia shule nyingine kuendelea na masomo.
Kipindi hicho Jongo alikuwa yupo tu nyumbani baada ya kumaliza kidato cha nne hakuweza tena kuendelea na masomo yake kwa kidato kinachofuata.Alijisikia vibaya sana kukaa tu nyumbani, alipenda kusomo ila kwa alama alizopata hakuchaguliwa kuendelea kidato cha tano.Jongo alijipa moyo kwani hakutaka kukaa tu nyumbani alimuomba mama yake ampeleke hata kusomea ufundi mama yake alikubali ila alimwambia ya kwamba asubiri mpaka pale atakapopata pesa ndipo atampeleka kusomea humakenika.Jongo alifurahi na kumwambia mama yake sawa yeye yupo tayari kwa lolote ili mladi apate angalau ufundi utakao muwezesha kujikimu kimaisha hapo baadae.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya siku mbili tatu hadithi ikawa hile hile mama upate pesa unipeleke nikapate elimu iweze kutukombua kiuchumi.Jongo alimlilia mama yake kila simu alimbembeleza lakini mama yake hakuwa na pesa hivyo alimuomba kuvumilia mpaka pale atakapopata pesa atampa na kwenda kusoma kile anachokitaka.Jongo hakuwa na jinsi aliamua kunyamaza ili kujua hatma ya maisha yake kila kitu alimuachia mama yake maana hakuwa na msaada wa mtu mwingine zaidi ya mama yake pekee.
********
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment