Search This Blog

Wednesday, 1 June 2022

CHAGUO LANGU NI WEWE - 1

 





    IMEANDIKWA NA : TATU KIONDO



    *********************************************************************************



    Simulizi : Chaguo Langu Ni Wewe

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ingawaje waliishi na mama yake, Ramla mambo yalimwendea vibaya.Ramla alikuwa mtu mwenye kushiba, si shibe ya chakula alichokipenda wala shibe ya uji ambayo aliijua vema, Ramla alishiba shibe ya mtu mzima mdundiko alioubeba mbele chini ya kifua chake ulikuwa mkubwa kweli. Ilikuwa tayari miezi nane tangia aletwe nyumbani kwa wazazi wake na mumewe Samir.Mkanganyiko ni juu ya giza nene lililotanda juu ya hali yake.Kipindi hicho Ramla alikuwa nyumbani Kisarawe kwa wazazi wake kwa ajiri ya kujifungu.Ukitaka kujua uzuri wa mwanamke mpe pakacha abebe.Lah! kachoka kama mbwa wa maskini hata hatamaniki.Siku moja Ramla alikuwa nje akipunga upepo majira ya saa moja jioni peke yake amejiraza chini ya mwembe nje ya nyumba yao.Ghafla akiwa hana ili wala lile alisikia sauti ya unyayo wa mtu ukimfuata pale alipokaa,alinyayuka haraka na kukimbilia ndani akafunga mlango.Mama yake alipomuona alistuka akamuuliza kilichomsibu huko nje alimjibu kwamba kuna mtu alikuwa anamfuata pale alipolala.Mama yake alimtoa wasiwasi na kumtaka aondoe shaka kwani historia ya kijiji chao hakuna matukio ya ajabu ajabu yanayotokea wala yaliyowai kutokea katika kijiji hicho.Ramla alimsikiliza mama yake lakini hakutaka tena kurudi nje kwani ameshaingi uwoga uliochanganyika na usingizi ni bora alale kabisa.



    Ramla alikuwa amechoka kweli kwa mzigo aliokuwa ameubeba mbele ya kifua chake aliagana na mama yake akaingia chumbani kwake akalala nahuku akimuacha mama yake akiendelea na kazi za jikoni.Nje kulikuwa na wingu zito angani,baada ya muda ulifuata upepo mkali uliokifagia kijiji kizima cha Kisalawe.Baada ya muda upepo ulivyokoma,mvua kubwa iliyoambatana na radi ilienea na kukifunika kijiji kizima.Giza likawa giza kweli kweli,ghoruba si dhoruba,kila sehemu kulitikisika.Ulikuwa usiku wa ajabu katika mwezi wa pili wa mwaka wenye mvua.Mwezi ambao walimwengu wa mahaba waliwatumia wapenzi wao maua na mavazi mekundu.Siku hiyo wenye kazi walitarajia na kuombea kuchwe haraka ili waweze kujipatia riziki na ujira wao.Usiku ule ule,hatimaye yakawa.Usiku wa saa nane Ramla uchungu ulimshika.Nyonga zilimbana kisha pumzi kumtoka.Chwaa!kama kiwembe ,maumivu ya uchungu yalimkata tangu kiunoni,yalizunguka mbele ya kinena cha tumbo na kusambaa mwili mzima.Aliugulia kwa maumivu makali kisha ganzi ikamkwida.mdomo wake aliupanua na kutoa sauti kumwita aliyemzaa, “Mamaa!” Uchungu wa kuzaa mwana aliye baba akiwa hajui kitendekacho kwa mama.Tena Ramla aliita, “Mamaaa!” Kimya! Hakuna aliyesikia na kukipokea kilio chake.Mama yake alikuwa amelala fofofo.Hata kama angelikuwa macho, kelele za radi na upepo mkali ziliyaziba masikio yake na kumfanya kujikunyata kama paka kando ya jiko.

    Shime!Alijikaza binti Ramla akijikokota kutambaa kukifuata kijinga cha moto uliokuwa ndani ya sebule yao.Baridi kali lilimsugua na kuugandisha mwili wake.Hakuweza kusimama, alijiburuza kwa shida akitaka kuufikia mlango wa kutokea chumbani kwake,lakini,nguvu zilimwishia.Alipumzika kidogo ingali radi iliendelea kupiga na kumfanya aone kupitia ule mwanga sehemu ya dirisha kisha kujivuta tena na tena.Alipofika sehemu hiyo iliyokuwa na moto lakini isivyobahati,moto ulizima kwa matone yaliyokuwa yakitoka juu ya paa la nyumba yao ya makuti.Alijiegemeza kwenye jifya akijalibu kuzivuta pumzi.Alizipandisha na kuzishusha, “Yalaa!”Sauti ya uchungu ilimtawala.Jasho jembamba katikati ya baridi lilimtoka na kulivuruga tumbo.Pwaaaa! kwa haraka alitapika.Aliipandisha pumzi kisha kuishusha kwa taratibu.Hali hiyo hakuwahi kuizoea wala kuhisi hivyo aliingiwa na shaka, “Mamaaa! Maa….”Ramla aliita kisha kukatiza.Alihisi nyonga kumbana kila alipovuta pumzi kwa pupa.Taratibu alianza kutweta kama jibwa wakati wa jua kali.Nguvu zilimwishia tena.Alitulia kwa sekunde chache.Tena! tumbo lilimvuruga na kuruhusu mdomo wake kutapika.Pwaa! Alitapika, mate yalimtililika akakishika kiuno chake na kujinyonga, “Shiiiih! Mamaa!” Ramla alikuwa akiongea na uchungu wa kumzaa mwana. Mmmmh! Sauti ilimtoka akaufunga mdomo wake haraka kusukuma.Tena na tena akiwa kalala chali sakafuni palipolowa maji. Bado safari ilikuwa ikimtaka kujaza pumzi upya.Alifundwa kufanya hivyo na ndio ilikuwa imemtokea.Tena akafumba aliufumba mdomo wake akaipandisha pumzi nyingi.Kimoyomoyo alijipa nguvu kwa kuhesabu “moja…mbili…tatu! Alizibana pumzi na kusukuma.Aaa! Kazi ilikuwa ikimwendea mwishoni.Alipumua haraka haraka kisha kujiegesha kwa ubavu akiinamia mikono yake. “Mungu ninusuru na haya majaribu” alisema na kelele alizipiga.Kama karatasi,mwili wake ulinywea,pumzi alizivuta akihisi kuutua mzigo mzito.Sauti ilimtoka tena “Mamaaa!” kimya!hakusikia mtu.Hakusikia kilio cha mtoto bali mtikisiko kidogo.Nguvu zilimwishia akaweweseka akiita.Ghafla akalegea na kuzimia.Kichanga hakulia wala hakutapatapa baada ya kuzaliwa.Je,alikuwa mzima au si riziki yake?Hayo yote angeyajua aliyemshuhudia kwa mara ya kwanza kuzaa kichanga hicho.



    Mvua iliendelea kunyesha na radi ilimulika kwa taratibu.Mama Ramla alihisi kibofu chake kushindwa kuyabeba maji yaliyochujwa mwilini mwake.Chapa! miguu yake aliishusha kitandani kwake na kuitua kwenye sakafu iliyojaa maji. “Haa! Maji au?” Alishangaa kidogo.Jubwi jubwi!alitembea akiyakanyaga maji yaliyofurika chumbani kwake.Kwa haraka alipapasa ukutani kwenye nguzo.Alikiagiza kidole chake kwenye kitufe cha kuwashia.Kwacha!Kuruzi iliwaka na mwanga wake kuking’arisha chumba alimokuwa.Alipiga hatua kuelekea mlango uliompeleka sebuleni.Mguu wa kwanza akatoka na kutua salama ukifuatiwa na wa pili,mkono wake aliuzungusha kumulika sebule kabla hajatoka.Alistuka Mama Ramla macho yake yalitua kwenye biwi la damu.Bintiye kanyooka na kidubwana katikati ya mapaja yake. “Mama yangu,!” Sauti ilimtoka.Alidumbukia chumbani kwake kwa haraka na akatoka na wembe uzi na kanga mkononi kisha kurejea akiwa amechanganyikiwa.Alikiviringa kichanga kwa kanga baada ya kukitenga na mama yake.Alirejea chumbani kwake haraka na kukilaza kisha akakifunika vizuri akatoka.Ramla kwa wakati ule alikuwa akiweweseka pasipo ufahamu.Damu nyingi zilimtoka na kuzihamisha nguvu zake zote.Alihitaji msaada wa haraka wakati ule.Mama yake alifika kisha kumshika na kumvuta akimtoa kwenye biwi la damu na maji.Alimkagua na kumvua nguo zote na kumfunika vizuri na kitenge.Ramla hakuwa na fahamu wala hakujua kilichokuwa kikiendelea.Mamaye aliushika mkono wa mwanae kujalibu kuunyanyua na kuachia,ulienda legelege na kutulia.Alimtikisa na kumgeuza kichwa chake kushoto,kulia,wala hakuweza kustamili.Mama Ramla alipatwa na kiwewe. “Ramla!”Aliita wakati akijaribu kumtikisa na kumwegesha kwenye mapaja yake.Maji yalizidi unga, ugali ushakuwa uji. “Ramla mama!” Aliita tena na tena, lakini kimya hakuitika, alichukua taa na kumulika machoni. “Mwa-na-ngu” kilio kilimtoka na kuene kijiji kizima. “Mamaaaaa! Mwananguuuuuu-uwiii!” Alipiga kelele kwa nguvu......



    .Aliendelea kumshika na kumpapasa Ramla na kumfunua lile tenge alilomfunika na kumshika kifuani.Kimya! Akili ilimhama. Alinyanyuka tena na kumshika akihaha kila upande.Hapakuwa na alilolifurahia kwa jinsi hali ya mwanae ilivyokuwa.

    Majirani walifika kusikia kilio cha mtu mzima waliingia na kumwangalia Ramla alikuwa hoi taabani hajui linalotendeka duniani.Kwani nguvu zilikuwa zimemuishia kutokana na kupoteza kiasi kikubwa cha damu wakati wa kujifungua. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Haraka majirani walitawala ndani ya nyumba hiyo ndogo,walimzunguka Ramla na kumshika shika ili kupima joto la mwili wake.Mapigo ya moyo wake yalisikika kwa mbali haraka hawakutaka kupoteza muda wakamfuata jirani aliyekuwa na gari ili awasaidie kupata usafiri kumuwaisha Ramla na kichanga hospitali.Mzee huyo anayeitwa Shabani hakusita alivaa nguo zake kisha alitoka moja kwa moja akafika nyumbani kwa mama Ramla,Haraka alimpakia Ramla pamoja na mama yake aliyekuwa na kichanga mkononi.Gari lilikata njia na kuyoyoma kuelekea hospitali ya rufaa,Mama Ramla,Ramla mwenyewe na mtoto wake wakiwa ndani ya gari hilo.Muda wote huo Ramla halikuwa mtu hasiyekuwa na fahamu hata kidogo,hakuelewa kilichokuwa kikiendelea duniani kwa wakati huo,fahamu zilimuhama na kumuachia usingizi mzito usiojulikana siku ya kuahamka wala kuteteleka aliendelea kulala vile vile.Kichanga nacho kiliendelea kulia pasipo kunyamaza,alilia akiwa mikononi mwa bibi yake mzaa chema pasipo kumpa nyonyo kwani tangia azaliwe hakuwa ameyaonja angalau kidogo radha ya maziwa ya mama yake.Bibi huyo mweupe mrefu kidogo akiwa na nywele nyingi zilizofungamana juu ya kichwa chake alikuwa makini kumbembeleza mtoto huyo aliyekuwa akiendelea kumsombua akitaka nyonyo kutoka kwa mama yake lakini loo! Mama yake alikuwa hajitambui.



    Gari lilizidi kuyoyoma kupanda mabonde na milima kukatisha njia kushoto na kulia,hatimaye waliwasili hospitali ya rufaa Kisarawe.Dereva alisimamisha gari mbele ya lango kuu la kuingilia hospitalini hapo,haraka wauguzi walifika na wengine walichukua kitanda cha magurudumu kwa ajili ya kumbebea Ramla.Wauguzi wote walikuwa makini sana,walimbeba Ramla na kumkokota kuelekea chumba maalumu cha kina mama.Walimuingiza kwenye chumba hicho akiwa na mtoto wake aliyekuwa amebebwa na nesi.Ilikuwa majira ya saa kumi na moja za alfajiri Ramla alikuwa bado ndani ya chumba hicho huku nje hakuna aliyekuwa akijua kinachoendelea,Mama Ramla akaanza kuingiwa na wasi wasi uenda mtoto wake akapatwa na matatizo makubwa mpaka madaktari wanashindwa kumudumia tatizo lake mapema.Lakini pia alijipa moyo na kuendelea kusubilia ili kujua hatma ya mtoto wake maana alimpenda sana Ramla na hakuwa tayari kumpoteza mtoto wake wa kipekee.Baada ya muda kupita hatimaye wakiwa bado wanaendelea kusubili na kumuomba mungu Daktari alitoka ndani ya chumba hicho akiwa na faili lake mkononi.Alipofika tu mlangoni alipokelewa na Mama Ramla na yule jirani yake aliyemleta na gari.

    “Vipi Daktari….Kitu gani kinaendelea?”Mama Ramla aliuliza mdomo ameuacha wazi

    “Anaendelea vizuri tu wala msiwe na wasi mama”

    “Ni kweli Daktari?” mama Ramla aliuliza

    “Msijali ni wajibu wangu kuhakikisha Ramla anarejea na hali yake ya kawaida”Daktari alimjibu

    “Vipi mtoto nae?”

    “Pia anaendelea vizuri na sasa mama yake anamnyonyesha.

    “Kweli Daktari……aisee siamini kabisa vipi tunaweza kuingia kumuona?”

    “Yes…mnaweza kuingia”Daktari alijibu huku akiwapisha mlangoni pale aliposimama waingie ndani kumuona mtoto wao.

    Mama Ramla aliingia moja kwa moja huku nyuma yake akiwa ameongozana na yule jilani mwema.Walipoingia Ramla alifurahi kumuona mama yake akiwa mwenye hali hile,Mama yake alikuwa na haya kwa jilani yake alipoingia tu alimkumbatia mwanae na kumpa pole kwa uchungu uliomkuta katika hali hiyo alimtaka kuwa makini na jambo hilo kwani kuzaa mtoto si kazi rahisi hata kidogo.Ramla alimuitikia mama yake na kisha alimsalimia yule jilani na kuendelea kumnyoyesha mtoto wake huku drip yenye damu ikiendelea kushuka taratibu kwenye mishipa yake ya damu.Siku hiyo Ramla alimuomba mama yake ampe simu ili ampigie mumewe na kumpa taarifa za kujifungua kwake.Mama yake alifungua mkoba mdogo uliokuwa mapajani mwake kwa wakati huo na kumpigia simu mumewe aliyekuwepo jijini Dar es Salaam. Simu upande wa pili ulipokelewa na maongezi ya wanandoa hao yakafuatia.Ramla alimwambia juu ya habari nzuri ya kujifungua mkewe,Bwana Samir alifurahi sana kusikia taarifa hizo kutokana mkewe kipenzi Ramla alimwambia jinsia ya mtoto,alishukuru na kumbusu mkewe ndani ya simu na kumwambia kweli amemletea zawadi kutoka kwa mungu mtoto wa kike ni furaha iliyoje kwa kupata kimwana.

    ********

    Kwa kipendi kirefu walilalamika na kusimanga juu ya uzao wa familia yake kwani walikaa miaka mingi bila kupata mtoto sasa leo mkewe amejifungua salama salimini.Bwana Samir alitamani afunge safari mara moja kwenda kijijini huko kumuona mke na mtoto wake,hiyo yote ilishindikana kutokana na furaha aliyokuwa nayo, alipanga na kwenda kuomba ruhusa kwenda huko kijijini akajionee mwenyewe juu ya utukufu wake muumba.Alipomaliza kuongea na simu aliacha kila kitu alichokuwa akifanya na kuamua kuandika barua ya kuomba ruhusa kwa ajili ya kumuona mkewe aliyejifungua, kumfuata kabisa ili arudi nyumbani kwa ajili ya kumlea mtoto wake.Akaandika barua na kupeleka kwa muhusika muda si mrefu Bwana Samir alipata barua ya majibu kutoka kwa bosi wake na kumtaka asiwe na wasiwasi aende tu kumuona mkewe pamoja na mtoto wake.Watu wengi majirani na wafanyakazi wenzake walifurahi na kumpongeza Samir kupata mtoto ni heshima ilioje kwake.Siku iliyofuata asubuhi na mapema akiwa na shauku tele moyoni ,alijipanga kwa safari ya kwenda msanga kumuona mkewe kipenzi.Kabla ajaanza safari aliamua kwenda Sinza kijiweni kununua mahitaji muhimu kwa ajili ya mke na mtoto wake...



    Bwana Samir alikusanya kila kitu alimnunulia mkewe vitu mbalimbali pamoja na nguo za mtoto, kisha alinunua baadhi ya vyakula kwa ajili ya familia yake huko aendako.Ilifikia saa sita mchana Samir alikamilisha kila kitu na kuanza safari ya kwenda kijijini Kisarawe kumuona mtoto na mke wake.Ilikuwa kama bahati alipokuwa anatoka standi ya daladala Sinza alikutana na rafiki yake aliyekuwa wakifanya kazi pamoja.Samir alimsimamisha rafiki yake huyo anayeitwa Msigwa kisha alimsabahi kwa pamoja wakasalimiana,kwa vile bwana Msigwa alikuw ndani ya gari yake Samir alimuomba Msigwa amuhazime gari yake kwa ajili ya kwenda kumuona mkewe huko kijijini Kisarawe.Msingwa hakuwa na shida alimsikiliza kwa makini rafiki yake kisha alimtaka hasiwe na mashaka kwani siku hiyo hakuwa na kazi nalo hivyo aliomba ampeleke nyumbani na kumuhacha ili yeye aweze kuchukua gari hiyo na kuelekea na safari yake.Samir alifurahi sana kusikia hivyo hakuwa na budi kukubaliana na rafikiye aliingia ndani ya gari na safari ya kuelekea nyumbani kwa Msigwa ilipoanza.Njia nzima Samir aliwaza na kuwazua,alifikiri na kuona muda mwingi unaisha bila kuanza kwa safari yake ,alizidi kuchanganyikiwa,kichwa chake kilimfikiria mke pamoja na mtoto wake huko walipo. Aliona Kama rafiki yake anamchelewesha kuanza kwa safari yake. Lakini hakuwa na jinsi aliamua kuvumilia jinsi itakavyokuwa, alijiapiza lazima siku hiyo aondoke na afike kuwaona mke na mtoto wake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya muda wa nusu saa walifika nyumbani kwa Bwana Msigwa.Mlinzi aliposikia mlio wa gari ya bosi wake akafungua geti ili aweze kuingia ndani.Lakini bila kutarajia ndivyo sivyo Bwana msigwa alishuka pamoja na rafiki yake Samir,wakaingia wote mpaka getini mlinzi alishangaa kumuona bosi wake akishuka na kuingia ndani kwa mguu, ingawa gari akiwa amelipaki pale nje ya geti bila kuingiza ndani kama inavyokuaga.Msigwa na Samir walipitiliza mpaka ndani lakini mlinzi hakutaka kusubili alimfuata bosi wake na kuanza kumuuliza “Kulikoni bosi mbona gari umelicha nje je,niliingize ndani?”.Msigwa hakutaka usumbufu alimfahamisha jinsi ilivyokuwa naye mlinzi alimuelewa alielekea getini na kuanza kulifunga geti hilo, huku Bwana Samir na rafikiye wakiingia ndani.Siku hiyo ilikuwa tofauti na siku zote kwani Samir hakutaka kukaa sofani wala kupumzika hata kidogo,Bi.Aisha ambaye ni mke wa Bwana Msigwa alipomkaribisha aliitikia huku akiwa wima wala hakukaa chini kabisa alikuwa na shauku ya kutaka kuwai kule anakotaka kwenda.Msigwa hakuwa na namna alimueleza kila kitu mkewe kuhusu gari kwa ajili ya kusafiri kwa Samir.Bi.Aisha mke alimkubalia mumewe na kumtaka ampatie tu Samir gari kwa ajili ya kwenda kijijini kumuona mkewe.Samir hakutaka kupoteza muda aliwaaga na kutoka kuelekea getini kwa ajiri ya kuendelea na safari.

    Ilikuwa yafikia saa mbili usiku gari iliingia ndani ya kijiji cha Kisarawe Bwana Samir aliwasili mbele ya nyumba ya wakwe zake,alipofika hapo alisogeza gari na kulipaki pembeni ya nyumba hiyo.Samir alishuka na kugonga mlango wa nyumba hiyo kwa bahati mbaya hakuitikiwa wala kuisikia sauti ya mtu kutoka ndani ya nyumba hiyo ndani ya nyumba hiyo,alijaribu kuzunguka nyumba nzima na kuchungulia ndani kupitia dirisha lakini hakukuwa na mtu ndani ya nyumba hiyo aliamua kuchukua simu yake na kumpigia mkewe.



    Ramla alipokea simu ya mumewe na kumfahamisha ya kwamba wao wapo hospitalini hivyo naye anaweza kwenda huko.Ramla alimueleza jinsi ya kufika hospitali hiyo ya Kisarawe.Samir hakuwa na namna aliingia ndani ya gari na safari ya kuelekea hospitali ya Kisarawe ilipoanza.Njia nzima Samir alikuwa mtu mwenye mawazo sana,alimfikiria mkewe huko alipo hospitali, kuna tatizo gani limemkumba Ramla maana mama yake alipomjulisha ya kwamba kujifungua kwa mkewe hakumwambia kama siku mbili zote bado yupo hospitalini.Alichojua yeye mkewe aliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kujifungua salama,kumbe bado yupo hospitali laa! Basi kuna tatizo kama sio kwake Ramla basi kwa mtoto wake.

    Aliendesha gari kwa mwendo wa haraka alitaka kufika mapema kumuona mke wake kipenzi muda wote alikuwa mtu wa mashaka juu ya hali ya mke na mtoto wake

    wanavyoendelea.



    Alifika hospitali sa lama aliingiza gari mpaka ndani ya hospitali hiyo kisha alishuka na kuelekea mapokezi.Alipofika hapo aliwasalimu wauguzi waliokuwa zamu siku hiyo na kuwaulizia alipolazwa mke wake Ramla,bila kusita walimwambia wodi aliyokuwepo mkewe Samir alienda.Kabla hajafika katika wodi aliyoambiwa alikutana na Mama yake Ramla,aliachia tabasamu ingawa moyoni alikuwa mtu mwenye mashaka makubwa.Walisalimia kisha mama Ramla alimtaka hasiwe na wasi wasi kwani hali ya Ramla ni nzuri,mama huyo hakutaka kumwambia hali halisi aliyokuwa nayo mkewe.Samir alihitaji kupelekwa wodi aliyolazwa mkewe ,Mama hakuwa na shida alimpeleka wodini,alipofika hapo Samir alifurahi hofu yote ilikwisha pale alipomuona mkewe akiwa amelala akinyonyesha mtoto wake.

    “Habari za huko mume wangu”Ramla alimsalimia huku akilitoa titi lake kutoka mdomoni mwa mtoto wake.

    “Salama kabisa sijui wewe….hongera mke wangu!” Samir alimpongeza mkewe kisha akambusu juu ya paji la uso.

    “Ahsante mume wangu yote ni kheri mwenyezi mungu amejaalia

    “Ni kweli lakini vipi unavyojisikia?”Samir alimuuliza mkewe

    “Tunaendelea vizuri tu, afadhali leo tofauti ya jana”

    “Nipe basi nimshike…naona umeng’ang’ania kama wako peke yako”Samir alisema kwa utani

    “Haya mchukue, utakuja kumchoka tu mwenye”Ramla alisema huku akimkabidhi Samir mtoto

    “Waooo! Samir alimpokea na kuanza kucheza na mtoto huyo mchanga aliyemuweka mikononi mwake.



    Baada ya kuridhika kumbeba mtoto huyo alimrudisha mikononi mwa mama yake kisha alimtaka mkewe amueleze kitu gani kilichokuwa kinamsumbua mpaka akalazwa siku tatu bado yupo hospitali na kwanini alimwambia kuwa amejifungua salama kumbe alikuwa bado hospitalini.Ramla alijifikiria jinsi gani atamwambia mumewe maana aliona akimwambia ukweli Samir atamchukia mama yake kutokana na kumuacha msiku peke yake akipata shida.Ramla alinyamaza na kumuomba awe mvumilivu kwani anaendelea vizuri hayo yote kutokana na masuala ya uzazi ndio ikamfanya kulazwa kwa siku tatu akichunguzwa afya yake.Samir alielewa na kumtaka mkewe ajiandae kwa ajiri ya kurudi nyumbani pale atakaporuhusiwa hospitali, kwa uangalizi zaidi kwa mtoto.Ramla alimuelewa na mama uyake hakuwa na tatizo hivyo alimtaka Samir kuwa karibu na mkewe na si muda mwingi kumuacha nyumbani peke yake.......



    Siku ilitofuata asubuhi na mapema Samir akiwa na mkwewe wakiwa wapo nyumbani walipata kifungua kinywa mapema kisha walijiandaa na kwenda hospitali.Samir alikaa nyuma ya usukani na mama Ramla alikaa kiti cha pili yake,njia nzima walikuwa na maongezi marefu kila wakati Samir alimfurahisha mama mkwe wake kwa maneno ya utani.Gari lilichanja mbuga na hatimaye waliwasili hospitalini hapo.Walipoingia wodini walimkuta walishangaa kumuona Ramla akikusanya nguo zake na kuziweka kwenye mkoba wake,alipowaona alifurahi wakakumbatiana na kuwaambia kwamba alikuwa ameruhusiwa hivyo wanaweza kurudi nyumbani.Samir aliona kama utani aliamua kwenda mwenyewe mapokezi na kuulizia.

    “Habari yako dada?”

    “Salama, karibu”alikaribishwa

    “Ahsante….hivi, samahani lakini”

    “Bila samahani”

    “Naomba kuulizia….mkewe wangu ameruhusiwa kurejea nyumbani?”

    “Anaitwa nani”

    “Ramla Karim mwenye mtoto mchanga”

    “Naam, Ramla ameruhusiwa tangu asubuhi kutokana na hali yake kuendelea vizuri yeye pamoja na mtoto tutawaandikia tarehe ya kurudi tena hospitali”

    “Oooo! Nashukuru sana kwa hilo…pia huduma zenu zimefurahisha sana”

    “Usijali karibu sana”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Samir alitoka pale mapokezi na kumfuata mkewe kisha alimgeukia mama Ramla na kumwambia vile alivyoambiwa na nesi yule wa zamu, mkewe alishukuru kisha kwa pamoja walijiandaa na safari ya kurudi nyumbani ilianza.Siku ya pili iliwadia siku ambayo Samir alitakiwa kurudi Kazini, hakutaka kuondoka na kumuacha mkewe kwa mama yake, alitaka amchukue na kurudi nae nyumbani kwake ili kuwa nae karibu.Kama ni kazi basi atamtafutia msichana wa kazi na si kumuacha na kurejea pekee.

    “Mama Kama nilivyokwambia kuhusu Ramla kurejea nyumbani”

    “Ndio baba najua hilo lakini vipi unapokuwa kazini Ramla atabaki peke yake nyumbani”

    “Hapana mama….nitafanya kila linalowezekana ili Ramla awe huru”

    “Sasa huo uhuru utatoka wapi kama nyumba nzima yupo pekee hakuna mtu wa kumsaidia wala nini uoni kama mateso atakayoyapata mkeo ni makubwa bora umuache tu huku”

    “Nitamtafutia msichana wa kazi ili aweze msaidia kazi mbali mbali za nyumbani”Samir alisema

    “Wasichana wengi kwa kipindi cha sasa si waaminifu hata kidogo hivyo naomba umuache tu mpaka pale angalau mtoto atapokuwa na miezi miwili au hata mwezi utakuja kumchukua mkeo”Mama Ramla alisema kwa hisia

    “Kama wasichana si waaminifu basi twende mama nyumbani ukakae na mtoto wako, huoni kama huku upo peke yako kijijini mama?”

    “Hapana Baba siwezi kuicha nyumba pamoja na mazao yangu nikaishi mjini”

    “Basi haina tatizo nitajua cha kufanya mama maana siwezi kuondoka bila ya Ramla”

    “Sawa uamuzi ni wako…mchukue tu mkeo”Mama Ramla alisema kwa shingo upande



    Siku hiyo ilikuwa ya furaha kwa Samir na mkewe Ramla wakiwa na mtoto wao,Bwana Samir alikuwa na shauku ya kuondoka mapema pale kijijini na familia yake,alitaka kuwa mjini ili kufurahi zaidi na kuwa karibu na mtoto wake mpenzi.Siku iliyofuata ndio siku ambayo Bwana Samir na mkewe Ramla pamoja na mtoto wao Shamsa walikuwa ndani ya gari alilokuja nalo Bwana Samir siku mbili zilizopita.Siku hiyo ilikuwa yafikia siku ya Tatu tangia afike kijijini pale kumuona mke wake,hivyo muda wa makubaliano kati yake na rafiki yake uliisha hivyo alitakiwa kulirejesha Gari ya watu kwa mwenyewe kama walivyoahidiana.Bwana Samir alimshukuru mama mkwe wake na kumpongeza kwa juhudi aliyoonesha kwa mke wake.Mama Ramla alifurahi sana wakakumbatiana na mwanae huku machozi yakimtoka na kuagana kisha Bwana Samir na mkewe pamoja mtoto wao mchanga wakaondoka kuelekea jijini Dar es Salaam.Ramla alikuwa mwenye hudhuni moyoni mwake alipomuona mama yake akijifuta machozi naye akajikuta akitokwa na machozi Bwana Samir kuona hivyo alimtuliza mkewe na kumtaka kuwa mvumilivu mpaka pale mama atakapomaliza kulima basi atamfuata na kuishi nae dar es Salaama.

    ********

    Shamsa ni mtoto wa kwanza kutoka kwenye familia ya Mzee Samir na Bi.Ramla.Bwana Samir ni mfanya kazi katika duka la dawa la Serikalini.Aliyekuwa akiishi jijini Dar es Salaam,wazazi wa Shamsa walimpenda sana mtoto wao kwani ndio alikuwa mtoto pekee katika familia hiyo ya Bwana Samir na mkewe Ramla.Muda wa miaka mingi Bwana Samir na Bibi Ramla waliangaika kutafuta mtoto bila mafanikio,waliangaika kwa waganga wa kienyeji na wakaguzi sehemu mbalimbali wakisaka mtoto,walikosa mpaka pale siku hiyo Bi.Ramla aliposindikizwa na rafiki yake kwa mtaalamu wa tiba mbadala za kina mama ndipo alipofanikiwa.Wiki mbili tangia kuanza kuzitumia dawa za miti shamba alizopewa na mtaalamu huyo, bila kutarajia Bi.Ramla alipata ujauzito,Bwana Samir baada ya kugundua kwamba mke wake ni mjamzito alimuuliza kitu gani kilichosababisha mpaka akashika ujauzito huku maana Bwana Samir aliona kama maajabu kwa mkewe kupata ujauzito ila zaidi alifurahi kupitiliza,ndipo alipomchukua mkewe na kumpeleka hospitali na majibu yalikuwa yale yale ya kwamba Ramla alikuwa mjamzito. Siku zilizidi kwenda na Bi.Ramla alizidi kuchoka kwa ujauzito aliokuwa nao.Bwana Samir alimpatia uduma zote mkewe na siku za karibuni kujifungua alimpeleka kwa mama yake kijijini ili Ramla akajifungue huko na hayo yakatimia kwa uwezo wa mungu.Akajifungua salama salmini mtoto wa kike....



    Bwana Samir akamshukuru mungu na kumpa pole mkewe kwa kazi aliyoifanya mpaka kujifunga mtoto wa kike mwenye afya bora.Bi.Ramla hakuwa na namna kwani alimshukuru sana mumewe kwa msaada aliopatia mpaka kupelekea kujifungua kwake salama.Siku hiyo ilikuwa ya furaha sana kwa kufika salama nyumbani kwao,walikuwa wamejenga nyumba kubwa yenye vyumba vitatu maeneo ya Ilala Boma.Muda huo Bwana Samir alipaki gari mbele ya nyumba yake akapiga honi kali mlinzi aliyekuwepo ndani ya uzio wa nyumba hiyo akakimbilia getini haraka na kuchungulia nje ambapo aliona gari akajua moja kwa moja na kutambua kuwa alikuwa bosi wale amerejea safari kama alivyomtaalifu.Mlinzi alifungua geti kisha Bwana Samir aliingiza ndani gari nyuma mlizi akafunga geti na kuwasogelea.Bwana Samir alishuka ndani ya gari na kuzunguka mpaka upande wa pili akafungua mlango na kumpokea mkewe mtoto mchanga aliyemshika.Bwana Samir alimtaka mlinzi kushusha mizigo na kuingiza ndani.Mlinzi alifanya kama alivyoambiwa huku Ramla na mumewe wakijikokota na kuingia ndani.

    ******

    Wazazi hao wawili Bwana Samir na mkewe kwa kipindi chote hicho walikuwa ni wafanyakazi tofauti kwani Bwana Samir alikuwa ni mfanya kazi katika duka la dawa la serikali (Madawa) na mkewe Bi.Ramla alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi Ilala boma.Kipindi chote hicho Bwana Samir alikuwa bado akiendelea kufanya kazi ndani ya duka hilo kubwa pia mkewe alipata likizo ya uzazi kwa kipindi cha miezi mitatu.Siku hiyo baada ya kurejea na mkewe wakitokea kijijini muda wote Bwana Samir alionekana kuwa na furaha,alizunguka huku na kule huku akicheza na mtoto,aliwapigia simu wafanyakazi wenzake na kuwaambia juu ya furaha aliyokuwa nayo.Wengi walimpongeza na wengine kumshangaa kwa kupata mtoto ndio awe katika hali hiyo ilishangaza.Bwana Samir hakujali yeye alijiona mtu mwingine kabisa kila alipokuwa akimwangali mkewe alihisi kumpenda zaidi kwani alimuona kama ndio siku ambayo mara ya kwanza kukutana nae pale Sinza mapambano.Alimbusu kwa mara nyingine tena kisha Ramla alimtaka kuwa na amani kwani alitakiwa kurejesha gari ya watu siku hiyo lakini Bwana Samir hakujali wala akulitilia maanani suala hilo.Mkewe alijua kitu ambacho mumewe kinamsumbu ni kwamba hataki kuondoka na kuwaacha, alihisi kama kuibiwa aliamua kuchukua simu yake na kuanza kumpigia rafiki yake.

    “Hallow!”Simu upande wa pili ulisikia

    “Hallow! Habari yako?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Salama tu….niambie bwana Samir”

    “Ramla amejifungua salama….kwanza kwa yote nisamehe sana kuchelewesha mpaka muda huu”

    “Wala haina neno bwana hongera sana…..amejifungua mtoto gani?

    “Wa kike anayeitwa Shamsah

    ‘He! Bwana daah hongera aisee naona unaitajika kufuga mmbwa sasa nyumbani kwako?”

    “Hahahhaa! Umeona hee...sasa ndugu naomba uje nyumbani maana leo sijisikii vizuri kutokana na safari hii pevu”Samir alimwambia

    “Sawa haina tatizo rafiki yangu ngoja nioge kisha nitafika hapo muda si mrefu”

    “Sawa sawa nashukuru sana ukifanya hivyo bwana”Kasimu alisema

    Miaka mitatu ikapita wanne ukawadia na hatimaye miaka mitano sasa tangia Bwana Samir na mkewe Ramla kupata mtoto wa kike waliyekuwa wakimuhita Shamsa Samir.Siku hiyo ilikuwa na hali ya mawingu mawingu Bwana Samiri akiwa kazini kwake kama kawaida alishangaa akiitwa na katibu mhuntasi wa duka hilo na kumtaka ahache kazi alizokuwa akifanya na kumfuata bosi ofini kwake.Bwana Samir kiroho kilimdunda hatari, hakujua kitu gani ambacho alikuwa akiitiwa na bosi wake huyo,alijiuliza tena na tena lakini hakupata jibu ndipo alipoona amfuate tu bosi wake akasikilize alichoitiwa.Ilikuwa majira ya saa sita mchana Samir akiwa ndani ya chumba kimoja kikubwa kilichojaa makabati ya mafaili kibao pale ukutani,bwana Samir akiongea na bosi wake aliyejulikana kwa jina moja la Mwapachu.Alishangaa alipomuona Bwana Samir akinywea tofauti na siku zote alipokuwa akimuona mtu mwenye furaha,Samir alikuwa mbali kimawazo akujua kitu gani alichokuwa ameitiwa na bosi wake,alimwangalia mara mbilimbili huku uso wake ukiwa dhaifu na alitia huruma mpaka Bwana Mwapachu akahisi labda Samir atakuwa ameambiwa kile ambacho aliitiwa hapo na ndio maana akawa katika hali hiyo. “Samir nimepata barua yako kutoka afisa ugavi serikalini na ndani ya barua hii ikisema ya kwamba umepatiwa uwamisho kutoka Dar es salaam na kuamia Mjini Mwanza, kuendelea na kazi yako mkoani humo.Bwana Samir alishusha pumzi ndefu alizishusha, huku akiwa ahamini kile alichokisikia kutoka kwa bosi wake kabla hajamjibu chochote alihachia tabasamu afifu kisha alimwangalia bosi wake na hatimaye akaachia kinywa chake kisha alichukua kitambaa cha leso na kujifuta jasho lililokuwa linamtoka kwa wakati huo.Alimwangalia tena bosi wake kisha akaanzisha mazungumzo baada ya kukaa kimya kwa kipindi kirefu akimsikiliza bosi wake.

    “Aisee! Nimekuelewa sana bwana Mwapachu ingawa sijui huko niendako nitafikaje?”

    “Utafika tu Bwana Samir….kwa sababu wewe mfanya kazi wa muda mrefu katika serikali yetu”

    “Nafahamu hilo ila ni kwamba hapa jijini dar nimejenga na ndipo makazi yangu ya kudumu nina familia inayonitegemea” Ingawa mke wangu ni mwalimu jijini hapa sasa itakuwaje?”

    “Usijali Bwana Samir tumeshafanya utaratibu kuhusu huamisho wako pamoja na kukupatia barua kwa ajiri ya kuomba mkeo nae apate uhamisho kwenda huko”

    “Nashukuru sana…kama mmeanza kulifuatilia suala la mke wangu kuhusu uwamisho wake kikazi maana nisingependa kuhiacha familia yangu dar es salaam”

    “Kwa hilo shaka ondoa kabisa tumeshalifuatilia na barua hii hapa unatakiwa uipeleke kwa afisa elimu wa manispaa ya Ilala kwa ajili ya mkeo”alisema huku akimkabidhi bahasha kubwa Samir akaipokea. mtu mwenye mawazo makubwa sana aliwaza jinsi ya kuama akiwa na familia yake kwani kipindi hicho Ramla bado akiwa ni mwalimu wa shule ya msingi na Shamsa akiwa ni mwanafunzi wa darasa la kwanza.

    Walikubaliana na bosi wake kisha alimtaka kuwa na amani kwani mambo yote kuhusu uhamisho wa mke pamoja na mtoto wake atafanyiwa taratibu na bodi inayousika.Alikubali kisha akaelekea nyumbani kuwaeleza mke na mtoto wake kuhusu uhamisho huo.Wote kwa pamoja walikubaliana Shamsa akiwa mtu mwenye mawazo mengi sana kuhusu hali hiyo kuhamia makazi mapya.Aliwaza marafiki zake, watoto wenzake wanaocheza wote, alifikilia kuwaaacha waalimu wake pamoja shule aliyosoma kwa malezi aliyokuwa akiyapata...



    Bwana Samir pamoja mkewe Ramla waliamia wakiwa na mtoto wao Shamsa mwenye miaka nane akiwa binti wa darasi la pili,Shamsa akiwa mwenye udhuni kila wakati alifikiria siku ya safari ya kuhama na kuamia makazi mapya hakika hakupenda kuwaaacha marafiki zake.Tarehe ishirini na tisa mwezi wa saba Bwana Samir alihama na familia yake kwenda mjini Mwanza kuanza maisha mapya huku nyumba yake jijini dar es salaam akihacha na kumomba dada yake kuja kuishi ndani ya nyumba hiyo kwa sababu dada huyo alikuwa amepanga.Baada ya safari ndefu yenye mabonde na milima hatimaye waliwasili jijini Mwanza.Shamsa alikuwa mpweke ndani kwa siku kadhaa kutokana na safari hiyo kwani hakuwa na mtu anayemfahamu wala rafiki katika makazi hayo.Siku zilipita,wiki ikafika hatimaye Shamsa akiwa bado yupo ndani kusubilia taratibu ili kuanza shule mpya iliyo maeneo hayo waliyofikia wazazi wake.Siku moja akiwa bado anasubilia siku inayofuata ili kwenda shuleni aliomba ruhusa kwa wazazi wake ili atoke nje na kwenda kucheza,sababu alikuwa mtoto wa kuwasikiliza wazazi wake kile anachoambiwa.Mama yake alimruhusu na kumwambia hasicheze mbali na nyumbani alimjibu kuwa hatocheza mbali.Akaondoka na kwenda kucheza huku akiwa na mpira mkononi,hakupata tabu sana akafika mtaa wa pili aliwaona watoto wenzake wakicheza katika uwanja mkubwa uliokuwepo maeneo ya nyumba waliyoamia.Kabla ajafikia karibu kabisa na pale wanapocheza wenzake alisimama na kuwaangalia huku waliruka na wengine wakibebana naye akajisogeza na kuwafikia watoto wale na kusimama kando yao.



    Wakati akiwa amesimama pale watoto wengine waliokuwa kando ya pale aliposimama walimuona, haraka walimkimbilia na kutaka awape mpira wacheze pamoja,Shamsa hakusita aliutoa mpira huo na kucheza pamoja na wenzake kwani ndio ilikuwa lengo lake kilichompeleka pale kucheza.Wakati wakiendelea kucheza na watoto wenzake waliruka na kushikana mikono kama michezo ya watoto ilivyo,ghafla Shamsa alisikia baadhi ya watoto wenzake wakiongea kwa fedhea na dhalau wakimkejeli na konyoosha kidole kule ilipo barabara ya wapiti kwa miguu.Laa! Shamsa aliogopa haraka aligeuza macho yeke na kuangaza kule wenzake walioangalia, alimuona mtoto wa kiume maeneo yale akiwa na fimbo mkononi, huku kuna wakati akipiga hatua moja mbele alikuwa akiichezesha chezesha fimbo nyeupe aliyokuwa nayo mkononi mwake.Mtoto huyo akiwa anapiga hatua za taratibu kuelekea kule walipo watoto wenzake, kila alipokuwa akitembea kelele za watoto hao zilipozidi.Aisee! Shamsa alichanganyikiwa hakujua kitu gani kilichokuwa kimetokea, alizidi kushangaa kule ambapo watoto wale walinyooshea vidole. Alimuona kijana huyo mwenye umri kama wake, alimwangalia kwa makini na kumdadisi jinsi alivyokuwa akitembea kwa shida.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mtoto yule alikuwa akitembea kuelekea kwenye mti mkubwa wa mwembe uliokuwa uwanjani hapo akaketi,shamsa sasa akamuona kwa uwazi zaidi kijana yule aliyekuwa amevaa miwani na fimbo yake mkononi.Ghafla bila kutalajia muda huo huo,kitendo cha hamaki kilitokea kwa watoto wale aliokuwa akicheza nao,wote kwa pamoja waliacha kucheza na kumwangalia kijana huyo,kisha Shamsa akasikia kila mmoja wao akisema la kwake kuhusiana na kijana yule mpole.Akasikia wengine wakisema “ameshakuja tena huyooo kipofu”wengine nao wakiongea “Yaani angejua kama hatumpendi kucheza nae wala hasikuwa anakuja hapa” Daa! Shamsa alishangazwa na kauli zao akaamua kuwageukia na kuwauliza wenzake aliokuwa jirani yake. “Kwani amefanya nini mbona mnamnyooshea sana vidole…..mnajua siwaelewi?” huku akiwangalia wenzake nao wakamjibu Kwa kumtajia jina la mtoto yule waliokuwa wakimwangalia na kumsimulia. “Huyo hapo aliyekaa mwembeni hapo ni kipofu anaitwa Jongo…sisi hatumpendi ila yeye anajipendekeza kwetu”.Shamsa hakuelewa kitu gani kilichokuwa kinaendelea kati yao na kijana yule kipofu kama walivyosema, ingawa Shamsa hakuwa na uhakika wa kile alichoambiwa na wenzake.Hakutaka kuendelea kusikiliza kashfa na dhihaka na maneno ya wenzake aliamua kukaa kimya na kujirundikia mawazo tele kichwani mwake.Licha ya watoto wenzake kuendelea kucheza lakini Shamsa hakukubaliana nao kwani alitaka kujua juu ya habari za mtoto huyo wanayemchukia.



    Laa! Kweli Shamsa madadisi.



    Muda wote Shamsa alikuwa akimwangalia kijana yule huku akiendelea kucheza na wenzake ambao hawakuonesha kumjali kijana huyo.Kila baada ya muda alikuwa anageuka na kumwangalia Jongo ambaye toka alipofika alikuwa bado ameketi pale pale akiwa peke yake na fimbo mkononi.Kipindi chote hicho hakuna mtoto hata mmoja aliyemsogelea au kujaribu kuzungumza nae.Mpaka ikafikia nusu saa nzima akiwa bado ameketi chini ya mwembe huo, alikuja kuchukuliwa na mtu aliyekuwa alionekana akimfahamu kama mtu wake wa karibu kumnyanyua na kuondoka nae.Muda wote Shamsa alikuwa akimwangalia kwa macho ya kuibia na kumdadisi kijana yule mwenye ulemavu wa macho.Katika udadisi wake alipata kujua ya kwamba watoto hao hawakuwa na ukaribu na upendo kwa watoto walemavu kama Jongo akawaza na kuwazua,ikafikia kipindi akajiuliza kama yeye pia angekuwa mlemavu basi wasingekubaliwa kucheza pamoja nae.Hakuwa akifahamu kwa sababu gani iliyowafanya watoto hao wakamsema na kumuonyeshea vidole kijana yule pia hawakuonyesha kuwa na ukaribu kwa watoto wenzao wenye ulemavu.Japo Shamsa alikuwa mwenye umri mdogo lakini alikuwa amejaaliwa kuwa na upeo mkubwa wa kufikiria,akajua moja kwa moja wazazi wao pia watakuwa hawana ushilikiano wa kutosha kuwafunza familia zao juu ya kuwapenda walemavu.Alijisikia vibaya sana kuwatenga walemavu, Baba yake pamoja na mama yake kila siku walipenda kumsisitiza juu ya ukalimu na upendo kwa kila binadamu awe mkubwa hama mdogo kwake lazima heshima iwepo.Akajilaumu kwa nini hakwenda kumfuata mtoto yule ili kumchangamsha angalau kucheza nae lakini alijipa moyo na kujisemea siku yoyote atakapomuona tena basi atakuwa nae karibu na sio kumtenga kama watoto wenzake.

    Shamsa baada ya kucheza na masaa kwenda sana na wenzake wakiwa wanaitwa mmoja mmoja na wazazi wao nae akaamua kuchukua mpira wake na kuwagana wenzake akaondoka kurudi nyumbani.Alipofika nyumbani alionekana ni mwenye furaha wazazi wake walifurahi kumuona mtoto wao akiwa mtu mwenye furaha kila wakati.



    Siku iliyofuata Shamsa alikwenda tena mapema kama alivyowahaidi wenzake,kwa vile hakuwa na kazi wala shule hakuwa ameanza kwani alikuwa anasubilia uwamisho ukamilike ili siku zijazo aendelee na shule atakayopelekwa na baba yake.Alipofika hapo hawakuchelewa wakaanza kucheza kama watoto wanavyopenda walicheza michezo mbalimbali kama mpira wa miguu,lede na kamba ya kuruka.Punde watoto wote waliacha kucheza na kumwangalia mtoto aliyekuwa anakuja,alikuwa yule kipofu Jongo ambaye hakuwa na mabadiliko yoyote kama jana yake alikuja mpaka karibu na watoto wenzake na kukaa pale sehemu aliyokaa jana.Shamsa alisikia kauli ile ile ya jana kutoka kwa watoto wenzake tena safari hii wakiambatanisha na kelele nyingi za kuzomea “Keshakuja tena huyoo….huyooo lione hiloo….. mtoto kipofu huyooo”wenzake waliongea huku wakiendelea kuzomea kwa fujo.Walisogeza mpaka njiani kabisa na mahali pale alipokuwa akija Kijana yule kisha walirudi mbilo mpaka uwanjani na kuendelea na michezo yao.Katika cheza cheza yao Shamsa alikuwa makini kumtazama Jongo ambaye tangia amefika hakudhubutu wasogelea watoto wale wala hakushughulika nao yeye aliendelea kushikashika fimbo yake na kucheza peke yake pale chini ya mwembe.....



    Ghafla wakiwa katika pilika pilika za michezo mara mpira uliruka na kumpiga hakiwa aliyerusha mpira huo akiwa ajulikani,kurushwa kwa mpira huo ilisababisha miwani yake kuanguka chini na kumuacha wazi machoni.Jongo akiwa amehamanika kutokana na kitendo hicho bila kutalajia kiliwafanya watoto wale waliomrushia mpira kuanza kumcheka.Jongo alijihisi vibaya sana moyoni mwake,akajiapiza kwa nini aliumbwa vile,kitu gani alichokuwa amemkosea kati ya watoto wale mpaka kumfanyia visa kama hivyo akashindwa kuvumilia akaanza kulia.Shamsa alijisikia vibaya kumuona Jongo akilia na kusaga meno peke yake pale mwembeni, hakuna hata mtoto aliyemfata kumpa pole au kumbembeleza,Shamsa alijawa na moyo wa huruma sana akaamua kwenda ili ajifanye ameufuata mpira huo.



    Shamsa aliufuata mpira,alipofika hapo alihisi moyo ukimuenda kasi huku mwili ukimtetemeka,alimaka na kupiga moyo konde akiwa karibu kabisa na Jongo alianza kuingiwa na moyo wa kishujaa jinsi gani atamfuata kijana huyo ingawa watoto wote hawakuwa karibu na nae.Shamsa wakati anainama na kuuchukua mpira huo alimuona wazi jinsi alivyokuwa analia hapo hapo akawarushia mpira wenzake na yeye akamsogelea Jongo na kuanza kumbembeleza.Jongo alishangaa mtu akimshika begani,hakuamini kile alichokuwa akikihisi kutoka pembeni yake,aliona maajabu ya karne kubembeleza na mtu ingawa hakujua mtu huyo ni nani na alikuwa ametokea wapi maana sio kawaida kwa watoto wa pale kumsogelea.Haikuchukua muda mrefu Jonh akanyamaza na kufuta machozi yake yaliyokuwa yakitililika toka machoni mwake, Shamsa akaanza kumuongelesha ingawa Jongo aliona kama anaota vile haraka akafuta machozi yake baadae Jongo akaanza kuogopa akajua watoto wakolofi wamemsogelea kwa nia ya kutaka kumpiga.

    “Kwanini uchezi na watoto wenzako?”Shamsa aliuliza baada ya kumuona Jongo akiweweseka

    “Hawataki mimi kuwa rafiki yao….tucheze pamoja”Jongo alijibu kwa woga ingawa sauti hakuijua

    “Kwa sababu gani mpaka wakukatae?”Shamsa alimuuliza kwa huruma

    “Jinsi nilivyo mlemavu….wanadai sina ushirikiano nao kwa sababu sina macho ya kuona”Shamsa alijisikia huruma sana akupenda Jongo ajisikie mpweke, Shamsa akamshika mkono Jongo na kumwambia maneno ambayo yalimuacha Jongo njia panda, CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kuanzia leo utakuwa rafiki yangu, tutacheza sote na kufurahi pamoja na wengine”, Jongo alishangaa akuamini kile alichokuwa akikisikia na kumwambia

    “Sauti yako ngeni kwangu…. Sijui unatokea wapi maana sijawai kuisikia sauti yako mahali popote pale?”

    “Tumeamia hivi karibuni ni mgeni katika mji huu na hapa uwanjani nimefika jana baada ya kuwaona watoto wakicheza na kufurahi pamoja”

    “Nashukuru Sana…nitafurahi sana kama tukicheza pamoja” Jongo alimjibu

    “Nashukuru pia ila sijui jina lako unaitwa nani? Shamsa alimuuliza ingawa alimjua kwa jina jana alipotajwa na watoto wale.

    “Naitwa Jongo…sijui wewe rafiki yangu”Jongo alimtupia swali

    “Naitwa Shamsa Samir”

    “Karibu sana Shamsa”

    “Ahsante sana

    Muda wote watoto wengine wakicheza Shamsa na Jongo walikuwa bado wapo pamoja wakicheza bao lililokuwa limechimbwa na shamsa chini ya mwembe ule na kutafuta vijiwe vidogo na kufanyia kete za kuchezea bao hilo.Waliendelea kuwa karibu huku Shamsa akimfundisha Jongo jinsi ya kuruka kamba walikuwa karibu sana, waliongea hili na lile na kufahamiana zaidi kwani siku hiyo ilikuwa yenye nuru kwa Jongo kupata furaha ya moyo wake kucheza pamoja na mwenzake wakati hakuna siku aliyowai kucheza na watoto wenzake kwa kumtenga.Ilipohitimu saa kumi na mbili ya jioni, Jongo alimwambia Shamsa kwa furaha aliyokuwa nayo moyoni angependa wakutane tena siku inayofuata.Shamsa alimuahidi watakutana tena kesho panapo majaaliwa ya muumba wao na kucheza pamoja.

    ********

    “Vipi baba …mbona waonekana una furaha leo mwanangu”

    “Yaani mama leo nimekutana na maajabu kweli kweli”

    “Maajabu gani tena Jongo mwanangu”

    “Leo nilipoenda kucheza nikakutana na dada mmoja hivi akanifuata na tukacheza pamoja”

    “Hee! Unasema kweli mwanangu…naona sasa wanaanza kukupenda marafiki zako”Mama yake alimwambia huku akiwa amehamaki kwani taarifa zote anazifahamu juu ya mtoto wake kutengwa na wenzake sababu ya ulemavu wa macho.

    “Kweli kabisa mama na kesho nitawai mapema ninapotoka shuleni nitakwenda tena kujumuika pamoja nae”Jongo alimwambia mama yake kwa furaha

    “Mungu ni mkubwa mwanangu naona sasa kilio chako kwa mda mrefu sasa kimeisha umepata marafiki wema”

    “Naamini hivyo mama”



    Siku hiyo baada ya kurudi nyumbani huku akiwa mtu mwenye furaha alizunguka nyumba nzima akiwa na fimbo yake mkononi.Mama yake alijisikia amani moyoni mwake kumuona Jongo akiwa na furaha.kitu tofauti na siku zote anavyoonekana.Jongo alikuwa na desturi yake akiaga kwenda kucheza umwambia mama yake kila kitu juu ya watoto wenzake kumtenga na kumsema maneno machafu.Mama yake alimuonya na kumtaka akae tu nyumbani na si kwenda kucheza kule kwa watoto wanafki wasiojua umuhimu wa mwenzao mwenye ulemavu.Aliumia kumuona mtoto wake anavyonyanyaswa na watoto wa majirani wenzake lakini Jongo hakukoma aliendelea kwenda na kukaa pembeni alipata faraja, japo kusikia sauti za watoto wenzake wakicheza peke yao.

    Siku iliyofuata Jongo aliwai kuamka asubuhi na mapema alijiandaa na kijana Saidi ambaye ndiye aliyemfuata siku hile kule uwanjani ni mtoto wa rafiki wa mama yake alimpitia na kuongozana kuelekea shuleni.Siku hiyo hata Said alishangaa alipomuona Jongo muda wote akiongea meno yake yote yalionekana, alikuwa akitabasamu.



    Tofauti na siku zote wanapokuwa pamoja Jongo hakuwa muoengeaji sana mpaka pale Saidi anapomuuliza na kumjibu basi lakini siku hiyo kila kitu alikisimulia yeye.Said alimshangaa na kumhoji kulikoni mbona siku hiyo alionekana kuwa na furaha kupitiliza,Jongo hakuwa na papala taratibu alimueleza kila kitu kilichotokea jana yake uwanjani pale.muda uliyoyoma huku wakiba shuleni wakisoma na kuandika kisha wakawa na michezo mbalimbali nae John alikuwa na mwalimu wake anayemfundisha kwa kutumia mashine (bleara) kwa ajili ya kufundisha walemavu wa uwoni kama alivyo Jongo...



    Shule ya msingi Majengo ambayoalikuwa akisoma Jongo, shule hiyo kulikuwa na watoto wenye ulemavu wa miguu hao walichanganywa na wanafunzi wa kawaida na walemavu wa uwoni wawili.Ambao ni Jongo na mtoto mwingine anayeitwa Mariam.Wanafunzi hawa wawili walikuwa wakifundishwa masomo ya kila aina kutumia mashine zao,kuna mwalimu wao maalumu ndio aliyekuwa akiwafundisha kutumia brela na mambo mengine kwa vitendo.Mwalimu huyo alikuwa akiishi mbali na kijiji hicho kwani pia alikuwa akifundisha shule nyingine tofauti na hiyo,katika shule hizo mbili alijiwekea utaratibu wa ratiba ya kila shule na muda wake,alifundisha kwa kila hatua kama kazi yake ndivyo.

    Siku hiyo Jongo alisoma kama kawaida na mwenzakewakifundishwa na mwalimu wao anayeitwa Uweso, aliwafundisha kwa amani na upendo wa hali ya juu huku akiwasisitiza kuendelea kujifunza zaidi juu ya kutumia mashine hizo zenye alama maalum kwa ajili ya walemavu wa uwoni.Walisoma mpaka saa nane mchana ndio muda ambao wanafunzi wote walitakiwa kurejea majumbani mwao.Jongo aliondoka huku akiwa mtu mwenye furaha alikuwa akienda huku akipapasa fimbo yake nyeupe mbele kwa kila hatua anayopiga ndivyo alivyokuwa akizidi kupapasa.Hakika ilikuwa mtihani mkubwa sana kwake kutokana na ulemavu wake,Ila hakuona tabu kwenda shuleni alisoma na kuhudhulia vizuri kama watoto wengine.Wakati Jongo akirejea nyumbani alikuwa na furaha ya ajabu pindi alimpomkumbuka sana Shamsa, aliona muda wa kucheza ndio ulikuwa umewadia na hakutaka kukaa mbali na Shamsa alijua kuwa msichana huyo ni mtu mwema kwake hivyo alifanya hima kuwai kurejea nyumbani mapema. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku hiyo alifika mapema nyumbani tofauti na siku zote arejeapo nyumbani alioupata, mama yake alimshangaa na kumuuliza kulikoni, Jongo hakuwa na shaka kumjibu mama yake, alikuwa ameshamwambia kuhusu urafiki aliopata siku iliyopita.Mama yake hakuwa na namna aliachia tabasamu pana na kutikisa kichwa kwa masikitiko.Jongo alikula chakula kama kawaida kisha alipumzika kidogo na kumuaga mama yake kuwa anakwenda kucheza uwanjani kwa watoto wenzake.Mama yake alishangaa na kumuuliza mbona bado mapema sana saa nane jua likiwa linawaka.Alihamaki sana kumuona mtoto wake akiwa kwenye harakati za kutafuta viatu vyake ili aweze kuondoka.Mama yake alipomuona akiangaika na kupapasa ili kuvipata viatu vyake pale mlangoni alimtafutia na kumpatie,Jongo alivipokea viatu hivyo na kuvitwika miguuni mwake na kumuaga mama yake “kwa heli mama tutaonana baadae” kisha akaondoka.

    *******



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog